Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WAZIRI LUKUVI ATEUA WAJUMBE WA BODI YA TAIFA YA KUSIMAMIA NA KUSAJILI WAPIMA ARDHI.


RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.SHEIN AWASILI ZANZIBAR AKITOKEA NCHINI UINGEREZA KWA ZIARA MAALUM

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, alipowasili Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Nchini Uingereza kwa ziara Maalum.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar, alipowasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Nchini Uingereza, alipokuwa na ziara Maalum.,(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,, akisalimiana na Wananchi waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kumpokea akitokea Nchini Uingereza kwa ziara Maalum.(Picha na Ikulu)

WALIOFUJA FEDHA MRADI WA MIYOGWEZI UKEREWE KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

$
0
0
Naibu Naibu Waziri wa kilimo, OMari Mgumba ( wa nne kutoka kulia) akihoji jambo wakati akikagua miundombinu ya mradi wa umwagiliaji wa Miyogwezi ambao umekwama kukamilika tangu ujengwe mwaka 2013.Hapa akiwa kwenye kimoja ya visambaza maji 16 vya mradi huo. Picha zote na Baltazar Mashaka 
……………………. 

NA BALTAZAR MASHAKA, UKEREWE 

SERIKALI imesema waliohusika kwenye ubadhirifu wa fedha za Mradi wa Umwagiliaji wa Miyogwezi wilayani Ukerewe na kusababisha ujengwe chini ya kiwango na kutokamilika licha ya sh. milioni 750 kutolewa watachukuliwa hatua za kisheria. 

Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba alisema jana wilayani Ukerewe baada ya kutembelea na kukagua miradi ya umwagiliaji ya Miyogwezi na Bugorola ambao miundombinu yake imechoka na kusababisha ushindwe kufanya kazi. 

Akizungumza kwenye eneo la mradi wa Miyogwezi na wakulima wanaotumia bonde la mradi huo kwa kilimo, alisema kuna harufu ya rushwa kwenye mradi huo ambao mkandarasi alilipwa sh. milioni 684 kati ya sh. milioni 750 bila kuukamilisha na kuhoji nani alisababisha fedha zikatumika kinyume cha utaratibu wa serikali. 

Alisema serikali iliamua kujenga miradi ya umwagiliaji ili kuleta maendeleo endelevu kwenye sekta ya kilimo baada ya kukusanya na kutenga fedha ili wananchi wafaidi keki ya nchi na kulima kwa tija lakini wajanja wa wizara yake wakaleta kampuni za mifukoni zila fedha, kwamba si haki na hawakuwatendea haki watanzania. 

Alisema cha kushangaza Ukerewe ilipewa mradi wa miyogwezi na kampuni ya CODA ya nchini Kenya iliyopewa kazi ya kujenga mradi huo ililipwa bila kustahili malipo ya sh. milioni 684 bila kukamilisha mradi huo kwa asilimia 55 baada ya kujenga mabanio mawili chini ya kiwango, magati, mitaro miwili ya maji lakini haikusakafiwa na haikufika mwisho pamoja na vigawa maji 16. 

“Siamini nilichokiona hapa na kilichopo kwenye nyaraka (mkataba), mradi huu una harufu ya rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma.Thamani ya mradi ni sh. milioni zaidi ya 700 bado haujakamilika,umetekelezwa kwa asilimia 45 tu.Mkandarasi amelipwa wakati kazi hailingani na thamani ya fedha na waliofanya hayo bado wapo ofisini na kwa nini bado wapo,” alisema Mgumba. 

Alionya fedha hizo hazitakwenda bure na kuiagiza Tume ya Umwagiliaji kuandaa taarifa ya kina ya mradi wa Miyogwezi ikiainisha nani alilipwa wakati kazi haikukamilika,waliohusika kwenye ubadhirifu huo, nani aliyesababisha fedha zitumike kinyume cha mipango ya serikali ili ijue njia wanazotumia kutafuna fedha za umma na makosa yasirudiwe. 

Naibu Waziri huyo wa Kilimo alisema miongoni mwa kanda ambazo hazikufanya vizuri kwenye miradi ya umwagiliaji ni Mwanza, kwani miradi hiyo ilijengwa chini ya kiwango na kushangaa kwa nini watendaji waliokuwa wakisimamia miradi hiyo bado wako ofisini na kuwataka wajipime kama wanafaa kukalia nafasi hizo. 

Mgumba akijibu ombi la wakulima hao la kutaka waletewe fedha zingine baada ya wajanja wakupiga (walikula) fedha za mradi huo alisema serikali haiwezi kuleta fedha hadi ijue nani aliipiga ili achukuliwe hatua za kisheria na liwe fundisho kwa wengine na kueleza kuwa serikali inafanya kazi kwa bajeti iliyopitishwa na bunge. 

Aidha, alieleza kuwa wataalamu wanayo kazi ya kuisaidia serikali ili mradi huo wa Miyogwezi ukamilike na itakuwa tayari kutoa fedha baad ya kujiridhisha kuwa fedha za awali zililiwa ndo maana Tume ya Umwagiliaji imeundwa kusimamia miradi ya umwagiliaji. 

Awali Mbunge wa Ukerewe (CCM) Josephat Mkundi alisema mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji uliokuwa ukisimamiwa na District Agriculture Investment Project (DASIP) ulijengwa mwaka 2013 kwenye kwa ajili ya kuwanufaisha wakulima 194 lakini haufanyi kazi kutokana na miundombinu yake kutokamilika. 

Mbunge huyo wa Ukerewe alisema sh. milioni 200 zilitolewa na Dairy Processing & Infrastructure Development Fund (DIDF) ambapo DASIP ilitoa milioni 550 kwa ajili ya mradi huo lakini hadi sasa haujakamilika ambapo akiwa bungeni Januari mwaka huu alihoji serikali ni lini mradi wa Miyogwezi utaboreshwa na kamilika ili kuweza kuwasaidia wakulima wanaotumia bonde hilo kwa kilimo, kulima kwa tija.

WAZIRI WA AFYA HAMAD RASHID MOHAMED AKUTANA NA WAANDISHI ZANZIBAR.

$
0
0
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed katikati akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mpango mkakati wa kupambana na maradhi ya Homa ya Ini katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo itafikia kilele chake tarehe 28 Julay 2019 hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar. 
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akionesha kitabu cha Mpango mkakati wa kupambana na maradhi ya Homa ya Ini katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo itafikia kilele chake tarehe 28 Julay 2019 hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
Msaidizi Mpango shirikishi Ukimwi,Homa ya Ini,Kifua kikuu na Ukoma Issa Abeid Mussa akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo itafikia kilele chake tarehe 28 Julay 2019 hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
Muakilishi wa Shirika la Afya Duniani(WHO)Dk,Ghirmany Andemichael akitoa taarifa ya WHO katika Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo itafikia kilele chake tarehe 28 Julay 2019 hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo itafikia kilele chake tarehe 28 Julay 2019 hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar. 

**************** 

Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 26/07/2019. 

Serikali kupitia Wizara ya Afya Zanzibar imeahidi kushirikiana na sekta mbalimbali za ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha inafikia lengo la kuondoa Homa ya Ini Zanzibar ifikapo mwaka 2030. 

Hayo aliyasema Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed huko katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi Mmoja wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini duniani ambayo hufanyika kila ifikapo Julai 28 ya kila mwaka . 

