Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

TUHUMA ZA RUSHWA KATIKA KUICHAGUA QATAR KUWA MWENYEJI KOMBE LA DUNIA 2022 KWAMWEKA HATIANI PLATIN

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
ALIYEKUWA  Rais wa shirikisho la mpira barani Ulaya (UEFA) kwa mwaka 2007-2015, mchezaji wa zamani wa Ufaransa na mshindi mara tatu wa tuzo ya Ballon I'or Michel Platini anahojiwa na mamlaka za uchunguzi wa masuala ya ufisadi na rushwa kwa kile kilichoelezwa ni kuipa nafasi Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la duniani mwaka 2022 vyombo vya habari nchini Ufaransa vimeripoti.

Michel (63) ambaye aliwahi kuwa Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya na baadaye kufungiwa kujihusisha na soka mwaka 2015 kwa kile kilichoelezwa ni ukiukwaji wa kanuni maadili.

Wakati wa kutafuta mwenyeji wa mashindano hayo ya kidunia mwaka 2010 Qatar iliibwaga Marekani, Australia, Japan na Korea Kusini. Michel amekana mashtaka hayo aliyohojiwa huko Nanterre magharibi wa mji mkuu wa nchi hiyo Paris.

Imeelezwa kuwa shutuma dhidi yake zilianza kuchunguzwa miaka miwili iliyopita na katika sakata hilo Sepp Blatter aliyewahi kuwa Rais wa shirikisho la mpira duniani (FIFA) ambaye pia alipigwa marufuku kujihusisha na soka alihojiwa mwaka 2017.

Aidha FIFA imetakiwa kuifanyia uchunguzi wa kina Qatar kuhusiana na sakata hilo.

Michel Platin alikata rufaa mara baada ya kufungiwa kutojihusisha na masuala ya soka  ambapo alipunguziwa adhabu hadi kufikia miaka minne ambayo anaimaliza Oktoba mwaka huu.

Mhandisi Mtigumwe ajionea maandalizi ya Nane nane ambayo Kitaifa yatafanyika Mkoani Simiyu

$
0
0





Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akipata maelezo kuhusu kilimo shadidi kutoka kwa mtaalamu wa Kilimo Dkt Kisa Kajigili
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka mara baada ya kuwasili Mkoani humo kujionea hmaandalizi ya maonesho ya Nanenane.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akiongozana na mtaalamu kutoka wizara ya Kilimo Dkt Kisa Kajigili wakati wa ukaguzi wa maandalizi ya maonesho ya Nanenane.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo - Simiyu


Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe jana Tarehe 17 Juni 2019 alitembelea Viwanja vya Nyakabindi vilivyopo Mkoani Simiyu kujionea maandalizi ya maonesho ya Wakulima (Nanenane) ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia Agosti 1-8 katika maeneo mbalimbali nchini. 

Akiwa katika viwanja vya Nyakabindi Katibu Mkuu huyo alijionea maeneo mbalimbali likiwemo eneo la Wizara ya Kilimo na kujionea vipando vya mazao mbalimbali ambavyo vimefikia hatua nzuri.

Akizungumza na maafisa wa wa Wizara ya Kilimo sambamba na maafisa wa Mkoa wa Simiyu Mhandisi Mtigumwe alisisitiza kuwa wataalamu hao wanapaswa kuandaa vipando vya mazao yote yenye tija kubwa ikiwemo Matunda na mboga mboga.

Kadhalika alisisitiza kuongezwa kasi ya maandalizi ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaagiza Maafisa hao kufanya maandalizi mazuri yatakayokuwa Mfano kwa wadau wengine.Aidha, baada ya kutembelea viwanja hivyo Mhandisi Mtigumwe alikutana na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka ambapo walifanya mazungumzo kuhusiana na shughuli za Kilimo katika mkoa wa Simiyu. 

Baada ya Ziara hiyo katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Geita na Simiyu Mhandisi Mtigumwe amerejea Jijini Dodoma kuendelea na shughuli zingine.

UKARABATI WA JAHAZI

$
0
0
Jahazi  likiwa linafanyiwa ukarabati pembeni ya Bandari ya Bagamoyo mkoa wa Pwani,Pichani mafundi wakiendelea na ukarabati wao katika jahazi hilo(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Pichani mafundi wakiendelea na ukarabati wa Jahazi katika Bandari ya Bagamoyo  Mkoa wa Pwani.

VOA SWAHILI: Duniani Leo June 18 2019

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO

Waziri Kabudi akutana na Balozi Al - Mashaan wa Kuwait

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait anayeshughulikia masuala ya Afrika, Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan.

Pamoja na mambo mengine walizungumzia kuhusu jinsi ya kuboresha mahusiano yaliyopo katika kati ya Tanzania na Kuwait, nchi ya Kuwait imekuwa ni kati ya wadau muhimu wa Maendeleo hapa nchini kupitia mradi wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait(Kuwait Fund). 


Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimwelezea jambo Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan
Balozi Mubarak Mohamed Al -Sehaijan pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwait nchini wakisikiliza kwa makini mazungumzo hayo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan (hawapo pichani)
Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan naye akimweleza jambo  Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.)
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan (hawapo pichani)
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan, Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohamed AlSehaijan (wa pili kutoka kulia) pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwaiti na Afisa Mambo ya Nje Bw. Odilo Fidelis (wa pili kutoka kushoto)









TANZANIA YAWAHAKIKISHIA MAZINGIRA BORA WAWEKEZAJI WA KIMAREKANI NCHINI

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akihutubia wakati wakufunga Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani, ulioandaliwa na Ubalozi wa Marekani Uliopo hapa nchini kwa kushirikiana na Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania, ambapo alieleza kuwa Tanzania kwa sasa kuna mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji. Aidha, aliezea kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, imeweka usawa kwa kuwasikiliza wawekezaji wa Ndani na wawekezaji kutoka Nje. 

Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania (AMCHAM) Bw. Garry Friend akipokea nakala za vitabu vya bajeti ya serikali kutoka kwa Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ili kujionea mabadiliko ya uwekezaji nchini yalivyoboreshwa.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania (AMCHAM) Bw. Garry Friend akimsikiliza kwa makini Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda wakifuatilia kwa makini mambo yaliyokuwa yakielezwa na Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)
Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi K. Patterson naye akizungumza kwenye Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Sehemu ya wageni waliohudhuria kwenye mjadala huo, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Marekani na Ulaya Bw. Jestas Nyamanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki (Mb.) naye akihutubia kwenye Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Mhe. Godfrey Mwambe naye akielezea namna kituo hichi kilivyoboresha na kinavyoshirikiana na taasisi nyingine katika kuhakikisha mwekezaji anapokuja nchini hapati shida. 
Juu na Chini ni Sehemu ya wageni waalikwa wakimsikiliza Bw. Godfrey Mwambe (hayupo pichani).


