Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

SHERIA MPYA YA DAWASA YAANZA KUTUMIKA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam DAWASA Florence Yamat amesema kuwa serikali imefuta sheria namba 20 ya mwaka 2001 na kuleta sheria mpya namba 5 ya 2019 ya mazingira.

Amesema hayo leo kwenye banda la Mamlaka hiyo kwenye maonesho ua 43 ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Yamat amesema sheria hiyo mpya ya mwaka 2019 imebadilisha Mamlaka ya Majisafi na Majitaka na kuwa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira.

Yamat amesema, sheria hiyo mpya itasimamia mazingira na itakuwa na mfumo endelevu wa kulinda vyanzo vya maji pamoja na miundo mbinu.
"Sheria hii mpya inatutaka kulinda miundo mbinu ya maji na kuongeza faini na adhabu kutoka 500,000 hadi 50,000,000 pamoja au kifungo," amesema

Sheria hiyo mpga iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kutumia Julai Mosi mwaka huu na inawataka DAWASA kusimamia usafi wa mazingira kiujumla. 

Naye Mkurugenzi Huduma kwa Wateja Ritamary Lwabulinda amewaomba wateja wa DAWASA kulipa bili zao kwa wakati ili kuweza kuendelea kuboresha huduma pamoja na kujenga miradi mipya ya maji ili wananchi wengine ambao hawapo kwenye mtandao waweze kupata huduma ya maji safi na salama.

Mbali na hilo, Ritamary amewataka wananchi kujitokeza kwenye banda lao kwa kupata maelezo zaidi na kufahamu jinsi ya kujiunga na DAWASA.
  Mkurugenzi wa kitengo cha Sheria DAWASA Bi. Florence Yamati akielezea sheria mpya ya huduma ya majisafi pamoja na usafi wa mazingira kwa waandishi wa habari katika banda la DAWASA lililopo kwenye viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva aliotembelea banda la DAWASA katika maonyesho ya Kimataifa yanayoendelea na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa katika banda hilo.




ZIARA YA WAZIRI UMMY KATIKA KUKAGUA UNYUNYIZIAJI WA VIADUDU-DENGUE

$
0
0
Iliyobebwa ni moja kati ya mashine mpya 14 za kupuliza dawa (motorised sprayers) zilizonunuliwa na Manispaa ya Ilala ikiwa ni moja ya jitihada yakupambana dhidi ya ugonjwa wa homa ya Dengue katika Manispaa hiyo. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyevaa buti) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu, wakielekea katika zoezi la upuliziaji wa viuadudu katika mazalia ya mbu, eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongoza zoezi la upuliziaji wa viuadudu katika mazalia ya mbu, katika eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyevaa buti) akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu, wakinyunyiza dawa katika mazalia ya mbu, eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyevaa buti) akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu, wakiwa katika zoezi la upuliziaji wa viuadudu katika mazalia ya mbu, eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam. 
……………………. 
Na WAMJW- DSM 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. ummy mwalimu leo amefanya ziara katika eneo la Mchikichini Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kukagua utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa Mikoa/Halmashauri ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Dengue. 

Kwa kiasi kikubwa Waziri ummy mwalimu ameridhishwa na hatua walizochukua na Manispaa ya Ilala ikiwemo kununua mashine mpya 14 za kupuliza dawa (motorised sprayers), kununua Viuadudu kutoka kiwandani Kibaha lita 3,980 (shs 53m) na kununua lita 210 za kuua mbu wapevu. Huku upuliziaji ukiendelea ktk kata 25. 

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa, Matokeo ya jitihada hizi yanaoneka, huku Idadi ya wagonjwa wa Dengue Wilaya ya Ilala ikipungua kutoka wagonjwa 527 mwezi Mei 2019 hadi wagonjwa 207 mwezi June 2019. 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa, katika Jiji zima la Dar es Salaam wagonjwa wa homa ya Dengue wamepungua kutoka 2,759 mwezi Mei 2019 hadi wagonjwa 790 mwezi June. 

Mbali na hayo, Waziri Ummy amewataka wananchi kushiriki kikamilifu ktk kutokomeza mazalia ya mbu, kwa kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka, kupulizia dawa maeneo yote yenye mazalia ya mbu, pia kutumia chandarua chenye dawa wakati wote.

IGP SIRRO AONGOZA KIKAO CHA UTENDAJI CHA MAOFISA WAKUU WA JESHI LA POLISI.

