Wakazi wa Kijiji cha Mitaranda kata ya Kitombondo wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, wametakiwa kujitolea kwa hali na mali katika ujenzi wa Zahanati ya kijijini hicho ili kuondokana na changamoto za huduma za kiafya zinazowakabili.
Wito huo umetolewa leo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo Mkuranga,Abdallah Ulega wakati akitoa msaada wa mifuko 50 ya saruji na fedha taslim laki tatu kwa ajili ya kuharakisha ujenzi huo.
Amesema ni muhimu kwa jamii kuwajibika kwa pamoja kwa maslahi yao na taifa kwani, kufanya hivyo kutawarahisishia upatikaji wa huduma hiyo kwa haraka.
Wakati akisoma risala mbele ya naibu waziri Ulega Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mtaranda Jembe Ndembo amesema sanjari na ujenzi wa Zahanati hiyo pia wanamkakati wa kuinua kilimo ambapo kufikia msimu ujao kila Raia mwenye umri wa kuanzia miaka 18 awe na Ekari zisizopungua 2 ikiwemo ya mazao ya biashara na chakula , kuondokana na balaha la njaa na kuwainua wananchi kiuchumi.
Akizungumzia changamoto ya zahanati katika kijiji hicho Ndembo amesema kuwa kijiji hicho mpaka sasa hakina zahanati hali inayopelekea kinamama kujifungulia njiani."mpaka sasa tunatofari 2100 yaliyopatikana kwa nguvu za wananchi na halmashauri ,kupatikana kwa msaada huu tutapiga hatua sana katika ujenzi huu"alisema .
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya mkuranga,Juma Abeid amabye pia ni Diwani wa kata ya Magawa amempongeza mbunge huyo katika kufanikisha miondombinu ya umeme,Elimu na hata afya kwani amefanikisha katika kuleta maendeleo kwa haraka."wakati anaingia madarakani 2015 Ulega kulikuwa nachangamoto kubwa ikiwemo barabara na zahanati,lakini mpaka sasa ameshajenga zahanati zaidi ya Kumi kwakweli haijawahi kutokea kwa viongozi waliopita" Alisema Abeid
Katika hatua nyingine Waziri Ulega amefungua bonanza la michezo ndani ya wilaya ya Mkuranga lililowashirikisha timu mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu na wa pete huku akiwataka wachezaji hao na jamii kushiriki kikamilifu katika sekta ya michezo hatua ambayo itaongeza ushirikiano kwa jamii na kusaidia kuimarisha afya na upendo na kupelekea chachu ya maendeleo kwa mustakabali wa taifa.
Naibu Waziri wa Mifugo an Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mitaranda kata ya Kitombondo katiaka mkutano huo wanachama wapya 50 walijiunga na Chama cha Mapinduzi kutoka Chama cha Wananchi (CUF)
Naibu Waziri wa Mifugo an Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo Mkuranga,Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wapya 50 walijiunga na Chama cha Mapinduzi kutoka Chama cha Wananchi (CUF)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega akikabidhi mifuko ya Saruji 50 kwa wanakijiji wa Mitaranda kata ya Kitombondo kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la Zahanati ya Mitaranda.
Naibu Waziri wa Mifugo an Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo Mkuranga,Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa mpira pete.
Naibu Waziri wa Mifugo an Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wachezaji wa mpira wa miguu ambapo aliwaomba wachezaji hao na jamii kushiriki kikamilifu katika sekta ya michezo hatua ambayo itaongeza ushirikiano kwa jamii na kusaidia kuimarisha afya.