Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

VOA SWAHILI: Fainali ya kandanda Afrika yashangaza wengi - Kalusha Bwalya


HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO

Dkt. Kigwangalla afafanua kuhusu utata wa Sanamu ya Baba wa Taifa

Serikali yatenga Bil 40 ujenzi wa vyuo vya Ufundi Stadi vya Wilaya

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetenga Sh. bilioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo 25 vya Ufundi Stadi katika Wilaya mbalimbali nchini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Urambo tarehe 9 Julai 2019, Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema ujenzi wa vyuo hivyo ni utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa kuhakikisha vijana wengi zaidi wanapata fursa za mafunzo ya Ufundi Stadi.

Prof. Ndalichako amesema vyuo hivyo vinatarajiwa kujengwa katika Wilaya za Chunya, Kilindi, Korogwe, Ukerewe, Igunga, Pangani, Kishapu, Rufiji, Uyui, Kwimba, Bahi, Mafia,  Longido, Mkinga, Uvinza, Ikungi, Iringa vijijini, Lushoto, Mbarali, Monduli, Buhigwe, Ulanga, Masasi, Butiama na Chemba.

Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inakuwa na chuo cha Ufundi Stadi katika kila Wilaya na Mkoa ili kuendana na kasi na maono ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda.
“Hatuwezi kuzungumzia uchumi wa viwanda bila kuwa na watu wenye ujuzi ambao ndio wataenda kufanya kazi katika viwanda ndiyo maana Wizara yangu imeongeza kasi ya ujenzi wa vyuo vya VETA nchini,” Alisema

Waziri Ndalichako amesema kuwa kwa sasa Serikali inaendelea kukamilisha ujenzi wa vyuo vya Wilaya za Nkasi, Ileje, Newala, Muleba, Kasulu, Itilima, Ngorongoro, Chato na Babati vinavyotarajiwa kumalizika ndani ya mwaka 2019 na matayarisho yanaendelea ya kuanza ujenzi wa vyuo vya Ufundi stadi katika Wilaya za Kongwa, Ruangwa, Nyasa na Halmashauri ya mji wa Kasulu.

Kwa ngazi ya Mkoa, Prof. Ndalichako amesema kuwa ujenzi wa vyuo vya Mikoa ya Geita na Rukwa unaendelea na kwamba ujenzi wa vyuo vya Mikoa ya Simiyu, Ludewa na Kagera utaanza punde.
 Alisema kuwa serikali inaamini kuwa chuo hicho cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Urambo kitakuwa chachu ya maendeleo ya viwanda Mkoani Tabora na kuwataka wananchi wakitumie vyema katika kujipatia ujuzi.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwandri alisema kuwa chuo cha VETA Urambo kimekuja wakati mwafaka ambapo changamoto ya ukosefu wa ujuzi ni kubwa hali inayosababisha vijana kukosa ajira kwenye miradi mbalimbali mkoani hapo.
Aliwasisitiza wananchi wa Urambo kutumia vyema chuo hicho kupata ujuzi wa aina mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji halisi ya soko la ajira ili waweze kujiajiri.

“Tufike mahali vijana wetu wa mkoa wa Tabora wakiulizwa unataka kuwa nani waseme wanataka kuwa waajiri wa watu wengine”Alisema.
Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Peter Maduki alisema kuwa VETA imedhamiria kuongeza udahili wa mafunzo ya Ufundi stadi nchi nzima, kuboresha ufundishaji kwa kuongeza vifaa na walimu pamoja na kuboresha miundombinu.

Alisema kuwa VETA imejipanga kukuza uzalishaji katika viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kwa kufanya ubunifu utakaowezesha kuanzishwa kwa viwanda pamoja na kurahisisha uchakataji wa mazao mbalimbali.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu alisema kuwa chuo cha Urambo kilitokana na kukarabatiwa kwa majengo yaliyotumiwa na mkandarasi aliyejenga barabara ya Ndono hadi Urambo na kisha kukabidhiwa kwa  Halmashauri ya Wilaya ya Urambo na baadae Halmashauri hiyo kuyatoa yatumike kunzisha chuo hicho kutokana na uhitaji mkubwa wa Chuo cha Ufundi Stadi katika Wilaya hiyo.

Alisema jumla ya kiasi cha Sh. milioni 218 kimetumika kwa ajili ya ukarabati wa chuo hicho chenye majengo 15 yatakayotumika kwa ajili ya madarasa, karakana, ofisi, mabweni na nyumba za walimu.
Dkt Bujulu alizitaja fani zitakazotolewa katika chuo hicho kwa kuanzia  kuwa ni Umeme wa Majumbani, Ushonaji, Ujenzi, na Uhazili na matumizi ya Kompyuta na kina uwezo wa kudahili wanafunzi 160 kwa mafunzo ya muda mrefu na wanafunzi zaidi ya wanafunzi 500 wa kozi za muda mfupi kwa mwaka.

Aliiomba Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kuwaongezea eneo zaidi linalopakana na chuo hicho kwa ajili ya kuongeza madarasa, karakana na mabweni ili kuongeza udahili wa wanafunzi kwa kuongeza fani mbalimbali kama vile fani za kilimo na ufugaji, uungaji na uchomeleaji vyuma, ufundi mekanika, ufundi bomba, n.k. kwa kadri ya mahitaji ya soko.
Naye Mbunge wa Urambo Mashariki Magreth Sitta aliipongeza VETA kwa kufanikisha ukarabati wa chuo hicho na kuwataka wazazi kuwapeleka watoto katika chuo hicho wajipatie ujuzi.

Ili kuleta hamasa kwa wazazi kuleta watoto wao katika chuo hicho, Mbunge huyo aliahidi kuwalipia ada ya kiasi cha Sh. 60,000 kwa kila mwanafunzi kwa wanafunzi 62 kutoka katika viijiji mbalimbali Wilayani hapo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggey Mwandri baada ya kuwasili katika chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Urambo.Kulia ni Mbunge wa Urambo Mashariki Mhe. Magreth Sitta
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Urambo.Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Urambo Mashariki Mhe.Magreth Sitta akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwandri na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Peter Maduki akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akivuta utepe kuzindua  chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Urambo.Kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwandri.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Peter Maduki wakati wa uzinduzi wa chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Urambo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi waliojitokeza kuhudhuria uzinduzi wa chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Urambo.
Mbunge wa Urambo Mashariki Mhe. Magreth Sitta akifurahi pamoja na baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi wa chuo hicho.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipata maelezo ya vifaa mbalimbali vya kufundishia fani ya Umeme kutoka kwa Mwalimu wa Chuo cha VETA Urambo Ali Musa alipotembelea karakana za chuo hicho.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipata maelezo juu ya vyerehani vya kufundishia fani ya Ushonaji kutoka kwa Mwalimu wa fani hiyo katika Chuo cha VETA Urambo Aines Sanduli alipotembelea karakana za chuo hicho.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa chuo cha VETA Urambo.
Jengo la utawala la Chuo cha VETA Urambo.

