Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 299 | 300 | (Page 301) | 302 | 303 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Freddy Macha

  Nimesalimiana na kusogoa kifupi na Mwalimu Nyerere, Rais Robert Mugabe (Dar es Salaam, 1978) na Rais Jakaya Kikwete. Vile vile nimekutana na kuwahoji washairi maarufu wa Kijamaika, Mutabaruka na Linton Kwesi Johnson; pia Ngugi wa Thiong’o wa Kenya, mtengenezaji sinema wa maisha ya Wamarekani weusi , Spike Lee, mwanariwaya wa Kizanzibari Adam Shafi na sasa Abdilatif Abdalla. Wote wana sifa moja. Mwandishi F Macha na gwiji Abdilatif Abdalla-London 2013
  Mwandishi nikiwa na gwiji Abdilatif Abdalla, London 2013. Sifa gani? Muda wote nliokuwa naye Abdilatif hakuacha kufanya masihara,utani, kutafuta maana katika jambo hata liwe dogo kiasi gani. Tulipoingia mkahawani kupata chai, aliwasikiliza hata watu asiowajua wanasema nini, huku akijumuika kucheka au kutojitenga. 
  Hiyo tabia ya kuchanganyikana kila nukta na wanadamu wenzake na jamii, nimeiona katika kila mtu mashuhuri niliyempa mkono wa salamu. Mathalan, nlipokuwa na Mwalimu Nyerere mjini Rio De Janeiro mwaka 1991, tuliongea utadhani rafiki wa karibu sana. 
  Kawaida unapogongana na watu wa aina hii hukujia hisia kwamba wao ni wadudu wa sayari nyingine; lakini Mwalimu alikufanya ujisikie mtulivu kabisa kwa utani na matani. Hali kadhalika mwimbaji maarufu, marehemu Miriam Makeba (aliyefariki 2008). 
  Nilikutana naye London, mwaka 1987, akiwa na mjukuu wake. Nilivyomsalimia wala hakushtuka. Aliongea kwa upole na tabasamu. Tabia yake ilijaa upole, unyenyekevu na ucheshi wa mwanamke wa kitongoji chochote cha Afrika. Kubali au usipokubali mtazamo wao, watu maarufu- (waliofanya ya maana) huwa na hilo. 


  0 0

  Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Moshi, Ally Janja (wa tatu kushoto) akikabidhi funguo ya jenereta la umeme kwa mshindi wa promosheni ya Weka Upewe ya NBC, Michael Charles Kipingu katika hafla iliyofanyika katika tawi hilo mjini Moshi hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Shedafa Omari Shedafa mmoja wa mashuhuda katika tukio hilo, Mhasibu wa Tawi, Rose Ntwale, Lazaro Mollel, teller na Digna Sawalla Meneja Huduma kwa Wateja na Mauzo katika tawi hilo.
  Mshindi wa promosheni ya Weka Upewe ya NBC, Michael Charles Kipingu (kushoto) akijaribu kuwasha jenereta yake mara baada ya kukabidhiwa na Meneja wa NBC Tawi la Moshi, Ally Janja (mwenye suti). Hafla hiyo ilifanyika mjini Moshi.
  Mshindi wa promosheni ya Weka Upewe ya NBC, Michael Charles Kipingu (aliyechuchumaa karibu ya jenereta) akipiga picha ya kumbukumbu pamoja na wafanyakazi wa Benki ya NBC Tawi la Moshi katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi huyo iliyofanyika katika tawi hilo hivi karibuni.

  0 0

   Baadhi ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi Kata za wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, wakiwa kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Kinondoni wakati wakisubiri kuanza safari ya kwenda Morogoro leo kwa ajili ya semina yao ya mafunzo itakayoanza kesho
  Wakiwa katika basi wakati safri ikiendelea kwenda Moro.


  0 0

  Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola barani Afrikaans wakisimama dakika moja ya ukimya ikiwa ni katika kumkumbuka Raid wa kwanza Mzalendo wa Afrika Kusini,Tata Nelson Mandela.Kikao hicho kilifanyika hapo jana katika hoteli ya Bahari Beach.
  Spika wa Bunge la Tanzania,Mhe Anne Makinda ambae pia ndio Rais wa Chama hicho barani Afrika akiwakaribisha rasmi wajumbe wa Kamati ya Uongozi.Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa mwaka 2014 unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai na kuhudhuriwa na takriban wabunge 500. Picha na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.

