Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 297 | 298 | (Page 299) | 300 | 301 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Leah Kihimbi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Leah Kihimbi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.Mkurugenzi Mtendaji wa UCA-Tz, Emmanuel Mushy akizungumza na vijana kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufanya uzinduzi. Mkurugenzi Mtendaji wa UCA-Tz, Emmanuel Mushy akizungumza na vijana kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufanya uzinduzi.Baadhi ya wasanii chipukizi wa muziki na sanaa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na baadhi ya viongozi wa UCA-Tanzania. Baadhi ya wasanii chipukizi wa muziki na sanaa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na baadhi ya viongozi wa UCA-Tanzania.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Joseph Kuzilwa (kulia) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Prof. Daniel Mkude (katikati) na Prof. Gerald Monela wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho, kampasi ya Mbeya mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
  Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, kampasi ya Mbeya, Prof. Ernest Kihange akiwa pamoja mkuu wa chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Andrew Mbwambo (kushoto kwake) wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho, kampasi ya Mbeya mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.

  Vijana wahitimu wa vyuo vikuu wameshauriwa kuingia katika soko la ajira wakiwa wanajiamini na kujipambanua kiuwezo kutokana na elimu waliyopata wakiwa chuoni.

  Akiongea wakati wa mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Mbeya jijini humo mwishoni mwa wiki, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Joseph Kuzilwa alisema kuwa vijana wahitimu hasa toka chuo hicho wanatakiwa kuonyesha kuwa wanaweza kazi kwa kuwa elimu waliyopata ni bora na iliwatayarisha kukabiliana na changamoto mbalimbali.

  Alifafanuwa kuwa pamoja na changamoto za ajira zilizopo nchini, bado nafasi zipo ila kinachotakiwa kwa vijana ni kujiamini na kutumia vizuri elimu waliyopata kwa faida yao nay a nchi.
  “Vijana waingie katika soko wakiwa wapambanaji na sio watu walioshindwa,” alisema.

  Akitoa ushauri zaidi alisema vijana hao watumie pia fursa za kujiajiri na biashara kwa kutumia vizuri elimu na maarifa ya ujasiriamali waliyopata chuoni.

  Alisema katika azma ya kutoa elimu bora zaidi na kutoa wahitimu wenye uwezo mzuri kiutendaji na kifikra, chuo hicho kimeanzisha mikakati ya kuboresha njia za kielektroniki na kampasi ya Mbeya ikihusishwa.

  Alisema tayari wahadhiri wa kampasi hiyo wamepewa mafunzo kuhusu njia hizo na bado mafunzo yanaendelea kwa wanafunzi pia.
  “Njia hizi mpya zinafaa hasa kwa kipindi hiki ambacho vyuo vingi sasa vinapanuka kwa idadi ya wanafunzi,” alisema.

  Pamoja na kuishukuru serikali kwa mafanikio ya kampasi hiyo, pia aliiomba pamoja na wadau wengine wa elimu ya juu, kuongeza juhudi katika kushirikiana na chuo kukabiliana na changamoto zinazokabili chuo.

  Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Prof. Gerald Monela, alisema uongozi utaendelea kuipanua kampasi hiyo ili kuongeza nafasi zaidi kwa wadau wengi wanaopenda kupata elimu katika chuo hicho.

  Alisema mpango wa kukamilisha taratibu za umiliki wa eneo la Iwambi kwa ajili ya upanuzi wa kampasi hiyo unaendelea vizuri na kuwa mara baada ya kukamilisha taratibu za umiliki, mikakati ya upanuzi itaanza.

  “Tunahitaji sana ushirikiano mkubwa na wananchi wa mkoa wa Mbeya na wadau wengine katika kutimiza azma hii,” alisema, huku akiushukuru uongozi mzima wa jiji la Mbeya na wananchi wake kwa kuwapatia eneo hilo.

  Aliwaasa wahitimu wote kujihadhari na janga la ukimwi na madawa ya kulevya ili taifa lisipoteze nguvu kazi adimu iliyowekezwa ndani yao.

  Jumla ya wahitimu 567 walitunukiwa shahada mwaka huu kulinganisha na 314 mwaka jana katika programu za astashahada, 235; stashahada, 121; shahada ya kwanza, 173 na shahada ya uzamili, 38.

  Kampasi ya Mbeya imeendelea kukua kwa idadi ya wanachuo ambayo imeongezeka kutoka 405 mwaka 2006 hadi kufikia 2241 mwaka huu, hii ikiwa ni ongezeko la takribani asilimia 453.

