Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 300 | 301 | (Page 302) | 303 | 304 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Maziko ya kitaifa ya Mfalme wa muziki wa Rumba mtindo wa Soukous, Rochereau,  Jumatatu tarehe Disemba 9, 2013 mjini Kinshasa

  0 0

  Na Hassan Hamad, OMKR
  Jeshi la polisi Zanzibar limehimizwa kutekeleza na kusimamia utekelezaji wa sheria za nchi, ili wananchi waendelee kuishi katika hali ya amani na usalama. 
  Akizungumza na kamishna mpya wa jeshi la polisi Zanzibar ofisini kwake Migombani, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema licha ya polisi kuwa na jukumu kubwa la kulinda usalama wa raia na mali zao, jeshi hilo pia linapaswa kuwa mstari wa mbele katika utekelezaji na usimamizi wa sheria. 
  Amesema licha ya kuwepo sheria nzuri katika nchi lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua, hali inayopelekea kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria na kupelekea kuwepo kwa vitendo vya uhalifu na ukiukwaji wa haki za binadamu. 
  Amelitaka jeshi hilo kuondosha muhali katika kusimamia utekelezaji wa sheria, ili kuona kwamba sheria zilizotungwa zinafuatwa na kuleta ufanisi katika jeshi hilo na taifa kwa ujumla. Makamu wa Kwanza wa Rais amesisitiza kuwa iwapo sheria zilizopo zitatekelezwa ipasavyo, jamii itaziheshimu na kuepukana na vitendo vya uvunjaji wa sheria, na hatimaye kufikia malengo yaliyokusudiwa. “Hata haya matuta tanayowekwa kila pahala barabarani sio dawa ya kuzuia ajali, lakini naamini alama za barabarani iwapo zitafuatwa ikiwa ni pamoja na kudhibiti mwendo wa madereva, basi ajali nyingi zingeepukwa”, alisema Maalim Seif. 
  Aidha Maalim Seif amelishauri jeshi hilo kuimarisha uhusiano wake na raia wema, ili kusaidia kuwafichua wahalifu na watu wanaojihusisha na vitendo viovu vikiwemo uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya. 
  Amesema ofisi yake bado inakabiliwa na changamoto ya dawa za kulevya, na kulitaka jeshi la polisi kufanya juhudi za makusudi kuona kuwa changamoto hiyo inatatuliwa. Amesema serikali itatoa kila ushirikiano kwa kamishna huyo mpya, ili kuhakikisha kuwa anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi. 
  Kwa upande wake Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame, amemuhakikishia Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa atatekeleza majukumu yake ya kusimamia sheria, ili wananchi waendelee kuishi katika hali ya amani na usalama. 
  Aidha amesema jeshi la polisi kupitia kitengo chake cha “Intelijensia” kitaimarisha utafiti ili kupata taarifa za uhakika za kuweza kukabiliana na wahalifu na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao. Ameongeza kuwa atatumia uzoefu alionao katika masuala ya teknolojia ya mawasiliano ili kuona kuwa kitengo hicho kinafanya kazi kwa uhakika na kuleta ufanisi uliokusudiwa. 
  Kamishna Hamdani amesema mafanikio aliyoyapata katika kipindi cha miaka 30 ndani ya jeshi la polisi, yametokana na mashirikiano aliyopata kutoka kwa viongozi na wananchi, na kuomba mashirikiano zaidi ili aweze kuyafikia matumaini na matarajio ya taifa katika ulinzi wa raia na mali zao.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na Kamishna mpya wa jeshi la polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame,   ofisini kwake Migombani.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Kamishna mpya wa jeshi la polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame, ofisini kwake Migombani.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Kamishna mpya wa jeshi la polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame, ofisini kwake Migombani. 
  Picha na Salmin Said, OMKR).

  0 0  ANITA'S DIARY. The one and only fiction novel about a Tanzanian Girl named Anita who studied abroad, and faced challenges living alone away from her rich family in college in the States, and then she fell in love. 
  People who are interested can order their copies online 
  Click the Link:  ANITA'S DIARY

  0 0

  Wanafunzi wa shule za sekondari kote nchini wameaswa kutumia vizuri maendeleo ya teknolojia yanayotokea kwa sasa ili kuongeza kiwango cha ufaulu nchini.

