Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

IGP SIMON SIRRO AKAGUA NYUMBA ZA KISASA ZA MAKAZI YA POLISI SHINYANGA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro ametembelea na kukagua nyumba 10 za kisasa za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga na kugharimu shilingi milioni 225.


Mkuu huyo wa jeshi la polisi amekagua nyumba hizo leo Jumanne,Julai 10,2019 na kueleza kuridhishwa jinsi zilivyojengwa kwa umaridadi na ubora wa hali ya juu. 

Nyumba hizo 10 ni sehemu ya nyumba 114 ambazo ujenzi wake umekamilika nchi nzima ikiwa ni sehemu ya nyumba 400 zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya makazi ya askari polisi.

"Ujenzi huu umegharimu shilingi milioni 225,ni kweli nyumba hizi ni nzuri sana,nimpongeze sana Mhe. Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe.Zainab Telack na kamati yake ya ulinzi na usalama,kamati ya ujenzi na wadau wote walioshiriki kwa kazi hii nzuri"

"Sasa tunamsubiri Mhe. Rais,Dkt.John Pombe Magufuli muda siyo mrefu atazindua hizi nyumba 114 nchi nzima. Pesa zilizotolewa ni kwa ajili ya kujenga nyumba 400,lakini mpaka sasa zilizokamilika sasa ni 114",alisema IGP Sirro. 

Kwa upande wake,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack alimshukuru Rais Magufuli kwa kutoa pesa kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya askari polisi huku akimuomba IGP Sirro kutafuta pesa kwa ajili ya ukarabati wa baadhi ya nyumba za askari ambazo hali yake siyo nzuri.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro akizungumza wakati akikagua nyumba 10 za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga leo Jumanne Julai 10,2019.Kulia ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Muonekano wa nyumba za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Nyumba za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Muonekano wa nyumba za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akimuonesha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro nyumba za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro akikagua nyumba za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro akikagua nyumba za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro akisamiliana na waendesha bodaboda katika eneo la nyumba za makazi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga na kuwakumbusha kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuwasihi kuacha kubeba mishikaki,wavae kofia ngumu na wawe na leseni. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Balozi Seif afanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akisalimiana na Mgeni wake Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung aliyefika Ofisini kwake kwa mazungumzo.
 Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung Kulia akiongozwa na Mwenyeji wake Balozi Seif kuelekea Ukumbi wa Mikutano kwa mazungumzo yao Rasmi.
  Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung akitia saini Kitabu cha wageni mara tu baada ya kufika Ofisini kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Ujumbe wa Vietnam ukiongozwa na Waziri Mkuu wake Bwana Trinh Dinh Dung ukifanya mazungumzo na Ujumbe wa Zanzibar ulioongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.
 Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung Kushoto akisisitiza ahaja ya nchi yake na Tanzania kuendeleza Uhusiano wa Kibalozi katika Nyanja za Kiuchumi zaidi badala ya Siasa.

 Bwana Trinh Dinh Dung Kushoto akimpatia zawadi Balozi Seif mara baada ya Mazungumzo yao ya Kidiplomasia yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga.

 Balozi Seif akimpatia Bwana Trinh Dinh Dung zawadi ya kasha ikiwa ni kumbu kumbu ya ziara aliyoifanya na Ujumbe wake Visiwani Zanzibar.
   Balozi Seif wa Tano kutoka Kulia pamoja na Mgenzi wake Bwana Trinh Dinh Dung akiwa Kulia yake wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Ujumbe wa Zanzibar na Vietnam.
Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baada ya kumaliza mazungumzo yao. Picha na – OMPR – ZNZ.

Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung alisema uhusiano wa Kidiplomasia uliyopo baina ya Mataifa ya Vietnam na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sasa unastahiki uelekezwe katika masuala ya Uchumi na Biashara.

Alisema uhusiano huo ulikuwa amejikita zaidi katika masuala ya Kisiasa hasa ikizingatiwa kwamba wakati huo ulikuwa kipindi cha mpito cha Mataifa hayo kutokan katika mikono ya Tawala za kikoloni.

Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar akiwa Nchini Tanzania kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya Siku Nne.

Alisema Sekta za Uchumi na Biashara kwa sasa kutokana na mabadiliko ya Dunia ndio fursa pekee itakayoendelea kuunganisha pande hizo mbili kupitia maingiliano ya Taasisi za Umma na hata sekta binafsi ya Watu wa Mataifa hayo mawili rafiki.

Bwana Trinh Dinh Dung alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba kwa sasa ipo haja ya kuundwa kwa Kamisheni ya pamoja kati ya Tanzania na Vietnam itakayotoa muelekeo wa kufanikisha ustawi wa Wananchi wa pande hizo mbili.

Alisema umadhubuti wa Kamisheni hiyo itakayopaswa kuhusisha Wataalamu, Wafanyabiashara na Watu maarufu unaweza kuibua Miradi ya Kiuchumi na kutoa fursa ya Uwekezaji kwa Makampuni na Wafanyabiashara wa Vietnam na Tanzania.

Bwana Trinh Dinh Dung alishauri kwamba masuala hayo ni vyema yakaenda sambamba na Mabadiliko ya Viwanda yaliyopo Ulimwenguni hivi sasa ambayo yatachangia kutoa ajira nyingi hasa kwa makundi ya Vijana na Wanawake.

Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba Nchi yake iko tayari kubadilishana uzoefu a Utaalamu katika hatua ya kuelekea kwenye Maendeleo.

Alifahamisha kwamba yapo maeneo ya kushirikiana katika kuimarisha Uchumi akiyataja baadhi kuwa ni pamoja na Sekta ya Utalii ambayo Zanzibar tayari imeshajiimarisha kuwa kituo maarufu cha kuunganisha safari za Watalii Ulimwenguni.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar na Vietnam zinafanana katika harakati zao zilivyokuwa wakati wa kudai Uhuru.

Balozi Seif alisema ziara za Viongozi Wakuu, wale Waandamizi pamoja na Wataalamu wakiwemo pia Wafanyabaishara za kutembeleana zinaweza kuongeza ukaribu zaidi wa ushirikiano wa pande hizo mbili rafiki.

Alisema Zanzibar na Tanzania kwa jumla imeweka Milango wazi kwa Wawekezaji wa Nje kuanzisha Miradi ya Kiuchumi ambapo aliwaomba Wawekezaji wa Vietnam kupitia Kiongozi wao huyo kuitumia fursa hiyo.

