Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

DKT. NDUGULILE AONEKANA KUTORIDHISHWA NA UTAYARI WA MKOA WA KIGOMA KATIKA KUKABILIANA NA EBOLA

$
0
0
Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile akikagua dawa na vifaa vinavyotumika katika kutibu mgonjwa wa Ebola, kulia ni Dkt. Praygod Swai wa Zahanati ya Bangwe iliyotengwa maalum kwa ajili ya kutibu wagonjwa wa Ebola akimuonesha vifaa hivyo. Hema lilotengwa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa Ebola katika bandari ndogo ya Kibirizi ikiyoko mkoani Kigoma.Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akipimwa joto la mwili na mhudumu wa uwanja wa ndege mara baada ya kufika katika mkoa wa Kigoma ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akimpima joto la mwili mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw. Samson Anga wakati alipotembelea bandari ya Kigoma kuona hali ya utayari wa mkoa huo katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akioneshwa vifaa vya kujikinga na Ebola kutoka kwa mhudumu wa afya wa bandari ndogo ya Kibirizi Mkoani Kigoma wakati wa ziara yake mkoani humo kuangalia utayari wa mkoa katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile (Kulia) akitoa maelekezo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Paul Chaote jinsi ya kuweka vifaa na kupangiliana hema (Isolation centre) kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga. 
…………………….. 
Na WAJMW-Kigoma 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo ametembelea baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kigoma kuona utayari wa mkoa huo katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola. 
Dkt. Ndugulile ametembelea maeneo ya Bandari kuu ya Mkoa, Uwanja wa ndege, bandari ndogo ya Kibirizi na Zahanati ya Bangwe ambayo imetengwa maalumu kwa ajili ya kutoa matibabu kwa mtu atakayebainika kuwa na virusi vya Ebola. 

Naibu Waziri ameonekana kutoridhishwa na utayari wa Mkoa katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini huku akiitaka timu iliyoandaliwa chini ya Mkuu wa Wilaya Samson Anga na Mganga Mkuu wa Mkoa Paul Chaote kuendelea kutoa mafunzo kwa timu iliyoandaliwa jinsi ya kujikinga na kutoa huduma kwa mgonjwa atakayebainika. 

“Hatuna mgonjwa wa Ebola ndani ya nchi, lakini kutokana na hali ya ugonjwa huu katika nchi jirani kuna umuhimu wa sisi kama nchi kuendelea kujipanga na kuhakikisha kwamba mifumo yetu yote imekaa vizuri kipindi mgonjwa atakapojitokeza, hivyo nakuomba Mkuu wa Wilaya na Mganga Mkuu wa mkoa kuendelea kusimamia hili”. Amesema Dkt. Ndugulile. 

Mapungufu aliyobaini Dkt. Ndugulile ni pamoja na wahudumu kutozingatia kanuni walizofunzwa juu ya kujikinga na maambukizi pindi watakapokua wakihudumia mgonjwa, kutokua na vifaa vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola kama vitanda kwenye vituo vya Isolation na watumishi kutokua na uelewa na utayari wa kutosha kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huu. 

Dkt. Ndugulile yupo Mkoani Kigoma kwa ziara ya siku tatu ambapo pamoja na maeneo mengine atatembelea mpaka wa Manyovu ili kuona hali ya utayari ya mpaka huo kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola na kisha atatembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma.

ZIARA YA MAFUNZO 5S-KAIZEN KWA WAGENI KUTOKA WIZARA YA AFYA NA WATUMISHI WA BANGLADESH

$
0
0
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mradi wa Kuimarisha Hospitali za Rufaa za Mikoa (RRHMP) katika kuendelea kuziwezesha Hospitali za Rufaa za Mikoa ilipanga kukaribisha wageni kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika ili kubadilishana uwezo katika utekelezaji wa 5S-KAIZEN katika kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.

Kulingana na mpango kazi wa mwaka huu, Mradi ukishirikiana na Wizara ya Afya ulitarajia kupokea wageni kutoka Wizara ya Afya na watumishi wa sekta hiyo kutoka nchini Ghana na Bangladesh kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya Falsafa ya 5S-KAIZEN-TQM. Pamoja na hao, tulitegemea kupokea watumishi wa Afya 14 kutoka nchi za kiafrika zikiwemo Uganda, Kenya, Malawi, Liberia, Siera Leoni, Sudan, Zambia, Zimbabwe, Benin. 

Tayari wageni wote hawa waliishafika na kupata mafunzo kutoka haya. 

Wiki hii, tumewapokea wageni kutoka Katika Wizara ya Afya na watumishi wa sekta saba na wawakilishi wawili wa JICA-Ghana hiyo kutoka nchini Bangladesh. Wageni hawa watakuwepo hapa nchini kwa wiki moja Katika kipindi hicho watapata mafunzo ya KAIZEN na leo wametembelea Hospitali za Rufaa ya Mkoa Amana na kesho wanategemewa kutembelea Hospitali za Taifa Muhimbili.

Lengo la ziara hii ni kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa 5S-KAIZEN-TQM katika hospitali zetu kwa ajili ya kujifunza na kuiga mazuri ya kujifunza watakaporejea nchini kwao. Aidha, Timu zetu zinategemewa kupata nafasi ya kupata uzoefu kutoka kwa nchi zinazotutembelea. 

Falsafa ya 5S-KAIZEN-TQM hii inalenga kuboresha mazingira ya kutoa huduma za afya na kukidhi mahitaji ya wateja wetu, wale wa ndani na wa nje. 

