Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 298 | 299 | (Page 300) | 301 | 302 | .... | 3270 | newer

  0 0


  0 0

  AFISA masoko wa soko la hisa la Dar es salaam, DSE, Magabe Maasa, akisisitiza jambo alipokuwa anawasilisha mada ya Soko la kukuza ujasiriamali, katika mafunzo ya wajasiriamali mkoani Mtwara,yaliyoandaliwa na DSE na kuhudhuriwa na wajasiriamali 100 ambayo yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa kanisa la kiinjili la kithule mjini hapa KKKT.
  WAJASIRIAMALI wa Mtwara wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika katika mafunzo yaliyoandaliwa na DSE na kuhudhuriwa na wajasiriamali 100 ambayo yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa kanisa la kiinjili la kithule mjini hapa KKKT.

  WAJASIRIAMALI na wafanyabiashara mkoani Mtwara, wamehimizwa kuchangamkia fursa ya kukuza mitaji inayotolewa na soko la hisa la Dar es salaam, DSE kupitia kitengo chake cha kukuza wajasiriamali na kujipatia mitaji itakayokuza na kuhimalisha biashara zao.

  Wito huo umetolewa leo na kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara Thimithes Pangisa, alipokuwa anafungua mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika katika ukumbi mikutano wa kanisa la KKKT mjini haa yaliyolenga kuwaelimisha wajasiriamali na wafanyabiashara juu ya huduma ya ukuzaji wa wajasiriamali inayoendeshwa na soko la hisa la DSM.

  Pangisa alisema kuwa kumekuwa na kawaida kwa baadhi ya watu kutojitokeza kushiriki pale fursa mbalimbali zinapojitokeza na pale wenzao waliojitokeza wanapoanza kunufaika ndipo nao huleta lawama kuwa wamebaguliwa au hawakushirikishwa jambo ambalo alisema linapaswa kuacha mara moja.

  "Ndugu zangu wajasiriamali hii ni fursa muhimu na adhimu kwenu ichangamkieni siku zote mmekuwa na changamoto ya ukosefu wa mitaji sasa DSE leo imekuleteeni elimu hii ili mujue ni namna gani mnaweza kunufaika kwa kujipatia mikopo na kukuza biashara zenu", alisema Pangisa.

  Akimkaribisha mgeni rasimi kufungua mafunzo hayo afisa masoko wa DSE,Magabe Maasa, alisema kuwa mafunzo hayo ni mwendelezo wa kampeni ya kuelimisha wajasiriamali na umma kwa ujumla juu ya huduma za kitengo hicho kipya kinacholenga kuwwainua wajasiriamali wadogo na wakati kwa kuwawezesha kupata mitaji ya kukuza biashara zao.

  Maasa alisema kuwa tayari mikoa zaidi ya kumi imeshafikiwa na huduma hiyo na itaendelea hadi mikoa yote nchini ambapo kila mkoa wajasiriamali 100 wanahusishwa katika mafunzo hayo, chini ya ufadhili wa taasisi ya kuendeleza huduma za fedha (Financial sector developing trust kwa kwa mikoani mafunzo hayo huratibiwa na TCCIA.

  Akiwasilisha mada ya Utawala bora wa kampuni na kuzingatia sheria, meneja wa utafiti na maendeleo wa soko la hisa la Dar es salaam, Ibrahimu Mshindo, aliwashauri wajasiriamali walio na makampuni kuzifanya kampuni zao kuwa za umma ili waweze kuuza hisa na kuingia katika mpango wa kukuza mitaji na hivyo kupata fursa ya kujikomboa na changamoto ya ukosefu wa mitaji walionao hivi sasa.

  Aidha washiriki wa mafunzo hayo wameliomba soko hilo kuweka utaratibu wa kutembelea mikoani mara kwa mara ili kutoa elimu kwa wajasiriamali waishio mikoani waweze kujua shughuli za soko hilo na kunufaika na huduma zinazotoleawa.

