Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109977 articles
Browse latest View live

NEWS ALERT: KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa 
Bw. Emanuel Mteming'ombe enzi za uhai wake

 Mzee Teming'ombe akilia  kwa  uchungu  kufuatia  kifo  cha kijana wake aliyekuwa katibu  wa CCM mkoa wa  Iringa Emanuel Mteming'ombe aliyefariki usiku wa   kuamkia  leo  katika Hospital ya Rufaa ya  mkoa wa Iringa 

Waombolezaji wakiwa  katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa katika maandalizi  ya mwili  wa aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa  


 Waombolezaji  wakishusha jeneza  la kuuweka mwili wa katibu wa CCM mkoa wa Iringa

Na Francis Godwin, Iringa
KATIBU  wa  chama cha mapinduzi  (CCM) mkoa  wa  Iringa Bw Emanuel Mteming'ombe amefariki  dunia katika hospital  ya  mkoa  wa  Iringa.

Katibu   huyo  alikuwa amelazwa  katika Hospital  ya  mkoa  wa  Iringa   moja akisumbuliwa  kwa ugonjwa athma kabla ya kufariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Mwenyekiti  wa  CCM  mkoa wa  Iringa Bi, Jesca Msambatavangu  amethibitisha   juu ya taarifa  hiyo  na  kuwa  taratibu  za mazishi  zinafanywa.
Taarifa zinasema mwili wa Maarehemu  unatarajiwa  kuombewa  katika kanisa la RC Kichangani ama nyumbani kwake Gangilonga mjini Iringa kabla ya  kuondoka mida ya saa 10  jioni kwenda Rujewa, Mbarali,  mkoa  wa Mbeya,  kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika  kesho  saa 5 asubuhi.

Katibu  huyo alifariki dunia majira ya saa 8 hivi  usiku  wa kuamkia leo baada ya kulazwa katika Hospital ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa kwa tatizo  la figo na Athma.

Mungu ailaze  roho  yake mahali pema peponi.
Amina


Vodacom yafungua duka Kibaha Mkoani Pwani

$
0
0
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Vodacom Hassan Saleh akimlaki Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Halima Kihemba wakati akiwasili kwenye hafla ya uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja la kampuni hiyo lililopo Maili Moja Mjini Kibaha. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Duka hilo linatoa huduma zote za mtandao wa Vodacom ikiwemo usajili wa laini, sim swap, M-pesa pamoja na mauzo ya simu na modem.
Kutoka Kushoto Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Halima Kihemba, Mkuu wa Moa wa Pwani Mwantumu Mahiza , Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Hassan Saleh, Diwani wa Kata ya Maili Moja,Andrew Lugano na Mkuu wa Usimamizi wa Maduka ya Vodacom Upendo Richard kwa pamoja wakigongesha glass mara baada ya kuzinduliwa kwa duka la Vodacom lililopo Maili Moja Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza,(wapili kushoto)akiongea mara baada ya kuzindua duka jipya la Vodacom lililopo Maili Moja Kibaha.Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Halima Kihemba na Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji wa kampuni hiyo,Hassan Saleh(watatu kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Halima Kihemba kushoto na Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Hassan Saleh wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom na watumishi wa duka jipya la Vodacom Kibaha mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa
Maandalizi ya kuweka sawa mazingira tayari kwa uzinduzi rasmi wa duka jipya la Vodacom lililopo Maili Moja Kibaha. Duka hizlo limezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza.

MAMA SALMA KIKWETE APOKEA TUZO KUTOKA KITUO CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA UONGOZI (CELD)

