Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

TTCL YAVUNA WATEJA WAPYA 215,000 NA KUTEKELEZA AGIZO WITO WA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Mtoa huduma kwa wateja wa Shirika la Mawasiliano Nchini (TTCL) akiwahudumia  wateja mbalimbali waliofika katika Banda la Shirika hilo kwa ajili ya kupata taarifa kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Mtoa huduma kwa Wateja katika Shirika la Mawasiliano Nchini (TTCL) Halima Mtui akimhudumia mmoja wa wateja waliofika katika Shirika hilo kwa ajili ya kupata taarifa kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 


SHIRIKA la Mawasiliano Nchini (TTCL) katika kipindi cha siku 30 limeweza kusajili wateja wapya 215,000, ikiwa ni Mpango Mkakati wa Shirika hilo katika kujiinua kibiashara na kuongeza wigo huduma ya Mawasiliano kwa Watanzania ikiwa ni utekezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli. 

Akizungumza leo Alhamisi (Julai 4, 2019) katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere, Meneja Mawasiliano wa TTCL Nicodemus Mushi alisema Shirika hilo limetekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilolitoa kwa Shirika hilo tarehe 21 Mei, mwaka huu. 

Mushi alisema hadi sasa huduma za Mawasiliano za Kampuni hiyo katika Mfumo wa 4G zinapatikana katika Mikoa 16 nchini na mpango uliopo ni kuhakikisha kuwa maeneo yaliyobaki yanapata huduma za Shirika kupitia Mpango Mkakati wa Shirika hilo uliojiwekea na hivyo kuweza kuleta ushindani wa huduma ya mawasiliano na makampuni mengine nchini. 

“Mwaka uliopita tulijiwekea Mpango Mkakati wetu ambao utahakikisha kuwa tunaweza kuleta ushindani na makampuni mengine na hivi sasa kama unavyoona tumeweza kupata wateja wapya 215,000 na kupitia maonesho hayo tutaweza kuongeza wateja wengi zaidi ” alisema Mushi. 

Aliongeza kuwa kwa sasa Shirika hilo limeweza kupata wateja wengi zaidi wakiwemo watumishi wa serikali, ambapo kwa kutambua umuhimu huo, TTCL imeanzisha kifurushi maalum cha ‘watumishi pack’ ambacho kinaweza kutumiwa na wafanyakazi wote wa serikali kwa kuweza kukamilisha taratibu mbalimbali ikiwemo vitambulisho vya kazi. 

Akifafanua zaidi Mushi, alisema kauli zinatolewa na watu mbalimbali kuhusu kauli ya Rais Dkt. John Magufuli kuwataka wafanyakazi wa serikali kutumia huduma za mawasiliano za shirika hilo, ni kuwa zitawahusu watumishi wa umma ambao wanalipiwa huduma za mawasiliano ya simu na serikali na si kinyume na maelekezo hayo. 

Aliongeza kuwa malengo ya Taasisi hiyo ni kuweza kujipanga ili kuendelea kutoa huduma bora na zenye viwango ili kuweza kuongoza na kuwa kampuni bora ya mawasiliano inayotoa huduma bora kwa wateja wake nchini. 

“Sisi kwa upande wetu tumeendelea kuwalipa vizuri mawakala wetu ikiwemo kutoa kamisheni nzuri kwao ili kuhakikisha kuwa huduma zetu zinazotolewa zinakuwa zinakidhi matakwa ya wateja na soko la mawasiliano kwa ujumla” alisema Mushi.

WAZIRI KAMWELE AFANYA MAZUNGUMZO NA WAMILIKI WA MELI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele akizungumza na wamiliki wa meli Duniani kuhusu namna watakavyofanya kazi nao ili kuongeza ufanisi kwenye bandari ya Dar es Salaam pamoja na kuangalia namna watakavyoweza kuunguza muda wa meli zenye mizigo kukaa bandarini ili kuhudumia meli nyingi wakati wa kikao hicho kilichofanyka katika ukumbi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi akizungumza na wamiliki wa meli Duniani kuhusu uhusiano uliopo kati ya Tanzania pamoja na nchi majirani katika ufanyaji wa biashara pamoja na kutoa historia ya Tanzania  kabla na baada ya ukoloni wakati wa kikao ili kuwahamasiha wamiliki hao kuweza kuleta meli zao kwa kutumia Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akizungumza na wamiliki wa meli pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wamiliki wa Meli wakiwasilisha changamoto kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele wanazozipata pale wanapotumia bandari ya Dar es Salaam wakati wa kikao kilichoandaliwa na Waziri huyo ili kutatua changamoto hizo ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) .
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko(katikati) akifuatilia kwa umakini kikao cha wamiliki wa Meli kilichoitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele ili kuweza kutatua changamoto wanazozipata katika Bandari ya Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wizara, Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na wamilii wa meli wakiwa kwenye kikao kilichoitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele ili kusikiliza changamoto wanazozipata wafanyabishara hao pale wanapotumia Bandari ya Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cha wamiliki wa meli pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kilichoandaliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele ili kuweza kutatua changamoto ili kuweza kuingeza ufanisi wa bandari hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele akizunguza na waandishi wa habari kuhusu baadhi ya changamoto wanazozipata wamiliki wa Meli kama vile tatizo la mzigo kukaa kwenye maji unakuwa na gharama kubwa  pamoja na kuondoa urasimu wowote kwenye masuala ya uendeshaji wa Bandari ili kuongezeka kwa meli zitazokuwa zinaleta mizogo kwenye bandari hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa gati nyingine ambayo itaongeza ufanisi wa bandari hiyo mara baada ya kumalizika kwa kikao cha wamiliki wa meli kilichoandaliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akiwaonesha meli ya kwanza iliyotia naga kwenye gati mpya na kuweza kushusha mbolea wakati wa wamiliki wa meli walipotembelea badari ya Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele akizungumza na wamiliki wa meli walipotembelea Bandari ya Dar es Salaam ili kujionea ufanisi wa bandari hiyo.

Wizara ya Mifugo na Uvuvi yangara Maonesho ya 43 Kimataifa

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imengara katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa kwa kuwa mshindi wa Tatu katika kundi la Wziara zinazoshiriki maonesho hayo.

Akizungumza na Michuzi Blog Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Rehema Mbulalemi amesema  kuwa ushindi huo umetokana na wizara kujipanga na kuahidi kuboresha zaidi na kuwa mashindi wa kwanza maonesho yajayo ya 2020.

Amesema kuwa wananchi watembelee banda la Wizara hiyo katika kupata elimu mbalimbali ikiwemo sekta ya Mifugo na Uvuvi. Rehema amesema kuna mabadiliko mbalimbali yameganyika katika sekta hizo katika kwenda na mahitaji ya wananchi. Aidha amesema kuwa katika sekta ya Mifugo na Uvuvi zinakwenda sambamba katika uchumi wa Viwanda ambapo ni fursa ya wadau kuchangamkia kuwekeza sekta hiyo.

Kwa upande Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) limewataka wananchi na hasa wavuvi kujitokeza kwa wingi Wizarani kuchukuwa fomu za kujiunga na kozi fupi za ufugaji wa samaki na ulinzi wa Mazingira. Wamesema kuwa kuna haja ya wananchi kujua namna ya kufuga samaki ili kuweza kupata tija katika mradi wake kuliko kufanya shughuli hiyo kimazoea.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Ufugaji viumbe kwenye Maji Emmanuel Magesa amesema kuwa Wakala wanatoa kozi mbalimbali zikiwemo  fupi na ndefu hivyo wananchi na hususani wavuvi wajitokeza kwa wingi ili kuchangamkia fursa hiyo.

