Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

WADAU WARIDHISHWA KASI YA USAJILI NGOs

$
0
0

Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Bi.Happy Msimbe akitoa huduma kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine akipata huduma ya kusajili Taasisi yake chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa kanda ya Mashariki. 
Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Bi. Idda Kombe akitoa huduma kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine akipata huduma ya kusajili Taasisi yake chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa kanda ya Mashariki. 
Wanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO kutoka kulia ni Denis Bashaka, wa pili kulia ni January kitunsi na wa pili kushoto Faki Shaweji wakifafanua jambo kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine akipata huduma ya kusajili Taasisi yake chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa kanda ya Mashariki. 

Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Vickness Mayao (Kushoto) akimsikiliza kwa makini aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Neema Mwanga wakati wa zoezi la kusajili Taasisi na Mashirika yaliyosajiliwa chini ya sheria nyingine kuja chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa kanda ya Mashariki. 

*************** 

Na Mwandishi Wetu 

Wadau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini ambao awali walisajiliwa katika Sheria nje ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wameridhishwa na kasi ya uhuishaji wa usajili wa Taasisi na Mashirika hayo. 

Hayo yamebainika leo jijini Dar es Salaam wakati wa zoezi linaloendelea la kuhuisha usajili wa Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine ikiwemo “Societies Act Cap 337” (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) ; “Trustees’ Incorporation Act Cap. 318 (RITA); na The Companies Act Cap 212 (Msajili wa Makampuni-BRELA) ambazo zinatakiwa kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019. 

Wakizungumza wakati wa zoezi hilo mmoja wa wadau kutoka Shirika la ‘SOS Village Children’ Bw. Dhiyant Patel Patel amesema kuwa Shirika lao lilikuwa limesajiliwa chini ya Sheria ya “Trustees’ Incorporation Act Cap. 318 (RITA) hivyo kuhitajika kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019. 

Bw. Patel ameongeza kuwa zoezi hilo lina umuhimu na manufaa kwa Taasisi na Mashirika hayo kwani litawasaidia kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa mujibu wa Sheria na taratibu zilizopo. 

“Niwapongeze Wizara na kwa hatua hii ya kasi ya kuhuisha usajili wa Mashirika yaliyokuwa nje ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini sisi tumeitikia wito na tuko pamoja katika hili” alisisitiza Bw.Patel 

Bw.Patel ametoa wito kwa Mashirika yanayotakiwa kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ili kuondokana na usumbufu mara baada ya Serikali kukamilisha zoezi hilo. 

“Zoezi hili linaenda vizuri na hatukuamini kwamba tunaweza tukapata huduma hii kwa muda wa masaa mawili kusajili na kupata cheti husika” alisema. 

Naye Mwakilishi wa Shirika la Bunjiri Community Development Support Bw. Ernest Mwanzi amesema kuwa Serikali imefanya jambo la muhimu kwa kuendesha zoezi hili kikanda na kushauri zoezi ili liendelee kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Haki Ardhi Bi. Gloria Msaki ameipongeza Wizara na Ofisi ya Msajili wa NGO kwa kujipanga katika zoezi la uhuishaji wa Taasisi na Mashirika yaliyosajiliwa katika Sheria nyingine ambayo yanatakiwa kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019. 

Akizungumza katika zoezi hilo Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Vickness Mayao amesema kuwa utaratibu wa usajili umerahisishwa sana hasa ule wa Mashirika yalikuwa yamesajiliwa katika Sheria nyingine. 

Ameongeza kuwa Wadau wameridhishwa na huduma zinazotolewa na Ofisi yake na kusema wanapata mrejesho mzuri kutoka kwa wadau kupitia fomu za mrejesho wa zoezi hilo. 

Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali inaendelea na zoezi la usajili wa Mashirika yaliyosajiliwa awali chini ya Sheria nyingine kama vile “Societies Act Cap 337” (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch); “Trustees’ Incorporation Act Cap. 318 (RITA); na The Companies Act Cap 212 (Msajili wa Makampuni-BRELA) ambazo zinatakiwa kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019. 

Usajili huu umeanza katika Kanda ya Mashariki (Dar es salaam, Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro) na Kituo kitakuwa Ofisi za Wizara ya Afya-Dar es Salaam kuanzia tarehe 10-19/07/ 2019.

MASAUNI AFANYA ZIARA SHINYANGA

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kangeme Kata ya Uloa Wilayani Ushetu mkoani Shinyanga ambapo katika mkutano huo uliofanyika leo masuala mbalimbali yanayohusu kudhibiti uhalifu yalizungumzwa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi Richard Abwao, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kangeme Kata ya Uloa Wilayani Ushetu mkoani Shinyanga ambapo katika mkutano huo uliofanyika leo masuala mbalimbali yanayohusu kudhibiti uhalifu yalizungumzwa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA YAJIWEKEA MKAKATI WA KUWA NA DAMPO LA KISASA LITAKALOGHARIMU BIL.3

$
0
0






NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA 


HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha,mkoani Pwani, imejiwekea mkakati wa kuwa na dampo la kisasa ,litakalokidhi vigezo ikiwemo kutokuwa na madhara hasi kwa wananchi, huko eneo la Misugusugu ambapo litagharimu kiasi cha sh.bilioni Tatu. 

Dampo lililopo sasa lipo Mitamba ambalo linaelezwa linahemewa hivyo kwa mkakati huo italeta ahueni kwa dampo hilo,miaka ijayo. 