Balozi Seif alieleza kwamba inapendeza kuona kwamba Timu ya Wataalamu kutoka Vietnam imeshafika Zanzibar Miaka ya nyuma kusaidiana na Wataalamu Wazalendo kufanya Utafiti katika Sekta za Baharini na Kilimo, Utafiti ambao unaweza kuleta tija hapo baadae.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Vietnam kwa jitihada inazochukuwa za kuendelea kuiunga Mkono Zanzibar Kitaalamu katika Sekta tofauti za Maendeleo.

Vietnam na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zimeanza ushirikian o wa Kidiplomasia mnamo Mwaka 1965 ambapoMataifa yote mawili yameshasini Mkataba wa ushirikiano katika sekta ya Uchumi, Biashara, Sayansi na Teknolojia.

Ziara ya Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung itakayomchukuwa siku Nne imeanzia Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE}, Tanzania na pia itamalizia Umoja huo wa Fame za Kiarabu.

Jarida la Dawasa kila wiki

VYAMA VYA WAMWAGILIAJI NCHINI VYATAKIWA KUWA NA USIMAMIZI THABITI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo na Utafiti kutoka Wizara ya Kilimo Bw. Wilhelm Mafuru, akifungua kongamano la mashindano ya vyama vya umwagiliaji kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mathew Mtigumwe leo Jijini Dodoma.
Bi Frida Tarimo Mkulima wa zao la Mpunga kutoka katika skimu ya kiloimocha Umwagiliaji Simanjiro akiongea kuhusu manufaa wanayopata kutokana na mafunzo ya utunzaji na uendeshaji wa miundombinu ya umwagiliaji, katika kongamano la mashindano ya vyama vya wamwagiliaji lililofanyika jijini Dodoma.
Katika Picha ni Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mbogo Mfutakamba akiongea na waandishi wa habari hawapo katika picha kuhusu umuhimu wa kilimo cha umwagiliaji na Tanzania ya viwanda.
katika picha ni sehemu ya washiriki katika kongamano la mashindano ya vyama wa Umwagiliaji lilifanyika Jijini Dodooma leo.
Picha ya pamoja ikionyesha baadhi ya washiriki katika kongamano la mashindano ya vyama vya umwagiliaji lililofanyikaJijini Dodoma Leo.


Na; Mwandishi Maalum - Dodoma

Wakulima wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini kupitia Skimu za umwagiliaji, wametakiwa kuwa na usimamizi thabiti wa skimu hizo ili kilimo hicho kuwa cha uhakika zaidi na chenye tija kwa mkulima na taifa kwa ujumla.

Akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya KIlimo Mhandisi Mathew Mtigumwe, Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo na Utafiti Bw. Wilhelm Mafuru, ameyasema hay o leo Jijini Dodoma katika kongamano kubwa lililoshirikisha vyama 36 na kushindanisha vyama vya umwagliaji 8 kutoka Kanda 8 za Umwagiliaji lenye lengo la kutoa motisha kwa skimu zilizowahi kupata mafunzo ya Matunzo na Uendeshaji chini ya Mradi wa kujenga uwezo kwa wataalamu wa Umwagiliaji wa TANCAID awamu wa pili kupitia Shirika la kimataifa la maendeleo la Japan JICA kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. 

Kadhalika warsha imetoa fursa kwa wadau wa umwagiliaji kuona namna ya kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji, pamoja na kutoa nafasi kwa vyama vya umwagiliaji kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kuendesha na kutunza skimu za umwagiliaji.

Bw. Mafuru Amesema kuwa, tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeendelea kusaidia wakulima kupata elimu kupitia wataalam ili kuweza kulima kwa tija na kuendelea kusimamia kuimarisha shughuli za kilimo cha umwagiliaji.

Akiongea kwa Niaba ya wakulima wa Skimu ya umwagiliaji ya Lemkuna Bi. Frida Tarimo, alisema kupitia mafunzo wanayopata wakulima wameweza kusimamia Uendeshaji na Matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji, upatikanaji wa maji ya kutosha kwa vitalu na maandalizi mazuri ya kalenda ya msimu wa kilimo jambo ambalo ameeleza limeongeza uzalishaji katika kilimo hususan cha zao la Mpunga.

Awali akiongea na waandishi wa Habari Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mbogo Futakamba alisema kuwa kuelekea Tanzania ya Viwanda kilimo cha umwagiliji kinahitaji uwekezaji mkubwa na miundombinu bora na mfumo sahihi wa umwagiliaji jambo ambalo linaweza kuleta uhakika wa chakula malighafi za viwanda na kilimo kuboreka kupitia mifumo sahihi ya umwagiliaji.

TAKUKURU TANGA YAOKOA MILIONI 23 KWA KIPINDI CHA MIEZI MIWILI

$
0
0
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Christopher Mariba akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga wakati akitoa taarifa ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Tanga kwa kipindi cha Aprili hadi June 2019 kwa waandishi wa habari mkoani humo
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Christopher Mariba akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga wakati akitoa taarifa ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Tanga kwa kipindi cha Aprili hadi June 2019 kwa waandishi wa habari mkoani humo
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Christopher Mariba akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga wakati akitoa taarifa ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Tanga kwa kipindi cha Aprili hadi June 2019 kwa waandishi wa habari mkoani humo
AFISA Miradi wa Takukuru Mkoani Tanga Didas Mchau akitolea ufafanuzi wa baadhi ya mambo kwenye kikao hicho kushoto ni Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Christopher Mariba
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua stori


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Tanga (Takukuru) imefanikiwa kudhibiti na kuokoa kiasi cha Sh.Milioni 23,009,860 kwa kipindi cha miezi miwili ambazo zimetokana na uchunguzi na wafanyabiashara “Wamachinga wa kigeni” 

Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Christopher Mariba wakati akitoa taarifa ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Tanga kwa kipindi cha Aprili hadi June 2019 kwa waandishi wa habari mkoani humo 

Alisema kwamba kati ya fedha hizo milioni 17.5 zinatokana na uchunguzi na milioni 5.5 zinatokana na wafanyabiashara “Wamachinga wa kigeni” waliobainika kufanya biashara katika Jiji la Tanga kinyume cha Sheria za Tanzania. 

Mkuu huyo wa Takukuru mkoa wa Tanga alisema hilo linatokana na operesheni ya kushtukizwa kwa kushirikiana na vyombo vyengine vya dola na TRA mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu alfajiri katika makazi ya wageni ambao iliamini kwamba wamekuwa wakifanya lakini hawalipi kodi. 

