Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

IGP SIRRO AONGOZA KIKAO CHA UTENDAJI CHA MAOFISA WAKUU WA JESHI LA POLISI

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (katikati), akiongoza Kikao cha Utendaji cha Maofisa Wakuu  wa Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam, kujadili utendaji wa kazi za Polisi, kufanya tathmini, Mafanikio, Changamoto na kuweka mikakati ya kutekeleza kazi za Polisi hususan kulinda maisha ya raia na mali zao, kushoto kwake ni Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Mussa A. Mussa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas na kulia kwake ni Kamishna wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi CP Shabani Hiki na Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu CP Benedict Wakulyamba. 
Maofisa Wakuu wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wakifuatilia hotuba inayotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCP Charles Kenyela (aliyesimama), Wakati wa Kikao cha Utendaji cha Maofisa Wakuu kilichofanyika jijini Dar es salaam na kujadili utendaji wa kazi za Polisi, kufanya tathmini, Mafanikio, Changamoto na kuweka mikakati ya kutekeleza kazi za Polisi hususan kulinda maisha ya raia na mali zao ili kuhakikisha jamii inakuwa salama. Picha na Jeshi la Polisi.


HOSPITALI YA HAYDOM YANUNUA X RAY MPYA YA KISASA

$
0
0
HOSPITALI ya rufaa ya Haydom Wilayani Mbulu, Mkoani Manyara imenunua mashine mpya ya kisasa ya uchunguzi (X-ray) kwa lengo la kuhudumia wagonjwa wengi, kuongeza ufanisi na kutoa huduma kwa urahisi zaidi.

Hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wa zaidi ya mikoa sita nchini, ikiwemo Manyara, Singida, Dodoma, Tabora, Arusha na Simiyu ambapo kifaa hicho kitaongeza mikakati ya kupandishwa hadhi kuwa hospitali ya kanda.

Mkurugenzi wa hospitali ya Haydom Dk Emmanuel Nuwass alisema mashine hiyo mpya ya kisasa ya kidigital imenunuliwa kwa gharama ya shilingi milioni 30.

Dk Nuwass alisema mashine hiyo ya kisasa kutoka Ufaransa itasababisha ufanisi mkubwa katika utendaji kazi wake katika kuwahudumia wagonjwa wa hospitali hiyo tofauti na awali.

Alisema mashine hiyo ina uwezo mkubwa wa kupiga picha kwa ubora na muda mfupi tofauti na ile iliyokuwa inatumika kwa teknolojia ambayo imepitwa na wakati.

"Mashine hii ni ya kisasa na ya kipekee kwani kwa hapa nchini zipo mbili za toleo hili katika hospitali ya Haydom na hospitali ya Bugando jijini Mwanza," alisema Dk Nuwass. 

Alisema mashine hiyo ya kisasa ya mionzi zaidi ya kuhudumia watu wengi kwa muda mfupi, ubora wa picha zake utasababisha tatizo la mgonjwa kuonekana kwa urahisi.

Alisema pamoja na kutoa huduma kwa wagonjwa pia mashine hiyo itaongeza mikakati yao ya kufanikisha hospitali hiyo kupandishwa hadhi kutoka ya rufaa hadi kuwa ya kanda.

Hata hivyo, mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo, John Matle aliyekuwa hospitalini hapo alipongeza jitihada za Dk Nuwass katika kuboresha miundombinu ya hospitali ya Haydom.

"Ile mikakati ya kuhakikisha hospitali ya rufaa ya Haydom inakuwa ya kanda inaweza ikafanyika kutokana na mikakati na mipango bora kama hii inayofanywa na Dk Nuwass," alisema Matle.
Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya Haydom Mkoani Manyara, Dkt Emmanuel Nuwass akiwaangalia mafundi wakifunga mashine mpya ya kisasa ya X-Ray ya thamani ya shilingi milioni 300.
 Mafundi wakiendelea kufunga mashine mpya ya kisasa ya hospitali ya rufaa ya Haydom Mkoani Manyara, wakiendelea kushoto ni Mkurugenzi wa hospitaki hiyo Dkt Emmanuel Nuwass.

VIJIMAMBO WAJIVUNIA UBORA WA DAWA LISHE WANAZOZALISHA KWA AJILI YA WATANZANIA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

VIJIMAMBO bidhaa zetu zina ubora unaokidhi viwango?Ndivyo anavyoeleza Katibu wa Kikundi cha Vijimambo Grace Ndege wakati anazungumzia bidhaa zao kwenye Maonesho ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Kikundi cha Vijimambo wamejikita zaidi kwenye bidhaa za kutengeneza dawa lishe kwa ajili ya kutibu maradhi mbalimbali kwenye mwili wa binadamu ikiwemo dawa inayotibu pumu, vidonda vya tumbo, gesi pamoja na dawa za kuzuia kukoroma wakati ukiwa umelala

Akifafanua zaidi kuhusu bidhaa zao kutokana na ubora wa bidhaa zao wananchi kutoka sehemu mbalimbali wamekuwa wakifika kwenye ofisiza kupata huduma kwa kununua dawa tiba ambazo zinatokana na mchanganyiko wa mazao.

"Dawa lishe ambazo tunatengeneza zimekuwa zikitibu magonjwa mbalimbali .tunazo dawa lishe za kuondoa gesi mwilini,kilungurila,vidonda vya tumbo na hata za kuondoa sumu mwilini. Pia tunazo dawa lishe za kuondoa aina mbalimbali ya fangasi mwilini, homa ya tumbo pamoja na inayotibu kuongeza uteute kwenye jointi kwa wale ambao wana matatizo ya kukosa uteute na hasa kwenye magoti kiasi cha kusababisha maumivu,"amesema Grasce Ndege.

Amesema kimsingi wanajiamini na bidhaa ambazo wanazitengeneza wao na katika kuhakikisha wanatengeneza dawa lishe zilizo na viwango wamefuata taratibu zote na wamekubalika na mamlaka zote za Serikali huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wanaofika kwenye Maonesho ya Sabasaba kufika kwenye bandao lao kupata dawa lishe kwa gharama nafuu.


"Dawa zetu zina ubora wa hali ya juu, na sisi tumejikita zaidi na dawa lishe.Kwa sasa tupo Sabasaba na baada ya hapo tutapatikana kwenye ofisi zetu zilizopo Dar free Makert ,Machinga Komplex na Kigogo Kati,"amesema Grace Ndege.

Amefafanua kwa sasa dawa lishe inayofanya vizuri kwenye soko ni ya Brain Actvater ambayo ina mchanganyiko wa mbegu za matunda na nafaka zilizo hai.Pia wanayo dawa lishe kwa ajili ya watu wenye kusumbuliwa na areji.

Ametuimia nafasi hiyo kutoa ushauri kwa Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wajasiriamaliili kuhakikisha wanadhalisha bidhaa zenye ubora unaokubalika na kutambua nakuwatangaza kokote wanakokwenda.
Pia ameiomba Serikali kuendelea kuwaunga mkono kwani wao ni wajasiriamali waliojikita

kwenye usindikaji na kikundi chao kinawatu watano lakini nyuma yao kuna kundi kubwa la Watanzania ambao wanahitahi bidhaa zao na kwamba wao wanaimani kubwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
 Grace Ndege akifafanua jambo kuhusu bidhaa wanazotengeneza  na kikundi chao cha  Vijimambo
Grace Ndege ambaye tupo kwenye kikundi cha Vijimambo wanaozalisha dawa lishe akiwa wateja ili wafike kwenye banda lake lililopo katika maonesho biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam
Mmoja ya wananchi kuangalia bidhaa za dawa lishe zinazotengenezwa na Kikundi cha Vijimambo baada ya kutembelea banda la kikundi hicho lililopo katika Maonesho ya Biashara  Sabasaba jijini Dar es Salaam

TANESCO WAJIVUNIA KUSHIKA NAFASI YA PILI MAONESHO SABASABA, WAAHIDI KUENDELEA KUTOA HUDUMA YA NISHATI KWA WATANZANIA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

SHIRIKA la Umeme Tanzania( TANESCO) wameibuka washindi wa pili katika Category ya Nishati na Madini katika Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.

