Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

MUHIMBILI YABORESHA HUDUMA ZA ICU KUTOKA VITANDA 25 HADI 78

$
0
0
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kina mama wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Vicenti Tarimo akizungumza na waandishi wa habari juu ya uboreshaji wa wodi zinazolaza wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU). Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ukunga na Uzazi wa MNH, Bi. Mugara Mahungururo akiwa kwenye mkutano leo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kina mama wa MNH, Dkt. Tarimo kuhusu uboreshaji wa miundimbinu inayotumika kutoa huduma kwa wagonjwa.
Meneja wa Jengo la Wazazi namba Moja wa MNH, Suzana Ndambala akitoa ufafanuzi katika kuhusu huduma inayopatikana katika ICU ya kina mama wajawazito (MAICU) ina vitanda 10.
………………
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeongeza idadi ya vitanda katika wodi za wagonjwa wanaohitaji huduma za uangalizi maalum (ICU) kutoka 25 hadi 78 ikiwa ni sehemu ya mkakati wa hospitali wa kuboresha miundombinu ya kutoa huduma kwa wagonjwa.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kina mama wa MNH, Dkt. Vicenti Tarimo amesema lengo la kuboresha miundombinu inayotumika kutoa huduma ni kupunguza vifo vya kina mama wanaofariki dunia kutokana na kifafa cha mimba.
“Hospitali imetengeneza chumba cha kina mama wanaohitaji huduma ya uangalizi maalum (MAICU) chenye vitanda 10, pia imeweka mashine tano za kusaidia kupumua na ultrasound. Hivi sasa, huduma hii inapatikana kwenye jengo lao ukilinganisha na zamani ambapo mama alipaswa kupelekwa ICU ya kawaida ambayo ipo umbali wa mita 150. 

Hali hii ya upatikanaji wa huduma ilikuwa inahatarisha uhai wa mama na mtoto. Maisha ya kina mama wengi yameokolewa kupitia MAICU,” amesema Dkt. Tarimo.Dkt. Tarimo amefafanua kwamba kuwapo kwa huduma ya MAICU kumesaidia kupunguza vifo vya kina mama kutoka 125 mwaka 2017/2018 hadi kufikia vifo 86 Julai 2018 hadi Juni 2019.

Amesema uboreshaji wa huduma MNH ni sehemu ya kutekeleza malengo ya Serikali pamoja na malengo ya milenia ya kupunguza vifo vya kina mama.
“Hatua hii inaifanya MNH kuwa Hospitali ya kwanza ya umma hapa nchini kuwa na ICU ya kina mama wajawazito wenye kuhitaji uangalizi maalumu,” amesema Dkt. Tarimo.

Dkt. Tarimo amebainisha pia MNH ina ICU ya watoto wachanga (NICU) yenye vitanda 18, PICU ya watoto wenye umri wa kuanzia mwezi yenye vitanda 12, wodi ya wagonjwa wa tiba (MICU) ambayo ina vitanda 15, wodi ya wagonjwa wa upasuaji wanaohitaji uangalizi maalum (SICU) yenye vitanda 18, wodi ya wagonjwa wanaopandikizwa figo wanaohitaji uangalizi maalum ambayo ina vitanda 5 na ICU ya kina mama wajawazito (MAICU) ambayo ina vitanda 10.

“Shirika la Afya Duniani (WHO) linazitaka Hospitali kuwa na asilimia 10 ya vitanda vya ICU. MNH ina vitanda 1,550 hivyo inatakiwa kuwapo kwa vitanda 155 vya ICU. Hivi sasa MNH ina vitanda 78 sawa na asilimia 50 ya takwa la WHO. Hizi ni jitihada kubwa za uboreshaji huduma kwa wananchi,” amesema.

Dkt. Tarimo amesema kwamba uwapo wa miundombinu ya ICU, imesadia watalaam kutoka hospitali nyingine nchini kuja kujifunza namna bora ya kuanzisha na kuendesha vyumba vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum kwa makundi mbalimbali.

“Baadhi ya hospitali za rufaa za mikoa zimeanza kuleta watalaam wake kujifunza jinsi ya kutoa huduma kwenye ICU. Vilevile huduma hizi zitasaidia katika utafiti wa mahitaji halisi ya huduma za ICU pamoja na gharama zake na hivyo kusaidia Wizara ya Afya na Serikali kwa ujumla katika kuweka mipango ya upanuzi wa huduma hii hapa nchini,” amesema Dkt. Tarimo.

Katika hatua nyingine, Hospitali imefanya ukarabati mkubwa katika wodi 3 hadi 6 za Mwaisela na kuweka mfumo wa oxygen pamoja na vitanda 7 kila wodi sawa na vitanda 28 vya kutoa huduma kwa wagonjwa maalum (HDU). Uboreshaji huu utawasaidia wagonjwa wa kiharusi kuonwa kitalaam zaidi na kuwa kwenye uangalizi wa karibu ikilinganishwa na awali walikuwa wakilazwa katika wodi za kawaida.