  Madai hayo yalitolewa na Meneja Biashara wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya ziwa Raphael Daudi wakati akikabidhi kompyuta kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kalangalala iliyopo mkoani Geita.

  Meneja huyo alisema kumekuwa na wimbi la wanafunzi ambao hutumia kompyuta kwa matumizi ambayo ni kinyume na maadili na kusababisha jamii kuelekea kwenye mkondo tofauti na uliokusudiwa.

  “Baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakibatilisha matumizi ya kompyuta kwa kujifunza mambo yasiyofaa badala ya kuitumia kupanua uelewa wao wa masomo. Wanasahau kuwa kufanya hivyo maadili humomonyoka kwa kiasi kikubwa katika jamii yetu,” alisema Daudi.

  Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Kalangala, Deusdedith Omchamba alisema mpango wa kuleta mapinduzi katika sekta ya elimu kwa kusababisha matokeo makubwa kwa wanafunzi unaofahamika kama “Big results now” utafanikiwa katika shule hiyo kwa kutumia teknolojia ya kompyuta kujifunzia.

  “Teknolojia ya kompyuta ni muhimu sana kwa maendeleo ya wanafunzi kwa sasa kwani wanafunzi wanaweza kutumia kompyuta kusomea na hata kutafuta habari mbalimbali zinazoshabihiana na masomo yao,” alisisitiza Mwalimu Omchamba.

  Aliongeza kwa kusema kuwa ni jukumu la wanafunzi kutambua umuhimu wa teknolojia hiyo na kuitumia vyema kwa kujiendeleza katika suala la elimu zaidi kuliko mambo mengine ambayo hayana kipaumbele kwa jamii yetu ya Tanzania.

  Baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo walielezea  hisia zao na kusema kuwa wanafurahia sana kuwa na somo la kompyuta shuleni hapo na pia watajitahidi kutilia maanani ushauri uliotolewa na Meneja biashara wa Airtel kuhusu matumizi yanayofaa.

  Pamoja na kutoa vitabu kwa shule za sekondari nchini Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imekuwa ikisaidiana na serikali kuhakikisha kiwango cha elimu kinaimarika na kuleta mapinduzi katikla sekta hiyo kwani elimu ndio ufunguo wa maisha.

  0 0
 • 12/18/13--01:04: Jokate azindua Kidoti Club

 •  Pichani kulia ni aliyewahi kuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006,Jokate Mwegelo akizungumza na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani) kutoka vyombo mbalimbali mapema leo Mikocheni jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa klabu yake iliyojulikana kwa jina la KIDOTI CLUB,Shoto ni mmoja waratibu,Mtangazaji wa East Africa Radio aitwaye Bhoke.
   Mmoja wa Mashuhuda akitoa ushuhuda wake mara baada ya kujiunga kwenye klabu ya KIDOTI CLUB,kwa njia ya simu kwa kutuma neno KIDOTI  kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.
   Baadhi ya wanahabari waliofika kwenye uzinduzi huo uliofanyika Mikocheni,jijini Dar.

  =========  ========  ========

  Baada ya kutamba na mitindo ya nywele na nguo aina ya Kidoti brand, msichana mwenye vipaji vingi hapa nchini, Jokate Mwegelo ameanzisha klabu yake ijulikanayo kwa jina la Kidoti Club.

  Akizungumza katika uzinduzi wa klabu hiyo  jana, Jokate alisema kuwa Kidoti Club ni tofauti na vilabu vingine kwani katika ujio wake huo mpya, atakuwa anajihusisha na mambo mbali mbali katika jamii hususani masuala ya urembo na mitindo. Jokate pia alizindua aina mpya ya nywele zake za kisasa katika mtindo wa kidoti Brand.

  Jokate alisema kuwa kupitia klabu yake atakuwa anatoa ushauri mbali mbali katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa za muziki, filamu, wasanii mbalimbali na nyinginezo kwa ajili ya rika tofauti. Alisema kuwa lengo lake kubwa ni kupanua mtandao wake kwa jamii na anaamini watu wengi watajiunga naye.

  Kwa mujibu wa Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, ili uwe mwanachama wa klabu hiyo, unatakiwa kutuma neno  kidoti kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.