  0 0

   Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) akiwasalimia vijana chini ya miaka 17 kabla ya kukutana na timu ya vijana wa timu ya Taifa chini ya miaka 17 katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa. 
   Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) akiwasalimia vijana chini ya miaka 17 kabla ya kukutana na timu ya vijana wa timu ya Taifa chini ya miaka 17 katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa.  
   Mchezaji wa zamanai wa Manchester United Andy cole(wa pili kulia) akisisitiza jambo kabla ya kujumuika na vijana wa timu ya Taifa chini ya miaka 17 jana - Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania. 
   Meya wa manispaa ya Ilala(wa pili kushoto) akikabidhi mipira iliyotolewa na Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bwana Jamali Malinzi (kushoto) katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni mchezaji wa zamani wa klabu Manchester UnitedAndy Cole na Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Sunil Colaso(kulia). 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Eng. Omari Jumanne Bakari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO).

  Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Desemba 04, mwaka huu, 2013.

  Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtafiti Mwandamizi katika Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam.

  Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtanzania mwenye elimu, weledi na uzoefu ambao umemfanya Mheshimiwa Rais aamini kuwa atakapoongoza SIDO, atasaidia kukidhi matarajio ya taifa kwa kueneza ujasiriamali, uwekezaji,uzalishaji na kutoa nafasi za ajira katika ngazi ya viwanda vidogo na vya kati kama msingi imara wa uchumi wa Tanzania, ikiwemo kwa kuingiza sayansi, teknolojia na ubunifu katika viwanda vidogo vidogo.

           “Mwisho”

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu.
  DAR ES SALAAM.
  16 Desemba, 2013

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, akimtunza Mmoja wa wasanii wa Jeshi la JKT Mgambo, waliokuwa wakitoa burudani katika la Utamaduni Handeni.
  Wasanii wa ngoma za asili kutoka JKT Mgambo, wakitumbuiza Mamia ya Wananchi waliofika katika Tamasha la Utamaduni Handeni, sherehe hizo zilifanyika Juzi katika Uwaja wa Azimio, wilayani Handeni, Mkoani Tanga.
  Kikundi cha Sarakasi kutoka JKT Mgambo wakionesha uwezo wao katika Tamasha la Utamaduni Handeni, Tamasha hilo lilifanyika juzi, katika uwanja wa Azimio, wilayani Handeni, Mkoani Tanga.


  0 0

  DSC_0181
  Mshehereshaji Bw. Salum Msellem kutoka Istiqama Radio akitambulisha meza kuu kwa washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali ya siku moja kwa Vijana Visiwani Pemba yaliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Madungu.
  DSC_0240
  Mratibu wa YUNA kisiwani Pemba, Bw. Mohammed Ali, akisoma taarifa ya maendeleo ya vilabu vya Umoja wa Mataifa visiwani humo na changamoto zinazowakabili kwa walezi wa vilabu hivyo.


  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa CEO Clubs Network, Bwana Tareq Ahmed Nizami, mwandaaji mwenza wa Mkutano wa Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia, 'The Africa -Middle East-Asia' unaofanyika katika Hoteli ya Atlantis The Palm, huko Dubai katika Jamhuri ya Falme za Kiarabu (UAE), tarehe 16.12.2013. Mwandaaji mwingine wa mkutano huo ni Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi (CELD).
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Penehupifo Pohamba, Mke wa Rais wa Namibia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika Dubai kuanzia tarehe 16.12.2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Balozi wa Tanzania katika nchi za Falme ya Kiarabu (UAE) wakati wa sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika katika hoteli ya Atlantis The Palm iliyopo Dubai, Jamhuri ya Falme za Kiarabu tarehe 16.12.2013. Kushoto kwa Mama Salma ni Mke wa Rais wa Namibia Mama Penehupifo Pohamba, na wa kwanza ni Mshauri Maalum wa Mama Pohamba Mchungaji Justina Hilukiluah na wa mwanzo kushoto no Bwana Tariq Nizami, Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa CEO Clubs Network.