Kwa ujumla wake, falsafa ya 5S-KAIZEN-TQM hii inarahisha kazi, inahakikisha usalama kwa wateja wa ndani na nje na inapunguza upotevu wa rasilimali, napunguza makosa na inapunguza gharama za uendeshaji.

Kwa Hospitali za Rufaa za Mikoa ambayo wanaitimia falsafa hii wameweza kufanya vizuri katika kutoa huduma bora, kuongeza katika mapato na wafanyakazi kufurahia mazingira yao ya kazi.Ni falsafa inayoweza kutumika katika maeneo mbalimbali pamoja na viwandani.
Mratibu wa Hospitali za Rufaa za Mikoa mutoka Wizara ya Afya Idara ya Tiba Kitengo cha Uratibu wa Hospitali za Rufaa za Mikoa,Dkt. Angelina Clarisa Sijaona (kulia) akiwa na wageni kutoka nchi ya Bangladesh akiwaonesha mambo mbalimbali yanayo tumika kwenye mfumo wa KAIZEN unatuka katika Hospital Amana leo jijini Dar es Salaam.
Muuguzi Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa Amana,Beauty Mwambebule (kulia) akitoa maelezo kwa wageni kutoka nchi ya Bangladesh namna mfumo wa KAIZEN unavyofanya kazi katika Hospital hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Wangeni kutoka nchi ya Bangladesh wakiwa katika Hospital ya Amana iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Picha ya pamoja.

Balozi wa Uingereza afanya ziara Muhimbili

$
0
0
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania amefanya ziara ya siku moja Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako amekagua vifaatiba vikiwamo vinavyotumika kutoa huduma kwa wagonjwa wa macho. Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke akiuliza jambo kuhusu matumizi ya Optical Coherence Tomography (OCT) inavyotumika kutambua magonjwa yaliopo kwenye pazia la macho (retina) kutoka kwa Dkt. Moin Mohamed wa Hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa MNH, Dkt. Sufiani Baruani wa MNH. Jana Shule ya Kwaya ya Westminister Cathedral ya nchini Uingereza kupitia Hospitali ya Mtakatifu Thomas iliyopo nchini humo ilitoa mashine ya OCT ili kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya macho nchini. 
Moja ya mashine inayotumika kutoa huduma ya magonjwa ya macho. 
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke aha akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa magonjwa ya macho wa MNH.

ETIENNE NDAYIRAGIJE AULA, AKABIDHIWA MIKOBA YA AMUNIKE

$
0
0
Kikao cha Kamati ya dharura cha Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambacho kimekutana leo,kimemtangaza Kocha Mkuu wa Azam Ndayiragije Etienne kuwa Kaimu Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.

Etienne,amependekeza benchi lake la ufundi kusaidiwa na kocha wa Coastal Union Juma Mgunda pamoja na kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania Suleiman Matola,ambapo uteuzi huo umezingatia programu maalumu ya kuendeleza makocha wazawa. 

Aliyekuwa kocha Mkuu wa Timu hiyo Emanuel Amunike alisitishiwa mkataba wake baada ya kukubaliana kwa pamoja na TFF mapema wiki hii.

Etieene ataiongoza Taifa stars kwenye mchezo wa kutafuta nafasi ya kucheza CHAN wakikabiliana na Kenya Harambee Stars kati ya Julai 24-28 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kwenye michuano ya Mataifa Afrika AFCON Taifa Stars walikuwa kundi moja na Kenya na katika mchezo wao wa hatua ya makundi Harambee Stars walishinda 3-2 na wote kuondolewa na Stars wakiambulia alama sifuri, Kenya alama 3.

Vijana Morogoro watuma salamu za pongezi na shukrani kwa Rais Magufuli

$
0
0
Na Charles James, Michuzi Tv

Vijana Wilayani Kilosa, Morogoro wamemshukuru na kumpongeza Rais Dk John Magufuli kwa hatua yake madhubuti ya kufuta hati ya mashamba makubwa yaliyokua yanamilikiwa na watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi.

Hayo yamesemwa leo mbele ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana Kazi na Ajira, Mhe Anthony Mavunde wakati wa mavuno ya mpunga katika shamba linalomilikiwa na Vijana wa Kampuni ya Agri-Ajira ambao ni wahitimu wa Chuo cha Kilimo Sokoine.

" Niwapongeze kwa uthubutu wenu na kazi kubwa mliyoifanya mpaka kufikia mafanikio makubwa, Kama Serikali tutawawezesha kimtaji kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo ili kupanua Kilimo chenu na kugawa ajira zaidi kwa Vijana, na kabla ya kuondoka hapa nimtake Afisa kutoka Benki ya Kilimo kutoondoka hapa bila kuweka sawa andiko la mkopo na mahitaji ya vijana hawa," amesema Mh Mavunde.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi amewahakikishia vijana wilayani hapo kuwa Serikali itaendelea kuwa bega kwa bega katika kuwapatia maeneo ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kuahidi kulifanyia kazi ombi la ekari 500 za ziada zilizoombwa na Kampuni hiyo ya vijana.

Awali wakisoma risala mbele ya Mhe Mavunde, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Charles Ibrahim ameishukuru Serikali ya Rais Magufuli kwa kuwapatia eneo la kilimo la ekari 50 ambapo pia amesema kama wataongezewa ekari 500 walizoomba basi wataongeza idadi ya ajira kutoka 200 kufikia 1000.

