Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

TCRA yazindua Maadhimisho wiki ya Utumishi wa Umma Arusha

$
0
0
Thadayo Ringo (kulia)Mkuu wa Kitengo kinachoshughulikia maswala ya watumiaji huduma na bidhaa za mawasiliano (TCRA) Rolf kibaja mtaalamu wa maudhui TCRA .


Na.Vero Ignatus, Arusha.
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA imezindua wiki ya huduma kwa mteja katika chuo cha uhasibu Njiro ikiwa sehemu ya kuielimisha jamii kwa kushirikiana na watoa huduma za simu za mkononi.



Thadayo Ringo ni mkuu wa kitengo kinachoshughulikia maswala ya watumiaji huduma na bidhaa za mawasiliano (TCRA) amesema dhima ya wiki ya utumishi wa umma  imesimama kuhakikisha jinsi gani Taasisi za Umma zinawezesha vijana kujiajiri pamoja na kuangalia muingiliano  wa uhamiaji kutoka vijijini kwenda mjini 


 Amesema kuwa wanaangalia  jinsi gani wanaweza kuikumbatia Teknolojia katika kusaidia utekelezaji wa utoaji huduma jumuishi  na kuhakikisha kwamba wanajenga utamaduni wa utawala bora.

Amesema katika kuzingatia hayo TCRA ilichagua mikoa 5 ambayo inaadhimisha siku hiyo ambapo ni pamoja na Arusha,Mwanza Mbeya Dar es saalam, Dodoma  ambapo wapo kwaajili ya kufanya kampeni ya kusajili watu wanaotumia  huduma za simu za mkononi kwa kusajili line zao kwa kutumia alama za vidole .

Ringo ametaja changamoto kubwa wanayokutana nayo ni pamoja na watu wengi kufikiria kwamba zoezi hilo linalengo la kuchuliwa alama za vidole,bali wao wanahakiki taatifa kwa kutumia alama za vidole,ambapo wengi wanasita kujidikisha.

Aidha amesema katika kipindi chote hicho wananchi wanaalikwa kuwatembelea,na wao wapo tayari kujibu maswali mbalimbali ambapo amesema kuwa tangia zoezi hilo limeanza muamko ni mkubwa na amesisitiza kuwa kabla ya kufika disemba watakuwa wameweza kukamilisha zoezi hilo kwa asilimia kubwa.Picha na Vero Ignatus.

Wanafunzi wa chuo cha uhasibu Njiro wakiwa kwenye foleni ya kuchukua namba ya kitambulisho cha Taifa kwaajili ya kusajili laini kwa mfumo wa Biometric ambapo zoezi hilo limefanyika siku mbili chuoni hapo na siku tatu watakuwa katika soko la kilombero .Picha na Vero Ignatus
Mmoja wa Afisa kutoka NIDA Julieth Raymond,akimsaidia kuelewa.mmoja ya mteja aliyetembekea banda hilo kwaajili ya kupata kitambulisho cha Kitaifa katika chuo cha uhasibu kilichopo Njiro Arusha.Picha na Vero Ignatus..

Wanafunzi wa chuo cha uhasibu Njiro wakiwa kwenye foleni ya kuchukua namba ya kitambulisho cha Taifa kwaajili ya kusajili laini kwa mfumo wa Biometric ambapo zoezi hilo limefanyika siku mbili chuoni hapo na siku tatu watakuwa katika soko la kilombero .Picha na Vero Ignatus.
Mmoja wa wafanyakazi kutoka NIDA akinsaidia mteja aliyefika kupatiwa huduma ya kitambulisho cha Taifa.Picha na Vero Ignatus.


MASAUNI ATEMBELEA MRADI WA NYUMBA ZA POLISI KUNDUCHI,MIKOCHENI NA KITUO KIPYA CHA POLISI OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akiongozana na wataalamu kutoka Kikosi cha Uzalishaji cha Jeshi la Polisi na Wasimamizi wa Mradi kutembelea   eneo la Kunduchi ambako  Mradi wa  Nyumba Mia Tatu Thelathini za Makazi ya Polisi zinazoonekana pichani  zikiwa  zishakamilika.Ziara hiyo imefanyika  jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Mussa Taibu, akimuelekeza jambo  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kutembelea eneo la Mikocheni ambako  kumejengwa  nyumba  zinazoonekana  pichani  ikiwa ni makazi kwa ajili ya  askari  polisi. Ziara  hiyo  imefanyika  jijini Dar es Salaam.
 Kamanda  wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Mussa Taibu, akitoa taarifa  ya hali ya uhalifu katika mkoa wake kwa   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati naibu waziri alipofika kituo cha polisi Oysterbay. Ziara hiyo imefanyika  jijini Dar es Salaam.
Naibu  Waziri  wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni  akisalimiana  na  Kamanda  wa  Polisi  Mkoa  wa  Kipolisi Kinondoni, ACP Mussa Taibu, baada  ya  kuwasili  kwa ziara ya kikazi katika Mradi wa Ujenzi wa Kituo  Kipya  cha  Polisi  Oysterbay. Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mwanza, Songwe kucheza nusu fainali kesho UMISSETA Soka wavulana

$
0
0
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Michuano ya UMISSETA inayoendelea mjini Mtwara imefikia hatua ya nusu fainali kwa upande wa soka wavulana ambapo katika michezo iliyomalizika leo jioni, timu za soka wavulana kutoka mikoa ya Lindi, Ruvuma, Mwanza na Songwe zimefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuwalaza wapinzani wao akiwemo bingwa mtetezi Tanga ambayo ilitolewa na Lindi.

Kwa matokeo hayo timu ya soka wavulana kutoka mkoa wa Lindi itakutana na Ruvuma kwenye nusu fainali ya kwanza inayotarajiwa kucheza kesho saa nane mchana na kufuatiwa na nusu fainali ya pili itakayowakutanisha vigogo Mwanza watakaochuana na timu ngumu ya Songwe.

Timu ya kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ilikuwa ni timu machachari ya kutoka  mkoa wa Lindi ambayo iliitoa timu ya mkoa wa Tanga kwa penati 3 kwa 1 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana baada ya dakika tisini za mchezo.

Pambano lingine la robo fainali lilizihusisha timu za kutoka mikoa Ruvuma na Kilimanjaro ambapo timu ya soka ya mkoa wa Ruvuma ambayo inaundwa na wachezaji 8 kutoka kwenye kituo cha michezo cha shule ya sekondari Ruhuwiko iliyopo nje kidogo ya Manispaa ya songea iliwafunga timu ya Kilimanjaro kwa magoli mawili kwa bila.