RAIS MAGUFULI -UZENI GESI MSIUZE MITUNGI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wafanyabiashara na wauzaji wa gesi nchini kuuza bidhaa ya gesi tu na sio mitungi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ghala la mitambo ya kuchakata gesi iliyoko Dar-es-salaam, Wilayani ya Kigamboni, Rais Magufuli amesema kuwa sekta binafsi ni muhimu katika ukuaji wa uchumi nchini na kuwahakikishia kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana nao.

“Nimefurahi kuona Taifa Ges mmeanza kukarabati na kutengeneza mitungi yenu wenyewe hii itashusha bei ya mitungi na kuwawezesha wananchi wengi kutumia gesi, tena kwa hii ikiwezekana fanyeni kama makampuni ya soda na bia’’, Alisema Rais Magufuli.

Akisisitiza jambo hili Rais Magufuli ametoa mfano wa Kampuni za Soda na Bia ambapo ukinunua soda na bia maana yake hulipii creti ila unalipia soda hii itasaidia kupunguza bei ya gesi na kuwafanya wananchi wengi kutumia nishati hii Rais Magufuli amewataka wananchi kutumia Nishati ya gesi ili kupunguza matumizi ya mkaa, uharibifu wa mazingira, kulinda afya na kupunguza gharama ya maisha, kwani gunia mbili za mkaa ni sawa na 120,000, lakini ukitumia gesi gharama yake kwa mitungi miwili ni sawa na 94,000 kwa hiyo wananchi wakitumia gesi wataweza kuokoa shilingi 26,000.

“uwekezaji huu mkubwa uliofanywa na Taifa Gas Ltd ni uthibitisho, Serikali yetu inaipenda sekta Binafsi na ipo tayari kushirikiana na ninyi, kwa hiyo Sekta Binafsiendeleeni kujiamini, endelezeni kazi pamoja, hapa Tanzania ni mahali salama kwauwekezaji”, Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisema kuwa Tanzania inahitaji wawekezaji muda wote ili kuwekezakatika sekta ya nishati kama vile kuzalisha umeme utokanao na Makaa ya mawe, Maji, Upepo pamoja na Jua ili kuwezesha upatikanajiwa umeme wa kutosha na kwa bei nafuu.

“Wawekezaji tuwahitaji leo, kesho, kesho kutwa na miaka yote, kwa sababu Tanzania ipo miaka yote, kwa hiyo wawekezaji na ninyi tunawahitaji kwa sababu tutakusanya kodi na watanzania watapata ajira kama ambavyo Taifa Gas mmefanya”, Alisisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia aliwataka wananchi kutumia Nishati ya gesi ili kupunguza matumizi ya mkaa, uharibifu wa mazingira, kulinda afya na kupunguza gharama ya maisha, kwani gunia mbili za mkaa ni sawa na 120,000, lakini ukitumia gesi gharama yake kwa mitungi miwili ni sawa na 94,000 kwa hiyo wananchi wakitumia gesi wataweza kuokoa shilingi 26,000.

Naye Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani alisema kuwa biashara ya gesi sasaimeendelea kukua nchini tofauti na hapo zamani ambapo kwa sasa gesi inafika hadi vijijini.“Biashara hii ya gesi imekwenda hadi kwenye baadhi ya mikoa, naipongeza nakuishukuru kampuni ya Taifa ya gesi, ambayo kwa afrika ina maghala makubwa na kuhifadhi na kupokea gesi kwa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, kwaniwanahifadhi tani 7,650, wakifuatiwa na Afrika ya Kusini tani 5,200 huku Morocco
wakihifadhi tani 5,077 kwa hiyo sisi ni namba moja”, Alisema Dkt.Kalemani.

Aidha Dkt.Kalemani aliongeza kuwa kwa sasa bei ya gesi imeshuka kuliko nchi zote Afrika Mashariki, kwani kilo moja ya gesi inauzwa Shilingi 3,080, kenya 3,500 huku Uganda ikiuzwa kwa 4,001.

Dkt.Kalemani alisema kuwa Sekta ya gesi imepunguza changamoto ya ajira kwa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 12,000 katika kampuni za gesi zilizowekeza nchini.Biashara ya gesi nchini ilianza mwaka 1965, huku kampuni ya gesi ya Tipper ilikuwa mshiriki mkuu wa biashara hiyo, ambapo gesi ilikuwa inatumika viwandani, Mashuleni, katika Taasisi za Serikali na Vyuoni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ghala na Mitambo ya kuchakata Gesi ya LPG vya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt Zainab Chaula afungua Mkutano wa Wakuu wa vyuo vya Serikali jijini Dodoma

$
0
0
Sauti za Dkt Chaula, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, katika akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa vyuo vya Afya vya Serikali uliofanyika jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mafunzo Wizara ya Afya Dkt Laizer wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Vyuo vya Afya vya Serikali, uliofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Laizer akifuatilia maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula (hayupo kwenye picha) pindi alipofungua Mkutano wa Wakuu wa Vyuo vya Afya vya Serikali uliofanyika Jijini Dodoma. 
Baadhi Wakuu wa Vyuo vya Afya vya Serikali wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula wakati alipofungua Mkutano wa Wakuu wa Vyuo vya Afya vya Serikali uliofanyika Jijini Dodoma. 
Jopo la Wakuu wa Vyuo na Makaimu Wakuu wa vyuo vya Afya vya Serikali wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt Zainab Chaula wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa vyuo vya Serikali uliofanyika Jijini Dodoma. 