  0 0

  MKUU wa wilaya ya Mtwara, Willman Ndile akisisitiza jambo alipokuwa anawasilisha mada katika kongamano la kimataifa la Uongozi unaowajibika na madhari ya Kitanzania,lililoandaliwa na taasisi ya Globethics.net lililofanyika katika chuo kikuu cha Stella Maris mjini Mtwara.Ndile aliwasilisha mada iliyohusu Utawala bora uwajibikaji na maadili ya uongozi Tanzania.
  Helbert Makinda mwakilishi kutoka taasisi ya Globethics.net nchini Kenya akiwasilisha mada katika kongamano la kimataifa la Uongozi unaowajibika na madhari ya Kitanzania,lililoandaliwa na taasisi ya Globethics.net lililofanyika katika chuo kikuu cha Stella Maris mjini Mtwara. (STEMMUCO).
  MWAKILISHI taasisi ya Globethics.ne na mkuu wa idara ya Dini na Philosophy katika chuo kikuu cha Stella Maris Mtwara University college STEMMUCO. Mchungaji. Profesa Aidan Msafiri, akisisitiza jambo wakati anawasilisha mada katika kongamano la kimataifa la Uongozi unaowajibika na madhari ya Kitanzania,lililoandaliwa na taasisi ya Globethics.net lililofanyika katika chuo kikuu cha Stella Maris mjini Mtwara. (STEMMUCO).
  WANACHUO wa STEMMUCO na waalikwa wengine wakifuatilia mada zilzokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa masuala ya utawala na uwajibikaji katika kongamano la kimataifa la Uongozi unaowajibika na madhari ya Kitanzania,lililoandaliwa na taasisi ya Globethics.net lililofanyika katika chuo kikuu cha Stella Maris mjini Mtwara.

  Hassan Simba, Mtwara.

  IMELEEZEZWA kuwa kukosa kwa maadili kwa baadhi ya viongozi nchini, wasomi kuwa walalamikaji badala ya kushiriki kuleta mabadiliko ni miongoni mwa sababu zinayochangia kuchelewesha maendeleo na kuminywa kwa utawala bora na kutokuwepo kwa uwajibikaji kwa umma.

  Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara, Willman Ndile, alipokuwa anawasilisha mada juu ya utawala bora uwajibikaji na maadili ya uongozi Tanzania katika kongamano la kimataifa la maadili na uongozi unaowajibika lililoandaliwa na taasisi ya Globethics.net, na kufanyika katika chuo kikuu cha Stella Maris mjini Mtwara.

  Ndile alisema kuwa viongozi wengi hapa nchini wanaingia katika nafasi hizo kwa rushwa au kujuana na wateuzi wenye mamlaka hali inayowafanya kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na badala yake wanawatumikia waliowateua au kutumia madalaka yao kuchuma mali ili kurejesha fedha walizotoa wakati wanasaka uongozi.

  Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa wasomi wananafasi kubwa ya kubadilisha hali hiyo endapo wataacha kulalamika tu na kuandika maandiko ya kitaalamu inayolenga kuwanufaisha wanaowafadhili badala yake washiriki katika kuleta mabadiliko na kuandika maandiko yenye tija na mwelekeo wa kuibadili mitazamo ya jamii.

  Alisema sheria ya maadili inapaswa kufanyiwa mabadiliko ili iweze kuwabana viongozi wengi zaidi badala ya ilivyo sasa ambapo katika ngazi ya wilaya inawahusu viongozi watatu tu huku kukiwa na viongozi wengi wenye mamlaka makubwa na ambayo wengi wao hawayatumii kwa manufaa ya umma na matokeo ni kukosekana kwa uingozi bora ambao ndio nyenzo muhimu kwa utawala bora.

  Aidha mkuu Ndile alisema shiria hiyo pia haina maana sana kwani inambana kiongozi kutaja malizake anapoingia lakini haimtaki kutaja mali anapoondoka, lakini pia Ndile alikosoa utaratibu wa baadhi ya watu kumuona fulani ndio mwenye jukumu la kubadili hali mbaya ya kuporomoka kwa maadili na badalayake kila mmoja ajione anajukumu hilo.

