Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WAZIRI LUGOLA AONGOZA MAANDAMANO MAADHIMISHO SIKU YA WAKIMBIZI DUNIANI

$
0
0



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kulia) akiongoza maandamano ya kuadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani ambayo imefanyika jijini Dar es Salaam, leo. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Katikati ni Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Nchini, Chansa Kapaya. Na kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA KUBORESHWA JULAI MWAKA HUU

$
0
0
* Kaijage aeleza kuwa haitawatumia wakurugenzi kusimamia uchaguzi kama mahakama ilivyoelekeza

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MWENYEKITI wa tume ya uchaguzi (NEC) ambaye pia ni jaji wa mahakama ya rufaa Semistocles Kaijage amesema kuwa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura utaanza rasmi mwezi huu hadi Aprili mwakani na kuwataka wale wote wenye sifa kutumia nafasi hiyo kupata vitambulisho vya kupigia kura.

Akizungumza na wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaijage amesema kuwa hatua za maboresho kuelekea uchaguzi mkuu yameanza na hiyo ni pamoja na  uandikishwaji wa majaribio uliofanyika katika kata za Kihonda Mkoani Morogoro na Kibuta Kisarawe, uandaaji wa vituo pamoja na ratiba huku akisema kwamba uandikishwaji wa mwaka 2015 ulihusisha wananchi wote ila kwa mwaka huu watakaoandikishwa ni wale wanaotimiza miaka 18 mwaka huu na watakaotimiza miaka 18 tarehe ya siku ya uchaguzi mwakani na uandikishwaji huo utaenda sambamba na wale waliopoteza kadi za kupigia kura, wenye kadi zilizoharibika na waliohama makazi ambao hao wote taarifa zao zitaboreshwa.

Kuhusiana na kuwatumia wakurugenzi katika kusimamia chaguzi Jaji Kaijage amesema  kuwa vifungu vya sheria ya uchaguzi vilivyolalamikiwa na kutenguliwa na Mahakama havitatumika kwenye utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo na 
Vifungu hivyo ni kifungu cha 7(1) na 7(3) vya sheria ya uchaguzi ambavyo vinavyowapa mamlaka wakurugenzi wa halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

 Vifungu tajwa vinawaelekeza wakurugenzi wa Manispaa, majiji, miji na wakurugenzi wa wilaya (DED) kuweza kuchaguliwa na tume ya uchaguzi na  kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

“Mahakama ilitimiza wajibu wake na kutengua  baadhi ya vifungu vya sheria vilivyolalamikiw, tutahakikisha  vifungu vilivyolalamikiwa havitatumika katika utekelezaji wa majukumu yetu" ameeleza Kaijage.

Vifungu viwili vilivyotenguliwa ni pamoja na Kifungu cha 7 (1) na 7(3) cha sheria ya taifa ya uchaguzi ambavyo vililalamikiwa na baadaye kutolewa maamuzi na mahakama.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa uchaguzi Dkt. Athuman Kihamia amesema kuwa uboreshaji utafanyika katika Mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar na kueleza kuwa idadi ya vituo imeongezeka kutoka 36,549 mwaka 2015 hadi 37,407 mwaka 2018 kwa upande wa Tanzania bara huku kwa upande wa Zanzibar vituo vikiongezeka kutoka 380 mwaka 2015 hadi vituo 407 mwaka 2018.

Kihamia amesema kuwa elimu itazidi kutolewa katika makundi yote ili kuhakikisha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura unakuwa na tija na uchaguzi unakuwa wa huru na haki na  yote hayo itategemea ushirikiano kutoka kwa wananchi na vyombo vya ulinzi ambavyo vimekuwa macho wakati wote katika kuhakikisha wakati wa uchaguzi amani na utulivu vinaimarika.

Kasi ya Magufuli yaipiga Break TLP kusimamisha Mgombea wa Urais 2020

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimesema wamekubaliana ndani ya Chama wameamua kuunga mkono Mgombea wa Urais chama  Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli.

Chama hicho kimejipambanua hakiwezi kusimamisha Mgombea wa Rais kwa Tiketi ya TLP badala yake watashirikiana na Mgombea Urais Dkt. John Magufuli katika kipindi cha pili.

Akizungumza na wa Habari Jijini Dar es Salaam Mwenyikiti wa Chama hicho Augustine Lyatonga Mrema amesema kumpoteza Rais Magufuli nchi itarudi nyuma. Amesema kuwa watu wanamtokana Rais Dkt.John Pombe Magufuli na kuacha kuangalia maendeleo yanayofanywa na serikali ya awamu ya Tano.

Amesema kuwa kuwa TLP inamuunga mkono na yeye atakwenda kugombea Ubunge Jimbo la Vunjo kushirikiana na Rais Dkt John Pombe Magufuli. Mrema amesema Dunia itapata mshangao kuona Rais Magufuli tunamuacha kutokana na hila ambazo hazina msingi.

Amesema kila kitu baadhi ya wanasiasa wanapinga maendeleo ya serikali ya awamu ya Tano. Amesema ingekuwa kuhongwa yeye angekuwa wa kwanza  hongwa fedha hizo lakini hawajafanya hivyo. Naibu Katibu wa TLP Dominata Rwechungura amesema TLP haijakurupuka kumuunga mkono Rais Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na vyama vingine kuwaunga maamuzi ya TLP.

Amesema wanawake wasidanganywe kuwa serikali hawapendi kutokana na kuongezwa kodi kwa nywele za Bandia wakati Rais ametoa elimu bure na mambo mengine yanayohusu wanawake.
Mtanzania anayeishi Ujerumani  Edward Leirings amesema kuwa wanaona maendeleo ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli na kutaka watanzania waendelee kumuamini.

Amesema kuwa vyama vingine vinaweza kushirikiana na Rais Magufuli katika kuchagiza maendeleo hayo. Amesema kuwa wanashangaa kuona wananchi wa Tanzania hawaoni jitihada hizo wakati watu wengine wakiulizwa wanaotoka Afrika Mashariki wanasema wanatoka Tanzania wakati hawatoki Tanzania.
Mwenyikiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Agustine Mrema akizungumza na waandishi habari kuhusiana na maamuzi ya Chama kutosimamisha Mgombea wa Urais 2020,jijini  Dar es Salaam.

TANAPA YAWAKUMBUKA WADAU WA UTALII,YAWAPA TUZO WALIOFANYA VIZURI KATIKA UHIFADHI NA UTALII.

$
0
0
Waziri wa Malisili na Utalii,Dkt Hamisi Kigwangalla akizindua mkataba wa huduma bora kwa mteja wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii ,hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha .Wengine kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi ,Mjumbe wa Bodi -Tanapa ,Kamishna Nsato Marijani na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro. Waziri wa Malisili na Utalii,Dkt Hamisi Kigwangalla akizindua amzezindua Mfumo a uendeshaji wa viwango vya kimataifa (ISO 9001:2015 Quality management system) wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii ,hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha .Wengine kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi ,Mjumbe wa Bodi -Tanapa ,Kamishna Nsato Marijani na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro. Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa utalii wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group ,Joseph Kusaga ni miongon mwa waalikwa walioshiriki hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii. Makamishna wasaidizi wa TANAPA wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla hiyo. Kamishna Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya TANAPA,Kamishna Nsato Marijani akizungumza wakati wa hafla hiyo.


Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro akizungumza wakati wa hafla hiyo. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji (TBC) Dkt Ayoub Ryoba akiwa na Mkurugenzi wa Channel ten Jafary Aniu pia walikuwa ni miongoni mwa waalikwa katika hafla hiyo. Baadhi ya Makamishna wasaidizi wa Uhifadhi wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi -Mawasiliano TANAPA,Pascal Shelutete akitangaza utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo kwa wadau wa utalii.Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akiwa katika pich ya pamija na Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group ,Joseph Kusaga ,Emilian Mallya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa tatu katika kutangaza hifadhi za taifa . Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akikabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji ,Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Ryoba (kushoto) ,Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro (kulia). Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Zara Adventure baada ya kuibuka mshindi wa Jumla kwa watoa huduma za Utalii katika Hifadhi za Taifa . Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mshindi wa jumla ,Zainabu Ansel ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Zara Adventure pamoja na Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi ,Mjumbe wa Bodi -TANAPA ,Kamishna Nsato Marijani na Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jeryy Muro. Washindi wa tuzo za Gold wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Malisili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla.



Na Dixon Busagaga .

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa mara ya kwanza limekabidhi tuzo kwa Wadau mbalimbali wa masuala ya Utalii na Uhifadhi ,tuzo zilizokabidhiwa na Waziri wa Malisili na Utalii jijini Arusha kwa lengo la kuthamini mchango mkubwa wanaotoa katika masuala ya Utalii na Uhifadhi.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Maount Meru ,Waziri Dkt Kigwangalla pia amezindua Mfumo wa uendeshaji wa viwango vya kimataifa yaani ISO 9001:2015 Quality management system pamoja na mkataba wa huduma bora kwa mteja .

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuliwa na viongozi kutoka kampuni na taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya Utalii na Uhifadhi ,Mgeni rasmi ,Waziri ,Dkt Hamisi Kigwangala aliipongeza TANAPA kwa uamuzi wa kutoa tuzo kwa wadau wa sekta ya utalii hapa nchini.

“Niwapongezeni TANAPA ,Bodi ya wadhamini na Menejenti ya TANAPA mnafanya kazi nzuri sana hasa katika kuisimamia ipasavyo sekta ya utalii, Hongereni sana.”alitoa pongezi hizo Dkt Kigwangalla.

“Nampongeza sana Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kwa kuweka mkazo kwenye sekta ya miundombinu na sekta ya anga kwani zimekuwa kichocheo katika ukuaji wa sekta ya utalii,niwahakikishie wadau wa Sekta binafsi katika sekta hii ya utalii, tutaendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha lengo ni kuhakikisha tunakuza na kuendeleza sekta hii kwa kasi kubwa kabisa.”aliongeza Dkt Kigwangalla.

Dkt Kigwangalla alisema tuzo walizopata wadau wa sekta ya Utalii kwa kazi nzuri wanazoendelea kufanya ziwe chachu katika kuimarisha ushindani katika utoaji huduma bora katika sekta ya utalii ambapo zitasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu.

“Natoa wito kwa wadau wa sekta ya utalii kuwekeza katika maeneo ya usafiri na malazi kwenye maeneo ya Kusini na Magharibi mwa nchi yetu.”alisema Dkt Kigwangalla.Mjumbe wa Bodi ya TANAPA ,Kamishna Nsato Marijani aliyemwakilisha mwenyekiti wa bodi hiyo,Jenerali George Waitara alisema uzinduzi wa Mkabata wa Huduma kwa Mteja utawezesha utoaji huduma kwa Haraka, ufanisi na kwa wakati ili kuondoa malalamiko na urasimu usio na tija kwa pande zote mbili.

“Sisi kama Bodi tunaahidi kuendelea kusimamia sekta hii kwa kikamilifu ili iwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini.”alisema Kamishna Nsato.Kwa upande wake KAmishna Mkuu wa Uhifadhi ,Dkt Allan Kijazi alisema TANAPA inatambua mchango mkubwa wa wadau wetu wote katika sekta ya utalii kwa jitihada zote wanazozifanya katika sekta hiyo ikiwemo kuiletea heshima nchi.

“ Tunathamini na tutaendelea kuthamini kila mdau anayefanya kazi na TANAPA,shirika limefanikiwa kuongeza ulinzi wa rasilimali zetu, tutaendelea kuimarisha miundombinu ili kuwezesha kufikika kwa urahisi katika hifadhi zetu.”alisema Dkt Kijazi .

Naye Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa kampuni za Utalii nchini (TATO) Wilbert Chambulo ameishukuru TANAPA kwa tuzo hizo na kwmba shirika hilo limekuwa likijitoa kwa wadau wa utalii hali ambayo imechangia kampuni hizo kukua kiuchumi.

“TANAPA imebadilika sana.nakuahidi Mhe. Waziri Tutaendelea kulinda na kudhitibi uharibufu wa hifadhi zetu na nina kukabidhi magari mawili kwa ajili ya zoezi hilo”alisema Chambulo.

Maadhimisho ya utumishi wa Umma yaendelea Jijini Arusha sambamba na Usajili wa laini za simu kwa mfumo wa alama za vidole

$
0
0
Mhandisi Imelda Salum ni Kaimu mkuu wa Kanda Mamlaka ya Mawasiliano akitoa msisitizo wa jambo kwa wananchi waliofika katika banda la TCRA kuhusiana na usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na Kitambulisho cha Taifa.Picha na Vero Ignatus
Mhandisi Imelda Salum ni Kaimu mkuu wa Kanda Mamlaka ya Mawasiliano akiwapa maelekezo wananchi waliofika katika banda la TCRA kuhusiana na usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na Kitambulisho cha Taifa.Picha na Vero Ignatus
Rolf Kibaja Mtaalamu wa Maudhui kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania akimsikiliza mwananchi aliyehitaji huduma kutoka TCRA ktika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa Umma inayoendelea katika maeneo ya Kilombero Jijini ARUSHA .Picha na Vero Ignatus
Afisa msajili kutoka NiDa Juliety Robert akizungumza na waandishi wa habari akitolea ufafanuzi wa namna vitambulisho vya vinavyopatikana kwa wananchi ambao tayari walishajisajili na wale ambao bado hawajajisajili .picha na Vero Ignatus.
Mhandisi Imelda Salum ni Kaimu mkuu wa Kanda Mamlaka ya Mawasiliano akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda la TCRA kuhusiana na usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na Kitambulisho cha Taifa.Picha na Vero Ignatus
Rolf Kibaja Mtaalamu wa Maudhui kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania akimsikiliza mwananchi aliyehitaji huduma kutoka TCRA ktika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa Umma inayoendelea katika maeneo ya Kilombero Jijini ARUSHA .Picha na Vero Ignatus

Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwaajili ya kupatiwa huduma katika maeneo ya standi ya Kilombero JIJINI Arusha kwaajili ya kupatiwa huduma kwenye Banda la Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA)Picha na Vero Ignatus.
Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwaajili ya kupatiwa huduma katika maeneo ya standi ya Kilombero JIJINI Arusha kwaajili ya kupatiwa huduma kwenye Banda Uhamiaji  na  kuhojiwa na Afisa Uhamiaji tayari kwa kwenda kupigan picha (NIDA)Picha na Vero Ignatus.
Wananchi wakiwa na fomu zao katoka Stendi ya Kilombero iliyopo JIjini Arusha ambapo wiki ya huduma kwa mteja inaadhimishwa iliyoandaliwa na TCRA kwaajili ya kusajili laini za simu.Picha na Vero Ignatus
Baadhi ya wananchi wakijaza fomu kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tcra tayari kwa kuzipeleka katika makampuni mbalimbali ya simu kwa usajili.
 Zoezi la utsmbuzi wa namba za NIDA likiendelea kama inavyoonekana katika picha.Picha na Vero Ignatus.

Maadhimisho ya utumishi wa Umma yanaendelea Jijini Arusha sambamba na Usajili wa laini za simu kwa mfumo wa Bayotria.

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Zoezi la kusajili laini za simu kwa wananchi linaendelea katika eneo la kilombero kwa njia ya Bayometria ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wiki ya utumishi wa Umma iliyoandaliwa ma Mamlaka ya Mawasiliano Tanzanzia (TCRA)

Mhandisi Imelda Salum ni Kaimu mkuu wa Kanda Mamlaka ya Mawasiliano amesema kuwa mamlaka hiyo imefanya jitihada za kuwajuLisha wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya habari ambavyo vipo katika ukanda huo wa kaskazini na muitikio umekuwa mkubwa.

Ametoa rai kwa wananchi watumie fursa ambayo ipo kwa wiki ya Utumishi kwa umma kwani ni nafasi ambayo Mamlaka ya mawasiliano imetoa kwaajili ya kuwapa wananchi fursa nzuri ya kuweza kusajili laini zao za simu.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kukamilisha usajili wao  kwa njia ya Bayometria pia amewakumbusha kuwa usajili ni bure na mwananchi hapaswi kulipa fedha yeyote anaposajili laini yake isipokuwa endapo mwananchi atananunua laini mpya ndipo atalazimika kulipa gharama za manunuzi ya laini hiyo kwa wahusika.

Amesema Mamlaka ya Mawasiliano kwa kushirikiana na NIDA  watoa huduma kwa siku hizo tatu  na wamejipanga kuhakikisha kuwa wananchi wanapewa huduma kama inayostahili .

Mhandisi Imelda (TCRA) amewataka wananchi kutokusubiria mwishoni mwaka ambapo zoezi la usajili litafikia mwisho,bali wajitokeze mapema ili kuepusha msongamamo tarehe za mwishoni,kwani kwa mujibu wa Mhe.Rais Magufuli usajili utaenda hadi 31 desemba2019 .

Amesema changamoto zipo haswa kwenye upande wa NIDA kwani watu wengi wamejitokeza kwenye swala la kujiandikisha kupata vitambulisho vya uraia ambapo walilazimika kuwaomba mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA waweze kuwa na vifaa vya kutosha na wahudumu waongezeke kwani wananchi ni wengi na wengi hawana vitambulisho,wengi wamejiandikisha ila hawazikumbuki namba zao

Kwa upande wake Afisa msajili kutoka NiDa Juliety Robert amesema kuwa zoezi linaloendelea linalenga kuhamasisha wananchi wote ambao wana umri kuanzia miaka 18- kusajili laini  zao za simu .

Amesema kama inavyofahamika ni kwamba kila mtu anatakiwa aweze kusajili laini inamlazimu awe na kitambukisho cha Taiafa au namba ya kitambukisho hicho ili waweze kujisajili katika makampuni mbalimbali ya simu.

Amesema wanaendelea kuwahamasisha wananchi kujitokeze kwa wingi na wale ambao hawajawahi kujiandikisha waende kujiandikisha ili kuchukua fomu na taarifa nyingine za serikali za mtaa,kata,pia kuonana na Afisa Uhamiaji ndipo wakapige picha ndipo wasubirie  kupewa namba za kitambukisho cha Taifa ambazo watazitumia kusajili laini zao.

Aidha Afisa huyo kutoka NIDA amesema kwa wale ambao waliokwisha jiandikisha tangia awali wafike ili kuziangalia namba zao kama zipo tayari wazichukue kawajili ya kukamilisha usajili wa laini zao za simu,na kwa  wale ambao wamejiandikisha wakakwama wanaangalia ni wapi penye makosa ili waweze kurekebesha waendelew na zoezi.

WALIOJIFANYA MAOFISA TAKUKURU WAFIKISHWA MAHAKAMANI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

WAFANYABIASHARA wawili pamoja na Mkuu wa Kitengo cha mauzo cha Ramada Hoteli William Mgatta (36) wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la kujifanya maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kushawishi rushwa ya Sh. milioni 300.

Mbali na Mgatta washtakiwa wengine ni, ambao Mohammed Abdallah (25) na Daniel Ileme (35) ambao wote kwa pamoja wamesomewa mashtaka yao leo Juni 20,2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali, Aneth Mavika amedai kati ya Juni Mosi 2019, na Juni 10, mwaka huu, katika maeneo tofauti tofauti ya Jiji la Dar es Salaam na Arusha, mshitakiwa Abdallah na Ileme wakiwa wafanyabiashara na mshtakiwa Mgatta akiwa Mkuu wa Kitengo cha mauzo cha Ramada hoteli walishawishi rushwa ya Sh. Milioni 300 kutoka kwa Francis Matunda kama kishawishi ili wasimchukulie hatua za kisheria kwa kukataa kuwalipa wafanyakazi wake kiasi cha Sh. Bilioni moja.

Aidha imedawa siku na mahali hapo, washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa la kujifanya ni watumishi wa umma. Katika shtaka la tatu imedaiwa, Juni10, mwaka huu katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam na Arusha washtakiwa hao walijifanya kuwa ni watumishi wa Takukuru huku wakijua kuwa siyo kweli.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo imemtaka kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja, kuwalisilisha Sh.Milioni 50 au hati ya mali isiyohamishika ya kiwango hicho cha fedha.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Julai 4, mwaka huu.

APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUSAFIRISHA DHAHABU BILA KIBALI

$
0
0
Mkazi wa Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam, Mirajdin Tajdin (32), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka ya  kusafirisha dhahabu bila kuwa na kibali.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali Ester Martin amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega, kuwa, Wakili Martin alidai kuwa, April 30, 2019 huko katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, 
(JNIA) mshtakiwa alikutwa na vipande vya dhahabu vyenye uzito wa gramu 98, vikiwa na thamani ya USD  3636.92, sawa na Sh 8, 364,914 Mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo,  mshtakiwa alikutwa akisafirisha dhahabu hiyo bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka husika.