AFYA: WAZIRI UMMY AKUNWA NA UBUNIFU HOSPITALI YA RUFAA KANDA YA MBEYA

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ZANZIBAR ATEMBELEA BANDA LA NMB SABASABA

$
0
0
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar, Mheshiwa Hamis Hafidh Hassan (kushoto) akiwa ndani ya Banda la Benki ya NMB alipotembelea banda hilo kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba. Kulia ni Kaimu Meneja wa Banda la Benki ya NMB kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa, Bi. Saumu Mohamed Mollel akiwa na mgeni wake. 
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar, Mheshiwa Hamis Hafidh Hassan akisaini kitabu cha wageni ndani ya Banda la Benki ya NMB kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa.
Kaimu Meneja wa Banda la Benki ya NMB kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa, Bi. Saumu Mohamed Mollel (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar, Mheshiwa Hamis Hafidh Hassan alipotembelea Banda la NMB Sabasaba.
Wateja mbalimbali wa Benki ya NMB wakipata huduma ndani ya Banda la Benki hiyo walipotembelea Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba.

KILIMO CHA UMWAGILIAJI SULUHISHO LA MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0
Katikati Mwakilishi mkazi wa Shirika la kimataifa la maendeleo la Japan (JICA) nchini Bw. Nahofumi Yamamula , akiongea na katibu mkuu mstaafu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mbogo Futakamba (kushoto) baada ya mapumziko wakati wa kongamano la kushindanisha vyama vya umwagiliaji lilofanyika Jijini Dodoma, Kulia ni Bw.Yoichi Yamauchi Mshauri wa Mradi wa kuwajengea uwezo wakulima katika eneo la umwagiliaji.
Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mbogo Futakamba akitoa neno la kufunga kongamano lililoshindanisha vyama wa umwagiliaji jijini Dodoma.
Picha ikionyesha majaji wakati wa kongamano la siku mbili la kushindanisha vyama vya umwagiliaji lililofanyika jijini Dodoma.
Kiongozi wa skimu ya kilimo cha umwagiliaji cha Mkombilenga iliyopo Wilayani Iringa katika kanda ya Umwagiliaji ya Mbeya Bw. Bwana Fundi Mihayo kaipokea kikombe toka kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Hapa nchini Bw.Nahofumi Yamamula baada ya skimu hiyo kushika nafasi ya kwanza katika Kongamano kubwa la kushindanisha vyama vya umwagiliaji lilofanyika jijini Dodoma.


NA MWANDISHI MAALUM DODOMA

Kuwekeza katika kilimo cha Umwagiliaji kunaweza kuwa ni njia sahihi ya kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi. Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba alipokuwa akifunga kongamano ya Wakulima lililoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Mhandisi Futakamba alisema kuwa, Serikali imeweza kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika miundombinu ya Umwagiliaji na kuchukua jukumu kubwa la kutoa mafunzo ya matunzo ya miundombinu hiyo kwa wakulima, ili kuweza kukabiliana na athari na hasara zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi, “ ili kuweza kufikia lengo hili ni lazima serikali na wakulima kwenda pamoja ili kufanikisha, hali ambayo inaweza pia kusaidia wakulima nao kuingia zaidi katika kilimo cha biashara kama vile wakulima wa skimu ya Lemkuna na Pawaga, pamoja na kuwa na uhakika wa chakula nchini.” Alisema Mhandisi Mbogo.

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Marco Ndonde alisema Tume hiyo imejipanga kuboresha Miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya kilimo na mashirika mbalimbali ya maendeleo.” Sambamba na hilo Tume ina mpango wa kujenga mabwawa ili kufanya kilimo cha umwagiliaji kiwe na uhakika wa kupata maji ya kutosha pamoja na kufungua miradi ya kilimo hicho kitakachoajiri vijana kutoka vyuo vikuu nchini.” Alisisitiza Bw. Ndonde

Akiwasilisha mada katika siku ya mwisho ya kongamano lililoshindanisha vyama vya wamwagiliaji nchini, Bw. Fundi Mihayo kiongozi wa skimu ya umwagiliaji ya Mkombilenga iliyopo Mkoani Iringa amesema, Lengo la Serikali kuwezesha wakulima kuuza mchele badala ya kuuza mpunga katika maeneo ya skimu za kilimo cha umwagiliaji limefanikiwa kwa kisia kikubwa kwani kwa sasa skimu nyingi zimeweza kufunga mashine za kukoboa nafaka kama vile mpunga, na kupaki katika madaraja na ujazo tofauti.

“Haya yote ni manufaa ya tokanayo na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa Mafunzo kwa kushirikiana na serikali ya Japan kupitia shirika lake la JICA, jambo ambalo limepelekea wakulima kuwa na soko la uhakika la zao la Mpunga hasa baada ya serikali kuhamia Makao makuu ya nchi Dodoma wakulima wa skimu ya umwagiliaji Mkombilenga wamepata soko la uhakika Jijini Dodoma.” Alisema Bw. Mihayo.

Wakitoa mawasilisho kwa baadhi ya skimu za umwagiliai zilizopo katika kanda nane (8) za umwagiliaji nchini, wakulima wameonekana kutaja changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika skimu hizo ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa hitaji la kuongeza mifereji inayopeleka maji katika skimu hizo pamoja na kuisakafia na kuishauri Serikali kuendelea kutoa mafunzo kwa skimu zote ili wakulima wapate uelewa na kutunza skimu jambo ambalo linaweza kusaidia Serikali kufikia lengo la kuweza kuongeza kipato kwa wanachi na kuwepo kwa uhakika wa chakula.