$
0
0
Na Anna Nkinda – Maelezo, Dubai 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo ya kimataifa ya Uongozi wenye Hamasa kwa mwaka 2013 (Global Inspirational Leadership Award 2013) kutokana na kazi anazozifanya za kuwasaidia wanawake na watoto wa kike nchini ambazo zimewahamasisha watu mbalimbali Duniani kuweza kuzisaidia jamii zenye mahitaji. 
Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ambazo zilitolewa jana na Kituo cha Maendeleo ya kiuchumi na Uongozi (CELD) cha nchini Nigeria zilifanyika katika Hoteli ya Atlantis, The Palm iliyopo Dubai , Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). 
 Akiongea mara baada ya kukabidhiwa tuzo hizo Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwashukuru waandaaji wa tuzo hizo kwa kuona na kutambua umuhimu wa kazi anazozifanya na kukipongeza kituo hicho kwa kazi wanayoifanya ya kuinua uchumi wa wanawake. 
 Mama Kikwete alisema vifo vingi vya wanawake vinatokana na uzazi, majeraha yanayosababishwa na ukeketwaji, ukatili wa kijinsia vinaleta wasiwasi na changamoto za kibinadamu hivyo basi ni lazima wanawake wafanikiwe kukabiliana na hali hii kwa kuwa wengi wanakufa kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika pia wanakosa nafasi ya kujikwamua kiuchumi. “Hatuna muda wa kupoteza lazima tuchukuwe hatua sasa bila ya kurudi nyuma kwa sababu zisizoeleweka nia ni kuweka nafasi yetu ya uongozi wa kimataifa ambao utakuwa ni mfano wa kujivunia kwa wanawake huku tukiona kuzaliwa kwa watoto kuwe ni hali ya kufurahia na siyo kipindi cha huzuni na kuomboleza”, alisema Mama Kikwete. 
 Alimalizia kwa kusema tatizo la vifo vya uzazi litaisha pale ambapo juhudi za makusudi zitafanyika, kuinua hali ya maisha ya wanawake wa Afrika na nchi zinazoendelea jambo linalotakiwa ni kutambua kuwa Dunia ina rasilimali za kutosha, utaalamu na ujuzi wa kuweza kufanya mambo hayo.
 Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha CELD Mama Furo Giami aliwapongeza wanawake hao viongozi kwa tuzo walizopewa na kusema hivi sasa wanawake wameweza kufanya njia kwa kuthubutu kupita njia ambayo wanaume walipita hapo zamani na kufanya kazi nzuri zaidi ambayo imewaletea maendeleo. 
 Mama Giami alisema wanawake wengi wenye sauti ndogo wameweza kuzitumia sauti zao kusikika katika jamii na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maisha yao. Wameweza kujitegemea na hivyo kupambana na hali ngumu ya uchumi. 
Kituo hicho ambacho kilitoa tuzo kwa wanawake viongozi 15 kutoka nchi za Afrika, Asia na Mashariki ya kati kinafanya kazi za kuwainua wanawake na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuhakikisha kuwa wanatimiza malengo yao. 
 Wengine waliopewa tuzo hiyo ni pamoja na Mke wa Rais wa Namibia Mama Penehufipo Pohamba, Mke wa Rais wa Burundi Mama Dk. Mchungaji Denise Nkurunziza na Mke wa waziri Mkuu wa Malaysia Mama Datin Paduka Seri Rosmah Monsor. 
 Utoaji wa tuzo hizo ulifanyika mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku tatu wa wanawake kutoka nchi za Afrika, Asia na Mashariki ya Kati ambao ulihudhuriwa na wajumbe kutoka mataifa 28 na kujadili kuhusu Uongozi ni Elimu: Ufunguo wa mustakabali wa wanawake katika nchi zenye uchumi unaoibuka.

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake  na Maendeleo, WAMA, Mheshimiwa Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Uongozi Uliotukuka kimataifa (Global Inspirational Leadership Award 2013) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Maendeleo ya  Kiuchumi na Uongozi Mheshimiwa Bibi Furo Giami, mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia.  Mkutano huo ulioandaliwa na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi  (CELD), wakishirikiana na CEO Clubs Network na African Leadership Magazine uliofanyika katika hoteli ya Atlantis The Palm, huko Dubai , Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE.) Tuzo hiyo imetolewa tarehe 18.12.2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba ya kushukuru mara tu baada ya kupokea Tuzo hiyo huko Dubai
 Mkurugenzi  Mtendaji  wa Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi (CELD), Bibi Furo Giami akikabidhi vyeti kwa Wake wa Marais na wanawake wengine waliotunukiwa tuzo hizo wakati wa kilele cha mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia uliofanyika huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA KILIMO NA MAENDELEO VIJIJINI YA NCHI ZA AFRIKA, KARIBIANI NA PACIFIC AMTEMBELEA BALOZI KAMALA OFISINI KWAKE BRUSSELS

$
0
0
Bwana. Michael Hailu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kilimo na Maendeleo Vijijini ya nchi za Afrika, Karibiani, Pacific na Jumuiya ya Ulaya (katikati) akimweleza Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala ( kulia) mipango mbalimbali ya kusaidia maendeleo ya kilimo katika nchi za Afrika, Karibiani na Pacific inayotekelezwa na taasisi yake. Bwana. Hailu alimtembelea Balozi Kamala leo ofisini kwake Brussels, Ubelgiji na kumuomba asaidie taasisi hiyo atakapokuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa nchi za Afrika, Karibiani na Pacific kuanzia tarehe 1, Februari 2014.