Mshtakiwa amekiri kutenda makosa hayo lakini amerudishwa rumànde kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka Serikali ya Mtaa, atakayesaini bondi ya Sh 8milioni.


Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na kesi hiyo itatajwa Julai 4, mwaka huu kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

TCRA wananchi watumie muda uliopangwa kujisajili kwa Kutumia alama za Vidole

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii,
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa wananchi watumie muda uliopo kujiandikisha kupata vitambulisho vya taifa ili waweze kusajili laini za simu kwa mfumo wa alama za vidole (biometria).

Kaimu Mkuu Kanda ya Mashariki wa TCRA, Jumanne Ikuja amesema ni vyema wananchi wakafahamu kuwa usajili wa simu ni kwa kutumia kitambulisho cha taifa pekee.

Ikuja amesema awali usajili wa simu ulitumia vitambulisho vya aina tano na kusababisha kuwepo kwa usajili holela na hivyo walishindwa  kudhibiti mawasiliano hayo.

Aidha amesema usajili huo utawasaidia kupata taarifa sahihi za watumiaji wa simu na kuondoa changamoto ya watu waliokuwa wanatumia vitambulisho vya ndugu, jamaa na marafiki pamoja na waliokuwa wanatumia laini bila kuzisajili.

"Lengo  kukomesha uhalifu wa mitandao hivyo tumejipanga hadi Desemba 31, mwaka huu  watanzania wote wawe wamesajili laini zao ili kupata huduma bora," amesema Ikuja.

Aliongeza kuwa wanafunzi waliochini ya miaka 18 ambao bado hawajapata vitambulisho vya taifa watatumia vitambulisho vya wazazi wao na kwamba pindi watakapofikia umri sahihi, watatakiwa kuboresha taarifa zao kwa kupitia mfumo huo.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (NIDA), Thomas Nyakabengwe amesema vitambulisho vya taifa ni muhimu kwani ndicho kinatambulisha uraia na kwamba huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi za serikali ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinahitaji mtu kuwa na kitambulisho hicho.

Nyakabengwe alisema hivi sasa mtu anayetaka kubadili umiliki au kumiliki ardhi anapaswa kuwa na kitambulisho hicho, kupata leseni ya biashara na kufungua kampuni.

Amesema mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa katika kupata vitambulisho hivyo kwa sababu ya kusajili laini hivyo wamejipanga kuhakikisha wanasogeza huduma kwa wananchi kadri itakavyowezekana ili wananchi wapate

Alisisitiza wanashirikiana na Idara ya Uhamiaji kuwatambua watanzania ili kukamilisha taratibu za kujiandikisha kupata vitambulisho hivyo.

Kwa upande wake, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kitengo cha Makosa ya Mtandao, Edga Massawe alisema usajili wa kutumia alama za vidole utawasaidia kuwapata watu wanaofanya makosa ya kimtandao na kuwachukulia hatua za kisheria.

Pia alisema usajili huo utawasaidia kuwabaini matapeli wanaotuma taarifa za kupitia mitandao mbalimbali kuomba fedha kwa watu.

Alisema pamoja na kuhamasisha usajili wa laini pia wanatoa elimu kuhusu  sheria ya mtandao ikiwemo makosa yaliyoainishwa pamoja na adhabu zake ili wananchi waweze kuepuka kujiingiza katika makosa hayo.
Kaimu Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Jumanne Ikuja akizungumza na waandishi wa habari wakati maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Wananchi wakipata huduma za usajili wa laini simu katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

SPIKA NDUGAI ATEMBELEA TIMU YA TAIFA STARS NCHINI MISRI

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amekutana jana na wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars katika kambi ya timu hiyo iliyopo nchini Misri.

Katika mazungumzo na wachezaji hao Spika alifikisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kuwataka vijana hao kupambana kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa katika mashindano ya Afrika yanayotarajia kuanza Juni 21 nchini Misri.
Spika aliwataka wachezaji hao kuingia uwanjani wakiwa wamejua wamebeba matumaini makubwa kwa Watanzania ambao macho na masikio yao wameyaelekeza kwao.

Kwa upande wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alimuahidi Spika kuwa wamepokea salamu za  Rais Magufuli na wamemuahidi kuwa wataingia uwanjani kupambana na kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa.
Alisema hawataki kumuahidi kitu kikubwa,ila watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha wanapambana na kupata ushindani katika mechi zote za makundi.

Serikali Kuajiri Wakaguzi wa Ndani 100

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege (Mb) amesema TAMISEMI imewasilisha maombi ya kupata kibali cha ajira ya Wakaguzi wa Ndani 100 ili kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi wa Kada hii katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. 

Mhe. Kandege ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Kazi wa Wakaguzi wa Ndani unaofanyika kwa siku mbili katika chuo cha Mipango Jijini Dodoma.
Kandege amesema Wakaguzi wa Ndani ni watu muhimu, Serikali inawaamini na inatambua mchango wao  katika usimamizi wa fedha na Uwajibikaji hivyo ni vyema rasilimali watu ikawa ya kutosha ili kazi hii iweze kufanyika kwa ufanisi.

“Napenda mfahamu kuwa Wakaguzi wa Ndani ndio Jicho la Kwanza la Serikali bila  ninyi Serikali haiwezi kuona vitu ambavyo vinavyotokea kwenye matumizi ya Fedha; Mmekua mkituonyesha yale yote yanayotendeka kinyume na matumizi stahiki yaliyoelekezwa hivyo ajira hiyo itakwenda kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi wa kada hii” Alisema Kandege.

Akizungumzia changamoto ya Ufinyu wa bajeti kwa vitengo vya ukaguziamesema  Serikali imeongeza bajeti za vitengo vya ukaguzi kutokaa shilingi 5.6 bilioni kwa mwaka wa fedha 2018/2019 hadi kufikia shilingi 6.4 bilioni kwa mwaka wa fedha 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 14.3.

“Ili kuleta tija na matokeo tarajiwa katika vitengo hivi Serikali itaendelea kuongeza bajeti ya rasilimali fedha ili muweze kujitegemea katika kutimiza majukumu yenu badala ya kutegemea fedha kwa wakaguliwa” Alisema Kandege.
Wakati huo huo Mhe. Kandege ameagiza Vitengo vya Ukaguzi wa Ndani kuhakikisha mianya yote ya ubadhilifu inabainishwa na kudhibitiwa kwenye mifumo ya kukusanyia mapato na usimamizi wa fedha. 

Pia aliziagiza Halmashauri zote kuhakikisha Hoja zote za CAG zinapatiwa majibu, kuhakikiwa na kufungwa, ushirikiano unatolewa kwa CAG na taratibu za kufunga hoja zinazingatiwa.
Halkadhalika  Mhe. Kandege alimpongeza aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Ndugu Mohamed A. Mtonga kwa kustaafu utumishi wa umma na kazi kubwa aliyoifanya katika kada hii ya ukaguzi.