Katika mechi zilizomalizika jioni hii timu za Songwe na Manyara na Mbeya na Mwanza zilimenyana vikali katika michezo mingine ya robo fainali ambapo Songwe waliwalaza Manyara kwa goli moja kwa sifuri na Mwanza waliifunga Mbeya kwa magoli ya penati 5 kwa 3 ya Mbeya baada ya timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za mchezo.

Hata hivyo Mwanza walikuwa na kila sababu ya kushinda mchezo huo kwani kwenye dakika ya 72 walikosa goli la wazi baada ya penati yao kupanguliwa na golikipa wa Mbeya Gerald Hatson na kuokolewa na mabeki wa timu hiyo.

Mara baada ya mchezo huo, Kocha wa Mwanza Mwalimu Tito Mkami amesema kuwa vijana wake walipambana kufa na kupona lakini akawasifu timu ya Mbeya kwa namna ilivyowasumbua na akakiri kuwa  timu hiyo ngumu kwani iliwapa wakati mgumu wachezaji wake wakati wote wa mchezo.

Aidha Mwalimu Mkami alitoa wito kwa Chama cha soka nchini TFF kutoshirikisha mashindano mengine pindi michuano inayoandaliwa na serikali ya UMISSETA na UMITASHUMTA inapofanyika ili kutosababisha michuano hii kukosa wachezaji muhimu kwa timu zao

Naye nahodha wa timu ya soka ya Mwanza Kimwaga Kalunga ambaye ni Mwanafunzi pekee anayechezea timu hiyo kutoka shule maalum ya soka ya Alliance ambaye alisema kuwa hawaihofii timu ya Songwe bali wanaiheshimu kwani timu zote zilizoingia hatua hiyo ni ngumu.

Mapema kesho asubuhi michezo ya nusu fainali kwa upande wa soka wasichana itachezwa katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara ambapo mchezo wa kwanza utawakutanisha wababe Dar es salaam watakaotoana jasho na timu kutoka mkoa wa Iringa, na mchezo mwingine utawakutanisha miamba Mwanza watakaochuana na Ruvuma.

Kwa upande wa mpira wa mikono matokeo ya robo fainali ya mchezo huo iliyochezwa leo jioni inaonyesha kuwa timu za Geita  na Unguja wavulana zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali na zimepangwa kucheza kesho, huku nusu fainali nyingine itawakutanisha Tanga na Morogoro.

Katika mpira wa mikono wasichana, timu zilizofuzu ni Unguja ambao watakuna kesho na Morogoro na Songwe watakaocheza na Mbeya.

Mchezo mwingine ambazo timu zilizofuzu zimejulikana ni netiboli ambapo timu za Morogoro, Tanga, Dar es salaam na Mwanza zimefuzu hatua hiyo ambapo michezo hiyo itachezwa kesho kwa Tanga kukutana na Mwanza na Morogoro kucheza na Dar es salaam.

Katika mchezo wa kikapu kwa upande wa wavulana timu zilizofuzu hatua ya nusu fainali ni Pwani, Unguja, Tanga na Shinyanga ambapo kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa Pwani itacheza na Unguja na Tanga itachuana na Shinyanga.

Kwa upande wa  mpira wa kikapu wasichana Kilimanjaro itamenyana na Mwanza na Morogoro watacheza na jirani zao Dar es salaam.
 Makamu mwenyekiti wa FEASA bwana Kariuki Gikonyo ambaye alikuwa mgeni rasmi wa pambano la robo fainali kati ya Mbeya na Mwanza akiwa sambamba na Mwenyekiti wa mashindano ya UMISSETA  Bwana Aaron Sokoni (mwenye kofia) wakiangalia mechi hiyo jana iliyofanyika kwenye uwanja wa chuo cha ualimu Mtwara.
 Mchezaji wa mpira wa volleyball kutoka Tabora Charles Idrisa akipiga smash kuelekea upande wa timu ya mkoa wa Mbeya kwenye mchezo wa nusu fainali ambapo Tabora waliifunga Mbeya kwa seti 2 kwa 1
 Beki wa kulia wa timu ya soka ya Mbeya Idrisa Hamidu akiondoa mojawapo ya hatari iliyoelekezwa kwenye eneo la lango la timu yake kutoka kwa washambuliaji hatari wa mkoa wa Mwanza wakati wa pambano la robo fainali baina ya timu hizo mbili.
 Baadhi ya watazamaji wakifuatilia mojawapo ya mechi za robo fainali zilizofanyika leo mjini Mtwara.
Wachezaji wa timu za mkoa wa Morogoro wakichuana vikali na wenzao wa shinyanga kwenye mchezo wa kikapu wavulana hatua ya robo fainali ambapo shinyanga walishinda pambano hilo.

TCRA: Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole unaruhusiwa zaidi laini unazohitaji kwa mtandao Mmoja

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Katika kuadhimisha wiki ya Utumishi kwa Umma Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Kanda ya Mashariki kwa kushirikiana na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa  NIDA pamoja na kitengo cha polisi makosa ya mtandaoni wamefungua kituo cha pamoja kwa lengo la kuwarahisishia wananchi usajili laini  za simu kwa kutumia alama za vidole Kadri wanavyohitaji kwa mtandao mmoja kusajili zaidi ya laini mbili ikiwa unahitaji laini hizo.

Sambasamba na hilo wageni nje ya nchi kuanzia miezi sita wanatakiwa wajisajili NIDA kwa makazi ya muda huku wale wanaongia na  hawezi kukaa muda mrefu watatumia hati zao za kusafiria. 

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye maadhimisho hayo  Kaimu Mkuu wa TCRA Kanda ya Mashariki Mhandisi Jumanne Ikuja amesema kuwa usajii huo wa kitambulisho cha taifa ni kuondokana na utitiri wa vitambulisho vingi ambapo baadhi ya watu walitumia vibaya kwa kuwa na laini zingine kufanya uhalifu.

Amesema mfumo utakomesha uhalifu licha mtu kuwa na laini zaidi moja katika mtandao Mmoja ukomesha wizi wa mtandaoni kutokana na taarifa zake akifanya uhalifu atafikiwa tu.

Aidha amewata wananchi wanaopoteza vitambulisho vyao kuhakikisha kuwa wanaripoti polisi ili kuweza kurudishiwa vitambulisho vingine katika kuepuka  kutumiwa kwenye matukio ya kihalifu.

Mhandisi Ikuja  amewasisitiza wananchi kufika katika viwanja vya mnazi ili kupatiwa huduma mbalimbali zinazohusiana na Mawasiliano kwani zoezi hilo ni la wiki moja kuanzia Juni 17- 21 mwaka huu.