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (katikati), akiongoza Kikao cha
Utendaji cha Maofisa Wakuu wa Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es
salaam, kujadili utendaji wa kazi za Polisi, kufanya tathmini, Mafanikio,
Changamoto na kuweka mikakati ya kutekeleza kazi za Polisi hususan
kulinda maisha ya raia na mali zao, kushoto kwake ni Kamishna wa
Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Mussa A. Mussa na Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas na kulia kwake ni
Kamishna wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi CP Shabani Hiki
na Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu CP Benedict Wakulyamba.
Picha na Jeshi la Polisi. 
Maofisa Wakuu wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wakifuatilia hotuba
inayotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
DCP Charles Kenyela (aliyesimama), Wakati wa Kikao cha Utendaji cha
Maofisa Wakuu kilichofanyika jijini Dar es salaam na kujadili utendaji wa
kazi za Polisi, kufanya tathmini, Mafanikio, Changamoto na kuweka
mikakati ya kutekeleza kazi za Polisi hususan kulinda maisha ya raia na
mali zao ili kuhakikisha jamii inakuwa salama. Picha na Jeshi la Polisi.

JKT YAKANUSHA TAARIFA ZA VIJANA WA JKT KUNDI LA KIKWETE NA OPERESHENI MAGUFULI KUKUSANYIKA KAMBI YA JKT MGULANI

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA MAWAKALA WANAOSAJILI LAINI ZA SIMU BILA IDHINI

$
0
0


Wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzaia (TCRA) inaendela na utekelezaji wa zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya biometria, TCRA imebaini kuwa kuna watu wanaojihusisha na usajili wa SIMU bila kuidhinishwa na watoa huduma za mawasiliano.

Kwa mujibu wa kifungu cha 92 na 97 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, 2010 na Kanuni ya 9,10, na 11 ya Kanuni za Usajili wa Laini za Simu (Sim Card Registration Regulations, 2018), TCRA inapenda kuutaarifu na kuukumbusha Umma kuwa:-

  1. Ni marufuku kwa mtu yeyote kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila kuwa na uthibitisho kuwa ameidhinishwa na mtoa huduma za mawasiliano kutoa huduma hizo;

  2. Yeyote anayejihususha na uuzaji, usambazaji au usajili wa laini za simu anatakiwa kuwa na ofisi ya kutolea huduma hiyo ya usajili wa laini za simu; na

  3. Ni kosa la jinai kwa mtu yeyoye kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila

kuwa na ofisi na uthibitisho wa idhini ya mtoa huduma husika.

Umma unakumbushwa na kuonywa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani pamoja na faini, kwa mtu yeyote atakaye bainika kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila kufuata taratibu.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Jengo la Mawasiliano, Kitalu Na. 20 Barabara ya Sam Nujoma, S. L. P 474, 14414 DAR ES SALAAM JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

Tabora yaibuka kinara wa mashindano ya UMITASHUMTA 2019

$
0
0
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Mkoa wa Tabora umefanikiwa kuwa mshindi wa jumla wa mashindano ya UMITASHUMTA 2019 baada ya timu zake kufanikiwa kufanya vizuri na hivyo kujipatia alama nyingi kuliko mikoa mingine 25 iliyoshiriki mashindano hayo mwaka huu.
Kwa mujibu wa matokeo ya washindi wa UMITASHUMTA mwaka 2019, mkoa wa Tabora ulifanya vizuri katika mchezo wa goli kwa wasichana ambapo walishika nafasi ya kwanza, netiboli walishika nafasi ya pili, na kwaya walishika nafasi ya pili.
Kutokana na matokeo hayo mkoa wa Tabora ulifanikiwa kuwa wa kwanza baada ya kujizolea jumla ya alama 153, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na mkoa wa Dar es salaam baada ya kujinyakulia alama 147.5.
 Mkoa wa Dar es salaam umekuwa ukifanya vizuri kwa kushika nafasi ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita mfululizo, ambapo kwa mwaka huu, timu zake zilifanya vizuri katika michezo ya mpira wa goli wavulana kwa kushika nafasi ya kwanza, mpira wa mikono wavulana nafasi ya tatu, fani za ndani nafasi ya kwanza, wavu nafasi ya tatu na soka wameshika nafasi ya pili
Nafasi ya mshindi wa tatu imechukuliwa na mkoa wa Mara baada ya kupata alama 143.7 ambazo zimetokana na ushindi kwenuye michezo ya usafi na nidhamu wavulana kwa kushika nafasi ya kwanza, riadha wasichana nafasi ya pili, mpira wa mikono wavulana na wasichana nafasi ya kwanza na soka wasichana nafasi ya pili.
Mkoa wa Mwanza ulishika nafasi ya nne ambapo timu zake zilifanya vizuri kwenye michezo ya riadha wasichana walishika nafasi ya kwanza, ngoma nafasi ya pili na soka kawaida nafasi ya tatu.
Nafasi ya tano ilichukuliwa na mkoa wa Geita ambapo timu yao ya soka iliifunga Dar es salaam kwa njia ya penati, huku nafasi ya sita ilikwenda Mbeya, Morogoro ilichukua nafasi ya saba, Manyara ilishika nafasi ya 8, Tanga ikashika nafasi ya 9 na Mtwara ilishika nafasi ya kumi.
Mkoa wa Kilimanjaro ulishika nafasi ya 11, Dodoma 12, Shinyanga 13, Pwani 14, Kagera 15, Lindi 16, Arusha 17, Simiyu 18, Songwe 19, Kigoma 19 na 20 Kigoma.
Mikoa mingine ni Singida iliyoshika nafasi ya 21, Katavi 22, Ruvuma 23, Iringa 24, Rukwa 25 na Njombe 26
Kilele cha mashindano ya UMITASHUMTA kilihitimishwa jana katika uwanja wa Nangwanda sijaona kwa hotuba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa zawadi ya kikombe kwa washindi wa mpira wa wavu wasichana timu ya mkoa wa Mtwara kwa mwakilishi wa mkoa huo
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akiagana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo jana kwenye uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara 

