Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live

Wajumbe wa Bodi Zanzibar waipongeza Mloganzila

$
0
0

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth
Magandi (kulia) akizungumza na viongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar ambao leo wametembelea Hospitali ya Mloganzila kwa lengo la kujifunza muonekano na upangaji wa huduma katika hospitali za kisasa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mnazi Mmoja Dkt. Abdulwakil Idrisa Abdulwakil.Viongozi wa Hospitali ya Mmnazi Mmoja Zanzibar wakiwa katika
mkutano kabla ya kuanza kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali. 
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi MNH- Mloganzila Mhandisi Andrew
Fungamali (katikati) akielezea kuhusu mfumo wa maji na mfumo wa kuzima moto unavyofanya kazi. 
Kiongozi kutoka kitengo cha usafishaji damu MNH-Mloganzila
Nurdin Mtumbuka (aliyesimama katikati) akiwaeleza viongozi wa Hospitali ya Mmnazi Mmoja kuhusu utoaji wa huduma ambapo kitengo hicho kina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 36 kwa siku. 
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Redemptha Matindi
(aliyesimama katikati) akizungumzia huduma zinazopatikana katika wodi ya wagonjwa mashuhuri katika Hospitali ya Mloganzila.Baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Mloganzila na Mmnazi Mmoja
Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutembelea maeneo mbalimbali ya hospitali hii leo. 

******************* 

Wajumbe wa Bodi Zanzibar waipongeza Mloganzila
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila- imewekea mikakati mbalimbali ya
kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwemo
huduma za kibingwa na kibobezi. 

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa
Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi wakati akizungumza na viongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar ambao wamefanya ziara ya siku moja katika Hospitali ya Mloganzila kwa lengo la kujifunza muonekano na upangaji wa huduma katika hospitali za kisasa. 

Ujumbe wa viongozi hao umeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali hiyo Dkt. Abdulwakil Idrisa Abdulwakil.  Dkt. Magandi amesema dhamira ya hospitali ni kuwawezesha wananchi wengi
kupata huduma za kibingwa sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali za kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi. 

Pia amesema idadi ya wagonjwa katika Hospitali ya Mloganzila inaendelea
kuongezeka ambapo katika kipindi cha Oktoba mwaka jana wagonjwa wa nje walikua takribani 200 kwa siku lakini kwa sasa wanafikia wagonjwa 500 kwa siku huku wagonjwa wa ndani wakiongezeka kutoka 100 mpaka zaidi ya 300. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Mnazi
Mmoja Dkt. Abdulwakil Idrisa Abdulwakil ameshukuru ushirikiano uliopo na
kueleza kuwa Hospitali ya Mloganzila na Mnazi Mmoja wamekuwa na ushirikiano wa karibu wa kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali ikiwemo huduma ya kusafisha damu na huduma ya mama na mtoto.

MSAFARA WA TTB NCHINI CHINA WAZIDI KULETA MATUNDA

$
0
0
Mkurugenzi ya mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi. Devota Mdachi (Kushoto) akizungumza na ndugu Qui Yu (katikati) ambaye ni Mtendaji wa kampuni ya Tibet Dexin International Financial Leasing Co. Ltd (TDIFL) ya China na Bi Xiao Xinzhu (Kulia) katibu wa TDIFL punde walipowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Julai, 2019. Haya ni matunda ya msafara wa kutangaza vivutio vya utalii uliyofanywa na TTB nchini China mwezi Novemba 2018. 

Kampuni ya TDIFL inayomilikiwa na Serikali ya jimbo la Sichuan nchini china imeonyesha nia ya kuwekeza katika sekta ya utalii na usafiri wa anga ambapo inatarajia kujenga hoteli za kitalii zenye hadhi ya nyota Tano (5) katika maeneo ya Hifadhi ya Ngorongoro na Karatu ambazo zitakazo gharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 100. 

Aidha, kwa upande wa usafiri wa anga, TDIFL inatarajia kushirikiana na Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) kuanzisha safari za moja kwa moja kutoka Tanzania (Dar es Salaam/Kilimanjaro) kwenda kwenye mji wa Chengdu uliyopo katika jimbo la Sichuan la nchini China.

THE TRENDY SHOW BY CYNTHIA MASASA MZIRAY WITH LE MUTUZ

MARAIS 16 KUKUTANA TANZANIA MKUTANO WA 39 WA SADC

$
0
0
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji na mwenyekiti wa mkutano wa 39 wa jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC utakaofanyika mwezi Agosti mwaka 2019 jijini Dar es salaam. Mkutano huo utatanguliwa na vikao vya awali kwaajili ya maandalizi na kutangulia kwa wiki ya maonyesho ya bidhaa za ndani ujulikanao kama wiki ya viwanda ya SADC 22-26 Julai. Mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa nchi 16 zinazounda jumuiya ya SADC. Mara ya mwisho nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo ilikuwa mwaka 2003 ambapo Rais Benjamini Mkapa alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo.

WIKI YA UWEKEZAJI MKOANI KAGERA

WAZIRI MHANDISI KAMWELWE ATOA MIEZI MITATU KWA TEMESA KUTOPELEKA MAGARI YA SERIKALI GEREJI BINAFSI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ametoa miezi mitatu kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kutopeleka magari ya Serikali kwenye karakana binafsi kwani Wakala unajitosheleza kwa kuwa na wataalamu  na vifaa vya kutosha.

