Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MKUTANO MKUU WA 26 WA EACO WAFAANA JIJINI WMANZA

$
0
0
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe (Mb), amefungua Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Tasisi za TEHAMA Afrika Mashariki (EACO) Jijini Mwanza, Julai 5, 2019.
Mkutano huo unahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi wanachama za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini. Wakati wa ufunguzi huo pia wadau wa taasisi hiyo pia walishiriki.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) (aliyesimama akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 26 wa Shirikisho la Tasisi za TEHAMA Afrika Mashariki(EACO) Jijini Mwanza, Julai 5, 2019. Wengine pichani katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Killimbe Mkurugenzi Mkuu, TCRA Mhandisi James M. Kilaba.
Washiriki wakisikiliza hotuba ya Mhe. Waziri.
Washiriki wakisikiliza hotuba ya Mhe. Waziri.
Washiriki wakisikiliza hotuba ya Mhe. Waziri.
Wadau wa sekta ya mawasiliano nchini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe (Mb), (wapili kulia), akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba (kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt. Jones Killimbe (watatu kulia) na Mtendaji Mkuu wa EACO, Dkt. Ally Simba.
Meza kuu wakiwa wamesimama kwa heshima wakati wa kupigwa wimbo wa Taifa na ule wa Afrika Mashariki.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Kikundi cha Wachezaji Ngoma cha BUJORA Kikibudisha Vongozi na Washiriki kwenye Mkutano Mkuu wa EACO, Mwanza
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) (wapili kulia) akitoka baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Tasisi za TEHAMA Afrika Mashariki(EACO) Jijini Mwanza, Julai 5, 2019. Wengine pichani kutoka kulia, mwakilishi wa Katibu Mkuu (Mawasiliano) Bw.Mulembwa Manuku, Mkurugenzi Mkuu, TCRA Mhandisi James M. Kilaba na Mtendaji Mkuu wa EACO Dr. Ally Simba.

Rais Magufuli Afurahishwa na Ujio wa Rais Kenyatta Nchini

$
0
0


Na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuwa Rais wa kwanza wa nje kutembelea Wilaya ya Chato. 

Amesema kuwa ukiachilia mbali ujirani uliopo baina ya Tanzania na Kenya, pia kuna undugu kwa kuwa tunazungumza lugha moja, tunamuingiliano wa kijamii ikiwemo kuoana na kuwa na utamaduni unaofanana. 

“Kufika kwako umeudhihirishia umma wa dunia kuwa sisi ni majirani, na marafiki wa kweli siku zote tutatembea pamoja kamwe tusikubali kulaghaiwa na watu,” amesema Rais Magufuli. 

Rais Magufuli amesema kuwa kutokana na ushirikiano huo wafanyabiasha wa Kenya na Tanzania wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kijamii ikiwemo kuwekeza katika nchi zetu. 

Kwa ujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Kenya imewekeza miradi 504 yenye thamani ya dola 1.7 biloni ikiwa na idadi ya watu 50,956 huku wawekezaji wa Tanzania nchini Kenya wakiwa wakekezaji 24. 

Aidha katika Sekta ya Utalii, Tanzania ni nchi ya pili kwa watu wake kutembela nchini Kenya ikitanguliwa na nchi ya Marekani ambapo kwa mujibu ya takwimu za Bodi ya utalii ya Kenya ya Mwaka 2018 Watanzania 222,216 walitembelea Kenya ambayo ni zaidi ya 10% ya watu wote waliotembelea Kenya. 

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameitaja miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kwa ushirikiano wan chi hizi mbili ikiwemo barabara ya Holili- Arusha hadi Namanga pamoja na maandalizi ya ujenzi wa Barabara kutoka Mombasa hadi Bagamoyo. 

Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ipo katika hatua mbalimbali za kujenga meli tano ambapo itaanzisha safari za kutoka Bukoba – Mwanza – Kisumu na Jinja. 

Vile vile Rais Dkt. Magufuli ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Kenya kuja kuwekeza nchini hapa kwa kuwa milango ipo wazi kwa mwekezaji yeyote na Watanzania waendelee kuwekeza Kenya ili kuendeleza ushirikiano uliopo kwa mustakabari wa maendeleo ya nchi zote mbili. 

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyata amesema anayofuraha kuwa Rais wa kwanza wa nje kukanyaga ardhi ya Chato. 

Ameongeza kwamba uwepo wake Chato Mkoani Geita ni udhibitisho kuwa nchi hizi ni ndugu na wapo kwa ajili ya kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Kenya. 

“Hakuna mtu anayeweza kututenganisha kamwe, sisi kama watu wa Afrika Mashariki yatupasa kuhakikisha tunaondoa vikwazo vyote vitakavyozuia kutembeleana, kufanyabiashara pamoja na pengine hata kuoana.” Alisema Kenyatta. 

Apongeza Ujenzi Uwanja wa Ndege Chato 

Rais Kenyatta ameipongeza Serikali kwa kujenga uwanja wa ndege wa Chato kwa kuwa ni utaimarisha na kukuza ukuaji wa biashara na shughuli nyingine za kimaendelea katika ukanda huo jambo ambalo halipaswi kubezwa. 

Amesema anashangazwa na baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakipuuza jitihada hizo za kujenga uwanja huo kwani ni muhimu na yeye kama Rais wa Kenya angependa kuona Afrika ya Mashariki inakuwa kitu kimoja. 

Amechukizwa na kauli za baadhi ya wanasiasa na kusema haiwezekani kumzuia Mtanzania kufanya biashara au kuoa nchini Kenya vivyo hivyo kwa Wakenya nchini Tanzania. 

Rais Kenyatta yupo hapa nchini ikiwa ni ziara yake binafsi kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 05 Julai hadi siku ya kesho Jumamosi ya tarehe 06 Julai 2019.

WAREMBO 13 LEO KUCHUANA FAINALI SHINDANO LA MISS SHINYANGA 2019

$
0
0
Jumla ya warembo/walimbwende 13 kutoka halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kishapu,Kahama Mji, Ushetu,Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga kesho watachuana kuwania taji la Miss Shinyanga 2019.

Fainali ya Mashindano ya kutafuta Mrembo wa Mkoa wa Shinyanga(Miss Shinyanga 2019) yatafanyika  leo Jumamosi kuanzia saa moja kamili katika ukumbi wa CCM Mkoa (NSSF ya Zamani Mjini Shinyanga).

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Burudani ya Makumbusho Entertainment ambao waandaaji wa Shindano la Miss Shinyanga 2019, George Foda amesema maandalizi yamekamilika hivyo kuwaomba wakazi wa Shinyanga na maeneo ya jirani kufika kujionea jinsi wanavyoonesha vipaji vyao katika tasnia ya urembo ya ubunifu.Amesema zawadi ya pesa taslimu na ufadhili wa masomo ya vyuo mbalimbali kwa washiriki wa mashindano hayo zitatolewa.

Miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza katika mashindano hayo ni Linah Sanga,Daz Baba na Five Star Modern Taarabu.Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Washiriki wa Shindano la Miss Shinyanga 2019.
Washiriki wa Shindano la Miss Shinyanga 2019.
Washiriki wa Shindano la Miss Shinyanga 2019.

VIJANA NCHINI TANZANIA KUJENGEWA UWEZO WA UJUZI ILI KUTATUA CHANGAMOTO YA AJIRA

$
0
0

Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mh Rais Dr John Pombe Magufuli imejizatiti katika kutekeleza mpango kabambe wa kuwajengea Ujuzi Vijana kwa lengo la kutatua changamoto ya Ajira ili kupitia ujuzi watakaoupata katika mafunzo mbalimbali yanayotolewa chini ya Programu ya kukuza ujuzi inayosimaniwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. 

Hayo yamesemwa leo Mirerani,Wilaya ya Simanjiro-Manyara na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde wakati wa Kongamano la Wajasiriamali na shindano la kusaka vipaji linaloratibiwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Manyara Mh Esther Mahawe ambapo Naibu Waziri Mavunde alitumia fursa hiyo kuelezea mipango mbalimbali ya Serikali katika kuwajengea ujuzi Vijana wa Kitanzania kupitia program ya kurasimisha ujuzi,mafunzo ya kilimo cha kitalu nyumba na mafunzo kupitia vyuo vya Ufundi yote yenye lengo la kumjengea uwezo wa ujuzi kijana wa kitanzania ili aweze kujiajiri mwenyewe na kuajiri Vijana wengine. 