Skimu ya umwagilijai ya Mkombilenga iliyopo katika kanda ya Mbeya imeibuka kidedea ikifuatiwa na skimu ya Lemkuna ya kanda ya Dodoma na skimu ya Nyida iliyopo katika kanda ya Mwanza kushika nafasi ya tatu katika mashindano hayo.

Kongamano hilo la siku mbili lilishirikisha wakulima, wataalam wa kilimo toka ngazi za Mikoa, Wilaya,Kanda za Umwagiliaji,Tamisemi na Ofisi za Tume ya Umwagiliaji.

DR.KUSILUKA AWAUMA SIKIO WALENGWA WA TASAF

$
0
0
Na Estom Sanga-Njombe 

Wananchi wanaonufaika na huduma za serikali kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAFwameaswa kutumia vizuri huduma hizo ili waweze kuboresha maisha yao na kupambana na umaskini. 

Akizungumza na Walengwa wa Mpango huo katika kijiji cha Ludilo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi wa Mfuko huo Dr. Moses Kusiluka amesema serikali imedhamiria kwa dhati kupunguza adha ya umaskini miongoni mwa Wananchi wake hivyo akataka wananchi na wadau wengine kuunga mkono jitihada hizo. 

Dr.Kusiluka amesisitiza umuhimu wa Walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini kuendelea kutumia huduma za TASAF kwa kuanzisha miradi itakayowawezesha kujiongezea kipato na hivyo kuwa na uwezo mzuri zaidi wa kuhudumia familia zao na kupunguza umaskini. 

Aidha Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF ambaye pia ndiye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Ikulu, amesema utekelezaji wa Mpango huyo ni wa Serikali na Wadau wengine wa Maendeleo ambao wanaendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa kuchangia fedha na ushauri mwingine wa kitaalamu. 

Akiwa katika kijiji hicho Dr. Kusiluka ameshudia miradi ya kilimo cha miti ya matunda ya parachichi, maharage na mabwawa ya samaki ambayo inatekelezwa na Walengwa wa TASAF kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda na kuonyesha kuridhishwa na miradi hiyo ambayo inawaongezea kipato Walengwa hao. 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Mufindi, Jamhuri William amepongeza jitihada za serikali kupitia TASAF katika kuchochea kasi ya maendeleo wilayani humo ambazo amesema zimeibua hamasa kubwa ya Wananchi kuboresha maisha yao hususani katika sekta ya makazi,elimu,Afya ,kilimo,mifugo ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya kuanza kwa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini.

Mwenyekiti wa kamati ya taifa ya Uongozi ya TASAF,Dr.Moses Kusiluka (aliyesimama) akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Ludilo wilaya ya Mfindi mkoani Iringa juu ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo kulia  kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William na kulia kwake ni Meneja wa Ukaguzi wa Ndani wa  TASAF Shadrack Mziray.


 Dkt.Kusiluka ( picha ya juu na chini ) akiwa katika shamba la parachichi la Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Ludilo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.


 Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa wa TASAF Dr.Moses Kusiluka picha ya juu na chini akikagua mabwawa ya samaki yaliyochimbwa na Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Ludilo wilayani Mufindi mkoani Iringa kupitia utaratibu wa ajira ya muda.

 
 
 Dr.Moses Kusiluka (wanne kutoka kushoto walioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Walengwa wa TASAF na viongozi wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

 Baadhi ya Walengwa wa TASAF wakisikiliza nasaha za Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya Mfuko huo katika kijiji cha Ludilo wilayani Mufindi mkoani Iringa.

 Baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Ludilo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wakitoa burudani baada ya kuwasili kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Ikulu Dr. Moses Kusiluka kukagua utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF.

RAIS MUSEVENI KUFANYA ZIARA YA SIKU MOJA NCHINI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kesho Jumamosi tarehe 13 Julai, 2019 atafanya Ziara Binafsi ya siku 1 moja hapa nchini.
Mhe. Rais Museveni atamtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kijijini kwake Mlimani katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita.


Akiwa Chato, Mhe. Rais Museveni atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli.



Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chato


12 Julai, 2019


WIZARA YA MADINI KUFUTA LESENI ZOTE AMBAZO HAZIFANYI KAZI NA KUWAPA WACHIMBAJI WADOGO

$
0
0


Meneja wa NMB kanda ya Ziwa - Abraham Augustino akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini.
Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na Kati wa NMB Filbert Mponzi (kushoto) akimpa mkono Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo baada ya kuzungumza na wachimbaji wadogo wa madini wa mkoa wa Geita, kwenye jukwaa la mtaji wa Maendeleo, katikati ni Mkuu Mkoa wa Geita- Robert Gabriel.


Geita. Wizara ya madini nchini imesema itaendelea kuzifuta leseni zote za utafiti ambazo hazifanyiwi kazi na zile ambazo hazilipiwi na kuwapatia wachimbaji wadogo hili waendelee kuzifanyia kazi ambazo zitasaidia kuinua uchumi wa nchi na kuzalisha ajira kwa vijana na watu ambao wanazunguka maeneo hayo.

Hayo yamesemwa Jana na Naibu waziri wa Madini Staslaus Nyongo wakati wa ufungaji wa Kongamano la Jukwaa la mitaji na maendeleo Mkoani Geita lililodhaminiwa na Benki ya NMB ambalo limefanyika kwa siku tatu kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Geita.

Amesema Wizara imejidhatiti kuendelea kutoa maeneo ambayo yataongeza uzalishaji kwa wachimbaji wadogo na kwamba wanataka kuona wachimbaji wadogo wanainuka kiuchumi ili waweze kulipa mrabahaa wa serikali pamoja na kodi.

