Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

SERIKALI YASHUSHA NEEMA KWA WANANJOMBE

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipanda mti wa matunda (mpalachichi) ikiwa ni ishara ya kuhifadhi mazingira, shughuli iliyofanyika baada ya uzinduzi wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka wakiongea na Wazee waliofika kupata huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe wakati alipofanya uzinduzi wa huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akieleza juu ya umuhimu wa kuwepo kwa mabango yanayohamasisha haki ya mgonjwa kupata huduma za Afya zilozo Bora wakati wa uzinduzi wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, kushoto kwake (mwenye Koti jeupe) ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe Dkt. Kyambile.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi ramani ya ujenzi wa majengo mengine mapya saba kwa Mkandarasi, shughuli iliyofuata baada ya uzinduzi wa huduma katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka baada ya uzinduzi wa huduma katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.

*******************
Na WAMJW-NJOMBE

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeshusha neema kwa Wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kutenga kiasi cha shilingi Bilion 7.6 kwaajili ya ujenzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ili kuboresha huduma kwa Wananchi.

Hayo yamejiri leo wakati wa zoezi la Uzinduzi wa huduma za Afya na lililoongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe iliyofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika uzinduzi huo, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha huduma za Afya katika Mkoa wa Njombe ikiwemo kujenga jengo la wazazi la ghorofa tatu, jengo la maabara, jengo la wagonjwa mahututi na jengo la upasuaji gorofa mbili, wodi za wagonjwa gorofa tatu, nyumba za Watumishi tano, pamoja na kichomea taka.

" Tunajenga jengo la wazazi la ghorofa tatu, tunajenga jengo la jengo la maabara, tunajenga jengo la wagonjwa mahututi na jengo la upasuaji gorofa mbili, tunajenga wodi za wagonjwa gorofa tatu, tunajenga jengo la kufulia, tunajenga kichomea taka na tunajenga nyumba za watumishi tano" alisema Waziri Ummy.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amemwagiza Mkandarasi wa Hospitali hiyo kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa majengo hayo hayo ndani ya miezi kumi ili wananchi wa Mkoa wa Njombe waanze kufaidika na huduma za Afya katika Hospitali hiyo, huku akiwatoa hofu wananchi kuwa pesa zote zipo tayari.

Mbali na hayo, Waziri Ummy mewaasa Wananchi kupambana dhidi ya magonjwa yasiyo yakuambukiza kama Kisukari, shinikizo la damu, Saratani na magonjwa ya Moyo kwa kubadilisha mtindo wa maisha ikiwamo ulaji mlo sahihi , kuacha uvutaji wa sigara na tumbaku, kuacha unywaji wa pombe kupita kiasi pamoja na kutofanya mazoezi mara kwa mara.

Aidha, Waziri Ummy ametoa with kwa vijana kujiepusha na mambo ambayo yatapelekea kipata maambukizi ya VVU, huku akiweka wazi kuwa maambukizi mapya ya VVU ni 82,000 kila mwaka nchini Tanzania, huku katika kila watu 100, watu 40 ni vijana wenye umri kati ya 15 hadi 24 umri ambao ni nguvu kazi ya taifa.

“Tunatambua kwamba kuna maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi Mkoani Njombe,lazima tuzingatie kanuni za kujikinga na maambukizi ya VVU, kujizuia kufanya mapenzi kwa vijana hasa kwa wasichana ambao muda wao haijafika, pili kuwa mwaminifu kwa mwenza wako au mpenzi wako na tatu kutumia kinga”. Alisema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amewatoa hofu wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kuweka wazi kuwa huduma za Afya katika Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe haitoathiri utoaji huduma katika Hospitali ya Kibena iliyokuwa Hospitali ya Mkoa, ambayo kwa sasa imerudishwa chini ya Halmashauri ya Mji wa Njombe.

“Na mimi ntahakikisha wale Watumishi ambao tilikubaliana waje kwenye Hospitali hii, waje na nguo zao , vifaa vyote waviache Kibena na huduma ya Kibena iendelee, na kazi ya Hospitali hii Mhe. Ummy Mwalimu na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wataweka vifaa vyote vitakavyohitajika na huduma zitaendelea”. alisema Mhe. Olesendeka.

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Mhe. Edwirn Mwanzinga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Afya kwa kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba jambo linalosaidia kuokoa kwa kiasi kikubwa maisha ya Wananjombe.

DC KASESELA ALIAGIZA JESHI LA POLISI IRINGA KUMKATA AYUBU MWENDA POPOTE ALIPO

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimpigia simu mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kuhakikisha anamkamata popote alipo Ayubu Mwenda ambaye anasababisha mgogoro wa shamba la familia ya mzee Mwenda
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa maelezo kwa familia ya marehemu mzee Mwenda katika kata ya Nduli mkoani Iringa. 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kuhakikisha anamkamata popote alipo Ayubu Mwenda kwa kuika makubaliano ya kuumaliza mgogoro huo.



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kuhakikisha anamkamata popote alipo Ayubu Mwenda ambaye anasababisha mgogoro wa familia ya Mwenda kwa kumkimbia mkuu wa wilaya na kamati yake walipokifika kusuhisha mgogoro huo.

Akizungumza kwenye shamba la familia mzee Mwenda Kasesela alisema kuwa Ayubu Mwenda ameleta dharau kwa kukimbia katika eneo usika la kutatua mgogoro ambao ameusababisha kwa makusudi kwa kutaka kuwadhurumu wanafamilia wenzake.

“Haiwezekani mtu aseme mara yupo mahakamani mara yupo msibani mara anazima simu huu ni utovu wa nidhamu kwa kuwa jana nilikaa nao na tukaongea nao vizuri na yeye akiwepo nay eye ndio chanzo cha mgogoro huo kwanini leo hayupo hapa” alisema Kasesela 

Kasesela alisema kuwa familia hiyo inagombea hekali mia moja na hasini na tisa (159) ambazo waliachiwa na marehemu mzee wao mzee Mwenda na kusema kuwa Ayubu ambaye ndiye kaka yao mkubwa amekuwa kisababishi cha mgogoro huo.

Aidha Kasesela alimtaka afisa mtendaji na afisa tarafa kuhakikisha shamba hilo linagawawiwa kwa wake wote sita wa mzee Mwenda ili kuondo na kumaliza mgogoro huo kwa kugawa kwa usawa na haki ili kila mmoja apate haki yake.

“Mzee Mwenda alikuwa na wake sita hivyo shamba hilo litagawiwa kwa kufuata familia za akina mama wote kwa haki ili kumaliza hili tatizo na hakuna mtu mwingine ataleta mgogoro kwa kuwa nitalipeleka shauri hili mahakamani kuweka zuio la kuanzisha kesi yeyoyte ile katika shamba hilo” alisema Kasesela

Kwa upande wake msimamizi wa mirathi hiyo Sadiki Abdalah Mwenda alimshukuru mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa kuasidia kutatua mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi bila kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.

Naye askari mstaafu Hawa Mwenda ambaye ni mwanafamilia alimshukuru mkuu wa wilaya na kumuomba awafikishie salaam kwa Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuongoza vizuri na kufanikisha wananchi wanyonge wafikiwe kirahisi na kutatuliwa matatizo yao.

MILIONI 42 BAKWATA KUJENGA MSIKITI

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
BARAZA Kuu la Waislamu (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza limezindua ujenzi wa msikiti wa baraza hilo utakaogharimu sh. milioni 42 kwa kuweka jiwe la msingi.

Akizungumza kabla ya kuweka jiwe hilo jana Sharif Said Jafari Swadiqu Bin Sayeid Muhammad kutoka Malindi nchini Kenya, alisema uongozi wa BAKWATA Mwanza umefikiria jambo jema kujenga msikiti kwenye soko ili kuwafanya waumini wa dini ya kiislamu wanaofanya biashara katika eneo hilo wasimsahau Mungu.

