Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

MBUNGE SEGEREA AIPA KONGOLE DAWASA

$
0
0
Na Zainab Nyamka na Cuthbert Kajuna, Michuzi Blog

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonna Kamoli amewapongeza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA kwa huduma nzuri wanayoitoa ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Ameyasema hayo alipotembelea banda la DAWASA ndani ya maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es salaam.

Bonna ameipongeza DAWASA kwa kuweza kupeleka huduma ya majisafi kwenye maeneo mengi hususani kwenye yale ambayo hayakuwa na mtandao wa maji kwani katika uchaguzi wa mwaka 2015 ilikuwa ni moja ya ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kufikisha maji kwenye maeneo yote nchini.

Amesema, Dawasa wamejitahidi kufikisha maji ndani ya Jimbo la Segerea ingawa changamoto sehemu nyingine maji bado hayapatikani.

Ameeleza, jitihada kubwa zilizofanywa na Dawasa ni kubadili miundo mbinu ya maji iliyokuwa chakavu na kufanikisha kupatikana kwa maji ndani ya Jimbo la Segerea na viunga vyake.

Mbali na hilo, Bonna ameutaka uongozi wa Dawasa kutoa elimu kwa wananchi namna ya matumizi ya maji hususani kwa wadada wa kazi au watoto wanaowaacha majumbani pia kujaribu kuweka matanki ya maji ili kufahamu matumizi halisi ya maji.

Mhandisi wa Uendeshaji na Matengenezo Mkoa wa Tabata DAWASA Mhandisi Gibson Baragula amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Segerea kwa kuona kazi inayofanywa ya kupeleka maji sehemu zote za Mkoa wa Dar es salaam.

Amesema kwa sasa wanatoa maji kutoka bomba la Kimara kwenda hadi Bonyokwa na matarajio ni kuwa na wateja 3000 ila tayari wameshawaunganishia wateja 1400 na wateja 300 wameshafanya maombi ya maunganisho mapya na hivi karibuni wataanza kuwaunganishia.

Dawasa wanaendelea kutoa huduma kwa wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam katika banda lao ndani ya maonesho ya ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es salaam.
 Mbunge wa Jimbo la Segerea (CCM)  Bonna Kamoli akipata maelezo kutoka kwa Afisa Huduma kwa kwa wateja  alipotembelea  banda la Dawasa kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea na kupongeza juhudi za Mamlaka za kusambaza huduma ya Maji kwenye maeneo mbalimbali Jimboni kwake. 
 Mbunge wa Jimbo la Segerea (CCM) Mhe Bonna Kamoli akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea banda la Dawasa kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea na kupongeza juhudi za Mamlaka za kusambaza huduma ya Maji kwenye maeneo mbalimbali Jimboni kwake. 
Mbunge wa Jimbo la Segerea (CCM) Mheshimiwa Bonna Kamoli akipata maelezo kutoka kwa Afisa Huduma kwa kwa wateja  alipotembelea  banda la Dawasa kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea na kupongeza juhudi za Mamlaka za kusambaza huduma ya Maji kwenye maeneo mbalimbali Jimboni kwake. 


WATUMISHI HOUSING YAWAHAMASISHA WATUMISHI WOTE WA SERIKALI KUNUNUA NYUMBA ZA SHIRIKA HILO AMBAZO BEI YAKE NI NAFUU

$
0
0

MENEJA Masoko na Mauzo kutoka Watumishi Housing ambao wanajishughlisha na uuzaji wa nyumba za bei nafuu Raphael Mwabuponde amewataka watumishi wote wa Serikali  kununua nyumba kutoka shirika hilo  la Watumishi Housing.

Amesema mtumishi wa serikali anapokosa nyumba ya kuishi ni aibu kubwa kwani kuna nyumba za bei  nafuu kutoka shirika hilo.

Akizungumza katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea viwanja vya Saba saba  jijini Dar es Salaam ,Meneja huyo amesema shirika hilo lina nyumba katika mikoa mingi  hapa nchini, hivyo watumishi wanatakiwa kuchangamkia fursa  hizo ili kuondokana na changamoto  za upangaji.

"Kila mfanyakazi amepanga nyumba huku akisahau kuwa fedha hiyo  anayolipa  kwenye upangaji anao uwezo wa kupata nyumba kutoka Watumishi Housing kwani tuna mpango  unaoitwa  mpangaji mnunuzi na malipo yake utokana na  kipato cha mtumishi huyo,"amesema  Mwabuponde

Aidha  ameongeza ili mtumishi wa umma uweze  kuheshimika ni lazima uwe unamiliki nyumba.

Kwa upande  Juma  Ally ambaye ni mtumishi wa Serikali  ameipongeza Watumishi Housing kwa jinsi inavyopambana kutoa misaada wa uelewa kwa watumishi katika umiliki wa nyumba Kwa watumishi wake.

Amesema kuwa jambo hilo ni njema kwani  watumishi wanapomilikishwa nyumba kwa malipo ya bei  nafuu na masharti ya kawaida, hivyo amewataka wananchi  wengine  kuchangamkia fursa  hizo na si  kutegemea pesa za kustaafu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Wakati huo huo  Ofisa Uhusiano wa Watumishi Housing Meryjane Makawia amewataka pia wananchi  wote kutembelea mahali pa miradi hiyo  ilipo ili kujionea nyumba za kipee kutoka watumishi housing kwani ni za mfano na za kipekee  na wala  hazijawai kutokea  hapa nchini.

"Siku zote katika maisha hakuna baba mwenye gari bali kuna baba mwenye nyumba hivyo  ni bora watumishi wakakimbilia kununua nyumba na si  magari,"amesema .