Mhandisi Kamwelwe, amesisitiza kwa Wakala huo kuhakikisha  unatengeneza magari kwa bei nafuu na muda na mfupi ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wateja wao.

Waziri Mhandisi Kamwelwe ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na uongozi pamoja na wafanyakazi wa Wakala huo ambapo pamoja na mambo mengine alikagua vitendea kazi vya kisasa vilivyofungwa katika karakana ya MT. Depot iliyopo jijini hapo.

"Ninyi ni taasisi ya Serikali fanyeni vitu viwe nafuu na mtengeneze kwa viwango ili watu wafurahie huduma zenu", amesisitiza Waziri Mhandisi Kamwelwe.

Aidha,  ametoa wito kwa Wakala huo kutoa ushauri wa magari ya Serikali kwa umahiri na weledi na kutokubali kutengeneza magari ya Serikali endapo gari hilo litaonekana gharama yake  ni sawa na kununua gari nyingine.

Waziri Kamwelwe ameupongeza Wakala huo kwa kupunguza gharama za kutengeneza taa za barabarani ambazo zinatumia mfumo wa dakika. 

"Wakala umetumia kiasi cha shilingi milioni 150 katika kitengeneza taa hizo badala ya milioni 250 na tayari zimeanza kufungwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo mkoa wa Morogoro" amesema Waziri Kamwelwe.

katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2019/20 Waziri Kamwelwe amefafanua kuwa Serikali imetenga kiasi cha Shilingi milioni 800 kwa ajili ya kununua boti za uokoaji kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kwa urahisi katika visiwa vya Ukerewe (Ilugwa, Nafuba na Gana).

Awali akitoa taarifa ya utendaji kazi wa TEMESA kwa Waziri huyo, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Masele, amemueleza kuwa Wakala umejipanga kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20 kuanzisha karakana katika ngazi za Wilaya ikiwemo Wilaya ya Kahama, Simanjiro, Same, na Chato lengo likiwa ni kupeleka huduma karibu na wateja hasa kwa walio mbali na karakana za mikoa.

Ameendelea kueleza kuwa hadi sasa Wakala umeshafanya uwekezaji wa shilingi bilioni 66 kwa ajili ya kununua vivuko 18 na hivyo kufanya kufikia jumla ya vivuko 31 na boti ndogo tano hapa nchini.

Kuhusu kukamilisha ujenzi wa vivuko  nchini Mhandisi Masele amesema kuwa tayari wakala umekamilisha ujenzi wa kivuko kipya cha MV Mwanza kinachotoa huduma eneo la kigongo-Busisi, ujenzi wa miundombinu katika kivuko cha Lindi Kitunda na inaendelea kukamilisha ujenzi wa Kivuko cha Kayenze- Bezi kitakachotoa huduma kati ya Kayenze na kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza.

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ulianzishwa chini ya sheria ya Wakala Na.30 ya mwaka 1997 ikiwa na majukumu ya kufanya matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali, matengenezo ya usimikaji wa mifumo ya umeme, uendeshaji wa vivuko vya Serikali, utoaji huduma za ukodishaji wa mitambo ya Serikali, kufanya usanifu na usimamizi wa usimikaji wa mifumo ya uhandisi wa mitambo, umeme na elektroniki

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua vitendea kazi vya kisasa vilivyofungwa katika karakana ya MT. Depot iliyopo jijini Dar es Salaam inayosimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), wakati alipofanya ziara ya kikazi katika karakana hiyo, mkoani humo.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Masele, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, kuhusu taa za barabarani zinazotumia mfumo wa dakika zinazotengenezwa na Wakala huo katika karakana ya MT. Depot ya jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kikazi katika karakana hiyo, mkoani humo.
 Muonekano wa vyuma vinavyotumika katika utengenezaji wa taa za barabarani zinazotengenezwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizungumza na menejimenti na wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi na Umeme Arch. Edwin Nnunduma,  akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


STEPHANIE SILAS KAAYA NA ROBERT FRANCIS LOWASSA WAMEREMETA ARUSHA

AIR TANZANIA YAZINDUA SAFARI YA KWANZA YA MUMBAI

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Isaack Kamwelwe akikata keki wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa safari ya Mumbai nchini India kwa ndege ya Air Tanzania ikiwa ni safari ya kwanza kwa ndege za Air Tanzania kutoka nje ya Bara la Afrika na ni safari ya moja kwa moja kutokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Ndege ya kwanza ya Air Tanzania imeondoka Julai 17, 2019 kuelekea Mumbai, nchini India.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Isaack Kamwelwe akikata utepe wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa safari ya Mumbai nchini India kwa ndege ya Air Tanzania ikiwa ni
safari ya kwanza kwa ndege za Air Tanzania kutoka nje ya Bara la Afrika na ni safari ya moja kwa moja kutokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Ndege ya kwanza ya Air Tanzania imeondoka Julai 17, 2019 kuelekea Mumbai, nchini India.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Air Tanzania, Ladislaus Matindi akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa safari ya Mumbai nchini India kwa ndege ya Air Tanzania ikiwa ni safari ya kwanza kwa ndege za Air Tanzania kutoka nje ya Bara la Afrika na ni safari ya moja kwa moja kutokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Ndege ya kwanza ya Air Tanzania imeondoka Julai 17, 2019 kuelekea Mumbai, nchini India.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Isaack Kamwelwe akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa safari ya Mumbai nchini India kwa ndege ya Air Tanzania ikiwa ni safari ya kwanza kwa ndege za Air Tanzania kutoka nje ya Bara la Afrika na ni safari ya moja kwa moja kutokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Ndege ya kwanza ya Air Tanzania imeondoka Julai 17, 2019 kuelekea Mumbai, nchini India.