Aidha alisema katika operesheni hiyo taasisi hiyo ilikamata madaftari ambamo wahusika huandika kumbukumbu za mauzo yao na kuyakabidhi TRA ili waweze kukokotoa ukwepaji wa kodi unaofanywa na wageni hao. 

Aliongeza kwamba Mamlaka ya Mapato TRA wamefanya kazi yao kwa mujibu wa sheria waliwafanyia makadirio kwa mwaka 2019 ambapo wamelipa kodi ya sh.milioni moja za kitanzania na faini ya milioni 4.5 kama adhabu kwa kukiuka sheria ya matumizi ya EFD. 

“Vilevile wageni hao wameamua kuachana na biashara za ujanja ujanja,wamesajili biashara yao na kupewa TIN na kuanzia sasa watakuwa wanafanya biashara na serikali nayo kupata kodi yake” Alisema Mkuu huyo wa Takukuru mkoa wa Tanga. 

Hata hivyo alisema kutokana na hali hiyo walitoa mapendekezo kwa ngazi za juu ili operesheni iliyofanyika Tanga iendeshwe kwa nchi nzima kuwabaini wageni wote wanaoshirikiana na wazawa kuhujumu uchumi wa nchi kwa kukwepa kulipa kodi huku wakijipatia fedha nyingi kwa kusingizio kwamba wanafanya utafiti wa soko kabla hawajaja kufungua biashara. 

Wakati huo huo alisema kwamba katika kipindi hicho Taasisi hiyo imepokea jumla ya taarifa 70 za vitendo vya rushwa katika idara mbalimbali na uchunguzi wa taarifa hizo bado unaendelea kabla ya kufikia maamuzi mengineyo kwa kadri ya ushahidi utakaokuwa umapetikana. 

Alisema kwa upande wa uendeshaji wa mashitaka mahakamani kuanzia Aprili hadi Juni mwaka huu Taasisi hiyo iliendesha jumla ya mashauri 25 ambapo mashauri 23 yalifunguliwa kabla ya Aprili 2019. 

Hata hivyo alisema katika kipindi tajwa shauri namba (CC 45/2017) lilifika mwisho na kutolewa maamuzi ambapo mtuhumiwa alitiwa hatiani na kwenda Jela kutumikia kifungo cha miaka saba au kulipa faini ya milioni nne na mtuhumiwa huyo amekwisha tekeleza hukumu hiyo kwa kulipa faini. 

WAZIRI MKUU AKUTANA NA RAIS WA MISRI

$
0
0

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fatah Al Sisi, katika Ikulu ya Rais, mjini Cairo, Julai 10.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fatah Al Sisi, katika Ikulu ya Rais, mjini Cairo, Julai 10.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

*Wazungumzia namna ya kuimairisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah Al- Sisi, ambapo wametumia fursa hiyo kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za Tanzania na Misri.

Mbali na kuzungumzia masuala hayo ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kisiasa, kiuchumi na kijamii, pia Waziri Mkuu amemfikishia Rais wa Misri salamu kutoka kwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Mazungumzo baina ya Waziri Mkuu na Rais wa Misri yamefanyika leo (Jumatano, Juni 10, 2019) Ikulu jiji Cairo, ikiwa ni katika siku ya tatu na ya mwisho ya ziara yake ya kikazi nchini Misri. Katika ziara hiyo ameambatana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga.

Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya kikazi nchini Misri ambapo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cairo ameagwa na Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi wa Misri, Dkt. Ezz Eldien Abo Setit.

Akiwa ziarani nchini Misri, Waziri Mkuu alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly katika siku yake ya kwanza ya ziara yake, ambapo aliwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Misri waje kuwekeza nchini.

Pia, Waziri Mkuu alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo nchini humo ambayo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa makao makuu mapya ya nchi hiyo, mradi wa awamu ya pili ya upanuzi wa mfereji wa Suez Canal na kiwanda kikubwa cha ngozi.

Tanzania yakabiliwa na upungufu wa samaki tani 350,000

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Tanzania ina Upungufu wa Tani zipatazo 350,000 za Samaki kwa mwaka huku mahitaji yakiwa ni Tani 700,000 ambapo kwa mwaka kiasi cha tani 350,000 kinazalishwa,hivyo watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa ya uzalishaji ili kufikia malengo ya mahitaji ya samaki.

Kauli hiyo imeelezwa jijini Arusha na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega wakati wa kutiliana saini makubaliano ya mashirikiano baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku.

Ulega amesema kuwa ushirikiano huo wa kimaendeleo na nchi ya Uholanzi umefikia miaka zaidi ya 40 katika njanja mbali mbali,ikiwemo kilimo cha Mboga mboga,Viazi Mviringo, Ufugaji wa kuku na Samaki yanayosaidia kuongeza uzalishaji wa protini na mapato kwa Taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa Tanzania inauhitaji mkubwa wa protini inayotokana na samaki na kuku ndio maana wamekubaliana na Taifa hilo la uholanzi kuweza kuboresha Nyanja hizo kwa lengo la kutoa elimu kwa wafugaji na wakulima wa mazao ya samaki.

“Kama nchi tumejipanga kuhakikisha ukuaji wa sekta ya ufugaji wa Samaki na kuku unakuwa kwa kiasi kikubwa kuongeza Pato la taifa kutoka asilimia 9 tunazochangia katika pato la taifa”

Amesema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha kwamba Uzalishaji wa kuku na Ufugaji wa samaki unaboreshwa na kuona viwanda vya kuchakata mazao hayo kuondoa changamoto mbali mbali ili kufikia malengo ya uzalishaji na kuondoa upungufu wa uhitaji wa soko.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega Ulega pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn Sonnema kutoka nchini Uholanzi wakitia saini makubaliano ya mashirikiano baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku (picha na Woinde Shizza,Arusha).
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega Ulega pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn Sonnema kutoka nchini Uholanzi wakibadilishana nyaraka mara baada ya kutia saini.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega Ulegaakiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutia saini nyaraka hizo za makuliano mashirikiano baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku .
Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn Sonnema kutoka nchini Uholanzi akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo, Elisante Ole Gabriel zawadi ambayo wametoka nayo nchini uholanzi.