ANKAL AJICHANGANYA NA WAFANYAKAZI WA VODACOM IDARA YA WATEJA WA MIKATABA

$
0
0
 Ankal (kati) akiwa amekula pozi na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Vodacom idara ya Wateja wa Mikataba  (Business Enterprise Unit) wakati alipofika kuwasabahi.toka shoto ni Edna Mtema, Somoe Wamala, Asteria Mallya,Bakari Kunenge, Happy Shuma pamoja na Nureen Nyagiro.
Ankal (pili kulia) na Wadau wa Vodacom idara ya Wateja wa Mikataba  (Business Enterprise Unit).toka shoto ni Dia Missana, Stima, Ankal na Simon Martin

NEWS ALERT: TUME YA KATIBA KUKABIDHI RASIMU YA KATIBA KWA MHE. RAIS DESEMBA 30 2013

$
0
0
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine wote kuwa Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida. 
Taarifa zaidi kuhusu hafla hii zitatolewa baadaye. 

Imetolewa na:
Assaa Rashid, 
Katibu, 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, 
Dar es Salaam, 
Alhamisi, Desemba 19, 2013

OFISI YA WAZIRI MKUU YAENDELEA KUTOA MAFUNZO YA MPANGO WA KUJIANDAA KUKABILI MAAFA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa, Bi. Naima Mrisho akifafanua utekelezaji wa Mpango Wa Kujiandaa Kukabili Maafa katika mkoa wa Shinyanga, leo.
Baadhi ya Wawezeshaji wa mafunzo ya Mpango wa kujiandaa kukabili Maafa Mkoani Shinyanga kutoka ofisi ya Waziri Mkuu- Idara ya Uratibu wa Maafa, wakifuatilia mafunzo hayo yanayoendelea mkoani Shinyanga leo, (wa kwanza) ni Mhandisi, Fanuel Karugendo na (wa pili) Mchumi, Magreth Sembuyagi. 
Baadhi ya Washiriki kutoka vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Shinyanga wakifuatilia mafunzo ya Mpango wa kujiandaa kukabili Maafa Mkoani Shinyanga leo, (wa kwanza) ni Kaimu Kamanda kikosi 516 KJ, Gabriel Nzunda na (wa pili) ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya Shinyanga, Richard Ngede.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tanzania-Qatar for stronger economic ties

$
0
0
On the 18th of December 2013, the State of Qatar celebrated its National Day, an historical event which was commemorated in Dar es Salaam in cooperation with the Qatar Embassy, the Ministry of Foreign Affairs, Members of the Diplomatic Corps and other distinguished guests.  The event took place at the Hyatt Regency (Kilimanjaro) Hotel, with Guest of Honor H.E. Ambassador Rajabu Gamaha, Acting Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.

In commemorating the Qatar National Day, H.E. Ali Hassan Mwinyi (3rd left), former President of the United Republic of Tanzania along with Ambassador Jassim Mohamed Mubarak Abdullah Darwish (3d right) of the State of Qatar to the United Republic of Tanzania, and Dr. Salim Ahmed Salim (2nd right), former Prime Minister of Tanzania and former General Secretary of Organization of African Union (OAU) assisted in cutting a special cake baring flags of Tanzania and Qatar, symbolizing the strong bilateral ties between the two countries.  

Others in the photo are H.E. Ambassador Rajabu Gamaha (center), Acting Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation and H.E. Ambassador Alfani Juma Mpango (left) Dean of the Diplomatic Corps, who is also an Ambassador of Congo-DRC and Mr. Mussaab Al-Fehaid (2nd left), Foreign Service Officer at the Qatar Embassy. 
Ambassador Hassan Simba Yahya, Director of the Department of the Middle East in the Ministry of Foreign Affairs in a discussing with Qatar Ambassador Jassim Mohamed Mubarak Abdullah Darwish.