Akielezea mpango huo, ofisa mahusiano,habari na mawasiliano ,halmashauri ya Mji wa Kibaha, Innocent Byarugaba alisema gharama zinazokadiriwa ni bilioni Tatu lakini halmashauri ikiweka fedha hiyo itashindwa kujiendesha . 

Aidha, alieleza juhudi za kuandika maandiko sehemu mbalimbali zinafanyika ili kupata wafadhili. 

Byarugaba alisema kwamba, halmashauri imeshatenga milioni 10.2 kwa ajili ya kuandaa barabara ya kuelekea katika dampo kwa kiwango cha changalawe, kutokea barabara kuu kutokana na barabara hiyo kuharibika. 

“TARURA nayo imetenga milioni 30 kwa mwaka wa fedha 2019-2020 ili kuboresha barabara hiyo iweze kupitika kirahisi”alielezea ofisa habari huyo. 

Ofisa mawasiliano huyo alifafanua,kwa sasa vipo pia vikundi vilivyosajiliwa katika kata mbalimbali ambavyo vinapita kukusanya taka kwenye kaya na kulipwa tozo kidogo. 

Byarugaba alibainisha, kwa sasa halmashauri haina kampuni yoyote ya kuzoa taka hivyo amewatahadhalisha wananchi kuwa chonjo na watu matapeli watakaodai wapo kwenye kampuni inayotambulika na halmashauri na kukusanya taka. 

Nae diwani wa kata ya Tumbi, Hemed Chanyika alisema kampuni ya kuzoa taka bado ni tatizo kwani kampuni iliyokuwepo awali imesimamishwa zaidi ya miezi mitatu . 

Aliwataka wakazi wa kata ya Tumbi ,kuendelea na utaratibu wa kuchimba mashimo kuhifadhi taka na kuzichoma badala ya kulundika uchafu kwenye mifuko kusubiria wakusanyaji taka.

WANANCHI DAR-PORI WAMPONGEZA KAMANDA WA POLISI RUVUMA

$
0
0
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma Simoni Maigwa ,akiongea na Wananchi wa Kitongoji cha Dar pori kijiji cha Lunyere, kata ya Mpepo Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma hivi karibuni, Wakati akihamasisha Ulinzi shirikishi katika maeneo ya Mpakani mwa Nchi ya Tanzania na Msumbijiili amani iwepo.picha na (Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa) 

************ 

Wananchi wa Kata ya Mpepo Wilayani Nyasa, wamempongeza Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Ruvuma Simon Maigwa, kwa kuwakikishia usalama wa mali na maisha licha ya kuishi Karibu na mpaka wa Tanzania na Msumbiji. 

Wananchi hao, wametoa pongezi kwa kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma,katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Lunyele kata ya Mpepo Wilayani Nyasa hivi karibuni. Mkutano aliokuwa na lengo la kuimarisha ulinzi shirikishi katika eneo la mpakani mwa Nchi ya Tanzania na Msumbiji. 

Wananchi hao walifafanua kuwa awali, kulikuwa na matukio yaliyokuwa yakiwapa hofu ya kufanya kazi zao, kwa kuwa ilikuwa haiwezekani kwenda hata kulima shambani, lakini mara baada ya kuimarisha Ulinzi na Usalama, sasa wanafanya kazi zao kwa amani, na kumtaka Kamanda huyo kuwapa kibali cha kujenga kituo cha Polisi katika Tarafa ya Mpepo ili kuweza kukabiliana na matukio ya kihalifu katika Tarafa ya Mpepo kwa kuwa ni tarafa inayopakana na Nchi jirani Ya Msumbiji. 

Wananchi hao waliongeza kuwa wana imani na kamanda huyo, kwa kuwa tukio linapotokea huwa anakuja mwenyewe, bila kutuma mwakilishi na hata leo katika mkutano wa kuimarisha ulinzi shirikishi na usalama wewe mwenyewe umekuja. “Kamanda wa Polisi sisi tuna imani kubwa sana na wewe kwa kuwa kila mara umekuwa pamoja na sisi bila kutuma mwakilishi unafika wewe mwenyewe. sisi sote uliyozungumza tumeyaelewa na tutayafanyia kazi na tunakupongeza sana kwa juhudi zako za ufanyaji kazi wako alisema Kiliani Kumburu huku akishangiliwa na wananchi wengine” . 

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma simon Maigwa, Akiongea na wananchi hao katika mkutano huo wa hadhara, aliwahakikishia Usalama wa mali na maisha yao, na kuwataka wafanye kazi za kujenga taifa bila woga wowote kwa kuwa mkoa wa Ruvuma ni salama na hakuna tatizo lolote na atakayeingia kwa kujaribu kuhatarisha Usalama kamwe hataweza,na hatatoka salama. 

Aliongeza kuwa kuhusu ombi la ujenzi wa kituo cha polisi cha kisasa kitakachohudumia Tarafa ya Mpepo Wilayani hapa, amelipokea na hana pingamizi lolote na atashirikiana nao kwa hali na mali katika kutatua changamoto za ujenzi huo, na atawaletea polisi na vifaa kwa ajili ya kuhakikisha jamii inakuwa salama muda wote na wanafanya kazi bila uoga wowote. 

“Napenda kuwaeleza ndugu wananchi wa kata hii ya Mpepo kuwa Ruvuma ni salama kila mtu aendelee kufanya shughuli zake za kujiletea maendeleo,yeyote atakayejaribu kuingia na kujaribu kutishia amani wananchi kamwe, hatatoka salama. Na nimesikia mnahitaji kujenga kituo cha Polisi hakuna tatizo tushirikiane tujenge na mimi nitaleta Askari mara baada ya kujenga kituo cha kisasa cha polisi kataka kijiji cha tingi ambapo ni makao makuu ya Tarafa ya Mpepo”alisema kamanda Maigwa. 