……………………………………………. 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Zainab Chaula amefungua Mkutano wa Wakuu wa Vyuo vya Afya vya Serikali uliofanyika Jijini Dodoma. 

Katika Mkutano huo Dkt. Zainab Chaula amewataka Wakuu wa vyuo kuongeza ubunifu katika utoaji huduma kwenye taasisi zao na kuboresha miundombinu jambo litakalosaidia kuinua kiwango cha elimu katika maeneo yao. 

Kwa upande mwingine, Dkt. Chaula amewataka Wakuu hao wa vyuo vya Afya kuondoa dhana ya kuitegemea Serikali katika kila jambo ili kuwaletea Maendeleo, huku akisisitiza uanzishwaji wa vitega uchumi katika vyuo hivo jambo litalosaidia kupambana dhidi ya ukata wa fedha. 

Aidha, Dkt Zainab Chaula amekemea vitendo vya uvunjaji wa maadili vinavyofanywa na baadhi ya Wakuu wa vyuo ikiwemo suala ya Rushwa, kufelisha wanafunzi, mambo yanayopelekea kutia doa Maendeleo ya taasisi hizo. 

“Mkuu wa Chuo ni kama mzazi, kuna baadhi ya maeneo unakuta Mkuu wa chuo anatongoza wanafunzi, wengine wanafukuzisha wanafunzi, mnaharibu Watoto wa wenzenu, kwa hali hii tutazipata wapi baraka za Mwenyezi Mungu ” alisema Dkt Chaula 

Mbali na hayo, Dkt Zainab amewapongeza Wakuu hao wa Vyuo kwa Juhudi wanazoendelea kuchukua katika kuboresha vyuo hivo licha ya changamoto lukuki wanazoendelea kukumbana nazo. 

Dkt. Chaula aliendelea kusema kuwa, Serikali inatambua Juhudi kubwa zinazofanywa na Wakuu wa vyuo vya Afya nchini na kuahidi kupokea changamoto zote na kuendelea kutafutia ufumbuzi kadiri inavyowezekana.

Kenya Government issues statetement After MP Jaguar's Xenophobic Remarks in Video clip

WANANCHI TANGA WAPEWA ELIMU KUHUSU MADHARA YA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
*Yaelezwa Jiji la Dar, Tanga vinara kwa utumiaji wa dawa hizo

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WANANCHI wa Jiji la Tanga wameendelea kupewa elimu kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya nchini yakiwemo ya magonjwa ya maambukizi kwa walioathirika na utumiaji wa dawa hizo.

Elimu hiyo imetolewa kwenye maeneo mbalimbali yakiwamo ya vijiwe ambavyo kuna vijana ambao wamekuwa wakijihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya au waliokuwa wanatmia na kuacha, pia elimu hiyo imetolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari pamoja na rika za makundi mbalimbali yaliyopo katika Jiji la Tanga.

Utolewaji wa elimu inayohusu madhara ya dawa za kulevya ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo kilele chake itakuwa ni kesho Juni 26 mwaka huu.

Hivyo Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imepiga kambi katika Jiji la Tanga kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa elimu hiyo ambayo itasaidia kuifanya jamii kuwa sehemu ya kushiriki katika kukomesha dawa za kulevya nchini.

Michuzi Blog na Michuzi TV ambayo imepiga kambi katika Jiji la Tanga ili kukuuza kila kinachoendelea imeshuhudia namna ambavyo wataalam mbalimbali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inavyotoa elimu hiyo kwa wananchi.

Kamishna wa Idara ya Kinga na Tiba wa mamlaka hiyo Dk.Peter Mfisi amefafanua kuwa lengo la kutolewa kwa elimu hiyo ni kuhakikisha kila mmoja wetu kwa nafasi yake anashiriki kwenye vita ya kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya kwa athari zake ni kwa jamii nzima na si mtu mmoja tu.

"Kwa wanaotumia dawa za kulevya na hasa ambao tayari wameathirika na dawa hizo madhara yake ni makubwa sana.Utafiti unaonesha asilimia 40 ya walioathirika na utumiaji wa dawa za kulevya wanaishi na virusi vya Ukimwi.

"Pia wapo wenye magonjwa ya Kifua Kikuu(TB) lakini wengine wanasumbulia na homa ya ini.Hivyo madhara yake ni makubwa na kibaya zaidi magonjwa ambayo wanayo ni ya kuambikiza, hivyo wanaweza kuambikiza na jamii nyingine,"amesema Dk.Mfisi.