Aidha  amewataka vijana na wananawake  kujitokeza kwa wingi  ili kujinyakulia nyumba za bei  nafuu na zisizo na masharti.
 Afisa Uhusiano na Masoko Watumishi Housing,Maryjane Makawia   akizungumza  leo jiji Dar as Salaam na  Michuzi TV kuhusu  wananchi  wote kutembelea mahali pa miradi ya nyumba  ilipo mikoa mbalimbali ili kujionea nyumba za kipee leo  kwenye Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
 Mfanyakazi Watumishi Housing Hellen Mwaihojo(kulia)kiwaelekeza wananchi namna kupata nyumba leo katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa katika banda la Watumishi Housing katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

WATANZANIA WAPATA MUAKO ZAIDI WA KUJIUNGA KATIKA CHUO CHA UALIMU VETA- MOROGORO

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi TV 

CHUO cha Ualimu wa  Ufundi Stadi Morogoro VETA kimesema kwa sasa Watanzania wamekuwa na muako mkubwa wa kujiunga na chuo hichohuku akifafanua ili kuwa na Tanzania ya viwanda lazima waandaliwe walimu mahiri watakaofundisha vijana mahiri kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Hayo yamesemwa na Mkufunzi kutoka Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro Mhandisi Enelisa Andengulile wakati anazungumza na Michuzi TV kwenye banda la VETA lililopo kwenye maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amefafanua kuwa  chuo hicho ni pekee nchini Tanzania ambacho kinatoa kozi za ualimu wa ufundi stadi ambapo wanapokea wanafunzi wa kada mbalimbali na kisha kuwaandaa kuwa walimu mahiri ambao watakwenda kufundisha vyuo vya ufundi stadi katika maeneo yote nchini.

"Muamko kwa Watanzanani kwa sasa  ni mkubwa kwani zamani tulikuwa tunatafuta wanafunzi na kwamba hata ilikuwa hadi inafika  Aprili hakuna kabisa wanafunzi wa kujiunga na chuo chetu.Lakini leo hii wanafunzi wengi sana wanajiunga na ukweli uwepo wa sekondari za kata umeongeza sana muamko.

 " Tunaweza kutangaza uhitaji wa wanafunzi 200 lakini wanaokuja kuomba kujiunga wanafika kuanzia 1000 au 2000 kutokana na muamko kuongezeka na jamii inaelewa kuwa ufundi ni ajira,"amesema Mhandisi Andengulile.

Ameongeza kuwa siku zote VETA wamekuwa wakitangaza kuwa Tanzania inaingia kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda ,hivyo ili kufika huko lazima wawepo walimu mahiri wa kufundisha watanzania katika fani mbalimbali.

Hivyo amefafanua chuo chao kinatoa mafunzo ya ualimu wa ufundi stadi mahiri ambao nao watakwenda kufundisha vijana mahiri ambao watakwenda kufanya kazi katika viwanda.

Kuhusu fani gani muhimu ambazo Watanzania wanaweza kusoma,Mhandisi Andengulile amesema VETA wanafundisha fani zote kwani ni muhimu na kutoa mfano wanafundisha watu kupika maana viwandani watu wnahitaji kula, wanafundisha mashono maana viwandani kunahitajika maovaroli na nguo nyingine za kazi.

"Kila fani kwetu ni muhimu kikubwa mhusika anatakuwa mwalimu wa fani gani.Lazima tufundishe kila aina ya utalaamu na tunafahamu kuwa hakuna fani ambayo ni zaidi ya nyingine.Hivyo wale ambao wanahitaji umeme watafundishwa kuhusu umeme na tunafahamu mitambo mingi inaendeshwa kwa umeme," amesema.

Akizungumzia aina ya wanafunzi wanaowachukua kujiunga na chuo hicho cha ualimu , Mhandisi Andungulile amesema wapo ambao wamemaliza kidato cha nne lakini ni mafundi tayari aidha wana grade ya tatu au wana grade ya kwanza ambao hao wanapewa ualimu wa ufundi stadi ngazi ya cheti kwa muda wa.miaka miwili.

Pia amesema wapo pia waliosoma vyuo vya kati vya ufundi kama DIT, Arusha Tech ,Mbeya Tech na vyuo vingine ambavyo vinafafana na hivyo anbapo hao wanapata diploma ya ualimu wa ufundi stadi na kuongeza kwa mwaka huu wameingia makubaliabaliano na Open Univesirty ambapo watatoa  Post graduate  ya Diploma kwa wanafunzi wote ambao wamesoma Digrii ya Uinjia na hao watafundishwa ualimu kwa njia ya mtandao.
 Mkufunzi wa Chuo Cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro -VETA Mhandisi Anelisa Andungulile akizungumza kuhusu chuo hicho kwenye maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam
Mhandisi Anelisa Andungulile ambaye ni Mkufunzi kutoka Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro akifafanua jambo

Vodacom kuwasajili wananchi kwa alama za vidole viwanja vya Sabasaba

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi, Vodacom, imewaomba wateja wanaotumia mtandao huo wanapoenda kujisajili kwa alama za vidole, ni wafike wakiwa na vitambulivyo ambayo vina majina yanayofanana na yale  ya kwenye  kitammbulisho cha Nida.

Meneja Uhusiano wa kamapuni hiyo ya simu, Alex Batekeye amesema hayo leo kwenye maonyesho ya 43 ya biashara  yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema, wamekuwa wakikutana na changamoto  katika zoezi hilo la usajili kwa watu kufika kujisajili wakiwa na vitambulivyo ambayo vina majina tofauti, yaani kitambulisho na jina alilojisajilia kwenye simu yanakuwa hayafanani na jin lililopo kwenye kitambulisho cha Taifa.
"Tunawaomba wananchi waje na vitambulisho stahiki yaani jina alilojisajilia kwenye simu ndio jina hilo hilo liwe  kwenye usajili wa kitambulisho cha Taifa" amesema

Aidha amewataka wateja wao kuendelea kujitokeza kwa wingi katika banda lao hilo kwani mpaka sasa kuna madawati zaidi ya matano katika kufanya shughuli hiyo ya usajili kwa haraka zaidi, bila ya kuwaweka watu foleni.

Pia katika  kuwaonyesha watanzania jinsi nchi yetu inavyoenda na maisha ya kidigitali na kuipeleka Tanzania kidigitali zaidi kampuni hiyo pia imeandaa dawati Unstance school yaani shule papo hapo na kuwataka wazazi wenye watoto wafike kwenye banda hilo ambapo wakifika hapo kuna sehemu dawati hilo lipo watajisajaili na kisha  wataweza kutuma maswali na kupata majibu ya maswali yao hapo hapo kutokana na darasa ambalo mtoto anasoma.