Aliongeza kuwa katika kila Kata ameleta polisi Kata ambaye anatakiwa Kuishi katika kata husika na kuhakikisha ulinzi na Usalama unaimarika kila kata.Hivyo aliwataka wamnanchi hao kushirikiana na Polisi kata aliyeletwa. 

Aidha katika hatua nyingine aliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Polisi, cha Tarafa ya Mpepo ambapo jumla ya shilingi laki mbili na ishirini na nne elfu (224,000/=) zilipatikana na kukabidhiwa kwa Ofisa Tarafa wa Tarafa ya Mpepo. 

Naye Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya hii aliwataka wananchi kuhamasika na kujitoa kwa dhati kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha polisi kwa kila kaya kuchangia nguvu zao kwa kuwa, ulinzi ni muhimu sana katika jamii . kwa sasa kituo kilichokuwepo ni kidogo ambacho hakina uwezo wa kuhudumia Tarafa yote ya Mpepo. 

Pia aliwataka viongozi wa serikali ya vitongoji, Kijiji, na Kata zote kuwa na Daftari la kusajli wageni wote wanaoingia ili kuweza kujua ni wahalifu au ni raia wema.

KIKAO KATI YA WIZARA NA WADAU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

BODI YA UWEKEZAJI YA CPA KANDA YA AFRIKA YAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Spika wa Bunge la Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Justin Muturi akiongoza kikao cha Bodi ya Uwekezaji ya Chama hicho Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Wajumbe wa Bodi hiyo na Wakwanza Kulia ni Katibu wa CPA-Kanda ya Afrika na ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Ndg. Stephen Kagaigai na wanaofuatia upande huo ni Wajumbe wa Sekretarieti ya Bodi hiyo. 
Spika wa Bunge la Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Justin Muturi (kushoto) akisalimiana na Katibu wa CPA-Kanda ya Afrika na ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Ndg. Stephen Kagaigai kabla ya kuanza kwa kikao. 
Katibu wa CPA-Kanda ya Afrika na ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Ndg. Stephen Kagaigai (kushoto) akizungumza na Katibu wa Bunge la Kenya Ndg. Michael Sialai. 
Spika wa Bunge la Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Justin Muturi (wanne kutoka kulia) katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Uwekezaji ya Chama hicho (waliokaa) na waliosimama ni Wajumbe wa Sekretarieti ya Bodi hiyo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI TANZANIA TOKEA NCHINI MISRI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, tokea nchini Misri, alipokua kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu, Julai 11.2019. Kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Ngalayainisi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Matukio Katika Picha Awamu ya Pili Mafunzo Kwa Waandishi wa Habari Kuhusu SADC

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayub Rioba
akiwasilisha mada wakati wa mafunzo kwa kundi la pili la waandishi wa habari wanaojengewa uwezo ili waweze wa kuandika na kuripoti habari za nchi wanachama wa SADC, Mafunzo hayo yanafanyika mjini Morogoro kuanzia Julai 11, 2019 ambapo yatafanyika kwa siku tatu. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari- MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akieleza umuhimu wa waandishi wa habari kufuatilia na kutangaza manufaa ya mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali za nchi wanachama wa SADC leo Julai 11, 2019 mjini Morogoro. 
Katibu Mkuu mstaafu Balozi Hebert Mrango akiwasilisha mada kuhusu historia ya SADC, masuala ya siasa, uchumi na kijami wakati wa mafunzo kwa kundi la pili la waandishi wa habari wanaojengewa uwezo ili waweze wa kuandika na kuripoti habari za nchi wanachama wa SADC, Mafunzo hayo yanafanyika mjini Morogoro kuanzia Julai 11, 2019 ambapo yanafanyika kwa siku tatu. 
Sehemu ya washiriki wa mafunzo kwa kundi la pili la waandishi wa habari
wanaojengewa uwezo ili waweze wa kuandika na kuripoti habari za nchi wanachama wa SADC, Mafunzo hayo yanafanyika mjini Morogoro kuanzia Julai 11, 2019 ambapo yanafanyika kwa siku tatu. 
Katibu Mkuu mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Mussa Uledi akiwasilisha mada wakati wa awamu ya pili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 11, 2019 ikiwa ni siku ya kwanza ya mafunzo hayo.

NDIKILO AIAGIZA HALMASHAURI YA MKURANGA KUWA MAKINI KUINGIA MKATABA NA MAWALA WABABAISHAJI

$
0
0
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo 


NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA 

MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Mkuranga,kuwa makini na mawakala wakusanyaji wa vyanzo vya mapato ili kuepuka kukimbia na fedha hatimae kuingia kwenye migogoro na kusababisha kukimbilia mahakamani . 

Aidha ,ameitaka halmashauri hiyo kuimarisha kitengo cha ukaguzi wa ndani ili kuongeza ufanisi. Ndikilo alitoa maelekezo hayo, katika baraza maalum la madiwani kupitia hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) 2017/2018 ,wilayani Mkuranga. 

Mkuu huyo wa mkoa alitaka wajipange kupata mawakala waaminifu wasioweza kupata fursa ya kukimbia na fedha za umma. Ndikilo aliiasa halmashauri hiyo pia ,kuendelea kuongeza mapato ya ndani na kuwa na wigo wa vyanzo vya mapato ili kuinua mapato hayo. 

