Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

RC HOMERA AMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA MLELE KWA KASI YA UJENZI WA HOSPITALI, AWAHAKIKISHIA WANANCHI UJENZI WA BARABARA USERVYA KATAVI KWA KIWANGO CHA LAMI

0
0
RC Katavi , Mhe. Homera ameipongeza Halmashauri ya Mpimbwe kwa mwenenendo mzuri wa Ujenzi wa Hospitali ya wilaya kwa kufikia 87%.

Aidha, RC Homera amewapongeza kutokana na kasi kubwa ya ujenzi wakiongozwa na mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ndugu Erasto Siwale ,aidha RC Homera amempongeza DED Erasto kwa kuwa msimamizi mahiri wa miradi na kuwaunganisha watumishi kuwa kitu kimoja katika halmashauri hiyo.

Hospitali hii inajengwa kwa Tsh Bilion 1.5. Mhe. Homera amewapongeza pia wafanyakazi na mafundi wanaoijenga hospitali hiyo na kuwataka waendelee kuwa wazalendo na kutotumia saruji na vifaa vingine kinyume na matakwa ya serikali.

Hata hivyo, RC Homera aliwaeleza wananchi waliokuwa hospitalini hapo kuwa ujenzi wa Hospitali hizo za mkoa mzima wa Katavi ni Jitihada za serikali ya CCM ya awamu ya Tano katika kutekeleza ilani yake ya mwaka 2015-2020  ibara ya 49,50 inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ikisimamiwa vyema na waziri wa Nchi Ofisi Ya Rais Tamisemi Mhe Suleiman Jafo.

RC Homera amewataka wananchi na mafundi kuhakikisha Hospitali inakamilika kwa wakati ili waendelelee kufurahia matunda yanayotokana na serikali ya awamu ya tano.

 Lakini pia RC Homera amewahakikishia wananchi wa Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoani Katavi ujenzi wa barabara kiwango cha lami KM 1.7-Mpaka 2 kwa Bajeti ya  mwaka 2019/2020 Katika Mji wa Uservya chini ya wakala wa Barabara Tanzania ,Tanroad. 

pia hayo yatafanyika sambamba na uanzishwaji wa Benki mojawapo katika mji huo ambao una uzalishaji mkubwa wa mazao ya biashara na chakula pamoja na Kata ya majimoto mkoani Katavi.

CSP KUPAMBANA NA UKEKETAJI MANYARA

0
0
KATIKA kupambana na ukeketaji ulioenea Mkoani Manyara, shirika lisilo la kiserikali la Civil Social Protection Foundation (CSP) limeanzisha mradi wa mwaka mmoja wa kubadili vikwazo vya kiutamaduni na kutokomeza vitendo hivyo.

Mkurugenzi wa CSP Nemence Iriya akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati alisema wameanzia wilayani Hanang' kisha watafuata wilaya nyingine za mkoa huo. 

Iriya alisema watawatumia wazee wa kimila wa eneo hilo katika kikao chao ili kuhakikisha wanatokomeza vitendo hivyo vya kikatili ambavyo mkoa wa Manyara unaongoza nchini kwa asilimia 58.

Alisema wameazimia kutumia mijadala kwa jamii ili kutokomeza vitendo hivyo kuliko kuwashurutisha kwani ni bora kubadili fikra zao wenyewe na kuongeza uelewa wa moja kwa moja. 

"Ukeketaji umejikita kwenye kanuni na taratibu za kijamii, imani za utamaduni na vichocheo vya kiuchumi na unatumika kama njia ya kudhibiti ashki ya kujamiiana kwa wanawake," alisema Iriya. 

Alisema katika jamii nyingi inachukuliwa kama jambo la muhimu kwenye shughuli za jando na unyago na simulizi potofu za ukeketaji zimekuwa zinajirudia mara kwa mara. 

Mwezeshaji wa mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia, Charles Odero alisema wamewajengea waandishi wa habari uwezo zaidi ili jamii izidi kufaidika kupitia vyombo vyao. 

Odero alisema kupitia taarifa za waandishi hao jamii itazidi kupata uelewa wa madhara ya vitendo vya kikatili vya ukeketaji ambapo mkoa wa Manyara unaongoza kwa vitendo hivyo kwa hapa nchini. 

Alisema waandishi hao wataeleza hali ipoje, nani anahusika, inasababishwa na nini, sheria, mipango, mikataba ya kimataifa inaelezeaje juu ya hayo na kusikiliza jamii pia ikizungumza juu ya hilo. 

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Manyara, (Mamec) Mary Margwe alisema hivi sasa baada ya serikali kuongeza nguvu za kupambana na ukeketaji jamii imebadili mtindo kwa kuwakeketa watoto wachanga kwa kutumia kucha. 

"Elimu inapaswa kuendelea kutolewa kwa jamii ili kuhakikisha vitendo hivi vinamalizika kwani vimepitwa na wakati na wanapaswa kubadilika tofauti na miaka iliyopita," alisema Margwe. 

Kuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukeketaji nchini, kumeelezwa kama eneo lenye kuleta wasiwasi wa utekelezaji wa mikataba ya haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia. 
 Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Civil Social Protection Foundation (CSP) Nemency Iriya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya kupambana na vitendo vya ukeketaji.
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Manyara, wakimsikiliza Mkurugenzi wa CSP, Nemency Iriya akizungumza nao juu ya mikakati ya kupambana na vitendo vya ukatili vya ukeketaji.

MAPAMBANO YA RUSHWA YANG’ARISHA OFISI YA RAIS NA OFISI YA WAZIRI MKUU

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema juhudi za Serikali za kupambana na rushwa, kudhibiti upotevu wa mapato, matumizi ya fedha za Serikali na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma ni sababu zilizowezesha Ofisi ya Rais pamoja na Ofisi ya Waziri kuaminika zaidi.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na viongozi wa Umoja wa Wanake Tanzania (UWT) akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma. Amesisitiza kuwa vita dhidi ya rushwa ni endelevu.

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya rushwa ambapo kwa Afrika Tanzania inaongoza kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya Transparency Internation iliyotolewa hivi karibuni.

