Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA KUFUNDSHIA NA KUJIFUNZIA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM

0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi walio kwenye ‘summer camp’ katika Chuo cha Ualimu Butimba Jijini Mwanza. Ametumia fursa hiyo kuelezea juhudi ambazo Serikali imekuwa ikizifanya katika kutatua changamoto za watoto wenye ulemavu ili waweze kupata elimu.
Wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William ole Nasha wakati alipokutana nao kuzungumzia juhudi ambazo Serikali imekuwa ikizifanya kutatua changamoto za watoto wenye ulemavu katika kupata elimu. 
……………………… 
Serikali imesema inatambua changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji maalum na ndio maana inachukua juhudi za makusudi kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili yawe rafiki kwao kupata elimu. 
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati akizungumza na wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi walio katika Kambi ya Joto (Summer Camp) inayoratibiwa na Taasisi ya Under the Same Sun. 

Naibu Waziri Ole Nasha alisema katika kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa sasa Wizara anayoiongoza inatekeleza Programu ya Elimu Jumuishi ambayo inamuweka shuleni mtoto mwenye ulemavu na yule asie na ulemavu kwa lengo la kuondoa fikra za kunyanyapaliwa lakini pia kujenga umoja upendo na urafiki baina yao utakaowawezesha kulindana kwani siku zote mlinzi mzuri ni rafiki na ndugu hivyo inasaidia kuondoa changamoto zilizopo. 

Aidha, Serikali pia inatoa mikopo kwa asilimia mia moja kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma elimu ya juu kwa lengo la kuwasadia waweze kupata elimu zaidi kwani watu wenye ulemavu wakipata elimu wanaweza sio tu kujikomboa wenyewe lakini kuwasaidia watu wengine wenye changamoto hizo. 

“Ninyi wenyewe mtakuwa mashahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Serikali yake kuna viongozi ambao wana ulemavu lakini kutokana na umahiri na uwezo walio nao katika utendaji wameteuliwa katika nafasi hizo. Tambueni kuwa watu wote wana haki sawa na hilo liko wazi,” alisema Naibu Waziri ole Nasha. 

Kiongozi huyo amewataka wanafunzi hao kutambua kuwa wao ni watoto wa kitanzania hivyo wanatakiwa kuwa huru kwenye nchi yao na kwamba Serikali itaendelea kuwalinda ili waweze kuishi lakini pia kusoma kama watu wengine bila kudhuriwa na kitu chotote. 

”wote ni mashahidi kwamba kwa sasa Serikali imefanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kwamba mnakuwa na usalama wa maisha yenu, sidhani kama kuna kosa ambalo sasa ukipatikana nalo unachukuliwa hatua kubwa zaidi kama kujaribu kuwadhuru watu wenye ualbino, na ndio maana sasa mnapata ulinzi kaeni mkiwa huru kwa kuwa serikali inawajali,”aliongeza Naibu Waziri Ole Nasha 

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ole Nasha amelitaka Shirika la Under The Same Sun kutambua kuwa Serikali inathamini mchango mkubwa wanaoutoa katika kuwasaidia wanafunzi na watoto wenye mahitaji maalum hasa watoto ambao wana changamoto ya ulemavu wa ngozi na kuwataka kuhakikisha mafunzo wanayoyatoa katika kambi za joto (summer camp) kila wanapokutana pamoja na mambo mengine yalenge katika kuwaonesha watoto hao kuwa jamii inawajali na sio vinginevyo. 

Nae Afisa kutoka Idara ya Elimu ya Shirika la Under the Same Sun Omary Mfaume amesema Shirika hilo linafadhili wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi kupitia programu za elimu zinazojihusisha na ufadhili wa elimu na ile ya uhamasishaji jamii ambayo inayowafundisha kwanini mtu anazaliwa na ualbino, changamoto zake na namna ya kuzikabili changamoto hizo. 

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake Clara Maliwa ameiomba Wizara kuwa na utaratibu wa kuwatambua Wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wanaofanya vizuri katika masomo ili kutoa changamoto kwa wengine ili waweze kufanya vizuri zaidi.

BARAZA LA UWT MKOA WA MAGHARIB WATAKIWA KUPIGA KAZI

0
0
MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Magharibi,Ndugu Zainab Ali Maulid (kushoto),akifungua Mkutano wa Baraza hilo la UWT Mkoa wa Magharibi. 
WAJUMBE wa Baraza la UWT Mkoa wa Magharibi wakisikiliza nasaha za Mgeni rasmi katika Kikao hicho 
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Magharib Ndugu Mohamed Rajab Soud,akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za Mkoa huo Mwera Unguja 
MJUMBE wa Baraza la UWT Mkoa wa Magharibi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Welezo Dkt.Saada Mkuya, akitoa shukrani kwa niaba ya UWT katika Mkutano huo. 

************* 

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR. 

JUMUIYA za Chama Cha Mapinduzi Nchini zimetakiwa kuzidisha juhudi katika kufanya kazi za kuimarisha CCM ili Taasisi hiyo iendelee kuwa bora kisiasa Nchini. 

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Magharibi Ndugu Mohamed Rajab Soud,wakati akiwahutubia Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la UWT Mkoa wa Magharibi Unguja. 

Amesema Jumuiya za CCM licha ya kufanya vyema katika majukumu yake ya kila siku bado zinatakiwa kuongeza kasi ya kiutendaji na kiubunifu hili kuhakikisha Chama ndani ya Mkoa huo kinaimarika Kisiasa,Kiitikadi na Kiuongozi. 

Kupitia Mkutano huo Mwenyekiti huyo Ndugu Rajab, amewambia Akina Mama hao kuwa Wanategemewa na Chama Cha Mapinduzi katika harakati mbali mbali za Kisiasa hivyo wanatakiwa kutumia uwezo wao wa Kisisa na Kitaaluma ili kuhakikisha CCM inapata ushindi katika Uchaguzi wa mwaka 2020. 

Amesema Akina Mama hao kwa juhudi zao za kutekeleza kwa wakati mwafaka hasa katika kufanya vikao mbali mbali vilivyoelekezwa na Katiba ya Jumuiya hiyo. 

Amesema Viongozi na Wanachama kila mmoja kwa nafasi yake wanatakiwa wanatakiwa kuwaeleza Wananchi katika maeneo yao Utekelezaji wa Ilani ya CCM unaotekelezwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wabunge,Wawakilishi na Madiwani. 

Aidha amesema Mkoa huo upo katika maandalizi ya kutekeleza kwa Vitendo kampeni ya Magharibi ya Kijani kwa kuhakikisha Mkoa huo unakuwa ni Ngome imara ya CCM Kisiasa. 

Awali akizungumza Mwenyekiti wa UWT Mkoa huo,Ndugu Zainab Ali Maulid amesema Jumuiya hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza kazi mbali mbali za kuleta maendeleo endelevu ndani ya CCM. 

Ameeleza kuwa kwa sasa jumuiya hiyo inaendelea na mipango ya kuongeza Wanachama wapya hasa Wanawake ili kuhakikicha CCM inaingia katika Uchaguzi Mkuu Ujao ikiwa na Takwimu sahihi za Wanachama wenye sifa za kupiga kura. 