Pamoja na hayo, aliielekeza menejimenti wilayani hapo kuhakikisha wanatekeleza hoja 32 ambazo hazijafungwa hadi ifikapo agost 30 mwaka huu,ili ziweze kufungwa. “Nimeona katika ya hoja ambazo hazijafungwa ,kuna kesi kama nne zinazohusu migogoro baina yenu na mawakala, hata mkikimbilia mahakamani haisaidii kama fedha zimeshaliwa ,mnapoteza fedha na muda,: Hivyo tafuteni mawakala wazuri kuepukana na shida hizi.” 

“Kumekuwepo na changamoto ya kiutendaji katika raslimali watu na fedha na kusimamia miradi ya maendeleo”:Hivyo basi wakurugenzi na watendaji simamieni ili sheria,kanuni na taratibu zifuatwe kwa lengo la kusaidia mkaguzi akipita kusiwepo na dosari”alifafanua Ndikilo. 

Nae mkurugenzi wa halmashauri ya Mkuranga, Mshamu Munde alisema, hoja ambazo hazijafungwa nyingi zipo katika hatua ya utekelezaji hivyo wamepokea maagizo waliyopatiwa na aliahidi kuyafanyia kazi. 

Awali kaimu katibu tawala wa mkoa huo, Shangwe Twamala alieleza, kutofungwa kwa hoja kunazalishwa na wakuu wa idara na wakuu wa vitengo ambao hawatekelezi majukumu yao kikamilifu kwa kutotunza na kuweka risiti za malipo.

WAKANDARASI WAMALIZE UJENZI KULINGANA NA MKATABA- JENERALI MSTAAFU MWAMUNYANGE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amewaagiza wakandarasi wanaoendelea na ujenzi  wa Tenki la Kisarawe kukamilika kulingana na  makubaliano  ya mkataba.

Mradi huo unatekelezwa na DAWASA ikiwa ni katika jitihada za kuboresha huduma za maji kwenye enye ujazo wa Lita Milioni 6.

Mradi huo utahudumia maeneo ya Pugu, Gongo la Mboto, Airwing, Ukonga na Majohe unatarajia kukamilika kufikia Septemba mwaka huu.

“Mradi huo ambao ulianza rasmi mwaka jana unategemea kukamilika September mwaka huu utanufaisha wakazi wa KIsarawe, Pugu, Gongo la Mboto, Ukonga pamoja na Airwing kwa Upatikanaji wa  maji ya uhakika,”amesema

Ameeleza kuwa, mradi mpaka sasa umefikia pazuri na kutaka wakandarasi waongeze juhudi katika kukamilika kwake kulingana na makubaliano ya mkataba.

“Mpaka sasa Maendeleo ya Mradi ni mazuri na nina amini Mpaka kufikia Septemba mwaka huu wameniahidi  utakuwa umekamilika na Wanachi wa wilaya ya Kisarawe na vitongoji vyake watanufaika kwa kupata maji safi na salama,”alisema Mwamunyange.

Mbali na hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo  amemshukuru Rais John Pombe Magufuli pamoja  na DAWASA kwa kupeleka mradi wa maji Kisarawe utakaowezesha wananchi kupata huduma ya maji safi na salama pamoja na kuwezesha wawekezaji aa Viwanda kuwa na maji ya uhakika kwa ajili ya uzalishaji.

Dc Jokate amesema, Changamoto Sugu Ya Maji Mji Mdogo wa Kisarawe lenye Kata Nne Kuwa Historia Ifikapo September 2019 mwaka huu.

"Leo nimepokea ugeni ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Mkuu wa Majeshi Ya Ulinzi Tanzania- JWTZ Mstaafu Jen. Mstaafu Davis Mwamunyange, katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi ya maji utakaoleta maji, Mradi huu utanufaisha pia eneo letu maalum la Viwanda la Visegese lilopo eneo la kimkakati karibu na Reli mbili za TRC-SGR na TAZARA," amesema

Mradi wa Kisarawe unagharimu Bilion 10 na utahudumia wananchi wa Majohe, Pugu, Gongo la Mboto na maeneo ya Ukonga

Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Mkuu wa majeshi mstaafu Jeneral Davis Mwamunyange alitembelea na kujionea Maendeleo ya ujenzi wa Tenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa Milioni sita pamoja na ujenzi wa tenki la Pugu  la ujazo wa lita milion 2.
 Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange akitoa maelezo kwa Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa Tanki la maji la Kisarawe na kuwataka wamalize kwa muda kulingana na makubaliano ya Mkataba. Ujenzi huo ulianza July mwaka jana na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu.

 Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa pampoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo baada ya kutembelea ulazaji wa mabomba yatakayosambaza maji katika kata zote za Kisarawe.
 Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo na watendaji wa DAWASA wakiwa kwenye picha ya pamoja  baada ya kutembelea ulazaji wa mabomba yatakayosambaza maji katika kata zote za Kisarawe.
Eneo la Pugu litakalojengwa tenki la maji lenye ujazo wa Lita Milioni 2 kwa siku.

Kesi ya Kitilya na wenzake yaendelea kuunguruma mahakama ya mafisadi.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi maarufu kama Mahakama ya Mafisadi imepokea barua mbili za uthibitisho kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, kwamba washitakiwa Benason Shallanda na Alfred Misana waliteuliwa kuwa makamishna katika Idara ya Sera.

Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara hiyo, Grace Sheshunga (52), amezitoa barua hizo leo Julai 11,2019 mahakamani hapo mbele ya Jaji Immaculata Banza wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya kesi ya utakatishaji inayomkabili Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake.

Mbali na hao, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Ofisa wa Benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sio Salomon ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 58 yakiwemo 49 ya utakatishaji fedha.

Akiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Hashimu Ngole, kutoa ushahidi wake shahidi Sheshunga amedai Oktoba Mosi, 2010 Shallanda aliteuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi wakati huo, Ramadhan Kija kuwa Kamishna wa Sera na kudai kuwa, barua ya kupandishwa cheo kwa Shallanda ilielekeza kwamba atalipwa Sh 2,062,000 bila nyongeza na kwamba atakuwa kwenye majaribio kwa miezi sita na endapo atashindwa kazi hiyo atatolewa.

Amedai kuwa, barua hiyo pia ilielekeza kwamba serikali itamdhamini mshitakiwa huyo kwa kumkopesha gari ndogo ya usafiri aina ya Sallon kwa ajili ya safari za kwenda kazini na kurudi nyumbani, nyumba ya kuishi na kumlipia gharama za umeme ya fedha isiyozidi Sh 205,000 na simu Sh 180,000 kwa mwezi huku majukumu yake kwa nafasi hiyo yakiwemo ya kuandaa sera za madeni na kupokea maombi mbalimbali ya mikopo ya fedha.

Aidha amedai, Agosti Mosi, 2013 mshitakiwa Misana ambaye alikuwa Mchumi Mkuu daraja II, aliteuliwa kuwa Kamishna Msaidizi wa Madeni katika Idara ya Sera huku akiongeza kuwa mamlaka iliyomteua mshitakiwa Misana ni aliyekuwa Katibu Mkuu, Dk Servacius 

Likwelile ambaye alielekeza kwamba mshahara ulioainishwa katika barua hiyo ni Sh 2,900,000.

Pia alielekeza mshitakiwa atafanya kazi kwa majaribio kwa miezi sita na endapo atashindwa kumudu majukumu hayo makubwa yanayohusu madeni ataondolewa kwenye nafasi hiyo kwa mujibu wa sheria. Na barua yake ya kupandishwa cheo ilielekeza kuwa serikali itamdhamini mshitakiwa huyo kukopa gari, kumpatia nyumba, kumlipia umeme usiozidi Sh 205,000 na simu Sh 180,000.

Baada ya kueleza hayo, shahidi aliiomba mahakama kupokea barua hizo kama kielelezo na upande wa utetezi haukuwa na pingamizi.

Shahidi huyo amedai majukumu yake ni kutunza nyaraka mbalimbali za mawasiliano ya ndani na nje ya wizara kwenye masijala zao na kwamba Januari Mosi, 2016 alipokea hati kutoka Takukuru ikimuelekeza kuwasilisha nyaraka zinazohusu muhtasari wa kikao cha 61 cha Kamati ya Kitaalamu ya Usimamizi wa Madeni (TDMC) na kuiwasilisha.

Hata hivyo, baada ya shahidi huyo kuomba mahakama kupokea nyaraka hiyo, Wakili wa Utetezi, Majura Magafu alipinga kupokelewa kwa sababu nyaraka hiyo haijaambatana na muhtasari wa kikao kama shahidi alivyoelekeza huku Wakili Alex Mgongolwa na Jeremiah Ntobesya walipinga pia kwa madai kuwa barua iliyowasilishwa ni ya siri kinyume na Sheria ya Usalama wa taifa pia inaonekana hakuna nyaraka iliyopelekwa Takukuru kwa sababu katika vielelezo hivyo havioneshwi.

Wakili Ngole, amedai hoja zilizowasilishwa hazina mashiko nakuomba mahakama kuzitupilia mbali kwani upande wa utetezi hawapaswi kuwapangia namna ya kuwasilisha ushahidi wao kwani nyaraka zilizowasilishwa zina maana kwenye shauri hilo na zinaonesha namna shahidi alivyohusika kutoa nyaraka aliyoombwa.

Kesi hiyo itaendelea kesho.

Washitakiwa katika kesi hiyo wanakabiliwa na mashitaka matatu ya kughushi, moja la kuongoza uhalifu, 49 ya utakatishaji fedha, mawili ya kutoa nyaraka za uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanyanyifu moja na la kutoa nyaraka kwa nia ya kumdanganya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KYAKA, RWAMISHENYE, KEMONDO NA MULEBA WAKATI AKITOKEA KARAGWE MKOANI KAGERA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Rwamishenye wakati akitokea Karagwe mkoani Kagera
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiandika kero mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wananchi wa Muleba mkoani Kagera wakati akielekea Chato mkoani Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Muleba Mjini mkoani Kagera wakati walipokuwa wakielezea changamoto  mbalimbali zinazowakabili.
 Mtume Venon Fernandes wa Kanisa la Agape akiwa pamoja na wananchi wa Rwamishenye wakifurahia wakati wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimama katika eneo hilo na kuwasalimu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mtume Venon Fernandes wa Kanisa la Agape katika eneo hilo la Rwamishenye wakati akielekea Chato mkoani Geita.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa na Mtume Venon Fernandes wa Kanisa la Agape pamoja na wananchi wa Rwamishenye Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kuzungumza nao wakati akitokea Karagwe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kemondo nje kidogo ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika eneo la Muleba mjini mara baada ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mbele ya Kaburi la Marehemu Mhandisi Leopard Mjungi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa barabara Kuu kutoka Wizara ya Ujenzi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza nyumbani kwa marehemu Mhandisi Leopard Mjungi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa barabara Kuu kutoka Wizara ya Ujenzi mara baada ya kuwasili kijijini hapo Muleba mkoani Kagera. Marehemu Mhandisi Mjungi alifariki mwaka 2007.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Muleba wakati akitoka nyumbani kwa marehemu Mhandisi Leopard Mjungi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa barabara Kuu wa Wizara ya Ujenzi. PICHA NA IKULU