   “Huu ni mfumo wa kisasa katika kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii,Beyonce amefanya hivyo na kwa sasa hakuna mtu anayeingia katika shoo zake bila kuwa mwanachama wa klabu yake, mimi pia naelekea huko kwani nitaweka taarifa zangu mbali mbali na ili kupata lazima uwe mwanachama,” alisema Jokate ambaye pia ni mtangazaji na mbunifu wa mavazi. Alisema kuwa pia ataendesha mashindano mbali mbali kwa wanachama wake na kutoa zawadi kwa washindi.

   “Kama unavyojua, lengo langu kubwa ni kutumia ujuzi na kipaji chake kwa watanzania wote, nataka wafaidike na vipaji vyangu name kusimama mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu yoyote, natoa wito kwa vijana wenzangu kuwa wabunifu katika kukabiliana na masuala mbali mbali ya maisha,” alisema.

  0 0

  Kama wewe ni mtumiaji wa website, basi moja ya vitu vinavyokera ni pale unapofungua website halafu haifunguki. Kutofunguka kwa website kunaweza kusababishwa na matatizo mengi. Kuna matatizo ambayo yanaweza kuwa ni upande wako wewe 

  mtumiaji kama (intaneti yako kuwa chini sana, au programu ya ulinzi (anti virus) inakuzuia kufungua hiyo website nk, pia inaweza kuwa ni tatizo la website husika. Ili kuweza kusaidia kutambua chanzo cha tatizo na kurahisisha matumizi, kila kosa linalotokea kwenye website limepewa namba husika ambayo italitambulisha, ama kwa watumiaji ama kwa wamiliko na hii tunaiita namba ya utambulishi wa error (error status code) .
  Kuna rundo la makosa unayoweza kukunana nayo, ila leo hii tutaangalia yale yanayotokea mara kwa mara;


  0 0

   Mwakilishi kutoks IOGT-NTO, Gunnar Lundstom akiwasilisha mada katika kongamano juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe kwa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Childen Care (IDYDC) na kufanyika katika ukumbi wa Valentine mjini Iringa.
   Mganga wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Iringa na Mratibu wa madhara ya pombe afya mkoa,Dk. Ally Ngala akizungumza katika kongamano juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe kwa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Childen Care (IDYDC) na kufanyika katika ukumbi wa Valentine mjini Iringa.
    Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kongamano juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe kwa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Childen Care (IDYDC) na kufanyika katika ukumbi wa Valentine mjini Iringa.
   
  ========  ======  ======== 

  WATU MILIONI 2 HUFARIKI DUNIA KWA POMBE

  Na Denis Mlowe na Pauline Kuye, Iringa

  UTAFITI uliofanywa na serikali kupitia Wizara ya Afya imebainika kuwa watu milioni mbili hufariki kila mwaka duniani kutokana na matumizi ya pombe.

  Hayo yameelezwa na Mganga wa Hospitali ya Rufaa ya
  Mkoa wa Iringa Dk. Ally Ngala wakati akizungumza  katika kongamano juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe kwa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Childen Care (IDYDC) na kufanyika katika ukumbi wa Valentine mjini hapa.

  Dk.Ngala alisema asilimia 4 ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa husababishwa na matumizi mabaya ya pombe kupita kiasi na kusababisha madhara mengi zaidi kwa watumiaji wa pombe ikiwemo mama wajawazito kuzaa mtoto kabla ya miezi tisa (njiti).

  Alisema utafiti huo ulifanywa Februari na Octoba 2012 ulibainisha asilimia 26.8 mpaka 31.9 sawa na watu milioni 15 nchini Tanzania wanatumia pombe, na kati ya hao asilimia 27.4 ya wanaume wanywaji wa pombe ni  walevi kupindukia na  huku  wanawake ikiwa ni asilimia 13.4.

  Aidha Ngala alisema  hunywaji wa pombe una hasara nyingi na  kubwa sana kuliko faida zake na alibainisha kuwa hasara mbaya za pombe kwa mtumiaji  ni upande wa kiafya.

  “Pombe ina hasara kubwa sana kwa binadamu kiuchumi kwa kusababisha umaskini kifamilia lakini kwa upande wa afya ndio zaidi hii inatokana na kuwa na mchango mkubwa katika kuleta magonjwa, ingawa sio kila ugonjwa husababishwa na pombe pekee” alisema Dk. Ngala

  Ngala alisema madhara mengine ya unywaji wa pombe kupita kiasi ni kusababisha  ugonjwa wa Ini kwa  kufa kwa seli za ini hivyo baadaye ini linapoteza uwezo kabisa kwa kushindwa kufanya kazi hivyo kusababisha vifo vingi kwa ugonjwa huo.