TCRA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamekamata watu 14 wanaondesha usajili laini simu

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendesha operesheni wahudumu 14 wanaosajili watu kwa kutumia alama za vidole bila kuwa na vitambulisho vya watoa huduma vya Kampuni za simu.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa waliokamatwa wanatakiwa mashitaka kutokana na kutumia mashine za kusajili alama za vidole bila kuwa kitambulisho cha mtoa huduma Kampuni ya simu husika.
Operesheni hiyo leo imeendeshwa katika Kanda zote za TCRA kwa watu wanaoendesha usajili wa alama za vidole bila kuwa vitambulisho vya watoa huduma.

Amesema ni kosa la kisheria kuendesha usajili wa laini za simu bila kuwa na kitambulisho na kuongeza kuwa baadhi yao wanafanya udanganyifu kwa wananchi kwa kuwatoza fedha.
Amesema mawakala waliowapa mashine  hizo wamefanya kosa la kisheria kwa utoaji wa mashine hizo kiholela.

Mhandisi Odiero amesema walishatoa namna ya usajili hivyo lakini baadhi wamekiuka utaratibu huo hivyo sheria lazima ishike mkondo wake.
Aidha ameongeza kuwa operesheni hiyo ni endelevu na kuwataka watoa huduma za usajili wakiwa na mashine kuacha ni mpaka pale watapokuwa na vitambulisho vya watoa huduma wa Kampuni za simu.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza kuhusiana na operesheni ya kuwakamata wanaoendesha huduma za usajili laini ya bila na vitambulisho kutoka Kwa watoa huduma wa Kampuni za simu ,jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa TCRA pamoja na Afisa wa Polisi wakichukua taarifa za mtoa huduma za usajili wa laini za simu kwa za vidole ambapo amekamatwa na Polisi kwa kuendesha huduma hiyo bila kuwa na kitambulisho cha Kampuni ya simu ya kumtambulisha kufanya huduma hiyo katika maeneo ya kariokoo jijini Dar es Salaam.
Afisa wa TCRA Noah Lalataika akichukua maelezo ya mtoa huduma za usajili wa laini ambapo anaendesha huduma hiyo bila ya kuwa na kitambulisho cha kumtambulisha kufanya huduma ya usajili wa laini kutoka Kampuni za simu katika eneo la Kariokoo jijini Dar es Salaam.

BEYONCE AIMBA KISWAHILI KATIKA WIMBO WAKE MPYA WA SPIRIT

$
0
0

Na Leandra Gabriel,  Michuzi TV
"UISHI KWA MUDA MREFU MFALME",  ni maneno yanayoanza katika wimbo mpya wa mwanadada Beyonce Knowles  unaojulikana kwa jina la 'Spirit '

Uingizwaji wa maneno hayo ya Kiswahili katika wimbo huo yamezidi kuiweka lugha ya kiswahili katika nafasi bora zaidi kwa kuwa lugha inazungumzwa kwa kiasi kikubwa duniani (kati ya lugha 10 zinazozungumzwa duniani)  na huzungumzwa zaidi nchini Tanzania.

Katika shairi la wimbo Beyonce ameanza kwa kuimba kwa sauti ya juu huku sauti nzito ikirudia maneno ya Uishi kwa muda mrefu mfalme akimaanisha long live the king  na kufuatiwa na maneno ya kiingereza ya Rise up to the light in the sky, yeah.... Watch the light lift your heart up na kuendelea.

Wimbo huo umeachiwa Leo Julai 11 na ni wimbo ambao umetumika katika filamu mpya ya Lion King iliyotengenezwa na kampuni ya Disney ya nchini Marekani.

Katika wimbo huo mfalme aliyeimbwa ni simba dume anayepambana kuwa mfalme wa nyika.

Albam hiyo ya Spirit inatarajiwa kuzinduliwa rasmi ndani ya siku tisa zijazo.

SabaSaba ya kipekee kwa StarTimes

$
0
0
Kila mwaka ifikapo tarehe 7 ya mwezi Julai watanzania tunasherehekea kilele cha maonyesho ya biashara ya SabaSaba. Siku ya Sabasaba hapo awali ilikuwa ni kwa ajili ya kuadhimisha kuanzishwa kwa Chama cha TANU kilichoipatia uhuru Tanganyika.

Siku zinavyozidi kwenda maonyesho haya yanazidi kuwa na mvuto zaidi kwani ubunifu unaongezeka na washiriki pamoja na wanunuzi ama watazamaji wanaongezeka kila mwaka. Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka katika viwanja vya SabaSaba vilivyopo Kurasini jijini Dar es Salaam na kwa sasa yapo chini ya TANTRADE. 

Maonyesho hayo yanahusisha zaidi ya wafanyabiashara 4000 ambao huonyesha bidhaa zao kutoka nyanja mbalimbali kuanzia kilimo-biashara, afya, vifaa vya viwandani, vifaa vya nyumbani, huduma za kibenki na elimu. Zaidi ya mataifa 30 yanashiriki katika maonyesho hayo kila mwaka na watu takriban 400,000 hufika kutembelea viwanja hivyo, na kufanya hilo kuwa soko kubwa sana kwa watangazaji wa biashara.

Katika banda la StarTimes mwaka huu walileta bidhaa mpya kabisa ambayo ni mtambo wa Solar ya kisasa kabisa inayokuja na luninga ya kisasa ya kidigitali yenye king’amuzi ndani.
“Mwaka huu ni tofauti na miaka mingine kwetu kwa sababu kwa mara ya kwanza tunatambulisha bidhaa yetu mpya ya Solar. Inakuja na TV ya kidigitali ambayo mteja wetu atatazama chaneli zote kwa miaka miwili bure kabisa.” David Kisaka Meneja Mauzo StarTimes Kanda ya Pwani.

“Bidhaa ya Solar pamoja na ving’amuzi vya StarTimes na luninga za kidigitali za StarTimes vinaendelea kupatikana kwenye maduka na ofisi za StarTimes hata baada ya Sabasaba kuisha, hivyo ni nafasi ya kujiunga na ulimwengu wa kidigitali hasa msimu mpya wa soka unapokaribia kuanza.” Samwel Gisayi, Afisa Mahusiano StarTimes.
 Mwakilishi wa Idara ya Mauzo, Vitus Lugulumu akitoa maelezo kwa Waziri wa Ulinzi Mhe. Hussein Mwinyi alipotembelea banda la StarTimes kujionea bidhaa mpya ya Solar iliyotambulishwa mwaka huu.
Msanii wa vichekesho Ebitoke akihudumia wateja katika banda la StarTimes, SabaSaba.