"Jukumu kubwa  la FETA  ni kutoa elimu katika upande wa Uvuvi kwani waje wananchi katika Ofisi z Wizara na katika maonyesho ya sabasaba ili kupata fomu na kusoma kozi zinazohusika ufugaji" alisema. Amesema kuwa kuna kozi zinazohusika watu walioishia kidato cha nne ambao watasoma kwa mwaka mmoja na wale wakidato cha sita watasoma kwa miaka miwili na akifanya vizuri anapata fursa ya kwenda chuo kikuu.

Alisema moja ya kozi ni kama vile ufugaji wa samaki,kuogelea,kutengeneza nyavu,mitambo ya baharini,pamoja na usimamizi wa Mazingira hivyo wajitokeze kuchukuwa fomu na wajiunge na kozi hizo.

 Pia alisema Wakala ya  Elimu na Mafunzo ya Uvuvi  FETA wanafanya tafiti mbalimbali za Uvuvi wa samaki na usimamizi wa rasilimali za bahari. Alisema lengo za tafiti hizo pia nikuongeza thamani katika.mazao ya bahari na kumekuwa na mwitikio mkubwa na wananchi wamejitokeza kwa wingi katika kufahamu ufugaji wa samaki ardhini .

"Kimsingi watu wamezoea kuona katika  samaki wanapatikana baharini ,Mito,pamoja na maziwa lakini sasa mahitaji ni makubwa hivyo wananchi wanaingia ufugaji wa ardhini"alisema
 Wananchi wakipata maelezo kuhusiana na Ufugaji wa Samaki katika eneo dogo wakati walipotembelea banda la Wakala ya Elimu ya  Mafunzo ya Uvuvi (FETA) katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Idara ya Ufugaji Viumbe Majini Wakala ya Elimu ya Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Emmanuel Magesa akizungumza na muandishi wa habari katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ufugaji wa Samaki katika Maonesho ya Sabasaba.

VETA yafurika watembeleaji katika Maonesho ya 43 Biashara Kimataifa

$
0
0
 Mbunifu wa VETA akionesha umahiri wa utengenazaji wa kiti ambacho kinaweza kutumika katika kunyoshea nguo wakati wa Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwalimu wa VETA Kibaha Haji Sanani akionesha umahiri utengenazaji bidhaa mbalimbali wakati Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa VETA Njilo Mkoani Arusha Abdul Abedi akionesha namna ya kutengeneza mchapalo wa kinywaji kwa kuchanganya vimiminika tofauti vya Juisi wakati walipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Wananchi wakipata maelezo kwa Mratibu wa Wanagezi wa Chuo cha VETA Moshi Theresa Mosha katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ngazi inayoenekana wakati mwingine kinaweza kutumika kama kiti ni ubunifu wa VETA katika Maonesho ya Sababa.

VITENDO VYA UKATILI MKOANI DODOMA VINAZIDI KUONGEZEKA

$
0
0
LICHA ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali pamojana na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu na vitendo vya ukatili wa kijinsia, lakini inaelezwa kuwa bado mkoani Dodoma vitendo hivyo vinazidi kushamili katika maeneo mbalimbali mkoani humo. 

Akizungumza na wanahabari juu ya utendaji wa jeshi la polisi mkoani humo, Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna msaidizi wa polisi, Gilles Muroto amebainisha kuwa vitendo hivyo vimezidi kushamimiri mkoani humo, amesema katika tukio la kwanza. 

Katika kijiji cha Mlazo, tarafa ya Mpyayungu, Wilaya ya Chamwino, Makame Wambura, (28) na mtoto wake Fidelika Walioba miezi mitatu(3) baada ya kumwagiwa mafuta ya petrol na mume wake aitwae Elias Warioba (30) na wote wawili kujeruhiwa vibaya na wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, na hapa kamanda anaelezea tukio lilivyotokea.
“Mnamo tarehe28,06,2019, katika jiji cha Mlazo Tarafa ya Mpyayungu Wilayani chamwino, Makame Wambura(28) na motto wake miezi 3 walijeruhiwa kwa kuchomwa moto baada ya kumwagiwa mafuta ya petrol na mume wake Elias Warioba” amesema. 

Tukio la pili katika kijiji cha Manchali, tarafa ya Chilonwa, Wilayani Chamwino, walimkamata Mazengo Chilatu(28) kwa kosa la kumlawiti mama yake mzazi ambaye hakujulikana jina wala umri wake kwa kumvizia akiwa amelala. 

“Huko katika kijiji cha Manchali tarafa ya Chilonwa, wilaya ya Chamwino tumemkamata Mazengo Chilatu(28) kwa kosa la kumlawiti mama yake mzazi ambapo alimvamia alimvamia chumbani akiwa amelala na kumfanyia kitendo hicho” amesema. 

Katika tukio la tatu huko katika eneo la Nane nane kata ya Nzuguni, Dodoma Mjini, kikongwe wa miaka 95, mkazi wa eneo hilo alibakwa na kijana mmoja Donald Justine(25) aliyemvizia akiwa amelala na kumkaba shingoni kasha kumtendea ubaya huo. 

“Na katika eneo la nanenane kata ya nzuguni halmashauri ya Jiji la Dodoma kijana mmoja Donald Jastine (25) mkazi wa eneo hilo alimbaka bibi kizee mwenye umri wa miaka 95 kwa kumvamia na kumtendea kitendo hicho, chanzo ni ulevi uliopindukia na imani za kishirikina” amesema. 

Lingine katika eneo la Maili mbili jijini humo ,ni tukio la Mwanaume mmoja anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25- 30 ambaye hakufahamika jina lake alifanya matukio matatu ya ubakaji kabla ya kukamatwa na wananchi na kupigwa na wananchi kabla ya kuokolewa na polisi na baadaye kufariki. 

Ambapo alifanya matukio hayo kwa watu watatu tofauti kabla ya jana kukamatwa na wananchi wenye hasira kali na kuupigwa vibaya na kuokolewa na jeshi la polisi hata hivyo alifariki baadaye. 

Aidha amepongeza kazi nzuri inayofanyawa na wanahabari katika kuripoti habari za ukatili huo, ambapo amesema kwa sasa kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi kuripoti matukio hayo kwa jeshi la polisi.
“kutokana na kuripoti kwenu habari hizi za ukatili tumeona sasa muamuko ni mkubwa sana kwa sasa katika kuripoti wananchi matukio haya yanapotokea katika maeneo yao” amesema. 

Pia amebainisha kuwa matokeo ya kuripoti matukio hayo ambapo kwa mwaka 2018 yalilipotiwa matukio mia moja sabini a nne(174) na kwa mwaka 2019 ni matukio 517 ambapo kutokana na mwamko wa wananchi kuripoti kuna ongezeko la matukio 343.