Alipoulizwa kwanini maadhimisho hayo yanafanyika katika Jiji la Tanga, amefafanua kuna sababu nyingi kwanza Mamlaka imekuwa ikifanya maadhimisho hayo kwenye mikoa mbalimbali kwa kila mwaka.

Hata hivyo kwa Tanga kuna umuhimu wake kwasababu utafiti wa mwaka 2014 ulofanywa na iliyokuwa Tume ya Dawa za kulevya unaonesha Tanga inashika nafasi ya pili kwa kuwa na watu 7000 wanaomia dawa za kulevya na nafasi ya kwanza kwa mujibu wa utafiti huo inashikwa na Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa na watumiaji 30,000.

"Pia tupo Tanga tukiendelea na utoaji wa elimu kwasababu wafanyabiashara hii ya dawa za kulevya wanaitumia Pwani ya Tanga kupitisha dawa hizo.Hivyo jamii ikiwa na uelewa wa madhara ya dawa hizo hawatakuwa tayari kuwa sehemu ya kushiriki kufanya biashara au kutumia kabisa,"amesema Dk.Mfisi.

Mmoja wa wakazi wa Jiji la Tanga, Athuman Shekimweri amesema anatoa pongezi kwa Mamlaka hiyo kwa namna ambavyo imeamua kuzunguka maeneo mbalimbali na kutoa elimu kwani imewafanya kutambua madhara ya kutumia dawa za kulevya na hivyo watakuwa mabalozi kwa wengine.

HALAIKI YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MICHAEL JACKSON MWAKA 2009

TCRA YAWEKA MIKAKATI KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KUBORESHA USALAMA WA TAARIFA ZA WATUMIAJI WA SIMU

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA akimkabidhi mmoja wa wadau wa mawasiliano Leseni ya Utambulisho ya Mamlaka hiyo.
Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha David Lyamong akizungumza na wadau wa sekta ya mawasiliano katika kikao kilichowakutanisha wadau wa sekta hoyo katia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha
Mmoja wa wadau wa Mawasiliano mkoani Arusha akichangia jambo katika kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Baadhi ya wadau wa mMawasiliano waliojitokeza katika mkutano.wa.wadau wa sekta ya Mawasikiano wakisikiliza mada mbalimbali zinazoendekea.



Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya kaskazini imesema imeweka mikakati ya kuboresha usajili wa laini za simu kwa njia ya vidole kwa wananchi mkoani Arusha kwa kushirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha watumiaji wa simu kwa njia ya kieletroniki katika kuboresha usalama na taarifa za watumiaji wa simu

Akizungumza katika mkutano wa sekta ya mawasiliano kanda ya kaskazini Kaimu mkuu wa mammlaka ya mawasiliano kanda ya kaskazino Mhandisi Imelda salumu amesema mamlaka hiyo inashirikiana vyema na jeshi la polisi katika kuhakikisha watumiaji wa simu wanasaijili laini zao usalama.

Amesema”changamoto ya kusajili laini za simu TCRA inashirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha watumiaji wa simu wanasajili kwa kutumia mfumo wa kieletroniki (alama za vidole) ili kuboresha taarifa za watumiaji wa simu “

“Usajili wa kwa njia ya vidole bado inaendelea na nawaomba wadau wote wa sekta hii ya mawasiliano mkataoe elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa wa kusajili wa laini kwa njia ya vidole kwani serikali imetoa muda wa kusajili hivyo kila mmoja anapaswa kusajili laini ili kuhakikisha usalama wa laini yake”

Hata hivyo wadau wa sekta ya mawasiliano mkoani Arusha wameiomba mamlaka hiyo kupunguza tozo zinazotolewa kwa vyombo vya habari kwani tozo hizo zinazidi kupanda kila wakati hali ambayo inaporomosha vyombo vingi vya habari mkoani Arusha

Sambamba na hayo wadau wa sekta ya mawasiliano kaimu katibu tawala mkoani Arusha David Diomongi wamelalamikia mitandao ya simu kushindwa kuboresha upatikanaji wa miamala kwa haraka kupitia simu ,kompyuta na kadhalika na kuiomba mamlaka hio kuhakikisha uboreshwaji wa miamalia

”Zamani ilikuwa unachukua alama ya kidole polisi lakini sasa alama hizo,tunaomba Mamlaka ya Masiliano ihakikishe mnaweka utaratibu mzuri ili hawa watumiji wa simu na wamiliki wa laini wanaboresha hii mitandao na kuzuia miamala pamoja na ujumbe ufupi zinazotumwa kwenye simu,mfano mimi kwa leo nimepokea ujumbe wa mfupi mara sita utakuta kampuni tofauti tofauti ndo wa natumia hii kutangaza biashara zao,tunawaomba hili nalo muangalie”

Mkutano huo wa wadau wa sekta ya afya umefanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Arusha wenye lengo la kuthamini mafanikio na changamoto zinazo wakabili mamlaka hiyo katika kupanua wigo wa mawasiliano kwa watumiaji.

