Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110088 articles
Browse latest View live

VETA YAJA NA PIKIPIKI SALAMA KATIKA KUKOMESHA AJALI ZA BARABARANI

$
0
0
Na Leandra Gabriel,  Michuzi TV 
KATIKA kuhakikisha ajali za barabarani hasa zile zinazosababishwa na pikipiki zinapungua Mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) wamebuni pikipiki salama ambayo itahakikisha usalama wa dereva na abiria unazingatia. 

Akizungumza na Michuzi TV mwalimu wa masuala ya umeme kutoka VETA Kipawa Aneth Mganga amesema kuwa ubunifu huo wa pikipiki salama umewalenga madereva na abiria na hiyo ni katika kuhakikisha usalama wao pamoja na abiria unazingatia. 

Aneth amesema kuwa pikipiki hiyo salama imebuniwa kwa kuhakikisha dereva akitumia pombe, akienda mwendo wa haraka, kutovaa kofia ngumu,   kwenda mwendo mkali pamoja na kubeba abiria zaidi ya mmoja pikipiki hiyo haitaruhusu kabisa,  aidha itagoma kwenda au kumpeleka kwenye mwendo wa wastani kama atakuwa kwenye mwendo wa kasi. 

"Pikipiki hii ina mfumo maalumu dereva akinywa pombe,  asipovaa kofia ngumu na akibeba abiria zaidi ya mmoja haiwezi kuwaka na akienda mwendo wa kasi pikipiki hiyo itampeleka katika mwendo wa kawaida" ameeleza. 

Pia amesema kuwa kutokana na mchango mkubwa wa usafiri huo ambao umetoa ajira kwa vijana na kwa kuangalia changamoto zinazoukabili ikiwemo ajali za barabarani wao Kama wataalamu wakaona ni vyema kuangalia namna ya kutatua changamoto hiyo. 

Na amesema kuwa pikipiki hiyo ina mfumo wa usalama ambao utamsaidia dereva kutoa taarifa katika kituo anachofanyia kazi akiona mashaka juu usalama wake juu ya abiria aliyembeba. 

Pikipiki iyo salama imekuwa kivutio kikubwa katika maonesho ya 43 ya biashara maarufu Kama sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Mkufunzi wa masuala ya umeme kutoka VETA Kipawa Aneth Mganga akionesha pikipiki salama ambayo wameibuni ili kupunguza ajali za barabarani, leo jijini Dar es Salaam.

UVCCM ARUSHA WAASWA KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Katika kupata viongozi wanaofaa Vijana wametakiwa kuchagua viongozi ambao wanaakili ,busara ,hekima,uwelevu pamoja na wale ambao wataweza kuwaletea maendeleo katika kipindi chake cha uongozi.

Hayo yamebainishwa na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa vijana Jafari Mghamba wakati akiongea na vijana leo katika mkutano mkuu wa maalum wa uchaguzi wa mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Arusha (UVCCM) ambapo amewataka vijana kuacha kuchagua viongozi kwa miamko ,pamoja na ushabiki kwani kufanya hivyo ndio kunapelekea kupata viongozi ambao hawawezi kuleta maendeleo wala mabadiliko yoyote katika jamii.

Alisema kuwa wanatakiwa kuchagua viongozi ambao wataleta twaswira nzuri na maendeleo katika chama cha mapinduzi ,kwa kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.

Aidha aliwataka wananchi kuwachagua viongozi bora kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla wake ,alibainisha kuwa nivizuri tusiwachague viongozi kwa majaribio wala kwa ushabiki bali wanatakiwa kuchagua viongozi wananaofaa na tuliowazoea na tunaowajua vizuri tabia na mienendo yao.

"vijana wa UVCCM msifanye makosa ya kudanyanywa na kuchagua viongozi wasiofaa na ambao hatuwafahamu vizuri mimi naamini kiongozi mtakae mchagua leo ni bora na sio bora kiongozi "alisema msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu CCM taifa Livingstone Lusinde.

Alimalizia kwakuwatakia uchaguzi mwema ambapo alisema anaamini amani itaendelea kutawala katika umoja huu wa vijana mkoa wa Arusha huku akisisitiza atasimamia uchaguzi huu kwa kufuata sheria inayoongozwa na ilani ya CCM. 

Wagombea wanaogombea nafasi ya uwenyekiti wa vijana wa mkoa wa Arusha ni pamoja na Rovet Philimon,Omary Lumato pamoja na Suleman Msuya.
Wagombea  wa nafasi  ya uwenyekiti wa vijana  mkoa wa Arusha wakiwa katika  picha ya pamoja kabla ya uchaguzi kuanza.
 Baadhi ya vijana wa Uvccm wakiwa ndani ya ukumbi kabla ya uchaguzi kuanza


ZIADI YA WAFUNGWA 640 WAMENUFAIKA NA MPANGO WA BODI YA PAROLE NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITATU

$
0
0
Na Lucas Mboje, Jeshi la Magereza
BODI ya Taifa ya Parole ya Awamu ya Tano imeelezea mafanikio mbalimbali katika kipindi cha miaka mitatu ambapo Bodi hiyo imewezesha kuachiliwa jumla ya wafungwa 648 katika mpango huo wa Parole na hadi sasa hakuna mfungwa yeyote aliyevunja masharti ya Parole na kurudishwa gerezani.
Hayo yamesemwa mapema leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Agustino Mrema katika Kikao cha 41 cha Bodi hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Maafisa Magereza Ukonga, jijini Dare es Salaam.

 “Jumla ya wafungwa 666 wamejadiliwa na Bodi ya Taifa ya Parole katika vikao vyake saba vilivyofanyika na kupendekeza kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo wafungwa 648 wamenufaika na mpango huo na wafungwa 18 hawakupendekezwa kutokana na sababu mbalimbali”. Amesema Mhe. Mrema.

