Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Mama Janeth Magufuli amjulia hali Mama Maria Nyerere Jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Mke wa Rais, Mhe. Mama Janeth Magufuli akimjulia hali Mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere anayepatiwa matibabu Jijini Dar es Salaam.


MASHINDANO YA MISS ARUSHA YAZINDULIWA RASMI

$
0
0
Warembo wanaopambania taji la miss Arusha wakiwa wamejipanga tayari kwa kumpokea ngeni rasmi katika Hotel ya Kibo Palace leo Jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya miss Arusha kama wanavyoonekana pichani.Picha na habari na Vero Ignatus.
Washiriki wa Miss Arusha wapatao 22 wakiwa katika pozi ambapo tarehe 5julai mwaka huu atapatikana atakayekalia kiti cha miss Arusha 2019
Mgeni rasmi Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi James Manyama msaidizi wa RPC akiwasili katika hotel ya Kibo Palace tayari kwa uzinduzi wa mashindano ya kumsaka miss Arusha 2019.
Mgeni rasmi Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi James Manyama msaidizi wa RPC akisalimiana na mmoja wawalimbwende wanaoshindania taji la Miss Arusha 2019.
Mgeni rasmi Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi James Manyama msaidizi wa RPC akikata utepe ishara ya uzinduzi rasmi wa mashindano hayo ya miss Arusha 2019
Mgeni rasmi Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi James Manyama msaidizi wa RPC akizungumza katika uzinduzi rasmi wa misa Arusha 2019
Walimbwende wakiwa wanatembea mara baada ya kumpokea mgeni rasmi katika hotel ya Kibo Palace Jijini Arusha
Walimbwende wakiwa wanatembea mara baada ya kumpokea mgeni rasmi katika hotel ya Kibo Palace Jijini Arusha
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi James Manyama msaidizi wa RPCakizungumza katika uzinduzi wa mashindano hayo
Walimbwende wanaoshindania taji la Miss Arusha wakiwa wanafungua Shampein mara baada ya mgeni rasmi kuzindua rasmk mashindano hayo.
Basil Elias meneja wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha , Tilly Chizenga mwekiti wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha 2019 wakigonganisha glass pamoja nalimbwende kama ishara ya uzinduzi wa mashindano hayo

Mgeni rasmi Msaidizi wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Basil Elias meneja wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha , Tilly Chizenga mwekiti wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha 2019 wakigonganisha glass pamoja nalimbwende kama ishara ya uzinduzi wa mashindano hayo.
Tilly Chizenga mwekiti wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha 2019.akizungumza na waandishi wa habari jatika uzinduzi wa Miss Arusha katika hotel ya Kibo Palace Jijini Arusha leo.


Na.Vero Ignatus ,Arusha.


Mashindano ya miss Arusha yamezinduliwa rasmi leo jijini Arusha na Afisa Mnadhimu Mkoa (SO 1) ACP Kamishina msaidizi wa polisi katika hotel ya kibo palace iliyopo jijini hapa.

Tilly Chizenga ni mwekiti wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha2019 amesema uzinduzi huo unatoa fursa kwa warembo hao 22 kuingia kambini kuanzia kesho juni 8 hadi hapo yatakapo hitimishwa rasmi julai 5 mwaka huu. 

Arusha ametaja zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa amesema ni zawadi zenye mlengo na fursa kwa washindi ,ikiwemo nafasi ya masomo the east Africa institute na Mahusiano ya Kimataifa,fursa ya kimasomo kutoka TCI

Akizindua mashindano hayo Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi James Manyama msaidizi wa RPC Arusha amesema jeshi ka Polisi nchini wanaamini katika kutengeneza Raia wema waliolelewa katika ngazi ya familia Kidini mashuleni na vyuoni ambapo kazi ya jeshi hilo inakuwa rahisi zaidi kwani vibaka,majambazi hawana nafasi katika jamii.

Amesema Jeshi la polisi linaunga mkono mafunzo ya uraia mwema wanayopata walimbwende hao ambapo amewataka viongozi wakiona watahitaji mafunzo kutoka katika jeshi la polisi wapo tayari kwaajili yao.