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi K. Patterson 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akijadiliana jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (wa kwanza kilia)
Prof. Palamagamba John Kabudi, Mhe. Angela Kairuki pamoja na Dkt. Faraji Mnyepe wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa Mjadala wa kwanza wa kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Marekani hapa nchini pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria kwenye mjadala huo














NAIBU KATIBU MKUU AELEKEZA MIRADI YA MAJI NJOMBE KUTUMIA PAMPU ZILIZOBUNIWA NA WAZAWA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo ameelekeza Wataalam wa Sekta ya Maji mkoani Njombe kuanza kutumia pampu za kusukuma maji zilizobuniwa na Mzee John Fute zenye uwezo wa kusukuma maji kwa umbali wa zaidi ya mita 200 kulingana na mahitaji ya mteja bila kutumia umeme.
Mhandisi Kalobelo ametoa maelekezo hayo kwa wataalam hao akiwa mkoani Njombe kwa kuwataka wafanye uchunguzi wa kupata vyanzo vya maji vinavyoweza kutumia pampu za aina hiyo ndani ya wiki moja kuanzia Juni 17, 2019 kwa lengo la kuachana na gharama kubwa za umeme zinazochangia miradi mingi ya maji vijijini kutofanya vizuri.
‘‘Pampu za aina hii zinahitajika sana kwenye Sekta ya Maji kwa sasa kwa kuwawezesha wananchi walio mbali na mifumo ya miradi mikubwa ya maji kufikiwa na huduma kwa gharama nafuu kuanzia Shilingi 300,000 kulingana na mahitaji ya mteja. Tutashirikiana na COSTECH tufanye utaratibu wa kuziboresha tuanze kuzitumia mara moja.
Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Kalobelo ameambatana na timu ya wataalam wa Sekta za Maji, Nishati na Elimu kwa dhumuni la kutoa ushauri na kuona namna bora ya kuongeza tija kwa wabunifu wa umeme John Fute na Lainery Ngailo   kulingana na maelekezo ya Mhe. Rais, Dkt. John Magufuli aliyoyatoa Julai 13, 2019 kwa taasisi husika za Serikali mara baada ya kukutana na wabunifu hao Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Wabunifu hao wa kuzalisha umeme kutoka mkoani Njombe wamejikita katika kazi ya uzalishaji umeme kwa kutumia nguvu za maji na teknolojia ya uundaji wa pampu za maji.

 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo akizungumza na John Fute (kulia) mtaalam wa uzalishaji umeme kwa kutumia nguvu za maji na teknolojia ya uundaji wa pampu za maji, mkoani Njombe.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo akiwa na timu wa wataalamu wa Sekta ya Maji, Nishati na Elimu kwenye eneo la kazi la wabunifu John Fute na Lainery Ngairo, mkoani Njombe.

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila yafanya upasuaji mkubwa wa kuondoa vivimbe kwenye ubongo

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji mkubwa wa kuondoa vivimbe katika mishipa ya damu kwenye ubongo (cerebral aneurysms) kwa mgonjwa aliyekywa akisumbuliwa na tatizo hilo.
Kufanyika kwa upasuaji huu ni hatua ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi na kuhakikisha matibabu ya ubingwa wa juu yanatolewa hapa nchini.
Upasuaji huu umechukua muda wa takribani saa sita na umefanywa na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Daktari Bngwa Mshauri wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu, Prof. Huh Seong kutoka Yonsei, Korea Kusini.
Kwa mujibu wa Daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu Dkt. Raymond Makundi, Hospiali ya Mloganzila inakua ya pili kwa hospitali za umma hapa nchini kufanya upasuaji huu wa kibobezi.
“Awali wagonjwa waliohitaji huduma hii walikuwa wakipelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na uchache wa wataalam na ukosefu wa vifaa tiba, hivyo kwa mgonjwa kama huyu mmoja ambaye tumemfanyia upasuaji endapo angepelekwa nje ya nchi ingegharimu zaidi ya shilingi milioni 40 ikiwa ni gharama za upasuaji, usafiri, malazi pamoja na msindikizaji,’’ amesema Dkt. Makundi.
Tatizo la vivimbe katika mishipa ya damu kwenye ubongo hutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kurithi vinasaba ambavyo mtu huzaliwa navyo, uvutaji wa sigara na maambukizi ya vijidudu kama bakteria vinavyoathiri mishipa ya damu.
 Ugonjwa huu huchelewa kugundulika kutokana na watu kutokufahamu dalili zake, upungufu wa vifaa vya uchunguzi pamoja na watalaam kuchelewa kubaini tatizo hilo mapema. Baadhi ya dalili ni kupata maumivu makali ya kichwa, kuona vitu viwili viwili (double vision) na kupoteza fahamu.
Naye Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu, Dkt. Alvin Miranda amesema lengo la upasuaji ni kufunga vivimbe hivyo kwa kutumia vifaa tiba maalum (aneurysm clips) ili kuzuia damu isiendelee kuvuja katika ubongo.
“Mgonjwa anapopata tatizo la kuvuja damu kwenye ubongo kwa mara ya kwanza anakua katika hatari ya kupoteza maisha kwa asilimia 30 na endapo akivuja damu kwa mara ya pili hali hii inaweza kusababisha kifo kwa asilimia 70 hadi 80,” amefafanua Dkt. Miranda.
Takwimu zinaonesha wastani wa asilimia 3 ya watu duniani hupata tatizo hilo kila mwaka na nusu kati yao, wanawahi kufika hospitalini baada ya mishipa kupasuka, huku wenginge wakipoteza maisha kabla ya kufikia huduma.
Kwa upande wake, Prof Huh Seong amesema Hospitali ya Yonsei ya Korea Kusini itaendelea kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kubadilishana utaalam na kupanua huduma hizi za kibobezi katika magonjwa ya ubongo na mishipa ya fahamu ili kuzifanya ziwe endelevu katika hospitali za umma.
 Madaktari bingwa wa Upasuaji Ubongo na Mishipa ya Fahamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Alvin Miranda (wa kwanza kulia) na Dkt. Raymond Makundi (wa pili kulia) wakiwa katika hatua ya kwanza ya upasuaji.
 Daktari Bingwa Mshauri wa Upasauji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu kutoka Korea Kusini, Prof. Huh Seong (katikati) akishirikiana na wataalam wa Hospitali ya Mloganzila katika upasuaji wa ubongo wa kuondoa vivimbe vilivyopo kwenye mishipa ya damu ndani ya ubongo (surgical aneurysm clipping).
 Daktari Bingwa mshauri wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kutoka Korea Kusini, Prof. Huh Seong (aliyevaa miwani) akifafanua jambo kuhusu upasuaji wa kuondoa vivimbe kwenye ubongo. Kushoto ni Bi. Cosila Tambila ambaye amefanyiwa upasuaji huo na wa kwanza kulia ni Dkt. Alvin Miranda akifuatiwa na Dk. Raymond Mkaundi.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi (kulia) akielezea mipango ya hospitali katika kuendelea kutoa huduma za kibingwa kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa huduma Dkt. Mohamed Mohamed.