Alisema chini ya uongozi wa Sheikh Mkuu Mufti wa Tanzania, Abubakar Zuberi uislamu umeanza kuwa na mabadiliko makubwa kwa muda mfupi kutokana na kauli mbiu ya Jitambue, Badilika, Acha mazoea.

“Heshima ya uislamu ni msikiti ( kuwa na nyumba ya ibada) na uislamu unazingatia kuwa na msikiti na ni fikra njema msikiti kujengwa sokoni. Pia jamii ya kiislamu kupitia mambo matatu ya Mufti Abubakar Zuberi, yanamfanya mtu ajitambue, abadilike na kuacha mazoea mambo ambayo yameufanya uislamu Tanzania kubadilika,”alisema Sharif Said Jafari Bin Sayeid.

Mjukuu huyo wa kizazi cha 42 cha Mtume Muhhamad S.A.W. alidai msikiti huo utakaoitwa Masjid Abubakar Zuberi una umuhimu mkubwa kwenye uislamu kwa sababu wapo baadhi wanajenga mioyo ya watu na si misikiti pekee.

Sharif Said Jafari bin Sayeid akizungumzia akina mama kiislamu alisema ni wanaharakati wakubwa wa kuendeleza uislamu hivyo wajitambue, wainuke kwa sababu wanayo nafasi na fursa kubwa wenye jamii.

Awali Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza alhaji Sheikh Hassan Kabeke alisema dhamira yao ilikuwa kujenga jengo la msikiti wa ghorofa tatu kwa sababu BAKWATA kati ya misikiti 324 haina hata mmoja ambo ni maalumu na unmilikiwa na mkoa.

“Tulikuwa na dhamira ya kujenga msikiti wa ghorofa tatu lakini baada ya serikali kuamua kutumia eneo la BAKWATA kwa ajili ya soko kwa miaka miwili tumebadili nia hiyo na kujenga msikiti wa muda utakaotumika kwa kipindi hicho wakati tukijipanga kujenga wa kudumu utakaokuwa na hadhi ya Mufti Zuberi,”alisema.

Alieleza kwa kuwa heshima ya uislamu ni msikiti hivyo wenye dhamira ya kuendeleza uislamu waunge mkono mradi huo wa ujenzi msikiti kwa fedha, vifaa vya ujenzi (mawe, kokoto, mchanga, nondo, saruji na misumari).

“Gharama za ujenzi wa msikiti huu wa muda ni sh. milioni 42, waumini watautumia kwa ibada wakati tukijipanga kujenga ule wa kudumu.Utatumika kwa miaka miwili kisha utajengwa mkubwa kwa hadhi ya Mufti,”alisema Sheikh Kabeke.

Aidha, Sheikh Kabeke alisema Mkoa wa Mwanza umepata heshima ya kuandaa Maulid ya Kitaifa mwakani na yatadhimishwa kwa kufanya mashindano ya kuhifadhi Quran, adhana, mpira kwa wanafunzi wa madrasa, mapishi ya akina mama,makongamano ya kiuchumi na maadili.
 Sharif Said Jafari Swadiqu Bin Sayeid Muhammad (wa tatu kutoka kulia) akiomba dua kabla ya kuweka jiwe la Msingi kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza jana.
 Sharif Said Jafari Swadiqu Bin Sayeid Muhammad (wa tatu kutoka kushoto) akifungua pazia kuashiria kuweka jiwe la Msingi la UJENZI wa Msikiti wa BAKWATA Mkoani Mwanza jana.
 Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakimsikiliza Sharif Said Jafari Swadiqu Bin Sayeid Muhammad (aliyesimama) wakati akizungumza kabla ya kuweka jiwe la Msingi la UJENZI wa msikiti wa BAKWATA mkoa wa Mwanza utakaoitwa Masjid Abubakar Zuberi.Walioaa wa tatu kutoka kushoto ni Sheikh Hassani Kabeke, sheikh wa Mkoa wa Mwanza.
 Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikh Hassani Kabeke akizungumza na waandishi wa habari mar baada ya kuzinduliwa kwa UJENZI wa msikiti wa BAKWATA mkoani humu jana. Picha zote na Baltazar Mashaka

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA HAROUN ALI SULEIMAN AZUNGUMZA NA WAANDISHI ZANZIBAR

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya kuzuia rushwa na Uhujumu Uchumi Mussa Haji Ali akitolea ufafanuzi juu ya Siku ya kupambana na Rushwa Afrika katika mkutano wa Waandishi wa Habari na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman kuzungumzia siku ya kupambana na Rushwa na Uhujumu uchumi ambayo huadhimishwa kila ifikapo 11/07/2019 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio Mazizini Zanzibar. 
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Yakut Hassan Yakut akitoa maelezo na kumkaribisha mgeni Rasmi katika Mkutano wa Waandishi wa Habari na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman kuzungumzia siku ya kupambana na Rushwa na Uhujumu uchumi ambayo huadhimishwa kila ifikapo 11/07/2019 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio Mazizini Zanzibar. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Waandishi wa Habari na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman kuzungumzia siku ya kupambana na Rushwa na Uhujumu uchumi ambayo huadhimishwa kila ifikapo 11/07/2019 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio Mazizini Zanzibar. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na namana Serikali inavyofanya jitihada za kuzuia rushwa na uhujumu uchumi katika siku ya kupambana na Rushwa na Uhujumu uchumi ambayo huadhimishwa kila ifikapo 11/07/2019 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio Mazizini Zanzibar. 

PICHA NA YUSSIF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

WAZIRI WA AFYA HAMAD RASHID AWAAGA MADAKTARI WA KICHINA ZANZIBAR

$
0
0

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum akitoa hotuba ya Shukrani kwa Madakari wa Kichina katika Hafla maalum ya kuwaaga baada ya kumaliza muda wao ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitoa hotuba katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari wa Kichina baada ya kumaliza muda wao ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
 Kiongozi wa Timu ya Madaktari wa Kichina waliomaliza muda wao wa kutumikia Dk,Zhang Zhen akitoa hotuba ya shukrani katika Hafla maalum ya kuwaaga baada ya kumaliza muda wao ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
 Kiongozi wa Timu ya Madaktari wa Kichina waliofika Nchini DK,Yang Xiaodong akitoa hotuba yake katika hafla maalum ya kuwaaga wenzao waliomaliza muda wao ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
 Waziri wa Afya Hamad Rashid (kulia)akimpa zawadi kiongozi wa Timu ya Madaktari waliomaliza muda wao Dk,Zhang Zhen katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari wa Kichina baada ya kumaliza muda wao ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
 Baadhi ya Madaktari wa Kichina waliohudhuria katika Hafla maalum ya kuwaaga baada ya kumaliza muda wao wa kutumikia ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Afya na Madaktari wa Kichina katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari hao baada ya kumaliza muda wao ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar. 
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA RAIS WA MISRI

$
0
0

*Wazungumzia namna ya kuimairisha 
ushirikiano baina ya nchi hizo mbili

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah Al- Sisi, ambapo wametumia fursa hiyo kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za Tanzania na Misri.

Mbali na kuzungumzia masuala hayo ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kisiasa, kiuchumi na kijamii, pia Waziri Mkuu amemfikishia Rais wa Misri salamu kutoka kwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Mazungumzo baina ya Waziri Mkuu na Rais wa Misri yamefanyika leo (Jumatano, Juni 10, 2019) Ikulu jiji Cairo, ikiwa ni katika siku ya tatu na ya mwisho ya ziara yake ya kikazi nchini Misri. Katika ziara hiyo ameambatana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga.

Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya kikazi nchini Misri ambapo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cairo ameagwa na Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi wa Misri, Dkt. Ezz Eldien Abo Setit.