Tan communications Media Ltd. yakabidhiwa rasmi leseni ya kuendesha ABC TV jijini Arusha

$
0
0
Afisa Mwendeshaji Mkuu (CEO)  wa Kampuni ya Tan communications Media Ltd. inayomiliki kituo cha Radio 5 na yenye makao yake makuu jijini Arusha Bw. Robert Francis Lowassa,  akikabidhiwa rasmi leseni ya uendeshaji wa ABC TV  jiiini Arusha na Meneja wa Mkoa wa TCRA Engineer Bi. Imelda Salum 
Afisa Mwendeshaji Mkuu (CEO)  wa Kampuni ya Tan communications Media Ltd. inayomiliki kituo cha Radio 5 na yenye makao yake makuu jijini Arusha Bw. Robert Francis Lowassa,  akiongea na kushukuru baada ya kukabidhiwa rasmi leseni ya uendeshaji wa ABC TV  jijini Arusha

NGOMA AFRICA BAND KUTIMUA VUMBI LA JIJI LA FRANKFURT AGOSTI 10


UKAGUZI WA MIKATABA YA AJIRA KWA MADEREVA

$
0
0
Katika kutimiza azma ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, Serikali inaendelea, pamoja na mambo mengine, kuimarisha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara katika sekta mbali mbali hapa nchini, ikiwemo sekta ya usafirishaji. Sekta hii ni miongoni mwa Sekta zenye mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kuongeza mapato ya Serikali. 

Aidha, sekta hii imekuwa ikichangia pia kuzalisha ajira kwa vijana wetu katika nafasi mbali mbali kama vile Madereva, Mafundi na kada nyingine nyingi.  Pamoja na mchango mkubwa unaotolewa na sekta hii, zipo changamoto kadhaa ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi na Serikali kwa kushirikiana na wadau. 

Kwa upande wa utekelezaji wa Sheria za Kazi, changamoto zimeendelea kujitokeza katika masuala ya Mikataba ya Ajira, Malipo ya Mishahara na Posho mbali mbali, ambapo imebainika yapo Makampuni machache yanayolenga kuchafua kazi nzuri inayofanywa na sekta hii, ambapo makampuni hayo machache yamekuwa yakifanya udanganyifu kwenye Mikataba ya Ajira za Madereva wao pindi yanapofanya maombi ya Leseni za Usafirishaji. 

Aidha, katika jitihada za kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi; Kitengo cha Usalama Barabarani na LATRA inatarajia kufanya Zoezi Maalum la  Ukaguzi kwa lengo la kukagua Mikataba hiyo na kuangalia utekelezaji wa Sheria kwa ujumla. 

Zoezi hili linatarajiwa kufanyika kwa namna mbili tofauti ambapo; (i) Maafisa Kaziwaliopo katika Ofisi za Kazi watapita katika Kampuni zote za Usafirishaji na (ii)Timu maalum ya Maafisa Kazi wa kushirikiana na Viongozi wa Vyama vyaWafanyakazi Madereva, LATRA na Jeshi la Polisi; Kitengo cha UsalamaBarabarani watafanya Ukaguzi wa Mikataba kwenye Vituo Vikuu vya Ukaguzikama vile Kituo cha Mabasi Ubungo, Kituo cha Kuegesha Malori chaMisugusugu na vituo vingine vinavyofanana na hivyo hapa nchini. 