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KYAKA, RWAMISHENYE, KEMONDO NA MULEBA WAKATI AKITOKEA KARAGWE MKOANI KAGERA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Rwamishenye wakati akitokea Karagwe mkoani Kagera.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiandika kero mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wananchi wa Muleba mkoani Kagera wakati akielekea Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Muleba Mjini mkoani Kagera wakati walipokuwa wakielezea changamoto  mbalimbali zinazowakabili.

 Mtume Venon Fernandes wa Kanisa la Agape akiwa pamoja na wananchi wa Rwamishenye wakifurahia wakati wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimama katika eneo hilo na kuwasalimu.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mtume Venon Fernandes wa Kanisa la Agape katika eneo hilo la Rwamishenye wakati akielekea Chato mkoani Geit
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa na Mtume Venon Fernandes wa Kanisa la Agape pamoja na wananchi wa Rwamishenye Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kuzungumza nao wakati akitokea Karagwe.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa na Mtume Venon Fernandes wa Kanisa la Agape pamoja na wananchi wa Rwamishenye Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kuzungumza nao wakati akitokea Karagwe.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Muleba Mjini mkoani Kagera wakati walipokuwa wakielezea changamoto  mbalimbali zinazowakabili.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Muleba Mjini mkoani Kagera wakati walipokuwa wakielezea changamoto  mbalimbali zinazowakabili.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kemondo nje kidogo ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika eneo la Muleba mjini mara baada ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mbele ya Kaburi la Marehemu Mhandisi Leopard Mjungi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa barabara Kuu kutoka Wizara ya Ujenzi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza nyumbani kwa marehemu Mhandisi Leopard Mjungi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa barabara Kuu kutoka Wizara ya Ujenzi mara baada ya kuwasili kijijini hapo Muleba mkoani Kagera. Marehemu Mhandisi Mjungi alifariki mwaka 2007.  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Muleba wakati akitoka nyumbani kwa marehemu Mhandisi Leopard Mjungi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa barabara Kuu wa Wizara ya Ujenzi.
PICHA NA IKULU

KISHINDO YAMLETA TENA IRENE ROBERT KWENYE MUZIKI WA INJILI

$
0
0
  
Na Hadija Seif
MSANII wa Muziki wa Injili nchini Irene Robert adondosha Mkwaju mpya kwa shabiki zake, ikiwa na bada ya kukamata anga la Muziki la Injili Tanzania na Nje ya Mipaka kwa wimbo wake uitwao "Kishindo".

Sasa ameshusha wimbo Mpya na video Uitwao Tembea, ambao ni wimbo wake wa nne kuachia baada ya kuachia "Unashuka",  "Nianze na wewe",  na sasa "Kishindo".

Irene ni mwimbaji ambaye amepata mafanikio kwa haraka sanaa kutokana na kufanya kazi nzuri za kiwango Cha juu sana.

Kazi ya video imefanywa na Enxer na audio ikifanyika pale Masai Record chini ya producer Yusuph Manamba akiwa  chini ya Lebo ya Famara Promotion.

Ni mwimbaji aliyejishusha kwa Unyenyekevu na anatamani kwenda kimataifa zaidi. 

BODI YA UWEKEZAJI YA CPA KANDA YA AFRIKA YAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Spika wa Bunge la Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Justin Muturi akiongoza kikao cha Bodi ya Uwekezaji ya Chama hicho Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Wajumbe wa Bodi hiyo na Wakwanza Kulia ni Katibu wa CPA-Kanda ya Afrika na ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Ndg. Stephen Kagaigai na  wanaofuatia upande huo ni Wajumbe wa Sekretarieti ya Bodi hiyo.
 Spika wa Bunge la Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Justin Muturi (kushoto) akisalimiana na Katibu wa CPA-Kanda ya Afrika na ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Ndg. Stephen Kagaigai kabla ya kuanza kwa kikao.
 Katibu wa CPA-Kanda ya Afrika na ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Ndg. Stephen Kagaigai (kushoto) akizungumza na Katibu wa Bunge la Kenya Ndg. Michael Sialai.
Spika wa Bunge la Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Justin Muturi (wanne kutoka kulia) katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Uwekezaji ya Chama hicho (waliokaa) na waliosimama ni Wajumbe wa Sekretarieti ya Bodi hiyo. 
PICHA NA BUNGE

BBC: PROFESA KABUDI NA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA

MAJAMBAZI WANNE WAUAWA KIBAHA BAADA YA MAJIBIZANO YA RISASI NA POLISI -WANKYO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA VIJIJINI

JESHI la Polisi Mkoani Pwani, limefanikiwa kuua majambazi wanne katika tukio la majibizano ya risasi baina ya polisi na majambazi hayo huko eneo la Kwala , Wilaya ya Kipolisi Mlandizi. 

Kamanda wa polisi mkoani hapa,Wankyo Nyigesa alisema, tukio hilo la kuuawa kwa majambazi hayo limetokea leo majira ya saa 8 mchana baada ya taarifa kulifikia Jeshi la Polisi kuwa wapo watu wamepanga kwenda kuvamia na kupora fedha ambazo zilikuwa zimepangwa kwenda kulipwa kwa wanaojenga Bandari Kavu ya Kwala.