BRELA YAPOKEA UGENI WA WANACHAMA KUTOKA NCHI ZA LCD’s

$
0
0
wakilishi Mkurugenzi wa (WiPO) Bw.Kiflie Senkurou aliyesimama (katikati) katika matembezi ya kujionea makumbusho ya Bagamoyo leo
Kaimu mtendaji mkuu wa BRELA akipokelewa na Mkuu wa chuo cha Sanaa (TASUBA) Alipotembelea kuongoza ujumbe wa washiriki kutoka nchi mbalimbali waliofadhiliwa na shirika la miliki bunifu Duniani (WIPO) pamoja na shirika la maendeleo nchini Sweden (SIDA)
Mkufunzi wa chuo cha Sanaa TASUBA Christa Komba, Kheli Kaale akitoa maelezo kwa washiriki kuhusu studio ya muziki
Washiriki wa WIPO na SIDA wakijionea bidhaa mbalimbali za uchongaji wa vitu mbalimbali vya asili katika chuo cha Sanaa kilichopo Bagamoyo (TASUBA)
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA) akiwaongoza wageni wake kutoka nchi mbalimbali kutembelea Sanaa na Makumbusho mbalimbali Bagamoyo leo 

Mkuu wa chuo cha sanaa TASUBA Dr. Herbert Makoye, Kaimu Afisa mtendaji Mkuu BRELA Emmanuel Kakwezi,Afisa Mtendaji Mkuu wa chama cha.hakimiliki Tanzania COSOTA Bi.Doreen Sinare na Mkurugenzi wa Miliki bunifu BRELA Bi.Loy mhando wakifurahia jambo katika matembezi ya makumbusho Bagamoyo 
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo walipotembelea chuo cha Sanaa TASUBA) KUONA SANAA na tamaduni. 
…………………….. 
Washiriki wa mafunzo kutoka nchi za LCD’s wakiwa katika matembezi ya vivutio vya kihistoria katika chuo Sanaa Bagamoyo (TASUBA). 
Mafunzo haya yamefadhiliwa na (WIPO) Shirika la miliki bunifu Duniani na Shirika la Maendeleo la nchini Sweden (SIDA) wenyeji wa mafunzo hayo ni Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA

UKAGUZI WA CAG SASA KUJA NA HATI MBILI

$
0
0


Na Danny Tweve Songwe 

Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali CAG itaanza kutoa hati mbili za ukaguzi badala ya moja ya awali kuanzia ukaguzi wa mwaka wa fedha 2019/2020 kwa mamlaka za serikali za mitaa, serikali kuu, wakala na mashirika na taasisi za umma. 

Akiwasilisha maoni ya jumla kwenye baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Mbozi kupitia taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali –CAG, Mkaguzi Mkazi wa Mkoa wa Songwe Bwana Abiud Sanga amesema, hati hizo zitahusu Uzingatiaji wa Kanuni, Miongozo, Sheria na taratibu za fedha. 

Alifafanua kuwa hati nyingine itahusiana na Mpangilio wa vitabu vya mahesabu kwa mujibu wa viwango vya Kimataifa. 

Halmashauri ya wilaya ya Mbozi ni miongoni mwa halmashauri zilizopata hati safi mfululizo katika kipindi cha miaka mitatu ukiwemo mwaka uliofanyiwa ukaguzi wa 2017/2018. 

Katika kaguzi zilizopita, ofisi ya CAG ilitoa hati moja kwa kila mamlaka katika madaraja ya hati inayorishisha(unqualified opinion), hati ya mashaka(qualified), hati isiyoridhisha(adverse) na Hati Mbaya(Disclaimer). 

Katika kikao hicho, Mkuu wa mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali mstaafu Nicodemus Mwangela, amezitaka halmashauri kuachana na dhana ya kuwa mabingwa wa kujibu hoja na badala yake wanatakiwa kuepuka kusababisha hoja ikiwa ni pamoja na usimamizi na ufuatiliaji wa miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao. 

Alisema hatua zilizoanza kuchukuliwa na Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji kwa kushirikisha madiwani na Mkuu wa wilaya katika kusimamia miradi, itasaidia kuzuia athari za matumizi mabaya ya fedha zinazoelekezwa vijijini hatua ambayo ni mwanzo mzuri kuelekea kuepuka hati mbaya. 

Katika hatua nyingine Baraza hilo limeiomba ofisi ya Mkuu wa mkoa kutoa mrejesho wa matokeo ya ukaguzi maalumu uliofanywa kwenye bodi ya Kahawa ambapo kwa muda mrefu kumekuwepo malumbano kwenye halmashauri hiyo kuhusiana na deni la ushuru wa Kahawa iliyouzwa kutoka Mbozi ambalo limekuwa likitumika kushambuliana kisiasa. 

Mwenyekiti wa Halmashauri Elick Ambakisye alisema, ikiwa ofisi ya Mkuu wa mkoa itasaidia kupatikana taarifa hiyo kwenye kikao kijacho cha baraza itasaidia kujenga ushirikiano wa pamoja miongoni mwa madiwani wenyewe na wananchi kutokana malumbano ya muda mrefu yakiwatuhumu miongoni mwao kushirikiana na bodi ya Kahawa. 

Akifafanua uwasilishaji wa taarifa hiyo, Mkuu wa mkoa wa Songwe Brigedia jenerali Mwangela ameahidi kuileta taarifa hiyo kwenye kikao kijacho, hata hivyo akaagiza Halmashauri kusainiana na Bodi ya Kahawa juu ya ukomo wa muda wa deni kwa fedha zisizokuwa na utata wakati maeneo yenye utata yakiendelea kufanyiwa kazi na vyombo vingine ikiwemo TAKUKURU. 

Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya wilaya ya Mbozi ilikuwa na hoja za ukaguzi 41 ambapo hadi sasa jumla hoja 18 zimefungwa huku zingine 23 zikiwa kwenye hatua za uhakiki na utekelezaji, huku maagizo 03 kati ya 07 yaliyotolewa na Kamati ya Bunge ya hesabu za serikali za mitaa LAAC yakiwa yametekelezwa.

WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS DR JOHN MAGUFULI NCHINI RWANDA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mjini Kigali aliko mwakilisha Rais Dkt . John Pombe Magufuli katika sherehe za miaka 25 ya Ukombozi wa Nchi hiyo .Julai 4/2019 anayeshudia ni Rais wa Sierra leon Mh Mada Bio
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa amejumuika na Viongozi wenzake katika Maadhimisho ya miaka 25 ya Ukombozi wa Rwanda
Askari wa JWTZ wakiwa katika sherehe ya miaka 25 ya Ukombozi wa Rwanda

MAWAZIRI WA SERIKALI YA ZANZIBAR WAFANYAZIARA MAALUM KUANGALIA VIFAA VIPYA VYA UJENZI WA BARABARA KIBELE MKOA WA KUSINI UNGUJA

$
0
0

Baadhi ya Vifaa vipya vya Ujenzi wa Barabara vilivyonunuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar vikiwa katika eneo la Kibele Mkoa wa Kusini ambapo jumla ya Vifaa 15 vimenunuliwa kwa ajili ya kuimarisha na kujenga Barabara za Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Ujenzi Utunzaji Barabara (UUB)Ali Tahir Fatawi akitoa maelezo kwa Mawaziri na Waandishi wa Habari katika Ziara maalum ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuangalia Vifaa vipya vya Ujenzi wa Barabara vilivyonunuliwa na Serikali huko Kibele pamoja na kuangalia daraja la Kibondemzungu na Mwanakwerekwe na Skuli ya Sekondari ya Ghorofa Fuoni Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuangalia Vifaa vipya Vya Ujenzi wa Barabara vilivyonunuliwa na Serikali katika Ziara maalum ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuangalia Vifaa hivyo huko Kibele pamoja na kuangalia Ujenzi wa Daraja la Kibondemzungu na Mwanakwerekwke na Skuli ya Sekondari ya Ghorofa Fuoni Zanzibar.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Sira Ubwa Mamboya akizungumza katika ziara maalum ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuangalia Vifaa vipya vya Ujenzi wa Barabara vilivyonunuliwa na Serikali huko Kibele pamoja na kuangalia Ujenzi wa Daraja la Kibondemzungu na Mwanakwerekwe na Skuli ya Sekondari ya Ghorofa Fuoni Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Abdalla Juma Mabodi akitoa neno la Shukrani kwa Serikali katika ziara maalum ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuangalia Vifaa vipya vya Ujenzi wa Barabara vilivyonunuliwa na Serikali huko Kibele pamoja na kuangalia Ujenzi wa Daraja la Kibondemzungu na Mwanakwerekwe na Skuli ya Sekondari ya Ghorofa Fuoni Zanzibar.
Hili ni Daraja la Kibondemzungu lililotembelewa katika ziara maalum ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuangalia Vifaa vipya vya Ujenzi wa Barabara vilivyonunuliwa na Serikali huko Kibele pamoja na kuangalia Ujenzi wa Daraja la Kibondemzungu na Mwanakwerekwe na Skuli ya Sekondari ya Ghorofa Fuoni Zanzibar.
Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Wakipita chini ya Daraja la Kibondemzungu wakiwa katika ziara maalum kuangalia Vifaa vipya vya Ujenzi wa Barabara vilivyonunuliwa na Serikali huko Kibele pamoja na kuangalia Ujenzi wa Daraja la Kibondemzungu na Mwanakwerekwe na Skuli ya Sekondari ya Ghorofa Fuoni Zanzibar.