  0 0

  Mkongwe wa muziki wa Taarab Malkia Khadija Kopa akiwapagawisha mashabiki wa muziki huo waliofurika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam,kwenye Tamasha maalumu lililoandaliwa na kituo cha Redio Times FM na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
  Mwimbaji wa bendi ya Five Star Taarabu Ali Jay akikonga nyoyo za mashabiki waliofurika katika Tamasha la muziki huo lililoandaliwa na Redio ya Times Fm katika ukumbi wa Dar live Mbagala,Na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
  Mwimbaji wa bendi ya Five Star Taarab ,Aisha Mgonjela akiimba kwa hisia kali wakati wa Tamasha liliofanyika Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam,Tamasha hilo liliandaliwa na Redio ya Times FM ,Na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Redio Times Fm ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la muziki wa taarabu uliofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala hapo jana na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

  0 0


  Kamera ya Globu ya Jamii ipo Ndani ya Hema maalumu ambamo shughuli ya mazishi ya marehemu Nelson Mandela inaendelea hivi sasa katika kijijini Qunu.Na kama ilivyo ada ya libeneke la Globu hili kwamba halilali na litakuwa linakuletea Live matukio yote yanayoendelea katika Mazishi ya Shujaa huyo wa Afrika na Dunia kwa Ujumla.
  Rais Jakaya Kikwete akitoa historia fupi ya Marehemu Mzee Nelson Mandela kuhusiana na mahusiano aliyokuwa nayo na Tanzania.
   Rais Jakaya Kikwete ni mmoja wa viongozi mbalimbali wanaoshiriki kwenye mazishi ya hayati Mzee Nelson Mandela yanayofanyika leo kijijini kwao Qunu, nchini Afrika Kusini.
  Watu wengi maarufu Duniani wapo eneo hili hivi sasa kuhudhuria mazishi ya Mzee Nelson Mandela yanayoendelea hivi sasa katika kijiji cha Qunu,baadhi yao ni Oprah Wilfrey na mumewe, Forest Whithaker, Richard Branson,Idris Elba na wengine wengi.
  Mwili wa Mzee Mandela ukiwasili ukumbini.
  Rais wa Zamani wa Zambia,Mzee Keneth Kaunda pia yupo.
  Ankal akisalimiana na Mcheza Filamu, Idris Elba ambaye amecheza Filamu ya Long Walk to Freedon inayoelezea mapambano ya Mzee Mandela wakati alipokuwa akihangaika kuutafuta uhuru wa mtu mweusi nchini Afrika kusini.

  0 0


  0 0

   KATIKA KIPINDI HIKI CHA MSIMU WA SIKUKUU YA KRISMAS NA MWAKA MPYA,DUKA LAKO PENDWA LENYE VIWALO VIKALI HAPA MJINI DAR ES SALAAM LIFAHAMIKALO KAMA J&M VIRGO,LIMESHUSHA MALI MPYA MAALUM KWA KIPINDI HIKI.

  HIVYO FIKA DUKANI KWAO PALE MIKOCHENI KWA WARIOBA,JENGO LA C&G PLAZA GHOROFA YA KWANZA ILI UWEZE KUJIPATIA PAMBA KALI,MOKA ZA KISASA NA MICHUCHUMIO MIKALI KWA KINA DADA.

  KWA TAARIFA ZAIDI TEMBELEA LIBENEKE LEO


  0 0

  Jumatano wiki hii, jarida maarufu na kongwe duniani la TIME, lilimtangaza kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, kuwa mtu aliyekuwa na ushawishi mkubwa kwa mwaka huu wa 2013.

  Tuzo hiyo, ijulikanayo kama PERSON OF THE YEAR, hutolewa kwa mtu ambaye ametawala vyombo vya habari kwa mwaka husika, iwe ni kwa mambo mema ama mabaya.

  Mwaka jana, Rais Barak Obama alishinda tuzo hiyo kwa kutetea kiti chake cha urais nchini Marekani.
  Na katika fainali ya tuzo za mwaka huu, walikuwemo pia Rais wa Syria Bashar al Assad ambaye amekuwa akituhumiwa kutumia gesi ya sumu kuua raia wake, pia mwanasayansi aliyevujisha siri za serikali ya Marekani Edward Snownden, Rais Obama na wengine sita.
  Hii ilikuwa ripoti ya Disemba 14, 2013


  Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC

  0 0

   Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL) wa mikoa ya Simiyu, Mwanza  na Mara, Josephat Changwe, akimwongoza Waziri wa Maji , Profesa Jumanne Maghembe (kulia) kuzindua moja ya visima 20 vya maji salama ya kunywa vilivyokarabatiwa na kampuni hiyo kwa gharama ya sh.49.5 milioni, wilayani Misungwi,Mwanza juzi.Anayepiga makofi (kushoto) ni Mbunge wa jimbo la Misungwi, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Charles Kitwanga.
   Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe (kulia), Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais,Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga (wa tatu kulia) na Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL) wa mikoa ya Simiyu, Mwanza  na Mara, Josephat Changwe wakisaidia kumtwisha dumu la maji mmoja wa wanawake wa Kijiji cha Mapilinga, Wilaya ya Misungwi, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa moja kati ya visima 20 vilivyokarabatiwa na TBL wilayani humo, kwa sh. mil 49.5.