Ethiopian Airlines statement regarding the incident of Flight ET-815 at Arusha vs KIA

$
0
0
Ethiopian Airlines Flight ET-815 of 18 December 2013 
Update 1 - 19 December, 2013

Ethiopian Airlines would like to refute all unfounded speculations regarding the incident of Ethiopian flight ET-815 from Addis Ababa to Kilimanjaro of 18 December 2013. Such unfounded speculations are against international procedure and practice of incident investigation and communications.

Although Ethiopian Airlines should strictly follow the international procedures and will not make pre-judgmental statements before the incident is fully investigated by relevant and competent authorities, there was miscommunication between the control tower and the flying crew, which resulted in landing at Arusha airport. The aircraft had adequate fuel to fly to an approved alternate airport.

All passengers and crew were unharmed and have been taken to their intended destinations. The aircraft did not sustain any damage.

Ethiopian Airlines would like to apologize to its esteemed passengers for the inconveniences caused.

Source: The Latest Press Releases from Ethiopian @ EthiopianAirlines.com.


YANGA YALAMBA MILIONI 90 ZA HAKI YA MCHEZO WAO NA AL AHLY KUONESHWA KATIKA TV

$
0
0

 Klabu ya Yanga imeanza kunufaika na haki za matangazo ya Televisheni baada ya kutangaza kusaini mkataba na kampuni ya SGM ya nchini Kenya kwa ajili ya kuonyesha mechi yao ya raundi ya  kwanza dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Katibu Mkuu wa Yanga Beno Njovu (pichani) aliwambia waandishi wa habari jana kuwa mkataba waliongia ni wa mechi moja tu dhidi ya Al Ahly itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa na tayari Yanga wameweka kibindoni dola 55,000 ambazo ni sawa na Sh90 milioni kwa mchezo huo.
" SGM imejipa  inaamini Yanga itavuka raundi ya awali dhidi ya Komorozine ya Comoro na kwenda kukutana na mabingwa Afrika, Ahly katika raundi ya kwanza."alisema Njovu
 Alisema haki za matangazo ya Televisheni za mechi ya ugenini wamepewa kampuni ya MGB ya Cairo, ambayo itarusha matangazo hayo kwa nchi za Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati pekee.


 Katibu huyo mpya wa Yanga ambaye amechukua mikoba ya Lawrance Mwalusako alisema televisheni za  Tanzania ambazo zitataka kuonyesha mechi hiyo, zitatakiwa kuwasiliana na kampuni ya SGM kupata haki hiyo.  
Kuhusu mchezo wa marudiano utakaofanyika  Misri, Njovu alisema  kuwa wao watakuwa ugenini, watawasiliana na wenyeji wao ili uwezwe kuonyeshwa kwa Tanzania pekee.
 Kwa upande wake, Mwakilishi wa SGM Francis Gaitho alisema  wana matumaini makubwa Yanga itaitoa timu ya Comoro na ndiyo maana wamechukua hatua hiyo.
 Yanga  itaanza na Komorozine ya Comoro katika raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na wakiitoa watacheza na Ahly katika raundi ya Kwanza.
 Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Febaruai 7, 8 na 9, wakati marudiano yatakuwa kati ya Februari 14, 15 na 16 February 2014

STATEMENT OF THE GOVERNMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA ON THE SITUATION IN SOUTH SUDAN ISSUED BY HON. BERNARD K. MEMBE (MP), MINISTER FOR FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION

$
0
0
Hon Membe
DAR ES SALAAM, TANZANIA, 
19TH DECEMBER, 2013

The Government of the United Republic of Tanzania is gravely concern with the deteriorating security situation in South Sudan, following the outbreak of fighting in capital, Juba, and other areas since 15 December, 2013, which resulted in a number of causalities of soldiers as well as civilian population. The fighting is a serious political setback to South Sudan, the world’s new nation which was formed in 2011 after two decades of war. Also, the fighting is a serious setback to the progress made, so far, in the last two years of the existence of South Sudan, as a sovereign state and will lead to the suffering of the civilian populations, who had already started to enjoy peace dividend.