Amesema Serikali imepanga mikakati kuweza kudhibiti homa hiyo kwa kuwapatia matibabu ya chanjo wenye mahitaji maalum ikiwemo wauguzi ambao wanawahudumia wagonjwa mbali mbali ili waweze kujiepusha na maambukizi. 

Amesema ugonjwa wa homa ya ini imeenea sana duniani kote hasa Bara la Afrika na zaidi kwenye nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara ikiwemo Zanzibar takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha wastani wa watu milioni 257 wanaishi na maambukizi ya homa ya ini B na milioni 71 ya homa ya ini C duniani na vile vile watu karibu milioni 1.4 hufa kila mwaka kutokana na madhara ya maradhi hayo . 

Ameeleza ripoti za utafiti maalum wa kutathmini hali halisi ya homa ya ini bado haujafanyika Zanzibar ambapo takwimu zinathibitisha uwepo wa maambukizi ya homa ya ini inaonyesha walioathirika zaidi na ugonjwa huo ni watu wa makundi maalum (key population )ambao wamefikia asilimia 2-6 kwa homa ya ini B na asilimia 1-25 ya homa ya ini C. 

Alifahamisha miongoni mwa watu waliopimwa kwa ajili ya kuchangia damu kwa hiyari katika mwaka 2011 -2016 walionekana kuambukizwa ya homa ya ini B ni asilimia 2.4 na ini C asilimia 0.4 

Waziri Hamadi amesema anza ya Serikali kuwapa huduma wananchi wake wote bila ya ubaguzi kwa lengo la kuwanusuru kutokana na madhara pamoja na vifo vinavyoweza kusababishwa na homa ya ini . 

Aidha alisema Wizara ya Afya imeunda kitengo maalumu cha huduma ya homa hiyo ili kupanga kuongoza na kusimamia utekelezaji wa huduma ya homa ya ini katika ngazi ya taifa wilaya vituo vya afya na jamiii 

Alieleza tayari Wizara imeanza kutoa elimu kuhusu homa ya ini katika ngazi zote za huduma ya afya ili kuengeza uelewa pamoja na kuhamasisha kinga kwa wafanyakazi ili kutoa ushauri na msaada wa kitaalamu katika mapambano dhidi ya homa ya ini . 

Kauli mbio ya mwaka huu ni WEKEZA KATIKA KUONDOA HOMA YA INI ZANZIBAR . 

Mapema Waziri wa Afya Hamadi Rashid Mohamed alizindua chanjo ya homa ya ini kwa wafanyakazi wa hospitali ya mnazi mmoja na kuwataka wafanyakazi hao kujikinga kwa chanjo hiyo 

Hata hivyo aliwataka wauguzi kufuata maadili ya kikazi kwa kutotoa taarifa za wagonjwa wanaowapatia tiba pale wanapofika hospitalini hapo kwa matibabu 

Alisema homa hii imeanza kuiathiri jamii hivyo mkakati wa pamoja unahitajika kwa kuweza kuutokomeza kwa kutumia chanjo na masharti yaliyowekwa 

Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dk Marijani Msafiri alisema zoezi la chanjo kwa wafanyakazi ni muhimu kwani maradhi hutoka kwa mgonjwa kuja kwa muunguzi 

Alisema chanjo zilizopo zitakidhi kwa wafanyakazi wa hospitali ya mnazi mmoja hivyo aliwataka wauguzi kuendelea na zoezi hilo ili kufikia malengo ya serikali kwani ugonjwa huu maambukizi yake huwa kama ya virusi vinavyosababisha ukimwi .

MKONGEA ANUSA UBADHILIFU MRADI WA MAJI IKWIRIRI ,ATOA WIKI MBILI KWA TAKUKURU KUFANYA UCHUNGUZI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,IKWIRIRI

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2019 ,Mzee Mkongea Ali amenusa ubadhilifu wa fedha, katika mradi wa maji Ikwiriri huko Rufiji ambao umejengwa na mamlaka ya maji safi Dar es salaam DAWASA kwa zaidi ya sh.bilioni 2.055.6.

Kufuatia shaka hiyo, Mkongea amemuagiza kamanda wa TAKUKURU wilayani hapo kukamilisha agizo hilo ndani ya wiki mbili, kisha kupeleka taarifa TAKUKURU makao makuu na nakala itumwe kwake ili kama kutabainika uchakachuaji hatua ziweze kuchukuliwa.

Alitoa agizo hilo wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea mradi huo na kubaini baadhi ya dosari na kukosa nyaraka muhimu zilizotumika katika manunuzi ya baadhi ya vifaa.

"Tunapotembelea miradi hii tunahitaji kupata taarifa kamili za mradi ,tumetembelea hapa na kutoonekana nyaraka mbalimbali,huku tukimuuliza mtaalamu kuhusiana na fedha na matumizi yaliyoainishwa lakini hana majibu na kudai vitu vingine havipo"

"Hili suala la matanki manne ya jengo ambayo yalitengewe kiasi cha sh milioni 64 .5,vifaa vilivyotumika wakati wa survey milioni 5 tumeomba taarifa za mchanganuo hamna,mtaalamu ameulizwa anasema havipo,fedha zilizotengwa kwa ajili ya zege ,kokoto ,mchanga laki tano ofisa wa TAKUKURU kachunguze hili na nakukabidhi taarifa za mradi ili kuendelea na kazi ya ufuatiliaji"alifafanua Mkongea.

Mkongea alimkabidhi nyaraka zinazoonyesha taarifa za mradi kwenda kuchunguza kwa kina baada ya wao kupitia kwa muda mchache na kunusa ubadhilifu huo.Nae mkuu wa wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo alimuhakikishia kiongozi huyo wa mbio za mwenge kuwa atalisimamia suala hilo.

Alieleza, kabla ya mwenge kuanza ziara hiyo viongozi wa wilaya hiyo walishiriki kikao cha kamati ya sherehe ambacho kiliitishwa na mkuu wa mkoa mhandisi Evarist Ndikilo na kuagiza kwamba wataalamu kutoka DAWASA kuwepo katika miradi yote ya maji itakayopitiwa na mwenge lakini cha kustaajabisha wataalamu hao hawakutokea katika mradi huo.

Wakati huo huo akipokea taarifa ya uchaguzi wa serikali za mitaa kijiji cha Kilimani ,Mkongea aliwataka wananchi kuchagua viongozi bora wasiopenda rushwa bali wawe wale watakaoleta mabadiliko ya nchi.

Aliwaomba wasirubunike na viongozi wanaopenda madaraka kwa kushawishi rushwa kwani kura moja italeta mabadiliko hivyo wasikubali kununuliwa wachague viongozi walio bora na si bora kiongozi.

Awali Njwayo alibainisha, mwenge wa uhuru ukiwa wilayani Rufiji umepitia miradi tisa yenye thamani ya sh.bilioni 2.562 .

