Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

RC MAKONDA AZINDUA SOKO LA KIMATAIFA LA MADINI NA VITO MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
*Awataka wafanyabiashara kuwa na ushirikiano na kulitumia soko hilo vyema pamoja na kutowafumbia macho watakaotorosha madini na kufanya biashara kinyemela

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo Julai 17 amezindua rasmi soko la kimataifa la madini na vito jijini Dar es salaam ikiwa utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kutaka kila Mkoa kuwa na soko hilo.

Akizungumza katika warsha hiyo Makonda amesema kuwa, uwepo wa soko hilo litasaidia Wananchi kununua madini na vito halali na kupunguza matapeli waliokuwa wakiuzia wananchi na raia wa kigeni madini na vito bandia.

Makonda amesema kuwa, uzinduzi wa soko hilo umekuja wakati muafaka ambao Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa nchi za SADC ambapo wageni wataanza kuingia nchini mwezi ujao wakiambatana na wafanyabiashara ambapo pia anaamini watapata nafasi ya kutembelea soko hilo na kutengeneza fursa zaidi kwa wafanyabiashara nchini.

Hata hivyo  Makonda amesema ndani ya soko hilo yanapatikana madini ya aina zote hivyo amewataka wananchi kulitumia kwakuwa ni halali na linatambulika na serikali.

Kwa upande wake mwakilishi wa wafanyabiashara wa madini nchini Othman Tharia amemshukuru Rais Magufuli kwa kutoa wazo la kujenga masoko hayo ambapo hadi sasa Mikoa 28 imetekeleza kwa kujenga masoko hayo hali itakayopelekea kukoma kwa mianya ya utoroshaji na wakiwa wafanyabiashara wanahaidi  kuunga jitihadi za Rais katika utendaji kazi.

Aidha amewataka wafanyabiashara hao kuwa na chama maalumu kitakachowatambulisha kote nchini na wameishukuru Wizara ya madini kwa kusimamia sheria katika usimamizi wa masoko hayo.

Ikumbukwe kuwa Mkoa wa Dar es salaam ndio soko na lango kuu la biashara ikiwemo madini hivyo uwepo wa soko hili ni fursa kwa wachimbaji, wafanyabiashara na wananchi kupata madini na vito halali kwa bei halali.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi wa soko la kimataifa la madini leo jijini Dar es Salaam.
 Mfanyabishara ya madini Othman Tharia (kushoto) akitoa maelezo kutoka sekta  ya madini mbele ya Mkuu was Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (kulia) mara baada ya kuzindua soko la kimataifa la madini katika Mkoa wa Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (aliyeketi) akisikiliza maelezo kutoka kwa mfanyabishara wa madini Othman Tharia kuhusiana na namna wanavyoendesha biashara hiyo, leo jijini Dar es Salaam.

RAIS MSTAAFU MWINYI AONGOZA VIONGOZI,WANANCHI HARUSI YA MTOTO WA LOSWASSA.

$
0
0
VIONGOZI mbalimbali Wastaafu na waliopo Madarakani wakiongozwa na Rais Mstaafu Alli Hassan Mwinyi wamepamba harusi ya Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Robert Lowassa na mkewe Stephanie Kaaya. 

Ndoa ya wawili hao ilifungwa katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mjini Kati na baadae katika tafrija iliyofanyika ukumbi wa Kiringa Gardens, Burka jijini Arusha.

Pichani juu ni Rais Mstaafu Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwapongeza Maharusi hao.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiwapongeza maharusi Robert 'Bob' na Mkewe Stephanie
  Viongozi mbalimbali waliohudhuria Sherehe hiyo wakisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa. 
 Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa.
Mke wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Edward Lowassa.
 Maharusi, Robert Lowassa 'Bob' akifurahia jamabo na mkewe  Stephanie Kaaya.
 Maharusi, Robert Lowassa 'Bob' akifurahia jamabo na mkewe  Stephanie Kaaya.
 Maharusi, Robert Lowassa 'Bob' wakiwa katika upigaji picha  na mkewe  Stephanie Kaaya.
 Alama ya Ndoa ya Robert na Stephanie
 Mfanyabiashara Rostam Aziz akiwasili ukumbini
 Maharusi wakiingia ukumbini 
 Mama Mwinyi na Mama Lowassa wakiingia 


PSTB YATAMBULISHA MFUMO MPYA WA KUJISAJILI NA MALIPO KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma moja ya jarida kwenye banda la bodi ya ununuzi na ugavi(PSPTB) kuhusu mfumo wa usajili na jinsi bodi hiyo uinavyofanya kazi wakati wa ufunguzi wa wa Maonesho ya Vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa bodi ya ununuzi na ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi  
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa bodi ya ununuzi na ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi(katikati) kuhusu mfumo wa usajili na jinsi bodi hiyo inavyofanya kazi wakati wa ufunguzi wa wa Maonesho ya Vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

WATAKIWA KUIMARISHA AFYA ZA MAMA MJAMZITO NA MTOTO KUONDOA VIFO

$
0
0
Waganga wafawidhi ,bodi ya afya ,kamati za usimamizi wa vituo vya afya na zahanati pamoja na kamati za ulinzi wa mtoto kwa pamoja wametakiwa kuimarisha afya za mama mjamzito na mtoto na kufanikisha vifo havitokei.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Dakaro(Daqqaro) ameyasema hayo mapema wakati akizindua kampeni ya JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA ngazi ya wilaya yenye lengo la kupunguza na kuondoa vifo vya mama na mtoto. 

Daqqaro(DAKARO) amesema kuwa miongoni mwa visababishi vya vifo kwa kina mama wajawazito ni uzembe unaofanywa na jamii husika,kutokufanya mazoezi pamoja na uzembe unao fanywa na baadhi ya watalamu wa afya ambapo amewataka watalaamu hao kuchunguza sababu ya ongezeko la kujifungua kwa opalesheni kwa kina mama .

Kwa upande wake kiongozi wa kimila mzee Tobikol amesema kuwa pamoja na serikali kuweka mipango mikakati ya kudhibiti vifo vya mama mjamzito bado baadhi ya vituo vya afya vina upungufu wa madakitali huku vingine vikiwa havifanyi kazi siku za wikiendi jambo ambalo huchochea ongezeko la vifo hivyo.

Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha Wedsoni Sichalwe amesema kuwa chanzo cha vifo hivyo ni pamoja na Kifafa cha mimba,upungufu wa Damu kutokana na kupoteza Damu nyingi wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua watoto kuzaliwa njiti na kushindwa kupumua.

