Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live

MAKAMBA AWAHAKIKISHIA WANANCHI KUSHUKA KWA BEI YA MIFUKO MBADALA

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba amewahakikishia wananchi kuwa bei ya mifuko mbadala itaendelea kushuka. 

Mhe. Makamba amesema hayo wakati akizungumzia tathmini ya kampeni ya katazo la mifuko ya plastiki lililoanza kutekelezwa na Serikali hapa nchini Juni mosi 2019. 

Amesema hivi sasa viwanda vingi vinaendelea kuagiza mitambo ya kutengeneza mifuko mbadala na kuwa hadi kufikia Septemba mwaka huu bei itakuwa imeshuka na ubora wa mifuko hiyo utaongezeka. 

Waziri Makamba alibainisha kuwa changamoto iliyojitokeza ni kwamba zuio la mifuko ya plastiki liliahirishwa mara kwa mara kwani lilishatangazwa siku za nyuma hivyo wawekezaji wa mifuko mbadala walidhani safari hii lingeahirishwa tena hivyo kupelekea kutoagiza mitambo ya kuzalisha mifuko mbadala kwa wakati. 

Itakumbukwa kuanzia mwaka 2010 hadi 2019 Serikali imekuwa ikikutana na wadau ili kujenga uelewa na kukusanya maoni kuhusu nia ya kupiga marufuku mifuko ya plastiki. 

Mhe. Makamba alifafanua kuwa moja ya kazi kubwa ilikuwa ni kuwashawishi tena wawekezaji na wafanyabishara wa mifuko mbadala kuwa safari hii Serikali imeamua kwa dhati kutekeleza katazo la mifuko ya plastiki. “Hivi tunavyoongea tayari wenye viwanda na wafanyabishara wameshtuka na kutumia fursa hii kuingiza mitambo na kuzalisha kwa wingi mifuko mbadala,” alisema. 

Akizungumzia kuhusu malalamiko ya ukubwa wa bei ya mifuko mbadala kutoka kwa wananchi alisema zamani ile mifuko ya plastiki si kweli ilikuwa inatolewa bure unaponunua bidhaa bali ilikuwa inajumuishwa na bei ya bidhaa yenyewe. 

“Unajua watu wanasahau kuwa katika mifuko ya rambo kulikuwa na gharama ya uzalisha lakini bei yake iliingizwa kwenye bidhaa na bei yake ilikuwa ni shilingi hamsini na mia lakini mtu hakwambii, unaenda kununua unga anakwambia ni bure lakini sasa hivi wameamua kutenganisha na watu wanaona bei ni kubwa,” alisema. 

Aliongeza kuwa unapoleta mabadiliko ni lazima uzungumze na wadau na wananchi wayaone mabadiliko unayotaka kuleta kuwa yana manufaa kwao na hawawezi kuyapinga. 

Alisema watu wanapinga mabadiliko kama hawana uhakika kama yatawasaidia, sisi tuliyochofanya ni kuwashawaishi kuyapokea mabadiliko yenye manufaa kwao. Wakati wa utekelezaji wa katazo hilo kumekuwa na changamoto ya bei ya mifuko mbadala kuwa kubwa ambapo mifuko ya non- woven inauzwa kati ya sh. 300 hadi 1500. 

Hata hivyo, Waziri Makamba ameuhakikishia umma wa watanzania kuwa mwenendo wa bei ya mifuko mbadala utaendelea kushuka siku hadi siku

BALOZI WA AFRIKA KUSINI AHAMASISHA WASICHANA KUSOMA SAYANSI NA UHANDISI

$
0
0
Balozi wa Afrika Kusini nchini,Thami Mseleku(wa pili kushoto),Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela(NM-AIST) anayeshughulikia Taaluma,Utafiti na Ubunifu,Profesa Anthony Mshandete(kushoto) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo,Utawala na Fedha,Profesa Charles Lugomela wakati wa maadhinisho ya Wiki ya Nelson Mandela mkoani Arusha. 
Balozi wa Afrika Kusini nchini,Thami Mseleku akimwagilia mti alioupanda katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela(NM-AIST)wakati wa maadhinisho ya Wiki ya Nelson Mandela mkoani Arusha. 
Balozi wa Afrika Kusini nchini,Thami Mseleku(kushoto) akimsikiliza Mtafiti Mwandamizi wa Magonjwa ya Mimea katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela(NM-AIST),Dk Kennedy Jamanga wakati wa maadhinisho ya Wiki ya Nelson Mandela mkoani Arusha . 
Wanafunzi wasichana kutoka Shule mbalimbali wilaya ya Arumeru wakifatilia mada wakati Wiki ya Nelson Mandela inayolenga kuwahamasisha kusoma masomo ya Sayansi na Uandisi. 



Na Mwandishi Wetu,Arusha

Balozi wa Afrika Kusini nchini,Thami Mseleku ameitaka jamii kuwaendeleza wasichana katika masomo ya sayansi kutokana na mchango wake katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nelson Mandela katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela(NM-AIST) mkoani hapa alisema mila na desturi za kuona wavulana pekee ndio wanaopaswa kuwa wanasayansi imepitwa na wakati.

“Jamii kwa ujumla wake inapaswa kuona umuhimu wa kuwapa elimu wasichana kufanya hivyo ni kuwatengenezea maisha yao katika siku zijazo jambo ambalo Hayati Nelson Mandela alilipa kipaumbele,unapompa elimu msichana unakua umeelimisha jamii nzima,”alisema Balozi Mseleku

Naibu Makamu Mkuu wa NM-AIST,Taaluma,Utafiti na Ubunifu,Profesa Anthony Mshandeti alisema uongozi wa Chuo hicho unaadhimisha kwa mwaka wa tano kwaajili ya kuhamaisha masomo ya sayansi na teknolojia kutoa mchango katika kuchangia uchumi wa viwanda.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo hicho,Dk Lilian Passape alisema wiki ya maendeleo itahusisha mambo mbalimbali kwaajili ya wanafunzi wa shule za sekondari,wajasiriamali wanaokutanishwa na taasisi za fedha, maonesho ya ubunifu na kuwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Mount Meru.

Alisema watatumia maadhimisho hayo kugharamia wananchi kupimwa Homa ya Ini na ambao hawatutwa na vimelea vya ugonjwa huo watapewa chanjo na ambao watakutwa nao wataunganishwa na hospitali ya Mount Meru kwaajili ya kuendelea na matibabu zaidi.

TATIZO LA MAJI NA MALISHO LATAFUTIWA UFUMBUZI WILAYANI BABATI

$
0
0

Na. Edward Kondela

Serikali imesema inatafuta suluhu ya kudumu ya upatikanaji wa maji kwa mifugo iliyopo katika kata za Nkaiti, Mwada na Magara zilizopo Wilaya ya Babati Mkoani Manyara bila kuathiri mazingira ya Mto Kou unaopita katika kata hizo.

Akizungumza na baadhi ya wananchi katika Kata ya Mwada mara baada ya kutembelea vijiji vya Vilima Vitatu na Magara ili kutafuta suluhu ya wafugaji kupata maji na malisho ya mifugo yao bila kuathiri Mto Kou uliopo katika Hifadhi ya Burunge ambao ni chanzo cha Ziwa Manyara, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema kuna haja ya kutafuta njia ya kutatua baadhi ya mambo ili kupata suluhu ya matatizo hayo.

