Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Benki ya Stanbic yatoa msaada wa vifaa tiba kwa hospitali ya taifa ya Muhimbili.

$
0
0
Mkuu wa kitengo cha Mikopo wa benki ya Stanbic Bank, Bwana Daniel Mbotto akimkabidhi baadhi ya vifaa tiba kwa mkuu wa jengo la wazazi block 2 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Bi. Suzan Ndambala hivi karibuni kama sehemu ya kuchangia upatikanaji wa huduma bora kwa kwa watoto wanaozaliwa na matatizo katika mfumo wa kupumua. Benki ya Stanbic imetoa mchango huo kama sehemu ya juhudi zake za kuchangia jamii katika sekta ya afya na elimu. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa benki na MNH. 
Mkuu wa kitengo Cha Mazingira ya Ndani kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Bi. Ester Mwambogoja (katikati) akiwashukuru baadhi ya wafanyakazi kutoka Benki ya Stanbic baada ya kupokea msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na benki hiyo hivi karibuni. Madhumuni ya kutoa vifaa hivyo ni kuchangia upatikanaji wa huduma bora kwa watoto wanaozaliwa na matatizo katika mfumo wa kupumua. Hii ni sehemu ya juhudi za Benki ya Stanbic katika kuchangia sekta ya afya na elimu katika jamii. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa MNH.

Ujenzi wa Barabara za Geita-Kagera

$
0
0
Muonekano wa barabara ya Bwanga- Biharamulo (km 68), ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika, barabara hiyo inaunganisha mkoa wa Kagera na Geita.
Muonekano wa barabara ya Lusahunga-Ushirombo (km 110), ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea, barabara hiyo ni sehemu ya barabara kuu ya Tinde – Isaka- Rusumo inayounganisha mikoa ya Kagera – Geita na Shinyanga
Mhandisi mshauri Thomas Kidane toka kampuni ya SMEC ya Australia akifafanua jambo kwa wahandisi Peter Sikalumba (kushoto), Joyce Mbunju, na Rubara Marandu (kulia) toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), walipokagua ujenzi wa barabara ya Lusahunga-Ushirombo (km 110), ambayo ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami.Muonekano wa barabara ya Lusahunga-Ushirombo (km 110), ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea, barabara hiyo ni sehemu ya barabara kuu ya Tinde – Isaka – Rusumo inayounganisha mikoa ya Kagera – Geita na Shinyanga.

DKT.NDUGULILE A TEMBELEA BANDA LA MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA (TMDA)

$
0
0
 Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza (wapili kulia)akitoka maelezo ya kiudhibiti  kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) leo alipo tembelea banda la  Mamlaka hiyo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Afisa Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),James Ndege akitoa elimu kwa wananchi namna Mamlaka hiyo inavyo kiudhibiti leo  walipo tembelea banda la  Mamlaka hiyo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), katika maonesho ya 43 ya Sabasaba mara baada ya kupata Maelezo ya kiudhibiti kwenye banda hilo tarehe 9 Julai, 2019

MRADI WA KUUNGANISHA UMEME VIJIJINI KATAVI WADAIWA KUSUA SUA

$
0
0


Na Mwandishi wetu, Katavi 

Mkuu wa mkoa wa Katavi bwana Juma Homera ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa kwanza; unaotekelezwa na kampuni ya ukandarasi kutoka china ya CRCEBG; kutokana na mradi huo kuonekana kusua sua ambapo umeunganisha umeme katika vijiji vinne tu kati ya vijiji ishirini na tisa vilivyopaswa kuunganishiwa huduma hiyo katika kipindi cha miezi mitatuiliyopita ya utekelezaji wa mradi 

Bwana Homera ameonyesha hali hiyo wakati wa kukagua mradi wa usambazaji umeme vijijini katika vijiji vya Mnyaki, Kapalala B na Society katika halmashauri ya nsimbo wilayani mpanda 

Akizungumza na watumishi wa TANESCO walioambatana na Meneja msaidizi wa REA awamu ya tatu mkuu huyo wa mkoa wa Katavi amewataka kuongeza kasi ya uwashaji umeme vijiji kwani wananchi wanasubiria huduma hiyo 

“Ukitazama mikoa mingine wako mbali sana ila hapa mmlelala, sasa hivi tunaandaa ilani ya chama cha mapinduzi tutaawaambia nini wananchi” alisema Homera .Aliongeza kuwa atawasilina na Waziri mwenye dhamana ili kuona kama kuna uwezekano wa kuweka usimamizi wa ziada katika utekelezaji wa mradi huo 

Akitoa sababu za kucheleweshwa kwa uwashaji wa umeme katika vijiji hivyo Meneja Msaidizi kutoka kampuni ya ukandarasi ya CRCEBG Mhandisi Arnold Nzali amesema wamepata changamoto ya uhaba wa vifaa ambapo wamelazimika kuagiza kutoka nchini China 

Nzali amesema mradi unahitaji vifaa vingi kwa wakati mmoja hali iliyoshindikana kupatikana kwa pamoja hapa nchini na hivyo kumlazimu Meneja wa mradi huo kuelekea nchini China kuvifuata .Hata hivyo amesema baadhi ya nguzo za umeme zimeanza kuwasili hivyo kazi inaendelea 

Naye Kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Katavi Mhandisi Dotto Chacha amesema kwa kila wiki mkandarasi anapaswa kuwasha umeme katika vijiji vitatu .Amesema kwa sasa mkandarasi amekwisha washa vijiji 4 kati ya 29 sawa na asilimia 18

MISS TANZANIA KUJULIKANA AGOSTI 23 , MWAKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Fainali za Taifa ya Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2019 chini ya uongozi mpya wa Kampuni ya The Look yatafanyika Agosti 23  2019 katika Ukumbi wa LAPF uliopo Makumbusho, maarufu kama New Millennium Tower.

Fainali  hizo zitafanyika baada ya kukamilika kwa mashindano ngazi ya Mikoa na Kanda ambayo bado yanaendelea kwa hivi sasa.
Mashindano hayo ya Mikoa na Kanda yamekuwa na msisimko sana kwa mwaka huu hasa baada ya kuongezeka kwa mikoa ya Songwe, Simiyu,Kagera ,Tanga na Shinyanga ambayo haikuwepo kwa mwaka jana.

Mara baada ya kukamilika kwa mashindano hayo ya mikoa na Kanda, washiriki wote wataanza kambi ya Taifa mnamo Agosti kwa takriban wiki 3 tayari kwa fainali hizo zitakazofanyika tarehe 23 Agosti 2019.