MAABARA INAYOTEMBEA YA UTAFITI WA UDONGO YAZINDULIWA RASMI ARUSHA

$
0
0


Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega watatu kulia , Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn kutoka nchini Uholanziwa tatu kushoto ,pamoja na Dkt Edmond Matafu wa kwanza kulia pamoja na viongozi wengine wakikata utepe ikiwa ni ishara ya maabara hiyo ya kutembea imezinduliwa rasmi.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn kutoka nchini Uholanzi wakikata utepe ishara ya kufungua rasmi maabara za utupimaji wa udongo
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipeana mkono na Dkt Edmond Matafu ambaye ni moja wa wawekezaji walioleta maabara hiyo ambayo itaidia sana wakulima kwani watakuwa wanapima udongo huo kabla ya kulima .
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiongea jambo mara baada ya kuzindua maabara hiyo ya upimaji wa udongo. 


Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amezindua Maabara ya kutembea ya kufanya utafiti wa kupima ubora wa udongo kwa wakulima ili kupata uhakika wa kuwa na mazao mengi yenye ubora kwa kutumia teknolojia hiyo mpya ya upimaji wa Udongo iliyoletwa kutoka nchini Uholanzi na Mtanzania Dkt.Edmund Matafu Makazi wa jijini Arusha.

Amesema kuwa Teknolojia hiyo ambayo ni yakwanza hapa nchini, itakuwa mkombozi kwa mkulima na kuongeza mapato na uzalishaji kwa kujua jiografia,eneo na udongo,kwani thamani ya malipo ya upimaji huo ni rafiki kwa wakulima kuchangamkia fursa ya upimaji.

Kwa upande wake ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya live support systerms limited inayojishuhulisha na shuhuli ya upimaji wa udongo pmoja na utengenezaji wa Mbolea Tanzania Dkt Edmond Matafu alisema maabara hiyo itawasaidia kubaini virutubisho na muundo wa udongo wa eneo husika ,hivyo kumwezesha mkulima kujua mazao gani yanayostahili kulimwa katika eneo husika na kuepuka kilimo cha kubahatisha ambacho kimekuwa kikiwaletea hasara wakulima walio wengi nchini.

‘’Maabara hii tulianza kuitumia nchini Kenya na sasa imeingia nchini na imekuwa na manufaa makubwa kwa wakulima kuweza kubaini mapungufu katika udongo na jinsi ya mahitaji ya mbolea’’.Alisema dkt Matafu

Alibainisha kuwa kabla ya kuzindua maabara hii watanzania walikuwa wanakosa huduma hii kwa hapa nchini kwani walikuwa wanalazimika kwenda hadi nje ya nchi ikiwemo Kenya kupima udongo huo 

Alisema kuwa huduma hii itamnufaisha mkulima kutokana na kupata mazao mengi mara baada ya kupima udongo ambao anataka kulima na baadae kupewa ushauri ni mbolea gani itakayomsaidia kumpa mavuno mengi,na pia itamsaidia kupunguza upotevu wa fedha kwani atakuwa analima sehemu ambayo kaipima pia atakuwa amepewa anunue mbolea gani itakayo msaidia.

WAZIRI WA AFYA HAMAD RASHID AWAAGA MADAKTARI WA KICHINA ZANZIBAR

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum akitoa hotuba ya Shukrani kwa Madakari wa Kichina katika Hafla maalum ya kuwaaga baada ya kumaliza muda wao ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitoa hotuba katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari wa Kichina baada ya kumaliza muda wao ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
 Kiongozi wa Timu ya Madaktari wa Kichina waliomaliza muda wao wa kutumikia Dk,Zhang Zhen akitoa hotuba ya shukrani katika Hafla maalum ya kuwaaga baada ya kumaliza muda wao ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
 Kiongozi wa Timu ya Madaktari wa Kichina waliofika Nchini DK,Yang Xiaodong akitoa hotuba yake katika hafla maalum ya kuwaaga wenzao waliomaliza muda wao ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
 Waziri wa Afya Hamad Rashid (kulia)akimpa zawadi kiongozi wa Timu ya Madaktari waliomaliza muda wao Dk,Zhang Zhen katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari wa Kichina baada ya kumaliza muda wao ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
 Baadhi ya Madaktari wa Kichina waliohudhuria katika Hafla maalum ya kuwaaga baada ya kumaliza muda wao wa kutumikia ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Afya na Madaktari wa Kichina katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari hao baada ya kumaliza muda wao ikiwa ni kawaida kila baada ya mwaka mmoja na kuwapisha wenzao wengine kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na Upasuaji na Kichocho,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

CHAWATIATA WAILILIA SERIKALI KUWAPA LESENI

$
0
0

Na Woinde Shizza michuzi blog, Arusha

Chama cha waganga na wakunga wa dawa za tiba za asili jijini Arusha CHAWATIATA leo kimetoa tamko rasmi la kusisitiza kupewa leseni zao ambazo walizilipia kwa mda mrefu bila kuzipata na hivyo kupelekea kushindwa kufanya tiba kwa jamii kutokana na kutokuwa na leseni hizo

Akizungumza wakati wa mkutano uliowakutranisha waganga wa tiba za asili jijini Arusha katibu wa chama hicho Omar Mpera amesema kuwa kutopata leseni za kufanya tiba kumekwamisha shushuli zao na hivyo kurudi nyuma kimaendeleo

Aidha amesema kuwa wamezilipia miaka mingi iliyopita mara baada ya serikali kutoa tamko la kuwataka wawe na leseni hizo lakini hawajaona mrejesho wowote hivyo kukwama kufanya huduma ya tiba

Nao baadhi wa waganga wa tiba za asili jijini Arusha wamesema kuwa serikali imekuwa ikiwasahau hasa katika kukamilisha usajili wao na kupata leseni ambapo kwa sasa wamekata tamaa ya kufanya kazi zao kwa uweledi kwa kuhofia kuchukuliwa hatua kutokana na kutokuwa na leseni hizo

Hata hivyo wameahidi kuhuduia jamii kwa uwaminifu na kutumia miti shamba ambayo haina madhara kwa afya ya binadamu ili kuweza kunusuru maisha ya wananchi.
Badhi ya wanachama wa chama cha waganga na wakunga wa dawa za tiba asili mkoa wa Arusha