“Sisi kama wizara hatutakaa kimya kuona namna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipatiwa maeneo kwa ajili ya kufanya utafiti wanakaa nayo bila ya kuyashughulikia tutaendelea kuyataifisha maeneo hayo na kuwapa wachimbaji wadogo hili waweze kuinua vipato vyao”Alisema Naibu waziri Nyongo.

Aidha Waziri Nyongo aliishukuru Benki ya NMB kwa namna ambavyo imeendelea kuwa mstari wa mbele kuwasaidia wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kufadhili Kongamano hilo ambalo limedumu kwa siku tatu na kwamba anaamini elimu ambayo wameipata itawasaidia kuweka akiba na kujulikana shughuli ambazo wanazifanya ili iwe Rahisi kupatiwa Mikopo.

Mkuu wa Mkoa huo,Robert Gabriel alisema mkoa huo bado unakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maeneo ya uchimbaji na kwamba ni vyema sasa kwa wizara kutuma wataalamu ambao wataweza kuja na kuona namna ambavyo watawasaidia kupata maeneo mengine ya uchimbaji.

Filbert Mponzi, ambaye ni afisa mkuu wa wateja wadogo na wakati NMB alisema Benki hiyo inatambua mchango wake mkubwa kwa jamii wakiwemo wachimbaji wadogo na ndio sababu ambayo imepelekea kufadhili semina hiyo ya siku tatu.

“Imani yetu ni kwamba maelekezo na elimu ambayo tumeitoa naamini wachimbaji wadogo wakiifanyia kazi sisi tupo tayari kuwakopesha tulikuwa tunashindwa kutokana na namna ambavyo walikuwa wakihama hama lakini naamini maelekezo tuliyowapa watayatekeleza”Alisema Filbert

Baadhi ya wachimbaji wadogo Mkoani humo,wameishukuru Benki ya NMB kuwa tayari kuwakopesha kwenye shughuli zao na kwamba kupitia mikopo ambayo watapatiwa itawasaidia kwa kiasi kuboresha shughuli zao za uchimbaji ambazo wamekuwa wakizifanya kila siku.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE AKAGUA SHAMBA LA KIMKAKATI LA MAHINDI GEREZA LA KILIMO NA MIFUGO KITENGULE, MKOANI KAGERA.

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza( wa Kwanza kulia) akikagua shamba la mahindiambalo liko katika hatua za mwisho za kuvunwa la gereza Kitengule. 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) akikagua ghala la kuhifadhia chakula cha wafungwa Gereza Kitengule alipotembelea gereza hilo leo Julai 11, 2019. 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) akiangalia moja ya mashine maalum inayotumika katika upandaji wa mbegu katika mashamba ya Gereza Kitengule alipotembelea gereza hilo leo Julai 11, 2019(Picha zote na Jeshi la Magereza)

Naibu Waziri Aweso Abaini Ubadhirifu Mradi wa Maji Kasulu

$
0
0

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akikagua Mradi wa Maji wa Heru Juu katika Wilaya yaKasulu, mkoani Kigoma. 
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiangalia Mradi wa Maji wa Rungwe Juu uliopo katika Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. 
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa njiani kuelekea kwenye Mradi wa Maji wa Heru Juu uliopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. 

***************** 

Naibu Waziri Aweso Abaini Ubadhirifu Kwenye Mradi wa Maji Kasulu
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametoa maelekezo ya kukamatwa kwa Meneja, Kwigize Venance na Mhasibu, Joshua Hendana waliokuwa wajumbe wa Kamati ya Jumuiya ya Watumia Maji ya Mradi wa Maji wa Heru Juu iliyovunjwa baada ya kubaini ubadhirifu wa fedha za mradi huo katika Wilaya yaKasulu, mkoani Kigoma. 

Aweso amechukua maamuzi hayo kutokana na mkanganyiko wa taarifa za viongozi wa kamati hiyo kuhusu kiasi cha fedha kilichopo kwenye akaunti ya kamati hiyo benki. Baada ya kupata maelezo ya kina akagundua mapungufu ya kamati hiyo yaliyomlazimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Simon Anangekuivunja na kuamuru ufanyike utaratibu wa kupata viongozi wengine na ukaguzi wa mapato na matumizi kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha. 

Baada ya kuulizia ripoti ya ukaguzi wa mapato na matumizi ya kamati hiyo kutoka kwa Mkaguzi wa Ndani, pamoja na mambo mengine ripoti imeonyesha kiasi cha Shilingi milioni 15 kimetumika kinyume na utaratibu. 

“Kuna tatizo kubwa kwa upande wa usimamizi wa fedha kwenye Kamati za Watumia Maji zinazosimamia miradi ya maji vijijini, zenye jukumu la kusimamia miradi iweze kuwa endelevu. Badala ya kutumia makusanyo kwa kuendeleza miradi, yanatumika na watu wachache kwa matumizi binafsi. Natakawatu hawa wakamatwe na kurudisha fedha zote, huu uwe mfano kwa wegine”. Naibu Waziri Aweso ameonya. 

Wanakijiji wa Heru Juu wametoa shukrani zao kwa Naibu Waziri kwa kulipatia suluhisho tatizo hilo la muda mrefu lililosababisha wananchi kuacha kuchangia gharama za uendeshaji za mradi huo uliogharimu zaidi ya Shilingi milioni 600 kutokana na kukosa imani na kamati.