"Sisi sote ni jamiii moja ya watanzania ambapo tukishirikiana kwa pamoja jamii zetu zitakuwa katika makuzi mema ambayo hayatakuwa na uhalifu.alisema"

Basil Elias meneja wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha 2019 Kamati ya miss amesema kuwa kamati hadi warembo wenyewe wamejipanga kuhakikisha kwamba wanauwakilisha mkoa vizuri siyo kwenye ulimbwende tu bali hata katika utalii na jitihada hizo watazifanya hadi katika ngazi ya taifa .

Tumeshirikisha wadau mbalimbaki haswa warembo kuelezea namna mkoa wa Arusha uko juu katika maswala ya utalii.Amesema kuwa wamejioanga kutembelea maeneo mbalimbali katika wilaya ya Arusha mjini wilaya za jirani ili waweze kushirikiana na jamii katika shughuli mbalimbali .

Tumeweza kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule namna ya matumizi sahihi taulo za kike ambapo ilienda sambaba na ugawaji wa taulo katika shule mbili Naurei na Sekei zote zikiwa za Arumeru.alisema

Amesema kuwa warembo hao hivi karibuni wameweza kushirikiana na jamii na wadau mbalimbali kutembelea kituo cha wazee cha mkoa wa Arusha kwaajili ya kutoa vyakula na huduma zingine.

Vijana waaswa kuchangamkia Fursa ya kutengeneza mifuko mbadala

$
0
0

Na.Vero Ignatus,Arusha

Vijana nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya kutengeneza mifuko mbadala ili kuinua vipato vyao na kupunguza tatizo la ajira linalowakabili vijana wengi hususan waliohitimu elimu katika vyuo mbali mbali.

Akizungumza katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya utengenezaji wa mifuko hivyo pamoja na mafunzo ,Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Okoa New Generation Neema Robert amesema kuwa vijana wanapaswa kutumia fursa hiyo ili kuongeza idadi ya wazalishaji wa vifungashio hivyo na kupelekea bei kuwa rafiki kwa wananchi kutokana na uzalishaji kuongezeka.

Kwa upande wao Vijana waliopatiwa mafunzo ya kutengeneza mifuko iliyotolewa kwa njia ya vitendo zaidi Rosemary Shedrack amesema kuwa kwa sasa wameanza kutengeneza mifuko na kuisambaza katika masokombalimbali pamoja na kujipatia fedha zinazowasaidia kujikimu na kujiendeleza kimaisha.

Mary Daudi ni moja kati ya vijana wanaotumia fursa hiyo amewataka vijana wengine kuiga mfano na kutumia fursa hiyo kubadilisha maisha yao kwani vifungashio hivyo vinahitajika kwa wingi nchini baada ya serikali kupiga marufuku mifuko ya plastiki.

KIONGOZI MBIO ZA MWENGE WA UHURU AHAMASISHA WANANCHI KUFANYA KAZI KWA BIDII,KUTUNZA VYANZO VYA MAJI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akikabidhiwa mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe tayari kabisa kwa kukimbizwa katika wilaya ya Arumeru, ambapo katika wilaya hiyo ina Halmashauri mbili, ambapo jumla ya miradi nane imezinduliwa Katika halmashauri ya Arusha na katika halmashauri ya Meru itakaguliwa na baadhi kuzinduliwa
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza jambo kabla ya kukabidhiwa mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe tayari kabisa kwa kukimbizwa katika wilaya ya Arumeru

 kiongozi wa mwenge wa uhuru  kiongozi wa Mbio za mwenge  wa uhuru kwa mwaka 2019 Mzee Mkongea Ally akifungua shule ya sekondari ya odonyowas 

 Mazungumzo na Wafadhili
kiongozi wa Mbio za mwenge  wa uhuru kwa mwaka 2019 Mzee Mkongea Ally akikata utepe ishara ya kuzindua mradi wa maji wa layout srwsita uliopo katika halmashauri ya Arusha Dc.


 Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mzee Mkongea Ally amewataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuendeleza kumpinga adui ujinga pamoja na kutunza vyanzo vya maji.

 Pia amesema Serikali  wameingia mikakati ya kuhakikisha  wananchi wanapata maji safi na salama kwa ajili ya wananchi wao huku akieleza kuwa Serikali imetenga kiasi cha  Sh.trilioni 9.2 kuhakikisha wananchi wao wanapata maendeleo.