Hata hivyo kampeni hii ambayo imezinduliwa Kiwilaya ni muendelezo ambapo Kimkoa ili zinduliwa tarehe 6 mwezi wa 4 mwaka huu na kitaifa ili zinduliwa tarehe 6 mwezi wa 11 mwaka 2018 kwa lengo la kuondoa vifo hivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akizindua kampeni ya JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA Kiwilaya uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Goldenrose Jijini Arusha
Mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt.Wedsoni Sichalwe akieleza vyanzo vya vifo kwa akina mama wajawazito.
Kiongozi wa kimila kutoka jamii ya wamaasai Njiani Arusha Mzee Tobikol akieleza baadhi ya changamoto zilizopo katika vituo vya afya mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro katika uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mganga mkuu wa jiji la Arusha Dkt.Simon Chacha aeleza sababu zinazopelekea mama wajawazito pamoja na watoto waganga kupoteza maisha ikionekana ni ucheleweshwaji wa mama mjamzito ngazi ya jamii kutokana na Mila na desturi katika kijamii.

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA 7 YA USAJILI WA NGO’s KANDA YA MASHARIKI

$
0
0
MkurugenziMsaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO’s Bw. Baraka Leonard (kushoto) akitoa huduma kwa mdau ya kusajili Taasisi chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine na yanayojisajili kwa mara ya kwanza katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki 
Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO’s Bw. Faki Shewaji (kulia) akitoa huduma ya kusajili Taasisi chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 kwa mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine na yanayojisajili kwa mara ya kwanza katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki. 
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.Victor Rugalabamu (kulia) akitoa huduma ya kusajili Taasisi chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 kwa wadau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine na yanayojisajili kwa mara ya kwanza katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO’s Bi.Grace Mbwilo (kulia) akitoa huduma ya kusajili Taasisi chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 kwa mmoja wa wadau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine na yanayojisajili kwa mara ya kwanza katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki wa pili kulia Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao.

WAZIRI MKUU AITAKA TCU IVISAIDIE VYUO VIKUU BINAFSI

$
0
0
*Asisitiza kwamba hakuna mbadala wa elimu bora
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) itafute mbinu bora zaidi na kuvijengea uwezo vyuo vikuu binafsi ili visaidie kuongeza udahili.

“Tume itafute mbinu bora zaidi ikiwa ni pamoja na kuvijengea uwezo vyuo vikuu binafsi ili visaidie kuongeza udahili. Ni wakati muafaka kwa Tume kujipambanua kwenye uwezeshaji na ushauri ili kuondoa taswira hasi miongoni mwa jamii kwamba kazi kubwa ya TCU ni kuvifungia vyuo vikuu badala ya kuvisaidia kutatua changamoto zinazovikabili,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo, (Jumatano, Julai 17, 2019) wakati akifungua maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yatafungwa Julai 20, mwaka huu.

Amesema Serikali inatambua kwamba vyuo vikuu binafsi ni washirika muhimu wa maendeleo ya sekta ndogo ya elimu ya juu nchini. “Naomba nieleweke vizuri kwamba hakuna mbadala wa elimu bora bali nasisitiza Tume ivisaidie vyuo vikuu kufikia viwango vinavyotakiwa na siyo kuwapunguzia viwango vya matakwa ya usajili,” amesema.

Akitoa ufafanuzi kuhusu idadi ndogo ya wahitimu wa elimu ya juu, Waziri Mkuu amesema takwimu za kimataifa za ushiriki wa elimu ya juu zinaonesha kwamba kufikia mwaka 2017 ni asilimia moja hadi tatu tu ya Watanzania kwa kila Watanzania 100 wenye umri chini ya miaka 25 wanapata elimu ya Chuo Kikuu.

“Idadi hii ni ndogo zaidi ya majirani zetu wa Kenya wenye asilimia nne, Zambia asilimia nne na Namibia asilimia 14. Bado tunayo kazi kubwa sana ya kufanya. Natoa maelekezo kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iongeze jitihada na mikakati ya kuboresha uwiano huu ambao upo chini ikilinganishwa na majirani zetu,” alisisitiza.

Amesema ili kuongeza idadi ya Watanzania wanaopata nafasi ya elimu ya juu, ni lazima tupange mikakati yetu kama nchi kwa kushirikiana na sekta binafsi, ambao ni wadau wakubwa katika elimu ya juu. “Taarifa nilizonazo ni kwamba, kati ya wahitimu wote wa vyuo vikuu kwa mwaka, asilimia 25 wanatoka katika vyuo vikuu binafsi. Mchango huu si mdogo, na ningetamani uongezeke zaidi,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewapa changamoto wakuu wa vyuo vikuu nchini wabadilishe mtazamo wao juu ya upimaji wa ufanisi wa wahitimu na badala yake upimaji wao ujielekeze kwenye kutoa suluhisho na kubadilisha maisha ya Watanzania badala ya kutumia machapisho ya kitaaluma.

“Kipimo cha ufanisi katika taaluma ilikuwa ni machapisho ya kitaaluma, ambapo mengi ya hayo, jamii pana haifaidiki nayo. Sasa ni wakati mwafaka kutafakari iwapo kipimo hicho kinatosheleza. Kwa vyuo vikuu ambavyo mmehudhuria hapa leo, naomba niwape mtazamo tofauti. Kipimo cha ufanisi wa wanataaluma wa Tanzania, kuanzia sasa kinafaa kiwe ni kiasi gani taaluma yao inawafikia na kubadilisha maisha ya wananchi, na kiwango cha bidhaa na hatimiliki (patents) zilizozalishwa na kusajiliwa na wasomi wetu waliopo vyuo vikuu.”

Amesema matarajio ya Serikali ni kuona kwamba tafiti na vipimo vya ufanisi kwenye vyuo vikuu viwe ni kiasi gani vyuo hivyo vinatoa bidhaa mbalimbali za kuleta ajira pamoja na kukabiliana na matatizo ya kijamii. “Ningefurahi iwapo kuanzia sasa kipimo cha ufanisi wa vyuo vikuu vyetu iwe katika kupima jitihada za vyuo vyetu kuisaidia Serikali katika azma yake ya kufikia kwenye uchumi wa kati,” amesema.

“Huu ni wakati muafaka kuanza kupima ufanisi wa wakuu wa vyuo kwa kuangalia kiasi gani mazao ya Chuo Kikuu hicho yamewafikia wananchi na pia katika utekelezaji wa mikakati ya maendeleo ya Serikali, hasa mapinduzi ya viwanda,” amesisitiza.

