Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

UTEUZI WA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI MPYA WA BENKI YA BIASHARA YA TIB (TIB CORPORATE BANK LTD)

0
0

TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) ni Benki ya  biashara inayomilikiwa na Serikali. Benki inatoa huduma zote za kibenki za kibishara kwa  mashirika na taasisi za aina mbalimbali za serikali na binafsi ,pia benki inatoa huduma kwa watu binafsi. Benki ina matawi 7 kwa sasa,  Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha, Mbeya na Dodoma.
Kwa mamlaka iliyopewa Benki kuu imechukua uamuzi wa kusitisha uteuzi wa Bw. Frank Nyabundege kuanzia tarehe 13 Julai 2019, kufuatia usitishwaji huo imemteua Bw. Fred Luvanda kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji. Benki kuu ilichukua uamuzi huo chini ya mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 33(1) na 33(2)(f)  pamoja na 33 (2)(b)cha sheria ya Mabenki na Taasisi za fedha ya mwaka 2006.
Ndugu waandishi wa habari, mkiwa na kazi kubwa ya kuhabarisha umma tunaomba muweze kutoa taarifa sahihi kuwa Benki ya TIB Corporate haiko chini ya usimamizi wa mabenki bali ni mabadiliko ya uongozi wa juu tu.              (Aliyeondolewa ni Mkurugenzi Mtendaji). Benki ya TIB Corporate inaendelea kuhudumia wateja wake kama kawaida kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu.

Nachukua nafasi hii kuwatoa wasiwasi wateja na wadau wote wa benki ya Biashara TIB na wananchi kwa ujumla, wajue kuwa  huduma zinaendelea kama kawaida, pia mfahamu kuwa Serikali na Benki kuu inatambua umuhimu wa Benki hii hivyo itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha Benki  inazidi kuboresha huduma zake na kukua kwa maendeleo ya nchi yetu.
Niwaombe menejimenti pamoja na wafanyakazi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha benki inatimiza malengo yake.



Fred Luvanda

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji


APPOINTMENT OF ACTING MANAGING DIRECTOR FOR TIB CORPORATE BANK LTD

0
0

TIB Corporate Bank Ltd (TIB- CBL) is a fully fledged commercial bank, owned by the Government of the United Republic of Tanzania. 
The Bank has a branch network in main cities of Tanzania, 3 in Dar-Es-Salaam namely Samora, Mlimani City, and TPA mini branch and 4 branches upcountry namely; Arusha, Mwanza, Mbeya, and Dodoma. The bank offers customized products including credit facilities, trade finance, cash management, and treasury products. 

Pursuant to the of section 33(1), 33(2)(f) and 33(2)(b) of the Banking andFinancial Institutional Act,2006 the Bank of Tanzania decided to suspend the appointment of Mr. Frank Nyabundege with effect from 13th July 2019. Consequently has appointed Mr. Fred Luvanda to oversee the affairs and daily business operations of the bank.
Regarding this decision, we would like to clarify to the public that the bank is NOT under the Bank of Tanzania (BOT) Statutory Management. The decision done is the suspension of the Managing Director only. The bank shall continue with its normal operations to serve customers proficiently and diligently. 

We take this opportunity to request our esteemed clients and other stakeholders to remain calm and assure you that the Government and Bank of Tanzania understand clearly the importance of this bank and they will continue  to provide the necessary support to TIB Corporate Bank Ltd to ensure that the bank achieve its desired objectives for the benefit of the country. 

Fred Luvanda

Acting Managing Director
Dar es Salaam 15th July 2019

Miss Kinondoni 2019 afunguka siri ya ushindi wake

Diwani alazimika kuwapigia magoti viongozi na wanachama UWT kuwaomba wasiwe wasaliti

0
0
Na Francis Godwin,  Iringa

Diwani kata ya Mwangata  jimbo la Iringa mjini Nguvu  Chengula alazimika kuwapigia magoti viongozi  na  wanachama  wa vikundi  vya wajasiliamali vya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kata ya Mwangata  kuwaomba  kutorudia  makosa ya usaliti waliyoyafanya  mwaka 2015  ya  kuchagua viongozi  wa upinzani na  kuomba sasa wachague viongozi wa   serikali za mitaa pia  madiwani ,wabunge na Rais Dkt John Magufuli mwaka 2020.

" Naomba  kuwaomba  sana  tena sana ninyi wanachama na viongozi wa UWT kata ya Mwangata tuepuke  usaliti wakati wa uchaguzi simamieni na waelimisheni wananchi  wachague viongozi  wanaotokana na CCM ili kuleta  heshima kwa chama ...kwanza naomba kuwapigia magoti kabisa maana  naomba  kutoka moyoni chagueni CCM "  alisema Chengula huku akiwa amepiga magoti 

 Diwani   huyo  aliyasema hayo alifikia uamuzi huo wa  kuwapigia magoti wanavikundi hao jana katika  ukumbi wa Damu ya Yesu wakati  wa  uzinduzi  wa   vikundi nane  vya ujasiliamali vya  umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kata ya  Mwangata  . 

Alisema kuwa  sehemu  kubwa   vikundi ndani ya Manispaa ya  Iringa havijafikiwa na  mikopo  hiyo  kutokana na uamuzi  wa  wananchi walioufanya  mwaka  2015  kwa  kuchagua madiwani wa upinzani na mbunge wa upinzani  ambao wamekuwa  hawashughuliki na kero za  wananchi  zaidi ya  kujitazama  wao  hivyo   njia pekee ni kutorudia makosa kwenye  uchaguzi wa  serikali ya mitaa  na uchaguzi mkuu mwaka 2020 kuhakikisha  wanachagua  viongozi  watokanao na CCM pekee.

Aidha  aliitaka Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  kutoa  mikopo  inayopaswa  kutolewa  kupitia makusanyo yake ya  ndani ya  kwa  vikundi  vya wajasiliamali wa kata ya Mwangata  ili  kuwawesha  kukuza  mitaji yao kwani  lengo  la  serikali  kuagiza  Halmashauri  kutoa mikopo  isiyo na  riba kwa wanawake ,vijana na  walemavu  ni  kuwawezesha  kupanua  wigo  zaidi ya shughuli zao .