Kwa upande wake  Mkaguzi Msaidizi wa polisi Kitengo Cha makosa ya mtandaoni Inspekta Edga Masawe amewatahadharisha wa anchi kuacha kutumia simu ambazo wamezinunua kiholela haswa kutoka kwa watu pamoja na zile wanazoziokota ikiripotiwa ni unachukuliwa kama mhalifu.

Hata hivyo amesema kuwa kupitia maadhimisho ya wiki ya utumishi watatoa elimu kwa wananchi kuhusu sheria za mtandaoni pamoja na  madhara ya matumizi mabaya ya mtandao ikiwemo matumizi ya lugha isiyokuwa na staha na picha zisiokuwa na maadili na maneno ya uchochezi.

 Mwananchi akiweka alama za vidole katika kukamilisha usajili wa laini ya simu.
 Kaimu Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Jumanne Ikuja  akitoa maelezo kwa mwananchi wakati waliotembelea banda lá TCRA katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika utoaji na elimu ya Mawasiliano Pamoja usajili wa laini za simu katika kituo kimoja ndani ya Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa katika foleni katika banda la NIDA kufanya Usajili wa kupata kitambulisho cha Taifa.
 Huduma za usajili na maelezo yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja

SEKTA YA NISHATI NCHINI IPO IMARA, WAWEKEZAJI WAKARIBISHWA KUWEKEZA

$
0
0
*Dkt. Kalemani aeleza kuwa shilingi bilioni 64 zimetengwa kwa ajili ya marekebisho kwa maeneo yanayokatika umeme kuanzia Julai mwaka huu

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa  sekta ya nishati nchini imeimarika zaidi kuanzia mwaka 2015 hadi sasa ambapo idadi ya viwanda, wateja na upelekaji wa umeme vijijini umeimarika kwa kasi zaidi na hiyo yote ni kutokana na kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli hasa kwa kuweka mikakati mizuri kwa wenye viwanda.

Akizungumza wakati wa kikao kilichokutanisha wizara ya nishati na jumuiya ya wamiliki wa viwanda nchini Dkt. Kalemani amesema kuwa kikao hicho kimelenga kusikiliza na kutatua kero na changamoto za wenye viwanda na kueleza kuwa ili sekta ya viwanda iendelee lazima wadau wahusishwe na hiyo ni mara ya nne kwa wadau kukutana.

Kalemani amesema kuwa uwepo wa nishati ya uhakika kumepelekea viwanda kuongezeka kutoka viwanda 2800 mwaka 2015 hadi zaidi ya viwanda zaidi ya 5200 mwaka huu huku wateja wa nishati ya umeme wakiongezeka kutoka milioni 1.4 hadi wateja milioni 2.45.

Kuhusiana na upelekaji wa umeme vijijini waziri Kalemani amesema kuwa vijiji  zaidi ya 7600 ambavyo ni sawa na asilimia 72 vimepata umeme  ukilinganisha na vijiji 1208 vilivyopata umeme kwa mwaka 2015 na kueleza kuwa hadi kufikia mwaka 2020 asilimia 85 ya wakazi wa vijijini watakuwa wamefikiwa na huduma ya umeme.

Aidha Kalemani amesema kuwa serikali ina mipango ya kutosha ya kuimarisha sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ambapo takribani shilingi bilioni 64 zimetengwa, kujengwa kwa transifoma katika maeneo mbalimbali pamoja na uwekaji wa miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo na nyaya ardhini mpango utakaoanza mwakani jijini Dodoma na baadaye jijini Dar es Salaam.

Vilevile Kalemani amewahakikishia wawekezaji pamoja na wenye viwanda uhakika wa soko na nishati na kusema kuwa serikali ipo nao sambamba na amezitaka mamlaka husika kutoa huduma kwa ufanisi pamoja na kuweka mazingira bora kwa wawekezaji kwa kuzingatia huduma ya umeme inakua imara, toshelevu, inayotabirika na yenye gharama nafuu.

Kwa upande wake mwenyekiti  wa taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Salum Shamte amesema kuwa serikali iangalie namna ya kutoa vipaumbele vya fursa kwa wazawa ili kuweza kujenga taifa la viwanda.

Shamte amesema kuwa wazawa wapewe fursa katika kujenga miundombinu ya aina hiyo ili kuokoa fedha na kujenga mabilionea wengi zaidi.

Aidha ameiomba mamlaka husika kutoa gesi kwa sekta binafsi ili waweze kusambaza majumbani pamoja na kuzalisha umeme.

Mkutano huo umehudhuriwa na wamiliki wa viwanda, mameneja wa TANESCO nchi nzima kikanda pamoja na watendaji wa sekta ya nishati.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na jumuiya ya wenye viwanda nchini kwenye mkutano uliowakutanisha ambapo wamejadili kero,  na utatuzi wa changamoto hizo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Salum Shamnte akizungumza wakati mkutano huo ambapo ameiomba serikali kutoa gesi kwa sekta binafsi ili waweze kuzalisha umeme na kusambaza gesi majumbani,  jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa shirikisho la wenye viwanda nchini (CTI) Frank Daffa akitoa salama katika mkutano huo ambapo ameiomba mamlaka husika kuangalia suala la ukatikaji wa umeme hasa katika maeneo ya uzalishaji,  jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali waliohudhuria Mkutano wa Waziri wa Nishati na Jumuiya ya Wamiliki wa Viwanda uliofanyika jijini Dar es Salaam.

WASHAURIWA KUCHANGIA FURSA ILI KUJIPATIA KIPATO, KUKUZA UCHUMI WA NCHI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv , Arusha 

WANANCHI wenye tabia ya kulalamika kuwa hawana kazi pamoja na kudai kuwa maisha magumu wameshauriwa kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana ili kujipatia kipato na kukuza uchumi wa nchi.

Ushauri huo umetolewa na Mtume Sekela Lolandi wa Huduma ya Ngurumo ya Upako wakati akizungumzia na waumini wa huduma ya Ngurumo ya Upako Ndani ya hema la kukutania la Chuo cha Unabii Kisongo mkoani Arusha .

Amesema kuna Watanzania wengi wamekua na tabia ya kukaa tu bila kufanya Kazi na kuitupia lawama Serikali kitu ambacho sio kizuri kwani kila mtu aliumbwa akiwa na ujuzi wake ambao akijiongeza hatakosa fedha wala kazi ya kufanya. 

"Baadhi ya watanzania haswa wanaosema mmesoma mmekuwa na tabia mbaya sana ya kulala mikia Serikali kuwa haiwapi kazi kitu kinachonifanya nishangae.