TCRA YAENDELEA KUFANYA ZIARA YA KUVITEMBELEA VYOMBO VYA UTANGAZI KANDA YA KASKAZINI

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Mhe. Richard Kwitega (Katikati) katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, waliomtembelea ofisini kwake, jijini Arusha leo. Wajumbe hao wako katika ziara ya kuvitembelea vyombo vya utangazaji vya Kanda ya Kaskazini ili kutoa elimu ya uandaaji na usimamiaji wa maudhui bora ya uchaguzi nchini. Maudhui ya Vyombo vya utangazaji ni muhimu katika kuhimiza amani na utulivu wakati wote wa kipindi cha uchaguzi. Tanzania inatazamia kufanya chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani.

USAJILI WA TAASISI NA MASHIRKA YALIYOSAJILIWA NJE YA SHERIA YA NGO WAENDELEA WADAU WARITHIKA NA KASI


Jafo ahoji Mil 60 ununuzi wa dawa ya mchwa Hospital ya Wilaya Morogoro Dc

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa maelekezo wakati alipotembelea ujenzi wa hospitali yaMorogoro Dc inayojengwa katika eneo ya Mvuha kulia ni Mhe. Mkuu wa Mkoawa Morogoro Mhe. Kebwe Steven Kebwe. 
Kutoka Kushoto ni Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Kebwe Steven Kebwe, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo na Mkurugenzi wa Morogoro Dc Masoud Riobawakifuatilia taarifa ya matumizi ya fedha za ujenzi wa hospital ya Morogoro Dcwakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo. 
Muonekano wa moja ya majengo ya Hospital ya Wilaya ya Morogoro 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo(katikati) akisisitiza jambo wakati alipotembelea ujenzi wa hospitali Wilaya ya Morogoro inayojengwa katika eneo ya Mvuha 
Muonekano wa moja ya majengo ya Hospital ya Wilaya ya Morogoro 

************* 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(Mb) amehoji matumizi ya shilingi mil 60 manunuzi ya dawa ya mchwa katika jengo la Hospital ya Wilaya ya Morogoro linaloendelea kujengwa katika eneo la Mvuha. 

Mhe. Jafo alihoji matumizi hayo baada ya kutoonekana kwa kipengele hicho kwenye taarifa ya matumizi za fedha za ujenzi wa hospital hiyo pamoja na gharama kubwa iliyotumika kununulia dawa hizo. 

Akiwa katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa hospital za Wilaya ya Morogoro Mhe. Jafo alipokea taarifa ya ujenzi yenye mchanganuo wa matumizi ya fedha zaidi ya Tsh Bilioni moja ilihali kipengele cha ununuzi wa dawa hizo za mchwa uliotumia zaidi ya Shilingi mil 60 kutoonekana kwenye matumizi yaliyowasilishwa. 

Mhe. Jafo alihoji endapo dawa ya kudhibiti mchwa iliwekwa kwenye majengo hayo na kujibiwa kuwa ndio na kazi hiyo ilifanyika kwa gharama ya shilingi milioni 60 ndipo alipouliza kwanini matumizi ya fedha hizo hayajawekwa kwenye taarifa. 

“Bei ya ununuzi wa dawa hiyo si halisi na sijui kama mlijaribu kujilinganisha na wenzenu wa halmashauri nyingine ili mfahamu kuwa walitumia kiasi gani kwenye ununuzi wa dawa kama hiyo ni kiasi gani au ninyi mmenunua dawa ya aina gani ambayo imegharimu kiasi hiki kikubwa cha Fedha” Alihoji Jafo. 

Jafo aliongeza kuwa kama mlinunua dawa hiyo kwanini matumizi ya fedha hizo hayaonekani kwenye taarifa yenu, napata mashaka na matumizi ya fedha hizo hapa ni lazima ije Timu maalumu kwa ajili ya kuchunguza matumizi mabaya ya fedha za Mradi wa Ujenzi wa Hospitali hii aliongeza Jafo. 

Wakati huo huo Jafo alisema kuwa kwa kipindi kirefu halmashauri ya Morogoro Dc imekuwa na matumizi yasiyoridhisha ya fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo hali hiyo inaonyesha dhahiri kuwa kuna changamoto ya kiungozi. 

“Hapa kuna tatizo kubwa na lazima tulipatie ufumbuzi haiwezekani nyie mara mnashindwa kutekeleza miradi kwa wakati kuanzia ujenzi wa Jengo la Halmashauri shilingi milioni 500 hazijulikani zilipo na mpaka leo Jengo halijajengwa sasa mnataka tena tabia hiyo muilete kwenye mradi wa Hospital safari hii mtamaliza ujenzi huu haijalishi fedha mnazo au mmezitumia ni lazima mkamilishe ujenzi. 

Mpaka sasa mmekwishatumia shilingi Bil 1 kujenga majengo haya ambayo hayaridhishi na hamjafikia hata kwenye hatua ya kupaua huku mnaniambia mmebakiwa na shilinginmilioni 400 sitaki kusikia sababu yeyote ninachotaka ni kuona ifikapo Julai 30 Hospital hii imekamilika” Alisema Jafo. 

Akitolea ufafanuzi changamoto zilizojitokeza katika ujenzi wa hospital ya Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama imekuwa ikishauri kila wakati namna bora na ya haraka ya kukamilisha mradi huo lakini kumekua na muitikio mdogo wa wataalamu wa Halmashauri katika kutekeleza yale yanayoshauriwa na Kamati hiyo. 

