Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

PAMBA ZA KUTOA UCHAFU MASIKIONI ZATAJWA KUSABABISHA MATATIZO YA USIKIVU

$
0
0

aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akitazama mtoto Ahmed Said akiwekewa vifaa vya usikivu toka kwa Dkt. Tani Austin wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa wa Masuala ya Masikio na Usikivu leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifuatilia mtaalam akifunga vifaa vya usikivu kwa mtoto Monica Denis kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa Taifa wa Masuala ya Masikio na Usikivu Jijini Dodoma.

“Furaha ilioje kusikia tena” Picha ya pamoja Bibi Tausi Mbonde na wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa Masuala ya Masikio na Usikivu leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kutoka kushoto) akizindua rasmi Mpango Mkakati wa Masuala ya Masikio na Usikivu akiwa pamoja na Bwana na Bibi Bill Austin (waliovaa makoti meupe) kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation, kushoto ni Dkt. Grace Maghembe Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya na Daktari Bingwa wa Masikio na Usikivu Dkt Edwin Liyombo (wa pili kutoka kulia)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifafanua jambo kutoka kwenye kitabu cha Mpango Mkakati wa Masuala ya Masikio na Usikivu leo Jijini kabla ya kuzindua mpango huo
Dkt. Bill Austin (kulia) kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Masuala ya Masikio na Usikivu leo Jijini Dodoma aliye kushoto ni mke wake Dkt. Tani Austin.
…………………

NA WAJMW-DODOMA
Imeelezwa kuwa vijiti na pamba za kusafisha masikio zinasababisha kwa kiasi kikubwa magonjwa ya usikivu yanayopelekea kuwa kiziwi.
Hayo yamebainika leo wakati wataalamu wa afya ya masikio na usikivu kutoka taasisi ya Starkey Foundation for Ear and Healing Care walipomweleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea mabanda ya utoaji wa huduma za masikio na usikivu kwa wananchi mbalimbali jijini Dodoma.
Kufuatia hatua hiyo, Waziri Ummy amewataka wananchi kulinda masikio yao kwa kufuata ushauri wa madaktari na kuacha tabia ya kutumia vifaa vinavyosababisha matatizo ya usikivu kama spika za masikioni na matumizi ya pamba za kutolea uchafu.

“Tatizo la usikivu ni kubwa katika nchi yetu, katika tafiti ndogo ndogo ambazo zimefanyika zinaonesha asilimia 3 ya wanafunzi ambao wako shuleni wana matatizo ya usikivu kwa kiwango fulani lakini pia takwimu zinaonesha kuwa kila watu 100 wenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza, 24 kati yao wanakua na matatizo ya usikivu”. Amesema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri ummy amesema tafiti zinaonesha pia waathirika wengine wenye matatizo ya usikivu ni wale wanaofanya kazi katika migodi na viwandani hasa viwanda vya nguo ambapo takwimu zinaonyesha asilimia 50 wanakua na matatizo hayo.

Waziri Ummy ameishukuru taasisi ya Starkey Foundation for Ear and Healing Care kwa kutoa huduma za masikio na usikivu nchini huku akisema Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha miundombinu, kununua vifaa na kuongeza wataalamu wa huduma za masikio na usikivu, kutoka wataalamu bingwa 11 mwaka 2009 mpaka kufikia wataalamu 46 mwaka 2018.

Hata hivyo Waziri Ummy amesema toka kuanzishwa kwa huduma hizi nchini kumesaidia kuokoa kupunguza idadi ya watoto kupelekwa India, ambapo kila mwaka takribani watoto 13 walikua wanapelekwa India kupata matibabu na mtoto mmoja alikua anagharimu Tsh. Milioni 80 mpaka Milioni 100. Lakini kuanzishwa kwa huduma hizi katika Hospitali ya Muhimbili mwaka 2017, watoto takribani 26 wamepata huduma kwa gharama ya Tsh. Milioni 35 na kuokoa fedha za Serikali kwa zaidi ya asilimia 60.


Kwa upande wake muanzilishi wa taasisi ya Starkey Foundation for Ear and Healing Care Dkt. Bill Austin ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo kuendelea kutoa huduma na vifaa vya masikio na usikivu kwa wananchi ambapo ilianza kutoa huduma hizo Jijini Mwanza na kuendelea kutoa huduma Jijini Dodoma.

MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA KHERI JAMES AZINDUA KAMPENI YA 'SHINYANGA YA KIJANI'

$
0
0


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James amezindua rasmi Kampeni ya ‘Shinyanga ya Kijani’,mkakati unaolenga kuwaandaa vijana wa CCM kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nchini utakaofanyika mwishoni mwaka 2019. 

Kampeni hiyo kabambe imezinduliwa leo Jumatano,Juni 19,2019 katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga. 

Akizindua Kampeni hiyo,Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James amesema Operesheni ya Kimkakati inayojulikana kwa jina la Mkakati wa kijani kwa upande wa mkoa wa Shinyanga itakuwa ni ‘Shinyanga ya Kijani. 

“Huu ni mkakati wa kuwaandaa vijana wanachama wa CCM kote nchini kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nchini,kwa hiyo vijana wote wanaandaliwa kwa maana ya kuwaarifu kwamba mwaka huu uchaguzi utakuwepo”,alisema. 

Alieleza kuwa mkakati huo unalenga kuwataarifu kuwa vijana wanalo jukumu la kujiandikisha katika madaftari ya wapiga kura kwenye maeneo yao na kujitokeza kugombea na kuwapigia kura wale watakaogombea pamoja na kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki na sheria za uchaguzi zinazingatiwa ili uchaguzi wetu uwe ni wa amani. 

“Leo nimepata heshima ya kuzindua mkakati huu katika mkoa wa Shinyanga, imani yangu ni kwamba vijana leo tunawatangazieni kwamba uchaguzi mwaka huu upo,lakini nyinyi kama wananchi wengine mnayo fursa ya kugombea sawa na wengine,ili mpate haki hiyo lazima mjiandikishe ili mpate uhalali wa kuwa wananchi wakazi kwenye maeneo utakapofanyika uchaguzi”,alifafanua. 

“Vijana mnalo jukumu la kushirikiana na chama chetu kuhakikisha wagombea wa chama chetu wanashinda uchaguzi wa serikali za mitaa,hiyo ni kazi ambayo tumekuja kuambizana leo na kuizindua rasmi katika mkoa wetu wa Shinyanga”,aliongeza James. 

Aidha aliwataka vijana walioaminiwa na kupewa nafasi za uongozi watambue kuwa kuwa wameaminiwa kwa maslahi ya umma hivyo watumike kwa maslahi ya umma huku akiwataka vijana wanaopewa madaraka na kujifanya siagi na kuyeyuka zama zao zinahesabika akidai hakuna cheo kinachodumu. 

“Tunahitaji kuwa wamoja,kushikana na kufanya kazi,MwanaCCM popote alipo ana jukumu la kuendelea kukijenga chama,kuwatumikia watanzania wenzetu kwa hali na mali ili mwisho wa siku ustawi wa Watanzania na taifa kwa ujumla viweze kupatikana na niwakumbushe tu kazi ya kuimarisha chama inaendelea kote nchini”,alisema. 

Katika hatua nyingine alisema jukumu la vijana wa UVCCM ni kuwalinda viongozi wa CCM na kulinda chama dhidi ya maadui nje na wa ndani ya chama /wasaliti ndani ya chama kwa sababu siyo watu wote wanaoitwa viongozi wa CCM wanania njema na CCM wengine ni vibaraka wanaotumika kuidhoofisha CCM. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack alieleza kuwa vijana wa CCM mkoani humo wapo imara na kwamba watahakikisha kuwa CCM inapata ushindi kila eneo na kwamba serikali itahakikisha kuwa Demokrasia inazingatiwa ili uchaguzi uwe huru na wa haki. 

Naye Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Mhe. Stephen Masele ambaye pia ni Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP),alisihi vijana kuwa na nidhamu na wavumilivu na kuwataka wanaCCM kupendana na kushirikiana huku akisisitiza kuwa CCM itashinda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu. 

“Mwaka huu tutatimiza miaka 20 tangu baba wa taifa,Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere afariki dunia,nataka niwaombe Jumuiya ya Vijana tujiandae kikamilifu kufikia mwezi Oktoba,na mimi nitatoa ushirikiano wote tushangilie maisha aliyoishi Baba wa taifa,yapo mambo matatu aliyapigania ambayo ni umaskini,maradhi na ujinga hao maadui bado tunao,naomba tuendelee kupigana na maadui hawa”,alisema Masele. 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James akivishwa skafu alipowasili katika Ofisi ya CCM mkoa wa Shinyanga kabla ya kuelekea katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani leo Juni 19,2019 . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James akipokelewa na vijana wa CCM alipowasili katika Ofisi ya CCM mkoa wa Shinyanga kabla ya kuelekea katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James (katikati) akiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa kuelekea katika Ofisi ya CCM mkoa wa Shinyanga kabla ya kuelekea katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye pia Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP). 


Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akizungumza katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga wakati akizindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani. 
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akizungumza katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga wakati akizindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani. 

Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani. 
Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye pia Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP) akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa (katikati) na Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James wakati akizindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani. 
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Mhe. Stephen Masele ambaye pia ni Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani. 
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akiimba pamoja na Msanii Beka Boy (kulia) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Shinyanga ya Kijani. 
Wanachama wa CCM wakicheza na kupiga picha wakati wasanii Papii Kocha na Beka Boy wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Shinyanga ya Kijani. 
Wasanii Papii Kocha na Beka Boy wakitoa burudani. 
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akiimba wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Shinyanga ya Kijani. 

Diwani kutoka Nzega,ambaye pia ni Msanii wa nyimbo za Asili,Madebe Jinasa (katikati) akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya Kijani. 
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Jafo Aonya Halmashauri Ambazo Hazijashiriki Mafunzo ya Kuandaa Maandiko ya Miradi ya Kimkakati

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akifungua semina ya kuandaa maandiko ya miradi ya kimkakati Washiriki wakimskiliza Waziri Jafo wakati wa ufunguzi semina ya kuandaa maandiko ya miradi ya kimkakati Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa Angelista Kihaga atoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa semina ya kuandaa maandiko ya miradi ya kimakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina hiyo. 
………………… 
Nteghenjwa Hosseah,OR-TAMISEMI 
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameionya mikoa ya Dodoma,Lindi na Njombe iliyoshindwa kupeleka watendaji wake kuhuduhuria semina ya kuandika miradi ya kimkakati. 

Onyo hilo juzi jijini hapa wakati akifungua semina ya siku mbili iliyoshirikisha mamlaka za serikali za mitaa zilizopo Tanzania Bara na sekretarieti za mikoa semina iliyofanyika katika Chuo cha serikali za mitaa Hombolo. 

Jafo alisema semina hiyo ni muhimu sana kwao kwa ajili ya kuwajengea uwezo utakaowawezesha kuibua miradi mbalimbali lakini ameshangaa mikoa hiyo kutopeleka watendaji wake. “Hapa hatuna wawakilishi wa mkoa wa Dodoma,Njombe na Lindi wakati Dodoma mradi mkakati walioupata ni Kondoa peke yake,hakuna Bahi,Chamwino wala Jiji,Njombe nao hakuna mradi mkakati walioupata cha kushangaza kwenye semina hii hawapo,”alisema. 

Alieleza Lindi wana mradi mkakati katika halmashauri ya Liwale na Ruangwa lakini bado hawajahudhuria semina hiyo na Mtwara halmashauri wana mradi katika halmashauri moja lakini anyumbu,Masasi,Newala,Tandahimba na Nanyamba hakuna mradi wowote walioupata lakini pia hawajahudhuria. 

“Hii Nanyamba ni halmashauri ya mwisho katika ukusanyaji wa mapato nawaagiza wahakikishe awamu ya pili ya semina hiyo wanakuwepo,”alisema. Jafo alisema mpaka sasa kiasi cha Sh.Bilioni 268.37 zimeshatolewa na serikali kwa ajili ya kugharamia miradi 38 na hapo kuna halmashauri hazijaguswa na miradi hiyo kutokana na maandiko yao kutokuwa na sifa za kuweza kupata fedha na hali yao ya uchumi bado ipo mbaya sana. 

“Leo hii unapoona halmashauri zimepewa nafasi hiyo lakini still zimelala kuanzia wilayani hadi mkoani hapo kuna matatizo,”alisema Waziri Jafo. 
Alibainisha kuwa ni lazima kubadili mbinu za ukusanyaji wa mapato kwa kuwa serikali lengo lake kubwa ni kuhakikisha inaondoa mzigo kwa watu wanyonge na ili hizo kodi na tozo zenye kero ziweze kuondoka ni lazima halmashauri iweze kupata mapato kwa njia nyingine mbadala. 

“Jiji la Dodoma hawapo hapa,sijui kiburi cha kukusanya mapato mengi ndio maana hawataki kuja hapa na fedha hizo ujue ni fedha za kwetu tumeandikia miradi sisi ya TSP wala hawajaandika ya kwao,nilitamani waje hapa wajifunze, leo hii Dodoma mpaka mwezi huu wameshakusanya Sh.Bilioni 60 wangekuja hapa wangepata maarifa mengine zaidi,”alisema. 

Alizitaka halmashauri kutekeleza miradi inayopelekwa kwao bila ya kusua sua kwa kuingiza maslahi yao hasa katika ajenda ya manunuzi ambapo kila mtu anaenda na makaratasi yake ikiwa na mkadarasi wake hali inayofanya miradi hiyo kutoendelea mbele . 

Awali, Mkurugenzi Msaidizi Idara za Serikali za Mitaa, Angelista Kihaga alisema miradi ya kimkakati ni utaratibu mpya wa serikali wa kutoa fedha za maendeleo kwa mamlaka za serikali za mitaa. Naye, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Hombolo Dk. Michael Msendekwa alisema mafunzo hayo yametokana na tafiti zilizofanywa na chuo hicho kuonyesha kuna changamoto katika maandishi ya miradi katika mamlaka za serikali za mitaa. 

Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa ushirikiano baina ya TAMISEMI na Wizara ya Fedha lengo likiwa ni kuelekezana na kusaidiana kutatua changamoto hiyo.

DC TANGA AWATAKA MADIWANI,WENYEVITI WA MITAA KUPIGA VITA BIASHARA ZA MAGENDO

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati akifungua semina ya wenyeviti wa Mitaa na Madiwani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Tanga .
KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim akizungumza wakati wa semina hiyo 
Mwakilishi wa Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Lucas Kaigarura ambaye ni Meneja Msaidizi Upande wa Madeni TRA Tanga 
Meneja Msaidizi Idara ya Forodha Edward Ndupa akizungumza katika semina hiyo 
Ofisa wa Elimu kwa Mlipakodi Mkoa wa Tanga Salim Bakari akizungumza wakati wa semina hiyo 
MKUU wa Kitengo cha Kodi za Majengo TRA Mkoa wa Tanga John Minja akieleza umuhimu wa ulipwaji wa kodi hizo wakati wa semina hiyo 
NAIBU Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu akizungumzaa 
Mwenyeviti wa Serikali Mitaa kwenye Jiji la Tanga Maimuna Ramadhani kutoka Mtaa wa Mabawa Mikanjuni A akiuliza swali wakati wa semina hiyo
Diwani wa Kata ya Majengo (CUF) 
Diwani wa Kata ya Msambweni Jijini Tanga (CUF) Abdurahamani Hassani katikati akiwa na madiwani wengine kwenye semina hiyo
Sehemu ya Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wakifuatilia semina hiyo

MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka wenyeviti wa mitaa na madiwani kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kupiga vita biashara za magendo ikiwemo kuwafichua wanaohusika kwenye maeneo yao kwani vinawatia doa. 

Mwilapwa aliyasema hayo leo wakati akizungumza na madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa katika semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Tanga. 

Alisema kwamba wilaya ya Tanga kuna tatizo kubwa hata wakati fulani Rais Dkt John Magufuli alikwisha kutaja kwani miongoni mwa wilaya zenye vipenyo vingi vya uingizaji bidhaa bila kufuata utaratibu kupitia Bandari rasmi. 

Mkuu huyo wa wilaya ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kwenye semina hiyo alisema kwamba hivi sasa wamejipanga imara kuweza kuhakikisha mianya yote haipitisha bidhaa kwa njia zisizo rasmi kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali. 

Aidha pia aliwataka viongozi hao kushirikiana na watu mbalimbali ikiwemo kuhakikisha biashara na shughuli zinazoendeshwa ndani ya wilaya zinakwenda kwa utaratibu unaokubalika. “Lakini suala la biashara ya magendo tumekuwa tukiipigia kelele kila wakati tumekuwa na tabia ya kuingiza bidhaa kwa njia za panya tabia hii inatukera tumekuwa tukipambana nalo na tunaamini litakwisha kabisa”Alisema 

Mkuu huyo wa wilaya alisema anaamini semina hiyo itawapa uelewa mkubwa ambao utakuwa chachu kwenye maeneo yao kwa sababu ni wanasiasa wana ushawishi kwa jamii watumie njia mbalimbali kuweza kuwapa elimu jamii itasaidia kupunguza na hatimaye kumaliza magendo. 

“Lakini pia wataalamu na wanasiasa tukishikamana kwa pamoja tunaweza kumaliza tatizo la magendo huku akiwataka viongozi wenye tabia za namna hiyo kuachana nazo kwani wakikamatwa wataishi kwenye mikono ya kisheria”Alisema 

Awali akizungumza katika semina hiyo Mwakilishi wa Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Lucas Kaigarura ambaye ni Meneja Msaidizi Upande wa Madeni TRA Tanga alisema wameitisha kikao hicho cha madiwani na wenyeviti ili kuwaelimisha masuala mbalimbali kuhusu kodi kwani wao ni nguzo kuu ya wananchi ili waweze kuipeleka elimu hiyo. 