  0 0


  Mdau Franklin Mziray
  Na Franklin Mziray 
  Nimesoma maoni ya Maggid juu ya hotuba ya Rais wakati wa maziko ya Mzee Mandela. 
  In deed Rais wetu amefunika kwa jinsi alivyotiririka na mchango wa taifa letu katika harakati za ukombozi si wa Afrika ya Kusini tu, bali bara zima. 
  Nilitamani tu angeongeza kwamba tulifanya hivyo kwa uchache wa uwezo wetu kiuchumi na tulitumia kidogo tulichonacho kuwasaidia ndugu zetu.
  Tulijijtolea kafara maendeleo ya uchumi wetu, tukapiga foleni kununua sabuni, acha sukari, ili tu wenzetu waweze kuwa huru, kuishi kama Waafrika na wenye haki ya nchi zao.
  Sisi tunaokaa nje ya nchi aghalabu tunakutana na mijadala ya hali ya uchumi wa Tanzania kuwa dhaifu ama duni, lakini wanaotucheka wanasahau kwamba kicheko chao, kimetokana na sadaka zetu. JK Rais wangu umenifanya nijisikie Mtanzania mara zisizohesabika. Kama ulivyosema mwenye macho haambiwi ona au mwenye masikio asikie. Wale ambao hawakusikia au kuyaona hayo zamani, basi wamesikia. 
  Kalale Pema Baba, babu na dira ya Afrika, Nelson Mandela. 
  Nakumbuka 2001 uliponipa zawadi ya kitabu chako 'The Long Walk to Freedom' na kukinafsisha kwangu na maneno Best Wishes Franklin...
  0 0

   Rais Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Dr.Reginald Mengi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa TNBC uliofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Chini akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya Tanzania National Business Council muda mfupi kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa TNBC uliofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo

  0 0
 • 12/16/13--09:30: BIFU LA MLELA NA HEMED LIVE!
 • Hemed (kushoto) akimtishia bastola Mlela
  Hemed na Mlela wakiwa wamelazwa hospitalini baada ya kuumizana huku mama yao akiwaangalia kwa huzuni
  Kasha la filamu mpya ya bifu la kina Mlela na PHD 
  inayotarajiwa kuingia mtaani keshokutwa Jumatano.


  LILE bifu lililowahi kufukuta kwa kasi mithiri ya moto wa kifuu baina ya ‘tozi’ wawili ndani ya tasnia ya filamu, Hemed Suleiman ‘PhD’ na Yusuf Godfrey Willard Mlela ‘Mlela’ linadaiwa kuibuka upya na kuzidisha uhasama baina ya wasanii hao.
  Aidha, alisema bifu hilo lilidhihirika hivi karibuni wakati wawili hao walipokutanishwa kuigiza filamu moja, kwani mara kwa mara walijikuta wakifanya kweli kwenye baadhi ya vipande vya ugomvi na mapigano jambo lililompa wakati mgumu muongozaji wa filamu hiyo inayotarajiwa kuingia sokoni kuanzia Desemba 18 mwaka huu iliyopewa jina la I Know You.
  “Walikuwa na muda mrefu sana bila kukutana, tukadhani bifu lao halipo tena, lakini hivi karibuni walikutana kwenye filamu iliyoandaliwa na Mtitu Game 1st Quality, wakawa wanafanya kweli kwenye baadhi ya sehemu za majibizano na mapigano huku wakifanyiana fujo mbalimbali huku kupigana vijembe vya wazi,” alisema rafiki huyo.
  “Ni kweli tulikuwa na utofauti, ule mvutano wa zamani bado ulikuwepo, kila mmoja hakutaka kuwa dhaifu kwa mwenzake, utaona baadhi ya vipande tulivyofanya kweli,” alisema Mlela ambapo simu ya Hemed iliita bila kupokelewa licha ya mwandishi wetu kuipiga mara kwa mara.
  Naye Meneja matayarishi wa Kampuni ya Game st Quality Ltd, Noel Amani ‘Futo’ alisema filamu ya I know You iliwapa wakati mgumu sana kutokana na bifu la wasanii hao kuonekana waziwazi.
  “Walitumbua sana, kuna wakati walifokeana kweli, kukunjiana ngumi hata hivyo kuna baadhi ya vipande walivyofanya kweli tumelazimika kuviacha ili kuleta uhalisia zaidi. Kila mmoja anaamini yuko juu ya mwenzake,” alisema Futo.

