Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

WAZIRI HASUNGA AJA NA MKAKATI WA KUKUZA KILIMO NCHINI

$
0
0
Na Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati   ifikapo mwaka 2025 imeelezwa kuwa ni lazima iwekeze kikamilifu katika kilimo hifadhi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika kilimo.

Hayo yamebainisha Jijini Dodoma na Waziri wa kilimo Japhet Hasunga, wakati akifungua Warsha ya Wadau wa Kilimo Hifadhi Tanzania.

Amesema serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki ikiwamo kufuta kodi nyingi pamoja na kuhamasishaa matumizi ya Teknolojia za kisasa ambazo ni rafiki katika kilimo.

Amebainisha kuwa ni muhimu kujadiliana pamoja kuhusu sheria kwani hatuwezi kufika uchumi wa kati mwaka 2025 bila kufikia kilimo imara na chenye tija.

“Lazima kuimarishwe mafunzo kwani kilimo nchini bado kipo chini, pia tuongeze utafiti kwakuwa bila utafiti hakuna kilimo na lazima ijulikane kilimo gani kitumike,pembejeo gani zitumike,pia tuongeze uzalishaji wenye  tija,” amesema Waziri Hasunga.

Katika kuimarisha na kuwapa uwezo wakulima amesema Serikali inakuja na mkakati wa bima kwa wakulima lengo likiwa ni kumsaidia mkulima pindi ambapo mazao yake yatakuwa yameharibika shambani.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa amesema kama Serikali itawekeza katika kilimo hifadhi basi sekta ya kilimo itafika mbali.

Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini (CCM) ameiomba Serikali kuongeza bajeti katika sekta ya kilimo hasa katika utafiti na kufanya mageuzi makubwa katika kilimo hasa katika sheria.

“Sera na sheria zina matatizo makubwa unakuta mkulima natayarisha shamba naanza kulima napalilia halafu wakati wa kuvuna Serikali inaanza kunipangia nikauze wapi sio sawa kabisa hapa ni lazima tutengeneze sheria nzuri” amesema Mgimwa.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kilimo, Hifadhi Barani Afrika(ACT) Saidi Mkomwa amesema kilimo hifadhi ni kilimo kinachozingatia uhifadhi wa rasilimali udongo na mazingira kwa ujumla.
 Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza katika warsha ya wadau wa kilimo hifadhi Tanzania iliyofanyika jijini Dodoma leo.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo azindua rasmi mashindano ya Buchimwe, Ampongeza Diwani Yindi

$
0
0

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Addo Komba amezindua rasmi mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.

Mashindano hayo yanashirikisha Timu nane Kwa kila mchezo ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia Kombe, Seti Moja ya Jezi na kiasi cha Sh 100,000 taslimu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Komba amesema Serikali kupitia Wizara ya Michezo itaendelea kuunga mkono maendeleo ya Michezo kwani wanaamini licha ya Michezo kuwa ni Afya lakini siku hizi imekua ni Ajira ambayo imenufaisha kundi kubwa la vijana.

" Nimpongeze Diwani wenu, Mhe Yindi kwa kuandaa mashindano haya, kila mwaka amekua akianzisha Ligi mbalimbali kwa ajili yenu, hii ni faida kwenu na myatumie mashindano haya kukuza vipaji venu na kuhakikisha mnapiga hatua nyingine ya kupata Timu zinashoriki Ligi kubwa," amesema Komba.

Nae Diwani wa Kata hiyo Mhe Yindi amesema pamoja na kuanzisha mashindano hayo pia kutakua na kozi za uamuzi kwa vijana waliomaliza kidato cha nne ambazo zitaendeshwa na wakufunzi kutoka Chama Cha Soka Mkoa wa Dodoma, (DOREFA).

" Lengo la mashindano haya ni kuhakikisha vijana wetu wanapiga hatua, lakini pia kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Dk John Magufuli kukuza sekta ya Michezo nchini, na sisi kama watu tunaomsaidia inatubidi kumuunga mkono kwa vitendo.

" Tunafahamu kuwa mna changamoto ya viwanja vya kuchezea, nimeshaanza kushughulikia na nina hakika kupitia Wizara ya Michezo tutamaliza changamoto hiyo," amesema Mhe Yindi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chinonwa, Mhe Joel Mwaka amempongeza Diwani Yindi kwa kuandaa mashindano hayo na kuahidi kutoa mchango wake wa hali na mali katika kila hatua ya mashindano hayo.

Nao wananchi wa Kata hiyo wamemshukuru Diwani huyo kwa kudhamini upatikanaji wa Jezi na Mipira kwa kila timu zinazoshiriki Ligi hiyo kwani kumeongeza ari ya kufanya vema.

TCAA YAWAKARIBISHA WANANCHI KUJIFUNZA MASUALA YA USALAMA WA ANGA

$
0
0
Wananchi waliofika katika maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba 2019 wakiuliza maswali kwa timu ya wataalamu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) walipotembelea banda hilo lililopo jengo la Saba Saba Hall kujionea shughuli zinazofanywa na mamlaka hiyo. Wananchi waliojitokeza katika banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  wakipewa elimu juu ya masuala ya usalama na usafiri wa anga. Mkufunzi wa Chuo cha Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Thamarat Abeid (kushoto) akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kujifunza masuala mbali mbali ya Usalama wa anga. Mhandisi Edina Mbwana wa TCAA akimuelezea mwananchi aliyetembelea banda hilo kujionea namna mitambo ya mawasiliano pamoja na uangalizi wa ndege inavyofanya kazi.

UKIONGEA NA SIMU YA MKONONI ZA KISASA ZAIDI YA DAKIKA TANO KUNASABABISHA MADHARA YA KIAFYA MWILINI -TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akiagana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Peter Ngamilo mara baada ya kutembelea banda hilo.

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MKUU wa Kitengo cha Mawasiliano katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Peter Ngami ametoa tahadhari kwa wananchi kukabiliana na mionzi iliyopo katika simu za mkononi za kisasa kwa kuzungumza chini ya dakika tano vinginevyo inaweza sababisha madhara mbalimbali mwilini.

Ametaja baadhi ya madhara yanayoweza kupatikana ni ugonjwa wa Saratani huku wakitaka kuacha kuwapatia watoto kutumia simu hizo mara kwa mara kwani mionzi yake inaathiri mifumo ya ukuaji kwa watoto.

Akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Ngami amesema kuwa wanashauri
wanapotumia simu zaidi ya dakika tano kutumia ‘Earphone’ au kuweka ‘Loudspeaker’ kuepuka madhara ya mionzi huku wakieleza matumizi ya simu hizo ikiwa imeisha au inalalamika chaji ni hatari zaidi kwani mionzi inakuwa mikubwa.

Ngamilo amefafanua wananchi kuwa lengo la kuwapo katika maonesho hayo ni kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kukabiliana na mionzi katika shughuli zao za kila siku."Mionzi ya simu iko katika aina ya mionzi ambayo haileti madhara ya moja kwa moja lakini unapozungunza kwa muda mrefu inaweza kusababisha kichwa kuuma au joto la mwili kupanda huku kwa watoto wadogo ubongo bado ni teke na wako katika ukuaji hivyo kuweza kuharibu ukuaji," amesema.

Ameongeza kuwa wanawashauri wazazi matumizi ya simu za mkononi hasa hizi Smartphone kwa watoto ,siyo mazui na kama wanatumia ni vema earphone au kuwawekea loudspeaker.