  0 0

  Ndugu zangu, 


  NOTHING can come from NOTHING. Wamesema hili Wanafalsafa wa Uyunani ya Kale .

  Nimemwona na kumsikiliza Rais wetu Jakaya Kikwete akizungumza kwenye siku muhimu ya kumuaga kwa mara ya mwisho Mzee wetu Nelson Mandela. 

  Muda wote wa hotuba yake, JK alibaki kwenye mstari kwa namna ile ile ya kuweka bayana kwa ulimwengu, kuwa ' msione vinaelea'. 

  Hakika alichofanya JK jana ndicho haswa alipaswa kukifanya, na amekifanya kwa kutumia weledi wake kwenye diplomasia na kuchanganya uzoefu wake kwenye uongozi wa kisiasa na dola kwa ujumla.

  Ni kuitumia fursa ile ambapo macho na masikio ya dunia yalielekezwa Qunu, kwa yeye rais kuiambia dunia, na si kuisubiri CNN au vyombo vya habari vya Kimagharibi kuifanya kazi hiyo, juu ya mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika ikiwamo mchango wa Tanzania kumfanya Mandela na viongozi wengine wa Kiafrika kuonekana kama walivyoonekana kwenye macho ya dunia. 

  Hakika, JK anastahili pongezi kwa kazi njema aliyoifanya leo ya kuiweka tena Tanzania katika ramani ya dunia, si tu kama nchi ile ya mbuga za wanyama na Mlima Kilimanjaro, bali ' Taifa Kubwa' lililochangia kushiriki mikakati ya ukombozi ikiwemo kutoa misaada ya silaha, mafunzo na hata makazi kwa wapigania ukombozi wa Afrika.

  JK aliipitia historia ya mchango wa Tanzania ambayo wengi waliokuwa wakimsikiliza, ama waliisahau au hawakuijua kabisa.

  Lakini, tujiulize pia kama Watanzania, katika aliyoyasema JK kule Quni, ni Watanzania wangapi wanayajua? Inahusu umuhimu wa kuipitia historia yetu ili, kama Watanzana, tuweze kumiliki ' K3'- Kujitambua, Kujiamini na kuthubutu. Imefika mahali tunaionea aibu hata historia yetu.

  Na nyongeza katika yale aliyoyasema JK leo ni kumbukumbu ya kihistoria ambayo haitajwi pia, kuwa Baba wa Taifa , Mwalimu Nyerere, ndiye aliyempa hifadhi Tanzania, Rais wa Pili wa Afrika Kusini huru. Ni Thabo Mbeki. Baada ya kutoroka Afrika Kusini. Baadae Thabo Mbeki akaenda kusoma Uingereza.

  Jambo hilo linathibitishwa katika kitabu alichoandika msomi mahiri wa Afrika Kusini, William Gumede. Anasema;

  " In 1962, Thabo slipped out of the country to which he would not return for twenty -eight years, travelling through Botswana to Rhodesia, where he was arrested and held in a Bulawayo prison for several weeks. The white Rhodesian authorities intended to deport him back to South Africa and waiting for security police, but British Labour MP, Barbara Castle intervened after being lobbied by the ANC, and Mbeki was granted asylum in Tanzania by President Julius Nyerere." ( William Gumede, Thabo Mbeki and The Search For Soul of The ANC, pg 36)

  Naam, ni wakati sasa wa viongozi wengine, bila kujali itikadi zao, wanapokuwa kwenye majukwaa ya kimataifa, kuzitafuta fursa za kuonyesha yale ambayo huko nyuma tumekuwa na uwezo nayo, na bado, kama nchi, tunaweza kuaminika katika kutoa mchango wa uzoefu wetu kwenye masuala mbali mbali ya Kimataifa. 

  Maggid Mjengwa.