Ikumbukwe kwamba mrembo atakae shinda taji la Miss Tanzania 2019 atawakilisha Nchi yetu katika mashindano ya urembo ya Dunia ambayo mwaka huu yatafanyika London Uingereza tarehe 14 Disemba 2019. Aidha kampuni ya The Look inapenda kutoa hamsa kwa watanzania kuudhuria mashindano ya Dunia ili kuongeza motisha kwa muwakilishi wetu. Wale wote watakao penda kuudhuria mashindano ya Dunia wawasiliane na uongozi wa The Look kwa taarifa zaidi.
Mwandaaji wa Miss Tanzania Basila Mwanukuzi na Nelly Kazikazi Miss Tanzania no 2 -2018. wakionesha ngao Crown atakayovalishwa mshindi wa shindano la Miss Tanzania wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati walipotangaza tarehe ya kufanyika kwa fainali za shindano hilo leo jijini Dar es salaam.
Nelly Kazikazi Miss Tanzania namba mbili -2018 akizungumza katika mkutano huo huku muandaaji wa shindano la Miss Tanzania Basila Mwanukuzi akisikiliza.
Mwandaaji wa Miss Tanzania Basila Mwanukuzi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mwananyamala wakati alipotangaza tarehe ya kufanyika kwa fainali za shindano hilo leo jijini Dar es salaam kulia ni Nelly Kazikazi Miss Tanzania no 2 -2018.

WANAKIJIJI NA SERIKALI KUPITIA MRADI WA EQUIP WAKAMILISHA UJENZI WA SHULE SHIKIZI MWIRINGO MKOANI MARA

$
0
0
KUTOKA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI 

Wananchi wa Kijiji cha MWIRINGO, Kata ya Busambara WAMESHIRIKIANA na SERIKALI yetu kupitia Mradi wake na Wafadhili wa EQUIP kufanikisha ujenzi wa Shule SHIKIZI Kijijini humo.

Shule hiyo imejengwa kwenye Kitongoji cha Ziwa ndani ya Kijiji cha Mwiringo.

Shule Shikizi Mwiringo ni kati ya SHULE KUMI (10) MPYA za MSINGI zinazojengwa kwenye Jimbo la Musoma Vijijiji lenye Jumla ya Shule za Msingi 113 (111 za Serikali na 2 za Binafsi). 

Ujenzi wa hizo Shule kumi (10) ukikamilika na baadae zikapanuliwa ili kuchukua Wanafunzi wa Darasa la I hadi VII, Jimbo letu litakuwa na Jumla ya Shule za Msingi 123 (121 za Serikali na 2 za Binafsi). Safari ya kuelekea kwenye SHULE ZA MSINGI MBILI (2) KWA KILA KIJIJI (Vijiji 68, Kata 21) inaenda vizuri!

EQUIP (The Education Quality Improvement Programme) ilitoa Shilingi MILIONI 60 kwa ajili ya ujenzi wa: (i) Vyumba viwili (2) vya Madarasa, (ii) Ofisi moja (1) ya Walimu, na (iii) Matundu sita (6) ya Vyoo, yaani 4 ya Wanafunzi na 2 ya Walimu.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mwiringo, Mwl Surusi Mnene ambae ndie Mlezi wa Shule hiyo SHIKIZI, alieleza kuwa ujenzi huo ulianza Januari 2019 na hadi hivi sasa ujenzi umekamilika. Matenki mawili (2) ya kuvuna MAJI yako tayari na Mafundi wanakamilisha MADAWATI 50.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mwiringo, Ndugu Coletha Felix alieleza kuwa amefurahishwa sana na Jitihada za Wananchi wa Kijiji cha Mwiringo kwa NGUVUKAZI zao na ushirikiano wao mkubwa waliouonesha katika kuhakikisha ujenzi huo unakamilika haraka. Wananchi hao wamejitolea kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji kwa ajili ya ujenzi huu. 

Wanakijiji cha Mwiringo na Viongozi wao wa Jimbo la Musoma Vijijini, kwa pamoja, wanaishukuru sana SERIKALI yetu kwa jitihada kubwa inazofanya kwa kuwaunga mkono kwenye MIRADI ya MAENDELEO ikiwemo Miradi ya ELIMU na AFYA Kijijini mwao.

Picha hapo chini zinaonesha Shule SHIKIZI Mwiringo ikiwa imekamilika na tayari kupokea Wanafunzi kutoka Kitongoji cha Ziwa na kwingineko Kijijini Mwiringo, Kata ya Busambara.
 
 Muonekano wa Shule hiyo kwa nje iliyojengwa katika Kitongoji cha Ziwa ndani ya Kijiji cha Mwiringo,Musoma vijijini mkoani Mara


MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 10,2019

Tamasha la ZIFF 2019 latoa mafunzo kwa Watoto mfanano (Down Sydrome)

$
0
0

Na Andrew Chale, Zanzibar


TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) la 22 kwa mwaka huu leo limeendesha mafunzo kwa Watoto wenye tatizo la Down Syndrome ama Watoto mfanano kama wanavyojulikana visiwani hapa.

Mafunzo hayo yanayotolewa na ZIFF kwa kushirikiana na taasisi ya kutoka Uholanzi ya Media Lab ambayo imekuwa ikitoa mafunzo kwa watoto mbalimbali visiwnai hapa kwa kutumia teknolojia kwa masuala ya sanaa ikiwemo utengenezaji wa vikatuni, Uigizaji, utangazaji, uandishi wa habari, kuchora na mambo mengine katika masuala ya Sanaa.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Warsha za ZIFF 2019, Ahmed Harith amebainisha kuwa, mafunzo hayo ni ya mara ya kwanza kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati ambapo wanatarajia Watoto zaidi ya 1,000 kushiriki mafunzo hayo.

“Mafunzo haya yanatolewa kila siku kuanzia Julai 5 na yataisha mpaka mwisho wa tamasha. Ambapo kwa siku watoto zaidi ya 100 wanapata kushiriki.Watoto hao wanatoka shule mbalimbali za visiwani hapa na baadhi yao nje ya skuli” alisema Ahmed Harith.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Down syndrome Initiative Zanzibar, Bi. Ahlam Abdalla Azzam amelipongeza tamasha la ZIFF 2019 kwa kuwakumbuka watoto hao ambao wameweza kujifunza mambo mbalimbali kama watoto wengine licha ya uelewa wao kuwa mdogo.

