Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 296 | 297 | (Page 298) | 299 | 300 | .... | 3270 | newer

  0 0

  TUMEPUNGUZA BEI ZA KUSHIP MAGARI KWENDA DAR/MOMBASA
  4 X 4 CARS TO DAR/MOMBASA NOW FROM  £800
  SALOON CARS NOW FROM £700
  TUNATOA  25 DAYS FREE STORAGE IN MOMBASA
  TELEX RELEASE KWA MOMBASA NI FREE

  20' CONTAINER TO DAR/MOMBASA £1,350
  40' CONTAINER TO DAR MOMBASA £1,800
  THIS IS MORE THAN £600 SAVINGS!!!!

  KWA NINI  ULIPE ZAIDI?
  BIASHARA NI SAVINGS NA FAIDA
  ONGEZA FAIDA NA SERENGETI

  WAPI UTAPATA BEI KAMA HIZI?

  AIR CARGO TO DAR NOW £3.80
  INCLUSIVE CLEARANCE
  FREE COLLECTION FROM ANY ADDRESS IN EAST LONDON
  AGENT WETU EAST LONDON
  SAFARI CARGO
  704 ROMFORD ROAD
  TEL 02085142285

  0 0

  Former President Of United Republic Of Tanzania (3tm),Hon. Benjamin Mkapa is a. Co-Chairman of ICF together with Neville Isdell a former boss of Coca Cola International. ICF is the main donor to the Ethiopian project together with International Finance Corperation (IFC). Other projects supported ans sponsored by ICF include Ethiopia Commodity Exchange, (ECX) a state of art Commodity Exchage only second to the Johannesburg Commodity Exchnge in Africa. Former President Benjamin. Mkapa is expected to return to Dar Es Salaam, later today (Saturday 14th. December 2013) after a long trip to Australia and Ethiopia.

  0 0

  Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Mkazi, Mhe. Goodluck Ole Medeye, akikabithi tuzo ya mshindi wa kwanza ya hesabu bora za mwaka 2012 katika sekta ya hifadhi ya jamii iliyochukuliwa na Mfuko wa Pensheni wa LEPF ambapo ilipokelewa na Mkurugenzi wa Fedha wa Lapf, John Kida. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Pius Maneno. Sherehe hizo zimefanyika jana usiku katika hoteli ya Naura Springs mjini Arusha.
  Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, John Kida, mwenye tuzo, akionyesha Tuzo ya Ubora wa mahesabu kwa wafanyakazi wa LAPF mara baada ya kukabidhiwa. Kutoka Kushoto ni Mhasibu Mkuu wa LEPF, Rock Massawe, Meneja Kanda ya Kaskazini, Rajab Kinande, na kulia ni mtumishi wa LEPF Arusha, Flowin Ngonyani wakati wa sherehe za kukabidhiwa tuzo za NBAA zilizofanyika jana usiku katika hoteli ya Naura springs, Arusha.
  Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, John Kida, mwenye tuzo, akizungumza na waandishi wa habari, (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya NBAA ya ubora wa mahesabu kwa sekta za hifadhi za jamii. Kulia ni Afisa Masoko wa LAPF, Rehema Mkamba na Kushoto ni Mhasibu Mkuu wa LAPF, Rock Masawe wakati wa sherehe za kukabidhiwa tuzo za NBAA zilizofanyika jana usiku katika hoteli ya Naura springs, Arusha.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia) akimkaribisha Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) mara tu baada ya kuwasili nchini kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Kati kati ni Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner.
  Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole akikabidhiwa maua mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania .
  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kushoto) akimuongoza Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (katikati) kuelekea sehemu ya VIP kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)mara tu baada ya kuwasili nchini jana usiku.
  Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) pamoja na Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner (kulia) wakikamilisha taratibu zakupata hati ya kuingia nchini kwenye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania .
  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia) akimuelekeza jambo Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner (katika) mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Kushoto ni Picha na Mpiga picha wetu. Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole.
  Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (mbele) akitoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwelekea hotelini alipofikia mara bada ya kuwasili nchini jana usiku. Nyuma yake ni mwenyeji waka ambaye ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando .

  0 0


  0 0

  Wafanyakazi wa Chuo kikuu kishiriki cha elimu dar es Salaam 'wakipasha'kabla ya kuanza kwa bonanza la wafanyakazi wa chuo hicho, bonanza hilo lilishirikisha wafanyakazi wote wa chuo hicho.
  Wafanyakazi wa Chuo kikuu kishiriki cha elimu dar es Salaam 'wakipasha'kabla ya kuanza kwa bonanza la wafanyakazi wa chuo hicho, bonanza hilo lilishirikisha wafanyakazi wote wa chuo hicho.
  Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu dar es Salaam (DUCE) Profesa Godliving Mtui akizundua Bonanza la wafanyakazi wa chuo hicho lililofanyika jana chuoni hapa na kuwashikisha wafanyakazi wote wa chuo hicho.  