"Wengine wanaona kabisa nikifanya hivi naweza nikapata fedha na maisha yakaenda lakini kwavile anajiona amesoma anaacha kufanya na kujihisi watu watamshangaa kitu ambacho ni cha ajabu,"amesema.

Amefafanua kuwa kazi yoyote ni nzuri mradi iwe halali na inakubalika na sheria za nchi yetu huku akisisitiza wananchi hasa vijana wasikae wakisubiria kuajiriwa bali wajiajiri wenyewe kwa kufanya kazi 

"Mnajua hata vitabu vya dini vimeandika asie fanya kazi asile sasa wewe umekaa kwa jirani kuna kibarua cha kufua badala ukafue upate fedha unasema mimi na elimu yangu nikafue .Kazi ni kazi, hivyo tufanye kazi kwani unaweza kufua nguo za jirani na baadae utafungua kiwanda,"amesema.

Kwa upande wake Nabii Mkuu Dk.Geordavie Kasambale wa Huduma ya Ngurumo ya Upako Arusha amesema kwa sasa hivi sio muda wa wananchi na hasa vijana kukaa na kujibweteka huku wakilalamika hakuna kazi bali ni muda wa kuamka na kuanza kuchangamkia fursa zilizopo. 

"Kuna mambo yanahitajika na yanafursa kubwa, kwa mfano kipindi hichi kuna uhitaji wa mifuko ambayo sio ya Plastiki, nenda tafuta anaejua kutengeneza tengeneza leta sokoni uza na si kukaa na kulalamika Serikali haikusaidii,"amesema.

Ameongeza nchi ya Tanzania ni nchi yenye fursa nyingi za kujipatia kipato lakini baadhi ya wananchi wamebaki kuwa maskini kutokana na kutofanya kazi na kubaki kuitupia lawama Serikali , jambo ambalo si sahihi.

KAIMU RC TANGA AKEMEA VIKALI BAADHI YA VYAMA VYA USHIRIKA KUFANYA UBADHIRIFU

$
0
0
 KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa akifungua Jukwaa la tatu la Ushirika Mkoa huo 2019 lililoshirikisha wadau kutoka wilaya zote za mkoa huo lililokwenda sambamba na kauli mbiu ya Ushirika kwa kazi wenye Staha”
 Katibu Tawala Msaidizi  Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Tanga Benedict Njau akizungumza wakati wa akifungua Jukwaa la tatu la Ushirika Mkoa huo 2019 lililoshirikisha wadau kutoka wilaya zote za mkoa huo lililokwenda sambamba na kauli mbiu ya Ushirika kwa kazi wenye Staha”
 Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Jacqueline Senzighe akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Mkoa wa Tanga Mashi Sopah akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
 MKUU wa Idara ya Ugani na Huduma za Jamii Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Ushirika (MoCU) Paulo Anania Fute akiwasilisha mada ya Elimu ya Ushirika ,Ukaguzi na Usimamizi wakati wa Jukwaa hilo
 Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Ushirika Moshi ofisi ya Mkoa wa Tanga Abel Ngowi akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
 Sehemu ya washiriki wa Jukwaa hilo
 MENEJA wa Bodi ya Korosho kulia akiwa kwenye Jukwaa hilo
 Sehemu ya wadau mbalimbali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kwenye Jukwaa hilo
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Tawala Msaidizi  Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Tanga Benedict Njau kulia na Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Jacqueline Senzighe mara baada ya kufungua Jukwaa hilo


KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa amekemea vikali vitendo vya baadhi ya viongozi vyama vya ushirika wanaofanya ubadhirifu huku akitaka wachukulia hatua kali ikiwemo kuwaondoa kwenye nafasi zao maana wanaweza kuwaharibia.

Mwalapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga aliyasema hayo leo wakati akifungua Jukwaa la tatu la Ushirika Mkoa huo 2019 lililoshirikisha wadau kutoka wilaya zote za mkoa huo lililokwenda sambamba na kauli mbiu ya Ushirika kwa kazi wenye Staha”

Alisema kwamba bila kufanya hivyo viongozi wa namna hiyo wanaweza kuwa kikwazo kikubwa cha vyama hivyo kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea hivyo ni vema wakakaa pembeni ili kutua fursa kwa wengine ambao wanaviendeshwa kwa tija na manufaa makubwa.

“Lipo tatizo kubwa ambalo lipo kwa baadhi ya viongozi ushirika kufanya ubadhirifu kwenye vyama vya ushirika hawa tusiwafumbie macho lazima tuchukue hatua za kuwadhibiti ikiwemo kuwaondoa kwenye nafasi maana wanataka kutuharibia”Alisema Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa.

Aidha pia aligusia tatizo sugu la ukopaji kwenye vyama hivyo huku aliwataka wanaonufaika na mikopo mbalimbali wahakikishe wanairudisha kwa wakati ili ili uweze kutumika kuwasaidia wengine

Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa alisema wanataka ushirika uleta manufaa zaidi kwa kuwasaidia wanachama,jamii na Taifa ili yafikwe malengo makubwa ya kuweza kupata maendeleo na kuweza kujikwamua kiuchumi.

“Lakini hayo yote yaweze kufikiwa lazima mambo yaenda kwa mujibu wa sheria na taratibu ...pia nitumie jukwaa hili kukemea tabia za baadhi ya viongozi wa wabadhirufu kwenye vyama vya ushirika tuchukue hatua za kuwadhibiti ikiwemo kuwaondoa kwenye nafasi maana wanataka kutuharibia”Alisema

Alieleza pia kwamba ikiwa watu wamekopa fedha na wanashindwa kuzirudisha na kupelekea kuwa mkopaji sugu maana yake anawazuia wenzake wengi fursa ya kunufaika na mkopo huo.

Hata hivyo alitoa wito kwa vyama hivyo kuhakikisha mali za ushirika huo zinatambuliwa na zirasimishwe ili kuweza kuleta tija na kuchochea shughuli za kimaendeleo.

Awali akizungumza katika Jukwaa hilo Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Jacqueline Senzighe alisema vyama vya ushirika vimezidi kuongezeka na kufikia 421 na vyama vikuu vitatu huku vikiwa wanachama 61,878.

Senzighe alisema hali ya vyama ya ushirika na mikopo vinaendelea vizuri na mpaka sasa wamekwisha kutoka mikopo yenye thamani ya Bilioni 42.2 na ambayo imerejeshwa kati ya hiyo ni bilioni 31.5.

Aidha alisema changamoto kubwa wanazokabiliana nazo ni uhaba wa maafisa ushirika kutokupata mafunzo mara kwa mara kuwajengea uwezo

Hata hivyo aliongeza kwamba changamoto nyengine ni baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Vijiji kukaataa ushirika kutokana na kujilimbikizia mali za ushirika huku wengine wakitaka mikataba ya kuuza bila utaratibu wa ushirika.