Mapema, akielezea kuhusu maonesho hayo, Mwenyekiti wa TCU, Prof. Jacob Mtabaji aliwataka wahitimu wa kidato cha sita wanaoomba kujiunga na vyuo vikuu, wasome kwa umakini mwongozo uliowekwa kwenye tovuti na wasikubali kupitia mawakala wanaodai kuwa wanaweza kufanya usajili kwa niaba yao. Pia aliwataka wazingatie kalenda ya udahili.

Akielezea changamoto za elimu ya juu nchini, Prof. Mtabaji alisema kuna uhaba wa wahadhiri wenye sifa stahiki katika vyuo vikuu vingi na akawaomba wakuu wa vyuo hivyo wawasomeshe wahadhiri katika ngazi mbalimbali ili wakirudi wajiunge na vyuo husika.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa alisema taasisi 81 za elimu ya juu zimeshiriki maonesho hayo ambapo taasisi 15 ni za nje ya nchi na taasisi 66 ni za hapa nchini.

Akitoa shukrani, Mwenyekiti wa Kamati ya Watendaji Wakuu wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki (CVCPT), Prof. Raphael Chibunda alisema anaishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa uboreshwaji uliofanywa kwenye upatikanaji na upelekwaji kwa wakati wa fedha kutoka Bodi ya Mikopo. “Zamani, sauala hili hiloi likuwa ni chanzo cha migomo mingi vyuoni lakini kwa sasa limekwisha,” alisema.

Pia aliishukuru Serikali kwa kukubali kurudisha jukumu la udahili wa wanafunzi katika Seneti za Vyuo Vikuu kwani hapo nyuma lilikuwa sehemu ya mgogoro baina ya TCU na vyuo vikuu.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakati akikagua mabanda katika, kwenye ufunguzi wa Maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam, Julai 17.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mashine ya kutotolea vifaranga, iliyobuniwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), kabla ya kufungua Maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam, Julai 17.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mita ya maji ya malipo ya kabla, iliyobuniwa na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Saint Joseph, Khadija Mustapha (kulia), kabla ya kufungua Maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam, Julai 17.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Meneja Usajili na Utambuzi (NIDA), Julien Bernard (kulia), kwenye ufunguzi wa Maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam, Julai 17.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mashine ya kutayarishia vitambulisho vya Taifa, wakati akikagua banda la (NIDA), kwenye ufunguzi wa Maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam, Julai 17.2019. Kulia ni Mtaalamu wa mashine hiyo, Marwa Mbolea. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi, waliyohudhuria kwenye ufunguzi wa Maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam, Julai 17.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, baada ya ufunguzi wa Maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam, Julai 17.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Jacob Philip Mtabaji, wakati alipowasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja, kufungua Maonesho ya 14 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, jijini Dar es salaam, Julai 17.2019. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Charles Kihampa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
            

Prof. Kabudi azungumza na Mabalozi wastaafu wa Tanzania

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wastaafu walioiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani kwa nia ya kupata ushauri na maoni yao kuhusu maandalizi ya Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo Prof. Palamagamba John Kabudi ameongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi (wa kwanza kulia). 
Juu na Chini ni sehemu ya Mabalozi wastaafu walioiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani wakimsikiliza Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani). 
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) 
Mkutano ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.), Naibu Waziri Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wastaafu walioiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani 

SERIKALI YAJARIBU KITINI KUTOKOMEZA UKATILI DAHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia Bi. Grace Mwangwa akifungua zoezi la majalibio ya Kitini cha Mafunzo ya masuala ya ukatili wa kijinsia yanayoendelea leo Mjini Morogoro.
 Baadhi ya Wadau wa masuala ya Jinsia wakijadiliana wakati wa zoezi la majalibio ya Kitini cha Mafunzo ya masuala ya ukatili wa kijinsia yanayoendelea leo Mjini Morogoro.
Baadhi ya Wadau wa masuala ya Jinsia wakijadiliana wakati wa zoezi la majalibio ya Kitini cha Mafunzo ya masuala ya ukatili wa kijinsia yanayoendelea leo Mjini Morogoro.

Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleao ya Jamii inakutana na wadau mjini Morogoro kufanya majaribio ya kitini kilichoandaliwa na Wizara hiyo kwa lengo la  kuimarisha uwezo wa wawezeshaji  kupata maarifa na stadi juu ya mikakati ya kijamii ya kuzuia  ukatili wa kijinsia hapa Nchini.

Akiongea na wadau mbalimbali Mkoani humo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Grace Mwangwa amesema kuwa kitini hicho kina mada mbalimbali zitakazowezesha kutoa mwongozo wa kitaifa wa mafunzo ya kijinsia  yatakayowawezesha  walengwa kubainisha na kukemea mila na desturi zenye kuleta madhara kwa jamii ikiwemo mafunzo kuhusu kuzingatia masuala haki za kijinsia.

Bi. Mwangwa amesema kwamba kuwepo kwa Kitini hicho pia kutasaidia katika kupunguza au kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia na hivyo kuwawezesha wanafamilia hususani wanawake kushiriki katika shughuli za kiuchumi. 

Bi. Mwangwa ameongeza kuwa utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria ya mwaka 2015-2016 unaonesha kuwa wanawake 4 kati ya 10 wamefanyiwa ukatili wa kimwili wakiwa na umri wa miaka 15 akiongeza kuwa Ukatili wa kimwili unaongezeka kadri umri unavyoongezeka.



Pamoja na idadi kubwa ya wanawake kufanyiwa ukataili wa kimwili Bi. Mwanga pia amesema 22% ya wanawake wenye umri wa miaka 15-19 wamefanyiwa  ukatili wa kimwili, ukilinganisha na asilimia 48 ya wanawake wenye umri wa miaka 40-49 na kuongeza kuwa  takwimu za hali ya Uhalifu  na Usalama barabarani zinaonesha pia  kwa kipindi cha Januari- Desemba  2016 mpaka Januari – Desemba 2016 zinaonesha kuwa jumla ya wanawake 307 walipata ukatili wa kimwili ukilinganisha na takwimu za kipindi cha Januari - Disemba 2017 ambapo jumla ya wanawake 350 ambao walipata ukatili wa kimwili.

Aidha Bi. Mwangwa amewaambia wajumbe wa kikao kazi hicho kuwa  serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imedhamiria kushughulikia ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kuweka sera, sheria na mipango inayolenga kulinda haki za wanawake, watoto na makundi mengine ya kijinsia.  