Amesema kuwa katika utendaji wa Bodi yake kwa miaka mitatu umechangia kuimarika kwa hali ya utulivu na usalama ndani ya magereza kwa wafungwa kwani wamekuwa na matumaini makubwa ya kuingizwa kwenye mpango huo sanjari na kupokea programu za urekebishaji katika magereza mbalimbali nchini.
Mafanikio mengine ni kuwa Wafungwa walioachiliwa katika mpango huo katika kipindi hiki wameshiriki na wanaendelea kushiriki vyema katika shughuli za maendeleo katika jamii zao ikiwemo kuziangalia na kuzihudumia familia zao; hivyo kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa hao kama wangekuwepo magerezani. 

Aidha, Mhe. Mrema amezungumzia changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili Bodi hiyo ikiwemo ufinyu wa bajeti katika kufanikisha shughuli za Bodi. Changomoto zingine ni katika maeneo ya kiutawala, kisheria ambazo hata hivyo amesema hatua mbalimbali za utatuzi zinaendelea kufanyiwa kazi na mamlaka husika.

“Bodi hii ya tano imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza majukumu yake katika kipindi cha miaka mitatu, licha ya changamoto hizo nilizozitaja, kipekee nitoe shukrani za dhati kwa wajumbe wa Bodi kwa ushirikiano wao kwangu. Pia natoa shukrani za kipekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuniteua kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi hii katika kutekeleza matakwa ya Sheria ya Bodi za Parole Sura ya 400”. Amesema Mhe. Mrema.

Bodi ya Taifa ya Parole ya Awamu ya Tano ilizinduliwa na kuanza kufanya kazi zake Machi 21, 2019 na inatarajia kumaliza muda wake wa kuwa madarakani kwa miaka mitatu ifikapo Julai 16, 2019.
 Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Magereza, Uwesu Ngarama(kulia) ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole akitoa taarifa fupi kabla ya kumkaribisha rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(kushoto) afungue rasmi Kikao cha 41 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole. Kikao hicho cha siku moja kimefanyika leo Julai 12, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga,  Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(hayupo pichani) akifungua kikao cha 41 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole. 
 Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakifuatilia majadiliano ya wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole leo Julai 12, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wajumbe Sekretarieti wakifuatilia kwa makini majadiliano katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(meza kuu) akiongoza Kikao cha 41 cha Bodi hiyo(Picha zote na Jeshi la Magereza).


KAMISHNA MHIFADHI WA MISITU PROF. DOS SANTOS SILAYO AWASILI MAKAO MAKUU YA TFS JIJINI DAR

$
0
0
Na Tulizo Kilaga,TFS

KWA mara ya kwanza tangu avishwe cheo cha Kamishna Mhifadhi wa Misitu na Dkt Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii na hatimaye kula Kiapo cha Utii na uadilifu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Magufuli Julai 9, 2019, Kamishna Prof. Dos Santos Silayo amewasili makao Makuu ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Jengo la Mpingo jijini Dar es salaam na kupokelewa na Viongozi Waandamizi na watumishi wa TFS.

Akizungumza na watumishi wake mara baada ya kuwasili ofisini hapo, Kamishna Prof. Silayo alisema mabadiliko yanayotokea katika sekta ya maliasili yamepelekea pia kubadili mfumo wa usimamizi na utendaji wetu toka ule wa Kiraia kwenda Jeshi Usu. 

“Namshukuru Mungu kuwa sehemu ya mabadiliko hayo. Hatua hiyo ikapelekea kuvishwa cheo cha Kamishna Mhifadhi wa Misitu na Mhe Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii na kula Kiapo cha Utii mbele ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Pombe Magufuli siku ya tarehe 9 Julai 2019.

“Mabadiliko haya yanalenga kujenga uwezo wa taasisi, uwezo wa watumishi ikiwa ni pamoja na kuwajengea ari, uzalendo, weledi na ujasiri katika kusimamia rasilimali za misitu na nyuki,” alisema Kamishna Prof. Silayo.

Kamishna Prof. Silayo anasema uwezo wa watumishi wa TFS utaenda sambamba na weledi katika matumizi ya mbinu na vifaa vya kisasa vinavyoweza kumudu mabadiliko ya changamoto za uhifadhi kuanzia usalama wao pamoja na usalama wa mali zenyewe unaotokana na kuongezeka kwa mbinu za kihalifu kila wakati.

Aidha Prof. Silayo alitoa shukurani kwa Mheshimiwa Rais na viongozi wote wa wizara ya Maliasili na Utalii kwa hatua hiyo waliyofikia ambayo anaamini itasaidia kukuwa kwa sekta ya misitu nchini na kuongeza ushirikiano na wadau wengine hususani wananchi katika kusimamia misitu yetu. 

Akiongea kwa njia ya simu Naibu Kamishna wa Huduma Saidizi, Emmanuel Wilfred alisema mabadiliko hayo yamepelekea kubadili mfumo wa usimamizi na utendaji wa TFS toka ule wa Kiraia kwenda Jeshi Usu na hivyo kulazimu watumishi wote kwenda kwenye mafunzo.

“Tunaendelea kutoa mafunzo kwa watumishi wachache waliobaki na kwa wale waliokwishakwenda kwenye mafunzo tunakamilisha taratibu ili Kamishna aweze kuwatunuku vyeo vyao, lakini niwatake wafanyakazi wote kuenda sambamba na mabadiliko kwa kasi hitajika,” alisema Kamishna Msaidizi huyo.

Rosemary Sabida mmoja wa watumishi wa TFS anasema mabadiliko hayo yataisaidia TFS kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhifadhi nchini.