TANESCO wametangazwa kuibuka na ushindi wa nafasi hiyo ya pili leo baada ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua rasmi maonesho hayo yaliyoanza Juni 28,mwaka huuu wa 2019.

Nafasi ya kwanza imechukuliwa na Tume ya Madini na kwamba walioshinda tuzo hizo ni baada ya majaji zaidi ya 25 kuchuja washiriki kwa video ambavyo vimewekwa katika kupata washindi ambapo tulikuwa na Category 27.

Baadhi ya vigezo ambavyo vimetumika kupata washindi kwa makundi mbalimbali ni ubora wa bidhaa, upambaji wa mabanda, namna wanavyohudumia wateja pamoja na namna washiriki anavyoweza kuielezea kauli mbiu ya mwaka huu inayosema Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa maendeleo ya viwanda.

Hata hivyo tangu kuanza kwa maonesho hayo Juni 28,2019 TANESCO wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo ya kusikiliza kero za wateja wao na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kueleza kazi wanazofanya huku pia wakitumia maonesho hayo kuzuzungumzia miradi mikubwa ya umeme nchini ambayo utekelezaji wake upo hatua mbalimbali.

Akizungumzia tuzo ambayo wameipata wakati akiwa kwenye banda la shirika hilo katika maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji wa Umeme na Huduma kwa Wateja TANESCO Mhandisi Raymond Seya amesema hiyo imetokana na maandalizi ambayo wameyafanya na kubwa zaidi ni kuwa karibu na wananchi katika kupatia huduma ya nishati ya umeme.

"Tuzo hii inatufanya TANESCO tuendelee kuwa karibu na wananchi na tutaendelea kuchapakazi kwa ajili ya Watanzania wote kwa kuhakikisha tunatekeleza mipango na mikakati ambayo tumeiweka kuhakikisha nchi inakuwa na nishati ya umeme wa kutosha na wa uhakika," amesema Mhandisi Seya.

Ameongeza kuwa TANESCO inaendelea kuboreka na changamoto chache zilizopo wanakabiliana nazo,kimsingi kuhakikisha nishati ya umeme nchini inapatikana ya kutosha huku akiwaomba wananchi kwa ujumla kuendelea kuchangamkia punguzo la gharama za kuunganishiwa umeme kutoka Sh.300,000 hadi kufikia Sh.27000 bila kujali mwananchi aliwepo awe mjini au kujijini.

Pamoja na mambo mengine Mhandisi Seya amesema TANESCO wanajivunia kuongeza idadi ya wateja wanaowahudumia na ongezeko hilo limetokana na mradi wa kuunganisha umeme vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini(REA) pamoja na kuwaunganishia umeme wateja wakubwa wanaomiliki viwanda vikubwa na vya kati.

Mhandisi Seya pia amegusia miradi mikubwa ya umeme nchini inayoendelea kutekelezwa ukiwemo mradi wa umeme Mto Rufiji ambapo amesema TANESCO wanahusika kwa asilimia kubwa kuusimamia na tuzo ambayo wameipata kwenye maonesho hayo inawapa hamasa kuendelea kujituma.

WAASILI ASILIA WATUMA UJUMBE KWA RAIS MAGUFULI, WAMWAMBIA KIATU CHAKE KIPO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV 

KAMPUNI ya Waasili Asilia Limited ambao wamejekita kuzalisha bidhaa za ngozi nchini wametuma ujumbe kwa Rais Dk.John Magufuli wakimuomba kuendelea kuwahamasisha Watanzania kuendelea kutumia bidhaa zinazo viwanda vya ndani huku wakieleza kuwa wanacho kiatu chake na siku yoyote akihitaji wapo tayari kumpatia.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Wasili Asilia Dedan Munisi maarufu kwa jina la Ras Mizizi amesema hayo wakati anazungumza na Michuzi TV na Michuzi Blog baada ya kutembelea banda lao lililopo kwenye Maonesho ya Biashara yanayoendelea Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Michuzi TV imeshuhudia idadi kubwa ya wananchi ambao wanafika kwenye banda la Waasili Asilia kupata bidhaa za ngozi zikiwemo za viatu, mikanda , mikoba, Sendozi, pochi zamkononi kwa ajili ya wanawake pamoja na mifuko ambayo imetengezwa kwa utundu wa haliya juu ulioambata na ubunifu kutoka kwa Ras Mizizi.

"Ombi letu kwa Rais Magufuli kama ambavyo ameamua kutushika mkono wajasiriamali,hivyo hivyo tunaomba sasa aendelee kusimamia na kushawishi Watanzania kununua bidhaaambazo zinatengenezwa na viwanda vilivyopo nchini.Kwetu Waasili Asilia tumedhamiria

kuendelea kufanya kazi kwa kujituma na kwa bidii zaidi na ndio maana ukifika kwenye banda letu utashuhudia namna ambavyo tumetengeneza bidhaa bora bora na zenye ubunifu,"amesema.

Amefafanua kutokana na ubora na ubunifu wa bidhaa zao na hasa za viatu hadi sasawanashukuru Mungu kwani wateja wao wakubwa ni viongozi wakiwamo mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na wananchi wengune wa kada mbalimbali.

"Viongozi karibu wote wameshafika kwetu , hivyo aliyebakia ni Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli na ukweli tumejiandaa na hata kiatu kwa ajili kipo.Wakati wowote akibahatikakufika tutakuwa tayari kumuuzia,"amesema.

Ras Mizizi amesema kuwa kama ambavyo jina lao la Waasili Asilia yoyote ambaye amekuwa akinunua moja ya aina ya bidhaa wanazotengeneza hurudi tena kukunua nyingine"Kwetu bwana Asilia ni asali na ukionja asali lazima urudie tena na sisi hatuna hiyana wanakuja tunawahudumia na tutaendelea kufanya hivyo siku hadi siku."

Kuhusu tuzo ambayo wameipata kwenye maonesho hayo kwa kushika nafasi ya pili kwa ubora wa bidhaa za ngozi nchini, Ras Mizizi amesema kwao ni jambo la faraja kwani ndiomara yao ya kwanza kushiriki lakini wameshika nafasi hiyo na kuongeza tuzo hiyo inatuma ujumbe kwao kuwa wanatakiwa kuongeza ubunifu zaidi ili kuwa bora ya zaidi walipo sasa.
 Viatu vya aina mbalimbali vikiwa vimepangwa katika Banda la Waasili Asilia lililopo katika maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wateja wakichagua viatu kwenye banda la Waasili Asilia lililopo kwenye maonesho ya biashara jijini Dar es Salaam
 Mmoja wa wateja akiangalia viatu kwenye banda la Waasili Asilia
Mkurugenzi wa Kampuni ya Waasili Asilia Dedan Munisi maarufu Rasi Mizizi akionesha baadhi ya vitu ambavyo vimetengenezwa na kampuni yake akiwa kwenye banda lake katika maonesho ya biashara  Sabasaba jijini Dar es Salaam

NAIBU WAZIRI HAMAD MASAUNI AKUTANA NA BOLOZI WA UFARANSA NCHINI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Fredrick  Clavier katika Ofisi ndogo ya Wizara iliyopo Jijini Dar es Salaam (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)  akimsikiliza  Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Fredrick  Clavier (katikati) Pamoja na Meneja wa Mauzo wa kampuni ya Air bus Helicopter Laurent Bouvillon kushoto  katika Ofisi ndogo ya Wizara iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Fredrick  Clavier akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni katika Ofisi ndogo ya Wizara iliyopo Jijini Dar es Salaam (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

WANAFUNZI NA WANANCHI WATEMBELEA BANDA LA BUNGE KATIKA VIWANJA VYA SABASABA KUJIFUNZA KUHUSU SHUGHULI ZA BUNGE

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa-Ofisi ya Bunge, Bw. Daniel Eliufoo akimueleza jambo Katibu wa Bunge Bw. Stephen Kagaigai alipotembelea Banda la Ofisi ya Bunge kujionea shughuli zinazofanyika katika Banda hilo katika maonyesho ya  43 Kimataifa ya Kibiashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
  Afisa wa Ofisi ya Bunge, Bw. Omary Machunda akiwapa Elimu kuhusu Bunge  Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maximillian iliyopo Tabata walipotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya  43 Kimataifa ya Kibiashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa Ofisi ya Bunge, Bw. Onesmo Laulau akiwapa Elimu kuhusu Bunge  Wananchi walipotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya  43 Kimataifa ya Kibiashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

 Afisa wa Bunge, Bw. Thomas Shawa akitoa elimu kuhusu Bunge kwa Wananchi waliotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya  43 Kimataifa ya Kibiashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

  Afisa Mwandamizi wa Bunge, Bw. Peter Magati akiwapa elimu kuhusu Bunge  Wanafunzi na Walimu kutoka Shule ya Msingi Real Hope kutoka Mbagala  waliotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya  43 Kimataifa ya Kibiashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

PICHA NA BUNGE

WAZIRI MKUU AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA VIETNAM

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Doanh ambapo amewakaribisha wafanyabiashara kutoka Vietnam waje nchini kuwekeze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.