WAZIRI UMMY ATOA MIEZI 3 KUKAMILISHA MRADI WA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA GEITA

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wakatikati) akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (Kulia kwa Waziri Ummy) wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wapili kushoto) akipokea maelezo ya ujenzi kutoka kwa Mhandisi kutoka Wizara ya Afya Eng. Mbuya (wakwanza kushoto) wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita,
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (watatu kushoto) akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (wakwanza kushoto) pamoja na Mhandisi kutoka TBA (wapili kushoto) wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita,
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyevaa kitambaa) akitoa maelekezo kwa Mhandisi kutoka Wizara ya Afya Eng. MBuya wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel
Baadhi ya miradi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita yenye thamani ya shilingi Bilion 2.5 inayotarajia kumalizika ndani ya miezi mitatu
……………….

Na WAMJW- GEITA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi wa Hospitali za Rufaa za mikoa nchini.

Katika ziara hiyo Waziri Ummy amemwagiza Mkandarasi kutoka TBA Mkoa wa Geita kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ndani ya miezi mitatu mradi huo unaisha ili huduma za Afya zianze kutolewa ifikapo Disemba 1, 2019.

“Nimemtaka Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana ikiwezekana tukamilishe ujenzi huu hata mwezi wa kumi mwishoni, lengo langu nataka tarehe 1 mwezi Disemba 2019, tunaanza kutoa huduma hapa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita” alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilion 2.5 ili kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali hiyo, ambayo itajenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la Maabara, jengo la upasuaji pamoja na jengo la mionzi.

Hata hivyo, Waziri Ummy amesema kuwa licha ya kuwepo changamoto ya upungufu wa Watumishi katika Sekta ya Afya, Wizara ya Afya imepata kibali cha kuajiri Watumishi wengine kutoka Wizara ya Utumishi jambo litalosaidia kupunguza Uhaba wa Watumishi katika Sekta ya Afya.

Waziri Ummy aliendelea, kwa kuwataka Wakurugenzi kujiongeza ili kupambana na uhaba wa Watumishi katika ngazi ya Mkoa, ikiwemo kuajiri baadhi ya Watumishi kupitia mapato ya ndani ili kupunguza changamoto ya uhaba wa Watumishi, huku akitoa Wito kwa vijana waliomaliza vyuo kujitolea katika Hospitali ili kuongeza uzoefu zaidi.

Mbali na hayo, Waziri Ummy amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuendelea kujali Afya za Watanzania kwa kuboresha Sekta ya Afya ikiwemo kuboresha miundombinu ya Hospitali na kuhakikisha Dawa, vifaa na vifaa tiba vinapatikana.

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amemuomba Waziri Ummy kuanza kwa awamu ya pili ya ujenzi wa Hospitali hiyo ili kupata wodi ambazo zitatumika kulaza wagonjwa wataofika kupata huduma za Afya.

“Uwepo wa wodi ndio utatoa taswira ya kuwa Hospitali hii kuwa ni Hospitali ya Mkoa, ili mtu akipata Rufaa aweze kulazwa na kuchukuliwa vipimo” alisema Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel.

JAMII YATAKIWA KUWAWEZESHA WATOTO WA KIKE KWENYE SANYANSI NA TEKNOLOJIA KWA MAENDELEO YA SASA NA BAADAE.

$
0
0
Thami Mseleku Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania akizungumza katatika wiki ya ufunguzi wa wiki ya Nelson Mandela inayoendelea katika Chuo hicho kilichopo Jijini Arusha.
Washiriki wa Maadhimisho Wiki ya Nelson Mandela inayofanyika katika Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela Jijini Arusha.


Na Vero Ignatus,Arusha

Jamii ya Watanzania imetakiwa kuwawezesha watoto wa kike katika masuala ya sayansi Teknolojia ili waweze kuchochea maendeleo katika Bara la Afrika kupitia sayansi na hata kupelekea maendeleo ya viwanda nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.

Thami Mseleku ni Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania amesema hayo katika ufunguzi wa Wiki ya Nelson Mandela inayofanyika katika Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela kilichopo jijini Arusha ambapo ameitaka jamii kuhamasisha na kujikita zaidi katika masomo ya sayansi ambayo yanachochea ugunduzi na uvumbuzi utakaosaidia maendeleo ya Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla.

Profesa Antony Mshandete ni Kaimu Makamu wa Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela amesema kuwa katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa nelson Mandela wanatafakari jinsi ambavyo Ubunifu,Ugunduzi na Uhandisi unachangia kufikia uchumi wa viwanda na kuharakisha maendeleo kwa ujumla.