Diwani   Chengula  alisema kwa  ajili ya  kuviwezesha  vikundi  hivyo  kusajiliwa katika Halmashauri  tayari  mbunge wa  viti maalum  mkoa wa Iringa Rose  Tweve ( CCM)  amevitembelea  vikundi  vya kata ya Mwangata  na kuvisaidia  fedha  kiasi cha shilingi 500,000 kwa  ajili ya  kukuza  mitaji huku  yeye kama  diwani wa kata  ameviongeza  kiasi cha shilingi 800,000 ili  kuviongezea  nguvu ya  kusajiliwa kisheria.

“ Serikali ya  chama cha mapinduzi (CCM) chini ya mwenyekiti  wetu Rais Dkt  John Magufuli  ipo  kuona  wananchi  wenye  sifa ya  kupewa  mikopo  hii wananufaika nayo na mikopo  hii haitakiwi  kurejeshwa kwa  riba yoyote  hivyo ni haki ya  kila mwenye sifa  kupewa mikopo  hiyo  iwapo atakuwepo  kwenye kikundi “  alisema Chengula.
Hivyo  alisema  fedha   hizo ni haki ya   makundi  husika na lazima Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  kutoa mikopo  hiyo kwa makundi hayo  bila  kuwepo kwa ubaguzi  wowote  iwapo  vikundi  vitakuwa  vimetimiza sifa  zinazohitajika .
“ Mimi kama  diwani  wenu nitahakikisha napambana  kuubana  uongozi wa  halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  ili  fedha  hizo  ziweze  kutolewa kwa  vikundi  vyote ambavyo  vitakuwa  vimetimiza   sifa  ya  kupewa  mikopo  hiyo na sitakubali  kuona  mnahangaika   kutafuta mitaji  wakati  fedha za  serikali zipo “  alisema Chengula
Kuwa  vikundi  vya kata  hiyo  vimekuwa mfano wa  vikundi  vingine   ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  kutokana na aina  ya  shughuli za uendeshaji wa  viwanda  vidogo vidogo  vya utengenezaji batiki na vikapu  vya  kisasa  ambavyo wanachama  wake  wamekuwa  wakifanya na shida  yao ni  mitaji ya  kuboreshea huduma  zao.
Naibu  meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Joseph Ryata  alisema kuwa  uhakika wa  vikundi  hivyo kupewa mikopo upo  na kutaka kukamilisha taratibu za usajili wa  vikundi  hivyo  hasa  vile ambavyo havijasajiliwa .

Aidha  alisema  wajibu  wa halmashauri  hiyo kuendelea  kuwaunganisha  wananchi wake  na taasisi za  kifedha  zinazotoa mikopo nafuu kama inayotolewa na shirika la kuhudumia  viwanda  vidogo vidogo (SIDO) mkoa wa Iringa .
Awali  wanavikundi hao wakitoa changamoto  zao wakati wa kikao  hicho cha  uzinduzi wa vikundi vya   vya wajasiliamali kata ya Mwangata  walisema changamoto  kubwa ni Halmashauri  kushindwa  kutoa mikopo kwa  wakati .

 Diwani  wa kata ya Mwangata  katika Halmashauri ya manispaa ya  Iringa  Nguvu  Chengula akiwa amepiga magoti kuomba wanachama  wa  vikundi vya ujasiliamali  vya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kata ya Mwangata  kusaidia CCM kushinda kwenye  uchaguzi wa serikali za  mitaa jana  wakati wa  uzinduzi wa vikundi hivyo ukumbi wa damu ya Yesu Mwangata (Picha na Francis Godwin)
 Diwani  wa  kata ya  Mwangata  Nguvu  Chengulla  akionyesha  fedha  kabla ya  kuwakabidhi  wanavikundi kwa  ajili ya usajili wa  vikundi
Diwani  wa  kata ya  Mwangata  Nguvu  Chengulla  akikabidhi   fedha   wanavikundi kwa  ajili ya usajili wa  vikundi