Amesema Rais Dkt. John Magufuli ameanzisha Wizara ya Uwekezaji iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kuifanya Tanzania kuwa ni mahali bora na salama kwa wawekezaji na wafanyabiashara.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Julai 3, 2019), wakati akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Balozi Doanh. Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar Es salaam. 

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaalika wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Vietnam waje kuwekeza katika sekta ya viwanda hususani vile vinavyotumia malighafi za mazao ya kilimo yanayolimwa hapa nchini. Hatua hiyo itawawezesha wakulima wa Tanzania kuwa na soko la uhakika la mazao yao. 

“Serikali imeendelea kuondoa  vikwazo vya  kuanzisha na kuendesha  biashara  kwa kupitia upya   sheria, kanuni na taratibu za biashara  na kuzifuta zile  ambazo zimethibitika  kuwa zinayafanya mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kuwa magumu.”

Waziri Mkuu amesema kwa kuwa nchi ya Vietnam imepiga hatua kubwa katika ujenzi na uendeshaji wa viwanda vya nguo, Tanzania ingefurahi kuona kwamba viwanda vya aina hiyo vinajengwa hapa nchini na wawekezaji kutoka nchi hiyo.

Amesema kuwa ununuzi wa mazao ya kilimo kama vile pamba, koroshao, kahawa na tumbaku ni fursa nyingine ya kibiashara ambayo wafanyabiashara wa Vietnam wanakaribishwa kuichangamkia hapa nchini.

Akizungumzia kuhusu soko la korosho Waziri Mkuu amesema Tanzania ina korosho za kutosha na inawakaribisha wafanyabiashara kutoka Vietnam waje kuzinunua. Kwa wale wenye uwezo wa kujenga viwanda vya kuchakata korosho nao amewakaribisha na kuahidi kuwa Serikali iko tayari wakati wote kuwasaidia. 

Kwa upande wake, Balozi Doanh alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu juu wa ujio wa Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Mhe. Trinh Dinh Dung anayetarajiwa kufanya ziara yake ya kikazi nchini kuanzia Julai 9 hadi 11 mwaka huu. 

Alisema Naibu Waziri Mkuu huyo anatarajiwa kuambatana na wafanyabiashara wasiopungua 20 kutoka kampuni kubwa za nchini Vietnam.

Nchi za Vietnam na Tanzania zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1965. Mwaka 1984, Vietnam ilifungua ofisi ya Ubalozi  wake hapa nchini kwa muda na kuufungua upya mwaka 2003.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen   Doanh, ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Julai 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen   Doanh, ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Julai 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


BRELA YAWAHMIZA WAFANYABIASHARA KUPATA VITAMBULISHO VYA TAIFA ILI KURAHISISHA URASIMISHAJI WA MAJINA YA BIASHARA ZAO

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umewataka wafanyabiashara nchini kuhakikisha wanapata vitambulisho vya Taifa ili kurahisisha urasimishaji wa majina ya biashara zao na makampuni ili kuondokana na usumbufu unaoweza kujitokeza wakati wa usajili kwa njia ya mtandao waweze kunufaika. 

Akizungumza kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara wa wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara zao Mkurugenzi wa Utawala na Fedha kutoka ( BRELA) Bakari Mketo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaweka wateja karibu na mfumo na namna ya kupata huduma kwa urahisi.

Amesema tatizo la baadhi ya wafanyabiashara kutokuwa na vitambulisho vya taifa limekuwa likikwamisha kukamilisha urasimishaji wa biashara kwa wafanyabiashara na kuwasababishia kutumia muda mwingi kukamilisha usajili Lea kutumia mfumo wa kisasa wa kielektoniki ambao ulianza rasmi mwaka Jana.

Alizungumzia changamoto ya ukosefu wa vitambulisho bus utaifa vimesababisha baadhi ya wafanyabiashara Juliana kujisajiki kwa mfumo huo kusababisha zoezi kuwa gumu.Amesema mfumo wa zamani wa kujisajili kwa njia ya makabrasha ndio uliokuwa ukitumika lakini kwa wanatumia teknolijia ya kisasa ambao umechangia mwitikio wa wafanyabiashara wengi kujitokeza.

Ameongeza Brela kwa kutambua umuhimu wa wateja wao imekuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyabiashara nchi nzima na kwamba mpaka sasa tayari wameshaendesha mafunzo hayo kwenye kanda tano. Amezitaja kanda ambazo tayari wameshatoa mafunzo ya aina hii kuwa ni pamoja na Kanda ya Ziwa, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kusini na Kanda ya Pwani.

Aidha amezitaja faida za wafanyabiashara kujisajili kuwa ni kuweza kuingia kwenye ushindani wa fedha sambamba na kutambulika rasmi na taasisi za kifedha katika upatikanaji wa mikopo itakayowawezesha kukuza biashara zao.

"Urasimishaji wa biashara na makampuni kwa njia ya mtandao mbali na kuwawezesha wafanyabiashara kwenye ushindani wa fedha na upatikanaji wa mikopo pia itarahisisha kuwadhibiti watu wanaotumia majina ya watu kwenye biashara zao,"amesema Mketo na kuongeza kuwa itawapunguzia usumbufu wa kutoka sehemu moja kwenda sehemu ingine. 

Pia amefafanua kwa kuzitaja gharama ya usajili kwa kusema kuwa ni nafuu na kwamba gharama ya chini kabisa ni ni Sh. 175,200 na ya juu ni Sh. 512,200 .Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Judicate Ndengerio alishukuru Brela kwa mafunzo hayo na kusema yatawarahishia kusajili biashara zao kwa njia ya mtandao bila usumbufu.

Naye Ofisa Msaidizi Msaidizi George Chuwa alisisitiza mafunzo hayo yatakuwa endelevu yatafanyika nzima ili kuwarahisishia wafanyabiashara wasipoteze muda kusafiri ama kutembea mwendo mrefu kusajili kupata huduma ya usajili wa viwanda ama kampuni zao.
 Ofisa Msajili Msaidizi wa BRELA George Chuwa akiwapa mafunzo wafanyabiashara wa kati na wakubwa Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani katika ukumbi wa Flexible kijiji cha Kiguza Mkuranga Mkoani Pwani.
Baadhi ya wafanyabiashara wa kati wakubwa wa Mkuranga wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na maofisa kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( Brela) kuhusu urahisi wa urasmishaji wa majina ya biashara zao na makampuni ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza kwa kutumia mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao.

WAZIRI WA UJENZI, MHANDISI KAMWELE AFANYA MAZUNGUMZO NA WACHIMBAJI WA MADINI WAKUBWA ILI KUTATUA CHANGAMOTO ZAO

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele akizungumza na wachimbaji wa madini wakubwa Duniani ili waweze kuitumia Bandari ya Dar es Salaam inayoendelea kupanuliwa pamoja na wachimbaji hao kueleza kueleza changamoto wanazozipata ili waweze kutumia Bandari hiyo na kurahisiha mizigo kupita kwa haraka na bila usumbufu wowote ili kufikia malengo waliyojiwekea katika bandari hiyo.