  Alibainisha pombe husababisha kansa za tumbo na kansa ya kongosho na mtumiaji wa pombe kwa kiasi kikubwa watoto huzaliwa katika hali ya utegemezi wa pombe(Fotal alcoholic syndrome) ambayo huweza kumpotezea maisha mtoto ndani ya mwezi wa kwanza au utaahira wa kudumu(matatizo ya akili).

  Alisema  pombe huathiri kiasi kikubwa watumiaji  mfumo mzima wa uzazi na hata kupelekea mtumiaji kupoteza uwezo wa kuzaa kabisa, na huanzia  kupoteza siku za hedhi kwa mwanamke.

  Aliongeza madhara mengine ya unywaji wa pombe kupita kiasi ni chanzo kikubwa cha ajali za barabarani na kusababisha hasara kubwa kwa taifa kwa ujumla. 

  0 0
  Habari iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde toka jijini Arusha,inaeleza kuwa Ndege ya abiria aina ya Boeing 767 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) mchana huu imeshindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani hapo na kulazimika kutua kwa dharula kwenye Uwanja wa Mdogo wa Arusha.
  Wataalam wa Ndege wapo eneo la tukio hivi sasa kutafakari namna watakavyoweza kuwashusha abiria hao na kutafuta namna ya kuweka sawa mambo ili Ndege hiyo iweze kuruka.
  Ndege hiyo ilikuwa na abiria zaidi ya 200 na wafanyakazi 9. kabla ya kupaa tena ilibidi abiria wote wateremke, na kupunguzwa mafuta ili kupunguza uzito wa ndege hiyo. Abiria waliamuriwa kwenda kupandia ndege hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA.
  Globu ya Jamii inaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo,na tutaendelea kufahamishana kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Ally Nassoro Rufunga akisisitiza juu ya utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa kukabili Maafa Mkoani Shinyanga wakati alikiuzindua mpango huo leo Mjini Shinyanga kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuu Lut Jen (Mst) Sylivester Rioba.
  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Ally Nassoro Rufunga akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Annarose Nyambi Mpango wa Kujiandaa kukabili Maafa Wilayani Shinyanga baada ya uzinduzi wa mpango huo leo Mjini Shinyanga kushoto .
  Baadhi ya wajumbe kutoka Wilaya za mkoa wa Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Ally Nassoro Rufunga(wa pili kushoto), baada ya uzinduzi wa Mpango wa Kujiandaa kukabili Maafa Mkoani Shinyanga leo, (wa tatu kushoto) ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuu, Lut Jen (Mst) Sylivester Rioba.

  0 0

  Afisa Mazingira Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Japhet Kanizius, Akimkaribisha Mgeni Rasmi Bi. Magdalena Mtenga, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kufungua rasmi warsha ya mafunzo kwa mafundi wa kuhudumia majokofu na viyoyozi kutoka Mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa. Mafunzo haya yanafanyika katika Hotel ya Mbeya Paradise Inn, Jijini Mbeya.
  Sehemu ya washiriki kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mgeni Rasmi, Bi. Magdalena Mtenga, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).
  Washiriki wa Warsha ya mafunzo kwa mafundi wa kuhudumia majokofu na viyoyozi kutoka Mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Bi. Magdalena Mtenga Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (Waliokaa - kwanza kushoto). Mafunzo haya yanafanyika katika Hotel ya Mbeya Paradise Inn, Jijini Mbeya.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiongea na wanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam alipokaribishwa kubadilishana nao uzoefu wake katika masuala ya habarai na maadili ya uandishi wa habari kazini. Vodacom imekuwa ikiruhusu wafanyakazi wake waliobobea kwenye fani mbalimbali kutoa ujuzi wao kwa wanafunzi vyuoni na amshuleni.
  Wanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umm ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim(hayupo pichani) aliyekaribishwa kubadilishana nao uzoefu wake katika masuala ya habarai na maadili ya uandishi wa habari kazini. Vodacom imekuwa ikiruhusu wafanyakazi wake waliobobea kwenye fani mbalimbali kutoa ujuzi wao kwa wanafunzi vyuoni na mashuleni.
  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiongea na wanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam alipokaribishwa kubadilishana nao uzoefu wake katika masuala ya habarai na maadili ya uandishi wa habari kazini. Vodacom imekuwa ikiruhusu wafanyakazi wake waliobobea kwenye fani mbalimbali kutoa ujuzi wao kwa wanafunzi vyuoni na amshuleni.
  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim (kulia) akifuatilia swali kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (wa kwanza kushoto alyeketi). Mwalim alikaribishwa Chuoni hapo kuzungumza na wanafunzi hao kuhusu uzoefu wake katika masuala ya habari na maadili ya uandishi wahabari kazini. Vodacom imekuwa ikiruhusu wafanyakazi wake waliobobea kwenye fani mbalimbali kutoa ujuzi wao kwa wanafuzni wa vyuo na shule za sekondari.
  Mhadhiri Mwandamizi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dk. Ayub Rioba (kulia) akimkaribisha Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim (pembeni yake) kuzungumza na wanafunzi wa mwaka w apili chuoni hapo. Mwalim alikaribishwa kluzngumzia uzoefu wa masula ya habari na maadili ya uandishi wa habari kazini. Vodacom huruhusu wafanyakazi waliobobe akwenye fania mbalimbali kutoa ujuzi wao kwa wanafuzni wa vyuo na sekondari.