“Ndugu Mohamed nakutakia Afya njema, naamini bado una nguvu za kuendelea kutoa mchango wako kwenye shughuli za kiuchumi za kujenga Taifa letu endelea kuwa Mwalimu kiongozi kwa wakaguzi wa ndani, ukiendelea kuwafundisha na kutoa ushauri, nakutakia kila la Kheri.  Alisema Kandege.

Akizungumza wakati wa Mkutano huo Karibu Mkuu OR-TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga amesema  kutokana na umuhimu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani fedha zilizotengwa kwenye bajeti kwa ajili ya Kitengo hiki zitalindwa na kuhakikisha zinatumika kwa ajili ya kazi za kitengo hiki pekee.
“Umefika muda sasa vitengo vya wakaguzi wa ndani kuimarishwa na Kila Mkoa na Halmashauri kuviwezesha vitengo hivi rasilimali fedha, watu na vitendea kazi vya kutosha wakati wote” Alisema Nyamhanga.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Ukaguzi na Ufuatiliaji Ofisi ya Rais TAMISEMI Miriam Mbanga amesema Mkutano wa kazi kwa wakaguzi wa ndani wa Mikoa na Halmashauri wa kwanza kufanyika na unalenga kujifunza, kubadilishana uzoefu, kushirikishana namna mbalimbali ya kutatua changamoto za kiukaguzi na kujiwekea malengo ya namna ya kufanya kazi ya ukaguzi wa ufanisi.

Mkutano huu umehudhuriwa na Wakaguzi wa Ndani zaidi ya mia moja na hamsini kutoka katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.  
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Josephat Kandege (Mb)  akifungua Mkutano wa Kazi wa Wakaguzi wa Ndani unaofanyika kwa siku mbili katika chuo cha Mipango Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga akitoa neno la utangulizia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kazi wa Wakaguzi wa Ndani unaofanyika kwa siku mbili katika chuo cha Mipango Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Ukaguzi na Ufuatiliaji OR-TAMISEMI Miriam Mbaga akieleza malengo ya Mkutano wakati wa ufunguzi wa akifungua Mkutano wa Kazi wa Wakaguzi wa Ndani unaofanyika katika chuo cha Mipango Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege akimkabidhi mfano wa hundi iliyotolewa kama zawadi kwa aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Serikali Ndg. Mohamedi Mtoanga iliyotolewa na Wakaguzi wa ndani wa Mikoa na Sekretariet za Mikoa.
 Wakaguzi wa Ndani wa Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakifuatilia Mkutano wa Kazi unaofanya katika chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

UBALOZI WA MAREKANI WAITWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akimsikiliza Mwakilishi wa Kaimu Balozi wa Marekani hapa Nchini Bi Ann Marie Warmenhoven – Tilias alipomwita Wizarani kutoa ufafanuzi kuhusu angalizo la kiusalama lilitolewa na ubalozi huo kupitia tovuti ya Ubalozi wa Marekani hapa Nchini June 20, 2019.

Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania ulitoa taarifa katika mitandao ya kijamii “Twitter” kuhusu angalizo la kiusalama “security alert”. Angalizo hilo la kiusalama lilitokana na uvumi unaodaiwa na ubalozi huo kusambaa kuhusu uwezekano wa kutokea kwa shambulio katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulimwita wizarani Kaimu Balozi wa Marekani ili kutoa ufafanuzi wa “twitter” yao. Ubalozi wa Marekani ulimtuma Mwakilishi wa Kaimu Balozi wa Marekani Bi Ann Marie Warmenhoven – Tilias kuonana na uongozi wa Wizara. 

Bi Ann Marie Warmenhoven – Tilias ameutambua na kukiri kuwa ujumbe huo umetumwa na ubalozi wa Marekani hapa nchini. Katika ufafanuzi wake amekiri kuwa Ubalozi umefanya makosa ya kutoa tetesi ambazo hazikuwalenga raia wa Marekani pekee bali raia wote wakitambua kuwa Ubalozi hauna mamlaka ya kufanya hivyo jambo lililosababisha taharuki kwa wananchi na wageni wanaotarajia kuitembelea Tanzania.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeukumbusha Ubalozi wa Marekani umuhimu wa kuzingatia sheria za nchi na taratibu za kidiplomasia zinazokubalika duniani kote katika utoaji wa taarifa za aina hii.

 Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe amewataka wananchi na Jumuiya za Kimataifa pamoja na wageni mbalimbali waliopo  nchini na wanaotarajia kuitembelea Tanzania kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani mpaka sasa hakuna taarifa yeyote iliyothibitishwa ya kuwepo kwa tishio la aina hiyo hapa nchini na kwamba Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimejizatiti kukabiliana na matishio yeyote.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
14 Juni 2019

UN KUSHIRIKIANA SERIKALI YA TANZANIA KUKOMESHA VITENDO VYA UKATILI WA JINSIA

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii.Kigoma

MRATIBU Mkazi umoja wa mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez amesema umoja wa mataifa uko tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto ambavyo hushusha utu wao.

Alvaro ameeleza vitendo vya ukatili si swala la Tanzania pekee ni swala la kiulimwengu hivyo mashirika mbalimbali yanapaswa kushirikiana kukomesha vitendo hivyo na kuwa wako tayari kuendelea kushirikia na serikali katika hilo.

Hayo ameyasema leo akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na mradi wa Kigoma Joints Program(KPJ) baada ya kukagua ofisi ya dawati la jinsia la polisi Mkoani Kigoma lililojengwa kwa ufadhili wa kupitia mradi wa Kigoma pamoja(KJP).

Pia ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Kigoma kwa ushirikiano wanaoutoa kwenye programu ya Kigoma pamoja na kusema wataendelea kuwa marafiki wa serikali ya Tanzania hususani Mkoa wa Kigoma.

Mwakilishi wa jeshi la polisi kutoka dawati la jinsia WP Anastazia Daud amesema kwasasa jamii imeendelea kuwa na mwamko wa kutoa taarifa matukio yanayohusiana na ukatili ambapo kwa wilaya ya Kigoma bado kumekuwa na matukio ya ukatili na mashambulio ya aibu.

"Kupitia elimu mbalimbali zinazoendelea kutolewa ssa hivi jamii imekuwa na mwitikio mkubwa wa kutoa taarifa ya matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto"alisema.Mkuu wa mkoa wa Kigoma mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga akahimiza jamii kuacha kuona aibu kutoa taarifa pindi zinapokumbana na unyanyasaji wa kijinsia.

"Wapo akina baba wanapigwa huko na kunyanyaswa na wake zao mje mtoe taarifa hapa malalamiko yenu yatafanyiwa kazi"alisema.

Maganga aliushukuru umoja mataifa(UN)kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na serikali kuleta mpango wa mradi wa Kigoma Joints Program(KJP)ulioanza mwaka 2017 na kuisha 2021 mpango huu unashirikisha katika maeneo ya afya,Elimu,Unyanyasaji wa kijinsia,mazingira.