 Baadhi ya wachimbaji wakubwa wa madini wakiwasilisha changamoto kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele wanazozipata pale wanapotumia bandari ya Dar es Salaam wakati wa kikao kilichoandaliwa na Waziri huyo ili kutatua changamoto hizo ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Naibu Waziri Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akifuatilia kikao kilichojumuisha wachimbaji wa Madini wakubwa pamoja Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele  kilichokuwa na lengo la kusikiliza changamoto wanazozipata wachimbaji hao ili waweze kutumia bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 100.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja za wachimbaji wa madini zilizowasilishwa kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele  wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa TPA jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wizara na wachimbaji wa Madini wakubwa wakiwa kwenye kikao kilichoitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele ili kusikiliza changamoto wanazozipata wachimbaji hao wanapotumia Bandari ya Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele akizungumza na waandishi wa khusu lengo la Serikali kuitisha kikao na Wachimbaji wa Madini wakubwa Duniani ili kuweza kusikiliza changamoto wanazozipata wanapotumia Bandari ya Dar es Salaam pamoja na kuzitafutia ufumbuzi ili waweze kutumia Bandari hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mamlaka hiyo ilivyojipanga kuhudumia wateja wao kwa ufanisi ili kufikia malengo waliyojiwekea kuelekea Uchumi wa Viwanda.

WOISO ORIGINAL PRODUCT CO WASHIKA NAFASI YA KWANZA KWA UBORA WA BIDHAA ZA NGOZI, WATUMA SALAM KWA SERIKALI

$
0
0
Na Sad Mwisehe, Michuzi TV

MENEJA Masoko wa Woiso Original Product Co Teya Herman amesema wamefurahishwa kushika nafasi ya kwanza katika utengenezaji wa bidhaa za ngozi nchini huku akieleza namna ambavyo wamejinga katika kuunga mkono azma ya Serikali kuwa nchi ya viwanda kueleka uchumi wa kati.

Woiso ambao wamepiga kambi kwenye Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam wamekuwa wakivutia wananchi wengi kufika kwenye banda lao kutokana na ubora na ubunifu wa bidhaa zao zinazotokana na ngozi.

Akizungumza leo wakati anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari , Teya Herman amesema bidhaa zote ambazo ziko kwenye maonesho ya Sabasaba zinatoka kwenye kampuni tanzu ya Himo Tanariz na kwamba ombi lao ni kuwataka Watanzania waitumie ngozi katika kuzalisha bidhaa mbalimbali.

“Kupitia ngozi hiyo tunawahimiza wajasiriamali wadogo kutumia ngozi badala ya kutumia malighafi nyingine ambazo zinaisha haraka.Hata hivyo tunamshukuru Mungu kwani ametupigania na kutuona kiasi cha kupata ushindi katika sekta ya ngozi kwa kuchukua kikombe cha mshindi wa kwanza,”amesema .

Pia amesema wanaishukuru Serikali ya Tanzania pamoja na Mamlaka ya Biashara nchini (TANTRADE) kwa kuwaona na kutupatia zawadi ya kikombe.Wamewaomba waendelee hivyo hivyo kututia moyo.

Akizungumzia banda lao, amesema wanawakaribisha wananchi kutembelea banda la Woiso Original Product Co ili kupata bidhaa kwa bei nafuu kabisa.”Tunaomba Serikali iwatangazie Watanzania kuhusu umuhimu wa kuvaa bidhaa za ngozi kwani Watanzania wengi hawajui tofauti kati ya ngozi na bidhaa nyingine.”

Akifafanua zaidi kuhusu bidhaa zao amesema wao wako bega kwa began a Serikali na ndio maana wanapambana kupanua kiwanda chao na kuongeza uzalishaji kwa lengo la kutengeneza ajira zaidi kwa Watanzania.
MENEJA Masoko wa Woiso Original Product Co Teya Herman akionesha moja ya baadhi ya bidhaa wanazotengeneza kwa kutumia bidhaa za ngozi
MENEJA Masoko wa Woiso Original Product Co Teya Herman akionesha baadhi ya bidhaa wanazotengeneza kwa kutumia bidhaa za ngozi 
Wateja wakiwa wajipatia bidhaa mbalimbali ndani ya banda la Woiso Original Product Co 
Sehemu ya mashine zitumikazo kutengenezea aina mbali mbali za bidhaa za ngozi

Rais Mstaafu Mkapa azindua safari ya SAUT kuelekea Jubilei ya Fedha

$
0
0
Na Eleuteri Mangi-SAUT
Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT) kimezindua safari ya miaka mitano kuelekea Jubilei ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1998.
Uzinduzi huo umefanywa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa uliofanyika chuoni hapo kwa kuweka jiwe la msingi katika jengo la ukumbi wa mikutano unaojengwa kutumika kwa shughuli mbalimbali za kitaaluma na kijamii.

Akiongea na hadhira ya viongozi mbalimbali, wahadhiri, wanafunzi pamoja na wananchi waliohudhuria  katika tukio hilo liliotanguliwa na ibada ya misa takatifu iliyongozwa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha SAUT na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Askofu Flavian Kassala, Rais Mstaafu Mkapa amesema kuwa vyuo vikuu vya binafsi vinamchango mkubwa nchini katika kutoa elimu kwa Watanzania bila kujali dini zao wala makabila yao hatua ambayo itawaweze kutoa mchango katika kutekeleza Sera ya Maendeleo ya Taifa ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Kuhusu Sera ya Maendeleo ya Taifa, Rais Mstaafu Mkapa amesema kuwa elimu ya juu ina mchango kwa taifa kwa kuzalisha wataalam wengi wenye ubora, ujuzi na uwezo wa kutatua matatizo ya jamii, kukabiliana na changamoto za maendeleo ili kufikia ushindani katika ngazi za kikanda na za kimataifa.
“Serikali inatambua na inathamini mchango wa sekta binfsi katika vyuo vikuu kwa kutoa elimu nchini, vyuo vikuu binafsi vina nafasi ya kuzalisha wataalamu mbalimbali kwa manufaa kwa mtu mmoja mmoja, jamii, taifa na hata nje ya mipaka ya Tanzania.” amesema Rais Mstaafu.

Katika kukuza na kupanua wigo wa kutoa elimu ya juu nchini, Rais Mstaafu Mkapa atakumbukwa kwa mchango wake wa kuwezesha dini mbalimbali nchini kuwa na vyuo vikuu vyake ikiwemo Chuo Kukuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) kinachomilikiwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM) kinachomilikiwa na Kinachomilikiwa na Baraza la Waislam Tanzania, Chuo Kikuu Cha Mt. John Dodoma kinachomilikiwa na Kanisa la Waangikana Tanzania, Chuo Kikuu cha Tumaini kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania pamoja na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Sebastian Kolowa.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha SAUT na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Askofu Flavian Kassala ameishukuru Serikali ya Tanzania kuwa msaada kwa kwa sekta binafsi ambapo baraza hilo linathamini na linaiunga mkono Serikali kwa kutoa elimu nchini ili wanaoipa waweze kutoa msaada kwa watu wanaohitaji msaada huo kwa wakati.
“Kanisa linatoa shukrani kwa Serikali, watu binafsi na taasisi zinazoendelea kutoa mchango kwa SAUT, elimu tunayotoa katika ngazi zote imewasaidia watu kutatua matatizo katika mazingira yao” amesema Askofu Kassala.

Aidha, Askofu Kassala aliendelea kusema “Tunajenga watu ambao wanazingatia maadili na utu wa mtu kwa kusaidia jamii inayohitaji msaada kutoka kwa watu ambao wamepata elimu, SAUT inamchango mkubwa katika kuwajenga na kuwalea watu kiroho na kimwili kupitia elimu” alisisitiza Askofu Kassala.
Naye Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Balozi Prof. Costa Ricky Mahalu amesema chuo chao kinaendelea kuzalisha wataalam kwa kwa ajili ya nchi hatua ambayo amemshukuru Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kuwa mlezi na msaada mkubwa kwa maendeleo ya SAUT.