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Morogoro Dc Masoud Rioba alifafanua manunuzi ya dawa za kuua Mchwa kuwa yalijumuishwa kwenye taarifa ya mradi katika kipengele cha vifaa vya ujenzi na sio kwenye kipengele kinachojitegemea ndio maana sio rahisi kuiona kwa uharaka. 

“Manunuzi ya dawa yamejumuishwa kwenye vifaa vya ujenzi haionekani kwa haraka kwa sababu hatukuiweka peke yake na gharama yake ni shilingi mil 60 hii ni baada ya kununua lita 1500 ambazo ndizo zilizokuwa zinahitajika na kila lita moja ilikua na gharama ya zaidi ya shilingi elfu 55 hivyo kuleta gharama ya zaidi ya shilingi milioni sitini” Alisema Rioba. 

Akifafanua kuhusu fedha zilizobakia kama zinaweza kukamilisha ujenzi wa Hospital hiyo amesema mpaka sasa vifaa vingi vimekwishanunuliwa hivyo fedha hiyo iliyobakia itaweza kufanya kazi za ukamilishaji wa majengo hayo na amemuhakikishia Mhe. Waziri wa Nchi kuwa kazi hiyo itakamilika kwa fedha zilizobakia. 

Wakatihuo huo mmoja wa mafundi wanaotumika katika kazi za ujenzi wa hospital hiyo amelalamika kukosekana kwa vifaa vya ujenzi kwa muda mrefu katika Hospitali hiyo huku malipo ya mafundi hao yakisuasua kitu kilichoplekea kuwakatisha tamaa na morali wa kuendelea kufanya kazi hiyo. 

Mbali na changamoto zote hizo zilizojitikeza Waziri Jafo ameagiza uchunguzi
ufanyikemara moja wakati huo huo kazi ya ujenzi ikiendelea na Uongozi uhakikishe ujenzi wa hospital hiyo ifikapo Julai 30, 2019.

Wananchi 1776 wapata huduma za ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo bila malipo JKCI maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam

$
0
0
Na Mwandishi Maalum

Wananchi 1776 wamepata huduma za ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo bila malipo zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo barabara ya Kilwa.

Wananchi hao waliotembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima afya zao walifanyiwa vipimo vya magonjwa ya moyo ambapo 448 walifanyiwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography), na 1097 walifanyiwa kipimo cha kuangalia umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiogram - ECG).

Asilimia 60 ya watu waliofanyiwa vipimo walikutwa na uzito mkubwa, asilimia 40 walikutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu na asilimia 20 walikutwa na tatizo la kuwa na sukari kwenye damu.

Aidha Taasisi hiyo hadi sasa imetoa rufaa ya moja kwa moja kwa watu 73 wakiwemo watoto 2 ambao baada ya kuwafanyia vipimo walikutwa na matatizo ya moyo yanayohitaji kufanyiwa uchunguzi wa kina na matibabu ya kibingwa .

Akizungumzia mara baada ya kupata huduma ya matibabu katika banda hilo mkazi wa Shekilango jijini Dar es Salaam Rehema Abdalah aliipongeza Taasisi hiyo kwa kutoa huduma ya matibabu ya moyo kwa wananchi bila malipo pamoja na kuwapa kipaumbele wazee waliojitokeza kwenda kupima afya zao.

“Nawashukuru wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wanaotoa huduma katika maonesho haya, kutokana na umri wangu wamenipa kipaumbele cha kufanyiwa vipimo kwa haraka. Nimekutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu na tayari nimepatiwa dawa kwa ajili ya matibabu,” alishukuru Rehema.

Naye mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam Hatibu Rashid ameishukuru Taasisi hiyo kwa kuwafikiria wananchi wenye uwezo wa chini kupata nafasi ya kufanyiwa vipimo vya magonjwa ya moyo na wafanyakazi wa Taasisi hiyo pindi watakapopata nafasi watoe huduma kama hiyo kwa wananchi waliopo maeneo mbalimbali hapa nchini hasa vijijini.

Rashid alisema, “Zamani vipimo kama hivi vilikuwa vinafanyika nje ya nchi tena kwa watu wenye hela. Lakini leo hii vipimo hivi vinafanyika hapa nchini na tunafanyiwa wananchi wa kawaida kabisa. Ninaishukuru sana Serikali kwa kuimarisha huduma ya matibabu ya moyo na ninawaomba wananchi wenzangu watumie maonesho haya kufika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa ajili ya kupima afya zao bila malipo”,.

Katika maonesho hayo Taasisi hiyo inatoa bila malipo huduma za ushauri wa lishe bora kwa afya ya moyo, umuhimu wa kufanya mazoezi, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo.
 Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mkuu wa kitengo cha Utafiti na Mfunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akiwafundisha watoto na watu wazima madhara ya mafuta katika mishipa ya damu ya moyo  wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa bila malipo ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo.

 Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mkuu wa kitengo cha Utafiti na Mfunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akiwafundisha watoto na watu wazima madhara ya mafuta katika mishipa ya damu ya moyo  wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa bila malipo ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo.

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakitoa huduma kwa wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa bila malipo huduma za ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo kwa wananchi wanaotembelea banda hilo lililopo katika banda la Jakaya Kikwete.