Serikali kuwawekea dhamana wanunuzi wa Pamba kwenye soko la dunia

0
0
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga amesema Serikali ya Tanzania kupitia Benki kuu, imeamua kuweka dhamana kwa kufidia hasara itakayopatikana kwa wanunuzi wa Pamba kwenye soko la Dunia ili waweze kununua Pamba kwa bei ya shilingi 1,200 kwa kilo.
Akizungumza na Viongozi wa Mkoa na Wakulima kwa nyakati tofauti leo tarehe 15/07/2019 wakati akianza ziara ya siku tatu Mkoani Shinyanga Mhe. Hasunga amesema Serikali imefikia maamuzi hayo katika kikao cha pamoja kati ya Serikali, wanunuzi na baadhi ya wamiliki wa Benki kilichoitishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Mkoani Tabora jana tarehe 14/07/2019.
"Kuanzia leo, Benki kuu itakuwa inakamilisha taratibu zote na wafanyabiashara wataanza kupewa fedha kwa ajili ya kununua pamba" amesema Mhe. Hasunga.
Aidha, amezidi kueleza kuwa, Serikali imezitaka Benki kupunguza riba kutoka asilimia 16 hadi asilimia 11 ili kuwawezesha wanunuzi kupata fedha za kununua pamba.
Hasunga amesema lengo la Serikali ni kuwasaidia wanunuzi waweze kupata fedha ya kununua pamba yote ya wakulima na wakulima wapate fedha kwa bei ya shilingi 1,200 kwa kilo kama ilivyotangazwa licha ya bei ya soko la Dunia kushuka.
Amewahakikishia wakulima kuwa, vituo vyote kutakuwa na fedha za kutosha kununua pamba na wakulima watapata fedha zao moja kwa moja na pia kuanzia mwaka ujao kutakuwa na mfumo mzuri zaidi wa ununuzi wa pamba usiokuwa na usumbufu kwa wakulima na wanunuzi.
Akielezea changamoto zilizotokana na wanunuzi kushindwa kununua pamba katika msimu huu, Mhe. Hasunga amesema kuwa Serikali ilitangaza bei ya sh. 1,200 kwa kilo baada ya kukokotoa na wanunuzi na kuona bei katika soko la Dunia ipo juu, lakini kutokana na vikwazo mbalimbali bei ya soko la Dunia imeshuka hivyo wakulima watapata hasara iwapo watanunua kwa bei hiyo, pia Benki zilikataa kuwapa fedha kwa kubaini hasara hiyo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amebainisha kuwa, Shinyanga ndiyo Mkoa wenye viwanda vinavyomilikiwa na wazawa ni vema pia kuzungumza na wenye viwanda hivi kufahamu wanahitaji kiasi gani ili waweze kununua pamba inayozalishwa Mkoani hapa. 
Akizungumza na wakulima katika kiwanda cha Afrisian kilichopo Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Telack amewataka wakulima kuhakikisha wanaitunza vizuri pamba ili isishuke ubora wake, kwani pamba ya Tanzania inasifika kwa ubora na nyuzi zinazofaa kwa kutengeneza nguo.
Mhe. Hasunga yupo Mkoani Shinyanga kwa siku tatu ikiwa ni ziara ya kikazi, pamoja na shughuli nyingine atatembelea vituo vya kununulia pamba.
 Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Shinyanga (hawapo pichani) katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa alipoanza ziara yake mchana wa leo
 Msafara wa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ukiwa katika kiwanda cha Afrisian kuona wakulima wakikusanya pamba yao kwa ajili ya kuuzwa, mbele ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimuongoza Mhe. Hasunga kushuhudia pamba hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizungumza na wakulima waliokuwepo katika kiwanda cha Afrisian Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuuza pamba yao  

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KUHUSU MATUKIO MBALIMBALI

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.



Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmojaMWAKILA S/O ALLY [32], mkazi wa Mwambene, Jijini Mbeya  kwa tuhuma za kupatikana na laini za simu [141] zenye usajili wa majina ya watu wengine.
Mnamo tarehe 12/07/2019 majira ya saa 13:00 mchana huko mtaa wa Itongo kata ya Mwambete tarafa ya Iyunga. Mtuhumiwa ambaye pia ni fundi umeme baada ya kukamatwa na kuhojiwa alikiri kumiliki laini hizo za simu 141 za mitandao tofauti zilizosajiliwa kwa majina tofauti ikiwemo “HALOTEL” laini 13, TIGO laini 29,TTCL laini 01, VODACOM laini 78 na AIRTEL laini 20. Pia alikutwa akiwa na vocha zilizotumika  za Vodacom 05, Tigo 04, Airtel 48, Halotel 03 pamoja na simu Itel03, “Oking01 na “Hotwave01
Chanzo ni kujipatia kipato. Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

AJALI YA GARI KUACHA NJIA NA KUPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI NA UHARIBIFU- WILAYA YA RUNGWE.
Mnano tarehe 14/07/2019 majira ya saa 09:00 huko Kanyegele kata ya kiwira tarafa ya Ukukwe wilaya ya Rungwe. Barabara ya kuu ya TUKUYU – MBEYA, Gari na. T. 359 DCA/T. 429 CMH Aina ya Howo mali ya kampuni ya “Overland” iliyopo “Dsm” ikiendeshwa na RAJAB S/O ISSA [40] ikiwa imebeba mafuta aina ya Petrol na Diesel kuelekea Tukuyu iliacha njia na kupindukia kolongoni na kusababisha uharibifu  wa mali na mafuta kumwagika baada ya “Tank” kupasuka. Aidha  msaidizi wa dereva aitwaye SALUMU S/O SAID[40] amepata majeraha. Chanzo cha ajali ni ubovu wa matairi ya gari hiyo.
Natoa wito kwa wananchi kutosogea maeneo ya ajali bila kuchukua tahadhari, kwani madhara ya kufanya hivyo ni kupata ulemavu wa viungo, au kupoteza maisha kutokana na hatari mbalimbali kama milipuko ya mafuta. 

AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO- WILAYA YA MBALIZI.
Mnamo tarehe 14.07.2019 majira ya saa 20:30 u0siku, CHRISTINA D/O ANTHONY @ MWALINGO[37] aligongwa na gari huko katika Kata Inyala, Tarafa Tembela, Wilaya Kipolisi Mbalizi, Mkoa Mbeya, barabara ya Mbeya - Njombe na kusababisha kifo chake papohapo.  Gari na dereva hajafahamika. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Igawilo. Ufuatiliaji kumkamata dereva na gari unaendelea.

TUKIO LA MAUAJI -WILAYA YA MBEYA.
Mnamo tarehe 14.07.2019 majira ya saa 09:00 asubuhi huko meneo ya mtaa wa Mponja  Kata ya Igawilo, Tarafa Iyunga, Jijini Mbeya, mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la MARIA D/O FAUSTINE@KISANJI[22] Mkazi wa Mwanyanje alikutwa  amefariki dunia kwenye Pagala linalomilikiwa na mtu aitwaye ESTER D/O JOHN @MWANSHEMELA

Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa mhudumu wa Bar itwayo SIKALAMANGA inayomilikiwa na DOMINICK S/O ABRAHAM.Ambapo mnamo tarehe 13/07/2019 majira ya saa 23:00 usiku marehemu aliondoka na  mtu asiyefahamika/jinsia ya kiume ambaye alikuwa anakunywa naye pombe. Kiini cha tukio ni ugomvi wa kimapenzi kati ya wawili hao. Msako mkali  unaendelea ili kubaini na kumkamata aliyehusika katika tukio hilo.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu  na wahalifu kwa kuweka mkazo zaidi katika kutoa elimu. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu pamoja na ajali za barabarani.
WITO:
Natoa wito kwa jamii kuacha, kujihusisha na vitendo vya kihalifu na kujishughulisha na kazi halali kwa ajili ya kujipatia kipato. Ni rai yangu kwa  wananchi/Madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuchukua tahadhari pindi wanapokuwa katika barabara zenye miteremko mikali, na milimani kwani ajali nyingi hutokea maeneo hayo na kusababisha madhara makubwa kwa jamii.

       Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI - SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


RC WA SONGWE BRIGEDIA MWANGELA ATOA SIKU SABA KITUO CHA AFYA IBABA KUANZA KUTOA HUDUMA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela amempa siku saba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ahakikishe kuwa kituo cha Afya cha Ibaba Wilayani humo kinatoa huduma za Afya hususani huduma za Mama na mtoto.

Brigedia Mwangela ametoa agizo hilo mara bada ya kukagua maendeleo ya ujenzi katika kituo hicho na kukuta miundombinu yote muhimu ikiwa ni pamoja na majengo yote yakiwa yamekamilika lakini huduma za afya hazitolewi.

“Mkurugenzi nakupa siku saba akina mama na watoto waanze kupata huduma hapa, kituo hiki kimekamilika isipokuwa kwa mambo machache ambayo yapo ndani ya uwezo wenu”, amesisitiza Brigedia Mwangela.

Amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa Daktari aliyepaswa kuhudumia kituo hicho anafika siku ya Jumatatu na pia halmashauri ihakikishe ujenzi wa njia za wagonjwa (walkways) wenye thamani ya shilingi milioni 20 unakamilika mapema.

Aidha Brigedia Mwangela amewataka wananchi wa Ibaba kukitunza na kukitumia hicho na endapo kutakuwa na ucheleweshwaji wa kuanza kutolewa huduma watoe taarifa ofisini kwake.

“Wananchi wa Ibaba nia ya serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya ndio maana kumekuwa na ujenzi wa Kituo hiki, sasa ikifika Jumatatu Daktari hamjamuona hapa mnitaarifu na mkiona imefika siku ya ijumaa akina mama na watoto hawapati huduma hapa nijulisheni”, amesema Brigedia Mwangela

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya amesema serikali imetoa shilingi milioni 400 zilizojenga majengo ya upasuaji, maabara, jengo la kuhifadhia maiti, wodi ya wazazi na nyumba ya daktari pia imepeleka vifaa vya kutolea huduma vyenye thamani ya shilingi milioni 92.2 katika kituo hicho.

Dkt. Kagya ameeleza kuwa kwa majengo ambayo tayari yamekamilia na vifaa vilivyokwisha tolewa kituo hicho kinaweza kutoa huduma za mama na mtoto isipokuwa huduma ya upasuaji ambayo itahitaji uwepo wa njia ya kupitia wagonjwa (Walkways).
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa watazingatia maagizo yake na kuhakikisha wananchi wa Ibaba wanapata huduma za Afya katika kituo hicho ndani ya siku ya saba walizopewa.
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela akizungumza na viongozi katika humba cha upasuaji katika kituo cha Afya Ibaba ambapo ameagiza huduma zianze kutolewa ndani ya siku saba.
Majengo ya Kituo cha Afya Ibaba, Wilaya ya Ileje yaliyojengwa kwa fedha za serikali shilingi milioni 400 ambayo yamekamilika lakini huduma za Afya hazijaanza kutolewa.

SERIKALI,BUZWAGI KUSHIRIKIANA KULINDA ULINZI NA USALAMA KAHAMA

0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,  akizungumza wakati   Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.
 Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ,Arthur Mgongo akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), wakati  Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo  ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akipokea zawadi ya kitabu cha kuhifadhia kumbukumbu kutoka kw Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ,Arthur Mgongo  wakati  Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akionesha zawadi ya kitabu cha kuhifadhia kumbukumbu alichopokea  kutoka kwa Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ,Arthur Mgongo(kushoto),  wakati  Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo  ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongozana na Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi , Arthur Mgongo (kulia) wakati  Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo  ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya  Ndani ya Nchi

JENGO LA TATU LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM KUANZA KUTUMIKA MWEZI UJAO - NDITIYE

0
0


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Mhandisi Atashasta Nditiye, amesema Ujenzi wa Jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) umekamilika, na Jengo linatarajiwa kuanza uendashaji mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

Pia amesema amefurahishwa kwa kukamilika kwa jengo hilo ambapo ni la kisasa na huduma zake zake ni nzuri.

Akizungumza mara baada ya Ziara ya kukagua Jengo hilo , amesema katika idadi ya miruko ya ndege Barani Afrika JNIA inachukua nafasi ya tano na nafasi ya sita kwa idadi ya abiria.

‘’ Nimefurahishwa kwa kukamilika kwa Ujenzi wa jengo la tatu la abiria wa Kiwanja cha Ndege ambapo utakapoanza kuhudumia abiria natarajia tutachukua nafasi nzuri zaidi Barani Afrika kwani ni Jengo la kisasa na litatoa huduma nzuri,’’ alisema.

Nae Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere( JNIA), Paul Rwegasha akitoa ufafanuzi wa Kiwanja hicho, alisema mara baada ya kukamilika kwa jengo la tatu itakuwa jumla ya majengo matatu yanaweza kuhudumia abiria milioni nane kwa mwaka.

Rwegesha alisema ujenzi wa jengo la kwanza lina uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka na ujenzi wa jengo la pili abiria milioni 1.5

Alisema kukamilika kwa jengo hilo la tatu kutaongeza idadi ya Ndege, abiria pamoja na Watalii baada ya kuwa na Miundombinu bora na ya kisasa.

Vile vile alisema Ujenzi wa jengo la tatu ni kwa ajili ya abiria wa safari za Kimataifa ambapo kwa sasa yako mashirika 23 na jengo la pili kwa ajili ya abiria wa safari za ndani ya nchi huku jengo la kwanza safari za ndani pia. .