  0 0  0 0

  Waziri wa Maji,Prof. Jumanne Maghembe hivi karibuni alifanya ziara ya kushtukiza ili kuangalia maendeleo yaliyofikiwa na Wahandisi wanaoandaa ujenzi wa miundombinu ya maji katika Tank la Maji la Muhalo, Tarafa ya Mashimba(Shinyanga Vijjijini) kwenda Ngudu, Wilaya ya Kwimba.

   Aidha, Waziri aliangalia michoro itokanayo na usanifu wa mradi huo ambao unatarajiwa kugharimu Shs. 2.8 bilioni.

  Wataalamu wanaosimamia ujenzi huo sasa wanapokea zabuni za utengenezaji wa mabomba yatakayo tumika kutoa Maji Mhalo hadi Ngudu. Katika ujenzi huo vijiji 7 vilivyoko njiani kati ya mhalo na Ngudu navyo vitafaidika na mradi huu. Mradi huu utakao tekelezwa katika kipindi cha miezi 6.
  Waziri wa Maji,Prof. Jumanne Maghembe akikagua Tank la Maji la Muhalo.


  0 0

  A Meeting of the Technical Working Group on Rules of Origin in the context of the COMESA-EAC-SADC Tripartite Free Trade Area (FTA) negotiations is ongoing at Le Méridien Hotel, in Pointe-aux-Piments in Mauritius.

  The four-day meeting, hosted by the Mauritius’s Ministry of Foreign Affairs, Regional Integration and International Trade, has brought together around 100 trade and custom experts from the 26 Member States of the Tripartite region i.e. COMESA, EAC and SADC countries. The East African Community Director General for Customs and Trade Directorate Mr. Peter Kiguta is among the participants.

  The second Tripartite Summit held in South Africa, in June 2011, launched the negotiations for the Tripartite FTA.  Following discussions on the modalities of the negotiations, Member States are now engaged in negotiating the draft Tripartite FTA text as well as its Annexes on Rules of Origin, Non-Tariff Barriers, Technical Barriers to Trade and Sanitary and Phyto-Sanitary Measures, Dispute Settlement and Trade Remedies, amongst others.  These Annexes will form the integral part of the text constituting the Tripartite FTA.

  The Tripartite FTA will cover some 6,000 products.  While most of the products will be aligned to the existing rules of COMESA, SADC and EAC, some products will be subject to “specific rule to each product” depending on the outcome of the negotiations.

  The present Technical Working Group on Rules of Origin in Mauritius is pursuing discussions on criteria that would qualify a product to be considered as originating from the Tripartite region.  The discussions are focusing on the level of processing in various products, type of ownership and operation of vessels and factory ships.

  The Tripartite initiative aims at harmonising the trade regimes of the COMESA, EAC and SADC through the establishment of an enlarged FTA. The objective of the Tripartite FTA is to achieve a larger market with a single economic space which will make it more attractive to investment and large scale production.

  0 0

  Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Industry and Trade Maria Bilia cuts a ribbon to officially inaugurate the Mbeya Cement Lafarge Tanzania new ultra modern Bag Filter at the company’s plant in Mbeya, Friday 13th who is also the Acting Industrial Director in the Ministry of Industry and Trade. December. She is flanked by the Mbeya Cement Board Member Deodatus Ndunguru,
  Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Industry and Trade Maria Bilia gets a brief from Mbeya Cement Lafarge Tanzania Plant Manager Vijay Komaragiri on how the ultra modern bag filter works. Looking on is the company CEO Catherine Langrency.
  The Acting Industrial Director in the Ministry of Industry and Trade and Mr Deodatus Nduguru and who is also a Board Member of the Mbeya Cement Lafarge Tanzania (centre) speaks to the Deputy Permanent Secretary Maria Bilia (right) of the same Industry after the company launched a new ultra Modern Bag Filter on Friday 13th Minerals John Shija. 