MADEREVA DALADALA WATAKIWA KUFATA SHERIA

$
0
0



Mwenyekiti wa usalama Barabarani, Salim Abri akizungumza wakati wa uzinduzi ofisi ya madereva daladala.
Mwenyekiti wa usalama Barabarani mkoa wa Iringa, Salim Abri akiwa katika picha ya pamoja na madereva daladala wa manispaa ya Iringa
**************

NA DENIS MLOWE, IRINGA
MWENYEKITI wa kamati ya Usalama Barabarani mkoa wa Iringa, Salim Abri, amewataka madereva daladala kuzingatia sheria za usalama pindi wanapokuwa wakiendesha daladala zao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi mpya ya madereva wa daladala manispaa ya Iringa, Abri alisema kuwa ifike wakati madereva wafate sheria kuepukana na usumbufu wa vyombo vya usalama.

Alisema kuwa imekuwa kawaida ya madereva wa daladala kuvunja sheria kisha kuanza malalamiko kwamba wanaonewa na polisi wa usalama Barabarani hali ambayo imesababishwa na madereva kutofata sheria.

Abri ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya usafirishaji ya Asas alisema kuwa kuna baadhi ya madereva wanaokiuka taratibu za ushafirishaji ikiwemo kutofika mwisho wa vituo hali inayoleta usumbufu kwa abiria.
Alisema madereva wanapaswa kufata sheria ikiwemo kutoa tiketi kwa abiria lakini pia kuepuka kuwanyanyasa abiria kwa kutotumia lugha mbaya  kwa abiria ambao wamewapakia.

Aliongeza kuwa licha ya kufata sheria madereva wametakiwa kuondokana na migomo isiyokuwa na maana kwa lengo la kufikisha kilio chao katika mamlaka husika kwani kugoma sio njia ya kutatua tatizo.

“Hivi unavyogoma mnajua kwamba wengine wanafurahia Sana hali hiyo?  Kumbukeni kuna njia nyingi za kufikisha ujumbe kwa serikali endapo mnaona mambo hayapo sawa hivyo acheni tabia ya kugoma” Alisema
Katika uzinduzi huo Abri aliwachangia sh. Milioni kumi kwa ajili ya kufungua Saccos ya madereva daladala na kuwataka kutumia vyema Saccos hiyo katika kukuza uchumi. 

Aliwataka pia kuacha tabia ya kushabikia mambo ya siasa zisizo na faida kwao ambazo haziwezi leta maendeleo kisa unafata mkumbo kutoka kwa watu wengine. 

Alisema kuwa wanatakiwa kuangalia viongozi ambao wapo kwa ajili ya kuwaletea maendeleo ambayo wanayataka na kukiamini chama cha Mapinduzi chenye nia haswa ya kuwaletea maendeleo wananchi wake. 
Kwa upande wao madereva wa daladala kupitia katibu wao, Rashid Ayubu waliomba mafunzo ya Mara kwa Mara ikiwezekana kila baada ya miezi Sita kutokana na mabadiliko ya sheria ya mara kwa mara. 

Ayubu alisema kuwa umoja huo Una mpango wa kupata gari aina ya Kosta kwa lengo  la kuwaongezea kipato lenye thamani ya sh. Milioni 56 na kufungua Saccos ya umoja huo. 

Aidha alisema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni baadhi ya barabara zimekuwa chakavu na zinahitajika matengenezo makubwa na nyingine kushindwa kuendelea na safari kutokana na kuvamiwa na bajaji na bodaboda.

KAMPUNI YA BAYER KUBORESHA KILIMO CHA MBOGA MBOGA

$
0
0
Na.Vero Ignatus,Iringa


Kampuni ya Bayer Crop Science ambayo zamani illiyokua ikijulikana kama Monsato inayo jishughulisha na usambazaji na uzalishaji wa pembejeo za kilimo ikiwa ni pamoja na viatilifu ,Mbegu za nafaka na mboga mboga imedhamiria kuboresha kilimo cha mboga mboga Tanzania haswa kwa wateja wake wa nyanda za juu kusini.

William Macha ni Mwakilishi wa kampuni ya Bayer Crop Science akizungumza na wakulima katika Kijiji cha Ilula amesema kuwa kwa sasa wana mbegu mpya za nyanya ambazo zinastahimili magonjwa na zimefanyiwa utafiti kwani kampuni hiyo inaongoza duniani kwa kufanya na kuendeleza tafiti.

Amesema kuwa Kitengo cha mboga mboga SEMINIS ndio kinachozalisha na kujikita Zaidi katika kuzalisha mazao ya mboga mboga tofauti kama nyanya, vitunguu, hoho,kabichi, na kadhalika.

“Kwa nyanda za juu kusini (Iringa na maeneo ya jirani) kampuni hii imefanya tafiti za kutosha na hivyo kuwaletea wakulima wa Tanzania Mbegu bora ya nyanya iitwayo FIRENZE F1 inayotoa nyanya ijulikanayo kama “Nyanya DumDum” Alisema Macha

Mtokambali Mrisho ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakulima wa nyanya na mboga mboga amesema kuwa kwa mara ya kwanza mbegu ya Firenze F1 kuingia, ilifanyiwa majaribio katika kijiji cha Tanangozi Iringa na kufanya vizuri sana baada ya hapo ilipendekezwa kuwa mbegu bora zaidi na wakulima walianza kuitumia na kupata matokea makubwa.

Mtokambali amesema kuwa kwa sasa wakulima kutoka mikoa ya Dodoma na Morogoro wanafika kujifunza kwenye shamba darasa la mbegu hizo ambazo zimeleta mavuno pesa kwa wakulima wengi mko wa Iringa na viunga.
Muwakilishi wa kampuni akiwaeleza waandishi umuhimu wa mbegu ya Firenze F1 kwa kilimo cha nyanya na wakulima
William Macha ambaye ni Muwakilishi wa kampuni ya Bayer Crop Science Akiwa na Directors wa KeyMedia Ltd Sarah &Hanna Keiya , kwa ajili ya kumpongeza mkulima mwenye bidii.
William Macha muwakilishi wa kampuni ya Bayer Crop Science Akiwa na Directors wa KeyMedia Ltd Sarah &Hanna Keiya , kwa ajili ya kumpongeza mkulima mwenye bidii.
Kampuni ya Bayer Crop science imeonyesha umuhimu wa michexo kwa wakulima kwa kuandaa tumu kutoka vijiji vya Iringa.