ROTARY CLUB UDSM MLIMANI WAPATA RAIS MPYA, NI DK HERI TUNGARAZA

$
0
0
UONGOZI NI KUPOKEZANA VIJITI: Rais Mpya wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Dk Heri Tungaraza (kushoto) akiwa na Rais Mstaafu Lulu Tunu Kaaya (kulia) wakionyesha ishara ya upendo mara baada ya Bi. Catherine Njuguna wa Rotary Club Dar es Salaam Mikocheni (katikati) kumaliza zoezi la makabidhiano kumalizika.
Rais Mpya wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Dk Heri Tungaraza (kushoto) akizungumza machache mara baada ya kutangazwa kuongoza kwa muda wa mwaka mmoja.
Rais Mstaafu wa Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Lulu Tunu Kaaya akizungumza wakati wa halfa ya kumsika Rais Mpya Dk Heri Tungaraza.
Mwanachana wa Rotary Club  Dar es Salaam Mikocheni, Bi. Catherine Njuguna wa Rotary Club Mikocheni (kushoto) akiongea na na Rais Mstaafu Lulu Tunu Kaaya (kulia).
Akivalishwa...
Rais Mstaafu wa Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Lulu Tunu Kaaya (kushoto) akikabidhiwa zawadi na Wanachama wa Rotary Club UDSM Mlimani Prof. Abel Ishumi (kulia).
Wanachama wa Rotary Club UDSM Mlimani Prof. Abel Ishumi akitoa zawadi.
Wanachama wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam wakipata burudani.
Wanachama wa Rotary Club UDSM Mlimani Prof. Abel Ishumi (kushoto) na Edwin Mashayo (kulia).
Rais Mpya wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Dk Heri Tungaraza akimkabidhi zawadi Mwanachana Prof. David Mfinanga ikiwa ni heshima ya kuweza kuifanya club ya UDSM Mlimani kusonga mbele.
Mwanachana wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam Prof. David Mfinanga akitoa shukrani mara baada ya kukabidhiwa zawadi.
 Mwanachama wa Rotary Club Catherine Dar North Club akizungumza machache.
Mwanachama wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam Mona Mwakalinga.
Mwanachama wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam Adolpho Mascharenas akizungumza machache.
Wanachama wa Rotary Club UDSM Mlimani Prof. Abel Ishumi akitoa wosia kwa uongozi mpya.
Picha ya pamoja na Rais Mpya...

Wanachama wakibadirisha mawazo.
Burudani ikiendelea...
Picha ya pamoja na rais Mpya.

Mwanza, Songwe kucheza nusu fainali kesho UMISSETA Soka wavulana

$
0
0
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Michuano ya UMISSETA inayoendelea mjini Mtwara imefikia hatua ya nusu fainali kwa upande wa soka wavulana ambapo katika michezo iliyomalizika leo jioni, timu za soka wavulana kutoka mikoa ya Lindi, Ruvuma, Mwanza na Songwe zimefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuwalaza wapinzani wao akiwemo bingwa mtetezi Tanga ambayo ilitolewa na Lindi.
Kwa matokeo hayo timu ya soka wavulana kutoka mkoa wa Lindi itakutana na Ruvuma kwenye nusu fainali ya kwanza inayotarajiwa kucheza kesho saa nane mchana na kufuatiwa na nusu fainali ya pili itakayowakutanisha vigogo Mwanza watakaochuana na timu ngumu ya Songwe.
Timu ya kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ilikuwa ni timu machachari ya kutoka  mkoa wa Lindi ambayo iliitoa timu ya mkoa wa Tanga kwa penati 3 kwa 1 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana baada ya dakika tisini za mchezo.
Pambano lingine la robo fainali lilizihusisha timu za kutoka mikoa Ruvuma na Kilimanjaro ambapo timu ya soka ya mkoa wa Ruvuma ambayo inaundwa na wachezaji 8 kutoka kwenye kituo cha michezo cha shule ya sekondari Ruhuwiko iliyopo nje kidogo ya Manispaa ya songea iliwafunga timu ya Kilimanjaro kwa magoli mawili kwa bila.
Katika mechi zilizomalizika jioni hii timu za Songwe na Manyara na Mbeya na Mwanza zilimenyana vikali katika michezo mingine ya robo fainali ambapo Songwe waliwalaza Manyara kwa goli moja kwa sifuri na Mwanza waliifunga Mbeya kwa magoli ya penati 5 kwa 3 ya Mbeya baada ya timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za mchezo.
Hata hivyo Mwanza walikuwa na kila sababu ya kushinda mchezo huo kwani kwenye dakika ya 72 walikosa goli la wazi baada ya penati yao kupanguliwa na golikipa wa Mbeya Gerald Hatson na kuokolewa na mabeki wa timu hiyo.
Mara baada ya mchezo huo, Kocha wa Mwanza Mwalimu Tito Mkami amesema kuwa vijana wake walipambana kufa na kupona lakini akawasifu timu ya Mbeya kwa namna ilivyowasumbua na akakiri kuwa  timu hiyo ngumu kwani iliwapa wakati mgumu wachezaji wake wakati wote wa mchezo.
Aidha Mwalimu Mkami alitoa wito kwa Chama cha soka nchini TFF kutoshirikisha mashindano mengine pindi michuano inayoandaliwa na serikali ya UMISSETA na UMITASHUMTA inapofanyika ili kutosababisha michuano hii kukosa wachezaji muhimu kwa timu zao
Naye nahodha wa timu ya soka ya Mwanza Kimwaga Kalunga ambaye ni Mwanafunzi pekee anayechezea timu hiyo kutoka shule maalum ya soka ya Alliance ambaye alisema kuwa hawaihofii timu ya Songwe bali wanaiheshimu kwani timu zote zilizoingia hatua hiyo ni ngumu.
Mapema kesho asubuhi michezo ya nusu fainali kwa upande wa soka wasichana itachezwa katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara ambapo mchezo wa kwanza utawakutanisha wababe Dar es salaam watakaotoana jasho na timu kutoka mkoa wa Iringa, na mchezo mwingine utawakutanisha miamba Mwanza watakaochuana na Ruvuma.
Kwa upande wa mpira wa mikono matokeo ya robo fainali ya mchezo huo iliyochezwa leo jioni inaonyesha kuwa timu za Geita  na Unguja wavulana zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali na zimepangwa kucheza kesho, huku nusu fainali nyingine itawakutanisha Tanga na Morogoro.
Katika mpira wa mikono wasichana, timu zilizofuzu ni Unguja ambao watakuna kesho na Morogoro na Songwe watakaocheza na Mbeya.
Mchezo mwingine ambazo timu zilizofuzu zimejulikana ni netiboli ambapo timu za Morogoro, Tanga, Dar es salaam na Mwanza zimefuzu hatua hiyo ambapo michezo hiyo itachezwa kesho kwa Tanga kukutana na Mwanza na Morogoro kucheza na Dar es salaam.
Katika mchezo wa kikapu kwa upande wa wavulana timu zilizofuzu hatua ya nusu fainali ni Pwani, Unguja, Tanga na Shinyanga ambapo kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa Pwani itacheza na Unguja na Tanga itachuana na Shinyanga.
Kwa upande wa  mpira wa kikapu wasichana Kilimanjaro itamenyana na Mwanza na Morogoro watacheza na jirani zao Dar es salaam.

