Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

kocha wa Taifa Stars ana matumaini ya kufanya vizuri dhidi ya Kenya leo

$
0
0

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars, Emmanuel Amunike,anamatumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wa pili wa mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON)  dhidi ya Kenya, katika mchezo utakaofanyika Juni 27,katika Uwanja wa 30 Juni,Misri.

Akizungumza na waandishi wa habari,Amunike,alisema anatambua Kenya ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri,lakini hilo halimpi shida kwakuwa viwango vya wachezaji wa Kenya na vya wachezaji wa Tanzania  vinalingana,hivyo hana wasiwasi wa kupata matokea katika mchezo huo..

“Timu zote ni za kutoka Afrika Mashariki na Kenya ni majirani zetu,na wote tunazungumza lugha ya Kiswahili,kwahiyo hakuna kitu cha kujificha ,kitu kikubwa ni kwamba ni kwa jinsi gani tutaweza kufanya katika huo mchezo,tulionao  katika mchezo wa Senegal wachezaji walikuwa na uoga,lakini siwezi kuwalaumu, kwakuwa haya ni mashindano yao makubwa kucheza,”alisema na kuongeza:

“Kitu kikubwa cha muhimu ambacho tunachokifanya kwasasa ni kuwapa moyo kuwajenga kiakili na kuwajengea ubora zaidi uwanjani wachezaji  kabla ya mchezo wetu unaofuata,binafsi  nina wachezaji bora na wenye uwezo,kwahiyo katika soka la kisasa naamini wanasifa za kushindana.”

Taifa Stars,inatarajia kushuka dimbani Alhamisi wiki hii, ikiwa na matumaini ya kupata alama tatu muhimu, ambazo zitaisaidia kuiweka katika mazingira mazuri ya kuweza kupata nafasi ya kufuzu kwa raundi ya pili ya mashindano.

WAAMBIENI UKWELI WATOTO KAMA WAMEAMBUKIZWA VVU

$
0
0

Washiriki wa Kambi ya Ariel 2019 wakicheza katika ukumbi wa Landmark Hotel Jijini Dar es salaam Juni 24,2019

Mwezeshaji Kiongozi, Mgunga Mwamnyenyelwa akitoa mada kwenye kambi ya Ariel inayofanyika jijini Dar es salaam
**
Baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwapa watoto wao wanaoishi na VVU dawa za kupunguza makali ya VVU bila kuwaeleza kuwa dawa hizo zinatibu nini hali inayochangia watoto hao kuacha dawa hizo kutokana na kutokujua umuhimu wake.
Hayo yameelezwa na watoto na vijana kutoka mikoa ya Mara, Shinyanga, Simiyu na Mwanza wanaoshiriki Ariel Camp 2019 iliyoandaliwa na asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI). 
Wakizungumza kwenye kambi hiyo inayofanyika katika hoteli ya Landmark, jijini Dar es Salaam, watoto walisema kutokuwaambia watoto ukweli kuhusu kuishi kwao na VVU ni moja ya sababu zinazofanya watoto hao waache kutumia dawa hizo muhimu.
“Utakuta mzazi anampa mtoto dawa za ARV kila siku lakini hamwelezi kuwa hizo dawa ni za ugonjwa gani. Watoto wakiuliza dawa hizo ni kwa ajili ya nini wanaambiwa ni za kifua ama za kuongeza akili,” alisema mtoto mmoja kutoka Simiyu na kuungwa mkono na wenzake. 
“Kutomwambia mtoto ukweli si sahihi kwani kunamfanya asijue umuhimu wa dawa hizo kwa maisha yake. Pia mtoto asipoambiwa ukweli kuhusu hali yake ni hatari kwani pindi atakapojua ukweli anaweza kuchukua maamuzi mabaya hivyo tunaomba wazazi wasiwafiche watoto wao,” aliongeza mtoto wa Mwanza. 
Watoto hao walitoa wito kwa wazazi na walezi ambao wanaendekeza waganga wa kienyeji badala ya kumpeleka mtu hospitali anapoumwa. Walisema kuwa kutokana na kuwapeleka kwa waganga hao wagonjwa, wazazi na walezi wamekuwa wakidanganywa kuwa mgonjwa amerogwa. Walisema matokeo ya kupelekwa mgonjwa kwa mganga wa kienyeji ni kukosa huduma sahihi za afya hali inayosababisha kupoteza maisha hivyo kuchangia vifo vingi vya watu wanaoshi na maambukizi. 
Na Kadama Malunde – Malunde1 blog 

TAARIFA YA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KITAIFA YATAKAYOFANYIKA JIJINI TANGA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU


   Simu: 026-2322480                                                             Sera, Uratibu, Bunge na Uwekezaji
            2 Mtaa wa Reli
Nukushi: 026-2324534                                                                          S. L. P. 980,
Barua-pepe: ps@pmo.go.tz                                                  40480 – Dodoma,                       
Tovuti:  www.pmo.go.tz                Tanzania.


25 Juni, 2019  
                                                                                                       

Tanzania ikiwa ni nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa inaungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya kwa lengo la kuikumbusha jamii juu ya tatizo kubwa lilipo katika jamii yetu juu ya Biashara na Matumizi ya Dawa za hizo.
Kitaifa Maadhimisho haya kwa mwaka huu yatafanyika jijini Tanga siku ya Jumatano tarehe 26 mwezi Juni, 2019 katika viwanja vya Tangamano na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa George H. Mkuchika (Mb).

Kauli mbiu ya Kimataifa ya maadhimisho haya kwa mwaka huu inasema Waathirika wa Dawa za Kulevya Wana Haki ya Kupata Huduma za Afya. Kwa kuzingatia Kauli mbiu hii inakumbusha kuwa mapambano dhidi ya Tatizo la Dawa za Kulevya yanahitaji mikakati mtambuka na jumuishi ikiwemo suala la tiba kwa waathirika. Ni muhimu kwa Waathirika wa Dawa za Kulevya kupata tiba stahiki na zilizothibitishwa kisayansi (evidence based practices) ili kuweza kupunguza madhara ya dawa hizo kwa waraibu na jamii inayowazunguka. Baada ya tiba hizo, huduma endelevu za Stadi za Kazi pamoja na Ushauri Nasaha kuzingatiwa ili kuwasaidia waathirika wasirudi kwenye matumizi ya dawa za kulevya. Aidha, mkakati huu unaenda sambamba na mkakati wa utoaji wa elimu kwa vijana ili wasiingie kwenye matumizi ya Dawa za Kulevya pamoja na Udhibiti wa wafanyabiashara wa Dawa hizo. 