Akiwa ziarani nchini Misri, Waziri Mkuu alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly katika siku yake ya kwanza ya ziara yake, ambapo aliwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Misri waje kuwekeza nchini.

Pia, Waziri Mkuu alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo nchini humo ambayo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa makao makuu mapya ya nchi hiyo, mradi wa awamu ya pili ya upanuzi wa mfereji wa Suez Canal na kiwanda kikubwa cha ngozi.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fatah Al Sisi, katika Ikulu ya Rais, mjini Cairo, Julai 10.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fatah Al Sisi, katika Ikulu ya Rais, mjini Cairo, Julai 10.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

SAMATTA ASAINI MKATABA KUWA BALOZI WA UTALII KUTANGAZA VIVUTIO VYA TANZANIA NJE YA NCHI

$
0
0
Na Humphrey Shao,Michuzi Tv Dar es Salaam

Mchezaji wa soka wa kimataifa na kulipwa anayekipiga na klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji na nahodha wa kikosi Cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Sammata amesaini mkataba wa kuwa balozi wa Utalii kutangaza vivutio vya Tanzania nje ya Nchi.

Akizungumza na Waandishi was Habari mapema leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kusaini mkataba huo Samatta Amesema kuwa mkataba huo wa kujitolea utaanza Leo na utadumu kwa kipindi Cha miaka miwili.

"Mkataba huu nimesaini leo sio wa malipo kwani Mimi Kama kijana mzalendo nitaendelea kuitangaza Tanzania nje ya Nchi rasmi Kama balozi mteule wa bodi ya Utalii hivyo kazi hii naifanya kwa moyo wangu wote bila ya kupata malipo yoyote kutoka bodi hivyo ileweke hivyo"Amesema Samatta.

Akizungumza kwa niaba ya bodi ya Utalii Tanzania Mkurugenzi wa bodi hiyo Devota Mdachi Amesema kuwa makubaliano waliyotiliana saini leo ni ya kumfanya Samatta kuwa balozi wa hiari wa Utalii wa Tanzania popote pale atakapokuwa Duniani.

"Heshima ya ubalozi wa Utalii wa Tanzania tunaitoa kwa watu mbalimbali watanzania na hata wasio watanzania ili mradi tu ni watu waliokidhi vigezo na ambao tunaamini wanamapenzi na uzalendo kwa Nchi yao na wanaweza kweli kutusaidia kuvitangaza vivutio vyetu na utalii wetu wa Tanzania" Amesema Mdachi.

Amesema kwa mujibu wa mkataba huo bodi ya Utalii pamoja na mambo mengine TTB itakuwa ikimuandalia Samatta ziara za kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya Utalii angalau Mara Mona kila mwaka.

Ametaja ziara hiyo Samatta ataruhusiwa kuambatana na watu wasiozidi watano wakiwemo Waandishi was Habari ambapo gharama za usafiri wa ndani,malazi na chakula vutabebwa na TTB hivyo Samatta atachagua muda atakaikuwa na nafasi ya kufanya ziara hiyo.

Amesema pia TTB itatumia picha za Mbwana Samtta kwa ajili ya matangazo mbalimbali ya kuhamasisha Utalii iwe kwa njia ya televisheni ,radio ,mabango ya matangazo na kadhalika.
 Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Mshambuliaji wa Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta akibadilishana mkataba na Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Tanzania, Devota Mdachi
 Mwenyekiti wa bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomasi Mihayo akijadili Jambo na Mbwana Samatta na Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Tanzania Devota Mdachi Mara baada ya mkutano wao na wanahabari
Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Tanzania,Devota Mdachi akifafanua Jambo kwa Waandishi wa Habari leo juu ya ziara ya China na Korea ya kusini.

 Mwenyekiti wa bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji      Thomas Mihayo akizungumza na Waandishi wa juu ya tathmini ya ziara ya China na Korea.
 Jaji Thomasi Mihayo akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.
 Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania na Mshambuliaji wa Klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kabla ya kusaini mkataba wa kuwa balozi wa kutangaza vivutio vilivyopo Nchini.

 Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Tanzania,Devota Mdachi pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa na Mshambuliaji wa Klabu ya Genk, Mbwana Samatta wakisaini makubaliano ya Samatta kuwa balozi wa Utalii nje ya Tanzania.

TTB YAELEZA MAFANIKIO ZIARA YA CHINA NA KOREA KUSINI KUTANGAZA UTALII

$
0
0

Na Humphrey Shao, Michuzi Tv Dar es Salaam

Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) imetoa tathmini ya ziara ya kikazi kutangaza na kutafuta masoko ya Utalii katika nchi za uchina na Korea ya kusini .

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa bodi hiyo Jaji Thomas Mihayo amesema kuwa miongoni mwa matunda ya ziara hiyo ilikuwa ni kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya bodi ya Utalii Tanzania na kampuni ya Touchroad international holding group ambayo imepanga kuleta watalii 10,000 kutoka China katika kipindi Cha mwaka 2019.

"Lengo kuu la ziara ya utangazaji Utalii ilikuwa ni kuhakikisha kuwa Tanzania inaongeza sehemu ya umiliki wa soko kwenye solo la Utalii la China kwa kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania,fursa za uwekezaji zilizopo nchini na safari za ndege za ATCL kwenda China" Amesema Jaji Mihayo.

Katika ziara ya Korea ya kusini Jaji Mihayo Amesema kuwa walifanya mazungumzo na kampuni ya Utalii inayoongoza kwa kutoa watalii nje ya Korea ya kusini na kuzihamasisha kuleta watalii wao nchini Tanzania kampuni hizo ni pamoja na kampuni ya Hanjin na HanaTour.

Jaji Mihayo ametaja kuwa walitumia fursa hiyo kuwaalika katika maonyesho ya Utalii yanayoandaliwa na TTB yajulikanayo kama Swahili international Tourism Expo(SITE) ambayo mwaka huu yatafanyika 20 Oktoba jijini Dar es Salaam na kampuni hizo zimekubali mwaliko.

Amesema Mkurugenzi wa kampuni ya shoestring travels ambayo inaongoza kwa Utalii wa upandaji milima Amesema kampuni yake ipo tayari kushirikiana na TTB katika kutangaza mlima Kilimanjaro na kuhamasisha watalii kutoka Korea kupanda mlima huu pamoja na kutangaza milima mingine Tanzania.

Alisema bodi ya Utalii Tanzania kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Korea ya kusini tunatarajia kuandaa ziara ya utangazaji Utalii (roadshow) ambapo wataweza tutaweza kukutana na kampuni nyingine zaidi za korea ya kusini .

Alimaliza kwa kusema katika ziara hiyo ya Korea ya kusini waliweza kufanikiwa kutembelea bustani ya Taifa ya Suncheon iliyopo katika mji wa Suncheon , na kukutana na uongozi wa bustani hiyo ambao umetoa eneo la umubwa was mita za mraba 1000 kwa ajili ya kutangaza Utalii katika bustani hiyo kwa kuanzisha bustani yenye taswira ya Tanzania.

Ametaja Tanzania ni Nchi ya Kwanza kwa bara la afrika kupata eneo katika bustani hiyo ambapo Nchi zingine zilizopata eneo hilo ni pamoja na Uholanzi, Mexico, Japan, Italia,Ufaransa, of China,Marekani, Uingereza na Uturuki.
Mwenyekiti wa bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji      Thomas Mihayo akizungumza na Waandishi  kuhusua tathmini ya ziara ya China na Korea.