Alieleza kwamba changamoto nyengine ni uwepo wa miundombinu mibovu ambayo husababisha hasara kwa vyama vya mazao kutokana na bidhaa zao kuharibika kabla ya kufika sokoni.

WAHAMIAJI HARAMU SITA NA WATU WENGINE 29 WANAOJIHUSISHA NA UHALIFU WAKAMATWA CHALINZE -WANKYO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
JESHI la polisi mkoani Pwani, linawashikilia wahamiaji haramu sita ambao ni raia kutoka nchini Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali, huku likikamata watu wengine 29 kwa kujihusisha na matukio ya uvunjaji nyumba usiku na kuiba.

Watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia msako mkali na oparesheni dhidi ya vikundi vya vijana wa mitaani wanaojihusisha na wizi kwa kuvunja, kupora na kukaba raia wema huko wilaya ya kipolisi Chalinze .

Akielezea kuhusiana na matukio hayo,kamanda wa polisi mkoani Pwani Wankyo Nyigesa alisema baadhi yao walikamatwa wakiwa na mali kadhaa,madawa ya kulevya aina ya bangi kete 142,puli nne,pombe haramu ya moshi lita 25 na pikipiki moja.

Anabainisha kwamba, pia kumekamatwa magunia 90 ya mkaa uliovunwa bila uhalali ,mashuka,raba,vitenge,mafuta ya pikipiki na mafuta ya kula yanayodaiwa kuingizwa kwa kukwepa ushuru lita 300.

Akizungumzia kuhusu wahamiaji haramu alisema ,watafikishwa katika idara ya uhamiaji kwa taratibu nyingine za kisheria. Kamanda huyo alitoa rai kwa jamii ,kuwa itambue uhalifu haulipi na hauna faida kwani siku za mwizi ni arobaini na akishikwa mtu akijihusisha na uhalifu atakiona.

Vilevile anawataka walioibiwa kufika katika kituo cha polisi Chalinze kutambua mali zao .

TUZO YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI YAPELEKWA KWA WANANCHI WA MIKOA YA MARA NA SIMIYU .

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt Hamis Kigwangalla akiwa na Wakuu wa Mikoa ya Mara ,Adam Malima na wa Simiyu ,Anthony Mtaka wakati wa kuionesha kwa wananchi wa mikoa hiyo miwili tuzo iliyopata Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ya kuwa Hifadhi Bora barani Afrika .Wengine Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu (kulia) na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi kanda ya Magharibi ,Martin Loibook .(kushoto)
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt Hamis Kigwangalla akizungumza wakati wa sherehe za kuoinesha kwa wananchi wa mikoa ya Mara na Simiyu tuzo iliyopata hifadhi ya Taifa ya Serengeti  ya kuwa Hifadhi Bora Barani Afrika .
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria sherehe hizo katika uwanja wa kijiji cha Robanda wilayani Serengeti. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ,Anthony Mtaka akizungumza katika sherehe hizo zilizo udhuliwa na viongozi mbalimbali zikiwemo kamati za ulinzi na usalama za mikoa ya Mara na Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Mara ,Adam Malima akizungumza katika sherehe hizo.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi kanda ya Magharibi, Martin Loibook akizungumza katika sherehe hizo alipomuwakilsha Kamishana Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi .
Waziri wa Malisili na Utalii,Dkt Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya  za mikoa ya Mara na Simiyu.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mara ,Adam Malima wakati akitizama ngoma kutoka kikindi cha wananchi wa jamii ya Maasai  wakati kikitumbuiza katika sherehe hizo.
Kamishna Msaidizi -Mawasiliano TANAPA ,Pascal Shelutete aakifanya utamburisho wa viongozi mbalimbali waliofika kwa ajili ya sherehe hizo .
Baadhi ya  Viongozi wa idara mbalimbali za serikali za mikoa ya Mara na Simiyu walipata fursa uya kupiga picha na tuzo hiyo kabla ya kupelekwa kwa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt John Pombe Magufuli.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV.

JPM Ang’ara Jarida la Forbes, Aendelea kukubalika Kimataifa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, ameendelea kukubalika kimataifa baada ya Jarida maarufu Duniani la Forbes kubashiri kwamba ataivusha Tanzania na kuwa nchi yenye kipato cha kati kupitia ajenda yake ya Tanzania ya viwanda chini ya mpango wa maendeleo wa 2025.

Katika jarida hilo la Forbes Afrika la Julai mwaka huu ambalo lilikuwa mahsusi kwaajili ya kelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano na uongozi wa Rais Magufuli kwa ujumla, imeelezwa maono yake kama kiongozi wan chi yameifanya  Tanzania kupiga hatua kubwa za maendeleo na inatarajiwa kuwa miongoni mwa nchi chache sana za Afrika zenye maendeleo yanayoonekana na yanayopatikana kwa muda mfupi.

Kwamujibu wa Jarida hilo ambalo limemwelezea Rais Magufuli kama Tingatinga katika kusimamia kile anachokiamini, miongoni mwa mambo makubwa yanayomfanya ang’ae kimataifa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya standard Gauge SGR, upanuzi wa bandari na ujenzi wa miundombinu ya barabara zinazounganisha nchi nzima ambazo ni kichocheo kikubwa cha maendeleo hapa nchini.

Aidha Rais Magufuli ameelezewa kuwa ni mtu asiye na masihara katika kusimamia masuala ya maendeleo, mfano  jinsi alivyosimamia na kuhakikisha uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere terminal three unakamilika kwa wakati na kwa kiwango cha kimataifa.
Jarida la Forbes limeendelea kumwelezea Rais Magufuli kuwa, mafanikio mengi anayopata ni kutokana na kuongozwa na mpango wa maendeleo  wa 2025 pamoja na ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015.
Miradi mingine iliyoainishwa kuonyesha utendaji wake ni ile ya umeme ya Kinyerezi  awamu ya kwanza ya pili nay a tatu, pamoja na mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika maporomoko yam to Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge,ambayo lengo lake ni kumaliza kabisa tatizo la umeme hapa nchini hasa kwa wananchi wa vijijini.

Kuhusu ukuaji wa uchumi Jarida la Forbes limeelezea kuwa katika kipindi cha utawala wake tangu aingie madarakani mwaka 2015, uchumi umeendelea kukua kwa kasi kwa kiwango cha asilimia 7 ambao ni ukuaji wa mfano na wakuridhisha   kwa nchi za Afrika ikilinganishwa na miaka mingi iliyopita.