“Tunaipongeza ZIFF kwa kuwajali watoto Mfanano wameweza kujifunza vitu vingi ikiwemo kuimba, kucheza na kufanya vitu vya ubunifu.Pia wameweza kujfunza namna ya kuchora michoro na na kutengeneza vikatuni kupitia program za kisasa za teknolojia ya Media Lab” alieleza Bi. Ahlam Abdalla Azzam.

Zanzibar inaelezwa kuwa na Watoto wengi wenye tatizo la Down Syndrome ambapo Serikali na wadau wamekuwa wakichukua hatua za kuwasaidia watoto hao. 









NAIBU WAZIRI MASAUNI, IGP SIRRO WAWASILI SHINYANGA KWA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Terack (katikati), baada ya kuwasili mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi.kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Terack, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Masauni amewasili mkoani Shinyanga leo kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana  na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Terack  baada ya kuwasili mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

ZIARA YA JPM NAMIBIA, YAWAIBUA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MIFUGO NCHINI

$
0
0
Na. Edward Kondela
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kufuatia ziara yake ya kikazi ya siku mbili aliyofanya nchini Namibia kuanzia Mei 27 hadi 28 Mwaka 2019, kuanza kuonesha mafanikio baada ya kupokea ugeni kutoka Kampuni ya Burmeister and Partners (PTY) Ltd inayomikili kiwanda cha kuchakata nyama nchini Namibia iliyoonesha nia ya kuwekeza hapa nchini.  
Akizungumza (09.07.2019) ofisini kwake katika mji wa serikali eneo la Mtumba Jijini Dodoma na mmoja wa wakurugenzi katika kampuni hiyo Bw. Hendrick Boshoff, Prof. Gabriel amesema lengo la ziara yake ni kupata taarifa za awali, kutoka kwa wataalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili waweze kuwa na njia sahihi ya uwekezaji ambao utakuwa na tija kwa watanzania kupitia Sekta ya Mifugo.
“Mheshimiwa rais alifanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Namibia akiambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na viongozi wengine, nichukue fursa hii kwa niaba ya wizara kumshukuru mheshimiwa rais kutuanzishia suala la soko la mazao ya mifugo hususan nyama, tumetembelewa na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Burmeister and Partners (PTY) Ltd inayomiliki kiwanda cha kuchakata nyama nchini Namibia ili kukutana na wataalam baada ya rais kuonesha muelekeo na wao wakaitikia.” Amesema Prof. Gabriel
Katika mazungumzo hayo Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo, amesema wameuhakikishia ugeni huo kutoka Namibia kuwa wizara iko tayari kupitia Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina kwa kuhakikisha nia ya kampuni hiyo kuanzisha kiwanda kingine cha kuchakata nyama hapa nchini inafikia katika utekelezaji kufuatia ziara ya mheshimiwa rais nchini Namibia.
Prof. Gabriel amefafanua kuwa ujio wa ugeni huo unaratibiwa na wizara nne zikiwemo za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Viwanda na Biashara, Ofisi ya Waziri Mkuu eneo la Uwekezaji na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Sekta ya Mifugo ambapo Prof. Elisante Ole Gabriel ndiye Katibu Mkuu anayeshughulikia sekta hiyo na kwamba ameupokea ugeni wa mkurugenzi wa kampuni hiyo kutoka Namibia kwa niaba ya makatibu wakuu kutoka katika wizara nyingine tatu.
Aidha, ametoa wito kwa watanzania kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali hususan zinazolenga kuongeza masoko ya kutengeneza na kuuza bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
“Viwanda kama hivi vikija ajira nyingi zitaongezeka na pia pato la taifa litaongezeka, bado tuko chini katika ulaji wa nyama takwimu zilizotolewa na Shirika la Chakula Duniani (FAO) zinaonesha walau mtu wa kawaida anatakiwa kula kilogramu 50 kwa mwaka, bado kwa watanzania tunakula kilogram 15 kwa mwaka mzima, tunaleta wenzetu waongeze bidii katika hilo ili wazalishe na soko la ndani liwepo tuuze na nje ya nchi.” Alifafanua Prof. Gabriel
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Burmeister and Partners (PTY) Ltd inayomikili kiwanda cha kuchakata nyama nchini Namibia Bw. Hendrick Boshoff amwemambia Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel kuwa, kampuni hiyo ilianza kuendesha shughuli zake miaka 40 iliyopita na  wamekuja nchini Tanzania wakilenga zaidi uwekezaji wa kuyaongezea thamani mazao ya mifugo hususan nyama.
Akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Viwanda Vidogo na Kati (DSME) Dkt. Consolata Ishebabi, amesema ugeni huo utafahamishwa pia fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ili kufahamu mazingira mbalimbali ya uwekezaji yakiwemo ya sekta binafsi.
Aidha, Dkt. Ishebabi amefafanua kuwa ugeni huo utafikishwa pia katika Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) ambapo watafikishwa katika Ranchi ya Kongwa ambayo ipo chini ya NARCO kuweza kuona aina ya mifugo iliyopo nchini na waweze kupata taarifa za jumla ambazo zitawapatia mwanzo mzuri wa kuwekeza hapa nchini katika Sekta ya Mifugo.
Kikao hicho kiliwahusisha wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiagana na mgeni wake  Mkurugenzi wa Kampuni ya Burmeister and Partners (PTY) Ltd Bw. Hendrick Boshoff mara baada ya kumaliza ma
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Hendrick Boshoff na (anayemfuata) pamoja na washiriki wa kikao.

Balozi Seif kuwaongezea muda madaktari wageni

$
0
0
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatafakari kuangalia uwezekano wa kuiomba Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kuwaongezea muda wa kutoa huduma za Afya Madaktari wa Nchi hiyo wanaopangiwa kufanyakazi katika Hospitali za Rufaa hapa Zanzibar.

Alisema kutokana na ukarimu na huduma bora za Madaktari hao wanazozitoa kwa Wananchi upo umuhimu wa kuombewa muda wa Miaka Miwili badala ya ule Mmoja uliozoeleka katika Mkataba uliosainiwa kati ya Serikali hizo mbili mnamo Mwaka 1965.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akiwakaribisha Zanzibar Madaktari Mabingwa Wapya na kuwaaga wale waliomaliza Muda wao Mwaka Mmoja wa kutoa huduma za Afya kutoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China.

Alisema Jamii ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla tayari wanazikubali huduma zinazotolewa na Madaktari Bingwa kutoka Nchini China kiasi kwamba uwepo wao katika kipindn cha Mwaka Mmoja kinaonyesha kutokidhi kiu na mahitaji halisi ya Wananchi hao katika kupata huduma hiyo.