MANGULA AKUTANA NA MAKAMU WAZIRI MKUU WA VIETNAM JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula leo amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Vietnam, ukiongozwa na Makamu Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ndugu Trinh Dinh Dung, katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao, walijikita zaidi katika mahusiano baina ya Chama Cha Mapinduzi na Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam na Serikali zinazoongozwa na vyama hivyo.
"Kwa kweli Sisi CCM na Serikali yake tunaridhirika na kufurahia sana jinsi Chama Cha Kimomunisti na Serikali yake ya Vietnam vinavyotupa ushirikiano katika masuala mbalimbali ya kisiasa na kimaendeleo", alisema Mangula.

 Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula akimkaribisha Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam Ndugu Trinh Dinh Dungkwa  katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula akimpa zawadi  Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam Ndugu Trinh Dinh Dungkwa  kabla ya kufanya mazungumzo na Ujumbe wake  katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula akipokea zawadi kutoka Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam Ndugu Trinh Dinh Dungkwa  kabla ya kufanya mazungumzo na Ujumbe wake  katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula katika mazungumzo na Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam Ndugu Trinh Dinh Dungkwa na Ujumbe wake  katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula akiwa na Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam Ndugu Trinh Dinh Dungkwa baada ya kufanya mazungumzo na Ujumbe wake  katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula katika picha ya pamoja na Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam Ndugu Trinh Dinh Dungkwa  na Ujumbe wake  katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.

RC MAKONDA ATANGAZA ZAWADI NONO KWA WADAU WA MITANDAO

$
0
0



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Julai 11 ametangaza Shindano litakakalohusisha Watu wote wanaoendesha Platform za Social Media ikiwemo Waandishi wa habari Blog, Website, Online Tv, Instagram, Twitter, Facebook na nyinginezo ambapo watakuwa na jukumu la kuuliza wananchi maswali kuhusu Jumuiya ya Nchi za SADC ambapo washindi wa shindano hilo watajishindia kitita cha mamilioni ya Fedha.

RC Makonda amesema utaratibu wa kushiriki Shindano hilo ni Wahusika kwende kwenye sehemu za Bar,Saloon,Vijiwe vya bodaboda na Sokoni kisha kuwahoji wananchi waeleze namna wanavyoifahamu jumuiya ya SADC na kurusha mahojiano hayo kwenye platform zao ambapo pia wananchi watakaoweza kutoa majibu kwa ufasaha nao watapatiwa kiasi cha shilingi Laki moja.

Aidha RC Makonda amesema Mshindi wa kwanza wa shindano hilo atapatiwa kiasi cha Shilingi Milioni 3, Mshindi wa pili Milioni 2 na Mshindi wa tatu Milioni 1 ambapo hafla ya kukabidhi zawadi hizo itafanyika August 05 mwaka huu.

Hata hivyo RC Makonda amewataka Wamiliki wa Platform za Social Network kudhihirishia jamii kuwa mitandao yao ina uwezo mkubwa wa kubadilisha jamii kama ikitumika vizuri ambapo kwa kufanya hivyo watazidi kuheshimika na pia kuingiza pesa kupitia matangazo.

Huu ni mkakati wa RC Makonda kuendelea kuboresha maisha ya vijana waliojiajiri na kuajiri wenzao kupitia mitandao ya kijamii akiamini kupitia mitandao hiyo wanaweza kupata kipato kikubwa na serikali ikapato kodi.

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3 BAADA YA KUKIRI KOSA LA KUMUUA KAKA YAKE BILA KUKUSUDIA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Rukia Ally, (18) kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kukiri kosa la kumuua bila ya kukusudia kaka yake wa tumbo moja.

Mshtakiwa, mapema mahakamani hapo alisomewa kosa la mauaji ya kukusudia na kulikana lakini upande wa mashtaka ulidai kuwa kutokana na ushahidi walionao waliomba kubadirisha hati ya mashtaka na mshtakiwa huyo akasomewa kosa la kuua bila kukusudia ambapo amekiri kosa hilo na ndipo akakumbushwa shtaka lake.

Akisoma Hukumu hiyo, Msajili wa Mahakama Kuu Pamela Mazengo amesema, mahakama imemkuta mshtakiwa na hatia na inamuhukumu kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani.

Awali mshtakiwa hiyo alikuwa akikabiliwa na shtaka la mauaji ya kukusudia lakini kufuatia ushahidi uliopokelewa na upande wa mashtaka, wameona kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa la mauaji ya bila kukusudia.

Akimsomea upya shtaka lake, Wakili wa serikali Mwasiti Ally, amedai, Januari 23,2015 huko Mivumoni eneo la Madale, katika Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa bila ya kukusudia alimuua kaka yake Said Ally.

Hats hivyo, kabla ya kusomewa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Mwasiti Ally, alimsomea mshtakiwa Maelezo ambapo alidai:

Marehemu alikuwa ndugu wa damu na mshtakiwa na wote walikuwa wakiishi na wazazi wao huko Mivumoni Madale ambapi Siku ya tukio majira ya jioni marehemu alirudi nyumbani kwao na kumkuta dada yake (mshtakiwa), ambae aliondoka nyumbani hapo kwa siku tatu bila kuonekana akiwa chumbani kwake.

Ameeleza kuwa, marehemu alimgongea mlango mshtakiwa (dada yake) chumbani humo na akamfungulia mlango na kutoka nje ambapo alimuuliza siku tatu zilizopita alikuwa wapi lakini hakumjibu kitu kitendo ambacho kilipelekea marehemu kukerwa na kwa kuwa alikuwa ameshika fimbo alianza kumchapa Mshtakiwa miguuni.

Ameendelea kueleza kuwa, wakati tukio hill linatokea marehemu alikuwa ameshikilia kisu mkononi, hivyo Mshtakiwa akampokonya na bahati mbaya akakumchoma nacho kifuani upande wa kushoto ndipo marehemu akadondoka chini huku damu nyingi zikimtoka huku mshtakiwa akakimbia

Mama wa marehemu baada ya kusikia purukushani ile alitoka na kwenda kumsaidia marehemu kwa kuomba msaada kwa majirani pamoja na ndugu ambapo baada ya hapo walienda polisi kutoa taarifa ndipo wakampeleka Hosp. Lakini walipofika wakathibitishiwa kuwa alikuwa amekwishafariki na walielezwa kuwa sababu ya kifo cha marehemu ni kutokwa na damu nyingi kulikosababishwa na kuchomwa kisu.

Ameeleza kuwa, Mshtakiwa baada ya kukamatwa alipelekwa kwa mlinzi wa amani mahakamani ya Mwanzo Kawe.Mshtakiwa kabla ya kusomewa adhabu yake, amekiri kuwa hivyo ndivyo ilovyotokea. 


Siridhishwi na kasi Mkandarasi anayetekeleza mradi wa REA, Kibondo Kigoma-Mgalu

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha umeme katika moja ya
saloni za kiume katika kijiji cha Nyange wilayani Kibondo mkoani Kigoma
alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini( REA) 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( mwenye kilemba cheusi) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Lois Peter Bura (mwenye Kaunda suti) mara baada ya kuwasha umeme katika kijiji cha Nyange na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini( REA) katika wilaya hiyo.

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu( kushoto) akiteta jambo na Meneja
wa Shirika la Umeme mkoani Kigoma, Mhandisi Masingija Lugata(kulia)
wakati wa mkutano na wananchi wa kijiji cha Nyange hawapo
pichani,Naibu Waziri alifika kijijini hapo kuwasha umeme na kukagua
maendeleo mradi wa usambazaji umeme vijijini( REA).
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Lois Peter Bura, akizungumza na wananchi
wa Kijiji cha Nyange hawapo pichani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa
Nishati ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika
Wilaya ya Kibondo na kuwasha umeme katika kijiji cha Nyange. 



Na Zuena Msuya, Kigoma 


Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu,amesema haridhishwi na kasi ya
usambazaji wa umeme vijijini inayofanywa na mkandarasi wa Kampuni ya
Urban and Rural Engineering Services, wilayani Kibondo mkoani Kigoma. 