In this respect, the Government of the United Republic of Tanzania joins the United Nations and the African Union in urging the parties concerned with the fighting in South Sudan to exercise restraint and refrain from any action that may further escalate violence, causalities and humanitarian crisis in that country.

Furthermore, the Government of Tanzania also calls upon the parties concerned to engage in dialogue in order to find a solution of their differences through peaceful means, with due respect of rule of law, human rights and constitutional legality.

Moreover, while reports indicate that so far no Tanzanian has been affected by the fighting, the Government of the United Republic of Tanzania calls upon all the parties concerned, most particularly the Government of the Republic of South Sudan to ensure the safety of all the people, not only the South Sudanese but also all the foreigners in South Sudan, including Tanzanian Nationals.

Finally, the Government of the United Republic of Tanzania wishes to express its readiness to support efforts by the United Nations, the African Union and the International Community, as a whole, aimed at finding a lasting peace to in South Sudan. 
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND


INTERNATIONAL COOPERATION

mama mwanamema shein na mama Asha Seif Iddi wakagua shughuli za wajasiriamali kinamama Pemba

$
0
0
  MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein (wa tatu kulia), na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Rais wa Zanzibar  Mama Asha Seif  Iddi (wa pili kulia) wakiangalia Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali wa Mkoa wa Kusini Pemba alipotembelea vikundi hivyo na kutowa mchango wao kwa Vikundi hivyo katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Fiedel Castro.
  MKE wa Rais wa Zanzibarb na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiangalia Bidhaa za Kikundi cha Wajasiriamali cha Nia Safi Iwpo Saccos, akiwa na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais Mama Asha  Seif na Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Mama Wu Yan.
 MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiangalia bidhaa za Kikundi cha Uwama Ngombeni cha Mkoani Pemba akiangalia bidhaa za sabuni ya chokaa
 MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi kiongozi wa kikundi cha Wanawake cha Hatugombani, Biharusi Khamis.
 MKE wa Rais wa Zanzibarb na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein akizungumza bidhaa za vikundi vya Wajasiriamali 
 MKE wa Rais wa Zanzibarb na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiangalia Bidhaa za Kikundi cha Wajasiriamali. Picha na Ramadhan Othman, Ikulu Zanzibar


Majimarefu awataka wana-CCM waache kuwashabikia wanaotaka uongozi

$
0
0
Na Mashaka Mhando,Korogwe 
MBUNGE wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani almaarufu kama 'Profesa Majimarefu', amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, kuacha kuwashabikia wanachama wanaotaka uongozi mwaka 2014/2015 badala yake washirikiane na viongozi waliopo ili watekeleze ahadi na ilani ya chama hicho. 
 Akizungumza kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Kizara wilayani hapa juzi, mbunge huyo alisema ipo tabia ambayo imeota mizizi miongoni mwa viongozi wa chama hicho kuwaunga mkono watu wanaotaka nafasi za Udiwani na Ubunge na kuwapiga vita viongozi waliopo katika nafasi hizo kwa sasa. 
 "Jamani viongozi wenzangu wa matawi na kata, tunapowaunga mkono watu wanaotaka uongozi mwaka 2015 hatukijengi chama chetu badala yake tunakipaka matope kwanini msisaidiane na madiwani na wabunge waliopo kutatua kero na kutekeleza ahadi na ilani yetu iliyotuweka madarakani," alisema mbunge huyo. 
 Alisema yeye amekuwa haumizi kichwa kwa watu wanaopita kwenye jimbo hilo na kumkashifu kwa maneno mabaya ikiwemo kumchonganisha kwa wapiga kura kwa hakusoma hatua ambayo aliwaeleza kwamba walipomchagua mwaka 2010 aliwapa sifa zake na wao wakampa kura nyingi, wakawaacha wasomi. 
 "Ubunge ni miaka mitano mkiniacha nitarudi kuagua na nyie mnajua mimi sijasoma lakini mlinichagua mkulima mwenzenu na hakika kazi naiweza na nitaendelea kutekeleza ahadi zangu nilizoahidi bado nina mwaka mmoja na nusu, nikirudi huku mwaka 2015 kama sijatekeleza ahadi zangu mtanisuta, lakini nawaomba nipeni ushirikiano," alisema. 
 Profesa Majimarefu katika harambee iliyofanyika kwenye kata hiyo, aliwasaidia wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho kwa kulipa michango yote iliyokuwa ikitakiwa kuchangia ukarabati wa ofisi hiyo kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni 1.9 kufaniklisha ukarabati huo. 
 Mbunge huyo kabla ya harambee hiyo alitoa kiasi cha sh. 300,000 kwa ajili ya kununulia mifuko 20 ya saruji lakini walipokuwa kwenye harambee hiyo alishitushwa na taarifa ya Katibu wa CCM kata hiyo Shabani Hiza kwamba ujenzi wa ofisi hiyo ulikwama tangu walipokuwa wabunge waliopita ambao walisema hawakuwa wamechangia. 
 "Ndugu zangu mimi nitajitolea fedha za ukarabati wa ofisi hii ili iendane na hadhi ya chama chetu, lakini wajumbve wenzangu fedha ambazo mlikuwa mmepanga kuchangia ofisi hii nendeni mkalipe ada kwenye makadi yenu ili mwakani muweze kuchagua viongozi wa chama chetu,"alisema. Mbunge huyo aliaahidi kutekeleza ahadi ya kata hiyo ya kukosa mawasiliano ya simu jambo ambalo linasababisha wananchi hasa wakulima washine kuingia sokoni kutokana na kutokujua hali ya soko ilivyo ikiwemo viongozi wa serikali kukosa taarifa na maagizo ngazi za juu. 
Kata hiyo ina idadi ya watu 14,660 ambapo watu wenye uwezo kumiliki simu ni 4,000 kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji wa kata Hamissi Mkinta.
 Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani 'almaarufu Profesa Majimarefu' (kwanza kulia) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mngazija Kimbwaimbwai, Diwani wa Kata ya Kerenge Idd Shebila wakiwa kwenye mkutano wa Halmashauri ya CCM kata ya Kizara, Korogwe
 Wajumbe wakimsikiliza Mbunge wao
Seehemu ya wajumbe kwenye mkutano huo. Picha na Mashaka Mhando