Alisema licha ya mazingira ya kupendeza kuona Madaktari wakongwe wanaondoka na wapya wanaingia kwa wakati katika kutoa matibabu ya Maradhi mbali mbali lakini bado muda wa ziada kwa mabingwa hao unahitajikja kwa vile tayari wameshakuwa kama Wana Jamii.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliishukuru na kuipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa moyo wake wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika Sekta ya Afya.

Mapema Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Hamad Rashid Mohamed alisema iliyoingia Nchini hivi sasa ni Timu ya 29 ya Madaktari Mabingwa wa China ikiwa ni mfumo maalum ulioasisiwa tokea Mwaka 1965 wa kuwapokea Wataalamu hao kwa lengo la kutoa huduma za Afya Zanzibar.

Mh. Hamad alisema Timu ya Madaktari ya Awamu ya 28 ilifanya kazi kubwa kama zilivyofanywa zile zilizotanguliwa kazi ambayo inastahiki kuendelezwa na Timu Mpya iliyoingia Nchini kushika dhamana hiyo.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Madaktari Mabingwa wa China waliomaliza Muda wao Kiongozi wa Madaktari hao Dr. Zhang Zhen alisema Timu hiyo imefanya kazi kubwa iliyoelata mafanikio makubwa kutokana na ushirikiano walioupata kutoka kwa Madaktari Wazawa.

Dr. Zhang alisema katika utumishi wao wa Mwaka Mmoja waliokuwepo Zanzibar Mabingwa hao wameweza kukabiliana na kesi 100 zilizokuwa zikiwasumbua Wananchi na kuzipatia ufumbuzi wa Kitaaluma.

Alisema Mabingwa hao waliomaliza muda wao walikuwa na mpango Maalum uliowawezesha kutoa huduma za Afya katika Hospitali mbali mbali za Mikoa, Wilaya hadi Vijijini.

Alifahamisha kwamba huduma hizo zilikwenda sambamba na utolewaji wa mafunzo kwa Madaktari Wazalendo pamoja na Semina zilizoshirikisha Watendaji wa Afya pamoja na wale wanaohusika na utoaji wa huduma ya kwanza.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwakaribisha Zanzibar Madaktari Mabingwa Wapya na kuwaaga wale waliomaliza Muda wao Mwaka Mmoja wa kutoa huduma za Afya wanaotoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara wa Afya Zanzibar Bibi Halima Salum Maulid akifafanua mafanikio ya huduma za Afya kutokana na uwepo wa Madaktari mabingwa kutoka China.
 Balozi Seif akipokea zawadi kutoka kwa Kiongozi wa Madaktari Mabingwa kutoka Jauhuri ya Watu wa China waliomaliza Muda wao hapa Zanzibar Dr. Zhang Zhen
 Balozi Seif kati kati waliokaa vitini katika katika picha ya pamoja na Madaktari Mabingwa Wapya na kuwaaga wale waliomaliza Muda wao Mwaka Mmoja wa kutoa huduma za Afya wanaotoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China.
Timu ya Madaktari Mabingwa Wapya na kuwaaga wale waliomaliza Muda wao wa China wakiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. Picha na – OMPR – ZNZ.

Basi Lingine lakamatwa likiwa na Abiria zaidi ya 90

$
0
0
Na Gasto Kwirini wa Polisi Arusha

Katika operesheni ya ukaguzi wa magari ambayo bado inaendelea leo tarehe 10.07.2019 muda wa saa 06:00hrs asubuhi Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP)Joseph Bukombe akiwaongoza Askari katika barabara ya Arusha - Kiteto walifanikiwa kukamata Basi lenye Namba za Usajili T. 735 AEM mali ya Kampuni ya COAST LINE likiwa limepakia abiria 95.

Basi hilo ambalo linafanya safari zake kati ya Arusha na Kiteto lilikua limepakia abiria 67 ambao walikua wamekaa kwenye siti, 25 walikua wamesimama, kati yao Abiria wa kawaida walikua 10 na Wanajeshi 15. Pamoja na hao walikuepo Dereva, kondakta, fundi na Msindikizaji wa basi hilo ambapo wanafanya idadi yao kuwa 95.

Akizungumza na Abiria wa Basi hilo Mkuu huyo wa Usalama Barabarani amewataka kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pindi wanapoona Basi limezidisha abiria, mwendo mkali na kutokubali kupanda basi ambalo limejaa.

Aidha ametoa wito kwa wamiliki wa Mabasi kuwasimamia Wafanyakazi wao hasa madereva na Makondakta ili waweze kufuata sheria bila kushurutishwa."Wamiliki tokeni majumbani, fanyeni ukaguzi wa kushtukiza kuliko kulaumu kila mara tunawakamata kwa kuwaonea, mmiliki atakapowasimamia watu wake Jeshi la Polisi halitaangaika na mtu kumkamata" Alisisisitza RTO Bukombe.

Meneja wa Mabasi ya Coast Line Bwana Petro Amsi Stanley amepongeza Operesheni hiyo inayoendelea kufanywa kwani itasaidia kuwadhibiti Madereva na Makondakta wanaofanya kazi bila kufuata sheria kwa sababu Wamiliki na Mawakala wanakua hawana taarifa za abiria kuzidi kwenye mabasi yao.

Pia amempongeza Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya kwa ufasaha."RTO huyu anajiamini na anafanya kazi yake kwa ufasaha mkubwa, na hii imebabishwa na kutokua na ushirika na Mtu hasa wamiliki wa Vyombo vya moto, hivyo tunampongeza kwa Opereshini hii anayoendelea kuifanya". Alisema bwana Esto.

Basi hilo limefikishwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kufanyiwa Ukaguzi zaidi. Aidha Mkuu wa wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha ameamuru wakala wa basi hilo awatafutie abiria wote waliozidi usafiri mwingine.

Sambamba na hilo, Dereva na Kondakta wa basi hilo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano, mara baada ya Upelelezi kukamilika watafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

SERIKALI YAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA VIWANDA VYA NGOZI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Misri ikiwemo kampuni ya Cairo for Investment and Development inayoshughulika na usimamizi wa kiwanda cha ngozi waje kuwekeza nchini Tanzania.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumanne, Julai 9, 2019) alipotembelea kiwanda kikubwa cha ngozi cha Robbiki kilichoko katika mkoa wa Sharkianchini Misri, ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji hao waje wawekeze nchini kwani kuna malighafi za kutosha.