Maadhimisho haya ni fursa kwa umma wa Watanzania kwa vile  Tatizo la Dawa za Kulevya linaathiri nchi yetu katika nyanja za kiafya, kijamii, kiuchumi pamoja na kutishia ulinzi na usalama wa nchi yetu.  Katika maadhimisho haya Watanzania wataweza kupata elimu na kukumbushwa kuwa matumizi na biashara ya dawa za kulevya yana athari kubwa kwa mtumiaji, kwa jamii na kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu.

Tatizo la dawa za kulevya husababisha madhara kiafya ikiwa ni pamoja na kuchocheakuenea kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI, virusi vya homa ya ini aina ya B na C, Kifua Kikuu, magonjwa ya akili, pamoja na usugu wa tiba ya kifua kikuu na UKIMWI. Aidha, baadhi ya dawa za kulevya husababisha matatizo ya uzazi ikiwemo upungufu wa nguvu za kiume, kuharibika kwa mimba, kuzaliwa kwa watoto wenye matatizo ya akili pamoja na kuenea kwa kansa mbalimbali kama vile kansa ya koo, mapafu na mara nyingine husababisha vifo ghafla vya  kutokana na dozi kuwa kubwa “overdose”.  Aidha Serikali imeendelea kusimamia utoaji tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya ili kupunguza madhara yanayotokana na matumizi ya dawa hizo, na kufanikiwa kuongeza idadi ya waathirika wa dawa za kulevya katika vituo vya tiba kutoka wagonjwa 2,400 mwaka 2015 hadi wagonjwa 7000 mwaka 2018. Hali hii imeasaidia kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwa waraibu wa dawa za kulevya wanaojidunga kutoka 35% mwaka 2015 hadi 18.5%.

Pia, Serikali inamtaka kila mwananchi kwa nafasi yake katika jamii kushirikiana na vyombo vya dola kutoa taarifa endapo kutabainika kuwepo kwa matumizi na biashara ya dawa za kulevya. Pamoja na hilo Serikali inatoa wito kwa viongozi wa dini kulikemea suala la matumizi ya dawa za kulevya misikitikini na makanisani. Sambamba na hilo, Serikali inawakumbusha  Viongozi wa dini zote kuwa wana nafasi kubwa katika jamii ya kuhakikisha watoto, vijana pamoja na jamii yote kwa ujumla wanapata mafunzo ya kuwajenga kiroho, kimwili na kisaikolojia ili wawe na tabia njema katika jamii na mfano wa kuigwa kwa matendo mema.

Serikali inaikumbusha jamii kushiriki kikamilifu katika kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya, kujenga malezi bora kwa watoto katika ngazi ya familia, na kuwapeleka kwenye matibabu watumiaji wa dawa za kulevya. Vilevile, Serikali inasisitiza Jamii kuzitambua, kuzienzi na kuziendeleza tamaduni zetu nzuri ili kuinusuru Wananchi wote hasa vijana ambao ndo nguvu kazi ya taifa na matumizi ya dawa za kulevya.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.

JUMANNE, JUNI 25, 2019

DIRISHA LA MAOMBI YA MKOPO KWA NJIA YA MTANDAO KUFUNGULIWA JULAI 1, 2019

$
0
0

Tunapenda kuwafahamisha waombaji mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2019/2020 kuwa dirisha la kuomba mkopo kwa njia ya mtandao litafunguliwa rasmi Jumatatu, Julai 1, 2019 na kufungwa Alhamisi, Agosti 15, 2019. Maombi yote yatafanywa kupitia mtandao utakaopatikana kupitia www.heslb.go.tz.
Kati ya leo (Jumanne, Juni 25) na Julai 1, 2019 wakati dirisha litakapofunguliwa, wanafunzi wanashauriwa kuhakikisha wanakamilisha nyaraka muhimu zinazotajwa katika ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo na Ruzuku kwa 2019/2020’ unaopatikana katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz).  
Nyaraka hizo na maelezo mengine ya ufafanuzi pia yanapatikana katika kitabu kidogo cha ‘Maswali na Majibu 26’ kuhusu uombaji mkopo kinachopatikana katika tovuti hiyohiyo.
 Kwa ajili ya kumbukumbu, nyaraka muhimu ni pamoja na:
i.             Nakala ya cheti cha kuzaliwa cha mwombaji wa mkopo iliyothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA);
ii.            Nakala ya cheti cha kifo cha mzazi wa mwombaji mkopo iliyothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA);
iii.           Barua ya Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO), Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji, Wilaya, Manispaa au Jiji inayothibitisha ulemavu wa mwombaji mkopo au mzazi wake; na
iv.           Barua kutoka kwa taasisi iliyofadhili masomo ya sekondari au stashahada ya mwombaji mkopo.
Ufafanuzi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na stashahada mwaka huu
Baada ya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita au stashahada (diploma) wamekuwa wakiuliza maswali kadhaa kuhusu utaratibu wa ujazaji wa fomu za uombaji mkopo wakiwa katika kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na iwapo wanaweza kujaza fomu kabla matokeo ya mitihani hayajatoka. 
Ufafanuzi ni kuwa HESLB inawasiliana na Makao Makuu ya JKT ili kuweka utaratibu bora kuwawezesha wanafunzi wahitaji waliopo katika kambi za JKT kuwasilisha maombi kwa njia ya mtandao. 
Aidha, mfumo wa uombaji mikopo kwa njia ya mtandao utakaofunguliwa Julai 1 mwaka huu haumlazimishi mwombaji kuwa na matokeo ya kidato cha sita. Mwombaji atapaswa kuwa na namba ya mtihani wake wa kidato cha nne tu.
Wito
Waombaji wa mikopo watarajiwa wanashauriwa kusoma mwongozo uliotolewa na kuandaa nyaraka zote muhimu zinazohitajika kuthibitisha uhitaji wao kabla ya kuingia katika mfumo wa uombaji. Uzoefu unaonesha kuwa mwombaji mkopo anaweza kutumia dakika 30 kukamilisha maombi yake katika mfumo ikiwa ana nyaraka zote muhimu. 
Imetolewa na: 
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Dar es salaam
Jumanne, Juni 25, 2019