ASILIMIA 90 YA WAGONJWA WA MOYO WANATIBIWA TANZANIA

$
0
0
Mratibu Mkuu wa kampuni ya SUKOS KOVA Foundation Rahma Kova akimwelezea Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile namna ambavyo kizimia moto cha kisasa kilichofungwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kinavyotumika wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo pamoja na kupokea vizima moto vilivyotolewa na kampuni ya SUKOS KOVA Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza na mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya moyo Asha Luhomo wakati wa ziara yake kutembelea taasisi hiyo pamoja na kupokea vizimia moto vilivyotolewa na kampuni ya SUKOS KOVA Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akimpatia zawadi mtoto aliyelazwa katika taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya moyo Sophia Kuduka wakati wa ziara yake kutembelea taasisi hiyo pamoja na kupokea vizimia moto vilivyotolewa na kampuni ya SUKOS KOVA Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akiwasalimia wananchi wanaosubiri kupatiwa huduma ya matibabu katika taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake kutembelea taasisi hiyo pamoja na kupokea vizimia moto vilivyotolewa na kampuni ya SUKOS KOVA Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akikagua jalada la mgonjwa alipotembelea wodi ya wototo wenye magonjwa ya moyo wakati wa ziara yake kutembelea taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na kupokea vizimia moto vilivyotolewa na kampuni ya SUKOS KOVA Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza na wazazi waliowapeleka watoto wao katika kliniki ya magonjwa ya moyo wakati wa ziara yake kutembelea taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na kupokea vizimia moto vilivyotolewa na kampuni ya SUKOS KOVA Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akimsikiliza Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka nchini Marekani Prof. Marath Aubyn wakati wa ziara yake kutembelea taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na kupokea vizimia moto “Fire Extinguisher” vilivyotolewa na kampuni ya SUKOS KOVA Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution leo katika taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi kizimia moto kilichotolewa na kampuni ya SUKOS KOVA Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution leo katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Jumla ya vizimia moto 12 vya kisasa vimefungwa katika maeneo mbalimbali ya taasisi hiyo.


Na.WAMJW,Dsm.

Asilimia tisini ya wagonjwa wanaokabiliwa na matatizo ya moyo waliokuwa wanatibiwa nje ya nchi, hivi sasa wanatibiwa ndani ya nchi kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete (JKCI).

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, alipofanya ziara kwenye hospitali hiyo ambapo alitembelea jengo la watoto lililofanyiwa ukarabati hivi karibuni.

Dkt.Ndugulile alisema Serikali inaendelea kufanya maboresho ya sekta ya afya kuanzia huduma za msingi hadi za kibingwa kwa kuwezesha vituo zaidi ya 352 kutoa huduma za upasuaji wa dharura wa kumtoa mtoto tumboni.

Alisema hivi sasa ujenzi wa hospitali 67 za wilaya unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba tangu Uhuru kumekuwako na hospitali 70 za Wilaya pekee, hivyo idadi itaongezeka.

“Nawapongeza sana JKCI kwa maboresho makubwa mliyofanya katika jengo ya watoto ni ya kiwango kikubwa sana, hongereni sana, hivyo hatutarajii hospitali kama hii iwe inatibu magonjwa madogo madogo ambayo yanaweza kutibiwa kwenye hospitali za rufaa za wilaya au mikoa,” alisema.

Aliongeza kusema kuwa, katika miaka minne ya uongozi, serikali imeweza kupiga hatua kubwa kwani ikiwamo kupunguza idadi ya wagonjwa wengi walikua wanatibiwa nje ya nchi.
“Kwa hatua hii, tumeweza kupunguza gharama za matibabu nje ya nchi tulikuwa tunaweza kuhudumia watu wachache lakini kwa kuwa yanapatikana ndani wananufaika watu wengi, kwa gharama ile ile nje ya nchi angetibiwa mtu mmoja, ndani wanatibiwa watu wapatao watatu,” alibainisha.

Alisema mafanikio hayo ni matokeo ya hatua za kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mafunzo madaktari wa ndani (wazalendo) ambapo sasa wanaweza kufanya upasuaji mkubwa wao wenyewe.

“Hivyo, Serikali itaendelea kuwapatia mafunzo wataalam wa afya na kuwapatia vibali kwenda kujifunza ama kusoma nje ya nchi ili kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini na kuweza kuwatibia wananchi.

Aidha, katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile alipokea vifaa vya kuzima moto vipatavyo kumi na mbili vya hospitali hiyo kutoka kampuni ya SUKOS Kova Foundation inayomilikiwa na Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova, kwa kushirikiana na kampuni ya One Extreme Solution ya hapa nchini.

Dkt. Ndugulile alisema Watanzania wengi wanafariki wakati wa uokoaji kwani watu wengi hawana elimu ya uokoaji kwani zipo kanuni zinazotumika wakati wa kumuokoa mtu anayepata ajali.

RAIA WA KIGENI WAKWEPA KIFUNGO CHA MIAKA 3, WALIPA FAINI.

$
0
0
Na EmanuelMadafa,MichuziMbeya .

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mbeya imewahukumu kwenda jela miaka mitatu raia watatu wa kigeni ama kulipa faini ya shilingi milioni kumi kila mmoja baada ya kukiri kukutwa na madini ya dhahabu gramu 1043 sawa na kilo 1.33 kinyume cha sheria ya madini No. 14 ya mwaka 2010.

Julai mwaka huu watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na shitaka moja la uhjumu uchumi ambalo ni kumiliki na kusafirisha Madini yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 98.5.

Washitakiwa hao ambao ni Clive Rooney (62) raia wa Ireland, na wenzake wawili Ross Stephen Harris 34 na Robert Charles Wheedon (59) raia wa Uingeza wamekutwa na madini hayo katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya julai 3 mwaka huu.

Hukumu hiyo imetolewa na Kaimu Hakimu Mfawidhi Venance Mulingi baada ya washtakiwa kukiri mashitaka yanayowakabili.Na kisha Mahakama hiyo ikaamuru madini hayo yataifishwe na yakabidhiwe Benki kuu ya Tanzania (BoT) hadi serikali itakavyoamua vinginevyo.

Mapema mwendesha mashtaka wa serikali Jacqueline Nyantori ameieleza mahakama kuwa washtakiwa walimwandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP wakiomba kupewa nafasi ya kukiri kosa.

Katika barua hiyo washtakiwa wamemwomba DPP kutoa kibali ili kesi yao ishuke kutoka mahakama kuu hadi mahakama ya wilaya na kueleza kuwa wako tayari kulipa faini ama kupewa adhabu yoyote ikiwemo kurejesha madini.Kabla ya hukumu kutolewa wakili wa upande wa utetezi James Kyando ameiomba Mahakama kuwapunguzia adhabu wateja wake kwa kuwa ni wageni na pengine wamefanya hivyo bila kujua kuwa ni makosa.