“Ni mpango mkakati wa serikali pia kuwajengea uwezo Vijana wa Mirerani kupata ujuzi wa kuongeza thamani katika madini ya Tanzanite ili kuongeza fursa zaidi za Ajira zitokanazo na sekta hii ya madini”Alisema Mavunde 
Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mbunge Wa Viti Maalum Mh Esther Mahawe ameeleza mikakati yake katika kuwakomboa wakina Mama na Vijana wa Mkoa wa Manyara kwa kuendelea kutoa elimu ya kujitambua na Ujasiriamali sambamba na kuchangamkia fursa zilizopo mkoani hapo. 
Kongamano hilo lilikwenda sambamba na shindano fupi la kutafuta vipaji vya wasanii ambao watalelewa na kufadhiliwa na Ofisi ya Mbunge Esther Mahawe.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 05.07.2019

Tanzania na Brazil zina Maeneo mengi ya kuimarisha uhusiano na kuendeleza Maslahi ya Pamoja

$
0
0

Ujumbe wa Tanzania uliojumuisha wafanyabiashara kutoka sekta binafsi na baadhi ya wakuu wa mashirika ya umma (pichani) wamefanya ziara ya kibiashara nchini Brazil yenye lengo la kutafuta fursa  za kibiashara, uwekezaji na masoko  kwa bidhaa zinozalishwa Tanzania.Ziara hii ilianza tarehe 28 Juni ina itakwenda hadi 08 Julai, 2019.



Ziara hiyo  ya siku kumi imebuniwa na sekta binafsi  kwa mashirikiano na ubalozi wa Brazil nchini Tanzania na kuratibiwa kwa pamoja na Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Brasilia, imejumuisha washiriki kumi na mbili ( 12) kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki, ofisi ya ubalozi wa heshima wa Brazil nchiniTanzania, jumuiya ya wafanya biashara Tanzania; kampuni ya Zest limited na Kampuni ya Alpha Group Afrika.  Washiriki wengine katika ziara hiyo ni kampuni ya  KC Land Development Plan, Kampuni ya Pivotec Company Ltd pamoja na Shirika la biashara la Taifa la Zanzibar(ZSTC), Mamlaka ya Uthibiti wa Matumizi wa Maji na Nishati Zanzibar(ZURA) na LAM Consultant. 

Katika Ziara hiyo ujumbe wa Tanzania umeonana na kufanya mazungumzo na Taasisi mbali mbali za Brazil zikiwemo  shirika kuu la uchimbaji mafuta  na gesi la Brazil (Petrobras), kampuni ya shughuli za idhibiti wa viwango na uendelezaji  wa masoko ya mafuta na gesi (IBP), Wakala wa uwekezaji na Biashara  ya Brazil (APEX), Muungano wa Jumuiya ya Wenye viwanda ya Brazil(NCI) na Taasisi ya Uendelezaji wa Wazalishaji wadogo na Wakati (SEBRAE).  Taasisi nyingine ambazo ujumbe huu ulikutana na viongozi na kuwa na mazungumzo ya ushirikiano ni Bodi ya Utalii ya Brazil(Embratur), Wizara ya Kilimo, Sehemu ya udhibiti wa biashara za Mazao ya matunda na mifungo, Muungano wa Wenye viwanda wa São Paulo na Taasisi ya uendelezaji wa Teknolojia na ubunifu (São Paulo Technlogy Incubator) ya mjini São Paulo.


Hali kadhalika, ujumbe wa Tanzania ulipata nafasi ya kutembelea Miji mbali mbali ya Brazil ikiwemo Rio de Janeiro , Brasilia, na São Paulo pamoja na kufanya mazungumzo  na Kaimu Balozi na Maofisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Brasilia na kukutana na Jumuiya ya Watanzania (Diaspora)  waishio mjini São Paulo.


Katika mazungumzo na shirika la uchimbaji wa mafuta na gesi la Petrobras na Kampuni ya uendelezaji wa masoko na Udhibiti wa mafuta na gesi (IBP) ilibainika kwamba pamoja na kampuni ya Petobras kusitisha shughuli zake za utafutaji wa mafuta nchini Tanzania, nchi hizi mbili zinaweza kuendeleza kushirikiana katika maeneo mbalimbali yakiwepo kujenga Uwezo, kuendeleza utafiti, kukuza masoko na shughuli za udhibiti wa bidhaa na viwango katika sekta ya mafuta na gesi, pamoja na kubadilishana uzoefu na wataalamu. Ili kuhakikisha utekelezaji wa maazimio yaliyokubaliwa pande mbili ( IBP na Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania-ATOGS ) zimekubaliana kuandaa mkataba wa ushirikiano na kusainiwa mara baada ya kukamilisha taratibu zinazohitajika.

Kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji imeonekana kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa bidhaa za Tanzania kama vile korosho, karafuu na mazao ya bahari kupata soko nchini Brazil. Pia wajumbe wamebaini kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa Tanzania kununua sukari kutoka Brazil. Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Brasilia umeahidi kufuatilia upatikanaji wa masoko hayo. Brazil ni mzalishaji mkubwa wa sukari na mazao ya mifugo.



Katika mazungumzo yaliyohusu ushirikiano wa uwekezaji kati ya nchi mbili yaliyofanyika katika Makao makuu ya wakala wa uwekezaji wa Brazil (APEX) mjini Brasília ilibainika kuwa Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza katika taratibu za kuvutia wawekezaji kutoka nje na kuendeleza wawekezaji wa ndani. Pia pande mbili zilikubaliana kushirikiana katika kuendeleza fursa za uwekezaji na kubadilishana Taarifa. Vile vilewajumbe walikubaliana kuhusu umuhimu wa kuwa na taarifa za kutosha kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania, hivyo wito ulitolewa kwa ofisi za Ubalozi wa Tanzania Brasilia, Ubalozi wa Brazil nchini Tanzania, wakala wa uwekezaji wa Brazil , mamlaka za uwekezaji Tanzania na jumuiya ya wafanya biashara na sekta binafsi Tanzania kuimarisha ushirikiano wa karibu sana kwa lengo la kuimarisha uwekezaji na kukuza biasharakwa maslahi ya maendeleo ya uchumi wa nchini hizi mbili.  



Kutokana na ziara hii, ujumbe wa Tanzania pia ulipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa Taasisi inayohusika na kuendeleza wazalishaji wadogo wadogo na wa kati (SEBRAE) nchini Brazil. Mazungumzo hayo yalifanyika katika makao makuu ya ofisi hiyo yaliyopo mjini Brasilia. Baada ya mazungumzo hayo pande mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya kubadilishana wataalam, uzoefu, na kujenga uwezo hasa kutokana na nchi ya Brasil kupiga hatua kubwa na kufanikiwa kuleta maendeleo katika kuimarisha uwezo wa wazalishaji wadogo wadogo na wa kati hasa wanawake. Pia ujumbe wa Tanzania ulitoa mwaliko kwa Viongozi wa taasisi hiyo na baadhi ya wazalishaji wa Brazil kutembelea Tanzania mwezi wa Oktoba wakati wa Tanzania Expo.




Kuhusu mazungumzo yaliyofanyika kati ya ujumbe wa Tanzania na Jumuiya ya Muungano wa viwanda wa Brazil, pande mbili zimekubaliana kwamba nchi hizi mbili zinashabihiana kimazingira, kijiografia, mila na utamaduni. Hivyo kuna haja kubwa wa kuimarisha mahusiano, kubadilishana wataalam, habari, na kukuza technologia ya uzalishaji katika viwanda. Brazil imeonesha nia ya kusaidia Tanzania katika kujenga uwezo wa wataaman wake kwa kutumia taasisi zake za mafunzo ya Technologia na kuendelea uzalishaji katika sekta ya viwanda. Kwahivyo imeonekana kwamba kuna haja ya kuweka saini makubaliano ya ushirikiano wan chi hivi mbili kati ya Jumuiya ya Muungano wa Viwanda wa Brazil na Jumuiya ya sekta binafsi pamoja na Jumuiya ya wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima wa Tanzania. Hatua hiyo itafikiwa baada ya kukamilisha taratibu za mikataba ya kimataifa




Kwa upande wa utalii imebainika kwamba licha ya kuwa Brazil na Tanzania kuwa zina mazingira na vivutio vinavyolingana vya utalii, Brazil inapokea zaidi ya mara tatu ya idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania. Hivyo Tanzania ina mengi ya kujifunza kutoka kwa ndugu zao wa Brazil. Wito umetolewa kwa pande mbili kushirikiana kwa kubadilishana uzoefu, taarifa na utalamu pamoja na kutembelea na.





Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dr Kebwe Steven Kebwe aipongeza Petrobena kwa kufadhili miradi ya vijana ya kilimo

$
0
0
  Mheshimiwa Mkuu wa  Mkoa wa Morogoro, Dr Kebwe Steven Kebwe (wa tatu Kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Petrobena Bw.Peter Kumalilwa  wakati alipotembelea shamba la Vijana la AgriAjira linalofadhiliwa na Petrobena. Pamoja nao ni Vijana wa AgriAjira wakiwa na Mkurugenzi wa Shirika la uzalishaji mbegu kutoka ASA.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mheshimiwa Dr. Kebwe Steven Kebwe akiangalia mafanikio makubwa ya shamba la mpunga ambalo limelimwa na vijana wa AgriAjira wilaya ya Kilosa ambao wamefadhiliwa na kampuni ya Petrobena.
Mkuu wa mkoa wa morogoro Dr Kebwe Steven Kebwe watatu kushoto  waliosimama  akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Petrobena Peter Kumalilwa wa kwanza kushoto waliosimama Katika picha ya pamoja na vijana wa Agri ajira alipotembelea shamba ambalo linafadhiliwa na kampuni ya Petrobena.

RAIS WA JAMHURI YA KENYA MHE UHURU KENYATTA APOKEWA KWA SHANGWE CHATO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita kwa ziara binafsi ya siku mbili.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakiwasalimia waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita mara baada ya kuzungumza na wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Chato.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakiwasalimia waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita mara baada ya kuzungumza na wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Chato
 Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakati akizungumza na wananchi waliofika kumpokea katika uwanja wa ndege wa Chato.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na kumkaribisha mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta akizungumza na wananchi wa Njia Panda Chato wakati akielekea katika Kijiji cha Mlimani na mwenyeji wake mara baada ya kuwasili.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakimjulia hali Mama mzazi Rais Bibi Suzana Magufuli ambaye anapatiwa matibabu kijijini kwake Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakimjulia hali Mama mzazi Rais Magufuli, Bibi Suzana Magufuli ambaye anapatiwa matibabu kijijini kwake Mlimani Chato mkoani Geita.
PICHA NA IKULU



Hukumu za Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa mashauri manne

$
0
0

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana kwa siku mbili Juni 22 na Juni 23,2019 ilisikiliza mashauri 4 na baadaye kuyatolea hukumu.

Shauri la Kwanza 

ERICK AMBAKISYE

Mlalamikiwa katika shauri hili hakuwepo katika kikao hiki licha ya kwamba taarifa ya wito ilitumwa kwa njia ya E-mail mnamo tarehe 16 Juni 2019 na kwa EMS Mnamo tarehe 17 Juni 2019 na risiti ya malipo ya kutumia nyaraka hizo iliwasilishwa mbele ya kikao kwa ajili ya uthibitisho lakini hata hivyo Mlalamikiwa hakutokea katika kikao hiki.Baada ya uthibitisho huo Kikao kiliazimia kuendelea bila uwepo wa Mlalamikiwa kwakuwa inaonekana alipata wito lakini hakutoa taarifa yoyote ya udhuru.

Tuhuma zilizomkabili ERICK AMBAKISYE ni mbili akiwa ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Songwe kama ambavyo zinaonekana katika hati ya mashtaka.

Pamoja na tuhuma hizo Mlalamikaji alikuwa na shahidi mmoja Nugu JAMES MHAGAMA ambaye aliitwa kwa nia ya kuthibitisha tuhuma hizo,Ambapo Shahidi alieleza namna ambavyo Mlalamikiwa alifanya vitendo kinyume na Katiba ya TFF ikiwemo kutokutoa ushirikiano kwake akiwa kama Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya TFF,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Msimamizi wa RCL Kituo cha Songwe.

Changamoto kubwa ilikuwa ni kuzuia kwa Maafisa,Waamuzi na watahmini wa mechi kutokana na deni la Tshs 5,700,000 na hatimaye shahidi huyu kufunguliwa kesi katika Mahakama ya Mwanzo Mkoani Songwe na kuwekwa ndani kwa siku tatu baada ya kukosa dhamana kitendo kilichofanywa na mmiliki wa hoteli ya Mkulima ambayo viongozi waliyofikia.

Pamoja na juhudi zote za kusuluhisha mgogoro huu na fedha kulipwa lakini Mmiliki wa hotel aliendelea kuwaghasi viongozi hao kwa kushirikiana na Mlalamikiwa.Kimsingi Mwenyekiti alitoa taarifa kuwa maandalizi yamekamilika na kila kitu kinaenda sawa jambo ambalo si kweli na hakuwahi kuonekana kipindi chote cha mashindano kuanzia tarehe 27 Machi 2019 hadi 9 Aprili 2019.Shahidi alifafanua zaidi kwa kusema kwamba mwenye mamlaka ya kuomba kituo ni Mkoa husika baada ya kujiridhisha kuwa umekamilisha maandalizi yote kwa ajili ya kuendesha mashindano ya RCL.

Wajumbe walipata fursa ya kumuuliza shahidi maswali mbali mbali kuhusiana na ushahidi uliotolewa kwa nia ya kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi katika shauri hili.

UAMUZI
Kamati imepitia vizuri mashtaka mawili dhidi ya Mlalamikiwa pamoja na ufafanuzi uliotolewa na Mlalamikaji akiungwa mkono na ushahidi wa Ndugu JAMES MHAGAMA ambaye alikuwa Mkoani Songwe wakati mashindano hayo yakiendelea.

Pia Shahidi ni mhanga wa vitendo visivyo vya kiungwana vilivyofanywa na Mlalamikiwa dhidi yake ikiwepo kufikishwa mahakamani kwa madai ya fedha ambayo yalilipwa na TFF lakini bado alifunguliwa kesi na kulazwa mahabusu baada ya kukosa dhamana.

Hii yote ilitokana na udhaifu ulionyeshwa na Mlalamikiwa katika uaandaaji wa mashindano haya ya RCL Kituo cha Songwe.

Kamati imeona kwamba TFF ilijitahi kuwa na mawasiliano yakaribu na Mlalamikiwa ili kujitahidi kuepesha fedheha hiyo lakini hakuonyesha juhudi zozote katika kutatua mgogoro huu zaidi ya kumtaka mimiliki wa hotel aendelee kudai fedha yake kwakuwa wageni/Viongozi wa TFF wanakaribia kuondoka na hata lipwa fedha zake jambo ambalo halikuwa na chembe ya ukweli.

Hivyo Kamati imejiridhisha kwamba Mlalamikiwa alikuwa na nia mbaya dhidi ya Shirikisho na hakujipanga kwa namna yoyote kuandaa mashindano haya na kutoa taarifa zisizo sahihi kuwa Mkoa una uwezo wa kuandaa mashindano jambo ambalo si kweli na kuonekana hana mahuasiano mazuri na viongozi wenzake akiwemo Katibu wake ambaye alitoa ushirikiano mkubwa tangu kuanza kwa mashindano hayo.

Pia kitendo cha kuto hudhuria kusikilizwa kwa shauri hili pasipo kutoa udhuru wowote inaonekana jinsi Mlalamikiwa alivyokusudia kutotoa ufafanuzi ambao ungekuwa ni utetezi wake kutokana na tuhuma ambazo zinamkabili.

ADHABU
Baada ya kupitia kwa kina ushahidi wa Mlalamikaji na vitendo vilivyoonyeshwa na Mlalamikaj, Kamati inamtia hatiani Mlalamikiwa kwa kumpa adhabu ya kutojihusisha na shughuli za Mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano (5) kwa mujibu wa Kanuni ya 73 ya Kanuni za Maadili za TFF za Mwaka 2013.
 
 
Shauri la Pili 
 
ATHUMAN KILUNDUMYA

Mlalamikiwa hakuwepo katika kikao hiki isipokuwa aliwakilishwa na Ndugu MAULID MWIKALO ambaye aliwasilisha mbele ya Kamati barua ya uwakilishi toka kwa Mlalamikiwa.