Alisema pia semina hiyo imelenga kwenye umuhimu wa kodi,Masuala ya EFD Mashine ,kutoa na kudai risiti,Elimu ya umuhimu wa kulipa kodi mbalimbali ikiwemo ada za mabango kwa sababu wapo karibu na wananchi wakifikisha huko inaweza kuwa chachu ya kuongeza mapato. Hata hivyo alisema suala la magendo sio mazuri kwa sababu yanaikoseka mapato serikali hivyo wanaimani watafanikiwa kuliondosha. 

Naye kwa upande wake Diwani wa Kata ya Msambweni (CUF) Abdurhamani Hassani alisema baada ya elimu hiyo wamejifunza mambo mengi hasa suala la magendo jambo ambalo linaathiri ukusanyaji wa mapato. 

Alisema yapo magendo yanafanyika kutokana na kuwepo kwa uelewa mdogo kwa wale wafanyabiashara kwa sababu ukitazama viwango cha kodi vinalipika watajiahidi kwenye kueilimisha jamii kwa sababu kodi sio jambo la hiari bali ni lazima. 

JIJI LA MBEYA KUSAIDIA WANAWAKE WAFANYABIASHARA MASOKONI

$
0
0
Ofisa wa EfG, Eva akizungumza na wafanyabiasha wa Soko Matola
Meya wa Jiji la Mbeya Mchungaji David Mwashitindi (katikati),akiwa pamoja na wanawake wafanyabiashara masokoni kutoka Dar es Salaam jana, ambao wapo jijini humo kwa ziara ya mafunzo na kuwahamasisha wanawake wenzao kujiunga na Umoja wa wanawake Sokoni wa Kitaifa.Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG).
Mwanasheria wa EfG, akizungumza na wafanyabiasha wa Soko Matola
Ofisa Ufuatilia na Tathmini wa EfG, Samora Julius akizungumza na wafanyabiasha wa Soko Matola
Mwenyekiti wa Soko la Uhindini, Joseph Mwakitalima akizungumza
Picha ya pamoja Soko la Uhindini
Mwenyekiti wa Bodi EfG,akisoma taarifa mbele ya Meya wa Jiji la Mbeya
Meya wa Jiji la Mbeya Mchungaji David Mwashitindi (katikati),akizungumza na wanawake wafanyabiashara masokoni kutoka Dar es Salaam jana, ambao wapo jijini humo kwa ziara ya mafunzo na kuwahamasisha wanawake wenzao kujiunga na Umoja wa wanawake Sokoni wa Kitaifa.Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya, Beatha Mtani,akizungumza na wanawake wafanyabiashara masokoni kutoka Dar es Salaam juzi, ambao wapo jijini humo kwa ziara ya mafunzo na kuwahamasisha wanawake wenzao kujiunga na Umoja wa wanawake Sokoni wa Kitaifa.Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)



Na Dotto Mwaibale, Mbeya

Meya wa Jiji la Mbeya Mchungaji David Mwashitindi amesema wataongeza nguvu ya kuvisaidia vikundi vya wanawake pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali.

Hayo aliyasema jijini humo jana wakati akizungumza na wanawake wafanyabiashara masokoni walioandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoka Dar es Salaam ambao wapo jijini humo kwa ziara ya mafunzo na kuwahamasisha kujiunga na Umoja wa wanawake Sokoni wa Kitaifa."Sisi kama jiji tutahakikisha tunaendelea kuwasaidia wanawake wajasiriamali kwa kuwapa mafunzo na mitaji ili kuinua maendeleo yao na Taifa kwa ujumla" alisema Mwashitindi.

Mwashitindi aliwaomba wanawake hao kuwa kwenye vikundi ili iwe rahisi kujulikana na kupata misaada badala ya kuwa mmoja mmoja.Aliongeza kuwa wakati wote atakuwa ana watuma maofisa maendeleo ya jamii kutembelea vikundi vya wanawake ili kujua changamoto zao na kuzitatua.

Afisa Maendeleo ya Jamii Beatha Mtani aliwaomba wanawake hao kujiunga pamoja na kuendelea kuitunza amani iliyopo nchini.Alisema mahali popote palipo na amani ndipo shughuli za maendeleo zinafanyika hivyo aliwaomba wanawake hao waendelee kuilinda.Mtani alimpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kumkomboa mwananchi wa kawaida ili awe na maisha bora badala ya kuwa na bora maisha.

Ruvuma, Songwe Zatinga Fainali UMISSETA 2019

$
0
0
Patashika katika mchezo wa mpira wa kikapu wasichana baina ya timu ya mkoa wa dar es salaam dhidi ya timu ya mkoa wa Morogoro ambapo Dar es salaam waliilaza Morogoro kwa 38-17
Mabingwa UMISSETA mwaka 2017 timu ya soka wavulana ya mkoa wa Songwe wakifuraia ushindi baada ya kuifunga kwa penati timu ya mkoa wa Mwanza
Golikipa wa Songwe Joseph shibanda akipangua shuti kali la penati lililopigwa na Felician Lucas wa Mwanza na kuipa ushindi timu yake ya Songwe kwa jumla ya magoli 4-3
…………………
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Timu za mpira wa miguu za wavulana kutoka mikoa ya Ruvuma na Songwe ndizo zitakazocheza hatua ya fainali kumtafuta bingwa wa UMISSETA mwaka huu, mchezo unaotarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Nangwanda ijumaa tarehe 21 juni 2019.

Ruvuma ndiyo walikuwa wa kwanza kufuzu hatua hiyo baada ya kuifunga Lindi kwa magoli 2-0. Magoli ya Ruvuma yakifungwa na Said Bakari dakika ya 29 na John Ching’uku alifunga goli la pili dakika ya 59.

Katika mchezo baina ya Mwanza na songwe ulilazimika kuamuliwa kwa mikwaju ya penati baada timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana katika dakika 90 za mchezo na hatimaye Songwe kushinda kwa penati 4-3.
Shujaa wa mchezo huo alikuwa ni golikipa wa Songwe Joseph Shibanda ambaye ndiye aliyewanyamazisha mashabiki wa Mwanza baada ya kudaka shuti kali la Felician Lucas wa Mwanza.

Penati nyingine kwa upande wa Songwe zilifungwa na Pascal Adriano, Joseph Shibanda, Michael kabuki pamoja na Justine Mwambungu huku penati ya Sekelo Kalinga ‘’kichuya mtoto’’ ikipanguliwa na golikipa wa mwanza.

Waliofanikiwa kufunga magoli kwa upande wa timu ya Mwanza ni Nassoro Omary, Frank Faustino na Boniface Ernest huku waliokosa kwa upande wa Mwanza ni Mashinyali Maira, na Felician Lucas.

Kocha wa Songwe, Mwalimu PrayGod Lugenge amesema kuwa amefurahia timu yake kuingia fainali kwani walijiandaa kwa muda mrefu baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu.

Alisema kuwa hashangazwi na timu yake kufika hatua hiyo kwani mwaka 2017 wakati wanashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza walifanikiwa kushinda mechi zao na hatimaye walitwaa kombe hilo ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano hayo.

Lugenge alisema kuwa timu yake pamoja na kucheza vizuri kwenye mchezo huo ndani ya dakika 90 walilazimika kusubiri mchezo huo uamuliwe kwa penati baada ya timu yake kufanya mashambuzi mengi dhidi ya Mwanza.
Mwalimu huyo kutoka shule ya sekondari J.K Nyerere iliyopo Tunduma aliwataka wadau wa soka nchini hususan TFF kutafuta vipaji katika maeneo mengi nchini badala ya kung’ang’ania wachezaji wa Dar es salaam peke yake.

Amesema timu ya Songwe ina fursa ya kufanya vizuri kwani wachezaji wake wengi wanaundwa na timu nne za mkoa huo na hivyo wachezaji wake wengi wanafahamiana kwani wamecheza muda mrefu.Aidha Kocha huyo wa Songwe ameisifu kamati ya kuratibu mashindano ya UMISSETA na TAMISEMI kwa namna ilivyokuwa makini kuhakikisha kuwa mashindano ya mwaka huu hayatawaliwi na mamluki.

Amesema mfumo wa kielektroniki uliotumiwa mwaka huu umerejesha msisimko uliokuwepo miaka ya nyuma ambapo wachezaji wanaoshiriki mashindano hayo ni wale wanaosoma katika shule za sekondari nchini.
Kwa upande wake nahodha wa Songwe Joseph Shibanda naye ameipongeza serikali kwa usimamizi thabiti wa michezo hiyo ambapo amesema kuwa kutokana na namna usimamizi ulivyokuwa mzuri utawezesha kupatikana kwa bingwa wa kweli na pia kuwezesha mikoa mingine kama Simiyu, Geita na Njombe kuwa na nafasi ya kushinda kombe hilo.

Wakati huo huo matokeo ya mpira wa kikapu yanaonyesha kuwa timu za kutoka mikoa ya Pwani na Shinyanga zitacheza hatua ya fainali kwa upande wa wavulana na timu za Mwanza na Dar es salaam zitakutana katika hatua hiyo kwa upande wa wasichana.Katika matokeo ya nusu fainali kwa kikapu wavulana Pwani iliwafunga Unguja kwa 66-32 na Tanga ilifungwa na Shinyanga kwa 47-55.