Alisema ujenzi wa jengo la tatu la abiria litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 2,800, kwa saa na maegesho ya magari mchanganyiko yasiopungua 2,075 kwa wakati mmoja.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama, alisema kwasasa kuna katika maandalizi ya Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa 39 wa SADC ambapo maadalizi yameambatana na ukarabati wa maboresho ya miundombinu na samani.

Ndyamukama, alisema wageni hao wanatarajia kuingia hapa nchini Agosti mwaka huu ambapo watapata huduma bora zaidi na yenye uhakika.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Tanzania Mhandisi Julius Ndyamukama (mwenye koti jeusi)akisoma Taarifa ya Mradi wa Jengo la III la abiria kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye alipofanya ziara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye akihoji jambo katika Ukumbi wa Watu mashuhuri alipotembelea jengo la III la abiria.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Bw, Paul Rwegasha ( mwenye koti kijivu) Akitoa maelezo ya jengo la mizigo linalokarabatiwa kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye wakati alipofanya ziara katika Kiwanja hicho

SAKATA LA KODI YA PANGO LA ARDHI LAZIDI KUWA CHUNGU KWA BAADHI YA KAMPUNI MWANZA

0
0

Na Munir Shemweta, WANMM,  MWANZA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amezidi kuzibana Taasisi na Makampuni yenye madeni makubwa ya kodi ya pango la ardhi ambapo ametua mkoani Mwanza na kuyabana makampuni na taasisi nane ambazo kwa ujumla wake zinadaiwa zaidi ya milioni 900.
Kampuni na taasisi alizotembelea Dkt Mabula ni Synergy Tanzania Ltd, Ideal Development Ltd, Birchard Oil Ltd, Shule za Musabe, Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Ndamavyo Auto Spares, Jesse & Company Ltd na Maabara ya Taifa ya Udhibiti Samaki na Mazao ya Uvuvi.
Akizungumza katika ziara yake hiyo ya kufuatilia madeni ya kodi ya pango la ardhi mwishoni mwa wiki, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema ziara hiyo anayoifanya ya kuwafikia wale wenye madeni makubwa inafuatia baadhi ya kampuni na taasisi zinazodaiwa kushindwa kulipa ama kurekebisha madeni yao baada ya kikao cha Juni 11, 2019 kilichowakutanisha wadaiwa zaidi ya 200 jijini Dodoma
katika mwanzo wa ziara yake kwenye shule za Musabe, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alimueleza mmiliki wa shule hizo Daniel Musabe kulipa deni lake la kodi ya pango la ardhi linalofikia milioni 57.4 katika viwanja vyake vinne anavyomiliki kufikia tarehe 31 Julai 2019 ili kuepuka kufikishwa katika Baraza la Ardhi na Nyumba.
Hata hivyo, Mmiliki wa Shule hizo ambazo ni za Chekechea, Msingi na Sekondari alimueleza Dkt Mabula kuwa yuko tayari kulipa deni la kodi ya pango la ardhi lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na changamoto za kibiashara ambapo hata hivyo aliahidi kulipa kiasi anachodaiwa kuanzia Agosti 2019 na kumaliza deni lote ifikapo Desemba 2019.
Akiwa katika Kampuni ya Birchard Oil Limited, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula ambaye aliambatana na Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami aliitaka kampuni hiyo kulipa kiasi inachodaiwa cha kodi ya pango la ardhi inayofikia milioni 85,235,050 ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya kodi za miaka ya nyuma.
Meneja uhusiano wa Kampuni hiyo inayojishughulisha na uzalishaji Mafuta na Marobota ya Pamba Arshad Jetha alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi kuwa kampuni yake pamoja na kudaiwa kodi ya pango la ardhi kwa baadhi ya viwanja inavyomiliki lakini baadhi yake alishalipia hivyo aliomba kuhakikiwa madeni yake ili kupata deni halisi.
Ideal Development Ltd kupitia Meneja wake Burnanuddin Rajbhai alikiri deni la kodi ya pango la ardhi linalofikia milioni 79 na kuomba kupewa muda wa kulipa katika awamu tatu tofauti. Hata hivyo, Naibu Waziri wa Ardhi alizitaka kampuni na Taasisi zilizokubali kulipa madeni kuandika barua ya kueleza namna zitakavyolipa na muda wa mwisho wa kulipa madeni yao katika ofisi za ardhi za halmashauri husika na nakala za barua hizo ziende ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Kanda ya Ziwa.
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo aliionya kampuni ya Ideal Development Ltd kwa kushindwa kutekeleza makubaliano yaliyofikia ya kulipa deni lake na kuieleza kuwa hatua itakayofuata kwa kampuni hiyo ni kufikishwa katika Baraza la Ardhi na suala la kuingia makubaliano ya malipo haliwezi kufanyika kwa mara ya pili.
Kampuni ya Synergy Tanzania Ltd Kupitia kwa Meneja Utawala wake Florence Kivamba iliahidi kuandika barua ya makubaliano ya kulipa deni la milioni 43 inayodaiwa ingawa alioamba kufanya mawasiliano na uongozi wa juu kwa kuwa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi ilikuwa ya kushtukiza na uongozi haukuwepo.
Akiwa katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula aliueleza uongozi wa Taasisi hiyo kuwa inadaiwa jumla ya shilingi milioni 515,713,900 ya kodi ya pango la ardhi na taasisi hiyo haijawahi kulipa kodi hiyo tangu mwaka 1996.
Mkurugenzi wa NIMR mkoa wa Mwanza Safari Kinuhi alijitetea kwa kueleza kuwa taasisi yake inapaswa kusamehewa kulipa kodi ya pango la ardhi kwa kuwa haiko kibiashara bali inatoa huduma kwa wananchi na kuboresha afya ingawa aliahidi kuwasiliana na uongozi wa juu kuhusiana na suala hilo.
Hata hivyo, Dkt Mabula alimueleza kuwa Taasisi yake inapaswa kufuata sheria wakati wa kuomba kusamehewa kodi ya pango la ardhi huku Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami akisisitiza kuwa hata kama Taasisi hiyo itasamehewa kulipa kodi hiyo lakini deni la nyuma lazima lilipwe kwa kuwa sheria ya msamaha itaanza pale tamko la msamaha lilipotoka.
Maabara ya Taifa ya Udhibiti Samaki na Mazao ya Uvuvi iliyopo eneo la Nyegezi ilionekana kutokuwa na hati ya eneo inalomiliki ingawa Afisa Mfawidhi wa Taasisi hiyo Emanuel Mundoko alijitetea kwa kueleza kuwa awali Taasisi hiyo ilikuwa sehemu ya chuo cha Uvuvi na sasa inajitegemea hivyo hawajui madeni halisi wanayodaiwa.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiagana na Afisa Mfawidhi wa Maabara ya Taifa ya Udhibiti Samaki na Mazao ya Uvuvi Emanuel Mundoko wakati wa oporesheni ya kufuatilia madeni ya kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akihakiki deni la kodi ya pango la ardhi la kampuni ya Jesse and Company Ltd wakati wa oporesheni ya kufuatilia madeni ya kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Jesse and Company ltd Sundeep Bachu.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimpa maelekezo Meneja Rasilimali Watu wa kapmuni ya Synergy Tanzania Ltd ( wa kwanza kulia) wakati wa oporesheni ya kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami.
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo (wa tatu kulia) akifafanua jambo kwa Meneja wa Kampuni ya Ideal Development Ltd Burnanuddin Rajbhai (wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipoitembelea kampuni ya Ideal Development Limited katika operesheni ya kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Dorothy Mwanyika na wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akihakiki deni la kodi ya pango la ardhi la kampuni ya Birchard Oil Limited pamoja na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Arshad Jetha (kushoto) wakati wa oporesheni za kuwatembelea wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami.