Mgalu ametoa kauli hiyo,kwenye mkutano na wananchi wakati alipofanya
ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini wilayani
humo na kuwasha umeme katika kijiji cha Nyange. 

Mgalu alisema kuwa, mkandarasi huyo amekuwa akitekeleza mradi huo
kwa kusuasua na hivyo kusababisha hofu kwa wananchi pamoja na
kuwakatisha tamaa kuwa huenda mradi huo usikamilike licha ya wananchi
hao kujiandaa kuupokea. 

Hata hivyo Mgalu aliongeza kuwa, mkandasi huyo tayari alikwisha lipwa
fedha zake ili kutekeleza mradi huo na kwamba endapo atashindwa
kutekeleza kwa muda uliopangwa basi sheria itachukuwa mkondo wake
kulingana na mkataba. Sambamba na hilo amemtaka mkandarasi huyo kuwepo eneo la mradi muda wote,pia kuongeza nguvu kazi katika kutekeleza mradi huo. 

Alifafanua kuwa Mkandarasi huyo anatakiwa kukamilisha mradi huo ifikapo mwezi Juni mwaka 2020 kwa kuunganisha vijiji 40 katika wilaya ya
Kibondo vilivyo umbali wa kilometa 283, lakini mpaka sasa ameunganisha
vijiji 3 tu, na kusimamisha nguzo umbali wa kilometa 90 zililovutwa nyaya
umbali wa kilometa 50 tu. 

“Kasi ya mkadarasi huyu katika kutekeleza mradi wa usambazaji wa
umeme vijijini hapa Kibondo hairidhishi kabisa, idadi ya vijiji vilivypo na
vilivyounganishwa ndogo mno,pia anafanya kazi kwa kusuasua na
akiendelea hivi serikali haitamvumilia itafanya maamuzi magumu, tunataka
wananchi wote wapate umeme kwa wakati, fedha alishalipwa,” Alisisitiza
Mgalu. 

Mbali ya kuwepo kwa changamoto hiyo, Mgalu aliwatoa hofu wananchi kwa
kuwataka kutokata tamaa na kwamba waendelee kusuka nyaya katika
nyumba zao kwakuwa mradi huo utatekelezwa kama ulivyopangwa wote
wataunganishiwa umeme. 

Pia aliwasisitiza kuwa malipo ya kuunganisha umeme katika nyumba zao ni
shilingi 27,000 tu na wasikubali kulipa zaidi na endapo itatokea mtu anadai
fedha zaidi basi watoe taarifa sehemu husika ili watu hao waweze
kushughulikiwa.Vilevile wananchi hao wasikubali kuuziwa vifaa vya umeme kama vilenguzo pamoja LUKU kwa kuwa vifaa hivyo hutolewa bure kwa wananchiwote. 

Kwa upande wake Meneja mradi wa kampuni ya ukandarasi ya Urban and
Rural Engineering Services, amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na
kueleza sababu kubwa ilikuwa ni kukwama kwa vifaa bandarini. 


Hata hivyo amesema kuwa sasa wamepata suluhisho hivyo muda wowote
vifaa hivyo vitafika katika eneo la mradi na watanzaa kufanya kazi usiku na
mchana kufidia muda waliopoteza. Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Lois Peter Bura, amewataka wananchiwa Kibondo kuendelea kuilinda miundominu ya umeme iliyopo katikamaeneo yao na kwamba mradi huo utatekelezwa kulingana na mkataba. 


Vilevile amemtaka mkandarasi kushirikiana na ofisi ya Wilaya na kueleza
pale walipokwama ili kutatua changamoto zilizopo kwa manufaa ya
wananchi.

SERIKALI YASHUSHA NEEMA KWA WANANJOMBE

$
0
0
Na WAMJW-NJOMBE
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeshusha neema kwa Wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kutenga kiasi cha shilingi Bilion 7.6 kwaajili ya ujenzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ili kuboresha huduma kwa Wananchi. 

Hayo yamejiri leo wakati wa zoezi la Uzinduzi wa huduma za Afya na lililoongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe iliyofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika uzinduzi huo, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha huduma za Afya katika Mkoa wa Njombe ikiwemo kujenga jengo la wazazi la ghorofa tatu, jengo la maabara, jengo la wagonjwa mahututi na jengo la upasuaji gorofa mbili, wodi za wagonjwa gorofa tatu, nyumba za Watumishi tano, pamoja na kichomea taka.

" Tunajenga jengo la wazazi la ghorofa tatu, tunajenga jengo la jengo la maabara, tunajenga jengo la wagonjwa mahututi na jengo la upasuaji gorofa mbili, tunajenga wodi za wagonjwa gorofa tatu, tunajenga jengo la kufulia, tunajenga kichomea taka na tunajenga nyumba za watumishi tano" alisema Waziri Ummy. 

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amemwagiza Mkandarasi wa Hospitali hiyo kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa majengo hayo hayo ndani ya miezi kumi ili wananchi wa Mkoa wa Njombe waanze kufaidika na huduma za Afya katika Hospitali hiyo, huku akiwatoa hofu wananchi kuwa pesa zote zipo tayari. 
Mbali na hayo, Waziri Ummy mewaasa Wananchi kupambana dhidi ya magonjwa yasiyo yakuambukiza kama Kisukari, shinikizo la damu, Saratani na magonjwa ya Moyo kwa kubadilisha mtindo wa maisha ikiwamo ulaji mlo sahihi , kuacha uvutaji wa sigara na tumbaku, kuacha unywaji wa pombe kupita kiasi pamoja na kutofanya mazoezi mara kwa mara.

Aidha, Waziri Ummy ametoa with kwa vijana kujiepusha na mambo ambayo yatapelekea kipata maambukizi ya VVU, huku akiweka wazi kuwa maambukizi mapya ya VVU ni 82,000 kila mwaka nchini Tanzania, huku katika kila watu 100, watu 40 ni vijana wenye umri kati ya 15 hadi 24 umri ambao ni nguvu kazi ya taifa.

"Tunatambua kwamba kuna maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi Mkoani Njombe,lazima tuzingatie kanuni za kujikinga na maambukizi ya VVU, kujizuia kufanya mapenzi kwa vijana hasa kwa wasichana ambao muda wao haijafika, pili kuwa mwaminifu kwa mwenza wako au mpenzi wako na tatu kutumia kinga" alisema Waziri Ummy 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amewatoa hofu wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kuweka wazi kuwa huduma za Afya katika Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe haitoathiri utoaji huduma katika Hospitali ya Kibena iliyokuwa Hospitali ya Mkoa, ambayo kwa sasa imerudishwa chini ya Halmashauri ya Mji wa Njombe. 

"Na mimi ntahakikisha wale Watumishi ambao tilikubaliana waje kwenye Hospitali hii, waje na nguo zao , vifaa vyote waviache Kibena na huduma ya Kibena iendelee, na kazi ya Hospitali hii Mhe. Ummy Mwalimu na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wataweka vifaa vyote vitakavyohitajika na huduma zitaendelea" alisema Mhe. Olesendeka 