Ally ameyasema hayo wakati akizindua miradi ,kuweka jiwe la msingi pamoja na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo .Amesema   maji ni rasilimali nzuri inayochingia kuleta maendeleo ya nchi yetu, hivyo wananchi wanatakiwa kutunza mazingira hususa ni vyanzo hivi vya Maji. 

"Nakatika suala hili la kutunza vyanzo vya maji niwasihi  wananchi wenzangu kuacha kuchunga mifugo yetu katika vyanzo vya maji pamoja na nakuacha kufanya shughuli za kibinadamu  katika vyanzo vya maji, "Mzee Mkongea Ally.Pia amesema maji ni haki ya kila mtu, hivyo ni wajibu wa na kila mwananchi  kutunza vyanzo hivyo vya maji 

 Ameongeza kuwa hivi karibuni nchi inaelekea katika kipindi cha uchaguzi wa Serikali za vijiji pamoja na mitaa, hivyo amewataka wananchi hususa vijana na wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ambazo zinagombaniwa 

Pia amewataka wananchi kujitokeza kusikiliza sera za wagombea hao na kufanya maamuzi ya kuchagua kiongozi ambaye ataweza kuiongoza vyema na kuwaletea wananchi maendeleo

"Wananchi wenzangu jitokezeni kusikiliza sera za hawa viongozi wanaogombea ili muweze kufanya uchaguzi sahihi katika chaguzi za serikali zijaazo na msichague bora kiongozi bali chagueni kiongozi bora,"amesema.

Pia amewataka wananchi kulipa kodi kwani kodi ndio msingi wa kuleta maendeleo ya taifa letu, kwani kwakufanya hivyo ndiko kunatusaidia kuleta maendeleo katika halmashauri zetu na hata vijiji vyetu  
 
Katika mbio hizo za mwenge katika halmashauri ya wilaya ya Arusha DC imezindua miradi mbalimbali ikiwemo kuzindua na kufungua shule Ya sekondari ya Odonyowas, mradi wa maji wa layout Srwsita,mradi wa Nyuki pamoja na hospital ya mama na mtoto ya orturmenti.

ILALA YAKABILIANA NA DENGUE,KIPINDUPINDU KWA KUPULIZIA DAWA YA KUUA MBU ,VIMELEA VYA MAGONJWA..JANGWANI CHINI YA UANGALIZI WA MJEMA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WILAYA ya Ilala jijini Dar es Salaam imeamua kupiga dawa ya kuua mazalia ya mbu wanaoneza homa ya dengue pamoja na kipindupindu katika eneo la Jangwani,Kariakoo na Mchikichini huku ikitangaza kuyaweka maeneo hayo chini ya uangalizi ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na wagonjwa ya mlipuko.

Wakati wa upuulizaji huo wa dawa ulioenda sambamba na usafi wa mazingira ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha wananchi kuendelea kusafisha mazingira ya maeneo yao,viongozi na watendaji wa Wilaya wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wameshiriki upuliziaji dawa na kufanya usafi.

Akizungumza baada ya kupulizia dawa ya kuua mbu katika mtaro wa maji taka uliopo kwenye maeneo ya Jangwani,Mjema amesema maeneo hayo ndio yenye wagonjwa wengi wa kipundupindu na homa ya dungue.

Amesema hivyo Ilala wameweka mkakati wa kuhakikisha inapulizwa dawa maeneo yote ili wananchi wasiendelee kung'atwa na mbu wanaoneza Dengue.Pia ni mkakati wa Wilaya ya Ilala kukomesha kipindupindu ndani ya Wilaya hiyo na kwamba upuliziaji huo wa dawa u kwenda sambamba na usafi wa mazingira.

Mjema amesema eneo la kata ya Mchikichini na Kata ya Jangwani ndio kwa sehemu kubwa wananchi wake wamekupatikana na kipindupindu.",Hivyo mini pamoja na wenzangu wote tumekuwa maeneo haya kufanya usafi na kupuliza dawa kwenye maeneo yote tunayodhani yatakuwa na mazalia ya vimelea vinavyosababisha magonjwa ya mlipuko,"

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa maeneo ya Jangwani hali ni tete zaidi hasa kea kuzingatia maeneo hayo yalitawaliwa na mvua kasi cha wakati wa maeneo hayo kuyahama Makazi yao kwa muda,hivyo mkakati wa Wilaya ya Ilala ni kuendelea kuweka chini ya uangalizi.