Linda Mathayo ni mwanafunzi wakike kutoka shule ya Star High Duluti aliyefika katika Wiki ya Mandela amesema kuwa wiki hiyo imewapa hamasa ya kusoma masomo ya sayansi ili waweze kuwa Wahandisi,Marubani na Watafiti na pia kuondoa utamaduni potofu wa kuwa masomo hayo wanayaweza watoto wa kiume peke yao

Dr.Lilian Pasape ni Mhadhiri Mwandamizi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya Mandela amesema kuwa katika wiki ya Mandela watakua na mafunzo Maalumu ya kuhamasisha watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi pamoja kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wanaozunguka chuo hicho.

WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIZINGA WILAYANI MULEBA

$
0
0
Taswira ya nyumba ya mkazi wa Kijiji cha Kizinga, wilayani Muleba, Venancia Joanes, kama ilivyonaswa muda mfupi kabla ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kuiwashia umeme akiwa katika ziara ya kazi, Julai 17, 2019. 
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kulia), na Mbunge wa Muleba Magharibi Charles Mwijage, wakisikiliza kwa makini salamu kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Siasa, wakati wa hafla ya uwashaji umeme katika kijiji cha Kizinga wilayani Muleba, Julai 17, 2019. 

Sehemu ya umati wa wananchi wa Kijiji cha Kizinga, wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera, wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), muda mfupi kabla hajawasha rasmi umeme katika eneo hilo, Julai 17, 2019.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kulia), na Mbunge wa Muleba Magharibi Charles Mwijage, wakisikiliza kwa makini salamu kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Siasa, wakati wa hafla ya uwashaji umeme katika kijiji cha Kizinga wilayani Muleba, Julai 17, 2019.

********************

Na Veronica Simba – Kagera 

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewasha rasmi umeme katika kijiji cha Kizinga, Kata ya Bulyakashaju wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera Julai 17, 2019 na kuibua shangwe kwa wananchi wa eneo hilo. 

Tukio hilo lilifanyika katika nyumba ya mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Venancia Joanes ambaye alikiri mbele ya Waziri kuwa alilipia shilingi 27,000 tu kama ambavyo Serikali imeagiza kuwa gharama za uunganishwaji umeme vijijini, zisizidi kiasi hicho. 

Akizungumza na wananchi wa Kizinga, Waziri Kalemani aliwataka kuiga mfano wa Mama huyo ambaye pamoja na kuwa na nyumba ya tope, ameunganisha umeme. 

“Wananchi nawasihi muige mfano wa huyu Mama ili nanyi muunganishiwe umeme katika nyumba zenu. Sisi kama Serikali tulikwishaweka wazi kuwa hatubagui aina ya nyumba kwani wananchi wote wanataka maendeleo,” alisema Waziri. 

Katika hatua nyingine, Waziri amekerwa na kukemea utendaji kazi duni wa Mkandarasi aliyekuwa akitekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II), wilayani Muleba na hivyo akaagiza kufanyika mabadiliko ya wasimamizi mbalimbali wa Mradi huo upande wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). 

Waziri alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga kufanya mabadiliko ya watendaji waliokuwa wakisimamia Mradi huo wilayani Muleba kwa lengo la kuboresha utendaji kazi. 

Aidha, aliuagiza Uongozi wa TANESCO kumchukulia hatua za kimkataba Mkandarasi huyo ikiwa ni pamoja na kumkata asilimia 10 ya malipo yake na hata kumfkisha mahakamani ikibidi, kutokana na kutotekeleza Mradi kadri ya makubaliano. 

“Zaidi ya Transfoma 110 katika Mkoa huu zimeharibika na hazijafanyiwa matengenezo, Nguzo nyingi zimechimbiwa lakini hazijafungwa nyaya, mashimo mengi yamechimbwa lakini hayajasimikwa nguzo, baadhi ya maeneo hata Transfoma hazijafungwa. Huu ni uzembe wa hali ya juu na hatuwezi kuuvumilia,” alisema Waziri. 

Waziri alimtaka Meneja wa TANESCO mkoani Kagera, Mhandisi Francis Maze, kuyafanyia kazi maeneo yote yanayohitaji marekebisho ya miundombinu ya umeme hususan nguzo na transfoma, kabla ya mwisho wa mwezi Agosti mwaka huu ili kuwaondolea kero wananchi. 

“Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ametupatia pesa ya kurekebisha miundombinu ya umeme iliyochakaa au kuharibika; na mimi siwezi kupewa pesa halafu nikashindwa kazi. Hivyo nakuagiza Meneja kufikia mwezi wa Nane mwishoni uwe umekamilisha kazi hiyo.” 

Pia, Waziri aliuagiza uongozi wa TANESCO kushughulikia malalamiko aliyopokea kutoka kwa Mbunge wa Muleba Magharibi, Charles Mwijage, kuhusu wananchi walioko visiwani kutozwa gharama kubwa za umeme na wazalishaji binafsi. 

“Fanyeni mapitio ya bei. Bei iwe moja; haitakiwi kutofautiana. Kero hiyo kwa wananchi iishe kufikia mwezi Septemba mwaka huu. Ufikapo muda huo, sitarajii kusikia wananchi wa visiwani wakilalamikia tozo kubwa ya umeme unaozalishwa na watu binafsi,” alisisitiza Waziri. 

Kuhusu maeneo ambayo umeme umepita juu lakini haujashushwa; Waziri alisema Serikali ilishatoa maagizo kwa mameneja wa TANESCO nchi nzima kuainisha vijiji vyote vyenye changamoto hiyo na kuifanyia kazi, hivyo alimtaka Meneja wa Muleba kushughulikia suala hilo kwa haraka. 