Ripoti hiyo mpya iliyotolewa Julai 11, mwaka huu inaonesha kwamba kwa sasa Tanzania inaongoza katika nchi 35 za Afrika baada ya kupungua kwa vitendo vya rushwa katika sekta nyingi, ambapo Ofisi ya Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu zimeonekana kuaminika zaidi.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwatahadharisha watumishi wa umma kwamba Serikali kamwe haitomvumilia mtumishi atakayebainika anayejihusisha na vitendo vya rushwa na aliwataka wahakikishe kuwa wanatekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi bila ubaguzi.



Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa, hivyo amewataka wananchi wasisite wakati wote kutoa taarifa kwa vyombo husika pale watakapobaini uwepo wa watumishi wanaojihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa.

“Watumishi wa umma wanatakiwa kutambua kwamba jukumu lao kubwa ni kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia maadili na kanuni za utumishi wa umma zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni na si vinginevyo. Serikali hii kamwe haitowaonea haya au kuwafumbia macho watumishi wa hovyo.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa suala la kuwaondoa kazini watumishi wazembe, wasiotimiza wajibu wao ipasavyo pamoja na wale wasiozingatia maadili ya utumishi wa umma ni endelevu kwa sababu Serikali inahitaji watumishi wa umma wenye heshima na nidhamu ya kazi.

Suala la kuwapokea, kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma kwa wananchi zikiwemo ofisi za Serikali kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo watumishi wa umma wanapaswa kuzingatia jambo hilo. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya  kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba, Julai 15, 2019. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Msingi cha cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao hilo, Julai 15, 2019. 
  Waziri Mkuu, Kasism Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Katibu na Meneja wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga kuhusu pamba iliyokusanywa na wakulima kwenye ghala la ushirika huo, Julai 15, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mikokoteni iliyosheheni pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Msingi cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga alikofanya ziara ya siku moja ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao hilo, Julai 15, 2019. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mkokoteni uliyosheheni pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Msingi cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga alikofanya ziara ya siku moja ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao hilo, Julai 15, 2019. Kushoto   ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. 
 Wananchi wa kijiji cha Mwabakima wilayani  Igunga wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya  kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba, Julai 15, 2019.

BRIGEDIA MWANGELA ATOA SIKU SABA KITUO CHA AFYA IBABA KUANZA KUTOA HUDUMA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela amempa siku saba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ahakikishe kuwa kituo cha Afya cha Ibaba Wilayani humo kinatoa huduma za Afya hususani huduma za Mama na mtoto.

Brigedia Mwangela ametoa agizo hilo mara bada ya kukagua maendeleo ya ujenzi katika kituo hicho na kukuta miundombinu yote muhimu ikiwa ni pamoja na majengo yote yakiwa yamekamilika lakini huduma za afya hazitolewi.

“Mkurugenzi nakupa siku saba akina mama na watoto waanze kupata huduma hapa, kituo hiki kimekamilika isipokuwa kwa mambo machache ambayo yapo ndani ya uwezo wenu”, amesisitiza Brigedia Mwangela.

Amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa Daktari aliyepaswa kuhudumia kituo hicho anafika siku ya Jumatatu na pia halmashauri ihakikishe ujenzi wa njia za wagonjwa (walkways) wenye thamani ya shilingi milioni 20 unakamilika mapema.

Aidha Brigedia Mwangela amewataka wananchi wa Ibaba kukitunza na kukitumia hicho na endapo kutakuwa na ucheleweshwaji wa kuanza kutolewa huduma watoe taarifa ofisini kwake.

“Wananchi wa Ibaba nia ya serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya ndio maana kumekuwa na ujenzi wa Kituo hiki, sasa ikifika Jumatatu Daktari hamjamuona hapa mnitaarifu na mkiona imefika siku ya ijumaa akina mama na watoto hawapati huduma hapa nijulisheni”, amesema Brigedia Mwangela

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya amesema serikali imetoa shilingi milioni 400 zilizojenga majengo ya upasuaji, maabara, jengo la kuhifadhia maiti, wodi ya wazazi na nyumba ya daktari pia imepeleka vifaa vya kutolea huduma vyenye thamani ya shilingi milioni 92.2 katika kituo hicho.

Dkt. Kagya ameeleza kuwa kwa majengo ambayo tayari yamekamilia na vifaa vilivyokwisha tolewa kituo hicho kinaweza kutoa huduma za mama na mtoto isipokuwa huduma ya upasuaji ambayo itahitaji uwepo wa njia ya kupitia wagonjwa (Walkways).

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa watazingatia maagizo yake na kuhakikisha wananchi wa Ibaba wanapata huduma za Afya katika kituo hicho ndani ya siku ya saba walizopewa.
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela akizungumza na viongozi katika humba cha upasuaji katika kituo cha Afya Ibaba ambapo ameagiza huduma zianze kutolewa ndani ya siku saba.
Majengo ya Kituo cha Afya Ibaba, Wilaya ya Ileje yaliyojengwa kwa fedha za serikali shilingi milioni 400 ambayo yamekamilika lakini huduma za Afya hazijaanza kutolewa.

SAFARI YA KIBIASHARA NCHINI MAREKANI

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI WA JESHI LA POLISI MKOANI GEITA

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugora watatu kutoka kulia, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, Wabunge pamoja na Viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi katika eneo la Magogo mkoani wa Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wakati akitoka kukagua moja ya nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
  Makamishna kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini wakifurahia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za uzinduzi wa Nyumba za makazi ya Askari Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
 Bendi ya Jeshi la Polisi ikitumbuiza katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.

 Sehemu ya Mradi wa  nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita ambao umezinduliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Magogo mkoani Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Geita mara baada ya  kuhutubia katika uzinduzi wa nyumba hizo za makazi ya Askari Polisi. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Geita wakati akielekea kuzindua nyumba za Askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Katoro na Buseresere hawaonekani pichani wakati akielekea Geita mjini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bwanga wakati akitokea Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

KAMPENI YA PLASTIKI NOMA YALENGA KUHAMASISHA JAMII KUHUSIANA NA MADHARA YA TAKA ZA PLASTIKI

0
0
* Wananchi waombwa kushiriki usafi katika eneo la daraja la Salender Alhamisi Julai 18 mwaka huu

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV 
UTAFITI wa madhara ya taka za plastiki katika bahari ya Hindi uliofanyika kuanzia Septemba 2018 hadi Sasa umekuja na kampeni kabambe ya kuelimisha jamii kuhusiana na madhara ya taka za plastiki katika bahari ya Hindi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mmoja ya watafiti hao ambaye pia  ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Vicensia Shule amesema kuwa utafiti huo ulifanyika katika maeneo kadhaa ya Pwani ya bahari ya Hindi likiwemo eneo la Salender jijini humo huku wakijiegemeza katika kuangalia aina na kiwango cha taka za plastiki zinazoingia au kutoka baharini pamoja na kuelimisha jamii ya tatizo hilo kwa kubuni mbinu za ukusanyaji na taka hizo.