  0 0


  0 0

    Katibu wa Itikadi na Uenezi mkoa wa Morogoro, Dorothy Mwamsiku, akifungua semina ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya ya Kinondoni, leo Des 17, 2013, katika hoteli ya Road View, nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro. Wengine ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Salum Madenge na Mwenyekiti wa Wazazi Kinondoni, Charles Mgonja.
  Baadhi ya Wajumbe wakiwa ukumbini kwenyesemina ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya ya Kinondoni, leo Des 17, 2013, katika hoteli ya Road View, nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro. 
  Picha zote na Latifa Ganzel)

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza Uongozi wa Jumuiya ya Milade Nabii,walipofika Ikulu Mjini Zanzibar,kwa Mazungumzo na Rais leo asubuhi. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Jumuiya ya Milade Nabii,walipofika Ikulu Mjini Zanzibar,baada ya Mazungumzo na Rais leo asubuhi.  

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kufungua kituo cha Afya Kijiji cha Kajengwa,Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja katika shamra
  shamra   kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar 
   Shein,akipata maelezo kutoka kwa Daktari dhamana Wilaya ya kusini (DMO) Daniel Francis Pius,(katikati) baada ya kukifungua kituo cha Afya Kijiji cha Kajengwa Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja 


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kajengwa Makunduchi,Wilaya ya Kusini Unguja,jana wakati wa sherehe za
  ufunguzi wa Kituo cha Afya,katika maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,
  Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu Zanzibar

  0 0

   Katibu Mkuu wa Dowuta Taifa, Bw. Jonathan Msoma akizungumza na Wanamichezo wa Bandari, katika siku ya kufunga michezo iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Sigara Chang’ombe. Kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadhi Massawe na Mganga Mkuu wa Mamlaka, Dkt. Mkunde Mlay.
  Katibu Mkuu wa Dowuta Taifa, Bw. Jonathan Msoma akisaini mprira kama kumbukumbu ya kufunga michezo ya Bandari iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Sigara Chang’ombe. Kushoto ni mwamuzi wa Kimataifa, Othaman Kazi na katikati ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadhi Massawe.
   Timu ya mpira wa soka ya Makao Makuu ikiwa katika picha ya pamoja.
  Mganga Mkuu wa Mamlaka, Dkt. Mkunde Mlay akisalimiana na wachezaji kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu.
   Mashabiki wa timu ya Bandari ya Dar es Salaam wakishangilia.
  Mstahiki Meya wa wilaya ya Temeke, Maabad Hoja akisoma hotuba yake wakati wa kufungua michezo ya Bandari iliyofanyika katika viwanja vya Sigara hivi karibuni.

  Mashabiki wa timu ya Makao Makuu wakishangilia.
  Shabiki wa timu ya Makao Makuu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya 'ufundi', Saidi Janguo akiwa kazini.

  0 0

  Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Sharon L. Cromer ameahidi kuendelea kushirikiana na TFDA katika kuhakikisha afya ya wananchi inalindwa kwa kuisaidia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) katika kuijengea uwezo kwenye masuala ya udhibiti wa usalama na ubora wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba nchini. 

  Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 17/12/2013 katika ziara ya ujumbe wa USAID iliyofanyika Makao Makuu ya TFDA kwa lengo la kujionea ufanisi wa utendaji wa Mamlaka kufuatia misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa na Shirika hilo la kimaendeleo kwa TFDA kuanzia mwaka 2011 hadi sasa.

  USAID imekuwa ikiisaidia TFDA katika kuwajengea uwezo watumishi wake hususan udhamini wa mafunzo kwa wakaguzi wa dawa, mafunzo kwa watumishi kuhusu mifumo bora ya utendaji kazi na utoaji huduma pamoja na manunuzi ya vifaa vya maabara ya Mikrobiolojia kwa lengo la kuendelea kukidhi vigezo vya Shirika la Afya Duniani (WHO).

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo, alikabidhi tuzo maalum kwa shirika la USAID ikiwa ni alama ya kutambua mchango wa USAID katika mafanikio yaliyofikiwa na Mamlaka kwa kipindi cha miaka 10 (2003-2013). 


  Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo akikabidhi tozo maalum kwa Mkurugenzi wa USAID Bi. Sharon L. Cromer katika hafla iliyofanyika TFDA makao Makuu.
  Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti ya TFDA na ujumbe wa USAID wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ziara hiyo.  Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo akiuonesha ujumbe wa USAID moja ya vitabu rejea vya viwango vinavyotumika katika maabara ya TFDA.

  0 0

  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (Kati kati) akiongoza Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma
  Katibu wa Chama cha Walimu Bw.Ezekiel Oluoch akitoa mchango wake mkutano huo Katibu wa TUGHE Bw. Ally Kiwenge akitoa maoni yake katika mkutano.
  Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome akijitambulisha kwa wajumbe wa mkutano ika mkutano.