Vilevile, Waziri aliagiza wateja wote 5,000 ambao wamelipia umeme katika Mkoa huo lakini bado hawajaunganishwa, waunganishwe ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kutoka hivi sasa. 

Waziri alisisitiza viongozi wa taasisi na miradi mbalimbali ya umma kama vile shule, vituo vya afya, nyumba za ibada, masoko, maji na nyinginezo kutenga fedha za kulipia gharama za kuunganishiwa umeme ili huduma hiyo muhimu ipelekwe katika maeneo hayo.

VIWANDA VYOTE NCHINI SASA KUWA NA TRANSFOMA ZAO

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mwenye miwani) na Ujumbe wake, akizungumza na mwakilishi wa Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoani Kagera, Justin Mrenga (kulia), alipotembelea Taasisi hiyo kukagua uunganishwaji wa umeme, akiwa katika ziara ya kazi, Julai 17, 2019.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kulia), akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti lengo la ziara yake mkoani humo, Julai 17, 2019.

********************

Na Veronica Simba – Kagera.

Serikali imetoa agizo kwa mameneja wote wa mikoa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuhakikisha viwanda vyote nchini vinafungiwa Transfoma mahsusi kwa matumizi ya viwanda pekee pasipo kuchanganya na matumizi ya wananchi.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alitoa agizo hilo jana, Julai 17, 2019 akiwa katika ziara ya kazi mkoani Kagera.Akizungumza na Uongozi wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), mkoani humo, mara baada ya kukagua Transfoma mpya iliyofungwa maalumu kwa matumizi ya Shirika hilo; Dkt. Kalemani alisema hatua hiyo itasaidia kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa viwanda hivyo kuviwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

“Wenye viwanda wawe na Transfoma zao, wasichangie matumizi na wananchi. Mwananchi akiunguza kwake anaathiri Kiwanda pia maana umeme utakosekana kote hivyo uzalishaji unasimama. Haifai.”Vilevile, Waziri aliwaagiza mameneja hao nchi nzima kuhakikisha wanabadilisha miundombinu yote ya umeme ambayo ni mibovu katika maeneo yao mathalani Transfoma, Nguzo, Nyaya na Mita ili kuwaondolea wananchi kero za kukatika kwa umeme mara kwa mara.

“Meneja yeyote ambaye eneo lake litabainika kuwa na Transfoma iliyoungua au kuharibika kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja na hajafanya jitihada yoyote kutatua, Mkurugenzi Mtendaji mchukulie hatua maana ni hasara kwa Shirika,” aliagiza Waziri.

Akifafanua zaidi, alisema miundombinu iliyoharibika isiporekebishwa kwa wakati, husababisha Shirika kupoteza mapato hivyo kuitia hasara Serikali.
Akisisitiza kuhusu agizo hilo, Waziri Kalemani alibainisha kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati, imetenga fedha nyingi kwa ajili ya matengenezo na urekebishaji wa miundombinu mbalimbali ya umeme kwa maeneo yote nchini, hivyo hakuna sababu ya kusuasua katika kutekeleza zoezi hilo.
“Mathalani, kwa Mkoa huu wa Kagera, tumetenga jumla ya shilingi bilioni 9.2 kwa mwaka huu kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu ya umeme,” alibainisha.

Katika ziara hiyo, Waziri alitembelea na kukagua uunganishwaji umeme katika Taasisi ya SIDO eneo la Rwamishenye na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) Tawi la Bulugo wilayani Bukoba, ambapo alikiri kufurahishwa na utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa awali kwa uongozi wa TANESCO, kuzifungia Taasisi hizo Transfoma.Waziri aliambatana na viongozi pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Wizarani, TANESCO na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). 

UJENZI KIVUKO CHA KAYENZE KWENDA KISIWA CHA BEZI MWANZA KUKAMILIKA NOVEMBA 2019

$
0
0
Mkurugenzi wa Songoro Marine Ltd Meja Songoro akimuonesha Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa kwanza kushoto) maendeleo ya ujenzi wa Kivuko cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilika Novemba 2019. 
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akishuka kutoka katika kivuko cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza wakati alipofanya ukaguzi wa kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilika Novemba 2019. 
Mkurugenzi wa Songoro Marine Ltd Meja Songoro akimuonesha Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa kwanza kushoto) maendeleo ya ujenzi wa Kivuko cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilikaNovemba 2019. 
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza ndani ya kivuko cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza na ujumbe alioambatana nao wakati alipofanya ukaguzi wa kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilika Novemba 2019. 
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia kivuko cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza wakati alipofanya ukaguzi wa kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilika Novemba 2019. 
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza wakati alipofanya ukaguzi wa kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilika Novemba 2019. 

Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza wakati alipofanya ukaguzi wa kivuko hicho kinachotarajiwa kukamilika Novemba 2019.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI) 
…………………. 
Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA 
Ujenzi wa kivuko cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza unaogharibu kiasi cha bilioni 2.7 unatarajiwa kukamilika Novemba mwaka 2019. 
Hayo yamebainika juzi wakati Mbunge wa jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipotembelea kivuko hicho kuangalia maendeleo ya ujenzi ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwa wananchi wa jimbo lake wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika 2015. 