Balozi Prof. Mahalu amesema kuwa wataalamu wanaoandaliwa katika chuo hicho watokana na vitivo vingine vinne (4) ambavyo ni Kitivo cha Sayansi ya Jamii na Mawasiliano ya Umma, Kitivo cha Biashara na Utawala, Kitivo cha Ualimu, Kitivo cha Sheria na Kitivo cha Uhandisi.
Hatua hiyo imeungwa mkono na Waziri wa Madini Dotto Biteko ambapo alitoa wito kwa Wanzania na wanafunzi wanaosoma na wanaotarajia kujiunga na chuo hicho kuwa katika utoaji wa elimu ya juu SAUT imejipambanua kuwa ni kinu cha kuandaa wanataaluma na viongozi mbalimbali nchini. 

“Tunabahati ya kuzaliwa kwenye nchi yenye usawa na haki, SAUT inatoa haki ya elimu kwa vijana wetu hatua inayowapelekea kuhama kwenye taifa la kulalamika na kuwa taifa la watu wa matokeo, tunathamini kazi inayofanywa na chuo hiki ambacho kimekuwa kuwa chachu ya malezi kwa kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.” Alisisitiza Waziri Biteko.

Chuo Kikuu cha SAUT kinamilikiwa na kusimamiwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kimeanzishwa kwa mujibu wa sheria za nchi na kinafanya kazi chini ya Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) kwa mujibu wa masharti ya vyuo vikuu sheria namba 7 ya mwaka 2005 ambapo awali kilikuwa kinajulikana kama Chuo cha Maendeleo ya Jamii Nyegezi (NSTI) kilichoanzishwa tangu mwaka 1960 na wamisionari wa kanisa katoliki ambao kwa sasa wanajulikana kama Wamisionari wa Afrika wakiwa chini ya Askofu Joseph Blomjous  wa Jimbo Kuu la Mwanza.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa safari ya miaka mitano ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha Tanzania (SAUT) kuelekea Jubilei ya miaka 25 tangu kuanzishwa hicho mwaka 1998. Uzinduzi huo umefanyika kwa kuweka jiwe la msingi katika jengo la ukumbi wa mikutano unaojengwa kwa matumizi ya kitaaluma na kijamii.  Wa pili kushoto ni wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha SAUT na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Askofu Flavian Kassala na Makamu wa Mkuu wa Chuo Balozi Prof. Costa Ricky Mahalu (wa tatu kutoka kulia).
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa safari ya miaka mitano ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha Tanzania (SAUT) kuelekea Jubilei ya miaka 25 tangu kuanzishwa hicho mwaka 1998. 
 Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha SAUT na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Askofu Flavian Kassala akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa safari ya miaka mitano ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha Tanzania (SAUT) kuelekea Jubilei ya miaka 25 tangu kuanzishwa hicho mwaka 1998.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa (kulia) akisalimia na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha SAUT na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Askofu Flavian Kassala (kushoto) wakati wa uzinduzi wa safari ya miaka mitano ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha Tanzania (SAUT) kuelekea Jubilei ya miaka 25 tangu kuanzishwa hicho mwaka 1998.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa (kulia) akipata maelezo kutoka mmoja wa wanachuo wa SAUT wakati wa maonesho ya kitaaaluma chuoni hapo. 

Baadhi ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wa miaka 20 na safari ya miaka mitano ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha Tanzania (SAUT) kuelekea Jubilei ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1998. Picha na Gehaz Makoga na Abubakari Yusuf-SAUT

NAIBU WAZIRI WA ELIMU WILLIAM OLE NASHA ATEMBELEA BANDA LA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM

$
0
0
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ametembelea banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 3 Julai, 2019 katika Maonesho ya 43 ya SabaSaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
 Waziri Ole Nasha ameweza kujionea tafiti mbalimbali zilifanywa na wanataaluma pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu na kuwataka kufanya tafiti zenye matokeo chanya na zenye kugusa jamii moja kwa moja.
 Waziri Ole Nasha, amewaasa wanafunzi waliofanya tafiti kutambua mapema kile wanachokifanyia utafiti kiwe na tija kwao na kwa jamii na wapomaliza elimu yao ya juu kutambua nini wanatakiwa kwenda kufanya.
 Ametoa pongezi kwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwa Ushindi na kuwataka kuongeza bidii katika masuala yote ya utafiti na ufundishaji.


Tumekuja na ufadhili wa masomo kutoka nje ya nchi -UAR

$
0
0


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

TAASISI inayowakilisha elimu ya Vyuo Vikuu vya Nje nchini Tanzania(UAR) imesema kwa sasa muitikio wa Watanzania kwenda kusoma nje ni mkubwa.

Pia ismesema wanafarajika kuwepo kwenye Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea Sabasaba jijini Dar es salaam kwani ni fursa kwao kutumia wingi wa watu wanaofika kwenye maonesho hayo kuzungumza nao.

Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya UAR nchini Tanzania Tony Kabetha amesema hayo kwenye Maonesho ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo nao wameweka banda kueleza shughuli wanazofanya.

“Sisi kama taasisi tunathamini nakutambua mkusanyiko wa watu kwasababu kubwa mbili, kwanza sisi ni washauri kwa watanzania nini cha kusoma ukizingatia suala la ajira na tunatambua Vyuo vikuu vingi vinafundisha elimu ya jumla(General Education).

“Kwa hiyo tumekuja na ufadhili wa masomo kutoka nje ya nchi lakini hatujakubali Scolashirp zote bali tumechagua zile ambazo zinaendana na mahitaji ya nchi kwa sasa kulingana na sera za nchi,”amesema Kabetha

Pia amesema wanatoa ushauri kwa Watanzania wakasome nini kuhusiana na hiyo sera ambayo itawapa ajira na itawatayarisha kwenye akili zao kwenda kujitegemea wao wenyewe.

“Kwa hiyo nafurahi kusema Serikali ya India na Serikali ya China wametoa hizo Scola shirp zaidi ya 200 ambazo Watanzania watakwenda kusoma kwa gharama nafuu na ndogo sana na wengine watakwenda kusoma bure.

“Pia wengine watakwenda kusoma kwenye vyuo vikuu ambazo gharama zake ni sawa na vyuo vya Tanzania.Na masomo ambayo yamechaguliwa ni mambo ya teknolojia ya viwandani, mambo ya utengenezaji dawa , usindikaji na masomo yanayohusu biashara pamoja na aina nyingine ya masomo kulingana na mahitaji ya mhusika”amesema.

Ameongeza pia masomo ya teknolojia ya kompyuta huku akifafanua hawajasahau masomo yanayohusu elimu ya tiba ya afya.Pia tumechukua wanafunzi wote wa masomo ya Art ili kwenda kusoma masomo mbalimbali,”amesema.

Hivyo amesema taasisi ya UAR inawakaribisha vijana wote waliomaliza ngazi ya Diploma, Digrii na Mastars.Pia wale waliomaliza elimu ya kdato cha sita ambao wanajiandaa kwenda vyuo vikuu.

Akizungumzia muitikio wa Watanzania kwenda kusoma nje , amesema kwa sasa kwa sasa muitikio ni mkubwa kwani kila mmoja anataka kwenda kusoma nje na kuna maelfu ya Watu ya wanataka kwenda na changamoto inakuwa uwezo wa wazazi kwani wengine hawana hata nauli.

Hata hivyo amesema kutokana na muamko wa vijana wa Tanzania kwenda kusoma nje ya nchi kupitia taasisi yao kuna wazazi wamekuwa wakilipa kidogo kidogo na kufafanua changamoto iliyopo nafasi ni chache kuliko idadi ya wanaohitaji.