  0 0
 • 12/17/13--12:00: KIJIWE CHA UGHAIBUNI • 0 0
  Kwa Maelezo Zaidi gonga hapa

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Irene Isaka akipokea tuzo ya  NBAA toka kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Goodluck Ole- Medeye   baada ya  kuwa  mshindi wa kwanza katika uwasilishaji wa hesabu safi  katika mwaka 2012,katika kundi la Mamlaka za Usimamizi zinazotumia mfumo wa “ International Public Sector Accounting Standards ( IPSAS) katika uandaaji wa mahesabu wakati wa hafla ya utoaji tuzo za NBAA  iliyofanyika katika hotel ya Naura  Spring Arusha.

   Mwenyekiti wa Bodi wa NBAA Professor Musa Assad  akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka wakati wa hafla ya utoaji tuzo za NBAA  iliyofanyika katika hotel ya Naura  Spring Arusha.

   Mjumbe wa  bodi ya NBAA na Mkurugenzi wa zamani wa bodi ya SSRA  bwana Juma Muhimbi  akimpongeza Mkurugenzi  Mkuu wa SSRA Bi.Irene  Isaka  mara baada ya kupokea tuzo ya NBAA, nyuma yake  Mkaguzi wa ndani wa SSRA  Bwana. Peter Mbelwa.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Rais wa kwanza Mzalendo na Mpigania Uhuru wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela ‘Madiba’ akiwa ameshikilia viatu vyake ambavyo aliviacha nyumbani kwa Mzee Nsilo Swai alipoingia Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 1962 akitokea Afrika Kusini ili kuanza harakati za ukombozi.

  Mzee Mandela aliahidi kuvichukua viatu hivyo pindi atakaporejea Tanzania lakini katika safari hiyo ndipo alipoishia mikoni mwa makaburu wa Afrika Kusini na kumfunga kwa miaka 27. Viatu hivyo vilihifadhiwa hadi alipotoka na kukabidhiwa kwa Mandela na mjane wa Mzee Nsilo Swai, Bi Vicky Nsilo Swai (pichani kulia)   Desemba 12,1995 Mandela alipotoka gerzani na hatimaye kuwa Rais wa kwanza Mweusi wa Afrika Kusini.

   Rais Kikwete akimtambulisha Mama Vicky Nsilo Swai na Mama Maria Nyerere kwa waombolezaji wakati wa shughuli ya mazishi ya Mzee Mandela kijijini Qunu Afrika kusini Desemba 15, 2015
   Mama Vicky Nsilo Swai na Mama Maria Nyerere wakiwa katika shughuli ya Mazishi ya Mzee Mandela kijijini Qunu
  Mama Vicky Nsilo Swai akishangiliwa na waombolezaji kwenye mazishi ya Mzee Mandela wakati Rais Kikwete alipomtambulisha na kueleza historia ya jinsi alivyomkaribisha Madiba nyumbani kwake na kumtunzia viatu vyake, simulizi ambayo ilimsisimua kila mtu aliyekuwepo ukumbini hapo na mamilioni waliokuwa wanaangalia tukio hilo live dunia nzima.

  Maandishi ya Mzee Mandela kwa Mama Vicky Nsilo Swai aliyoyaandika kwenye kitabu alichompa kama zawadi baada ya kurudishiwa viatu vyake mwaka 1995

  0 0

   Meneja Rasilimali watu kutoka Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Eliezer Mwasele, akishuka kutoka ndani ya ndege mara baada ya ndege ya Air Tanzania kutua wakati wa uzinduzi wa safari za kwenda Bujumbura- Burundi. Nyuma yake ni aliekuwa Balozi wa Tanzania Burundi, Francis Mndolwa.
   Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Nzagi (kushoto) akiwa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Francis Mndolwa (wa pili kushoto) mara baada ya kupokea ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania, Air Tanzania, iliyoanza sarai za kwenda Bujumbura mwishoni mwa wiki. Wengine mbele ni baadhi ya mawaziri wa serikali ya Burundi.