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, kivuko cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi chenye uwezo wa kubeba abiria 250, magari 10 na ukubwa wa tani 10 kitaondoa kero ya muda mrefu waliyokuwa wakiipata wananchi wa Kayenze na Bezi katika suala la huduma ya usafiri wa majini. 

‘’Wananchi wa Kisiwa cha Bezi na Kayenze Mwaloni wamekuwa na shida ya usafiri majini kwa muda mrefu na mimi niliahidi kuwapatia kivuko wakati wa uchaguzi mwaka 2015 na ombi langu la kujenga kivuko hicho lilipokelewa vyema na serikali toka mwaka 2016 kwa ahadi ya kujenga kivuko hicho’’ Alisema Dkt Mabula. 

Mbunge huyo wa Jimbo la Ilemela alisema, kuchelewa kukamilika mapema kivuko hicho kulitokana na changamoto kadhaa na mojawapo ni kukwama kwa vifaa bandarini kulikosababishwa na msamaha wa ushuru ambapo hata hivyo, Dkt. Mabula aliahidi kushughulikia suala hilo na kufafanua kuwa Oktoba mwaka 2019 kivuko hicho kitafanyiwa majaribio rasmi kabla ya kukabidhiwa mwezi mmoja baadaye kwa ajili yua kuanza kazi rasmi. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni inayotengeneza kivuko hicho ya Songoro Marine Ltd Meja Songoro alisema ujenzi wa kivuko higho ulioanza Januari 2019 uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji ambapo sasa kampuni yake inakamilisha kufunga mifumo ya maji, umeme, zimamoto , kufunga ingini na vifaa vya kuendeshea kivuko hicho. 

Kwa mujibu wa Songoro, kampuni hiyo ya Songoro Marine Ltd ni mahiri katika kutengeneza vivuko na kutolea mfano wa vivuko vya Mv Mwanza, Kazi pamoja na kile cha Geita kuwa ni vivuko vilivyofanyiwa kazi na kampuni yake na kufafanua kuwa hivi sasa kampuni hiyo imepata kazi za vivuko katika nchi jirani za Kenya na Uaganda.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JULAI 18,2019

Wanafunzi wa sekondari watakiwa kujiandaa kwa masomo ya mitaala

$
0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Wito umetolewa kwa wanafunzi wa sekondari nchini kuona umuhimu wa kujiandaa wao kwa masomo ya mitaala ya vyuo vikuu watakavyochukuwa wakati wa kujiunga kwa kuwa na uelewa wa masomo watakayoyachagua na kuyachukuwa.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya chuo cha Uhasibu kwa wanafunzi wa shule za sekondari 18 za wilaya ya Arusha iliyofanyika chuo hapo jijini Arusha.

Mwaisumbe amesema kujiandaa mapema kunasaidia wanafunzi hao kuzoea mazingira ya masomo ya elimu ya juu kwani wakifanikiwa wanapata uzoefu wa kuzoea fani mbali mbali zinatotolewa na vyuo hivyo.

Amehimiza chuo cha uhasibu kuendeleza maonyesho hayo kwa lengo la kuwaandaa vijana kuweza kufikia ndoto zao za kitaaluma na wasiishie kwenye wilaya ya Arusha pekee na waende mbali zaidi katika mkoa mzima na nchi kwa ujumla.

Awali Mkuu wa chuo cha Uhasibu Prof.Eliamani Sedoyeka amesema kuwa maonyesho hayo yanalengo kubwa la kuwapa nafasi vijana waliopo sekondari kidato cha nne na sita kwa ajili ya kujiandaa kuchukuwa kozi anayopenda itakayomsaida kufikia ndoto zake.

Amesema kwamba maonyesho hayo yatawasaidia wanafunzi hao kukutana na wataalamu na wakufunzi wa chuo hicho pamoja na wanafunzi kujionea taaluma mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho na kubadilisha mawazo ya kufikia elimu ya juu.

Amesema kuwa mwisho wa maonyesho hayo wanatarajia kupata wanafunzi wengi watakaopenda kujinga na mafunzo chuo hapo kama lilivyo lengo la chuo hicho na uwepo wake unategemea wanafunzi kuweza kujiendesha.

Maonyesho hayo pia yamelenga namna ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa lengo la kuwasaidia vijana kuweza kujiajiri na kutotegemea kuajiriwa jambo litakalosaidia azma ya serikali ya uchumi wa kati wa viwanda.
Mkuu wa chuo cha Uhasibu Prof.Eliamani Sedoyeka pamoja na wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe wakisikiliza maelekezo ya mwanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha wakati walipotembelea Maonyesho ya chuo cha Uhasibu kwa wanafunzi wa shule za sekondari 18 za wilaya ya Arusha yanayofanyika chuo hapo jijini Arusha.