KIKAO CHA 24 CHA BODI YA TAIFA YA PAROLE CHAANZA LEO JIJINI ARUSHA

$
0
0
Na Inspekta Lucas Mboje, Arusha 
 Kikao cha 24 cha Bodi ya Taifa ya Parole kimeanza leo Desemba 19, 2013 chini ya Uenyekiti wa Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity iliyopo Jijini Arusha. Kikao hiki cha siku mbili kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole kitajadili Wafungwa waliopendekezwa kuachiliwa kwa Parole. 
Aidha, Wajumbe watapitia mapendekezo ya Maboresho ya Sheria ya Bodi za Parole(Cape 400 RE 2002) pamoja na kuchambua maoni yanayohusu taarifa ya Mhe. Jaji Kiongozi ya kusamehe theluthi moja (1/3 ) ya Kifungo kwa washitakiwa watakaokiri Mahakamani. 
 Utaratibu huu wa Parole hapa nchini ni moja wapo ya adhabu mbadala wa kifungo ambao ni matokeo ya mfumo uliobuniwa na jamii katika nchi nyingi kwa miaka ya hivi karibuni ikiwa ni njia moja wapo ya kupunguza ongezeko la wafungwa ndani ya Magereza hivyo kuipunguzia Serikali na Wananchi ambao ndio walipa Kodi, Mzigo mkubwa wa kuwahudumia Wafungwa wawapo ndani ya Magereza. 
 Lengo Kuu la Sheria ya Bodi ya Parole ya Mwaka 1994 ambayo ilifanyiwa marekebisho Mwaka 2002 ni kuweka masharti Maalum kuhusu utaratibu wa Urekebishaji wa Wahalifu nje ya Magereza baada ya Mfungwa kutumikia sehemu ya kifungo chake na kuonesha mwelekeo wa kurekebika unaokubalika kwa mujibu wa Sheria hii na Kanuni zake. 
 Kumekuwepo changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa Sheria hii ikiwa ni pamoja na ufinyu au wigo mdogo wa Kisheria uliowekwa na Sheria yenyewe. Kutokana na wigo mdogo uliopo wa Kisheria takwimu zilizopo zinaonesha kuwa wafungwa wengi hawawezi kujadiliwa kwa kuwa hawana sifa zinazotakiwa kwa mujibu wa Sheria iliyopo.
 Kwa mujibu wa Sheria hiyo Mfungwa anayestahili Parole ni yule anayetumikia kifungo cha miaka minne(4) na kuendelea na awe ametumikia theluthi moja (1/3) ya kifungo chake na kuonesha mwelekeo wa kurekebika unaokubalika kwa mujibu wa Sheria hii na Kanuni zake. 
 Hiki ni Kikao cha Tatu kufanyika chini ya Uenyekiti wa Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo tangu ateuliwe na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Aprili, 2013.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo(kushoto) akiongoza Kikao cha kujadili wafungwa waliopendekezwa kuachiliwa kwa Parole(kulia) ni Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole ambaye pia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja. Kikao hiki kimeanza leo Disembark 19 katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini Arusha.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakipitia makabrasha yenye mapendekezo ya Wafungwa waliopendekezwa kuachiliwa kwa msamaha wa Parole(wa kwanza kulia) ni Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole, Bw. Francis Stolla akipitia makabrasha hayo kama anavyoonekana katika picha.
Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole ambaye pia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(suti nyeusi) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo mara baada ya kuahirisha Kikao hicho ambacho kitaendelea kesho Desemba 20, 2013 (kushoto) ni Mjumbe wa Bodi hiyo Dkt. Joseph Chuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole(walioketi) na Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole(waliosimama). Wa tatu kutoka kulia ni Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole ambaye pia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja.

