Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 295 | 296 | (Page 297) | 298 | 299 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Watanzania waishio Korea Kusini walipata bahati ya kutembelewa na Mh. Bernard Membe; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa siku ya tarehe 8 Disemba 2013, katika Chuo Kikuu cha Dongguk jijini Seoul. 

  Katika mkutano huo, Waziri alifurahishwa sana na muamko, uelewa, na malengo kabambe ya Jumuiya ya Watanzania nchini Korea (TANROK) katika kujiendeleza na kuendeleza nchi yao. 

  Waziri alitoa taarifa ya hali ya uchumi, siasa, na kijamii nchini Tanzania na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wanadiaspora ili waweze kutumia vizuri elimu na ujuzi wanaopata ughaibuni katika kuendeleza nchi yao.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Korea Kusini jijini Seoul.
  Mh. Bernard Membe (wapili toka kushoto) akijibu hoja mbalimbali za Watanzania waishio Korea Kusini. Katikati ni Mwenyekiti wa TANROK Bw. Rayton Kwembe, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia Balozi Mbelwa Kairuki, na wa mwisho kulia ni Katibu wa TANROK Bw. Innocent Lugendo. Wa kwanza kushoto ni afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Japan anayeshughulikia Masuala ya Korea Kusini, Bw. Francis Mossongo.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe na Mkewe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa idara ya Asia na Australia katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Mbelwa Kairuki wakipozi kwa picha ya pamoja na baadhi Watanzania Waishio nchini Korea Kusini.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo kubwa ya mwezi ya Promosheni ya “Timka na BodaBoda”kulia ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Humudi Abdulhussein,Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

  Watanzania washauriwa kuchangamkia Promosheni ya Timka na Bodaboda,kwani zimebaki siku 44 tu zinazoweza kubadilisha maisha yao kabisa na kuwa mazuri na yenye maendeleo.

  Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambayo ndiyo inaendesha zoezi hilo imetoa wito huo kupitia Meneja Uhusiano wa Umma na kuweza kutangaza kwamba mpaka sasa jumla ya washindi 230 wamejishindia pikipiki maarufu”Bodaboda” na jumla ya fedha taslimu kiasi cha shilingi Milioni 142 zikiwa tayari zimekwisha tolewa ambapo Milioni moja moja zilikwenda kwa washindi 92, Milioni 5 zikienda kwa washindi 8, wakati mjasiriamali mwanamama, ambaye ni mkazi wa Arusha,Haika Mosha akiibuka kinara wa mwezi na kujishindia kitita cha shilingi Milioni 10.

  Akizungumzia kuhusiana na promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu alisema “mwitikio umekuwa mkubwa sana tangu wamezindua promosheni hiyo mpaka hapa tulipofikia kwani watu wamekuwa wakijishindia bodaboda kwa ajili ya usafiri ama kuanzisha biashara na pia fedha taslimu ambazo zimekuwa zikitumika kufanyia biashara ama kuongeza mitaji yao na matumizi mengine ya kimaisha.”

  “Promosheni hii inamlenga kila mwananchi kwani tatizo la usafiri ni letu sote na pia kilio cha watu kutokuwa na fedha za kukuza au kuongeza mitaji yao ya kibiashara ni sugu kwa kila Mwananchi. Hivyo basi kwa hali niliyoiona kwamba mitaji ni kilio kikubwa cha wajasiriamali wengi nchini,kwa kuunga mkono jitihada za wajasiriamali nchini Vodacom ndiyo maana tumekuja na promosheni hii,Hivyo tunaamini kupitia promosheni hii ya kuwafanya wateja wetu kushinda bodaboda pamoja na fedha hizi tunazozitoa kwa washindi zitasaidia kupiga hatua na kuweza kubadilisha maisha ya watanzania.

  Pia napenda kuwaasa washindi wote wa promosheni hii kutumia pesa zao ipasavyo kwa kuwekeza katika masuala ya kimaendeleo na kuleta manufaa katika jamii inayowazunguka.Alisema Nkurlu.Ili kujiunga na promosheni hii wateja wanatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.