Aidha, sambamba na ukaguzi huo, Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi
Madereva na Vyama vya Waajiri watapatiwa elimu kuhusu haki na wajibu waokatika kutekeleza Sheria za Kazi. 

Hivyo, ninapenda kuwaarifu Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji, WafanyakaziMadereva na Umma kwa ujumla kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajirana Wenye Ulemavu inatarajia kuanza rasmi Zoezi la Ukaguzi wa Mikataba yaAjira ya Madereva na Utekelezaji wa Sheria za Kazi kwa ujumla ifikapo tarehe 15Julai, 2019. 

Ili kulifanya zoezi hili kuwa lenye ufanisi, ni vema Wamiliki wa Vyombo vya
Usafirishaji kuhakikisha kuwa Mikataba ya Madereva wenu inakuwepo katikamaeneo yenu ya kazi, na kwa upande wa Madereva, kuhakikisha mnakuwa nanakala za Mikataba yenu mnapokuwa katika kazi zenu ili iwe rahisi kwaWakaguzi kuiona. 

Aidha, ninapenda kuwaarifu kuwa Zoezi la Ukaguzi wa Mikataba ya ajira na
Utekelezaji wa Sheria kwa ujumla litakuwa endelevu na litaendelea pia katikaSekta nyingine hapa nchini. 

Mwisho, ninapenda kutoa wito kwa Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji,
Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva pamoja na Madereva wote
nchini kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wakaguzi wakati wote wa utekelezajiwa zoezi hili ili kutoathiri utoaji wa huduma kwa wananchi kwa namna yoyote ile.

HOSPITALI YA HAYDOM YANUNUA X RAY MPYA YA KISASA

$
0
0

Mafundi wakiendelea kufunga mashine mpya ya kisasa ya hospitali ya rufaa ya Haydom Mkoani Manyara, wakiendelea kushoto ni Mkurugenzi wa hospitaki hiyo Dkt Emmanuel Nuwass. 

************* 

HOSPITALI ya rufaa ya Haydom Wilayani Mbulu, Mkoani Manyara imenunua mashine mpya ya kisasa ya uchunguzi (X-ray) kwa lengo la kuhudumia wagonjwa wengi, kuongeza ufanisi na kutoa huduma kwa urahisi zaidi. 

Hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wa zaidi ya mikoa sita nchini, ikiwemo Manyara, Singida, Dodoma, Tabora, Arusha na Simiyu ambapo kifaa hicho kitaongeza mikakati ya kupandishwa hadhi kuwa hospitali ya kanda. 

Mkurugenzi wa hospitali ya Haydom Dk Emmanuel Nuwass alisema mashine hiyo mpya ya kisasa ya kidigital imenunuliwa kwa gharama ya sh300 milioni. 

Dk Nuwass alisema mashine hiyo ya kisasa kutoka Ufaransa itasababisha ufanisi mkubwa katika utendaji kazi wake katika kuwahudumia wagonjwa wa hospitali hiyo tofauti na awali. 

Alisema mashine hiyo ina uwezo mkubwa wa kupiga picha kwa ubora na muda mfupi tofauti na ile iliyokuwa inatumika kwa teknolojia ambayo imepitwa na wakati. 

“Mashine hii ni ya kisasa na ya kipekee kwani kwa hapa nchini zipo mbili za toleo hili katika hospitali ya Haydom na hospitali ya Bugando jijini Mwanza,” alisema Dk Nuwass. 

Alisema mashine hiyo ya kisasa ya mionzi zaidi ya kuhudumia watu wengi kwa muda mfupi, ubora wa picha zake utasababisha tatizo la mgonjwa kuonekana kwa urahisi. 

Alisema pamoja na kutoa huduma kwa wagonjwa pia mashine hiyo itaongeza mikakati yao ya kufanikisha hospitali hiyo kupandishwa hadhi kutoka ya rufaa hadi kuwa ya kanda. 

Hata hivyo, mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo, John Matle aliyekuwa hospitalini hapo alipongeza jitihada za Dk Nuwass katika kuboresha miundombinu ya hospitali ya Haydom. 

“Ile mikakati ya kuhakikisha hospitali ya rufaa ya Haydom inakuwa ya kanda inaweza ikafanyika kutokana na mikakati na mipango bora kama hii inayofanywa na Dk Nuwass,” alisema Matle.