  0 0

  HATIMAYE ile siku iliyokuwa inasubiriwa na wengi, imewadia, ni GURUMO 53 ndani ya viwanja vya TCC Club, Chang’ombe leo Jumamosi Disemba 14.

  Kama tangazo linavyojionyesha, ni tamasha kubwa la muziki wa dansi la kustaafu kwa gwiji Muhidin Maalim Gurumo aliyeitumikia fani hiyo kwa miaka 53 mfululizo. Gurumo ataimba angalau wimbo mmoja au zaidi wa kila bendi aliyopitia katika safari yake ndefu kimuziki.

  Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha, Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma ambayo hapo awali ilijulikana kwa majina ya NUTTA, Juwata na OTTU. Gurumo ameitumika Msondo katika majina yote ya nyuma.

  Ama kwa hakika ni burudani ya kukata na shoka, bendi kibao, wasanii kibao – ni burudani mwanzo mwisho kuanzia saa 12 jioni mpaka majogoo.

  0 0

  Meneja wa Vodacom Tanzania,Manispaa ya Morogoro Kamanda Kasapila[kushoto] akihakika kadi za pikipiki za washini wa bodaboda wanaoshuhudia kulia kabla ya kuwakabidhi washindi hao,waliojishindia katika promosheni ya Timka na Bodaboda inayoendeshwa na kampuni hiyo.
  Washindi wa nne wa Promosheni ya Timka na Bodaboda kutoka wilaya mbali mbali za mkoa wa Morogoro'
  Baadhi ya Washindi wa promosheni ya Timka na Bodaboda wakiwa juu ya pikipiki zao mara baada ya kukabidhiwa rasmi pikipiki zao na Meneja wa Vodacom Tanzania,Manispaa ya Morogoro Kamanda Kasapila[hayupo pichani]

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpatia zawadi ya Krismas na Mwaka Mpya Binti Asnah Sudi, kutoka kituo cha kulelea watoto yatima cha Umra kilichoko Magomeni, wakati wa sherehe ya mwaka kwa watoto yatima aliyoiandaa kwa kushirikiana na Twiga Cement na Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam tarehe 14.12.2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia baadhi ya michezo iliyokuwa ikichezwa na watoto yatima kutoka baadhi ya vituo hapa Dar es Salaam kwenye sherehe ya mwaka ya watoto hao iliyofanyika tarehe14.12.2013.
  Father Krismas akiwagawia watoto yatima zawadi zao wakati wa hafla iliyoandaliwa na Mama Salma Kikwete kwenye ofisi za WAMA, tarehe 14.12.2013.
  Baadhi ya watoto yatima kutoka vituo vya kulelea vya, Umra, Kurasini MUMalaika wakiwa katika hafla ya kumaliza mwaka zilizofanyika kwenye ofisi za WAMA. Sherehe hiyo iliandaliwa kwa pamoja na Twiga Cement, Rotary Club na WAMA tarehe 14.12.2013.PICHA NA JOHN LUKUWI

  0 0

  NA BASHIR NKOROMO

  Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kikao chake kilichofanyika jana mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete imeibuka na masuala mazito kadhaa, ambayo leo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (pichani) ameyaeleza wakati akizungumza na waandishi wa Habari, Katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lumumba jijini Dar es Salaam.

  Moja ya mambo ambayo Nape amezungumzia, ni kuhusu Kamati Kuu hiyo kuwahoji Mawaziri saba, kujibu kero au mambo kadhaa ambayo yaliibuliwa wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana iliyomalizika hivi karibuni katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe.

  Nape  alisema, Kamati Kuu iliwahoji mmoja baada ya mwingine, kuanzia saa tano asubuhi hadi jioni, baada ya kila mmoja kufika akiwa ameandaa majibu ya tuhuma au hoja alizokuwa ametakiwa kujibu mbele ya Kamati Kuu hiyo.