  0 0

  In recognition of Computer Science Education Week, the United States Department of State’s Global Partnership Initiative together with CoderDojo and the LIONS@FRICA partnership, launched a new initiative today called afriCoderDojo to teach youth in Africa 21st century computer technology skills.  

  afriCoderDojo is a pan-African effort to teach young people the ability to understand and build fluency in coding, and learn the computer languages that are used to develop websites, mobile phone applications, computer programs, and electronic games. Based on the global open-source CoderDojo movement, afriCoderDojo will rely on a volunteer network of implementers and experienced coders located across Africa to run the two-month learning program. 

  afriCoderDojo aims to provide young people with the basics of coding through a fun and motivating curriculum. Guest lecturers, local technology entrepreneurs, and United States Embassies across Africa will also be invited to participate in the learning program to highlight and showcase career opportunities in the field of internet technology. 

  The inaugural afriCoderDojo clubs are due to launch in Dar-es-Salaam, Tanzania and Lagos, Nigeria in January 2014.  The groups will be sponsored by the Dar Teknohama Business Incubator – a national incubator for technology businesses – in Tanzania and Oando Foundation – the foundation for Africa’s largest integrated energy company– in Nigeria. 

  For more information about afriCoderDojo, please go to www.africa.co/africoderdojo or follow us on Twitter @afriCoderDojo.  If you are interested in hosting an afriCoderDojo in your community, please email partnerships@state.gov.

  0 0

  Makamu wa Rais (TBF) Phares Magesa kushoto akirudisha fomu za kugombea uongozi wa TBF leo katika ofisi za baraza la michezo la Taifa (BMT), anayepokea fomu ni afisa mwandamizi wa michezo wa BMT, Ndg. Magesa anagombea nafasi ya Rais wa shirikisho la mpira wa Kikapu (TBF).

  0 0


  0 0

  Mbunge wa jimbo la Kongwa mkoani Dodoma, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, akihutubia mamia ya wakulima huko Kibaigwa mkoani humo Jumatano Desemba 11, 2013. Ndugai akiwakilisha wabunge kutoka majimbo ya mkoani humo yanayopakana na wilaya ya Kiteto, mkoani manyara, wamekemea vikali uamuzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, kuwafukuza wakulima kutoka nje ya wilaya ya Kiteto na kuwakumbatia Wafugaji kuendelea na wa kimasai kuendelea na shughuli za uchungaji wa mifugo na kufananisha kitendo hicho ni sawa na ubaguzi.
  Mbunge wa Kondoa Kusini Mkoani Dodoma aliyekuwa ameambatana na Naibu Spika Mhe. Juma Nkamia akiwahutubia wakulima hao katika Mji wa Kibaigwa na kuwahakikishia kuwa watafikisha kero zao kwa Mhe. Waziri Mkuu ili kupata ufumbuzi wa tatizo la kufukuzwa kwa wakulima hao katika maeneo yao huko Kiteto.
  Mhe. Richard kapinye Diwani wa Kata ya Kibaigwa akieleza kwa hisia kali baadhi ya kero zinazowakabili wakulima hao kutokana na kunyanyaswa na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa kuwafukuza katika maeneo yao na kufumbia macho vitendo vya wafugaji kuwaua wakulima na hakuna hatua zinazochukuliwa.


  0 0

  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akipokea boksi la simu kutoka kwa Bi Safia Telatela ambae ni Mratibu wa Mradi wa Wazazi na Mwana nchini (The WnM Project) kwa ajili ya kusaidia mawasiliano kwa vituo vya afya Mkoani Rukwa katika kupambana na vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga. Jumla ya simu sitini aina ya Nokia zimetolewa katika maeneo ya mradi huo Mkoani Rukwa ambayo ni Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Kalambo na Nkasi. Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Tawala Mkoa hu amelishukuru shirika la maendeleo CIDA kwa kufadhili mradi huo utakaosaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto kwa kurahisisha mawasiliano na sehemu zenye huduma sahihi za afya.
  Afisa Tawala wa Mradi huo wa Wazazi na Mwana (MnW) Bwana Mashauri Ndebile akionyesha moja ya simu hizo aina ya Nokia kwa waandishi wa habari waliohudhuria katika hafla hiyo ya makabidhiano. Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo CIDA na kutekelezwa na Miradi Mitatu ya Plan, Africare, Jhpiego kwa kushirikiana na MOHSW. Mradi huo unatekelezwa katika Mikoa miwili nchini ambayo ni Mwanza kwa Wilaya za Ilemela na Sengerema na Rukwa kwa Wilaya za Kalambo, Nkasi na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.
  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Kimulika Galikunga Boksi moja lenye simu ishirini kwa ajili ya vituo vya afya katika halmashauri hiyo. 
  Bi Safia Telatela ambae ni Mratibu wa Mradi wa Wazazi na Mwana nchini (The WnM Project) akizungumza katika hafla hiyo ambapo alisema lengo kubwa la mradi huo ni kuona vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga vinapungua na hatimae kuisha kabisa, alisema hilo litawezekana pale jamii, taasisi binafsi, mashirika ya maendeleo na Serikali zitakaposhirikiana katika kuleta ustawi katika eneo hilo.
  Picha ya Pamoja.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya
  Baraza la Taifa la Biashara, Balozi Ombeni Sefue

  Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa 'Big Results Now' ni miongoni mwa agenda kuu zitakazojadiliwa kwenye mkutano wa saba wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam,siku ya jumatatu wiki ijayo.

  Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Baraza, Balozi Ombeni Sefue, amewaambia waandishi wa habari jana kuwa mada maalum juu ya ushiriki wa sekta binafsi katika mpango huo wa matokeo makubwa sasa utawasilishwa kwenye mkutano.

  "Kuna maeneo sita ambayo yaliainishwa katika utekelezaji wa mpango huo na wajumbe wa mkutano watajadiliana namna ya utekelezaji wake na  maboresho mbalimbali ilikuleta ufanisi zaidi," alisema.

  Mwenyekiti huyo ambaye hakutaka kwenda kwa undani zaidi kuhusu mpango huo alielezea matumaini yake kwamba wajumbe kutoka sekta zote za umma na ile ya binafsi watatoa mchango mkubwa kwenye mkutano huo na swala kubwa mbele yao ikiwa kuleta maendeleo ya taifa na watu wake.

   " Hakuna shaka, mkutano utakuwa makini na ni matarajio yangu kuwa wajumbe wote watakuwa na lengo moja badala ya kulaumiana kila upande bila sabubu za msingi," aliongeza Balozi Sefue.

  Kwa mujibu wa Balozi Sefue,kikundi Kazi cha baraza kitawasilisha pia mada kuhusu mazingira ya kufanya Kazi na uwezeshaji kiuchumi,ukizingatia kuwa serikali ya awamu ya nne imedhamiria kwa dhati kuona utekelezaji wa mambo hayo unafanikiwa.

  " Maswala haya mawili ( economic empowerment and business environment) yanahitaji ufahamu wa kina na kuona ni namna gani kwa pamoja tunaweza kuyashughulikia na kuleta matokeo mazuri," alisema na kuongeza kuwa mkutano utakuwa chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza.

  Balozi Sefue amewataka wajumbe toka pande zote kutoa michango yao ya mawazo kwenye mkutano ili mwisho wake suluhisho ya matatizo iweze kupatikana kwani pande zote zinaaminika na umma wa Tanzania.

  Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF),Bw.Godfrey Simbeye alisema wajumbe kutoka taasisi hiyo wamejiandaa na agenda zao kwenye mkutano huo muhimu.

  Bw.Simbeye amesema kuwa sekta binafsi inaitaka serikali iwe makini katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara ilikuiwezesha sekta hiyo kufanya biashara kwa faida na kupanua wigo wa ukusanyaji kodi ambayo ni kichocheo kikubwa kwa maendeleo ya nchi.

  "Kama mazingira ya kufanya biashara yatakuwa mazuri na kuvutia, basi mafanikio kufikia malengo ya milenia 2025 yanaweza kufanikiwa kwa urahisi," alisema na kuongeza kuwa ni lazima serikali itoe kipaumbele zaidi kwa eneo hilo.

  Bw.Simbeye alisema jitihada za pamoja zinahitajika kuhakikisha nchi inasonga mbele na kuwa na uchumi wa kati na kuleta manufaa makubwa kwa watanzania wote.

  " Sisi kama TPSF tunapenda suala la uwezeshaji kiuchumi linapata msukumo stahiki na serikali ukilinganisha na jitihada zinazofanywa kwa sasa katika kushughulikia suala hilo," alisisitiza.