INTRODUCING: "NAKUJA" BY ZEE & HAMADAI

0
0
ZEE and HAMADAI both are artists under Kwetu studios Label. NAKUJA official audio is a song talking about a girl who is waiting for his Boyfriend and the Boyfriend tells her that " I'm coming" in Kiswahili "NAKUJA" 

DAR ES SALAAM CITY

0
0

.
There are literally countless ways to tell a story. We use cinematography, Design, Drone and Social media to turn entrepreneurs message into a movement.
.
Storyteller @moizhusein 
.

Rais Dkt. Magufuli apokewa kwa shangwe Mwanza mjini

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Abiria wa Kivuko cha MV Mwanza na MV Misungwi kuhusu ujenzi wa Daraja  litakalopita ziwani katika eneo la Kigongo na Busisi mkoani Mwanza. Mkandarasi wa Daraja hilo anatarajiwa kupatikana ndani ya miezi miwili na Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilometa tatu zitakazopita majini. Daraja hilo litagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 300.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono abiria wa Kivuko cha MV Mwanza na MV Misungwi mara baada ya kuzungumza nao katika eneo la Busisi Sengerema mkoani Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kupanda Kivuko cha MV Mwanza katika eneo la Busisi wakati akitokea Geita. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mwanza mjini mara baada ya kuwasili akitokea mkoani Geita. PICHA NA IKULU



RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA NA KUFUNGUA MIRADI NA MABORESHO YA HUDUMA ZA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA BUGANDO IKIWEMO HUDUMA YA TIBA ZA SARATANI PAMOJA NA KIWANDA KIDOGO CHA OXYGEN

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Mwanza wakati akiwasili katika viwanja vya hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando kabla ya kuzindua maboresho ya huduma za hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando ikiwemo huduma ya Tiba za Saratani pamoja na Kiwanda Kidogo cha Oxygen huduma ambayo inapatikana pekee katika hospitali hiyo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali  ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza Renatus Nkwande pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Hospitali hiyo Profesa Abel Makubi wakati akitoka kupata maelezo ya maboresho ya huduma za hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando ikiwemo huduma ya Tiba za Saratani pamoja na Kiwanda Kidogo cha Oxygen huduma ambayo inapatikana pekee katika hospitali hiyo.

 Sehemu ya jengo linalotoa huduma ya Tiba za Saratani pamoja na Kiwanda Kidogo cha Oxygen huduma ambayo inapatikana pekee katika hospitali hiyo.


Hospitali ya Rufaa ya Bugando. PICHA NA IKULU

MAPAMBANO YA RUSHWA YANG’ARISHA OFISI YA RAIS NA OFISI YA WAZIRI MKUU

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema juhudi za Serikali za kupambana na rushwa, kudhibiti upotevu wa mapato, matumizi ya fedha za Serikali na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma ni sababu zilizowezesha Ofisi ya Rais pamoja na Ofisi ya Waziri kuaminika zaidi.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na viongozi wa Umoja wa Wanake Tanzania (UWT) akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma. Amesisitiza kuwa vita dhidi ya rushwa ni endelevu.

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya rushwa ambapo kwa Afrika Tanzania inaongoza kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya Transparency Internation iliyotolewa hivi karibuni.

Ripoti hiyo mpya iliyotolewa Julai 11, mwaka huu inaonesha kwamba kwa sasa Tanzania inaongoza katika nchi 35 za Afrika baada ya kupungua kwa vitendo vya rushwa katika sekta nyingi, ambapo Ofisi ya Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu zimeonekana kuaminika zaidi.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwatahadharisha watumishi wa umma kwamba Serikali kamwe haitomvumilia mtumishi atakayebainika anayejihusisha na vitendo vya rushwa na aliwataka wahakikishe kuwa wanatekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi bila ubaguzi.



Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa, hivyo amewataka wananchi wasisite wakati wote kutoa taarifa kwa vyombo husika pale watakapobaini uwepo wa watumishi wanaojihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa.

“Watumishi wa umma wanatakiwa kutambua kwamba jukumu lao kubwa ni kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia maadili na kanuni za utumishi wa umma zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni na si vinginevyo. Serikali hii kamwe haitowaonea haya au kuwafumbia macho watumishi wa hovyo.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa suala la kuwaondoa kazini watumishi wazembe, wasiotimiza wajibu wao ipasavyo pamoja na wale wasiozingatia maadili ya utumishi wa umma ni endelevu kwa sababu Serikali inahitaji watumishi wa umma wenye heshima na nidhamu ya kazi.