Waziri Mkuu ambaje jana alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi nchini Misri alisema Tanzania inamifugo mingi hivyo inahitaji wawekezaji watakaojenga viwanda vya kuchakata bidhaa mbalimbali zitokanazo na mifugo hiyo ikiwemo ngozi.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeboresha mazingira ya biashara na ya uwekezaji pamoja na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma, hivyo Tanzania ni mahali bora na salama kwa wawekezaji na wafanyabiashara.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kampuni ya Cairo for Investment and Development ya nchini Misri, ambayo inasimamia kiwanda cha ngozi cha Robbiki, Yasser Mohamed Ahmed Al Maghraby alisema kiwanda hicho kinauhitaji mkubwa wa ngozi kutoka Tanzania.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea mradi mkubwa wa mabwawa ya kufugia samaki, mradi wa upanuzi wa awamu ya pili ya mfereji wa suez canal, ambapo aliipongeza Serikali ya Misri kwa ujenzi wa mradi huo mkubwa kwa kutumia fedha za ndani (Dola bilioni 8.2).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Watanzania waishiyo nchini Egypt, katika hoteli ya Almasa, mjini Cairo, Julai 9, 2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea picha ya Rais Magufuli, iliyochorwa na Binti wa Dereva wa Ubalozi wa Tanzania nchini Misri, Hadeer Mohamed, kwenye mkutano na Watanzania waishiyo nchini Egypt, uliyofanyika katika hoteli ya Almasa, mjini Cairo, Julai 9.2019. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Misri, Meja Jenerali Mstaafu, Issa Suleiman. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa ya ngozi, wakati alipotembelea kiwanda kikubwa cha ngozi cha Robbiki, kilichopo katika mkoa wa Sharkia, nchini Misri, Julai 9.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez Canal, Admiral Mohab, wakati alipotembelea mfereji huo mpya nchini Misri, Julai 9.2019. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea zawadi ya ngao, kutoka kwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez Canal, Admiral Mohab, wakati alipotembelea mfereji huo mpya nchini Misri, Julai 9.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez Canal, Admiral Mohab, wakati alipotembelea mfereji huo mpya nchini Misri, Julai 9.2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa kwenye boti,wakati alipotembelea mfereji wa Suez Canal, katika mji wa Ismailia, Misri Julai 9.2019. 



Mbunge Mavunde awatoa hofu wananchi kuhusu migogoro ya Ardhi

$
0
0
Na Charles James, Michuzi TV

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira n Mh Anthony Mavunde amewasihi wananchi wa eneo la Mjimwema kata ya Chang'ombe Jijini Dodoma kuendelea kuwa watulivu kwani mgogoro wa ardhi unaowakabili kwa muda mrefu umefanyiwa kazi na muda sio mrefu wataona matokeo yake.

Mh Mavunde ameyasema hayo Julai 9, mwaka huu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Shina la wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika katika eneo la Soko la Mavunde-Chang'ombe.

Mbunge huyo amesema katika utatuzi wa mgogoro huo hadi sasa tayari kuna hatua kadhaa zimekwisha chukuliwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

"Hivi sasa Mkuu wetu wa Mkoa ameunda ile kamati yake na ilirudi hapa kutoa taarifa na baadhi ya mambo yanaendelea naomba tusubiri tukamilishe zoezi hili kama kutakuwa na mapungufu yatakayojitokeza kama viongozi wenu tupo tutasaidia kuweza kutatua lakini cha msingi ni kwamba ile kero kubwa tayari hatua zimeanza kuchukuliwa" Amesema Mavunde.

Kuhusu mikopo Mh Mavunde amewaahidi wananchi na wafanyabishara wa kata hiyo kuwa atashirikiana na viongozi wenzake ili kuwasaidia wale wote wenye vikundi kuweza kupata mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Jiji pamoja na mifuko mingine ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.

"Sasa hivi Jiji lenu linatoa mikopo ya hadi Shilingi Milioni kumi kwa kikundi niwaombe wafanyabiashara kama mna utaratibu wenu wa vikundi mmeuweka niletee ili niweze kuwasaidia kupata mikopo kupitia fedha hizi za Halmashauri ambazo vijana na akina mama wengi wamenufaika nazo "Amesema Mhe Mavunde.

Aidha katika ufunguzi wa Shina hilo Mh.Mavunde pamoja na kuelezea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika Jiji hilo pia ameahidi kuweka uzio wa kuzuia jua katika Soko la Chang'ombe,Mipira na Jezi katika Timu ya shina pamoja na kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya kutunisha mfuko wa shina.

Wakizungumza katika tukio hilo baadhi ya wananchi wamekiri Mbunge wao kuwa na mchango mkubwa katika kuwaletea maendeleo katika kata yao na kumshukuru kwa mchango wa mabati na gharama za ufundi wa ujenzi wa soko na kuahidi kushirikiana nae katika kuwaletea wananchi maendeleo.


KWAYA YA WATOTO YATOA MSAADA WA MASHINE YA MILIONI 100 MUHIMBILI

$
0
0
Mwalimu wa Kwaya ya watoto katika Shule ya Westminister Cathedral nchini Uingereza, Matthew Wright akikabidhi Optical Coherence Tomography (OCT) kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru katika shughuli fupi iliofanyika MNH leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa MNH, Dkt. Sufiani Baruani
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru akizungumza baada ya kukabidhiwa machine ya OCT na Mwalimu wa Kwaya ya watoto katika Shule ya Westminister Cathedral nchini Uingereza, Matthew Wright. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho, Dkt. Paul Nyaluke wa MNH. 
Pichani ni machine ya OCT inatumiwa na wataalam wa magonjwa ya macho kutambua magonjwa yaliopo katika pazia la macho (retina) ili kumsaidia daktari kuamua matibabu sahihi kwa mgonjwa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho, Dkt. Paul Nyaluke akieleza jinsi machine ya OCT inavyotumika kutambua magonjwa yaliopo kwenye pazia la macho (retina) kwa mgonjwa mwenye matatizo ya macho.


Na John Stephen


Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepatiwa msaada wa machine ya kisasa ya Optical Coherence Tomography (OCT) ya kusaidia kupima magonjwa ya macho yenye zaidi ya thamani ya Shilingi milioni 100.

Msaada umetolewa na Shule ya Kwaya ya Westminister Cathedral ya nchini Uingereza kupitia Hospitali ya Mtakatifu Thomas iliyopo nchini humo kwa lengo la kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya macho nchini. Mashine ya OCT inatumika kutambua magonjwa yaliopo katika pazia la macho (retina) kwa ajili ya kumsaidia daktari kuamua matibabu sahihi kwa mgonjwa wa macho.