Amesema, katika kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wengi na kuwa mkombozi wa elimu basi unaweza kujisajili hata ukiwa nyumbani kwa kutimia tovuti yao.
 Meneja uhusiano wa kampuni ya simu. Ya Vodacom, Alex Batekeye akizungumza na wanahabari  katika maonyesho ya 43 ya biashara, namna wateja wao wanavyoendelea kujisajili kwa alama za vidole.
Wananchi waliofika katika banda la Vodacom, wakipata maelezo ya jinsi ya kujiunga na na mtandao wa shule papo hapo

WAFANYAKAZI WAOMBWA KUTEMBELEA BANDA WCF SABASABA ILI KUPATA ELIMU NA KUJUA HAKI ZA MFANYAKAZI NA MWAJIRI

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma na Tathimini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF),Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam amesema mfanyakazi aliyeumia kutokana na kazi aifanyayo au maradhi yaliyosababishwa na kazi ifanyayo.
Mfuko utagharimia matibabu kwa ujumla baada ya kufanyiwa tathmini na madaktari ambao tayari wamepatiwa mafunzo ya namna ya kufanya tathmini kwa Mfanyakazi aliyeumia au kupata maradhi kutokana na kazi anayoifanya.
Naye Mkuu wa kitengo cha Mahusiano kwa Umma wa (WCF),Bi. Laura Kunenge, aliwahimiza waajiri na wafanyakazi kutembelea banda hilo ili kupata elimu lakini pia kujua haki za mfanyakazi na mwajiri.
“Mfulo huu unatoa nafuu sio tu unasaidia Mfanyakazi kulipwa Fidia Stahili bali pia unatoa nafuu kwa mwajiri kwani ghara hizo zitasimamiwa na WCF na sio Mwajiri. “Ndio maana tunawahizimiza waajiri kote nchini kutoka sekta binafsi na umma, kutoa michango ya kila mwezi kama sheria inavyotaka.”Amesema Bi. Laura.

 Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar,(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya kupatiwa Fidia na WCF katika  banda la mfuko huo  kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa leo Dar es Salaam 2019, barabara ya Kilwa.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

  Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano kwa Umma wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD),Bi. Laura Kunenge akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewaomba  wananchi wafike katika banda la mfuko huo ili kujua haki za mfanyakazi na mwajiri kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya barabara ya Kilwa Dar es Salaam 2019.

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgencealie (wapili kulia) akiwapatia maelezo waandishi wa habari (kushoto) kuhusu shughuli zifanywazo na WCF.


Watumishi wa WCF (kulia) wakiwahudumia mwananchi waliofika kwenye kwenye banda            hilo kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya barabara ya Kilwa Dar es Salaam2019.

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda atumia masaa matano kutembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho 43 ya Biashara

$
0
0

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda  ametumia masaa matano kutembelea mabanda mbali mbali kwenye  maonesho  43  ya kimataifa ya biashara yanayofanyika Jijini Dar es salaam.

Baada ya kutembelea mabanda hayo, Pinda amesema hawezi kufananisha Maonesho hayo na mengine mengi yaliopita kwani amebaini mengi katika maonyesho haya ikiwemo wafanyabiashara walioshiriki wamekua kibiashara, vifungashio vimeboreshwa, bidhaa na pia kuna mpangilio mzuri wa vitu.

Aidha amezisisitiza Mamlaka husika zinazosimamia  na kudhibiti bidhaa na vyakula ikiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Viwango Nchini (TBS) kutokubweteka badala yake ziendelee kusimamia zaidi ili waweze kushindana kimataifa.

"Biashara katika Maonesho haya   zimeboreshwa lakini pamoja na mafanikio haya Mamlaka zinazohusika na Udhibiti zisibweteke zikazane kusimamia zaidi ili tuweze kufika katika soko la ushindani la kimataifa"alisema Pinda

Ameongeza kuwa, kati ya vitu vingine alivyovibaini katika Maonesho haya kuwepo kwa mwitikio mkubwa wa bidhaa za asali .

Pinda amesema katika Maonesho yaliyopita Asali ilikuwa miongoni mwa bidhaa ambazo zilikuwa adimu lakini sasa nimefurahi kuona zao la Asali limeonekana kuwa maarufu katika maonesho haya,nimekutana na watu wengi wanaouza zao hili.tuomba watu wajiwekeze zaidi.

Aidha ametoa wito kwa Wananchi ambao awajafika katika Maonesho haya kujitokeza kwa wingi kuja kuona Mambo mbalimbali ikiwemo vilivyomo 

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI KUFANYIKA 31 JULAI, 2019

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Singida Mashariki baada ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kuitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Mahakama ya Rufaa) Semistocles Kaijage alisema kuwa alitoa ratiba ya Uchaguzi huu Mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kutokana na barua ya Spika wa Bunge inayoeleza kuwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu kapoteza sifa ya kuwa Mbunge kutokana na kushindwa kuwasilisha kwa Spika tamko la mali na madeni na kushindwa kuhudhuria mikutano saba (7) mfululizo ya Bunge bila ruhusa ya Spika.

Mwenyekiti wa Tume, Kaijage, alizingati  matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, kutoa taarifa kwa Umma kuhusu uwepo wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki.

Jaji Kaijage kwa kuzingatia Katiba ya nchi na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi alifafanua ratiba ya Uchaguzi Mdogo huu kwa kueleza kuwa, Fomu za Uteuzi wa Wagombea zitatolewa kati ya  tarehe  13 hadi 18 Julai mwaka huu, Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe  18, Julai mwaka huu na Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 19 hadi tarehe 30 Julai 2019 na Siku ya Uchaguzi itakuwa ni tarehe 31  Julai, 2019.

Aidha, Mwenyekiti, Jaji Kaijage alivikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na Maelekezo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi chote cha Uchaguzi huu mdogo. 

VIONGOZI WA DINI IMARISHENI MALEZI KWA VIJANA-MAJALIWA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na waumini wa Kikristo, kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 53 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ulioambatana na harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kitegauchumi cha jumuiya hiyo, uliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma Julai 5, 2019. Waziri Mkuu, amemwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Askofu, Alinikisa Cheyo, kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 53 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ulioambatana na harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kitegauchumi cha jumuiya hiyo, uliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma Julai 5, 2019. Waziri Mkuu, amemwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
3 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Askofu, Alinikisa Cheyo, wakati akiwasili katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 53 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ulioambatana na harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kitegauchumi cha jumuiya hiyo, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma Julai 5, 2019. Waziri Mkuu, amemwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema viongozi wa dini waendelee kuimarisha malezi na mafundisho ya kiroho kwa vijana na kuepusha mmomonyoko wa maadili ili Taifa liendelee kung’ara, kuheshimika na kusifika duniani kwa utulivu, amani na umoja. 