Suala la kuwapokea, kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma kwa wananchi zikiwemo ofisi za Serikali kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo watumishi wa umma wanapaswa kuzingatia jambo hilo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Msingi cha cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao hilo, Julai 15, 2019. 
  Waziri Mkuu, Kasism Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Katibu na Meneja wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga kuhusu pamba iliyokusanywa na wakulima kwenye ghala la ushirika huo, Julai 15, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mikokoteni iliyosheheni pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Msingi cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga alikofanya ziara ya siku moja ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao hilo, Julai 15, 2019. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mkokoteni uliyosheheni pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Msingi cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga alikofanya ziara ya siku moja ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao hilo, Julai 15, 2019. Kushoto   ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. 
 Wananchi wa kijiji cha Mwabakima wilayani  Igunga wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya  kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba, Julai 15, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya  kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba, Julai 15, 2019. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA 16 WA ELIMU WA KIMATAIFA MKOANI TANGA

0
0


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kwenye Ufunguzi huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha kumbukumbu Sabastian Kolowa  kanda ya Afrika Bishop Dkt. Stephen  Munga wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kwenye Ufunguzi huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa walipokutana kwenye Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kwenye Ufunguzi huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe.



 Baadhi ya washiriki wa  Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE)wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga. .  Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Baadhi ya Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo.  Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe.

TIB CORPORATE BANK YAWAONDOA HOFU WATEJA WAKE

0
0

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) Fred Luvanda akizungumza na waandishi wa habari na kutolea ufafanuzi wa Benki Kuu (BOT) kumuondoa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo pamoja na kuwaondoa hofu wateja na wadau wote wa benki ya Biashara TIB na wananchi kwa ujumla.

Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) Fred Luvanda ametolea ufafanuzi wa Benki Kuu (BOT) kuondolewa kwa aliyekuwa Mtendaji mkuu wa benki hiyo  Frank Nyabundege.
Akizungumza na waandishi wa habari, Luvanda amesema kuwa kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kupelekea kwa BOT kufanya maamuzi ya kuichukua benki inayoshindwa kulinda amana za wateja na kuiweka chini ya mamlaka yake.
Luvanda ameeleza, Benki ya TIB Corporate haiko chini ya usimamizi wa mabenki bali ni mabadiliko ya uongozi wa juu tu kwa kuondolewa kwa Mkurugenzi Mtendaji  ila Benki ya TIB Corporate inaendelea kuhudumia wateja wake kama kawaida kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu chini ya menejimenti na bodi ya wakurugenzi iliyokuwapo awali.

Benki kuu ilichukua uamuzi huo chini ya mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 33(1) na 33(2)(f)  pamoja na 33 (2)(b)cha sheria ya Mabenki  na Taasisi za fedha ya mwaka 2006," 

Nachukua nafasi hii kuwatoa wasiwasi wateja na wadau wote wa benki ya Biashara TIB na wananchi kwa ujumla, wajue kuwa  huduma zinaendelea kama kawaida, pia mfahamu  kuwa Serikali na Benki kuu inatambua umuhimu wa Benki hii hivyo itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha Benki  inazidi kuboresha huduma zake na kukua kwa maendeleo ya nchi yetu.

TIB ni Benki ya  biashara inayomilikiwa na Serikali. Benki inatoa huduma zote za kibenki za kibishara kwa  mashirika na taasisi za aina mbalimbali za serikali na  binafsi ,pia benki inatoa huduma kwa watu binafsi. Benki ina matawi 7 kwa sasa,  Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha,  Mbeya na Dodoma

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Yaipongeza Mvomero kwa Skimu bora ya Umwagiliaji

0
0
Pichani kulia Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo kwa ajili ya kupata taarifa kuhusu Maendeleo na mafanikio waliyoyapata baada ya ukarabati mkubwa wa miundombinu kufanyika katika shamba la Ushirika la Wakulima Wadogowadogo Kilimo cha Umwagiliaji Mpunga Dakawa (UWAWADA),Wilayani humo,ambapo ukarabati wa miundominu hiyo umefadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani kupitia Shirika la Misaada la USAID-Tanzania,aidha gharama za ufadhili huo wa Ukarabati wa Miundombinu hiyo ya shamba imegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 24.

RAIS MAGUFULI ASHUTUKIZA GEREZA LA BUTIMBA...AGUSWA NA ALIYOYASIKIA NA KUYAONA, AAHDI KUYASHUGHULIKIA HARAKA

0
0
*Wafungwa wamuomba Rais Magufuli dua maalum
*Ni baada ya kuamua kusikiliza changamto zao 
*Awaambia amepata soko kubwa na limemuingia 


Na Said Mwishehe-Michuzi TV

RAIS Dk.John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Butimba mkoani Mwanza ambapo amekiri  kuona na kuyasikia mengi, hivyo ameahidi kuyafanyia kazi.

Akiwa katika gereza la Butimba Rais Dk.Magufuli amepata nafasi ya kusikiliza changamoto mbalimbali za wafungwa ikiwemo ya kufungwa baada ya kubambikiziwa kesi, kuombwa rushwa, kesi kukaa muda mrefu pamoja na aina nyingine za malalamiko.

Wakati kwa upande wa Askari Magereza wa Butimba nao wameeleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo na kufafanua changamoto kubwa ni usafiri, nyumba za askari na kukosa mtaji wa kuendeleza mradi wao wa kokoto na mradi wa kuvua samaki.

Akizungumza baada ya kuwasikiliza wafungwa na askari magereza , Rais Magufuli amesema kufika kwake gerezani hapo kuna somo kubwa limemuingia na akwenda kulifanyia kazi.