“Baada ya Maonesho ya Sabasaba tunapatikana pale Posta Mpya katika jengo la Mkapa jijini Dar es Salaam.Ukifika kwenye jengo hilo nenda ghorofa ya kwanza na uliza UAR , basi utafikishwa tulipo. Pia tupo mikoani ambako nako tuna ofisi zetu,”amesema Kabetha.
 Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya UAR nchini Tanzania Tony Kabetha pichani kulia alipokuwa akizungumza na Michuzi TV,leo kwenye banda lake ndani ya  Maonesho ya Biashara almaarufu saba saba yanayoendelea jijini Dar es Salaam, ambapo alieleza shughuli wanazofanya.

“Sisi kama taasisi tunathamini nakutambua mkusanyiko wa watu kwasababu kubwa mbili, kwanza sisi ni washauri kwa watanzania nini cha kusoma ukizingatia suala la ajira na tunatambua Vyuo vikuu vingi vinafundisha elimu ya jumla(General Education).

CHAI BORA YAENDELEA KUUNGA MKONO KILIMO TANZANIA KUPITIA BIDHAA ZAO

$
0
0
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Chai Bora Limited katika banda lao katika viwanja vya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Chai Bora imekaribisha wateja wanaotembelea maonesho ya saba saba kutembelea banda lao na kuonja bidhaa tofauti zikiwemo bidhaa za chai, kahawa na Dabaga.

Chai Bora ni wachanganyaji na wapakiaji wa aina za chai zinazokiji mahitaji ya makundi mbalimbali ya watumiaji nchini na nje ya nchi. Wakiwa na uzalishaji wa zaidi ya kilo Milioni 3.5 kwa mwaka, Chai Bora hutumia nguvukazi kutoka kwenye jamii zinazowazunguka na hivyo kutengeneza fursa za ajira katika jamii na katika mnyororo wa usambazaji wa bidhaa kote nchini.

“Tuna furaha kukaribisha Watanzania katika banda letu ili waonje bidhaa zetu. Katika jitihada za kuunga mkono kilimo, chai zetu zinatengenezwa kutokana na malighafi bora zinazozalishwa hapa nchini na pia tunachangia katika kutengeneza fursa za ajira. Tunatumia malighafi bora za kitanzania na ubunifu wa hali ya juu. Na kupitia ubunifu huu, tunafurahi kuwa washindi wa kwanza katika kipengele cha banda bora la bidhaa za chakula na vinywaji katika maonyesho haya” Alisema Awatif Bushiri, Meneja Masoko.

Majani ya chai ya Chai Bora yamekuwa yakitumika na watanzania kwa miaka mingi. Wakiwa na aina nyingi za majani, chai bora wanaendelea kuunga mkono wakulima huku wakiwapatia watumiaji bidhaa kulingana na mahitaji yao.

“Iwe ni majani ya kawaida au yale yaliyo katika vipakti vidogo, wateja wetu wanaweza kufurahia bidhaa zetu zikiwa katika mfumo wowote wanaopendelea.” Aliongezea Awatif

Chai Bora pia huuza bidhaa zao nje ya nchi katika nchi za Kenya, Afrika Kusini, Nchi za Falme za Kiarabu, Rwanda na Ghana. Katika kukuza usambazaji wa bidhaa nje ya nchi, Chai Bora imeshirikiana na TWIGA ALPHA kuzindua mfumo wa MDUKA ambao unaruhusu watumiaji popote duniani kufanya manunuzi ya Chai Bora kupitia mfumo huo.

Kuhusu Chai Bora Limited

Chai Bora ilianza shughuli zake mwaka 1994 kama nembo ya chai, na kusajiliwa kama kampuni ya Chai Bora Limited mwaka 2006. Chai Bora huchanganya na kufungasha bidhaa za ubora wa hali ya juu huku wakitengeneza fursa za ajira nchini Tanzania.

Mwaka 2015, Chai Bora ilichukua rasmi uendeshaji wa nembo ya DABAGA na kujenga kiwanda cha kisasa huko Ilula, Iringa. Pia, Chai Bora imetambulisha kahawa yake iitwayo CAFEBORA ambayo inapatikana kama kahawa ya unga na kahawa ya kusagwa.

Chai Bora ni nembo inayotambulika nchini ikiwa na kiwanda chake wilayani Mafinga ambapo ni kitovu cha kilimo cha chai nchini. Pia, Chai Bora inaongoza katika soko la chai kupitia bidhaa zake za chai zenye viwango vya ubora kimataifa – ISO 22000:2005.

Hivi karibuni, Chai Bora imeanza kufanya kazi chini ya kampuni ya Catalyst Principal Partners, na kampuni hiyo ina lengo la kuwa kinara katika biashara ya vinywaji nchini na kusini mwa Afrika.

NI MUDA MUAFAKA WA KUWA NA KILIMO HIFADHI-WAZIRI HASUNGA

$
0
0



Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)



Sehemu ya washiriki wakifatilia kwa karibu hotuba ya waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.



Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi cheti cha pongezi Bi Gloria Emmanuel ambaye ni mkulima wa kilimo hifadhi Wilayani Monduli wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi cheti cha pongezi Shaban Minja ambaye ni mkulima wa kilimo hifadhi Wilayani Same wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Mahamoud Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.






Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Jitihada za kuongeza uzalishaji zinakuwa na mafanikio hafifu kutokana na kutotumia teknolojia sahihi zinazoendana na mahitaji na wakati; Mathalani, matumizi ya zana za kulimia ama zikiwa za mkono au zinazokokotwa na wanyamakazi au matrekta, zimekuwa zikisababisha mmomonyoko wa udongo hasa katika maeneo yasiyo tambarare na kusababisha upotevu mkubwa wa rutuba na kujengeka kwa jasi (hard pan).

Kwenye maeneo yenye mvua chache njia hizo za kilimo cha kukatua ardhi hazitunzi unyevu na kusababisha uzalishaji kuwa wa chini hasa pale panapokuwa na vipindi virefu vya ukame (dry spells) kama ilivyotokea msimu huu wa kilimo katika baadhi ya maeneo nchini ikiwemo Mkoa wa Dodoma.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 03 julai 2019 kwenye ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma.

Mhe Hasunga anasema kuwa kwa sababu hiyo basi, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ni muhimu kubadilisha mifumo inayotumiwa katika kuandaa mashamba ili kupata matokeo mazuri.

Amewashukuru Washirika wa Maendeleo (Development Partners) pamoja na Wadau wote wa Kilimo Hifadhi waliowezesha kufanikisha warsha hiyo muhimu wakiwemo African Conservation Tillage Network (ACTN), Canadian Food GrainBank (CFGB), Diocese of Central Tanganyika (DCT), na Conservation Farming Unit (CFU) –Tanzania.

Alisema juhudi hizo wanazofanya za kuendeleza Kilimo Hifadhi kwa kushirikiana na Serikali kwa maendeleo ya wakulima na Taifa kwa ujumla, ni sehemu ya mwelekeo wa kufikia Uchumi wa Viwanda kwa kukuza uzalishaji wenye tija.

Aliongeza kuwa jitihada hizo zinaendana na Sera ya Kilimo ya mwaka 2013 na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (Agricultural Sector Development Programme - ASDP II) ambazo zinahimiza usimamizi endelevu wa matumizi bora ya maji na ardhi, kuongeza tija na faida katika uzalishaji, biashara na kuongeza thamani ya mazao na kuiwezesha Sekta katika uratibu, ufuatiliaji na tathmini.

Kadhalika Waziri Hasunga amesema kuwa ili kuleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo, Serikali imeongeza juhudi za kuwaunganisha wakulima na masoko, huduma za kifedha, usindikaji wa mazao na kuongeza thamani.

Alisema kuwa katika kutimiza azma hiyo, Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Kilimo inaendelea Kuweka mazingira mazuri yanayovutia uzalishaji na uwekezaji, Kuimarisha mafunzo, Utafiti, ubunifu na uenezaji wa teknolojia za kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja na Kilimo Hifadhi na kuboresha Huduma za Ugani, Kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, uongezaji thamani ya mazao, kuimarisha ushirika, kuwaunganisha wakulima na masoko na huduma za fedha; na Kuhamasisha na kusimamia matumizi ya teknolojia za kisasa za kilimo ikiwemo teknolojia za kilimo hifadhi kwa kushirikiana na wadau mbali mbali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Mahamoud Mgimwa (Mb) alisema kuwa serikali inapaswa kujipanga vizuri kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini kwa kufanya utafiti wa kina kwa utafiti ndio nguzo ya kilimo.