Amesema Serikali inatambua mchango wa madhehebu ya dini ikiwemo CCT katika kutengeneza mustakabali mwema na ustawi wa familia kupitia mahubiri ya injili na malezi ya kiroho kwa waamini. “Mtakubaliana nami kuwa siku zote Taifa imara msingi wake hujengwa na familia imara.” 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Julai 5, 2019) wakati alipomwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 53 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ulioambatana na harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kitegauchumi cha jumuiya hiyo. Mkutano huo umefanyika jijini Dodoma.

Amesema Serikali inatambua mchango wa malezi ya kiroho katika ustawi wa wananchi na Taifa kwa ujumla na mafundisho yake kwani yamesaidia kujenga watumishi wa umma ambao wamelelewa katika misingi bora ya kumcha Mwenyezi Mungu.    

Waziri Mkuu amesema Serikali inaamini kwamba watumishi wa namna hiyo watachapa kazi kwa bidii, uadilifu, uaminifu na kupiga vita vitendo vyote vya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma. Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za kidini kwa ajili ya ustawi wa Taifa na watu wake.

Akizungumzia kuhusu harambee hiyo ambayo jumla ya sh. milioni 357.35 zilipatikana, Waziri Mkuu amesema ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa CCT wa miaka mitano (2017 – 2022) wenye lengo la kuiwezesha CCT kujitegemea kwa kuwa na vitega uchumi vyake ambavyo vitawawezesha kujiendesha kwa asilimia 80.

Waziri Mkuu ameipongeza CCT kwa kuanza kuchukua hatua za kujenga uwezo wa ndani wa kujitegemea kiuchumi kwani zinahitajika nguvu za pamoja katika kuhakikisha wanawahudumia Watanzania na kuwaletea maendeleo. 

“Kujizatiti kwa CCT katika kufikia malengo yake ya kujitegemea kiuchumi ni muhimu katika kutimiza kusudio na agizo la Mungu la kuwahudumia wahitaji ambao ni Watanzania lakini pia mtakuwa mnajaliza juhudi za Serikali katika wajibu wake wa kuwahudumia wananchi.”

Waziri Mkuu amesema kwa msingi huo, Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za CCT na madhehebu mengine ya dini katika kuwahudumia Watanzania kupitia sekta za elimu, maji, afya na shughuli za ujasiriamali.

Amesema suala la kujitegemea ndiyo msingi wa uongozi wa Rais Dkt. Magufuli wa kujenga uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025 na katika kufanikisha hilo, Serikali imeendelea kupunguza kiwango cha utegemezi.

Amesema kiwango cha utegemezi kutoka kwa Washirika wa Maendeleo katika bajeti kimepungua kutoka asilimia 12.5 mwaka 2017/2018 hadi asilimia nane 2019/2020. “Kuimarika huko kwa bajeti yetu kunakwenda sambamba na kuimarika kwa huduma za kijamii kama vile elimu, maji na kupungua kwa umaskini wa mahitaji muhimu.”


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCT, Mchungaji Canon Moses Matonya, amesema jumuiya hiyo imeanzisha mkakati wa kuwa na vitegauchumu vyake kwa lengo kuondokana na utegemezi wa fedha za ufadhili ambazo zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka.


RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA AWASILI CHATO MKOANI GEITA NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFULI KATIKA ZIARA YAKE BINAFSI YA SIKU MBILI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita kwa ziara binafsi ya siku mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshma iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita kwa ziara binafsi ya siku mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipungia mikono wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Chato katika mapokezi ya Rais huyo wa Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakizungumza wa wananchi wa Chato njiapanda wakati wakitokea uwanja wa Ndege wa Chato.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakizungumza wa wananchi wa Chato waliofika kumpokea katika uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakiangalia vikundi vya Kwaya mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili Chato.
Ndege ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Chato Mkoani Geita. PICHA NA IKULU


SERIKALI YASHAURIWA KUTENGA FUNGU MAALUMU KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA VIJIJINI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha

Serikali kipitia maafisa ugani hapa nchini, imeshauriwa kutenga fungu maalumu ambalo litatumika kwenda kutoa elimu kwa wakulima vijijini ikiwa ni pamoja na kutengeneza sheria za kuwabana maafisa kilimo na maafisa ugani 

Akizungumza na vyombo vya habari katika maandalizi ya kuelekea maonyesho ya kilimo ambayo yanatarajiwa kufanyika hivi karibuni jijini Arusha, Afisa kilimo kutoka kampuni ya pembejeo za kilimo ya Agrichom Bryson Saimon amesema sekta ya kilimo ina wigo mpana hivyo wamejipanga kutokomeza wadudu wanaoshambulia Mazao

Aidha amesema kuwa Mazao ya mbogamboga yamekuwa yakishambuliwa na wadudu kwa urahisi na hivyo kusababisha kukosekana kwa mazao hasa zao la nyanya hapa nchini hivyo kwa kuliona hivyo wametengeneza kirutubisho kijulikanacho kama LIBERATE 

Hata hivyo amewataka wakulima kuwa na mazoea ya kuhudhuria semina za kilimo ili kuweza kupata ujuzi wa kulima kilimo bora cha kisasa na chenye tija ili kuoweza kuuza na kupata faida pamoja na kuongeza pato la taifa.

Mfanyabiashara alalamikia kudaiwa rushwa na Trafiki jijini Arusha

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Mfanyabiashara na Mmiliki wa Mabasi ya kusafirisha abiria mikoani kutoka kampuni ya KIMOTCO ,Benedict Mberesero,amewalalamikia Askari wa usalama barabarani katika Mkoa wa Arusha,kwa vitendo vya Rushwa iliyokithiri akidai wamegeuka mamlaka ya mapato TRA.

Akizungumza kwenye  kikao cha wadau wa usafirishaji jijini Arusha,mbele ya Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Nchini,(SACP) Fotunatus Muslimu, alimshutumu Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha ,RTO Joseph Bukombe kuwa amekuwa kinara kwa kuongoza kikosi cha askari kukusanya Rushwa kutoka kwa wasafirishaji .

Amedai kuwa vibanda vya ukaguzi wa mabasi katika eneo la kituo kikuu cha mabasi jijini hapa ,vimegeuka vibanda vya kukusanya Rushwa kwa mabasi mbalimbali yanayoelekea mikoani na fedha hizo huwasilishwa kwa wakubwa .