RAIS DKT.SHEIN AMETUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA AZAM MEDIA LIMITED

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Makampuni ya S.S. Bakhresa, Sheikh Said Salim Bakhressa kufuatia vifo vya wafanyakazi watano wa Azam Media Limited kutokana na ajali ya barabarani.

Ajali hiyuo imetokea juzi (Jumatatu) Julai 8, 2019 katika eneo la katikati ya Igunga (Tabora) na Shelui (Singida). Wafanyakazi hao ni kati ya watu saba waliofariki dunia katika ajali hio baada ya basi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari la mizigo wakati wakielekea Wilayani Chato kwa ajili ya uzinduzi wa Hifadhi hiyo ya Taifa ya Chato-Burigi. 

Katika salamu hizo za rambirambi Rais Dk. Shein alieleza kuwa amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya ajali hio na kwamba yeye binafsi pamoja na wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania nzima kwa jumla wamejawa na simanzi nzito kufuatia vifo vya wafanyakazi hao.

“Kutokana na msiba huu, natoa salamu za rambirambi kwako Sheikh Said Salim Bakhressa, ndugu, wanafamilia wa marehemu, marafiki, wafanyakazi wote wa Makampuni ya S.S. Bakhressa pamoja na watazamaji, wasikilizaji na wafuatiliaji wa vipindi na habari mbali mbali zinazotolewa na Azam Media Limited, ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, ilieleza sehemu ya salamu za rambirambi alizozituma Dk. Shein. 

Kadhalika, Rais Dk. Shein katika salamu hizo za rambirambi amemuomba Mwenyezi Mungu ampe moyo wa subira Sheikh Said Bakhressa katika kipindi hiki kigumu pamoja na wale wote walioguswa na msiba huo wakiwemo wafanyakazi wote wa nyanja ya habari. 
Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein amemuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu hao pahala pema peponi na awape afuweni na afya njema wale wote waliojeruhiwa katika ajali hio, ili waweze kuendelea na majukumu yao mbali mbali.  

Uongozi wa Azam Media Limited umethibitisha wafanyakazi waliofariki kuwa ni Salim Mhando, Said Haji, Florence Ndibalema, Sylvanus Kasongo, Charles Wandwi pamoja na dereva na utingo wa gari hilo ambapo waliojeruhiwa na kulazwa ni Mohamed Mwinshehe, Mohamed Mainde na Artus Masawe.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822  
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


Vodacom yazindua huduma m pya inayowawezesha wateja wa M-Pesa kutumia pesa zaidi ya kiasi walichonacho kwenye akaunti

$
0
0

Mkurugenzi wa 'M-Commerce' Vodacom Tanzania (Wapili kushoto), Epimarck Mbeteni , Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Bi.Herieth Lwakatare (watatu kulia) na Mkurugenzi wa Wateja wa Mikataba (Business Enterprise Unit), Arjun Dhillon (wa kwanza kulia) wakishikana mikono na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Hatari na Utekelezaji, Moses Manyatta (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara, Deogratius Kwiyukwa (watatu kushoto) na Mkuu wa matawi, Bonaventura Paul (wapili kulia) kutoka Tanzania Postal Bank (TPB) , kuashiria uzinduzi wa huduma mpya ya kifedha iitwayo 'M-Pesa songesha' amabayo inawawezesha wateja wa Vodacom Tanzania kutumia fedha zaidi ya kiwango walichonacho kwenye akaunti zao, Dar es Salaam, Jana. Kampuni ya Vodacom imedhamiria kubadili Tanzania kuwa jamii inayofanya malipo kidigitali zaidi.Mkurugenzi wa 'M-Commerce' Vodacom Tanzania, Epimarck Mbeteni akizungumza katika sherehe ya uzinduzi wa huduma mpya ya kifedha itwayo 'M-Pesa songesha' amabayo inawawezesha wateja wa Vodacom Tanzania kutumia fedha zaidi ya kiwango walichonacho kwenye akaunti zao, Dar es Salaam, jana. Kampuni ya Vodacom imedhamiria kubadili Tanzania kuwa jamii inayofanya malipo kidigitali zaidi.


Kampuni inayoongoza nchini kwa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu, Vodacom, leo imezindua huduma ya kwanza na ya kipekee nchini ambayo inaruhusu wateja wa M-PESA kukamilisha miamala wakati hawana fedha za kutosha katika akaunti zao za M-PESA. Uvumbuzi huu wa kibunifu uitwao M-Pesa Songesha umezinduliwa leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya kampuni hiyo.

Kwa kutumia huduma hii, wateja wa M-Pesa sasa wataweza kutumia huduma hii kwa urahisi zaidi wakiwa na uhakika wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kukamilisha miamala yao kama vile kulipia bili, kutuma pesa kwa ndugu jamaa na marafiki au hata kununua bidhaa pasipo kuwa na fedha za kutosha katika akaunti zao.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi wa M-Commerce, Epimack Mbeteni alisema, "dhamira yetu ya kuleta mifumo bunifu ya kifedha kwa kutumia simu za mkononi ilitupelekea kutazama kwa makini vikwazo vya mara kwa mara vinavyowazuia wateja wetu kukamilisha miamala yao kwa sababu ya upungufu wa fedha katika akaunti zao. Uchunguzi huo umepelekea kuja na ufumbuzi wa kibunifu wa wateja wetu kuweza kukamilisha miamala ya M-Pesa ambayo ingeshindikana kukamilika kwa sababu ya upungufu wa fedha".

Songesha ni moja kati ya huduma nyingi za M-Commerce zilizozinduliwa mwaka huu. Huduma hizi ambazo nyingi zinaendana na maisha ya kidijitali zimewezesha Vodacom kuendelea kuongoza katika huduma za simu na fedha nchini kupitia miamala ya simu, umiliki wa soko na wateja. Katika mwaka wa fedha uliomalizika mwezi Machi mwaka huu, M-Pesa iliongeza umiliki wa soko hadi kufikia asilimia 40 na kuingiza watumiaji zaidi ya milioni 9 katika mifumo rasmi ya kifedha ambao wanafanya miamala ya zaidi ya trilioni 4.1 kwa mwezi.

Watumiaji wa M-Pesa wanaweza kufikia Songesha kwa kupiga namba za huduma ya M-Pesa, *150*00#, kisha kuchagua huduma za kifedha na kujiunga na huduma hiyo ya M-Pesa Songesha. Mara tu baada ya mteja kujiunga na Songesha, atapata ujumbe wa kiwango ambacho anastahili na ataweza kutumia kiwango hicho kukamilisha miamala yake. Kiasi hicho kitarejeshwa pale ambapo mteja atapokea fedha katika akaunti yake ya M-Pesa.