Mwakilishi alifafanua kwamba Mlamikiwa ni mtumishi wa Umma na ameshindwa kufika mbele ya Kamati kwa kuwa ana majukumu mengine kwa Mwajiri wake Mkoani Tabora.

Baada ya uthibitisho huo Kikao kiliazimia kuendelea na shauri kwakuwa Mwakilishi wa Mlalamikiwa alikuwepo.

Tuhuma tatu ambazo zinamkabili Ndugu ATHUMANI KILUNDUMYA akiwa ni Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora kama ambavyo zinaonekana katika hati ya mashtaka.

Mlalamikiwa aliingiziwa fedha kiasi cha Tshs 680,000/= kwa ajili ya kuhudhuria mkutano Mkuu wa TFF Jijini Arusha katika akaunti yake Namba 51001612542 iliyopo katika Benki ya NMB mnamo tarehe 29 Januari 2019 lakini hakudhuria kikao hicho ingawa fedha alipata na hata alipotakiwa kurejesha fedha hizo alikaidi maelekezo ya TFF.

Mlalamikiwa pamoja na kutuma Mwakilishi aliwasilisha utetezi wake kwa njia ya maandishi na katika tuhuma zote tatu alitoa majibu ya kufanana kuwa hajawahi kupokea fedha hizo wala maelekezo ya namna ya kurejesha fedha hizo na alijipanga kwa safari bahati mbaya safari yake iliishia Wilayani Nzega baada ya kuitwa kazini na Mwajiri wake kwani yeye ni Mtumishi wa Umma.

Hata hivyo Mwakilishi wa Mlalamikiwa alifafanua kuwa ni kweli Mlalamikiwa hakudhuria mkutano huo jijini Arusha pia ni hivi karibuni ndio amebaini uwepo wa fedha katika akaunti yake kwa zaidi ya miezi mitano isipokuwa mpaka sasa hajapewa utaratibu wa kurejesha,Iwapo atapewa utaratibu huo yupo tayari kurejesha fedha hizo kiasi cha Tshs 680,000/=.

Kamati ilimuuliza maswali ili kupata ufafanuzi wa iwapo aliingiziwa fedha hizo na kwakuwa hakuhudhuria Mkutano Mkuu Jijini Arusha kuanzia tarehe 2 Februari 2019 basi anapaswa kurejesha,Mwakilishi alikiri kuziona fedha isipokuwa hajaambiwa taratibu za kurejesha na akipewa hata leo yupo tayari kurejesha.

UAMUZI
Kamati imepitia vizuri mashtaka matatu dhidi ya Mlalamikiwa pamoja na ufafanuzi uliotolewa na Mlalamikaji na utetezi wa maandishi wa Mlalamikiwa ukiungwa mkono na ushahidi wa Ndugu MAULIDI MWIKALO,Kamati imejiridhisha kwamba Mlalamikiwa ametenda makosa yote matatu na hakuna utetezi wa msingi uliotolewa na ikizingatiwa kwamba maelezo yake na ufafanuzi wa Mwakilishi unaonekana kukinzana.Fedha kiasi cha Tshs 680,000/= kiliingizwa kwa Mlalamikiwa kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa TFF Jijini Arusha katika akaunti yake Namba 51001612542 iliyopo katika Benki ya NMB mnamo tarehe 29 Januari 2019 lakini hakuhudhuria kikao hicho ingawa fedha alipata na hata alipotakiwa kurejesha fedha hizo alikaidi maelekezo ya TFF.

Mkanganyiko wa maelezo yake unaonekana Mlalamikiwa si muaminifu pamoja kuwa ni mtumishi wa umma na hakuwasilisha vielelezo vyote ili kuonyesha kwamba alisafiri ingawa safari yake iliishia njiani na Mwakilishi wake hajui aina ya usafiri ambao ulitumiwa na Mlalamikiwa wala tarehe ya safari hivyo alikusudia kutumia fedha hizo kwa makusudi yasiyokusudiwa.

Mlalamikiwa akiwa mtumishi wa Umma anafafahamu taratibu za kurejesha fedha ambazo hazikutumika kwa lengo lililopangwa na kama angeona ni utaratibu tofauti basi alipaswa kufanya mawasiliano na viongozi wake waliondaa Mkutano huo jambo ambalo hakulifanya.

Maelezo kwamba fedha hii ameiona katika akaunti yake wili moja iliyopita yanaonekana hayana ukweli wowote.

ADHABU
Baada ya kupitia kwa kina ushahidi wa Mlalamikaji na vitendo vilivyoonyeshwa na Mlalamikaji hasa ubadhirifu wa fedha za Taasisi, Kamati inamtia hatiani Mlalamikiwa kwa kumtaka kwanza arejeshe fedha hizo kwenye taasisi, pili kumpa adhabu ya kutojishusisha na shughuli za Mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano (5) kwa mujibu wa Kanuni ya 73 ya Kanuni za Maadili za TFF za Mwaka 2013 tatu,TFF kumchukulia Mlalamikaji hatua za jinai iwapo itaona inafaa kwa ubadhirifu wa fedha alioufanya .
 
 
Shauri la Tatu 
 
CONSTATINE MORANDI

Tuhuma tatu ambazo zinamkabili Ndugu CONSTATINTE MORANDI akiwa ni Mwenyekiti wa Geita Gold Football Club kama ambavyo zinaonekana katika hati ya mashtaka.

Mlalamikiwa alizuia kuonyeshwa moja kwa moja na Azam TV kwa mechi ya mchezo wa mchujo play off kati ya timu yake dhidi ya Mwadui,Pia alikaidi maelekezo ya ufafanuzi wa kuonyeshwa kwa mechi hiyo kutoka katika shirikisho na kufanya vitendo vilivyoshusha hadhi ya TFF.

Mlalamikiwa katika utetezi wake alikana tuhuma zote tatu kuwa hakuhusika katika vitendo hivyo wala maandalizi ya mchezo huo kwa kuwa katika kipindi chote hicho alikuwa wilayani Chato katika kikao cha Wenyeviti wa Halmashauri kwa kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Geita,Hivyo alifika siku ya mchezo Timu zikiwa tayari na maandalizi yote yalifanywa na viongozi wenzake hasa Katibu wa Klabu ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za Klabu yao.

Aliiomba Kamati imuone hana hatia kwakuwa hakuna mawasiliano yoyote aliyofanya na TFF kwa niaba ya Klabu kuhusiana na mechi hiyo na hajawahi kuwazuia watu wa Azam TV kuonyesha moja kwa moja (Mubashara) mechi yao ya mchujo dhidi ya Mwadui,Hivyo alimalizia kwa kusema hakushiri katika kikao chochote cha maandalizi ya mechi hiyo kutokana kuwa nje ya Mji kwa muda huo wakati maandalizi yanafanyika.

Kamati ilimuuliza maswali ili kupata ufafanuzi hasa ushiriki wake katika kuzuia mechi, utendaji wa klabu yao namna mawasiliano yanavyofanyika ya kutoka nje ya Klabu yao,Majibu yake ni kuwa Katibu wa Klabu ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za kila siku na yeye huwa anapewa tu taarifa na kubariki lakini hili la kuzuia mechi hakushirikishwa.

UAMUZI
Kamati imepitia vizuri mashtaka matatu dhidi ya Mlalamikiwa pamoja na ufafanuzi uliotolewa na Mlalamikaji na utetezi wa Mlalamikiwa na kuona kwamba upande wa Mlalamikaji umeshindwa kuthibitisha tuhuma zote tatu dhidi ya Mlalamikiwa,Mlalamikiwa hakushiri kuzuia kuonyeshwa kwa mchezo kwakuwa hakuna uthibitisho wowote uliotolewa,Hakuwahi kupewa maagizo au maelezo yoyote toka TFF na kuyakaidi na wala hakufanya vitendo vyovyote vile ambavyo vilishusha hadhi ya TFF Kinyume na Ibara ya 50 (1) vya Katiba ya TFF.Hivyo kwa ujumla mashtaka dhidi yake hayajathibitishwa.

ADHABU
Baada ya kupitia kwa kina tuhuma dhidi ya Mlalamikiwa, Ushahidi wa Mlalamikaji na Utetezi wa Mlalamikiwa, Kamati imemuona Mlalamikiwa hana hatia yoyote na inamuachia huru.


Shauri la Nne 

SEIF KULUNGE

Tuhuma tatu ambazo zinamkabili Ndugu SEIF KULUNGE akiwa ni Katibu wa Geita Gold Football Club kama ambavyo zinaonekana katika hati ya mashtaka.