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Mhe. Edwirn Mwanzinga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Afya kwa kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba jambo linalosaidia kuokoa kwa kiasi kikubwa maisha ya Wananjombe.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka wakiongea na Wazee waliofika kupata huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe wakati alipofanya uzinduzi wa huduma  za Afya katika Hospitali hiyo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwa uongozi wa Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe  wakati alipotenbelea kukagua chumba cha kuhifadhia Dawa katika Hospitali hiyo, wakatikati (mwenye Koti jeupe) ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe Dkt. Kyambile.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua kadi inayoonesha kiasi cha dawa kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe pindi alipofanya ziara ya kuzindua Huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akieleza juu ya umuhimu wa kuwepo kwa mabango yanayohamasisha haki ya mgonjwa kupata  huduma  za Afya zilozo Bora wakati wa  uzinduzi wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, kushoto kwake (mwenye Koti jeupe) ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe Dkt. Kyambile.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali moja kati ya wagonjwa waliofika kupata matibabu kwa mara ya kwanza katika Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, ni baada ya kufanya  uzinduzi wa  huduma za Afya katika Hospitali hiyo, Kulia kwake (mwenye Koti jeupe) ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe Dkt. Kyambile.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka wakati wa uzinduzi wa Huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipanda mti wa matunda (mpalachichi) ikiwa ni ishara ya kuhifadhi mazingira, shughuli iliyofanyika baada ya uzinduzi wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.
 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka akipanda mti wa matunda (mpalachichi) ikiwa ni ishara ya kuhifadhi mazingira, shughuli iliyofanyika baada ya uzinduzi wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ulioongozwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi ramani ya ujenzi wa majengo mengine mapya saba  kwa Mkandarasi, shughuli iliyofuata baada ya uzinduzi  wa huduma katika Hospitali hiyo ya Rufaa  ya Mkoa wa Njombe.
 Moja kati ya vyumba vya Wagonjwa kilicho na vitanda pamoja na mashine zakutambua hali ya Mgonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, iliyoanza kutoa huduma rasmi Julai 10, baada ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kufanya uzinduzi huo
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka baada ya uzinduzi  wa huduma katika Hospitali hiyo ya Rufaa  ya Mkoa wa Njombe.

WANANCHI WILAYANI NYASA WAMPONGEZA KAMANDA WA POLISI RUVUMA

$
0
0
Na Netho Sichali, Afisa habari wilaya ya Nyasa
Wananchi wa Kata ya Mpepo Wilayani Nyasa, wamempongeza Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Ruvuma Simon Maigwa, kwa kuwahakikishia usalama wa mali na maisha licha ya kuishi Karibu na mpaka wa Tanzania na Msumbiji. 
Wananchi hao, wametoa pongezi kwa kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma, katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Lunyele kata ya Mpepo Wilayani Nyasa hivi karibuni. Mkutano aliokuwa na lengo la kuimarisha ulinzi shirikishi katika eneo la mpakani mwa Nchi ya Tanzania na Msumbiji. 
Wananchi hao walifafanua kuwa awali, kulikuwa na matukio yaliyokuwa yakiwapa hofu ya kufanya kazi zao, kwa kuwa ilikuwa haiwezekani kwenda hata kulima shambani, lakini mara baada ya kuimarisha Ulinzi na Usalama, sasa wanafanya kazi zao kwa amani, na kumtaka Kamanda huyo kuwapa kibali cha kujenga kituo cha Polisi katika Tarafa ya Mpepo ili kuweza kukabiliana na matukio ya kihalifu katika Tarafa ya Mpepo kwa kuwa ni tarafa inayopakana na Nchi jirani Ya Msumbiji. 
Wananchi hao waliongeza kuwa wana imani na kamanda huyo, kwa kuwa tukio linapotokea huwa anakuja mwenyewe, bila kutuma mwakilishi na hata leo katika mkutano wa kuimarisha ulinzi shirikishi na usalama wewe mwenyewe umekuja. 
“Kamanda wa Polisi sisi tuna imani kubwa sana na wewe kwa kuwa kila mara umekuwa pamoja na sisi bila kutuma mwakilishi unafika wewe mwenyewe. sisi sote uliyozungumza tumeyaelewa na tutayafanyia kazi na tunakupongeza sana kwa juhudi zako za ufanyaji kazi wako alisema Kiliani Kumburu huku akishangiliwa na wananchi wengine” . 
Kamanda huyo akiongea na wananchi hao katika mkutano huo wa hadhara, aliwahakikishia Usalama wa mali na maisha yao, na kuwataka wafanye kazi za kujenga taifa bila woga wowote kwa kuwa mkoa wa Ruvuma ni salama na hakuna tatizo lolote na atakayeingia kwa kujaribu kuhatarisha Usalama kamwe hataweza,na hatatoka salama. 
Aliongeza kuwa kuhusu ombi la ujenzi wa kituo cha polisi cha kisasa kitakachohudumia Tarafa ya Mpepo Wilayani hapa, amelipokea na hana pingamizi lolote na atashirikiana nao kwa hali na mali katika kutatua changamoto za ujenzi huo, na atawaletea polisi na vifaa kwa ajili ya kuhakikisha jamii inakuwa salama muda wote na wanafanya kazi bila uoga wowote. 
“Napenda kuwaeleza ndugu wananchi wa kata hii ya Mpepo kuwa Ruvuma ni salama kila mtu aendelee kufanya shughuli zake za kujiletea maendeleo,yeyote atakayejaribu kuingia na kujaribu kutishia amani wananchi kamwe, hatatoka salama. 
"Na nimesikia mnahitaji kujenga kituo cha Polisi hakuna tatizo tushirikiane tujenge na mimi nitaleta Askari mara baada ya kujenga kituo cha kisasa cha polisi kataka kijiji cha tingi ambapo ni makao makuu ya Tarafa ya Mpepo”alisema kamanda Maigwa. 
Aliongeza kuwa katika kila Kata ameleta polisi Kata ambaye anatakiwa Kuishi katika kata husika na kuhakikisha ulinzi na Usalama unaimarika kila kata. Hivyo aliwataka wamnanchi hao kushirikiana na Polisi kata aliyeletwa. 
Aidha katika hatua nyingine aliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Polisi, cha Tarafa ya Mpepo ambapo jumla ya shilingi laki mbili na ishirini na nne elfu (224,000/=) zilipatikana na kukabidhiwa kwa Ofisa Tarafa wa Tarafa ya Mpepo. 
Naye Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya hii aliwataka wananchi kuhamasika na kujitoa kwa dhati kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha polisi kwa kila kaya kuchangia nguvu zao kwa kuwa, ulinzi ni muhimu sana katika jamii.
Kwa sasa kituo kilichokuwepo ni kidogo ambacho hakina uwezo wa kuhudumia Tarafa yote ya Mpepo. Pia aliwataka viongozi wa serikali ya vitongoji, Kijiji, na Kata zote kuwa na Daftari la kusajli wageni wote wanaoingia ili kuweza kujua ni wahalifu au ni raia wema. 
 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma Simoni Maigwa ,akiongea na Wananchi wa Kitongoji cha Dar pori kijiji cha Lunyere, kata ya Mpepo Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma hivi karibuni, Wakati akihamasisha Ulinzi shirikishi katika maeneo ya Mpakani mwa Nchi ya Tanzania na Msumbijiili amani iwepo. Picha na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa
 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma Simoni Maigwa akisalimiana na Wananchi wa Kitongoji cha Dar pori kijiji cha Lunyere, kata ya Mpepo Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma hivi karibuni, Wakati akihamasisha Ulinzi shirikishi katika maeneo ya Mpakani mwa Nchi ya Tanzania na Msumbijiili amani iwepo. Picha na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa

THE TRENDY SHOW NA CYNTHIA MASASI MZIRAY AND COMPANY


MSHINDI WA NDONDO CUP JIMBO LA CHUMBUNI KUONDOKA NA GARI AINA YA KERI.

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Mwembemakumbi Ussi Salum Pondeza akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa kuhusu mashindano ya soka ya Vijana ya Jimbo hilo yajulikanayo kwa jina la “Jimbo la Chumbuni Ndondo Carry Cup” ambapo mshindi wa kwanza atazawadiwa gari aina ya Keri na mshindi wa pili shilingi milioni moja ikiwa ni moja ya ahadi alizoto kwa wapiga kura wake. 