Amezitaja juhudi za Serikali katika kupambana na ukatili wa kijinsia kuwa ni pamoja na kuridhia mikataba za kimataifa na Kikanda yenye lengo la kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuleta usawa wa kijinsia lakini pia kutunga sheria mbalimbali zenye mlengo wa kulinda na kuendeleza haki za binadamu.

Bi. Mwangwa amezitaja sheria hizo kuwa  ni pamoja na za sheria ya  Mtoto (2009),Sheria ya  watu wenye ulemavu, UKIMWI, makosa ya Jinai, ajira, ardhi, msaada wa kisheria, usafirishaji haramu wa binadamu, ndoa, mirathi, elimu, na uwezeshaji kiuchumi.

Maandalizi ya Kitini hiki ni moja ya hatua muhimu ya utekelezaji wa mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa miaka mitano ambao uliandaliwa mahususi kupambana na kutokomeza vitendo vyote vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

BASATA YAWATAKA WASANII KUSAJILIWA KWA MUJIBU WA SHERIA

$
0
0
Na.Khadija seif, Michuzi tv

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kufuata utaratibu wa kusajiliwa kwenye baraza hilo ili watambulike kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamesema leo baada ya Wasanii Wa maigizo (Bongo Movie) Irene Uwoya na Steve Nyerere kutotambulika na BASATA kutokana na kushindwa kufuata utaratibu wa kisheria wa kusajiliwa.

Kaimu Katibu Mtendaji BASATA, Onesmo Kayanda amesema kuwa kwa sasa wasanii wengi wanafanya kazi zao za Sanaa bila ya kufuata taratibu za kujisajili.

"Wengi wanaingia katika sanaa bila utaratibu wanafanya kazi kwa ujanja ujanja mambo ya utandawazi pia yamekua yakichangia kutoona umuhimu wa kujisajili , badala yake linapotokea tatizo ndipo linapokuja swala la yeye kutotambulika na Basata,"

Kayanda amesema wasanii wengi wanafanya kazi zao bila kutambulika na mamlaka husika zaidi mitandao ya kijamii ndiyo inawatambua zaidi na anakua kinyume na kazi zake.

Aidha,Onesmo ameeeeza lengo la kuwaita wasanii hao wawili Irene uwoya pamoja na Steve Nyerere kufika Basata ni kufanya mazungumzo kuhusu mambo ya tansia ya sanaa na pamoja kupatiwa elimu,faida na hasara zitakazojitokeza endapo utakua unatambulika kisheria kama msanii kupitia Baraza la sanaa (BASATA).

" Tumezungumza mambo muhimu yanayohusu sanaa hichi ni kikao cha familia ndio kikubwa zaidi na tumegundua pia wao ni baadhi ya wasanii ambao hawajasajiliwa Basata na hawatambuliki kisheria.

Katibu huyo alifafanua Kitendo cha Msanii wa Bongomovie Irene Uwoya kudhalilisha waandishi katika Mkutano wa Kampuni ya kuuza filamu mtandaoni ya Swahiliflix kilichofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam cha kuwarushia pesa wanandishi kwa dharau kuwa waandishi wasione limepuuzwa bali sio la kuliweka wazi sana kwa sasa.

"Tunatambua kuwa amefanya kosa sisi kama viongozi tunalifanyia kazi ila si lazima kuliweka wazi".

WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI 'BLOGGERS' WAPEWA MAFUNZO NAMNA YA KUANDIKA HABARI ZA UCHUNGUZI

$
0
0
Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wamepatiwa mafunzo kuhusu namna ya kuandika habari za uchunguzi 'Investigative Journalism' ili waweze kuandika kwa weledi habari zinazohusu utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu.

Mafunzo hayo ya Waandishi hao wa habari mitandaoni yanafanyika jijini Dodoma kwa muda wa siku mbili Julai 17,2019 hadi Julai 18,2019 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media).

Mradi huo unatekelezwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha, Claud Gwandu akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania kuhusu namna ya kuandika habari za uchunguzi 'Investigative Journalism'. Picha zote na Kadama Malunde na Albert G. Sengo
Mwezeshaji katika mafunzo ya Uandishi wa habari za uchunguzi, Charles Kayoka akitoa mada wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV).
Mwezeshaji katika mafunzo ya Uandishi wa habari za uchunguzi, Charles Kayoka akisikiliza hoja kutoka kwa Mshiriki wa mafunzo hayo,William Bundala wa Kijukuu blog wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV).

Washiriki wa mafunzo hayo wakioneshana kitu kwenye Laptop
Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa katika mafunzo kuhusu namna ya kuandika habari za uchunguzi 'Investigative Journalism'. Picha zote na Kadama Malunde na Albert G. Sengo.

BASATA YAWATAKA WASANII KUSAJILIWA KWA MUJIBU WA SHERIA

$
0
0
 Na Khadija Seif, MichuziTV

BARAZA  la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kufuata utaratibu wa kusajiliwa kwenye baraza hilo ili watambulike kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamesema leo baada ya Wasanii Wa maigizo (Bongo Movie) Irene Uwoya na Steve Nyerere kutotambulika na BASATA kutokana na kushindwa kufuata utaratibu wa kisheria wa kusajiliwa.

Kaimu Katibu Mtendaji BASATA, Onesmo Kayanda  amesema kuwa kwa sasa wasanii wengi wanafanya kazi  zao za Sanaa bila ya kufuata taratibu za kujisajili.

"Wengi wanaingia katika sanaa bila utaratibu wanafanya kazi kwa ujanja ujanja mambo ya utandawazi pia yamekua yakichangia kutoona umuhimu wa kujisajili , badala yake linapotokea tatizo ndipo linapokuja swala la yeye kutotambulika na Basata,"

Kayanda amesema wasanii wengi  wanafanya kazi zao bila kutambulika na mamlaka husika zaidi mitandao ya kijamii ndiyo inawatambua zaidi na  anakua kinyume na kazi zake.

Aidha,Onesmo ameeeeza lengo la kuwaita wasanii hao wawili Irene uwoya pamoja na Steve Nyerere kufika Basata ni  kufanya mazungumzo kuhusu mambo ya tansia ya sanaa na  pamoja kupatiwa elimu,faida na hasara zitakazojitokeza endapo utakua unatambulika kisheria kama msanii kupitia Baraza la sanaa (BASATA).

" Tumezungumza mambo muhimu yanayohusu sanaa hichi ni kikao cha familia ndio kikubwa zaidi na tumegundua pia wao ni baadhi ya wasanii ambao hawajasajiliwa Basata na hawatambuliki kisheria.