DC WA TANDAHIMBA MHE> WARYUBA ACHANGIA UJENZI ZAHANATI MPYA YA KIJIJI CHA MITONDI B

$
0
0

Mkuu wa wilaya Tandahimba Mhe Sebastian Waryuba Leo Jumanne Juni 25, 2019 ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati mpya ya Mitondi iliyopo Kijiji cha Mitondi B kata ya Kitama na kuzungumza na Wanakijiji ambapo amehaidi kutoa mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya kusaidia mradi huo wa ujenzi.
DC Waryuba ametoa ahadi hiyo kupitia mkutano na Wananchi uliofanyika kwenye Zahanati hiyo jambo ambalo liliibua shangwe kwa Wakazi hao.

"Natoa mifuko 30 ya saruji. Mkiwa tayari mje kuichukua wakati wowote ule." Alisema DC Waryuba huku akishangiliwa na Wananchi.

Pia Ndugu Khasim S. Lihumbo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba alisema Zahanati hiyo  imetengewa Tsh. Milioni 37 kwa kila Mwaka wa fedha kuanzia 2018/19 na 2019/2020 kwa ajili ya kuikamilisha na ianze kazi mara moja.
Katika ziara hiyo DC Waryuba aliambatana na Katibu Tawala wilaya Tandahimba Ndugu Benaya Kapinga, Mwakilishi Mkurugenzi Ndugu Khasim Lihumbo, Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu na kupokelewa na wenyeji wao Halmashauri ya Serikali ya Kijiji cha Mitondi B.
Mkuu wa wilaya Tandahimba Mhe Sebastian Waryuba akizungumza na wanamchi  alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati mpya ya Mitondi iliyopo Kijiji cha Mitondi B kata ya Kitama
Mkuu wa wilaya Tandahimba Mhe Sebastian Waryuba akikagua mradi wa ujenzi wa Zahanati mpya ya Mitondi iliyopo Kijiji cha Mitondi B kata ya Kitama

KINGDOM OF NORWAY ACCREDITS ENVOY TO EAC

$
0
0
 cid:5cc40b6c-53ac-4312-8698-e2bfa635d25b
EAC Secretariat

The Kingdom of Norway has today accredited its Ambassador Extraordinary and Plenipotentiary to the United Republic of Tanzania, Ms. Elisabeth Jacobsen, to also serve as Ambassador to the East African Community.

H.E. Jacobsen, who was accredited at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania, said that there were a growing interest and knowledge about the EAC, which she noted was setting the stage for closer cooperation. She said that Norway views the Community as an important partner especially in efforts aimed at ensuring peace and security in the region.

Amb Jacobsen commended the EAC Secretariat for the good work that has led to the attainment of several achievements and assured the Secretary-General of her country's commitment to continue supporting the integration process.

She expressed her country's interest towards supporting integration agenda particularly in areas such as peace and security, human rights and intra-regional trade among the EAC Partner States.

“We consider EAC as an important player in economic and political development in the region and I assure you of our continued support to the integration agenda,” said the envoy.

On his part, EAC Secretary General Amb Liberat Mfumukeko hailed the existing cordial relations between the EAC and Norway. Amb. Jacobsen welcomed the continued support from Norway saying it had enabled the Community to achieve its ambitious agenda.

Amb. Mfumukeko also shared the steady progress made by the Community in promoting integration through the four pillars as set out in the EAC Treaty, namely the: Customs Union, Common Market, Monetary Union, and Political Federation, adding that the achievements attained so far were due to political goodwill among the EAC Heads of State.

Present at the accreditation ceremony was the EAC Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sectors, Hon. Christophe Bazivamo, and the Lake Victoria Basin Commission Executive Secretary, Mr. Said Ally Matano.
 EAC Secretary-General Amb Liberat Mfumukeko receives a letter of accreditation from  Norway Ambassador Ms.Elisabeth Jacobsen
 Ambassador Jacobsen, Amb Liberat Mfumukeko, EAC Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sectors, Hon. Christophe Bazivamo and Lake Victoria Basin Commission Executive Secretary, Mr. Said Ally Matano
 Norway Ambassador Ms.Elisabeth Jacobsen in discussion with the EAC Secretary General, Amb Liberat Mfumukeko
Norwegian Ambassador Ms.Elisabeth Jacobsen and EAC Secretary General Amb Liberat Mfumukeko displaying EAC plaque