Baadhi ya viongozi wa timu, waamuzi na wasimamizi wa mashindano ya Jimbo la Chumbuni Ndondo Carry Cup wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa 
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza akionyesha moja ya jezi ambazo zitatumika kwenye mashindano ya vijana ya Jimbo la Chumbuni “Jimbo la Chumbuni Ndondo Carry Cup” yatakayoanza tarehe 14.7.2019 katika Uwanja wa Saateni. 
Mwenyekiti wa mashindano ya Jimbo la Chumbuni Ndondo Carry Cup Shazil Foum Khamis akipokea ufunguo na namba ya gari ya mshindi wa kwanza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa iliopo mtaa wa Maruhubi.

SERIKALI YATOA BILION 7 UJENZI WA JENGO LA WAZAZI HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA.

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongoza msafara wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongozana na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifuatilia ramani ya ujenzi wa mradi wa ujenzi wa ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200. 
Ujenzi wa mradi wa ghorofa sita wenye gharama ya shilingi Bilion 7, katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200 ukiendelea katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya. 
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji baada ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya. 
……………………………………………….. 

Na WAMJW- MBEYA 

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya inajenga jengo la Wazazi lenye thamani ya shilingi Bilioni 7 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuboresha huduma za Afya kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nyanda za juu kusini. 

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na ujenzi wa miradi katika Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya. 

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imedhamiria kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya nchini ikiwemo huduma za kibingwa ili kuondoa usumbufu kwa Wananchi wanaohitaji huduma hizo kwa kusafiri umbali mrefu i jambo linalopelekea gharama kubwa na usumbufu kwa wananchi. 

“Tunajenga jengo la wazazi na watoto wachanga la ghorofa sita, ambalo litakuwa na jumla ya vitanda 200, vyumba vitatu vya upasuaji kwa ajili ya wanawake wajawazito ,vyumba sita kwa ajili ya uangalizi maalum (ICU) kwa wanawake wajawazito, pia vyumba maalum vinne kwa ajili ya vitoto vichanga (NICU)” alisema Waziri Ummy. 

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amemwagiza Mkandarasi wa majengo hayo kuhakikisha wanaharakisha ujenzi wa majengo hayo ili wananchi waanze kupata huduma mapema jambo litalosaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto nchini. 

Aidha, Waziri Ummy ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nyanda za juu kusini kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili kurahisisha gharama za matibabu. 

“Nitoe Wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nyanda za juu kusini ili waweze kufurahia huduma nzuri lazima wajiunge na huduma za Bima ya Afya, Kuna NHIF Toto Afya kadi kwa mtu yoyote mwenye umri wa chini ya miaka 18 ni shilingi 50,400 huduma mwaka mzima ndani ya Mbeya na Tanzania kwa ujumla” alisema Mhe. Ummy Mwalimu 

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa katika kila wanawake 100, wanawake 85 wanajifungua bila matatizo yoyote, huku akisisitiza kukamilika kwa ujenzi huu kutasaidia kukokoa wanawake 15 waliobaki kutokana na huduma Bora zakibingwa zitakuwa zikitolewa. 

Naye, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kukubali kutenga fedha ili kujenga jengo la ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200 jambo litalosaidia kutatua changamoto ya ufinyu wa nafasi. 

“Tunapenda kutoa shukurani za dhati kwa Serikali ya awamu ya tano, kwa kukubali kutenga fedha kupitia Wizara unayoiongoza ili kuweza kujenga jengo la ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta, ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda 200.” Alisema Waziri Ummy

Wafanyabiashara wa Nyama Arusha watishia kuteketeza Ngozi wanazozalisha baada ya kukosa soko

$
0
0
Na Woinde Michuzi Tv ,Arusha

Wafanyabiashara wa Nyama zaidi ya 135 katika jiji la Arusha wametishia kuanza kuziteketeza Ngozi za Mifugo wanazozalisha baada ya kuchinja Mifugo, kwa kile walichodai ni kushindwa kupata masoko ya uhakika ya zao hilo kufuatia kampuni zinazojihusisha na biashara hiyo kuwalipa kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne.

Wakiongea katika kikao cha Pamoja leo,mwenyekiti wa wafanyabiashara hao wa Nyama katika jijini la Arusha ,Alex Lasike amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kukata tamaa na zao hilo kutokana na kukosekana kwa masoko ya uhakika na bei ya zao hilo ikiendelea kuporomoka.

Amesema hali hiyo imewafanya wafanyabiashara hao kutishia kuachana na biashara ya Ngozi badala yake watakuwa wakiziteketeza kwa moto au kuwapa Mbwa kama chakula baada ya kampuni ya Salex Limited na Ngozi Center za jijini Arusha ,zinazonunua bidhaa hiyo kushindwa kuwalipa mamilioni ya fedha wanazozidai katika kipindi cha miaka Minne.

"Ni mwaka wa Nne tunauza Ngozi tena kwa bei ndogo ya shilingi 100 kwa kilo katika kampuni hizo binafsi lakini hatujawahi kulipwa kwa muda mrefu na watu wanazidi kuumia " Alisema Alex

Alifafanua kwamba kila siku wafanyabiashara hao wanachinja ng'ombe,Mbuzi na Kondoo zaidi ya 150 lakini Ngozi zinazopatikana zinakusanywa na kampuni hizo kwa ajili ya malipo, lakini hadi leo wanasotea malipo yao ya zaidi ya miaka minne.

Wameiomba serikali kuwatafutia soko la uhakika ili waachane na kampuni hizo zinazonunua kwa mkopo na kushindwa kuwalipa kwa wakati.

Baadhi ya wafanyabiashara wa Nyama,Katika jiji la Arusha, Hopson Minja na Elius Lazaro wamesikitishwa na kampuni ya Salex na Ngozi Center zinazonunua ngozi kushindwa kuwalipa fedha zao na kuitaka serikali iingilie kati ili wapate haki zao.

"Kwa mfano Mimi nadai zaidi ya sh,million nne sijalipwa kwa zaidi ya miaka minne ,tunaiomba serikali itusaidie kupata haki zetu pamoja na kututafutia soko la uhakika la Ngozi" Alisema Minja.

Mmoja ya wamikili wa kampuni ya Ngozi ya Salex Limited ya jijini Arusha, Mahsin Ghalib amesema biashara ya soko la Ngozi duniani imeporomoka kwa kiasi kikubwa kutokana na Nchi zilizokuwa zikinunua siku hizi hazinunui kwa wingi jambo linalopelekea biashara hiyo kudorora.

"Kiwandani kwangu kuna shehena ya Ngozi zaidi ya Kilo milioni 2.8 , sina mahala pa kuuzia masoko hakuna nchi zilizokuwa zikinunua siku hizi hawataki Ngozi za chumvi" Alisema Ghalib

Ameiomba serikali imsaidie kupata mkopo wa fedha ili anunue machine zitakazomsaidia kuchakata Ngozi hapa nchini na kuuza katika masoko ya ndani na nje ya Nchi.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Nyama katika jijini la Arusha ,Alex Lasike akiongea katika kikao chao  kilichofanyika leo jijini hapa

TEMESA TANGA YAALIKA WADAU KUSIKILIZA KERO ZAO

$
0
0
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mkoa wa Tanga jana umealika wadau wanaotumia huduma zake ili kujadilli na kupata mrejesho kuhusu namna zinavyotolewa. Kikao hicho cha wadau kilichoandaliwa na meneja wa mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina kilifanyika katika eneo la wazi la karakana ya wakala huo na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na wadau mbalimbali wa taasisi za umma, taasisi binafsi, wazabuni, pamoja na wauzaji wa vipuri vya magari na mitambo.

Awali, Akifungua kikao hicho, meneja wa TEMESA mkoa wa Tanga alisoma taarifa ya utendaji kazi kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 ambapo taarifa hiyo imeonyesha kiwango kikubwa cha ukuaji wa uzalishaji ambapo hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu uzalishaji wa mkoa huo umeweza kufikia zaidi ya shilingi Bilioni moja nukta tano sawa na asilimia tisini nukta nne ya uzalishaji wa mkoa.