Jumla ya Makamishna wanne, Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt Allan Kijazi, Kamishna wa Uhifadhi wa Misitu toka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof Dos Santos Silayo na Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Dkt.James V. Wakibara pamoja Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Freddy Manongi walivishwa vyeo vya kijeshi Julai 9, 2019 katika sherehe za Uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi – Chato zilizofanyika wilayani Chato mkoani Geita.
 Kamishna Mhifadhi wa Misitu Prof. Dos Santos Silayo katika muonekano mpya mara baada ya kuwasili makao makuu ya Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania akiwa na jukumu la kuwaongoza maofisa wake kwenye muundo wa kijeshi.
 Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Tehama, Harold Chipanha akimuongozo Kamishna Mhifadhi wa Misitu Prof. Dos Santos Silayo kwenda kwenye ukumbi wa mikutano wa Ngorongoro uliopo makuu ya Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuzungumza na watumishi.
 Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Tehama, Harold Chipanha akimpigia saluti Kamishna Mhifadhi wa Misitu Prof. Dos Santos Silayo mara baada ya kuwasili makao makuu ya Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza tangu kuvishwa cheo hiko cha kijeshi Julai 9,2019 wilayani Chato mkoani Geita.
 Kamishna Mhifadhi wa Misitu Prof. Dos Santos Silayo akikagua baadhi ya maofisa wa  Jeshi Usu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mara baada ya kuwasili makao makuu ya Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
 picha ya pamoja na na maofisa waJeshi Usu
Maafisa wa Jeshi Usu wa TFS wakifurahia jambo wakati Kamishna Mhifadhi wa Misitu Prof. Dos Santos Silayo alipokuwa akizungumza nao kw amara ya kwanza tangu aanze kutekeleza majukumu yake akiwa si raia tena.

Wakandarasi tumieni vijana wanaomaliza JKT, kujenga miradi ya umeme

$
0
0
Na Zuena Msuya, Kigoma
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewashauri wakandarasi nchini kuwatumia vijana wanaomaliza mafunzo katika jeshi la kujenga taifa wenye  taaluma na ujuzi mbalimbali ikiwemo sekta ya Nishati ya Umeme.

Mgalu alisema idadi kubwa ya vijana wanaohitimu mafunzo ya JKT wanakuwa na nidhamu, pamoja na uzalendo  katika kutekeleza majukumu yao  kwa maslahi ya Taifa.

Naibu Waziri alitoa ushauri huo alipokuwa akikagua maendeleo ya usambazaji wa Umeme vijijini katika kikosi Jeshi la Kujenga Taifa cha 825KJ Katika Kambi ya Mtabila, wilayani Kasulu mkoani Kigoma na kuzungumza na uongozi wa kituo hicho pamoja na Makuruta, Julai 11,2019. 
Aidha walishauri vijana wanaopata mafunzo ya jeshi kujifunza taaluma ya umeme wanapokuwa vyuoni ili kuwepo na mafundi mchundo wengi pale watakapohitajika kutumiwa na wakandarasi katika kujenga miradi ya umeme.

Aliongeza kuwa endapo kutakuwa na vijana wengi wzalendo katika taaluma hiyo, itasaidia kuondoa changamoto ya vishoka mitaani na watu wasiowaaminifu katika kutekeleza miradi ya umeme na mafundi mchundo katika kuwatanda nyaya kwenye nyumba za wananchi.
"Vijana wanaopitia mafunzo ya jeshi wengi huwa waadilifu na wazalendo kwa miradi inayotekelezwa katika nchi yao, hivyo nawashauri wakandarasi wote nchini kuwatumia vijana hao katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa ile yenye gharama kubwa na inayotumia fedha nyingi, kwa maslahi yao na nchi kwa ujumla", alisisitiza Mgalu.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa kikosi cha 825 KJ katika Kambi ya Mtabila, Meja  Peter Lyanga alimueleza Naibu Waziri Mgalu kuwa katika hiyo vijana wengi wanahitimu wakiwa na taaluma mbalimbali wakiwa na nidhamu ya hali ya juu hivyo amewatoa hofu wakandarasi juu wa vijana hao.
Aidha aliomba kuharakishwa kwa utekelezaji wa mradi wa umeme katika eneo hilo ili kambi hiyo iweze kupata huduma hiyo,ambayo itawasaidia vijana kuongeza ujuzi zaidi katika mafunzo yao yanayoendana na teknolojia ya kisasa zaidi. 

Katika hatua nyingine Mgalu aliwasha Umeme katika vijiji vya Wilaya za Kasulu na Buhigwe mkoani Kigoma na kuwataka wananchi kutumia Umeme huo kujiletea maendeleo. 
Katika Wilaya ya Kasulu, Mgalu aliwasha Umeme katika Zahanati ya Ruhita, Shule ya Sekondari ya Kasange pamoja na kijiji cha Ruhita.

Vilevile alizungumza na wakazi wa vijiji vya Shunga, Ruhita na Kasange ambapo pamoja na mambo mengine alimtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa usambazaji Umeme katika  vijiji hivyo kuongeza kasi zaidi kwani wananchi wamekuwawakiusubiri kwa muda mrefu.
Katika ziara hiyo pia, Mgalu alikagua kazi ya usambazaji wa umeme kijiji cha Nyankoronko wilayani  Buhigwe na kuwasha umeme katika jengo la halmashauri ya Wilaya hiyo na kuzungumza na wananchi wa wilaya hiyo.

Kwa upande wao, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Samson Anange  na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Michael Ngayalina waliwataka wananchi wa wilaya hizo  kutunza miundombinu ya umeme iliyopo katika maeneo yao wakati wakiendelea kusubiri hadi pale watakapowafikiwa na mradi huo katika nyumba zao.

Pia amewataka kutoa ushirikiano wa nguvu kazi hasa kwa vijana pale ambapo wakandarasi watakuwa wakiwahitaji vijana hao kwa kuwa watapata ajira za muda mfupi na kukidhi mahitaji yao. 
Sambasamba na hilo waliwasisitiza wakazi wa wilaya hizo kuwa wasikubali kulipa gharama za kuunganishiwa umeme kwa zaidi ya shilingi 27,000 wala kuuziwa vifaa vya umeme kama vile nguzo pamoja na LUKU.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na makuruta wa kikosi cha 825KJ katika kambi ya Mtabila wilayani Kasulu mkoani Kigoma, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme vijijini katika wilaya hiyo.
 Makuruta wa kikosi cha 825KJ kambi ya Mtabila wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, hayupo pichani, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme vijijini katika wilaya hiyo.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( katikati) akizungumza na mkazi wa kijiji cha Ruhita,wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, kabla ya kukata utepe kuwasha umeme katika nyumba yake ikiwa ni ishara ya kuwasha umeme katika kijiji hicho. 
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu,( katikati) akimkabidhi kifaa cha umeme tayari( UMETA) mama mwenye ulemavu,Merania Katekwa, mkazi wa Kijiji cha Nyankoronko wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, ambaye hana uwezo wa kulipia gharama za kuunganisha umeme licha ya  nyumba yake kukidhi viwango  na kupitiwa na mradi wa usambazaji umeme vijijini.
Akina mama wa kijiji cha Shunga, Kasulu mkoani Kigoma, wakifurahi na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, alipowaeleza kuwa umeme katika kijiji hicho utafika hivi karibu na tayari mkandarasi anaendelea na kazi ya kusimika nguzo.