JAJI MKUU WA TZ AONGOZA MKUTANO WA MAJAJI WAFAWIDHI, WASAJILI PAMOJA NA WATENDAJI WA MAHAKAMA LENGO LIKIWA NI KUJADILI KASI YA UTOAJI HAKI NCHINI NA KUPENDEKEZA NJIA MBADALA ZENYE LENGO LA KUBORESHA HUDUMA YA UTOAJI HAKI NCHINI.

$
0
0
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati), Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Fakih Jundu (wa Tatu kulia), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Mhe. Simon Lukelelwa ( wa pili kushoto), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju (wa kwanza kulia), Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga ( wa kwanza kulia), Msajili Mkuu wa Mahakama, Mhe. Ignas Kitusi, wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu katika Mikoa mbalimbali pamoja na Divisheni zake katika Mkutano wa kiutendaji unaofanyika Mjini Bagamoyo wenye lengo la kuboresha huduma ya utoaji haki nchi
 Viongozi wa Mahakama pamoja na Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na Wasajili wa Mahakama na Maafisa wengine wa Mahakama waliohudhuria katika Mkutano huo ambao unatarajia kumalizika kesho ambapo utatoka na Mikakati na mapendekezo mbalimbali yenye lengo la kuboresha huduma ya utoaji haki nchini.
 Viongozi wa Mahakama na Viongozi wengine wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mahakama wanaoiwakilisha Mahakama katika Mikoa mbalimbali nchin
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (kulia), akisalimiana na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju katika Mkutano huo unaofanyika Mjini Bagamoyo wenye lengo la kuboresha huduma ya utoaji haki nchini. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania).

MAMA SALMA APOKEWA KWA SHANGWE BAADA YA KURUDI NA TUZO YA UONGOZI KUTOKA DUBAI

$
0
0

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili kwenye ofisi yake iliyoko karibu na Ikulu mara baada ya kuwasili nchini akitokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu alikopokea tuzo ya uongozi huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuja kumpoke
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea maua kutoka kwa Mwenyekiti wa wake wa viongozi, Mke wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa William Lukuvi na Mwakilishi kutoka ofisi ya WAMA, mara baada ya kuwasili ofisini hapoakitokea Dubai kupokea Tuzo ya uongozi itolewayo na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi (CEL
 Hongera sana mama....
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ofisi za WAMA, ambako mamia ya wananchi walikusanyika kwa ajili ya kumpongeza baada ya kurudi na Tuzo ya uongozi aliyopokea huko Dubai leo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Cabin Crew Course