  0 0

   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula akisoma hotuba ya ufunguzi katika warsha ya kufunga mradi wa matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa katika Chuo ChaTaifa cha Utalii jijini Dar es Salaa

   Sehemu ya Washiriki wa warsha ya matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mgeni rasmi (hayupo pichani). Warsha hiyo ya kufunga mradi imefanyika leo katika Chuo cha Taifa cha Utalii jijini Dares Salaam.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (kushoto) akikabidhi kifaa maalumu kwa Bw Haji Saleh, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kilimo - Zanzibar. Kifaa hicho ni kwa ajili ya kufanya tathmini na usimamizi angalifu wa bidhaa za mazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Zantel, Divine Mosi na Fadhil Nandonde kutoka UCA-Tz, kulia ni mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma. Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Zantel, Divine Mosi na Fadhil Nandonde kutoka UCA-Tz, kulia ni mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma.Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es SalaamMwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwakilishi wake wa UCA, na kuzungumzia tamasha kwa ujumla. 
  Mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwakilishi wake wa UCA, na kuzungumzia tamasha kwa ujumla.Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy alipozungumza nao juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA THEHABARI.COM Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy alipozungumza nao juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA THEHABARI.COM

  KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tamasha la vipaji vya sanaa na muziki lililoandaliwa na asasi ya ukuzaji vipaji (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz). 
  Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa asasi hiyo, Emmanuel Mushy alisema tamasha hilo la pekee litakalofanyika Uwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam linatarajia kushirikisha vijana zaidi ya 500 kutoka maeneo anuai ya jiji. 
   Akifafanua zaidi juu ya tamasha hilo, Mushy alisema UCA-Tz ni program yenye dhumuni la kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji vya muziki na sanaa ili vijana hao waweze kukua katika vipaji vyao. “…Neno ‘unscripted’ linamaanisha kitu ambacho kipo lakini hakijaandikwa, yaani kwa maana nyingine ni kitu kilichopo nyuma ya pazia.
   UCA-Tz baada ya utafiti imebaini kuwa kuna vijana wengi ambao wanajihusisha na muziki pamoja na sanaa lakini hawapati ile nafasi (platform) ya kuendeleza vipaji vyao, hivyo ni kama vijana hawa wapo nyuma ya pazia,” alisema Mushy. 
   Aliongeza kuwa UCA Tz kwa kutambua umuhimu wa vipaji vya vijana vinavyopotea imeona umuhimu wa kutengeneza njia kwa vipaji hivyo ili vitoke nyuma ya pazia kukua na hatimaye kujionesha kwa jamii. Aidha alisema moja ya njia ambazo UCA-Tz inazifanya ni kuandaa matamasha ya vipaji kwa kila mwaka kuwashirikisha vijana na kwa mara ya kwanza inazindua Tamasha la vipaji nchini Tanzania, ambalo litashirikiza vijana zaidi 500 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. 
   “…Tamasha hili la vipaji linatarajia kufanyika kesho, Jumamosi ya tarehe 14th December pale Uwanja wa Kinondoni Biafra, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 12 za jioni. Katika tamasha hilo vijana wenye vipaji vya kuimba, ku-rap, kucheza, kuchora na ubunifu (ku-design) watawasilisha kazi zao kwa umati utakao jitokeza na vijana wenzao,” alisema Mushy. 
   Alisema ili kuleta radha na hamasa zaidi asasi hiyo imealika wawakilishi vijana kutoka nchi mbalimbali za Africa kama Kenya, Uganda na Ghana ambao nao watashiriki. “…Kutakua na outside performances kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao wameshapiga hatua kwenye tasnia za muziki na sanaa nao watashiriki kwa pamoja. 
   Naye Mwakilishi kutoka kampuni ya Zantel, Divine Mosi ambao ni moja wa makampuni yaliofanikisha tamasha hilo, akizungumza alisema kampuni yao itaendelea kuunga mkono shughuli anuai za kuwawezesha vijana ikiwa ni sehemu ya kurudisha mchango wa wateja wao wanaotumia mtandao wao. 
   Kampuni nyingine zilizounga mkono kiushirikiano (supporters/sponsers) kufanikisha tamasha hilo ni pamoja na kampuni ya Coca Cola, Maezeki, Arise Media, LGBY Media na mtandao wa kijamii wa habari-Thehabari.com (www.thehabari.com) na mitandao mingine ya kijamii nchini.