"kiwango hicho kina riba ya asilimia 1 kwa siku 18 na wateja wetu wanaweza kufanya miamala kwa kutumia huduma hii kadri watakavyo ikiwa ni ndani ya kikomo cha kiwango chao. Tumeungana na benki ya TPB kuwezesha huduma hii na ili kuamua kiwango mteja anachostahili, benki itatumia taratibu zilizowekwa kulingana na miamala ya mteja husika katika matumizi yake ya M-Pesa" alisema Epimack.

Akiongea kuhusu huduma hii mpya, kaimu Afisa mtendaji mkuu wa TPB Bank Moses Manyatta alisema, “lengo letu kama benki ni kuhamasisha huduma jumuishi za kifedha huku tukiwahamasisha Watanzania kujenga tabia ya kujiwekea akiba na kujipatia mikopo kwa urahisi, Songesha ni kila kitu na inapatikana masaa 24 kwa siku saba kupitia simu yako ya mkononi! Tunajivunia kuwa na uhusiano huu na tuna Imani kwamba mapinduzi haya yatasaidia katika huduma jumuishi za kifedha,” alisema.

"Tunaendeleza nia ya kubadili Tanzania kuwa jamii inayofanya malipo kidijitali, tunawekeza katika teknolojia ya simu ambayo itaingiza watu wengi zaidi katika mifumo ya kifedha na hatimaye, kufikia malengo ya kijamii na kiuchumi ya nchi." alielezea Mbeteni. 

SAKASAKA KODI YA PANGO LA ARDHI LAANGUKIA MGODI WA GGML GEITA

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANNM GEITA
Operesheni maalum inayofanywa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kupita ofisi moja hadi nyingine kuzibana taasisi na Makampuni yanayodaiwa kodi ya pango la ardhi imeangukia Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) uliopo mkoani Geita ambapo imebainika mgodi huo hauna hati miliki ya eneo hilo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 196.27 sawa na takriban hekta 19,927 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000 na hivyo kushindwa kulipa kodi ya pango la ardhi.

Akiwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Geita tarehe 10, Julai 2019, Dkt Mabula alitembelea Mgodi huo wa Dhahabu wa Geita kwa lengo la kufuatilia ulipaji kodi ya pango la ardhi sambamba na kuangalia iwapo mgodi huo una hati miliki ya ardhi katika eneo hilo.

Hata hivyo, Dkt Mabula alielezwa na Mshauri wa Masuala ya Sheria ya Mgodi huo Elizaberth Karua kuwa GGML imekuwa ikilipa kodi mbalimbali serikalini lakini haijawahi kulipa kodi ya pango la ardhi kwa kuwa ina Leseni Maalum ya Uchimbaji Madini.

Kwa mujibu wa Karua, Mgodi wa Dhahabu wa Geita ambao uko ndani ya kampuni ya AngloGold Ashanti ya Afrika Kusini katika kipindi chote cha shughuli zake haujawahi kupewa wito wa kutakiwa kulipa kodi ya pango la ardhi na umekuwa ukizingatia Mkataba wa Uendelezaji Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement).

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Denis Masami alieleza kuwa, kodi ya pango la ardhi inapaswa kulipwa na haina uhusiano wowote na leseni za uchimbaji madini kwa kuwa mmiliki wake anakuwa kama amepangishwa eneo na sheria ya Tanzania imetamka bayana kuwa ardhi itakuwa chini ya Raisi na kusisitiza kuwa kodi ya pango la ardhi inalipwa kama zinavyolipwa ankara za umeme na maji.

Kwa mujibu wa Masami, cha muhimu katika suala la kodi ya pango la ardhi ni umilikishwaji ambapo Mgodi wa Dhahabu wa Geita unatakiwa kutambulika kwa kuwa na nyaraka sahihi za umiliki na kusisitiza tafsiri ya sheria ya madini siyo sehemu ya ardhi.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula pamoja na kuipongeza GGML kwa kuwa mlipaji mzuri wa kodi ya Serikali lakini eneo la Mgodi huo linapaswa kipimwa kutokana na kuwa katika mipango miji na sheria yake inaelekeza maeneo yote ya mipango miji kipimwa na kupangiwa matumizi.

‘’Eneo la Mgodi GGML lazima lipimwe na kupangwa kwa kuwa ndani ya mgodi kuna maeneo ya makazi, ofisi na matumizi mengine na vyote hivyo lazima vioneshwe katika ramani’’alisema Dkt Mabula.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, upimaji katika Mgodi huo wa GGML una faida kubwa kwa kuwa utaondoa migogoro ya ardhi ambayo baadhi yake husababishwa na wananchi kuingia maeneo ya mgodi na kutolea mfano Mgodi wa Nyamongo uliopo Tarime mkoa wa Mara baada ya kupimwa umeepusha migogoro iliyokuwa ikitokea sambamba na kulipa kodi ya pango la ardhi na kuutaka mgodi wa GGML kueleza ni lini utakuja na majibu wa kutaka kupimwa eneo lake.

Mshauri wa Masuala ya Sheria wa GGML Elizaberth Karua aliomba Mgodi huo kupewa muda wa wiki mbili kushauriana na uongozi wa juu kuhusiana na suala hilo kwa kuwa ujio wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ulikuwa wa kushtukiza ambapo Dkt Mabula aliupa Mgodi huo hadi tarehe 29 Julai 2019 kuja na majibu kuhusiana na suala hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita Richard Jordison alieleza kuwa ofisi yake iko tayari kushirikiana na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhakikisha suala hilo linafikia muafaka ili kuondoa migogoro.

Taarifa ya idara ya ardhi katika halmashauri ya Mji wa Geita inaeleza kuwa eneo la mgodi wa GGML halijapimwa bali lina alama za eneo lenye leseni ya uchimbaji ambazo hazina rekodi za upimaji na hivyo kuleta ugumu katika kuhakiki maeneo.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) Richard Jordison alipotembelea mgodi huo kufuatilia ulipaji kodi ya pango la ardhi  mkoa wa Geita tarehe 10 Julai 2019.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiondoka katika ofisi za Mgodi wa Dhahabu wa Geita uliopo mkoani Geita tarehe 10 Julai 2019 wakati wa ziara yake ya kufuatilia ulipaji kodi ya pango la ardhi katika Mgodi huo tarehe 10 Julai 2019. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Geita Josephat Maganga na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) Richard Jordison.
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao baina yake na uongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita uliopo mkoani Geita tarehe 10 Julai 2019 katika ziara yake ya kufuatilia ulipaji kodi ya pango la ardhi tarehe 10 Julai 2019. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa wilaya ya Geita Josephat Maganga na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) Richard Jordison.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimsikiliza Mshauri wa Masuala ya Sheria wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita Elizaberth Karua (hayupo pichani) wakati alipoutembelea mgodi huo kufuatilia ulipaji wa kodi ya pango la ardhi tarehe 10 Julai 2019. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Geita Josephat Maganga na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) Richard Jordison.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi Denis Masami (wa kwanza kulia) wakati alipofanya zaiara ya kufuatilia ulipaji kodi ya pango la ardhi katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita tarehe 10 Julai 2019. Wa tatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Geita Josephat Maganga na wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) Richard Jordison.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao baina yake na uongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita uliopo mkoani Geita katika ziara yake ya kufuatilia ulipaji kodi ya pango la ardhi katika taasisi na makampuni mbalimbali yanayodaiwa kodi hiyo tarehe 10 Julai 2019. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa wilaya ya Geita Josephat Maganga na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) Richard Jordison. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA HAROUN ALI SULEIMAN AZUNGUMZA NA WAANDISHI ZANZIBAR

