Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
KAMPUNI ya Candy & Candy imetoa msaada wa vyakula, vinywaji baridi
na fedha za kununulia nguo za ndani watoto yatima wanaolelewa kwenye
kituo cha Faraja cha jijini Arusha.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Joe Kariuki aliongoza wafanyakazi wa kampuni hiyo kugawa vitu hivyo pamoja na kuzungumza na watoto wa kituo hicho zaidi ya 200.
Akizungumza zaidi Kairuki amesema kampuni ya Candy & Candy itaendelea kuwa karibu na kituo hicho ambapo aliahidi kurudi kituoni hapo baada ya miezi miwili na endapo akiwakuta wamebadilika na kuwa na mwenendo mwema basi atawapatia zawadi ya luninga.
"Baba yenu (Faraja) ameniambia hapa kuna waliokuwa wamehukumiwa na
kufungwa, tunashukuru sasa mko kwenye hiki kituo mnalelewa vizuri basi
badilikeni tabia ili msirudi tena kule kwenye matatizo," amesema
Kariuki na kuongeza.
"Nitakuja hapa baada ya miezi miwili, baba yenu akiniambia
mmebadilika tabia, hampigi watoto wa majirani na mnafanya usafi wa
mwili (kuoga) nitawanunulia TV nitaifunga hapo (akionyesha
ukutani),".Walikabidhi kituoni hapo kilo 100 za mchele, unga wa mahindi gunia nne, mafuta ya kupikia ndoo mbili zenye lita 20 pamoja na juisi na biskuti ambazo waliwagawia watoto kituoni hapo.
Mkurugenzi huyo wa Candy& Candy ambaye kampuni hiyo ina matawi maeneo mbalimbali nchini huku makao makuu yake yakiwa nchini ,Uingereza alitoa fedha kwa ajili ya kusaidia masomo ya ziada ya mwanafunzi, Baraka Eli ambaye alidai kuwa endapo asingelipa kwa siku ya Jumatatu basi asingeruhusiwa kuingia darasani kujifunza.
Kariuki alilazimika kutoa fedha kwa ajili ya kuwanunulia nguo za ndani watoto wenye umri wa kati ya miaka tisa na 16 kwenye kituo hicho baada ya
kumweleza kuwa wengi wanayo moja huku wachache wakiwa na ambazo
hazizidi tano.Kwa upande wake Naye Rais wa programu ya U & I, (you and I) inayoendeshwa na Candy & Candy, Nasra Swai akiongea na watoto wenye umri wa kati ya miaka tisa na 17 aliwaleza umuhimu wa kujitambua kama watoto.
Aidha aliwaeleza watoto hao jamii inawapenda na kuwathamini ndiyo
sababu wamefika kwenye kituo hicho kuongea nao na kubadilishana
mawazo ambapo aliwaahidi kurudi tena kwenye kituo hicho kwa ajili ya
kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali ya makuzi.Akizungumza kwa niaba ya watoto kwa niaba ya wenzake mtoto, Barakaeli
Faraja amesema wanashukuru kampuni hiyo kuwasaidia kupata vitu
hivyo kwani wmekuwa wakivihitaji kwa muda mrefu.
Ameiomba kampuni hiyo iangalie uwezekano kuwasaidia zaidi kuwalipia
ada baadhi ya watoto, kupata vitanda kwani kwa sasa wanabanana mno,
kompyuta na runinga kwa ajili ya chumba cha watoto wakubwa.Wakati huo huo Mkurugenzi wa kituo hicho Faraja Mollel amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa chakula cha kutosha kwa ajili ya watoto hao ambapo wakati mwingine huwapa milo miwili tu kwa siku.
Amesema kuwa yeye aliguswa kuanzisha kituo hicho kutokana na historia
ya maisha yake ambapo yeye akiwa na umri mdogo aliwahi kuishi kwenye
mitaa ya jiji la Arusha akiwa na dd yake, Jenipher ambaye kwa sasa
anaishi Marekani.Amesema walipata msamaria mwema mama wa Kizungu aliyewachukua na kwenda kuishi nao ndipo maisha yao yalipobadilika, hivyo baada ya kufanikiwa akaguswa kuwasaidia watoto waliopitia magumu kama ya kwake.
Faraja amesema awali kwnye kituo hicho hapakuwa na shida ya ada
kwa watoto wa kituo hicho kwani kulikuwa na mfadhili aliyekuwa
akiwasaidia kununua chakula na kulipia ada baadhi ya watoto hao lakini
alifariki mwaka jana jambo linalowaweka katika wakati mgumu kwa sasa.
Mkurugenzi wa kituo cha faraja wa pili kushoto akitoa maelezo ya jinsi kituo hicho kinavyowahudumia watoto hao
Mkurugenzi wa kampuni ya Candy &Candy , Joe Kariuki akimkabidhi mkurugenzi wa kituo cha Faraja,Faraja Mollel baazi ya bidhaa waliopeleka katika kituo cha kulelea watoto yatima cha faraja