Balozi seif Ali Iddi akutana na ujumbe wa serikali ya uswisi

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekusudia kuweka kipaumbele katika kuendeleza mpango maalum wa kufanywa utafiti katika maeneo yote ya Kiuchumi, maendeleo na ustawi wa jamii. 
Kauli hiyo aliitoa wakati wa mazungomzo yake na Ujumbe wa Viongozi Wanane kutoka Serikali ya Uswisi  unaoongozwa na Waziri wa Sayansi, Utafiti na Elimu Bwana Mauro Dell Ambrogio aliokutana nao hapo Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar. 
Balozi Seif alisema mpango huo utakwenda sambamba na ongezeko la mitaala pamoja na masomo ya utafiti kupitia skuli za Sekondari na vyuo vikuu ili Taifa lifikie daraja ya kujitosheleza kwa wataalamu wa fani hiyo kufikia daraja la Udaktari. 
Aliueleza Ujumbe huo wa Serikali ya Swisszerland ambao upo Zanzibar kuhudhuria Kongamano la Utafiti na Ubunifu Zanzibar la kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya mwaka 1964 kwamba Zanzibar na Tanzania kwa ujumla zimebahatika kuwa na rasilmali nyingi baharini na Ardhini. Alifahamisha kwamba Rasilmali hizo hadi sasa bado hazijatumika vyema kutokana na ukosefu wa Taaluma ya kina ya utafiti ambazo baadaye zinaweza kusaidia ustawi wa kipato cha Wananchi walio wengi pamoja na Taifa kwa ujumla. 
Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifafanua kwamba zipo baadhi ya tafiti zilizowahi kufanywa na baadhi ya wataalamu wa hapa nchini kwa kushirikiana pia na wale wa kigeni lakini mara nyingi tafiti hizo huishia kuwekwa maofisini bila ya kufanyia kazi zilizokusudiwa. Mapema Waziri wa Sayansi, Utafiti na Elimu wa Uswisi Bw. Mauro Dell Ambrogio ameipongeza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kutokana na mipango yake ya kutilia mkazo suala la utafiti. Bwana Mauro alieleza kwamba utafiti popote pale ndio silaha na uti wa mgongo wa harakati za maendeleo katika taasisi zote ziwe za kiserikali, Mashirika ya Umma na hata sekta Binafsi. 
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi na Utafiti ya chuo Kikuu cha Basel Nchini Swisszerland Bwana Marcel Tanner aliyekuwa miongoni mwa ujumbe huo alisema Taasisi mbali mbali Duniani hivi sasa zimejikita zaidi katika kuona suala la Utafiti linapewa msukumo unaostahiki. 
Bwana Tanner alisema kuwa umuhimu wa tafiti hasa katika sekta za Afya na Kilimo ndio chachu inayosaidia kustawisha maendeleo na ustawi wa jamii popote pale Ulimwenguni.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na akisalimiana na Waziri wa Sayansi, Utafiti na Elimu wa Uswisi  Bwana Mauro Dell Ambrogio na ujumbe wake walipofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kwa mazungumzo.

 Balozi Seif akibadilishana mawazo na Waziri wa Sayansi,, Utafiti na Elimu wa Uswisi  Bwana Mauro Dell Ambrogio hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Serikali wa Uswisi ukiongozwa na Waziri wa Sayansi, Utafiti na Elimu Bwana Mauro Dell Ambrogio. Picha na Hassan Issa wa OMPR

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS IKULU NA UTAWALA BORA ZANZIBAR AWEKA JIWE LA MSINGI LA KITENGO KIPYA CHA UTIBABU WA UTI WA MGONGO NA UBONGO

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mhe. Mwinyi Haji Makame akiwahutubia wageni mbalimbali katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la kitengo cha matibabu ya Uti wa mgongo na Ubongo huko Hospitali kuu ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
 Wageni mbalimbali kutoka tasisi za Serikali na madaktari wakimsikiliza mgeni rasmin Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mhe. Mwinyi Haji Makame (hayupo pichani) alipokua akitoa nasaha mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika sherehe zilizofanyi Hospitali kuu ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mhe. Mwinyi Haji Makame akifungu pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la kitengo cha matibabu ya Uti wa mgongo na Ubongo katika sherehe zilizofanyi Hospitali kuu ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Jengo jipya la kitengo cha matibabu ya Uti wa mgongo na Ubongo linalojengwa kwa mashirikiano ya Serekali ya Spen na ya Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

Dar by night

$
0
0
 Taswira la jiji la Dar es salaam usiku huu...
Viewing all 109977 articles
Browse latest View live




Latest Images