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya kuzuia rushwa na Uhujumu Uchumi Mussa Haji Ali akitolea ufafanuzi juu ya Siku ya kupambana na Rushwa Afrika katika mkutano wa Waandishi wa Habari na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman kuzungumzia siku ya kupambana na Rushwa na Uhujumu uchumi ambayo huadhimishwa kila ifikapo 11/07/2019 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio Mazizini Zanzibar. 
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Yakut Hassan Yakut akitoa maelezo na kumkaribisha mgeni Rasmi katika Mkutano wa Waandishi wa Habari na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman kuzungumzia siku ya kupambana na Rushwa na Uhujumu uchumi ambayo huadhimishwa kila ifikapo 11/07/2019 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio Mazizini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Waandishi wa Habari na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman kuzungumzia siku ya kupambana na Rushwa na Uhujumu uchumi ambayo huadhimishwa kila ifikapo 11/07/2019 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio Mazizini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na namana Serikali inavyofanya jitihada za kuzuia rushwa na uhujumu uchumi katika siku ya kupambana na Rushwa na Uhujumu uchumi ambayo huadhimishwa kila ifikapo 11/07/2019 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio Mazizini Zanzibar. PICHA NA YUSSIF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

A TO Z YAWASHAURI WATANZANIA KUPENDA KUNUNUA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KIWANDA cha A to Z cha mkoani Arusha kimewashauri Watanzania kununua bidhaa zinazolishwa na viwanda vya ndani ili kuijenga Tanzania pamoja hasa kwa kuzingatia viwanda vya ndani vinatengeneza bidhaa bora kuliko zinatoka nje.

Kiwanda hicho ambacho kimeshika nafasi ya kwanza kwa kuzalisha bidhaa bora katika Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa kwa mwaka 2019.

Akizungumza wakati anazungumza na Michuzi TV na Michuzi Blog katika maonesho hayo yanayoelekea kumalizika Shom Darlami kutoka A to Z amesema wanajivua bidhaa bora ambazo zinatengenezwa na Watanzania zaidi ya 8000 waliopo kiwandani hapo.

Hata hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa A to Z inatamani na kuona bidhaa za Tanzania zikipewa kipaumbele kwa kununuliwa na Watanzania wenyewe na kwa kufanya hivyo usaidia kwanza kutafanya wenye viwanda kuendelea na uzalishaji lakini pili itakuwa fursa ya kuijenga Tanzania ya viwanda kwa pamoja.

"Kwanza tueleze A to Z tunazalisha bidhaa bora kwa gharama nafuu.Hata hivyo tunashauri wananchi wote wawe na utamaduni wa kupenda kununua bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vya Tanzania.

"Viwanda vya Tanzania kikiwemo A to Z  tunazalisha bidhaa bora sana kuliko hata hizo bidhaa zinazotoka katika nchi nyingine na kuingizwa nchini.Watanzania tupende vya kwetu ili kuijenga nchi yetu kwa pamoja na hatimaye kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya tano katika kuelekea uchumi wa kati utokanao na viwanda,"amesema Darlami.

Kuhusu kiwanda chao amesema katika maonesho ya biashara ya 43 kimeshika nafasi ya kwanza katika utengenezaji wa bidhaa bora huku akieleza kufurahishwa na idadi kubwa ya wananchi ambao wamekuwa wakifika kwenye banda la A to Z kununua bidhaa za nguo.

"Ahadi yetu ni kuendelea kuzalisha bidhaa bora kama kawaida yetu na kwa gharama nafuu.Ubora wa bidhaa zetu umetufanya tusiwe tunatangaza sana katika vyombo vya habari kwani akija mtu akanunua bidhaa yetu basi huyo atakwenda kuwaambia na wengine tena mdomo kwa mdomo na matokeo yake bidhaa zetu zinapendwa na tunapata wateja wengi sana,"amesema.

Amesisitiza kuwa ubora wa bidhaa zao unatokana na ari ya kazi kutoka kwa wafanyakazi wazawa 8000 ambao wameajiriwa kiwandani hicho kuhakikisha uzalishaji bidhaa unafanyika na tena kwa kiwango chenye ubora wa hali ya juu.

"Kila mwaka tunaona watu wanavyoongezeka katika kununua bidhaa zetu,"amesema Darlami na kuongeza wamekuwa na utaratibu wa kutangaza bidhaa zao mara moja tu kwa kila mwaka kupitia maonesho hayo na baada ya hapo huduma zao zinapatikana moja kwa moja kutoka kiwandani kwao.

"Baada ya maonesho haya tunarudi kiwandani, hivyo wanaohitaji bidhaa zetu tunawahudumia kutoka kiwandani.Kutokana 3na ubora wa bidhaa zetu tumekuwa tukifuatwa kokote tulipo na hasa kiwandani,"amesema.

Alipoulizwa ni aina gani ya bidhaa ambazo zimenunuliwa sana katika maonesho hayo ya biashara, amejibu nguo za watoto zimenunuliwa sana pamoja na nguo za wanawake.
 Baadhi ya bidhaa za nguo zinazozalishwa na viwanda cha A to Z mkoani Arusha zikiwa zimepangwa kwenye maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wananchi wakiendelea kuchagua nguo katia banda la A to Z katika maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Shoma Darlami akiwa ameshika  fulana ambayo imenunuliwa na moja ya wateja waliofika katika banda la A to Z katika maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Shom Darlami akionesha moja  fulana ambayo inatengenezwa na kimwanga cha A to A cha mkoani Arusha katika maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam
Muonekano wa banda la A to Z Katika maonesho ya biashara ya 43 ya Kimataifa jijini Dar es Salaam

MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola unaofanyika London,Uingereza. July 10,2019. 

Tanzania imeshiriki mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Madola ambao umelenga kujadili utekelezaji wa maazimio na vipaumbele vya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ikiwemo masuala ya utawala bora,usalama,biashara pamoja na namna kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na utunzaji wa mazingira. 