Mchakato wa Tathmini Mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga Katika Uchumi Waiva

$
0
0


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari. akizungumza wakati wa kikao cha kujadiliana hatua zilizofikiwa katika mchakato wa kuanza matumizi ya mfumo wa kutathmini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika ukuaji wa uchumi wa Taifa leo jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta kuu ya Uchukuzi, Mhandisi. Aron Kisaka na Mtakwimu Mkuu, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar, Mayasa Mahfoudh Mwinyi. 
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kubaini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika uchumi wa Taifa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi(hayupo pichani) alipokuwa akifungua kikao cha kujadiliana hatua zilizofikiwa kabla ya kuanza matumizi ya mfumo wa kutathmini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika ukuaji wa uchumi wa Taifa leo jijini Dodoma.Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta kuu ya Uchukuzi, Mhandisi. Aron Kisaka akizungumza wakati wa kikao cha kujadiliana hatua zilizofikiwa katika mchakato wa kuanza matumizi ya mfumo wa kutathmini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika ukuaji wa uchumi nchini. Kutoka kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ua Usafiri wa Angaa (TCAA), Hamza Johari. Katibu wa Kamati ya Kubaini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika Uchumi wa Taifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumu toka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Danieli Malanga akiwasilisha taarifa fupi ya hatua zilizofikiwa katika mchakato wa kuelekea kuanza matumizi ya mfumo rasmi wa tathmini ya mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika uchumi wa Taifa wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dodoma. Katibu wa Kamati ya Kubaini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Daniel Masolwa akichangia hoja wakati wa kikao cha kujadili hatua zilizofikiwa katika mchakato wa kuelekea kuanza matumizi ya mfumo rasmi wa tathmini ya mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika uchumi wa Taifa wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mwenza wa Kamati ya Kubaini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika Uchumi wa Taifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumu toka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Danieli Malanga Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta Kuu ya Uchukuzi), Mhandisi. Aron Kisaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kubaini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika Uchumi wa Taifa wakati wa kikao cha kujadiliana hatua zilizofikiwa katika mchakato wa kuanza matumizi ya mfumo wa kutathmini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika ukuaji wa uchumi nchini. (Picha na: Idara ya Habari MAELEZO)

HIFADHI MPYA YA MWL.NYERERE KUKUZA UTALII SELOUS.

$
0
0


Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka wizara ya Maliasili na Utalii kutenganisha eneo la uwindaji Selou (Hunting block) kwa kutengeneza Hifadhi ya Taifa ambayo itaitwa Hifadhi ya taifa ya Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji mkoani Pwani utakaozalisha megawatt 2,115, Rais Magufuli amesema kuwa eneo la uwindaji la Selou ni eneo ambalo limezunguka mradi huo mkubwa wa umeme na lina urefu wa kilomita za mraba elfu 57.

“Eneo la Selou ni eneo kubwa ambalo linachukua takribani kilomita 50, hivyo ni lazima Wizara itenge eneo ambalo litatengenezwa na kuwa Hifadhi kuweza kukidhi mahitaji ya utalii na kukisaidia kizazi kijacho kuendelea kuenzi mambo ambayo ameyafanya baba wa Taifa,” amesema Rais Magufuli.

Amesema maeneo ya uwindaji wa wanyama yanafikia 47 katika mbuga ya wanayama Selou hivyo Wizara ya Maliasili lazima itenge eneo la hifadhi na la uwindaji, ili kuimarisha utalii na kuvutia watalii wengi katika mbuga hiyo

Rais Magufuli alisisitiza kuwepo kwa utaratibu kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia maeneno ambayo yanavitalu wa uwindaji ili kuhakikisha kuwa Serikali inafaidika na maeneno hayo, pia aliagiza barabara ya kutoka Fuga kilomita 60 kwenda mahari ambapo mradi unajengwa ianze kutengenezwa kwa rami ili kufungua sekta ya utalii katika Mbuga ya wanayama Selous.

Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji ni mradi ambao unaweza kudumu kwa muda wa miaka 60 ambapo utasaidia kuzalisha umeme wa kutosha na kusaidia Tanzania kuweza kutekeleza malengo ya milenia ya maendeleo endelevu.

Amesema mradi wa mto Rufiji utasaidia kuchochea maendeleo katika sekta ya viwanda ambapo wewekezaji wataweza kupata umeme wa uhakika na kwa bei nafuu na wenye kuaminika ili kuweza kuzarisha bidhaa zenye ubora.

“Mradi huu wa umeme wa mto Rufiji unaweza kudumu kwa muda wa miaka 60 na kusaidia watanzania kupata umeme wa uhakika na wenye gharama nafuu ambao utasaidia wawekezaji kupata huduma ya umeme kwa uhakika bila mgao ili kuweza kuzarisha bidhaa zenye ubora na kuweza ushindano kwenye masoko mbalimbali ya kimataifa,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisisitiza kuwa katika utekelezaji wa mradi huo, mkandarasi anatakiwa kutumia wafanyakazi walioko karibu kwa kazi ambazo siyo za kitaalamu, akasisitiza ajira zitolewe kwa wenyeji wa maeneo ya mradi kwa mikoa ya Morogoro na Pwani, na amewataka wananchi kuchangamkia fursa kwa miezi hiyo 36 ya ujenzi.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema kuwa Ndoto ya Rais Magufuli ya kuenzi mambo makubwa ya Baba wa Taifa, Mwl.Julias Nyerere ikiwemo utekelezaji wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji.

“Mhe. Rais, ndoto yako leo imeanza kupata mafanikio, ndoto yako ni kupeleka umeme hadi kule kijijini kwa wananchi wa kawaida na umetoa agizo kuwa kila nyumba ya mtanzania iwe ya bati, nyasi au tembe lazima iwake umeme, kwa hiyo umeme huu ambao ujenzi wake umezinduliwa leo ni kukamilisha azma yako bila kujali maisha ya watanzania”, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu alisema kuwa kampuni zinazojenga mradi huo mkubwa wa kufua umeme Tanzania, Els weldey na Arab Contructors, zinafanya kazi nzuri kwa hiyo zitatekeleza mradi huo kwa weledi mkubwa, kama zinavyofanya kule Misri.

Naye Waziri wa Nishati amesema mradi huo unabainisha mambo mawili ya kumuenzi Rais wa kwanza Tanzania, hayati Julius Nyerere, ambayo Rais Magufuli anatekeleza likiwemo kuhamisha makao makuu ya nchi kwenda Dododma, ambayo tayari yanatekelezwa, likiwemo la ujenzi wa Bwawa la Rufiji.

“Naomba niwakumbushe watanzania Mhe. Rais ametengeneza mambo makubwa mawili ya ndoto ya baba wa Taifa ikiwemo kuhamisha makao makuu ya nchi kwenda Dododma na utekelezaji wa mradi mahususi wa bwawa la kufua umeme, mradi mkubwa wa kwanza Tanzania, Afrika Mashariki na wa nne barani Afrika, huku ukiingia kwenye mabwawa 70 makubwa duniani yakuzarisha umeme,” Waziri Kalemani.

Aidha Waziri Kalemani amesema kuwa mradi huu utekelezaji wake utachukua miezi 42 ambapo hadi sasa miezi sita imeshapita na kubaki miezi 36 kukamilisha ujenzi wa mradi huo ambao unategemewa kukamilika Juni 13, 2022.

Waziri Kalemani aliongeza kuwa katika ujenzi wa mradi huo kazi kubwa ya mkandarasi ni pamoja na ujenzi wa bwawa kubwa litakaloweza kuhifadhi maji ya mita za ujazo billioni 33.2, ujenzi wa Power house itakayokuwa na mashine tisa zenye kuzalisha megawati 235 kwa kila mashine na kazi ya mwisho ni kujenga substation yenye kilovolt 400, ambapo ni umeme mkubwa utakaotumika kwenye uchumi wa viwanda.

Umeme huo utasafirishwa kutoka Rufiji kwenda Chalinze umbali wa kilomita 127 kwa dola za kimarekani 188 Chalinze mpaka Dar es Salaam na Dodoma na ndio umeme utakao tumika kuendesha Treni ya kisasa (SGR), lengo la Serikali ni kufikisha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025 kwahiyo mradi huu mkubwa ni kichocheo kikubwa sana kuelekea uzarishaji wa hizo megawati.