Ametumia nafasi hiyo kushauri kuwa simu ikiwa chaji ndogo isitumike kwani mionzi inakuwa katika hatua kubwa na kuchaji tena huku kwa wale wanaopenda kulala na simu kwa kuweka pembeni ya mito ni hatari kwani mionzi inakuwa kwa kasi zaidi.Akizungumzia katika sekta ya Afyamionzi amesema ina madhara kwa wanawake wenye mimba changa, hivyo ukitakiwa kupiga X-Ray kumwalifu Daktari kwani mionzi itaathiri kiumbe kilichopo tumboni na kuzaa mtoto mwenye mapungufu.

Amesema katika vipimo vya X-Ray na CT -Scan ni vipimo haviwezi kuepuka kutokana na madaktari kutaka kufahamu ukubwa wa tatizo kwa mgonjwa ila ni vema wagonjwa kujiridhisha kama mtaalam huyo anaruhusiwa na leseni za kutoa huduma kwani unaweza kuzidisha au kupunguza dozi kwa metu mnene au mwembamba na kulazimu daktari kurudiwa.

Ametoa rai kwa wananchi kufuatilia kama vituo vinavyotoa vipimo hivyo wana leseni ,kama hawana leseni ya tume inawezekana ajakidhi taratibiu na kutoa matibabu kinyume cha taratibu ."Tunawaomba wananchi kuwa makini katika kupata huduma za afya hususan vipimo vyenye kama vipimo vya x- Ray , CT scan, Gama Camera na vinginevyo wakati tume hiyyo ikiendelea kukagua vituo mbalimbali vya afya kuhakikisha usalama wa wananchi," amesema Ngami.

Kuhusu mionzi inayotolewa kwa wagonjwa wa saratani, Ngami amesema inasaidia kuua seli zilizoleta madhara kwa wagonjwa pale inapokuwa mgonjwa yuko katika hatua za awali na kupona kabisa.Pamoja na mambo mengine amewahamasisha wananchi wanaofika kwenye maonesho hayo kutembelea kwenye banda lao ili kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo yanayohusu mionzi.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akitia saini kitabu cha Wageni ,pichani shoto anaeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Peter Ngamilo wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya biashara ya TANTRADE viwanja vya JK Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akifafanua jambo kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika banda la  Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Peter Ngamilo wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya biashara ya TANTRADE viwanja vya JK Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Sylvia Lupembe.

SERIKALI YAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANANCHI VIJIJINI

$
0
0
MCHANGO WA MRADI WA SERIKALI WA EP4R - Shule ya Msingi Chimati iliyopo Kata ya Makojo imepokea kiasi cha Shillingi Million 12.5 kutoka kwenye MRADI huo wa Serikali na Wafadhili wake.

Fedha hizo (Tsh 12.5M) zimetolewa kwa ajili ya UPAUAJI na UKARABATI wa Vyumba vya Madarasa shuleni hapo.

Shule ya Msingi CHIMATI ina jumla ya Wanafunzi 437, Vyumba vya Madarasa vilipo ni vitatu (3), Mahitaji ni Vyumba vya Madarasa kumi (10), kwa hiyo WAPO Wanafunzi wanaosomea nje chini ya MITI. Kwa hali hiyo MRUNDIKANO ni mkubwa na Chumba kimoja cha Darasa kinachukua Wanafunzi kati ya 37 na 87.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Michael Hasunga ameeleza kwamba kwa sasa Shule ina MABOMA Matatu (3) na Ofisi moja (1) ambayo yakikamilika yatapunguza adha hizi, yaani mrundikano madarasani na kusomea chini ya miti.

Mwenyekiti Kijiji cha Chimati, Ndugu Masinde Bwire, ameeleza kwa namna ambavyo wameendelea kushawishi Wananchi kuhusu ukamilishaji wa Vyumba vya Madarasa. Wananchi wamekubali kuchangia NGUVUKAZI zao na Fedha taslimu Shillingi 5,000 (elfu tano) kutoka kila KAYA.

Aidha Mwenyekiti huyo, kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji cha Chimati, amewashukuru WANANCHI wake na WADAU mbalimbali waliofanikisha ujenzi huo ikiwa ni pamoja na Mbunge wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo ambae AMECHANGIA SARUJI MIFUKO 110, Madawati na Vitabu vingi. 

MFUKO wa JIMBO umechangia MABATI 54. Vilevile Ndugu Beredy Maregesi amechangia Shilingi LAKI TANO (Laki 5). 
Pichani ni Upauaji wa Vyumba vya Madarasa na Ofisi kwenye Shule ya Msingi Chimati iliyoko Kata ya Makojo. 