Hata hivyo upande wa Jamhuri ukiongozwa Jaqueline Nyntori umepinga vikali madai hayo na kueleza sababu kuu tatu za kuitaka mahakama itoe adhabu kali ili iwe funzo kwa wengine kutokna na serikali kuwa kwenye vita kali ya kiuchumi na kwamba walikuwa wnakwepa kulipa kodi.

Baada ya maelezo ya mawakili wa pande zote mbili Washitakiwa hao wamekiri kosa kukubali kulipa faini ya shilingi milioni 10 kila mmoja huku wakikwepa kwenda Jela kutumikia kifungo cha miaka mitatu.

TAKUKURU YAELEZEA HATUA KWA HATUA ILIVYOMNASA ALIYEJIFANYA OFISA USALAMA WA TAIFA IKULU NA KUTAKA KUMTAPELI DC WA KISARAWE

$
0
0
*Yasema kwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa Kisarawe  basi atafikishwa Mahakama ya Mkoa wa Pwani

*Yatoa onyo kwa wote wenye tabia ya kufanya vitendo vya kitapeli kwani TAKUKURU iko  macho, itawanasa


Na Humphrey Shao, Michuzi Tv Dar es Salaam

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ofisi ya Dar es Salaam inamshikilia mkazi wa Chamazi Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za kujifanya Ofisa wa Serikali – kutoka ofisi ya Usalama wa Taifa na kutaka kumtapeli Mkuu wa Wilaya Kisarawe mkoani Pwani.

Hata hivyo TAKUKURU imesema kwa kuwa watuhumiwa huyo alitaka kufanya UTAPELI katika Wilaya ya Kisarawe basi atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani ili sheria ichukue mondo wake.

Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa TAKUKURU Ali Mfuru kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Julai 10,2019 amefafanua kuwa mtuhumiwa huyo anayejulikana kwa jina la Omari Khamis Chuma( 55), alikamatwa na maofisa wa TAKUKURU baada ya kupokea taarifa kuwa mtuhumiwa huyo alifika katika Ofisi zaMkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kwa nia ya kumtapeli kwa kujifanya kuwa yeye ni Ofisa wa Serikali kutoka Usalama wa Taifa – IKULU.

Amesema baada ya kupokea taarifa hizo pamoja na taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali, TAKUKURU ilianzisha uchunguzi dhidi ya mtuhumiwa huyu na kuthibitisha makosa chini ya sheria zifuatazo ikiwemo Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007:

Amesema makosa hayo ni kujifanya Ofisa wa Serikali kinyume na kifungu Na 100 (b) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) Sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002 pamoja na kuomba, kushawishi au kujaribu kujipatia au kujipatia rushwa kinyume na Kifungu Na. 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na 11/2007

"Hatua ya kumkamata tapeli huyu imefikiwa takriban wiki tatu tu tangu TAKUKURU iutangazie umma kuhusu kukamatwa kwa matapeli wengine sita waliokuwa wakishirikiana kufanya utapeli. Kati ya watuhumiwa wale – Wanne kati yao walijifanya kuwa ni maofisa wa TAKUKURU pamoja na maofisa wa byombo vingine vya Dola na wawili kati yao walitoka katika kampuni ya Simu.

"Uchunguzi wetu umebaini kuwa matapeli hawa wana mtandao unaojumuisha watu kutoka maeneo na ofisi mbalimbali zikiwemo za Serikali na wamekuwa wakiwafuatilia watumishi au viongozi ambao kwa njia moja au nyingine wanaweza kuwa na tuhuma na hivyo kuwadai fedha rushwa  huku wakijifanya wao ni maofisa kutoka TAKUKURU au Usalama wa Taifa"amesema Mfuru.

Hata hivyo ametoa agizo kupitia vyombo vya habari kuwataka matapeli kuacha mchezo huo mara moja kwani TAKUKURU iko macho na inayo mamlaka kisheria ya kuwachukulia hatua wale wote wanaojihusisha na vitendo vya utapeli.

Kuhusu wapi mtuhumiwa aliyekata kumtapeli DC Mwegelo, amesema kuwa "Kwa kuwa mtuhumiwa huyu alitenda makosa haya katika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, basi atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi - Mkoa wa Pwani leo Jumatano Julai 10, 2019 ili kujibu mashitaka yanayomkabili,"amesema.

Pia anaendelea kutoa tahadhari kwa jamii na kuwataka kuwa makini na kutokubali kurubuniwa kwa njia hizo wanazozitumia matapeli wa aina hiyo kujinufaisha na kuongeza anaendelea kuwahimiza wananchi kutupatia taarifa sahihi za matapeli wa aina hiyo au yeyote anayejihusisha na vitendo vya Rushwa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa bila kumwonea mtu au kumpendelea yeyote.

"Taarifa hizi zinaweza kutumwa kwetu kupitia mfumo rasmi wa mawasiliano lakini pia wanaweza kuwatumia Viongozi wa Dini au chombo chochote cha Dola na taarifa hizo zitatufikia.Tunatoa shukrani kwa wananchi ambao wamekuwa ni msaada mkubwa katika kutupatia taarifa ikiwa ni pamoja na wadau mbalimbali tunaoshirikiana nao katika kueneza elimu dhidi ya rushwa kwa jamii yetu,"amesema.
 Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi wa TAKUKURU, Ali.S.Mfuru Kulia akiwa na Mtuhumiwa anayejifanya usalama wa Taifa ndugu Omar Chuma mbele ya Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika makao makuu ya Tasisi hiyo jijini Dar es Salaam 
 Kaimu Mkurugenzi wa uchunguzi TAKUKURU Ali.S.Mfuru akizungumza na Waandishi wa habari juu ya kumkamata tapeli aliyejifanya usalama wa Taifa

MUHIMBILI YAPOKEA MASHINE MPYA YA KISASA YA KUCHUNGUZA NA KUPIGA PICHA WAGONJWA WA MACHO.

$
0
0
Na Humphrey Shao, Michuzi Tv Dar es Salaam

Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia idara ya watoto imepokea Mashine mpya ya kisasa ya kuchunguza na kupiga picha kwa wagonjwa wa macho wanaofika hospitalini hapo.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Rawlence Mseru amesema mashine hiyo yenye uwezo wa kupiga picha nyuma ya retina itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la wagonjwa kutoka hospitalini happy kwenda kufanya vipimo sehemu nyingine.