   Baadhi ya abiria wakipanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania –Air Tanzania- kabla ya kuanza safari ya kuelekea Bujumbura –Burundi, wakati wa uzinduzi wa safari hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
   Baadhi ya viongozi wakisindikiza abiria walioshuka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania –Air Tanzania- mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bujumbura- Burundi kama ishara ya uzinduzi rasmi wa safari hizo. Kutoka kushoto ni Waziri wa Burundi wa Afrika Mashariki, Bi Nziyemana Leontine akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Nzagi na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Francis Mndolwa
   ========   ========   ==========
  Air Tanzania yarudisha safari za ndege za kwenda Burundi
  ·       Waanza safari za kwenda Mbeya
  ·       Warejesha safari za Mwanza

  SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL) limezindua rasmi huduma za usafiri wa anga kutoka Dar es Salaam kuelekea Bujumbura, Burundi kwa kupitia mkoani Kigoma, safari hizo zitafanyika mara tatu kwa wiki yaani Jumatano, Ijumaa na Jumapili.

  Hatua hiyo imekuja baada ya hali ya amani kutengamaa katika nchi hiyo ya Burundi ambayo ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuilazimu Tanzania kusitisha huduma hizo kwa muda wa miaka 20.

  Wakati huo huo, ATCL pia imeanza safari za Dar es Salaam kwenda Mbeya, safari hizo zitafanyika mara nne kwa wiki yaani Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili. imerejesha safari za Dar es Salaam – Mwanza kila siku, safari  zilizoanza rasmi Jumapili iliyopita. 

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Bujumbura Burundi katika uzinduzi wa huduma hizo juzi, Meneja Rasilimali watu wa Shirika hilo la ndege, Ndugu Eliezer Mwasele, alisema uzinduzi wa safari hizo utakuwa ni njia mojawapo ya kuchochea maendeleo ya uchumi kwa nchi zote mbili.

  Alisema kutokana na hali hiyo Watanzania wanatakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika nchi hiyo ya Burundi, kwani asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa nchi za Kongo na Burundi wanatarajiwa kuanza kutumia usafiri huo kwa wingi.

  Akizungumzia hatua hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Nzagi, alisema kuanza kwa safari hizo ilikuwa ni ndoto ya siku nyingi ambayo aliipigania na kutamani kuona wananchi wa pande zote mbili wananufaika kwa pamoja.

  “Tumefurahi sana kwa kutimiza ndoto hii leo (juzi), kwa sababu sasa uhusiano kati ya nchi hizi mbili unazidi kuimarika hasa ukizingatia tunategemena kibiashara kulingana na fursa zilizopo.

  Kwa upande wake, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Francis Mndolwa, alisema kwa kuwa ATCL imefunga mkanda na kuanzisha tena safari hizo, ni vyema ikazingatia muda na kuhakikisha huduma stahiki zinatolewa ili kukuza shirika hilo.

  Naye Waziri wa Burundi katika Bunge la Afrika Mashariki, Nziyemana Leontine alisema, “kuanzishwa kwa Air Tanzania kuja Burundi, kutasaidia wananchi wa Burundi, hususani wafanyabiashara kwani walikuwa wanauganisha ndege kupitia nchi nyingine, lakini sasa hivi wananchi watakuja moja kwa moja. Tunashukuru sana,” alisema.

  Naye mmoja wa abiria kutoka Burundi waliopanda ndege hiyo, Dk. Owera Kodime, alisema, kuanzishwa kwa safari hizo kutawapunguzia sana gharama za usafiri wananchi wa Burundi, kwa sababu Tanzania imepunguza gharama kuliko mashirika mengine.

  “Tulikuwa tukitumia muda mrefu sana kuzunguka lakini sasa tutaweza kuja moja kwa moja Dar es Salaam, ni hatua nzuri ambayo imetuletea faraja sana Warundi,” alisema.

  Kwa upande wa abiria kutoka Tanzania, Joseph Kisaro, alisema, “ Muda mrefu sana kulikuwa hakuna huduma, tangu mwaka 1993 huduma zilikatatika, lakini uongozi wa Tanzania umefanya juhudi baada ya mapigano kuisha. “Tunashukuru ubalozi ulioteuliwa mwaka 2003 kwani ulianza harakati haraka za kurudisha huduma hizi ambazo sasa tumefanikiwa.