JAMII CHIBUMAGWA YAHAMASISHWA KUACHANA NA NYUMBA ZA TEMBE ILI KUBORESHA MAKAZI

$
0
0
Mzee Wilfred Nyaombo mkazi wa Kijiji cha Chibumagwa kilichopo kata ya Sasajila Wilayani Manyoni akishiriki kubeba tofali wakati ya Kampeini ya Kitaifa kuhamasisha wananchi kuboresha makazi yao kampeini inayoendelea kijijini hapo kuhamasisha wananchi kuachana na nyumba za asili zijulikanazo kama Tembe. 
Wananchi wa Kijii cha Chibumagwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu mwenye miwani ya jua na shati nyeupe wakibeba tofali jana wakati wa Kampeini ya Kitaifa kuhamasisha wananchi kuboresha makazi kazi inayoendelea katika kijiji hicho kilichopo kata ya Sasajila Wilayani Manyoni. 
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Badru Abdunul akisaidiana na wananchi wa Kijiji cha Chibumagwa kilichopo kata ya Sasajila Wilaya ya Manyoni kubeba tofali jana wakati wa Kampeini ya Kitaifa kuhamasisha wananchi kuboresha makazi kazi inayoendelea katika kijiji hicho kilichopo kata ya Sasajilwa Wilayani Manyoni. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu akishirikiana na wananchi wa Kijiji cha Chibumagwa kilichopo kata ya Sasajila Wilayani Manyoni kuandaa pumba kwa ajili ya uchomaji tofauli zitakazotumika katika maandalizi ya ujenzi wa nyumba bora wakati wa Kampeini ya Kitaifa kuhamasisha wananchi kuboresha makazi kazi inayoendelea katika kijiji hicho kilichopo kata ya Sasajilwa Wilayani Manyoni. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu akiongea na wananchi wa Kijiji cha Chibumagwa kilichopo kata ya Sasajila Wilayani Manyoni wakati wa Kampeini ya Kitaifa kuhamasisha wananchi kuboresha makazi kazi inayoendelea katika kijiji hicho kilichopo kata ya Sasajilwa Wilayani Manyoni. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu akikabidhi zawadi ya mpira wa Miguu kwa moja wa kiongozi wa Timu ya Mpira wa Miguu iliyoko katika moja ya kitongoji kilichopo katika Kijiji cha Chibumagwa kilichopo kata ya Sasajila Wilayani Manyoni kama zawadi kwa vijana wanaoshiriki katika kazi za kuhamasisha wananchi kuboresha makazi kazi inayoendelea katika kijiji hicho kilichopo kata ya Sasajilwa Wilayani Manyoni. 
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Chibumagwa kilichopo kata ya Sasajila Wilayani Manyoni wakishiriki kusomba tofali kwa ajili ya maandalizi ya tofali za kuchoma zitakazotumika katika ujenzi wa nyumba bora wakati wa Kampeini ya Kitaifa kuhamasisha wananchi kuboresha makazi kazi inayoendelea katika kijiji hicho kilichopo kata ya Sasajilwa Wilayani Manyoni. 
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 
………………….. 
Na Anthony Ishengoma Singida. 
Wakazi wapatao 5,997 wa Kijiji cha Chibumagwa kilichopo kata ya Sasajila Wilayani Manyoni wanaendelea na uboreshaji wa makazi yao baada ya kupata hamasa kutoka kwa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kupitia kampeni yake kitaifa ya kuboresha Makazi na kuachana na nyumba za jadi. 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu Maendeleo ya Jamii hivi karibuni itazindua kampeni hiyo Kitaifa na kwa kuanzia imeanza na Chibumagwa kama kijiji cha mfano kwa kuanza na maboresho ya makazi ya nyumba sita za wazee wasiojiweza na watu wenye mahitaji maalumu kwa kushirikisha wananchi kijijini hapo ili wao kama sehemu ya jamii waone umuhimu wa kujiletea maendeleo kwa kuboresha makazi kwa njia ya kujitolea kwa pamoja. 
Akiongea na wakazi wa Kijijini Chibumagwa wilayani Manyoni mkoani Singida Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa kampeni ya kuboresha makazi bora imeanzia kijijini hapo lakini ni matarajio ya Serikali kuwa kampeini hiyo itaendelea nchini kote na kuwataka wakazi wa kijiji hicho kuachana na nyumba za Tembe na waboreshe makazi ya kwa kutumia nyumba zilizojengwa kwa tofali. 
Aidha Katibu Jingu aliongeza kuwa nyumba za Tembe zimekuwa na usumbufu mkubwa kwa kuwa zinatakiwa kufanyiwa maboresho hasa wakati wa kipindi cha mvua jambo ambalo uwafanya wakazi hao kulazimika kujenga kila mwaka kutokana maji ya mvua kuleta usumbufu mkubwa na kusababisha kuwepo kwa ujenzi mpya kila mwaka. 
Dkt. Jingu ameyataja madhara mengine ya nyumba za jadi kuwa ni kukosekana kwa hewa ya kutosha ndani ya nyumba hizo, kuwepo kwa wadudu kama vile mijusi na lakini pia kuwa na madhara makubwa kiafya hivyo kuwataka wakazi hao kwapamoja kushirikiana ili kila familia kijijini hapo kuwa na makazi yaliyoboreka. 
Akisoma Risala fupi kuhusu kampeni hiyo Kijijini hapo Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bw. Benjamin Njauka alisema kuwa lengo la kampeni hiyo Kijijini hapo ni kuhamasisha jamii kuboresha makazi kwa mtu mmoja mmoja kwa njia ya kushirikiana akiongeza kuwa jamii hiyo inahamasishwa kwa njia ya mikutano ya hadhara ikiwemo ushauri kutoka kwa viongozi wa dini. 
Aidha Bw. Njauka Kijiji chake tayari kimefanikiwa kufyatua tofali 14,553 na kati ya hizo tofali 18,000 hizo zitatumika kujenga nyumba sita za awali na kuhaidi kuwa uifikapo tarehe 6 mwezi huu vitongoji vinavyounda kijji hicho vitakuwa vimekamilisha ufyatuaji tofali na nyumba sita za awali zitakuwa tayari ifikapo Julai 30. 
Wakati huo huo Mkazi wa Kitongoji cha Msakile Kijiji cha Chibumagwa Wilfred Nyaombo alisema kuwa kampeni imepokelewa kijijini hapo kwa mwitikio mkubwa na vijana wamehamasika vya kutosha na kushiriki kikamilifu katika hatua ya wali ya ufyatuaji tofali kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba za watu wenye mahitaji maalumu. 
Aidha Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Manyoni Bi. Maua Ngusa amesema mradi wa makazi bora katika Kijiji cha Chibumagwa ni wa mfano na unaanza na kwa wananchi wenye maisha duni kabisa lakini nyumba zitakazo jengwa zitatumika pia kwa watu wengi kuiga ujenzi wake ili kuboresha makazi yao. 
Kijiji cha Chibumagwa na vitongoji vyake vinashiriki katika kampeni hii ambayo ni ya kitaifa yenye kaulimbiu ya piga kazi boresha makazi na tayari kampeni itaanza na mikoa mitano na moja ya mikoa ya mwanzo ni mkoa Singida pamoja na mkoa wa Geita na inafanyika ili kuwawezesha wananchi kuishi kwenye makazi yaliyobora.

NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI ATEMBELEA KIKOSI KAZI KINACHOANGALIA MABORESHO MFUMO WA HAKI JINAI JIJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Tixon Nzunda amekitembelea kikosi kazi kinachoangalia maboresho ya mfumo wa haki jinai nchini na kuwataka kuzingatia weledi, haki za binadamu na utawala bora ili kupata mfumo utakaotoa haki na kuzingatia utawala wa sheria. 

Bw. Nzunda ametoa rai hiyo alipokutana na kuzungumza na wataalamu kutoka serikalini na katika mashirika yasiyo ya serikali wanaoendelea na kazi ya kuangalia namna ya kuboresho mfumo wa haki jinai nchini jijini Dodoma. 
“niwapongeze kwa kuwa sehemu ya kazi hii, nyinyi ni sehemu ya mabadiliko, kwa kazi hii lazima mzingatie weledi, uwazi, ukweli na haki za binadamu, ili wananchi ambao mmewaacha huko uraiani waweze kupata haki zao pale wanapostahili,” alisema na kuongeza kuwa mfumo unaofanyiwa maboresho lazima ulinde haki za wananchi. 

Amesema ni matumaini ya Serikali kuwa kupitia maboresho hayo utapatikana Mfumo ambao utalinda haki za binadamu na kuzingatia utawala wa sheria kwa kuwezesha haki kutendeka na kupatikana baina ya watendaji na wananchi.

Be. Nzunda pia amewataka wataalamu hao kuzingatia uadilifu kwa kufanya yaliyo sahihi huku wakiwafikiria wananchi.

Amesema maboresho hayo yakizingatia mambo hayo yataleta Mfumo utakaomaliza tatizo la rushwa, mgongano baina ya taasisi na kuleta uwazi, kutenda haki kwa wananchi hivyo kuwa na mfumo wa watu ambao unazingatia utawala wa sheria

MILIONI 931 ZA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI ZAANZA UKARABATI WA SEKONDARI YA KIGONSERA

$
0
0
Shule ya Sekondari ya Kigonsera iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma ambayo ilianzishwa mwaka 1938 ikiwa na Historia kubwa ya kusomesha viongozi wengi wa kitaifa akiwemo Rais wa awamu ya tatu. Mh. Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu wa sasa, Mh. Kassim Majaliwa imeanza kufanyiwa ukarabati mkubwa baada ya Rais John Pombe Magufuli kutoa kiasi chaA fedha milioni 931 kwa ajili ya ukarabati mkubwa katika shule hiyo.

WATANZANIA WASHAURIWA KUNUNUA MAGARI YANAYOTUMIA GESI ILI KUPUNGUZA GHARAMA

$
0
0


Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba akizungumza na wanahabari katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba 2019 kuelezea mikakati mbali mbali ambayo shirika limejipanga kuongeza mikakati ya upatikanaji wa gesi nchini Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Muonekano wa Banda hilo. 


Wananchi wakipata maelezo juu ya mfumo wa usambazaji gesi wakati walipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) lililopo viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Saalaam. 



Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa akipata maelezo juu ya gari lililofungwa mfumo wa kutumia gesi asilia wakati alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) lililopo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 


Wananchi waliotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) wakiangalia gari lililofungwa mfumo wa kutumia gesi asilia. 




Wafanyakazi wa TPDC wakiwa katika picha ya pamoja Kaimu Mkurugenzi Mhandisi Msomba. 

Na Zainab Nyamka, Michuzi TV. 

SHIRIKA la maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) wamesema mpaka kufikia mwezi Septemba mwaka huu watakuwa wameshafungua vituo vingi vya huduma ya gesi kwa magari. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba wakati wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam. 

Musomba amesema, mpaka sasa kuna kituo kimoja cha kuuzia gesi ambacho kipo Ubungo ila mkakati wao ni kuwa na vituo vingi sana vitakavyotoa huduma kwa wananchi. "Kuna kituo kimoja cha gesi ambacho kipo Ubungo ila mikakati tuliyokuwa nayo kufikia Septemba mwaka huu tutakuwa na vituo vingi vya kuuzia gesi, " amesema Musomba.

Ameeleza kuwa, TPDC wapo kwenye mkakati wa kuongea na wamiliki wa Mwendokasi na kuwashauri kuleta magari yatakayokuwa yanatumia gesi ili kupunguza gharama za uendeshaji ikiwemo na kushusha bei kwa abiria. Akielezea faida za Gesi, Masumbo amesema mpaka sasa uzalishaji wa umeme unategemea asilimia 50 ya gesi na kupelekea kupungua kwa changamoto ya kukatika kwa umeme. 

Musumbo amesema, wameshaanza kusambaza gesi katika maeneo ga Mlalakuma, Mikocheni, Mbezi, Mwenge na wapo kwenye njiani kusambaza Mkoa wa Mtwara na Lindi na hiyo ni kwa matumizi ya kawaida majumbani. Ameshauri, watu kuagiza magari yanayotumia gesi, au yanayotumia vyote ili kupunguza gharama za uendeshaji.

WEMA SEPETU AACHIWA HURU,AKAMATWA TENA,AZUA 'KASH KASH'.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

BAADA ya Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu mwezi uliopita kufutiwa dhamana na kukaa rumande kwa siku saba, kwa kukiuka masharti ya dhamana na baadae kurudishiwa dhamana yake, leo tena kwa mara nyingine amezua tafrani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatia kugoma kukamatwa baada ya kesi yake kufutwa.

Wema ambae anakabiliwa mahakamani hapo kwa makosa ya kusambaza video za ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani, amegoma kukamatwa na polisi baada ya mahakama hiyo kumwachia huru chini ya kifungu cha sheria cha 225 na kisha kumkamata tena na kumuweka mahabusu.

Baada ya kuachiwa huru leo Julai 4.2019 Wema alitoka nje na wakati askari wakimkamata kwa nguvu, Wema aligoma kukamatwa hali iliyosababisha mvutano kwa muda kati ya askari na mawakili wanaomtetea, Albert Msando na Reuben Simwanza.

Hata hivyo, askari walifanikiwa kumkamata msanii huyo ambae pia ni Miss Tanzania mwaka 2006.

Hatua hiyo imefikwa baada ya wakili wa Serikali, Glory Mwenda kudai mahakamani hapo kwa hana shahidi kwani shahidi aliyemuandaa, Koplo Safi kudai ni mgonjwa.

Hata hivyo, hoja hiyo imepingwa na Wakili Msando kwa madai kwamba haina mashiko kwani mahakama ilishatoa ahirisho la mwisho hivyo hawawezi kuahirisha tena. Amedai kesi hiyo ipo mahakamani hapo kwa zaidi ya siku 60 na upande wa mashtaka wameshindwa kuleta mashahidi, "tunaomba chini ya kifungu namba 225(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 mshtakiwa aachiwe huru".

Kauli hiyo ilipingwa na wakili Mwenda akidai sheria ya siku 60 inatumika pale tu ambapo upelelezi haujakamilika hivyo aliomba kesi iahirishwe.

Hakimu Kasonde, alikubaliana na maombi ya upande wa utetezi kuwa sheria hiyo inatumika wakati wowote hata hivyo alimuachia huru mshtakiwa Wema chini ya kifungu hicho cha sheria

WIZARA YA ELIMU YAIPONGEZA VETA KWA JUHUDI ZA KUWAINUA VIJANA KUPITIA BUNIFU MBALIMBALI

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Michuzi Tv
WIZARA ya Elimu kupitia naibu waziri wa wizara hiyo William Ole Nasha wametoa pongezi kwa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) kwa jitihada wanazoonesha katika kuwainua vijana kwa kuwapa fursa za kujiajiri wenyewe kupitia ubunifu mbalimbali.

Akizungumza Leo katika viwanja vya maonesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea banda la VETA waziri Ole Nasha amesema kuwa matunda ya mamlaka hiyo ya elimu yanaonekana dhahiri kabisa na Kila mwaka VETA inapiga hatua mbele zaidi katika kuzalisha ajira nyingi kwa vijana.

Amesema kuwa vijana watumie fursa zinazotolewa na mamlaka hiyo kwa kupata ujuzi utakao wawezesha kujiajiri wenyewe kupitia fani za ufundi, upishi, kilimo na ufugaji zinazotolewa na mamlaka hiyo na sio kutegemea kuajiriwa pekee.

Aidha amewapongeza VETA kwa kushinda tuzo mbili katika maonesho hayo ya kibiashara ikiwemo tuzo ya taasisi bora ya elimu katika masuala ya ubunifu na kuwashauri  kuwa ubunifu unaooneshwa na vijana hao usiishie katika maonesho pekee bali wawasaidie kupitia bunifu zao.

Vilevile ameelekeza taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kubadilisha mitaala ya elimu huku akitolea mfano mabadiliko ya nyaya za umeme ambapo hadi sasa wanafundishwa kupitia mtaala wa zamani licha ya mabadikiko hayo.

Ole Nasha amewaelekeza time ya sayansi na teknolojia nchini (COSTECH) kuwa karibu na wabunifu hao ili waweze kufika mbali zaidi na kueneza na kutumia maarifa yao.
 Gema Ngoo mkufunzi wa masuala ya kilimo akizungumza na Michuzi Tv na kueleza kuwa vijana wasitegee zaidi katika kujiajiri kwani mafunzo yanayotolewa na VETA ni mtaji tosha wa kuweza kujiajiri, leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa elimu William Ole Nasha (kulia) akisikiliza maelekezo kutoka kwa afisa uhusiano wa VETA Sitta Peter (kushoto)  mara baada ya  kutembelea banda hilo katika  viwanja vya mwalimu Nyerere, Leo jijini Dar es Salaam.

WEMA SEPETU AGOMA KUKAMATWA MAHAKAMANI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
BAADA ya Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu mwezi uliopita kufutiwa dhamana na kukaa rumande kwa siku saba, kwa kukiuka masharti ya dhamana na baadae kurudishiwa dhamana yake, leo tena kwa mara nyingine amezua tafrani  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatia kugoma kukamatwa baada ya kesi yake kufutwa.

Wema ambae anakabiliwa mahakamani hapo kwa makosa ya kusambaza video za ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani, amegoma kukamatwa na polisi baada ya mahakama hiyo kumwachia huru chini ya kifungu cha sheria cha 225 na kisha kumkamata tena na kumuweka mahabusu.

Baada ya kuachiwa huru leo Julai 4, 2019  Wema alitoka nje na wakati askari  wakimkamata kwa nguvu, Wema aligoma kukamatwa hali iliyosababisha mvutano kwa muda kati askari na mawakili wanaomtetea, Albert Msando na Reuben Simwanza.