"Napenda niseme ya Moyoni naona watu wamekuwa waoga kusema ,ukweli ni kwamba suala la Rushwa ni kubwa kwa Trafiki hapa Arusha naomba uchunguze mwenyewe ujionee" Alisema Ben

Aliongeza kuwa hivi karibuni alibambikiwa kesi ya matumizi mabaya ya Silaha ambapo alipigwa na askari wa usalama barabarani na kutupwa selo kituo cha Polisi kwa makosa aliyodai ni ya usalama barabarani.

"Namshukuru RPC alilishughulikia suala langu na bila yeye bila shaka ningekuwa nimefungwa kwa kubambikiwa kesi za uongo kwani si kweli kwamba Mimi nilitishia askari kwa silaha" Alisema .

Alimtuhumu RTO Bukombe kutoa ushirikiano pindi anapopigiwa Simu kwa nia ya kuomba msaada.

Akijibu hoja hizo ,RTO Bukombe Alisema tuhuma zilizoelekezwa kwake hazina ukweli Bali ni choko choko zilizolenga kumchafua.

Alisema wao kama kitengo cha usalama barabarani wanatoza faini kwakufuata kanuni sheria na awawezi kumtonza mtu faini bila kufuata sheria.

Alitoa wito kwa wamiliki wa magari makubwa ya abiria kukaa na madereva wao na kuwaambia waongee ukweli na sio kuwatupia lawama tu askari wa barabaeani,pia aliongeza kuwa mara baada ya kuwa kupelekewa malalamiko wanatakiwa kufuata sheria kwa kuuliza au kupeleka malalamiko hayo kwa viongozi wa juu wa askari hao wa usalama barabarani.

065Picha ikionyesha Mfanyabiashara na Mmiliki wa Mabasi ya kusafirisha abiria mikoani kutoka kampuni ya KIMOTCO ,Benedict Mberesero akiongea katika kikao hicho cha wamiliki wa mabasi na Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Nchini,(SACP)Futunatus Musilimu.


NDIKILO ATOA MIEZI MITATU KWA DED KISARAWE KUIONGEZEA NGUVU IDARA YA UKAGUZI WA NDANI

$
0
0




NA MWAMVUA MWINYI,KISARAWE

MKUU wa Mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ametoa miezi mitatu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Mussa Gama na Ofisa Utumishi , kuhakikisha idara ya ukaguzi wa ndani inajitosheleza kwa ikama ya watumishi na vitendea kazi.

Ameeleza idara hiyo iangaliwe kwa jicho la tatu, ili iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu wakati wa ukaguzi.

Akizungumza katika baraza maalum la madiwani kupitia hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) ,Ndikilo alieleza baada ya utekelezaji wa agizo hilo ,mkuu wa wilaya hiyo Jokate Mwegelo ampelekee taarifa.

“Kumekuwepo na changamoto ya kiutendaji katika raslimali watu na fedha na kusimamia miradi ya maendeleo”:Hivyo basi wakurugenzi mkoani hapa na watendaji wasimamie ili sheria,kanuni na taratibu zifuatwe kwa lengo la kusaidia mkaguzi akipita kusiwepo na dosari”alifafanua Ndikilo.

Ndikilo aliongezea kwamba, CAG asionekane ni adui kwani ni mshirika wa kuweka mambo vizuri kuhakikisha fedha za serikali haziliwi wala kufujwa.

Nae Mkaguzi wa hesabu wa nje mkoani Pwani, Hamis Juma alitaka ushauri na maoni yaliyotolewa katika hoja 26 zinazoendelea kufanyiwa kazi na halmashauri hiyo zifanyiwe kazi na uhakiki utafanyika 2018/2019.

Awali akimkaribisha mkuu huyo wa mkoa, Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo alisema halmashauri hiyo imepokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha 2017/2018 kutoka kwa mdhibiti wa hesabu za serikali mwezi april 2019 ikionyesha hati safi na hoja za ukaguzi.

Nae mkurugenzi wa halmashauri ya Kisarawe ,Mussa Gama alipokea maagizo waliyopatiwa na kudai watahakikisha wanapata hati safi nyingine kipindi kijacho na kuondoa mapungufu yaliyoonekana .

Alibainisha wakati wa ukaguzi imegundua kuwa kitengo cha ukaguzi hakifanyi kazi kwa sababu watumishi wachache watatu badala ya watano na uhaba wa vitendea kazi lakini wameshughulikia na kuongeza mtumishi mmoja na kufikia wanne

MKURUGENZI MKUU OFISI YA TAKWIMU AKUTANA NA BALOZI WA JAMHURI YA KOREA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Balozi wa Jamhuri ya Korea Nchini, Tae-ick Cho (katikati) wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika leo (Ijumaa Julai 5, 2019) katika Ofisi za NBS Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtaalamu wa Utafiti wa Ubalozi wa Korea, Hae-ju Yong 
Balozi wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa yaliyofanyika leo Ijumaa Julai 5, 2019 katika Ofisi za NBS Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Takwimu za Kilimo wa NBS, Titus Mwisummba na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa NBS, Bw. Daniel Masolwa. 
Balozi wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho akimwonesha nakala ya jarida Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa kuhusu miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelzwa na Serikali ya Nchi hiyo Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa NBS, Bw. Daniel Masolwa. Mkutamo baina ya Balozi huyo na NBS ulifanyika leo Ijumaa (Julai 5, 2019) katika Ofisi za NBS Jijini Dar es Salaam. 
Balozi wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (katikati) na baadhi ya watendaji wa NBS akiwemo Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi- Daniel Masolwa kulia, mara baada ya kumalizika kwa kikao baina yao leo (Ijumaa Julai 5, 2019) katika Ofisi za NBS Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA MAELEZO) 

 BALOZI wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho amesema Serikali ya Nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takiwmu (NBS) kwa ajili ya kuimarisha miundombinu yake ikiwemo mifumo ya Tekonojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kumalizia Ujenzi wa Ofisi za NBS katika Mikoa ya Dodoma na Kigoma. 

Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dkt. Albina Chuwa leo Ijumaa (Julai 5, 2019) Jijini Dar es Salaam, Balozi Cho amesema Serikali yake ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitajika katika kuhakikisha kuwa NBS inatekeleza majukumu yake. 