Akichangia katika majadiliano juu ya taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyokubaliwa katika mkutano wa Marais na Wakuu wa Serikali wa Nchi wanachama wa umoja huo ulifanyika mwaka 2018 London,Uingereza, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amewaeleza Wajumbe wa Mkutano huo kuwa Tanzania imeendelea kutekeleza maazimio ya mkutano uliopita kwa kusimamia ipasavyo misingi ya demokrasia na utawala bora na haki za binadamu na pia imehakikisha kuwa inatoa huduma bora za kijamii kwa watu wote ikiwa ni pamoja na kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, na pia imeongeza bajeti ya na kusogeza karibu huduma za afya karibu na wananchi kwa kujenga hospitali na vituo vya afya, nyumba za watumishi wa afya na kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba. 

Vile vile Mheshimiwa Kabudi aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa, Serikali inaendelea kuhakikisha kuwa wananchi wake wanapata huduma ya maji safi na salama na pia kuongeza upatikanaji wa huduma ya umeme vijijini na mijini ili kuchochea maendeleo katika maeneo yote ya nchi. 



Aidha ameongeza kuwa katika kutekeleza maazimio ya Umoja huo ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa mazingira, Tanzania tayari imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia tarehe 1 Juni, 2019 na amewahakikishia wajumbe kuwa mwitikio wa wananchi umekuwa chanya. 



Awali wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Katibu mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa Sekretarieti ya Jumuiya hiyo inafanya mageuzi makubwa ya kiutawala ili iweze kutoa huduma bora na kwa ufanisi miongoni mwa nchi wanachama. 



Pia amesema kuwa Jumuiya ya Madola inaendelea kuunga mkono na kutekeleza kauli mbiu ya umoja wa mataifa ya “hakuna atakayeachwa nyuma” katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ili kuhakikisha nchi zote wanachama wa Jumuiya zinapiga hatua mbele za kimaendeleo hususani katika nyanja za kiuchumi,kisiasa na kijamii. 



Bi. Scotland amewashukuru Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya hiyo kwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo na kuwataka kuendelea kushirikiana na sekretarieti ya jumuiya ili iweze kutekeleza malengo mahususi yanayoendana na mahitaji ya nchi wanachama. 



Katika hatua nyingine, Wajumbe wa Mkutano huo wameridhishwa na taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Richard Sezibera kuhusu maandalizi ya mkutano ujao wa Wakuu wa Serikali wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola unaotarajiwa kufanyika Kigali nchini Rwanda mwaka 2020.

USAHILI WA MSIMU WA PILI WA KUSAKA VIPAJI KWA WAONGOZAJI FILAMU WAFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0
Na Khadija Seif, Michuzi Tv
KAMPUNI ya Multichoice nchini imeendesha usahili wa  pili wa  Kusaka vipaji kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18 mpaka 26 na wenye ndoto ya kuwa waongozaji wa filamu.

 Akizungumza na Michuzi tv Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Multichoice nchini  kupitia  King'amuzi Cha (DSTV)  Grace Mgaya amesema kuwa msimu huo ni wa pili na umeanza rasmi na vijana wanne (4) kutoka Tanzania ambao watakuwa miongoni mwa vijana 60 kutoka kote barani Afrika na hiyo ni  kupitia  Mpango wa umoja wa Afrika ambao unatafuta wabunifu 60 wa filamu na televisheni barani  Afrika na kuwaweka sehemu ya darasa la mwaka 2019.

"Vijana 60 kutoka kote barani Afrika ikiwemo Tanzania watapata fursa ya udhamini wa kujifunza uzalishaji wa filamu na vipindi vya televisheni kwa mwaka mmoja katika awamu ya pili ya programu ya kusaka vipaji  vya waongozaji wa filamu Multichoice Talent Factory (MTF)," ameeleza.

Pia ameeleza kuwa fursa hiyo imezingatia vijana wenye uchu wa kuwa wabobezi watakaodhaminiwa kwa mafunzo hayo ya kitaalamu yanayoendeshwa  katika vituo vitatu barani Afrika ikiwa ni Nairobi, Lusaka na Lagos.

Aidha, Mgaya amefafanua kwa upande wa Tanzania, kuna nafasi nne za udhamini katika awamu hii ya pili ambapo  wanafunzi hao wataungana na wenzao kutoka Kenya,Uganda na Ethiopia katika kituo cha mafunzo cha Nairobi.

"Lengo la kuwanoa vijana wa kiafrika katika tasnia ya filamu ili kuwajengea uwezo, upeo,  ujuzi na weledi wa kiwango cha kimataifa katika uzalishaji na mapinduzi ya biashara ya filamu kwa ujumla. " ameeleza Mgaya.

Kwa upande wake Muongozaji bora wa filamu pamoja na picha jongefu nchini Adam Juma amesema ni wakati wa mapinduzi makubwa kwenye sekta ya filamu hapa nchini.

Juma amesema kuwa niaka miwili ijayo tutegemee mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Multichoice yataibua waongozaji wazuri na wanaofata mifumo mizuri ya uongozaji kutokana na tayari watakua wameshaiva kitaaluma.

 Pia ametoa wito kwa vijana watakaobahatika kuchaguliwa watumie fursa hiyo na watakaporejea nchini wasiache kuwashika mkono vijana wenzao ambao wanawiwa katika sekta ya filamu.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Multichoice nchini Grace Mgaya akitoa ufafanuzi kuhusu muitikio wa vijana waliojitokeza kwenye usahili wa pili wa Kusaka vipaji vya waongozaji wa filamu.

BREAKING NEWS: MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YATOKA, YATAZAME HAPA