Kwa upande wake Waziri wa nishati na umeme kutoka Misri Dkt. Mohamed Shaker amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo unaimarisha mahusiano ya Tanzania na Misri katika sekta mbalimbali, ikiwemo ya nishati.

“Ujenzi wa mradi huu mkubwa ni moja ya hatua kubwa katika mahusiano ya nchi mbili ambayo itahamasisha zaidi utekelezaji wa miradi mingine ya undugu kati ya Tanzania na Misri, hususani kwenye nyanja ya umeme, nipende kusisistiza kwamba mradi huu wa umeme Rufiji unaungwa mkono na Rais wa Misri, Abdel Fattah El-Sisi” Waziri Shaker.

Nchi ya Misri itaendelea kushirikiana na Tanzania katika utoaji wa mafunzo ya teknolojia ya kuzalisha umeme, kwani ina vituo 22 vya kutolea mafunzo hayo na imetoa nafasi 50 kwa wataalamu kutoka Tanzania kwenda kujifunza masuala ya ufuaji na uzalishaji umeme.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia eneo la bonde katika mto Rufiji mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo wa umeme.

KAMISHNA WA MAGEREZA, UWESU NGARAMA AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI YA SAJINI WA MAGEREZA, CHUO CHA MAFUNZO YA AWALI CHA MAGEREZA KIWIRA, MBEYA

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Awali cha Magereza Kiwira, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Adriano Mduda akitoa taarifa fupi ya Chuo Ofsini kwake mbele ya Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama jana Julai 26, 2019.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama akikagua gwaride la wahitimu wa Mafunzo ya Sajini wa Magereza Kozi namba moja jana Julai 26, 2019.
Mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo hayo Koplo Inocent Mutoka akivishwa cheo cha Sajini wa Magereza kwa niaba na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama jana Julai 26, 2019.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama akimkabidhi cheti cha sifa mhitimu wa Mafunzo hayo, Koplo Mariam Mwakababile aliyefanya vizuri kwenye medani ya ulengaji wa shabaha jana Julai 26, 2019.
Kikundi namba tatu cha gwaride kikipita mbele ya mgeni rasmi katika mwendo wa haraka jana Julai 26, 2019.
Wahitimu wa Mafunzo hayo ya Sajini wa Magereza wakionesha umahiri wao katika onesho maalum la medani ya kujihami na adui jana Julai 26, 2019.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama (wa nne toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Julius Chalia(wa nne toka kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mathias Mkama, jana Julai 26, 2019(Picha zote na Jeshi la Magereza).

BENKI YA POSTA (TPB) YATOA MSAADA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI PONGWE JIJINI TANGA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki TPB Sabasaba Moshingi kulia akimkabidhi madawati hamsini (50),meza ya ofisi pamoja na viti, vitakavyotumiwa na wanafunzi pamoja na waalimu na vitasaidia kupunguza uhaba uliopo wa madawati shule ya Msingi Pongwe Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki TPB Sabasaba Moshingi kulia akimkabidhi madawati hamsini (50),meza ya ofisi pamoja na viti, vitakavyotumiwa na wanafunzi pamoja na waalimu na vitasaidia kupunguza uhaba uliopo wa madawati shule ya Msingi Pongwe Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Ramadhani Possi
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katikati akiwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki TPB Sabasaba Moshingi kulia wakiwa wamekaa kwenye madawati mara baada ya kuyapokea kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Ramadhani Posi na kulia ni Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi
Sehemu ya madawati yaliyokabidhiwa kwa shule ya Msingi Pongwe na TPB Benki


BENKI ya TPB imetoa msaada wa madawati na samani za ofisini kwenye shule ya msingi Pongwe Mkoani Tanga ikiwa ni kupunguza uhaba uliokuwepo awali. 

Madawati hayo hamsini (50),meza ya ofisi pamoja na viti, vitavyotumiwa na wanafunzi pamoja na waalimu na vitasaidia kupunguza uhaba uliopo wa madawati shuleni hapo. Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi madawati hayo shuleni hapo, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sabasaba Moshingi alisema benki hiyo ilipokea maombi kutoka uongozi wa shule ya msingi Pongwe ukiomba benki hiyo isaidie kutatua pamoja na changamoto nyingine, uhaba wa madawati na samani kwa ajili ya shule hiyo. 

“Benki ya TPB inaipa sekta ya elimu umuhimu mkubwa, kwa kuiweka juu katika vipaumbele vyake kwenye sera zake za msaada kwa jamii ( Corprate Social Responsibility). Kila mwaka benki inafanya miradi mingi zaidi kwenye sekta ya elimu kuliko maeneo mengine inayoyaangalia”, alisema Moshingi 

Akipokea msaada huo, Mkuu wa Shule ya Msingi Pongwe Mwalimu Yahya Ally Mafita aliipongeza benki ya TPB kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitoa kwa sekta ya elimu nchini, hususan kwenye shule hiyo ya Pongwe. 

Alisema shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo uhaba wa madawati, samani za ofisi ya waalimu zikiwamo meza na makabati ya kuhifadhi vitabu. “Msaada huu utapunguza uhaba wa madawati uliokuwa ukitukabili, hivyo tunaishukuru sana benki ya TPB. Shule yetu ilipata bahati ya kujengewa madarasa matatu na taasisi ya TAWAH hapo mwaka jana, hivyo madawati haya kutoka benki ya TPB yatakwenda kutumika ndani ya madarasa hayo”, alisema mwalimu Mafita

Naye kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini Mhe. Thobias Mwalipwa aliishukuru benki ya TPB kwa msaada huo, na kusema kwamba utaisaidia kupunguza changamoto kubwa ya madawati pamoja na samani iliyokuwa ikiwakabili. 

Alisema shule inapokuwa na madawati pamoja na vifaa vingine vinavyohitajika hujenga ari ya kujifunza kwa wanafunzi na kutoa motisha kwa walimu ili waweze kufundisha vizuri katika mazingira bora.

TRA YAKUSUDIA KUKIFANYA KITUO CHA FORODHA HOROHORO KUWA KITUO CHA PAMOJA

$
0
0
NAIBU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo akizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo kituo cha Forodha Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga mpakani mwa Tanzania na Kenya wakati wa ziara yake kushoto ni Kamishna Msaidizi Ushuru wa Forodha na Bidhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Benard Asubisye kulia ni Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure

Kamishna Msaidizi Ushuru wa Forodha na Bidhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Benard Asubisye akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza wakati wa ziara hiyo
Afisa Mfawidhi wa Kituo cha forodha Horohoro Bakari Athuman akizungumza wakati wa ziara hiyo
NAIBU Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo kulia akionyeshwa kitu na Afisa Mfawidhi wa Kituo cha forodha Horohoro Bakari Athuman wakati wa ziara yake
NAIBU Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo katikati akiingia mpakani mwa Tanga na Kenya eneo la Horohoro wakati wa ziara yake kulia ni Afisa Mfawidhi wa Kituo cha forodha Horohoro Bakari Athuman wakati wa ziara yake
NAIBU Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo kushoto akisalimiana na Afisa Mfawidhi wa Kituo cha forodha Horohoro Bakari Athuman mara baada ya kufika eneo la Horohoro wilayani Mkinga mpakani mwa Tanzania na Kenya wakati wa ziara yake kulia ni Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure
Sehemu ya watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo
Sehemu ya watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo
Sehemu ya watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo


NAIBU Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo amesema kwamba wanatarajia kukifanya kituo cha Horohoro kuwa kituo cha pamoja (One Stop Board Post) ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

Mbibo aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea kwenye kituo hicho cha forodha kilichopo mpakani kwa Tanzania na Kenya eneo la Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga ikiwemo kuzungumza na watumishi sambamba na kukikagua kituo hicho. 