Baadhi ya watazamaji wakifuatilia mojawapo ya mechi za robo fainali zilizofanyika leo mjini Mtwara
 Mchezaji wa mpira wa volleyball kutoka Tabora Charles Idrisa akipiga smash kuelekea upande wa timu ya mkoa wa Mbeya kwenye mchezo wa nusu fainali ambapo Tabora waliifunga Mbeya kwa seti 2 kwa 1
 Beki wa kulia wa timu ya soka ya Mbeya Idrisa Hamidu akiondoa mojawapo ya hatari iliyoelekezwa kwenye eneo la lango la timu yake kutoka kwa washambuliaji hatari wa mkoa wa Mwanza wakati wa pambano la robo fainali baina ya timu hizo mbili.
 Makamu mwenyekiti wa FEASA bwana Kariuki Gikonyo ambaye alikuwa mgeni rasmi wa pambano la robo fainali kati ya Mbeya na Mwanza akiwa sambamba na Mwenyekiti wa mashindano ya UMISSETA  Bwana Aaron Sokoni (mwenye kofia) wakiangalia mechi hiyo jana iliyofanyika kwenye uwanja wa chuo cha ualimu Mtwara.
Wachezaji wa timu za mkoa wa Morogoro wakichuana vikali na wenzao wa shinyanga kwenye mchezo wa kikapu wavulana hatua ya robo fainali ambapo shinyanga walishinda pambano hilo.

SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA INAENDELEA MALI ZA VIONGOZI WOTE WA UMMA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inaendelea na zoezi la kuhakiki  kwa viongozi wote wa Umma wanaojaza fomu  za tamko la rasilimali na madeni  ili kuepusha mgongano  wa maslahi miongoni mwao.
Kauli hiyo imetolewa leo na  Kamishna wa  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati wa Mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.
Aidha Mh Nsekela amewata Viongozi hao kufanya kazi kwa Uadilifu kwa kufuata Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 ambayo inawataka Viongozi wa Umma kutekeleza Majukumu yao kwa Maslahi ya Taifa.
Alisema lengo ni kutaka viongozi wa umma wafanye kazi kwa kuzingatia maadili na kuweka maslahi ya Taifa mbele badala ya maslahi binafsi.
Mh Jaji Nsekela katika hotuba yake aliongeza kuwa mgongano wa maslahi kwa baadhi ya viongozi wa umma unaweza kulisababisha Taifa hasara ya kuwa na miradi inayotekelezwa chini ya viwango.
Katika hatua nyingine Kamishna huyo wa  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma aliwataka viongozi wote wanaohusika katika ujazaji wa fomu  za tamko la rasilimali na madeni  kutenga muda wa kutosha kujaza fomu zao kwa ufasaha.
Alisema mara nyingi Viongozi wanaojaza fomu  za tamko la rasilimali na madeni wamekuwa wakisubiri siku za mwisho ndio wanaanza kujaza , jambo ambalo linaweza kusababisha kuachwa baadhi ya mali bila kuorodheshwa katika fomu hiyo ya Tamko.
Aliongeza kwamba Kiongozi wa Umma kujaza fomu za Tamko la Raslimali na Madeni ni takwa la Kisheria na ni lazima wala sio ombi. Na kwamba Kiongozi asipojaza fomu hizo na kuzirejesha kwa Kamishna wa Maadili kwa wakati ni kosa la kimaadili kisheria.
Alifafanua kwamba Kiongozi wa Umma anatakiwa kutoa Tamko lake la Raslimali na Madeni yake kila mwaka ifikapo mwishoni mwa Mwaka yaani tarehe 31 Desemba ya kila mwaka.
Mafunzo haya ya Maadili yamehudhuriwa na  Viongozi wa Umma wa Manispaa  zaidi ya Tabora  zaidi ya 200 wakiwemo Wakurugenzi, Makamanda wa polisi na jeshi la wananchi, wakuu wa wilaya, Madiwani, wakuu wa Idara na Vitengo
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua leo Mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.
 Kamishna wa  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Jaji Mstaafu Harold Nsekela akitoa elimu  leo wakati wa mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.

Kamishna wa  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Jaji Mstaafu Harold Nsekela akitoa elimu  leo wakati wa mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.  

Picha na Tiganya Vincent


Introducing Juma Sharobaro's "Cha Upepo" (Offiicial Video)

TCRA YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA ARUSHA

$
0
0
Thadayo Ringo (kulia)Mkuu wa Kitengo kinachoshughulikia maswala ya watumiaji huduma na bidhaa za mawasiliano (TCRA) Rolf kibaja mtaalamu wa maudhui TCRA .


Na.Vero Ignatus, Arusha.

Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA imezindua wiki ya huduma kwa mteja katika chuo cha uhasibu Njiro ikiwa sehemu ya kuielimisha jamii kwa kushirikiana na watoa huduma za simu za mkononi.



Thadayo Ringo ni mkuu wa kitengo kinachoshughulikia maswala ya watumiaji huduma na bidhaa za mawasiliano (TCRA) amesema dhima ya wiki ya utumishi wa umma  imesimama kuhakikisha jinsi gani Taasisi za Umma zinawezesha vijana kujiajiri pamoja na kuangalia muingiliano  wa uhamiaji kutoka vijijini kwenda mjini 



 Amesema kuwa wanaangalia  jinsi gani wanaweza kuikumbatia Teknolojia katika kusaidia utekelezaji wa utoaji huduma jumuishi  na kuhakikisha kwamba wanajenga utamaduni wa utawala bora.



Amesema katika kuzingatia hayo TCRA ilichagua mikoa 5 ambayo inaadhimisha siku hiyo ambapo ni pamoja na Arusha,Mwanza Mbeya Dar es saalam, Dodoma  ambapo wapo kwaajili ya kufanya kampeni ya kusajili watu wanaotumia  huduma za simu za mkononi kwa kusajili line zao kwa kutumia alama za vidole .