  0 0

  Bondia wa ngumi za kulipwa nchini shafii Ramdhan ameumia akiwa mazoezini  akijiandaa na pambano la tarehe 22 decemba pale friends corner hotel manzese ,Ramadhan aliyekuwa acheze na Hassan kiwale”moro best” alikutana na mkasa huo mazoezini kwake, taarifa hii iliripotiwa na kocha wa shafii ambae ni jafari ndame kwa Ibrahim kamwe wa bigright promotion kuwa kutokana na hali hiyo shafii hatoweza tena kucheza na moro best  na daktari pia hatoweza kucheza, na sasa imepangwa Hassan kiwale `moro best` atacheza na issa omar NAMPEPECHE, kwa kuwa issa omar ni mkali kiasi bigright promotion imekubali kumuongeza kiasi cha pesa moro best kucheza pambano hilo.


  Moro best na  issa Omar watacheza pambano hilo katika kuwasindikiza Japhet kaseba  anaetetea ubingwa wake dhidi ya Alibaba Ramadhan  ambae ni bingwa wa kanda ya kaskazini, pia kutakuwepo na pambano lingine la ubingwa kati ya fadhili awadh atakaeminyana na karage suba.
   Wakati Mbaruku heri na Mbabe mwenzake lusekelo daudi wanajaribu kumalizia kiporo chao kisichoisha kwani wameshacheza mara mbili katika ushindani mkubwa na mara zote wametoka sare mara hii wote wameahidi chochote na kitokee lazima pambano liwe na mshindi. 
  Nae Adam yahaya [baby edo] atazipiga na Harman Richard, huku mkongwe ernest bujiku[tyson] atacheza na shah kasimu , jocky hamis mkongwe wa zamani atazipiga na bondia sawa na mwanae  mbena rajabu, nae  shaban bodykitongoji akizipiga na mwinyi mzengela . pia siku hiyo kutakuwepo na lile pambano la mateke (kickboxing) la mtanzania anayeishi Canada Kareem kutchi  na mbongo halisi said juma `tata boy`. Tayari kiwango security ikisaidiana na jeshi la polisi wameahidi kutoa mchango mkubwa katika ulinzi na usalama wa watu wote watakaokuja katika  pambano hilo. 

  0 0

   Kikosi timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais
   Kikosi cha timu ya Istiqaama
   Meza kuu ya mgeni rasmi, Balozi msaidizi wa Urusi, Vicent Kalchenko wa tatu (kulia) na baadhi ya viongozi. 
   Katibu wa Timu ya VPO, Neemia Mandia, akisalimiana na mgeni rasmi Balozi msaidizi wa Urusi, Vicent Kalchenko kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
   Mtanange ukiendelea, (kulia) ni Sufiani Mafoto na (kushoto) ni Lucas, wakiwadhibiti wachezaji wa Istiqaama. Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Dar es Salaam Zoo Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar, timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais ilishinda mabao 2-1, yaliyofungwa na Kifaru katika kipindi cha kwanza.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Jengo la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar liliopo Maruhubi lililofunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad leo Dec 15 2013.
  Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar ikiwa pia ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi huko Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad (hayupo pichani) katika sherehe za ufunguzi wa Jengo la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
  Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad akiwahutubia wananchi na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar katika sherehe za ufunguzi wa Jengo la ofisi, madarasa na library (kulia) Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk na (kushoto) naibu wake Mhe. Bihindi Hamadi Khamis katika sherehe zilizofanyika Chuoni Maruhubi.
  Picha ya pamoja ya Mgeni rasmin Mukamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad Mawaziri mbalimbali na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).     

  ========  ======= =======  =======
  Na Maryam Fumu  Maelezo Zanzibar.
  Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad  amesema serikali imekuwa na muelekeo mkubwa wa kuimarisha  sekta ya Utalii  na kuleta mafanikio makubwa  yanayoweza kuingiza watalii kutoka nchi mbali mbali duniani.

  Alisema Zanzibar inaimarika mwaka hadi mwaka katika sekta hiyo ambapo hivi sasa imekuwa ikichangia wastani wa asilimia 80 ya fedha za kigeni katika kukuza uchumi wa Zanzibar.

  Alieleza hayo katika ufunguzi wa jengo la ofisi, Madarasa na Lebrary ya chuo cha maendeleo ya Utalii Maruhubi ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Alisema  kuwa serikali ina malengo makubwa  ya kuiendeleza sekta hiyo  kwa lengo la kuwanufaisha Wazanzibar na kufikia dhana ya utalii  kwa   wote kupitia katika ngazi zote za wilaya za Unguja na Pemba.
  Hata hivyo Maalim Seif amewataka viongozi kufanya juhudi kwa kukiimarisha na kuletea maendeleo Chuo hicho kwa  kuweka msimamizi mzuri wa historia ya  utamaduni, mila na silka za Wazanzibar ili zienendelee kuchafuliwa. 