Pia ameshauri kuwa kwa sasa wakazi wa Jangwani ni vema badala ya kukaa kwenye makazi hayo kuwa makini na ikiwezekana waaondoke hadi hali itakapokuwa salama kwa afya zao.Kwa upende wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Dk.Emily Lihawa amesema kutokana na kuwepo wa ugonjwa wa kipindupindu na Dengue wameona ni vema wakapiga dawa ya kuua mazalia ya mbu wa Dengue pamoja kipindupindu na kwa kuzingatia Kata ya Mchikichini,Jangwani na Kariakoo ndio zenye wagonjwa wengi hasa wa kipindupindu.

"Hatua ya kwanza ni hii ya kulipuza dawa kwenye mitarajo ya maji taka,na baada ya hapo tutapiga dawa kwenye makazi ya watu yakiwamo ya chooni. Eneo hili la Jangwani kuna watu wameupata kipindupindu na ndani ya Wilaya yetu kuna mwananchi mmoja amefariki kwa ugonjwa huo.Tumefanya pia usafi wa mazingira katika maeneo hayo,"amesema Dk.Lihawa.

Wakati huo huo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk.Tudas Ndungile amefafanua kuwa kuna mikakati mbalimbali imewekwa kukabiliana na homa ya dengue na kipindupindu,ukiwemo wa kuendelea kuhamasisha usafi wa mazingira na kupuuliza dawa ya kuua mazalia ya mbu na vimelea vya magonjwa hayo.

"Hivyo wakati sisi yuko hapa, maeneo mengine ya Mkoa wa Dar es Salaaam nako usafi unafanyika .Wilaya zote ziko kwenye usafi.Kama mnavyojua hadi sasa wakazi 98 wameugua kipindupindu,"amesema Dk.Ndungile.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema  akishiriki kupuliza dawa ya kuua mbu na vimelea vya magonjwa ya homa ya dengue na kipindupi ndu katika eneo la Jangwani.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa amebeba vyombo cha kuhifadhia dawa ya kuua mbu wanaoneza homa ya dengue kabla ya kuanza kupuliza katika mtaro wa maji taka eneo la Jangwani
 Mmoja watumishi wa Wilaya ya Ilala akiendelea kupuliza dawa ya kuua mbu wanaoneza homa ya dengue maeneo ya Kata ya Jangwani jijini Dar es Salaam
 Upuliziaji dawa ya kuua mbu wanaoneza homa ya dengue pamoja na vimelea vya kipindupindu kuendelea eneo la Jangwani
 Mmoja wa wapuliziaji dawa ya kuua mbu wa homa ya dengue akiwa ameweka began vyombo kilichohifadhiwa dawa kabla ya kuanza kupuliza katika eneo la Jangwani
 Mtaro wa maji taka uliopo Kata ya Jangwani jijini Dar es Salaam ukiwa umezungukwa na makazi ya watu
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam akizungumza na wananchi wa Jangwani baada ya kumalizika kwa upuliziaji dawa kwenye mtaro wa maji taka na makazi ya watu,ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na dengue pamoja na kipindupindu

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UJUMBE WA TAASISI YA AL-HIKMA UKIONGOZWA NA SHEIKH NURDIN KISHKI IKULU ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Taasisi ya Al -Hikma Foundation ya Jijini Dar es Salaam Sheikh Nurdin Muhammed Ahmed Kishki, alipofika IKulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 8-6-2019.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Al-Hikma Fundation ukiongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo kulia Sheikh Nurdin Muhammed Ahmed Kishki, Sheikh Suleiman Khamis Habib,walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kumsalimia leo 8-6-2019, (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Mwenyekiti wa Usalama na Itifaki na Mnadhimu Mkuu wa Al Hikma Fundation Sheikh Suleiman Khamis Habib, akitowa maelezo kuhusiana na Taasisi yao wakati wa mazungumzo hayo yaliofanyika Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi,hayuko pichani baada ya kumaliza mazunguymzo na Ujumbe wa Taasisi ya Al -Hikma Foundation ya Jijini Dar es Saalam ukiongonzwa na Mkurugenzi Mkuu Sheikh.Nurdin Muhammed Ahmed Kishki kulia Sheikh Suleiman Khamis Babib na Mussa Rajab Mushi, wakiwa katika ukumbi wa Ikulu.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Taasisi ya Al – Hikma Foundation ya Jijini Dar es Salaam iikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo kulia Nurdin Muhammed Ahmed Kishki, Sheikh Suleiman Khamis Habib, Ndg. Mussa Rajab Mushi na Omar Hussein Mussa., Mwenyekiti wa Al -Hikma Foundation Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Taasisi ya Al -Hikma Foundation Zanzibar, Sheikh Omar Hussein Mussa, akitowa neno la shukrani baada ya kumaliza mazungumzo hayo yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo 8-6-2019, walipofika kumsalimia Rais wa Zanzibar.(Picha na Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.,Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Taasisi ya Al -Hikma Foundation ya Jijini Dar es Salaam waliokaa kutoka kushoto Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Sheikh Nurdin Kishki, Sheikh. Suleiman Khamis Habib na Sheikh.Omar Hussein Mussa na kulia Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Katibu Ofisi ya Mufti Mkuu Sheikh Fadhil Soraga na Mussa Rajab Mushi.(Picha na Ikulu)