“La kwanza kabisa ni upatikanaji wa maji tuangalie namna ya upatikanaji wa maji haraka, la pili tutaunda timu ya wataalam kutoka Wizara za Mifugo na Uvuvi, Maliasili na Utalii, Ardhi, TAMISEMI, Maji na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, la tatu kuna haja ya kuona hawa watu ambao wameondolewa wanatakiwa kwenda wapi na watakwendaje, pia ni vyema kuendelea kushirikiana serikali na wadau hautakaa ufanikiwe kwa kushindana na serikali kikubwa ni mazungumzo na kushauriana pia ule mpango wa matumizi bora ya ardhi unapaswa pia kuangaliwa vizuri.” Amesema Prof. Gabriel

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Babati Bibi Elizabeth Kitundu akizungumza na wafugaji wanaoishi katika eneo la malisho katika Kijiji cha Vilima Vitatu, amewataka waondoke na kwenda kuishi eneo lingine jirani na hapo la Mfulang’ombe ili kupisha eneo hilo libaki kwa malisho ya mifugo pekee.

“Hapa bado serikali ya wilaya na mkoa inasema kwamba hamstahili kukaa hapa eneo lenu linaeleweka mnalotakiwa kukaa ni Mfulang’ombe mtakuwa mnatoa ng’ombe kule mnakuja kuchungia hapa ili muendelee sasa kushirikiana na serikali kuweka miundombinu ya kutosha na maji na hapa mtakuwa mnachungia kwa hiyo muisikilize serikali inavyosema kama kutakuwa na maelekezo mengine mtajulishwa.” Amesema Bibi Kitundu

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa vijiji vilivyopo katika vijiji ambavyo Mto Kou unapita wamesema ni vyema wakapata maji ya kutosha kwa ajili ya mifugo yao bila kuathiri mazingira ya mto ambapo baadhi ya vijiji vimeamua kuchimba visima ili kupata maji ya mifugo yao.

Mara baada ya kikao cha Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo na Prof. Elisante Ole Gabriel wananchi katika Kata ya Mwada, alikaa na viongozi wa Mkoa wa Manyara, Wilaya ya Babati, viongozi wa vijiji na wafugaji ambapo wamejadili baadhi ya mambo ili kupata suluhu ya maji na malisho kwa ajili ya wafugaji wanaoishi katika kata za Nkaiti, Mwada na Magara.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo prof. Elisante Ole Gabriel akimsaidia mwananchi kuchota maji kutoka kwenye kisima kwa ajili ya kunyweshea mifugo.

 Baadhi ya wafugaji wanaotakiwa kuhama kutoka eneo la malisho kwenye Kijiji cha Vilima Vitatu, baada ya kukutwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo prof. Elisante Ole  akikagua Mto Kou  katika Kijiji cha Magara ambao wafugaji wamekatazwa kunyeshwea mifugo ili kulinda mazingira.

BENKI YA NMB YAWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA WILAYANI KIBAHA

$
0
0
Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Baraka Ladislaus (wa pili kushoto) akimkabidhi cheti maalum cha pongezi kwa kufanya biashara kwa uaminifu, mmoja wa wafanyabiashara kilichotolewa na Benki ya NMB kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha jana. 
Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Idara ya Biashara Makao Makuu, Bw. Wogofya Mfalamagoha akimkabidhi cheti maalum cha pongezi kwa kufanya biashara kwa uaminifu, Bi. Salome Shayo kilichotolewa na Benki ya NMB kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha jana. 
Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Baraka Ladislaus (katikati) akizungumza na wafanyabiashara kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Idara ya Biashara Makao Makuu, Bw. Wogofya Mfalamagoha pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kibaha, Hosea Lyatou (wa kwanza kulia) wakifuatilia warsha hiyo.
Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Idara ya Biashara Makao Makuu, Bw. Wogofya Mfalamagoha (kulia) akizungumza na wafanyabiashara hao(hawapo pichani). 
Meneja Mahusiano Biashara wa Benki ya NMB, Kanda ya Mashariki, Bi. Prisca Lius (kushoto) akijibu baadhi ya maswali ya wafanyabiashara (hawapo pichani) kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha. Kongamano hilo lililokuwa na kaulu mbiu ya 'Habaki Mtu...tunasonga Mbele Paamoja' liliandaliwa na Benki ya NMB. 
Meneja wa Benki ya NMB Kibaha, Hosea Lyatou (kulia) akimpongeza mmoja wa wafanyabiashara (kushoto) mara baada ya kutunukiwa cheti maalum na Benki ya NMB kwa kufanya vizuri zaidi katika biashara yake. 
Mkurugenzi Mtendaji wa True Maisha Training Company, Erick Chrispin aakiwasilisha mada kwenye Kongamano la Wafanyabiashara lililoandaliwa na Benki ya NMB Wilayani Kibaha. 
Mmoja wa washiriki katika Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha akiuliza swali jana mara baada ya kupata mafunzo namna ya kukuza biashara zao. Kongamano hilo lililokuwa na kaulu mbiu ya 'Habaki Mtu...tunasonga Mbele Paamoja' liliandaliwa na Benki ya NMB. 
Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha wakiuliza maswali mara baada ya kupata mafunzo namna ya kukuza biashara zao. Kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu ya 'Habaki Mtu...Tunasonga Mbele Pamoja' liliandaliwa na Benki ya NMB. 
Meneja Mikopo NMB Kibaha, Alfred Matovelo akizungumza na wafanyabiashara katika kongamano hilo. 
Sehemu ya washiriki katika Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha wakifuatilia mada mbalimbali kwenye Kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu ya 'Habaki Mtu...Tunasonga Mbele Pamoja' liliandaliwa na Benki ya NMB.

SHULE YA VIPAJI YA KIBAHA SEKONDARI YAJA NA MPANGO KABAMBE WA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANAFUNZI

$
0
0
VICTOR MASANGU, PWANI 

SHULE kongwe ya wavulana ya vipaji maalumu  ya Kibaha sekondari iliyopo  Mkoani  Pwani licha ya  kushika nafasi ya kwa kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita kwa  mwaka wa 2018 na kushika nafasi ya sita kwa mwaka 2019  bado wanafunzi wake kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa walimu ya masomo ya sayansi,uhaba wa vitabu, uchakavu wa miundombinu ya madarasa,uhaba wa vitanda pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo.

Hayo yamebaishwa  na baadhi ya wanafunzi hao akiwemo Jonasi Baraka ambaye ni kaka mkuu wa serikali ya wanafunzi wa shule hiyo  pamoja na Kalani Mahila  ambapo wamedai kuwa serikali ya awamu ya tano inapaswa kulivalia njuga suala hilo kwa kuharakisha kufanya ukarabati wa majengo hayo ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa maisha yao.

Aidha  wanafunzi hao wamesema kwamba   lengo  kubwa ni kuhakikisha wanasoma  katika mazingira rafiki ambayo yatawafanya waongeze kiwango cha ufaulu hivyo wameiomba serikali ya awamu ya tano kuwakarabatia majengo ..vyoo vinavyotumika kwa sasa ni vinne tu, kwa idadi ya wanafunzi ..vyoo vingine vimefungwa kutokana na ubovu ..maabara na walimu wa masomo ya sayansi

“Kwa sasa kwa kweli shule yetu ya Kibaha tunakabiliwa na changamoto mbali mbali lakini kitu kikubwa tunachohitaji kutoka kwa serikali yaawamu ya tano ni kutuboreshea  sekta ya elimu kwa kutufanyia ukarabati wa miundombinu ya majengo mbali mbali yakiwemo ya madarasani, vyoo, pamoja na mabweni ambayo kwa hali yake kwa sasa sio nzuri yamechakaa, na sisis nia yetu ni kushika nafasi ya kwanza kitaifa,”walisema wanafunzi hao.
  