  0 0

   Kaimu Mhandisi wa Maji Manispaa ya Temeke, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Meckiline Haule (katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa gharama ya sh. mil. 35 katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Wanaoshuhudia ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Isabela Ipopo (kushoto),Mwakilishi wa Mauzo wa TBL, Allen Mwebuga (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Rumelius Bakilane.
   Mwebuga wa TBL (kushoto) na Bakilane wakifujaza maji kwenye ndoo wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
   Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Rumelius Bakilane  akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Kijiji cha Kibada, Diana Salvatory baada ya kampuni hiyo kukabidhi kisima cha maji katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kisima hicho chenye uwezo wa kuhifadhi maji lita za ujazo 1,600 kwa saa uchimbaji umegharimu sh. mil 35 zilizotolewa msaada na TBL.
  Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akielezea mikakati ya TBL kusaidia miradi ya maji nchini ambapo kwa mwaka wafedha wa TBL tayari imetenga sh. mil. 450 kwa kazi hiyo.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

  0 0

    Mashabiki wakifurahi burudani iliyokuwa ikitolewa juu ya steji.
   Msanii Nguli wa muziki wa kizazi kipya,Chege Chigunda a.k.a Mtoto wa Mama Said akitumbuiza mbele ya mashabiki kibao waliofika kwenye tamasha la After Skull Bash,lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar. Tamasha hilo limeratibiwa na Clouds FM kwa kushirikiana na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd.
   DJ Mahiri kutoka Clouds FM,Dj Zero akifanya makamuzi ya nguvu ndani ya Mbalamwezi Beach,wakati wa tamasha la After Skull Bash likiendelea,Tamasha hilo limewakutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali jioni ya leo.
   Msanii wa muziki wa Kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga ya muziki wa bongofleva,Rich Mavoko akikamua vilivyo jioni ya leo kwenye tamasha la After Skull Bash,lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar.
   Watangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu na Dj Fetty wakijadiliana jambo nyuma ya jukwaa.
   Mashabiki kibao wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri jukwaani jioni ya leo

  0 0

  Kikosi cha Yanga.
   Kocha wa Yanga, Ernstus Brands (kulia), akifuatilia pambano la kirafiki kati ya Yanga na KMKM lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo. Yanga imeshinda ilishinda 3-2. (Picha na Francis Dande)
  Benchi la Ufundi la timu ya KMKM ya Zanzibar.
   David Luhende wa Yanga akiwania mpira.
   Mshambuliaji wa Yanga, Reliants Lusajo akichuana na mchezaji wa KMKM, Mwinyi Ameir Makungu.
   Beki wa KMKM, Faki Ali Amad (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka mshambuliaji wa pembeni wa Yanga, Simon Msuva katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
   Msuva akichuana na Faki Ali Hamad.
   Kipa wa Yanga Juma Kaseja akiokoa moja ya hatari langoni mwake.

  Mshambuliaji wa KMKM, Nassor Ali Omar akiruka juu kuwania mpira sambamba na Simon Msuva wa Yanga.
   Mashabiki wa Yanga.

  0 0

   Fuso ikiwa imekwama.
  Jamaa akichimba ili aweze kupita  
   Lori likiwa limebeba nguzo za umeme likiwa limekwana eneo la Lwamadovela wilayani Makete
   Basi la kampuni ya Mwafrika likipenya kwa tabu pembezoni lilipokwama lori lililobebe nguzo za umeme
  Basi la kampuni ya Japanese nalo likivutwa kunasuka kwenye tope zito wakati likitafuta upenyo wa kupita.Picha zote na Edwin Moshi, makete

  0 0

  Mahafali ya 19 ya chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) yamefanyika ijumaa ya desemba 13 mwaka huu ambapo wahitimu katika ngazi za stashahada na cheti kwenye fani ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma, na mahuasiano ya umma wamehitimu.

  Tazama picha za baadhi ya matukio wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
   Mgeni  rasmi akiwa katika meza kuu  na Mkuu wa chuo , pamoja na viongozi wengine wa chuo na viongozi wa Serikali ya wanafunzi 

   Kutoka kushoto ni Fabian, Dotto Mandolin Kahindi, Abushehe Nondo, Benjamin Mwangoka
    Wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

  0 0
 • 12/14/13--13:43: KUMBUKUBU
 • MZEE HUDSON CHACHA RYOBA
  (08/12/1933 – 15/12/2007)

  Baba yetu mpenzi ni miaka sita saa imetimia tangu ulivyotuacha kimya bila ya kuongea. Uliweza kuona kila kilichokuwa kinatendeka lakini kwa maumivu makali uliyokuwa nayo hukuweza kuzungumza. Ni huzuni kubwa sana kutengana nawe mpenzi wetu, lakini tunajua kwamba ipo siku itafika tutakuwa pamoja nawe mbinguni kwa Mungu.