  0 0

  Na Badru Kimwaga

  HOMA ya pambano la watani wa jadi katika muziki wa dansi nchini kati ya Mlimani Park 'Wana Sikinde' na Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' litakalofanyika siku ya Krismasi imeanza kupanda kwa bendi hizo kujificha kambini na huku wakipigana vijembe.


  Bendi hizo kongwe nchini zinatarajiwa kuonyeshana kazi katika onyesho litakalofanyika kwenye viwanja wa TCC Club Chang'ombe, Temeke Dar es Salaam katika kunogesha sikukuu hiyo ya Krismasi.


  Katika kuonyesha wamelipania pambano hilo bendi ya Sikinde tayari imeiendea Msondo wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kuweka kambi yao na wamewatahadharisha 'mahasimu' wao hao wasije wakatoa visingizio baada ya kugaragazwa kwenye onyesho hilo.

  "Sisi tumeamua kuweka kambi yetu mjini Bagamoyo ambako tutatua viwanja vya TCC kutokea huko ili kuisambaratisha Msondo, na tunataka wajipange sawasawa ili wasije wakatoa visingizio tena kwa maana kama vyombo vipya bendi zote imepewa na Konyagi," Katibu wa Sikinde, Hamis Milambo alisema.

  Milambo alisema mashabiki wa dansi wajitokeze kwa wingi kushuhudia namna gani wanavyowachachafya wapinzani wao hao, ikizingatiwa hawajakutana kwa muda tangu mwaka jana.

  Upande wa Msondo kupitia Meneja wao, Said Kibiriti, alisema hawana haja ya kutaja mahali kambi yao ilipo isipokuwa wamejiandaa kuwatoa nishai wapinzani wao siku ya onyesho hilo litakaloanza saa nane mchana.


  "Sisi hatuna mchecheto wowote na mpambano huo, tunaendelea kujifua kimya kimya mahali ambapo siwezi kupataja kwa sasa," alisema Kibiriti.


  Naye muimbaji anayekuja juu wa bendi hiyo ya Msondo alitokea Sikinde, Athuman Kambi, alisema amejipanga kuonyesha umahiri wake katika mpambano huo baada ya kufanya hivyo wakati akiwa Sikinde dhidi ya Msondo kwenye ukumbi wa Diamond na kuwawehusha mashabiki wa muziki wa dansi nchini.

  "Najua watu watataka kuona nafanya kitu gani dhidi ya bendi yangu ya zamani iliyonitangaza vyema, wasiwe na hofu waje Desemba 25 waone nini nitakachofanya TCC Club Chang'ombe," alisema Kambi.

  Mpambano huo wa Sikinde na Msondo umeandaliwa na kampuni ya Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, gazeti la NIPASHE, Integrated Communications, CXC Africa na Salute5.