Wakazi Zaidi ya 1000 Kanda ya Ziwa Wanufaika na Huduma ya Upasuaji Bure

$
0
0
Madaktari wakiendelea na zoezi la Opereshi kwa wagonjwa wakati wa siku ya kuhitimisha zoezi la huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wanaosubiri kwa muda mrefu toka Kanda ya Ziwa hivi karibuni.Zoezi hilo la siku tano limefanyika kwa ushirikiano baina ya Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania na Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bungando.
Madaktari wakiendelea kuwashauri wananchi kuhusiana na afya zao katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza hivi karibuni.
Wananchi wakiendelea kupewa utaratibu kuhusiana na matibabu maalum katika wiki ya tiba katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza hivi karibuni.
Dakta Catherine Mung’ong’o Rais wa Chama Cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania akizungumza na Wanahabari katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza hivi karibuni 


Zaidi ya wakazi 1000 wa Kanda ya Ziwa wamenufaika na matibabu bure hasa kwa upande wa upasuaji unaofanywa na Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania. 

Hayo yamebainishwa na Rais wa Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania, Dkt. Catherine Mung’ong’o wakati wa siku ya kuhitimisha zoezi la upasuaji lililofanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 03 hadi 07 Juni 2019 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza. 

Alisema kuwa lengo la upasuaji huo ni kupunguza idadi ya wahitaji wa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wanaosubiri kwa muda mrefu toka Kanda ya Ziwa, nakuongeza kuwa zoezi hilo limefanyika kwa ushirikiano baina ya Chama hicho, Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bungando na Madaktari wengine. 

Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa huduma hii ya upasuaji inayotolewa na Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania imekuwa ikifanyika kila mwaka katika mikoa mingine huku ni ikiwa ni mara ya kwanza katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. 

Kwa upande wake Kiongozi wa Chama hicho Kanda ya Ziwa ambaye ni Daktari Bingwa wa Upasuaji toka Hospitali ya Rufaa Bugando, Dkt. Olivia Kimario amesema kuwa zoezi hilo ni utaratibu uliowekwa na Chama cha Madaktari hao ambapo mwaka huu wamehudumia katika mikoa ya Mwanza , Shinyanga , Mara na Geita. 

Katika hatua nyingine Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa baada ya kukamilisha zoezi hilo la upasuaji kwa wagonjwa wanaosubiri kwa muda mrefu Chama hicho kitatoa huduma bure za upasuaji kwa wagonjwa wenye matatizo ya Mdomo Sungura litakalofanyika tarehe 10 na 11 Juni 2019 bila ya malipo.

TANZIA *TANZIA * MSIBA LUTON,UINGEREZA-TANZANIA

$
0
0


*Ndugu Wanafamilia na Watanzania Wote Waishio UK *

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania nchini Uingereza TZUK DIASPORA kwa masikitiko makubwa inawatangazia taarifa ya msiba wa Mke wa mwanajumuiya mwenzetu Abdulkadir Rashid , Bi Rachel Maona kilichotokea  leo asubuhi tarehe 08/06/2019 Keech Hospices - Luton nchini Uingereza.