Alisema kuwa asilimia kubwa ya mbegu zinaagizwa nje ya nchi hivyo aliiomba aserikali kuongeza Bajeti ya Wizara ya Kilimo hususani katika kuendeleza sekta ya mbegu.

Amesema Tanzania bado kuna tatizo kubwa la Masoko kwani wakulima wengi wanazalisha mazao yao lakini hawana mahali pakuyauza kwa bei nzuri huku wengine wakishindwa kusafirisha mzao yao kutokana na miundombinu kutoimarika kwa kiasi kikubwa. Kadhalika ameipongeza wizara ya Kilimo kwa kuanzisha mchakato wa mapitio ya sera ya kilimo ya 56mwaka 2013 itakayopelekea kuwa na sheria mpya ya Kilimo.

Awali akitoa salamu za wizara ya Kilimo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe alisema kuwa Lengo la warsha hiyo ni kuwawezesha washiriki kupata uzoefu na kufahamu juhudi na matokeo ya kazi za kuendeleza kilimo hifadhi zinazofanyika nchini na kuweka mpango utakounganisha, kuratibu na kusimamia shughuli za kuendeleza matumizi bora na endelevu za teknolojia za kilimo hifadhi nchini.

Alisema kuwa matumizi ya kilimo cha kisasa (smart agriculture) ikiwa ni pamoja na kilimo hifadhi ni nguzo katika kuendeleza kilimo nchini kwa kongeza tija, kuboresha ardhi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hasa katika maeneo yanayopata mvua chache.

Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa Katika miaka ya hivi karibuni, matumizi ya teknolojia ya kilimo hifadhi yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka. Tathmini zilizofanywa na Wizara zinaonyesha kuwa karibu hekta 40,000 nchini zinalimwa kwa kutumia kilimo hifadhi na matokeo yanaonyesha kuwa mavuno (yields) wanayopata wakulima kutoka kwenye mashamba ya kilimo hifadhi ni mazuri hata wakati wa mvua chache.

Aliongeza kuwa Katika kipindi hiki, ambacho Serikali inajitahidi kuongeza miundo mbinu ya umwagiliaji na kuongeza matumizi ya mbolea za viwandani kwa gharama kubwa ili kuongeza tija na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, matumizi ya teknolojia ya kilimo hifadhi ni njia mbadala ya kufikia malengo hayo kwa haraka na kwa gharama nafuu.

PPRA YATOA ELIMU KUHUSU SHERIA YA MANUNUZI YA UMMA, TANePS

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), imewataka wananchi kuendelea kutembelea banda lao katika maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam, ili kupata elimu ya sheria na Mfumo wa Manunuzi kwa Njia ya Mtandao (TANePS).

Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo ambaye alikuwa kwenye banda hilo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa Mamlaka inaendelea kusimamia Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2011 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 ili kuhakikisha kuwa manunuzi yanayofanywa yanazingatia thamani halisi ya fedha. 

Aidha, aliwataka wananchi kushirikiana na Mamlaka kutoa taarifa kuhusu ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ya umma na kwamba wahusika watachukuliwa hatua. 

Mhandisi Kapongo alisema kuwa uzingatiaji wa Sheria ya Manunuzi ya Umma ni nyenzo ya kudhibiti matumizi ya fedha za umma katika kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa kwa ajili ya maendeleo zinatumika kama zilivyokusudiwa ili kufikia malengo ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati na kuboresha maisha ya Watanzania. 

Katika maonesho hayo, PPRA inatoa elimu kuhusu Mfumo wa Manunuzi ya Umma kwa Njia ya Mtandao (TANePS), ambao unalenga katika kuongeza uwazi na uwajibikaji katika michakato yamanunuzi nchini. 

Kwa mujibu wa Mamlaka, wazabuni 1,958 wameshajiandikisha katika TANePS. Wazabuni hao ni kutoka katika mikoa mitano iliyofanyiwa majaribio katika Mwaka wa Fedha 2018/19. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Mhandisi Leonard Kapongo akizungumza na waandishi wa habari (wapo picha) juu ya wananchi na wadau mbalimbali watembelee banda la (PPAR) ili wapate elimu mbalimbali kuhusu huduma za manunuzi wanazozitoa,leo katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Mhandisi Leonard Kapongo katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka, kwenye Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, jijini Dar es Salaam.

MKUCHIKA: TANZANIA INAZIDI KUPATA HESHIMA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akifuatilia mada mbalimbali kwenye kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally na kulia ni Mkurugenzi Mkuu Takukuru, Diwani Athuman.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akifurahia jambo katika kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Assad, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally, akiteta Jambo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Assad, kwenye kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius NyerereJijini Dar es Salaam,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika akufuatilia mijadala mbalimbali kwenye kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Assad (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Takukuru, Diwani Athuman akisisitiza jambo wakati wa kuwasilisha Mada yake kuhusu Mwelekeo wa Taasisi hiyo katika mapambano dhidi ya Rushwa, katika kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa lililofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini kongamano hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Takukuru, Diwani Athuman akiwasilisha Mada mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maanajimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Kapt.Mstaafu George Mkuchika, kuhusu Mwelekeo wa Taasisi hiyo katika mapambano dhidi ya Rushwa, kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam huku kauli Mbiu yake ikiwa ni ‘Usindikazi wa Mazao ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda’ 
(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)
…………………..
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
DAR ES SALAAM
WAZIRI wa nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), George Mkuchika amesema Tanzania inaendelea kupata heshima kubwa katika Jumuiya ya Kimataifa katika vita vya mapambano dhidi ya rushwa kutokana na mshikamano na nguvu ya pamoja iliyopo katika vyombo na taasisi zinazosimamia utawala bora nchini.

Akizungumza katika kongamano la siku maalum dhidi ya rushwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Julai 3, 2019) Waziri Mkuchika alisema utafiti uliofanywa na taasisi hizo zimesifu juhudi za zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano na kuitaja Tanzania kuwa ni nchi ya mfano katika vita vya mapambano dhidi ya rushwa.

Mkuchika aliasema taasisi hizo zikiwemo MO Ibrahim, Transparency International, APRM na taasisi nyingine kubwa duniani zinazosimamia masuala ya utawala bora zimefanya utafiti na kusifu juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo tafiti mbalimbali zimeifanya Tanzania kushika nafasi ya pili nyuma ya nchi ya Rwanda.

Waziri Mkuchika alisema Serikali ya Awamu ya tano imeendelea kuweka mkazo na msukumo katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo taasisi zote zinazosimamia masuala ya utawala bora zimekuwa zikiunganisha nguvu ya pamoja na kulifanya suala la rushwa sasa kuwa na nguvu na msukumo mpya wa mapambano katika jamii.

“Kwa sasa vyombo vyetu vyote serikalini si TAKUKURU pekee bali pia polisi, tiss (usalama wa taifa), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ICAG) na vingine vyote, vimeendelea kuunga katika kusimamia masuala ya utawala bora na hili limeleta msukumo na hamasa mpya katika vita dhidi ya rushwa hapa nchini” alisema Waziri Mkuchika

Akizungumzia rushwa katika sekta ya viwanda na biashara, Waziri Mkuchika alisema Serikali imeendelea kuweka mikakati mbalimbali katika kupunguza tatizo hilo ambalo limekuwa likiathiri sekta binafsi ambayo imekuwa mshirika wa karibu wa serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika alisema rushwa katika sekta biashara imekuwa ikiathiri sana masuala ya uwekezaji wa kigeni, ambapo eneo lililonyesha kutawala kwa rushwa ni katika eneo la utoaji wa vibali na leseni kutoka katika taasisi na idara muhimu za serikalini na hivyo serikali imeendelea kulifanyia kazi ili kuhakikisha kuwa vikwazo hivyo vinaondolewa kwa wawekezaji na hivyo kuharakisha ukuaji wa uchumi.