Katibu huyo alifafanua Kitendo cha Msanii wa Bongomovie  Irene Uwoya kudhalilisha waandishi katika Mkutano wa Kampuni ya kuuza filamu mtandaoni ya Swahiliflix kilichofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro hotel  jijini Dar es salaam cha kuwarushia pesa wanandishi kwa dharau kuwa waandishi wasione limepuuzwa bali sio la kuliweka wazi sana kwa sasa.

"Tunatambua kuwa amefanya kosa sisi kama viongozi tunalifanyia kazi ila si lazima kuliweka wazi".

POLISI VITAVISHUGULIKIA VYAMA VYA SIASA VITAKAVYOSHAWISHI WANANCHI KUVURUGA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA-LUGOLA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Mji wa Kibara, Jimboni kwake Mwibara, Bunda, leo. Lugola amesema Jeshi la Polisi litahakikisha linawashughulikia wanasiasa watakaojaribu kuwashawishi wananchi kufanya fujo kwa lengo la kuvuruga uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi oktoba, 2019. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akiwasili Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara, leo, kwa ajili ya kwenda kuwasalimia wanaCCM wilayani humo, kabla ya kuanza ziara yake ya kuzungumza na wananchi jimboni kwake Mwibara. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, (wapili kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, Isack Maela, wakati alipokua anatoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Waziri huyo kuzungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Mji wa Kibara, Jimboni kwake Mwibara, leo. Katika hotuba yake kwa wananchi hao, Lugola amesema Jeshi la Polisi litahakikisha linawashughulikia wanasiasa watakaojaribu kuwashawishi wananchi kufanya fujo kwa lengo la kuvuruga uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi oktoba, 2019. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

…………………. 

Na Felix Mwagara, Mwibara (MOHA) 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Jeshi la Polisi litahakikisha linawashughulikia wanasiasa watakaojaribu kuwashawishi wananchi kufanya fujo kwa lengo la kuvuruga uchaguzi wa Serikali za Mitaa. 

Lugola alisisitiza kuwa, kisitokee chama chochote cha siasa kitakachojaribu kuvuruga uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu 2019, ambao Watanzania wengi wamejipanga kufanya uchaguzi huo kwa amani na utulivu. 

Lugola ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara alipokuwa anazungumza na wananchi wa Mji wa Kibara, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo, ambapo amesema wananchi wajiepushe kudanganywa au kutumbukia katika mtego wowote wa wanasiasa. 

“Wizara yangu kupitia Jeshi la Polisi haita kuwa tayari kuona na kumuacha raia wa Tanzania au asiye raia akijihusisha na vitendo vya kuhujumu uchaguzi au kuleta fujo, atadhibitiwa bila kujali nafasi yake, au uwezo wake kiuchumi, hii Serikali siyo ya kuchezewa, hivyo natuma salamu kama mlikuwa na mawazo hayo yaondoeni, hatutamuonea mtu huruma ambaye analengo la kuvuruga amani yetu,” alisema Lugola. 

Pia Waziri Lugola alivitaka vyama hivyo viwe na uzalendo na nchi yao na pia viwe na hitikadi na malengo ya kisiasa ambayo hayaleti fujo kwa kufuata sheria za nchi. 

Aidha, Lugola kwa mara nyingine alizungumzia uhalifu katika ziwa Victoria, akiwataka Polisi waongeze kasi kwa kufanya operesheni za mara kwa mara katika maeneo hayo ya ziwa kwa lengo la kudhibiti uhalifu huo. 
“Huu uhalifu katika ziwa Victoria utashughulikiwa, hii ni awamu ya tano ambayo inaongozwa na Rais Dkt John Magufuli, hivyo tunataka wananchi muishi katika nchi yenu kwa amani na utulivu,” alisema Lugola. 

Waziri Lugola anaendelea na ziara jimboni kwake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kufanya mikutano ya hadhara akisikiliza kero za wananchi jimboni humo, na pia kuiongoza ligi yake, Kangi Bomba ambayo inashirikisha wananchi jimboni humo kufanya mashindano ya mpira wa miguu, pete, pamoja na michezo mbalimbali.

Mahakama yataka upande wa mashtaka kukamilisha nyaraka wanazoziandaa katika kesi dhidi ya vigogo wa Six Telecoms

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv,
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi likiwemo shitaka la kuisababishia serikali hasara  inayowakabili vigogo wa Kampuni ya  Six Telecoms akiwemo Wakili Dk Ringo Tenga kukamilisha nyaraka wanazoziandaa katika kesi hiyo ili iweze kuanza kusikilizwa.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, amesema kwa sababu shauri hilo ni la uhujumu uchumi, mahakama hiyo haina meno ya kuisemea lakini ni vema upande wa mashitaka kukamilisha taratibu hizo mapema.

Hatua hiyo imekuja kufuatia upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali Wankyo Simon kudai mahakamani hapo leo Julai 17, 2019 kuwa kwa sasa wanaandaa nyaraka muhimu katika kesi hiyo wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

"Mheshimiwa hakimu, tupo katika hatua za kuandaa nyaraka mbalimbali ikiwemo vielelezo ambavyo ni muhimu katika kesi hii hivyo tunaomba mahakama iahirishe kesi hii kwa wiki mbili ili kukamilisha hatua hiyo.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 26, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Tenga, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo na Noel Chacha.

Washtakiwa hao wanadai kuwa, kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14,2016 maeneo ya Dar es Salaam, walitoza malipo ya mawasiliano ya simu za kimataifa chini ya kiwango cha Dola za Marekani 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida.

Pia katika kipindi hicho, wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA) kwa kutoza gharama chini ya kiwango na kushindwa kulipa kiasi cha Dola za Marekani 3,282,741.12 kwa TCRA, kama malipo ya mapato.

Washtakiwa hao ,wanadaiwa katika kipindi hicho walishindwa kulipa ada za udhibiti za Dola za Marekani 466,010.07 kwa TCRA.

Katika shtaka la utakatishaji wa fedha, Hafidhi, Noni,Tenga na Chacha, wanadaiwa kuwa walitumia ama walisimamia Dola za Marekani 3,282,741.12 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya udanganyifu linalotokana na mashitaka yaliyotangulia.

Vile vile ,washitakiwa hao wanadaiwa kuwa waliisababishia TCRA hasara ya Dola za Marekani 3,748,751.22 (sawa na Sh bilioni nane.