Balozi Cho alisema Serikali ya Jamhuri ya Korea inatambua umuhimu wa takwimu katika shughuli za kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, hivyo itahakikisha kuwa mahitaji yote ya msingi kwa yanayohitajika na NBS ikiwemo uimarishaji wa miundmbinu ya TEHAMA inapewa kipaumbele. 

Mwezi Juni mwaka 2018, tulianza mazungumzo ya ushirikiano na NBS kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, hivyo utekelezaji wa masuala yote ya msingi katika mazungumzo hayo yapo katika hatua nzuri na nitawasiliana na Serikali yetu ili kuona jinsi ya kusukuma jambo hili kwa haraka zaidi. 

Aidha Balozi Cho aliongeza kuwa Serikali ya Korea itahakikisha kuwa makubaliano hayo yanaanza kutekelezwa kwa haraka kwa kuwa inatambua ukubwa na umuhimu wa majukumu ya NBS katika uzalishaji na upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya kuharakisha shughuli za Maendeleo ya wananchi. 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dkt. Albina Chuwa alisema NBS kupitia Wizara ya Fedha na Mipango tayari ilianza hatua za awali za makubaliano ya ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Korea na hivyo kupitia sheria ya misaada ambapo wameahidi kujenga na kuimarisha miundombinu ya Ofisi za NBS zilizopo katika Mikoa ya Kigoma na Dodoma. 
“Katika Mkoa wa Kigoma wameahidi kujenga Ofisi hiyo na kusimika miundombinu ya TEHAMA wakati katika Mkoa wa Dodoma wameahidi kuweka miundombinu ya TEHAMA katika Jengo la Ofisi zetu za Dodoma” alisema Chuwa.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AELEKEA NCHINI UINGEREZA KWA SAFARI MAALUM

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akiondoka Zanzibar kuelekea Nchini Uingereza kwa safari Maalum, akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Viongozi na Wananchi waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, wakati akiondoka kuelekea Nchi Uingereza kwa Safari Maalum 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar, wakati wa kuondoka Nchini leo kuelekea Nchini Uingereza kwa Safari Maalum, hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.(Picha na Ikulu)

WAZIRI HASUNGA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA MBOLEA YA TOPIC YA NCHINI MISRI

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TOPIC ya Mjini Cairo nchini Misri Mhandisi Raouf Bakry (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya mbolea ya Taifa (TFC) Ndg Salum Mkumba mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kazi uliofanyika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo tarehe 5 Julai 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo) 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TOPIC ya Mjini Cairo nchini Misri Mhandisi Raouf Bakry mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kazi uliofanyika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo tarehe 5 Julai 2019. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya mbolea ya Taifa (TFC) Ndg Salum Mkumba na Steven Kihwele ambaye ni mchumi Wizara ya Kilimo.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo – Dar es salaam 

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) leo tarehe 5 Julai 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TOPIC ya Mjini Cairo nchini Misri Mhandisi Raouf Bakry katika kikao kazi kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam. 

Katika mkutano huo Mhandisi Raouf amemueleza Mhe Hasunga kuwa lengo la ziara yake ni kuangalia uwezekano wa kutumia fursa inayopatikana na kutolewa na Benki ya EXIM inayotoa mikopo nafuu ili kufanya biashara kati ya nchi za Afrika. 

Amesema kuwa akipatiwa mkopo huo ataongeza uwezekano wa kusambaza mbolea na viuatilifu ili kuongeza tija na kasi ya uzalishaji wa mazao mbalimbali ya wakulima. 

Kwa uoande wake Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amemueleza Mhandisi Raouf kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kutekeleza kwa vitendo hivyo ina wakaribisha  awekezaji katika uwekezaji mbalimbali ikiwemo sekta ya viwanda vya kusindika mazao. 

Alisema kuwa Mhe Magufuli amejipambanua katika kuimarisha uwezekano wa wawekezaji kuwa na uwekezaji uliotukuka ili kuwanufaisha watanzania sambamba na manufaa kwao wenyewe. 

Katika mkutano huo baina ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TOPIC ya Mjini Cairo nchini Misri Mhandisi Raouf Bakry ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya mbolea ya Taifa (TFC) Ndg Salum Mkumba. 

UZINDUZI WA VITUO MAALUMU VYA UKAGUZI WA MAGARI YA UTALII KUFUNGULIWA KARIBUNI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha

Chama cha waongoza watalii (Tato) kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani , wanatarajia kufanya uzindua wa vituo maalumu vya ukaguzi wa Magari ya utalii baada ya kukamilika kwa matengenezo ya makontena Manne na Gari moja yatakayotumika kuhudumia watalii.

Akiongea Mara baada ya kutembelea na kujionea Makontena manne yaliyofanyiwa ukarabati na kampuni ya Hanspaul, yatakayotumika kama ofisi kwenye vituo maalumu vya ukaguzi pamoja na Gari moja jipya aina ya Rand Cruiser,

Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Nchini,,Fortunatus Muslim alisema kuwa vituo hivyo vitaondoa malalamiko ya muda mrefu katika sekta hiyo na kusaidia kutoa Huduma kwa watalii wanaotembelea vivutio mbalimbali katika Mkoa wa Arusha.

"Natamani uzinduzi huu ufanywe na Mkuu wa jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro kwa kuwa wenzetu wa Tato na Mdau wa maendeleo Hanspaul wamefanya mambo makubwa kwa kulisaidia jeshi la Polisi kuimarisha Utalii nchini na zoezi hili lisiishie tu hapa Arusha lifanyike pia mikoani "Alisema

Musilimu pamoja na kuipongeza kampuni ya Hanspaul na Tato kwa hatua ya kusaidia miundo mbinu hiyo katika sekta ya utalii, alitaka Huduma kama hiyo ipelekwe pia mikoani kwa lengo la kuhudumiwa watalii ili kuimarisha sekta ya utalii nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Hanspaul,Satbir Singh amesema kuwa kampuni yake imefikia hatua ya kukarabati Kontena hizo kwa lengo kwa kuimarisha sekta ya utalii nchini ili kuwaondolea kero watalii mbalimbali wanaotembelea vivutio nchini.