"Mpango huu utasaidia kuendelea mkoa wetu wa Kigoma kwenye hizo nyanja ambazo zinagusa"alisema.Naye muelimishaji maswala ya kijinsia kutoka asasi ya kividea Vitalis Cosmas alisema kuna ushirikiano mdogo wa mwendelezo wa ufuatiliaji kwa wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
 Mratibu wa mashirika.ya wa umoja wa mataifa Tanzania Alvaro Rodriguez akipanda mti wa kumbukumbu nje ya ofisi ya dawati la kijinsia la Polisi Kigoma iliyojengwa kupitia mradi wa Kigoma Joints Program(KJP)
 Mkuu wa Mkoa Kigoma brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akitoa maelekezo kwa mafundi wanaojenga vizimba vya kuuzia katika soko la Kasulu linalojengwa kupitia mradi wa Kigoma pamoja

Ujenzi wa vizimba vya kuuzia kwa ufadhili wa mradi wa Kigoma pamoja katika soko la Kasulu unaendelea.

TPDC YAMPA TUZO PROF. MARK MWANDOSYA

$
0
0


HIVI Karibuni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), lilifanya Maadhimisho ya Miaka 50. Ambapo mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa Mh. Majaliwa Kassimu Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye aliwakilishwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuuu- Uwekezaji Mhe. Angela Jasmine Kairuki. Pamoja na Maadhimisho hayo, TPDC ilitoa TUZO kwa baadhi ya WASTAAFU waliokuwa na michango mbalimbali katika utumishi wao. Pichani juu Bi Marie Msellemu, MKUU wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TPDC, akimkabidhi Prof. Mark Mwandosya TUZO ya kuutambua mchango wake mkubwa kwa TPDC kwa nafasi yake kama Kamishna wa kwanza wa Petroli nchini na Mwenyekiti wa BODI ya Shirika la TPDC katika utumishi wake.
Picha ya pamoja.

MPAKA SASA HAKUNA TISHIO LA KIGAIDI NCHINI-IGP SIRRO

RC CHALAMILA ANGILIA KATI MGOGORO WA MADIWANI NA MKURUGENZI KYELA, ATAMKA MAZITO


HIVI NDIVYO UBALOZI WA MAREKANI ULIVYOITWA WIZARA MAMBO YA NJE

WAKALA WA VIPIMO YASISITIZA MATUMIZI YA VIPIMO SAHIHI KATIKA UNUNUZI WA ZAO LA PAMBA TABORA

$
0
0

Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Tabora inaendelea kufanya uhakiki wa mizani ya vyama vya msingi vya ushirika pamoja na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo katika Wilaya mbalimbali za mkoa wa Tabora ili kuweza kuwalinda wakulima wa zao la pamba waweze kupata faida kwa kuuza mazao yao (pamba) kwakutumia vipimo mizani sahihi iliyohakikiwa na wakala wa Vipimo.

Meneja wa WMA Tabora ndugu Mrisho Mandari, amesema kuwa mpaka sasa Wakala wa Vipimo Tabora imeshafanya uhakiki wa mizani ya vyama vya msingi vya ushirika katika Wilaya tano za Mkoa wa Tabora ambazo ni Igunga, Nzega, Uyui, Urambo pamoja na Kaliua. Katika wilaya zote Jumla ya Mizani 158 imehakikiwa na Wakala wa Vipimo na kusambazwa katika vituo vyote vya kununulia pamba Mkoani hapo.

Amesema kuwa, Kati ya Mizani 158 iliyohakikiwa jumla ya mizani 130 ilipitishwa haikubainika kuwa na tatizo lolote, na mizani 18 ilikutwa na hitilafu ndogo ndogo ambapo baadaye zilirekebishwa na 16 kati ya hizo zilifikia wigo wa usahihi. Mizani miwili ilikataliwa kabisa kutumika kutokana na matatizo yake kuwa makubwa.

Ndugu Mrisho Mandari, amesema kuwa mara baada ya kukamilisha uhakiki wa mizani ya vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS), sasa wanatoa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa Wakulima wa pamba na wanachi wote kwa ujumla ili waweze kutambua mambo muhimu ya kuzingatia mara wanapoenda kuuza pamba katika vituo maalumu vilivyoandaliwa.

Pia, amewaasa wakulima wawe makini pindi wanapoenda kuuza pamba kwa kuhakikisha mizani inasoma sufuri (0) kabla ya kuanza upimaji kwa kutumia mizani ya digitali. Mara baada ya kupima furushi la pamba mizani inatakiwa kurudi katika sufuri, na wahakikishe mizani haisomi hasi (-) baada ya kutoa mzigo na ikitokea imesoma hasi mwambie karani  anayesimamia mizani aweze kuizima na kuiwasha tena mizani hiyo kisha zoezi la upimaji liendelee.

Wakala wa vipimo inaendelea kuboresha ulinzi katika mizani zinazotumika katika ununuzi wa zao la pamba, kwa mizani iliyohakikiwa na kukudhi vigezo inawekewa stika maalumu ya Wakala wa Vipimo pamoja na kufunga lakiri katika maeneo muhimu ya mizani ili kuzuia mizani isije ikachakachuliwa na wanunuzi wa pamba wasio waaminifu.

Vilevile, amewataka wanunuzi wa pamba waweze kujiepusha na viendo vya dhuruma kwa wakulima wa pamba kwa kutumia mizani ambazo hazija hakikiwa na kupata idhini ya kutumika katika msimu wa ununuzi wa pamba. Amewakumbusha kuwa kwa sasa sheria ya vipimo sura na. 340 na mapitio yake ya mwaka 2002 imefanyiwa marekebisho na adhabu zimekuwa kali ambapo ukikutwa na kosa la kuchezea mizani na ukakiri faini yake ni kiasi kisichozidi shilingi milioni ishirini (20,000,000/=) kwa kosa la kwanza na kiasi kisichozidi milioni hamsini (50,000,000/=) kwa mkosaji wa kosa la kujirudia.

Zoezi hili la uhakiki wa mizani na utoaji elimu kwa wakulima wa pamba ni zoezi endelevu ambalo hufanyika mara kwa mara ili kuwalinda wakulima wa pamba na hufanyika kabla ya kuanza kwa msimu wa ununuzi wa pamba na mara baada ya kuanza kwa msimu maafisa vipimo hupita katika vituo mbalimbali vinavyotumika kununulia pamba na kujiridhisha kama mizani inatumika kwa usahihi bila kupunja kama ilivyo hakikiwa.