Ringo ametaja changamoto kubwa wanayokutana nayo ni pamoja na watu wengi kufikiria kwamba zoezi hilo linalengo la kuchuliwa alama za vidole,bali wao wanahakiki taatifa kwa kutumia alama za vidole,ambapo wengi wanasita kujidikisha.



Aidha amesema katika kipindi chote hicho wananchi wanaalikwa kuwatembelea,na wao wapo tayari kujibu maswali mbalimbali ambapo amesema kuwa tangia zoezi hilo limeanza muamko ni mkubwa na amesisitiza kuwa kabla ya kufika disemba watakuwa wameweza kukamilisha zoezi hilo kwa asilimia kubwa.Picha na Vero Ignatus.


Wanafunzi wa chuo cha uhasibu Njiro wakiwa kwenye foleni ya kuchukua namba ya kitambulisho cha Taifa kwaajili ya kusajili laini kwa mfumo wa Biometric ambapo zoezi hilo limefanyika siku mbili chuoni hapo na siku tatu watakuwa katika soko la kilombero .Picha na Vero Ignatus
Mmoja wa Afisa kutoka NIDA Julieth Raymond,akimsaidia kuelewa.mmoja ya mteja aliyetembekea banda hilo kwaajili ya kupata kitambulisho cha Kitaifa katika chuo cha uhasibu kilichopo Njiro Arusha.Picha na Vero Ignatus.
.

Wanafunzi wa chuo cha uhasibu Njiro wakiwa kwenye foleni ya kuchukua namba ya kitambulisho cha Taifa kwaajili ya kusajili laini kwa mfumo wa Biometric ambapo zoezi hilo limefanyika siku mbili chuoni hapo na siku tatu watakuwa katika soko la kilombero .Picha na Vero Ignatus.
Mmoja wa wafanyakazi kutoka NIDA akinsaidia mteja aliyefika kupatiwa huduma ya kitambulisho cha Taifa.Picha na Vero Ignatus.

HAKUNA UPENDELEO NAFASI ZA JKT ARUMERU - DC JERRY MURO

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewahakikishia mamia ya vijana waliojitokeza katika usahili wa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuwa usahili utafanyika kwa Uwazi na Ukweli na kusisitiza kuwa hapatakuwa na upendeleo zaidi ya kufuata Sheria pmoja na  sifa zinazotakiwa kwa vijana kujiunga na jeshi.
Aliyasema hayo leo ofisini kwakwe  wakati akiongea na Vijana waliojitokeza kwa wingi kuomba nafasi za kuingia katika mafunzo ya JKT ambapo kwa sasa usahili wa kuandikisha vijana hao kwa wilaya ya Arumeru unaendelea. 
DC Muro alibainisha kuwa wao kama watachagua vijana wote wenye sifa ya kujiunga na jeshi hilo na hawatamfumbia macho mtu yeyote ambaye atakuwa anawadanganya Vijana hao kuwa watoe ela ndio wapate nafasi 
"Wapo watu wanaopita uko barabarani wakiomba hela  huku wakiwa wanajinadi 
kwa kuwalaghai vijana hawa kuwa wanauwezo wakuwapa nafasi kitu ambacho sio chakweli hivyo kueni makini na msikubali kudanganywa mkatoa fedha zebu, nanapenda kusema ole wenu nyie tuwakute nyie walaghai hatua kali za kisheri tutawachukulia, na vijana iwapo mtu akiwafata kutaka fedha msisite kutoa taarifa sehemu husika"alisema DC Muro
Alifafanua kuwa zoezi hili la usahili linafanywa kwa uwazi na ukweli na katika zoezi hili hapatakuwa na upendeleo wowote ule Kwani sheria zitafutwa. 
Aidha alibainisha mara baada ya kukamilisha uchambuaji wa majina kwa vigezo vya sifa na nafasi zilizopo watabandika majina kwa vijana watakaopita awamu ya kwanza na kisha kuingia awamu ya pili ya vipimo vya kubaini afya za vijana kikiwemo kipimo cha madawa ya kulevya pamoja na bangi.
Aliwapongeza vijana wote waliojitokeza kujiunga na jeshi lakujenga taifa (JKT) Na kubainisha kuwa wametaka kumuunga mkono Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kufanya kazi kwa uweledi ,ukweli na uwaminifu. 
"Vijana hawa wamejitokeza kwa wingi na hii wameonyesha dhamiranzuri yakutaka kutumikia taifa lao kupitia jeshi la ulinzi na usalama nanapenda kuwapongeza sana kwani wameuonyesha uzalendo mzuri wa kutaka kutumikia taifa lao "alisema Muro. 
Alisema kuwa wanaamini kuwa unapokuwa na jeshi imara najeshi lenye nithamu ,basi hilo ndio jeshi sahii kwaajili ya Kupambana ,  Kulinda nakupigania taifa letu .
Mkuu Wilaya ya Arumeru  Mhe. Jerry Muro akiongea navijana waliojitokeza ofisini kwakwe kwa ajili wa usahili wa kuingia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). 