  Baba urithi mkubwa wa maneno yako ya busara na hekima ndiyo imekuwa nguzo kubwa katika maisha yetu ya kila siku. Unakumbukwa sana na wake zako na watoto wako Marwa, Leah, Debora, Bhoke, Taifa, Muniko, Mariba, Nyangi, Samwel, Wankyo na Stan.

  Pia bila kuwasahau wadogo zalo, marafiki zako, watani na wote waliokufahamu . Tunakosa vichekesho vyako kwani ulikuwa ni changamamoto ya furaha pale palipo kuwa na huzuni.

  Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi.
  Amen. 
   (Revelation 15:4) (Psalms 100)

  0 0

  Timu ya Netiboli ya Bunge la Tanzania imefanikiwa kuibuka mabingwa kwa mara ya pili mfurulizo katika michuano ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika Jijini Kampala nchini Uganda kuanzia Desemba 07,2013 mwaka huu.

  Fainali za michuano hii zimefanyika katika uwanja wa Mandela Namboole jijini Kampala Uganda.

  Bunge Tanzania imenyakua ubingwa huo baada ya kuichalaza timu ya wenyeji Bunge la Uganda kwa Jumla ya Mabao 35-32, na hivyo kutetea kombe lake ililoshinda kuanzia mwaka jana.

  Mshindi wa tatu timu ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki imefanikiwa kuchukua nafasi ya tatu baada ya kuichapa timu ya Bunge la Kenya.

  Katika Soka timu ya Bunge la Uganda imefanikiwa kutetea ubingwa wake kwa mara ya tatu mfurulizo baada ya kuichapa timu ya jumuiya ya Afrika Mashariki 3-0, mshindi wa tatu katika Soka ni timu ya Bunge la Kenya iliyoichapa timu ya Bunge la Rwanda 2-1

  Rais wa Uganda Yoeri Kaguta Museven alikua mgeni rasmi katika fainali za mashindano haya ambapo amesema anafurahishwa na jinsi mashindano yanavyowaleta wana Afrika Mashariki pamoja na kwamba mshindi wa mashindano haya ni Afrika Mashariki. Museven pia amesema anawapongeza wote huku akisema nchi zote ni watoto wake.
  Kepteni wa timu ya Jumuiya ya Afrika akinyanyua Kombe la Mshindi wa tatu katika Netiboli.
  Rais Yoeri Kaguta Museveni akipiga danadana kabla ya pambano la Soka la fainali kati ya timu ya Bunge la Uganda na timu ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Uganda imeshinda kwa 3-0.
  Kepteni wa timu ya Netiboli ya Bunge la Tanzania Grace Kihwelu akinyanyua kombe juu baada ya kukabidhiwa na kutangazwa rasmi kuwa mabingwa wa michuano hiyo kwa netiboli.


  0 0
 • 12/14/13--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • RIP Nelson Mandela - Allstars Tribute Song - 46664

  0 0

  Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa na kamanda wa vijana ccm Iringa Salim Abri Asas Abri akiwa katika moja ya matukio ya kuwahudumia wananchi  kulia ni RTO  SP Panfil Honono
  ==========  ========  =========
  SALIM ABRI ASASI AWAPA SOMO UVCCM IRINGA

  Na Denis Mlowe, Iringa

  KAMANDA wa umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Iringa, Salim Asas ameunga mkono wito wa Mwenyekiti wa UVCCM mkoani humo, Tumaini Msowoya la kutaka vijana wa jumuiya hiyo wasikubali kugawanywa kwenye mambo ya siasa na watu wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo ubunge,udiwani  ili kulinda heshima ya jumuiya hiyo na chama kwa ujumla.

  Akifunga mkutano wa uchaguzi wa Chipukizi wa mkoa huo, Abri alisema heshima ya jumuiya hiyo ni vijana kufanya kazi kwa mujibu wa kanuni na taratibu na sio mapenzi ya mtu bali ni sera ya chama ndio wanayotakiwa kuifuata na kuepuka ushawishi kutoka kwa watu wenye nia ya kuwagawanya.

  Alisema ni jukumu ya UVCCM mkoa wa  Iringa ni kuhakikisha vijana hawafanyi kazi kwa maslahi ya watu wanaotaka uongozi mwaka 2015, jambo ambalo likiachwa liendelee linaweza kuimega na kuidhoofisha jumuiya yao inayojitegemea katika maamuzi kwa upande wa vijana.