Katika uwekezaji Rais Magufuli amenukuliwa akiwahakikishia wawekezaji na dunia kwa ujumla kwamba, Tanzania ni nchi salama na kwa uwekezaji na akawakaribisha kuja kuwekeza kwani ameendelea kufanya mapinduzi makubwa katika uwekezaji lengo kuu ikiwa ni kuvutia wawekezaji wengi zaidi.

Mahojiano ya Rais Magufuli yaliyotolewa na Jarida la Forbes Africa,  yalifanyika mapema mwaka huu ambapo Jarida hilo lilikuwa na toleo maalum la Tanzania kuhusiana na mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali.

MUIMBAJI WA KASWIDA INDONESIA ASHAURI WANAWAKE WA KIISLAMU KUPEWA FURSA KUANDAA MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAAN

$
0
0
Na Khadija Seif,Globu ya jamii

MUIMBAJI wa Kaswida kutoka nchini Indonesia Ustadhat Mastia lestaluhu amelipongeza kundi la Nasaha Crew kwa kumpa fursa ya kuja nchini kufanya burudani kwa mashabiki zake walioko nchini Tanzania.

Pia amewahimiza waumini wa dini ya Kiislam hasa waimbaji wa kaswida kuendelea kuwa kwenye misingi ya dini na kutunga Kaswida zenye kuelimisha na kuwakumbusha watu kufanya matendo ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, amesema kuwa dini huwaleta wanadamu karibu na ndio maana hata yeye ameweza kutoka nchini kwake na kuja Tanzania, ametoa rai waumini wa dini hiyo kuhakikisha wanapendana na kuiheshimu Quraan Tufuku.

Kwa upande wake Muandaaji wa hafla hiyo fupi ya kusoma Quraan kwa wanawake Ukhty Salama amesema japo kwa sasa wanawake hawajapewa kipaumbele kuanda matamasha na mashindano ya kuhifadhi Quran kupitia hafla hiyo viongozi wataiona nafasi ya kuwaacha wakina mama kuratibu shughuli hiyo.

"Wanawake tunawekwa nyuma sana hasa linapokuja suala la kuratibu vitu vingi ,ila kwa hili la kuandaa mashindano,majukwaa ya kuhifadhi Quraan wanawake wapo tayari kujitoa na kufanikisha hilo,"amesema.

Pia Ukhty salama amewapongeza wanafunzi wake walisoma Quraan Tukufu mbele ya mgeni rasmi Mastia na kueleza ni moja ya nafasi peke ya yeye kubeba mazuri ya nchi yetu nakutangaza sehemu mbalimbali ikiwemo nchini kwake Indonesia.

WASANII WAOMBA KAMPUNI YA KC LAND KUTENGA MAENEO YA NYUMBA ZA IBADA

$
0
0
Na Khadija seif,Globu ya jamii

WASANII wa Bongo Movie nchini wametoa ombi kwa Kampuni ya KC Land inayouza viwanja kutenga maeneo ya kujenga nyumba za ibada.

Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na msanii mkongwe wa vichekesho Seif Hassan a.k.a M'bembe ameseam kampuni hiyo inayoshirikiana na kundi la Uzalendo Kwanza bado ina lengo la kumpa heshima msanii kumiliki ardhi kwa manufaa ya kizazi chake.

"Tupo watu wa dini mbalimbali, hivyo ni vema kukatengwa na maeneo ya kujenga nyumba za ibada na lengo kubwa ni kuhakikisha wasanii wanapata nafasi ya kufanya ibada,"amesema.

Hata hivyo M'bembe amewataka wasanii wa kundi la Uzalendo Kwanza kuchukua viwanja, hivyo kwani ni kampuni peke ilionesha dhamira ya dhati ya kuwasaidia wasanii.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya KC Land Khalid Mwinyi amepongeza wasanii wote ambao tayari wameshachukua viwanja na baadhi yao kulipia fedha.

Mwinyi amesema kwa kuwa asilimia 70 tayari wameshalipa , sasa wataweza kukipeshwa fedha kwa ajili ya kununua vifaa ili kuanza ujenzi mara moja.

" Tumefanya hivyo ili kuona kwa jinsi gani mji huu utajengeka kwa haraka zaidi na wasanii kuhamia huku kijiji cha Mwasonga,"

Pia Mwinyi amepongeza watu wa ughaibuni (TDC) kuona ni fursa ya kipekee kuwekeza nyumbani ili kuleta maendeleo nchi ya Tanzania.

"Tayari wameshakatiwa viwanja 200 bado utekelezaji wa kujenga viwanja hivyo na matumaini yangu kutakuwepo na fursa nyingi hasa za kibiashara kutokana na watu hao kuwepo kwenye kijiji hichi hivyo hata huduma za jamii zitakua karibu na wananchi ikiwemo hospital pamoja na nyumba za ibada,"amesema.

MASAUNI AONGOZA WANAJUMUIYA WA CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA CHA KAMPALA (KIU) KUMUAGA MWANAFUNZI ANIFA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Simpoliunus, aliyefariki baada ya kuvamiwa na vibaka maeneo karibu na chuo hicho.Ibada ya kuaga mwili imefanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi SalaSala,jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Iringa kwa mazishi .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa  akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Simpoliunus, aliyefariki baada ya kuvamiwa na vibaka maeneo karibu na chuo hicho.Ibada ya kuaga mwili imefanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi SalaSala,jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Iringa kwa mazishi .
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa  akizungumza wakati wa ibada ya kumuaga  mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Simpoliunus, aliyefariki baada ya kuvamiwa na vibaka maeneo karibu na chuo hicho.Ibada hiyo imefanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi SalaSala,jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Iringa kwa mazishi .
Waombolezaji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani)wakati wa ibada ya kuaga mwili wa  mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Simpoliunus, aliyefariki baada ya kuvamiwa na vibaka maeneo karibu na chuo hicho.Ibada hiyo  imefanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi SalaSala,jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Iringa kwa mazishi .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MAJALIWA AKISALIMIANA NA MSANII PIERRE LIQUID BUNGENI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Msanii Pierre Liquid kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 19, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Msanii Pierre Liquid kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 19, 2019.  Wa pili kulia ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Mhandisi Ramo Makani.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WCF YASHIRIKI KWENYE MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2019

$
0
0
Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia  kwa Wafanyakazi (WCF) wafanya usafi, watoa elimu ya kutambua na kuzuia vihatarishi vilivyopo  kwenye maeneo ya kazi pamoja na kutoa misaada kwa wagonjwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI) kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma, 2019.