TEMESA TANGA YAALIKA WADAU KUSIKILIZA KERO ZAO

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akizungumza na wadau (hawapo pichani) wakati wa kikao cha wadau kilichoandaliwa na Wakala huo kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo, maoni na ushauri kuhusu huduma za TEMESA. Kikao hicho kilifanyika katika karakana ya mkoa wa Tanga. Kulia ni Meneja wa mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina na kushoto ni msaidizi wake Mahangaiko Ngoroma. 
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katikati akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa TEMESA mkoa wa Tanga kilichofanyika katika karakana ya wakala huo kwa ajili ya kupata maoni, ushauri na changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau wa TEMESA mkoani humo. Kulia ni Meneja wa mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle 
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina kulia akisoma taarifa ya utendaji kazi ya karakana ya Wakala wakati wa kikao cha wadau (hawapo pichani) kilichofanyika katika karakana hiyo. Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle na kushoto ni Meneja msaidizi wa mkoa huo Mhandisi Mahangaiko Ngoroma. 
Baadhi ya wadau walioshiriki katika kikao cha wadau wa TEMESA mkoa wa Tanga wakichangia mada mbalimbali kuhusu utolewaji wa huduma za karakana ya mkoa huo wakati wa kikao kilichofanyika katika karakana ya TEMESA mkoa wa Tanga. Kikao hicho kiliandaliwa na meneja wa mkoa huo kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau hao na namna ya kuzipatia ufumbuzi. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katikati mara baada ya kumalizika kwa kikao cha wadau kilichofanyika katika karakana ya TEMESA. Kulia ni Meneja wa (TEMESA) mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina. 
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA TANGA) 
………………….. 
ALFRED MGWENO (TEMESA) TANGA 
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mkoa wa Tanga jana umealika wadau wanaotumia huduma zake ili kujadilli na kupata mrejesho kuhusu namna zinavyotolewa. Kikao hicho cha wadau kilichoandaliwa na meneja wa mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina kilifanyika katika eneo la wazi la karakana ya wakala huo na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na wadau mbalimbali wa taasisi za umma, taasisi binafsi, wazabuni, pamoja na wauzaji wa vipuri vya magari na mitambo. 
Awali, Akifungua kikao hicho, meneja wa TEMESA mkoa wa Tanga alisoma taarifa ya utendaji kazi kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 ambapo taarifa hiyo imeonyesha kiwango kikubwa cha ukuaji wa uzalishaji ambapo hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu uzalishaji wa mkoa huo umeweza kufikia zaidi ya shilingi Bilioni moja nukta tano sawa na asilimia tisini nukta nne ya uzalishaji wa mkoa. 
Mhandisi Margareth alizungumzia pia changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ikiwemo kucheleweshewa malipo ya madeni wanayodai wateja hasa wa Umma, ‘’hadi kufikia Juni mwaka 2019 tunadai zaidi ya shilingi milioni mia sita, tunaendelea na usuluhishi wa madeni hayo na wateja wetu ili kuingiza deni sahihi katika taarifa zetu za fedha za mwaka,’’alisema. 
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle alieleza mabadiliko mbalimbali yanayotokea katika Wakala ambapo huduma za karakana zimeanza kusogezwa kwa wateja wa mbali hasa uanzishwaji wa karakana mpya za Wilaya ikiwemo uanzishwaji wa karakana ya TEMESA katika Halmashauri ya mji wa Ifakara ambayo tayari imekwishaanza kufanya kazi, 
‘’TEMESA imeanza kubadilika, tuna mpango wa kuanzisha karakana katika Wilaya ya Same, Wilaya ya Simanjiro, Wilaya ya Korogwe pamoja na Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, tumesambaza vifaa vipya vya kisasa kwa ajili ya karakana kumi na mbili na tayari vingine vipo kwenye mchakato wa manunuzi’’. Alisema Mhandisi Maselle. 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alimshukuru meneja kwa kumkaribisha kwenye kikao hicho kama mdau, pia aliipongeza TEMESA kwa ubunifu na hatua wanazochukua kutatua kero za wateja wao ambapo alisema malalamiko mengi kwa sasa yamepungua tofauti na hapo awali ambapo akiwa Wilayani Manyara malalamiko yalikuwa mengi sana na kwa sasa hayapo tena. 
Nao baaadhi ya wadau walizungumzia kero zinazowakabili ikiwemo kucheleweshewa matengenezo ya magari, gharama kuwa juu pamoja na upungufu wa vipuri. Pia wadau hao waliomba mafundi wa karakana wapewe elimu ya kumhudumia mteja kwani wengi wao wamekuwa na kauli ngumu kwa wateja wao. 
Akijibu malalamiko hayo Mtendaji Mkuu alisema kucheleweshwa kwa matengenezo ni kutokana na kukosekana kwa vipuri katika karakana husika lakini tatizo hilo limekwishatatuliwa kwa kuwa sasa Mkoa wa Tanga una akiba ya kutosha ya vipuri, aliongeza kuwa Wakala sasa unaanzisha huduma ya kuhudumia wateja maarufu ambapo kipaumbele kitatolewa kwa wateja hasa wa magari ya viongozi ikiwemo wakuu wa Wilaya, wakuu wa Mikoa pamoja na Mawaziri ambao magari yao yatakuwa yakipatiwa huduma ya haraka pindi yanapofika katika karakana husika. Kikao kingine cha wadau kinategemewa kufanyika mkoani Kilimanjaro pamoja na mkoani Arusha siku ya Ijumaa.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KIKAZI KATIKA MKOA WA KAGERA WILAYA YA BUKOBA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti (kushoto) akimkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike ofisini kwake baada ya Kamishna Jenerali Kasike kufanya ziara katika Wilaya ya Bukoba na kwenda kumsalimia ofisini kwake.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akiweka saini katika kitabu cha wageni alipokaribishwa katika ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoa wa Kagera.
 Mkuu wa gereza la kilimo la Rwamulumba, Mrakibu Msaidizi Elly M Jacob akimkaribisha Kamishna Jenerali Phaustine Kasike kuingia ndani ya gerezani ili kufanya ukaguzi.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akitoa maelekezo kwa Koplo Arnold ambaye ni mganga wa gereza la kilimo la Rwamulumba.
 Mkuu wa gereza la kilimo la Rwamulumba, Mrakibu Msaidizi Elly M Jacob akimpa ufafanuzi Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike kuhusu kilimo cha chai na changamoto zake alipomtembeza Kamishna Jenerali Kasike kwenye shamba hilo la chai lililopo katika gereza la kilimo la Rwamulumba.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akizungumza na wafungwa pamoja na Mahabusu wa gereza kuu la Bukoba .
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Magereza Mkoa wa Kagera, Gereza Bukoba na Gereza Rwamulumba, wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike(hayupo pichani) alipofanya kikao nao kwenye ukumbi wa gereza Bukoba.

Picha zote na Kitengo cha Habari,Makao Makuu

WAZIRI LUGOLA ASHIRIKIANA NA WANANCHI KUJENGA SHULE MPYA YA MSINGI MWIBARA, SERIKALI YAWAPA NGUVU, YATOA MILIONI 96

$
0
0
Na Felix Mwagara, Mwibara (MOHA)
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewataka wananchi nchini wawe na utamaduni wa kushirikiana na Serikali kujenga shule, zahanati, vituo vya polisi katika maeneo wanayoishi kuliko kuwa na akili potofu miradi hiyo inajengwa na Serikali pekee.

Lugola ameyasema hayo wakati akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo, ambapo pia alishirikiana na wananchi wa Kijiji cha Namalebe kushiriki ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Ibwagulilo iliyopo katika Kata ya Chitengule jimboni humo ambayo Serikali imetenga shilingi milioni 96 kwa ajili ya kuikamilisha shule hiyo.