USAJILI WA NGO’s KANDA YA MASHARIKI LAENDELEA KUANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine Bi.Vick Ntetema (kushoto aliyekaa) akipata huduma ya kusajili Taasisi yake ya Khulisa Social Solutions Tanzania (KSST) katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki.
 Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Denis Bashaka (kulia), akifafanua jambo kwa mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati akimpatia huduma ya kusajili Taasisi yake chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki.
 Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Bi.Happy Msimbe akitoa huduma ya kusajili Taasisi kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki.
 Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Victor Rugalabamu akitoa huduma ya kusajili kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki.
  Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Grace Mbwilo akitoa cheti kwa Bi. Vick Ntetema mmoja wa mdau kutoka Taasisi ya Khulisa Social Solutions Tanzania (KSST) katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Vodacom donated 300 desks in Bariadi District benefiting more than 400 students

$
0
0
  Bariadi-Simiyu: Vodacom Tanzania has donated 300 desks worth TZS 61,360,000 to Salunda and Somanda primary schools in Bariadi, Shinyanga, at a handover ceremony held at Sengerema Primary School that was witnessed by Bariadi District Commissioner, Festo Kiswaga. The move is in support of the government’s effort to curb the existing shortage of desks in primary schools and increase availability of basic school infrastructure countrywide.

Speaking during the ceremony, DC Festo Kiswaga said the 300 desks will greatly improve access of learning facilities as well as the learning condition for children in Bariadi, and called upon other well-wishers to come forward and join the effort to offset the remaining shortage of desks in the District.

“As we all know, education is an instrumental vehicle of development. We sincerely want to thank Vodacom for supporting us in our effort to improve access of learning facilities and offset the existing shortage of desks in schools here. We believe these 300 desks will go a long way in enabling hundreds of children with a conducive environment needed for effective learning.” Kiswaga said.

Vodacom Tanzania Lake Zone, Head of Consumer Business Department, Dominician Mkama, said the donation is in line with the company’s vision of being a purpose led brand and the new Vodacom Tanzania Foundation’s strategy of contributing towards fostering Tanzania human development through inclusive and quality education.

“Education is a fundamental human right and a key aspect of achieving the Sustainable Development Goals. The donation is part of Vodacom’s investment in human development projects that have high impact to the community. Through this donation, Vodacom is playing a key role in shaping the future leaders, doctors, engineers and other experts of this country” Mkama said.

He added that the company has been actively engaging with communities and collaborating with social partners to tackle national challenges including education and last year, they were able to reach 60,023 students through Instant schools’ platform. Vodacom continues to support government’s effort to make education accessible and conducive for every child in Tanzania under the country’s Development Vision 2025.


Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga (Kushoto) akipeana mkono na Meneja mauzo mwandamizi wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa, Ahmed Akberali (Kulia) katika hafla ya kukabidhi madawati 300 yenye thamani ya TZS millioni 61 yaliyotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya shule ya msingi ya Salunda na Somanda jana, Dutwa wilayani humo. Taasisi hiyo imetoa msaada wa madawati ikiwa ni njia mojawapo ya kuisaidia serikali kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi nchini.
Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Salunda na Somanda wakiwa wamekalia madawati yaliyokabidhiwa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, jana wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Taasisi hiyo imetoa madawati 300 yenye thamani ya TZS milioni 61 kwa shule hizo ikiwa ni njia mojawapo ya kuisaidia serikali kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi nchini.

NBAA YATOA UAMUZI DHIDI YA MAKAMPUNI MATATU YA UKAGUZI YANAYOTUHUMIWA KUKIUKA MAADILI KWA KUANDAA VITABU VIWILI VYA HESABU

$
0
0
KUFUATIA mazungumzo ya Rais Dkt. John Joseph Magufuli na Wawakilishi wa wafanyabiashara  kutoka wilaya zote nchini Tanzania yaliyofanyika Mjini Dar Es Salaam Ijumaa tarehe 7 Juni mwaka huh Rais Magufuli aligusia kuwa kuna baadhi ya makampuni yamekuwa yakiandaa vitabu viwili viwili vya hesabu (Financial Statements). Kimoja ni kwa ajili ya kuwasilishwa benki, ambacho kinaonesha matokeo makubwa na kitabu kingine kwa ajili ya kuwasilishwa Mamlaka ya mapato (TRA), ambacho kinaonesha hasara au faida ndogo na kueleza kuwa mchezo huo mchafu umekuwa ukifanywa kwa pamoja na wakaguzi (Auditors) ambao kimsingi wamesajliwa na NBAA ambayo  ni Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Rais Magufuli alisema kuwa wakaguzi/wahasibu hao hupitisha vitabu hivyo wakijua kabisa kuwa wanawasaidia wateja wao kukwepa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NBAA  CPA Profesa Isaya Jayambo Jairo amesema kufuatia  taarifa hizo NBAA kwa kushirikiana na TRA iliweza kupata majina ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu waliotuhumiwa pamoja na kampuni zilizohusika na udanganyifu huo katika kuandaa hesabu za kampuni za M / s Mek One General LTD na Mek One Industries LTD. 