Marehemu Bi. Rachel Maona ambaye alikuwa akifanya kazi Luton and Dunstable Hospital nchini Uingereza alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kansa na ameacha watoto watatu na mume. 

Taratibu za msiba na kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi zinaendelea kufanywa kwa kushirikiana na East Africa Muslim Community na Luton Tanzanian Community , Kwa kushirikiana na watanzania wanaoishi UK.

Wanajumuiya, Watanzania, Ndugu, Jamaa, na marafiki  Uongozi kwa niaba ya familia ya tunawaomba ushirikiano wenu na faraja kwa familia.


UONGOZI 

JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO UK (TZUK DIASPORA

SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUKUZA UTALII NCHINI

$
0
0

Muonekano wa eneo lililobuniwa na TAWA kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya KARIBU KILIFAIR 2019 jijini Arusha linaloakisi Pori la Akiba la Selous.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumzia mikakati ambayo Serikali imeipanga ya namna ya kushirikiana na Wadau wa sekta ya utalii mara baada ya kufungua Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya KARIBU KILIFAIR 2019 jijini Arusha.(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati)wakiwa na waandaaji wa maonesho hayo ya Kimataifa ya Utalii ya KARIBU KILIFAIR 2019, Bw.Dominick Shoo (kulia) akiwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Kilifair Promotion, Tom Kunkler (kushoto). na kwenye mfano wa kilele cha Mlima Kilimanjaro mara baada ya kufungua Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya KARIBU KILIFAIR 2019 jijini Arusha.(Picha na Wizara ya Maliasili na  Utalii)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya KARIBU KILIFAIR 2019 jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na waaandaji na waalikwa walioshiriki kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya KARIBU KILIFAIR 2019
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Benki ya NMB ambao ni wadhamini wakubwa wa kwa mwaka huu kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya KARIBU KILIFAIR 2019
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki kwenye nembo ya Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya KARIBU KILIFAIR 2019
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo wakipewa maelezo na Wily hida kuhusu uimara wa gari maalum ya kubeba watalii jinis inavyoweza kuhimili hali zote pindi ikiwa mbugani na watalii mara baadfa ya kufungua Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya KARIBU KILIFAIR 2019 jijini Arusha. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
*********************************
WMU – ARUSHA

Serikali imesema kuwa itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta binafsi waliowekeza katika Sekta ya Utalii na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili kwa lengo la kuimarisha sekta hiyo na kuvutia wawekezaji wengi zaidi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,        Mhe.Constantine Kanyasu wakati akifungua Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya KARIBU KILIFAIR 2019 jijini Arusha.

Amesema ushirikiano huo unalenga kuifanya sekta ya utalii iwe zao namba moja na chanzo kikuu cha mapato nchini na kuongeza kuwa Tanzania inaendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege kwa lengo la kufungua shughuli za utalii katika maeneo yote yenye vivutio vya utalii.

Mhe.Kanyasu amesema  kufanyika kwa maonesho hayo ambayo ni makubwa mara mbili ya yale yaliyofanyika mwaka jana ni ishara ya kukua kwa sekta ya utalii na kueleza kuwa washiriki kutoka nchi 40 za ndani na nje Afrika na mashariki ya nje yameshiriki.

 “Maonesho haya yana sura ya Kimataifa hili linatambulika kwa kuona washiriki hao  sisi kama nchi tumepata bahati, tungeweza kutumia gharama kubwa kuwaleta hawa watoa huduma za utalii huko kwenye nchi zao, hawa wamekuja wenyewe na hii imesaidia kampuni za Tanzania badala ya kwenda nje kuuza biashara zao wamekutana na kampuni za kimataifa hapa hapa Tanzania” Amesema Mhe. Kanyasu.

Amesema onesho la KARIBU KILIFAIR linasaidia kukuza utalii nchini kutokana na umuhimu wake wa  kuuza  huduma na bidhaa za utalii kwa kutangaza fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini na kuongeza kuwa ili utalii uweze kukua ni lazima kazi ya kutambulisha na kuuza bidhaa za utalii ifanyike.

Mhe. Kanyasu amezitaka taasisi za uhifadhi zilizo chini ya Wizara ambazo zinashiriki maonesho hayo zikiwemo TANAPA, Ngorongoro, TAWA, Bodi ya Utalii Tanzania na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) zifikiri kibiashara na kutafuta wawekezaji wapya watakaowekeza na kufanya biashara kwenye Mapori ya Akiba, Misitu ya Asili na hifadhi za Taifa ambazo bado hazijapata wawekezaji ili nazo zichangie katika pato la Taifa.