"Ndipo Jeshi la Polisi Mkoani hapa tuliweka mtego na majambazi hao kujikuta wakinasa na kuanzisha majibizano ya risasi na kupelekea majambazi wanne kati ya sita wanaodhaniwa kuwepo kupoteza maisha"alieleza Wankyo.

Hata hivyo majambazi wawili walitoweka eneo la tukio kwa kutumia gari lingine na msako wa kuwatafuta bado ungali ukiendelea. Wankyo alifafanua, katika tukio hilo majambazi hao wamekutwa wakiwa na bunduki mbili aina ya pump action, radio call moja, hirizi, dawa za kupulizia watu, kamba za kufungia watu na, plasta za kuziba watu midomoni.

Vitu vingine ni pamoja na leseni za udereva, vitambulisho mbalimbali vya uraia, kadi ya bima ya afya, koti, kaniki, kanzu, suruali, kaptula . 

Kamanda huyo alibainisha, miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi .




MBUNGE VITI MAALUM JIJINI ARUSHA,CATHERINE MAGIGE AKABIDHI MASHINE YA KUKOBOA KWA CHAMA CHA UWT

$
0
0

Na,Jusline Marco.Arusha

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Arusha kupitia chama cha mapinduzi Catherine Magige amekabidhi mashine ya kukoboa na kusaga yenye thamani ya shilingi milioni 3 na laki 5 kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kimaendeleo za chama hicho katika Wilaya ya Arumeru.

Akikabidhi mashine hiyo kwa viongozi wa UWT Wilaya ya Arumeru Mbuge Magige amewataka viongozi hao kukemea vitendo viovu vinavyoendelea katika kata zao vikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia na unywaji wa pombe uliokithiri katika baadhi ya maeneo.

Kwa upande wake mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii wilayani humo Bi.Angela Mvaa akitoa ufafanuzi wa idara hiyo kwa wanawake hao amesema kuwa ili kuweza kuwa na jamii yenye maadili ni lazima wanawake wawe chachu ya mabadiliko katikati ya jamii zao.

Aidha amesema kuwa katika Wilaya hiyo vitendo vya ukatili wa kijinsia na kingono vimekithiri katika Kata ya sokoni 2,olmotonyi pamoja na oltrument na vimeonekana kushika kasi huku baadhi ya wazazi na wazee wa uko kuwa visababishi vya kumnyima mtoto haki zake za msingi kwa kumaliza matukio hayo kimila huku wengine wakikataa kutoa ushirikiano katika vyombo husika.

Ameongeza kuwa wapo baadhi ya watu huzuia kupatikanaji wa haki za mtoto aliyefanyiwa ukatili wa kingono kwa kutokutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama huku wengine wakisuluhisha matatizo hayo kwa njia ya kimila.

Hata hivyo hivi karibuni kumetokea tukio katika kata ya Olorien kijiji cha Olosiva baada ya mzazi aliyefahamika kwa jina la Aristerico Silayo kumbaka mtoto wake Angel Aristerico akiwa na umri wa miaka 11 tangu mwaka 2016 mpaka sana kitendo ambacho wanakijiji wa kijiji hicho wamekilaani vikali kutokana na mzazi huyo pamoja na kukutwa na hatia ya kutenda kosa hilo aliachiwa huru na mahakama ya Hakimu mkazi Arusha,M Mwankunga kupitia kifungu cha 235 cha Sheria ya makosa ya jinai.
 Mbunge wa Viti maalum Catherine Magige akikabidhi mashine ya kusaga na kukoboa kwa chama cha UWT Wilaya ya Arumeru zitakazo wasaidia katika uongezaji wa kipato katika chama chao
Mbunge Magige akikabidhi bati hamsini kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Charles Mahera,akiunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika elimu.

DKT NDUGULILE AITAKA SEKTA YA AFYA KIGOMA KUTOA ELIMU KUHUSU UGONJWA WA EBOLA

$
0
0
Na Editha Karlo,Michuzi TV.

NAIBU Waziri wa afya,maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Faustin Ndugulile ameitaka sekta ya afya Mkoani Kigoma kutoa elimu kwa watumishi wote wa afya kutambua hatua za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola

Ndugulile amesema kuwa endapo elimu itatolewa kwa wakati ikiwa ni sambamba na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama na kuwashirikisha wananchi kikamilifu ugonjwa wa Ebola utathibitiwa kwakuwa kila mmoja atakuwa anafahamu namna ya kuutambua ugonjwa huo.

"Elimu ikitolewa kwa wakati kwa kuwashirikisha wananchi kikamilifu ugonjwa wa Ebola tutaweza kuuthibiti kwani kila mtu anakuwa anaufahamu baada ya kupata elimu"alisema 

Pia alisema kuwepo na uangalizi katika mipaka ili kuzuia watu kuingia kutoka nchi za jirani na kuingia nchini kiholela.Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amesema Mkoa wa Kigoma unachangamoto ya mipaka,lakini hatua mbalimbali zinachukuliwa kuthibiti wanaoingia kihohela nchini.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chaote amehaidi kuyafanyia kazi maagizo ya Naibu Waziri ikiwemo la kutoa elimu ili kuthibiti ugonjwa wa Ebola.
Naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua bandari ya Kigoma ambapo wageni kutoka nchi za jirani wanaitumia kuingia nchini
Naibu Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua vituo vya dharula katika bandari ya Kibirizi.
Naibu wa Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile akiongea na mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga juu ya mikakati ya kuthibiti ugonjwa wa ebola usiingie Tanzania