Akitoa Shukrani kwa niaba ya Jumuiya hiyo,Mbunge wa Jimbo la Welezo Dkt.Saada Mkuya amesema nasaha zilizotolewa na Mgeni rasmi watazifanyia kazi kwa vitendo.

BRELA YAWAPIGA MSASA WAFANYABIASHARA MKOA WA PWANI JINSI YA KUJISAJILI KWA MFUMO WA MTANDAO

0
0

Afisa Mfawidhi kutoka Brela kanda ya kusini ambaye ni mtaalamu wa mfumo wa usajili Francis Mwakalebela aliyesimama akitoa maelekezo kwa kwa njia ya vitendo washiriki wa mafunzo hayo kuhusina na namna ya kuweza kusajili makampuni ya na majina ya biashara kwa njia ya mtandao.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika zoezi la kujifunza jinsi ya kufanya usajili kwa kutumia mfumo wa mtandao
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani wakiwa wanaelekezana jinsi ya kuweza namna na kujisajili makampuni na majina ya biashra kwa kwa kutumia njia ya mtandao.
Wafanyabishara wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika mafunzo ya kujifunza namna ya kusajili makampuni na majina ya biashara kwa njia ya mtandao.
Afisa maendeleo ya jamii katika halmashauri ya mji Kibaha Lea Lwanji kushoto akiwa na mshiriki mwenzake wakiwa wanafuatilia kwa umakini mafunzo ya usajili kwa kutumia mfumo wa njia ya mtandao
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa wanaangalia jinsi ya mfumo wa kujisajili kwa njia ya mtandao unavyofanya kazi
Moja ya bango la Brela ambalo linaonyesha maelezo kuhusiana na mfumo wa kufanya usajili kwa kutumia mfumo wa mtandao.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
……………………
VICTOR MASANGU, PWANI 
BAADHI ya wafanyabiashara Mkoani Pwani ambao kwa kipindi cha muda mrefu waliokuwa wanakabiliwa na changamoto sugu ya kufanyiwa vitendo vya utapeli pindi wanapotaka kupatiwa usajili wa makampuni yao pamoja na majina ya biashara hatimaye wamepata ufumbuzi baada ya kupatiwa mafunzo maalumu kutoka Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) kwa lengo la kujifunza sheria na taratibu za usajili.

Wakizungumza katika ufunguzi rasmi wa mafunzo maalumu yaliyoandaliwa kwa umma juu ya kujifunza jinsi ya kutumia mfumo wa usajili wa makampuni na majina ya biashara baadhi ya wafanyabiashara hao akiwemo Abdala Ndauka na Elina Mgonja wamesema kwa miaka mingi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya upateli hivyo kujikuta wanaingia hasara kubwa katika zoezi zima la upatikanaji wa leseni.

Aidha wafanyabiashara hao wametoa pongezi kwa Brela kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa changamoto mbali mbali ambao ilikuwa zikiwakabili katika siku za nyuma katika kutekeleza majukumu yao hususan kuweza kutumia mfumo wa usajili wa kampuni na majina ya biashara zao.

“Kwa kweli sisi kama wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani tunatoa pongezi zetu za dhati kwa mamlaka husika ya Brela kwa kuona umuhimu ya kutupatia mafunzo hayo ya kujisajili kwa kutumia njia ya mtandao, maana hapo awali tulikuwa tunapata usiumbufu mkubwa na wakati mwingine kutapeliwa na baadhi ya watu hivyo kwa sasa tunaweza kutimiza majukumu yetu kwa weledi wa hali ya juu,”walisema wafanyabiashara hao.


Kwa upande wake mkurugenzi wa utawala na fedha kutoka Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA)Bakari Mketo alibainisha kwamba lengo la kuandaa mafunzo hayo kwa wafanyabiashara pamoja na umma kuhusina na kupata huduma za usajili kwa njia ya mtandao ikiwemo kuwajengea uwezo katika suala zima la ulipaji wa madeni kwa wateja wao ili kuondokana na usumbufu waliokuwa waliokuwa wanaupata.

“Lengo letu kubwa kwa sasa tunazunguka katika mikoa mbali mbali na kwa sasa tumeamua kuwakutanisha wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani ili tuweze kuwapa mafunzo maalumu ambayo yatawawezesha kuweza kujisajili kwa kutumia njia ya mtandao pamoja na kujifunza mambo mbali mbali ambayo yanahusiama ma utoaji wa leseni za viwanda,”alisema Mketo.

Pia alibainisha kwamba lengo lao kubwa ni kuweka mikakati kabambe ambayo iytaweza kuwasaidia wafanyabiashara kuondokana na changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikiwakabili katika utekelezaji wa majukumu yao,ili waweze kufanya usajili wa makampuni yao pamoja na majina ya biashara zao bila ya kuwepo na usumbufu wowote.

Naye Afisa biashara mkuu kutoka Wizara ya viwanda na bishara Jane Lyatuu aliwataka wafanyabishara wote nchini kuhakikisha wanazisajili biashara zao zote pamoja na makampuni,taasisi, viwanda kwa lengo la kuweza kuhimili ushindani uliopo katika soka la bara la afrika kwa kuzingatia ubora wa bidhaa zinazotengezwa nchini.

KATIKA mafunzo hayo yaliyokuwa ya siku mbili yalitolewa kwa umma juu ya kutumia mfumo wa usajili wa kampuni na majina ya biashra , pamoja na alma za bishara na utoaji wa leseni za viwanda yamewashirikisha wadau mbali mbali wa maendeleo, maafisa biashara, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, maafisa maendeleo, mkaguzi wa ndani pamoja na wanasheria.

Wadau PS3, GHSC TA – TZ, Waunga Mkono Juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano

0
0

Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA,Ofisi ya Rais TAMISEMI, Erick Kitali, akitoa mada wakati wa kikao hicho cha wadau juu ya uboreshaji wa Mfumo wa GoTHOMIS Ofisi za Wizara za Afya eneo la Mtumba mjini Dodoma. (Picha na Maktaba ya OR-TAMISEMI).
Kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Bakari Kambi, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula na Naibu Katibu Mkuu OR-TA,MISEMI (Afya), wakati wa kikao cha pamoja na Wadau wa Maendeleo kujadiliana namna yakuboresha Mfumo wa GoTHOMIS.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula akiongoza kikao cha pamoja baina ya Wizara ya TAMISEMI na Wizara ya Afya kilicho wakutanisha Wadau wa Maendeleo kujadili uboreshaji wa Mfumo wa GoTHOMIS ili uweze kutumika katika ngazi zote za kutolea huduma za Afya nchini (Picha na Maktaba ya TAMISEMI) 
…………………… 

Na Atley Kuni- TAMISEMI. 

Wadau wa Maendeleo nchini kupitia mradi wa Uimarishaji Mifumo katika Sekta za Umma (Public Sector Strengthening System-PS3) na (Global Supply Chain Technical Assistance Tanzania-GHSC TA – TZ), wameitikia wito wa serikali na kujitokeza katika kufanikisha zoezi la kuimarisha mfumo wa Uendeshaji wa Shughuli za Afya katika maeneo yote yakutolea huduma za Afya serikalini, ujulikanao (Government of Tanzania Health Operations Management Information System -GoTHOMIS). Wadau hao wameitika wito kufutia maelekezo ya Serikali kutaka mfumo huo uimarishwe kwa kuongezewa maeneo ya kiutendaji. 