"Mashine hii ya kisasa imenunuliwa na kikundi Cha kwaya ya watoto kutoka kanisa kuu London uingereza ambalo watoto hao walichangishana na kununua mashine hii yenye thamani zaidi ya milioni 100"

Kwa upande wake Dr John Kisimbi Daktari bingwa wa magonjwa ya macho kwa watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili idara ya watoto Amesema kuwa kwa Sasa mashine hiyo katika hospitali hiyo ni Moja tu tangu ile iliyonunuliwa miaka ya nyuma kuharibika kutokana na kukaa kwa muda mrefu.

Ametaja kuwa uwepo wa mashine hiyo itasaidia kuhudumia wagonjwa wengi ambao walikuwa wanachelewa kupata huduma kutokana na vipimo vyao kuchelewa kutoka nje.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Rawlance Mseru akipokea kifaa hicho kutoka na kiongozi wa kundi la wasamaria wema kutoka nchini uingereza , Mathew Wright wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jengo la Watoto Muhimbili.

Afisa uhusiano wa Hospitali y Taifa Muhimbili,Aminiel aligaisha akizungumza na wafachili pamoja na wadau wa Hospitali ya Muhimbili.

KESI YA KUMILIKI MALI KULIKO UWEZO WAKE INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU TAKUKURU YAUNGURUMA TENA MAHAKAMANI,ALIYEMUUZIA KIWANJA ATOA USHAHIDI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa mkataba wa mauziano ya kiwanja kati ya aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru Godfrey Gugai, na aliyemuuzia Abubakar Hamis uliandikwa Sh.milioni 60 lakini walipewa Sh.milioni 80 ili wapate ahuweni ya kodi.

Hamis (46), ambae ni mkazi wa Boko, na shahidi wa 20 katika kesi utakatishaji fedha na kumiliki mali zilizozidi kipato, inayomkabili Gugai na wenzake wanne.

Akiongozwa na Wakili wa serikali kutoka (Takukuru) Awamu Mbagwa, kutoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, shahidi huyo amedai mahakamani hapo  kuwa Gugai ni jirani yake na amewahi kufanya nae biashara.

Amedai walifanya makubaliano baina ya familia ya Gugai ya kuuziana kiwanja namba 64 kilichopo kitalu C eneo la Boko Ununio Dar es Salaam, kwa Sh. milioni 80 na malipo yalifanyika kwa fedha taslimu ambapo mwanasheria wake alienda kuandaa mkataba na walipofika nyumbani kwake jioni aliwapa na kuusoma kisha akawakabidhi fedha.

Shahidi ameendelea kudai kuwa mkataba huo uliandikwa Sh.milioni 60 tofauti na makubaliano lakini walikabidhiwa fedha taslimu Sh.milioni 80 na uliandikwa hivyo ili kuweza kupata ahuweni ya kodi.

Baada ya maelezo hayo, shahidi huyo aliiomba Mahakama kupokea mkataba wa mauziano ya kiwanja kama kielelezo baada ya kuutambua kwa majina na saini lakini upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Semi Malimi ulipinga kupokelewa kwa mkataba huo wakidai kuwa ni nakala na sio nyaraka halisi ya mkataba.

Alidai nakala yoyote inayotolewa mahakamani lazima iwe halisi kwa mujibu wa sheria kifungu 67 (1) na kama ni nakala yapo mazingira yanayoruhusu ipokelewe.Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 11, mwaka huu atakopotoa uwamuzi kama kielelezo hicho kipokelewe au la.

Gugai na mwenzake watatu wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Kwa mara ya kwanza washitakiwa hao walifikishwa Mahakamani Novemba 16 mwa 2017 ambapo walinyimwa dhamana kutokana na shtaka la utakatishaji kutokuwa na dhamana.Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.


Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decembea 2015.Inadaiwa kuwa akiwa Takukuru Dar es Salaam, Gugai alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh bilioni 3.6 ambazo hazilingani na kipato chake huku akishindwa kuzitolea maelezo.

ENVIRONMENTAL INSTITUTIONS TO DEVELOP, SUPPORT ENVIRONMENT INVOLVEMENT

$
0
0
By Michuzi TV Reporter 

ENVIRONMENTAL stakeholders in the country have asked the government to ensure that researchers and innovators of renewable energy are given priority and assistance. 

The stakeholders expressed their unhappiness over devastation of the environment in which its impact has started to be seen including the increasing temperatures in some countries, citing India where people died because of the high temperature.

However, the government said innovation in energy generating is one of areas that generate jobs, increase productivity and alleviate poverty for bringing sustainable development.

It said that the community should change the focus and open the scope of the sensitivity to the positive eye because it provides a wide range of commercial and productive opportunities.

This was stated by Deputy Director General of Business Development Authority (TANTRADE), Ratifa Hamisi, on behalf of the Minister of State, Vice President's Office, Union and Environment, Mr January Makamba.

She was speaking yesterday during the Climate Change Forum on Trade Showers at Dar es Salaam International Trade Fair (DITF).

She said the government recognizes the presence of the various cadastics designers in the energy sector as one of the key players to address climate change impacts.

She clarified that the Climate Change Forum, which was developed by the FORUMCC Agency to provide energy education, she said the Government recognizes the challenges of environmental degradation and the effects of climate change to achieving country's goal to reach middle income economy.

"The Government of Tanzania through the Ministry of Energy and Minerals has developed a program on energy development since 2016 ( Power System Master Plan (PSMP). This system focuses on economic growth and government policies and guidelines," she stated.

On his part, Acting Director of Rural Energy Agency (REA) Engineer Amos Magang recognized the contribution made by the university researchers and innovators in the country's development.

"Almost 20 projects REA has been able to assist various innovators in ensuring that they are doing their work properly and assist the country in various challenges," he said.There are programs that are ongoing that help various innovators.

At the same time the Director of ForumCC Agency Rebecca Muna has highlighted the importance of Tanzania's industries to develop confidence.

However, Mu has called on designers to see the potential of energy in this energy and the Government advised to start creating a positive environment for policy and legislation in nurturing and promoting innovative talent in this renewable energy sector.He insisted that "If these talents are developed for our designers we will be able to provide a very large amount of access to clean and safe energy for our industries in the country."

"Tanzania is a source of so much natural resources so that investments are made in such sources we have a great potential for producing energy, including animal droppings," he said.Adam Nalima, a student of Saint Joseph College, said they decided to come up with the idea of ​​enabling them to improve the environment in the country that was the power of electricity through the energy of the sun and the wind at the same time.

She added that the use of renewable energy will significantly reduce the impact of climate change.