  0 0

  Kocha wa timu ya Taifa ya Basketball Bahati  Moses Mgunda

  0 0
 • 12/13/13--05:00: Article 9


 • 0 0

  National Geographic ya Washington, DC siku ya Jumatano, Dec 11, 2913 walionyesha vivutio mbalimbali vilivyopo kwenye mbuga zetu za wanyama kwa wahudhuriaji ambao wengi wao walikua Wamarekani pia ulialikwa Ubalozi wa Tanzania akiwemo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba,
  Mhe. January Makamba akitoa shukurani zake kwa Nafional Geographic kwa jitihada zao za kusaidia kutangaza hifadhi za Taifa za wanyama pori/
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwapongeza National Geographic kwa kuwa Mabalozi wa Tanzania nchini Marekani na kuahidi kufanya nao kazi kwa karibu zaidi na mlango wa Ubalozi wa Tanzania upo wazi pindi wanapohitaji msaada.
  Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania National Parks, Bwn. Allan Kijazi nae akiwapongeza National Geographic kwa jitihada zao za kutangaza mbuga za wanyama pia aliwahakikishia wahudhuriaji Tanzania ndio mahali pekee kwenye vivutio na aina nyingi ya wanyama hao.
  Andrew Evans mfanyakazi wa National Geographic ambaye ndiye aliyetembelea mbuh=ga za wanyama Tanzania, akiwaonyesha wahudhuriaji picha mbalimbali za wanyama na kuwaelezea kuhusu Tanzania kwamba ni nchi ya Amani na Utulivu na Watanzania waliojaa na upendo kwa kila mtu.

  Akianza kuelezea alianza kuwaonyesha Khanga kwamba hutumika kwenye shughuli nyingi na kwamba utaiona kila pahala,
  Pia alionyesha picha ya kukutana na marafiki zake hao kwenye picha na yeye alipewa jina la Mzungu, Andrew Evans anaufahamu mkubwa wa hifadhi za Taifa jinsi alivyozielezea na vitu vilivyomo lazima uatatamani kuelekea huko kesho.
  Mhe. January Makamba akimpongeza Andrew Evans kwa jinsi anavyoitangaza Tanzania.
  Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mhe. January Makamba wakiongea na wahudhuriaji walijaribu kudadisi mambo mengine kutoka Tanzania na kuahidi kuja nchini Tanzania kutembelea mbuga za wanyama.
  Mhe. January Makmba akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula ndani ya thieta za National Geographic, Washington, DC.
  Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Afisa wa Ubalozi Mindi Kasiga, Mkurugenzi mkuu wa Tanzania National Parks, Bwn. Allan Kijazi, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na wahudhuriaji wengine waliofika National Geographic ya Washington, DC. Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog

  0 0

  FA MIKOA YAPATA MIPIRA TFF
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa mipira kumi kwa kila chama cha mpira wa miguu cha mkoa ili isaidie kuendesha ligi za mikoa husika. 
  Mipira hiyo 250 yenye thamani ya sh. 16,250,000 tayari imeanza kutumwa kwa makatibu wa vyama vya mikoa husika. Mpira mmoja una thamani y ash. 65,000. 
  Ni maratajio ya TFF kuwa mipira hiyo itakuwa chachu kwa vyama vya mikoa katika uendeshaji wa ligi hizo.

  MITIHANI YA WAAMUZI KUFANYIKA JUMAPILI
  Robo ya mwisho ya mitihani ya waamuzi (Cooper Test) na utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa mwaka 2013 kwa waamuzi inafanyika Jumapili (Desemba 15 mwaka huu). 
  Mitihani hiyo inayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam inashirikisha waamuzi wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (TFF) na wale wa kundi la waamuzi (elite) ambao wanaweza kupendekezwa kupewa beji za FIFA. 
  Wakufunzi wa mitihani hiyo ya waamuzi ni Leslie Liunda, Soud Abdi na Riziki Majala. 
  Waamuzi wa FIFA watakaofanya mitihani hiyo ni Ferdinand Chacha, Hamis Chang’walu, Israel Mujuni, Jesse Erasmus, John Kanyenye, Josephat Bulali, Mgaza Kinduli, Oden Mbaga, Ramadhan Ibada, Samwel Mpenzu na Waziri Sheha. 
  Washiriki kutoka kundi la elite ni Charles Simon, Dalali Jaffari, Hellen Mduma, Issa Bulali, Issa Vuai, Janeth Balama, Jonesia Rukyaa, Judith Gamba, Lulu Mushi, Martin Saanya, Mfaume Nassoro na Mohamed Mkono.