Vicensia amesema kuwa  malengo mahususi ya utafiti huo yalilenga kupima taka za plastiki katika ukanda wa bahari jijini humo na kutafuta njia ya kurekebisha madhara hayo.

Amesema kuwa pia utafiti huo ulilenga kutathimini ufanisi wa sheria za nchi, sheria ndogondogo, sheria za kitaifa na kimataifa, kanuni na sera za taasisi zinazoingiza, kuzalishaji na kuagizaji vifaa vya plastiki ndani na nje ya nchi.

Vilevile ameeleza kuwa baada ya kufanya utafiti huo wameona ni vyema wakaja na kampeni hiyo ya kujenga uelewa na kuhamasisha jamii juu ya madhara yanayoletwa na taka hizo.

Kwa upande wake Dkt. Rose Massalu ambaye ni kiongozi wa utafiti huo amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kunategemewa kuzalisha ajira katika sekta mbalimbali huku wakiishukuru serikali kwa kukataza matumizi ya mifuko ya plastiki licha ya kuwepo kwa baadhi ya plastiki zikiwemo chupa za maji, mifuko ya pipi na kadharika.

Amesema kuwa kampeni hiyo itaenda sambamba na usafi utakaofanyika katika eneo la daraja la Salender na kwa kushirikiana na taasisi ya Baba Watoto Centre  watahusisha watoto na vijana 125 kutoka Manispaa zote ambao wamekuwa wadau wakubwa wa kufatilia shughuli za namna hiyo.

Kwa upande wake Dkt. Benjamini Ngatunga amesema kuwa katazo matumizi ya plastiki lililoanza Juni  na sheria juu ya katazo hilo wananchi wamelitii ndani ya mwezi mmoja pekee, jambo ambalo linatia moyo na kuona mwanga wa matumizi hayo ya plastiki kukoma.

Utafiti huo umehusisha watafiti wanne wakiwemo Dkt. Lydia Gaspare, Dkt. Rose Massalu, DKt. Benjamin Ngatunga na Dkt. Vicensia Shule.
 Mtafiti Kiongozi wa Utafiti wa madhara ya Takataka za Plastiki kwenye Bahari ya Hindi Dkt. Vicensia Shule akizungumza na waandishi habari kuhusiana Uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha jamii madhara ya Plastiki itakayofanyika katika Ufukwe wa Selander jijini Dar es Salaam.
Mtafiti Dkt.Benjamin Ngatunga akizungumza madhara ya Plastiki na nchi zilizochukua hatua ya kuzuia Plastiki jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA ABIRIA WA KIVUKO KATIKA ENEO LA BUSISI SENGEREMA MKOANI MWANZA

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Abiria wa Kivuko cha MV Mwanza na MV Misungwi kuhusu ujenzi wa Daraja  litakalopita ziwani katika eneo la Kigongo na Busisi mkoani Mwanza. Mkandarasi wa Daraja hilo anatarajiwa kupatikana ndani ya miezi miwili na Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilometa tatu zitakazopita majini. Daraja hilo litagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 300.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono abiria wa Kivuko cha MV Mwanza na MV Misungwi mara baada ya kuzungumza nao katika eneo la Busisi Sengerema mkoani Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kupanda Kivuko cha MV Mwanza katika eneo la Busisi wakati akitokea Geita. PICHA NA IKULU


Watatu kortini kwa kudaiwa kuiba Madini katika Tume ya Madini

0
0
 Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
WATU watatu wakazi wa Jijini Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi likiwemo shtaka la kuiba madini  yenye thamani ya Sh 507,347,000.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Donald Njonjo (30) Mkazi wa Kigamboni, Gamba Muyemba (51) Mkazi wa Tandika na Kashif Mohamed (41) Mkazi wa Upanga jijini Dar es Salaam.

 Mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Kelvin Mhina imedaiwa kuwa kati ya Novemba 30, 2017 na Juni 29, mwaka huu katika Ofisi ya Tume ya Madini iliyopo Masaki wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam washtakiwa waliiba madini ya dhahabu yenye uzito wa Kilogramu 6.244 yenye thamani ya Sh 507,347,000 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imeendelea kudaiwa kuwa, Julai 8, mwaka huu katika Mtaa wa Indiragandhi wilayani Ilala jijini Dar es Salaam mshtakiwa Mohamed alikutwa na madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 2794.5 ya Dola za Marekani 121,155.45 sawa na Sh 278,714,478.06 mali ambayo imeibiwa kwenye Tume ya Madini.

Katika shtaka la tatu imedaiwa kati ya Julai Mosi, 2018 na Novemba 31, mwaka jana katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Ilala, washitakiwa kwa pamoja waliuza madini ya dhahabu yenye uzito wa Kilogramu 6.244 ya thamani ya Sh 507,347,000 bila kuwa na kibali.

Pia inadaiwa, kati ya Julai Mosi, 2018 na Novemba 31, 2018 katika maeneo mbalimbali washtakiwa hao walijihusisha moja kwa moja na muamala unaohusu madini hayo ya dhahabu wakati wakijua kuwa dhahabu hiyo imetokana  na kosa tangulizi la wizi.

Hata hivyo, washitakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakani hapo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 29, mwaka huu kwa kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande kwani mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ama kuwapatia dhamana.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA 16 WA KIMATAIFA WA ELIMU MKOANI TANGA

0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kwenye Ufunguzi huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha kumbukumbu Sabastian Kolowa  kanda ya Afrika Bishop Dkt. Stephen  Munga wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kwenye Ufunguzi huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa walipokutana kwenye Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kwenye Ufunguzi huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe.



 Baadhi ya washiriki wa  Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE)wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga. .  Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Baadhi ya Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo.  Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe.

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI MWANZA, AZUNGUMZA NA WANANCHI

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mwanza mjini mara baada ya kuwasili akitokea mkoani Geita. PICHA NA IKULU

Majaji wa shindano la East Africa Got Talent watangazwa leo ofisi ya Coca Cola jijini Nairobi.