JESHI LA MAGEREZA WAIBUKA WASHINDI WA JUMLA MAONESHO YA 43 YA BIASHARA YA KIMATAIFA KWA MWAKA 2019, JIJINI DAR

$
0
0


Jeshi la Magereza limeibuka Mshindi wa Kwanza wa jumla(Overal Winner) kwenye maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam. Pichani ni Maafisa Washiriki kutoka Jeshi la Magereza wakiwa na tuzo hizo(Picha na Jeshi la Magereza)

WANAFUNZI KUANZA KUIMBA NYIMBO ZA KUHAMASISHA UZALENDO WIKI IJAYO

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akihutubia maelfu ya wanafunzi, walimu na wakazi wa mkoa wa Mtwara wakati wa hafla ya kufunga mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA jana katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara. 
Sehemu ya washiriki wa mashindano ya UMITASHUMTA kutoka mkoa wa Tabora wakipita mbele ya jukwaa kuu, wakati wa hafla ya kufunga mashindano hayo jana kwenye uwanja wa Nangwanda Mtwara. 
Mhe. Jafo akisalimiana na wachezaji wa timu ya soka wavulana ya mkoa wa Dar es salaam kabla ya kufanyika kwa fainali ya soka kati ya Dar es salaam na Geita ambapo Geita walifanikiwa kutwaa ubingwa wa soka kwa njia ya mikwaju ya penati jana katika uwanja wa Nangwanda, Mtwara 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na mabingwa wapya wa Soka wavulana UMITASHUMTA 2019 kabla ya mchezo baina ya Geita na Dar es salaam jana katika uwanja wa Nangwanda. 
………………………….. 

Na Mathew Kwembe, Mtwara 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka Maafisa elimu wa mikoa, na wilaya kuhakikisha kuwa kuanzia wiki ijayo julai 8, wanasimamia agizo la serikali linalowataka wanafunzi wote wanaosoma katika shule za msingi na sekondari zilizo chini ya Ofisi yake, kuimba nyimbo tatu za kuhamasisha uzalendo kila siku asubuhi kabla ya kuanza masomo. 

Akifunga mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari (UMISSETA) na yale ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara jana, Mhe.Jafo amesema kuwa kuanzia jumatatu ijayo, pindi shule zitakapofunguliwa maafisa elimu wa mikoa, wilaya na maafisa utamaduni wahakikishe kuwa wanafunzi wanaimba wimbo wa Taifa, wimbo wa tazama ramani, na wimbo wa Tanzania, Tanzania. 

Ameongeza kuwa nyimbo hizi ni nzuri sana kwani zikiimbwa kwa pamoja zinaweza kumtoa mtu machozi kwani kielelezo cha kujenga umoja na utaifa kwa watanzania. 

“Nyimbo hizi zinajenga umoja wetu, zinajenga utaifa wetu, lakini siyo wote wanaoweza kuimba nyimbo hizo, wengine wakianza kuimba nyimbo hizo wanaishia kugugumia gumia tu,” amesema Mhe.Jafo 

Waziri Jafo amesema kuwa uamuzi wa kuagiza nyimbo hizo ziimbwe na wanafunzi kila siku asubuhi kabla ya kuanza masomo unalenga kujenga uelewa kwa wanafunzi ili waweze kuzielewa na kuziimba kwa ufasaha nyimbo hizo zinazojenga utaifa na umoja wa Tanzania. 

Hivyo Mhe.Jafo ameagiza kuwa shule zote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizo chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI zihakikishe kuwa wanafunzi wake wanaimba nyimbo hizo tatu kila siku asubuhi kabla ya kuanza masomo ili kuhamasisha uzalendo, kujenga umoja na utaifa kwa wanafunzi. 

Amesema maafisa elimu wahakikishe kuwa wanasimamia utekelezaji wa agizo hilo la serikali na wawafundishe wanafunzi wao ili waweze kuimba kwa ufasaha nyimbo hizo tatu za wimbo wa taifa, Tanzania Tanzania, na Tazama ramani. 

Mhe.Jafo amesema kuwa licha ya ugumu utakaojitokeza mwanzoni mwa utekelezaji wa agizo hilo kwa kuzingatia kuwa hata baadhi ya walimu wanaweza wasiimbe kwa ufasaha nyimbo hizo, viongozi hao wanapaswa kuhakikisha kuwa agizo hilo linatekelezwa kwa shule zote nchini. 
“Ninajua mtakapoanza jambo hili pengine, hata baadhi ya walimu watakuwa hawajui kuimba nyimbo hizo, nitoe maelekezo kuwa kila shule iwe na nyimbo hizo na ziimbwe kila siku asubuhi ili kujenga umoja na utaifa wetu watanzania,” amesema. 