Naye  mmoja wa wajumbe wa kamati ya wazazi ya maendeleo katika shule ya Kibaha Sekondari  Dk. Hamisi Likuli amekiri kuwepo kwa changamoto mbali mbali  zinazowakabili wanafunzi hao,ambapo alibainisha hatua ambazo  tayari wameshazichukua ni kuimarisha huduma ya afya, kuboresha miundombinu ya majengo na vyoo  ,kujenga uzio pamoja na upatikanaji ya huduma ya maji kwa kuweka matanki pamoja na kuchimba kisima.
 
Katika kukabiliana na changamoto hizo Mkuu wa shule hiyo ya Kibaha Chrisdom Ambilikile ameamua kuja na mpango wa kuwakutanisha viongozi mbali mbali wa serikali pamoja,wabunge  pamoja na wadau wengine ambao wamesomea katika shule hiyo kwa  dhumuni la kufanya harambee ambayo inanatajia kufanyia Septemba 9 mwaka huu lengo ikiwa ni kusaidia kutatua changamoto ambazo zinaikabili shule hiyo kwa kipindi cha miaka mingi.
 
Mkuu huyo alibainisha kuwa licha ya shule yake  kushika nafasi ya sita kwa mwaka huu katika matokeo ya kidato cha sita kitaifa  lakini kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kimeongezeka  kwa daraja la kwanza kuwa na wanafunzi wapatao 143 waliopata divisheni 1.
 
“Kwa kweli ukizungumzia kitaalamu utaona sisi shule yetu kwa matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka huu wa 2019 tumeshika nafasi ya sita kitaifa lakini mwaka jana tulishika nafasi ya kwanza lakini kiwango cha daraja la kwanza kimeongezea sana tumepata wanafunzi 143 kwa hivyo utaona tumefanya vizuri na kuwa na nafasi kubwa ya kuwapeleka wanafunzi wengi vyuoni,”alisema Mkuu huyo.
  
Pia mikakati yetu tuliyojiwekea ni kushirikiana bega kwa began a wazazi, pamoja na wadau wa maendeleo katika kuiboresha shule hiyo ambayo wanatarajia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya  mradi mkubwa wa ujenzi wa jengo kubwa la kisasa ambalo litakuwa likitumika kwa matumizi mbali ikiwemo maktaba,kompyuta pamoja na mambo mengine yanayohusiana na elimu.
  

Shule  hiyo kongwe ya Kibaha sekondari yanye wanafunzi 669 na walimu 56 ilianzishwa mwaka 1965  ambapo viongozi mbali mbali wa serikali na wabunge wameweza kusomea hapo akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Spika wa Bunge Goroge Ndugai sambamba na Free Man Mbowe Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pamoja na Razaro Nyarandu.
 Mkuu wa shule  ya  Kibaha Sekondari  Chrisdom Ambilikile akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake  kuhusiana na mikakati mbali mbali  aliyojiwekea katika kuhakikisha anapandisha zaidi kiwango cha elimu, pamoja na mpango wa kufanya harambee kubwa ya kuwakutanisha viongozi wa serikali na wabunge waliosomea katika shule hiyo ili kuzitatua changamoto zilizopo katika sekta ya ellimu.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
 Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita wanaosoma katika shule ya Kibaha sekondari  mkoani Pwani wakiwa darasani wakiendelea na masomo yao ya kawaida kwa ajili ya kujiandaa na mitihani yao mbali mbali ya majaribio na ule wa Taifa.
 Mkuu wa shule  ya  Kibaha Sekondari  Chrisdom Ambilikile akiwaonyesha baadhi ya waandishi wa habari hawapo pichani chumba cha maabara ambacho kimefanyiwa ukarabati na serikali kwa lengo la kuweza kuwapa fursa wanafunzi kujifunza zaidi kwa vitendo
 Kaka mkuu wa serikali ya wanafunzi wa shule  ya Kibaha Sekondari  Jonasi Baraka  akizungumzia changamoto mbali mbali zinazowakabili katika shule hiyo pamoja na mipango waliyojiwekea katika kuongeza kiwango  cha ufaulu katika matokeo yajayo ya kidato cha sita.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya wazazi ya maendeleo katika shule ya Kibaha Sekondari  Dk. Hamisi Likuli akifafanua jambo kuhusiana na hatua mbali mbali ambazo tayari wameshazichukua katika kuhakikisha wanashirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu katika shule hiyo.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).

TASTE OF TANZANIA EXPO SEPT 14, 2019 DMV

$
0
0


ATTN ALL ENTREPRENEURS

VENDORS ARE WELCOME, IT IS YOUR DAY!

COME & SHOWCASE YOUR PRODUCTS/ SERVICES

FOR US BY US

Themes:
Entrepreneurship& Networking
Sectors:
1)Tourism
2)Agro bussiness
3)Mining
4)Real Estate
5)Finance
6)Technology
7)Health
&Many more

For vendor registration please send $25/table to
ATC Metro Treasure Lysa Bantu CashApp (919) 452-2746
or TD Bank acc# 5350560920
Routing # 054001725


Thank you.
Free Entrance for All
KARIBUNI

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada Bukoba katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole.

$
0
0
Wakazi wa Bukoba mkoani Kagera na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Meneja wa Kanda ya Ziwa wa TCRA Francis Mihayo amesema ni fursa kwa wananchi wa Bukoba kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa mawasiliano. 

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano.

Mihayo amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole. "TCRA iko karibu na wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema Mihayo.
 Mkuu wa Kitengo wa Huduma za Bidhaa za Mawasiliano wa TCRA, Thadayo Ringo akizungumza na wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada wilayani Bukoba.
 Wananchi wakisoma kitabu cha Muongozo cha TCRA.
 Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akizungumza katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada kwa kushirikiana na wadau Wilayani Bukoba mkoani Kagera.
 Mwananchi akitoa maelezo katika fomu katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Bukoba
 Wananchi wakipata huduma katika banda Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA
 Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Mawasiliano (TCRA) Thadayo Ringo akisilimiana na wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA ndani ya Bukoba.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) Thomas William akizungumza na wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA wilayani Bukoba.

NBAA yajihimarisha usajili wa mitihani

$
0
0
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imesema kuwa wanaohitaji kufanya mitihani ya Bodi usajili umeanza sasa.

Akizungumza katika maonesho ya elimu ya Vyuo Vikuu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA Magreth Kageya amesema kuwa mithani hiyo inatarajiwa kufanyika  mwezi Novemba mwaka 2019.

NBAA inashiriki maonesho ya Vyuo Vikuu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ili kuonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi waliofika kwenye banda la Bodi hiyo.

Baadhi ya huduma zinazotolewa na NBAA katika kipindi hiki cha maonesho ya Vyuo Vikuu ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali  kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician)  mpaka  ile ya Taaluma (Profession) pamoja na usajili wa wanachama  na makampuni ya kihasibu na Kikaguzi.