Akizungumza na Wadau wa Maendeleo mwanzoni mwa Mwezi Mei, 2019 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, wakati wa kikao cha pamoja baina ya Wizara hiyo na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) alisema, umefika muda kwa wadau kuungana na kujenga mfumo wa GoTHOMIS kwani mfumo huo umeonesha kuwa na tija na ufanisi kwenye nyanja ya Afya. 

“Kwa Muda mrefu tumeshuhudia mifumo mbali mbali lakini yote hii ikiwa kwenye maeneo machache ya nchi ikifanywa kwa majaribio ambayo hata hivyo tija yake imekuwa sio yakuridhisha, alisema Chaula na kuongeza kuwa, suala lakutuambia unafanya shughuli ya Jamii halafu hatuoni tija ya unacho kifanya sio wakati wake kwa sasa, lazima wote tuungane na tukubali kutembea kwa pamoja na mfumo huu ambao umeonesha tija na ufanisi” alisema Dkt. Chaula. 

Wito wa Katibu Mkuu huyo, ulikuja wakati ambapo tayari mfumo ulikuwa umesimikwa kwenye maeneo yakutolea huduma za afya yapatayo 383 ikiwepo Zahanati 91, Vituo vya Afya 180, Hospitali Teule za Wilaya 12, Hospitali za Wilaya 77 na Hospitali za Rufaa za Mikoa 23 na kufanya asilimia 6 ya maeneo yote yakutolea huduma za afya nchini. 

Akiwasilisha mada katika kikao hicho juu ya uboreshaji wa mfumo wa GoTHOMIS, Mkurugenzi wa TEHAMA Ofisi ya Rais TAMISEMI, Erick Kitali, alisema shabaha iliyo mbele yao nikuimarisha mfumo kwa kutumia wataalam wazawa na wanaamini katika nguvu ya pamoja ikiwepo kushirikiana na wadau wa maendeleo wote. 

Akizungumza kando ya wataalam wanao endelea na kazi ya uimarishaji wa mfumo huo mkoani Morogoro, Mtaalam kutoka Global Supply Chain Tanzania, Alfredy Mchau, alisema wamewiwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha mfumo huo wa GoTHOMIS kwani ni moja ya vipaumbele vyao katika kushirikiana na serikali kuboresha huduma za Afya kwaajili ya upatikanaji wa taarifa sahihi na kwa wakati. 

“Alipotoa wito Katibu Mkuu, kwa wadau juu ya kuunga mkono suala hili, sisi kama Global Supply Chain Technical Assistance Tanzania (GHSC TA – TZ), tulielewa nini dhamira ya Serikali hii ya awamu ya tano inayo ongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, katika sekta ya Afya, ambayo kimsingi ndio msingi wa maendeleo ya nchi yoyote. 

Mchau aliongeza kuwa, GHSC TA – TZ ilikwisha anza harakati za uboreshai wa mfumo wa GoTHOMIS ili uweze kubadilishana taarifa na mfumo wa eLMIS ili kuboresha upatikanaji wa taarifa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi nchi nzima hivyo tunaamini kwa nguvu hii ya pamoja tutapiga hatua kubwa katika kuihudumia jamii, kwani Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu” alisisitiza Mchau. 

Kwa upande wake mmoja wa wafanyakazi kutoka mradi wa kuimarisha Mifumo ya Sekta za Umma nchini PS3 Mhandisi, Revocutus Mtesigwa, alisema huo ni muendelezo wa juhudi ambazo wamekuwa nazo hususan katika uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma nchini. 

“PS.3 Hii kwetu ni muendelezo wa shughuli ambayo tayari tulisha anza hapo awali, kwani tayari kuna maeneo yakutolea huduma za Afya yasiyo pungua 400 ikiwepo Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati tumewezesha kufungwa kwa mfumo na unafanyakazi, maeneo ambayo kama mradi tuliokwisha fanyia kazi ni eneo la Mafunzo kwa watumiaji, ufungaji Miundombinu ya Mtandao Kiambo (Local Area Network-LAN), hivyo Kauli ya Katibu Mkuu kwetu ilituongezea chachu na ari yakuendelea kushirikiana zaidi na Serikali lakini pia Wadau wengine wa Maendeleo katika kujenga nchi. 

Serikali bado inaendelea kuwakaribisha wadau wa maendeleo kujitokeza kwaajili yakufanikisha uboreshaji wa Mfumo wa GoTHOMIS, ambao utakuwa Madhubuti na wenye tija katika ngazi zote za kutolea huduma za Afya nchini. 

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA POLSI SABA SABA

0
0
Rais  mstaafu Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mrakibu wa Jeshi la Polisi, Simon wakachu alipotembelea banda la Jeshi hilo wakati kwenye maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Jk Nyerere barabara ya Kilwa
 Rais mstaafu Jakaya Kikwete akisaini kitabu alipotembelea banda la benki ya TIB kwenye maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam

MWALIMU WA MAGARI MAKUBWA VETA ABUNI TAA YA KUONGOZA MAGARI BILA TRAFIKI KUINGIA KATIKATI YA BARABARA

0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MWALIMU wa madereva wa magari makubwa kutoka Chuo cha VETA-Kihonda mkoani Morogoro William Munuo amesema amebuni taa ambayo haitakuwa na ulazima tena kwa trafiki kuingia katikati kuongoza magari.

Kwa mujibu wa Munuo lengo si kuwaondoa askari wa usalama barabarani bali wanachotaka ni kuwapusha na ajali wanazozipata kwa baadhi yao kwa kugongwa na magari wakati wakiongoza na wakati mwingine kusababisha kupoteza maisha.

Akizungumza na Michuzi TV kwenye banda la VETA katika Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam Munuo amesema taa hizo ambazo amebuni zitakwenda kusaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la foleni na kubwa zaidi kuokoa maisha ya trafiki.Akifafanua zaidi Munuo amesema madereva wawapo barabarani kwa sehemu kubwa wanatumia lugha ya alama ikiwemo michoro, taa na askari wa usalama barabarani.

Hata hivyo, baada ya kuona askari hulazimika kuingia kati kati ya barabara kuongoza magari kutokana na taa zilizopo sasa kuwa za automatiki ndio maana amebuni aina mpya ya taa ambayo itaongozwa na binadamu kulingana na wingi wa magari.

"VETA-Kihonda tumeamua kubuni taa ambazo ni tofauti na hizi ambazo tumezoea kuziona barabarani. Zilizopo sasa ni taa ambazo zimeshawekwa muda maalum na haubadiliki, hivyo hulazimisha wakati mwingine trafiki kuingia katikati ya barabara kuongoza magari.

"Changamoto iliyopo dereva anaweza kuona taa ya kijani na akadhani ameruhusiwa kumbe wakati huo kuna askari anangoza kwa mikono.Hivyo taa ambazo nimebuni trafiki hataingia tena barabarani bali ataseti taa kulingana na foleni iliyopo kwa wakati huo,"amesema Munuo.

Amesisitiza kupitia taa ambazo amebuni askari atakaa pembeni ya barabara na ataendelea kuongoza magari kama kawaida kwa kutumia taa hizo.