DC MBONEKO AFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO..AKERWA NA DOSARI HALMASHAURI YA SHINYANGA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kukumbana na dosari ambapo baadhi ya  majengo yameanza kutoa nyufa kabla hata ya kuanza kutumika.
Mboneko amefanya ziara hiyo leo Juni 18,2019 kwa kukagua ujenzi wa madarasa mawili, matundu ya vyoo pamoja na nyumba mbili za walimu katika shule ya msingi Masunula iliyopo kata ya Usule, Shule ya sekondari Itwangi, kukagua madarasa mawili, shule za msingi Tinde “A” na “B” pamoja kukagua madarasa na matundu ya vyoo kwenye shule hizo  na kukumbana na dosari hizo.Mkuu huyo wa wilaya pia amekagua  huduma za matibabu katika kituo cha afya Tinde.Mradi mwingine alioukagua ni Skimu ya umwagiliaji iliyopo kata ya Nyida ambapo Mboneko ameagiza ukamilishwe kwa wakati kabla ya mvua kuanza kunyesha mwezi Oktoba mwaka huu, ili wakulima wanufaike kwa kulima zao la mpunga na kuwainua kiuchumi.Akikagua miradi hiyo ya ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu na matundu ya vyoo, Mkuu huyo wa wilaya alieleza kutofurahishwa na ujenzi wake kutokana na kujengwa chini ya kiwango na tayari majengo yameanza kutoa nyufa kabla hata ya kuanza kutumika na kuagiza dosari hizo zifanyiwe kazi haraka sana.Alisema serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo, lakini thamani ya fedha hizo imekuwa haionekani kutokana na miradi yake kujengwa chini ya kiwango matokeo yake inaendelea kuwagharimu kwa kuifanyia marekebisho ya mara kwa mara.“Nakuagiza Mhandisi wa ujenzi wa halmashauri, muwe mnakagua miradi hii pale inapojengwa pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu na siyo kuwaachia hawa mafundi pekee (Local Fundi) kufanya kazi peke yao, na kututekelezea miradi chini ya kiwango,” alisema Mboneko.“Kuna baadhi ya miradi hamjawahi kufika kabisa kukagua hadi inamalizika kujengwa kama ujenzi huu wa madarasa katika shule ya Sekondari Itwangi, hakuna kitu kilichofanyika, jengo lina nyufa huku rangi zake zikipakwa hovyo hovyo tu, hivyo nakutaka usimamie marekebisho yote haya,”aliongeza.Katika hatua nyingine aliuagiza uongozi wa halmashauri kuongeza idadi ya wahudumu wa afya katika kituo cha afya Tinde baada ya kukuta kuna upungufu mkubwa wa wauguzi, huku akitoa wito kwa wazazi kuwanyonyesha maziwa ya mama watoto wao ili wapate afya njema na kukua kiakili. Hata hivyo, Mhandisi wa ujenzi wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga William Lusiu, alikiri kutofika kwenye ujenzi wa  baadhi ya miradi hiyo ya maendeleo, kwa madai ya kukabiliwa na ukosefu wa gari  kwa ajili ya kutembelea miradi, huku akiahidi kusimamia marekebisho yote ya mapungufu ambayo yamejitokeza kwenye ujenzi wa miradi.TAZAMA PICHA HAPA CHINIMkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Masunula Kata ya usule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini,kulia ni mkuu wa shule hiyo Gladius Kujerwa na (kushoto) ni Mhandisi wa halmashauri hiyo William Lusiu akiandika dosari ambazo zimejitokeza kwa ajili ya kuzifanyia marekebisho.Ukaguzi ujenzi wa madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Masunula.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiangalia nyufa katika madarasa ya shule ya msingi Masunula.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akikagua utengenezaji wa madawati katika shule ya msingi Masunula na kubaini yametengezwa chini ya kiwango na kuagiza yarekebishwe.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa nyumba za walimu katika shule ya msingi Masunula.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiendelea na ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari Itwangi.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akiangalia nyufa katika ujenzi wa madarasa katika Sekondari ya Itwangi.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akimwonyesha nyufa kwenye ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Tinde "A" Mhandisi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga William Lusiu.Ukaguzi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Tinde "A" ukiendelea.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji katika kata ya Nyida na kuagiza ukamilike kwa wakati kabla ya mvua kuanza kunyesha.Ukaguzi wa Skimu ya umwagiliaji katika kata ya Nyida ukiendelea.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiangalia mtoto aliyezaliwa kwenye kituo cha Afya Tinde.Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiangalia kitabu cha mahudhurio ili kubaini kama mhandisi wa ujenzi wa halmashauri huwa anahudhuria kwenye kukagua ujenzi wa miradi ya maendeleo na kubainika huwa hatembelei miradi hiyo na kusababisha kujengwa chini ya kiwango.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akitoa maelekezo kwa mhandisi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga William Lusiu, kuwa anatembelea ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa mafundi wa mitaani (Local Fundi) ili kuondoa changamoto ya kujengwa miradi chini ya kiwango.Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

SPECIAL REPOT - Investing In The Future: Tanzania’s Blueprint To Become A Middle Income Nation

$
0
0

Under the guidance of President John Pombe Joseph Magufuli, Tanzania is scheduled to become a middle-income nation by 2025. The Development Vision 2025 is focused on creating peace and stability, freedom from corruption, investment in the education of the Tanzanian people and a competitive and sustainable economy. The key to Magufuli’s Vision is industrialization. “There is no economy in the world that can thrive without industrialization and we are just beginning,” states Mr. Subhash Patel, Chairman of the Motisun Group. Magufuli’s Vision of an industrialized nation is well underway.


The construction of Tanzania’s US$14.2 billion Standard Gauge Railway, stretching 2,561 kilometres connecting Dar es Salaam port to its land-locked neighbours, is an infrastructure project that will enhance trade opportunities for Tanzania. “Projects such as the SGR could help lower transport costs and improve economic activity from a reduction of production and operational costs, lower cost of consumer goods and increased transit of goods passing through Tanzania to landlocked countries,” says Faraj Abri, director of ASAS. This will increase relationships with East African countries and strengthen all economies of the region.
“As a country, our vision is clear. My administration is determined to make sure that Tanzania achieves its development aspiration of being a middle-income country by 2025 as stated in the National Development Vision. I insist to my government officials and the people that our Vision can be achieved with close collaboration of the public and private sector. As you have seen, I am pioneering the undertaking of major reforms to create more favorable investment environment to ensure that private sector drives our future growth.”
H. E. President John Pombe Joseph Magufuli

The Tanzania Port Authority is working toward this same agenda with the construction of the Dar es Salaam Maritime Gateway Project (DMGP), which “will support the financing of crucial investments in the Port with the aim of improving its effectiveness and efficiency for the benefit of the public and private stakeholders,” says Eng. Deusdedit C.V Kakoko, Director General of TPA. In conjunction with the DMGP, TICTS is working to expand the additional capacity that will be needed at Tanzania’s ports. Chief Executive Officer, Jared Zerbe, states: “The assistance and cooperation received from the government of Tanzania, TPA and our customers using the port have been the source of growth.”
In addition to opening new doors for local and international trade, Tanzania has signed a groundbreaking contract with Egypt to build a new 2,115 MW hydroelectric power station. In an effort to decrease reliance on fossil fuels, the Rufiji Hydro Plant will be the largest in East Africa and is invaluable to Tanzania’s transformation. “The national target for the energy sector is to make sure that we reach 5,000 MW by 2020 and at least 10,000 by 2025. Construction on the 2,115 MW Rufiji Hydro Power Plant Project has just begun and this will greatly help us meet our target,” says, Hon. Medard Kalemani, Tanzania’s Minister of Energy.
            Accessible and reliable energy sources will aid the Finance and ICT sectors in their dedication to the Vision 2025 to create financial inclusion and reliable communication services for the Tanzanian people. As the economy of Tanzania inevitably improves, a system must be in place for its people to benefit from it. Abdulmajid Mussa Nsekela, Managing Director of CRDB Bank states, “In line with the financial inclusion framework, we have developed a digitalization strategy roadmap, which is aimed at ensuring all Tanzanians and residents have proximity to affordable superior financial services.” Other banking entities such as Stanbic approach inclusivity in a way that allows ease of use and convenience. Kenrick Cockerill, CEO of Stanbic Bank Tanzania says, “We have an ecosystem approach to our clients, which means we like to bank entire communities and not just individual clients, which enables us to offer more seamless transactability across all the players in the ecosystems and value chains that we are supporting.“
            Financial inclusion is made even more possible through mobile money transactions, which rely upon a stable telecom sector in order to function effectively. TCRA works to ensure access to reliable, affordable and secure communication services for Tanzanians and foreign investors alike. “Ninety-four percent of the population is now covered by mobile networks,” says Eng. Kilaba. These coverage and technological goals are shared with Tigo, the fastest growing telecom company in Tanzania. Managing Director Simon Karikari says, “We pride ourselves in being committed to Tanzania as a country. We have been here for 25 years and our determination is for long term growth and potential of this country. We continue to invest in the latest technology such as 4G+ because we believe data is the future.”
            With this level of investment in the infrastructure, communication, technology, energy, and finance sectors, the Vision 2025 is on schedule to become a reality, placing Tanzania on the map as a middle-income country, and surely as the guiding light for other African nations to follow their example.