TANZANIA YAPEWA JUKUMU KURATIBU MRADI WA KUWAUNGANISHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KATIKA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Pichani kulia ni Naibu Katibu Mkuu (EAC),Christopher Bazivamo akizungumza kwenye Warsha ya siku moja mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) hivi karibuni kuhusu mradi wa 50 Milioni African Women Speak Networking,unaotarajiwa kuratibiwa nchini Tanzania ili kuwaunganisha wanawake Wajasiriamali katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki,Kushoto ni
Mkurugenzi wa Idara ya Jamii (EAC),Mary Makoffu.Picha na Michuzi JR.
Warsha hiyo ya Wanahabari ikendelea
 Naibu Katibu Mkuu (EAC),Christopher Bazivamo akifafanua zaidi kwenye Warsha ya siku moja mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) hivi karibuni kuhusu mradi wa 50 Milioni African Women Speak Networking,unaotarajiwa kuratibiwa nchini Tanzania ili kuwaunganisha wanawake ,pia katika nchi za Ecowas na Commesa  na lengo lake kubwa ni kuwawezesha wanawake kiuchumi na hususani wanawake wajasiriamali,Pichani kulia ni  Mkurugenzi wa Fedha (EAC) Juvenari Ndimurirwo na  kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Jamii (EAC),Mary Makoffu
Mkurugenzi wa Idara ya Jamii (EAC),Mary Makoffu(katikati) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),kwenye Warsha hiyo ya siku moja iliofanyika jijini Dar,kushoto ni Ofisa Maendeleo Mwandamizi wa Wizara hiyo kutoka Idara ya Jinsia Mapunda John
Mratibu wa Mradi wa 50 Milioni African Women Speak Networking,Bw. Wilson Muyenzi akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari katika semina hiyo.
Mkurugenzi wa Fedha (EAC) Juvenari Ndimurirwo akifafanua namna ya umuhimu wa kupanga na matumizi ya fedha katika mambo mbalimbali ikiwemo mradi wa Mradi wa 50 Milioni African Women Speak Networking,hasa kwa watakaosiriki kwa namna moja ama nyingine.

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeeleza faida za upatikanaji wa taarifa muhimu zikiwemo za fedha kwa Wanawake wajasriamali kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi nyingine Barani Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Ofisa Maendeleo Mwandamizi wa Wizara hiyo kutoka Idara ya Jinsia Mapunda John amesema wajasiriamali hao wanaunganishwa kupitia mradi wa 50 Milioni African Women Speak Networking.

Amesema ni mradi ambao unatekelezwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki,pia katika nchi za Ecowas na Commesa  na lengo lake kubwa ni kuwawezesha wanawake kiuchumi na hususani wanawake wajasiriamali.

"Kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mradi unatekelezwa kwenye nchi sita. Na sio jumuiya ya Afrika Mashariki tu bali hata katika nchi nyingine nje. Kuhusu kuwawezesha wanawake kiuchumi ni katika suala zima la kuwapatia taarifa muhimu ikiwa pamoja na taarifa za fedha na taarifa ambazo sio za fedha.

"Sasa kwa maana ya taarifa za fedha tunamaanisha taarifa kwa mfano za wapi mikopo inapatikana ,wapi grants zinapatikana lakini ili waweze kutumia kama mitaji kuendesha biashara zao lakini tunavyosema taarifa ambazo sio za fedha kuna taarifa mbalimbali ambazo ni muhimu kwa wajasiriamali kuzipata," amesema John.

Pia amesema taarifa zinazohusu masoko na mambo mengine ya kutambua thaman na wapi kwenye uhitaji na hata usalama wa biashara kwani kuna baadhi ya nchi nyakati za uchaguzi hahuko salama ,hivyo lazima wajasiriamali hao wawe na taarifa.

Amesisitiza kwamba lengo kubwa la mradi huo ni kuhakikisha ni namna gani taarifa hizo zitawafikia wanawake wajasiriamali na ndio maana matarajio ni kuandaliwa kwa Website ambayo ndani yake kutakuwa kunawekwa taarifa zote muhimu.

"Na kwamba si tu bali wanafikiria kwa kuwa na eneo moja la wajasiriamali kukutana watakuwa na mijadala mbalimbali kati ya wafanyabiashara wakubwa na wakati ikiwa pamoja na kubadilishana uzoefu," amesema John.

Amefafanua kuwa wameona kuwa wanaweza kutengeneza Website nzuri na kuwekwa taarifa zote lakini kama wanawake wajasiriamali hawajui haitakuwa na maana yoyote.

Hivyo amesemani fursa muhimu kwao kukutana na vyombo vya habari kwani kwa kutumia njia zao za kufikisha taarifa watawafikishia wanawake wajasiriamali taarifa za nchiradi huo  na wanafanya hivyo kwa kuamini kuna takribani ya wanawake milioni 500 na malengo ni kuwafikia wanawake asilimia 10 ambayo ukiiigiwa unapata wajasiriamali milioni 50 kwa jumuiya tatu ambazo kuna nchi 38.

"Wanawake wapo wengi,wapo ambao wamefanikiwa na wapo ambao hawajafanikiwa.Kwa kutumia Poto hii au Website tunaamini itakuww chachu ya maendeleo yao na nchi husika kwa ujumla," amesema John.

KASI YA UJENZI MRADI WA UMEME WA MAJI MTO RUFIJI YAMRIDHISHA MHANDISI LUOGA

$
0
0
NA K-VIS BLOG, RUFIJI 

UJENZI wa mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya mto Rufiji (RHPP), unaendelea kwa kasi ambapo Kaimu Kamishina wa Umeme na Nishati Jadilifu Mhandisi Innocent Luoga amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inautekeleza mradi huo kama ilivyo ahidi.

Mhandisi Luoga ameyasema hayo kwenye eneo la mradi(site) Julai 4, 2019 wakati wa ziara yake aliyoifanya kwa pamoja na Naibu Waziri wa Nyumba na maendeleo ya Makazi wa Misri, Mhandisi Mahmoud Fahmy Nassar.

Kampuni ya Arab Contractors kwa pamoja na ile ya Elsewedy Electric zote kutoka nchini Misri ndizo zinatekeleza ujenzi wa mradi huo.Mradi wa umeme wa maporomoko ya Mto Rufiji utakuwa na uwezo wa kufua umeme Megawati 2,115.

"Huu ni moja ya miradi mikubwa ambayo Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais wa Jamhuri Dkt. John Mgufuli inatekeleza na kusimamiwa na wazawa (Watanzania) wenyewe.” Alibainisha Mhandisi Luoga. 

Alisema tayari manufaa ya mradi huo yako bayana ambapo watanzania elfu 10,000 wamefaidika na ajira zikiwemo za moja kwa moja kwenye mradi lakini pia za watoa huduma kwa wakandarasi na wajenzi wa mradi huo. 

Naye Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Misri Mhandisi Mahmoud Fahmy Nassar alisema mradi wa Rufiji utakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa mwezi Juni 2022. 

Alisema, Serikali ya Misri imekuwa ikipata taarifa kuhusu utekelezaji wa mradi na ndiyo maana ameamua kuja kujionea na wao kama Serikali Wameridhika na maendeleo ya utekelezaji wake. 

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka ambaye naye alikuwepo katika ziara hiyo aliwahakikishia Watanzania kuwa TANESCO imehakikisha eneo hili la mradi linabaki salama kwa maana ya utunzaji wa mazingira. 