"Tunahitaji kumsaidia askari wetu asigongwe na gari.Wasikae juani , lakini pia hatutaki wawe wanavuta hewa yenye moshi wa magari.Ukweli taa ikogongwa na kuharibika itatengenezwa nyingine lakini askari akigongwa ni hasara kwa nchi,"amesema.

Ameongeza kuwa tayari ubunifu wa taa hiyo ya kuongoza magari umeshapelekwa COSTECH ili kuuthibitisha na baada ya hapo wanaweza kuwapa TEMESA ambao ndio wanahusika na kufunga taa za barabarani na kufafanua kwa sasa bado hazijaanza kutumika.

Alipoulizwa iwapo taa hizo zitawadhibiti madereva bodaboda ambao wengi hawajali taa za barabarani, amesema ni ngumu kuwadhibiti lakini amewashauri wafuate sheria za usalama ili kuepuka ajali ambazo zinaepukika.
 Mwalimu wa madereva wa magari MAKUBWA kutoka VETA-Kihonda mkoani  Morogoro William Munuo akielezea aina ya taa ambazo ameobi kwa ajili ya kuongeza.magari ambazo ni tofauti  na taa zilizopo sasa
Mwalimu wa madereva wa magari makubwa kutoka VETA -Kihonda mkoani Morogoro William Munuo akionesha taa ambazo amebuni (pembeni kulia) ambazo ni maalum kuongeza magari bila trafiki kuingia barabarani.

UWT Dodoma Mjini wampongeza Rais Magufuli, Watoa mafunzo kwa Wanawake

0
0

Charles James, Blogu ya Jamii

ZIARA ya Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini ya kutoa elimu kuhusu ujasiriamali kwa Wanawake imehitimishwa leo katika Kata za Mihuji, Makole na Uhuru.

Akizungumza katika mafunzo hayo ya ujasiriamali Katibu wa UWT, Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa amesema kupitia ziara hiyo ambayo iliwahusisha wataalamu kutoka SIDO na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake wameweza kunufaika na Elimu hiyo ya ujasiriamali.

" Tumekua na ziara kwa kata 41 za Jiji la Dodoma, kote huko tulizunguka na kuzungumzia na akina Mama kuhusu elimu ya kujitegemea na kujikwamua na umaskini.

" Tunampongeza na Kumshukuru Rais wetu Dk Magufuli, kwa kuondoa riba katika mikopo inayotolewa na Halmshauri za Wilaya Nchini kwa wanawake, vijana na walemavu lakini haswa tunamshukuru kwa kuwakumbuka walemavu ambao ni kundi lililokua limesahaulika katika suala zima la mikopo.

" Kuna fursa nyingi sana hivi sasa jijini Dodoma hasa baada ya Rais kuturasimisha kuwa Makao Makuu ya Nchi na Jiji, ni jukumu letu kama UWT kuandaa mafunzo na warsha mbalimbali za kuwakomboa Wanawake kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi," amesema Diana.

Amesema ziara hiyo imekua na mafanikio makubwa kwani imechangia idadi kubwa ya wanawake kujiunga katika vikundi vidogo vidogo ambavyo vitawasaidia kupata mikopo Jiji huku wengine wakienda SIDO kupata mafunzo kamili ya fani mbalimbali.

Kwa upande wake Afisa Uendelezaji Biashara SIDO, Crispin Kapinga amesema muamko wa Wanawake katika kujiunga na SIDO ili kupatiwa mafunzo mbalimbali umekuwa ni mkubwa baada ya ziara hiyo ya UWT.

" Hakika UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, wanastahili pongezi. Wamezunguka Kata zote kutoa elimu kwa akina Mama Na Vijana ili waweze kujiajiri fursa ni nyingi sana kwenye Jiji letu hivi sasa.

" Mfano kuna akina Mama ambao baada ya kupata mafunzo haya wamekuja pale SIDO kwenye ofisi zetu kufundishwa jinsi ya kutengeneza mifuko mbadala na sasa uchumi wao umekua mkubwa kutokana na uhitaji wa mifuko hiyo kwa saa, nitoe rai kwa Taasisi nyingine kuiga mfano huu wa UWT katika kutoa elimu kwa vijana na akina mama," amesema Kapinga.

Nae Hidaya Mizega ambaye ni Mratibu dawati la uwezeshaji Jiji la Dodoma, amewataka wanawake Wilayani humo kujitokeza kwa wingi katika kuchukua mikopo inayotolewa na Manispaa ya Jiji la Dodoma kwa Wanawake, Vijana na Walemavu.

"Tunapaswa kuwashukuru UWT Wilaya ya Dodoma kwa kuandaa mafunzo haya, ni ombi langu kwenu akina Mama kujihamasisha nyie wenyewe pamoja na watoto wenu kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili kuweza kupatiwa mikopo." Wanawake ndio uti wa mgongo wa Familia, hampaswi kuwa tegemezi, tuamke tuzikimbilie fursa lakini tusiamke peke yetu, tuwashike mikono na Vijana wetu waache kukaa vijiweni," amesema Hidaya.

Mmoja wa akina Mama waliohudhuria Mafunzo hayo, Amina Abdallah ameushukuru Uongozi wa UWT Wilaya ya Dodoma kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yamewafungulia njia katika kujikwamua kiuchumi.


JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA MKOA WA PWANI WATOA PONGEZI KWA BRELA

0
0

Na Mwandishi Wetu, Pwani

JUMUIYA ya Wafanyabiashara Mkoa wa Pwani imepongeza hatua ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni Brela(BRELA) kutoa mafunzo kuhusu usajili wa biashara zao kwa njia ya mtandao.

Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Abdalla Ndauka alisema leo mkoani hapa kuwa mafunzo yamewasaidia namna ya kujua kusajili majina ya biashara nembo za biashara jambo ambalo litawasaidia Katika kuzalisha na kudhibiti wezi wa Brand za biashara zao vilevile watafuata sheria za nchi kwa kuzingatia usajili huo.

Hata hivyo Ndauka amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni uhakika wa upatikanaji wa mtandao katika baadhi maeneo baadhi yao kutokujua matumizi ya kompyuta hivyo alishauri mafunzo yawe endelevu ili wote wanufaike na elimu iliyotolewa.

Kwa upande wake akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti katika mafunzo hayo wilayani Mkuranga na Kibaha Mkoani Pwani Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Bakari Mketto amesema mafunzo hayo yamewashirikisha wafanyabiashara, wanasheria, maafisa biashara pamoja na wajasiriamali wilayani Mkuranga na Kibaha Mkoani Pwani.

Katika kujua umuhimu wa matumizi ya mfumo huo kujisajili kwa njia ya mtandao kwakuwa sasa imerahisishwa ukilinganisha na ya zamani kwa njia ya makabrasha.Amesema mafunzo hayo yamelenga kurahisisha 

usajili na kuondoa changamoto zilizokuwepo ambapo mtu anaweza kujisajili popote alipo ambapo wanasheria maafisa biashara walionufaika na mafunzo hayo katika kila Halmashauri watawaelimisha wafanyabiashara wengine katika maeneo yao.Amesema wanasajili kampuni yenye mtaji kuanzia 20,000 hadi milioni moja ambapo makampuni 149,929 yamesajiliwa kabla ya mfumo na baada ya mfumo majina ya biashara 456,152.