Akizungumza katika shughuli fupi ya kukabidhi mashine ya OCT, mwalimu wa kwaya ya watoto katika Shule ya Kwaya ya Westminister Cathedral nchini Uingereza, Matthew Wright amesema watoto wa kwaya hiyo wenye umri kuanzia miaka minne hadi 13 wametoa msaada ili kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya macho nchini.

“Mashine ya OCT itasaidia kutoa matibabu kwa maelfu ya wagonjwa wanaohitaji huduma, huu ni mchango wa watoto wa Shule Kwaya ya Westminister Cathedral ambao wamechanga fedha zao ili kutoa msaada huu,” amesema Mwalimu Wright.

Wright amesema mashine ya OCT pia itasaidia kutoa elimu kwa madaktari zaidi ya 20 wanaosoma jinsi ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya macho.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru baada ya kupokea msaada amemshukuru Mwalimu Wright pamoja na watoto waliochanga fedha ili kununua machine ya OCT.

Prof. Museru amesema mashine ya OCT itatoa mchango mkubwa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya macho na ameahidi kwamba wataitunza ili iweze kufanya kazi kwa muda mrefu.

Pia, Prof. Museru amewataka wataalam kuhakikisha wanaitumia OCT kwa uangalifu wakati wa kuchukua vipimo kwa wagonjwa ili iweze kuwanufaisha watu wengi zaidi.

KAMISHNA JENERALI MAGEREZA ATEMBELEA MIKOA YA KIMAGEREZA NA MAGEREZA KANDA YA ZIWA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike(wa pili kushoto) akipata maelezo kwa mfungwa anayehusika na upikaji wa chakula Gerezani hapo. Picha zote na Kitengo cha Habari, Makao Makuu.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (kushoto) akipokelewa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi Msaidizi Hamza Sadik mara baada ya kutua kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza akitokea Dar es Salaam.
 Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi Raymond Mwampashe (kushoto) akimpokea Kamishna Jenerali wa Magereza Kasike( wa kati) mpakani mwa Wilaya ya Chato na Wilaya ya Muleba baada ya Kamishna Jenerali kumaliza maudhurio ya hafla ya uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa Burigi-Chato.Kulia ni msaidizi wa Kamishna Jenerali Mrakibu Msaidiza Melkior Komba.
 Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Muleba, Mrakibu Hadar Yuda(kulia) akimkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (kushoto) Gerezani hapo. Katikati yao ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi Raymond Mwampashe.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akiweka saini katika kitabu cha kumbukumbu  ndani ya Gereza la Wilaya la Muleba.
 Mganga wa Gereza la Wilaya ya Muleba, Koplo Diana(kulia) akitoa maelezo kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Kasike (wa kati) jinsi anavyowahudumia Wafungwa na Mahabusu wa Gereza hilo. Kushoto ni Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Muleba, Mrakibu Hadar Yuda. 

Shilingi Bilioni 600 Kuondoa Tatizo la Upatikanaji wa Maji Tabora

$
0
0
Na Jonas Kamaleki-MAELEZO
Manispaa ya Tabora itaanza kupata maji safi na salama wakati wote baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji toka Ziwa Victoria utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 600.
Mji wa Tabora au mkoa huo kwa ujumla una tatizo la vyanzo vya uhakika vya maji, hivyo kuondokana na tatizo hilo, Serikali imefanya juhudi za makusudi za kujenga mradi mkubwa wa maji toka Ziwa Victoria.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Tabora (TUWASA), Mhandisi Mkama Bwire ameeleza hayo kwa Maafisa wa Idara ya Habari (MAELEZO) walipofanya ziara mkoani humo hivi karibuni.
“Tunamshukuru sana Rais John Pombe Magufuli kwa utekelezaji wa mradi huu wa maji ambao utakuwa mkombozi kwa Manispaa ya Tabora na maeneo mengine ya mkoa wetu ikiwemo Nzega na Igunga,”anasema Mhandisi Bwire.

Serikali ya Awamu ya Tano inataka ifikapo Juni 2020, upatikanaji wa maji safi na salama maeneo ya mijini ufikie asilimia 95, lakini Manispaa ya Tabora imejipanga kuwafikishia wananchi wake huduma hiyo kwa asilimia 100.
Kwa mujibu wa Mhandisi Bwire, upatikanaji wa maji safi na salama katika kata 20 zinazopata huduma hiyo, ni asilimia 84 tu. Hivyo kuna kila sababu ya kukamilisha mradi huo mapema iwezekanavyo na kufanya upatikanaji wa huduma hiyo kwa asilimia 100 na kwa kata zote za Manispaa ya Tabora.

Upatikanaji wa maji safi na salama katika Manispaa ya Tabora utaondoa magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama kama vile homa ya matumbo, kipindupindu na kuhara, na hivyo kuwafanya wakazi wa maeneo hayo kuwa na afya njema.
Mhandisi Bwire anasema upatikanaji wa maji safi na salama utaongeza na kuchochea shughuli za kiuchumi kwani muda mwingi uliokuwa ukipotea kwa watu kufuata maji zaidi ya kilomita 5 kwa sasa utatumika kwa shughuli za kiuchumi.

Serikali ya Awamu ya Tano inayolenga kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda, inatekeleza azma hiyo kwa kuwapatia wananchi maji ya uhakika ambayo pia ni kiungo muhimu kwa ujenzi wa viwanda, hivyo Mhandisi Bwire anatumia fursa hiyo kuwaalika wawekezaji kuwekeza katika Mkoa wa Tabora kwani maji ambayo yalikuwa ni kikwazo cha uwekezaji sasa yatapatikana kwa uhakika.

“Natoa wito kwa wawekezaji hasa kwenye viwanda waje Tabora kwa wingi ili wawekeze kwani maji yatakuwepo ya kutosha kwa muda wa saa 24,”anasema Bwire.
Akizungumzia Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria, Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mhe. Komanya Kitwala anasema kuwa mradi huu utafanya uhaba wa maji Mkoa wa Tabora kuwa historia na utasaidia katika kukuza uchumi wa mkoa huo.

“Tunapongeza juhudi za dhati za Jemedari wetu Mkuu, Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza Ilani ya Chama Tawala kwa vitendo, nasi wasaidizi wake tutahakikisha miradi mikubwa ya maendeleo hasa ya maji, elimu, miundombinu na afya tunaisimamia kikamilifu ili wananchi wafaidi matunda ya Serikali yao,”anasema Komanya.