“Tunataka taasisi zote wakati zinashiriki uhifadhi zifikiri kibiashara, tunataka tuondokane na mfumo wa kizamani wa kufikiri kuhifadhi bila kufikiri kibiashara, tuna mapori mengi ambayo ambayo hayaingizi fedha, tunataka taasisi za usimamizi wa mapori haya watafute wawekezaji kwa kuainisha fursa za uwekezaji zilizopo” Amesisitiza Mhe. Kanyasu.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya ukanda wa kusini ikiwemo barabara, ununuzi wa ndege kubwa za kisasa na kuboresha viwanja vya ndege ili kufungua Utalii wa ukanda wa Kusini na kuongeza shughuli za utalii katika hifadhi za ukanda huo zikiwemo  Ruaha  Selous, Mikumi na Udzungwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumzia maonesho hayo amesema kuwa mwaka huu Tanzania imepata wageni wengi walioshiriki  maonesho hayo kutoka ndani na nje ya Afrika.

Amesema ujio wa washiriki hao utasaidia kwa kiwango kikubwa kuitangaza Tanzania kimataifa na kusaidia kukuza na kuongeza idadi ya watalii wanaoitembelea Tanzania.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambaye na Mbuge wa Iringa mjini, Mhe. Peter Msigwa ameeleza kuwa ushiriki wa makampuni mengi ya utalii ya ndani na nje ya Tanzania unaeleta chachu katika dhana nzima ya kukuza utalii nchini.
“Hili ni jambo jema na lenye heri ambalo kwa kufanya maonesho haya yanasababisha tujulikane, biashara ni matangazo tunapokuwa tunajulikana ndani ya nchi na kimataifa inasaidia sana kukuza utalii” Amesema Mhe. Msigwa.

Mhe. Msigwa amesema ushirikiano wa sekta binafsi na Serikali ni muhimu katika kukuza utalii nchini akibainisha kuwa hilo litaiwezesha serikali kuendelea kukusanya kodi kutoka sekta binafsi kwa lengo la kuendesha nchi.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya KILIFAIR ambao ni waandaaji wa maonesho hayo ya Kimataifa ya Utalii ya KARIBU KILIFAIR 2019, Bw.Dominick Shoo ameeleza kuwa maonesho hayo kwa mwaka huu yamewahusisha washiriki zaidi ya 450 kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Bw. Shoo ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaoutoa kwa sekta binafsi na kazi kubwa kazi kubwa inayoendelea kufanyika ya kufungua vituo vipya vya utalii katika mikoa ya Kanda ya ziwa na kueleza kuwa wao kama wadau wa sekta binafsi wataendelea kuvitangaza vivutio hivyo kwa nguvu kubwa.

“ Ninaishukuru Serikali kwa kuweka msukumo mkubwa katika uanzishaji wa vituo vipya vya utalii na kazi kubwa inayoendelea ya kuboresha miundombinu, ninaamini utalii wa Tanzania utakua kwa kasi na hii inaashiria kwamba ushirikiano tunaoupata kutoka Serikalini utalii utakua kwa kasi kubwa na tutapata watalii wengi zaidi” Amesisitiza Bw. Dominick.

Wafanyabiashara Wadogo Jijini Dodoma Wampongeza Rais Magufuli

MCHOTEKA WAISHUKURU SERIKALI KWA UKARABATI WA KITUO CHA FYA

$
0
0
WANANCHI wa Kijiji cha Mchoteka kata ya Mchoteka wilayani Tunduru,wameishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha Afya, jambo wanaloamini ukarabti huo utarahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu.