  Pia makamo wa kwanza wa Rais aliahidi kulichukulia hatua barabara liliopo chuoni hapo ili liweze kupatiwa ufumbuzi.                  
  Nae mkurugenzi wa chuo hicho Bi Zuleikha Kombo Khamis amewaomba viongozi kushirikiana na  sekta Utalii katika kukijenga chuo hicho katika sehemu ilioharibika ili iweze kuwa na mazingira mazuri.
     
  Aidha Mkurugenzi   huyo alisema kuwa changamoto  zinazokikabili chuo hicho ikiwemo ukosefu wa barabara pamoja na mmongonyoko wa ardhi  sehemu ya nyuma ya chuo hicho linapelekea kuharibu maendeleo ya chuo.
  Hata hivyo Bi Zulekha ameshukuru serikali ya awamu ya saba kwa kuwajengea Jengo la Ghorofa mbili  jambo ambalo linawapa faraja katika kuleta maendeleo chuoni hapo.  

  0 0

  Na Samia Mussa.
   
  IKIWA zimesalia siku 13 kufanyika kwa Tamasha la Kimataifa la Krisimasi, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Temeke limewahakikishia ulinzi wa uhakika Watanzania  wote watakaohudhuria tamasha hilo linalotarajia kuanza Desemba 25 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 

  Kutokana na hali halisi ya kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakijitokeza katika matamasha ya kila mwaka yanayoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions, Dira ya Mtanzania lilitaka kujua kuhusiana na Jeshi la Polisi lilivyojipanga kuimarisha usalama siku ya Krimasi ambako Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo anasema kuwa kawaida Jeshi hilo limekuwa likijipanga vilivyo katika mikusanyiko ya namna hiyo hasa katika matamasha ya muziki wa Injili.

  Kiondo anasema kuwa Jeshi la Polisi ni wajibu wake kuhakikisha hali ya usalama inapatikana katika kila mkusanyiko mkubwa wa watu hasa katika matamasha kama itakavyokuwa katika siku ya Krisimasi katika Uwanja wa Taifa. Anasema kuwa kawaida katika matukio makubwa kama Tamasha la Krismasi ambalo litakwenda kukusanya umati wa watanzanzia kwa nia ya kusikiliza neno la Mungu kupitia nyimbo za injili wataweka ulinzi wa hali ya juu kulingana na hali halisi ya kiusalama ilivyo ulimwenguni.

  “Ni wajibu wetu kulinda usalama na kwamba tamasha linafanyika katika Uwanja wa Taifa, unawekwa ulinzi wa hali ya juu na wataalam wa mabomu pamoja na Mbwa wanakuwepo pale siku tatu kabla ya tamasha kwa ajili ya kufanya ukaguzi kila mahali eneo la uwanja,’’ anasema Kiondo.

  Anasema mbali ya kufanya ukaguzi huo pia kuna  wingi wa maaskari watakao eneo kila upande kwa ajili ya kuimarisha ulinzi baada ya kujiridhisha na hali ya usalama wa kutokuwepo kwa hatari ya mabomu.
  Kiondo anaeleza kuwa pamoja na kuwa hali si nzuri ya kiusalama kutokana na matishio ya ugaidi, Jeshi la polisi limejipanga vya kutosha ambapo alisisitiza kuwa wakazi wa Temeke na Watanzania kwa ujumla wasiwe na wasiwasi kwa kuwa hali ya usalama imeimarishwa hasa katika mikusanyiko.

  “Katika kipindi cha Krisimasi tunalazimika kufanya kazi ya ziada, kutokana na hali ilivyo hivi sasa, tunapenda kuwahakikishia watanzania kwamba kila atakayekwenda kwenye Tamasha ajihakikishie kwamba yupo salama kabisa,” anasema Kiondo.

  Anasema kila kamanda anawajibika katika eneo lake na endapo linatokea tatizo anawajibika moja kwa moja ikiwa ni pamoja na kuulizwa na rais Jakaya Kikwete kwamba alikuwa wapi wakati tatizo linatokea jambo ambalo Kiondo amesema halitatokea kwake ndio maana amejipanga vilivyo kuhakikisha hakuna hatari yoyote itakayotokea wakati wa Tamasha hilo la kimataifa.