Leo ni siku ya kumbukumbu ya Kifo cha Amina Chifupa na Vita ya dawa za kulevya

KAMISHNA WA UHIFADHI TANAPA,DKT ALLAN KIJAZI AWAVISHA VYEO ASKARI UHIFADHI WAKUU NA WAANDAMIZI

$
0
0
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akiwavisha vyeo vipya vya kijeshi Askari Waandamizi wa shirika hilo programu iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mto wa Mbu wilayani Monduli. 
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akiwavisha vyeo vipya vya kijeshi Askari Wakuu wa shirika hilo programu iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mto wa Mbu wilayani Monduli.
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akizungumza mara baada ya kuwavisha vyeo vipya vya kijeshi Askari Wakuuu na Askari Waandamizi wa shirika hilo programu iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mto wa Mbu wilayani Monduli.
Baadhi ya Makamishna Wasaidizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) pia walikuwa ni miongoni mwa walioshuhudia uvishwaji huo wa vyeo vipya kwa Askari Wakuu na Askari Waandamizi .
Naibu Kamishna-Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara TANAPA ,William Mwakilema akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Naibu Kamishna wa Uhifadhi -Fedha na Rasilimali watu -TANAPA, Nassoro Mndeme akizungumza wakati wa zoezi la uvishaji vyeo vipya kwa Askari Uhifadhi Wakuu na Waandamizi.
Baadhi ya Makamishna Wasaidizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) pia walikuwa ni miongoni mwa walioshuhudia uvishwaji huo wa vyeo vipya kwa Askari Wakuu na Askari Waandamizi .
Kamishna wa Uhifadhi Msaidizi Mwandamizi Mawasiliano TANAPA,Pascal Sheletete akitoa maelezo ya namna ya zoezi la upigaji picha za pamoja litafanyika.
Mgeni Rasmi Kamishna Uhifadhi (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na Askari Wakuu mara baada ya kuvikwa vyeo vipya . 
Mgeni Rasmi Kamishna Uhifadhi (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna Uhifadhi Wasaidizi Waandamizi mara baada ya baada ya kuwavisha  vyeo vipya kwa Askari  Uhifadhi Wakuu na Waandamizi .
Askari Uhifadhi  Wakuu na Waandamizi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuapishwa na kuvikwa vyeo vipya.
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akikagua Gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya programu ya kuvalisha Vyeo Askari Uhifadhi Wakuu na Askari Waandamizi .
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Dkt Allan Kijazi akipokea saluti kutoka kwa kiongozi wa  Brass Bendi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)  mara baada ya kufanya ukaguzi.
  Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt, Allan Kijazi akiongozwa kuelekea katika Jukwaa mara baada ya kuhitimisha zoezi la ukaguzi kwa askari wa Uhifadhi wakati wa Gwaride Maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya programu ya kuvalisha Vyeo Askari Uhifadhi Wakuu na Askari Waandamizi .
Askari Uhifadhi Wakuu na Askari Waandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakila kiapo cha utii wakati wa programu ya kuvalisha Vyeo Askari Uhifadhi Wakuu na Askari Waandamizi iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mto wa Mbu katika wilaya ya Monduli..
Brass Band ya  Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikiongoza Gwaride Maalumu kutoka nje ya uwanja.
Gwaride likitoka nje ya Uwanja.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV.

KAMBI MAALUM KWA WANAWAKE WENYE MAKOVU,ULEMAVU ULIOTOKANA NA VURUGU MAJUMBANI AU AJALI KUFANYIKA JUMAMOSI HII KISARAWE

$
0
0




KISARAWE PWANI Juni, 2019. Programu ya Reconstructive Women and Children ni jitihada ya ushirikiano kati ya Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam (AKHD), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) pamoja na shirika la kibinadamu la Reconstructing Women International (International Confederation for Plastic, Reconstructive and Aesthetic Surgery) ili kutoa huduma ya upasuaji wa kubadili na kuboresha maumbile au ngozi iliyokakamaa kwa wanawake na watoto wa kike maskini wenye ulemavu uliosababishwa na ukatili wa majumbani, kuungua na ajali.


 Ushirikiano huu unalenga kubadlishana na kuimarisha utaalamu wa upasuaji kwa ajili ya kushughulikia hitaji la kitiba la upasuaji wa kubadili na kuboresha maumbile katika maeneo mbalimbali ya Tanzania na Kanda ya Afrika Mashariki. 


Programu hii ilianzishwa mnamo Januari 2016 ikihusisha wapasuaji kutoka Marekani, Canada na Ulaya wakifanya kazi kwa karibu na wanatiba wa Kitanzania. Tangu hapo, kupitia awamu NNE, operesheni 143 za upasuaji zimefanywa bila gharama yoyote kwa wagonjwa (ambao ni wahanga wa ukatili wa majumbani, kuungua na ajali), na kurejesha utendaji wa kimwili na mwonekano wa wanawake na watoto wanaoishi katika mazingira magumu. 


Kwa kuwa upasuaji huu  wa kuboresha maumbile, ngozi iliyokakamaa, umeonesha kuboresha kwa kiwango kikubwa maisha ya wale wanaosumbuliwa na unyanyapaa na ulemavu, Hospitali ya Aga Khan na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zinayo furaha kushirikiana kwa mara nyingine tena katika mradi huu wa kipekee. 


Kambi kubwa ya uchunguzi ili kuwatambua wagonjwa wenye uhitaji kwa ajili ya awamu ya 5 Hospitali ya Aga Khan  Muhimbili pamoja na shirika la SADAKA network  Tunapanga kuwa na kambi hii kwa mara ya kwanza kabisa wilayani Kisarawe .kambi hii itafanyika  hospitali ya wilaya ya kisarawe na mganga mkuu wa wilaya ya kisarawe atakuwepo  na kambi hii imepewa Baraka zote na Halmashauri ya wilaya ya kisarawe 


Ambapo wanawake na watoto wenye ulemavu mbalimbali wanaalikwa kuhudhuria kambi hii ya tathmini ya awali; wataonwa na wataalamu waliobobea katika upasuaji wa Kubadili na Kuboresha Ngozi/Maumbile iliyokakamaa. 



KWA Mawasiliano 


AKH-D: Olayce S. Lotha, olayce.lotha@akhst.org, Simu: +255-717-516-650 


SD ; Viola Julius ,viola.m@sadakanetwork.com , simu : 0763858029

Tigo yazindua mtandao wa 3G Longido

$
0
0
 Meneja wa Tigo kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo (kati kati) akipongezana na Mtendaji wa kijiji cha Longido Leiyo Laizer (kushoto)  na mwenyekiti wa kijiji hicho Theresia Kashuma  (kulia)muda mfupi baada ya kuzindua mnara mpya ulio ongezewa uwezo kutoka 2G kwenda 3G 


Maofisa wa Tigo wakiwahudmia wateja ambao ni wakazi wa Longido mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa mnara mpya ulio ongezewa uwezo kutoka 2G kwenda 3G  uliofanyika Longido jana.