  0 0


  0 0

  Action Music Tanzania (AMTZ) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza desemba 19 mwaka huu, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
  Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.
  Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge karibu na magorofa ya jeshi ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828 au barua pepe, actionmusictz@yahoo.com, Like Facebook Page au tembelea www.amtz.org
   Mwalimu Abeid Mussa akitoa maelekezo ya wakati wa mazoezi ya kufanya onyesho la muziki
   Mwalimu wa Kinanda Prosper Shirima (katikati) akifundisha
  Mwalimu wa Gita, Ashimba (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kupiga chombo hicho

  0 0

    
  Karibu katika kipindi hiki cha FAMILIA kutoka Jamii Production. Katika kipindi cha wiki hii, mjadala ulikuwa KWANINI WANANDOA HUTEMBEA NJE YA NDOA?
  Mbali na washiriki waliokuwa studio, pia tuliweza kusoma maoni toka kwa wasikilizaji wetu wanaoacha katika kurasa zetu za FACEBOOK
  Karibu uungane nasi.


  Ukiwa na maoni, maswali ama ushauri usisite kuwasiliana nasi kupitia jamiiproduction@gmail.com

  0 0

   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Goodluck Ole-Medeye (katikati), akiongoza wahitimu wa Mahafali ya 15 ya Chuo cha Uhasibu Arusha (AII) kuelekea kwenye viwanja vya chuo hicho, muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti kwenye fani mbalimbali mkoani humo mwishoni mwa wiki, wa kwanza ( kushoto) ni Mkuu wa Chuo hicho Prof Johannes Monyo, na Mwenyekiti wa Bodi ya uongozi wa (AII), Mwanaidi Mtanda. 
   Maandamano yakielekea eneo la tukio
   Wahitimu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (AII), wakivaa kofia zao muda mfupi baada ya kutunukiwa vyeti vya fani mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo, kwenye sherehe za mahafali ya 15 zilizofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho mwishoni mwa wiki.  
   


  0 0

   Wachimbaji wa madini ya Tanzanite (WanaApolo) wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara wakiwa na askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji wa mkoa huo (aliyevaa sare) wakati wa ukaguzi wa usalama migodini. 
  Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Mkoa wa Manyara, (aliyevaa sare) akiwa na wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro (WanaApolo) wakati wa ukaguzi wa usalama migodini. 

  0 0

  Taswira Kwa niaba ya watanzania na Wakenya Luton Uingereza na kwa kushirikiana na Wenzetu wa Uganda, Burundi na Rwanda kama wana Jumuiya Afrika Mashariki katika sherehe za uhuru wa Tanzania na kenya zilizofanyika hapa Luton Jumamosi tarehe 14/12/13 


  “DJ DOUBLE T” MKONGWE WA MUZIKI WA TZ , EAST AFRICA, AFRICA NA NGOMA KALI ZA MAGHARIBI HAPA UINGEREZA AKICHANGANYA BEATS NA KATIBU WA LUTON TANAZANIAN COMMUNITY NDUGU ABRAHAM SANGIWA KATIKA SHEREHE ZA UHURU TANZANIA (52YRS) PAMOJA NA KENYAN(50YRS) HAPA UK.