  “Tunaomba uongozi wa ATCL uangalie pia kuwa na safari za kuelekea Kongo mashariki kwa sababu kuna abiria wengi sana ambao ni wafanyabiashara wanaokuja Tanzania,” alisema

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi. 
  WIMBI la wahamiaji haramu kuingia nchini limeendelea kushika kasi katika siku za karibuni kufuatia kukamatwa kwa wahamiaji haramu wengine 11 raia wa Ethiopia katika kijiji cha Mlele kata ya Mashati wilayani Rombo wakiwa wamehifadhiwa katika nyumba ya kulala wageni.
  Tukio la kukamatwa kwa wahamiaji hao linakuja ikiwa ni wiki moja imepita baada ya kukamatwa kwa kundi jingine kubwa la wahamiaji haramu wapatao 56 katika kijiji cha Jiungeni wilayani Same wakiwa katika harakati za kufanya safari kuelekea nchini Afrika Kusini kwa lengo la kutafuta kazi. Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz amesema kuwa wahamiaji hao walikamatwa juzi majira ya saa 7 mchana baada ya askari polisi waliokuwa doria kupata taarifa ya kuwepo kwa wahamiaji hao haramu katika moja ya nyumba za wageni.
   “Jana(Juzi) saa 7 mchana askari wakiwa doria walipata taarifa kuwa kuna wahamiaji haramu na kwamba kwamba wamefichwa kwenye nyumba moja katika kijiji cha mlele kata ya Mashati na askari baada ya kufika katika nyumba hiyo waliwakuta”alisema Kamanda Boaz. 
   Alisema baada ya kukamatwa kwa wahamiaji hao polisi ilianza ufuatiliaji juu ya wahusika waliowaingiza nchini na kuwahifadhi ndipo wakafanikiwa kumkamata mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Leocadia Gapiti ambaye anadaiwa kuwa ndiye mmiliki wa nyumba hiyo. “Tumemkamata mwanamke mmoja anaitwa Leokadia Gapiti ambaye alikuwa amewahifadhi kwenye nyumba hiyo na mwingine Paulo Endevayesu ambaye ndiye wakala halisi ambaye alikuwa anawasafirisha watu hao.”alisema. 
  Kamanda  Boaz alisema uchunguzi zaidi unafanyika ili kujua watu hao walikuwa wanatoka wapi wanaenda wapi na kwamba pindi utakapo kamilika watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Kwa upande wake kamishna msaidizi wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Bw. Johanes Msumule alisema wamebaini kuwepo kwa mtandao mkubwa katika suala hilo na kwamba tayari wanaendelea kuwahoji watu wawili waliokamatwa ambao ni Leokadia na Paulo Endevayesu raia wa Burundi. Alisema katika kipindi cha wiki tatu kilichopita tayari wamesafirishwa zaidi ya wahamiaji haramu 74 kurudi nchini mwao Ethiopia ambapo kundi la kwanza lilikuwa la wahamiaji haramu 18 ambao walikabidhiwa kwa askari wa Kenya . 
   Alisema kundi la pili lilikuwa la wahamiaji haramu 56 lililokamatwa hivi karibuni lilisafirshwa hivi karibuni kupitia mpaka wa Namanga hadi katika kijiji cha Moyale kilichopo mpakani ma nchi za Kenya na Ethiopia. 
  Tukio la karibuni lilihusisha kukamatwa kwa wahabeshi 56 katika kijiji cha Jiungeni –Same wakiwa katika Lori aina ya Fuso, yenye namba za usajili, T188 AYU,linalotajwa kama mali ya kampuni ya ELyimo Trans ya Mjini Moshi likiwa na jina la Godbless Mbasha wa mkoani Manyara.
   Kamishna wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Johanes Msumule akizungumza na wanahabari ofisini kwake baada ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu 11 wilayani Rombo 
   Afisa wa uhamiaji wilaya ya Rombo akiwasindikiza watu wawili ambao wanatuhumiwa  kuwa ndio wahusika wa usafirishaji wa wahamiaji haramu hao.
  Bi.  Leokadia Tarimo raia wa Tanzania na  Bw. Paulo Endevayesu raia wa Burundi ambao wanatuhumiwa kujihusisha na biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu hao
   Wahamiaji haramu waliokamatwa wilayani Rombo katika moja ya nyumba ya wageni.
  Askari wakiwa katika gari lililopeba wahamiaji haramu hao waliokamatwa wilayani Rombo katika moja ya nyumba ya wageni.

older | 1 | .... | 299 | 300 | (Page 301) | 302 | 303 | .... | 3286 | newer