 Meneja wa Tigo kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo (kushoto) akiongea na wananchi wa Longido mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa mnara mpya ulio ongezewa uwezo kutoka 2G kwenda 3G . Wa kwanza kulia ni Mtendaji wa kijiji cha Longido Leiyo Laizer na Mwenyekiti wa kijiji Theresia Kashuma

 Mwenyekiti wa kijiji cha Longido Theresia Kashuma (kati kati) akiongea na wananchi wa Longido mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa mnara mpya wa Tigo ulio ongezewa uwezo kutoka 2G kwenda 3G. Kushoto ni Meneja wa Tigo kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo na kulia ni Mtendaji wa kijiji cha Longido Leiyo Laizer

RC SHIGELLA AHIMIZA JAMII KUSHIRIKI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA, AZUNGUMZIA MADHARA YAKE

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martini Shigella amesema umefika wakati kwa jamii kushiriki kikamilifu kukomesha biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Akizungumza leo Juni 25,2019 wakati anafungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Tanga, Shigella amesema athari za dawa za kulevya ni tatizo la jamii nzima, hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha sote wote tunashiriki kukomesha matumizi ya dawa za kulevya.

"Maelezo ya awali ambayo yametolewa na Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibi na Kupambana na Dawa za Kulevya Valite Mwashusa yameonesha ukubwa wa tatizo la dawa za kulevya , na kwamba dawa za kulevya limeendelea kuwa tatizo kubwa na limeathiri jamii,"amesema Shigella.

Amefafanua kwa Mkoa wa Tanga kuna dawa za aina ya bangi, Heroine na Cocain na kwamba ukiangalia takwimu utabaini bado matumizi ya dawa za kulevya ni makubwa.

Ameeleza takwimu zinaonesha mwaka 2016 kulikuwa na kesi 331 na kati hizo kesi zaidi ya 381zimetolewa hukumu na waliohusika kuhumiwa kufungwa jela au kunyongwa.

Wakati kwa mwaka 2017 Shigella kulikuwa na kesi 221 ambazo zilihusisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilogramu 1,584 na watu zaidi ya 2945 walihusishwa na kwamba ukifuatilia mtiririko wa takwimu kesi za dawa za kulevya zimepungua sana.

"Kwa Mkoa wa Tanga moja ya changamoto ni uwepo wa dawa za kulevya kwenye mitaa mbalimbali na jamii inawajua wanaohusika na wanaojihusisha na dawa hizo.Hata hivyo jamii bado jamii bado haijaona umuhimu wa kushirikiana na vyombo vya ulinzi kwa kutoa taarifa.

"Umefika wakati kwa jamii kutoa ushirikiano kwa kuhakikisha wanaojihusisha na dawa za kulevya wanabainishwa na kuchukuliwa hatua. 
"Kwa kufanya hivyo tutaokoa jamii ya Watanzania kwani matumizi ya dawa za kulevya yamekuwa yakisababisha madhara mengi yakiwemo ya jamii kupotea kwa nguvu kazi ya Taifa,"amesema.

Amesisitiza kuwa ni wakati muafaka sasa kwa wananchi wote kujipanga vizuri kukomesha dawa za kulevya.Amezungumzia zaidi kuhusu dawa za kulevya amesema ni tatizo kubwa na kutoa mfano kuwa katika nchi jirani ya Kenya Mirungi imeruhusiwa na inauzwa sokoni lakini kwa Tanzania ni marufuku, hivyo ametoa rai kwa jamii kuhakikisha dawa za kulevya haziingii.

Pia amesema Serikali ya Awamu ya Tano imejidhatiti kuhakikisha nchi ya Tanzania inakuwa salama na kukomesha biashara ya dawa za kulevya na ndio maana Rais Dk.John Magufuli aliamua kuanzisha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.

"Sote ni mashahidi hivi sasa hata wale waliokuwa mapapa wa biashara za dawa za kulevya leo hawasikiki na hawaonekani kabisa maana wamedhibitiwa.Kwa Mkoa wa Tanga tumejipanga vema kuhakikisha tunaendelea kudhibiti dawa za kulevya,"amesema.

Kuhusu maadhimisho hayo, Shigela amewataka wananchi wa Jiji la Tanga kuhakikisha wanafika kwenye maonesho hayo ambayo yanafanyika Viwanja vya Tangamano kwa lengo la kujifunza kwani kuna mabanda ambayo yanatoa elimu mbalimbali kuhusu dawa za kulevya nchini na madhara yake.

Pia ameseme kuna kila sababu za nyumba za kutibu walioathirika na dawa za kulevya wanashirikiana na taasisi nyingine ikiwemo taasisi ya fedha kuhakikisha waliokuwa wanatumia dawa za kulevya na kupata nafuu wanashirikishwa kikamilifu kwenye shughuli za ujenzi wa nchi yetu.

 Mkuu wa Tanga Martin Shigella (aliyeva suti) akikapata maelezo  kwenye moja banda lililopo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika Jiji la Tanga.Kushoto  ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya   Valite Mwashusa
Kaimu Kamishna Jeneral wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Valite Mwachusa (kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga wakati anatembelea maganda yaliyopo katika maadhimisho ya siku ya dawa za kulevya Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika Jiji la Tanga

WAKAZI 2,073 JIJINI ARUSHA WASAJILI LAINI WAKATI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0

 Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

WAKAZI wapatao 2073 katika Jiji la Arusha wamesajiri laini zao katika kipindi cha siku saba cha maadhimisho ya utumishi wa Umma ambapo TCRA ilitumia nafasi hiyo kutoa elimu na kuhamasisha watumiaji wa mawasiliano kusajiriwa laini zao kwa njia ya vidole.

Aidha wananchi wapatao 4, 757 wameweza kuchukua fomu na kujisajiri kwa ajili ya vitambulisho vya Uraia ,vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho, NIDA na kuweza kusajiriwa laini za simu ,ambapo miongoni mwao walisajiri laini mpya 417.
.
Akizungumza katika Viwanja vya Kilombero ,jijini hapa,Kaimu Mkuu wa Kanda wa TCRA Landa ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salumu amewataka watumiaji wa mawasiliano ya simu kuendelea kusajiri laini zao ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza mara baada ya mchakato kufungwa Desemba 30,mwaka huu.