ForceAccount nusura iondoke na Afisa Elimu Kongwa

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo ameagiza Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuandika barua ya kujieleza kwanini amekaidi kutekeleza miradi ya Elimu kwa kutumia Force Account.
Akizungumza katika ziara yake Wilayani humo Mhe. Jafo amemtaka Afisa Elimu Nelson Milanzi ambaye yuko Mtwara kwenye UMISETA kurejea kwenye kituo chake cha kazi, kurejesha fedha za safari alizopewa kwa siku ambazo alitakiwa kuwepo kwenye mashindano hayo ya michezo ya shule za sekondari ambayo yatamalizika mwishoni mwa wiki hii na kuandika barua ya kujieleza kwanini asichukuliwe hatua.
Jafo amesema haiwezekani Miradi ya Elimu kukwama kwa sababu ya Afisa Elimu kutofautiana na uongozi kwa maslahi  binafsi kwa kutaka kujenga miundombinu ya shule kwa kutumia mkandarasi na sio mafundi wa jamii (Force Account) kama ilivyoada ya miradi ya Halmashauri.
“Fedha zimeletwa tangu January 2019 kwa ajili ya shule ya Sekondari Sejeli na Kongwa kujenga Mabweni, bwalo la chakula, maabara, madarasa pamoja na nyumba za mwalimu lakini mpaka leo hii ujenzi wa majengo hayo ndio kwanza uko katika hatua za msingi huu ni uzembe wa hali ya juu;
Kazi hii imeanza asubuhi ya leo baada ya kusikia nakuja ziara, hata haya matofali hayajauka, mchanga ndio unashushwa na inaonekana mafundi mmewakusanya huko kijijini ili ujenzi uonekane unaendelea vizuri ila kiuhalisia kazi hii ilikua imesimama kabisa hili ni tatizo kubwa na mnamuangusha Spika kwa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai ambaye anawapigania wananchi wake ili wapate miradi lakini watendaji mnakwamisha alisema Jafo.
Miradi mikubwa karibu kila kona ya Tanzania tumetekeleza kwa kutumia Force Account na imefanikiwa kwa kiwango kikubwa tumejenga majengo ya kutosha na yenye ubora wa hali ya juu sasa inakuwaje mtu mmoja anaanza kujadili kuhusu kutumia Force Account tena kwa muda mrefu hii ni hujuma na inakwamisha maendeleo ya wananchi wa Kongwaaliongeza Jafo.
Sasa nimtake huyo Afisa Elimu ambaye ametajwa kuwa sababu ya kuchelewesha utekelezaji wa miradi hii aandike barua ya kujieleza kwanini miradi hii ipo katika hatua hii wakati fedha zilishaletwa kuanzia Januari na kupitia barua hiyo ndiyo itatupa mwelekeo kama anastahili kubaki hapa au apangiwe kazi nyingine.
Akizungumzia ucheleweshaji wa miradi hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dr. Omary Nkulo amesema pamekuwa na mvutano wa namna ya kutekeleza miradi hiyo wakati Afisa Elimu akitaka kazi hizo apewe mkandarasi baraza la madiwani waliamua itumike force account hapo ndipo pakawa na ucheleweshaji sababu Afisa Elimu alikua anachelewesha kupitisha baadhi ya vitu  kwa sababu mapendekezo yake hayakukubalika.
Dr. Nkulo aliongeza kuwa halmshauri  inachangamoto ya wahandisi wa ujenzi kwa namna kubwa wanatakiwa kusimamia miradi hiyo na aliyepo ni fundi mchundo(Technician)  ambaye ndiye anayesimamia miradi yote inayotekelezwa hapa Kongwa hiyo pia imekuwa ni miongoni mwa sababu ya kuchelewa kwa baadhi ya miradi.
Miradi hiyo ya Elimu imetakiwa kukamilika mapema Mwezi August,2019 ili iweze kuchukua wanafunzi wa bweni na miundombinu mingine itumike kama ilivyokusudiwa.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (mbele) akiwasili katika shule ya Sekondari Sejeli kukagua maendeleo ya ujenzi wa bweni, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe.Deo Ndejembi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (mbele) akitoa amelekezo baada ya kutorishihwa na maendeleo ya ujenzi katika Shule ya Sekondari Kongwa.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akiangalia namna ambavyo mafundi wanaendelea na ujenzi wa bweni la Sekondari Sejeli
 Mafundi wakiendelea na ujenzi wa bweni la Seleji sekondari

TASAF YAWAJENGEA UELEWA VIONGOZI KUHUSU MAJARIBIO YA UTAMBUZI WA KAYA ZA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI SEHEMU YA PILI MKOANI MTWARA.

$
0
0
Na .Estom Sanga-Mtwara. 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umeanza mkakati wa kuwajengea uelewa viongozi ,Watendaji na Wawezeshaji katika ngazi ya halmashauri za Wilaya juu ya zoezi la utambuzi wa Kaya za Walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini ili kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa ufanisi mkubwa . 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi kilichofanyika mjini Mtwara, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,bwana Ladislaus Mwamanga amesema zoezi hilo linakusudia kuboresha mapungufu yaliyojitokeza kwenye sehemu ya kwanza ya utekelezaji wa Mpango huo inayotarajiwa kukamilika hivi karibuni na kuwa majaribio hayo ambayo kwa kiwango kikubwa yatatumia njia ya mfumo wa kompyuta yatafanyika katika Halmashauri za wilaya ya Siha,Mtwara na Tandahimba. 