Ametaja baadhi ya changamoto kwenye mfumo huo kuwa ni pamoja na kutokuwa rafiki na wafanyabiashara,uhitaji wa vitambulisho vya utaifa na mawasiliano kutokuwa mazuri.

""Wengi wa wafanyabiashara hawana vitambulisho vya Taifa inawawia vigumu kumudu mfumo huu licha ya mfumo kuongeza idadi kubwa ya usajili wa makampuni ukilinganisha na mfumo wa zamani kwa njia ya makabrasha,"amesema.

Mketto pia amewakumbusha wadau umuhimu wa kulipia mizania ya mwaka kwa upande wa makampuni na ada kwa upand we wa wafayabiashara kwani ni muhimu kwa kuwa baadhi hulimbikiza madeni mwisho wa siku inawawia vigumu kulipa kutokana na malimbikizo ya madeni.

"Mwisho wa siku inakuwa maumivu kwa taasisi sisi sio taasisi kazi yetu kutoa huduma kwa wadau lipieni mizania kwa wakati ukichelewesha unalimbikiza faini inaongezeka,"amesema Mketto.Kwa upande wa makampuni yaliyojisajili muda mrefu kwa dhumuni fulani Mketto aliyataka yakishindwa kujiendesha wasifunge biashara badala yake wajiridhishe kila mwaka wanalipia kwani ipo siku itawafaa katika biashara zao kuingia katika zabuni zenye ushindani Kwa vile kampuni zao zitakuwa hai.

Hata hivyo wafanyabiashara wa MKuranga wameelezea ugumu wa kusajili kupitia mfumo huo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mtandao ktk maeneo wanayoishi na upatikanaji wa vitambulisho vya taifa.Dk Judicate Ndosi Ndengerio alisema mafunzo yamepanua wigo wa uelewa kwa upande wao lakini changamoto zifanyiwe Kazi.

Kwa mujibu kwa kujibu wa Mketto ni kwamba mafunzo hayo yamefanyika mikoa yote kupitia kanda ikiwa ni pamoja nyanda za juu kusini,kati,kaskazini,magharibi na kumalizia mkoa wa Pwani zoezi ambalo ni Endelevu litafanyika mikoa yote ili kuwarahisishia wafanyabiashara kutembea umbali mrefu kufanya usajili wa makampuni ama leseni za viwanda.
 Meneja wa Utawala na Fedha Bw. Bakari Mketto akitoa somo kwa maafisa biashara wanasheria wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani katika mafunzo yaliyohusu Usajili wa Biashara na makampuni kwa njia ya mtandao ambayo Tanganyika mjini Kibaha katika ukumbi wa mikutano jengo la ofisi za mkuu wa Mkoa huo.
Baadhi ya wadau wakisikiliza kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na maofisa wa Brela hawapo pichani katika ukumbi WA mikutano jengo la ofisi za Mkuu wa Mkoa huo wilayani Kibaha mkoani Pwani.

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YANG'ARA MAONESHO YA SABASABA 2019

0
0

Na  Said Mwishehe,Michuzi Blog

WIZARA  ya mifugo na Uvuvi imeendelea kung'ara katika maonesho ya Biashara ya 43 Kimataifa ya Biashara 2019 kwa kunyakua tuzo ya Mifugo na Uvuvi

Akizungumzia ushindi huo Afisa Mifugo mkuu na Mratibu wa Maonesho Kitaifa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mary Yongolo amesema tuzo hiyo imechagiza uwajibikaji katika wizara na kuongeza Moroli ya kazi kwa wafanyakazi wote

Amesema kwa sasa wizara imesogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi na kuhakikisha kila mteja anahudumiwa kwa wakati katika mabanda ya sabasaba 

Afisa huyo amewataka wadau wa sekta ya Mifugo na uvuvi kufika katika mabanda hayo kupata huduma za haraka kwani maonesho hayo yamekuwa ni fursa kubwa kwa wakazi wa kanda ya mashariki mikoa ya Pwani na Morogoro hasa baada ya serikali kuhamia Dodoma

Aidha amewataka wananchi kutembelea Banda la wizara kuja kujifunza teknolojia mbalimbali za uongezaji thamani wa mazao ya nyama, maziwa na samaki na mbinu ambazo zitawasaidia katika kuboresha bidhaa zao katika masoko 

Ameongeza kuwa kutokana na umuhimu mkubwa katika wizara hiyo hivi karibuni wadau watakutana na Dawati la sekta binafsi katika maonesho hayo ambalo ni maalumu katika shughuli zao ikiwa ni pamoja na kuangalia changamoto zinazoikabili sekta pamoja na mikopo kwa wadau

Malengo ya serikali ni kuhakikisha wafugaji wanafuga kibiashara badala ya kufuga kimazoea, hivi karibuni serikali imeongeza kasi katika ujenzi wa viwanda vya nyama na samaki na endapo wadau hawa watawezeshwa basi sekta hii itakuwa kwa kasi kubwa kutokana na rasilimali zilizopo kwenye mifugo na uvuvi

Amekiri kuwa na changamoto katika soko la ndani ambapo amesema ubora wa masoko umekuwa mdogo lakini serikali ya Awamu ya tano inalifanyia kazi na hivi karibuni kutakuwa na masoko ya kiwango cha kimataifa hapa nchini 

Kwa upande wa watoa huduma wa nyama amewataka kuja kujifunza njia nzuri ya kuwahudumia wateja kwani awali Changamoto kubwa ilikuwa ni kukata nyama kwa kutumia magogo katika mabucha kitu ambacho kilikuwa si kizuri kwa afya kwa sababu kukatia nyama kwenye gogo kunafyonza  uchafu wa majimaji na mifupa midogo ambayo ni hatari kwa afya ya mlaji lakini mpaka hivi sasa wauzaji wa nyama wanatumia mashine za kisasa kukatia nyama kitu ambacho kinaongeza thamani ya bidhaa hiyo sokoni

Amesema  idadi kubwa ya ng'ombe millioni 30.5 kufikia mwaka 2020 lazima iongeze pato kwa serikali, hivi sasa wizara inaendelea na kazi kubwa ya utoaji elimu kwa wafugaji ambao wengi awali hawakuwa na mwamko wa elimu kitu ambacho kilidumaza soko la bidhaa ya mifugo na kutowasaidia wafugaji kujikwamua kiuchumi

Kwa upende wake Ofisa wa Utafiti wa wizara ya mifugo Neema Urasa amesisitiza umuhimu wa wafugaji kufika kujifunza mambo mbalimbali yaliyopo katika Maonesho hayo kwani wafugaji watakuja kujionea namna bora ya ufugaji wa kisasa.Amesema wafugaji wengi wanafuga kwa mazoea na ukiangalia bidhaa za mifugo zimekosa mvuto sokoni na kushuka kwa thamani ya bidhaa kama ngozi, kwato pamoja na nyama

Ameongeza  hivi sasa kila kitu kwa mifugo kina thamani, ametoa mfano wa damu, ngozi pamoja na nyama yenyewe.Pia siku za hivi karibuni wafugaji wameelewa umuhimu wa kulima nyasi za kisasa kwa ajili ya malisho ya wanyama kitu ambacho kitaongeza thamani ya zao la nyama sokoni