Mlalamikiwa alizuia kuonyeshwa moja kwa moja na Azam TV kwa mechi ya mchezo wa mchujo play off kati ya timu yake dhidi ya Mwadui.Pia alikaidi maelekezo ya ufafanuzi wa kuonyeshwa kwa mechi hiyo kutoka katika shirikisho na kufanya vitendo vilivyoshusha hadhi ya TFF.

Katika shauri hili Mlalamikaji aliwasilisha vielelezo mbalimbali ambavyo ni barua za mawasiliano kati ya Mlalamikaji,Bodi ya Ligi dhidi ya Mlalamikiwa ili vielelezo katika ushahidi wake na Kamati ilivipokee kwa kuwa hakukuwa na pingamizi lolote.

Shahidi wa Mlalamikaj iambaye ni Msimamizi wa Matangazo ya Moja kwa moja kutoka kituo cha Azam TV aliileza kamati kuwa alikuwa Geita katika Uwanja wa Nyankumbu kwa ajili ya maandalizi ya kuonyesha mechi hiyo lakini walizuiwa getini kwa maelezo kuwa mechi hiyo haitaonyeshwa mubashara la sivyo watapasua gari la matangazo,Hivyo kama msimamizi alichukua jukumu la kuwasiliana na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ambaye alimuunganisha kwa kiongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Geita Ndugu PIUS KIMISHA ambaye alimpa ushirikiano mkubwa,Kimsingi alieleza hakuwafahamu watu hao isipokuwa lilikuwa ni kundi la Vijana waliokuwa getini kuanzia saa tatu asubuhi hivyo mechi hiyo haikuonyeshwa kutokana na vitendo vya vijana hao.

Mlalamikiwa katika utetezi wake alikana tuhuma zote tatu kuwa hakuhusika katika vitendo hivyo wala maandalizi ya mchezo huo kwa kuwa katika kipindi chote hicho alikuwa anaumwa hapa Kigamboni Jijini Da Es Salaam na hajaenda Geita zaidi ya Miezi sita.

Alifafanua kuwa mnamo tarehe 2 Juni 2019 alipigiwa simu na Katibu wa TFF kwa kumuuliza yupo wapi kwa wakati huo,Ambapo baada ya muda kidogo alipigiwa tena simu kuwa kuna watu wamezuia gari la matangazo la Azam TV na alimjibu kuwa hafahamu watu waliozuia ingawa watu walikuwa wanahoji uhalali wa matangazo hayo na faida kwa Klabu ukizingatia kuwa timu inategemea viingilio vya mashabiki na Katibu akamsihi aruhusu na matatizo hayo yatamalizwa.Shahidi anasema alifanya juhudi binafsi za kuwasihi watangazaji wa Azam warejee kuonyesha mechi ambapo aliwasiliana na Watangazaji hao ambao ni Pascal Kabombe na Ahmed pia alimtaarifu Katibu Msaidizi wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Geita lakini juhudi zake hazikuzaa matunda.Azam TV walimjibu kuwa maandalizi yao yanachukua muda mrefu hivyo hawako tayari kurejea na usalama wao ni mdogo hasa mali.

Mlalamikiwa alikiri kuwa kulikuwa na mawasiliano baina yake na TFF pamoja na Bodi ya Ligi kwa emails na njia ya simu.

Kamati ilimuuliza maswali ili kupata ufafanuzi hasa ushiriki wake katika kuzuia mechi, utendaji wa klabu yao namna mawasiliano yanavyofanyika ya kutoka nje ya Klabu yao,Majibu yake ni kuwa hakuzuia mechi kuonyeshwa na yeye kama Katibu wa Klabu ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za kila siku na yeye huwa anawasilisha taarifa za utendaji kwa Mkurugenzi wa Mji kwakuwa timu hiyo si ya wanachama ni ya Halmashauri hivyo hakuna viongozi wengine,Pia alikiri kuandika barua kwenda TFF ili kujua namna ambavyo Klabu yao itanufaika na matangazo ya moja kwa moja ya mechi yao na alipata ufafanuzi toka kwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi.

UAMUZI
Kamati imepitia vizuri mashtaka matatu dhidi ya Mlalamikiwa pamoja na ufafanuzi uliotolewa na Mlalamikaji na utetezi wa Mlalamikiwa hasa vielelezo na kubaini kwamba kulikuwa na mawasiliano ya pande tatu juu ya uhalali wa mechi hiyo kuonyeshwa ambao ni Mlalamikaji,Bodi ya Ligi na Mlalamikiwa jambo ambalo halikupingwa na Mlalamikiwa.

Kamati imemtia hatiani Mlalamikiwa katika tuhuma zote tatu kwa kuwa ameonekana kushiriki katika kuzuia, kukosa uaminifu ikizingatiwa alikiri kuwepo mawasiliano baina yake na TFF na Bodi ya Ligi hasa barua yake ya ufafanuzi kwenda Bodi ya tarehe 31 Mei 2019 yenye Kumb na. GGFC/350/GT ambapo aliomba ufafanuzi wa mambo matano na ninakuu jambo la tano aliloliomba "Natumaini mawazo na ombi letu kama hakuna majibu au malipo ya pesa hatutakubali kuonyesha mubashara mechi yetu maana haina faida na timu" Kauli hii inathibitisha namna ambavyo Mlalamikiwa alishiriki katika kuhamasisha mechi isionyeshwe pamoja na kupewa ufafanuzi kutoka Bodi ya Ligi,Pia ni dhahiri kwamba hakuonyesha uaminifu kwa TFF ikizingatiwa kwamba alifanya maawasiliano na kupewa ufafanuzi kuanzia tarehe 31 Mei 2019 hadi 2 Juni 2019 na mwishoni akakiri makosa hayo kwa kukiri makosa na kupokea ushauri kwa mikono miwili na kuahidi kuimarisha ulinzi kwa mujibu wa email ya Mlalamikiwa kwenda TFF,vitendo hivyo vilishusha hadhi kwa wadau mbalimbali waliohudhuria mechi hiyo tangu siku ya kwanza.

ADHABU
Baada ya kupitia kwa kina tuhuma dhidi ya Mlalamikiwa, Ushahidi wa Mlalamikaji na Utetezi wa Mlalamikiwa, Kamati inamtia hatiani Mlalamikiwa kwa kumpa adhabu ya kutojihusisha na shughuli za Mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano (5) kwa mujibu wa Kanuni ya 73 ya Kanuni za Maadili za TFF za Mwaka 2013.

Kwakuwa vitendo vyake vingweza kuhatalisha usalama wa raia na mali zao hasa wapenzi wa mpira waliofika uwanjani kwa siku hiyo,Kitendo hicho kingeweza kuwaondoa Azam TV na wadhamini wengine kutodhamini mpira wa miguu nchini Tanzania,Hivyo kama kuna hasara iliyotokea basi Mlalamikiwa anapaswa kurejesha au kufidia hasara hiyo.


Wakili Kichere Mwita Waissaka
Mwenyekiti Kamati ya Maadili,TFF
Julai 5,2019

SHUKURANI

MAKATIBU TAWALA WAOMBWA KUENDELEA KUZISIMAMIA HOSPITALI ZA RUFAA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula akisema jambo kwa wajumbe wa kikao cha Viongozi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa kilichofanyika jana Jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Makatibu Tawala Mikoa Bi. Zena Said, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga akisema jambo katika kikao kazi cha Viongozi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa kilichoandaliwa na Wizara ya Afya na kufanyika katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango Dodoma.
Makatibu Tawala Mikoa nchini Tanzania wakisikiliza mada zinazowasilishwa katika Kikao Kazi na Viongozi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amewataka Makatibu Tawala nchini kuendelea kuzisimamia Hospitali za rufaa za mikoa ambazo kwa sasa zinasimamiwa na Wizara ya Afya.

Dkt. Chaula amesema hayo leo alipokutana na Makatibu Tawala kutoka Mikoa ya Tanzania Bara katika Kikao Kazi cha Viongozi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa kinachoendela kufanyika katika ukumbi wa Chuo cha mipango Jijini Dodoma.

“Licha ya Hospitali hizi kuhamishiwa usimamizi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  lakini bado zipo kwenye maeneo yenu, tunawategemea nyie Makatibu Tawala kuzisimamia hospitali hizi.” Amesema Dkt Chaula.