Kampuni hizo za Kihasibu na Kikaguzi ni, Y.H. Malundo & Co, TEG Consultancy na MATSAB & Co na kupitia kikao cha dharura cha nne cha Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu kilichofanyika tarehe 9 Julai 2019, chini ya Mwenyekiti wake CPA. Prof.Isaya Jairo, kiliidhinisha maamuzi na adhabu mbali mbali zilizopendekezwa na Kamati ya nidhamu kama ifuatavyo, Jina la kampuni "TEG Consultancy" lifutwe (Delete) kutoka kwenye rejista ya makampuni ya Ukaguzi (Practising Firms) baada ya kupatikana na hatia ya kosa kubwa la ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kitaifa  na kimataifa ya ukaguzi wa hesabu (Gross Professional Misconduct) (kusaini seti tatu sambamba za taarifa za kifedha ambazo hazikukaguliwa kwa madhumuni mbalimbali). 

Kampuni hiyo imeshindwa kuzingatia sheria na kanuni na viwango vya kitaaluma, hivyo, kwenda kinyume na masharti ya sheria. Kwa hiyo, kampuni hii inashtakiwa chini ya Kifungu cha 17 (1) (c) & (5) kinachosomwa pamoja na Kifungu cha 21 (e), Kifungu cha 31 (1), (4) & (5) na S. 42 (c) cha Sheria kuu ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002), pamoja na Kifungu cha 16 (a) na (d), 20 a) na (b) , 27 (1) (a) na (e), Kifungu cha 29 (b) na (e) cha Kanuni za Ukaguzi za 2017 na Sehemu 210.1 210.2 na 210.3 za Kanuni za Maadili za Wahasibu na Wakaguzi Hesabu.

Pia jina la kampuni "MATSAB & CO" liondolewe) kutoka kwenye rejista ya makampuni ya Ukaguzi (Practising Firms) baada ya kupatikana na hatia ya kosa kubwa la ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kitaifa na Kimataifa ya ukaguzi wa hesabu (Gross Professional Misconduct) (kusaini taarifa za kifedha bila kukagua) kwa kuwa kampuni imeshindwa kuzingatia sheria na kanuni na viwango vya Kimataifa, hivyo, kwenda kinyume na masharti ya Sheria.

 Kwa hiyo, anashitakiwa chini ya Kifungu cha S.17 (1) (c) kikisomwa pamoja na Kifungu cha 21 (e), na kifungu cha 31 (1), (4) Na (5) ya Sheria kuu, Kifungu cha 16 (a) na (d), 20 (a) na (b), 27 (1) (a) na (e), 29 (b) na (e) ya cha Kanuni za Ukaguzi, 2017 na Sehemu 210,1 210.2 na 210.3 za Kanuni za Maadili za IFAC, Kwa hiyo, kampuni imeshtakiwa chini ya Kifungu cha 21 (e), Sehemu ya 31 (1), (4) & (5) na 42 (c) ya Sheria kuu.

Vilevile  jina la kampuni "Y.H. Malundo & Company ",(kampuni ya ukaguzi), kusimamishwa kuendelea kufanya kazi za Ukaguzi  kwa kipindi cha miaka miwili (Suspension) baada ya kupatikana na hatia ya kosa la ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kitaifa na Kimataifa ya ukaguzi wa hesabu (Professional Misconduct) (kukagua na kusaini taarifa hesabu za kifedha bila kufuata taratibu za kisheria na miongozo ya kitaifa na kimataifa).

 Kampuni imeshindwa kuzingatia sheria na kanuni na viwango vya Kitaifa na Kimataifa vya  ukaguzi wakati wa ukaguzi wa taarifa za fedha za M/S Mek One Industries kwa kipindi cha 2014, 2015 na 2016. Kampuni hiyo ilivunja masharti ya kifungu cha 27 (1) (b) na S. 28, Kanuni za Ukaguzi, 2017 na Sehemu ya 210.1,2 & 3 za Kanuni za Maadili ya IFAC. Hivyo Kampuni hiyo inashtakiwa  chini ya S.21 (d) ya Sheria kuu.

Jina la CPA Mazengo Kasilati (Managing Partner TEG Consultancy), kuhamishiwa kwenda kwenye orodha ya chini katika rejista (lower classification) ya (Graduate Accountant) baada ya kupatikana na hatia ya kosa kubwa la ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kitaifa  na Kimataifa ya ukaguzi wa hesabu (Gross Professional Misconduct) (kusaini seti tatu za sambamba za taarifa za hesabu za kifedha ambazo hazikukaguliwa kwa madhumuni mbalimbali).

CPA Mazengo Kasilati (Mkaguzi) ameshindwa kuzingatia sheria na kanuni na viwango vya kitaaluma, hivyo, kwenda kinyume na masharti ya Sheria. Kwa hiyo, anashitakiwa chini ya Kifungu cha 21 (c), na kifungu cha 31 (1), (4) & (5) cha Sheria kuu, kikisomwa pamoja na Kifungu cha 16 (c) na (d) cha Kanuni za Ukaguzi, na sehemu 210,1 210.2 na 210.3 ya Kanuni za Maadili za IFAC. 

Kwa hivyo, anashtakiwa chini ya Kifungu 21 (c), na kifungu cha 31 (1), (4) & (5) cha Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002) na CPA Mazengo Kasilati atarudisha vyeti vyote alivyopewa na NBAA vikimruhusu kufanya ukaguzi na kutoa ushauri wa kihasibu.