Wazee wa baraza watoa maoni yao dhidi ya kesi ya mauaji, wadai mtuhumiwa hana hatia

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

WAZEE wa baraza katika kesi ya mauaji dhidi ya  Yusuph Mussa Mkazi wa Mchikichini, anayedaiwa kumuua mke wake, wameieleza Mahakama kuwa, upande wa mashitaka katika kesi hiyo, wameshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya mshtakiwa hivyo wanamuona mshitakiwa hana hatia.

Wakitoa maoni yao leo, mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu, Pamela Mazengo wazee hao wamedai kati ya mashahidi tisa waliotoa ushahidi  dhidi ya mshitakiwa huyo, hakuna hata shahidi mmoja aliyeeleza kuwa alimuona mshtakiwa akitenda nia hiyo ovu.

Hatua ya wazee hao ambao ni washauri wa mahakama imefikwa baada kufungwa kwa ushahidi wa pande zote mbili pamoja na mawasilisho yaliyofanywa na mawakili kama mshitakiwa ana hatia au la.

Wakitoa maoni hayo, wazee hao wamedai ushahidi wa upande wa mashitaka una mashaka mengi na hauna muunganiko wa matukio yaliyotokea wakati wa kifo cha marehemu Fatuma Mbaga.

Wamedai mashahidi pamoja na mshitakiwa waliieleza mahakama kuwa sababu ya kifo ilidhaniwa imetokana na shoti ya umeme lakini upande wa mashitaka umeshindwa kuwaleta mafundi umeme ili kuthibitisha kama ni kweli nyumba ya mshitakiwa na marehemu ilikuwa na shoti na walirekebisha tatizo hilo kabla ya tukio.

Pia wamedai mahakama haikuletewa tiketi ya ndege aliyosafiria mshitakiwa kwenda Mwanza  kama alivyodai wala tiketi za gari aliyotumia askari mpelelezi kwenda kuchunguza kama baba wa mshitakiwa ni mzima au amekufa pia mpelelezi alishindwa kwenda kwenye kampuni aliyokuwa anafanyia kazi baba wa mshitakiwa ili kuthibitisha kama ni mzima licha ya jitihada za kwenda Mwanza kujua ukweli.

Wameeleza, kuna maswali mengi katika kesi hii kwa sababu daktari alieleza kuwa kifo cha marehemu kilisababishwa na matatizo kwenye ubongo yaliyosababisha kuvuja damu, michubuko sehemu za haja kubwa na ndogo na alivunjika mgongo je yote haya yamesababishwa na hitilafu ya umeme? Amehoji mzee wa baraza.

Kufuatia hayo,  wazee hao wamedai kuwa mshitakiwa hana hatia kwa sababu ushahidi uliotolewa ni wa hisia hivyo,  mahakama imuachie huru.

Mapema, upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Robert Kusalika umedai kuwa ushahidi wa upande wa mashitaka ni wa mazingira na kwamba hakuna mtu aliyemuona mshitakiwa akitenda kosa. Kusalika amedai ushahidi uliotolewa umekata kata hna haumuunganishi moja kwa moja mshitakiwa na tukio hilo.

Aidha Msajili Mazengo amesema ni wajibu wa upande wa mashitaka kuhakikisha wanathibitisha mashitaka bila kuacha shaka na kwamba hakuna shaka kuwa Mbaga alikufa kwani daktari aliyechunguza mwili huo aliithibitishia mahakama na kwamba mshitakiwa na marehemu walikuwa mke na mume ambao waliishi pamoja.

Mussa anadaiwa,  Mei 11 ,2015 eneo la Jangwani ,Ilala, jijini Dar es Salaam, alimuua  kwa makusudi Fatuma Mbaga.

RC GAMBO APOKEA MABATI YA SHILINGI MIL.15 KUTOKA KAMPUNI YA MOUNT KILIMANJARO CLUB.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipokea mabati yenye thaman ya takribani milioni.15 mkurugenzi mtendaji wa kutoka Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club George Ole Meing'arrai .
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi Afisa Tarafa Mabati mara baada ya kuyapokea kutoka ya Mount Kilimanjaro Safari Club.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akikagua moja ya vyumba vya mahabara katika shule hiyo mpya inayotazamiwa iliyopo katika kata ya Olasiti mkoani hapa kuingiza wanafunzi kuanzia januari mwakani 2020.Picha/Habari na Vero Ignatus Michuzi Blog.
Mkuu wa mkoa Mrisho Gambo akielekea kukagua msingi wa ujenzi wa nyumba xa Waalmu katika shule mpya ya sekondari ya Mrisho Gambo ambayo inatazamiwa kuanza kuingiza wanafunzi januari mwakani 2020.

Msingi wa nyumba za Waalimu katika Shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo kama ubavyoonekana katika picha.
Diwani wa Kata ya Olasiti Alex Marti akizungumza na cwasndishi.wa habari katiks eneo la shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo.
Afisa Tarafa ya Elerai Titho Maulilyo Cholobi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa mabati ya kuezekea shule ya sekondari ya Mrisho
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club George Ole Neing'arrai akizungumza na waandishi ww habari mara baada ya kukabidhi mabati yenye thamani ya takribani Mil.15 katika shule ya Sekondari ya Mrisho Gambo.
Mkuu wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua madarasa pamoja na ujenzi unaoendelea katika shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo iliyopo katika kata ya Olasiti mkoani hapo.

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amepokea mabati yenye thamani ya takribani milioni 15 kutoka kwa Kampuni ya Mount Meru Kilimanjaro Safari Club ya Jijini Arusha.

Akizungumza baada ya kupokea mabati hayo amesema mwaka jana 2018 Jiji la Arusha lilipata changamoto kubwa ya wanafunzi zaidi ya 10,000 kukosa madarasa ya kusoma katika hivyo mkoa ukadhamiria kushirikiana na wilaya zote kujenga shule ya hiyo ambayo itakayoweza kuwachukua wanafunzi watakaokaa sawasawa na matakwa ya serikali 

Amesema kuwa hadi sasa wanajenga madarasa 8 yenye maabara 3 za sayansi ,kemia,bayolojia na Fizikia lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto kwa waalimu wa sayansi katika nchi ya Tanzania.

Mhe.Gambo amesema kuwa changamoto ya walimu wa sayansi ni kubwa hivyo wameona wanapojenga shule lazima watengeneze miundombinu kwa wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo.

Victoria Moshi ni Afisa ustawi wa jamii Kata ya Olasiti amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo utasaidia sana katika kipengele cha ulinzi wa ntoto kwani hawataenda mbali kufuata elimu na wazazi pia watanufaika kwani hawatakuwa na hofu juu ya usalama wawatoto wao.