"Jiografia ya eneo hili ni miamba, eneo ambalo litakuja kujazwa maji kwa ajili ya kufua umeme kingo zake ni miamba na mteremko mkali kwa hiyo kitaalamu sio maeneo ambayo yanakaliwa na Wanyama." Alisema Dkt. Mwinuka. 
Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Misri, Mhandisi Mahmoud Fahmy Nassar (watatu kushoto), Kaimu Kamishina wa Umeme na Nishati Jadilifu Mhandisi Innocent Luoga (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka (wakwanza kushoto), wakiwa na wakandarasi kutoka kampuni za Arab Contractors na Elsewedy za Misri wakiwa eneo la mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya mto Rufiji (RHPP) wa megawati 2, 115 wakati w aziara ya viongozi hao eneo la mradi Julai 4, 2019. 
Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Misri, Mhandisi Mahmoud Fahmy Nassar (wakwanza kushoto) na Kaimu Kamishina wa Umeme na Nishati Jadilifu Mhandisi Innocent Luoga (wapili kushoto), wakimsikiliza mkandarasi kuhusu maendeleo ya mradi. 
Ujenzi ukiendelea eneo la mradi 


Mashine zikichimbua miamba na majabali huku malori yakipeba mawe. 
Dkt. Luoga (mbele) akifuatana na Meneja Miradi wa TANESCO Mhandisi Stephen Manda, (katikati) 
Naye Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Misri Mhandisi Mahmoud Fahmy Nassar(wapili kulia) akitembeela eneo la mradi. 
Picha ya mshikamano baina ya Tanzania na Misri. 
Meneja Miradi TANESCO Mhandisi Stephen Manda (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la mradi (site), kuhusu utekelezaji wa mradi huo Julai 4, 2019. 






Picha ya pamoja

KAMPUNI YA UENDELEZAJI JOTOARDHI TANZANIA WAFAFANUA MAJUKUMU YAO.

$
0
0
*Yawahamasisha Watanzania kutembelea katika banda lao kuelezwa umuhimu wa nishati ya Jotoardhi nchini

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

OFISA Mawasiliano wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania( TGDC) Augustino Kasale amefafanua kwa kina majukumu ya kampuni hiyo huku akitoa rai kwa Watanzania wanaofika kwenye Maonesho ya Biashara viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam kufika kwenye banda lao.

Akizungumza na Michuzi Blog pamoja na Michuzi TV leo akiwa kwenye maonesho hayo Kasale amesema kuwa kampuni hiyo ilianzishwa Desemba 2013 kwa madhumuni ya kusimamia na kuongoza maendeleo ya jotoardhi nchini Tanzania kamaa kampuni tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) .

"Kampuni hii inamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 na ilianza rasmi shughuli zake Julai 2014 kwa jukumu na mamlaka ya kutafiti,kuchimba na kutumia rasilimali za jotoardhi kuanzisha umeme na matumizi mengine ya moja kwa moja.

" Sababu za kuanzishwa kwanTGDC imetokana na miongo mingi nchi yetu kukabiliwa na upungufu wa uzalishaji wa umeme wa kutosha kutokana na sababu mbalimbali .

"Serikali imechukua hatua kadhaa za kutanzua tatizo la mgao wa umeme na baadhi ya hatua hizo ni ghali sana na zimeathiri mazingira .Hivyo ili kuepuka kujirudia kwa matatizo haya ndipo iliamuariwa kuwa na vyanzo mbalimbali vya uzalishaji wa umeme vya nishati jadidifu vikiwemo jua, upepo na jotoardhi,"amesema Kasale.

 Akifafanua zaidi amesema dhamira ya Kampuni hiyo ni kutoa huduma za maendeleo ya nishati ya jotoardhi za uhakika na ufanisi ,kusaidia dira ya maendeleo ya Taifa ,kuongeza ajira mpya kwa Watanzania,kuongeza uelewa na njia mbalimbali za matumizi ya moja kwa moja ya jotoardhi na kuchangia maendeleo ya uchumi wa nchi.

Wakati lengo kuu la kampuni hiyo ni kuzalisha megawati 200 ifikapo mwaka 2025 huku baadhi ha majukumu ya msingi ni kuhimiza maendeleo ya rasilimali za jotoardhi ikiwemo utafiti,uchunguzi juu ya ardhi,kuchimba na uhakiki wa awali.Pia kufanya uendelezaji wa rasilimali ya jotoardhi kufikia hatua ya upembuzi yakinifu.

Kasale akizungumzia kuhusu nishati ya jotoardhi amesema nishati hiyo inatokana na joto linalotoka kwenye mwamba wenye joto unaochemsha maji yaliyoingia ardhini .Ni nishati safi na endelevu .

Amesema pia nirasilimali inayojulikana kuwa nishati jadidifu kutokana na mfumo wa kutumika tena unaorudisha maji ardhini baada ya mvuke kugeuzwa kuwa maji na kupoozwa kwa desturi joto linalotoka chini ya ardhi kwa kawaida halina kikomo.

" Rasilimali ya nishati ya jotoardhi inaanzia  kwenye ardhi isiyo ya kina kirefu hadi kwenye maji ya moto na miamba ya joto iliyoko kilometa  chache chini ya uso wa ardhi ,na chini zaidi kwenye miamba iliyoyeyuka yenye joto kali inayoitwa Magma,"amefafanua Kasale.

Kuhusu maendeleo ua jotoardhi nchini Tanzania Kasale amesema kuwa kwa kuwa miongoni mwa nchi zilizoko kwenye mfumo wa bonde la Ufa la Afrika Mashariki ,Tanzania imejaaliwa kuwa na rasilimali nyingi za jotoardhi ambazo hazijaendelezwa na zimefanyiwa utafiti wa kiwango kidogo tu.

"Kulingana na makadirio ya kinadharia ,Tanzania imejaaliwa kuwa na zaidi ya 5000 za nishati za jotoardhi zinazosibiri kuendelezwa.Wakati uzalishaji umeme wa jotoardhi ni kwamba chini ya ardhi kunatarajiwa kubaki na joto zaidi kwa mabilioni ya miaka ijayo na hivyo kuhakikisha upatikanaji wa mtiririko wa joto usio na kikomo," amesema.

Pamoja na mambo mengine amesema kwa sasa maendeleo duniani yanategemea kwa kiasi kikubwa nishati ya uhakika  na kwamba vipo vyanzo mbalimbali ambavyo kwa miaka mingi vimekuwa tegemeo la uzalishaji wa nishati kwa ajili ya viwanda na matumizi mengine.

"Kutokana na ongezeko la uhitaji wa nishati ya uhakika duniani ili kuendesha shughuli za uzalishaji mali baadhi ya nchi mfano Kenya, Ethiopia, Iceland na Marekani zimepiga hatua katika uvunaji na utumiaji wa nishati ya jotoardhi .Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizopitiwa na bonde la Ufa na bonde hilo lina viashiria vingi  vinavyoonesha uwepo wa hifadhi ya rasilimali kubwa ya nishati jotoardhi ambayo inaweza kutumika kuzalisha umeme na matumizi mengine moja kwa moja," ameongeza.

Hata hivyo ametoa rai kwa wananchi kufika kwenye banda lao ambalo lipo katika banda la TANESCO kwenye maonesho ya biashara kupata ufafanuzi kuhusu nishatii ya jotoardhi na faida zake kwa nchi.
Ofisa Mawasiliano kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania Augustino Kasale akifafanua jambo wakati akitoa maelezo kuhusu kampuni hiyo ambapo ametumia nafasi hiyo kuomba wananchi kufika kwenye banda llilipo kwenye Maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Banda la Kampuni ya Uendelelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) katika Maonesho ya 43 Kimataifa ya Bashiashara ya Dar es Salaam
 Wageni waliotembelea banda la TGDC wakipata elimu ya nishati ya jotoardhi katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Bashiashara ya Dar es Salaam

MBUNIFU KUTOKA VETA ATOA USHAURI KUHUSU MUONGOZO KWA WABUNIFU,WAGUNDUZI NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MBUNIFU Ernest Maranya kutoka Taasisi ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi nchini(VETA) ametoa ushauri kwa Serikali kuangalia namna ya kuwepo kwa miongozo kwa ajili ya wagunduzi kwani kwa sasa changamoto iliyopo hakuna muongozo.

Maranya ambaye yupo katika banda la VETA katika maonesho ya biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ameeleza kuwa ili kuhakikisha wagunduzi na wabunifu wanaeleweka kisheria kuna kila sababu ya wadau wa elimu kuhakikisha inakuwa na muongozo kwa ajili ya wabunifu.