  Awali, akimkaribisha Kamanda huyo, Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Iringa, Tumani Msowoya alitoa wito kwa CCM na wanachama wanachama wake kuhakikisha kuwa, wanaiacha jumuiya yao ifanye kazi kwa mujibu wa kanuni na taratibu zilizopo kwa manufaa ya chama hicho na sio mtu au watu wenye nia ya kujinufaisha kupitia umoja wao.

  Aliwaagiza viongozi wa UVCCM kwa ngazi zote kutoa taarifa ya kuwepo kwa baadhi ya watu wenye nia ya kuwania nafasi za uongozi, ambao wanataka kuitumia jumuiya yao kama njia ya mafanikio yao kiuongozi.

  “UVCCM ya sasa haitakubali kuyumbishwa wala kugawanywa na mtu yeyote mwenye nia ya kuomba madaraka, itafanya kazi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa na katiba ya chama hicho kwa upande wa vijana” alisema Msowoya.

  Msowoya aliwataka vijana kufanya kazi kwa juhudi zote kwa lengo lakujiongezea kipato ikiwepo kujiunga kwenye vikundi vidogo vidogo kuweza kupatiwa mikopo ya riba nafuu kuliko kuwa mmoja mmoja na kushindwa kupata mikopo katika taasisi zinazohusika katika kutoa mikopo.

  “Vijana wenzangu tuepuke kuchagua kazi kwa maisha ya sasa ebu jiulieze kama tutachagua kazi, tutaendelea kugawanywa kwani watatupatia fedha ili tulinde maslahi yao, nawaomba sana tusikubali kuwatetemekea wenye fedha wanaotaka madaraka kwa njia ya kuhonga badala yake kila mmoja afanye kazi kwa bidii ili kuwa na uhakika wa kipato anachokipata kwa kazi halali kuliko fedha ya muda mfupi majuto baadaye,”alisema Msowoya

  Akizungumzia uchaguzi wa chipukizi mkoani humo, Katibu wa UVCCM mkoani humo Alawi Haidar alisema umefanyika kwa amani na utulivu na kwamba, watoto hao wameweza kuwapata viongozi bora walioona wanawafaa.

  Akitangaza matokeo hayo, Haidar alisema Mwenyekiti mpya wa chipukizi mkoani humo, Enock Luhala alifanikiwa kushindwa kwa kura 18 kati ya 33 zilizopigwa na kuwashinda wenzake, Ashraf Mpogole aliyepata kura 12 na Magreth Lusingo kura nne.

  Katika nafasi ya mkutano mkuu wa chipukizi taifa, Junior Mlelwa alishinda kwa kura 26 na kuwabwaga wenzake, Halid Aziz na Christopher Dalu.

  Wengine walioshinda ni Tausi Mgambo, Rukia Kimweli na Amina Kimweli kuwa wajumbe wa kamati ya uendeshaji mkoa.

  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Luteni usu Evarist Mawalla wakati alipowatunuku Kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi Tanzania baada ya kuhitimu mafunzo yao katika Chuo Cha Jeshi Monduli Juu mjini Arusha jana.Luteni Usu Mawalla aliibuka mwanafunzi bora katika mafunzo hayo yaliyochukua takribani mwaka mmoja ambapo wanafunzi kutoka nchi za kigeni pia walishiriki.
  Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Luteni Usu Immaculata Leodgar Mapunda baada ya kuibuka mwanafunzi bora wa kike katika kozi ya maafiseshi la Wananchi wa Tanzania iliyofanyika Chuo Cha Jeshi Monduli mjini Arusha jana.Katika mafunzo hayo yaliyochukua takriban mwaka mmoja baadhi ya wanafunzi kutoka nchi za kigeni nao walishiriki mafunzo hayo.
  Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa hafla ya kuwatunuku Kamisheni Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania iliyofanyika Chuo Cha Jeshi Monduli mjini Arusha jana.Katika mafunzo hayo yaliyochukua takriban mwaka mmoja baadhi ya wanafunzi kutoka nchi za kigeni nao walishiriki mafunzo hayo.(picha na Freddy Maro)
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole na kumrekebisha tai mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa ambaye juzi alinusurika katika ajali ya ndege baada ya ndege aliyokuwa akisafiria inayomilikiwa na Shirika la Ndege ya Precision kupasuka matairi yote ya nyuma wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa mjini Arusha. Rais Kikwete alikuwa Monduli Mkoani Arusha kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania katika chuo cha jeshi Monduli.

older | 1 | .... | 296 | 297 | (Page 298) | 299 | 300 | .... | 3270 | newer