Wameahidi kwamba wataendelea kuihamasisha jamii ili waendelee kushiriki katika kuchangia maendeleo ya shule katika nyanja mbalimbali na katika kuitunza shule hiyo ili kizazi kijacho nao wanufaike kwa kupitia shule hiyo. 

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji kutoka Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club amesema amemshukuru mkuu wa mkoa kwa.kuwashirikisha kama wakala wa utalii katika maendeleo ya jamii ikiwepo maswala ya Elimu .

Amesema kuwa wataendelea kuwepo kushiriki ambapo ametoa wito kwa sekta mbalilimbali iki nyingine za kiraia kushiriki ikiwemo ya Madini utalii na sekta mbalimbali wajitokeze kushiriki katika swala la maendeleo haswa sekta ya elimu. 

Amesema kuwa azma ya nchini ua Tanzania watoto wapate maeneo ya.kusoma na wapate elimu bora kwa kuboresha madarasa,mahabara na mazingira ya kumvutia mtoto.

TAARIFA KUTOKA MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA (TMDA)

DC KOROGWE AUNGANA NA WANANCHI KUSHUHUDIA MAJARIBIO YA TRENI YA MIZIGO RELI YA TANGA-MOSHI.

$
0
0
Ikiwa zimebaki siku chache kuelekea katika sherehe za ufunguzi wa Reli ya kutoka Tanga kwenda Kilimanjaro, Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mh Kissa Kasongwa akiwa katika mkutano na wananchi wa Kata ya Magila gereza amelazimika kusimamisha mkutano na kushuhudia majaribio ya Treni ya mizigo iliyokuwa ikifanya safari zake katika reli ya kutoka Tanga kwenda Kilimanjaro ambayo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi ifikapo julai 20-2019 wilayani Moshi.

Dc Kissa amesema kuwa ni bahati kubwa kwa wanakorogwe kuhushudia majaribio hayo ya Treni ya mizigo ikifanya safari katika reli ambayo inapita wilayani Korogwe ikitokea Tanga na kwamba nao wameshiriki kwa namna moja au nyingine katika shagwe za sherehe hizo za uzinduzi ambapo ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa maana iliahidi na sasa imetekeleza.
Kufunguliwa kwa Reli hii ya kupitisha treni za mizigo kutoka Tanga kwenda Kilimanjaro kutasaidia sana kukuza uchumi katika mikoa hii miwili inayounganishwa na reli pamoja na Taifa kwa ujumla.

BENKI YA DUNIA NA TANZANIA WAWEKA HISTORIA MENEJIMENTI YA MAAFA AFRIKA

$
0
0

Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongea na wataalam kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa Utekelezaji wa Mipango ya menejimenti ya maafa nchini, mjini Arusha, tarehe 16 Julai, 2019. 
Mkurugenzi Msaidizi (Utafiti na Mipango), Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu Bashiru Taratibu akisisitiza jambo kwa wataalam kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa wa Utekelezaji wa Mipango ya , tarehe 16 Julai, 2019. 
Mwezeshaji kutoka Benki ya Dunia Adam Mc Allister akisisitiza umuhimu wa Mipango ya Menejimenti ya Maafa kwa taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima Utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, mjini Arusha, Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe (mwenye tai nyekundu), kushoto ni kwake Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi hiyo (Utafiti na Mipango), Bashiru Taratibu, kushoto kwake ni Wawezeshaji kutoka Benki ya Dunia, Elad Shenfeld, Adam Mc Allister na HugoWesley, wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, kwa taasisi za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa , mjini Arusha tarehe 16 Julai, 2019. 
Mtaalam wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, Charles Msangi akieleza jinsi ofisi hiyo inavyoratibu shughuli za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa Utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, kwa taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa mjini Arusha, Julai 16, 2019. 
Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini, Balele Edward, akiandika katika moja ya nyenzo za kujifunzia wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa Utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini kwa taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa, mjini Arusha Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ufadhili wa Benki ya Dunia. 
Baadhi ya washiriki kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti ya maafa wakijadiliana wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, mjini Arusha Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia. 

************* 

Kwa mara ya kwanza Barani Afrika na kwa mara ya kwanza katika utendaji wake Benki ya Dunia, kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, wamefanya zoezi la mezani la Kupima uwezo utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na kukabili Maafa kwa kutumia maafa ambayo yamepata kutokea kweli hapa nchini, ambapo zoezi hilo limetumia maafa ya mafuriko mkoani Morogoro, wilayani Kilosa kwa mwaka 2014 na mwaka 2016. Mazoezi mengine ya mezani ya kujiandaa na kukabli maafa hutumia matukio ya maafa ya kinadharia na hufanyika kabla ya maafa kutokea. 

Mtaalam Mwandamizi wa menejimenti ya Maafa, kutoka Benki ya Dunia, Elad Shenfeld, amebainisha mambo matano ambayo yameifanya Benki hiyo kuichagua Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufanya zoezi hilo, kuwa ni Uwajibikaji na uwazi katika kuratibu shughuli za menejimenti ya maafa unaofanywa na serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, uwepo wa Sheria ya Maafa, ambayo ni Sheria ya Menejimenti ya Maafa ya mwaka 2015, Mpango wa Taifa wa kujiandaa na Kukabili maafa wa mwaka 2012, Uwezo, Weledi na Uwajibikaji wa watumishi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa katika menejimenti ya maafa pamoja na Ushirikiano mzuri wa serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia Tanzania na Kanda ya Afrika katika masuala ya menejimenti ya maafa nchini. 

Akiongea mara baada ya kufunga zoezi hilo mjini Arusha, tarehe 16, Julai, 2019, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amebainisha kuwa nchi nyingi barani Afrika ikiwemo Tanzania zimekuwa zikifanya mazoezi ya kujiandaa na kukabili maafa kwa kutumia nadharia za maafa yanoyoweza kutokea, lakini zoezi hilo ni tofauti kwani limejikita kwa maafa ambayo yamewahi kutokea kweli hapa nchini. 

“Zoezi hili ambalo limeangalia maafa ya mafuriko yaliyotokea, Kilosa kwa mwaka 2014 na 2016, litatusaidia kuimarisha mifumo yetu serikalini ya kujiandaa na kukabili maafa ya mafuriko na majanga mengine kwani tumejua ni wapi hatukufanya vizuri na namna gani ya kuboresha mifumo yetu, lakini pia zoezi hili litawajengea uwezo waratibu wa maafa serikalini na wataalam kutoka katika mashirika yasiyokuwa ya serikali katika kushirikiana na serikali katika kujiandaa na kukabili maafa yatapotokea” Alisema Matamwe. 