  0 0

   Kaimu mkurugenzi  mkuu  wa hifadhi  za Taifa (TANAPA ) Dr Ezekiel Dembe ( kulia) akimakabidhi  Bi Jane Mwakinyuke kutoka Hifadhi ya Taifa Mikumi , cheti  cha  kuhitimu mafunzo  ya mwezi mmoja ya kuongoza  watalii katika hifadhi  za Taif
  Kaim mkurugenzi mkuu wa TANAPA DR Ezekiel Dembe wa pili kulia waliokaa akiwa na  kaim mhifadhi wa Ruaha Bw John Nyamhanga kulia ,Godwell ole Meing'ataki Mratibu wa mradi wa kuboresha mtandao wa maeneneo yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania. ' SPANEST kushoto wa  pili na kaimu RAS Iringa pamoja na  walimu wa mafunzo  hayo na askari  waliohitimu mafunzo  waliosimama.

  BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI ZAIDI

  0 0

  H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to His Highness Sheikh Tamim bin Hamad bin Khalifa Al Thani, Emir of the State of Qatar, on the occasion of the Anniversary of the Qatar National Day of the founder of the state of Qatar Sheikh Jassim Bin Mohammed Al Thani.

  The message reads as follows:

  “His Highness, Sheikh Tamim bin Hamad bin Khalifa Al Thani,

  Emir of the state of Qatar,

  DOHA,

  Your Highness,  On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf, I would like to sincerely convey my warm congratulations to you, Your Highness and through you, to the Government and the people of Qatar on this significant celebration of the Anniversary of the State of Qatar National Day.  The state of Qatar and the United Republic of Tanzania have enjoyed cordial bilateral relations over the years. As you commemorate this joyous occasion of your country’s independence, I wish to take this opportunity to reiterate my Government’s desire and commitment to further enhance the traditional bond of friendship and cooperation existing between our two countries for our mutual benefits.  Please accept, Your Highness, my most sincere congratulations and best wishes for the continued good health and happiness, and for the friendly people of the state of Qatar, further progress and prosperity.  Dr. Jakaya Mrisho Kikwete

  PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA”

  Issued by: 

  The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation,

  Dar es Salaam.

  18TH DECEMBER, 2013


  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda akiongea na Wanahabari katika Bonanza la Viongozi Wanawake wa Afrika lililofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Viongozi Wanawake wa Michezo wa Afrika wakiangalia Michezo katika Bonanza lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akipokea zawadi kutoka kwa Bwana Joachim Coens Rais wa Bandari ya Zeebrugge. Uongozi wa Bandari ya Zeebrugge umekubali kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji kuweka mikakati mbalimbali ya kuongeza biashara kati ya Tanzania, Ubelgiji na Jumuiya ya Ulaya. Balozi Kamala yuko kwenye ziara ya kutembelea Bandari za Ubelgiji.

  0 0
 • 12/18/13--07:38: TAARIFA KUTOKA TFF LEO

 • 0 0


  Kivuko kikubbwa cha MV Magogoni leo kimekwama katikati ya bahari katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na hitilafu za kiufundi.Pantoni hilo linafanya safari kati ya Kigamboni na Magogoni, Dar es Salaam. Kiini cha kizaazaa hicho bado hakijafahamika, ila mashuhuda wanasema  Kivuko kilipoteza mwelekeo majini  kikiwa na abiria na magari baada ya injini zake kushindwa kufanya kazi.   0 0

  In an initiative to promote Tanzanian football and recruit players for international teams,  Safarihub in collaboration with Eton College and the Tanzanian high commission intend to develop the future stars football academy which starts with a pilot project in Arusha in 2014. Above is a football jersey handing-over ceremony held today at the Tanzanian High Commission  in London with the Tanzanian High Commissioner  Mr. Peter Kallaghe (left), Eton College Head of sports Glen Pierce and Safarihub director Navraj Hans.

  0 0

  Kaimu Konseli Mkuu katika ubalozi mdogo wa Tanzania Dubai Ndugu Omar Mjenga amewakaribisha kupata mawazo yao jinsi ya kuongeza idadi ya watanzania katika shirika hilo la Ndege la Emirates. Wadau hao wameweka mikakati ambayo itawawezesha kufikia Machi 2014 kupata Watanzania zaidi kujiunga na Shirika hilo.
  Kaimu Konseli Mkuu Ndugu Omar Mjenga akipokea Tuzo kutoka kwa Mtawala wa Ajman kwa niaba ya Tanzania wakatinwa Chakula cha Jioni na Maonyesho ya Uwekezeji na Biashara katika Emirate ya Ajman.


older | 1 | .... | 300 | 301 | (Page 302) | 303 | 304 | .... | 3272 | newer