Amemaliza kwa kusema ni vema mifugo ikawa michache lakini yenye ubora sokoni kuliko kuwa na kundi kubwa la mifugo ambalo lina wanyama dhaifu.
 Waziri Mkuu Mstaafu, mhe.Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni cha Bodi ya Maziwa wakati akitembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo kwenye maonesho ya biashara ya Kimataifa ya 43 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl.Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
 Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi msaidizi (uvuvi) Bw.Antony Dadu kuhusu bidhaa zitokanazo na zao la mwani alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa ya 43 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl.Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu mstaafu, mhe. Mizengo Pinda, akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa Bodi ya Nyama Tanzania, Bw.Nicholai Chiweka wakati akitembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa ya 43 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl.Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ASIFU MAONESHO YA 43 YA SABABSABA JIJINI DAR

0
0

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa
Maafisa wa Kampuni ya uzalishaji wa mbegu bora za mazao ya Kilimo ya Seed Co.wakati wa ziara yake aliyoifanya leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Maafisa wa Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) wakati wa ziara yake aliyoifanya leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa
Wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wa ziara yake aliyoifanya leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa ziara yake aliyoifanya leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mmoja wa Maafisa wa Idara ya Sera na Machapisho wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa ziara aliyoifanya leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 


RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amezipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa maandalizi mazuri ya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere. 

Akizungumza leo Jumamosi (Julai 6, 2019) mara baada ya kutembelea na kukagua mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho hayo, Rais Mstaafu Kikwete alisema hizo ni dalili njema kwa maonesho hayo kwa kuwa yamekuwa bora zaidi ya maonesho yaliyofanyika mwaka jana. 

Aidha aliongeza kuwa maonesho ya mwaka huu, yameonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kujenga uchumi wake kupitia viwanda, kwa kuwa katika maonesho ya mwaka huu malighafi nyingi za kilimo zimepewa kipaumbele na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali. 

“Maonesho ya mwaka huu yamekuwa bora zaidi, kwani tumeshuhudia malighafi nyingi za kilimo zikipewa kipaumbele na hii imekuwa ni dalili njema na point (alama) tunayotakiwa kuifikia kwa sasa” alisema Kikwete. 

Awali akitembelea Banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rais Mstafu Kikwete alilitaka jeshi hilo kuwa wabunifu kwa kuzalisha bidhaa bora zitakazoweza kutumika nje ya Tanzania hususani bidhaa za ngozi ikiwemo viatu vinavyozalishwa na Jeshi hilo.

MAOFISA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI WAFAFANUA NAMNA MAMLAKA INAVYOFANYA KAZI

0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MAOFISA wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali waliopo kwenye Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Mwalim Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam wameendelea kutoa maelezo ya kina kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo.

Idadi ya wananchi wanaofika kwenye maonesho hayo wamekuwa wakienda katika banda la Mamlaka hiyo ambapo wengi wao wamekuwa wakitaka kufahamu zaidi kuhusu namna mtambo wa DNA unavyofanya kazi na wengine wakitaka kufahamu wanawezaje kutumia mamlaka hiyo katika shughuli zao za kila.

Akizunguza kwenye maonesho hayo ya biashara yanayoendelea katika viwanja hivyo Mkurugenzi wa Usimamizi, Udhibiti na Ubora wa Bidhaa Sabanitho Mtega ametumia nafasi hiyo kuelezea majukumu ya msingi yanayofanywa na mamlaka hiyo.

Ametaja baadhi ya majukumu hayo ni kufanya uchunguzi wa bidhaa mbalimbali kama vile vyakula, kufanya uchunguzi kwa ajili ya kusaidia vyombo vya ulinzi kufanya uchunguzi wa sampuli ambazo ni za makosa ya jinai kama vile dawa za kulevya, sampuli za sumu na aina nyingine za sampuli zote.

Pia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inadhamana ya kusimamia sheria namba tatu ya mwaka 2003 ambapo sheria hiyo pamoja na mambo mengine inasimamia utoaji wa vibali vya katika maeneo yote nchini ikiwemo kwenye viwanja vya ndege, mipakani na bandarini.

"Kwa kufanya hivyo inatuhakikishia kuwa Kemikali zote zinazoingizwa nchini hazileti madhara kwa mazingira na wakati huo huo kwa usalama wa nchi. Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ndio iliyopewa dhamana kupitia sheria namba 8 ya mwaka 2016 kuwa matokeo yanayotolewa na mamlaka hiyo ndio ya mwisho na hayabishaniwi.

Pia ni chombo cha serikali ambacho kazi yake ni kuhakikisha vyombo vya maamuzi vinatapa matokeo ya uchunguzi ili kufanya maamuzi sahihi. "Tunawakaribisha wananchi kwenye banda la mamlaka yetu ili wapate maelezo ya kina kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo.Pia kupata maelezo yatakayowasaidia kwenye maisha yao ya kila siku,"amesema.

Kuhusu uelewa , amesema kwa sasa wananchi wengi wanailewa mamlaka hiyo na wao wamekuwa wakitumia maonesho mbalimbali kutoa elimu kwa umma.Akizungumzia mtambo wa DNA amesema unafanya kazi nyingi zaidi ya kupima vinasaba vya kutambua uhalali wa mtoto na kwamba mtambo huo unatumika hata kupima sampuli za makosa ya jina, majanga ya moto, ndege, kubaini askari walipoata majanga.Pia kupima wanaohitaji kuwekewa figo ili kujua kama damu zao zinaendana.

Kwa upande wake Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Cletus Reuben Mnzava amesema wananchi wengi wanaofika kwenye banda lao kna mambo mengi wanapenda kufahamu.Baadhi ya mambo hayo ni kufahamu namna ambavyo maabara ya mkemia mkuu wa serikali inafanya kazi.Wengine wanataka kujua kuhusu mtambo wa DNA unatumika kupima sampuli za aina gani hasa ukiondoa kujua uhalali wa mtoto.

"Wapo baadhi ya wananchi ambao wanataka kufahamu kuhusu ubora wa bidhaa, pia wanaotaka kufahamu kuhusu usalama wa chakula na dawa ambazo wanazitumia."Wengine wanapenda kufahamu kuhusu uchunguzi wa sampuli ambazo zinafanywa na maabara ya mkemia mkuu.Kuna wajasiriamali ambao wao wakifika hapo wanataka kufahamu ni kwa namna gani maabara hiyo inaweza kutumika katika kuwafanya kuzalisha bidhaa zilizo bora.Wote wenye maswali tunawajibu na wanaridhika,"amesema Mnzava.
 Mkurugenzi wa Usimamizi, Udhibiti na Ubora wa Bidhaa Sabanitho Mtega pichani kushoto akizungumza na mmoja wa wadau waliofika kwenye banda la Mkemia Mkuu kuusu majukumu ya msingi yanayofanywa na mamlaka hiyo.Ametaja baadhi ya majukumu hayo ni kufanya uchunguzi wa bidhaa mbalimbali kama vile vyakula, kufanya uchunguzi kwa ajili ya kusaidia vyombo vya ulinzi kufanya uchunguzi wa sampuli ambazo ni za makosa ya jinai kama vile dawa za kulevya, sampuli za sumu na aina nyingine za sampuli zote.Picha na Michuzi Jr.
 Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Cletus Reuben Mnzava akizungumza na na baaadhi ya Wananchi waliofika kwenye banda hilo kufahamu mambo mbalimbali kuhusu mamlaka hiyo
  MAOFISA wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali waliopo kwenye Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Mwalim Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam wameendelea kutoa maelezo ya kina kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo. 
 Baadhi ya Wananchi wakiendelea kupata elimu na kufahamu mambo mbalimbali yahusuyo Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutoka kwa Mkurugenzi wa Usimamizi, Udhibiti na Ubora wa Bidhaa Sabanitho Mtega 
Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Cletus Reuben Mnzava akizungumza na na baaadhi ya Wananchi waliofika kwenye banda hilo kufahamu mambo mbalimbali kuhusu mamlaka hiyo.
 MAOFISA wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali waliopo kwenye Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Mwalim Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam wameendelea kutoa maelezo ya kina kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo.