Kwa upande wa kikapu wasichana Mwanza iliwafunga Kilimanjaro 38-18 na Dar es salaam iliwafunga Morogoro kwa 38-17.

Pwani, Simiyu na Singida Zaongoza kuzoa Medali Nyingi UMISSETA 2019

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akifurahia jambo wakati akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Shule za Sekondari kwa Ukanda wa Afrika Mashariki (FEASA) bwana Kariuki Gikonyo mara baada ya Mkuu wa mkoa kugawa medali za dhahabu kwa washiriki wanne wa riadha maalum leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara. 
Washindi wa kwanza hadi wa tatu kutoka mikoa ya Pwani, Unguja na Njombe wakisubiri kupewa medali zao za dhahabu, fedha na shaba leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara 
Mjumbe wa kamati ya usimamizi UMISSETA taifa kutoka Wizara ya Elimu Salum Salum (mwenye tracksuit ya kijani) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa riadha maalum na makocha wao mara baada ya kuwakabidhi medali zao 
……………… 

Na Mathew Kwembe, Mtwara 
Mikoa ya Pwani, Simiyu, na Singida ndiyo inayoonekana kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya UMISSETA yanayotarajiwa kukamilika tarehe 21 juni 2019. 

Mkoa wa Pwani umepata medali 7 za dhahabu, 1 ya fedha na 2 za shaba, na hivyo kujipatia jumla ya medali 10 kwenye mashindano hayo. 
Simiyu imepata medali 2 za dhahabu, 5 za fedha na 2 za shaba jumla ina medali 9 

Mkoa wa Singida nao haukuwa nyuma katika kupata medali ambapo walipata medali 3 za dhahabu, 5 za fedha na 3 za shaba, hivyo jumla wamepata medali 11. 

Mkoa wa Mwanza nao haukuwa nyuma katika kupata medali ambapo walifanikiwa kupata medali 3 za dhahabu, huku jirani zao shinyanga wakipa media 1 ya dhahabu, 1 ya fedha na 2 za shaba. 

Mkoa wa Geita nao ulipata media 1 ya dhahabu, wakati Tabora wao walipata media 1 ya dhahabu, 3 za fedha na 1 ya shaba, na Manyara wamepata medali 2 za fedha na 5 za shaba, huku wenzao wa Arusha wamepata medali 2 za dhahabu 1 ya fedha. 

Mkoa wa Unguja nao haukuwa nyuma katika ushindi wa medali mwaka huu ambapo walijinyakulia medali 3 za dhahabu, 1 ya fedha na 1 ya shaba. 
Mikoa mingine ambayo haikutoka kapa ni pamoja na Dar es salaam ambao wamepata medali 3 za dhahabu, 1 ya fedha na 1 ya shaba, mkosa wa Lindi nao ulipata medali moja ya fedha huku mikoa mingine 11 ikiambulia patupu. 

Mikoa iliyokosa kabisa medali katika mashindano ya riadha mwaka huu ni pamoja na Katavi, Ruvuma, Tanga, Pemba, Mtwara, Njombe, na Rukwa. 
Mikoa mingine ni pamoja na Iringa, Kagera Songwe na Morogoro.

NBS Yaadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa Kuwajengea Uelewa Wanafunzi Dodoma Sekondari

$
0
0
Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Dodoma wakiangalia vitabu walipotembelea Maktaba ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kuwajengea uelewa wa masuala ya Takwimu yaliyoandaliwa na NBS ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija).
Kaimu Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Stambuli Mapunda akizungumza na Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma. Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bibi. Mariam Katemba akiwasilisha mada kuhusu matokeo ya hali ya maambukizi ya Ukimwi kwa vijana mbele ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma. 
Mtakwimu Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Seif Kuchengo akiwasilisha mada kuhusu Sensa mbele ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma. Mwanafunzi wa Kidato cha Nne, Shule ya Sekondari Dodoma, Bi. Najma Mussa akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kuwajengea uelewa wa masuala ya Takwimu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma. Mwanafunzi wa Kidato cha Nne, Shule ya Sekondari Dodoma, Hassan Hamis Hassan akiuliza swali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa wa masuala ya Takwimu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma. Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Dodoma wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya Takwimu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Dodoma wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya Takwimu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. 

SERIKALI KUWEKA BAYANA MAJINA YA WAKANDARASI WABABAISHAJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akiongea kwa simu na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nangai Engineering Ltd alipokuwa akikagua Mradi wa Maji wa Itigi, uliopo katika Halmashauri ya Itigi, wilayani Manyoni, mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akimsikiliza Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Itigi, Evaristo Mgaya kwenye moja ya vituo vya maji vinavyojengwa wakati akikagua Mradi wa Maji wa Itigi, uliopo katika Halmashauri ya Itigi, wilayani Manyoni, mkoani Singida. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Itigi, Rahabu Mwangisa.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akiwa kwenye kisima cha maji kilichopo eneo la Kanisani, moja ya visima 5 vya Mradi wa Maji wa Itigi, uliopo katika Halmashauri ya Itigi, wilayani Manyoni, mkoani Singida.
………………
Serikali imesema itaweka bayana majina ya makandarasi wote wanaoharibu miradi ya maji kwa kuitekeleza chini ya kiwango na kuwachukulia hatua kali za kisheria katika hatua ya kumaliza tatizo la utendaji mbovu kwenye kazi za miradi ya maji linalochangia wananchi kukosa huduma ya maji.

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametoa kauli hiyo mara baada ya kutoridhishwa na Mkandarasi wa Kampuni ya Nangai Engineering Ltd kufanya kazi kwa asilimia 30 ukilinganisha na kiasi cha Shilingi milioni 250 alizolipwa, wakati mkandarasi wa Kampuni ya Nipo Africa Ltd akiwa amefanya kazi kwa asilimia 68 huku akidai fedha za malipo za ujenzi wa Mradi wa Maji wa Itigi uliopo katika Halmashauri ya Itigi, Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida alipokuwa akikagua mradi huo.

‘‘Wakandarasi wababaishaji wa namna hii wote tutawaanika hadharani na watachukuliwa hatua kali za kisheria na Bodi ya Wakandarasi (CRB), Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) utakapoanza Julai Mosi, 2019 utakuwa ni mwisho wa wakandarasi wababaishaji kupata kazi za miradi ya maji ’’, amesema Aweso.

‘‘Serikali imelenga kufikisha huduma ya maji kwa wananchi, hatutakubali mkandarasi au mtu yeyote kukwamisha juhudi zetu za dhati za kumaliza tatizo la maji. Kuanzia sasa tutaorodhesa wakandarasi wote wasio na sifa na kuwafungia wasipewe kazi miradi yoyote ya maji nchini, ameelekeza Naibu Waziri.

Aidha, Aweso ameipongeza Kampuni ya Nipo Africa Ltd kwa kufanya kazi nzuri, akiahidi kuyafanyia kazi madeni yao na kuwalipa haraka. Pia, amewataka Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni za Nangai Engineering Ltd na Nipo Africa Ltd kukutana nae siku ya Alhamisi Julai 20, 2019 kwenye kikao kitakaochuhusisha viongozi na wataalam wa Sekta ya Maji mkoani Singida kitakacholenga kukwamua mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.

Wakati huo, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwangisa amemshukuru Naibu Waziri kwa ahadi yake ya kumlipa mkandarasi huyo na kumuahidi kuwa viongozi wa Wilaya ya Manyoni watasimamia mradi huo kwa ukaribu uweze kukamilika haraka.

Ujenzi wa Mradi wa Maji Itigi umeanza kutekelezwa mnamo 3/12/2018 na unategemewa kukamilika 2/9/2019 kwa zaidi ya Shilingi bilioni 2.6 ukihusisha uchimbaji wa visima 5 virefu vyenye uwezo wa kutoa jumla lita za ujazo 112,000 kwa saa, pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji.

Mradi huu utakapokamilika unatarajiwa kuhudumia vijiji 6 vya Songambele, Mlowa, Majengo, Tambukareli, Zinginali na Itigi unahusisha Mradi wa Maji wa Itigi utakaogharimu zaidi ya Shilingi bilioni 2.6.



UKAGUZI WA KINGA, TAHADHARI YA MOTO UFANYIKE SHULE ZA BWENI KUEPUSHA MAJANGA: KAMISHNA JENERALI ANDENGENYE

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye akiweka kizimia moto katika moja ya vyumba vya madarasa katika shule inayotarajiwa kuwa shule ya wanafunzi wenye vipaji vya michezo Simiyu Sekondari, wakati wa ziara yake Mjini Bariadi Mkoani Simiyu, Juni 19, 2019. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akimtambulisha Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi kabla ya kuzungumza nao juu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Juni 19, 2019. 
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiwasha moto kwa ajili ya kuwaonesha wananchi namna ya kuzima moto pindi moto unapotokea, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Juni 19, 2019. 
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kuhusu tahadhari na kinga dhidi ya majanga ya moto,wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimuongoza Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye kukagua moja ya mabweni yanayojengwa katika Shule ya Sekondari ya Simiyu, wakati alipotembelea shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kuhusu tahadhari na kinga dhidi ya majanga ya moto,wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimuongoza Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye kukagua moja ya mabweni yanayojengwa katika Shule ya Sekondari ya Simiyu, wakati alipotembelea shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kuhusu tahadhari na kinga dhidi ya majanga ya moto,wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019. 
Askari wa jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu, akimuelekeza mmoja wa wanafunzi namna ya kuzima moto wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye katika shule ya Sekondari Simiyu, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019. 
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake Mkoani hapa Juni 19, 2019. 
………………… 
Na Stella Kalinga, Simiyu 
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kuendelea kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto kwa shule zote za sekondari za mabweni nchini kujiridhisha ikiwa vigezo vimezingatiwa, kwa lengo la kuepusha majanga ya moto yanayogharimu maisha ya watu na mali. 