Hata hivyo, askari walifanikiwa kumkamata msanii huyo ambae pia ni miss Tanzania mwaka 2006.

Hatua hiyo imefikwa baada ya wakili wa Serikali, Glory Mwenda kudai mahakamani hapo kwa hana shahidi kwani shahidi aliyemuandaa, Koplo Safi kudai ni mgonjwa.

Hata hivyo, hoja hiyo imepingwa na Wakili  Msando kwa madai kwamba haina mashiko kwani mahakama ilishatoa ahirisho la mwisho hivyo hawawezi kuahirisha tena.
 Amedai kesi hiyo ipo mahakamani hapo kwa zaidi ya siku 60 na upande wa mashtaka wameshindwa kuleta mashahidi, "tunaomba chini ya kifungu namba 225(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 mshtakiwa aachiwe huru".

Kauli hiyo ilipingwa na wakili Mwenda akidai sheria ya siku 60 inatumika pale tu ambapo upelelezi haujakamilika hivyo aliomba kesi iahirishwe.

Hakimu Kasonde, alikubaliana na maombi ya upande wa utetezi kuwa sheria hiyo inatumika wakati wowote hna hivyo alimuachia huru mshtakiwa Wema chini ya kifungu hicho cha sheria

MTOTO ASIMULIA MAHAKAMANI TUHUMA ZA BABA KUMYONGA MAMA YAKE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MTOTO mwenye umri wa miaka 10, jina (limehifadhiwa) ameisimulia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jinsi alivyoshuhudia  baba yao wa kambo, Godfrey Samweli au Nkwabi akimnyonga mama yake Bahati Hussein na kimsababishia kifo.

Mtoto huyo anayesoma darasa la tatu, leo Julai 3/2019 ameeleza mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu, Pamela Mazengo kuwa alishtuka usingizini wakati wa usiku na kumshuhudia baba yao akimkunja shingo mama yake kama anaivunja na kumwambia asipige kelele.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Erick Shija, kutoa ushahidi  wake dhidi ya kesi ya mauaji inayomkabili Godfrey, mtoto huyo ambae ni shahidi wa tatu kati ya mashahidi watano waliotoa ushahidi leo, amedai mama yake amefariki mwaka 2014.

Akitumia takribani dakika tano kuelezea alichoona, mtoto huyo amedai kuwa, Juni 20,2014 yeye ambae wakati huo alikuwa na miaka mitano akiwa amdogo wake Rahimu ambao walikuwa wanalala chumba kimoja na wazazi wao hao ambapo baba na mama yao wanalala kitandani huku wao wakilala chini kwenye godoro walienda kulala kati ya saa 2 au 3 usiku lakini baadaye usiku alishituka na kuona mama yake akirusha rusha miguu na kumwambia asipige kelele ndipo alipomnyonga mama yao.

Amedai kuwa, alinyamaza hakupiga kelele, baadae usingizi  ulimpitia hadi asubuhi ambapo alipoamka alimuona mama yake akiwa amelala kitandani na hakujua kama alikuwa amekufa,
alifungua mlango wa chumbani ambao haikuwa imefungwa na kutoka nje ambapo alienda kupiga mswaki na kwenda kucheza. Lakini akiwa anacheza alisikia kelele nyumbani kwao na alipofika ndugu zake walimwambia kuwa mama yao amefariki.

Ameongeza kwamba siku hiyo hakumuona baba yake (Godfrey) kuanzia alipoamka

Ameeleza kuwa, kwa marehemu mama yake wamezaliwa watoto wanne ambao ni Hadija, Hassan, Hemed na yeye mwenyewe na kwa baba huyo hakuwa na mtoto na mama yao.

Naye mtoto wa pili wa marehemu, Hadija Juma (16) ambae wakati mama yake anauwawa alikuwa na miaka 10 amedai, Juni 20,2014 alienda kulala kati ya saa 5 au 6 usiku akiwa na mtoto wa mama yake mdogo anayeitwa Mwanahamisi Hussein ambapo usiku mkubwa alisikia mama na baba yake wanagombana na kumpelekea, mdogo wake kuogopa  lakini alimtoa hofu nakumwambia asiogope kwani wanaongea kuhusu ugomvi wao wa mchana.

"Hata hivyo, hatukulala tulikaa kitandani na mdogo wangu akaniambia nimpeleke kukojoa  tukatoka na tulipofunua pazia tulimuona Godfrey akiwa amekaa kwenye kochi huku amevaa kipensi na shati liko begani huku akitokwa na jasho," amedai na kuongeza; walipofika hapo sebuleni, Godfrey alituuliza tunaenda wapi mimi nikamwambia tunaenda kukojoa akatujibu sawa..., tulienda kukojoa na kurudi chumbani...baadaye nilimsikia akifungua mlango wa sebuleni na kutoka nje alipotoka tulijificha nyuma ya mlango wa sebuleni," alidai.

Akiendelea kitoa ushahidi wake, shahidi huyo  wa pili amedai, walimsikia baba yao akigonga mlango wa chumba cha jirani na kumuuliza kama amesikia chochote lakini walisikia yule kijana akimjibu kuwa hajasikia chochote na kumwambia akalale

Shahidi huyo alipoulizwa alijuaje kama aliyekuwa akigonga kwa jirani ni Godfrey alidai kuwa, anaitambua sauti ya baba yake huyo.

Ameendelea kudai kuwa, walisubiri kuona kama baba yao kama angeingia ndani lakini hawakusikia chochote mpaka wakapotiwa na usingizi hadi asubuhi alipoamshwa na mama mwenye nyumba akimtaka apeleke vyombo chumbani kwa mama yake.

Akadai, aligonga chumbani kwa mama yake zaidi ya mara moja lakini hakufungua na alipofungua mlango alimuona mama yake akiwa amefunikwa shuka jeupe na alipomfunua aliona kipande cha kanga mdomoni, alama za kucha shingoni na alianza kumtingisha huku akimuita lakini hakuitika na mapigo ya moyo yakiwa yamesimama.


Amedai alipiga kelele huku akikimbilia nje ndipo mama mwenye nyumba alimuuliza kuna nini na alipomwambia alikataa kuingia ndani na kwenda kumuita mama yake mdogo ambaye nae aliogopa kuingia ndani humo mpaka majirani walipofika pamoja na dada yake Hadija Shaban ambao waliingia ndani na kumuhifadhi mama yao kisha wakampeleka polisi na baadae hosp. Ambapo alipewa taarifa ya kifo baadae baada ya ndugu zake kutoka hospitali ya Amana.

"Kabla mama hajafariki aliwahi kuniambia kwamba akifa atakayemuua ni Godfrey. Lakini kuna kipindi niliwahi kumsikia mara mbili akimwambia mama kwamba atamuua na familia yetu popote itakapoiona ataiua. Pia kuliwahi kuwa na ugomvi kati ya mama na Godfrey akitaka kuuza nyumba tuliokuwa tumepanga na mama alimkataza," alidai Hadija.

Naye, sahidi wa kwanza katika kesi hiyo ya mauaji, Hadija Shabani (26)  amedai Juni 20, 2014 alienda kwa shangazi yake Bahati na kumkuta na ugomvi baada ya Godfrey kumuhisi mkewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi na jirani yake.