WIZARA YA ARDHI YAELEZEA NAMNA LESENI YA MAKAZI INAVYOPATIKANA

0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inatumia Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea Dar es Salaam kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala yanayohusu ardhi na kubwa namna leseni za makazi .

Akizungumza na Michuzi TV kwenye maonesho ya biashara ya 43 ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam Ofisa Ardhi wa Wizara hiyo David Malisa amefafanua leseni za makazi ni nyaraka inayotolewa kwa mmiliki wa ardhi katika eneo ambalo halijapangwa wala kupimwa.

Amesema na sifa kubwa ya kutolewa leseni hiyo ni kwamba eneo hilo linatakiwa liwe limeendelezwa kiasi cha kuwa na msongamano mkubwa ambao hata uwekaji miundombinu muhimu kama barabara , mabwaya ya maji taka kutowezekana kuwekwa.

Malisa amesema pia leseni hiyo inaweza kutolewa katika maeneo ambayo Serikali ina mipango mingine baadae na kutoa mfano kuwa huenda kwa baadae Serikali inataka kufanya mradi mkubwa wa bandari au kujenga mradi mkubwa kama ule wa umeme wa mto Rufiji.

"Hivyo maeneo kama hayo wananchi wanaweza kupewa leseni ya makazi kwa kukaa nayo kwa mufa mfupi wakati wanasubiri kupisha mradi husika kulingana na uamuzi wa Serikali.

"Na kwamba leseni hiyo inatolewa kwa miaka mitano na ni nyaraka tu ya kumtambua mwananchi kwamba yeye ndio mwenye haki katika eneo hilo,"amesema.Hata hivyo Malisa amesema katika maonesho hayo wananchi wengi wamekuwa na maswali lakini yanachanganya urasimishaji wa makazi ambao ni mpango mkubwa wa Wizara unaoendelea nchini na mpango wa kutambua na kusajili kila kipande cha ardhi na kutoa leseni ya makazi.

"Nifafanua leseni ya makazi inatolewa katika eneo ambalo halijapangwa na wala halijapimwa na unaweza kushiriki kwenye mradi huo ambao unatekelezwa kwa Dar es Salaam wa kutambua na kusajili kila kipande cha ardhi lakini vile vile ukawa upo kwenye mpango wa urasimishaji,"amesema.

Ameogeza kuwa urasimishaji ni mchakato unaoendeshwa na kampuni binafsi kwa niaba ya Serikali na inafanya kazi kwenye mitaa ambayo inawezekana kupangwa kwa jinsi wananchi walivyoedeleza na kupimwa na kumiliki.Kampuni zinazofanya kazi hiyo zinatambuliwa na mamlaka husika.

Hata hivyo wananchi ambao wamefika kwenye banda la wizara hiyo kwa sehemu kubwa wamekuwa wakipata ufumbuzi wa changamoto ambazo zinawakabili katika ardhi.Na wengine wamekuwa wapewa maelezo ya kufika kwenye ofisi za Serikali kwa ngazi zinazohusika na masuala ya ardhi ambako ndiko changamoto zao zinaweza kupata utatuzi sahihi.
  Ofisa Ardhi wa Wizara hiyo David Malisa akifafanua  jambo kwa baadhi ya ya wananchi waliotembelea banda hilo katika maonesho ya sabasaba kuhusu leseni za makazi zinavyotolewa kwa mmiliki wa ardhi katika eneo ambalo halijapangwa wala kupimwa. 
 Mmoja wa maofisa wa Ardhi akiwaelimisha baadhi ya wananchi umuhimu wa kupata hati

SGR TANZANIA 2019 - JARIBIO LA TRENI YA UHANDISI KUPITA JUU YA RELI

VOA Swahili: Zulia Jekundu Episode 231

PROFESA KABUDI AKUTANA NA MICHUZI TV CREW UWANJA WA SABASABA

0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi ametembelea Maonesho ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam. Katika pita pita zake akakutana na Crew nzima ya Michuzi TV ambayo imefunga kambi uwanjani hapo kurekodi na kutangaza kinachoendelea. Walipomuomba kupata naye picha ya pamoja Profesa Kabudi hakusita.


WAZIRI MBARAWA AKABIDHI UJENZI MRADI WA MAJI MWAUWASA BAADA YA MKANDARASI KUSHINDWA KUKAMILISHA KWA WAKATI

0
0

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amekabidhi ujenzi wa mradi wa maji wa Shilima Wilayani Kwimba kwa Mamlaka ya Maji Mwanza (MWAUWASA) baada ya Mkandarasi Kampuni ya Palemon Construction Ltd ya Mwanza kushindwa kukamilisha kwa wakati.

Makabidhiano hayo yalifanyika Julai 3, 2019 katika Kijiji cha Shilima na kushuhudiwa na watendaji mbalimbali wa Serikali na mamia ya wananchi wa Shilima na maeneo ya vijiji vya jirani.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mradi, Waziri Mbarawa alieleza kwamba ujenzi wake ulianza tangu mwaka 2013 na kwamba ulipaswa kukamilika ndani ya miezi sita lakini hadi sasa mradi huo haujakamilika.

Alisema Serikali iliamua kusitisha mkataba na Mkandarasi ambaye alishindwa kutekeleza ujenzi wa mradi kama ilivyo kwenye makubaliano.

Mara baada ya kuukabidhi mradi huo, Profesa Mbarawa aliiagiza MWAUWASA kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya Siku 60 ili kuwaondolea mateso ya muda mrefu wanachi wa maeneo hayo hasa ikizingatiwa kwamba mradi ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2013.

“Tunataka wataalam hawa wafanye kazi usiku na mchana na baada ya miezi miwili wananchi wapate maji safi na salama, uwezo tunao, tunaweza kumaliza tatizo la maji hapa kwa muda mfupi sana,” alisema Profesa Mbarawa.

Aliongeza kuwa kuna miradi ipatayo 88 kote nchini ambayo ujenzi wake ulianza kati ya Mwaka 2010 hadi 2015 ambayo ilipaswa kuwa imekwisha kamilika lakini hadi hivi sasa bado inasuasua na huku akiutolea mfano mradi huo wa Shilima.Alibainisha kwamba Serikali kupitia Wizara ya Maji imeamua kuwa na utaratibu mpya wa kuzikabidhi Mamlaka za Maji miradi ambayo ujenzi wake una changamoto inayosababisha isikamilike kwa wakati.