Katika maonesho hayo Maranya ambaye amekuwa akionesha kifaa alichobuni kinachotoa elimu ya anga amesema pia ipo haja kwa Serikali kuangalia namna ya kuharakisha elimu ya anga kwa kutumia mfumo aliobuni ili utumike katika shule zote na kuongeza anashukuru Rais Dk.John Magufuli kwani wanatambua na kwa kupitia wasaidizi wake amekuwa akipata ushirikiano.

Pamoja na mambo mengine amefafanua changamoto ambayo anakumbana nayo ni kutokuwepo kea muongozo kwa ajili ya wagunduzi na kwamba nakumbuka huko nyumba alitaka kuingia jeshini lakini alikosa nafasi kwasababu ya kukosekana kwa muongozo.

"Nakumbuka nilitaka kwenda jeshini lakini watu wa michezo aina mbalimbali wakipata nafasi lakini waliofika kwangu inabidi iundwe kamati ya kujadili wanafanyaje na sababu hakuna muongozo. Ushauri wangu umefikia wakati wa kuwa na muongozo kwa ajili wagunduzi,"amesema Maranya.

Akizungumzia zaidi kuhusu namna ambavyo amefanya ugunduzi,Maranya amesema kuwa anawashukuru sana VETA ambao ndio wanamlea na hata mambo yote ya ugunduzi anayofanya anayafanyia akiwa hapo hata mfumo wa anga ameugundua akiwa VETA.

"Nipo VETA na ukweli ni kwamba wamenichukua na sasa wananilea na kunisaidia katika kuhakikisha naendelea kufanya ugunduzi. Mbali na kubuni mfumo wa anga pia kuna mfumo ambao nimeshauchora unaohusu mashine itakayokuwa inajiendesha bila kutumia mafuta wala umeme bali itaitumia nguvu itokanayo na uzito,"amesema Maranya.

Wakati huo huo amesema anaiomba Serikali na wadau wa elimu nchini kuhakikisha wanaendelea kumuunga mkono katika kufanikisha ubunifu wake unafika maeneo yote nchini.

Amesema pamoja na kugundua mfumo huo na kukubalika lakini bado msukumo wa kuruhusu kuanza kutumia mashuleni bado ingawa anashukuru wadau wa elimu wamekuwa waliofika kwake kujifunza na kualikwa kwenye baadhi ya shule kuuelezea kwa wanafunzi.
Mgunduzi Ernest Maranya akifafanua jambo kuhusu kifaa alichogundua kinachotoa elimu ya mfumo wa anga akiwa kwenye banda la VETA katika maonesho ya biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam
Mgunduzi Erest Maranya akielezea mfumo wa sayari unavyofanya kazi angani
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la VETA wakimsikiliza mgunduzi Ernest Maranya wakati anaelezea kifaa akichobuni ambacho kinazungumzia elimu ya anga

HAYA NDIYO MAAJABU MAKUBWA DAWA YA ALOVERA.

WAZIRI LUGOLA: MAKANISA, MISIKITI ITAKAYOKWEPA KUHAKIKIWA NCHINI KUCHUKULIA HATUA KALI

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mwiseni, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, katika Mkutano wa hadhara, uliofanyika Kijijini hapo, leo. Lugola ameyataka Makanisa na Misikiti pamoja na Taasisi nyingine za kiroho nchini zifanye uhakiki na endapo zitashindwa kufanya hivyo, zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, (kushoto), akimsalimia Mkazi wa Kijiji cha Mwiseni, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, baada ya kumaliza ya kuzungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara, uliofanyika Kijijini hapo, leo. Lugola ameyataka Makanisa na Misikiti nchini ifanye uhakiki na endapo yatashindwa kufanya hivyo, yatachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
……………………………………….. 
Na Felix Mwagara, Mwibara (MOHA) 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Makanisa na Misikiti nchini ambayo itashindwa kwenda kufanyiwa uhakiki itachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. 
Waziri Lugola ameyazungumza hayo katika Mkutano wa hadhara wa Wananchi wa Kijiji cha Mwiseni, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo, ambapo alifafanua kuwa; uhakiki huo ni lazima na unalenga kuzifuatilia taasisi hizo za dini kujua utendaji wake wa kazi kama unaendana na sheria za usajili. 
Lugola amesema Serikali haikuweza kuendelea na usajili wa Makanisa na Misikiti pamoja na Taasisi za kiroho nchini, wakati kwa hivyo ikaona ifanye uhakiki kwanza kwa lengo la kujua taasisi hizo zinaweza sawa na sheria za usajili. 
“Tuhakikishe tunaendesha Makanisa na Misikiti na hizi taasisi za kiroho na kijamii kwa mujibu wa masharti ambayo mmesajiliwa kufanya, na pale ambapo utakuta, Kanisa lolote, Msikiti wowote, taasisi ya kiroho yoyote inafanya shughuli zake kinyume ne kusajiliwa kwake, kujihusisha na mambo ambayo hawaruhusiwi, sisi kama Wizara tumeapa kumsaidia Mhe. Rais tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria na utaratibu,” alisema Lugola. 
Aidha, Waziri Lugola aliwatoa hofu wananchi kutokana na kuwepo kero ya upatikanai wa vitambulisho vya taifa, alisema hakuna mwananchi atakayekosa kitambulisho hicho na mwanzoni mwa wiki hii amewaelekeza Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kutoa namba kwa wakati ili waweze kufanyiwa na usajili wa simu zao za mkononi. 
“Narudia tena, kitambulisho ni haki ya kila mwananchi na hakuna atakayekosa kitambulisho cha taifa, pia nimewaelekeza NIDA waniletee takwimu za Wilaya zote ili kujua ukubwa wa tatizo la usajili wa vitambulisho hivyo unavyoendelea,” alisema Lugola. 
Pia, Waziri Lugola alisema Tanzania ina amani kwasababu inautamaduni wa kuwa na amani, hivyo asitokee mtu akaharibu utamaduni huo ambao nchi inaendelea kuhudumisha. 
“Ndugu zangu wana Mwiseni, Wana Mwibara, amani tulionayo ndiyo inatuwezesha leo tunalima vizuri, tunavua samaki, leo tunakula vizuri, leo tunafanya shughuli mbalimbali za maendeleo, hivyo tuendelee kuitunza amani hii,” alisema Lugola. 
Aliongeza kuwa, Wizara yake kupitia Jeshi la Polisi ipo imara, Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli ipo imara na inaendelea kuwalinda Watanzania mahali popote walipo nchini, na hakuna mtu atakaye ivunja amani hiyo. 
Aidha, Lugola aliwataka wananchi hao kuhifadhi vyakula vizuri ili kuepusha janga la njaa kwa hapo baadaye na kusababisha wananchi kuja kuteseka kwa ukosefu wa vyakula na kusababisha mateso katika familia. 
“Tutunzeni vyakula vyetu, msitumie hovyo, kuweni makini na matumizi ya vyakula, sitaki nije kuona mnateseka na njaa, hakikisheni mnatunza vyakula kwa ajili ya matumizi ya baadaye, ogopeni njaa kama ukoma,” alisema Lugola. 
Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, ameanza ziara jimboni kwake ya kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi kupitia kufanya mikutano ya hadhara.