Safari ya Kwanza ya Air Tanzania kutoka DAR - MUMBAI

WANANCHI WATAKIWA KUJENGA TABIA YA KUTEMBELEA MAKUMBUSHO ZETU KUJIFUNZA MAMBO MBALIMBALI YA KALE

$
0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Ili kuweza kuongeza kasi kubwa ya jamii kuwa na mazoea ya kutembelea makumbusho na kujionea mambo ya kale sekta ya elimu imeshauriwa kujenga msingi mzuri kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kutoa masomo yanayohusiana na mambo ya kale 

Wito huo umetolewa na afisa elimu wa makumbusho ya azimio la Arusha Mkoani Arusha Godfrey Emanuel wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya umuhimu wa kutembelea makumbusho

Aidha amesema kuwa, jamii imekuwa ikisahau kwenda kujifunza mambo ya kale na kuwaachia wanafunzi jambo linalosababisha kushindwa kufanya ubunifu wa mambo mbalimbali kupitia mambo ya kale

Kwa upande wake mkurugenzi wa makumbusho ya Azimio la Arusha Costantine Misago amesema kuwa kupitia sheria mbalimbali za makumbusho jamii inapaswa kutembelea bila kizuizi chochote na kukaribisha wageni kutoka mataifa mbalimbali kujionea historia mbalimbali zilizofanywa na watu wa kale

Alibainisha kuwa kunamambo mengi ya kale yanapatikana katika makumbusho yetu hivyo ni muhimu wanafunzi wananchi kutembelea makumbusho haya na kujionea mambo mbalimbali yaliofanywa zamani pamoja na yaliogunduliwa na wanasanyansi pamoja na historia mbalimbali za watu wakale

Alisema kuwa kutembelea makumbusho hizi pia zitasaidia kuongezea mapato ,pia aliwasihi wanahabari kutumia kalamu zao kutangaza makumbusho mbalimbali zilizopo nchini nakuwahamasisha wananchi kuwa natabia ya kutembelea wananchi hao 

Makumbusho iliopo jijini Arusha ipo kwenye boma lililojegwa na wajerumani miaka ya 1900 iliokuwa ikitumika kama jengo la utawala na mawasiliano wakati wa ukoloni wa kijerumani na makumbusho haya yalifunguliwa rasmi mnamo mwaka 1987 na kuonyesha historia ya binadamu wa kale ,ikiwepo pamoja na tafiti zilizofanywa katika tafiti zilizofanywa katika bonde maarufu la Olduvai na alama za miguu wa binadamu wa kale za Lawtoli .

Aidha makumbusho haya inafanya maonyesho juu ya entomolojia ambayo huwasilisha baadhi ya wadudu ,ndege,na wanyama pamoja na umuhimu wao kiuchumi ambapo pia ni kivutio kikubwa kwa wageni wanaotembelea makumbusho hayo.

DC KYERWA AMSWEKA NDANI MKANDARASI ALIYESHINDWA KUKAMILISHA MRADI WA MAJI .

$
0
0

Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Kutokana na kushindwa kukamilika kwa wakati mradi wa Maji safi na salama kwa Wakazi wa Eneo la Murongo Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimu amelazimika kumsweka ndani Meneja wa Kampuni ya CSR ambao ndio wanaotekelezaji Mradi wa Maji unaotokana na Mradi Mkubwa wa kufua umeme wa Kikagati - Murongo (Kikagati/Murongo Hydro power Project).

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi Kyerwa kumshikilia na kumuweka chini ya uangalizi kwa muda wa wiki mbili Meneja wa Masoko wa Kampuni ya CSR , Alice Bachuta (34), ambae pia ndiye aliyesaini mkataba, ambapo kwa muda wote huo Kandarasi huyo anatakiwa kufanya linalowezekana kupatikana Maji, au kurudisha hela yote zaidi ya Shilingi Milioni 26 ambayo ni malipo ya awali.

Imebainika kuwa licha ya kandarasi huyo kupewa zabuni hiyo, utendaji kazi wake umekuwa dhaifu kiasi cha kusogeza mbele muda wa kazi zaidi ya Mara mbili, akiomba aongezewe muda wa kukamilisha mradi huo (extension of time), licha ya awali kudai angemaliza kazi yote ndani ya mwezi mmoja. 

Mkandarasi huyo CSR kutoka Jijini Mwanza ameshindwa kukamilisha kwa wakati mradi huo Mkubwa wa kuchimba kisima cha Maji, wenye kugharimu zaidi ya Shilingi Milioni Hamsini na Tatu, ikiwa tayari 50% ya pesa yote imeshalipwa Kwa Mkandarasi huyo na Maji yameshindikana kupatikana, makubaliano yakiwa ni kupatikana Maji ndani ya mwezi mmoja toka Mwezi wa Tatu, mpaka sasa Mwezi wa saba, na kwa kazi yote imefanyika 30% tu.


 Pichani Meneja Masoko kutoka CSR Drilling Co Ltd. Akipanda gari la Polisi kuelekea Kituoni kwa hatua nyingine baada ya DC Mwaimu kuelekeza hivyo.
 Pichani DC Rashid Mwaimu akitoa maelekezo ya kushikiliwa kwa Alice Bachuta (hayupo pichani) mpaka Mradi wa Maji ukamilike vinginevyo atalazimika kurudisha pesa ya awali aliyopewa.
 Pichani ni Alice Bachuta Meneja Masoko na mwakilishi wa Kampuni ya CSR Drilling Co ltd, ambaye pia ndiye aliyesaini mkataba na kupewa kiasi cha pesa Milioni 26 ili kutekeleza Mradi wa Maji Murongo, akiwa ofisini kwa DC Kyerwa akitoa Maelezo yake.
 Kikao Cha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimu kikiwa kimeketi kujadili kero ya Maji na kushindwa kukamilika kwa Mradi wa Maji wa unaotokana na Mradi mkubwa wa Kikagati - Murongo.
 Pichani Gari lenye Mtambo wa Kuchimba Visima virefu la Kampuni ya CSR Drilling Co. Ltd likiwa limetelekezwa kwa muda wa Miezi miwili na Mkandarsi, huku hatma ya Mradi wa Maji kwa wakazi ikiwa haifahamiki.
 Pichani Ni bomba lenye urefu wa Mita Tisa likiwa limezamishwa ardhini sehemu kinapochimbwa kisima, licha ya uhitaji wa bomba hilo ni Mita 100, na hiki ndicho kimefanyika mpaka sasa ingawa Mkandarasi ameshalipwa Milioni 26.
 Pichani ni Eneo unapotekelezwa Mradi wa Maji kwa wakazi wa Murongo, ambapo Mkandarasi Kampuni ya CSR Drilling Co. Ltd ya Jijini Mwanza imeshindwa kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
Pichani ni Binti Mkazi wa Murongo Yasintha John akiteka maji ya kutumia kutoka Mto Kagera kwa ajili ya matumizi ya Nyumbani kama alivyokutwa na Kamera yetu.