0
0

  Jopo la majaji hao linamjumuisha Jeff Koinange, ambaye ni maarufu zaidi katika vyombo vya habari nchini Kenya ambaye pia amefanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari Duniani.

Mwingine ni Gaetano Kagwa, mwigizaji wa Uganda na mtangazaji ambaye amejizolea umaarufu mkubwa zaidi katika eneo hilo ambaye pia anatangaza katika kituo cha Capital FM, akiongoza kipindi cha Tusker Project Fame na alikuwa mshiriki wa Big Brother Africa.

Jaji mwingine ni Vanessa Mdee, mwimbaji wa Kitanzania na mtunzi wa nyimbo na Mtanzania wa kwanza MTV VJ, mwenyeji wa Epic Bongo Star Search na pia alishiriki kwenye shoo ya runinga ya Coke Studio Africa 2019 kati ya nyota wengine wa muziki wa Afrika.

Pia yumo Makeda Mahadeo aliyebobea katika vyombo vya habari nchini Rwanda na DJ wa kwanza wa kike nchini Rwanda.

Majaji watakuwa na jukumu muhimu katika kuidhinisha washiriki ambao wanatakiwa kuendelea kwa hatua inayofuata mwishoni mwa kila hatua na kutoa maoni au kukosoa juu ya waliyoshuhudia jukwaani. Washiriki wataondolewa ikiwa hawapati kura nyingi kutoka kwa majaji wanne.

Hii ni shoo ambayo itakuwa kinyumbani zaidi kufuatana na soko ambapo itatangazwa katika nchi nne za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Tanzania, Uganda na Rwanda. Vyombo vya habari vishiriki vitakuwa ni Citizen TV, Clouds Tv, NBS na RTV.

Kampuni ya Coca-Cola pia itakuwa na jukumu la kutoa huduma mbalimbali zikiwemo ushauri wa ushiriki wa fursa katika kanda nne zilizoshiriki.

"Mfumo wa Coca-Cola unaamini kusaidia sekta ya ubunifu nchini na kutoa jukwaa ambapo watu wanaweza kuonyesha na kuendeleza vipaji vyao katika kanda. Tunaamini kwamba majaji waliochaguliwa wana uwezo wa kuchagua vipaji bora kwa wasikilizaji wetu wa Afrika Mashariki, ili waweze kufahamu na kufurahia shoo, "alisema Beatrice Nyamari, Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano wa Coca-Cola Kanda ya Biashara Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEABU).

Wanajiunga na Safaricom PLC ambao ni wadhamini wa shoo hiyo Kenya na moja wa wafadhili wa Afrika Mashariki kupitia huduma yao ya M-PESA; na Challenge Access, ambayo inaongoza Kampeni ya Moja kwa Moja, kwa msaada wa Programu ya Huduma za Afya Duniani na Mpango wa UHC wa Kenya, Afya Care.

"Afrika ya Mashariki ina vipaji vya kuonyesha ambavyo vinatoa fursa kwa Waafrika Mashariki kuonyeshea talanta zao na kampuni yetu inaamini katika kutoa majukwaa ya watu kustawi, tunafurahi sana kuwa sehemu ya shoo,"alisema Sitoyo Lopokoiyit, Afisa Mkuu wa Huduma za Fedha, Safaricom.

Jukwaa hilo litaonyesha vipaji mbalimbali kutoka kwa watu wote wa umri tofauti wa Afrika Mashariki, na litajumuisha vipaji vinavyotokana na kuimba, kucheza, maigizo na aina nyingine nyingi za vipaji.

"Sisi tunafarijika kuleta msisimuko huu wa kidunia nyumbani. Tunaamini kuwa jukwaa hili litaamua wafuatiliaji wa kimataifa kwa vipaji vya kipekee vya Afrika Mashariki, "alisema Joseph Kusaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media International na mmiliki wa Franchise.

Majaji wanne watakuwa na vitufe vyao vyekundu ambavyo vinaweza tu kubonyezwa mara moja, pale jaji anapoona imetosha na inapotokea wakati mmoja, vikabonyezwa vyote basi kinachoendelea itapasa kisitishwe.

Kila mshiriki anahitaji kupokea idhini tatu kutoka kwa majaji kwenda kwenye duru ijayo.

Kutokana na kuanzia mwezi wa Agosti mwaka huu, kuonyesha EAGT itakuwa na vipindi 10, pamoja na nusu fainali na finali kubwa kuishi eneo moja nchini Kenya. Mshindi wa shooo atajinyakulia fedha za Kenya milioni tano (dola 50,000) kwa kupigiwa kura na watazamaji, ambayo itamuwezesha kuingia ubia wa kufanya kazi muda mrefu na mafunzo ya ujasiriamali.

Vipindi vitahaririwa katika vipengele sita ambavyo vitaanza kurushwa kuanzia Jumapili ya Agosti 4 saa mbili usiku (saa moja usiku Rwanda) katika sehemu zote nne za ukanda.
Meneja Mwandamizi wa Chapa ya Coca-Cola nchini Tanzania, Kabula Nshimo (kushoto) akitambulishwa na mshereheshaji rasmi wa mashindano makubwa ya kuibua vipaji kwa ukanda wa Afrika Mashariki (East Africa’s Got Talent) Anne Kansime wakati hafla ya kuwatambulisha majaji wa mashindano hayo iliyofanyika katika makao makuu ya Coca-Cola jijini Nairobi hivi karibuni.


Meneja Mwandamizi wa chapa ya Coca-Cola nchini Tanzania, Kabula Nshimo akizungumza kuhusu ushirikiano baina ya Coca-Cola na mashindano makubwa ya kuibua vipaji kwa ukanda wa Afrika Mashariki ya East Africa’s Got Talent kwa Tanzania wakati wa hafla ya kuwatambulisha majaji wa mashindano hayo iliyofanyika katika makao makuu ya Coca-Cola jijini Nairobi hivi karibuni.

Vijiji Vyote Nchini Kufikiwa na Umeme Ifikapo Juni 2021 No views

AMDT YAWAJENGEA UWEZO WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Biashara Oliver Vengula akizungumza na wakuu wa wilaya, wakurugenzi na maafisa biashara wa mikoa ya Singida na Manyara juu ya mwongozo mpya wa uendeshaji wa Mabaraza ya biashara, wakati wa warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo watendaji hao iliyokuwa imeandaliwa na taasisi ya kuendeleza mifumo ya masoko ya kilimo nchini – AMDT. 
Mkuu wa Wilaya ya Babati Bi. Elizabeth Kitundu akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wa namna ya kuendesha Mabaraza ya Biashara watendaji wa sekta ya umma kutoka mikoa ya Manyara na Singida. 