Naye Mkazi wa Manispaa ya Tabora Anicet Masanja anasema kuwa upatikanji wa maji utarahisisha hata kwenye shughuli za kilimo cha mbogamboga na matunda pia na ufagaji.
“Tutalima mbogamboga na kujipatia kipato pasipo kutegemea mvua kwani tutakuwa na maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, tutafuga kwa sababu tutakuwa na maji ya uhakika kwa ajili ya kunyweshea mifugo yetu,”anasema Masanja.

Mkoa wa Tabora kwa kipindi kirefu umekuwa ukikabiliwa na uhaba wa maji kwani vyanzo vya maji vimekuwa ni mabwawa ambayo wakati mwingine yamekuwa yakikauka na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa mkoa huo.
Mtandao wa maji katika Manispaa ya Tabora kwa sasa umeenea kwa kata 20 kati ya kata 29 za manispaa hiyo, ambapo mradi ukikamilika, kata zote 29 zitapata maji kwa saa 24 bila mgao. 

Katika utekelezaji wa mradi huo, yanajengwa matenki makubwa manne yatakayokuwa yanasambaza maji katika Manispaa nzima ya Tabora muda wote.
Wahenga walisema haja ya mja hunena, muungwana ni vitendo. Kauli hii iliyojaa hekima inatimia kwa Serikali ya Awamu ya Tano kutekeleza ahadi zake kwa vitendo.

Mradi huu wa maji ulitarajiwa kukamilika Februari 2020 lakini kutokana na juhudi za wakandarasi mradi huo utakamilika mwishoni mwa mwaka huu (2019) na kufanya upatikanaji wa maji kuwafikia wakazi wote wa Manispaa ya Tabora kwa wakati wote yaani saa 24.

Hakika maji ni uhai na uhai huo unaendelea kupatikana Mkoa wa Tabora kwa kutekeleza mradi mkubwa maji ili kuwapatia wakazi wa mkoa huo huduma hiyo wakati wote.
Moja ya Matenki yatakayotumika kusamba maji katika Manispaa ya Tabora ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Mkubwa wa Maji toka Ziwa Victoria, Mradi huu hadi kukamilika utagharimu zaidi ya Shilingi bilioni 600. 

ALIYELAZWA MWAKA MMOJA MLOGANZILA APATIWA MASHINE YA KUPUMUA

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, imempatia msaada wa mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) Bw. Hamad Awadhi kutokana na matatizo yake ya afya ambayo yanamlazimu kutumia mashine ya oxygen muda wote ili aweze kupumua.

Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH-Prof. Charles Majinge amesema hospitali imempatia msaada Bw. Awadhi kwa lengo la kuokoa maisha yake sanjari na kuimarisha afya yake lakini pia kumuwezesha kuendelea na shughuli zake za kawaida ili kutokua tegemezi kutokana na hali yake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru ameeleza kwamba mashine hiyo inathamani ya shilingi milioni tatu na nusu imenunuliwa na Hospitali ya Mloganzila ambapo wataalam wamempatia mafunzo Bw. Awadhi namna ya kuitumia na kuitunza ipasavyo.

Prof. Museru amemtaka Bwan. Awadhi kuitunza na kuitumia vema mashine hiyo kama ambavyo ameelekezwa na wataalam ili afya yake itakapoimarika iweze kusaidia watanzania wengine.

"Hospitali imekupatia msaada wa mashine hii ya kukusaidia kupumua- kwa lengo la kuhakikisha afya yako inaimarika zaidi hivyo tunaomba uitunze na utakapopona kabisa utairejesha hospitali ilituwasaidie wengine" amesema Prof. Museru.

Naye Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani MNH- Mloganzila Dkt. Patricia Munseri amesema, Bw. Awadhi kwa muda wote aliokuwepo hospitalini ameishi kwa kutegemea mashine ya oxygen ambayo inamsaidia kupumua ambapo kwa siku alikua akitumia gesi wastani wa lita 5,760.

Bw. Hamad Awadhi alifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila Julai 9 mwaka 2018 na kuruhusiwa Julai 9 mwaka 2019 baada ya afya yake kuimarika.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Charles Majinge (kushoto) akimpatia msaada wa mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) Bw. Hamad Awadhi ambaye alilazwa kwa muda wa mwaka mmoja katika Hospitali ya Mloganzila.
 Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi MNH- Mloganzila Redemptha Matindi (aliyevaa gauni la bluu) akitoa maelezo namna mashine ya oxygen inavyounganishwa ili iweze kutumika kwa mgonjwa, anayemfuatia ni Prof. Charles Majinge, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Mohamed Mohamed, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru.
 Prof. Lawrence Museru (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MNH Prof. Majinge (wa pili kuli) kuhusu ununuzi wa mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) ambayo imegharimu shilingi milioni tatu na nusu, kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.
  Dkt.  Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani MNH- Mloganzila Dkt. Patricia Munseri (kulia) akizungumzia kuhusu matibabu aliyopatiwa Bw. Awadhi kwa kipindi chote alichokua amelazwa hospitalini. 
 Hamadi Awadhi akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Muhimbili-Mloganzila kwa huduma aliyoipata na kwa kumpatia msaada ambao utamuwezesha kuendelea na shughuli zake za kawaida.
 Mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) ambayo amepatiwa msaada Bw. Hamad Awadhi.

Malkia wa Afrika Chaka Chaka atua ZIFF, kufanya makongamano

$
0
0
Malkia wa Afrika Yvonne Chaka Chaka atua Zanzibar, kufanya onesho dogo na makongamano ZIFF 2019


Na Andrew Chale, Zanzibar, Tanzania

Malkia wa Muziki wa Afrika, Mama Yvonne Chaka Chaka tayari yupo visiwani hapa kwenye tamasha la 22 la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) ambapo atafanya shughuli mbalimbali ikiwemo makongamano na Wanawake pamoja na wadau wengine wakiwemo wasanii wa filamu na muziki.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa ZIFF, Isihaka Mlawa amebainisha kuwa, Mama Yvonne ni miongoni mwa wageni maalum kwa mwaka huu ambapo pia atafanya shughuli za kijamii ikiwemo makongamano na warsha ya Wanawake, wasanii wa filamu na wale wa muziki shughuli zilizoandaliwa na ZIFF 2019.

“Mama Yvonne Chaka Chaka amefika jana Zanzibar na leo ataendelea na programu maalum ikiwemo kukutana na Wanafunzi wanaopata mafunzo ya filamu lakini pia atakutana na Wasanii wa muziki kutoka Chuo cha Muziki cha Dhow Country Music Academy.” Alieleza Isihaka.