Wakala wa vipimo inatoa wito kwa Wafanyabiashara na Wakulima wote kuhakikisha wanazingatia matumizi ya vipimo sahihi na kujiepusha na uchezeaji wa vipimo na endapo mkulima utakutana na udanganyifu wa aina yeyote atoe taarifa katika ofisi zetu za wakala wa vipimo zilizopo makao makuu ya mikoa yote Tanzania Bara au kupitia namba yetu ya bure kabisa ambayo ni 0800 11 00 97.
 Meneja wa Wakala wa Vipimo Tabora akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mizani kwa Wakulima wa kijiji cha Mtunguru waliokuja kuuza pamba zao katika Chama cha msingi cha ushirika cha Nguzujise
 Afisa Vipimo Mkoa wa Tabora akihakiki usahihi wa mizani inayotumika kununulia pamba kwa kutumia jiwe maalumu la Wakala wa Vipimo
 Afisa Vipimo Mkoa wa Tabora akihakiki usahihi wa mizani inayotumika kununulia pamba kwa kutumia jiwe maalumu la Wakala wa Vipimo
 Wananchi wakioneshwa alama za kukagua ili kubaini usahihi wa mizani kabla ya kuuza pamba

CHONDE CHONDE UBALOZI WA MAREKANI ANGALIENI MFUMO WENU WA KUTOA TAARIFA ZA USALAMA WA NCHI...USHAURI WANGU KWA VIONGOZI WA TANZANIA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

NIELEZE mapema tu Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania utoaji wa hii taarifa yenu ya tishio la shambulio la ugaidi haiko sawa hata kidogo.Mnashangaa nini!

Jana jioni kupitia mitandao ya kijamii ubalozi huo ulitoa taarifa ukidai kuna tishio la kufanyika ugaidi nchini Tanzania.

Iko hivi Juni 19, kwenye saa 19:19 ya jioni ndipo ubalozi huo ukatoa taarifa ya kwamba kuna tetesi ya kutokea shambulio la ugaidi eneo la Masaki na hasa maeneo ya hoteli na migahawa inayotumiwa mara nyingi na watalii.

Taarifa hiyo ilitolewa kupitia akaunti ya Twitter ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania .Hata hivyo ubalozi huo umekiri kuwa haina ushahidi wa kuwepo kwa tishio hilo na muda ambao mashambulizi yatafanyika na inawataka wananchi kuchukua tahadhari.

Binafsi nimeshtushwa sana na taarifa ya Ubalozi wa Marekani.Sio kwamba nimeshtushwa kwa sababu naogopa magaidi, Hapana nimeshtuka kwa sababu aina ya utolewaji wa taarifa yenyewe.Kwa ubalozi kama wa Marekani kweli umeshindwa kufuata taratibu za kutoa taarifa.

Nafahamu kuna mjadala unaoendelea kwenye maeneo mbalimbali ya mijadala ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii.Kuna ubishi unaendelea kati ya pande mbili.Wapo wanaosema taarifa hiyo iko sawa na wengine haiko sawa.Kila mmoja anatoa sababu zake wapo wanaosema taarifa hiyo ya tahadhari ifanyiwe kazi kama sehemu ya kujihami na shambulio na wapo wanaosema sio sawa maana inaonekana kuna ajenda nyuma yake.

Kwa ujinga wangu sitaki kuwa kwenye kundi lolote kati ya hao wanaobishana kama Ubalozi wa Marekani uko sahihi au sio sahihi kwenye kutoa hiyo taarifa.Kwangu taarifa ya Marekani inanipa tafakuri kichwani.Tafakuri yenye maswali lukuki.Ndio, hata hivyo najiuliza hivi kweli Ubalozi wa Marekani umeshindwa kutambua kama Tanzania ni nchi huru na ina utaratibu wake wa kutoa taarifa kwa Watanzania na wasio Watanzania.

Sawa wamepata taarifa ya tishio la shambulio kupitia minong'ono, hivi ni kweli wameshindwa kuwasiliana na vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania kufikisha hiyo minong'ono yao.Sitakai Marekani ni miongoni mwa nchi ambazo ziko vizuri kwenye masuala ya ulinzi lakini wakati huo huo sina mashaka na Tanzania yangu kwenye masuala ya ulinzi.Tuna vyombo vya kutosha ambavyo vinaauwezo mkubwa wa kushughulika na taarifa zikiwemo hizo za matishio.

Kwa ujinga wangu nahisi Ubalozi wa Marekani una ajenda zaidi ya hiyo, Wana ajenda zaidi ya hiyo taarifa ya tishio la shambulio.Tuwasiwapuuze kwa upande wa kushoto lakini wapuuzwe kwa upande wa kulia.Ninazo sababu lakini itoshe kueleza huenda kitu ambacho wanakitafuta kwa Tanzania.Tuwe makini nao.Nitakataa leo na kesho utaribu ambao wameutumia haukuwa sahihi hata kidogo , narudia tena kusema zipo taratibu kwa kila nchi kufikisha taarifa.Unapozungumzia shambulio la ugaidi unazungumzia usalama wa nchi.Unaposhughulika na usalama wa nchi lazima taratibu zifuatwe na ndio sahihi. 

Nawaza ujinga tu kichwa kwangu kwa kujiuliza vimaswali ambavyo havina kichwa wala miguu.Kwa mfano najiuliza tu hivi Ubalozi wa Tanzania uliopo kwenye nchi yoyote ile unaweza kutoa taarifa ya tishio la usalama kwenye nchi husika bila hata kutoa taarifa kwa wenye nchi?Baada ya kusambaza taarifa wamechukua hatua gani? Kwa kweli taarifa hizo za tishio lina madhara makubwa sana katika nchi yetu.

Weka akilini na kisha fuatilia pole pole kuanzia jana na hasa kwenye sekta ya utalii .Kwangu naamini kuna uwezekano mkubwa wa kupungua kwa idadi ya watalii wanaokuja nchini Tanzania.Wanawezaje kuja kwenye nchi ambayo imetolewa tahadhari ya shambulio la ugaidi.Najiuliza, ni kweli Ubalozi wa Marekani hauoni jitihada za Serikali ya Tanzania katika kuhamasisha utalii? Wameliangalia hilo kwa mapana yake au wameangalia tu taarifa za minong'ono ya tishio la shambulio?

Wakati naendelea kutafakari , kuna jamaa yangu mmoja akaniambia hiyo taarifa ya Marekani sio kwetu tu bali imetolewa kwa nchi ya Uganda.Nikamjibu sawa lakini hizi ni nchi mbili tofauti na kila mmoja inao utaratibu wake wa kutoa taarifa hasa zinazohusu usalama wa nchi.

Nitoe rai kwa viongozi wa Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha inakuwa makini katika kuzungumzia taarifa hiyo ya tishio ambayo imetolewa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania. Nashauri hakuna sababu ya kutumia nguvu kubwa kujibu walichokieleza. Hakuna sababu ya kulumbana nao na wala hakuna sababu ya kubishana. Kikubwa na ndicho naamini mmeisoma hiyo taarifa. Mmeona ambao ubalozi huo unawaza.

Marekani ni marafiki zetu wa muda mrefu, hivyo tunapaswa kwenda nao kwa urafiki hivyo hivyo lakini tukitambua huenda kuna maeneo hatuko pamoja.Kwa upande wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, nitoe ombi kwenu, mnayo nafasi ya kuwasiliana na vyombo vyenye mamlaka pale mnapoona kuna jambo ambalo linagusa usalama wa nchi.Ni uungwana tu na ninafahamu mawasiliano ya vyombo vya ulinzi na usalama au mawasiliano ya wenye mamlaka mnayo.