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK


MATUKIO KATIKA PICHA BUNGE LIKIPITISHA BAJETI KUU YA SERIKALI YA SH. TRILIONI 33.1 KWA KISHINDO

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akifanya majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya mwaka 2019/20 kabla ya kupitishwa na Bunge, Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akijibu hoja za Wabunge wakati wa majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20 kabla ya kupitishwa kwa kishindo Bungeni Jijini Dodoma.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashugwa akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizotolewa na Bunge wakati wa majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20 kabla ya kupitishwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mawaziri wakati wakijibu hoja mbalimbali za Wabunge kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20, kabla ya kupitishwa Bungeni Jijini Dodoma.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto), akifurahia jambo wakati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), alipokua akifanya majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2019/20.
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akiwapongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya kufanya majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20, kabla ya kupitishwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (wa pili kushoto), akiwa na Wakuu wa Idara na Taasisi za Wizara hiyo wakifuatilia majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20, kabla ya kupitishwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Mawaziri na  Wabunge wakifurahia baada ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20 kuidhinishwa na Bunge Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wabunge wakiwapongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Sh. trilioni 33.1, katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati), Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa tatu kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James (wa pili kulia) na viongozi wengine, wakuu wa idara na Taasisi, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20, jijini Dodoma

VOA Swahili - AFCON 2019 MISRI : Pierre Liquid Atoa Nasaha Zake

VOA SWAHILI: DUNIA LEO

Rais Magufuli amteua Dkt. Mussa Juma kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA)

DIAMOND PLATNUMZ AWEKA HADHARANI HAYA,ASEMA TAMASHA LA WCB PATACHIMBIKA.

OCD PANGANI AKARABATI KITUO CHAKAVU CHA POLISI WILAYANI HUMO

$
0
0

Mkuu wa Jeshi La Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi amefanya jitihada binafsi na kuchukua hatua kufanya marekebisho ya kituo kikuu cha Polisi Pangani chenye historia toka mwaka 1958 na kuanzisha mchakato wa kukijenga upya akishirikisha nguvu za wananchi.
Hatua hii ya kibunifu imepongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh.Martine Shigela baada ya mwaliko wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Pangani kufika na kujionea kazi hii kubwa ya Jeshi la Polisi Pangani.
Mh.Shigela na Mbunge wa Pangani Mh.Jumaa Aweso kwa pamoja wametoa vifaa vya kuezeka na umaliziaji wa kituo hiki kikuu cha Polisi Pangani.

Dekula Band new music video is coming soon!