Picha na JKCI


Vodacom yadhamini Mbio za Capital City Marathon kuhimiza umuhimu wa mazoezi

$
0
0
 Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc kanda ya kati wakiwa  tayari kwa ajili ya kuanza mbio za Capital City Marathon zilizofanyika Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, kampuni hiyo ilidhamini wanafunzi 51 kutoka vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko jijini humo pamoja na wafanyakazi wake 35 ili kuwajengea tabia ya kufanya mazoezi na kuboresha afya zao. 
Mkuu wa mauzo wa kanda ya kati wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Grace Chambua (wa nne kutoka kulia mwenye kofia) akijiandaa kuanza mbio za Marathon za Capital City zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma, kampuni hiyo ilidhamini wanafunzi 51 kutoka vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko jijini humo pamoja na wafanyakazi wake 35 ili kuwajengea tabia ya kufanya mazoezi na kuboresha afya zao.

SIFURAHISHWI NA KASI YA MKANDARASI ALIEYEPEWA TENDA YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI WILAYANI KIBONDO,KAKONKO MKOANI KIGOMA-NAIBU WAZIRI MGALU

$
0
0
Moureen Rogath, Kibondo. 

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, amesema hajafurahishwa na kasi ya mkandarasi wa kampuni ya Urban and Engineering Service aliyepewa tenda ya kusambaza umeme vijijini katika wilaya ya Kibondo na Kakonko mkoani Kigoma. 

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyange, kata ya Mabamba na kusema kuwa endapo mkandarasi huyo hatobadilika katika utendaji wake serikali itamchukulia hatua za kisheria.

Naibu Waziri alisema wilaya ya Kibondo ni vijiji 3 vilivyowashwa umeme kati ya 40 huku wilaya ya Kakonko vijiji 5 vimewashawa kati ya 29 na kwamba hadi June 2020 vijiji vyote vinatakiwa kuwaka umeme. 

"Dhamira ya serikali ni kuona watanzania wote wanapata umeme kwenye makazi yao na kuwataka wananchi katika maeneo ya vijijini kuchangamkia fursa hiyo," amesema Naibu waziri huyo. 

Mapema akizungumza mkuu wa wilaya ya Kibondo Louis Bura, ameishukuru serikali kwa kuipa kipaumbele wilaya hiyo kupata nishati umeme kwa mara ya kwanza katika kijiji hicho.

Hata hivyo mkanadarasi wa kampuni hiyo, Shuda Ndanya amesema kuwa kasi ya kazi ilipungua kwa muda kutokana na uhaba fedha kwenye kampuni uliosababisha baadhi ya vifaa kukwama bandarini jambo ambalo amedai kuwa tayari limepatiwa ufumbuzi na kuahidi kukamilisha kazi kwa wakati.

Mkazi wa kijiji hicho Rajabu Husein amesema kuwepo kwa umeme katika eneo lao utawasaidia wao katika kukuza shuguli za kuinua uchumi.
Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyange,  kata ya mabamba wilayani kibondo mkoani Kigoma
Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu akizindua umeme kwa mara ya kwanza katika zahanati na kijiji cha Nyange , kata ya mabamba wilayani Kibondo mkoani Kigoma.



SERIKALI KUZIMA UMEME WA KUTUMIA MASHINE IFIKAPO 2020 MKOANI KIGOMA

$
0
0
Moureen Rogath, Kasulu.

Serikali imesema iko mbioni kuzima umeme wa kutumia mashine mkoani Kigoma ifikapo 2020, na kuunganisha na umeme wa gridi ya Taifa ambao utakidhi mahitaji ya wananchi mkoani humo.

Akizungumza Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu wakati akiwasha umeme katika kijiji cha Shunga wilayani hapa, amesema serikali imejipanga na lengo ni kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na umeme. 

Amesema katika kutimiza dhamira hiyo tayari ujenzi wa msongo wa umeme 132 KV kutoka Tabora Urambo hadi Kigoma umeanza na kwamba fedha kwaajili ya kukamilisha kazi hiyo ipo tayari. 

"Lengo ni kuwa na umeme wa uhakika wa kukidhi mahitaji ya wananchi mkoa wa Kigoma kwani umeme unaozalishwa kwa sasa wa kutumia mashine ya mafuta hautoshelezi mahitaji na kupunguza gharama za uendeshaji. 

Amelitaka shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwasimamia wakandarasi kuhakikisha wanafanya kazi kulingana na mikataba yao ikiwemo kutowatoza fedha zisizo rasmi ili kuwaunganishia umeme. 

"Kwa upande wa vijijini gharama za kuungansihwa kwa umeme uwe wa REA au Tanesco ni Sh. 27,000 kwa wote na kwamba wananchi hawatakiwi kutozwa zaidi ya kiasi hicho cha fedha," alisema Naibu waziri. 

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Simon Annange alisema, wilaya hiyo ni moja ya wilaya yenye shughuli nyingi za kiuchumi lakini pamoja na maswala ya kiusalama kutokana na wilaya hiyo kupakana na nchi jirani ya Burundi.

Mkazi wa Kijiji hicho Faustina Pyeni mbali na kuishukuru serikali, alisema wao pia wanawajibu wa kuhakikisha wanafanya shughuli za uzalishaji mali katika kukuza uchumi wao baada ya kupata nishati hiyo. 

Naibu waziri huyo aliwasha umeme wa REA awamu ya pili katika kijiji cha Ruhita, pamoja na kukagua shughuli za zinazoendelea katika kikosi cha jeshi la kujenga taifa (jkt),mtabila.
Wanafunzi walio hitimu kidato cha sita na kupita jeshini kwa mujibu wa sheria katika kikosi cha jeshi la kujenga Taifa (jkt )wakitumbwiza mbele ya naibu waziri wa nishati Subira Mgalu wakati alipotembelea kikosi hapo kuangalia shughuli za uwekezaji umeme katika kambi hiyo.
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia mkutano huo

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images