Yatumieni kufikisha taarifa.Tanzania haina ugomvi wa aina yoyote na Marekani na wala haitarajii kuingia kwenye malumbano.Ni vema kila mmoja akaheshimu mwingine. Watazania kwa umoja wao wako tayari kutoa ushirikiano kukabiliana na ugaidi nchini na kupitia Serikali yao walishakubali kusaini makubaliano ya kupambana na ugaidi.

Kwa wananchi , naomba niwaeleze tunayo nafasi ya kusikiliza kila tunachoambiwa aidha kupitia vyombo vya habari au kwenye maeneo yetu ambayo tunayatumia kupeana taarifa.Lakini ni wakati sahihi kuhakikisha taarifa ambayo unaipata unaifanyia kazi na kisha kusikiliza mamlaka inasemaje.Tunaweza kutumia nguvu kubwa ya kujihami na shambulio kiasi cha kukwamisha shughuli za kimaendeleo za kila siku.Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania chonde chonde angalieni mfumo wa namna ya utoaji taarifa hasa zinazohusu usalama wa nchi

SERIKALI YA TANZANIA YAJIPANGA KUTEKA SOKO LA WATALII CHINA

$
0
0
Naibu wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi ya vitabu kutoka TANAPA ikiwa ni ishara ya shukrani kwa Mkuu wa kitengo cha mafunzo wa chuo cha JXCFFS, Yang Jing mara baada kufanyika mkutano uliolenga kuimarisha ushirikiano katika ya China na Tanzania jijini Dodoma.
Makamu wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS Prof.Xiong Nanyong ( wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya picha ya Chuo hicho Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bw. Lucius Mwenda mara baada ya kufanyika mkutano mara baada kufanyika mkutano uliolenga kuimarisha ushirikiano katika ya China na Tanzania jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza jambo na Viongozi wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS mara baada ya kuwatambulisha wageni hao Bungeni Dodoma leo waliokuja nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wa mafunzo watumishi na wadau wa utalii nchini
Naibu wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akikabidhiwa zawadi ya pichana Makamu wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS Prof.Xiong Nanyong ( wa pili kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa mafunzo ya chuo hicho ,Wanga Jiaxin leo katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma
Naibu wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akikabidhiwa zawadi ya pichana Makamu wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS Prof.Xiong Nanyong ( wa pili kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa mafunzo ya chuo hicho ,Wanga Jiaxin leo katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma

**************

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kwa sasa muelekeo wa soko la Utalii nchini umelenga kupata watalii wengi kutoka nchini China na kama Wizara inayoshugulikia masuala ya Utalii, suala la kujifunza lugha ya kichina kwa baadhi ya watumishi na wadau wa utalii ili kuteka soko hilo ni jambo lisiloepukika.

Imesema nguvu nyingi kwa sasa zinaelekezwa nchini China hivyo ni muda muafaka wa kuandaa timu ya wataalamu mbalimbali wakiwemo waongoza watalii watakaoweza kuzungumza lugha ya kichina ili kuweza kulimudu soko hilo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS


Amesema lengo mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya
China na Tanzania katika suala la kuwajengea uwezo watumishi na wadau wa Utalii nchini.Mkutano huo umehudhuriwa na ujumbe kutoka China ukiongozwa na Makamu wa Chuo hicho,Prof.Xiong Nanyong,Kaimu huku kwa upande wa Wizara Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.Lucius Mwenda pamoja na ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara.

Amesema ni muhimu kwa watumishi wa wizara pamoja na wadau wa utalii kujiandaa ili kuweza kuzungumza lugha ya kichina badala ya vifaa maalum vya kutafsiri lugha ilhali kuna uwezekano kwa Watanzania kujifunza.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Xiong Nanyong amesema wamejipanga kutoa mafunzo mbalimbali likiwemo suala la lugha ya kichina pamoja na utalii ili kuwajengea uwezo Watumishi hao.Ameongeza kuwa tayari wameshaomba kibali kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa umma na Utawala Bora kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Lucius Mwenda ameahidi kutoa ushirikiano kwa Uongozi wa Chuo hicho ili kujengeana uwezo baina ya Serikali ya Tanzania na China

NAIBU WAZIRI OLE NASHA ATAKA WATOTO KULINDWA NA KUWEZESHWA ILI WAWEZE KUSHIRIKI FURSA MBALIMBALI ZA ELIMU

$
0
0

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afirika yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam Juni 20, 2019 
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha,akichangia mjadala wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Afrika yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipokea risala kutoka kwa mmoja wa watoto walioshiriki Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Jijini Dar es Salaam. 

………………………. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amesema Serikali inatambua na kuthamini umuhimu wa mtoto wa kitanzania na ndio maana imekuwa ikizifanyia kazi haki za msingi za mtoto ili aweze kuishi katika mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kupata elimu. 

Naibu Waziri Ole Nasha ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaiwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF) ambapo amesema watoto wanapaswa kulindwa na kuwezeshwa ili waweze kushiriki katika fursa mbalimbali zilizopo kwenye elimu. 

Amesema maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanatoa fursa ya kujadili changamoto na fursa katika kuhakikisha kuwa haki za mtoto zinalindwa na kwamba Serikali imefanya jitihada kubwa na za makusudi katika kuhakikisha kuwa watoto wanapata haki zao za msingi katika jamii zetu za kitanzania. 

Ole Nasha amezitaja jitihada hizo kuwa ni pamoja na kuridhiwa kwa mikataba mbalimbali ya Kimataifa inayolinda haki za watoto, kutunga sheria zinazolinda haki za watoto dhidi ya uonevu na ubaguzi wowote na pia imepitisha Sera zinazowalinda na kuwapatia fursa watoto. 

Jitihada nyingine ni pamoja na ujenzi wa shule karibu na makazi ya watu ili kupunguza watoto kutembea umbali mrefu, ujenzi wa mabweni na pia mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuweka mkazo juu ya stadi za maisha, elimu ya afya ya uzazi na ujinsia katika shule za msingi na sekondari na vyuo vya ualimu. 

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ole Nasha ameutaka umma kutambua kuwa jukumu la kuwaendeleza watoto kielimu ni la kila mmoja wetu na kwamba ifahamike kuwa watoto wa kike na wa kiume wote ni sawa, hivyo hatuna budi kuwapunguzia watoto wa kike mzigo wa kazi za nyumbani ili wapate muda wa kujisomea sawa na ilivyo kwa watoto wa kiume. 

Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa Juni 16 ya kila mwaka ambapo kwa mwaka 2019 maadhimisho hayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Geita na yalikuwa na Kauli Mbiu isemayo “Mtoto ni Msingi wa Taifa Endelevu: Tumtunze, Tumlinde na Kumuendeleza”.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images