Mwanza yazidi kutamba soka wavulana UMITASHUMTA 2019

$
0
0
Na Mathew kwembe, Mtwara
Timu ya soka ya wavulana ya mkoa wa Mwanza imeendelea kufanya vizuri kwenye michuano ya UMITASHUMTA inayofanyika katika viwanja vya chuo cha Ualimu Mtwara ambapo katika mechi iliyochezwa jana ya kundi B linaloundwa na mikoa ya Pwani, Mwanza, Iringa, Lindi na Mtwara iliiadhibu vikali timu ya soka ya mkoa wa Pwani kwa magoli 3-0.
Magoli yote matatu ya Mwanza yalifungwa na mshambuliaji hatari wa timu hiyo Haroub Juma ambaye ni mwanafunzi wa shule ya academy ya Alliance ya jijini humo.
Huu ni mchezo wa pili kwa timu hiyo ya mwanza kuibuka na ushindi wa kishindo baada ya juzi kuifunga timu ya soka ya wavulana kutoka mkoa wa Mbeya kwa magoli 5-2.
Kufuatia matokeo hayo, timu hiyo imeshinda michezo yake yote miwili ambapo Mshambuliaji wake Haroub Juma ndiye anaongoza kwa kufunga magoli mengi katika michuano hiyo baada ya kufunga magoli matano katika michezo miwili iliyocheza.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, mchezaji Haroub ambaye pia ndiye nahodha  wa timu ya soka wavulana Mwanza alisema kuwa timu yake ilistahili ushindi kwani walijiandaa vya kutosha kuikabili timu yoyote watakayopangiwa kucheza nayo.
Naye kocha wa timu hiyo Mwalimu Mathias Wandiba aliipongeza serikali kwa kufanyika kwa mashindano  hayo na kuwataka wadau wa michezo nchini hususani TFF kurekebisha kalenda zao ili kwanza wapishe kufanyika kwa mashindano hayo.
“TFF hawana budi kuwasiliana na serikali ambao ndiyo wanaoandaa mashindano ili kutofautisha kalenda za michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA na kalenda TFF.
Matokeo mengine katika kundi B yanaonyesha kuwa Mbeya ilifungwa na Mwanza magoli 2-5,  Pwali iliifunga Iringa 4-0, Lindi ikaifunga Mtwara 2-1, Simiyu imeifunga Iringa 2-0 na Mbeya imeifunga Mtwara 1-0.
Katika matokeo ya kundi A Tanga iliichapa Singida 4-0, Dodoma iliifunga Mara 2-1, Dar es salaam na Kilimanjaro zilitoka sare 1-1, Singida na Kilimanjaro wametoka suluhu ya bila kufungana, Mara imefungwa na Dar es salaam 0-1, na Tanga imeifunga Dodoma 2-1.
Katika kundi C linaloundwa na timu za mikoa ya Geita, Kigoma, Manyara, Njombe, Shinyanga, na Ruvuma, matokeo yanaonyesha kuwa Geita iliifunga Kigoma 1-0, Manyara iliifunga Njombe 2-1, wakati ambapo Shinyanga ilifungwa na Ruvuma 0-2, Kigoma iliifunga Ruvuma 1-0, Njombe iliichapa Shinyanga 4-1, Geita iliifunga Manyara 2-0.
Katika michuano hiyo inayoendelea hapa Mtwara katika kundi D Katavi ilifungwa na kagera 1-2, Moro ilifungwa na Tabora 1-2, Rukwa iliifunga Songwe 3-1 Morogoro na Rukwa zilitoka sare1-1, Kagera iliifunga Arusha 3-0 na katavi na Tabora zilitoka ya bila kufungana.
Kwa upande wa soka wasichana Dar es salaam na Lindi zilitoka sare ya goli 1-1, Kilimanjaro iliichapa Ruvuma 4.30, Ruvuma na katavi zilitoka suluhu ya bila kufungana na Dar es salaam iliichapa katavi.
Pia Tabora iliifunga Simiyu 1-0, Manyara iliifunga arusha 4-0, Aruaha ilitoka suluhu na singida 0-0, Tabora ilifungwa na Manyara kwa 0-1.
Katika kundi A wasichana, Dar es salaam ilitoka sare ya 1-1 na Lindi, Katavi ilifungwa  na kagera 1-2, Kilimanjaro ilishinda Ruvuma 4-0, Ruvuma na Katavi zilitoka sare ya bila kufungana na Dar es salaam iliwafunga Kilimanjaro 3-1.
Katika kundi B Tabora iliifunga Simiyu 1-0, Manyara iliifunga Arusha 4-0, Arusha na Singida zilitoka suluhu Na Tabora ilifungwa na Manyara 0-1.
Matokeo ya kundi C wasichana Mwanza iliifunga Iringa 3-0, Kagera na Geita zilitoka sare 2-2, Mwanza na Kagera  1-1 na Geita iliichapa Mbeya 1-0 na kundi D shinyanga ilifungwa na Morogoro 1-3 na Morogoro iliifunga Rukwa 2-1
Kundi maalum Kigoma ilifungwa na Njombe 1-3, Shinyanga ilifungwa na Kilimanjaro 1-3, shinyanga ilifungwa na kilimanjaro 2-3, Kilimanjaro iliifunga Rukwa 10-0 na kigoma iliifunga  shinyanga 1-0.
Katika kundi B maalum Tabora  iliifunga Kagera 2-1, Manyara iliifunga katavi 7-0, Katavi ilifungwa na Singida 0-5 na tabora na manyara zilitoka suluhu
Katika kundi C maalum matokeo yanaonyesha Mwanza walifungwa na Dodoma 0-1, Tanga imeifunga geita 4-1, Mwanza na Tanga zilitoka sare na Geita ilifungwa na Mtwara 0-4.
Matokeo ya kundi D yanaonyesha Iringa iliifunga mara 1-0, Dar es salaam ilifungwa Ruvuma na irina  ilichabangwa bna DSM 0-8
 Beki wa Mwanza Wallace Paulo akipiga mpira kuelekea lango la timu ya Pwani wakati timu hizo zilipokutana jana kwenye uwanja wa chuo cha ualimu Mtwara.
Mpambano wa Mwanza na Pwani