Akifafanua zaidi Mkuchika anasema kutokana na serikali kutambua mchango wa sekta ya viwanda na biashara katika kukuza uchumi na uzalishaji wa ajira nchini ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, Serikali imekuwa ikifanya marekebisho mbalimbali ya sheria na sera mbalimbali ambazo zimekuwa ni sehemu ya mianya ya rushwa nchini ikiwemo eneo la kodi.

“Kutokana na kudhibiti rushwa kwa sasa kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya mwezi yameweza kuongezeka kutoka Tsh Bilioni 800 kwa mwezi hadi kufikia Tsh trilioni 1.3 hii inaoyesha kuwa kulikuwa na maeneo ambayo kulikuwa na uvujaji wa mapato ya serikali kulikochangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo rushwa”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Diwani Athumani alisema serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa sekta binafsi kupitia Mpango Mkakati dhidi ya mapambano ya rushwa (NASCAP III) ili kuhakikisha kuwa mapambano na vita dhidi ya rushwa yanapata mafanikio nchini.

Anaongeza kuwa kupitia NASCAP III, ofisi yake imeendelea kutekeleza masuala mbalimbaliu ikiwemo kufanya tafiti kubaini ukubwa na kiwango cha rushwa nchini, kupokea maoni, kutoa elimu kwa umma kupitia makongamano, rushwa pamoja na kufanya uchunguzi na kufungua mashtaka kwa watu mbalimbali wanaopatikana na hatia dhidi ya rushwa

WAZIRI HASUNGA ASISITIZA KUTILIWA MKAZO KILIMO CHA KISASA

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia kwa karibu hotuba ya waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kilimo, Hifadhi Barani Afrika (ACT) Saidi Mkomwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika leo jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Mahamoud Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika leo jijini Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akimkabidhi cheti cha pongezi Shaban Minja ambaye ni mkulima wa kilimo hifadhi kutoka Wilayani Same.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akimkabidhi cheti cha pongezi Bi Gloria Emmanuel ambaye ni mkulima wa kilimo hifadhi toka Wilaya ya Monduli.

Waziri wa Kilimo Mhe.Japhet Hasunga,akiwa katika picha ya pamoja na wadau baada ya kufungua warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika jijini Dodoma.

...........................

Na.Mwaandishi wetu,Dodoma
KATIKA kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 imeelezwa kuwa ni lazima iwekeze kikamilifu katika kilimo hifadhi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika kilimo.
Hayo yamebainisha Jijini Dodoma na Waziri wa kilimo Japhet Hasunga, wakati akifungua Warsha ya Wadau wa Kilimo Hifadhi Tanzania.

Amesema serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki ikiwamo kumefuta kodi nyingi, amesema licha ya hayo lazima kuhamasishana matumizi ya Teknolojia za kisasa ambazo ni rafiki katika kilimo.

Amebainisha kuwa ni muhimu kujadiliana pamoja kuhusu sheria kwani hatuwezi kufika uchumi wa kati mwaka 2025 bila kufikia kilimo imara na chenye tija.“Lazima kuimarishwe mafunzo kwani kilimo nchini bado kipo chini, pia tuongeze utafiti kwakuwa bila utafiti hakuna kilimo na lazima ijulikane kilimo gani kitumike,pembejeo gani zitumike,pia tuongeze uzalishaji wenye tija,” amesema Waziri Hasunga.

Katika kuimarisha na kuwapa uwezo wakulima amesema Serikali inakuja na mkakati wa bima kwa wakulima lengo likiwa ni kumsaidia mkulima pindi ambapo mazao yake yatakuwa yameharibika shambani.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa amesema kama Serikali itawekeza katika kilimo hifadhi basi sekta ya kilimo itafika mbali.

Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini (CCM) ameiomba Serikali kuongeza bajeti katika sekta ya kilimo hasa katika utafiti na kufanya mageuzi makubwa katika kilimo hasa katika sheria.“Sera na sheria zina matatizo makubwa unakuta mkulima natayarisha shamba naanza kulima napalilia halafu wakati wa kuvuna Serikali inaanza kunipangia nikauze wapi sio sawa kabisa hapa ni lazima tutengeneze sheria nzuri” amesema Mgimwa.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kilimo, Hifadhi Barani Afrika(ACT) Saidi Mkomwa amesema kilimo hifadhi ni kilimo kinachozingatia uhifadhi wa rasilimali udongo na mazingira kwa ujumla.

Amesema kilimo hicho kimejengwa katika misingi mikuu mitatu ambayo ni kusumbua udongo,kuacha masalia shambani na kufanya kilimo mzunguko.
“Kilimo hiki ni cha miaka mingi na kilianza miaka 40 iliyopita Ulaya ila kwa Barani Afrika bado kipo nyuma ndio kimefika sasa ila ni kilimo chenye faida na tija kubwa kwa mkulima,”amesema Mkomwa.

WAZIRI MHAGAMA AFUNGUA WARSHA YA WADAU KUJADILI FURSA ZA BOMBA LA MAFUTA -EACOP SHINYANGA

$
0
0
Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama amefungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga. 

Warsha hiyo imewakutanisha pamoja wawakilishi 100 wa makundi mbalimbali kutoka mikoa 11 ili kujadili mikakati na maendeleo ya utekelezaji wa dhana ya ushiriki wa Watanzania katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Tanga, Tanzania na sekta ya madini kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo leo Jumatano Julai 3,2019 katika ukumbi wa Karena Hoteli Mjini Shinyanga, Mhe. Mhagama aliwataka viongozi wa maeneo ambako bomba litapita wawahamasishe wananchi kuchangamkia fursa zitakazokuwepo katika utekelezaji wa mradi huo na kujiletea maendeleo.

"Mradi wa EACOP ni moja kati ya miradi mikubwa ambao una manufaa mengi kwa nchi yetu katika kuzalisha Ajira, kuendeleza urithishaji wa ujuzi na teknolojia, ubia kati ya makampuni ya Tanzania na wageni, ununuzi wa bidhaa zinazozalishwa na kupatikana nchini, utoaji wa huduma za makampuni ya ndani, ushiriki wa jamii, ununuzi wa hisa kwa Serikali ya Tanzania na tozo za kodi.

Hivyo, Watanzania tuna wajibu wa kuhakikisha tunashiriki ipasavyo kama ilivyo katika miradi ya sekta za ujenzi, madini na kadhalika",alisema. 
"Bomba hili la Mafuta lina urefu wa km 1443 kati ya hizo km 296 zipo nchini Uganda na km 1147 zipo Tanzania. Hii ni fursa kubwa kwa kuwa zaidi ya robo tatu ya Bomba litapita Tanzania na kunufaisha Watanzania",aliongeza Mhe. Mhagama.

Aliitaja mikoa nane itakayopitiwa na Bomba kuwa ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga huku akibainisha kuwa bomba litapita katika wilaya 24, Kata 134 na vijiji zaidi ya 180 na kusisitiza kuwa juhudi na jitihada za dhati zinapaswa kufanyiwa kazi ili kuwezesha ongezeko la ushiriki wa Watanzania.

Warsha hiyo imefadhiliwa na Taasisi ya Haki Rasilimali kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) PSF kwa kuzileta pamoja Asasi za Kiraia, wawakilishi wa jamii, wataalamu kutoka Wizarani, na Taasisi za Serikali,waratibu wa madawati ya uwezeshaji kutoka katika mikoa ya Shinyanga, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Singida, Manyara, Arusha, Tanga, Simiyu na Tabora ili kuwawezesha wadau hao na Watanzania kwa ujumla kufahamu maendeleo na fursa za sekta ya uziduaji. 
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga leo Julai 3,2019.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bengi Issa akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Haki Rasilimali,Donald Kasongi akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo.
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo.
Wadau wakifuatilia matukio ukumbin.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Mhe. Nyabaganga Talaba akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack wakati wa warsha hiyo.
Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Haki Rasilimali,Donald Kasongi na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bengi Issa wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu),Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack baada ya kufungua warsha ya siku mbili ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images