"Tumedhamiria kutoa huduma zetu kiurahisi kwa wale wanaofanya mitihani ya Bodi na wanachama wetu ili waweze kutambulika na Taasisi mbalimbali katika umahiri wa kazi za Kihasibu na Kikaguzi" amesema Kageya 
Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye(katikati) akiwaonesha namna wanavyotoa mafunzo pamoja na utoaji wa Mitihani  kwa baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkaguzi wa Viwango vya Wakaguzi wa Hesabu wa NBAA, CPA Winnington Makaka.
Mwanafunzi Geraldina Tarimo(kulia) akiuliza swali kwa maofisa wa NBAA alipotembelea Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye. na Katikati ni Msaidizi wa Uhasibu wa NBAA, David Iman.
Msaidizi wa Uhasibu wa NBAA, David Iman akitoa maelezo kwa mwanafunzi Geraldina Tarimo(kulia) alipotembelea Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye.
Afisa Masoko na Mawasiliano kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Magreth Kageya(wa pili kushoto) akitoa maelezo jinsi Bodi hiyo inavyofaya kazi kwa wanafunzi waliotembelea banda hilo kwenye Maonesho ya Vyuo vikuu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkaguzi wa Viwango vya Wakaguzi wa Hesabu wa NBAA, CPA Winnington Makaka.
Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye(kushoto) akitoa maelezo kuhusu namna mitihani ya Bodi hiyo inavyotolewa pamoja na gharama kwa mwanafunzi Stanley Beli(kulia) alipotembelea Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 
Mkaguzi wa Viwango vya Wakaguzi wa Hesabu wa NBAA, CPA Winnington Makaka (kushoto) akitoa ufafanuzi namna ya kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa Trypone Richard (kulia) alipotembelea Banda la Bodi ya TaifaA ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye(katikati) akitoa ufafanuzi kwa mwanafunzi Stanley Beli (kulia) aliyefika kwenye Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mkaguzi wa Viwango vya Wakaguzi wa Hesabu wa NBAA, CPA Winnington Makaka.
Msaidizi wa Uhasibu wa NBAA, David Iman  akimsikiliza mwananchi aliyefika kwenye banda la NBAA katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU AZINDUA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA

$
0
0
*Ahimiza vijana wajitokeze kwa wingi, aonya asasi za kiraia za kutoa elimu ya mpigakura zisijihusishe na ushabiki wa kisiasa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua rasmi zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuwahimiza vijana waliotimiza miaka 18 wajitokeze kwa wingi kujiandikisha.

“Nitoe rai kwa vijana wote wa Kitanzania waliotimiza umri wa miaka 18 au wale ambao watatimiza umri huo ifikapo Oktoba, 2020 wajitokeze kwa wingi na kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Hawa ndio walengwa wakuu kwa sababu wanaingia kwa mara ya kwanza katika uchaguzi.”

“Ikumbukwe kwamba, bila kujiandikisha hawataweza kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka. Hivyo, kujiandikisha kwao kutawahakikishia ushiriki wao katika uchaguzi wa viongozi,” amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu ametoa rai hiyo leo, (Alhamisi, Julai 18, 2019) wakati akizindua zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililofanyika kwenye uwanja wa Mandela, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkuu ambaye amewasili mkoani Kilimanjaro leo asubuhi kwa ziara ya kikazi za siku nne, ametumia fursa hiyo kuwasisitiza vijana na wale wanaorekebisha taarifa zao kwamba hakuna mtu atakayeruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kama hajajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ama hana kadi ya mpigakura.

Amesema zoezi hilo ambalo limeanza leo, linafanyika kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Amesema litafanyika nchi nzima na linatarajiwa kukamilika Machi, 2020.

“Watakaohusika awamu hii ni wapigakura waliotimiza miaka 18 hivi karibuni, wale watakaotimiza miaka 18 wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020, waliohama kata au Jimbo na kuhamia maeneo mengine ya kiuchaguzi, waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika, wanaohitaji kurekebisha taarifa zao mfano majina ambayo hapo awali yalikuwa yamekosewa sambamba na kuwaondoa wapiga kura waliopoteza sifa kama vile kufariki,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziasa asasi za kiraia ambazo zimepewa vibali vya kutoa elimu ya mpigakura, zijiepushe na ushabiki wa kisiasa na badala yake zizingatie mwongozo wa elimu ya mpigakura uliotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

“Nimeambiwa, Tume imetoa vibali vya kutoa elimu ya mpigakura kwa baadhi ya Asasi za Kiraia. Rai yangu kwa asasi zilizopata vibali hivyo ni kuendelea kutoa elimu hiyo kwa wananchi kwa kuzingatia mwongozo wa uliotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Niendelee kuwaasa pia kutohusisha ushabiki na mijadala ya kisiasa muda wote mtakapokuwa mkitoa elimu hiyo,” amesema.

Amesema ana imani kuwa wananchi wakipata elimu kuhusu uboreshaji kama inavyoendelea kutolewa, basi watahamasika kutumia haki yao ya kikatiba ya kujiandikisha katika daftari hilo na hatimaye kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Amesema zoezi la majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kata ya Kibuta katika Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe na Kata ya Kihonda katika Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Morogoro, lilifanyika kwa mafanikio makubwa.

Mapema, akitoa maelezo kuhusu zoezi hilo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage, alisema katika zoezi la sasa, Tume itaendelea kutumia teknolojia ya kielektroniki ya Biometric (BVR) na imeandaa BVR kits 3,000.

Alisema kwa Tanzania Bara, Tume hiyo imeongeza vituo vya uandikishaji kutoka 36,549 vilivyotumika mwaka 2015 hadi kufikia 37,407; kutokana na zoezi la uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura lililoendeshwa mwaka jana.

“Kutokana na hilo, vituo 6,208 vilibadilishwa majina, vituo 817 vimehamishwa kutoka mtaa mmoja au kijiji kimoja na kwenda kingine na vituo 19 vilihamishwa kutoka kata moja kwenda kata nyingine.”

“Kwa upande wa Zanzibar, vituo vya uandikishaji vimeongezeka kutoka 380 na kufikia 407. Kwa sasa kila kijiji au mtaa, utakuwa na kituo kimoja,” alisema.

Alisema vituo vya uandikishaji vitafunguliwa saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni na zoezi la uboreshaji litafanyika kwa siku saba kwa kila kituo cha kujiandikisha iwe ni Tanzania Bara au Zanzibar.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe, wakati akizindua zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, katika viwanja vya Mandela mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akishuhudia kijana Nehemia Mhando, akiandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, katika uzinduzi wa daftari hilo, uliyofanyika kwenye viwanja vya Mandela mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimkabidhi kadi ya kupigia kura, kijana Nehemia Mhando, baada ya kuzindua daftari la kudumu la wapiga kura, katika uzinduzi wa daftari hilo, uliyofanyika kwenye viwanja vya Mandela mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).   
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Walemavu, Jenista Mhagama, katika uzinduzi wa daftari la kudumu la wapiga kura, uliyofanyika kwenye viwanja vya Mandela mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiketa jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage, kabla ya uzinduzi wa daftari la kudumu la wapiga kura, uliyofanyika kwenye viwanja vya Mandela mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Walemavu, Jenista Mhagama, akizungumza na wananchi waliyohudhuria katika uzinduzi wa daftari la kudumu la wapiga kura, uliyofanyika kwenye viwanja vya Mandela mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi waliyohudhuria katika uzinduzi wa daftari la kudumu la wapiga kura, uliyofanyika kwenye viwanja vya Mandela mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019.

KAMPENI YA PLASTIKI NOMA YATIKISA DARAJA LA SALENDER

$
0
0

*Vijana wajitokeza kufanya usafi na wahaidi kuwa mabalozi bora kuhusiana na madhara yatokanayo plastiki

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
VIJANA kutoka Wilaya zote za jiji la Dar es Salaam wamejitokeza na kufanya usafi katika daraja la Salender ikiwa nk kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupiga vita matumizi ya plastiki pamoja na kutekeleza kampeni iliyozalishwa kupitia utafiti uliofanywa na watafiti kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam kuhusiana na madhara ya taka za plastiki katika bahari ya Hindi.