  DJ DOUBLE T AKIKONGA NYOYO ZA WANA EAST AFRICA  WADAU WA EAST AFRICA KWENYE MNUSO WAO
  DJ KAZINI

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM  Kata ya Jangwani  Ndg. Mohamed Bawazir katikati akizungumza wakati wa kufungua kikao cha kujadili na kutafutia ufumbuzi kero  mbalimbali zinazowakabiri katika kata hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Ilala  Ndg. Asaa Simba ambaye pia ni Diwani wa Vingunguti na kulia  ni katibu wa kata ya jangwani, Ndg. Majala Balawa.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Qunu ni kijiji kidogo katika jimbo la Eastern Cape la Afrika Kusini, kilomita 32 Kusini-Magharibi ya mji wa Mthatha, katika barabara ya Butterworth na Mthata. Kijiji cha Mvezo, pembezoni mwa mto Mbashe, ni jirani ya mahali ambapo Mzee Nelson Mandela alizaliwa. 
  Hapo Qunu ndipo alipokulia na aliweka nadhiri ya kurejea. Kijiji cha Qunu ndipo baba yake Mandela alipohamia baada ya kuvuliwa Uchifu wa Mvezo. 
  Katika kitabu chake cha ‘Long Walk to Freedom’ Mzee Mandela amekitaja kijiji hicho kuwa ndipo alipoishi maisha ya furaha wakati wa utotoni. Jumapili ya Desemba 15, 2013 Mzee Mandela alizikwa kijijini Qunu katika mazishi ya Kitaifa yaliyoshuhudiwa dunia nzima. 
  Alizikwa kwa heshima zote za kiongozi wa Taifa na Chifu wa kimila katika sehemu aliyochagua mwenyewe kuwa nyumba yake ya milele.
  Mandhari ya kijiji cha Qunu.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

   Na Mwandishi Maalum
   Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa imesema itawatumia vijana walioko shuleni na nje ya shule katika Mradi wa kuzijengea uwezo jamii wa kuzuia, kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame. 
  Kauli mbiu ya Mradi huo ni “ Athari za Ukame Zinapunguzika, Jamii ikielimishwa.” Akiongea wakati wa Uzinduzi wa Mradi huo jana wilayani Kishapu, Mkurugenzi Wa Idara Ya Uratibu Wa Maafa, Ofisi Ya Waziri Mkuu, Luteni  Jeneral;i mstaafu  Sylivester Rioba alisema lengo la kujumuisha vijana walioko shuleni na nje ya shule, ni kuwajengea utamaduni wa kutambua viashiria na vihatarishi vinavyoweza kusababisha maafa ili waweze kukabiliana na maafa yanapotokea na hatimaye kuwaanzishia miradi midogo midogo ya ufugaji na Kilimo kwa ajili ya kipato na kujikimu na maisha. 
  “Kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi yameleta athari nyingi ikiwemo ukame, kupitia mradi huu ulioanza kutekelezwa kwa majaribio katika Wilaya ya Same kwa Mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Kishapu kwa Mkoa wa Shinyanga vijana na akina mama wataelimishwa juu ya upandaji wa miti na kilimo cha mazao yanayohimili ukame hususan mihogo na viazi vitamu.” Alisema Rioba
   Rioba alifafanua kuwa katika kuijengea jamiii uwezo wa kukabiliana na kupunguza vihatarishi vinavyoweza kusababisha maafa ya ukame mradi utaainisha na kutoa mafunzo kwa wadau kuhusu matumizi ya mbegu na pembejeo za kilimo, mifugo na misitu. 
  Pia mafunzo kwa wataalam kuhusu matumizi ya vifaa vya kukusanyia takwimu na mawasiliano yatatolewa pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu na mifugo utaboreshwa.
  Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa - Ofisi ya Waziri Mkuu Luteni Jenerali mstaafu  Sylivester Rioba akieleza umuhimu wa  Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa Kwa Mikoa Iliyoathirika Zaidi Na Ukame wakati wa Uzinduzi wa Mradi huo kwa Wilaya ya Kishapu, Shinyanga jana,  katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Kishapu (watatu kushoto) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu  Bw. Octavian Mangosongo

older | 1 | .... | 298 | 299 | (Page 300) | 301 | 302 | .... | 3270 | newer