" Hizi kontena zitatumika kama ofisi na zitasaidia kutatua changanoto mbalimbali kwa watalii na sisi kama Hanspaul tunaunga mkono serikali yetu kupitia sekta ya utalii ili watalii waendelee kuja kwa wingi mchini"Alisema Singh

Naye makamu mwenyekiti Tato,Henry Kimambo Alisema kuwa Tato imegushwa na changamoto mbalimbali zinazowahusu watalii na kuamua kujitolea kutafuta miundo mbinu ya Kontena na Gari kwa ajili ya kuhudumia watalii ili nankubiresha sekta hiyo.

Alisema Gari hilo aina ya Land cruise limewagharibu kiasi cha zaidi ya dola 45,000 wakishirikiana na jeshi la Polisi ambao wamelipia kodi ya Gari hilo.

Huhusu Kontena nne zilizokarabatiwa na kampuni ya Hanspaul ambano ni wadau wakubwa wa utalii nchini,alisema zitasaidia kutoa huduma kwa watalii kama ofisi na choo ,na kupunguza changamoto ya muda mrefu ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wasafirishaji wa watalii .
Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Nchini,Fortunatus Muslim akijaribu moja ya gari itakayo tumika katika kituo cha utalii
Mkurugenzi wa kampuni ya Hanspaul,Satbir Singh akimfafanulia jambo Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Nchini,,Fortunatus Muslim wakati alipotembelea kukagua kontena nne zilizokarabatiwa na kampuni yao.
Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Nchini,,Fortunatus Muslim akiwa na viongozi wa chama cha waongoza watalii

UJENZI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA JNIA UMEKAMILIKA-NAIBU WAZIRI NDITIYE

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Tanzania Mhandisi Julius Ndyamukama (mwenye koti jeusi)akisoma Taarifa ya Mradi wa Jengo la III la abiria kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye alipofanya ziara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Tanzania Mhandisi Julius Ndyamukama (mwenye koti jeusi)akisoma Taarifa ya Mradi wa Jengo la III la abiria kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye alipofanya ziara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. 
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye akihoji jambo katika Ukumbi wa Watu mashuhuri alipotembelea jengo la III la abiria. Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Bw, Paul Rwegasha ( mwenye koti kijivu) Akitoa maelezo ya jengo la mizigo linalokarabatiwa kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye wakati alipofanya ziara katika Kiwanja hicho. 

…………………………. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Mhandisi Atashasta Nditiye, amesema Ujenzi wa Jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) umekamilika, na Jengo linatarajiwa kuanza uendashaji mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu. 

Pia amesema amefurahishwa kwa kukamilika kwa jengo hilo ambapo ni la kisasa na huduma zake zake ni nzuri. Akizungumza mara baada ya Ziara ya kukagua Jengo hilo , amesema katika idadi ya miruko ya ndege Barani Afrika JNIA inachukua nafasi ya tano na nafasi ya sita kwa idadi ya abiria. 
‘’ Nimefurahishwa kwa kukamilika kwa Ujenzi wa jengo la tatu la abiria wa Kiwanja cha Ndege ambapo utakapoanza kuhudumia abiria natarajia tutachukua nafasi nzuri zaidi Barani Afrika kwani ni Jengo la kisasa na litatoa huduma nzuri,’’ alisema. 

Nae Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere( JNIA), Paul Rwegasha akitoa ufafanuzi wa Kiwanja hicho, alisema mara baada ya kukamilika kwa jengo la tatu itakuwa jumla ya majengo matatu yanaweza kuhudumia abiria milioni nane kwa mwaka. 

Rwegesha alisema ujenzi wa jengo la kwanza lina uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka na ujenzi wa jengo la pili abiria milioni 1.5 
Alisema kukamilika kwa jengo hilo la tatu kutaongeza idadi ya Ndege, abiria pamoja na Watalii baada ya kuwa na Miundombinu bora na ya kisasa. 

Vile vile alisema Ujenzi wa jengo la tatu ni kwa ajili ya abiria wa safari za Kimataifa ambapo kwa sasa yako mashirika 23 na jengo la pili kwa ajili ya abiria wa safari za ndani ya nchi huku jengo la kwanza safari za ndani pia. . 
Alisema ujenzi wa jengo la tatu la abiria litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 2,800, kwa saa na maegesho ya magari mchanganyiko yasiopungua 2,075 kwa wakati mmoja. 

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama, alisema kwasasa kuna katika maandalizi ya Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa 39 wa SADC ambapo maadalizi yameambatana na ukarabati wa maboresho ya miundombinu na samani. 

Ndyamukama, alisema wageni hao wanatarajia kuingia hapa nchini Agosti mwaka huu ambapo watapata huduma bora zaidi na yenye uhakika.

DKT. NDUGULILE ATAKA UONGOZI BORA NA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ILI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi cheti cha pongezi kwa uongozi bora na usimamizi kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi Dkt. Yustina Tizeba wakati akifunga kikao cha waganga wafawidhi kilichofanyika Jijini Dodoma. 
Mkurugenzi wa tiba Dkt. Grace Maghembe akiongea wakati wa kilele cha kikao kazi cha Waganga Wafawidhi kilichofanyika Jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa wakati akifunga Kikao kazi kilichofanyika kwa siku tano na kupitisha maazimio ya kuimarisha huduma Jijini Dodoma 

************** 

Na WAJMW-DOM 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka Waganga wafawidhi kutekeleza maazimio waliyopitisha katika kikao kazi kilichofanyika kwa siku tano Jijini Dodoma. 

Dkt. Ndugulile amesema hayo wakati akifunga kikao hicho kilichohusisha Waganga Wafawidhi, Makatibu Tawala wa Halmashauri na Manispaa pamoja na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya nchini waliohudhuria kikao hicho. 

“Ninatambua kuwa katika kikao hiki tumepitia mwongozo wa uendeshaji wa Hospitali za Rufaa za Mikoa na kuweka mipango na mikakati endelevu kwa timu za uendeshaji wa Hospitali hizi, ninaomba sana muende mkatekeleze ili kuimarisha Hospitali zetu za Rufaa za Mikoa. Amesema Dkt. Ndugulile. 