Akizungumza katika zoezi hilo mhadhiri na mtafiti kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Lydia Gasper amesema kuwa zoezi la usafi ni endelevu na katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililoanza mapema mwezi Juni limesaidia sana na kinachotakiwa kwa sasa ni kuzidi kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya matumizi ya plastiki.

Amesema kuwa utafiti kuhusiana na madhara ya plastiki unaendelea na wanaamini suluhu ya tatizo hilo ambalo linaathiri mazingira na viumbe hasa wabaharini itapatikana.

Aidha amesema kuwa usafi huo ulioshirikisha taasisi ya baba watoto unategemewa kuzaa matunda na hiyo ni baada ya watoto hao kuwa mabalozi kwa wenzao katika kutoa elimu kuhusiana na madhara ya kutumia mifuko ya plastiki.

Baadhi ya watoto hao wameeleza kuwa baada ya kupata elimu kutoka kwa wataalamu hao watayatumia vyema maarifa hayo kwa kutoa elimu kwa vijana wengine kuhusiana na madhara yatokanayo na plastiki pamoja na fursa wanazoweza kujipatia kupitia plastiki hizo.

Utafiti huo umehusisha watafiti wanne kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam wakiwemo Dkt. Lydia Gaspare, Dkt. Rose Massalu, DKt. Benjamin Ngatunga na Dkt. Vicensia Shule.
 Mhadhiri na mtafiti kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Lydia Gasper  akizungumza na wanahabari mara baada ya kufanya usafi katika eneo la daraja la Salender ambapo amesema kuwa wataendelea na utafiti pamoja na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
 
 
Baadhi ya vijana wakiendelea na shughuli ya usafi katika eneo la daraja la Salender, leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya taka zilizokusanywa katika kampeni hiyo ya Plastiki noma iliyofanyika leo katika daraja la Salender jijini Dar es Salaam.

FINLAND YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 24 KWA AJILI YA PROGRAM YA KUPANDA MITI KIBIASHARA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Finland imeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 9.4 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 24 kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Program ya Panda Miti Kibiashara.

Mkataba wa msaada huo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Kaimu Balozi wa Finland hapa nchini Bw. Kari Leppanen.

“Ninaishukuru Jamhuri ya Finland kwa kutoa msaada huu ukitanguliwa na msaada mwingine kama huo wa Euro milioni 19.5, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 49.8, ambazo Finland ilizitoa kwa ajili ya kutekeleza Awamu ya Kwanza ya Mradi huo kati ya mwaka 2014-2018” alisema Bw. James

Alisema kuwa program hiyo ya Upandaji Shirikishi wa Miti awamu ya Pili, ni mojawapo ya vipaumbele vya juu katika ajenda ya maendeleo ya Serikali, yenye malengo ya kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi.

“Lengo kuu la program hii ni kuchochea upandaji miti endelevu na jumuishi kwa ajili ya kuchangia katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini” aliongeza Bw. James

Bw. James alifafanua kuwa program hiyo itasaidia kuongeza mashamba ya misitu itakayoleta faida za kijamii, kimazingira, kifedha katika maeneo ya mradi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania ikiwemo Ruvuma, Iringa, Njombe na Morogoro

“Program hii pia itaongeza kipato cha wamiliki binafsi wa misitu, Vikundi Vidogovidogo na vya Kati vya Ujasiriamali (SMEs) na Kaya mbalimbali katika eneo la mradi” alisisitiza Bw. James

Alizitaja faida nyingine za mradi kuwa ni pamoja na kuimarisha vikundi wa wapandaji miti kwa kuviwezesha kupata usajili, kuviwezesha kiuongozi na namna ya kujiendesha. 

Aidha, wadau wote wa misitu watajengewa uwezo kupitia upandaji miti na usimamizi wa mashamba hayo, kuongeza uwezo na rasilimali za kudhibiti moto katika mashamba ya miti, kusaidia vijiji kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi na kuongeza ubora wa mazao ya misitu katika mnyororo wa thamani.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Finland hapa nchini Bw. Kari Leppanen, pamoja na kuipongeza Tanzania kwa ufanisi mzuri katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa program hiyo, alisema Tanzania ni moja ya mataifa yanayofanya vizuri katika usimamizi wa misitu hatua iliyolivutia taifa hilo kushiriki katika kuilinda.

Aliwataka wasimamizi wa program hiyo ya Panda Miti Kibiashara kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo majukumu ya usimamizi wa misitu hiyo na hivyo kustawisha hali kijani kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James walioketi (kulia) na Kaimu Balozi wa Finland hapa nchini Bw. Kari Leppanen, wakisaini hati ya makubaliano ya msaada wa shilingi bilioni 24 ambazo Serikali ya Finland imeipatia Tanzania kwa ajili ya kutekeleza Awamu ya Pili ya Program ya Panda Miti Kibiashara.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James walioketi (kulia) na Kaimu Balozi wa Finland hapa nchini Bw. Kari Leppanen, wabadilishana mikataba ya makubaliano ya msaada wa shilingi bilioni 24 ambazo Serikali ya Finland imeipatia Tanzania kwa ajili ya kutekeleza Awamu ya Pili ya Program ya Panda Miti Kibiashara.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James aliyeketi (kulia) akizungumza na vyombo vya habari wakati wa tukio la kusaini  mkataba wa makubaliano ya msaada wa shilingi bilioni 24 ambazo Serikali ya Finland imeipatia Tanzania kwa ajili ya kutekeleza Awamu ya Pili ya Program ya Panda Miti Kibiashara Leppanen, wabadilishana. Kushoto ni Kaimu Balozi wa Finland hapa nchini Bw. Kari Leppanen.
Kaimu Balozi wa Finland hapa nchini Bw. Kari Leppanen, aliyeketi mbele (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari wakati wa tukio la kusaini  mkataba wa makubaliano ya msaada wa shilingi bilioni 24 ambazo Serikali ya Finland imeipatia Tanzania kwa ajili ya kutekeleza Awamu ya Pili ya Program ya Panda Miti Kibiashara Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

SUA yajiimarisha katika utoaji wa elimu bora

$
0
0
Wanafunzi wakisoma machapisho  ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha  Kilimo (SUA) wakati walipotembelea Banda la SUA katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Afisa Udahili John Lyatuu wa SUA akifanya udahili wa Wanafunzi katika maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakiwa katika banda SUA katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Huduma zikiendelea
Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibuda akiwa picha ya pamoja Wafanyakazi wa Chuo hicho katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Cha SUA Profesa Raphael Chibuda akijadiliana na Watendaji Wakuu katika Vyuo Vikuu katika maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibuda akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam William Anangisye katika ufunguzi maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

BODI YA URATIBU MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YAKUTANA YAJIDHATITI KATIKA KUSIMAMIA USAJILI NA URATIBU WA MASHIRIKA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Dkt. Faustine Sambaiga (kushoto) akifungua kikao cha 41 cha Bodi hiyo kilichokutana katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili mwenendo wa uratibu na usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.
 Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao (wa kwanza kulia) ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya NGO’s akisoma muhtasari wa kikao cha 41 cha Bodi hiyo kilichokutana katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili mwenendo wa uratibu na usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.
 Wajumbe wa Bodi ya Mashrika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia agenda mbalimbali katika kikao cha Bodi hiyo kilichokutana katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili mwenendo wa uratibu na usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.