Aidha, Isihaka Mlawa ameongeza kuwa, wanatarajia Mama Yvonne Chaka Chaka na mwanamuziki aliyeimba wimbo wa Zanzibar miaka 40 iliyopita, Sipho Mabuse kufanya tukio maalum la muziki kidogo kwenye shughuli za tamasha hilo linaloendelea visiwani hapa na kutarajiwa kufikia tamati Julai 14, mwaka huu.

Mama Yvonne Chaka Chaka na Sipho Mabuse wapo visiwani hapa kama wageni maalum waalikwa wa tamasha hilo kwa mwaka huu ambapo wamekuwa kioo na kielelezo kutokana na nyimbo zao mbalimbali zilizotamba Bara la Afrika pamoja na umaarufu wao katika jamii inayowazunguka.

Msanii Mama Yvonne Chaka Chaka (Jina la kuzaliwa Yvonne Machaka ambapo alizaliwa mnamo mwaka 1965 ni mwimbaji kutoka Afrika ya Kusini.
Kuitwa kwake Malkia wa Afrika ni kutokana na kuwa mstari wa mbele katika muziki maarufu wa Afrika Kusini kwa miaka 20.

Nyimbo kama "I'm burning Up", "I'm in Love with a DJ", "I Cry for Freedom", "Makoti", "Motherland" na "Umqombothi" ("Pombe ya Afrika") zimeweza kumuweka kwenye ramani ya Afrika na kuwa maarufu zaidi.

Msanii huyo alizaliwa Dobsonville huko Soweto na alikuja kuwa mototo wa kwanza wa Kiafrika kuonekana kwenye televisheni Afrika Kusini. Mwaka 1981 "Sugar Shack", kipindi cha wenye talanta, kilimjulisha kwa umma wa Afrika Kusini.Katika harakati za muziki, Chaka Chaka alianza kuimba akiwa na miaka 19 mwaka 1985 wakati Phil Hollis wa Dephon Records alimgundua mjini Johannesburg- Muda mfupi baada ya albamu yake "I'm in Love With a DJ", kuuzwa nakala 35,000.

Pia katika nyimbo zake zilizowahi kushinda tuzo mbalimbali ni kama "Burning Up", "Sangoma", "Who's The Boss", "Motherland", "Be Proud to be African", "Thank You Mr DJ", "Back on my Feet ", " Rhythm of Life "," Who's got the Power "," Bombani (Tiko Rahini), "Power of Afrika", "Yvonne and Friends" na "Kwenzenjani".
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, ambaye ni Waziri wa Habari, Utalii na mambo ya Kale, Mahmoud  Thabit  Kombo akiwa katika picha  ya pamoja na Mama Yvonne Chaka Chaka Mjini Unguja, Zanzibar.

MEYA MWITA AMWAGA VIFAA VYA KUJIFUNGULIA WAKINA MAMA HOSPITALI ZA JIJI LA DAR

$
0
0
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita , leo amekabidhi vifaa vya kujifungulia wakina mama (Delivery Pack) katika Hospital za jijini hapa ikiwa ni sehemu ya kuwasaidia wa kimama wenye hali hiyo.

Hospital zilizopatiwa vifaa hivyo ni Mnazi mmoja iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,ambapo imepewa vifaa hivyo 300 na zile zilizopo katika Halmashauri ya Kigamboni.

Akizungumza na wauguzi katika hospitali hiyo,Mstahiki Meya Mwita aliagiza kuwa vifaa hivyo vitolewa bure kwa wakina mama wenye uhitaji na kuagiza hospital hizo zisiwauzie.
 Alifafanua kuwa wakina mama wajawazito wanapaswa kuthaminiwa na kwamba sio wote wenye uwezo wa kununua vifaa hivyo na kushauri wenye uwezo kuwasaidia.

Alifafanua kuwa serikali kwa kiasi kikubwa imekuwa ikijali wakina mama wajawazito na kushauri kuwa kama wadau wa maendeleo wanapaswa kushirikiana na serikali kuwalinda wa mama wajawazito.
 “ Ukiangalia serikali inatilia mkazo jambo hili, inajali wakina mama na kuhakikisha kuwa wanajifungua salama, wote tunapaswa kujali maisha yao, nijukumu letu kulinda mama mjamzito “ alisisitiza.

Changamoto ni nyingi,uhitaji wa vifaa ni mkubwa kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wakina mama wanaojifungua,nitoe rai kuwa hili ni jukumu la kila mmoja wetu kuisaidia serikali” aliongeza.

Alisema “Wakina mama ni watu wamuhimu sana katika Taifa hili, tunapaswa kuwaheshimu na kuwathamini, pia wanakazi kubwa ambayo kwao inachangamoto, lakini kama viongozi na wadau wengine tunajukumu la kuwasaidia” alisema Meya Mwita.
“ Vifaa hivi najua havitoshi kulingana na Idadikubwa mliyonayo katika Hospitali hii, ila niwaombe muwapatie bure msiwauzie, huu ni msaada kwao, napindi tutakapopata nyingine tutawaletea” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Meya Mwita ameipongeza hospitali hiyo kutokana na huduma wanazozitoa na hivyo kuwasihi kuendelea na utoaji mzuri wa huduma hiyo.

Mganga Mfadhiwi wa Hospitali hiyo Sophinias Ngonyani alimpongeza Meya Mwita kwakutoa vifaa hivyo na kusema kuwa zitawasaidia wakina mama na kusisitiza kwamba watazigawa bure kama walivyoagizwa.

Alisema kuwa hospitali hiyo imekuwa ikihudumia wakina mama wajazito kutoka sehemu mbalimbali jijini hapa kwani hali hiyo imetokana na huduma nzuri wanazozitoa.

Aliongeza kuwa hospital hiyo inazingatia utoaji huduma bora kama ambavyo serikali inasisitiza kila wakatii jambo ambalo alisema limepelekea kuwa na idadi kubwa ya wakina mama wanaojingulia katika hospitali hiyo.

“ Tunampongeza Mstahiki Meya kwa kutupatia vifaa hivi, tunauhitaji mkubwa kulingana na idadi ya wakinamama wanaojifungua hapa kwetu, ametusaidia sana tunampongeza” alisema.

Hata hivyo vifaa hivyo vitaendelea kutolewa kwa hospitali nyingine zilizopo jijini hapa ,huku nyingine zikichukuliwa katika ofisi ya Mstahiki Meya.

Vifaa hivyo vimetolewa na Mstahiki Meya wa jiji kwa kushirikiana na Kampuni ya usafirishaji abiria kwa njia ya mtandao ya Bolt vyenye thamani ya shilingi milioni 25.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images