Shabani alidai baada ya marumbano ya muda mrefu alifika Mrisho Hussein ambaye ni mdogo wa shangazi yao na kusuluhisha ugomvi huo na yeye aliondoka Ulongoni saa 2 usiku kwenda nyumbani kwake Vingunguti.

Alidai saa 11 alfajiri alipigiwa simu na Godfrey akimtaka aongee na shangazi yake akamwambia hawezi kwenda nyumbani muda huo asubiri hadi asubuhi na alipofika nyumbani kwa Bahati walimkuta akiwa amefunikwa na alama za kucha shingoni na walimpeleka hospitali na kugundulika amekufa.

Mama mwenye nyumba waliyopanga Godfrey na Bahati, Fatuma Adam (46) alidai hakusikia ugomvi usiku wa tukio na siku iliyofuata alisikia mtoto wa marehemu akipiga kelele na kwenda kumuita  mdogo wa marehemu  na walisaidia kumuhifadhi marehemu.

Alidai walipomkagua marehemu walimuona na alama za kucha shingoni na kwamba walipompeleka hospitali waliambiwa amefariki.

Hata hivyo, shahidi wa tano alitoa ushahidi wake kuhusu tukio hilo na mahakama iliahirisha kesi hadi Julai 9, mwaka huu kwa kusikilizwa.

Katika kesi hiyo inadaiwai Juni 21, 2014 huko Ulongoni A wilayani Ilala, Dar es Salaam, Godfrey alimuua k wa makusudi mke wake Bahati Hussein.
Mtuhumiwa Godfrey Samwel akitoka katika ukumbi wa wazi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo kesi yake ya mauaji dhidi ya mke wake ilikuwa inasikilizwa ambapo mashahidi watano wametoa ushahidi wao wakiwemo watoto wa marehemu.

Rais Magufuli kuzindua hifadhi ya Taifa ya Burigi, Chato

$
0
0
Na Humphrey Shao, Michuzi Tv, Mwanza
Rais Dk. John Magufuli anatarajia kuzindua rasmi Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato Julai 9 mwaka huu.
 Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangala wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  mwaka 2019 wa TANAPA  kwa Wahariri na Wanahabari Waandamizi uliofanyika jijini Mwanza.

Awali hifadhi ya taifa ya Burigi  CHATO ilikua pori la akiba lililojulikana kwa jina la Burigi kabla ya kupandishwa hadhi na TANAPA.

Mkutano huo umebeba kauli mbiu "Miaka 60 ya Tanapa kuimarisha uhifadhi pamoja na kupanua wigo na fursa za Utalii Kusini Magharibi na kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Aidha Waziri Kigwangala amesema kuwa Uhifadhi wa rasilimali za misitu na vyanzo vya maji pamoja na wanyamapori ni kitu pekee ambacho kinaweza kuendelea kutusaidia kuwa na uchumi imara hapo mbeleni.

Ametaja kuwa sekta ya Utalii uchangia zaidi ya asilimia 17.6 katika pato la Taifa na ajira za moja kwa moja ni laki sita huku watu zaidi ya milioni mbili wakiwa wameajiriwa katika mfumo usio rasmi.

Anasema kuwa uhifadhi umekuwa  na faida kubwa Sana kwa watanzania sio kwa kuleta kipato tu bali hata katika mfumo wa ecolojia ya maisha ya binadamu kwani sisi tunapata oxygen safi kutokana na uhifadhi mzuri wa misitu.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dr Hamisi Kigwangala akizungumza na wahariri pamoja na waandishi waandamizi katika mkutano wa mwaka unaofanyika jijini Mwanza
 Kamishna Wa huifadhi Tanapa, Allan Kijazi akitoa someone juu ya mabadiliko kutoka mfumo wa kiraia kwenda jeshi usu
 Kamishna wa Mawasiliano wa Tanapa, Pascal Shelutete akitoa utambulisho was wanahabari kwa Waziri.
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Kigwangala kuzungumza na Wahariri.
 Mhariri was gazeti la Jamhuri Jackton Manyerere akichangia mada katika mkutano huo
 Baadhi ya Wahariri wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo
Waziri Dr Hamisi Kigwangala akiwa katika picha ya pamoja na washiriki

WAZIRI LUGOLA AWATAKA WANANCHI KUDUMISHA AMANI, WAOGOPE NJAA KAMA UKOMA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akikagua ujenzi wa darasa wa Shule ya Msingi Kamulebya, Kijiji cha Buzimbwe, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwataka wananchi wachape kazi. Waziri Lugola pia alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa madarasa ya shule na Zanahati. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkazi wa Kijiji cha Kamulebya, Kata ya Butimba, Jimbo la
Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, Wambura Chacha Wambura, akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kufanya kazi. Lugola aliwapa nafasi wananchi kutoa kero zao ndani ya Jimbo lake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Diwani wa
Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa
Mara, Abyudi Mugesi, wakati alipokuwa anawasili Kijiji cha
Buzimbwe kwa ajili ya kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi
wa Kijiji hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Felix Mwagara, Mwibara (MOHA) 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka wakazi wa Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, kuilinda amani iliyopo nchini ili waweze kuendelea kufanya shughuli zao za kilimo wakiwa na amani. 

Lugola ameyasema hayo leo, katika Kata ya Butimba, jimboni kwake, alipokuwa anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwiseni, mara baada ya kushiriki shughuli za mazishi ya mtoto wa dada yake katika Kijiji hicho, aliyefariki hivi wiki hii mkoani Mwanza. 

Lugola alisema Tanzania ina amani kwasababu inautamaduni wa kuwa na amani, hivyo asitokee mtu akaharibu utamaduni huo ambao nchi inaendelea kuhudumisha. 

“Ndugu zangu wana Mwiseni, Wana Mwibara, amani tulionalo ndiyo inatuwezesha leo tunalima vizuri, tunavua samaki, leo tunakula vizuri, leo tunafanya shughuli mbalimbali za maendeleo, hivyo tuendelee kuitunza amani hii,” alisema Lugola. 

Aliongeza kuwa, Wizara yake kupitia Jeshi la Polisi ipo imara, Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli ipo imara na inaendelea kuwalinda Watanzania mahali popote walipo nchini, na hakuna mtu atakaye ivunja amani hiyo. 

Aidha, Lugola aliwataka wananchi hao kuhifadhi vyakula vizuri ili kuepusha janga la njaa kwa hapo baadaye na kusababisha wananchi kuja kuteseka kwa ukosefu wa vyakula na kusababisha mateso katika familia. 

“Tutunzeni vyakula vyetu, msitumie hovyo, kuweni makini na matumizi ya vyakula, sitaki nije kuona mnateseka na njaa, hakikisheni mnatunza vyakula kwa ajili ya matumizi ya baadaye, ogopeni njaa kama ukoma,” alisema Lugola. 

Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, alifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo akikagua madarasa ya shule ya msingi pamoja na zahanati. 

“Nataka hili darasa likamilike kwa wakati, natoa mifuko ya saruji 100 ili kuikalimisha zahanati hii katika Kata hii, na pia nitaleta mabati ili maendeleo yazidi kuwafikia wananchi wa jimbo hili,” alisema Lugola. 

Waziri Lugola ameanza ziara yake leo, ambapo anatarajia kufanya ziara hiyo katika vijiji vya Kata zote jimboni humo.

WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA ATEMBELEA BANDA LA MOBISOL NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ametoa pongezi kwa kampuni ya Mobisol kwa juhudi wanazozifanya kwa kusambaza nishati ya nguvu ya jua (solar power) nchi nzima.