Andengenye ametoa maagizo hayo Juni 19, 2019 Mkoani Simiyu wakati akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi katika shule ya sekondari Simiyu, katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi. 

Akizungumza na wanafunzi Kamishina Jenerali Thobias Andengenye amesema kumekuwa na matukio ya moto katika shule kadhaa za bweni ambayo yameleta athari mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo kwa wanafunzi, kuteketea kwa mali, hivyo jeshi la zimamoto na uokoaji linaendelea kuweka mikakati ya kukabiliana na majanga hayo. 

Amesema mikakati hiyo ni pamoja na kusogeza huduma za zimamoto karibu na wananchi kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya moto katika majengo, kusoma ramani za majengo na kuanzisha klabu za zimamoto katika shule, ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujua vitu vya kufanya na vya kuepuka na uwezo wa kukabili moto katika hatua za awali na kuuzima. 
Katika hatua nyingine Andengenye amewataka wamiliki wa shule kuzingatia ushauri wa kitaalam unaotolewa na wataalam wakati wa ukaguzi juu ya namna ya kufanya mabweni , madarasa na ofisi ziwe salama kwa kuwasilisha michoro ya majengo hayo katika Ofisi za Zimamoto ili ushauri wa kitaalam uweze kutolewa. 

“Niwaombe wanaomiliki shule wazingatie ushauri wa kitaalam unaotolewa, wazingatie ujenzi unaofuata ushauri wa kitaalaam kwa kuwasilisha michoro kama wanataka kujenga mabweni, kuongeza madarasa au kuongeza vyumba vya ofisi basi wazingatie ushauri ili majengo yanayojengwa yawe salama zaidi” alisema. 

Aidha, amewaasa wananchi kuacha kuweka mitungi ya gesi ndani na kutikisa mitungi ya gesi kama njia ya kufahamu kiasi cha gesi kilichopo; kwa kuwa kunaweza kusababisha moto na kushauri kuwa njia sahihi ya kupima kiasi cha gesi katika mtungi ni kuweka mtungi katika maji, ambapo baada ya kuutoa sehemu isiyo na gesi itaonekana kuwa kavu. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kumekuwa na mwamko mkubwa wa watu kutumia gesi, hivyo ameshauri Jeshi la Zimamoto na uokoaji kuendelea kutoa elimu katika mikusanyiko ya watu na kupitia vyombo vya habari kuhusu dhana ya matumizi sahihi ya gesi ili kuepusha majanga ya moto. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amelishukuru Jeshi la Zimamoto na uokoaji kutoa elimu kwa wanafunzi na akawataka wanafunzi wote waliopata elimu hiyo kuwa mabalozi katika maeneo yao wanayoishi. 

Magreth Sonda mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Simiyu ameshukuru kupata elimu ya tahadhari na kinga dhidi ya moto na kuahidi kuwa yeye pamoja wanafunzi wenzake watakuwa mabalozi wa kueneza elimu hiyo kwa jamii inayowazunguka ili kuepusha majanga ya moto ambayo yana athari nyingi ikiwemo vifo na kuteketea kwa mali.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA HARAMBEE YA KUCHANGIA TIMU YA TAIFA STARS

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Hundi ya Shilingi Milioni 10 kutoka kwa Viongozi wa CRDB Bank ikiwa ni mchango kwa Timu ya Taifa Stars kwenye Harambee ya kuchangia Timu ya Taifa Stars ilioyofanyika leo Juni 20, 2019 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 370 zilichangishwa hapo hapo.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kuzindua Harambee ya kuchangia Timu ya Taifa Stars ulioyofanyika leo Juni 20, 2019 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 370 zilichangishwa hapo hapo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini kwenye Jezi Mpya ya Timu ya Taifa Stars ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Jezi hiyo wakati wa Harambee ya kuchangia Timu ya Taifa Stars ilioyofanyika leo Juni 20, 2019 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 370 zilichangishwa hapo hapo.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachangiaji kwenye Harambee ya kuchangia Timu ya Taifa Stars ilioyofanyika leo Juni 20, 2019 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 370 zilichangishwa hapo hapo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuzungumza na msemaji wa Timu ya Simba Haji Manara kwenye Harambee ya kuchangia Timu ya Taifa Stars ilioyofanyika leo Juni 20, 2019 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 370 zilichangishwa hapo hapo.

WAKULIMA WA TUMBAKU NAMTUMBO WACHUNGUZWA AFYA ZAO

$
0
0
Na Ripota Wetu,Ruvuma

BAADHI ya Wakulima wa Tumbaku wilaya ya Namtumbo, wameupongeza mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kuweka utaratibu wa uchunguzi wa Afya kwa wakulima wa zao hilo waliojiunga kwenye vyama vya msingi vya Ushirika.

Wakulima hao wamesema, ni jambo la mfano na kuigwa na mashirika mengine ya umma hapa nchini kwani mpango wa huo wa NHIF utasaidia sana kuwa na wakulima wenye Afya njema ambao wataweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na hivyo kuongeza idadi ya wananchi wengi ambao watajiunga na mfuko huo.

Wakizungumza wakati wa ufunguzi wa mpango wa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa yasio ambukiza na Ushauri wa kitaalam kwa wakulima wa Tumbaku ambao ni wanachama wa wa Chama cha msingi vya ushirika Namtumbo AMCOS.

Walisema, NHIF imefanya uamuzi sahihi hasa wakati huu ambao baadhi ya wanachama wanajianda kusafisha mashamba yao kwa ajili ya msimu mpya wa kilimo 2019/2020.Fadhil Kitete alisema, mpango huu wa uchunguzi wa Afya una manufaa makubwa kwa wana ushirika kwani watapata kufahamu hali ya Afya na kutibiwa katika Hospitali yoyote Nchini.

Hassan Kwitenda ameshauri kiwango cha shilingi 76,800 ambacho mwana Ushirika anapaswa kuchangia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa ajili ya kupata matibabu katika kipindi cha mwaka mmoja ni kikubwa na kushauri kipunguzwe ili kutoa nafasi kwa wakulima wengi waweze kujiunga na mfuko huo.

Alisema, hapo mwanzo Serikali ilitaka kila mwana Ushirika na mwananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) ambayo gharama yake ilikuwa elfu Ishirini,lakini sio watu wote waliojiunga na mfuko huo kwani baadhi walishindwa kutokana na kukosa fedha.

Kwa upande wake Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Dkt Mchelle Starmius alisema, katika ufunguzi huo walifanya uchunguzi wa Kisukari,Moyo(Pressure)kuangalia uwiano kati ya uzito na urefu, na kutathimini hali ya lishe kwa wanachama.

Alisema, zoezi la uchunguzi litahusisha wanachama wa Vyama vyote 22 vya Msingi vya Ushirika katika wilaya ya Namtumbo lina lenga kuweka ufahamu wa Afya za wanachama na atakayebainika kuwa na matatizo atapewa ushauri wa kitaalam na kupewa matibabu katika Hospitali yoyote hapa nchini kwa gharama za mfuko huo.

Alisema, mpango huo una faida kubwa kwa mwanachama kwani ataweza kutambua hali yake,kupata ushauri sambamba na kupata tiba sahihi ya ugonjwa alionao.

Hata hivyo,amewashauri wakulima wa Tumbaku na mazao mengine ya kimkakati Kahawa,na Korosho ambayo yanalimwa kwa wingi mkoa wa Ruvuma kujiunga kwa wingi kwenye vyama vya msingi vya ushirika ili wapate nafasi ya kuwa Mwanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulioboreshwa ambao utamwezesha kupata fao na kadi ya Matibabu.

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo amewaondoa wasiwasi Wanachama wa Vyama vya Ushirika kuwa, Huduma za matibabu zinazotolewa na NHIF ni tofauti na zinazotolewa na Mfuko a Afya ya Jamii kwani wale watakaojiunga na NHIF watapata fursa ya kutibiwa katika Hospitali yoyote hapa Nchini ikilinganisha na CHF ambayo mwanachama anatibiwa ndani ya wilaya yake.

Alisema,Serikali kwa kutambua kero wanayoipata wanachama wa CHF ndiyo maana imekuja na mpango mpya abao unamwezesha mwanachama wa chama cha Ushirika kuchangia shilingi 76,800 ambazo zitamwezesha kupata matibabu bora na imeongeza Bajeti ya fedha kutoka shilingi Biliono 30 hadi kufikia Bilioni 200 kwa mwaka.