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara mhandisi Zephania Chaula akitoa uzoefu wa utendaji wa mabaraza ya biashara katika wilaya yake wakati wa warsha hiyo.
Mwezeshaji wa Warsha hiyo Dr Donath Ollomi akifafanua mbinu mbalimbali za uendeshaji mabaraza ya biashara na namna mabaraza yanavyoweza kutumika kama majukwaa ya majadiliano baina ya sekta ya umma na sekta binafsi. 
Bi Tertula Swai – Mtaalamu wa Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara wa AMDT, akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo. 
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bwana Joseph Mkirikiti akisisitiza jambo kwa watendaji wenzake wakati wa warsha hiyo, ambapo alisisitiza kwa viongozi wenzake kuisaidia serikali ya awamu ya tano kuweza kutekeleza ahadi zake na hasa kwa kuweka mazingira bora na Rafiki ya kibiashara katika maeneo yao
Baadhi ya Washiriki wa mkutano h uo wakichangia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa.
Washiriki wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano huo.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV.

Manyara. 

Proramu ya kuendeleza mifumo ya Masoko katika Kilimo (AMDT) imeanza kuwajengea uwezo viongozi mbalimbali wa ngazi za Wilaya na Mikoa ili kuongeza chachu ya kufanya mijadala baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi,lengo likiwa ni uboreshaji wa mazingira ya ufanyaji Biashara katika maeneo yao.

Hatua hii inakuja ikiwa takribani mwezi mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli azitake serikali za mitaa kutilia mkazo mabaraza ya Biashara kwenye maeneo yao.

Katika mkutano uliofanyika wilaya ya Babati mkaoni Manyara na kuwakutanisha Wakuu wa wilaya ,Wakurugenzi wa Halmashauri,Wenyeviti wa Mabaraza ya Biashara kutoka wilaya za Mikoa ya Singida na Manyara ,Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akaziasa Vyombo vinavyotunga sheria kuwashirikisha wadau kutoka sekta Binafsi

Akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Mkuu huyo wa Mkoa ,Mkuu wa Wilaya ya Babati Bi Elizabeth Kitundu ,Mnyeti alisema ipo haja kwa mamlaka zinazosimamia utungaji wa Sheria katika ngazi za wilaya, miji na majiji kuhakikisha zinawashirikisha wadau muhimu, hususani kupitia mabaraza ya biashara.

“ Tunayochangamoto kubwa sana ya fursa ya ajira, kati ya wahitimu zaidi ya laki nane wanaohitimu kila mwaka ni asilimia kumi tu ndio hupata ajira, hivyo tunalojukumu kuhakikisha kupitia mabaraza ya biashara tunatengeneza fursa nyingi ili kundi hili liweze kujiajiri ” alisema Mnyeti. 

Mnyeti ameongeza kuwa licha ya hali ya uchumi nchini kuimalika,bado kumekuwepo na tofauti kubwa sana ya kipato kati ya kundi la masikini na wale waliojaliwa kupata kipato . 

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Hanang Joseph Mkirikiti alisema ili ndoto na matamanio ya serikali ya awamu ya tano iweze kutimia ni lazima watendaji wa serikali na hususani katika ngazi za wilaya kutekeleza wajibu wao kwa kuhakikisha wanamsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli. 

“ Inasikitisha sana wengi wetu hatufanyi vile Mh. Rais anavyotaka tufanye na badala yake tumekuwa watu wa matamko tu na kuweka mbele vyeo vyetu hali ambayo imezorotesha mahusiano yetu na sekta binafsi” Alisema Mkirikiti. 

Mkirikiti ameongeza kuwa ni jambo la ajabu na kusikitisha pale matatizo ambayo yangeweza kutatuliwa katika ngazi ya wilaya yanamfikia kiongozi Mkuu wa nchi kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi. 

“Hii siyo sawa…tunaowajibu kuhakikisha mazingira mazuri ya biashara yanakuwepo katika maeneo yetu,…nitoe rai kwa wakuu wenzangu wa wilaya tukitoka hapa tubadilike na tumsaidie mheshimiwa Rais katika kuhakikisha anawapatia watanzania maendeleo. Aliongeza Mkirikiti. 

Naye Naibu Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa, Bi. Oliver Vengula alisema kwa sasa baraza hilo limetoa mwongozo mpya ambao ndio utakaokuwa ukitumika katika kuendesha mabaraza.  

“Majuzi tumemuona mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaita wafanyabiashara kutoka wilaya zote hapa nchini kwa ajili ya kujadiliana nao namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara, na kama mtakuwa mmegundua sehemu kubwa ya mambo yaliyojadiliwa au kulalamikiwa mengi yanatuhusu sisi watendaji wa huku chini, hatukutekeleza wajibu wetu…..,tubadilike sasa na tuanze kuyatumia mabaraza ya biashara kumaliza kero mbalimbali.Alisema Bi.Vengula 
Waandaaji wa mkutano huo ambao ni Programu ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo nchini (AMDT) kupitia Mwenyekiti wake wa Kamati ya Ufundi Mike Laizer walisema malengo ya warsha hiyo yalikuwa kuwajengea uwezo watendaji hao wa sekta ya umma pamoja kutambua vikwazo vinavyoikabili sekta ya umma katika kutekeleza majukumu yake. 

“AMDT imelenga kuboresha mifumo mbalimbali ya kimasoko ili iweze kumsaidia mkulima na hususani mkulima wa mazao ya alizeti, mahindi na mikunde,Tumelenga kuwa na mazingira wezeshi kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa kuwa na mazingira rafiki ya kibiashara baina ya pande husika," alisema Laizer 

Akizungumza kuhusiana na mpango huo, Mtaalamu wa kuendeleza Mifumo ya Masoko wa AMDT, Bi Tertula Swai amesema mpango wa kuwakutanisha watendaji hao wakuu kutoka katika wilaya tofauti hapa nchini umelenga kuwajengea uwezo na kuweka mifumo endelevu ya mabaraza ya biashara katika kutatua kero mbalimbali. 