“Mradi huu unaendelea vizuri, ambapo Serikali imetupa milioni 96.9 kuukamilisha mradi huu, nami nipo hapa na nimeshirikiana na wananchi wangu kujitolea kujenga shule hii ambayo itawasaidia wananchi wa Kata hii ili Watoto wao waweze kupata elimu,” alisema Lugola.

Waziri Lugola pia aliwahamasisha wananchi hao kushiriki matukio ya maendeleo, pia alitoa mabati, saruji, nondo kwa ajili ya ujenzi wa zanahati, na kuongeza madarasa katika shule mbalimbali zilizopo katika jimbo lake.
Naye Fundi Mkuu wa Shule ya Msingi, Marco Malima, alimshukuru Waziri huyo kwa kufika katika eneo la ujenzi huo na imewapa nguvu zaidi kufanikisha ujenzi huo kwa wakati.

“Fedha na vifaa kukamilisha ujenzi huu zipo, ujenzi huu ulianza mwezi mei mwaka huu na unatarajiwa kukamilika mwezi wa saba mwaka huu, ambapo tunajenga madarasa, nyumba za walimu pamoja na vyoo,” alisema Malima.
Waziri Lugola anaendelea na ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo jimboni humo pamoja na kuzungumza na wananchi na kutatua kero zao zinazowakabili.

Lugola amewataka wananchi wa jimbo lake, waendelee kumuamini na kushirikiana naye wakati wanahakikisha jimbo hilo linakua jipya zaidi kimaendeleo.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Namalebe, Kata ya Chitengule, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola amewataka wananchi nchini wawe na utamaduni wa kushirikiana na Serikali kujenga shule, zahanati, vituo vya polisi katika maeneo wanayoishi kuliko kuwa na akili potofu miradi hiyo inajengwa na Serikali pekee. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akibeba tofali kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Ibwagulilo, ikiwa ni kuwahamasisha wananchi wa Kijiji cha Namalebe, Kata ya Chitengule, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo mpya. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akikagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Ibwagulilo, iliyopo Kijiji cha Namalebe, Kata ya Chitengule, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara. Lugola amewataka wananchi nchini wawe na utamaduni wa kushirikiana na Serikali kujenga shule, zahanati, vituo vya polisi katika maeneo wanayoishi kuliko kuwa na akili potofu miradi hiyo inajengwa na Serikali pekee. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Unesco kuendesha mafunzo kwa radio 25

$
0
0

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) litaendesha mafunzo kwa vituo vya radio 25 nchini Zanzibar kuanzia leo hadi Julai 18 mwaka huu.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha waandishi wa habari wa radio na watangazaji kutengeneza vipindi vya maendeleo huku vikizingatia jinsi.

 UNESCO itawajengea uwezo waandishi wa habari kuwa na uwezo wa kutengeneza taarifa za habari zenye uhusiano na maendeleo na jinsi.

Aidha radio zote zinazoshiriki zitapatiwa kiasi cha fedha kutumika katika kuboresha uzalishaji wa vipindi na taarifa za habari kwa kuzingatia jinsi na maendeleo kwa muda wa miezi sita.

Lengo kuu la kuboresha vipindi hivyo ni kuwezesha zaidi sauti za wanawake kusikika kupitia vipindi mbalimbali vya mahojiano.

UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswisi linaendesha mradi wa kuwezesha radio za wananchi kuwa na  mifumo ya tehama inayosaidia kutengeneza vipindi vizuri na vyenye kuwezesha maendeleo endelevu nchini.

Wafanyabiashara Kutumia Fursa kutoka NMB

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Babati Mjini,Pauline Gekul amewataka wafanyabiashara kutumia fursa ya kuendeleza biashara zao baada ya serikali kuondoa mlolongo wa tozo mbalimbali zilizokua zikitozwa na Mamlaka ya Mapato(TRA) kabla ya kufungua biashara.

Akizungumza katika mkutano uliondaliwa na benki ya NMB kwa wafanyabiashara mkoani Manyara(NMB Business Club) mjini Babati alisema waache kulalamikia mazingira ya biashara kwani katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 serikali imesikiliza kilio chao.

“Nawapongeza NMB kuwa na utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara na kuwapa maarifa ya mikopo na kukuza biashara zenu,naamini mtaendelea kutoa mikpo zaidi kwa wananchi wangu ili waweze kujiletea maendeleo kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi,”alisema Gekul

Meneja Mwandamizi wa NMB Wogofya Mfalamagoha alisema NMB ipo tayari kuwahudumia wafanyabiashara wa ngazi zote kutokana na mtandao uliosambaa nchini nzima ikiwa na matawi zaidi ya 228 na mawakala 6,800.

“NMB ina wafanyabiashara zaidi ya 200,000 nchi nzima ambao wamechukua mikopo yenye thamani ya Sh 600 bilioni,mtakubaliana name kuwa mikutano ya wafanyabiashara ambayo tunaifanya kuwaelimisha mambo ya biashara imekua na tija kwetu sote,”alisema Mfalamagoha

Aliwataka wafanyabiashara kutokutanguliza dhamana zao wanapotaka kuchukua mikopo bali wazo la biashara ambalo linaweza kuwaletea faida kwani benki haipendi kuuza dhamana za wateja baada ya kushindwa kurejesha mikopo waliyochukua.

Alisema shughuli za wafanyabiashara wadogo na kati ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi ikizingatiwa kuwa uchumi kwa ujumla wake unategemea mafanikio ya shughuli za kibiashara zinazofanywa na wafanyabiashara wadogo na kati nchini na duniani.

“Lengo la kukutana nanyi ni kuhakikisha mnakuza mitaji yenu, kutoa ajira kwa watanzania wengi zaidi na kuchangia uchumi kupitia ulipaji wa kodi na kwamba NMB imejipanga kuhakikisha inatoa huduma bora kwa jamii ya wafanyabiashara katika makundi yao,”alisema Mfalamagoha

Mwenyekiti wa wafanyabiashara(NMB Business Club) Mkoa wa Manyara, Ally Msuya alisema wamekua na mahusiano mazuri na NMB hiyo kupitia umoja wao ambao wameutumia kutatua changamoto za wafanyabiashara wanaochipukia na wenye uzoefu wa muda mrefu. 
 Meneja Mwandamizi Uhusiano Kitengo cha Biashara Benki ya NMB, Wogofya Mfalamagoha akizungumza wakati wa mkutano wa NMB na Wafanyabiashara (NMB Business Club) mjini Babati Mkoani wa Manyara. 

Mfanyabiashara Ophii Urasa akizungumza wakati wa mkutano wa NMB(NMB Business Club) na wafanyabiashara wanaonufaika na mikopo ya benki hiyo kwa wilaya za Babati, Hanang na Mbulu mkoani Manyara.
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images