  KILIMANJARO STARS YAREJEA DAR
  Timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) iliyoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika jana jijini Nairobi, Kenya inarejea jijini Dar es Salaam leo. 
  Kilimanjaro Stars iliyomaliza michuano hiyo katika nafasi ya nne inatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12 kamili jilioni kwa ndege ya RwandAir. 
  Wenyeji Kenya (Harambee Stars) ndiyo walioibuka mabingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Sudan mabao 2-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa jana Uwanja wa Nyayo.

  Boniface Wambura Mgoyo
  Kaimu Katibu Mkuu
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

  In recognition of Computer Science Education Week, the United States Department of State’s Global Partnership Initiative together with CoderDojo and the LIONS@FRICA partnership, launched a new initiative today called afriCoderDojo to teach youth in Africa 21st century computer technology skills.  
  afriCoderDojo is a pan-African effort to teach young people the ability to understand and build fluency in coding, and learn the computer languages that are used to develop websites, mobile phone applications, computer programs, and electronic games. Based on the global open-source CoderDojo movement, afriCoderDojo will rely on a volunteer network of implementers and experienced coders located across Africa to run the two-month learning program.
  afriCoderDojo aims toprovide young people with the basics of coding through a fun and motivating curriculum. Guest lecturers, local technology entrepreneurs, and United States Embassies across Africa will also be invited to participate in the learning program to highlight and showcase career opportunities in the field of internet technology.
  The inaugural afriCoderDojo clubs are due to launch in Dar-es-Salaam, Tanzania and Lagos, Nigeria in January 2014.  The groups will be sponsored by the Dar Teknohama Business Incubator – a national incubator for technology businesses – in Tanzania and Oando Foundation – the foundation for Africa’s largest integrated energy company– in Nigeria.


  For more information about afriCoderDojo, please go to www.africa.co/africoderdojoor follow us on Twitter @afriCoderDojo.  If you are interested in hosting an afriCoderDojo in your community, please email partnerships@state.gov.   

  0 0

  Habari zimetujia sasa hivi zinasema abiria kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli  Mh Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuwa pasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Arusha leo mchana. 
  Ndege hiyo ya shirika la ndege la precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua, ambapo Matairi yote manne ya nyuma yalipasuka na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria. Ila hakuna mtu aliyedhurika katika ajali hiyo. 
  "Yaani Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiangalia kopo lenye Kahawa inayozalishwa Tanzania - Ruvuma ambayo imeanza kuuzwa kwenye Supa Maketi ya Colruyt ya Ubelgiji.

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akingoza kikao cha kamati kuu ya CCM kilichofanyika katika makao makuu ya CCM Mjini Dodoma mchana huu.Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein na kulia ni katibu Mkuu wa CCM Bwana Abdulrahman Kinana. 
  Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

  0 0
 • 12/13/13--10:06: TAARIFA KUTOKA TFF LEO

 • 0 0

  Leo ni siku ya mwisho ya kuaga mwili wa Mzee Madiba kabla ya kusafirishwa kuelekea kijijini kwake Qunu kwa mazishi siku ya Jumapili. Mitaa ya mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria, bado imefurika maelfu ya waombolezaji wakiwa katika foleni ndefu kwenda kuamuaga Tata Madiba. Wengine wanaimba na kucheza kusherehekea maisha ya Nelson Mandela, Rais wa Kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini. Globu ya Jamii ipo eneo la tukio na Libeneke litaendelea hadi mazikoni kijijini  Qunu.

older | 1 | .... | 295 | 296 | (Page 297) | 298 | 299 | .... | 3283 | newer