Pia imeadhimiwa kuwana la CPA Mathew J. Marapachi (Msimamizi wa M/s MATSAB na Co.), liondolewa kutoka kwenye rejista ya ACPA na yeye mwenyewe achukuliwe hatua za kisheria (mashtaka) baada ya kupata idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (Director of Public Prosecution-DPP) baada ya kupatikana na hatia ya kosa kubwa la ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kitaifa ya ukaguzi wa hesabu (Gross Professional Misconduct) (kutumia sifa ya kada ya Ukaguzi-  CPA PP) huku akijua wazi kwamba yeye hana sifa ya kufanya kazi kama 

Imeelezwa kuwa Mkaguzi wa Hesabu CPA Mathew J. Marapachi amekiuka masharti  ya   sheria na kanuni na viwango vya Kimataifa, hivyo, anashtakiwa chini ya Kifungu cha  S.17 (c), S.21 (c) cha Sheria kuu na Kifungu 14 (2), 16 (c) na (d) cha Kanuni za Ukaguzi, 2017 zikisomwa pamoja kifungu cha 27 c) kusoma pamoja na S. 42 (c) ya Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002)

CPA Y.H. Malundo (Managing Partner- M/S Y.H. Malundo & Co.), amesimamishwa kwa muda wa miaka miwili (Suspension) baada ya kupatikana na hatia ya kosa la ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kitaifa na Kimataifa ya ukaguzi wa hesabu (Professional Misconduct) (kukagua na kusaini taarifa za kifedha bila kufuata taratibu za kisheria na miongozo ya kitaifa na kimataifa). CPA Y.H. Malundo ameshindwa kuzingatia sheria na kanuni na viwango vya Kitaifa na Kimataifa vya  ukaguzi wakati wa ukaguzi wa taarifa za fedha za M /S Mek One Industries kwa kipindi cha 2014, 2015 na 2016). CPA Y.H. 

Malundo  amevunja masharti ya kifungu cha 27 (1) (b) na S. 28, cha Kanuni za Ukaguzi, 2017 na Sehemu 210.1, 2 & 3 za Kanuni za Maadili za IFAC. Kkwa hiyo, anashtakiwa chini ya kifungu cha.21 (d) ya Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002)

Aidha bwana Mathew Kumalija (mfanyakazi wa M / s MATSAB na Co), achukuliwe hatua za kisheria (mashtaka) baada ya kupatikana na hatia ya kosa kubwa la ukiukwaji wa sheria ya Sheria kuu ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002) ( kusaini taarifa za kifedha ambazo hazijakaguliwa bila kuwa na sifa za Ukaguzi).

Vile vile, afunguliwe mashtaka baada ya kupata idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (Director of Public Prosecution-DPP) kwa kosa la pili baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kutumia mitindo na majina kinyume na mahitaji ya Sheria hii.Imeelezwa kuwa  Mathew Kumalija ana sifa ya National Accountancy Diploma (NAD), sifa ambayo haitambuliwi tena na Bodi. Kwa hivyo, sio sifa ya kuajiriwa kama "Mkaguzi wa Hesabu" na pia hakuruhusiwa kusaini taarifa yoyote ya ukaguzi ya kifedha.

Hivyo, Mathew Kumalija anashtakiwa chini ya Kifungu cha 42 (c) kwa kuvunja masharti ya kifungu cha 27 b) na kifungu cha 31 (1), (4) & (5) cha Sheria kuu. Kwa hivyo ameshtakiwa chini ya kifungu cha 31 (1), (4) & (5)  42 (c) vya Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002)

Pia bodi imeamuru majina ya wote waliokutwa na makosa yachapishwe kwenye vyombo vya habari (magazeti), tovuti ya NBAA na kwenye Gazeti la serikali  vilevile makampuni na watu ambao wametuhumiwa,  kusimamishwa na kushtakiwa baada ya kupata idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka ( DPP) kama inavyotakiwa na S. 8 (1) ya Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002).

Pia a wamependekeza Makampuni mawili  ya M / s Mek One General LTD na Mek One Industries LTD) ambayo Ripoti ya uchunguzi ilibainisha kuwa Makampuni hayo yalivunja masharti ya vifungu cha 30 (1) (a) & (b) na kifungu cha 31 (1), (4) & (5) ikisomwa pamoja na kifungu 42 (c) cha Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002) kuchukuliwa hatua za kisheria.

Pia wameeleza mkakati wa kuzuia au kurekebisha hali hii isitokee tena bodi imeeleza kuwa  NBAA ipo katika hatua za kupendekeza marekebisho ya sheria iliyoiunda ili iwe na uwezo zaidi wa  kupambana na changamoto zinazojitokeza sasa ili iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NBAA , CPA Profesa Isaya Jayambo Jairo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi uliochukuliwa na Bodi hiyo mara baada ya kupata majina ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu wanaotuhumiwa pamoja na kampuni zilizohusika na udanganyifu huo katika kuandaa hesabu za kampuni.

UINGEREZA YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA

$
0
0
Uingereza imeihakikishia Tanzania kuwa itaendelea kuwa mshirika wake katika masuala mbalimbali ya ubia wa maendeleo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wawekezaji wengi kutoka Uingereza kuwekeza Tanzania kama moja ya hatua za kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano ili iweze kufikia azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025.

Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza katika Idara ya Ushirikiano wa Maendeleo, Mhe. Harriett Baldwin ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, Jijini London, Uingereza kwa nia ya kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo na ushirikiano baina ya Tanzania na Uingereza.

Katika mazungumzo hayo Waziri Harriett na Prof. Kabudi wamezungumzia kuhusu hali ya ushirikiano wa ubia wa maendeleo uliopo hivi sasa na kuonesha kuridhishwa na Serikali ya Tanzania inavyosimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza katika sekta za elimu,afya, maji, kilimo pamoja na miundombinu ya barabara hususani vijijini ikiwemo maboresho ya mifumo ya fedha,utumishi wa umma, serikali za mitaa miongoni mwa miradi mingine mingi.

Pia, Waziri Harriett ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kupambana na rushwa,kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma katika sekta ya umma, kuongeza uwajibikaji na utawala bora mambo aliyoyataja kama hatua muhimu ya kufikia malengo ya haraka na kuondoa umasikini.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba John Kabudi ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa kuwa mbia mkubwa wa maendeleo na kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa uwekezaji,biashara na utalii nchini Tanzania.

Aidha, Prof Kabudi amemhakikishia Waziri Harriett nia thabiti ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kufanya mageuzi muhimu ya kiuchumi na kiutawala yanayolenga kuifikisha Tanzania katika mojawapo ya nchi za uchumi wa kati.