Mhe.Jafo amesisitiza kuwa hata atakapokuwa akifanya ziara zake shuleni jambo la kwanza kabla ya kufanya ukaguzi wowote litakuwa ni kuhakikisha kuwa anasikiliza jinsi vijana katika shule atakazotembelea wanavyoziimba. 
Ameongeza kuwa serikali inaamini kuwa maafisa elimu mikoa, wilaya, maafisa utamaduni na wakuu wa shule, na walimu wakuu watasimamia utekelezaji wa agizo hilo ili kuwawezesha wanafunzi wa kitanzania kuweza kuimba nyimbo hizo kwa ufasaha. 

“Hatutaki kuona vijana ambao wanapoteza hata uzalendo, hawajui hata kuimba wimbo wa taifa, tutengeneze uzalendo wetu, tutengeneze utaifa wetu kama taifa letu, imani yangu jambo hili litaleta faraja,” amesema. 
Kuhusu mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Mhe. Jafo amesema kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kuhakikisha kuwa michezo hii inaendelea kudumishwa kwa nguvu zote kwa kuhakikisha vipaji vya wanafunzi vinaendelezwa. 

Aidha Mhe.Jafo amemwagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha kuwa taarifa za wanafunzi wote walioshiriki UMISSETA na UMITASHUMTA mwaka huu zinahifadhiwa katika kanzi data ya wizara na akataka kazi hiyo ikamilishwe ndani ya wiki mbili kuanzia sasa.

Tabora Yaibuka kinara wa Mashindano ya UMITASHUMTA 2019

$
0
0
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa zawadi ya kikombe kwa washindi wa mpira wa wavu wasichana timu ya mkoa wa Mtwara kwa mwakilishi wa mkoa huo jana 
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akiagana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo jana kwenye uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara 
……………………. 
Na Mathew Kwembe, Mtwara 

Mkoa wa Tabora umefanikiwa kuwa mshindi wa jumla wa mashindano ya UMITASHUMTA 2019 baada ya timu zake kufanikiwa kufanya vizuri na hivyo kujipatia alama nyingi kuliko mikoa mingine 25 iliyoshiriki mashindano hayo mwaka huu. 

Kwa mujibu wa matokeo ya washindi wa UMITASHUMTA mwaka 2019, mkoa wa Tabora ulifanya vizuri katika mchezo wa goli kwa wasichana ambapo walishika nafasi ya kwanza, netiboli walishika nafasi ya pili, na kwaya walishika nafasi ya pili. 

Kutokana na matokeo hayo mkoa wa Tabora ulifanikiwa kuwa wa kwanza baada ya kujizolea jumla ya alama 153, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na mkoa wa Dar es salaam baada ya kujinyakulia alama 147.5. 

Mkoa wa Dar es salaam umekuwa ukifanya vizuri kwa kushika nafasi ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita mfululizo, ambapo kwa mwaka huu, timu zake zilifanya vizuri katika michezo ya mpira wa goli wavulana kwa kushika nafasi ya kwanza, mpira wa mikono wavulana nafasi ya tatu, fani za ndani nafasi ya kwanza, wavu nafasi ya tatu na soka wameshika nafasi ya pili 

Nafasi ya mshindi wa tatu imechukuliwa na mkoa wa Mara baada ya kupata alama 143.7 ambazo zimetokana na ushindi kwenuye michezo ya usafi na nidhamu wavulana kwa kushika nafasi ya kwanza, riadha wasichana nafasi ya pili, mpira wa mikono wavulana na wasichana nafasi ya kwanza na soka wasichana nafasi ya pili. 

Mkoa wa Mwanza ulishika nafasi ya nne ambapo timu zake zilifanya vizuri kwenye michezo ya riadha wasichana walishika nafasi ya kwanza, ngoma nafasi ya pili na soka kawaida nafasi ya tatu. 

Nafasi ya tano ilichukuliwa na mkoa wa Geita ambapo timu yao ya soka iliifunga Dar es salaam kwa njia ya penati, huku nafasi ya sita ilikwenda Mbeya, Morogoro ilichukua nafasi ya saba, Manyara ilishika nafasi ya 8, Tanga ikashika nafasi ya 9 na Mtwara ilishika nafasi ya kumi. 