Pinda amesema hayo leo alipotembelea banda la Kampuni hiyo liliopo ndani ya Karume Hall wakishiriki maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika banda hilo, Pinda amepata maelekezo mbalimbali kuhusiana na vifaa vinavyotumia nishati jmya nguvu ya jua na namna vinavyofanya kazi kwenye Televisheni, Jokofu na hata feni ambazo vyote vinapatikana kwao.

Meneja masoko wa Mobisol, Seph Materu amesema kuwa kampuni yao imesambaa nchi nzima isipokuwa Mtwara ila wapo mbioni kuweka tawi lao kwenye Mkoa huo.

Materu amesema, watanzania wengi wanaamini kuwa solar ni kwa ajili ya kuwasha taa tu ila inafanya kazi kubwa sana ikiwemo kuwasha televisheni, majokofu na hata vifaa vingine vya umeme.

Amesema kampuni yao imekuwa inasambaza umeme huo kwenye mikoa mbalimbali ila changamoto kubwa ni elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya nishati hiyo ila wamekuwa wanaelewa na kuanza kutumia bidhaa za mobisol. 

Aidha, kampuni ya Mobisol ina solar kubwa zinazoweza kuwasha hospital, mashuleni pia wanauza bidhaa zao kwa kulipa kidogo kidogo na kuwataka wananchi watembelee banda lao na kujionea namna nishati jua inavyofanya kazi.

Kampuni ya Mobisol ipo nchini toka mwaka 2015 na imejizatiti kuondoa kero ya umeme kwa wananchi wa mjini na vijijini kote nchini.
.Afisa Masoko wa Mobisol Farid Abdallah (kulia) akitoa maelezo kwa  Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda  na Mkurugenzi wa TANTRADE Edwin Rutageruka walipotembelea banda la Kampuni ya Mobisol katika maonesho ya  43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan awasili Nchini Niger

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu wa Niger Mhe. Brigi Rafini alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Diori Hamani, Niamey Nchini Niger. Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa 12 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali kuhusu Eneo Huru la Biashara Afrika(African Continental Free Trade Area-AfCFTA) (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

TANZANIA BILA DENGUE INAWEZEKANA

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (aliyevaa buti) akiongoza zoezi la upuliziaji wa viuadudu katika Manispaa ya Kinondoni 


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (aliyevaa buti) wakielekea katika eneo lenye mazalia ya mbu wanaosababisha homa ya Dengue, zoezi limefanyika katika eneo la Msisili Manispaa ya Kinondoni. 
*************** 

Na WAMJW-DSM 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. @ummymwalimu leo ametembelea katika Manispaa ya Kinondoni ikiwa ni muendelezo wa ziara yake kukagua utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa Mikoa/Halmashauri ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Dengue. 

Katika ziara hiyo Waziri @ummymwalimu ameridhishwa kwa kiasi kikubwa na jitihada zinazochukuliwa na Manispaa ya Kinondoni za kupambana na Ugonjwa wa Homa ya Dengue hali iliyochangia kupungua kwa Idadi ya Wagonjwa kutoka Wagonjwa 604 Mwezi Mei hadi kufikia Wagonjwa 450 Mwezi Juni. 

“ Nafurahi kuona kwamba idadi ya Wagonjwa wa homa ya Dengue katika Wilaya ya Kinondoni, Mwezi Mei kulikuwa na Wagonjwa ambao wamepima na kuthibitishwa 604, lakini mwezi wa tano Wagonjwa wamepungua hadi 450” Alisema Waziri Ummy 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa, takwimu za Kitaifa za Wizara ya Afya, mwezi Mei tulikuwa na idadi ya Wagonjwa wa homa ya Dengue 3170, na wamepungua Mwezi wa Sita hadi kufikia Wagonjwa 1446, hali inayotoa matumaini katika kuimaliza vita hii ya homa ya Dengue. 

Aidha, Waziri Ummy amewapongeza Watendaji wa Sekta ya Afya katika Manispaa ya Kinondoni kwa hatua wanazoendelea kuchukua, ikiwemo kununua Viuadudu vya kuangamiza mazalia ya mbu na kununua mashine mpya za kupuliza dawa (motorised sprayers), katika maeneo yenye mazalia ya mbu. 

Mbali na hayo, Waziri Ummy amesisitiza juu ya ushiriki wa Wananchi katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa homa ya Dengue, huku akieleza kuwa mapambano dhidi ya mbu wa Dengue yatasaidia kupunguza magonjwa mengine kama Malaria, Matende, Chikungunya, Zika, Homa ya Manjano. 

“Ushiriki wa Wananchi ni muhimu sana katika kupambana na ugonjwa wa Dengue, tukipambana na Dengue, kwa upande mwingine tunakuwa tunapambana na ugonjwa wa Malaria, Matende, Chikungunya, Zika, Homa ya Manjano, kwhiyo ni lazima tuhakikishe kila mtu anashiriki katika kupambana dhidi ya mbu.” Alisema Waziri Ummy. 

Kwa upande wake Mbunge wa Kinondoni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Maulid Mtulia amekazia kwa kuwahasa Wananchi juu ya ushiriki katika vita hii dhidi ya ugonjwa wa Dengue na kusisitiza kuwa Serikali haiwezi kushinda vita hii bila ushirikiano wa Wananchi. 

Nae, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Sitta amesema kuwa Jumla ya shilingi Milion 132 kwaajili ya zoezi lakutokomeza homa ya Dengue, 90 zimetumika kwaajili ya zoezi zima la upuliziaji wa viuadudu katika mazalia ya mbu, huku 42 kwaajili ya kununua Mashine za kubwa ya upuliziaji wa dawa hizo. 

“Tumetumia gharama ya takribani Milion 90 kwaajili ya upuliziaji katika kila kata na tupo mbioni kuongeza Milioni 42 kwajili ya mashine kubwa yenye uwezo wa kusambaza mara moja kwa kata 10, kwahiyo kwa ujumla tutakuwa tumetumia takribani Milion 132 kwaajili ya zoezi la kuhakikisha tunatokomeza ugonjwa wa Dengue.” Alisema Mhe. Benjami Sitta. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Festo amesisitiza kuwa Huduma za vipimo vya homa ya Dengu zinapatikana katika vituo vya Serikali vya Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na Hospitali ya Lugalo bila malipo na vituo binafsi bei elekezi isizidi shilingi 50,000/ 

“Huduma hizi za vipimo zinapatikana kwenye vituo vyetu, na katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na Hospitali ya Lugalo bila malipo, lakini katika vituo binafsi, bei elekezi isizidi 50,000/ kwa kipimo cha Dengue” alisema Dkt. Festo 

Pia, amewaasa Wananchi kuwahi katika vituo vya Afya, pindi waonapo dalili za ugonjwa wa homa ya Dengue na kuachana na mawazo potofu ya matibabu ya Dengue kama majani ya mpapai kwani yanawezapelekea kupata matatizo mengine yakiafya.

Marufuku mbolea kuchelewa kufika kwa wakulima – Mhe Hasunga

$
0
0





Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Serikali imetangaza kiama kwa wanaochelewesha mbolea kuwafikia wakulima kwa wakati kwani kuchelewa kwa mbolea ni miongoni mwa sababu zinazopunguza uzalishaji wa mazao mbalimbali ya wakulima nchini.

Mbolea kutofika kwa wakulima kwa wakati ni wazi kuwa Taasisi iliyopewa jukumu la kusimamia na kudhibiti mbolea ya TFRA imeshindwa kufanya kazi yake kwa ufasaha hivyo ikibainika kuchelewa kwa mbolea pasina sababu za msingi watendaji hao watachukuliwa hatua za kisheria.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa kauli hiyo ya onyo leo tarehe 4 Julai 2019 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye kikao kazi na wafanyakazi wa Taasisi ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA).