Katika Hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Aden Nchimbi, Kizigo ameipongeza NHIF kuboresha huduma kwa mwanachama na kuwataka wananchi wa Namtumbo kuona kuwa,hiyo ni fursa muhimu ambayo itamsaidia kupata matibabu katika Hospitali yoyote hapa Nchini.

Alisema, na kila Mtanzania anatakiwa kuwa na Afya njema ambayo itamwezesha kushirika kikamilifu kazi za kujiletea maendeleo na mpango huo utawasaidia wanachama hata kupunguza gharama za matibabu pale wanapokwenda kupata huduma.

WAKOPESHWA ML 80 KWA AJILI YA KUIMARISHA VIKUNDI VYA KIUCHUMI

$
0
0

JUMLA ya shilingi milioni 50,363.400 zimetolewa kama mkopo usiokuwa na riba kwa vikundi 32 vya vijana,wanawake na walemavu katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Gasper Balyomi alisema, lengo la mikopo hiyo kuyawezesha makundi hayo kiuchumi ili yaweze kukuza miradi,kuhimarisha vikundi na kutoa nafuu kwa wanavikundi namna Bora ya kufanya shughuli zao bila bughuza.

Balyomi alisema, mkopo huo kwa vikundi hivyo pia ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 inayotaka kila Halmashauri hapa nchini kutenga na kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kusaidia makundi maalum .

Kwa mujibu Balyomi, hii ni mara ya pili kwa Halmashauri kutoa mikopo kwa vikundi mwaka 2019 ambapo Mwezi Februari walitoa shilingi milioni 33.500.000 kwa vikundi 10 vya vijana,10 wanawake na vikundi 4 vya walemavu.

Aidha,amewahasa wana vikundi kubuni miradi iliyo na faida na ya kiushindani kutokana na utandawazi uliopo kwa sasa kwa kutengeneza na kuzalisha bidhaa zitakazokuwa na ushindani na wazalishaji wengine kwani uzoefu unaonesha kuwa baadhi ya vikundi vlivyopo katika wilaya hiyo uzalisha bidhaa duni na zisizo na ubora katika soko.

Balyomi, amewataka kuepuka kuanzisha miradi wasiokuwa na uzoefu nayo kwani inaweza kuwagharimu wakati wa marejesho,bali kuanzisha miradi yenye faida watkaomudu kurejesha mkopo kwa wakati ili watu wengine nao wapate fursa ya kukopeshwa.

Amewaomba wataalam wa fani mbalimbali kuwasaidia wana vikundi katika kuendesha miradi kwa miradi ya vikundi vingi hufa na kukosa uendelevu kutokana na wataalam kuwa mbali na wana vikundi husika.

Amewaagiza maafisa wa idara ya maendeleo ya jamii kwenda kuwasaidia wana vikundi jinsi ya kuendesha miradi kusudi kama vile miradi ya kilimo na mifugo ambayo inahitaji ukaribu wa wataalam ili ilete faida na kumudu kurejesho mkopo kwa muda muafaka.

Pia amewaelekeza wataalam wa idara mbalimbali katika halmashauri kuvisaidia vikundi kutafuta fursa nyingine za uwezeshaji badala ya kutegemea halmashauri pekee kama ufungaji nyuki ambavyo vitaunganishwa na wakala wa misitu(TFS) ili viwezeshwe fedha za uendeshaji wa miradi.

Awali Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya Tunduru Fadhil Chidyaonga amewaomba wananchi kuitumia fursa hiyo kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali vya vijana,wanawake na walemavu.

Alisema, kumekuwa na chagizo la vikundi vinavyo bahatika kukopeshwa na Halmashauri kutoridhika na kuona mkopo wanaoupata kuwa mdogo kilinganishwa na mahitaji ya mradi husika.

Mmoja wa wana kikundi hao Fatuma Mtesa alisema, mikopo hiyo itawasaidia kuendeleza shughuli zao na kuongeza uzalishaji wa bidhaa ili kujikwamua na umaskini.

Hata hivyo,ameiomba Serikali kuongeza kiwango cha mkopo ili waweze kuanzisha miradi mikubwa ambayo itawapatia faida kubwa na kufanya mambo mengi ya maendeleo kama kujenga nyumba bora.

SERIKALI YAJADILI MPANGO KABAMBE WA UJENZI WA MJI WA SERIKALI AWAMU YA PILI

$
0
0
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Kujadili Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma, kuhusu mpango wa michoro ya Majengo ya Wizara Awamu ya Pili katika Mji wa Serikali na Michoro ya Miundombinu ya Chini ya Ardhi walipokutana na kikosi kazi cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma hii leo Juni 20, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi hiyo Jijini Dodoma.
 Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia neno la ufunguzi kutoka Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi (hayupo pichani).
 Baadhi ya wajumbe wakikao hicho wakifuatilia neno la ufunguzi kutoka Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi (hayupo pichani) walipokutana kujadili masuala ya mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma ikiwa ni sehemu ya uratibu wa zoezi la Serikali kuhamia Dodoma.
 Mwenyekiti wa Timu ya Kutengeneza Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma Prof. John Lupala akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akifuatilia michango ya wajumbe walioshiriki katika kikao kazi cha Kujadili Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma, kuhusu mpango wa michoro ya Majengo ya Wizara Awamu ya Pili katika Mji wa Serikali na Michoro ya Miundombinu ya Chini ya Ardhi walipokutana na kikosi kazi cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma hii leo Juni 20, 2019.
Baadhi ya wajumbe wa kikao kazi cha Kujadili Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma, kuhusu mpango wa michoro ya Majengo ya Wizara Awamu ya Pili katika Mji wa Serikali na Michoro ya Miundombinu ya Chini ya Ardhi walipokutana na kikosi kazi cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma Juni 20, 2019.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Shule ya Wasichana kondoa yakabidhiwa serikalini

$
0
0
 Mhandisi akiwaonyesha wajumbe madarasa yaliyofanyiwa ukarabati katika Shule ya Wasichana Kondoa.
 Mhandisi Mshauri wa mradi wa ukarabati wa Shule ya Wasichana Kondoa Marco Daniel akisoma taarifa ya mradi wakati wa makabidhiano ya mradi huo.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Tija Ukondwa (wa kwanza Kushoto) akikabidhi taarifa ya makabidhiano ya mradi wa ukarabati kwa Mkuu wa Shule ya Wasichana Kondoa Frola Nussu.
Moja ya choo kilichojengwa kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum katika Shule ya Wasichana Kondoa.

TEA yakabidhi Shule ya Wasichana Kondoa kwa Halmashauri ya Mji

$
0
0
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wamekabidhi rasmi majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasiichana Kondoa kwa uongozi wa Halmashauri ya Mji Kondoa baada ya kukamilisha ukarabati mkubwa.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi ya Mkuu wa Shule hiyo na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Mamlaka ya Elimu Tanzania, Bodi ya Shule na uongozi wa shule.

Akikabidhi mradi huo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Tija Ukondwa alisema kuwa mradi huo umefanikiwa kwa viwango vya hali ya juu kwasababu wasimamizi wa mradi waliweka tamaa nyuma na kutanguliza uzalendo hadi wanakabidhi majengo hayo.

“Fedha hizi zimetolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania lakini ni kutokana na juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha kuwa shule kongwe zinafanyiwa ukarabati hivyo ni jukumu lenu kuitunza shule hii ili itumike kwa kipindi kirefu.”Alisema Tija

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kaunga Amani aliwashukuru TEA kwa kuichagua shule ya Wasichana Kondoa kwa kuwa shule zipo nyingi nchini ila wakaona shule hiyo inafaa katika awamu hii.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru pia bodi ya shule kwa usimamizi mzuri maeneo mengine wengi wanaishia kuvunja bodi sababu ya maslahi ila hapa hatukuliona hilo, pia washauri wa mradi huo Chuo Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya walifanya kazi nzuri ya usimamizi kazi ambayo tunafanya nao kwa kipindi cha pili sasa.”Alisema Kaunga

Naye Mwenyekiti wa bodi ya Shule Emanuel Mkubwa alisema ukarabati huo ulikuwa mgumu ila usimamizi ulikuwa mkali kuhakikisha malengo yanatimia na yametimia kutokana na ushirikiano uliokuwepo kati ya uongozi wa shule na Halmashauri.

“Pongezi nyingi ziende kwa Mhe.Rais Dkt. John Magufuli kwa kutuwezesha shule yetu kukarabatiwa na leo lengo lake limetimia na katika kipindi chote hicho cha mradi ajira zilipatikana na mzunguko wa fedha uliongezeka tunashukuru sana ila tunaomba pia mtusaidie kisima cha maji na ukarabati wa nyumba za walimu ili kuzidi kuongeza hali ya ufaulu shuleni hapa.” Alisema Emanuel

Tigo na DStv wazindua kifurushi cha kuangalia michuano ya AFCON

$
0
0
 
Mkuu wa Huduma na bidhaa wa Tigo David Umoh (kushoto) akiwa na Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo (kati kati) na Mtaalamu wa Huduma za Intaneni wa Tigo Allen Salaita wakipongezana baada ya uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Tigo na Dstv utakaowawezesha wateja wa kampuni hizo kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vifurushi vya gharama nafuu. 
Wafanyakazi wa Tigo pamoja na Dstv wakifurahi pamoja muda mfupi baada ya uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya hizo mbili utakaowawezesha wateja wao kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vifurushi vya gharama nafuu. 

Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Tigo na Dstv utakaowawezesha wateja wa kampuni hizo kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vifurushi vya gharama nafuu. Kushoto ni Mkuu wa Huduma na bidhaa wa Tigo David Umoh na kulia ni Mtaalamu wa Huduma za Intaneni wa Tigo Allen Salaita.
Mkuu wa Huduma na bidhaa wa Tigo David Umoh (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Tigo na Dstv utakaowawezesha wateja wa kampuni hizo kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vifurushi vya gharama nafuu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo na kushoto ni Mtaalamu wa Huduma za Intateni wa Tigo Allen Salaita.
 
Wateja wa Tigo na DStv sasa wataweza kufurahia mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika mubashara wakiwa sehemu yeyote na kwa muda wowote, baada ya makampuni haya mawili kuzindua ushirikiano maalum na mahususi ya huduma ya DStv itakayowapa wateja wake fursa ya kutazamaa mechi hizo kupitia DStv Now mobile App kwa gharama nafuu. 

Akizungumzia na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo, tMkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema ushirikiano huo na DStv unaendana sambamba na lengo la kampuni hiyo kukuza maisha ya kidijitali kwa kila Mtanzania. . 

“Tunayofuraha ya kuzindua huduma hii maalum ya DStv Now itakayowapa wateja wetu wa Tigo katika msimu huu wa michuano ya Afrika kupata fursa nzuri ya kutazama mechi mtandaoni na kushuhudia timu yao pendwa ya Taifa Stars na timu nyingine zinazoshiriki mashindano haya makubwa barani Afrika,” alisema Umoh. 

Aliongeza, “Kupitia mtandao wetu bora wa 4G, tunaweza kuwahakikishia wateja wetu wanaotumia DStv fursa ya uhakika ya kuunganishwa mubashara na bila usumbufu wowote kuangalia Kombe la Mataifa ya Afrika, kutoka sehemu yeyote na muda wowote kupitia DStv Now App katika vifaa walivyonavyo. Hii ni fursa nzuri pia kwa wale wateja ambao kwa sababu mbalimbali hawatakuwa na nafasi ya kutazama kupitia televisheni zao.” 

Kwa mujibu wa Umoh, Tigo inawapa wateja wake waliounganishwa na DStv nafasi ya kuchagua vifurushi vitatu. Cha kwanza ni kifurushi cha GB 1.5 kwa gharama ya TSH 2000 kwa masaa 24, cha pili ni cha GB 6 kwa gharama ya TSH 7000 kwa siku 7, na kifurushi cha tatu ni ya GB 16 kwa TSH 20,000 tu kwa siku 30. 

Vifurushi hivi maalum na vya gharama nafuu kwa watumiaji wa DStv Now vinapatikana kupitia www.tigosports.co.tz, Tigo Pesa App, na menyu za *147*00# na *148*00#. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo, alisema uzuri wa DStv Mobile app ni kwamba inaweza ikafanya kazi katika vifaa aina nne bila nyongeza ya gharama yeyote. 

“Hakutakuwa na gharama ya ziada kutazama DStv kupitia vifaa mbali mbali, kwa sababu gharama zote zinakuwa zimeshalipiwa katika kifurushi cha mwezi cha DStv. Ili kuweza kuangalia mechi za AFCON, wateja wa DStv wanachohitaji kufanya ni kupakua DStv App katika simu janja zao, kompyuta mpakato, tablet au vifaa janja vingine,” alisema Shelukindo. 

Uzuri mwingine wa kipekee ambao mteja anaweza kuupata kupitia huduma hii ni kuwa wateja wa DStv wanapewa uwezo wa kuunganisha hadi vifaa vinne tofauti kwa wakati mmoja kutazama vipindi vya DStv wakati huo televisheni nayo ikiwa nayo imeunganishwa na kuendelea kutumika kuangalia vipindi. 

Shelukindo aliongeza, “Kujiunga na DStv Now wateja wanatakiwa kutembelea now.dstv.com, na kufuata maelekezo ya kuweka jina na neno siri. Baada ya kumaliza hatua hiyo rahisi, watakuwa na uwezo wa kupakua na kuingia katika kifaa janja yeyote na taarifa zao walizoweka na kuanza kutazama mubashara vipindi.” 

Shelukindo aliongeza kuwa, mechi za AFCON zitakuwa zinaonyeshwa kupitia vifurushi vyote vya DStv kuanzia kifurushi cha bei ya chini kabisa mpaka kifurushi cha DStv Premium. “Wateja wa DStv katika vifurushi vyote watakuwa na uwezo wa kufurahia mechi zote 52 ya mashindano haya maarufu ya mpira. Ushirikiano wetu na Tigo umefanya maisha kuwa rahisi kwa sababu inatoa fursa kwa yeyote kufurahia mechi hizi popote pale,” alisema.
 

MAPITIO YA MWONGOZO YAKINIFU WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI YAFANYIKA

$
0
0
SERIKALI Kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la maendeleo la Japan (JICA) kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, imefanya mapitio ya mwongozo yakinifu wa Umwagiliaji unaolenga kufanya mabadiliko na maboresho katika kilimo cha Umwagiliaji nchini. 

Bw. Anthon Nyarubamba ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa kujenga uwezo (TANCAID) kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji amesema hayo leo Mjini Morogoro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa kikosi kazi wa kupitia mwongozo huo. 

Bw. Nyarubamba alisema kuwa, mwongozo huo ambao ulikuweo tangu mwaka 2010 ambao ulikuwa katika mfumo wa kitabu kikubwa utaboreshwa na kuwekwa katika lugha rahisi na rafiki kwa watumiaji ambao ni wataalam, wakulima na wadau wote katika sekta hiyo, ambao utarahisisha na kuonyesha matumizi sahihi ya maji katika skimu za kilimo cha umwagiliaji. 

“Kabla ya kuwepo kwa Mwongozo huu wakulima wengi walikuwa wanadhani kuwa kilimo cha umwagialiaji ni kilimo chenye kutumia maji mengi lakini Mwongozo sasa utaonyesha matumizi sahihi ya maji sambamba na kujenga uwezo kwa wataalam na wakulima nchini.” Alisema Nyarubamba. 

Aidha Bwana Nyarumbana aliendelea kusema kuwa, mtu yeyote atakayeshughulika na kilimo cha umwagiliaji nchini atatakiwa kuufuata mwongozo huo ambao pia utachangia skimu za kilimo cha umwagiliaji nchini kujengwa katika ubora. 

Awali, Akiongea na waandishi wa Habari baada ya sehemu ya kwanza ya mapitio ya mwongozo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Ronald Komaga amesema tangu kuwepo kwa mwongozo huo mwaka 2010 kumejitokeza changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kitabu cha mwongozo huo kuwa kikubwa na siyo rafiki kwa watumiaji, mwongozo kutoeleweka kwa wadau wengi na baadhi ya vipengele kutotekelezeka jambo ambalo limepelekea kuwa na awamu hii ya pili ya mapitio na maboresho ya mwongozo huo. 

Pamoja na changamoto hizo Bw. Komanga amesema kuwa Mwongozo wa awali pia ulitumika katika skimu nyingi za kilimo cha umwagiliaji zilizopo katika mradi na kuongeza uzalishaji hasa wa zao la mpunga. 

Kikosi kazi hicho chenye kufanya mapitio na maboresho ya mwongozo huo wa kilimo cha umwagiliaji umehusisha washiriki kutoka Serikali za Mitaa, Ofisi za kanda za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, na wawakilishi kutoka JICA. 
Bw. Ronald Komanga Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, akiongelea mafanikio ya Maboresho ya Mwongozo yakinifu wa Kilimo cha umwagiliaji.
Katika Picha Bwana Anthon Nyarubamba ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa kujenga uwezo (TANCAID) kutoka Tume a Taifa ya Umwagiliaji akiongea na waandishi wa Habari kuhusu mwongozo wa Umwagiliaji. (Habari na Picha Kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Morogoro) 

Sehemu ya washiriki (kikosi kazi) katika mkutano wa mapitio ya mwongozo yanikifu wa kilimo cha umwagiliaji.

SERIKALI YA TANZANIA YAJIPANGA KUTEKA SOKO LA WATALII CHINA

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kwa sasa muelekeo wa soko la Utalii nchini umelenga kupata watalii wengi kutoka nchini China na kama Wizara inayoshugulikia masuala ya Utalii,  suala la  kujifunza lugha ya kichina kwa baadhi ya watumishi na wadau wa utalii ili kuteka soko hilo ni jambo lisiloepukika.

Imesema nguvu nyingi kwa sasa zinaelekezwa nchini China hivyo  ni muda muafaka wa kuandaa timu ya wataalamu mbalimbali wakiwemo  waongoza watalii watakaoweza kuzungumza lugha ya kichina ili kuweza kulimudu soko hilo.