"These challenges have affected productivity in the agricultural sector which is a major contributor to industrial raw materials, water shortages that are used in manufacturing and the production of energy and the destruction of infrastructure that is used to combine raw materials, manufacturing and marketing, we believe the use of energy efficiency will help. substantially eliminate this climate of climate change, ”he said

He said the energy in Tanzania requires a detailed information system for the energy sector in order to identify future development strategies and to ensure policy makers and decision makers have accurate information about renewable energy.

MATUKIO YA PICHA ZA RAIS DKT MAGUFULI AKIWA WILAYANI KARAGWE MKOANI KAGERA.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amembeba mtoto wa mmoja wa abiria wa daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Bukoba mjini kuelekea Karagwe mjini mara baada ya kuwasalimu wakati waliposimama katika Kituo hicho cha Daladala kilichopo katika kijiji cha Kihanga nje kidogo ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mwanafunzi wa Shule ya Sekondary aragwe ambaye alikuwa akisafiri na daladala hiyo. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Abiria wa Daladala iliyokuwa ikitoka Bukoba mjini kuelekea Karagwe mjini mara baada ya kuwasalimu wakati waliposimama katika Kituo cha Daladala kilichopo katika kijiji cha Kihanga nje kidogo ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

DKT. KIJAJI AAHIDI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI IHARI

$
0
0

Mbunge wa Kondoa Vijijini (Naibu Waziri wa Fedha na Mipango), Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akifafanua jambo kwa wananchi wa Kijiji cha Ihari ambapo aliahidi kuufikisha mgogoro wa ardhi wa Kijiji hicho kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wiliam Lukuvi, kwa ajili ya utatuzi 
Mbunge wa Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi – Ihari, Bw. Issa Juma baada ya mkutano wa hadhara. 
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kondoa, Dodoma, Alhaji Othman Gora akiwasalimia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ihari wilayani humo ambapo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alikuwa mgeni rasmi.

Na Mwandishi wetu, Kondoa, Dodoma 


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameahidi kuupatia ufumbuzi mgogoro wa ardhi katika Kijiji cha Ihari wilayani Kondoa, baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wanaoishi katika Kijiji hicho. 

Ahadi hiyo aliitoa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji hicho ambapo wananchi na viongozi walipata nafasi ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili. 

Wananchi wa Kijiji hicho walieleza kuwa mgogoro huo umesababisha wengi wao kukosa mahala pa kuchungia mifugo yao kwa kuwa eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya malisho limevamiwa na kubadilishwa matumizi kuwa mashamba. 

Dkt. Kijaji ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini, alisema taarifa za mgogoro huo ataziwasilisha kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ili aweze kutatua changamoto hiyo ambayo imekuwa kero kwa wananchi hao. 

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mheshiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni Serikali ya wanyonge na imepanga kutatua kero mbalimbali za wananchi ikiwemo migogoro yote ya ardhi nchini. 

Dkt. Kijaji aliwaomba wananchi hao wawe na Subira katika kipindi hiki ambacho Serikali inaenda kushughulikia tatizo lao huku akibainisha kuwa utatuzi wa mgogoro huo unategemea sana utulivu wao kama walengwa. 

“Niwaombe ndugu zangu tueendelee kuilinda amani ya Ihari, tuendelee kuilinda amani ya Kondoa na nchi yetu kwa ujumla katika kipindi hiki ambacho tunamsuburi Waziri wa Ardhi ambaye anajua matumizi ya kila kipande cha ardhi nchini, atatue mgogoro huu”, alisisitiza. 

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihari, Bw. Idi Lumba amemshukuru Dkt. Kijaji kwa kutenga muda wa kusikiliza changamoto zao hususan tatizo la ardhi ambalo lilianza kuwagawa wananchi wake. 

Bw. Lumba alimhakikishia Mbunge huyo kuwa hali ya Kijiji cha Ihari itaendelea kuwa tulivu kwa kipindi chote ambacho watakuwa wanasubiria suluhu ya mgogoro huo, huku akielezea changamoto ya maji na umeme katika Kijiji hicho ambazo Dkt. Kijaji aliahidi kuzitatua kwa haraka.

TUNA OFISI 29 MIKOA YOTE TANZANIA BARA NA ZANZIBAR, FIKENI MUHUDUMIWE - PSSSF

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) popote pale walipo Tanzania bara na Visiwani, wamesogezewa huduma karibu ambapo Mfuko una jumla ya ofisi 29 mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar.
Meneja wa Mfuko huo Mkoa wa Temeke, Bi. Ritha Ngalo, amewaambia waandishi wa habari kwenye banda la PSSSF namba 13 kwenye viwanja vya Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam leo Julai 10, 2019 kuwa kwa wale watakaofanikiwa kufika kwenye Maonesho hayo, yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, wasisite kupita kwenye banda hilo ili wapatiwe huduma sawa na zile wanazohitaji kuzipata kwenye ofisi mbalimbali za Mfuko.
Serikali kupitia Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma namba 2 ya mwaka 2018 ilifuta mifuko ya hifadhi ya jamii ya PPF, PSPF, LAPF  na GEPF na kuanzisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Waatumishi wa Umma PSSSF.
Maonesho hayo yanatarjiwa kufikia kilele Julai 13, 2019.
Mstaafu Francis Ramadhan Njau, (kulia), ambaye alikuwa Afisa Ushirika Daraja la I, akihudumiwa na Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mkoa wa Temeke, Bi.Ritha Ngalokwenye banda la Mfuko kwenye viwanja vya Maonesho Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 10, 2019. Aliyesimama kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi.
Wanachama wa PSSSF, wakiwa tayari wamehudumiwa.
Mwanachama akipatiwa taarifa alizohitaji kutoka PSSSF alipotembelea banda la Mfuko huo Julai 10, 2019.
Afisa Michango PSSSF Bi. Getrude Athanas (kulia), akimpatia maelezo ya kina mwanachama huyu aliyetembelea banda namba 13 la Mfuko huo kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Donald P. Maeda (kulia), akihakikisha kila swali alilokuwa nalo Mwanachama huyu linapatiwa majibu kwa vielelezo.
Meneja wa Mfuko huo Mkoa wa Temeke, Bi. Ritha Ngalo, (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Mfuko huo Julai 10, 2019. Kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfukmo huo Bw. Abdul Njaidi.
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mkoa wa Temeke, Bi.Ritha Ngalo (kulia) na Afisa Mafao Mfuko wa Mfuko huo, Bw. Salvatory Matemu, wakiwahudumia wanachama wa PSSSF waliotembelea banda la Mfuko kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 10, 2019.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 10.07.2019

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images