Alisema yapo mambo machache wanayokamilisha kabla ya kituo hicho kuanza kazi hivyo kuhaidia kwenda kuyashughulikia kwa haraka kwa kuwasiliana na taasisi, mamlaka nyengine ikiwemo upande mwengine wa wenzao wa nchi jirani ya Kenya ili kuhakikisha kwamba kituo hicho kinafanya kazi kama ilivyokusudiwa. 

“Lakini pia nimeambiwa changamoto ya Jenereta nimeambiwa inafanyiwa kazi na inakaribia kukamilika tutakaporudi dar tutahakikisha vifaa hivyo vinafika na kufungwa suala la uhakika wa umeme litakuwa sio tatizo tena na suala la maji litashughulikiwa”Alisema 

Hata hivyo aliwataka watumishi wa umma kwenye kituo hicho kuhakikisha wanashirikiana kwenye kufanya kazi na kutanguliza uzalendo kwenye shughuli zao ili kufikia malengo ambayo yamekudiwa. 

Naibu Kamisha huyo alisema kwamba nchi haiwezi kuendelezwa na mtu mwengine isipokuwa watanzania wenyewe na kila mtanzania sehemu aliyopo afanye kazi kwa kiwango cha juu ili waweze kuyafikia malengo yao. 

Hata hivyo pia aliwataka watumishi wa mamlaka hiyo kwa nchi nzima kuhakikisha wanakuwa waadilifu kwa kiwango cha juu kwa sababu ndio silaha ya mafanikio yoyote na kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu. 

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Kamishna Msaidizi Ushuru wa Forodha na Bidhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Benard Asubisye alionyeshwa kushangazwa na ukusanyaji wa mapato kwenye kituo cha Forodha cha Horohoro wilayani Mkinga kushuka kutoka bilioni 25 hadi 23. 

Hiyo ilitokana na taarifa iliyotolewa na Afisa Mfawidhi wa Kituo cha forodha Horohoro Bakari Athumani kuonyesha kushuka kwa kiwango cha ukusanyaji wa mapato 

Katika taarifa yake Afisa Mfawidhi huyo alimueleza Naibu Kamishna huyo kwamba alisema mwaka wa fedha 2017/2018 walifanikiwa kukusanya kiasi cha Bilioni 25 lakini mwaka wa fedha 2018/2019 ukusanyaji huo ulishuka mpaka kufikia bilioni 23 jambo ambalo liliwashutua viongozi hao. 

Alisema kwamba waliosoma masomo ya sayansi hiyo sio kupanda badala yake wana shuka chini na sio kwenda mbele bora wangebaki kwenye makusanyo ya awali ili waangalie namna ya kujipanga kuongeza mapato. 

Mbunge Ditopile ampongeza Rais Magufuli kwa kutimiza ndoto za Baba wa Taifa

$
0
0


Mbunge wa vijana Taifa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Nishati na Madini Mh Mariam Ditopile kwa niaba ya vijana amemshukuru Rais Magufuli kwa uzinduzi wa mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji Mkoani Pwani kupitia bwawa la kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki na kati, utakaogharimu kiasi cha Shilingi Trilioni 6.5.

Mradi huo unategemewa kukamilika mwezi June 2022 utazalisha megawati 2115 na unatajwa kuwa mwarobaini wa umeme jambo ambao litachochea ukuaji wa Tanzania ya viwanda.

" Nina imani sasa ile ahadi ya Tanzania ya viwanda kupitia chanzo hiki cha uhakika na cha gharama nafuu cha Umeme inaenda kutimia rasmi sanjari na uhakika wa umeme wa kutosha ktk mradi mkubwa wa treni ya mwendo kasi (SGR).

Sisi kama vijana hatuna budi kuishukuru serikali yetu sikivu chini ya Rais wetu kipenzi Dk Magufuli na wasaidizi wake wote kwa kuisimamia vyema na kwa dhati kabisa miradi hii, kwani vijana ndio tunaenda kuwa wanufaika wakubwa," amesema Mhe Ditopile.

Amesema kupitia miradi hii kuna ajira za kudumu na ajira za vipindi maalum zitazaliwa jambo ambalo litapunguza wimbi kubwa la vijana ambao hawana ajira.

" Kupitia miradi hii kuna fursa mbalimbali za kibiashara kwa mfano, mahoteli, migahawa, mama lishe, vifaa mbalimbali vya ujenzi.

Pia itakapokamilika miradi hii kwa upande wa wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla tutakuwa na umeme wa uhakika na kushuhudia ndoto ya Rais Magufuli kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati kupitia viwanda," amesema.

Mhe Ditopile amesema kwa upande wa wakulima kupitia treni ya umeme utakaotokana na mradi huo wa Stiglera Gorge watakuwa na uhakika wa kupata soko lenye tija.

" Kwenye hili tunamuahidi kwa dhati kabisa Rais wetu tupo nae bega kwa bega kwa kuwa Watanzania wa leo wanataka kazi na serikali yetu chini ya Rais Magufuli sasa ipo kazini," amesema Mhe Ditopile.

Asasi za kiraia na Mashirika ya Kimataifa Yatakiwa kujenga Miundombinu ya Elimu

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu bwana Tixon Nzunda (aliyevaa suti) akizungumza mara baada ya kukagua mojawapo ya madarasa manne ya elimu ya awali kati ya madarasa 30 yanayojengwa na asasi ya kiraia ya TAHEA chini ya ufadhili wa shirika la kimataifa kutoka nchini Scotland la Children in Cross fire wilayani Misungwi jana.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu bwana Tixon Nzunda akizungumza na wanafunzi wa elimu ya awali wa shule ya Msingi Mamae iliyopo wilayani Misungwi mara baada ya Naibu Waziri kutembelea shule za msingi Magaka na Mamae ambazo ujenzi wake ulifadhiliwa na asasi ya TAHEA wakishirikiana na shirika la kimataifa la Children in Crossfire jana wilayani Misungwi.

………………………

Na Mathew Kwembe, Mwanza
Serikali imezitaka asasi za kiraia, taasisi za umma pamoja na mashirika ya kimataifa ambayo yanafanya kazi na serikali kwenye sekta ya elimu kuhakikisha kuwa yanaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kujenga miundombinu ya elimu nchini kwa sababu ndiyo changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo hivi sasa.

Wito huo umetolewa jana katika kijiji cha Magaka wilayani Misungwi na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu bwana Tixon Nzunda wakati akikagua mojawapo ya madarasa manne ya elimu ya awali kati ya madarasa 30 yanayojengwa na asasi ya kiraia ya TAHEA chini ya ufadhili wa shirika la kimataifa kutoka nchini Scotland la Children in Cross fire katika wilaya za Misungwi na Ukerewe mkoani Mwanza.

Amesema kuanzia sasa asasi zote za kiraia na mashirika ya kimataifa yanayojihusisha na masuala ya elimu mbali na kufanya kazi ya kufundisha na kujenga uwezo yatalazimika kujenga angalau darasa moja pamoja na matundu ya vyoo ili kuwezesha uwepo wa mazingira rafiki ya ufundishaji na ujifunzaji kwa ajili ya watoto wanaosoma elimu ya awali nchini.