  Wajumbe wa Bodi ya Mashrika Yasiyo ya Kiserikali na Sekretarieti kutoka ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia agenda mbalimbali kikao cha Bodi hiyo kilichokutana katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili mwenendo wa uratibu una usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.
Baadhi ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakipata huduma ya kusajili Mashirika yao katika zoezi linaloendeshwa na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa Kanda ya Mashariki katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar Es Salaam.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

PICHA MBALI MBALI ZA KUWASILI KWA NDEGE YA ATCL MJINI MUMBAI NCHINI INDIA

$
0
0

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Isaack Kamwelwe akikata utepe muda mfupi baada ya Ndege ya Air Tanzania Boing 787-8 Dreamliner kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chhatrapati Shivaji, Mumbai nchini India alfajiri ya leo Julai 18, 2019. Ndege hiyo imeanza safari yake ya kwanza ya kutoka nje ya bara la Afrika huku zingine zikitazamiwa siku za mbeleni. Hii ni safari ya sita kwa safari za kimataifa kwa Ndege za Air Tanzania.

TANZANIA YANG’ARA UMOJA WA MATAIFA UTEKELEZAJI SDGs

$
0
0
Na Saidina Msangi, WFM, New York, Marekani

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amewasilisha ripoti ya Tanzania kwa mara ya kwanza ya Mapitio ya Hiyari ya Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Mikutano ya Jukwaa la Juu la Kisiasa la Ngazi za Mawaziri chini ya Umoja wa Mataifa inayofanyika New York nchini Marekani.

Akiwasilisha ripoti hiyo Waziri Mpango ameeleza kuwa Tanzania imefanikiwa katika utekelezaji wa malengo 17 yaliyoamuliwa kutekelezwa na nchi zote ulimwenguni ili kuondokana na umasikini na kuharakisha maendeleo katika nyanja zote.

Akizungumzia lengo namba nne lenye kuangazia elimu jumuishi na bora kwa wote, Dkt. Mpango ameeleza kuwa Tanzania imepiga hatua katika uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza ambao wana mwaka mmoja wa elimu ya awali kwa asilimia 95.6 mwaka 2018 ambayo ni juu ya makadirio ya asilimia 87.5 ifikapo mwaka 2020.

Aidha, wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza wameongezeka kwa asilimia 17.4 ikiwa ni kutokana na mafanikio ya elimu bure chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Pia Dkt. Mpango aliongeza kuwa Tanzania imefanikiwa katika maeneo ya utoaji huduma bora za afya, uongozi bora na amani ya nchi kwa ujumla.

Ripoti hiyo imepokelewa vizuri katika Jukwaa hilo la Umoja wa Mataifa ambapo nchi zilizotoa maoni kuhusu ripoti hiyo ikiwemo Kenya zimepongeza juhudi zilizofikiwa na Tanzania katika utekelezaji wa malengo endelevu.

“Malengo haya ndio dira ya maendeleo na yanaunganika na mipango yetu ya maendeleo kwa pande zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanaendana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, na MKUZA kwa upande wa Zanzibar hivyo ni lazima tutekeleze malengo haya kwa bidii,” alisema Waziri Mpango.

Dkt. Mpango ametoa wito kwa Jumuiya ya Umoja wa Mataifa na nchi zenye utaalamu kuisaidia Tanzania katika matumizi ya teknolojia ili kuweza kufikia azma ya malengo endelevu upande wa utunzaji wa mazingira.

Waziri Mpango amewashukuru wadau wote, sekta binafsi na taasisi zisizo za kiserikali kwa ushiriki wao katika kuandaa ripoti hiyo kwa kiwango kizuri. Aidha ametoa wito kwa taasisi na sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa rasilimali fedha na utaalamu zitumike kwa ajili ya kushughulikia utekelezaji wa malengo endelevu. 

Tanzania imeungana na nchi zote duniani katika utekelezaji wa malengo 17 yaliyoazimishwa miaka minne iliyopita ikiwa ni mkakati wa kufikia ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu.

Mikutano hiyo yenye kauli mbiu uwezeshaji wa watu na kuhakikisha ujumuishwaji na usawa imekutanisha nchi mbalimbali ambazo zimetuma wawakilishi kutoka Serikalini na Sekta binafsi, inatoa fursa kwa nchi kuweza kutathmini mafanikio, changanoto na mambo ya kujifunza katika kuelekea utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipongezwa na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez, baada ya kuwasilisha ripoti ya Tanzania kwa mara ya kwanza ya Mapitio ya Hiyari ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika mikutano ya Jukwaa la Juu la Kisiasa la Ngazi za Mawaziri chini ya Umoja wa Mataifa inayofanyika New York nchini Marekani. Katikati ni Mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Balozi Modest Mero
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania baada ya kuwasilisha ripoti ya Hiyari ya Utekelezaji wa Malengo Endelevu katika mikutano ya Jukwaa la Juu la Kisiasa la Ngazi za Mawaziri New York nchini Marekani.(Picha na Saidina Msangi, WFM, New York Marekani)
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto), akiwasilisha ripoti ya Tanzania kwa mara ya kwanza ya Mapitio ya Hiyari ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika mikutano ya Jukwaa la Juu la Kisiasa la Ngazi za Mawaziri chini ya Umoja wa Mataifa inayofanyika New York nchini Marekani.

Mradi wa DMDP Kuliboresha Jiji la Dar es Salaam.

$
0
0
 Muonekano wa barabara zilizojengw kupitia fedha za Dar es Salaam Metropolitan Development Project (DMDP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wilayani Temeke. 

Ujenzi wa soko kisasa linalojengwa Jijini Dar es Salaam kwa ufadhhili wa mradi wa Dar es Salaam Metropolitan Development Project (DMDP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.




Na. Lilian Lundo - MAELEZO.

Jiji la Dar es Salaam ni kati ya majiji sita yaliyoko nchini Tanzania, likiwa Jiji la kwanza lenye idadi kubwa ya watu, ambapo kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 ilikuwa na watu 4,364,541 kati ya watu 44,928,923 nchi nzima. 

Kutokana na wingi huo wa watu, Jiji hilo limekuwa na changamoto nyingi kama vile foleni za magari, miundo- mbinu hafifu pamoja na baadhi ya maeneo kuathirika na mafuriko katika kipindi cha mvua.

Serikali ya Awamu ya Tano kwa kushirikiana na Mradi wa Dar es Salaam Metropolitan Development Project (DMDP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ipo katika utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu katika Jiji hilo, ujenzi unaofanyika kwa mafungu kumi ambao ujenzi huo ulianza rasmi mwaka 2016 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.

Ujenzi unaofanyika ni pamoja na ujenzi wa barabara za lami katika mitaa ya Jiji ambazo zinajengwa sambasamba na mifereji ya maji , taa za barabarani za sola, madaraja, masoko ya kisasa ambayo pia yatakuwa na huduma za kibenki pamoja na vyoo vya umma.

Akizungumza kuhusu mradi huo, mratibu wa DMDP Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, Mhandisi Mkelewe Masalu Tungaraza amesema ujenzi wa miundombinu unaendelea ambapo mpaka sasa kuna barabara ambazo ziko katika hatua za ukamilishaji kama vile barabara za kuzunguka stendi za Makumbusho na barabara za Shekilango, Sinza

"Tunataka mtu akiwa Dar es Salaam aweze kuchepuka kwenda barabara nyingine, ili kupunguza foleni katika barabara kubwa.Vile vile, taa zitakazojengwa katika barabara hizo zitaimarisha usalama katika maeneo yanayozungukwa na barabara hizo," amesema Mhandisi Tungaraza.

Ameendelea kusema, barabara zitakazojengwa ni suluhisho kubwa kwa maeneo ambayo yalikuwa yanakumbwa na mafuriko kwani barabara hizo zinajengwa sambasamba na mifereje ya maji ya mvua na madaraja kwa maeneo ambayo ni sumbufu.