  Ni mara ya kwanza kufanyika kwa tamasha la Krismasi ambako kampuni ya Msama imekuwa ikiandaa pia Tamasha la Pasaka ikiwa ni miaka 13 sasa kwa nia ya kusaidia jamii ikiwa pamoja na kusomesha watoto waliopo katika mazingiza magumu katika ngazi ya shule ya msingi, Sekondari na Vyuo, vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wanawake wajane. 

  Lengo la Tamasha hilo ni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kutolea misaada (Center)  pamoja na kiwanda cha kisasa cha kuzalishia kazi za wasanii  kwa manufaa ya Taifa na watu wake, kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imesaidia Watanzania wengi wenye ndoto ya kuwa wasanii wakubwa nchini.

  Tamasha la Kimataifa la Krismasi linatarajia kuanzia kufanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Desemba 25, Morogoro Desemba 26, ambako pia linatarajia kuwafikia wakazi wa  Tanga Desemba 28, Arusha Desemba 29 na Dodoma  Januari 1 mwaka 2014.

  0 0


  0 0
 • 12/16/13--04:40: Cabin Crew Course

 • 0 0

  Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Chriss Lenana (kushoto) na Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh wakikata utepe kuzindua rasmi duka la Vodacom ndani ya Uchumi Supermarket ikiwa ni huduma ya kwanza na ya kipekee nchini. Duka hilo linawawezesha wateja wa Vodacom kupata huduma za kampuni ikiwemo moderm, vocha, usajili wa nambari zao, M-pesa n.k wanapofika kwenye Supermarket hiyo kwa ajili ya kupata kufanya manunuzi ya mahitaji mengine.
  Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh akiongea na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa duka la Vodacom ndani ya Supermarket ya Uchumi. Vodacom imezindua pia huduma za malipo kwa M-pesa kwa wateja wanaofanya manunuzi ndani ya Supermarket hiyo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
  Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh akitumia huduma ya M-pesa kulipia bidhaa alizonunua ndani ya Supermarket ya Uchumi ya jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Chriss Linana. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Huduma za Maduka ya Vodacom Upendo Richard.
  Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh akikagua risiti aliyopatiwa baada ya kulipia huduma kwa njia ya M-pesa kwenye Supermarket ya Uchumi ya jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo. Kushoto ni Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Chriss Lenana na Mkuu wa Maduka ya Vodacom Upendo Richard.


  Katika muendelezo wa mapinduzi ya kuyaleta maisha kiganjani, sasa wateja wanaofika kupata huduma kwenye SuperMarkert ya Uchumi lililopo katika jengo la Quality Center jijini Dar es salaama wanauwezo wa kulipia huduma zao kwa njia ya M-pesa.

  Aidha, Vodacom pia imefungua duka la huduma kwa wateja wake ndani ya Supermarket hiyo ikiwa ni ubunifu wa aina yake hapa nchini na hivyo kuwapa nafasi ya kipekee wateja wa Vodacom kumaliza mahitaji yao yote kwa nwakati mmoja.

  “Tunazidi kuongoza katika ubunifu hili ni jambo tunalolipa kipaumbele kw alengo la kuhakikisha tunatoa nafasi kwa wateja wetu kufaidi matumizi ya teknolojia na kubadili maisha yao, hakuna shaka kila tunachokifanya kinawatimiza matarijio yao kwetu.”Alisema Ofisa Mkuu wa Mauzo na Mahusiano wa Vodacom.

  Kila mmoja Wakati huu w amsimu wa siku kuu angependa kuona anatumia muda mfupi na kwa urahisi zaidi kupata huduma, hatua moja muhimu ni kuwawezesha kuwa na njia rahisi na nyepesi zaidi ya kukamilisha mahitaji yao na hivyo ndivyo tunavyofanya leo kwa kuwatanagzi wateja wetu kutumia M-pesa wanapofika Uchumi SuperMarket.”Aliongeza

  Kwa sasa M-pesa inawaunganisha wateja wetu na biashara zaidi ya 300 katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kulipia tiketi za ndege ving’amuzi,LUKU, maji, kutoa na kuweka fedha katika akaunti za benki zaidi ya 20 na hivyo kuongoza soko miongoni mwa huduma za fedha kwa njia ya simu.. Kwa upande wake Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Tanzania, Chriss Lenana amebainisha kuwa ni jambo la furaha na kujivunia kuzinduliwa kwa ubia huo kati ya kampuni yake na Vodaco na hivyo kuwawezesha wateja wake kutumia simu zao kwa ajili ya malipo ya manunuzi.