Imelda ameonya matumizi ya laini za simu zisizosajiriwa kuwa ifikapo Desemba 30 mwaka huu laini hizo zitazimwa  na hatua kali zitachukuliwa kwa atakayetumia lini bila kusajiriwa.

Amesema katika zoezi hilo la kutoa elimu kwa mtumiaji wa mawasiliano waliambatana  na maofisa wa NIDA Idara ya Uhamiaji, huku makampuni ya simu kutoka Vodacom,Tigo,Halotel,TTCL na Airtel zikishiriki katika kuhakikisha wananchi wanasajiri laini huzo kwa njia ya Vidole.

"Kwa ujumla mchakato umefanyika kwa mafanikio kwani wananchi  4757 walichukua fomu za kusajiri vitambulisho vya uraia, huku  laini zipatazo  2073 zilisahiriwa kwa njia ya vidole , laini mpya zilizonunuliwa na kusajiriwa zilikuwa 417,"amesema Imelda

Awali Mkuu wa Kitengo cha Huduma za watumiaji bidhaa za mawasiliano,Zakayo Ringo amesema zoezi hilo limekuwa na mwitikio mkubwa na kuwataka waliokosa fursa ya kusajiri vitambulisho vya  NIDA na  Kilombero wataendelea kusajiriwa katika ofisi za NIDA zilizopo Kisongo nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wakati usajili huo kuendelea katika viwanja vya Kilombero na Chuo cha Uhasibu  Arusha wamelalamikia utaratibu mbovu wa NIDA katika kuhakiki namba za vitambulisho  na kusababisha wananchi kutumia muda mrefu kukaa kwenye foleni jambo ambalo linazorotesha zoezi hilo la kusajili. 
Kaimu Mkuu wa Kanda wa TCRA Landa ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salumu 

Benki ya Stanbic yatoa mafunzo kwa Meneja Rasilimali watu

$
0
0
 Mtaalamu wa masuala ya Kiuchumi,  Paulsen Mrina (kulia shati  la blue bahari) akiwaelezea Meneja Rasilimali Watu kutoka kampuni mbali mbali jinsi ya kutunza fedha, katika semina ya kuwawezesha kiuchumi iliyoandaliwa na Benki ya Stanbic Tanzania, Coral Beach Hotel, Dar es Salaam.
Meneja Rasilimali Watu kutoka kampuni mbali mbali wakijadili jambo katika semina kwaajili ya kuwapatia mafunzo ya kuwawezesha kiuchumi, iliyoandaliwa na Benki ya Stanbic Tanzania, Coral Beach Hotel, Dar es Salaam.

WAAMBIENI UKWELI WATOTO KAMA WAMEAMBUKIZWA VVU

$
0
0

Washiriki wa Kambi ya Ariel 2019 wakicheza katika ukumbi wa Landmark Hotel Jijini Dar es salaam Juni 24,2019

Mwezeshaji Kiongozi, Mgunga Mwamnyenyelwa akitoa mada kwenye kambi ya Ariel inayofanyika jijini Dar es salaam
**
Baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwapa watoto wao wanaoishi na VVU dawa za kupunguza makali ya VVU bila kuwaeleza kuwa dawa hizo zinatibu nini hali inayochangia watoto hao kuacha dawa hizo kutokana na kutokujua umuhimu wake.
Hayo yameelezwa na watoto na vijana kutoka mikoa ya Mara, Shinyanga, Simiyu na Mwanza wanaoshiriki Ariel Camp 2019 iliyoandaliwa na asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI). 

Wakizungumza kwenye kambi hiyo inayofanyika katika hoteli ya Landmark, jijini Dar es Salaam, watoto walisema kutokuwaambia watoto ukweli kuhusu kuishi kwao na VVU ni moja ya sababu zinazofanya watoto hao waache kutumia dawa hizo muhimu.

“Utakuta mzazi anampa mtoto dawa za ARV kila siku lakini hamwelezi kuwa hizo dawa ni za ugonjwa gani. Watoto wakiuliza dawa hizo ni kwa ajili ya nini wanaambiwa ni za kifua ama za kuongeza akili,” alisema mtoto mmoja kutoka Simiyu na kuungwa mkono na wenzake. 

“Kutomwambia mtoto ukweli si sahihi kwani kunamfanya asijue umuhimu wa dawa hizo kwa maisha yake. Pia mtoto asipoambiwa ukweli kuhusu hali yake ni hatari kwani pindi atakapojua ukweli anaweza kuchukua maamuzi mabaya hivyo tunaomba wazazi wasiwafiche watoto wao,” aliongeza mtoto wa Mwanza. 

Watoto hao walitoa wito kwa wazazi na walezi ambao wanaendekeza waganga wa kienyeji badala ya kumpeleka mtu hospitali anapoumwa. Walisema kuwa kutokana na kuwapeleka kwa waganga hao wagonjwa, wazazi na walezi wamekuwa wakidanganywa kuwa mgonjwa amerogwa. Walisema matokeo ya kupelekwa mgonjwa kwa mganga wa kienyeji ni kukosa huduma sahihi za afya hali inayosababisha kupoteza maisha hivyo kuchangia vifo vingi vya watu wanaoshi na maambukizi. Na Kadama Malunde – Malunde1 blog 

KAMATI YA UONGOZI YA MKURABITA YATEMBELEA WAJASIRIAMALI WA WILAYA YA KASKAZINI B UNGUJA

$
0
0
 Mjasiriamali Chum Makame Chum akielezea changamoto wanazokutana nazo katika utendaji wa shughuli zao kwa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kamati hiyo kukagua shughuli wanazozifanya visiwani Zanzibar. 
 Machano Haji akitoa maoni yake kwa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA iliyopo Zanzibar inayoendelea na ziara yake ya kukagua Wajasiriamali waliowapatia mafunzo visiwani Zanzibar. Wajasiriamali hao waliiomba Kamati hiyo kusaidia kupata Soko la bidhaa wanazozozalisha.