Dkt. Chaula amesema kuwa ni dhahiri lengo lilikuwa ni jema tuu kutoka kwa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, kwamba Hospitali zisimamiwe na Wizara ya Afya ili ziweze kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na Wizara ya Afya ambayo ndiyo Wizara mama inayotunga Sera na Miongozo pamoja na kusimamia Wadau.

Naye Mwakilishi wa Makatibu Tawala wa Mikoa katika kikao hicho Bi. Zena Said amempongeza Katibu Mkuu Wizara ya Afya kwa kuandaa kikao hicho cha kihistoria ambacho hakijawahi kufanyika kabla.
“Hili ni jambo la busara, pamoja na kwamba hizi Hospitali zimeondolewa kwenye mamlaka za Tawala za Mikoa lakini bado kuna mambo mengi ambayo bado tunayafanya kwa niaba ya Wizara” amesema Bi. Zena na kuendelea “Sisi kama viongozi tupo mikoani hatuwezi kukaa kuangalia mambo yakiharibika tukisea hizi Hospitali sio za kwetu” 

Bi Zena Said amesema kuwa Bado wanawajibika kwa njia moja au nyingine kuzisimamia kwa ajili ya kuleta ustawi kwa wananchi wetu na sisi wenyewe ambao tunatibiwa huko” amesema Bi. Zena Said.

Kikao hicho cha kihistoria kinafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuhamishiwa kwa usimamizi wa wa Hospitali za Rufaa za Mikoa tarehe 25, Novemba 2017 ambacho kitakuwa endelevu kila mwaka huku kikiwakutanisha viongozi wa hospitali, Waganga wakuu wa Mikoa pamoja na watendaji na wadau wa Sekta ya Afya nchini.

IGP SIRRO AKUTANA NA WATUMISHI RAIA NA KUFANYA TATHIMINI YA UTENDAJI WA MWAKA JANA NDANI YA JESHI LA POLISI MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na watumishi raia wa mkoa wa Dar Es Salaam ambao hawapo pichani katika kikao cha utendaji kazi pamoja na kufanya Tathimini ya mwaka jana ili kuweza kutatua changamoto zilizokuwepo zisijirudie kwa mwaka huu. Picha Na Jeshi na Polisi.
 Mkuu Wa Jeshi La Polisi Nchini IGP Simon Sirro,  Akimkabidhi Zawadi Ya Utendaji au utumishi Bora Mtumishi Raia Ndani Ya Jeshi La Polisi Aliefahamika Kwa Jina La Mwasi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Polisi na watumishi Raia wa Jeshi hilo baada ya kumalizika kwa kikao cha utendaji kazi. Picha na Jeshi na Polisi.

Balozi Amina: Bidhaa za viungo hazina ubora katika kupeleka Masoko mbalimbali

$
0
0
 Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar Balozi Amina Salum akizungumza wakati Siku ya Mwani na Viungo katika Maonesho ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Edwin Rutageruka akizungumza katika siku ya mwani na viungo katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 Wadau wa mwani na viungo wakiwa siku ya mwani na viungo.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SERIKALI  imesema bado  bidhaa za viungo na zile zitokanazo na zao la mwani  zinazozalishwa  nchini  hazina ubora stahiki jambo linalosababisha  wazalishaji kushindwa kuzipeleka  katika masoko  mbalimbali  ndani  na nje ya nchi. 

Aidha imesema mdalasini wa Tanzania unahitajika sana duniani,  kutokana na kutokuwa na kiwango cha kemikali na kuwataka wananchi kuchangamkia  fursa  hiyo. 

Kadhalika zao  la Iliki linahitajika kwa wingi  Pakstani ambapo  soko  lake  kubwa Kimataifa. 

Waziri  wa  Viwanda  wa Serikali  ya Mapinduzi Zanzibari, Balozi Amina  Salum  Ali alisema  hayo  jana katika siku  maalum ya bidhaa  za viungo na mwani katika  maonesho  ya 43 ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea  katika viwanja  vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa. 

Akizungumza, Waziri Amina  alisema kilimo cha mazao  ya viungo  kina  tija  na kimekuwa  kuwalipa sana na kuhimiza  wazalishaji  kutumia fursa  hiyo  kuzalisha bidhaa  zenye  ubora. 

Alihimiza  wazalishaji kutumia teknolojia ya kisasa na kutaka  vyombo  vya taifa  kuangalia teknolojia rahisi  ya kutumia  yenye  kuwasaidia wananchi. 

Kadhalika alihimiza kuwepo  kwa ubunifu katika  kutengeneza bidhaa zinazotakiwa na hata kuwa  na vifungashio  imara  na bora ili kumudu  soko la ndani na nje  ya nchi. 

Aidha alisema gharama kubwa  za uzalishaji  zinasababisha  bidhaa  kushindwa  kwenda sokoni na kuishauri  Mamlaka  ya Maendeleo  Ya Biashara  nchini  (Tantrade)  kuwezesha wazalishaji  hao  kufikia viwango  vya juu  katika uzalishaji na pia kuondoa changamoto  mbalimbali  wanazokabiliana nazo. 

Awali  akizungumza, Mkurugenzi wa Tantrade Edwin Rutageruka alisema zipo  fursa  mbalimbali  za uzalishaji wa bidhaa  za  viungo na kuwataka  wazalishaji kushirikiana na Mamlaka  hiyo  ili  kuweza kufika  mbali. 
Alisema  wapo  baadhi ya wafanyabiashara  ambao  sio  wakweli  wakiahidi  kusambaza  bidhaa  katika masoko  ya kimataifa lakini  wakiwa  hawawezi  kufanya  hivyo. 

Kuhusu  ushuhuda wa mafanikio  ya bidhaa  za viungo,  Mengi  Sume  aliwataka watanzania  kwa ujumla  kuzalisha  mdalasini  kwa wingi kwa kuwa unahitajika sana na  kemikali kama ilivyo  kwa  mingine. 

MAGOGO YA KUKATIA NYAMA MWISHO SEPTEMBA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
BODI ya Nyama Tanzania imesema, mwisho wa kutumia magogo ya kukatia nyama ni Septemba 30, mwaka huu, ambapo atakayekaidi atachukuliwa hatua za kisheria kwa sababu magogo hayo yanamadhara kiafya, ambayo yanatengeneza mazingira ya kuzaliana kwa wadudu  au vimelea vya magonjwa.

Aidha, imesema magogo hayo pia yanasababisha hasara ya upotevu wa nyama, kitaalamu katika kilo 100 inapotea kilo moja, ambapo kwa mwaka muuzaji anapoteza Sh milioni 3.8 ambayo inatosha kununua machine ya kisasa kukatia nyama.

Hayo yamesemwa leo Julai 5, 2019 na Ofisa Usajili kutoka katika bodi hiyo, Geofrey Sosthens katika maonesho ya 43 ya sababa  yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini  Dar es Salaam, ambapo aliwataka wafanyabiashara wa bidhaa hiyo kutembelea banda lao ili waweze kupata elimu.

Amesema watakao kaidi agizo hilo watachukuliwa hatua na Msajili wa bodi hiyo, kwa sababu tayari amekwisha ziandikia mamlaka za Serikali za Mitaa tangu  Februari, mwaka huu kwa maana ya wakurugenzi wa idara zote kuhakikisha wanaboresha maeneo yote yanayizalisha nyama ukiwa pamoja na machinjio, makalo na mabucha.

Ofisa huyo, ameongeza kuwa, hawapendi kuyatumia magogo kwa sababu yanamdhara kutokana na kwamba hayasafishiki, ukiwa unakata nyama baada ya mwezi yanakuwa ni mabaki ya muda mrefu na yanatengeneza vimelea vya magongwa ambavyo vinaweza kuleta madhara kwa walaji.

Aidha, amesema, utumiaji wa magogo pia husababisha hasara kwani mtu akitumia gogo, Kumbuka anatumia na shoka, kinachotokea nyama inagawanyika.

"Kama una bucha inauza kilo 200 kwa siku unaona ni kiasi gani unapoteza, ukipiga hesabu yak kwa mwaka unapoteza sh milioni 3.8 ambayo inatosha kununua mashine ya kisasa ya kukatia nyama, tunawasihi kuacha kuyatumia magogo kwa sababu si salama kwa afya za watumiaji," alisema Sosthens.