  “Kufunguliwa kwa duka la Vodacom hapa kwetu kutasaidia sana wateja wetu si tu kuweza kupata huduma za M – PESA bali pia huduma nyingine za kimawasiliano na hatimaye kuepukana na matatizo ya kimawasiliano yanayowakabili. Tunapokea idadi kubwa ya wateja kila kukicha na kwa kufunguliwa kwa duka hili Vodacom wamefanya suala la msingi ambapo awali iliwalazimu wateja kusafiri mpaka makao makuu kufuata huduma hizo kitu ambacho ni usumbufu na kiusalama ni changamoto.” Alisema Lenana.

  “Huduma hii ya malipo kwa njia ya M-pesa tutaisamabza kwenye maduka yetu yote ambayoyapo kwenye mipango yetu ya mwaka 2014/2015, ni wazi tumewaptia wateja wetu kitu kizuri na tunawaomba watumie njia hii ya malipo kwa kujiamini kwani mteja hupatiwa pia stakabadhi ya mununizi”Aliongeza.

  Duka hilo ni moja kati ya maduka 200 ya Vodacom ambayo yapo mbioni kufunguliwa nchi nzima na pia ni muendelezo wa uboreshwaji wa huduma ya M – PESA na huduma nyinginezo za kampuni hiyo nchi nzima.

  0 0

  Tanzania’s President Jakaya Mrisho Kikwete was accorded a stunning ovation in his tribute to the late Nelson Mandela.
  President Kikwete’s speech made shame of Jomo Kenyatta regime that failed to help ANC set base in Kenya. Kikwete highlighted the support given by Mwalimu Julius Nyerere to the struggle against apartheid in South Africa.
  Kikwete named TANU, ANC, ZANU PF, FRELIMO and SWAPO as comrades, KANU was left OUT!
  “Tanzania under Julius Nyerere helped Black people struggle for emancipation in SA. Kenya under Jomo Kenyatta helped Boers/Whites to oppress and subjugate Black people in SA. Today, Jakaya Kiwete was global platform to pay tribute to global icon” George Nyongesa posted in his Facebook Page.

  0 0

  Mshindi wa Tatu wa Makala za mapambano dhidi ya UKIMWI kwa upande wa magazeti ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la The Citizen Peter Muthamia(kushoto) akipokea hundi ya shilingi laki tatu (300,000/-) kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) baada ya kuwa miongoni mwa washindi.
  Mshindi wa pili wa Makala za mapambano dhidi ya UKIMWI kwa upande wa magazeti ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la TanzaniaDaima Hellen Ngoromera (kushoto) akipokea hundi ya shilingi laki tatu na nusu(350,000/-) kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) baada ya kuwa miongoni mwa washindi.
  Mshindi wa nne kwa Makala za mapambano dhidi ya UKIMWI kwa upande wa magazeti ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Jamboleo Eben –Ezey Mende(kushoto) akipokea hundi ya shilingi laki mbili na nusu(250,000/-) kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) baada ya kuwa miongoni mwa washindi.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI(AJAAT) Simon Kivamo (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) jana(leo) jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza washindi wa shindano la makala za UKIMWI lilioendeshwa na AJAAT kwa mwaka 2013. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) na Meneja Mawasiliano wa AJAAT Perege Gumbo(kushoto).
  Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) jana(leo) jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza washindi wa shindano la makala za UKIMWI lilioendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI(AJAAT) kwa mwaka 2013. Wengine katika picha ni Mwenyekiti Mtendaji wa AJAAT Simon Kivamo (katikati) na Meneja Mawasiliano wa AJAAT Perege Gumbo(kushoto).Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa (kushoto) akikata akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Jengo la Ofisi za huduma kwa wateja za Azam TV, zilizopo kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, Tazara jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Rhys Torrington.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa akizungumza na vyombo mbali mbali vya habari vilivyokuwepo kwenye ufunguzi huo wa Jengo la Ofisi za huduma kwa wateja za Azam TV, zilizopo kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, Tazara jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Rhys Torrington akisisitiza jambo mbele ya waandishu wa habari (hawapo pichani) juu ya huduma mbali mbali wazitoazo kama Azam TV.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa akisalimiana na baadhi ya waigizaji wa Filamu nchini kutoka kundi la (Bongo Movie) waliokuwepo kwenye Ufunguzi huo uliofanyika leo jijini Dar.


older | 1 | .... | 297 | 298 | (Page 299) | 300 | 301 | .... | 3283 | newer