IGP SIRRO AWAONYA ASKARI WANAOJIHUSISHA NA UHALIFU NA KUWATAKA KUTIMIZA WAJIBU WAO

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, amewataka Maofisa na askari kuhakikisha wanaendelea kutimiza wajibu wao kikamilifu na kutokujiingiza kwenye masuala ya uhalifu ikiwemo kushiriki kwenye wizi wa dhahabu sambamba na uhujum uchumi.

IGP Sirro, ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati alipokuwa akizungumza na Maofisa na Wakaguzi wa Jeshi hilo ambapo amesema kuwa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa askari anayeshiriki kwenye uhalifu ikiwemo kufukuzwa kazi pamojana kufikishwa mahakamani.


Hata hivyo IGP Sirro amesema Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha suala la uchaguzi linafanyika kwa amani na utulivu na kwamba amewahakikishia wananchi usalama wao na mali zao na kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa sahihi za uhalifu na wahalifu.

MAHAKAMA KUU YA TANZANIA YAMTIA HATIANI RAIA WA KIGENI KWA KUKUTWA NA HATIA YA KUSAFIRISHA PIPI 56 ZA DAWA ZA KULEVYA AINA YA HEROIN

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blog ya Jamii

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi, imemtia hatiani raia wa Nigeria Christian Ugbechi baada ya kumkuta na hatia ya kusafirisha pipi 56 za dawa za kulevya aina ya heroin hydrochloride.

Uamuzi huo umefikiwa leo, Juni 19, 2019 na Jaji Sirrilius Matupa  ambae amesema upande wa mashitaka katika kesi hiyo umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kupitia mashahidi wake 11 na vielelezo 22 waliofika mahakamani hapo kuthibitisha mashitaka hayo, kuwa mshitakiwa ametenda kosa hilo.

Amesema pamoja na mshtakiwa kujitetea kwamba alifanyiwa upekuzi mara tatu na hakukutwa na kitu chochote na hivyo upande wa mashitaka ulipaswa kuleta ushahidi wa CCTV, haikuwa lazima kuwapangia upande wa mashitaka mashahidi wa kuwaleta na kwamba walikuwepo mashahidi wengine waliothibitisha mashitaka.

Amesema mkemia mkuu wa serikali katika uchunguzi wake, amethibitisha dawa za kulevya alizozichunguza ndizo alizokutwa nazo mshitakiwa huyo.

Kabla ya kusomwa kwa adhabu Jaji Matupa aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ambapo Wakili wa Serikali, Constantine Kakula amedai kuwa hawana kumbukumbu ya makosa ya nyuma ya mshitakiwa lakini wameiomba mahakama itoe adhabu kali iwe fundisho kwa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Upande wa utetezi, Jeremiah Ntobesya aliomba mahakama kumpunguzia adhabu mteja wake kwa sababu ana mke na watoto wawili wanaomtegemea na pia mshtakiwa anasumbuliwa na matatizo ya moyo na kwamba amekaa gerezani kwa mwaka mmoja na nusu nankipindi hicho chote alikuwa na tabia njema.

Pia alisema, pamoja na kwamba kifungu cha sheria kinaamuru mshtakiwa kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani lakini siyo lazima, itolewe adhabu hiyo, mahakama inaweza kuamua vinginevyo.
Kutokana na ubishani wa kisheria juu ya adhabu anayopaswa kusomewa mshitakiwa mahakama imesema itamsomea mshitakiwa huyo adhabu yake, Juni 21, 2019 (Ijumaa).

Mapema katika ushahidi wake, askari wa upelelezi kutoka Kituo cha  Uwanja wa ndege namba G 1782 D/C Peter alidai kuwa aliandika maelezo ya mshitakiwa huyo na katika mahojiano alimueleza kuwa amemeza pipi za dawa za kulevya.

Alidai baada ya kueleza hayo alimuweka mahabusu ili aweze kuzitoa na kwamba hadi  Januari 30,2018 saa 10:30  jioni alitoa pipi 23 alizomeza.

Pia alidai walichukua kielelezo hicho na pipi nyingine zilizokutwa kwenye begi na kuzipeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali ambapo kwa pamoja zilikutwa na uzito wa gramu 947.17.

"Matokeo ya uchunguzi yalionesha kuwa pipi zote zilikuwa ni dawa za kulevya ambazo ni heroin hydrochloride zilizochanganywa na paracetamol metronidazole na papavirine," alidai Peter.

Mkuu wa Kituo cha Uwanja wa ndege, Inspekta Dickson Haule alidai siku ya tukio majira ya saa 14:00 mchana akiwa ofisini alijulishwa na askari huyo wa upelelezi kuwa kuna mtuhumiwa amekamatwa na dawa za kulevya.

Haule alidai baada ya taarifa hiyo alienda Ofisi ya Polisi Interpol walipokuwa na alishuhudia mtuhumiwa akipekuliwa  ndipo aliona begi dogo la mgongoni kuna pipi 56 zikiwa zimeviringishwa ndani ya soksi mbili nyeusi.

Katika kesi hiyo, inadaiwa Januari 28, mwaka jana maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa akisafirisha sha dawa za kulevya aina ya  Heroine hydrochloride zenye uzito wa gramu 947.57.
RAIA wa Nigeria, Christian Ugbec akiwa katika kizimba cha Mahakama  Kuu Tanzania Kitengo cha makosa ya Rushwa na uhujumu uchumi maarufu kama mahakama ya mafisadi,  akisubiri kusomewa hukumu yake dhidi ya kesi ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride. Hata Hata hivyo, mshitakiwa huyo ametiwa hatiani na atasomewa adhabu yake Juni 21,2019.

WAZAZI WATUMIA ZAIDI YA MILIONI 70 KUKARABATI SHULE YA MSINGI MAPINDUZI ENGLISH MEDIUM

$
0
0
Mwenyekiti wa shule ya msingi Mapinduzi English medium Haliel Abdallah akionyesha jinsi gani ukarabati wa madarasa na ofisi sita za walimu za shule hiyo kwa lengo la kuboresha miundombinu ya shule hiyo
Mafundi wakiwa kazini kuendelea na ukarabati wa majengo ya shule hiyo ya msingi Mapinduzi English medium iliyopo manispaa ya Iringa.
Mwenyekiti wa shule ya msingi Mapinduzi English medium Haliel Abdallah akiwa na kiongozi mwingine kwenye kama hiyo wakikagua ukarabati ambao unaendelea


NA FREDY MGUNDA,IRINGA. 

Wazazi wa shule ya msingi Mapinduzi English medium iliyopo manispaa ya Iringa wameamua kuikarabati ili kuboresha mazingira ya shule kwa lengo la kukuza taaluma ya wanafunzi katika shule hiyo.