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. SHEIN AKITOA MKONO WA POLE KWA FAMILIA YA DR. BADRIA NA KUHUDHURIA HITMA MASJID MAAMUR UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitowa mkono wa Pole kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi alipofika nyumbani kwao Mtaa wa Msasani Jijini Dar es Salaam kutowa Mkono kwa familia ya Dr. Badria. Abubakar Gurnah
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwafariji Watoto wa Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah, alipofika nyumbani kwao kutowa mkono wa pole na kuwafariji kwa msiba huo, katikati Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibae Dr. Abdalla Juma Mabodi mume wa Marehemu Dr.Badria Abubakar Gurnah
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,. Dk. Ali Mohamed Shein, akisaini kitabu cha maombolezi cha Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah, alipofika nyumbani kwao Msasani Jijini Dar es Salaam kutowa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, akisaini kitabu cha maombolezi alipofika nyumbani kwa marehemu Dr. Badria Abubakari Gurnah, Msasani Jijini Dar es Salaam
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akimfariji Mtoto wa Marehemu Zaina Abdalla Juma Mabodi, alipofika nyumbani kwao Msasani Jijini Dar es Salaam, kutoa mkono wa pole, kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr, Abdalla Juma Mabodi
 BAADHI ya Wananchi wakishiriki katika kisomo cha Hitma ya Marehemu Dr, Badria Abubakar Gurnah, iliofanyika nyumbani kwao Msasani Jijini Dar es Salaam
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein , kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr, Abdalla Juma Mabodi, wakiitikia dua kumuombea Marehemu Dr.Badria Abubakar Gurnah, alipofika nyumbani kwao Msasani kutowa mkono wa pole
 MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushoto Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi wakishiriki katika hitama na dua  ya kumuombea Marehemu Dr.Badria Abdubakar Gurnah, iliofanyika nyumbani kwao Msasani Jijini Dar es Salaam.
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi Jijini Dar es Salaam, katika hitma na dua kumuombea marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah, iliofanyika nyumbani kwao Msasani Dar es Salaam
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akipiga fatha kabla ya kuaza kwa kisoma cha dua na hitma ya kumuombea marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah, iliofanyika katika Masjid Mahamur Upanga Jijini Dar es Salaam, kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar mume wa marehemu Dr, Abdalla Juma Mabodi
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akishiriki katika kisoma cha Hitma na dua kumuombea Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah, kushoto Imamu wa Masjid Mahamur Upanga Sheikh Ayoub Ali Seif na Sheikh Zeni Shariff na kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ramadhani Abdalla
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na kushoto Imamu wa Masjid Mahamur Upanga wakiitikia dua wakati wa kuhitimisha Hitma ya marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah ikihitimishwa na Sheikh Zeni Shariff.
 Sehemu ya waombolezaji
MWAKILISHI wa Familia ya Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurhan akitowa shukrani kwa Wananchi na Viongozi wa Serikali kujumuika katika msiba wa ndugu yao Dr. Badria Abubakar Gurnah, baada ya kumalizika kwa kisoma cha hitma kilichofanyika katika Masjid Mahamur Upanga jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

TAMASHA LA WASAFI KURINDIMA KUANZIA MWEZI JULAI

$
0
0
Na Khadija Seif, Michuzi TV
MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya anayetengeneza kundi la Wasafi Classic (WCB) Nasib Abdul a.k.a Daimond Platinum amesema hakutegemea mapokezi ya kanyaga. Daimond Platinum amesema mwaka huu umekua ni wa mafanikio makubwa kwake kutokana na nyimbo zake alizoziachia kupokelewa vizuri na mashabiki zake wa ndani na nje ya nchi. 
"Mwanzoni mwa mwezi Mei niliachia "The one" na badaae nikaamua nihamie kwenye midundo ya bolingo ambapo niliachia ngoma ya "INAMA" niliyomshirikisha Fally Ipupa kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na ilipokelewa vizuri sana na mwezi huu nimeachia "KANYAGA" ambayo pia imepokelewa vizuri sana na mashabiki," 
Aidha amesema ni baraka kupata Rais Dkt. John Pombe Magufuli anayejali, anaependa sanaa na hata hivyo ameendelea kuboresha kila sekta hasa kwenye upande wa usafirishaji ameleta ndege na amehakikisha kila mkoa kuna kuwa na viwanja vya ndege ili wasanii waweze kuwafikia mashabiki zao kwa wakati muafaka. 
"Kuna vitu vingine Serikali ikivifanya watu wanavitafsiri vibaya na kuona kwa jicho la tofauti na ndiyo maana ndege zilivoletwa ilionekana Kama Serikali ya awamu ya tano inamaliza pesa kwenye kununua ndege lakini umuhimu wake unaonekana kwa sasa kutokana na usafiri unakua sio wa tabu tena,". 
Daimond Platinum ametangaza rasmi kuwa Tamasha la Wasafi limezinduliwa rasmi na kwa mwaka huu litaanza kufanyika Julai 12 Muleba mkoa wa Kagera, Julai 14 mkoa wa Tabora huku ikifuatiwa na mkoa wa Iringa Julai 20 mwaka huu . 
"Nina hamu sana na kufanya show Muleba kwani sijawahi kukutana na mashabiki zangu, hata hivyo sababu ya kuchagua mkoa wa Iringa ni kutokana na mapokezi yao mazuri kwa misimu iliyopita," amesema. 
Pia amewataka mashabiki wategemee vitu vingi vizuri na vya tofauti kwa msimu huu wa nne wa tamasha la wasafi kuanzia jukwaa, mavazi, muziki na wasanii watakaotumbuiza.
Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya anayetengeneza kundi la Wasafi Classic (WCB) Nasib Abdul a.k.a Daimond Platinum akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kuanza kwa Tamasha la Wasafi linalotarajia kufanyika hivi karibu katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania.
Meneja wa Msanii Diamond Platinum Hamis Tale Tale a.k.a Babu Tale akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Wasafi litalotarajia kufanyika hivi karibuni.
Meneja wa Msanii Diamond Platinum, Said Fela akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Wasafi litalotarajia kufanyika hivi karibuni.
Mwakilishi wa BASATA, Prona Masenge akizungumza machache.
Mtaribu wa Masuala ya vijana TACAIDS, Grace Kessy akifafanua jambo.