"Tunataka kuona kupitia mifumo tunayoiweka sasa mabaraza haya ya biashara yanakuwa endelevu na utendaji wake unakuwa wenye ufanisi hata baada ya kuisha kwa mradi wa AMDT.” alisema Bi Swai

JWTZ yasaini Mkataba na Chuo cha Uhasibu Arusha

0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ)kupitia chuo cha Mafunzo ya kijeshi TMA kilichopo wilayani Monduli mkoani Arusha , kimetiliana saini mkataba wa pili wa Makubaliano ya kutoa Mafunzo ya Elimu ya Shahada ya Sayansi ya kijeshi na chuo cha uhasibu (IAA) cha jijini Arusha yatakayofanyika kwa miaka Mitatu.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mikataba ya Makubalino Mbele ya Waandishi wa habari ambayo yamefanyika katika chuo hicho ,mkuu wa chuo cha Uhasibu ,Njiro prof,Eliamani Sedoyeka amesema kuwa ushirikiano huo kati ya TMA na IAA ni malengo ya muda mrefu katika kuongeza ubora wa elimu kwa jeshi ili kwendana na sera ya serikali kuweza kufikia malengo ya uchumi wa viwanda hapa nchini

Alisema mkataba wa kwanza wa uashirikiano ulisainiwa desemba mwaka 2015 na Novemba 20,2017 walizindua rasimi shahada ya sayansi ya Kijeshi(Bachelor of Military Science).

Aidha amesema kuwa hadi sasa shahada hiyo ina jumla ya wanafunzi, wanajeshi wapatao 208 wanaosoma chuoni hapo huku akiahidi chuo hicho kuwapatia elimu iliyo bora kwa maendeleo ya nchi na kuhakikisha jeshi la wananchi linapata elimu bora inayoendana na mtizamo wa rais John Magufuli katika ukuaji wa technolojia na hatimaye kujenga jeshi lenye nguvu 

"Ushirikiano huu umekiweka chuo katika hali nzuri na kwamba na tunaahidi kutoa elimu bora kwa jeshi letu na pia kuongeza Nyanja nyingine za ushirikiano zaidi na vyuo vingine" Amesema Frof.Sedoyeka

Alisema Chuo cha uhasibu Arusha,Kinatoa kozi mbalimbali kwa ngaIbza cheti,Stashahada(Diploma),Shahada (Degree), Shahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) na shahada ya Uzamili(Masters) katika maaomo UA Uhasibu, Manunuzi na Ugavi,Benki na Fedha ,Uchumi,Uwekezaji,Biashara,Sayansi ya Kompyuta na teknolojia ya Habari.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli(TMA) ,Brigedia Jenerali ,Stephen Mnkande amekishukuru chuo cha uhasibu Arusha kwa ushirikiano mkubwa waliyouonyesha kwa kuwa amelenga kuandaa mahusiano mazuri baina ya jeshi hilo na chuo cha uhasibu katika nyanja ya Elimu ya juu.

Makubaliano hayo yanahitinisha mchakato wa makubaliano hayo ambayo tayari yamesasainiwa tangu Julai 9 mwaka huu 2019 na kwamba tukio hilo lilizikutanisha tasisi hizo mbili chuo cha kijeshi ,Monduli na chuo cha uhasibu Njiro kwa lengo la kudumisha mahusiano kwa mustakabari wa mahusiano mapana ya Taifa la Tanzania.
Picha ikionyesha mkuu wa chuo cha Uhasibu ,Njiro prof,Eliamani Sedoyeka pamoja na mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli(TMA) ,Brigedia Jenerali ,Stephen Mnkande wakikabidhiana mikataba waliosaini hafla fupi ya makabidhiano ya mikataba ya Makubalino hayo.

MWENYEKITI WA KITONGOJI CHA NYAKAHAMBA HUKO KEREGE AONDOKA NA KITONGOJI CHAKE KUKIMBILIA CCM

0
0
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ,Kitongoji cha Nyakahamba ,kata ya Kerege Frenk Masihaga na wakazi wengine 300 wa kitongoji hicho wamekihama chama hicho na kurudi CCM ,ili kuunga mkono juhudi za serikali na maendeleo yanayoletwa kwa kasi na Rais dk.John Magufuli.

Akipokea wanachama hao ,katika ziara yake ya kufanya vikao vya ndani kukosoana na kuwekana sawa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa,vitongoji ,huko Kerege Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bagamoyo,Alhaj Abdul Sharif alisema, wamerejea CCM wakati muafaka.

"Hamjafanya makosa kurudi kwa Chama dume ,ila mkafanye kazi ya CCM Nyakahamba kuhakikisha CCM inarudi madrakani na kukikomboa kitongoji hicho"alisema alhaj Sharif.

Hata hivyo alieleza, wanachama waonyeshe ushirikiano ,waondoe makundi na kukisemea Chama na serikali kwa yale yanayofanyika.

Sharif alielezea kwamba, mkakati uliopo kiwilaya ni kujipanga kushinda uchaguzi nafasi zote na ndio maana yupo katika ziara ya vikao vya ndani kurekebishana wenyewe na kurejesha wanachama ndani ya chama kwani mtaji wa chama ni kuongeza wanachama.

Alifafanua ziara yake imezaa matunda tayari kwa maeneo ambayo ameshapita ikiwemo Kibindu wapinzani 200 wamerudi CCM akiwemo mwenyekiti na diwani waliogombea uchaguzi uliopita.Kata ya Talawanda wapinzani wawili,Mandela wanne akiwemo aloyegombea udiwani uchaguzi mkuu uliopita na kata ya Mkange watano.

Sharif alielezea,ni wajibu wa kila kiongozi wa shina,tawi,kijiji,kitongoji na kata kusimama imara ,kujipanga ili kupambana CCM iweze kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji 2019 na uchaguzi mkuu ujao 2020.

Awali mwenyekiti wa kitongoji cha Nyakahamba Masihaga alisema, kitongoji hicho kina wakazi 420 ambapo ameondoka na wakazi 300 .


 


CCM ARUSHA YAENDELEA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha 

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha wameitikia Wito wa kuhudhuria Kikao cha ndani kilichoandaliwa na Wazee wa Mila ya Kimasai kwa kushirikiana Mahususi Kwa Kusikiliza Mgogoro uliopo Kati ya Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Manongi na Wananchi wanaoishi Katika Hifadhi hiyo. 

Wazee hao wakiwakilisha Makundi mbalimbali ya Wafugaji, Wanawake, Watumishi walioachishwa Kazi Katika Hifadhi hiyo walilalamikia Kwa vilio na Masikitiko Makubwa Kutokana na Unyanyasi Mkubwa Kutoka Kwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Manongi.