Mkoa wa Kilimanjaro ulishika nafasi ya 11, Dodoma 12, Shinyanga 13, Pwani 14, Kagera 15, Lindi 16, Arusha 17, Simiyu 18, Songwe 19, Kigoma 19 na 20 Kigoma. Mikoa mingine ni Singida iliyoshika nafasi ya 21, Katavi 22, Ruvuma 23, Iringa 24, Rukwa 25 na Njombe 26 

Kilele cha mashindano ya UMITASHUMTA kilihitimishwa jana katika uwanja wa Nangwanda sijaona kwa hotuba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo

MADIWANI NAMTUMBO WATUPIWA LAWAMA YA STENDI

$
0
0
NA YEREMIAS NGERANGERA-NAMTUMBO

Akiongea na wakuu wa idara na vitengo pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo bwana Aden Nchimbi alisema madiwani wamehusika katika kukwamisha stendi ya wilaya ya Namtumbo kutofanya kazi.

Bwana nchimbi alisema kuna maswala ambayo hayahitaji siasa katika kutekeleza kwake lakini hili la stendi ya wilaya ya Namtumbo aliwataja madiwani hasa diwani wa kata ya Rwinga kuwa kinara kukwamisha stendi hiyo isifanye kazi.

Hata hivyo bwana Nchimbi alimtaja aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Namtumbo Luckness Adrian Amlima kuwa alisimamia stendi hiyo ifanya kazi kwa maslahi ya Halmashauri pamoja na wilaya lakini madiwani hao walikuja juu na kumshambulia katika vikao mpaka stendi hiyo imekwama kutumika huku miundombinu iliyowekwa kwa fedha nyingi za Halmashauri kukaa bila kutumika.

Aidha bwana nchimbi alimwambia katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Namtumbo Mohamed Mavallah kuwa ipo changamoto ya wadau wa maendeleo kushindwa kuchangia shughuli za maendeleo katika wilaya ya yao kutokana na kutazamwa vibaya na viongozi wa chama na wakifanya hivyo wanaambiwa kuwa wanataka kutangaza nia nawao wanadai hawataki migogoro wanashindwa kutoa misaada hiyo kwa wananchi na kurudisha nyuma shughuli za maendeleo alisema katibu tawala huyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Evance Nachimbinya naye alimwambia katibu wa chama cha mapinduzi kupitia kikao hicho kuwa miundombinu ya lazima katika stendi hiyo Halmashauri yake imekamilisha .

Alitaja kuwepo kwa choo ya kisasa ,jengo la mapato,jengo la kituo kidogo cha polisi, kuwepo kwa banda la abiria zuri kusubiria usafiri pamoja na kuwepo kwa huduma ya maji na huduma nyingine ya umeme katika stendi hiyo.

Mohamedi Mavallah katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo alisema hayupo tayari kuona wadau wa maendeleo wanakwama kuchangia shughuli za maendeleo katika wilaya yao kwa kuhofia migogoro na akadai atahakikisha wadau wanaendelea kuchangia shughuli za maendeleo kama kawaida ili kuifanya wilaya iendelee kupiga hatua .

Pia aliwataka viongozi wa chama na serikali kushirikiana bega kwa bega ili kuondoa changamoto zilizopo kwa wananchi na kucheza wimbo mmoja katika kutatua changamoto za wananchi badala ya kupishana kimtazamo wakati wa kutatua changamoto hizo.

Halmashaauri ya wilaya ya Namtumbo kupitia idara ya ardhi ilitenga eneo la stendi ya wilaya ya Namtumbo na kisha kujenga miundombinu ya lazima na kufunguliwa na kiongozi wa Mbio za mwenge kitaifa bwana Amour Hamadi Amour tarehe 10mei 2017 lakini stendi hiyo ilipingwa na waheshimiwa madiwani na mpaka sasa haifanyi kazi iliyokusudiwa na Halmashauri na badala yake magari yanaendelea kupakia abiria katika maeneo yasiyorasmi.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Aggrey Mwansasu mwenye shati jeupe mbele mara baada ya kikao hicho kwisha. 

MAKAMU WA RAIS KUMUWAKILISHA RAIS DKT MAGUFULI MKUTANO WA 12 WA DHARURA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI UMOJA WA AFRIKA


TAARIFA KWA WANAOSAJILI LINE ZA SIMU HOLELA,BILA IDHINI

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LASHINDA TUZO MAONESHO YA 43 YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA 2019