BALOZI SEIF ALI IDDI AITAKA TANTRADE KUIMARISHA MITANDAO YA KUWASAIDIA WAFANYABIASHARA

$
0
0

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akimkabidhi cheti cha ushindi mmoja wa washiriki wa makampuni kutoka nchini Rwanda, wakati wa hafla kufunga Manoesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) leo Alhamisi (Julai 11, 2019)yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi, Balozi Seif Alli Idd akimkabidhi cheti cha ushindi mmoja wa washiriki wa makampuni yaliyoshiriki katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam wakati hafla kufunga maonesho hay oleo Alhamisi (Julai 11, 2019) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Alli Idd akimkabidhi cheti cha ushindi Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi Dorina Kaaya wakati wakati wa hafla kufunga Manoesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) leo Alhamisi (Julai 11, 2019)yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Alli Idd akimkabidhi cheti cha ushindi mmoja wa washiriki kutoka Kampuni ya uzalishaji maziwa ya Asasi Diaries wakati wakati wa hafla kufunga Manoesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) leo Alhamisi (Julai 11, 2019)yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Manoesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere leo Alhamisi (Julai 11, 2019). 
(PICHA NA PASCHAL DOTTO-MAELEZO) 

………………………… 
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO 
DAR ES SALAAM 

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi ameitaka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuendelea kuimaisha mitandao na mifumo ya biashara nchini ili kuwawezesha wafanyabiashara wa Tanzania kuweza kuwa na uhakika wa masoko bora ya bidhaa za ndani na nje ya nchi. 

Akifunga Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) leo Alhamisi (Julai 11, 2019) Balozi Idd alisema Maonesho hayo ya mwaka huu yameonesha dhamira na mwelekeo wa Serikali katika kutumia fursa biashara na viwanda katika kujenga uchumi imara pamoja na kutengeneza ajira kwa wananchi. 

Balozi Idd alisema ni wajibu wa TANTRADE kutumia fursa za uwepo wa makampuni ya wazalishaji, wauzaji na wafanyabiashara kutoka nje wanaoshiriki katika maonesho hayo kuweza kujenga mitandao imara ya mahusiano na ushirikiano kwa wafanyabiashara wa ndani ili kuweza kuwatafutia masoko ya bidhaa zao ambazo kwa sasa zimeanza kuzalishwa katika viwango bora nchini. 

“Nawapongeza TANTRADE kwa juhudi zenu za kuanzia klinilki za biashara, na hili limewezesha wafanyabiashara wetu kuweza kukutana na wanunuzi mbalimbali ambao huweza kuwapa uzoefu wa namna bora zaidi ya kuzalisha bidhaa zenye kukithi viwango na ubora unaotakiwa” alisema Balozi Idd. 

Aidha Balozi Idd alisema Serikali kwa sasa inatekeleza Mpango Kazi wa Kuboresha Mfumo Udhibiti wa Biashara Nchini (Blue Print), ambao umekusudia kuondoa changamoto mbalimbali za wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, hivyo aliitaka TANTRADE kushirikiana na wadau na wazalishaji wa sekta binafsi ili kuiwezesha sekta ya biashara kuvutia wawekezaji wengi zaidi. 

Kwa mujibu wa Balozi Iddi pia aliitaka TANTRADE kuweka utaratibu wa kufuatilia oda za maombi mbalimbali zinazotolewa na wafanyabiashara kutoka nje ya nchi ili kuendelea kupanua wigo wa soko la bidhaa za Tanzania nje ya nchi ambalo kwa sasa limeendelea kupanuka kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali. 

Balozi alisema ni wajibu wa Watanzania kujenga utamaduni wa kuthamini bidhaa za ndani ili kuziwesha kupata masoko ya uhakika kwa kuwa kwa kufanya hivyo kutatoa fursa ya kuweza kutambulika kwa haraka pamoja na kumudu changamoto ya ushindani wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi. 

Alisema kuwa maonesho hayo ya 43 yamethibitisha uwezo wa wafanyabiashara wa Tanzania katika kutengeneza na kuzalisha bidhaa mbalimbali kwani idadi ya washirki wa maonesho kutoka nje ya nchi imeweza kuongezeka kutoka makampuni kutoka nje 2956 mwaka 2018 hadi kufikia 3250 mwaka 2019, hivyo kudhibitisha uwezo wa serikali katika kusimamia sekta ya biashara nchini. 

Balozi Idd anasema kuwa Makampuni ya wafanyabiashara ya Tanzania yaliyoshiriki maonesho hayo yanapaswa kupata uzoefu na uelewa mkubwa katika namna bora zaidi ya kusimamia na kuratibu sekta ya biashara nchini katika viwango bora ili kuweza kutengeneza masoko ya uhakika katika nchi za nje. 

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa alisema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini ikiwemo kuanza kufanya mapitio ya sera na sheria mbalimbali ambazo awali zilikuwa zikileta changamoto mbalimbali kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi. 

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa sekta ya viwanda na biashara inaleta tija katika ukuaji uchumi nchini, Serikali imekusudia kuweka msisitizo katika kujenga uchumi jumuishi kwa kuziweka sekta ya uvuvi, kilimo na mifugo kuwa kipaumbele muhimu katika kuzitumia rasilimali mbalimbali zilizopo katika sekta hizo katika kutengeneza ajira kwa wananchi walio wengi.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>