Hayo yamesemwa leo  jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu  wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa  Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii  cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS

Amesema  lengo mkutano huo ni  kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya China na Tanzania katika suala la kuwajengea uwezo watumishi na wadau wa Utalii nchini.

Mkutano huo  umehudhuriwa na ujumbe kutoka China ukiongozwa na Makamu wa Chuo hicho,Prof.Xiong Nanyong,Kaimu huku kwa upande wa Wizara  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.Lucius Mwenda pamoja na ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara.

 Amesema ni muhimu kwa watumishi wa wizara pamoja na wadau wa utalii kujiandaa ili kuweza kuzungumza lugha ya kichina badala ya vifaa maalum vya kutafsiri lugha ilhali kuna uwezekano kwa Watanzania kujifunza.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Xiong Nanyong amesema wamejipanga kutoa mafunzo mbalimbali likiwemo suala la lugha ya kichina pamoja na utalii ili kuwajengea uwezo Watumishi hao

Ameongeza kuwa tayari wameshaomba kibali kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa umma na Utawala Bora  kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Lucius Mwenda  ameahidi kutoa ushirikiano kwa Uongozi wa Chuo hicho ili  kujengeana uwezo  baina ya Serikali ya  Tanzania na China.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza jambo na Viongozi wa  Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii  cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS mara baada ya kuwatambulisha wageni hao  Bungeni Dodoma  leo  waliokuja nchini kwa lengo la  kuwajengea uwezo wa mafunzo  watumishi na wadau wa utalii nchini
 Naibu wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akikabidhiwa zawadi ya pichana Makamu wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii  cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS  Prof.Xiong Nanyong ( wa pili kulia) akiwa pamoja na  Mkuu wa mafunzo ya chuo hicho ,Wanga Jiaxin leo katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.
 Naibu wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akikabidhiwa zawadi ya pichana Makamu wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii  cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS  Prof.Xiong Nanyong ( wa pili kulia) akiwa pamoja na  Mkuu wa mafunzo ya chuo hicho ,Wanga Jiaxin leo katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.
 Naibu wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi ya vitabu kutoka TANAPA ikiwa  ni ishara ya shukrani kwa   Mkuu wa kitengo cha mafunzo wa chuo cha JXCFFS, Yang Jing mara baada  kufanyika mkutano uliolenga kuimarisha ushirikiano katika ya China na Tanzania jijini Dodoma.
 Naibu wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii  cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS mara baada ya kumaliza mkutano uliolenga kumaimarisha mahusiano baina ya Tanzania na China.
 Makamu wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii  cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS  Prof.Xiong Nanyong ( wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya picha ya Chuo hicho Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bw. Lucius Mwenda mara baada ya kufanyika  mkutano  mara baada  kufanyika mkutano uliolenga kuimarisha ushirikiano katika ya China na Tanzania jijini Dodoma.
 Viongozi wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii  cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS wakiwa wamesimama wakati wakitambulishwa Bungeni jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wabunge pamoja na viongozi wa chuo cha mafunzo ya nje na utalii cha China wakiwa nje ya Bunge jijini Dodoma.

Muhimbili kupandikiza ULOTO mwaka huu

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inatarajia kufanya upandikizaji wa ULOTO (bone marrow transplant) mwishoni mwaka huu ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi na kugharimu fedha nyingi.

Katika kufanikisha upandikizaji huu, wataalam 11 wa MNH wanatarajiwa kwenda nchini India katika Hospitali ya Apollo iliyopo Chennai kwa kipindi cha mwezi mmoja ambako watajifunza kwa vitendo jinsi ya kufanya upandikizaji wa ULOTO.

Katika kuhakikisha huduma hii inafanyika hapa nchini, Serikali imetoa Tshs. 6.2 bilioni na kati ya hizo, Tshs. 3.7 bilioni zimetumika kufanya maandalizi ya kununua vifaa na kuweka miundombinu ya kutoa huduma ya upandikizaji wa ULOTO.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dkt. Hedwiga Swai amesema wataalamu wanaosafiri kwenda India ni madaktari bingwa watatu wa magonjwa ya damu, watalaam wa maabara watatu, waandisi watatu wakiwamo wa ufundi, ujenzi na vifaa tiba, mtalaamu wa fedha ambaye atafanya uchambuzi wa gharama halisi za huduma hii.

Dkt. Swai amesema mtalaam mwingine ni wa manunuzi ambaye atafanya uchambuzi yakinifu wa dawa na vitendanishi vinavyotumika na upatikanaji wake ili huduma ya upandikizaji ULOTO itakapoanza iwe na mzunguko wa upatikanaji wa vifaa ambao hauna changamoto.

Amesema tayari wauguzi watatu, watalaam wa saratani ya watoto watatu, mfamasia mmoja na watalaamu wengine wawili wa damu wamepata mafunzo ya huduma hiyo katika Hospitali ya Apollo iliyopo New Delhi India kwa kipindi cha miezi mitatu.

Dkt. Swai amesema wataalam hawa wanatarajia kurejea nchini Julai, 2019 na kwamba gharama za kupeleka watalamu hawa kwenye mafunzo ni Tshs. 91 milioni zikijumuisha gharama za mafunzo, nauli, fedha za kujikimu pamoja na gharama nyingine za mafunzo. Fedha hizi zote zitalipwa na Muhimbili ili kujenga uwezo wa watalaamu wake.

Amefafanua kwamba uwepo wa huduma hii hapa nchini, itasaidia wananchi wengi kutibiwa hapa nchini, kujenga uwezo kwa wataalamu wa ndani na kupunguza mzigo kwa Serikali kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwani gharama za kufanyia hapa zitashuka kufikia kiasi cha chini ya asilimia 50 kwa mgonjwa mmoja.

Amesema takwimu za Muhimbili zinaonyesha wagonjwa takribani 130 hadi 140 wanahitaji huduma ya kupandikizwa ULOTO kwa mwaka na pia, zaidi ya theluthi mbili ya wagonjwa hao hufariki dunia kwa kukosa huduma hii.

Dkt. Swai amesema nje ya nchi, huduma hii inagharimu kiasi cha Tshs. 200 milioni kwa mgonjwa mmoja ambaye anapandikizwa ULOTO kutoka kwa ndugu yake wakati akipandikizwa ULOTO wake mwenyewe si chini ya Tshs. 150 milioni,” amesema Prof. Museru.

Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu, Dkt. Stella Rwezaura amesema hatua ya kwanza ya kupandikiza ULOTO ni kumuandaa mgonjwa ambaye chembechembe zake za damu zina tatizo kama saratani, selimundu au wagonjwa ambao mifupa yao imekuwa ikishindwa kuzalisha damu.

Amefafanua kwamba chembechembe zinazotumika kupandikiza ULOTO ni chembechembe mama za kuzalisha damu ambazo hupatikana kwenye ULOTO (Pluripotent Haemopoietic Stem Cells) au chembechembe mama kutoka kwenye kitovu cha mtoto mchanga (umbilica cord blood) au kondo la nyuma la mama.

“Njia ambayo hutumika mara nyingi ni ile ya upandikizaji wa chembechembe mama za damu (HSCT) kutoka kwenye ULOTO,” amebainisha Dkt. Rwezaura.

Dkt. Rwezaura amebainisha kuwa huduma hii hufanyika kwa kuwapa tiba maalum wagonjwa ili kuua chembechembe zote zenye matatizo na kisha kupandikiza chembechembe mpya zilizopo kwenye ULOTO kutoka kwa ndugu yake mwenye vinasaba vinavyofanana au chembechembe mpya zilizozalishwa kutoka kwa mgonjwa mwenyewe baada ya kupata tiba maalum. Huduma hii ndiyo tiba pekee inayoweza kuponya wagonjwa wenye matatizo hayo,” amesema Prof. Rwezaura.

Tanzania itakua nchi ya kwanza kupandikiza ULOTO katika Ukanda wa Afrika Mashariki na pia nchi ya sita katika Bara la Afrika. Kwa sasa huduma hii Afrika inatolewa Afrika ya Kusini, Tunisia, Misri, Komoro na Nigeria.

Mbali na kuanzishwa kwa huduma hii, hadi kufikia Juni, 2019, MNH imeweza kupandikiza figo kwa wagonjwa 43, na wagonjwa 339 wamenufaika na tiba radiolojia (interventional radiology), na watoto 21 wamepandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia (cochlear implant).
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Hedwiga Swai akizungumza na waandishi wa habari kuhusu MNH kupeleka wataalam nchini India kwa ajili ya kujifunza upandikizaji wa ULOTO kwa wagonjwa ambaye chembechembe zake zina tatizo kama saratani au selimundu. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu wa MNH, Dkt. Stella Rwezaura.
 Baadhi ya wataalam wa MNH wakimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa MNH, Dkt. Hedwiga Swai wakati akizungumza na waandishi wa habari leo.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu wa MNH, Dkt. Stella Rwezaura akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano leo kuhusu upandikizaji wa ULOTO.
Wataalam wa MNH wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka nchini kwenda India kujifunza kwa vitendo upandikizaji wa ULOTO.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images