“Tumeamua kubadilisha utendaji wa Sekta ya Maji, kila mahala tatizo ni maji, hili halikubaliki, tumejipanga na tunadhamira ya dhati kuhakikisha kero hii inakuwa historia kote nchini,” alisema Waziri Mbarawa.

Kuhusu utaratibu huo mpya, Profesa Mbarawa alibainisha kuwa ni wa nchi nzima na kwamba wakandarasi wanaoshindwa kutekeleza miradi waliyokabidhiwa kwa wakati hawatovumiliwa na watanyanganywa na itakabidhiwa kwa Mamlaka za maji kwenye maeneo husika.“Tumeamua miradi yote yenye changamoto tutaisimamia wenyewe na tutahakikisha inafanya kazi. Wananchi wamechoka kuendelea kuisubiri miradi hii ikamilke, fedha nyingi zinapotea, Serikali haitokubaliana na Mkandarasi anaechelewesha ujenzi wa mradi tayari tumefanya hivi Rungwe na sasa tumefanya hapa Shilima,” alisema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga alisema wamepokea agizo hilo la kutekeleza mradi huo ambao umesuasua kwa kipindi kirefu na kwamba wataukamilisha kwa wakati kama ilivyoagizwa.

“Tunaahidi hadi kufikia Septemba 3, 2019 tutakuwa tumeukamilisha mradi kwani itakuwa tayari ni Siku 60 na wananchi wataanza kupata majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria,” alisema Mhandisi Sanga.

Aidha, kwa mujibu wa Mhandisi wa Maji, Wakala wa Maji Vijijini Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Boaz Pius ni kwamba mradi huo utakapokamilika utahudumia wakazi 16,675 kutoka vijiji vinne ambavyo ni Shilima chenye wakazi 7,526, Mhande chenye wakazi 1,967, Kasang’wa wakazi 2,730 na Kijiji cha Izizimba “A” chenye wakazi wapatao 4,452.

Mhandisi Boas aliongeza kwamba kukamilika kwa mradi huo pia kutaweza kuhudumia vijiji vya Sangu, Gurumwa, Mwalubungwe na Kikubiji, ambapo bomba kuu linapita.
 Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amekabidhi ujenzi wa mradi wa maji wa Shilima Wilayani Kwimba kwa Mamlaka ya Maji Mwanza (MWAUWASA) baada ya Mkandarasi Kampuni ya Palemon Construction Ltd ya Mwanza kushindwa kukamilisha kwa wakati.

MATOKEA YANAYOTOLEWA NA MKEMIA MKUU WA SERIKALI NI YA MWISHO NA HAYABISHANIWI-GCLA

WIZARA YA ARDHI YAELEZEA NAMNA LESENI YA MAKAZI INAVYOPATIKANA

0
0

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inatumia Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea Dar es Salaam kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala yanayohusu ardhi na kubwa namna leseni za makazi .

Akizungumza na Michuzi TV kwenye maonesho ya biashara ya 43 ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam Ofisa Ardhi wa Wizara hiyo David Malisa amefafanua leseni za makazi ni nyaraka inayotolewa kwa mmiliki wa ardhi katika eneo ambalo halijapangwa wala kupimwa.

Amesema na sifa kubwa ya kutolewa leseni hiyo ni kwamba eneo hilo linatakiwa liwe limeendelezwa kiasi cha kuwa na msongamano mkubwa ambao hata uwekaji miundombinu muhimu kama barabara , mabwaya ya maji taka kutowezekana kuwekwa.

Malisa amesema pia leseni hiyo inaweza kutolewa katika maeneo ambayo Serikali ina mipango mingine baadae na kutoa mfano kuwa huenda kwa baadae Serikali inataka kufanya mradi mkubwa wa bandari au kujenga mradi mkubwa kama ule wa umeme wa mto Rufiji.

"Hivyo maeneo kama hayo wananchi wanaweza kupewa leseni ya makazi kwa kukaa nayo kwa mufa mfupi wakati wanasubiri kupisha mradi husika kulingana na uamuzi wa Serikali.

"Na kwamba leseni hiyo inatolewa kwa miaka mitano na ni nyaraka tu ya kumtambua mwananchi kwamba yeye ndio mwenye haki katika eneo hilo,"amesema.

Hata hivyo Malisa amesema katika maonesho hayo wananchi wengi wamekuwa na maswali lakini yanachanganya urasimishaji wa makazi ambao ni mpango mkubwa wa Wizara unaoendelea nchini na mpango wa kutambua na kusajili kila kipande cha ardhi na kutoa leseni ya makazi.

"Nifafanua leseni ya makazi inatolewa katika eneo ambalo halijapangwa na wala halijapimwa na unaweza kushiriki kwenye mradi huo ambao unatekelezwa kwa Dar es Salaam wa kutambua na kusajili kila kipande cha ardhi lakini vile vile ukawa upo kwenye mpango wa urasimishaji,"amesema.

Ameogeza kuwa urasimishaji ni mchakato unaoendeshwa na kampuni binafsi kwa niaba ya Serikali na inafanya kazi kwenye mitaa ambayo inawezekana kupangwa kwa jinsi wananchi walivyoedeleza na kupimwa na kumiliki.Kampuni zinazofanya kazi hiyo zinatambuliwa na mamlaka husika.

Hata hivyo wananchi ambao wamefika kwenye banda la wizara hiyo kwa sehemu kubwa wamekuwa wakipata ufumbuzi wa changamoto ambazo zinawakabili katika ardhi.

Na wengine wamekuwa wapewa maelezo ya kufika kwenye ofisi za Serikali kwa ngazi zinazohusika na masuala ya ardhi ambako ndiko changamoto zao zinaweza kupata utatuzi sahihi.
 Ofisa Ardhi wa Wizara ya Ardhi,David Malisa akifafanua kwa Wananchi kuhusu leseni za makazi,kwenye banda lao ndani ya maonesho ya biashara ya 43 ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam,alisema kuwa Leseni za makazi ni nyaraka inayotolewa kwa mmiliki wa ardhi katika eneo ambalo halijapangwa wala kupimwa.Picha na Michuzi Jr.
 Mmoja wa Maofisa kutoka Wiara ya Ardhi akifafanua mambo mbalimbali kuhusu masuala ya Ardhi na kusikiliza baadhi ya Changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo wakati wa ufuatiliazi wa nyaraka zao za Ardhi,kwenye ya maonesho ya biashara ya 43 ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam 
 Pichani juu na chini baadhi ya Wananchi wakimsikiliza  Ofisa Ardhi wa Wizara ya Ardhi,David Malisa alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali yahusuyo Ardhi na mifumo mipya inayotumika katika kupata Ardhi na hatua zake. 

ASKOFU MALEKANA ATEMEBELEA BANDA LA BUNGE

0
0


Afisa wa Bunge Ndg. Omary Machunda (Kulia) akimpa Elimu kuhusu Shughuli zinazofanywa na Mhimili wa Bunge Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Askofu Mark Malekana alipotembelea banda la Bunge katika Maonyesho ya 43 ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam hii leo. ( Picha na Ofisi ya Bunge)

JE WAJUA.? LESENI YA MAKAZI INATOLEWAJE WIZARA YA ARDHI

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images