Wananchi hao walilalamikia mbalimbali yakiwemo Kuharasiwa Kila kukicha na askari usu wa Hifadhi hiyo ya Ngorongoro tofauti na ilivyokuwa huko nyuma miaka zaidi ya Kumi iliyopita pia walisema jambo lingine linalowakera ni pamoja na Ardhi yao Kuendelea kumegwa na Hifadhi ya Ngorongoro ambapo walisema hawashirikishwi Katika Matumizi mbalimbali ya Ardhi Katika Maeneo wanayoishi.

Aidha walilalamikia kitendo Kunyimwa Kujiletea Maendeleo na huduma Muhimu Kwa Kujenga Shule, Kanisa na Zahanati huku wakibainisha kuwa walijitoa Kwa nguvu zao ili Kujenga Shule Kwa ajili ya watoto wao lakini badala yake juhudi hizo zimezuiliwa na kuwekwa katazo kabisa la kutojengwa shule, zahanati, Kanisa na hata Majengo ya nyumba za asili Au Kudumu za kuishi.

"Katika Maeneo tunayoishi wananchi tuna Changamoto ya Usafiri hivyo hulazimika Kutumia Usafiri wa Pikipiki (bodaboda) ili kufikia huduma muhimu za afya pindi akina Mama wajawazito na wagonjwa wanakwenda kutafuta huduma ,sisi Wananchi tumezuiliwa Matumizi ya Bodaboda ,Pikipiki na magari binafsi na Mwananchi yeyote atakayeonekana anatumia Pikipiki anakamatwa na kupigwa, kuwekwa ndani na Kunyanganywa Pikipiki yake ,Ikumbukwe Mwaka 2017 ulitokea mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu ambapo Usafiri wa Pikipiki ulitumika kuokoa Maisha ya ndugu zao"alisema mengori laizer

Aidha Wakinamama walilalamikia kuzuiwa kuchota maji Katika mto unaopita Katika Maeneo wanaoishi Kwa ajili ya Matumizi Kibinadamu na kunyweshea mifugo yao. 

Walisema kuwa Menejimenti ya Hifadhi ya Ngorongoro imeshidwa Kushindwa kuiongoza na kuisimamia vizuri Hifadhi hiyo kwani Ndugu Manongi ametafutwa na kuombwa mara nyingi mno ili kukaa pamoja Kwa ajili kutatua changamoto mbalimbali na kuweka namna nzuri ya Mambo kadha wa Kadha lakini Wananchi hao wamesema Rais Magufuli anapatikana wakati wote na Ndugu Manongi yuko busy siku zote. 

Wananchi hao wamewaomba viongozi hao wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha waliofika Kusikiliza kero zao kuzifikisha kwa Rais Magufuli ambaye wamesema pamoja na upepo wa Uchaguzi wa Mwaka 2015 lakini Ngorongoro waliendelea kuwa waaminifu kwa kukichagua Chama cha Mapinduzi akiwemo yeye Rais Magufuli, Mbunge wao na hakukuwa na Kata hata moja iliyobebwa na Wapinzani na Kwamba wanamfahamu vizuri Rais Magufuli ni Rais wa Wanyonge hivyo wameomba sasa Serikali itamke kitu juu ya Changamoto zao ambazo kiukweli imekuwa ni tatizo. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Comrade Loata Sanare alisema kuwa wamesikia changamoto zao na waliwahaidi kuzifanyia kazi kero hizo zote na changamoto zote ambazo zinawakabili.

"napenda kuwahaidi kuwa changamoto zenu zote tumezikia na sisi kama viongozi wa ccm chama ambacho kinashika dola tunawahaidi kuzifanyia kazi kero zenu zote ambazo mmezitaja "alisema Loata 

Katika kikao hicho mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha alifuatana na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Musa Dadi Matoroka, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa anayewakilisha Mkoa wa Arusha Comrade Daniel Awaki, Robert Kaseko Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, Olemoko Moloimet Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, Yasmin Bachu - Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi ( UWT) Mkoa wa Arusha, Neema Mollel ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Arusha Ally Baro.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Comrade Loata Sanare akiongea na Wazee wakiwakilisha Makundi mbalimbali ya Wafugaji, Wanawake, Watumishi walioachishwa Kazi Katika Hifadhi ya Ngorongoro

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA 16 WA KIMATAIFA SEKOMU MKOANI TANGA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa walipokutana kwenye Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kwenye Ufunguzi huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE)wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga. . Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Baadhi ya Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha kumbukumbu Sabastian Kolowa kanda ya Afrika Bishop Dkt. Stephen Munga wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu (International Association of Special Education (IASE) leo Julai 15,2019 katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kwenye Ufunguzi huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe.

PAMBA YOTE KUNUNULIWA –WAZIRI MKUU

0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mikokoteni iliyosheheni pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Msingi cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga alikofanya ziara ya siku moja ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao hilo, Julai 15, 2019. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
………………. 
NA TIGANYA VINCENT 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imelipatia ufumbuzi tatizo la kusuasua kwa masoko ya pamba nchini baada ya kufanya mazungumzo na wadau muhimu wa zao hilo na kufikia muafaka. 

Lengo ni kutaka kuhakikisha pamba yote inanunuliwa ifikapo mwaka mwishoni mwa Mwezi huu na wakulima wanalipwa pesa zao zote. 

Ameyasema hayo leo (Jumatatu 15, 2019) wakati akizungumza na wakulima wa pamba katika Kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga . 

Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imeshafanya mazungumzo na Benki Kuu na Benki mbalimbali ili ziweze kuzikopesha Kampuni mbalimbali za ununuzi wa pamba ili zihakikishe zinanunua pamba yote ya wakulima nchini. Alisema wamefanya mazungumzo na wanunuzi wa pamba,Wakuu wa Mikoa inayolima pamba,viongozi wa mabenki na Gavana wa Benki kuu na kufikia makubaliano. 

Waziri Mkuu alisema wanunuzi walishindwa kununua pamba yote kwa pesa zao kwa vile hawakuweza kukopeshwa na benki ambayo nayo hayakuhakikishiwa dhamana na Benki kuu. Alisema baada ya mazungumzo wamekubaliana Benki kuu ya Tanzania kuanza kutoa dhamana kwa benki ambayo nazo zitatakiwa kutoa mikopo kwa wanunuzi wa pamba. 