Aidha, washiriki wa zoezi hilo waliweza kutoa uzoefu wao katika kujiandaa na kukabili maafa ya mafuriko ambayo yalitokea wilayani Kilosa kwa mwaka 2014 na 2016. Washiriki hao kwa nyakati tofauti walibainisha kuwa wamejifunza kutoka mafuriko ya Kilosa kuwa ipo haja ya kila Serikali za mitaa na Taasisi za serikali pamoja na wadau wa menejimenti ya maafa kutenga bajeti kwa ajili ya masuala ya usimamizi wa shughuli za maafa. 

Zoezi hilo lililofanyika kwa muda wa siku mbili tarehe 15 hadi 16, Julai, 2019, liliwashirikisha wataalam wa usimamizi wa shughuli za maafa kutoka serikalini na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali, limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

Wafanyakazi JKCI wampongeza Prof.Janabi kwa kuteuliwa kwa mara ya pili kuongoza Taasisi hiyo

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akikata keki iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kumpongeza baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu kuanzia Julai 16, 2019.
Mfanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Justina Lugali akimpatia ua la pongezi lililotolewa na wafanyakazi wa Taasisi hiyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi wakati wa hafla fupi ya kumpongeza baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu kuanzia Julai 16, 2019.Picha na JKCI

RC Hapi Aagiza Askari Polisi Iringa Kukatwa Mshahara Kumlipa kijana Aliyevunjwa Mguu

$
0
0
Mkuu wa Iringa Alli Hapi akitoa akiwahutubia wakazi wa Miyomboni mjini Iringa wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ufunguzi wa stendi mpya ya mkoa eneo la Igumbilo nje kidogo na mji wa Iringa iliyoanza kutumika jana 
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas (kulia) akimkabidhi fedha kiasi cha shilingi 500,000 kijana Maniani Mwakajenge ambae ni mjasiriamali aliyevunjwa mguu wake na polisi baada ya kijana huyo kulalamika katika mkutano wa hadhara wa mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi juu ya polisi kushindwa kumlipa gharama za matibabu kiasi cha Shilingi milioni 1 pamoja na Asas kumsaidia pia mkuu wa mkoa alimchangia Tsh 500,000 kijana huyo 
(Picha na Francis Godwin) 


…………………….. 
NA FRANCIS GODWIN, IRINGA 
Mkoa wa Iringa Alli Hapi ameliagiza jeshi la polisi kuwakata mshahara kiasi cha shilingi milioni 1 askari wake 10 waliohusika kumvunja mguu kijana Maiman Mwakajenge akiwa katika shughuli zake za ujasirimali . 
Kuwa fedha hizo watakazokatwa apewe kijana huyo aliyevunjwa mguu kama sehemu ya kulipia gharama zake za matibabu alizotumia baada ya kuvunjwa mguu na askari hao . 

Mkuu huyo wa mkoa alitoa agizo hilo kwa kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire jana jana katika eneo la stendi kuu ya mkoa baada ya kijana huyo Mwakajengela kulalamika kwenye mkutano wa mkoa huyo wa mkoa kuhusu kutotendewa haki na jeshi la polisi baada ya kuvunjwa mguu. 
Kijana huyo alimweleza mkuu wa mkoa kuwa Februari 2 mwaka huu akiwa katika shughuli zake za biashara eneo la Samora mjini Iringa alikutana na askari polisi waliokuwa doria ambao walimchukua na kumpakia katika gari la polisi na kuanza kumshambulia kwa kipigo na kumvunja mguu wake wa kushoto . 

“ Askari hao walichukua uamuzi wa kunipiga hadi kunivunja mguu wakidai kuwa nimewatukana na baada ya kunivunja mguu nilifanyiwa upasuaji Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa gharama zangu kabla ya uongozi wa chama cha machinga mkoa wa Iringa kuingilia kati na kukaa na jeshi la polisi ambao waliahidi kuwa watakuwa akitoa fedha ya chakula na matibabu kwa ajili yangu na familia ila hadi leo hawafanyi hivi na nawadai kiasi cha shilingi milioni 1 hadi sasa naomba mheshimiwa mkuu wa mkoa nisaidie maana hadi hivi sasa ninatembea na chuma mguuni “ alisema kijana huyo. 

Kwa upande wake Hapi alimtaka kamanda wa polisi mkoa wa Iringa kwa kuwa anataarifa ya kuwepo kwa tukio hilo lililofanywa na askari wake kuwafuata askari wote waliohusika ambao hata hivyo wanafahamika na kuwakata fedha zao za mshahara ili kumlipa kijana huyo fedha yake anayowadai ya gharama za matibabu na chakula kwa muda wote ambao alikuwa Hospitali kiasi hicho cha Tsh milioni 1 anayowadai. 

‘’ Ninakuagiza RPC Bwire fyeka misharaha yao askari sio una posho zao za mishahara Nikishuka kama mwewe nikawadokoa itakuwa balaha sawa bwana utapewa shilingi milioni 1 na mimi kama mkuu wako wa mkoa nitakuchangia shilingi 500,000 na MNEC Salim Asas nae namsemea atakuchangia shilingi 500,000” alisema mkuu huyo wa mkoa huku akimkabidhi fedha taslim kutoka kwake na MNEC Iringa kiasi cha shilingi milioni 1 

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuwa atalifanyia kazi kwa wakati . 
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ametangaza kuvifuta viwanja vyote vilivyopo mbele ya stendi kuu ya mkoa wa Iringa iliyojengwa eneo la Igumbilo viwanja ambavyo walijimilikisha watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na baadhi ya madiwani kuwa viwanja hivyo vitatumika kwa ajili ya wananchi kujenga maduka ya biashara kuzunguka stendi hiyo . 

“ Haiwezekani stendi kubwa kama hii iliyojengwa na serikali kwa shilingi bilioni 3 kujengwa bila maduka ya biashara ama kutenga maeneo ya wafanyabiashara kufanyia shughuli zao ila nimebaini kuwa viwanja vyote vya mbele wamejigawia wao ili kuja kunufaika wao na stendi hii sasa sitaangalia kiwanja kinamilikiwa na naibu meya ama Meya , diwani ama mtumishi wa Manispaa kuanzia sasa nimevifuta vyote na sitaki suala hili kujadiliwa kwenye baraza la madiwani nataka wananchi wote wapate maeneo ya biashara sio vkiongozi “ alisema Hapi .

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images