Bwana Mwamanga amesema baada ya kukamilika kwa majaribio hayo, kazi ya kutambua Kaya za Walengwa watakaojumuishwa kwenye Mpango itafanyika nchini kote ili kutekeleza maagizo ya Serikali ya kujumuisha maeneo yote kwenye shughuli za Mpango. Katika Awamu ya Kwanza ya Mpango serikali kupitia TASAF imeweza kutekeleza Mpango huo kwa asilimia 70 ya mitaa/vijiji/shehia na hivyo asilimia 30 iliyosalia itakamishwa katika sehemu ya pili ya Mpango itakayotekelezwa kwa takribani miaka mitano ijayo. 

Akifafanua Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema mkazo mkubwa katika sehemu ya pili ya Mpango imewekwa zaidi katika kuhamasisha Walengwa wa Mpango kufanyakazi kwenye miradi ya Maendeleo watakayoiibua na kisha kulipwa ujira ili waweze kujiongezea kipato na kupunguza adha ya umaskini. 

“…tumeweka mkakati bora zaidi ya kutekeleza maagizo ya serikali ya kupunguza dhana ya Walengwa wa Mpango kuwa tegemezi” amesisisitiza bwana Mwamanga. 

Amewahimiza Viongozi,Watendaji na Wawezeshaji kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye mikutano ya utambuzi wa Kaya za Walengwa ili kuondoa uwezekano wa kaya zenye uhitaji kutojumuishwa kwenye Mpango na hivyo kuondoa manung’uniko baada ya kuanza kwa sehemu ya pili ya Mpango unaotarajiwa kuzifikia takribani Kaya milioni 1.3 ikilinganishwa na Kaya Milioni 1.1 zilizoandikishwa katika sehemu ya Kwanza. 

Bwana Mwamanga amesema kutokana na usimamizi thabiti wa Serikali katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, kumekuwa na mafanikio makubwa kwa Kaya za Walengwa kuanza kuboresha maisha yao huku sehemu kubwa ya kaya hizo zikitumia fursa ya kuwemo kwenye Mpango kuanzisha shughuli uzalishaji mali jambo ambalo amesema limeendelea kuvutia Wadau mbalimbali wa Maendeleo kutaka kuchangia zaidi raslimali fedha na Utaalam. 

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara bwana Evold Mmanda amesema TASAF kwa kiwango kikubwa imekuwa kielelezo bora cha kuwafikia wananchi wanaoendelea kuishi katika mazingira ya umaskini kutokana na namna Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini walivyotumia fursa hiyo kupunguza athari za Umaskini. 

Bwana Mmanda amewataka viongozi katika maeneo ya utekelezaji wa shughuli za Mpango kuendelea kuwahamasisha wananchi kuuchukia umaskini kwa vitendo jambo ambalo amesema linawezekana ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF(aliyesimama) akizungumza kwenye kikao kazi cha viongozi ,watendaji na wawezeshaji wa majaribio ya utambuzi wa Kaya za Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika  Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evold Mmanga (aliyesimama) akizungumza kwenye kikao kazi cha viongozi ,watendaji na wawezeshaji wa majaribio ya utambuzi wa Kaya za Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika  Mtwara.

 Mtaalamu wa Mafunzo na Uwezeshaji wa TASAF Bi. Mercy Mandawa akitoa maelezo katika kikao kazi cha viongozi,watendaji na wawezeshaji kuhusu utekelezaji wa majaribio ya utambuzi wa kaya za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

 Baadhi ya Washiriki wa kikao kazi cha kujenga uelewa wa uetekelezaji wa majaribio ya utambuzi wa kaya za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini (picha ya juu na chini).


 Picha ya pamoja

Vijana watakiwa kurudisha mikopo yote waliyokopeshwa

$
0
0
Na.Vero Ignatus,Arumeru

Vijana wametakiwa kuhakikisha wanarudisha mikopo yote waliyokopeshwa kwenye vikundi vyao ili kusaidia kukuza mfuko wa Wazira na kutoa fursa ya vikundi vingine kukopeshwa.

James Kajugus ni Mkurugenzi wa idara ya vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu, ametoa maelekezo hayo alipokuwa akitembelea vikundi mbalimbali vya vijana katika 
halmashauri ya Meru.

Amesema Wizara kupitia mfuko wake wa maendeleo ya vijana ulitoa kiasi cha fedha Milioni 103 kwa halmashauri ya Meru kwa lengo la kukopesha vikundi mbalimbali vya vijana vinavyofanya shughuli za maendeleo na ukuzaji wa uchumi.

“Nashangwazwa sana na taarifa hii ya vikundi vingi vya vijana kupata 
fedha za serikali lakini wameshindwa kurejesha na hata Saccoss ya vijana 
Meru ambayo ndio inasimamia fedha hizo imeshindwa kuvifuatilia vikundi 
hivi ili virejeshe mikopo hii”.

Amesisitiza zaidi juu ya fursa mbalimbali zinazotolewa na Wizara kupitia 
idara ya vijana mbali na mikopo kuwa ni fursa za kuongeza ujuzi kwa 
vijana wabunifu ambao hawajasomea na fursa za mafunzo mbalimbli kwa 
vijana.

Akielezea changamoto zinazosababisha vikundi vya vijana kushindwa 
kurejesha mikopo Mkurugenzu Mtendaji wa Halmashauri ya Meru bwana 
Emmanuel Mkongo, amesema vijana wengi hawaaminiani kwenye vikundi 
vyao na hiyo kupelekea vingi kuvunjika au wanavikundi kukimbia na 
mikopo hiyo

Pia, amesema kuna hali ya siasa kuingilia ufuatiliaji wa fedha hizi za 
mikopo na hivyo kufanya mazingira ya urejeshaji kuwa magumu zaidi na 
baadhi ya vikundi vya vijana kuingia kwenye siasa hizo.Aidha, amesema mbali na changamoto hizo bado halmashauri yake kushirikiana na maafisa husika wanaendelea kuhakikisha fedha zotezilitolewa na Wizara na halmashauri zinarejeshwa ili kutoa nafasi ya vikundi vingine kunufaika pia.

Nae mwenyekiti wa kikundi cha Old is Gold Arts group bwana Samola Mloe, 
amesema mikopo ya vijana inayotolewa na Wizara imesaidia sana kikundi 
chao kukua na mafunzo waliyopewa na halmashauri yamewasaidia pia 
kupata masoko kupitia mitandao ya kijamii nje ya nchi.

Bwana Kajugusi yupo katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Arusha kwa 
lengo la kutembelea vikundi mbalimbali vya vijana na kukagua miradi ya 
maendeleo inayofanywa na vikundi hivyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana bwana James Kajukusi(mwenye suti nyeusi)akisisitiza jambo kama anavyoonekana katika picha.

Mkurugenzi wa Idara ya Vijana bwana James Kajukusi(mwenye suti nyeusi) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Emmanuel Mkongo katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images