Mhandisi Tungaraza ametaja maeneo ambayo yatajengwa vyoo vya umma kwa Wilaya ya Kinondoni kuwa ni Tandale, Mburahati na Mwananyamala, ambapo uanishaji wa maeneo hayo umetokana na uhitaji wa huduma hiyo kwa wananchi wa maeneo husika.

Kwa upande wa Mchumi wa Manispaa ya Ubungo, George Maiga amesema mradi wa DMDP unatarajia kujenga soko kubwa na la kisasa Mburahati kwa gharama ya shilingi bilioni. 2.079 ambapo itahusisha Jengo Kuu, eneo la Mama na Baba Lishe, Maliwato, eneo la wafanyabiashara wadogo wadogo , maduka, benki, machinjio ya kisasa na maduka ya kisasa.

"Ujenzi wa masoko haya umetokana na ongezeko kubwa la watu Jijini Dar es Salaam hivyo kusababisha kuzuka masoko mengi yasiyo rasmi katika mitaa," amesema Maiga. Amesema katika gharama hiyo ya mradi, Serikali imetoa shilingi milioni 900 ambayo ilitolewa ili kukamilisha mradi huo badala ya kwenda kukopa benki.Ameeleza kuwa, mara soko hilo litakapokamilika litaongeza mapato ya Halmashauri na wafanyabiashara wadogo wadogo watapata eneo la uhakika la kufanyia biashara.

Aidha, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kijichi, Manispaa ya Temeke, Anaclet Hayuka amesema soko linalojengwa Kijichi litakuwa na huduma zote muhimu pamoja na ofisi za maafisa Afya ili kufanya ukaguzi wa bidhaa mara kwa mara."Miaka mitatu ya utawala wa Rais Magufuli wananchi wameanza kuona cheche za maendeleo kupitia mradi wa DMDP," amesema Hayuka.

ULEGA AKUTANA NA WATENDAJI WA VIJIJI,KATA ZOTE WILAYANI MKURANGA

$
0
0
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la mkuranga mkoani Pwani mh ABDALLAH H ULEGA alifanya kikao na watendaji wa vijiji na kata zote zilizo katika Jimbo lake la mkuranga,

Ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa ni tathmini ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa chama Cha mapinduzi na maendeleo Kwa wananchi wilayani hapo,

Pi kikao hicho kilijikita katika kujadili Kero na changamoto mbalimbali Ktk utekelezaji wa kazi zao ili kurahisisha maendeleo kwa wananchi Mkuranga.

Watendaji hao pamoja na kueleza Baadhi ya Changamoto chache katika utendaji wao kazi wametoa pongezi Kwa Mbunge huyo wa mkuranga Kwa jinsi wanavyoshirikiana nae vizuri na kupongeza uchapakazi wake uliotukuka Kwa kuwapigania wanamkuranga ktk kuwaletea maendeleo wananchi wake na kuahidi kutoa ushirikiano kwake pale itakapohitajika Kwa maslahi mapana ya wananchi,

Vile vile watendaji hao hawakusita kuipongeza serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais JOHN POMBE MAGUFULI na watumishi wake wote Nchini Kwa uwajibikaji na uchapaji kazi na Nidhamu katika kazi.

Mh Abdallah Hamis Ulega ambaye ni Mbunge wa Jimbo la mkuranga pia hakusita kuwapongeza watendaji hao Kwa jinsi wanavyowajibika na kuwataka wafanye kazi zao naye Yuko pamoja nae kwaajili ya kuwatumikia wanamkuranga wote bila kujali itikadi zao.

MBUNGE JIMBO LA MUHEZA BALOZI ADADI AUMIZWA NA ZAO LA MACHUNGWA

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akizungumza wakati akifungua kikao cha Jukwaa la Wadau wa Machungwa wilayani humo kushoto ni Afisa Kilimo wa wilaya ya Muheza Hayange Mbwambo na kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo
Afisa Kilimo wa wilaya ya Muheza Hayange Mbwambo akizungumza wakati wa Jukwaa hilo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu
Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Benard Mhagama akizungumza katika Jukwaa hilo
MBUNGE wa Viti Maalumu (Chadema) Mkoa wa Tanga Yosepher Komba akizungumza katika Jukwaa hilo
Mtaalamu wa Kilimo kutoka Chuo cha Kilimo Mlingano wilayani Muheza akisisitiza jambo kwenye Jukwaa hilo
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho wakifuatilia Jukwaa hilo
Sehemu ya washiriki wa Jukwaa la Machungwa wakifuatilia kikao
Sehemu ya washiriki wa Jukwaa la Machungwa wakifuatilia kikao hicho
Sehemu ya wadau kwenye Jukwaa hiloSehemu ya wadau wa kikao hicho
Sehemu ya washiriki kwenye kikao hicho


MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu amesema anaumia sana anapoona zao la machungwa ambalo linalimwa kwa wingi wilayani humo kutokupata thamani kama yalivyokuwa mazao mengine hapa nchini. 

Lakini pia amesema anapokaa na kuona zao la chungwa linaharibika kwa kutupwa onyoovyo jambo hilo limekuwa likiwakera na kuwapa wakati mgumu kutokana na kuona linashuhwa thamani yake iliyonayo 

Balozi Adadi aliyasema hayo juzi wakati akizungumza katika Jukwaa la Wadau wa Machungwa lililofanyika wilayani humo na kushirikisha wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kifedha,wasafirishaji,wakulima ,vyama vya ushirika,wafanyabiashara ,walaji na wasindikaji. Alisema kwamba kwani zao hilo ambalo linalimwa wilayani humo na tamu nchi nzima linapatikana huko lakini bado limekuwa halipewi thamani ambayo inashahili jambo ambalo limekuwa likimnyima raha kila wakati 

“Mimi ni mdau wa zao machungwa na ninalima eka nyingi lakini ninapata uchungu ninapoona Tunda ,zao la hili ambalo linalimwa Jimboni kwangu Muheza na Tamu nchi nzima kuona halipati thamani ile ambavyo inastahili”Alisema Mbunge huyo. 

Aidha pia alisema tunda hilo limekuwa halina thamani kutokana na kwamba wakulima wake tunauza kwa bei ya kutupa ndogo hivyo ninaamini jukwaa hili ni zuri kwa sababu hiyo changamoto kama hizo tutaona namna ya kuzipatia ufumbuzi kuweza kuondokana na hilo tatizo 

Mbunge huyo alisema kwamba changamoto zinaanzia kwenye mbegu yenyewe ,ulimaji,utunzaji,uvunaji mpaka kwenye kuvuna,kuuza na soko lenyewe huo msururu wote una vikwazo vipo katikati na ndio maana kwenye jukwaa hilo wanatakiwa kukaa mara kwa mara ili kuweza kujua namna ya kukabiliana nazo. 

Hata hivyo alisema kwamba wanapokaa na kuona zao la chungwa linaharibika linatupwa ovyoovyo inamuuma sana huku akieleza namna alivyopambana kuwashawishi wawekezaji na kuwafikisha wilayani humo . 

“Niliwashai kuleta wawekezaji na mara ya kwisho walikuja wachina na wote wanasema matunda ya muheza ni matamu sana mazuri lakini ni machache kwa hiyo sio matunda ya kuweza kuweka kiwanda lakini ukipita barabarani machungwa yamesambaa lakini unaambiwa hawatoshi kuweka kiwanda wawekezaji wawili wamekiwsha kufika lakini naambiwa hivyo hii inaniumiza sana “Alisema 

Awali akizungumza katika Jukwaa hilo Afisa Kilimo wa wilaya ya Muheza Hayange Mbwambo alisema wameamua kuitisha Jukwaa hilo ili kujadili kwa pamoja na wadau kwenye wilaya na nje ya wilaya hiyo changamoto za uzalishaji wa zao la machungwa na usindikaji kwa sababu wamegundua wilaya muheza ina uwezo wa kuzalisha kwa kiwango kikubwa zao hilo na kuwaletea wakulima kipato kikubwa kwa kukuza uchumi wao na halmashauri kwa ujumla. 