Alisema kuwa mbolea inayohitajika kwa wakulima ni Lazima ipatikane kwa wakati katika maeneo ya kilimo. “Kupatikana kwa wakati maana yake ni kwamba kila mtu anapoishi anapaswa kuipata kirahisi kupitia maduka au masoko” Alisema

Aliongeza kuwa kazi ya Taasisi ya udhibiti wa mbolea Tanzania ni kuhakikisha mbolea inawafikia wakulima sio kusalia Jijini Dar es salaam ilihali wakulima wapo mikoa yote Tanzania na endapo mbolea ikikosekana kwa wakulima watendaji wa TFRA watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Kadhalika alisema kuwa kupatikana pekee kwa mbolea kwa wakulima ni jambo moja lakini muhimu ni kuwa na bei nafuu ambazo wakulima wataweza kuzimudu.

“Sasa hivi kuna malalamiko mengi kwa wakulima kuwa mbolea zinauzwa bei ya juu hivyo wameshindwa kuzimudu, haiwezekani mbolea itoke Ulaya ikiwa na bei nafuu lakini kumfikia mkulima inakuwa na bei ghali, hapo ni wazi kuwa TFRA hamjafanya kazi yenu sawasawa” Alikaririwa Mhe Hasunga

Alisema kuwa endapo TFRA itatekeleza majukumu yake ipasavyo mbolea itapungua bei na wakulima watanufaika na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Tanzania.

“Na kama tatizo la gharama linaongezeka kutokana na usafirishaji kuna sababu gani za kutumia magari kusafirisha wakati kuna usafiri muhimu wa reli (TRC) ambapo mawakala wangepakua na kusambaza mizigo hiyo baada ya kufika katika maeneo mbalimbali inapoishia reli” Alisema

Hata hivyo amesisitiza kuwa serikali imeanzisha mchakato wa kupitia mbolea kote nchini ili uagizaji wa mbolea iweze kuagizwa itakayoendana na uwezo wa udongo.

Makete yaja viwanda vya Mianzi badala ya kunywa Ulanzi

$
0
0
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa MDA wakifuatilia mada mbalimbali juu ya uwekezaji wilayani Makete 
Festo Sanga kushoto akiwa na washiriki wengine kwenye mkutano huo wakimsikiliza mkurugenzi wa kituo cha Uwekezaji Bw. Geofrey Mwambe juu ya fursa zilizopo wilayani Makete 


Na Danny Tweve- Mianzi 

Wilaya ya Makete inajipanga kutumia raslimali zilizomo ikiwemo mianzi kuanzisha viwanda vya usindikaji wa vijiti vya Meno (toothpeak) ambavyo licha ya wingi wa mmea huo katika mikoa ya Iringa na Njombe bado Tanzania imeshindwa kuwa na kiwanda cha aina hiyo. 

Mikoa hiyo miwili imekuwa maarufu kwa uzalishaji wa pombe ya Ulanzi ambayo kwa karne sasa licha ya matumizi ya wakazi wake kwaajili ya burudani ya kilevi,bado tafiti za namna ya kusindika hazijaweza kufanikishwa licha ya njia za asili za uhifadhi ambazo hata hivyo hazijaweza kuthibitisha ubora wake. 

Akizungumza kwenye mkutano wa Chama cha Maendeleo Makete (MDA) uliomalizika juzi katika Hotel ya Nefaland jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wake Bw. Clement Sanga, alisema tayari wilaya imeainisha maeneo kadhaa ya uwekezaji ambayo sasa inayawataka wafanyabiashara walio nje ya wilaya hiyo kwenda kufungua viwanda. 

Kulingana na takwimu kutoka ndaki ya misitu ya Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine, Tanzania ina hekta za mianzi 127,824 ambapo kwa nchini kuna jamii nne ambazo kwa pamoja zina uwezo wa kudumu kwa miaka 50 zikitoa faida kwa wazalishaji kwa kipindi chote, hata hivyo bado matumizi yam mea huo bado yamekuwa hayana tija kiuchumi ukiachilia kijamii kwenye burudani yta pombe ya ulanzi. 

Miongoni mwa bidhaa za mianzi kulingana na utafiti uliofanywa na ndaki hiyo ni pamoja na samani za ndani kama Makabati, meza, vitanda,vikapu na kwamba zaidi ya bidhaa 1500 zinaweza kutengenezwa na Mianzi. Rwanda katika Afrika ndiyo nchi pekee iliyotengeneza sera ya Muanzi ya 2011 baada ya kutambua faida za mmea huo kibiashara. 

Kulingana na Mwenyekiti huyo , baadhi ya viwanda vinavyotajwa wilayani Makete ni pamoja na mahitaji ya kiwanda cha usindikaji wa juisi za matufaa (apple) ambapo wilaya ya Makete ni moja ya maeneo ambayo wafanyabiashara wa matunda wamekuwa wakitangaza kuwa yanatoka nchini Afrika Kusini wakati ukweli yanazalishwa hapa hapa nchini hasa wilaya ya Makete na Njombe. 

Katika kutekeleza mkakati huo, Umoja huo umeitisha mkutano huo ukihusisha wafanyabiashara wa jamii ya WanaMakete kutoka maeneo mbalimbali duniani ambako wawakilishi kutoka wafanyabiashara maarufu kama wakinga wanaoishi China walionyesha nia ya kujenga viwanda kwa kutumia teknolojia ndogo ndogo zinazopatikana nchini humo. 

Vipaumbele katika hamasa hiyo ni kutumia fursa ya rasrimali zilizopo wilayani humo zikiwemo vyanzo vya maji safi na salama vya asili ambavyo vinaweza pia kutumika kuanzisha viwanda vya maji ya kunywa nay a dawa(drips), umeme wa maji na bidhaa nyingine za mianzi zikiwemo samani za ndani. 

Katika ufunguzi wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Godfrey Mwambe amesema, jukumu la taasisi yake ni kuhakikisha inatafsiri maono ya serikali ya awamu hii ikiwa ni pamoja na kushauri uanzishwaji wa mifumo itakayosaidia ukuaji wa sketa binafsi na kupitia Ubia. 

Alisema mtazamo wa Chama cha MDA, kwa sasa wanapaswa kuangalia pia uwekezano wa kuanzisha Kampuni ya Uwekezaji Makete sambamba na Mfuko wa Maendeleo wa Makete ambapo kupitia vyombo hivyo vitasaidia kukuza shughuli za uwekezaji wilayani wilayani humo. 

Ametolea mfano fursa zilizopo kwenye Hifadhi ya Kitulo, kuwa bado hazijatumika vyema kutokana na namna hifadhi hiyo ilivyoanza kupata umaarufu kutokana na upatikanaji wa maua na mimea ambayo watu kutoka nje wanatamani kufika na kutumia bustani hiyo kwa mapumziko ingawa bado hakuna hoteli zenye mvuto kwenye ukanda huo. 

Mkutano huo wa Mwaka wa Chama cha Maendeleo Makete kwa mwaka 2019 umedhaminiwa na Benki ya NMB na umeshirikisha wanachama kutoka mikoa yote ya Tanzania na wawakilishi wa wafanyabiashara wana-Makete kutoka nchi za China na Hong Kong ambako wamejiimarisha zaidi kibiashara.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images