 Mratibu na Katibu wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Tanzania Dkt. Seraphia Mgembe akizungumza na Wajasiriamali wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja ambapo Kamati hiyo ipo visiwani Zanzibar kukagua shughuli zinazofanywa na MKURABITA Zanzibar.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA wakikagua bidhaa kutoka kwa Mjasiriamali Asha Juma huko Kinduni Kaskazini Unguja. Kamati hiyo ilietembelea Wajasiriamali wa Kaskazini na kusikiliza maoni yao ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kamati hiyo kukagua shughuli wanazozifanya visiwani Zanzibar. 
Mfanyabiashara wa Mchele Visiwani Zanzibar (Zanzibar Rice)Yussuf Faki akitoa maelezo kwa baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kamati hiyo kukagua shughuli wanazozifanya visiwani Zanzibar. Picha na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar

MWENYEKITI MPYA WA BODI YA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI AKUTANA NA MENEJIMENTI NA WATUMISHI WA REA

$
0
0
 Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini Wakili Julius Kalolo akizungumza na Menejimenti na Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Jijini Dodoma.Mwenyekiti uyo amewataka wafanyakazi hao kufanikisha azma ya Serikali ya kufikisha umeme kila kijiji inatimia kufikia mwaka 2021.
 Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini Wakili Julius Kalolo akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Jijini Dodoma.
 Kaimu Mkurugenzi wa REA Mhandisi Jones Olotu akimkaribisha Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini Wakili Julius Kalolo katika Ofisi za Wakala wa Nishati Vijijini JIjini Dodoma.
 Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini Wakili Julius Kalolo

 Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini Wakili Julius Kalolo(hayupo pichani) wakati akizungumz anao Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini Wakili Julius Kalolo akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Jijini Dodoma.
 
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini Wakili Julius Kalolo akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Jijini Dodoma. Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.

MA -DC MKOANI PWANI WAAGIZWA KUANZA UTEKELEZAJI WA CHF ILIYOBORESHWA HADI IFIKAPO JULAI 31 -NDIKILO

$
0
0
 Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
SERIKALI mkoani Pwani, amewaagiza wakuu wa wilaya mkoani humo, kuhakikisha wanaanza utekelezaji wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF)kuanzia sasa na ifikapo Julai 31 mwaka huu apewe taarifa juu ya utekelezaji huo kwa halmashauri zote.

Aidha amewahamasisha wananchi, kujiunga na CHF iliyoboreshwa kwa sh.30,000 kwa familia ya watu sita, badala ya 10,000 ya awali ili kupata matibabu kirahisi kwa kipindi cha mwaka mzima.
 Akizindua utekelezaji wa mfuko huo kwa mkoa wa Pwani, Miono Bagamoyo, mkuu wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo alieleza hataki kusikia visingizio hivyo ifikapo Julai 31 utekelezaji uanze kwa kila wilaya.

"Ila isiwe tena hamasa hii ikaachiwa kwa wakuu wa wilaya pekee kisa nimewaagiza hapana, hamasa hii ikafanyike kwa madiwani,maofisa tarafa,wenyeviti wa vijiji,kata,mitaa,watendaji na wadau waelimishe wananchi katika vijiji ,kata,tarafa na mitaa yao"alifafanua Ndikilo.
Mkuu huyo wa mkoa alisema, mikoa ya Shinyanga,Dodoma na Morogoro imeshafanikiwa sana hivyo na mkoa wa Pwani ni zamu ya kuhamasisha ili watu wajiunge kwa wingi .

"Kiwango hicho cha 30,000 ambacho ni kama 5,000 kwa kila mmoja kwa wanafamilia sita kitasaidia kutibiwa mwaka mmoja kuanzia ngazi ya zahanati,hospitali ya wilaya na hospitali ya mkoa badala ya zamani ambapo 10,000 ilikuwa ukitibiwa katika kituo na kijiji ulipo pekee""Magonjwa hayapigi hodi tusiweke rehani maisha yetu kwa kuona 30,000 ni kubwa ,tulinde afya zetu ,alisema Ndikilo.

Ndikilo aliongeza, katika kukabiliana na changamoto zilizokuwepo kipindi cha nyuma na kuzingatia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015-2020 na mipango mkakati wa sekta ya afya 2015-2020 serikali imeweka mkakati ikiwemo kuongeza bajeti katika sekta ya afya hususan kwenye vifaa tiba na dawa.

"Kwa hili, sisi mkoa wa Pwani, bajeti yetu ni zaidi ya bilioni mbili tumepokea 2018-2019 kwajili ya dawa na vifaa tiba ili kuboresha sekta hiyo'"aliweka bayana.

Pia ameelekeza, serikali ya kijiji cha Miono kata ya Miono Bagamoyo,kumthibitishia majina ya wajane na wagane wote waliopo katika kijiji hicho ili awalipie kujiunga na mfumo huo .

Awali meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) Mkoani Pwani,Ellentoruda Mbogoro aliwatoa shaka wananchi na kuwaomba wasikate tamaa kwani kwa sasa vifaa tiba na dawa zitakuwepo za kutosha katika vituo vya afya na hospital.

Mkazi wa kijiji cha Miono ,Fatma Mrisho alisema mpango huu ni mkombozi hasa kwa kaya zilizo na maisha duni.

SPIKA NDUGAI AKABIDHI UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS MAGUFULI CAIRO NCHINI MISRI

$
0
0
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Balozi Aboubakr Mahmoud katika hoteli ya Semiramis Intercontinental,Cairo nchini Misri.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Balozi Aboubakr Mahmoud ambae alimuwakilisha Rais wa Misri katika hoteli ya Semiramis Intercontinental, Cairo nchini Misri.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akimkabidhi ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Balozi Aboubakr Mahmoud ambae alimuwakilisha Rais wa Misri katika hoteli ya Semiramis Intercontinental, Cairo nchini Misri. Kulia ni Afisa mwandamizi kutoka Bunge la Misri
Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akipokea ujumbe maalum wa Rais wa Misri kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Balozi Aboubakr Mahmoud ambae alimuwakilisha Rais wa Misri walipokutana katika hoteli ya Semiramis Intercontinental,Cairo nchini Misri. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WADAU WATAKIWA KUJISOMEA ZAIDI ILI KUJIONGEZEA MAARIFA YA MASUALA YA SHERIA

$
0
0
 Na Kulwa Mayombi
Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu watu (AfCHPR) yenye makao yake makuu jijini Arusha imewahimiza  wadau mbalimbali kuitumia kikamilifu Maktaba iliyopo katika Mahakama hiyo kwa lengo la kujiongeza maarifa hasa yanayohusu masuala ya sheria.