“Hatutakubali taasisi yoyote inayotaka kujihusisha na masuala ya elimu nchini kutumia raslimali kubwa katika maeneo ya aina moja tu ya kujenga uwezo na kwenye masuala ya advocacy (ushawishi) na kuaacha kwenda kwenye matatizo ya kweli ambayo yanawakabili watoto, hasa haya maeneo ya watoto wa shule za awali,” amesema Naibu Katibu Mkuu na kuongeza:
“Kwasababu eneo hili bado hatujawekeza vya kutosha, kwa hiyo tunawataka wadau wote waje kutusaidia pale kwenye miradi mbalimbali inayohusiana na elimu ya awali kwa kutujengea angalau darasa moja kwa ajili ya choo na elimu ya awali.”

Naibu Katibu Mkuu amesema kuwa serikali sasa imeazimia kuhakikisha kuwa watoto wote walio ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanapata fursa ya kupata elimu ya awali, elimu ya msingi, na elimu ya sekondari bila ya vikwazo vyovyote.

Pia bwana Nzunda amewataka jamii na wazazi waendelee kuchangia elimu hasa katika maeneo ya chakula cha watoto wao wanapokuwa shuleni kama wanavyowajibika kuwapatia chakula watoto wao wanapokuwa majumbani kwao.

“Lengo ni kuwawezesha watoto wetu wawapo shuleni angalau wapate uji na chakula cha mchana ili waweze kusoma vizuri na kuchangamka wawapo madarasani,” amesema.

Sambamba na hilo, jambo la pili ambalo Naibu katibu Mkuu amelisisitiza ni kuwataka jamii na wazazi kuisadia serikali kwenye miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali na wadau wa maendeleo kwa kuanza kujenga maboma kwa ajili ya watoto wanaosoma kwenye elimu ya awali,
Ameongeza kuwa kukamilika kwa maboma hayo kutawawezesha watoto wa elimu ya awali kuchangamka, wanajifunza mbinu za maisha, wanajenga mbinu za namna ya kuhusiana, wanajenga misingi ya utu, upendo, na furaha miongoni mwa watoto.

“Kwa kufanya hivi ninaamini tunaenda kujenga taifa la watoto wanaojitambua ambao wamejengewa misingi mizuri, tofauti na hao tutakuwa tunapoteza nchi na taifa,” amesisitiza Naibu Katibu Mkuu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Children in Crossfire bwana Craig Ferla alimweleza Naibu Katibu Mkuu kuwa taasisi hiyo kwa kushirikiana na asasi ya kiraia ya TAHEA watajenga madarasa 100 ya aina hiyo katika mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dodoma katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Pia ameelezea kufurahishwa kwake kwa jinsi uongozi wa juu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, mkoa wa Mwanza, halmashauri ya wilaya ya Misungwi, na kata za Mamae na Magaka kwa jinsi walivyompa ushirikiano katika kufanikisha ujenzi wa madarasa hayo changamshi ya elimu ya awali katika wilaya ya Misungwi.

Bwana Craig amemhakikishia Naibu Katibu Mkuu kuwa Children in Cross fire pamoja na TAHEA wana nia njema ya kuchangia maendeleo ya Tanzania.

“Tunaamini kwamba hawa watoto wetu ambao ndiyo wako kwenye madarasa ya awali ndiyo taifa la kesho na tunaamini kuwa kama watapata mwanzo bora, wataweza kuchangia maendeleo ya taifa letu kwa ufanisi wa hali ya juu,” amesema.

MKOA WA KAGERA WATEKELEZA ILANI YA CCM KWA 85% 2015 - 2020 .

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV - Kagera.

Serikali ya Mkoa wa Kagera imeendelea kutekeleza kwa vitendo ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 - 2020 kwa kuhakikisha wakazi wa Mkoani Kagera wanaondokana na hali duni kwa maendeleo endelevu.

Akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, mbele ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, amesema kuwa Mkoa wa Kagera kwa ujumla umeendelea kuhakikisha unajikwamua kiuchumi kwa kuweka miundo mbinu sahihi katika kila sekta, ili kufanya mazingira rafiki kwa mwananchi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

Mhe. Gaguti amesema pato la Mkoa limeongezeka kupitia makusanyo ya Halmashauri za Wilaya na kufanya mapato ya Mkoa kufikia shilingi Bilioni 48.747 kwa mwaka 2018/19 ukilinganisha na makusanyo ya shilingi Bilioni 44.162 kwa mwaka wa fedha 2017/18. 

Aidha katika sekta za Afya, Uvuvi, Kilimo, Elimu Mkoa umendelea kutekeleza Ilani kwa kuweka mazingira bora kwa kuendeleza ujenzi wa zahanati, vituo vya Afya na Hospitali tatu mpya za Wilaya, sambamba na ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu maabara na Vyuo vya Ufundi VETA.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Bi. Costancia Buhiye akisisitiza jambo mara baada ya Kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-20 kwa Mkoa wa Kagera.
 Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mhe. Gaguti  wakati akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani katika ukumbi waHalmashauri ya Bukoba.
 Pichani ni Mbunge wa Viti maalum Kagera anaewakilisha Vijana Mhe. Halima Bulembo akichangia taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM Mkoa wa Kagera, kubwa akisisitiza ujenzi wa kituo kikubwa cha Uwekezaji Mkoa wa Kagera.
 Pichani Mweyekiti wa CCM (W), Bukoba Ndg. Joas Muganyizi Zachwa akitoa shukrani zake kwa Utekelezaji wa Ilani zaidi akiomba marekebisho upande wa sekta ya Afya.
Pichani ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera wakiendelea kufuatilia mkutano wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani 2015-20