ASSEMBLY PASSES SUPPLEMENTARY EAC BUDGET PROPOSALS FOR FINANCIAL YEAR 2018/2019

$
0
0

cid:5cc40b6c-53ac-4312-8698-e2bfa635d25b
East African Legislative Assembly

…debate on current financial budget continues today

East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: 25 June 2019: The Assembly late yesterday passed a supplementary budget amounting to USD 390,000 for the Financial Year 2018/19. 

The Supplementary budget is (to be utilized) for the repair and maintenance of the EAC headquarters in Arusha and to facilitate negotiations with development partners during the financial year ending 30th June 2019.

Out of the said amount, USD 305,000 will support the maintenance of the bloc’s headquarters while the balance (USD 85,000) is to support the negotiations for development partners. With it, the Assembly also passed the EAC Supplementary Appropriation (No 2) Bill, 2019. The passage of the EAC Supplementary Bill was preceded by a report presented to the House by Chairperson of the General Purpose Committee, Hon Abdikadir Aden. The House then dissolved itself into a Committee to consider the ‘nuts and bolts’ of the Bill before its eventual passage.

In accordance with the provisions of Article 132 of the Treaty for the Establishment of the East African Community and Rules 66 and 75 of the Rules of Procedure of the Assembly, the Chairperson, Council of Ministers presented to the House and read for the first time the EAC Supplementary Appropriations Bill (2), 2019 on the 20th day of June, 2019.  In the same vein, the Chairperson Council of Ministers laid on the table the Financial Statement for the Supplementary Budget for the FY 2018/2019.

According to Hon Aden, at its sitting held on 8th June 2018, in Nairobi, Kenya, the Assembly passed a total budget of USD 99,770,716 for the East African Community for the FY 2018/2019. In addition to this, during the 4th Meeting of the 2nd Session of the 4th Assembly held from 16th February – 8th March 2019, in Zanzibar, United Republic of Tanzania, the Assembly approved a Supplementary budget amounting to USD 12,679,598.

The Chairperson further informed the House that during the consideration and approval of the budget, most Organs and Institutions of the EAC remained with a number of unfunded priorities due to budgetary constraints.“Over the course of the financial year, the unfunded priorities continued to affect the effective functioning of these Organs and Institutions”, the Chair added.

The Committee was informed that in FY 2018/2019, the People’s Republic of China granted the EAC USD 200,000 under the framework agreement on technical cooperation between the EAC and government of Peoples’ Republic of China. USD 115,000 of the grant provided was allocated to transport and works to engage development partners to support implementation of Heads of State infrastructure projects among others.

The Council, therefore, sought for approval of USD 85,000, part of the unallocated balance of the Chinese Government grant to convene the Joint Technical Experts Meeting of Energy, Finance and EAC Affairs to agree on the Roadmap for the next ten years.

Hon Isabelle Ndahayo represented the Council of Ministers during the debate. Meanwhile, the debate on the substantive budget amounting to USD $111,450,529 for the Financial Year 2019/2020 will continue this afternoon.
The EAC Budget is themed: “Transforming lives through Industrialization and Job Creation for shared prosperity.  According to the Chair of Council of Ministers, the priority interventions for FY 2019/2020, will focus on the consolidation of the Single Customs Territory and promotion of intra and extra EAC trade and export competitiveness, development of regional infrastructure, effective implementation of the Common Market Protocol and the enhancement of regional industrial development.

Other areas include the implementation of the roadmap towards the EAC Monetary union, institutional transformation focusing on the implementation of the institutional review recommendations and improvement of performance management at the EAC Organs and institutions.
 Hon Aden Abdikadir presenting the report of the General Purpose Committee
 Hon Rose Akol makes a point at the debate. The Assembly passed the supplementary EAC budget proposals for Financial Year 2018/2019
Hon Isabelle Ndahayo representing the Council of Ministers during the debate

Makamu wa Rais Mhe. Samia ashiriki Dua ya pamoja msiba wa mke wa Dkt. Mabodi

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  Juni 25, 2019 ameshiriki katika Dua ya pamoja na Familia ya Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Sadallah Mabodi wakati Makamu wa Rais alipofika nyumbani kwa Dkt. Mabodi Mikocheni jijini Dar es salaam kumfariji kutokana na kifo cha mkewe Dkt. Badriya Abubakar Gurnah kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Dkt. Abdallah Juma Sadallah Mabodi
 Sehemu ya waombolezaji


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamema Shein (kushoto) na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif Iddi 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Familia baada ya Dua.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images