Alizungumza katika Juma la Maktaba (Library Week) liloratibiwa na AfCHPR. Msajili wa Mahakama hiyo Jaji Sylvain Ore’ alisema kuwepo kwa vitabu vingi,majarida kadhaa na rasilimali nyingine katika Mahakama hayo kunatoa fursa zaidi kwa wadau na wananchi kwa ujumla wa ndani na nje ya nchi kujijengea uwezo wa kujifunza hasa katika masuala ya utetezi na ukuzaji wa haki za binadamu.

“Maktaba na huduma zake ni njia ya kutoa maarifa katika jamii na inatoa nafasi za kujifunza, inasaidia kuboresha mawazo mapya na pia huhakikisha masjala ya kuaminika ya maarifa yaliyopatikana na kukusanywa na vizazi vilivyopita alisema  Jaji Ore’’.”

Kwa mujibu wa Jaji Ore’,AfCHPR imetambua umuhimu huo wa Maktaba hivyo kuiweka moja kwa moja chini ya idara ya usajili tangu ianzishwe Mahakamani hapo mwaka 2009 kwa lengo la kusaidia shughuli za kisheria za  watumishi wa Mahakama,watafiti na wadau mbalimbali.

Alisema kwa sasa Maktaba hiyo katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ina zaidi ya vitabu 6000 na inatarajiwa vitaongezeka katika kipindi cha Miaka michache ijayo na kuiiomba menejimenti ya Maktaba hiyo kuangalia uwezekano wa kuongeza bajeti ya kununua vitabu zaidi na rasilimali nyingine  za Maktaba ili kuimarisha upatikanaji wa vitabu vya rejea kwa watumiaji wa Maktaba hiyo.

Kwa upande wake Mkutubi wa Maktaba ya Mahakama ya Afrika ya haki za Binadamu na Watu.DR.Fidelis Katonga alisema pamoja na mambo mengine Juma la Maktaba katika Mahakama hiyo  kuonyesha jukumu la Maktaba katika kukuza na  kulinda haki za Binadamu barani Afrika,kuhimiza matumizi ya Maktaba.kupata mrejesho wa watumiaji wa Maktaba hiyo na pia kutafuta Washirika  zaidi wa Maktaba na taasisi nyingine.

Dr.Katonga pia alitaja mafanikio ya Maktaba hiyo tangu kuanzishwa kwake kuwa ni pamoja na kuwa na vitabu Zaidi ya 6000,kuruhusu wadau mbalimbali wakiwemo wananchi kutumia huduma za Maktaba,kuchapisha na kusambaza Nyaraka zinazohusu masuala ya haki za Binadamu na pia shughuli ya AfCHPR.

Alisema upo mpango wa miradi mipya ya Maktaba katika Mahakama hiyo ukiwemo ule wa msingi wa maarifa ya Kiafrica (AKB) utakaohusu takwimu msingi za machapisho kuhusu Afrika na utazileta pamoja Maktaba zote za nchi za Umoja wa Afrika ili kuziweka nyaraka mbalimbali za Afrika katika jukwaa moja na ziweze kupatikana kwa urahisi.

Wadau mbalimbali wamekuwa wakisaidia uimarishaji wa huduma za Maktaba hiyo iliyopo katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu na watu ambao ni Umoja wa Ulaya(EU),Shirika la misaada la Ujerumani(GIZ),Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,Taasisi ya Raone Walenberg na Maktaba za ndani ya nchi.

AHAMIAJI HARAMU 12 RAIA WA ETHIOPIA WAKAMATWA MOROGORO

$
0
0
Na Hussein Stambuli, Morogoro
Ofisi ya uhamiaji mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamewakamata wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia waliokuwa wamejificha katika pori la kijiji cha Lugono wilayani Mvomero wakitokea Tanga kuelekea mpaka wa Tunduma ili kwenda  nchini Afrika ya Kusini…

Akizungumza na waandishi wa habari afisa uhamiaji mkoa wa Morogoro kamishna msaidizi wa uhamiaji angela shija amesema kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu 12 kumetokana na taarifa za kiintelijensia walizozipata juni 24 mwaka huu, ambapo kati ya wahamiaji hao haramu 12 waliomamatwa,tisa walikuwa na pasi za kusafiria ingawa hazikuwa na vibali kwa kuwaruhusu kuingia nchini..

“mnamo tarehe 24/6/2019 tulipata taarifa ya kiintelijensia kuwa kuna wahamiaji haramu waliokuwa wanasafirishwa kutoka Tanga kwenda Afrika ya Kusini kupitia mpaka wa Tunduma ndipo tukaweka mtego wa kuwanasa wasafirishaji wa wahamiaji haramu hao” amesema kamishna angela shija..

Afisa huyo wa uhamiaji mkoa wa Morogoro amesema wamefanikiwa kumkata msafirishaji wahamiaji hao ambaye alishawahi kushikwa mwaka 2014 mkoani Morogoro akifanyabiashara hiyo na akiachiliwa baada ya kulipa faini huku akitoa wito kwa wananchi kuwa na uzalendo kwa nchi yao ikiwemo kwa kushiriki kuwafichua au kutoa taarifa za kufanikisha kukamatwa kwa wahamiaji haramu ambao huingia nchini kwa malengo tofauti na kuahidi msako mkali utaendelea kuwabaini sambamba na elimu kwa wananchi ili kusaidia kuwafichua.
 Afisa Uhamiaji mkoa wa Morogoro, Angela Shija akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la kukamatwa kwa wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia waliokuwa wamejificha katika pori la kijiji cha Lugono wilayani Mvomero.
Wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia waliokamatwa wakiwa wamejificha katika pori la kijiji cha Lugono wilayani Mvomero
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images