Akizungumza na blog hii mwenyekiti wa shule hiyo,Haliel Abdallah alisema kuwa shule hiyo ilikuwa na miundombinu mibovu ambayo ilikuwa sio rafiki kwa walimu na wanafunzi hivyo ilikuwa inachangia kutoingia kwenye shule nyingine za aina hiyo.

“Kwa kifupi sana kamati ilibaini kwamba mazingira ya madarasa pamoja na ofisi za walimu hazikuwa rafiki hivyo tukaamua kuanza kufanya tathimini kwa lengo la kuanza kukarabati shule hiyo ili irudi kwenye ubora kama uliokuwepo hapo awali” alisema Abdallah 

Abdallah alisema kuwa lengo la kujenga darasa jipya katika shule hiyo ili kupanua wigo wa kuwa na vyumba vingi ambavyo vitatuasaidia kuleta ushindani na shule nyingine zenye mchepuo wa masomo ambayo yanafundishwa kwa lugha ya kingereza 

“Tunataka kuhakikisha kuwa shule hii inakuwa kwenye ubora wa hali ya juu kwenye miondombinu kuanzia madarasa,ofisi za walimu na mazingira ya shule lazima yawe ya kuvutiwa kwa walimu,wanafunzi na hata wazazi wawe wanajisifia watoto wao kusoma katika shule hiyo” alisema Abdallah

Abdallah aliongeza kwa kusema kuwa katika ukarabati huo utahusisha pia ukarabati wa madawati pamoja kuhakikisha walimu wanakuwa na samani bora ambazo nazo zinakuwa rafiki na mazingira ya kufundishia na kuandalia masomo.

Aidha Abdallah amewapongeza wazazi ambao watoto wao wanasoma katika shule hiyo kwa kujitoa kukakikisha shule hiyo inakarabatiwa kwa lengo la kuwa nashule yenye kushindana na shule nyingine zilizopo mkoani Iringa na nje ya Iringa.

Awali akitoa taarifa ya hali ilivyokuwa hapo awali walimu mkuu wa shule hiyo Emanuel Mwakyusa alisema kuwa miundombinu ya shule hiyo haikuwa rafiki kwa kutoa elimu iliyobora kwa kuwa madarasa na majengo mengi yalikuwa chakavu sana.

“Madarasa mengi yakuwa chakavu hivyo ikawa ngumu kufanya usafi kukiwa na mashimo,paa zilikuwa zimechoka na kuvujisha maji kipindi cha vua hiyo hali ya usafi ilikuwa mbaya na kusababisha kutoa elimu ambayo ilikuwa haistahili” alisema Mwakyusa

Mwakyusaalisema kuwa ukarabati huo umefanywa na wazazi tu bila kuigusa serikali kwa kuwa wazazi hao wanapenda kufanya maendeleo kwa lengo la kuhakikisha waoto wao wanasoma katika mazingira yaliyo bora.

“Mimi niwapongeze wazazi ambao watoto wao wanasoma katika shule hii kwa kujitoa kwa moyo wao wote kuhakikisha kuwa shule hii inakarabatiwa vilivyo na kuwa na mazingira yaliyo bora” alisema Mwakyusa

Mwakyusa alisema kuwa ukarabati huo utasaidia kukuza taaluma za wanafunzi wa shule hiyo kwa kuwa miundombinu itakuwa imeboreshwa vilivyo na itakuwa rafiki wa pande zote 

Kwa upande wake mwalimu Rahab Mahenge alisema uboresha wa miundombinu ya shule hiyo kutachangia kuongezeka kwa ufaulu kwa kuwa watu wote watakuwa na furaha na mazingira yaliyopo.

POLISI WAMSHIKILIA KIJANA WA MIAKA 19 KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MWANAFUNZI JIJINI DAR

$
0
0
*Ni mwanafunzi wa kike aliyekuwa anasoma Chuo Kikuu cha Kampala
*Mtuhumiwa asema baada ya kumchoma kisu alichukua Tekno, 8000/
*Kisu alichotumia kufanya mauaji chanaswa, kufikiswa muda wowote mahakamani

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inamshikilia kijana mweye umri 19 Ernest Joseph kwa tuhuma za mauji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) kilichopo Gongolamboto jijini Anifa Mgaya(21).

Kijana huyo anayetuhumiwa kufanya mauaji hayo tayari amekiri kuhusika na ameliambia Jeshi la Polisi kuwa baada ya kufanya tukio hilo la mauaji kwa kumchoma kisu kifuani upande wa kulia alichukua simu aina ya Tekno na fedha Sh.8000 ambazo zilikuwa kwenye pochi.

Akizungumza kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema mtuhumiwa huyo amefanya tukio hilo la mauaji Juni 16 mwaka huu saa tatu usiku maeneo hayo ya Chuo cha Kampala.

"Mtuhumiwa amekiri kuhusika na mauaji ya mwanafunzi Anifa Mgaya (21) ambaye alikuwa anasoma chuoni hapo ngazi ya Diploma.Mtuhimiwa alimchoma kisu mwanafunzi huyo kifuani na kisha kuchukua simu ya Tekno na fedha Sh.8000.

"Mwanafunzi alifariki dunia muda mfupi baada ya kutokwa na damu nyingi, na mtuhumiwa alikimbia baada ya kutenda kosa hilo.Jeshi la Polisi tuliahidi kumsaka aliyehusika kokote aliko na jana tukamkata akiwa maeneo ya Madale Mivumonijijini Dar es Salaam,"amesema Kamanda Mambosasa.

Akifafanua zaidi kuhusu tukio hilo, Kamanda Mambosasa amesema katika mahojiano mtuhimiwa amekiri kumchoma kisu na kueleza namna ambavyo Anifa alikuwa amevaa siku hiyo kwa kueleza alikuwa amevaa fulana nyeusi , suruali ya jinsi na kapelo.

"Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili,"amesema Mambosasa na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi liliahidi kumsaka mtuhumiwa aliyehusika na mauji ya mwanafunzi huyo kwani damu yake haijamwagika bure.

Wakati huo huo Kamanda Mambosasa amesema kuwa wakati wa msako huo , wamekamata wahalifu wengine 31 ambao wamekuwa wakifanya matukio ya uhalifu chuoni hapo na kusababisha hofu kwa wanafunzi, ambao Polisi imeeleza kuwa itaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na kisha sheria ichukue mkondo wake.

Mambosasa amesema kuwa Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam litaendesha msako kusaka wahalifu wote walioko kwenye maeneo ya vyuo na kufafanua yoyote ambaye anajihusisha na matukio ya uhalifu atachukuliwa hatua.

UPASUAJI WA NJIA YA MATUNDU MADOGO HOSP YA BENJAMIN MKAPA

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images