 Pichani ni Maji ya Mto Kagera yanayotumiwa na wakazi wa Murongo Wilayani Kyerwa, ambao mpaka sasa wameshindwa kupata Maji safi na salama kutokana na Mkandarasi kushindwa kukamilisha Mradi wa Maji Eneo hilo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasili katika uwanja wa KIA, kwa ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Kilimanjaro, Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).       
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, wakati akiwasili katika uwanja wa KIA, kwa ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Kilimanjaro, Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).       

Waombaji wa hati za kusafiria sasa kulipa kwa M-Pesa

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji nchini wamezindua huduma mpya iitwayo ‘Malipo ya Pasipoti kwa M-Pesa’ katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za makao makuu ya Uhamiaji, kurasini, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa M-Commerce, Epimack Mbeteni alisema huduma hii mpya inalenga kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo kufanya malipo kwa haraka na urahisi zaidi. “Napenda kuwataarifu wateja wetu na Watanzania kwa ujumla kwamba, sasa wanaweza kulipia hati zao uhamiaji kwa kupitia M-Pesa”. 

“Ili mteja aweze kulipia inabidi aingie kwenye menu ya M-Pesa na kufuata utaratibu wa kulipa malipo ya serikali au kupitia zana (app) M-Pesa. Lengo letu ni kuhamasisha Watanzania wapate hati mpya za kieletroniki lakini pia kuwasogezea huduma za malipo viganjani kwao, ndio maana tumeona umuhimu wa kushirikiana na Uhamiaji kufanikisha hili” Aliongeza Mbeteni 

Huu ni mkakati wa kuwarahishia waombaji wa hati za kusafiria (Passport) ulipaji wa malipo kwa idara ya Uhamiaji, kwa vile walikuwa wakipanga foleni na kusubiria kwa muda mrefu ili kukamilisha malipo hayo 

Kamishna wa Passport wa Uhamiaji Marry Palmer alisema “tuna furaha kuungana na Vodacom Tanzania Plc kuwawezesha wateja kufanya malipo kirahisi, vile vile kuiwezesha idara yetu kufanya kazi kwa urahisi zaidi. Nategemea kuona bunifu nyingi zaidi kutoka Vodacom”. 

Vodacom imedhamiria kufikia idadi kubwa ya watu ambao hawapo kwenye mifumo rasmi ya kifedha, kuchochea ujumuishwaji, na uwezeshaji kupitia huduma rafiki na salama hivyo hii ni moja ya njia ya kufanikisha lengo hilo. 

“Tunaendeleza nia ya kubadili Tanzania kuwa jamii inayofanya malipo kidijitali, tunawekeza katika teknolojia ya simu ambayo itaingiza watu wengi zaidi katika mifumo ya kifedha na hatimaye, kufikia malengo ya kijamii na kiuchumi ya nchi”, alisisitiza mbeteni. 

Kampuni ya Vodacom imedhamiria kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali ikiwa ni pamoja na kukuza matumizi ya pesa mtandao (E-money) kupitia mtandao wake ulioshamiri nchi nzima ambayo itasaidia wananchi kuepuka hatari mbalimbali zitokanazo na kubeba fedha kila wanapotaka kufanya manunuzi. 
Mkurugenzi wa M-Commerce Vodacom Tanzania, Epimarck Mbeteni akishikana mkono Kamishna wa Vibali, Mary Palmer, kuashiria uzinduzi wa huduma ya ‘Malipo ya Uhamiaji kwa M-Pesa’ wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika makao ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Wateja wa Vodacom sasa wanaweza kufanya malipo ya huduma za Uhamiaji moja kwa moja kupitia menu ya M-Pesa na Vodacom App.
Kamishna wa Vibali, Mary Palmer, (wa pili kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya ‘Malipo ya Uhamiaji kwa M-Pesa’ iliyofanyika makao ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Wateja wa Vodacom sasa wanaweza kufanya malipo ya huduma za Uhamiaji moja kwa moja kupitia menu ya M-Pesa na Vodacom App. Katikati ni Mkurugenzi wa M-Commerce, Epimarck Mbeteni, Mkurugenzi wa Wateja wa Mikataba (Business Enterprise Unit), Arjun Dhillon (wa pili kushoto) na Afisa Udhibiti wa Pasipoti, Peter Lucas Mwita (kushoto)
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live




Latest Images