Miongoni mwa maboresho hayo, Waziri Kabudi ameyataja kuwa ni pamoja na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara,maboresho katika usimamizi wa utendaji wa Serikali katika kuwahudumia wananchi na utoaji huduma za kijamii hususani sekta zinazowagusa wananchi wengi hususani wa kipato cha chini.

Akihitimisha mazungumzo hayo Waziri wa masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza, Mhe. Harriett Baldwin amemhakikishia Waziri Kabudi kuwa Uingereza inafuatilia kwa ukaribu mageuzi na maboresho ya kiutendaji yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli yakiwemo, kuimarisha mazingira ya uwekezaji.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Uingereza, Mhe. Harriett Baldwin,London Uingereza. July 12, 2019.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Uingereza, Mhe. Harriett Baldwin mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo baina yao kuhusu masuala mbalimbali kati ya Tanzania na Uingereza. Mazungumzo hayo yamefanyika London Uingereza. July 12, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Uingereza, Mhe. Harriett Baldwin mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo baina yao kuhusu masuala mbalimbali kati ya Tanzania na Uingereza. Mazungumzo hayo yamefanyika London Uingereza. Pembeni kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dr. Asha -Rose Migizro. July 12, 2019.

Mwenyekiti wa zamani UWT kortini kwa tuhuma za kughushi cheti cha ndoa

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu kama Nora Mzeru amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni  akikabiliwa na tuhuma za kughushi cheti cha ndoa.

Wakili wa serikali , Benson Mwaitenda amedau leo Julai 12, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Anifa Mwingira kuwa Februari 4,1995 jijini Dar, es Salaam, mshtakiwa kwa nia ya kudanganya, alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078 kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na marehemu Silvanus Mzeru Februari 4, 1995 katika kanisa la Roman Catholic la Mburahati huku akijua kuwa si kweli.

Hata hivyo, mshtakiwa  amekana shtaka hilo na kudai kuwa marehemu huyo ni mume wake.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na mshtakiwa yuko nje kwa dhamana baada ya kufanikisha kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama ambapo Mahakama imemtaka
mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili ambapo mmoja kati ya wadhamini hao atoke katika Taasisi inayotambulika kisheria.

Pia kila mdhamini alitakiwa kusaini bondi ya Sh milioni moja milioni. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 17, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Awali, Oktoba 24,2018 mshtakiwa hiyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kusomewa shtaka la kughushi mbele ya hakimu mkazi Flora Hauled.

Hata hivyo, kesi hiyo ilifutwa mahakamani hapo kwa sababu mahakama ile haikuwa na mamlaka ya kusikiliza na kufunguliwa upya mahakamani hapo leo.

KONGAMANO LA UWEKEZAJI WA ZAO LA KOROSHO WAFANYIKA MKOANI MTWARA

$
0
0
 Naibu waziri wa kilimo Omary Mgunda akifungua kongamano la siku mbili la Uwekezaji la kimataifa la zao la Korosho nchini linalofanyika mkoani Mtwara.
 Naibu Waziri wa kilimo Omary Mgunda katikati  akiwa meza kuu wakati wa kufungua kongamano la siku mbili la uwekezaji la kimataifa la korosho nchini kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Geofrey Mwambe ambalo linalofanyika mkoani Mtwara

Washiriki wa kongamano la siku mbili la uwekezaji la Kimataifa wa zao la Korosho nchini linalofanyika mkoani mtwara (PICHA NA FATNA MWINYIMKUU).

Mambo matatu muhimu yatajwa miaka mitano ya M-Pawa

$
0
0
Benki ya CBA ikishirikiana na kampuni ya Vodacom imefanya droo yake ya 5 ya kuadhimisha miaka 5 ya huduma ya MPawa yenye lengo la kuongeza ushirikishwaji wa kifedha kwa wateja wake kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam.

Katika kusherehekea maadhimisho hayo, promosheni hiyo inajumuisha droo za kila wiki zilizohusu kuwekeza na kukopa na MPawa huku ukitoa washindi zaidi ya 340 walioibuka na mara mbili ya akiba zao kuanzia kiwango cha Tsh 1000-200,000, simu janja na muda wa maongezi.

Katika kuongelea kuhusu huduma hii ya MPawa, Meneja Masoko wa benki hiyo Bw Solomon Kawiche aligusia mambo 3 muhimu kwenye maadhimisho hayo ya Miaka 5.

M-Pawa inasherehekea miaka 5, ni mafanikio gani yameonekana tangu kuanzishwa kwa huduma hii? Mpawa ilianza na wateja 4 tu ila hadi leo hii imefikisha wateja Mil 8.5 na imefanikiwa kurahisisha Maisha ya wananchi wengi ambao wapo mbali na huduma za kibenki kwa kuwapatia huduma nafuu za kibenki ikiwemo kukopa kiasi kidogo cha hadi 1000 ambacho hauwezi kupata kupitia huduma za benki.

M-Pawa imefanikiwa kutoa huduma ya kuhifadhi akiba kwa kiwango cha chini cha hadi Tsh 1, hakuna benki nyingine ndani ya Tanzania inayotoa huduma kama hii na kurahisisha huduma za kibenki bila ya kuwa na utaratibu mrefu kukamilisha miamala. Watumiaji wa M-Pawa hawana haja ya kutembelea matawi yetu na kupitia huduma hii, wateja wetu wanapata faida kupitia akiba zao.

Akiba za wateja wa MPawa pia zipo kwenye usalama wa hali ya juu kwasababu hakuna makato au gharama zilizofichika. MPawa imeinua hali ya Maisha ya mamilioni ya watanzania hususani wafanyabiashara wadogo na bila kusahau kuwa imekuwa ikitoa uhakika wa kifedha wakati wa dharura; mteja anaweza kukopa muda wowote na wakati wowote ule.