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA SIMIYU YARIDHISHWA NA KASI YA TBA UJENZI WA OFISI YA DC BUSEGA

$
0
0
Meneja wa Wakala wa Majengo nchini TBA Mhandisi Likimaitare Naunga (wa pili kulia) akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega, Julai 04, 2019. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza majumuisho ya ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega, Julai 04, 2019. 
Meneja wa Wakala wa Majengo nchini TBA Mhandisi Likimaitare Naunga akizungumza majumuisho ya ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega, Julai 04, 2019. 
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akizungumza majumuisho ya ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega, Julai 04, 2019. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza katika majumuisho ya ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega, Julai 04, 2019. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa tatu kushoto) na viongozi wengine wakikagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega, Julai 04, 2019. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa sita kushoto) katika picha ya pamoja na viongzoi mabalimbali wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega unaoendelea wilayani Busega, Julai 04, 2019. 
Sehemu ya nyuma ya Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busaga ambalo linatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu na wananchi kuanza kupata huduma. 

…………………….. 
Na Stella Kalinga, Simiyu 
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka imeridhishwa na kasi ya Ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega na majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, chini ya Mkandarasi Wakala wa Majengo nchini (TBA ). 

Hayo yamebainishwa na kamati hiyo ,mara baada ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Busega ambapo ujenzi umeanza mwezi Aprili mwaka huu na unatarajia kukamilika ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu. 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema miradi yote inayotekelezwa na TBA Simiyu imekuwa ikitekelezwa kwa wakati na wakati mwingine imekuwa ikitekelezwa na kukamilika kabla ya muda uliopangwa katika mkataba, huku akiishukuru serikali kwa kutenga fedha za ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Busega ambayo itatua changamoto za wananchi za upatikanaji wa huduma kwa karibu . 

“Tumepata Meneja mzuri wa TBA ambaye anatekeleza miradi yake kwa wakati, miradi yote tuliyompa imetekelezwa mbele ya muda uliowekwa kwenye mkataba; kwa mradi huu umeenda kwa kasi ambayo inaendana na uhitaji wa wananchi wa Busega waliokuwa wanahitaji mahali pa kupata huduma” alisema Mtaka. 

Mkuu wa wilaya ya Busega Mhe.Tano Mwera amesema utendaji wa kazi kwa sasa ni mgumu kutokana na ufinyu wa jengo wanalolitumia kama ofisi, hivyo kukamilika kwa jengo hilo kutawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi. 

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutupa fedha za ujenzi wa jengo hili, litakapo kamilika litatuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi kwa sababu ofisi tunayoitumia sasa hivi ni finyu sana na watendaji wametawanyika sana hivyo inatuwia vigumu kiutendaji”alisema Mwera. 

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema kazi zote zinazofanywa na Wakala wa majengo nchini TBA Mkoa wa Simiyu zimekuwa zikifanywa kwa viwango na zinakamilika kwa wakati, huku akiahidi kulipa fedha zilizobakia kwa wakati. 

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Majengo nchini TBA Mhandisi Likimaitare Naunga amesema mkataba wa ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega ni miezi mitano na wanatarajia kukamilisha ujenzi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu. 
Kukamilika kwa ujenzi awamu ya kwanza ya jengo hilo utagharimu kiasi cha shilingi milioni mia saba nukta saba.

RC MTAKA ATAKA MAFUNDI WANAOTOKA KWENYE JAMII WATAMBULIWE, WAJENGEWE UWEZO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Busega, Itilima na Bariadi katika majumuisho ya Ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa katika Hospitali za Wilaya hizo, iliyofanyika Julai 04,2019. 
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi(kushoto) akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na wajumbe wengine wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Itilima, Julai 04, 2019. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye koti jeusi) na viongozi wengine wakitoa katika moja ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Bariadi wakati wa ziara maalum ya kukagua ujenzi wa hospitali hiyo iliyofanyika Julai 04,2019 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye shati la kitenge mbele) na viongozi wengine wakitoa katika moja ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Busega wakati wa ziara maalum ya kukagua ujenzi wa hospitali hiyo iliyofanyika julai 04, 2019 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye shati la kitenge mbele) na viongozi wengine wakitoa katika moja ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Busega wakati wa ziara maalum ya kukagua ujenzi wa hospitali hiyo iliyofanyika Julai 04, 2019 
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakikagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bariadi Julai 3, 2019. 
Baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Busega yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi 
Baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Bariadi yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi 
………………………………….

Na Stella Kalinga, Simiyu 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia kwa wahandisi wa ujenzi kuwatambua na kuwajengea uwezo mafundi wote wanaotoka kwenye jamii wanaofanya kazi za serikali kwa kutumia mfumo wa ujenzi usiotumia wakandarasi (Force Account) hususani waliofanya kazi nzuri kwenye ujenzi wa hospitali za wilaya ya Mkoa wa Simiyu. 

Mtaka ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara katika hospitali za wilaya ya Itilima, Bariadi na Busega zinazoendelea kujengwa lengo ni kujua hatua ziizofikiwa katika ujenzi, ambapo amesema mafundi hao wakitambuliwa na kujengewa uwezo utendaji wao utaimarishwa na kazi watakazofanya zitafanywa katika ubora. 

“Ni lazima kama Mkoa tuwe na mfumo wa kuwatambua mafundi wote waliofanya kazi ya kujenga hospitali zetu zote tatu na tuanze kuwajengea uwezo,ili miradi yetu ya Serikali tunayoendelea kuifanya tusiwe na watu wapya sana na kama tukipata wapya watakuwa wanafanya kazi chini ya uangalizi wa watu wenye uwezo mzuri zaidi” Mtaka 

Mbali na hayo amezipongeza wilaya hizo kwa mfumo walioutumia wa kununua vifaa kiwandani moja kwa moja kwani umesaidia kuokoa fedha nyingi ambazo zimefanikisha ujenzi kufikia katika hatua nzuri, huku akizisisitiza wilaya hizo kuwashirikisha Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwenye ununuzi wa vifaa vya umeme ili kupunguza gharama zisizo za lazima. 

Kwa upande wao Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya SACF James John (Bariadi) Elizabeth Gumbo (Itilima) wamesema kuwa miongoni mwa changamoto zilizopelekea kutokamilisha kwa miradi hiyo ambayo ilitakiwa kukamilika Juni 30 , 2019 ni fedha kutotosheleza na kusisitiza kuwa ikiwa watapokea fedha mapema watakamilisha majengo yote. 

“Tulipokea bilioni 1.5 tumebakiwa na shilingi milioni 75 kwa ajili ya kulipa mafundi tulioingia nao mkataba, ili tuweze kukamilisha hatua zilizosalia katika ujenzi wa majengo saba ya awali tunahitaji shilingi milioni 370” alisema James John mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi. 

“Tulipokea shilingi bilioni 1.5 tumebakiwa na shilingi milioni ambazoo zimetengwa kwa ajili ya malipo ya mafundi, tukiongezewa shilingi milioni 360 tutamaliza majengo kwa hatua zilizobaki” alisema Elizabeth Gumbo mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Itilima. 

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Busega Tano Mwera amebainisha kuwa kwa hatua walioyofikia fedha zinatosha kukamilisha mradi na kwamba changamoto iliyopelekea wasiweze kukamilisha kwa wakati ni ucheleweshwaji wa mfumo na kwamba ikifanyiwa kazi mradi utakamilika kwa wakati. 

Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesisitiza Halmashauri za Wilaya ya Bariadi, Busega na Itilima kumalizia ujenzi wa Hospitali za wilaya kwa wakati ambapo pia alitoa rai ya kuhakikisha barabara zinatengenezwa, miti na bustani za maua zinapandwa katika maeneo hayo ambayo hospitali hizo zinajengwa. 

Katika ujenzi wa hospitali za wilaya ya Bariadi, Itilima na Busega ambao ni wa awamu ya kwanza kuna jumla ya majengo takribani ishirini na moja yanapaswa kujengwa (21) ikiwa ni majengo saba kwa kila Hospitali (kwa awamu ya kwanza) ambayo yapo katika hatua mbalimbali.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 5,2019

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images