Katika kikao hicho Waganga Wafawidhi wameweka maazimio ambayo yataratibiwa katika Hospitali zote za Rufaa za Mikoa nchini ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya kukusanya mapato na kuondoa mianya ya upotevu wa mapato, kuimarisha na kuendelea kuzijengea uwezo timu za uendeshaji za Hospitali za rufaa za Mikoa katika kusimamia rasilimali watu, fedha, miundombinu n.k. Kuweka mikakati endelevu ya kupunguza vifo vya mama na mtoto, kila Hospitali kuandaa mkakati wa kununua vifaa na vifaa tiba vitakavyowezesha huduma za kibingwa kutolewa wakati wote, pamoja na kila Hospitali kuja na ubunifu/mikakati ya kukabiliana na upungufu wa watumishi katika maeneo yao kwa kushirikiana na wadau wa mikoa yao. 

Aidha, Dkt. Ndugulile ametoa maagizo kwa Waganga Wafawidhi kutekeleza mambo muhimu katika maeneo yao ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwa na mfumo wa uongozi na utawala, upatikanaji wa watumishi wenye sifa stahiki katika kada zote, uimarishaji wa miundombinu kwa ajili ya huduma zilizokusudiwa, upatikanaji wa vifaa na vifaa tiba na vitendanishi pamoja na uimarishaji wa matumizi ya teknolojia, taarifa za afya na mawasiliano. 

Pamoja na hayo Naibu Waziri amewapongeza Waganga Wafawidhi kwa kushiriki kikao hicho na kuwataka kwenda kutekeleza maazimio waliyopitisha ili kuboresha Hospitali za Rufaa za Mikoa katika maeneo tofauti yaliyokusudiwa ili kutoa huduma bora kwa wananchi. 

Kabla ya kufunga kikao Dkt. Ndugulile alitoa vyeti vya ubora wa huduma na pongezi, ambapo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Katavi Dkt. Yustina Tizeba alipata cheti cha pongezi kwa muongozo wa maono, uongozi bora na usimamizi huku Hospitali ya Rufaa ya Amana ikipata vyeti vitatu vya ubora ikiwa ni pamoja na kuongoza katika kupunguza vifo vya mama na mtoto, uongozi bora na mikakati endelevu ya kukusanya mapato na kuwepo kwa vifaa na vifaa tiba vinavyotumika katika huduma za kibingwa.

JAFO AKEMEA UGOIGOI WA WATENDAJI KISARAWE

$
0
0

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo ameonyesha kukerwa na kasi ndogo iliyoonyeshwa na watendaji katika kukamilisha miradi ya afya na elimu iliyopata fedha wilayani Kisarawe.
Waziri Jafo ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea katika Shule za sekondari zikiwemo Sekondari za Kibuta, Kurui, Mzenga, na Kimani, pamoja na ukarabati wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe alipofanya ziara ya kikazi Jimboni kwake kukagua miradi ya maendeleo.

Amewataka watendaji wote hususani Mkurugenzi na wakuu wake wa Idara kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kuwa wananchi wanataka huduma kutoka kwenye serikali yao ambayo inajitahidi kuleta fedha ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Awali, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe, Mussa Gama amekiri kuchelewa kwa miradi hiyo kutokana na upatikanaji wa vifaa hususani saruji.
Hata hivyo amemhakikishia Waziri Jafo kwamba watafanya kila liwezekano ili miradi yote iwe imekamilika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

MADAM RITA, HOYCE TEMU, SAIDA KESSY KUAMUA MISS SIMIYU 2019

$
0
0
Washiriki wa Shindano la Miss Simiyu 2019 linalotarajiwa kufanyika kesho Julai 06, 2019 Mjini Bariadi. 
Mwalimu wa warembo wanaoshiriki Shindano la Miss Simiyu 2019, Bi. Doreen Robert Pastory akizungumza na waandishi wa habari Julai 04, 2019 Mjini Bariadi kuhusu shindano la Miss Simiyu litakalofanyika kesho Julai 06, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Simiyu Talent Compay Ltd, Bi. Zena Mchujuko ambayo inaandaa shindano hilo kwa kushirikiana na Grace Entertainment, akizungumza na waandishi wa habari Julai 04, 2019 Mjini Bariadi. 

………………….. 
Na Stella Kalinga, Simiyu 
Rita Paulsen, Hoyce Temu (Miss Tanzania 1999) na Saida Kessy (Miss Tanzania 1997) wanatarajiwa kuwa majaji wa Shindano la kumsaka Miss Simiyu 2019, litakalofanyika kesho Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu. 
Hayo yamesemwa Julai 04, 2019 na Mkurugenzi wa Simiyu Talent Compay Ltd, Bi. Zena Mchujuko ambalo linaandaa shindano hilo kwa kushirikiana na Grace Entertainment, wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bariadi 

Amesema kama waandaaji wameamua kuwaleta majaji hao ambao ni mahiri na wenye uzoefu katika masuala ya ulimbwende ili kupata Miss Simiyu ambaye atakuwa na uwezo kuuwakilisha mkoa katika Shindano la Miss Tanzania. 

“Tumeamua kuwaleta majaji hawa kwa sababu ya uzito wa tukio lenyewe, uzoefu na umahiri wao, lengo letu ni kutoa Miss Simiyu atakayeweza kutuwakilisha katika Miss Tanzania na tuna uhakika kila mshiriki atapata haki yake” alisema Mchujuko. 

Aidha, Mchujuko amesema Mgeni Rasmi katika Shindano la Miss Simiyu 2019 atakuwa ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kwa upande wa Burudani Mwanamuziki wa Kizazi kipya Nasib Abdul alimaarufu Diamond Platinum atatumbuiza shindano hilo. 

Kwa upande wake mwalimu wa washiriki wa Miss Simiyu 2019 Doreen Robert Pastory alibainisha kuwa majaji hao wanastahili kuwajaji warembo hao huku akiongeza kuwa suala la urembo linatakiwa kuchukuliwa kama ajira nyingine badala ya kuchukulia kama jambo la kihuni ambapo alitoa rai kwa Mikoa mingine kuiga jambo hilo kwani ni ajira kama zilivyo ajira nyingine. 

Naye mmoja wa washiriki Rebeka Manoti amesema wamefundishwa kwa kuzingatia maadili mema, hivyo wana matarajio makubwa ya kupata mlimbwende atakayepeperusha vyema tasnia hiyo ya urembo kimkoa ,kitaifa na kidunia. 

Jumla ya warembo 15 watachuana katika shindano hilo na kiingilio itakuwa Shilingi 10,000 (Regular),Shilingi 50,000(Corparate) na Shilingi 100,000(VIP), na Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Shilingi Milioni moja na washiriki wengine pia watapatiwa zawadi.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images