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWATAKA VIJANA KUENZI MCHANGO WA BABA WA TAIFA

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Viongozi, Watumishi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na wakazi wa Marangu wakati wa hafla fupi ya kuwaaga vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kumbukizi ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba akielezea jambo kwa vijana 8 walioshiriki katika shughuli hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Kushoto ni Mkurugenzi wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Mwanaidi Ali.
Baadhi ya Watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuwaaga vijana hao.
Sehemu ya Vijana wanaotarajiwa kupanda Mlima Kilimanjaro kwa awamu ya pili wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima huo, Julai 26, 2019.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akimkabidhi Bendera ya Taifa Kiongozi wa msafara huo Bw. Agustine Gusha mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo iliyofanyika Mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (wenye kofia ya Bluu) akiwasindikiza vijana hao kuashiria kuanza kwa safari yao ya kupanda Mlima huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akiwaaga Vijana hao nane (8) kutoka Mkoa wa Songwe, Arusha, Tanga, Kaskazini Unguja na Kusini Unguja alipowasindikiza vijana hao waliokuwa wakipanda Mlima huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Warioba.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuwaaga vijana kutoka Mkoa wa Songwe, Arusha, Tanga, Kaskazini Unguja na Kusini Unguja kabla ya kupanda Mlima huo.
Kamishna Mwandamizi wa Kanda ya Kaskazini, Herman Batiho akimfafanulia Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (kulia) kuhusi hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, alipowasilia Mkoani huo kwa lengo la kuwaaga vijana hao.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akielezea kuhusu vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro kwa awamu ya pili ikiwa ni ishara ya kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (kulia) akijadili jambo na Kamishna Mwandamizi wa Kanda ya Kaskazini, Herman Batiho alipowasili katika hifadhi hiyo kwa lengo la kuwa kuwaaga vijana waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa awamu ya pili.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro, alipowasilia Mkoani huo kwa lengo la kuwaaga vijana hao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghirwa alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuelekea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
………………….
Na; Mwandishi Wetu
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (Mb) amewataka vijana kuenzi mchango wa Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuwa wazalendo na wenye mshikamano katika kujenga Taifa.
Mhe. Mavunde amesema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga vijana kutoka Mkoa wa Songwe, Arusha, Tanga, Kaskazini Unguja na Kusini Unguja kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyerere iliyofanyika Mkoani Kilimanjaro katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).
Alisema kuwa vijana wanapaswa kuwa wazalendo kwa kuiga kivitendo yale yote yaliyotendwa na waasisi wa taifa hili, Mwl. Julius K. Nyerere na Hayati Mzee Abeid Karume kwa kuendelea kudumisha upendo, amani na mshikamo kwa mustakabali wa Taifa.
“Vijana waliowengi kipindi hiki wameweka pembeni uzalendo wa kulipenda taifa lao hali ambayo inatubidi tujitahmini na kuenzi falsafa walizokuwa nazo waasisi wetu ambao waliweka maslahi ya Taifa mbele wakati wote,” alisema Mavunde
Akitolea mfano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kuwatumikia wananchi kwa kutekeleza masuala mbalimbali ya kitaifa wakati wote ili nchi isonge mbele kimaendeleo.
Pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza vijana waliopanda mlima huo awamu ya kwanza na awamu hii ya pili kwa kuonesha ushujaa na uzalendo kwa Taifa lao ikiwemo kuwa mabalozi wazuri katika kutangaza sekta ya utalii.
Aidha, Naibu Waziri Mavunde alitoa wito kwa vijana kuacha kukaa kwenye vijiwe na kujihusisha kwenye mambo yasio na tija, bali wajishughulishe kwenye miradi mbalimbali itakayo wawezesha kiuchumi na kusaidia kukua kimaendeleo, kwa kuwa waasisi wa taifa walikuwa wachapakazi, waadilifu na wabunifu ambao ni mfano mzuri wa kuigwa.
“Hakuna nchi yoyote dunia ambayo inaweza kuendelea pasipo kuhusisha nguvu kubwa ya vijana katika maendeleo ya taifa,” alieleza Mavunde
Aliongeza kuwa ili kufikia malengo kwenye uchumi wa viwanda ni lazima vijana wazingatie uzalendo, utaifa na bidii katika kazi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba alisema kuwa kitendo cha vijana hao kushiriki katika kupanda Mlima huo ni jambo muhimu kwa taifa na inaashiria namna gani vijana wameanza kutambua historia ya waasisi wa taifa lao.
Naye, Kiongozi wa Vijana hao waliopanda Mlima Kilimanjaro Bw. Augustine Gusha aliunga mkono maelezo yaliyotolewa na Naibu Waziri na alitumia nafasi hiyo kuwasihi vijana kudumisha amani ya nchi wakati wote.
Katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana inaratibu shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa Vijana 100 kwa ajili ya kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Awamu ya kwanza vijana walipanda mlima huo tarehe 26 Machi, 2019 na awamu ya pili 26 Julai, 2019. Awamu ya Tatu itakuwa mwezi Oktoba.

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA DAR ES SALAAM KWA TRENI YA TAZARA AKITOKEA KWENYE SHEREHE ZA UWEKAJI JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA UMEME WA MW 2,115 RUFIJI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli akiagana na dereva wa treni ya TAZARA iliyomchukua kwenda na kurudi kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Mradi wa kuzalisha umeme MW 2,115 wa Rufiji katikati ya mkoa wa Pwani na Morogoro Ijumaa Julai. 26, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa TAZARA alipowasili stesheni ya Dar es salaam baada ya kwenda na kurudi kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Mradi wa kuzalisha umeme MW 2,115 wa Rufiji katikati ya mkoa wa Pwani na Morogoro Ijumaa Julai. 26, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na wananchi katika stesheni ia Kisaki wakati akiondoka kwa treni ya TAZARA iliyomchukua kwenda na kurudi kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Mradi wa kuzalisha umeme MW 2,115 wa Rufiji katikati ya mkoa wa Pwani na Morogoro Ijumaa Julai. 26, 2019
PICHA NA IKULU

Serikali Kutumia Maji ya Ziwa Victoria Kumaliza Tatizo la Maji Kanda ya Ziwa

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akifungua maji mara baada ya kuzindua Mradi wa Maji wa Bulugala katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bulugala katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita.

Kaimu Meneja RUWASA Wilaya ya Mbogwe, Mhandisi Daudi Amlima akisoma taarifa kwa Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso inayohusu Mradi wa Maji wa kisima kirefu wa Iboya uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Bulugala katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mbogwe, Augustino Masele.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi mkoani Geita.
…………………
Serikali imejipanga kuachana na uchimbaji wa visima na kutumia maji ya Ziwa Victoria kikamilifu kwa ajili ya kupeleka huduma ya maji kwa wananchi kama suluhisho la muda mrefu la kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji.

Naibu Waziri Aweso amesema Wizara ya Maji imeweka mkakati maalum wa kutumia moja kwa moja maji ya Ziwa Victoria hususan kwa eneo la Kanda ya Ziwa baada ya visima, ambavyo vimekuwa na changamoto mbalimbali zinazosababisha miradi yake mingi kutokuwa endelevu kwa kuwa maji yake si ya uhakika.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Iboya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita, Naibu Waziri Aweso amesema hakuna sababu ya kuendelea kuchimba visima kwa ajili ya wananchi waishio karibu na Ziwa Victoria wakati wana chanzo cha uhakika chenye maji ya kutosha.

‘‘Tumeweka mkakati wa kutumia Maji ya Ziwa Victoria na vyanzo vingine kikamilifu kupeleka huduma ya majisafi na salama kwa wananchi, mpaka sasa kwa uchache tumefanikiwa kufikisha maji kwenye mikoa ya Shinyanga, Simiyu na tunaendelea na utekelezaji wa mradi mkubwa utakaopeleka maji kwenye miji ya Nzega, Igunga na Tabora Mjini kwa kutumia maji ya Ziwa Victoria, Naibu Waziri Aweso amesema.

‘‘Hakuna sababu ya kutumia fedha nyingi kwa kuchimba visima wakati tuna vyanzo vingi vya maji juu ya ardhi kwenye maeneo mbalimbali, ukiacha maeneo yaliyo na uhaba wa vyanzo vya juu ya ardhi amb. Tumejipanga vizuri kutumia maji ya Ziwa Victoria, mito na maziwa mengine kumaliza tatizo la maji kaaytika Wilaya ya Mbogwe na maeneo mengine’’, Naibu Waziri Aweso amefafanua.

Aidha, Naibu Waziri wa Maji, Aweso amezindua Miradi ya Maji ya Lulembela na Bulugala yenye gharama ya zaidi Shilingi milioni 517 katika Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe inayohudumia wananchi 7,615.

Maafisa Michezo Nchini Watakiwa Kusimamia Michezo na Sio Kukaa Ofisini

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza
akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kongamano la wadau wa michezo mkoani Mtwara (hawapo pichani) wakati Naibu Waziri huyo alipofungua kongamano la siku mbili mapema hii leo Julai 26,2019 mjini Mtwara.
Baadhi ya wajumbe wa kongamano la wadau wa michezo mkoani Mtwara
wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Juliana Shonza (hayupo pichani) wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa akifunguakongamano la wadau wa michezo mapema hii leo Julai 26,2019 Mjini Mtwara.






Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA), Edward Kapopo akisisitiza jambo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (hayupo pichani) wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa akifungua kongamano la wadau wa michezo mapema hii leo Julai 26,2019 Mjini Mtwara.


Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA), Edward Kapopo (kulia) akimkabidhi mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza risala ya chama hicho wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa akifungua kongamano la wadau wa michezo mapema hii leo Julai 26,2019 Mjini Mtwara.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia)akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini, Evodi MManda wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa akifungua kongamano la wadau wa michezo mapema hii leo Julai 26,2019 Mjini Mtwara.

***************

Na. WHUSM -Mtwara

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amewatakamaofisa Michezo kote nchini kusimamia michezo na sio kukaa maofisini wakisubirimashindano ya UMISHUMTA.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku mbili la wadau wa michezo mkoani Mtwara, Naibu Waziri Shonza ametoa rai kwa wajumbe kuhakikisha wanatumia siku hizo kwa kujadili changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo ya michezo.

“Ndugu washiriki, kutokana na umuhimu wa mafunzo haya ni vyema mtakapohitimisha muweke maazimio, Maafisa Michezo mpo hapa, hakikisheni maazimio yakongamano hili yanawasilishwa Idara ya Michezo kwa ajili ya kufanyiwa kazi,” Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara(MTWAREFA), Edward Kapopo, amemuomba Naibu Waziri, Shonza kuwapatia maeneo kwa ajili ya kujenga vituo vya michezo ambavyo vitasaidia kukuza soka katika ukanda wa Kusini.

“Mheshimiwa Naibu Waziri, kituo cha Viva Soccer Academy kwa sasa tuna ofisi tuhivyo tunalazimika kukodisha au kuomba maeneo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za michezo,” alisema Bw.Kapopo.

Aidha, Naibu Waziri, Shonza ameiomba Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara kuona namna ya kukisaidia kituo hichbo kwa kuwapatia eneo litakaloendelezwa kwa ajili ya shughuli za michezo ili kuwa kitovu cha kuzalisha vipaji vya mpira wa miguu ukanda wa Kusini.

Kongamano hilo limewakutanisha maafisa michezo, viongozi wa vyama vya mpira wa miguu, walimu, waamuzi, wachezaji na waandishi wa habari za michezo ambapo watapata fursa ya mafunzo kwa wawezeshaji toka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na wadau mbalimbali wanaojishughulisha nampira wa miguu hapa nchini.

BRIGEDIA JENERALI MKEREMY ATUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA

$
0
0
 Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy akiwa na familia yake (juu) pamoja na Dr Lucy Shule wa NDC  (Kulia) na Dr Vicensia Shule wa UDSM (chini) mara baada ya Brigedia Jenerali Mkeremy kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) leo Jumamosi Julai 27, 2019. Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo yaliyofanyika Chuo Cha Ulinzi Kunduchi jijini Dar es salaam alikuwa Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan

ULINZI KUIMARISHWA KATIKA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA

$
0
0
Mhandisi Burton Komba (wanne kulia) anayesimamia mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB3), akimweleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Hamad Masauni (mwenye suti) alipotembelea jengo hilo hivi karibuni.
Afisa Usalama Mwandamizi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Ramadhani Mkumbukwa (aliyenyoosha mkono), akimweleza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (wapili kulia) namna ya ukaguzi wa abiria na mizigo unavyofanyika wakiwa kwenye jengo la tatu la abiria la JNIA hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (mwenye suti), akionyesha jambo akiwa kwenye eneo la ukaguzi wa abiria na mizigo wakati alipotembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa la Julius Nyerere (JNIA TB3) hivi karibuni.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (kulia) akiongozana na maafisa wa ulinzi na usalama kukagua sehemu za kupitisha mizigo kwenye Jengo la tatu la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa la Julius Nyerere (JNIA TB3), alipofanya ziara hivi karibuni.
………………..

Na Mwandishi Wetu

Wizara ya Mambo ya Ndani nchini, itaongeza askari watu na mbwa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama kwenye viwanja vya Ndege nchini.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Hamad Masauni amesema hayo alipofanya ziara ya kikazi katika Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB3).

Masauni amesema serikali inatarajia kuongeza askari mbwa wengi wenye mafunzo na sifa, ili kuongeza ufanisi na ulinzi wa viwanja vyote vya ndege.
“Idadi ya mbwa inatakiwa iongezwe hasa inapokaribia kuhamia kwenye jengo jipya la tatu la abiria, ambalo litakuwa na idadi kubwa ya abiria na changamoto nyingi, pia kwa viwanja vingine navyo vitaangaliwa kwa suala la ulinzi,” alisema Masauni

Hatahivyo, amesema hatasita kukifuta kitengo cha mbwa endapo hakutakuwa na mbwa wa kukidhi mahitaji na wenye sifa zote, kwani kwa sasa askari binadamu ni wengi zaidi.

Ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kuhakikisha mfumo na ushiriki wa askari wake unaweza kuboreshwa na wale wanapelekwa viwanja vya ndege wawe na sifa na vigezo maalum vya kuweze kubaini vitu kama nyara za serikali, madini na madawa ya kulevyia.
“Hii itasaidia kwa kuwa na mfumo wa pamoja wa ushirikiano katika udhibiti, jingine ni kuhakikisha IGP analisimamia na kulitekeleza kwa haraka sana, kwani tumekuwa na askari mbwa waliopata mafunzo maalum ya kubaini vitu mbalimbali vinavyopitishwa kwenye viwanja vya ndege, hivyo maelekezo yangu kwake tuongeze idadi ya mbwa wenye sifa hapa JNIA ili kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,” alisema Masauni.

Masauni amefanya ziara hiyo siku moja baada ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kushughudia makabidhiano ya kilo 35.267 za dhahabu zilizokamatwa Februari 15, 2019 katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya.

WAZIRI WA AFYA HAMAD RASHID APOKEA MSAADA WA VIFAA TIBA ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akipeana mikono na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifat Sheikh Abdalla Hadhar Abdalla ikiwa ni ishara ya kupokea kwa Msaada wa Vifaa Tiba vilivyotolewa na Jumuia hio wakishirikiana na Shirika la H,H,R,D kutoka Marekani hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Mnazi mmoja Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akimpandisha Mtoto Sulhia Idi Nassor ambae ni Mlemavu katika kigari katika hafla ya makabidhiano ya Vifaa Tiba vilivyotolewa na Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat wakishirikiana na Shirika la H,H,R,D kutoka Marekani hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Mnazi mmoja Zanzibar.



Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifat Sheikh Abdalla Hadhar Abdalla akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Msaada wa Vifaa Tiba uliotolewa na Jumuiya wakishirikiana na Shirika la H,H,R,D kutoka Marekani hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.Naibu Katibu wa Jumuiya ya Wazee(JUWAZA)Kombo Mohamed Khamis akielezea kuhusiana na kupatiwa misaada mbalimbali kwa Wazee na Walemavu katika hafla ya makabidhiano ya Msaada wa Vifaa Tiba kutoka Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat wakishirikiana na Shirika la H,H,R,D kutoka Marekani hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitoa hotuba katika hafla ya makabidhiano ya Msaada wa Vifaa Tiba kutoka Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat wakishirikiana na Shirika la H,H,R,D kutoka Marekani hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Mnazi mmoja Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images