Alibainisha makubaliano hayo sasa yanafungua mlango wa wanunuzi kununua pamba yote ya wakulima tena kwa pesa taslimu na sio mkopo. Aidha Waziri Mkuu,aliwaonya wanunuzi kutotumia pesa wanayopata kufanya mambo tofauti na badala yake waitumie kununulia pamba pekee. 

Waziri Mkuu aliwapongeza wakulima kwa kuzalisha na kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka tani 135,000 mwaka 2017,mwaka 2018 tani 220,000 na mwaka huu wanatarajia kupatikana tani zaidi ya 300,000. Kwa upande wa Waziri wa Kilimo,Japhet Hasunga alisema uzalishaji wa pamba msimu huu unaweza kuongezeka hadi kufikia tani kati ya 300,000 hadi 350,000. 

Aidha alisema maghala mengi ya pamba hayana ubora na kwamba wanafanya jitihada kuhakikisha yanakuwa na ubora sio kama ilivyo sasa. 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Aggrey Mwanri,alisema wamefanikiwa kuwafanya wakulima walime kwa tija kwa kuongeza uzalishaji kwa kilo kutoka kilo 300 hadi 800 kwa ekari. 

Awali Mkuu wa Wilaya ya Igunga,John Mwaipopo,alisema wakulima walikuwa bado hawajapeleka pamba zikiwa bado majumbani huku wale waliopeleka ghalani,kuwa bado hawajalipwa. Mbunge wa jimbo la Manonga,Seif Gulamali alisema kuwa wakulima wana hali mbaya kutokana na kutouza pamba yao na hivyo kushindwa kufanya mambo ya msingi kama kujikimu kwa chakula na gharama zingine za maisha. 

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewashauri wakulima wa mazao mbalimbali hapa nchini kujenga utaratibu wa kuweka mipango mizuri ya kujiandaa ya kilimo kijacho kwa kuweka akiba kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo. 

Alisema Serikali haiwezi kutoa pembejeo kwa kila zao la Mkulima hapa nchini badala yake ni jukumu la wakulima kujenga utaratibu wa kujiwekea akiba kwa ajili ya uboresahaji wa kilimo kijacho

Waziri Jafo akagua ujenzi wa Hospitali ya Uhuru, kukamilika Januari 2020

0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mhe Suleiman Jafo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ziara maalum ya kukagua ujenzi wa Hospital ya Uhuru inayojengwa kwa maelekezo ya Mhe Rais Dk John Magufuli katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma. 
Mhandisi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Daniel Mwakasungura,akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mpango wa ujenzi wa Hospitali hiyo ya Uhuru iliyopo Chamwino,Mkoani Dodoma. 
Mhandisi wa Suma JKT, Luteni Kanali Onesmo Njau,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambao wamepewa jukumu la kujenga Hospitali hiyo.
Sehemu ya eneo ambapo ujenzi wa Hospitali ya Uhuru .

Na Charles James, Michuzi TV

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mhe Suleiman Jafo amefanya ziara maalum ya kukagua ujenzi wa Hospital ya Uhuru inayojengwa kwa maelekezo ya Mhe Rais Dk John Magufuli katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Hospitali hiyo inajengwa baada ya Rais Magufuli kuelekeza kufanya hivyo katika sherehe za Uhuru mwaka 2018 ambapo alifuta sherehe hizo na kupeleka Fedha zilizokua zimetingwa kwa ajili ya sherehe hizo kujenga Hospitali mkoani Dodoma.

" Nishukuru leo kwa kufanya ziara hii maalumu ya kukagua ujenzi wa Hospitali hii ambayo ni malekezo kutoka kwa Mhe Rais, lakini pia hata hivyo baada ya gawio la Serikali kutoka Kampuni ya Airtel Mhe Rais alielekeza Fedha hizo kuletwa kwenye mradi wa ujenzi wa Hospitali hii ya Uhuru.

" Na kama mnavyokumbuka nilikuja siku za nyuma Juni 19 kukagua lakini sikuridhishwa baada ya kukuta ujenzi haujaanza ndio maana nimetoa maelekezo kwamba ujenzi uanze mara moja kwa kutumia vikosi vya Jeshi ili kutimiza azma ya Mhe Rais katika kutoa huduma za Afya kwa wananchi, na tayari wenzetu wa Suma JKT wameshaanza kazi hii," amesema Mhe Jafo.

Amesema tayari eneo lote la Ekari 40 limeshasafishwa ikiwemo kujenga uzio pamoja na ofisi kuleta vifaa vya ujenzi huku pia akieleza kwamba TBA wataendelea kusimamia suala la ramani na kutoa ushauri wa mradi huo na wataendelea kutumia utaratibu wa 'false acount' kutokana na kuwapatia mafanikio katika kufanikisha kazi za Serikali za Mitaa.

" Kwa kweli leo nimeridhishwa na hatua ya awali ambayo tumefikia katika ujenzi wa Hospitali hii, na niwaombe wataalamu wangu kuacha kufanya kazi kwa mazoea na tunapotoa maagizo basi wayatekeleze kwa wakati, lakini ni matarijio yetu hadi kufikia Januari, 2020 tutakua tumeshamaliza ujenzi huu," amesema Mhe Jafo.

Kwa upande wake Mhandisi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania TBA, Daniel Mwakasungura amesema Hospital hiyo ya Uhuru itakuwa ni ya Ngazi ya Wilaya ambapo kwa agizo la Mhe Rais awamu ya kwanza ni kujenga majengo ya wagonjwa wa nje ikiwemo huduma za maabara na Kliniki ya Mama na Mtoto.

" Hela iliyotengwa ambayo Tumeingia mkataba na Suma JKT ni Shilingi Bilioni 3 ambazo zitajenga hivyo nilivyovitaja na tunatarajia kukamilisha mradi huu baada ya miezi sita kama ambavyo tuliekezwa," amesema Mwakasungura.

Nae Mhandisi wa Suma JKT, Luteni Kanali Onesmo Njau amesema walikabidhiwa jukumu la ujenzi huo Juni 19 mwaka huu na tayari washatekeleza maelekezo kutoka kwa Mhe Jafo ikiwemo kuandaa ofisi, sehemu za kuishi kwa watendaji na muda sio mrefu wataanza ujenzi ili kukamilisha mapema kama ilivyoelekezwa.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images