Nini malengo ya baadae ya M-Pawa? Ikiwa ni huduma ya kwanza ya kidigitali Tanzania, MPawa itaendelea kugusa miasha ya wananchi wengi ambao wapo mbali na huduma za kibenki na itaendelea kujidhatiti kwenye kuwajumuisha kifedha wateja wake. Kama benki, tuna maleno ya kuwekeza zaidi kwenye huduma hii kuhakikisha kuwa inaendana na maendeleo ya sasa ya kisayansi na Teknolojia na kuwezesha huduma hii kwenye application. Nini maoni yako kwenye huduma za kifedha za kiditali hususani M-Pawa?

Huduma za kifedha za kidigitali kwenye dunia ya leo ni sio kitu ya kupuuza hususani huduma kama MPawa kwa sababu ya urahisi wake kwenye gharama, uaminifu wake na urahisi wake katika kuitumia. MPawa inapatika kupitia simu yoyote ya mkononi, ni huduma ya kibenki iliyorahisishwa kutumia mahali popote kwa gharama nafuu na humpatia mteja faida kupitia akiba anayoweka bila kuwa na gharama zilizofichwa. Hili linaupa upekee huduma hii ya M-Pawa

Mshindi mkubwa wa maadhimisho haya ya Miaka 5 ya MPawa ataibuka na zawadi ya Million 15 za kitanzania kwenye droo ya mwisho ya promosheni hiyo. Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma hii, wateja wanaweza kutembelea mitandao ya kijamii ya benki ya CBA/Vodacom au kutembelea menyu ya MPawa kwa kubonyeza *150*00# kupitia mtandao wa simu.

MAJALIWA AZUNGUMZA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA VIETNAM, TRINH DINH DUNG

$
0
0

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Trinh Dinh Dung, katika mazungumzo ya faragha yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Julai 12, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam,  Trinh Dinh Dung (wa pili kulia)  katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa  Ofisi ya  Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Julai 12, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam,  Trinh Dinh Dung  (kulia)  katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa  Ofisi ya  Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Julai 12, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimkabidhi  zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro, Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Trinh Dinh Dung, baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Julai 12, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Trinh Dinh Dung wakitoka ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam baada ya mazungumzo yao, Julai 12, 2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam,Trinh Dinh Dung wakigonganisha glass katika chakula cha mchana alichoandaa Waziri Mkuu wa Tanzania  kwa heshima ya mgeni huyo kwenye hoteli ya Hyatt Regency- Kilimanjaro jijini Dar es salaam, Julai 12, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NEWS ALERT: BOT SLAPS 1BN/- FINE ON DIAMOND TRUST BANK FOR FAILURE TO ESTABLISH DATA CENTRE

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO


UINGEREZA YAAHIDI KUENDELEA KUIUNGA MKONO TANZANIA KATIKA MASUALA MBALIMBALI

$
0
0


Uingereza imeihakikishia Tanzania kuwa itaendelea kuwa mshirika wake katika masuala mbalimbali ya ubia wa maendeleo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wawekezaji wengi kutoka Uingereza kuwekeza Tanzania kama moja ya hatua za kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano ili iweze kufikia azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025.

Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza katika Idara ya Ushirikiano wa Maendeleo, Mhe. Harriett Baldwin ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, Jijini London, Uingereza kwa nia ya kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo na ushirikiano baina ya Tanzania na Uingereza.

Katika mazungumzo hayo Waziri Harriett na Prof. Kabudi wamezungumzia kuhusu hali ya ushirikiano wa ubia wa maendeleo uliopo hivi sasa na kuonesha kuridhishwa na Serikali ya Tanzania inavyosimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza katika sekta za elimu,afya, maji, kilimo pamoja na miundombinu ya barabara hususani vijijini ikiwemo maboresho ya mifumo ya fedha,utumishi wa umma, serikali za mitaa miongoni mwa miradi mingine mingi.

Pia, Waziri Harriett ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kupambana na rushwa,kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma katika sekta ya umma, kuongeza uwajibikaji na utawala bora mambo aliyoyataja kama hatua muhimu ya kufikia malengo ya haraka na kuondoa umasikini.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba John  Kabudi ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa kuwa mbia mkubwa wa maendeleo na kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa uwekezaji,biashara na utalii nchini Tanzania.

Aidha, Prof Kabudi amemhakikishia Waziri Harriett nia thabiti ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kufanya mageuzi muhimu ya kiuchumi na kiutawala yanayolenga kuifikisha Tanzania katika mojawapo ya nchi za uchumi wa kati.

Miongoni mwa maboresho hayo, Waziri Kabudi ameyataja kuwa ni pamoja na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara,maboresho katika usimamizi wa utendaji wa Serikali katika kuwahudumia wananchi na utoaji huduma za kijamii hususani sekta zinazowagusa wananchi wengi hususani wa kipato cha chini.

Akihitimisha mazungumzo hayo Waziri wa masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza, Mhe. Harriett Baldwin amemhakikishia Waziri Kabudi kuwa Uingereza inafuatilia kwa ukaribu mageuzi na maboresho ya kiutendaji yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli yakiwemo, kuimarisha mazingira ya uwekezaji na biashara,kukuza demokrasia na utawala bora na hivyo Tanzania itegemee ongezeko la wawekezaji kutoka Uingereza.
 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Uingereza, Mhe. Harriett Baldwin,London Uingereza.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Uingereza, Mhe. Harriett Baldwin mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo baina yao kuhusu masuala mbalimbali kati ya Tanzania na Uingereza. Mazungumzo hayo yamefanyika London Uingereza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Uingereza, Mhe. Harriett Baldwin mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo baina yao kuhusu masuala mbalimbali kati ya Tanzania na Uingereza. Mazungumzo hayo yamefanyika London Uingereza. Pembeni kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dr. Asha -Rose Migizro. July 12, 2019.

Naibu Waziri wa kazi Antony Mavunde ausifu Mkoa wa Morogoro kutatua migogoro ya ardhi.

Vijana wasomi waliofanya maajabu katika Kilimo wafunguka kuwa Petrobena ndio msaada wao.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 12.07.2019

Uandikishaji wa Kitambulisho cha Taifa NIDA katika maonesho ya Sabasaba...

Viewing all 110088 articles
Browse latest View live




Latest Images