Mhandisi Margareth alizungumzia pia changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ikiwemo kucheleweshewa malipo ya madeni wanayodai wateja hasa wa Umma, ‘’hadi kufikia Juni mwaka 2019 tunadai zaidi ya shilingi milioni mia sita, tunaendelea na usuluhishi wa madeni hayo na wateja wetu ili kuingiza deni sahihi katika taarifa zetu za fedha za mwaka,’’alisema.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle alieleza mabadiliko mbalimbali yanayotokea katika Wakala ambapo huduma za karakana zimeanza kusogezwa kwa wateja wa mbali hasa uanzishwaji wa karakana mpya za Wilaya ikiwemo uanzishwaji wa karakana ya TEMESA katika Halmashauri ya mji wa Ifakara ambayo tayari imekwishaanza kufanya kazi.

‘’TEMESA imeanza kubadilika, tuna mpango wa kuanzisha karakana katika Wilaya ya Same, Wilaya ya Simanjiro, Wilaya ya Korogwe pamoja na Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, tumesambaza vifaa vipya vya kisasa kwa ajili ya karakana kumi na mbili na tayari vingine vipo kwenye mchakato wa manunuzi’’. Alisema Mhandisi Maselle.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alimshukuru meneja kwa kumkaribisha kwenye kikao hicho kama mdau, pia aliipongeza TEMESA kwa ubunifu na hatua wanazochukua kutatua kero za wateja wao ambapo alisema malalamiko mengi kwa sasa yamepungua tofauti na hapo awali ambapo akiwa Wilayani Manyara malalamiko yalikuwa mengi sana na kwa sasa hayapo tena.

Nao baaadhi ya wadau walizungumzia kero zinazowakabili ikiwemo kucheleweshewa matengenezo ya magari, gharama kuwa juu pamoja na upungufu wa vipuri. Pia wadau hao waliomba mafundi wa karakana wapewe elimu ya kumhudumia mteja kwani wengi wao wamekuwa na kauli ngumu kwa wateja wao. 

Akijibu malalamiko hayo Mtendaji Mkuu alisema kucheleweshwa kwa matengenezo ni kutokana na kukosekana kwa vipuri katika karakana husika lakini tatizo hilo limekwishatatuliwa kwa kuwa sasa Mkoa wa Tanga una akiba ya kutosha ya vipuri, aliongeza kuwa Wakala sasa unaanzisha huduma ya kuhudumia wateja maarufu ambapo kipaumbele kitatolewa kwa wateja hasa wa magari ya viongozi ikiwemo wakuu wa Wilaya, wakuu wa Mikoa pamoja na Mawaziri ambao magari yao yatakuwa yakipatiwa huduma ya haraka pindi yanapofika katika karakana husika. Kikao kingine cha wadau kinategemewa kufanyika mkoani Kilimanjaro pamoja na mkoani Arusha siku ya Ijumaa.  
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akizungumza na wadau (hawapo pichani) wakati wa kikao cha wadau kilichoandaliwa na Wakala huo kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo, maoni na ushauri kuhusu huduma za TEMESA. Kikao hicho kilifanyika katika karakana ya mkoa wa Tanga. Kulia ni Meneja wa mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina na kushoto ni msaidizi wake Mahangaiko Ngoroma.
 Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katikati akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa TEMESA mkoa wa Tanga kilichofanyika katika karakana ya wakala huo kwa ajili ya kupata maoni, ushauri na changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau wa TEMESA mkoani humo. Kulia ni Meneja wa mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle
 Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina kulia akisoma taarifa ya utendaji kazi ya karakana ya Wakala wakati wa kikao cha wadau (hawapo pichani) kilichofanyika katika karakana hiyo. Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle na kushoto ni Meneja msaidizi wa mkoa huo Mhandisi Mahangaiko Ngoroma.
 Baadhi ya wadau walioshiriki katika kikao cha wadau wa TEMESA mkoa wa Tanga wakichangia mada mbalimbali kuhusu utolewaji wa huduma za karakana ya mkoa huo wakati wa kikao kilichofanyika katika karakana ya TEMESA mkoa wa Tanga. Kikao hicho kiliandaliwa na meneja wa mkoa huo kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau hao na namna ya kuzipatia ufumbuzi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katikati mara baada ya kumalizika kwa kikao cha wadau kilichofanyika katika karakana ya TEMESA. Kulia ni Meneja wa (TEMESA) mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA TANGA)

TANTRADE KUENDELEA KUJENGA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAFANYABIASHARA NA WAJASIRIAMALI WADOGO NCHINI.

$
0
0


MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imesema itaendelea kuimarisha mitandao ya wadau na makampuni mbalimbali wafanyabiashara ili kuhakikisha kuwa wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo nchini wanapatiwa fursa za masoko ili kuweza kukuza sekta ya biashara nchini. 

Hayo yamesemwa leo Alhamisi (Julai 11, 2019) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Zanzibar, Latifa Khamis wakati wa mkutano wa ana kwa ana baina ya wafanyabiashara, wazalishaji na wanunuzi wa bidhaa za ngozi na shule katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere. 

Latifa alisema kuwa Serikali kupitia TANTRADE itaendelea kutumia majukwaa na fursa mbalimbali za kibiashara kwa ajili ya kuwawezesha wajasirimali na wafanyabiashara kuweza kutumia fursa zilizopo ikiwemo kupata masoko ya uhakika ya biashara zao kupitia kwa wadau mbalimbali waliopo ndani na nje ya nchi. 

“TANTRADE imeandaa mkutano huu maalum kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo kuweza kupata fursa za masoko ya kuuzia masoko yao ambapo utaratibu huu utakuwa endelevu, hivyo kampuni ya DHL kupitia Market Plaze Africa wametoa fursa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wa hapa nchini kutangaza biashara zao” alisema Latifa. 

Aidha Latifa alisema mara baada ya kuisha kwa maonyesho ya 43 ya DITF, TANTRADE imeandaa mkakati maalum wa kuwaunganisha wajasiriamali wadogo na wafanyabiashara kupitia maonesho ya bidhaa za wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo nchi nzima ambapo wataanzia katika Mkoa wa Ruvuma na baadae Zanzibar. 

Aidha Latifa alisema katika mkutano huo pia TANTRADE imewakutanisha wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo na taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo Benki ya NMB ambayo imekuwa na utaratibu wa kutoa mikopo kwa wajasiriamali kuanzia kiwango cha Tsh 500,000 hadi Milioni 50,000,0000. 

Kwa upande wake Meneja Mkazi wa Kampuni ya DHL Tanzania, Paul Makolosi aliwataka wajasirimali na wafanyabiashara wadogo kutangaza bidhaa zao katika taasisi hiyo kwa kuwa masoko ya bidhaa zao yapo kwani nchi nyingi za mabara ya Ulaya na Amerika yamekuwa wakivutiwa na bidhaa zinazozalishwa katika nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania. 

Aliongeza kuwa taasisi hiyo ina uzoefu wa miaka 30 ya kufanya biashara duniani, ambapo katika utendaji kazi wake imekuwa ikiwasaidia zaidi wajasiriamali wadogo waliopo katika Bara la Afrika, hivyo ujio wa taasisi hiyo hapa nchini ni fursa kwa wajasiriamali na wafanyabiashara hao. 

“Katika Nchi za Bara la Ulaya na Amerika, bidhaa za ngozi hususani viatu vimekuwa na soko kubwa sana, na kwa kuwa wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo wa hapa Tanzania wamekuwa wakizalisha bidhaa hiyo, sisi DHL kupitia Market Place Africa tupo tayari kuwasaidia ili kupata masoko ya uhakika” alisema Makolosi. 
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images