Tutahakikisha tunawashauri wamiliki wa mabucha kuhakikisha wanakuwa na mabucha ya viwango ambayo yapo kwenye sheria, viwango hivyo ni pamoja na kuacha kutumia magogo jambo ambalo tumeisha lisisitiza".

Ofisa huyo pia ametoa ombi kwa wadau wote wanaojishughulisha na mnyororo wa thamani wa nyama au anayefanya biashara hiyo au msafirishaji au mfugaji ahakikishe amesajiliwa na kumiliki cheti kutoka katika bodi hiyo.
Ofisa Usajili wa bodi ya nyama nchini, Geofrey Sosthens akifafanua jambo kww wananchi waliotembelea banda la bodi hii katika maonesho ya 43 ya sababa  yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini  Dar es Salaam.

WAZIRI MABULA AANZA KUSAKA MABILIONI YA KODI YA PANGO LA ARDHI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Munir Shemweta
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameanza operesheni maalum ya kuzibana Taasisi ambazo ni wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika jiji la Dara es Salaam kwa kutembelea ofisi moja hadi nyingine ili zilipe madeni yao katika muda uliopangwa ambapo katika ziara hiyo taasisi sita kati ya saba alizotembelea zimeahidi kulipa zaidi ya bilioni 4.5 kufikia Desemba 2019.

Dkt Mabula alizitembelea taasisi hizo juzi ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhakikisha wadaiwa wote sugu wa kodi ya pango la ardhi wanalipa madeni yao kabla ya hatua za kuwafikisha kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya wale watakaokaidi kulipa ambapo adhabu yake ni kulipa ama kupigwa mnada kwa mali za taasisi husika kufidia deni la kodi ya pango la ardhi.

Taasisi alizotembelea Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi juzi ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linalodaiwa bilioni 3, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) bilioni 1.4, EPZA milioni 200, Shirika la Reli Tanzania (TRC) bilioni 2.5, Shirika la Masoko Kariakoo milioni 249 pamoja na Chuo cha Taifa cha Utalii milioni 26.8.

Akiwa katika Shirika la Masoko Kariakoo, Dkt Mabula alishangazwa na Shirika hilo kudaiwa zaidi ya milioni mia mbili huku likiomba kulipa deni lake katika kipindi cha miaka miwili jambo alilolieleza kuwa ni kinyume na taratibu za ulipajia madeni ya kodi ya pango la ardhi ambazo humtaka mdaiwa kulipa nusu ya deni.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo Bw. Hetson Kipsi katika barua yake, Shirika lake liliahidi kulipa kwa awamu deni hilo katika kipindi cha miaka miwili kwa kutoa milioni saba kila mwezi jambo lililokataliwa na Dkt Mabula ambapo alieleza kuwa Shirika hilo linapaswa kulipa nusu ya deni kwanza ndipo liingia makubaliano ya kulipa kiasi kilichobaki kwa awamu. Hata hivyo Shirika la Masoko Kariakoo lilikubali kutoa milioni mia moja kufikia 29 Julai 2019 na kukamilisha kiasi kilichobaki desemba 2019.

Kwa upande wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mkurugenzi Mtendaji wake Masanja Kadogosa alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi Dkt Mabula kuwa Shirika lake halipingi kulipa deni inalodaiwa bali inachofanya ni kuhakiki upya deni hilo kwa kuwa kumekuwa na uhamisho wa umiliki wa mali za TRC kwenda TBA tangu mwaka 1999 sambamba na baadhi ya nyumba za Shirika kuuzwa kwa wananchi huku baadhi ya mali za TRC zikiwa hazina hati.

Kadogosa alisema, kiasi cha shilingi bilioni 2.4 wanachodaiwa ni kikubwa na hakilingani na uhalisia wa deni la TRC na kubainisha kuwa uhakiki utakapokamilika ana imani deni hilo litapungua kwa kiasi kikubwa. Dkt Mabula alimueleza kuwa, Shirika lake linapaswa kulipa robo ya tatu ya deni hilo wakati uhakiki ukiendelea na iwapo itaonekana deni limepungua basi kiasi cha fedha kilichozidi kitarudishwa.  Hata hivyo, Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TRC alikubali kulipa kiasi cha milioni 400 kwa awamu hadi kufikia oktoba 2019 wakati zoezi la uhakiki wa deni hilo unaohusisha Wataalamu wa Shirika hilo na Wizara ukiendelea.

Chuo cha Taifa cha Utalii kupitia kwa Kaimu Mkuu wa Chuo Boniface Mwaipaja kilikiri kudaiwa kiasi cha milioni 26.8 na kuahidi kulipa kwa awamu deni hilo ambapo Mkuu huyo wa Chuo aliahidi kulipa kiasi cha milioni saba kwanza na baadaye kulipa kwa awamu kiasi kilichobaki na kukamilisha deni hilo kufikia desemba 2019.

Taasisi nyingine zilizotembelewa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kuahidi kulipa madeni yao baada ya uhakiki ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) inayodaiwa bilioni 1.4, na EPZA milioni 200 ambapo kwa upande wake TBA tayari imeandaa utaratibu wa kulipa deni hilo kwa awamu na tayari milioni 40 zimetengwa wakati EPZA ilihidi kutoa mchanganuo wa jinsi itakavyolipa deni hilo wiki hii.

Juni 11, 2019 Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliitisha kikao cha Taasisi ambazo ni wadaiwa Sugu wa kodi ya Pango la Ardhi takriban 200 kwa kuwapa taarifa ya kulipa madeni yao sambamba na kuhakiki madeni hayo kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa kwa watakaokaidi kulipa madeni hayo. Ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ilikuwa ni kuangalia taasisi zinazodaiwa zimekwama wapi kutekeleza agizo lililotolewa.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizunguma na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa wakati alipokwenda ofisi za Shirika hilo kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni maofisa kutoka Wizara ya Ardhi pamoja na Shirika la Reli.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa wakati wa kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoka katika ofisi za Shirika la Masoko Kariakoo wakati alipokwenda ofisi za Shirika hilo kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Boniface Mwaipaja wakati alipokwenda ofisi za Chuo hicho kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipokewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosi mara baada ya kuwasili ofisi za Shirika hilo kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI) 

Mwenyikiti wa Bodi VETA aitaka Menejimenti ya VETA kupeleka bidhaa kwa wakulima

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Mwenyikiti wa Bodi ya VETA Peter Maduki ameitaka Menejimenti ya VETA kupeleka  bidhaa mbalimbali kwa wakulima na isiwe kuonekana katika Maonesho.

Maduki ameyesema hayo wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam amesema kuwa VETA imekuwa na ubunifu wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kuwatambua wabunifu wa VETA.

Amesema kuwa katika kwenda katika uchumi wa Viwanda ni kazi kwetu VETA kupeleka bidhaa kwa wakulima. Aidha amesema kuwa Menejimenti ya VETA  iendelee kubuni bidhaa mbalimbali na kupeleka kutatua changamoto ya wananchi. Kufika uchumi wa Kati na uchumi viwanda.
Aidha amesema kuwa bidhaa VETA ni bora kuliko zile za kutoka nje hivyo wananchi wawe na uzalendo wa kutumia bidhaa hizo.
Mwenyikiti wa Bodi wa VETA Peter Maduki akipata maelezo kwa mwanafunzi wenye uhitaji Maalum kuhusiana ubunifu wa mashine mbalimbali wanazounda kwa ajili ya kilimo wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwenyikiti wa Bodi ya VETA Peter Maduki akizungumza na waandishi habari mara baada ya kumaliza  kutembelea banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwenyikiti wa Bodi wa VETA Peter Maduki akipata maelezo katika banda la  VETA kuangalia ubunifu wa mashine mbalimbali.

MIRADI YOTE ITAKAMILIKA KULINGANA NA MAKUBALIANO YA MKATABA- DAWASA

$
0
0
Zainab Nyamka, Michuzi Tv
Mkurugenzi wa ukaguzi  wa Ndani ( Internal Audit)  wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam DAWASA Rosemary Lyamuya amesema wanahakikisha wakandarasi wanafanya kazi kulingana na makubaliano ya mkataba.

Rosemary ameyasema hayo alipotembelea banda la DAWASA lilipo kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Amesema, kazi kubwa inayofanywa na kitengo chao ni kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na Dawasa ambapo ni miradi ya maji safi na ile ya maji taka.

"Tunakagua miradi yote inayosimamiwa na Dawasa, ile maji safi na maji taka pamoja na kuhakikisha wakandarasi wanafanya kazi kulingana na makubaliano ya mikataba," amesema Rosemary.