$
0
0
Tuzo ya “Best Logistics and Transportation Exhibitor” ambayo Shirika la Posta Tanzania limeshinda katika maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba 2019. Shirika la Posta Tanzania wamenyakua Tuzo ya washindi wa kwanza katika kipengele cha BEST LOGISTICS AND TRASPORTATION EXHIBITOR iliyofanyika katika maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba 2019 iliyotolewa na Makamu wa Raisi Mama Samia Suluhu Hassan wakati akifungua maonyesho hayo. Baadhi ya wafanyakazi wakishika tuzo waliyoiopata baada ya Shirika kushinda tuzo ya Best Logistics and Transportation Exhibitor. Maonesho haya ya 43 ya Sabasaba yenye kauli mbiu “ Usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda” yalianza rasmi Juni 28 na yatamalizika Julai 13 mwaka huu ambapo Shirika la Posta Tanzania ni mmoja wa washiriki kwa mwaka huu. Unapoingia kwenye Geti kuu la viwanja vya maonesho, Shirika la Posta tupo kwenye barabara ya kwanza kushoto mita chache kutoka geti hilo. Na 1ni jengo la pili kulia unapoingia Geti la mizigo (Geti 2). Duka la kiamtandao lililoko ndani ya viwanja vya sabasaba. Usajili kwa wafanyabiashara na wenye bidhaa ni bure, kujisajili pitia wesite yetu ya www.postashoptz.post Huduma zinazotolewa ni kubadisha fedha za kigeni, kusajili bure kwa makampuni, wakulima, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, pamoja na sekta ya usafirishaji kujiunga na huduma yetu ya E-commerce na kufanya biashara kupitia mtandao wetu wa Posta online. Pia wana duka la kubadilishia fedha ndani ya viwanja vya Sabasaba ambapo mteja ataweza kubadili fedha yake ya kigeni ndani ya viwanja. Wanahuduma ya EMS, kusajili masanduku mapya na huduma ya kulipia masanduku, tunatoa maelezo juu ya huduma yetu mpya ya Posta mlangoni, ambapo mteja anaweza kupelekewa vifurushi na barua zake mpaka mlangoni kupitia wahudumu wetu wa Posta walioko nchi nzima. 
Tunatoa huduma ya posta mlangoni na virtual Box, na kusajili masanduka mapya ya barua. 
Watoa huduma wakiwa na nyuso za furaha kukukaribisha katika banda la Shirika la Posta Tanzania ili kuweza kujipatia huduma mbali mbali.

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAKABIDHI BAISKELI YA UMEME KWA KIJANA MWENYE ULEMAVU

$
0
0
Akiwa katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es salaam Ndg. Ngemela Lubinga Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kwa niaba ya Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM, amekabidhi baiskeli ya umeme ( Electric Wheelchair ) kwa Kijana mwenye ulemavu ili kuhamasisha moyo wa kujitolea kwa wenye uhitaji.

Akifafanua uamuzi huo wa CCM Ndg. Lubinga amesema Chama kilipokea maombi ya mahitaji ya baiskeli ya watu wenye ulemavu kutoka kwa Ndg. Yusuph Samweli kijana mwenye ulemavu wa miguu ili apate wepesi wakushughulika na shughuli mbalimbali ikiwemo masomo yake ya Sekondari. 

"Baiskeli hii imetengenezwa na kiwanda chetu cha ndani, tuvitumie viwanda vyetu vya ndani, watanzania wanaweza na Tanzania ya Viwanda imewezekana" amesisitiza Ndg. Lubinga

Huu ni muendelezo wa utekelekezaji wa kazi za Chama ndani ya Jamii Nje ya chama.

Imetolewa na:
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI


MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JULAI 4,2019

CHUO CHA MWALIMU NYERERE CHAVUMBUA MFUMO WA UMWAGILIAJI WA KISASA

$
0
0
CHUO Cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kimeeleza kujipanga vyema katika kutoa elimu kwa njia ya kisasa katika mifumo mbalimbali ya sayansi na teknolijia,ikiwemo mfumo wa simu ya kiganjani kurahisisha mawasiliano na elimu kuwafikia walengwa kwa wakati . 

Akizungumza na Michuzi tv wakati wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa (maarufu maonesho ya sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam,Bakari Ramadhani ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho amesema kukua kwa sayansi na teknolojia kumepelekea maboresho ya vitendea kazi pamoja na miundombinu katika sekta ya kilimo. 

"Mfumo wa umwagiliaji ni rahisi na uhakika haraka kutokana na simu kutumika Kama nyenzo ya umwagiliaji ambapo mkulima anaweza kupakua programu itakayomuwezesha kufanya umwagiliaji hata akiwa mbali na shamba lake," 

Aidha, mbunifu huyo ameeleza mfumo huo umetengenezwa takribani wiki moja kupitia mafunzo waliopata chuo cha Mwalimu Nyerere katika somo la tehama na mawasiliano. "Changamoto nilizopata ni kutopata vifaa vya kutengeneza mfumo huo kwa haraka hapa nchini," 

Pia ametoa wito kwa wanafunzi kusoma masomo ambayo yatakua na manufaa kwa nchi yao ili kuendelea kufikia uchumi wa viwanda .

Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images