"Niliyoyasikia lazima nifanyie kazi, nimesikia changamoto za wafungwa na nimesikia pia changamoto za askari wangu.Niahidi nitayafanyia kazi yote ambayo nimeyasikia kwenu wote,"amesema Rais Magufuli na kuongeza hayuko tayari kuona askari magereza wanalalamika wakati yeye yupo.

Rais Magufuli amefafanua kwenye gereza hilo la Butimba amegudua mambo mengi , amebaini kuna kuombwa rushwa wafungwa na mahabusu na uamuzi wake wa kufika hapo umetokana na kufahamu mambo mengi ambayo mengine wafungwa wameshindwa kueleza.

Amewahakikishia wafungwa hao kwamba amewalewa wafungwa na mahabusu hao na kuahidi kuwa amewasikia na yote ambayo ameleezwa yatafanyiwa kazi."Niahidi nimewasikia, nimewasikia na yote nitayafanyia kazi.Naomba muwe wavumilivu na niaminini."

Rais Magufuli amesema hata walioko uraiani ni wafungwa au mahabusu wabadae na kwamba kufungwa au kuwa mahabusu haina maana ya kukosa haki za kibinadamu.

"Ndio maana nimekuja hapa kuwasalimu, nimesikia changamoto zenu lakini wakati huo huo nimeona changamoto za askari wangu ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu.Pia nafahamu kuna watu wamefungwa kwa kubambikiziwa kesi, kuna watu kesi zao zinacheleweshwa kwasababu hawajazungumza na polisi.Nimeguswa na niliyoana hapa gereni,"amesema Rais Magufuli.

Wakati anazungumza gerezani hapo Rais Magufuli amewaomba wavumilie na kuwaeleza wafungwa amekwenda gerezani hapo na viongozi wa ngazi mbalimbali na kwamba nao wamesikia yaliyosemwa.

Baadhi ya wafungwa wametumia nafasi hiyo kumueleza Rais namna ambavyo wananyanyaswa na baadhi ya askari wa magereza huku wengine wakilalamikia kukaa muda mrefu bila kusi kusikilizwa.Pia wapo wafungwa ambao wamemuomba Rais Magufuli aangalie namna ya kuwasaidia ili watoke kwani wamejirekebisha na kuwa raia wema.

Kabla ya Rais kuondoka gerezani hapo, wafungwa na mahabusu wamefanya ombi maalumu ili Mwenyezi Mungu azidi kumpa baraka katika kulitumikia Taifa letu huku pia wakieleza kuwa wao wafungwa wameeleza kazi kubwa na nzuri anayoifanya, hivyo wametumia dua hiyo kuomba wale ambao hawajamuelewa Rais nao wamuelewe.

Naibu Waziri Aweso awataka Mameneja wa RUHASA kutomuangusha Rais Magufuli

0
0
Na Charles James, Michuzi TV

Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso amewataka Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa Wakala wa Majisafi, Usafi na Mazingira Vijijini kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanaondoa changamoto za Maji katika maeneo yao.

Mhe Aweso ameyasema hayo wakati alipokutana na Mameneja hao jijini Dodoma ambapo amesema kwa sasa Wizara hiyo imeunda kitengo cha usanifu ambacho kitasaidia katika kuangalia upya usanifu, mikataba na gharama zinazowekwa na wakandarasi kabla ya ujenzi wa miradi.

Amewataka Mameneja hao kutumia weledi na taaluma zao kuhakikisha wanamtua mama ndoo kichwani na kuwataka kuacha mambo ya hovyo yaliyokuepo awali.

" Katika ziara zangu zote katika maeneo mbalimbali nimekua mkali sana kwa wahandisi na wakandarasi, baadhi ya wataalamu wametuangusha kwa kutumia miradi kujipatia fedha, nimejionea mwenyewe miradi mingi wakishindwa kuimaliza kwa wakati. Wakandarasi hawa hatuwezi kuwavumilia hata kidogo.

" Mhe Rais ametuamini sana katika nafasi hizi tulizoteuliwa, ni jukumu letu kumsaidia kazi na kutumia taaluma zetu kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wananchi waliopo vijijini inafikiwa kwa asilimia 85 au zaidi ifikapo mwaka 2020," amesema Mhe Aweso.

Amewataka Mameneja hao kutosubiri Waziri au Katibu Mkuu kufika katika maeneo yao ya kazi na kuwaonesha changamoto badala yake waunde mikakati ya kuwawezesha kufikia maeneo yenye changamoto ya Maji ili waweze kuitatua.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof Kitila Mkumbo amesema malengo ya Wizara hiyo ni kuongeza upatikanaji wa Maji kufikia asilimia 84 kutoka asilimia 64 kwa maeneo ya Vijijini, lakini pia wakifikia asilimia 95 kutoka asilimia 84 kwa maeneo ya Mjini.

" Tumekua tukiwekeza sana kwenye miradi mipya lakini kama tukiongeza nguvu na kumaliza miradi ambayo imekwishaanza na kuanza kufanya basi tungekua mbali sana hivyo katika bajeti zetu lazima tupange bajeti zetu Katika kukarabati miradi ya zamani.

" Mhe Naibu Waziri kazi kubwa na ya haraka kufanywa na RUHASA ni kujenga imani kubwa kwa Mhe Rais na Wananchi, na imani hiyo itajengwa na wahandisi hawa kwa kuhakikisha miradi ya wananchi inafanya kazi lakini kubwa zaidi ni kumaliza tatizo la Maji," amesema Prof Mkumbo.
 Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso akizungumza na Mameneja wa RUHASA kwa ngazi ya Mikoa na Wilaya (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof Kitila Mkumbo akitoa neno katika kikao cha Mameneja wa RUHASA kwa ngazi ya Mikoa na Wilaya jijini Dodoma.
 Mameneja wa RUHASA kwa ngazi za Mikoa na Wilaya wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma walipokutana na Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso (katikati) akiwa Katika picha ya Pamoja na watendaji wa Wizara hiyo na Mameneja wa RUHASA kwa ngazi za Mikoa na Wilaya jijini Dodoma.
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images