Alisema kwamba muda mrefu wamekuwa wakizalisha zao la machungwa lakini changamoto nyingi ni magonjwa wakiwemo wadudu pamoja na tatizo la wafanyabishara wanaokuja kuwarubini wakulima kwa kuwapa fedha kabla ya machungwa kukomaa. 

Alisema hali hiyo inapelekea kulazimisha kuivisha machungwa kwa moto na kufanya ubora wa machungwa kwenye soko kuwa mdogo lakini pia kufanya walaji wa wa nje ya wilaya kuona machungwa sio bora na hivyo mwisho ya siku inawezekana zao hilo likashuka kupata wanunuzi kutokana na kwa sababu ya ubora hafifu unaotokana na kulazimisha kuivisha machungwa kwa moto. 

BENKI YA TPB YATOA MSAADA WA RANGI KUPENDEZESHA SHULE YA SEKONDARI BULUBA

$
0
0
Benki ya TPB imetoa msaada wa rangi ndoo 50 katika shule ya Sekondari Buluba iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kupendezesha mandhari ya shule hiyo na kuiweka katika mazingira mazuri ili wanafunzi wajisomee kwa bidii na kupata ufaulu mzuri.

Msaada wa ndoo za rangi umetolewa leo Julai 18,2019 shuleni hapo na Mkurugenzi wa Masoko kutoka makao makuu ya benki ya TPB, Deogratius Kwiyuka akimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sabasaba Moshigi na kuhudhuriwa pia na Uongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU) ambao ndiyo wamiliki wa shule hiyo. 

Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya makabidhiano hayo,Mkurugenzi wa Masoko wa Benki hiyo Kwiyuka, amesema wanaunga Juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuboresha elimu hapa nchini, hivyo wao kama wadau wakubwa wa elimu wakaona ni vyema kutoa msaada huo wa rangi ili kuboresha mandhari nzuri ya shule hiyo ya sekondari Buluba.

 Amesema shule inapokuwa katika mandhari nzuri inaleta ari ya wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo yao na kupata ufaulu mkubwa, huku akitoa wito kwa wanafunzi wa shule hiyo ya Sekondari Buluba kujituma kwenye masomo ili waje kuwa tegemezi katika familia zao na taifa kwa ujumla.

 “Benki ya TPB huwa tunahusika na masuala ya Ustawi wa Jamii, Afya pamoja na Elimu, hivyo kutokana na sisi kuwa wadau wakubwa wa elimu tumetoa sehemu ya faida ya beki ili kutoa msaada huu wa rangi kwa ajili ya kupendezesha shule ya Sekondari Buluba na kuiweka katika mandhari nzuri,”amesema Kwiyuka. Naye Mwalimu wa Shule hiyo, Emmanuel Kazyoba akisoma risala ya shule hiyo, amesema ina miaka 50 ambapo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu na kupongeza msaada huo wa rangi ambao utasaidia kuipendezesha shule hiyo. 

Amesema licha ya kukabiliwa na uchakavu wamekuwa wakifanya vizuri kwenye masomo ambapo matokeo ya kidato cha sita mwaka huu (2019), daraja wa kwanza wamefaulisha wanafunzi 4, daraja la pili 24, la tatu 46, la nne 10 pamoja na zero moja, Kwa upande Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) Richard Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo, amepongeza msaada huo wa rangi na kuahidi kuendelea kusimamia ufaulu wa shule ambapo wametoka kwenye zero saba mwaka jana hadi moja. Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog 
Mkurugenzi wa Masoko kutoka Benki ya TPB Makao makuu Deogratius Kwiyuka, akizungumza wakati wa kukabidhi ndoo za rangi 50 kwenye shule ya sekondari Buluba Shinyanga Mjini kwa ajili ya kupendezesha shule hiyo na kuwa katika mazingira mazuri na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Meneja wa Benki ya TPB tawi la Shinyanga, Faraji Basu, akizungumza kwenye kukabidhi ndoo za rangi 50 katika shule hiyo ya sekondari Buluba. Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), Richard Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi wa shule ya sekondari Buluba, akishukuru kwa msaada huo wa ndoo za rangi, na kuahidi kuendelea kuboresha miundombinu ya shule hiyo. Ndoo za rangi 50 zikiandaliwa kwa ajili ya kukabidhiwa kwenye shule ya Sekondari Buluba. Mkurugenzi masoko kutoka Benki ya TPB Makao makuu Deogratius Kwiyuka (kulia) akikabidhi ndoo za rangi 50 kwa ajili ya kupendezesha shule ya Sekondari Buluba, katikati ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) Richardi Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo na Meneja wa (SHIRECU) Ramadhani Kato wakipokea rangi hizo. Mkurugenzi wa masoko kutoka benki ya TPB Deogratius Kwiyuka katikati akikabidhi ndoo za rangi 50 katika shule ya Sekondari Buluba kama sehemu ya faida kwenye benk hiyo, wa kwanza kulia ni mwanafunzi Thomas Majuto,na mwisho kushoto ni meneja wa (SHIRECU) Ramadhani Kato, akifuatiwa na mwenyekiti wa SHIRECU Richard Luhende. Mkurugenzi wa masoko kutoka benk ya TPB makao makuu Deogratius Kwiyuka, akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi rangi ndoo 50 katika shule ya Ssekondari Buluba. Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU) Mkoani Shinyanga Ramadhani Kato akishukuru kwa kupokea msaada huo wa ndoo za rangi zilizotolewa na benki ya TPB kwa ajili ya kuweka mandhari nzuri ya shule hiyo. Awali Mwalimu wa shule ya Sekondari Buluba Emmanuel Kazyoba, akisoma taarifa ya shule hiyo na kuelezea kuwepo na changamoto ya uchakavu wa majengo ambapo rangi hizo zitasaidia kuiweka shule katika mandhari nzuri. Mwanafunzi Thomas Majuto akishukuru kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya sekondari Buluba kuhusu msaada huo wa rangi na kuahidi kujituma kusoma kwa bidii ilikuongeza ufaulu katika shule hiyo. Wanafunzi wa shule ya Sekondari Buluba wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa rangi ndoo 50 kutoka benki ya TPB. Wanafunzi wa shule ya Sekondari Buluba wakisikiliza nasaha za kusoma kwa bidii ili waje wasaidie familia pamoja na taifa kwa ujumla. Wafanyakazi wa (SHIRECU) wakiwa kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa rangi ndoo 50 kutoka Benki ya TPB. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

VACANCY ANNOUNCEMENT AT ITU

$
0
0

VACANCY ANNOUNCEMENT FROM THE INTERNATIONAL TELECOMMUNICATION UNION (ITU)


The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received Vacancy Notice No. 21D-2019/BDT-DDR/External/D2 from the International Telecommunication Union (ITU) inviting qualified Tanzanians to apply for the post of  Deputy to theDirector and Chief of the Administration and Operations Coordination Department (DDR).


Application details can be found through the ITU website: http://www.itu.int/employment/Recruitment/index.html.


Closing date for application is Sunday 25th August 2019.



Issued by;

Government Communication Unit,

Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,

Dodoma.

18th July 2019.



Viewing all 110109 articles
Browse latest View live




Latest Images