Amesema, katika miradi inayokaguliwa na kitengo cha ukaguzi wa ndani (Internal Audit) wanahakikisha miradi inayojengwa na ile iliyomalizika kujengwa inaendana na mkataba pamoja na bajeti iliyopangwa.

Akizungumzia mikataba sita iliyosainiwa mapema wiki hii na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja na wakandarasi mbalimbali, Kitengo cha ukaguzi wa ndani  wamejipanga  kusimamia na kukagua miradi yote  na kuhakikisha wakandarasi wanafanya kazi zao na kufuata mikataba inavyosema.

Mbali na hilo, Rosemary ameeleza kuwa inapotokea kuna kuhujumiwa kwenye miundo mbinu ya Dawasa wamekuwa wanatoa ushauri kwenye menejimenti ili wayafanyie kazi.

Ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa pale wanapoona kuna miundo mbinu ya Dawasa inahujumiwa, ikiwemo watu kujiunganishia maji kiholela kwani hilo linasababishia hasara kwa mamlaka na kushindwa kufikia malengo ya asilimia 95 mwaka 2020.
 Mkurugenzi wa ukaguzi  wa Ndani  ( Internal Audit) DAWASA Rosemary Lyamuya akizungumza na waandishi wa habari na kuwahakikishia wanachi miradi yote iliyosainiwa na DAWASA wanaikagua na kuisimamia ili iendane na makubaliano ya mkataba na inamalizika kwa muda uliopangwa. Hayo ameyasema wakati wa  maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa ukaguzi  wa Ndani (Internal Audit) DAWASA Rosemary Lyamuya akipata maelezo kutoka kwa Afisa ubora wa maji Sizya Mongela alipotembelea banda la Mamlaka hiyo wakati wa maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa ukaguzi  wa Ndani (Internal Audit) DAWASA Rosemary Lyamuya akipata maelezo ya vifaa vinavyotumia kuunganishia maji kutoka kwenye bomba na kupeleka kwa mteja ili apate huduma ya maji safi na salama wakati alipotembelea banda la DAWASA kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Wafanyabiashara wa viungo watakiwa kuboresha bidhaa zao

$
0
0

MKURUNGEZI wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Edwin  Rutageluka amewaonya  wafanyabiashara wa viungo waache udanganyifu wanapotayarisha bidhaa ili viwe katika ubora unaofaa kuweza kupata soko mpaka nje ya nchi.

Akizungumza leo katika Maonesho ya 43 ya kimataifa na biashara Rutageluka amesma, baadhi ya  wafanyabiashara hasa wa kiungo cha pilipili manga wamekuwa na tabia ya  kuchanganya mbegu za mapapai ili kuzidisha ujazo katika kiungo hicho

Rutageluka amesema, no bora wafanyabiashars wakaacha udanganyifu katika bidhaa zao lengo likiwa ni kuhakikisha viungo vya Tanzania vinatumika ndani ya Nchi na nje ya Nchi.

Amesema TANTRADE imebaini udanganyifu unaofanywa kwa baadhi ya mikoa na wafanyabiashara wamekuwa wakichanganya viungo na vitu vingine ili kuleta uzito udanganyifu ambao huwezi kuubaini mara moja.

Kwa upande wake, waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Amina Salum Ali amewataka Watanzania kuthamini bidhaa zinazotengezwa ndani ya Nchi na wale wanaofanya biashara ya viungo kutengeneza viungo vyao kwa umakini ili waweze kupata soko nje ya nchi.

Amesema,  japokuwa sekta hiyo imekuwa na changamoto nyingi lakini serikali itahakikisha inazipunguza.

Akiongelea kilimo cha Mwani,  Waziri Amina aliongelea kilimo Cha mwani na kusema kuwa hivi Sasa kimekuwa na tija kwa maendeleo ya wananchi.

RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA AMALIZA ZIARA YAKE BINAFSI YA SIKU MBILI CHATO MKOANI GEITA NAKUREJEA NCHINI KWAKE

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta katika uwanja wa ndege wa Chato mara baada ya kumaliza ziara yake binafsi ya siku mbili Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshma iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni  wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta wakati wakisikiliza nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na wanakwaya wa Mwagazege ya Chato kabla ya Rais Kenyatta kuondoka na kurejea nchini Kenya.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta Chato mkoani Geita.

 Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta akimsalimia Mama mzazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Bibi Suzana Magufuli ambaye anapatiwa matibabu kijijini kwake Mlimani Chato mkoani Geita kabla ya kuondoka kurejea Kenya mara baada ya kumaliza ziara yake binafsi ya siku mbili.
 Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
  Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta akiweka shada la maua katika moja ya makaburi ya Familia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli yaliyopo katika kijiji cha Mlimani Chato wakati akiwa katika ziara yake binafsi ya siku mbili.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na  mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta mara baada ya mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta  ambaye aliambatana na ujumbe wake kutoka Kenya katika ziara yake binafsi ya siku mbili katika kijiji cha Mlimani Chato Mkoani Geita.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kabla ya kuondoka katika kijiji cha Mlimani Chato na kurejea nchini kwake Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpungia mkono mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati akipanda ndege kurejea nchini Kenya. PICHA NA IKULU



LUGOLA ASEMA POLISI WANAOSHIRIKIANA NA MAFISADI KUDHULUMU ARDHI YA WANANCHI MASKINI, DAWA YAO IMEIVA

$
0
0

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Haruzale, Kata ya Nyamihyolo, Mwibara, Wilayani Bunda, leo. Lugola alisema tabia ya baadhi ya polisi nchini wanaoshirikiana na mafisadi kudhulumu ardhi ya wananchi maskini, dawa yao imeiva, hatamuonea mtu huruma. 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiwaelekeza wananchi wa Kijiji cha Kabainja Kata ya Kasuguti, Mwibara, Wilayani Bunda, jinsi ya kujenga darasa lililoimara katika shule ya msingi Kabainja kijijini hapo, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
……………………… 
Na Felix Mwagara, Mwibara (MOHA) 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema baadhi ya polisi wasiokuwa waaminifu nchini wanaoshirikiana na mafisadi kudhulumu ardhi ya wananchi maskini, sasa dawa yao imeiva. 
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Haruzale, Kata ya Nyamihyolo, Jimbo la Mwibara, Bunda akiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo jimboni mwake, Lugola amesema amepokea malalamiko mengi ya ardhi katika jimbo lake na sehemu mbalimbali nchini. 

Amesema mafisadi wa ardhi hukimbilia kufungua kesi vituoni wakilazimisha kwa kutumia fedha ardhi iwe mali yao wakiwatumia polisi wasiokuwa waaminifu ili kufanikisha matwaka yao. 

“Haiwezekani tabia hii ikachekewachekewa na kuonekana ni kawaida, nimekemea sana katika mikutano yangu hapa Mwibara na sehemu zinginezo hapa nchini, nitahakikisha napambana na mafisadi pamoja na polisi hao wasiokuwa waaminifu,” alisema Lugola. 

Waziri Lugola alisema kila kukicha anapata malalamiko mengi kutoka sehemu mbalimbali nchini kuwa mafisadi wanaendelea kuwaonea wananchi maskini kwa kupora ardhi wakidai wao ndio wamiliki halali. Aliongeza kuwa, utumia polisi wasiokua waaminifu kuwakandamiza wananchi ambao hawana nguvu ya kifedha na kufanikiwa kudhulumu ardhi zao. 

“Dawa yao ilikuwa jikoni, sasa imeiva, siwezi mwangusha Mheshimwa Rais Dkt. John Magufuli, Serikali hii haichezewi hata siku moja, sasa nitawashughulikia ipasavyo,” alisema Lugola. 

Aidha, Lugola aliwataka wananchi wa Mwibara kuhifadhi vyakula vizuri ili kuepusha janga la njaa kwa hapo baadaye na kusababisha wananchi kuja kuteseka kwa ukosefu wa vyakula na kusababisha mateso katika familia. 
“Tutunzeni vyakula vyetu, msitumie hovyo, kuweni makini na matumizi ya vyakula, sitaki nije kuona mnateseka na njaa, hakikisheni mnatunza vyakula kwa ajili ya matumizi ya baadaye, ogopeni njaa kama ukoma,” alisema Lugola. 
Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, alifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo akikagua madarasa ya shule ya msingi pamoja na zahanati.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images