Aidha wamempongeza  Rais Dkt John Magufuri kutokana na kazi nzuri  anayofanyak kusimamia na kuboresha sekta ya Afya  hapa nchini ambayo hapo  nyuma ilikuwa na changamoto nyingi za kiutendaji ikiwemo uchakavu wa majengo na upungufu wa Dawa,vifaa tiba na watumishi katika  hasa maeneo ya vijijini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana,baadhi ya wananchi  Hussen Yusuf, Hausi Yasini na Ajika Kasembe wamesema,  wana furahi sana kuona Serikali imeamua kutoa fedha ili kukarabati kituo cha Afya Mchoteka ambacho ni tegemeo kubwa kwa wananchi zaidi ya elfu nane na mia tano wa kata  hiyo ambao  kwa sasa wanalazimika kwenda hadi Hospitali ya MIsheni Mbesa  kufuata  huduma ikiwemo ya upasuaji.

Hussen alisema, hata hivyo bado  litakuwa la upungufu wa Watumishi na kuikmba Serikali kuhakikisha mara ukarabati utakapokamilika ni vema kupeleka watumishi wa kutosha ambao watasaidiana na waliopo kuwahudumia wananchi.

Hamisi Yasini ameomba kazi ya ukarabati ikamilike haraka ili wananchi waweze kupata huduma ambazo zinakosekana katika kituo hicho kama upasuaji kwa wajawazito kwa kuwa hivi sasa  wanalazimika kwenda vituo vingine hivyo kulazimika kutumia fedha nyingi na  muda  mwingi.

Alisema, ukarabati wa majengo hayo uendene na utoaji huduma bora  kwa watu wakaofika kupata matibabu na kusisitiza kuwa,Serikali lazima iwachukulie hatua baadhi ya watumishi  wenye lugha chafu kwa wagonjwa na wale wanaoendelea kufanya kazi kwa mazoea.

Naye fundi anayesimamia ujenzi huo Moshi Lukandamila alisema, hadi sasa ukarabati umefikia asilimia 85 na  unatarajia kukamilika baada ya mwezi mmoja iwapo Serikali kupitia kamati ya ujenzi itapeleka vifaa kwa wakati.

Alisema, kwa sasa wanamalizia kuweka malumalu na  kupaka rangi huku akitaja kuwa,kazi zote muhimu ikiwemo  mfumo wa maji safi na taka, nyaya za umeme imeshakamilika.

Kwa upande wake,Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Dkt Wendy Robert alisema, ukarabti ulianza tangu Mwezi Agosti mwaka jana,lakini umechelewa kukamilika kutokana na upatikanji wa baadhi ya vifaa kama mawe ambayo yanapatikana mbali na eneo la ujenzi huo.

Kwa mujibu wa Dkt Wendy ukarabati wa kituo hicho kimsingi utasaidia sana wakazi zaidi ya 850 wa kata ya Mchoteka na wale wa kata jirani kama Nalasi kupata matibabu ya uhakika n ahata kukoa muda mwingi ambao walikuwa  wanatumia kwenda maeneo mengine kufuata huduma.

Alisema, Serikali ya awamu ya tano imetoa shilingi Ml 400 kwa ajili ya ukarabati huo ukihusisha majengo matano ya upasuaji,mochwari,kichomeo taka, nyumba ya mtumishi na maabara ambayo  yako katika hatua ya mwisho kukamilika.
 Jengo  la upasuaji linalojengwa katika kituo cha Afya Mchoteka wilayani Tunduru likiwa katika hatua ya mwisho kumalika ambapo litawezesha wananchi hasa akina mama wajawazito kupata huduma ya upasuaji.
Jengo la Wodi ya akina mama linalojengwa katika kituo cha Afya Mchoteka wilaya ya Tunduru ambalo limefikia asilimia 85 ya ujenzi wake,Serikali imetoa shilingi Milioni 400 ili kukarabati kituo hicho.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wamshukuru Rais Magufuli.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Prof. Mohammed Janabi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuisaidia Taasisi hiyo kupata jengo la Kitengo cha Matibabu ya Moyo kwa Watoto.

Prof. Janabi amefafanua kuwa kufuatia maelekezo ya Mhe. Rais Magufuli aliyoyatoa mapema mwaka jana (2018), moja ya majengo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili lililopo jirani na Taasisi hiyo lilikabidhiwa kwa Taasisi hiyo na Serikali ikatoa fedha za kulikarabati na kuwekewa miundombinu ya kutolea huduma za matibabu ya moyo kwa watoto.

Ameongeza kuwa jengo hilo lina lina vitanda 40 vya kawaida na vitanda 8 vya watoto wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) na kwamba kukamilika kwake kutaiwezesha Taasisi hiyo kupata vyumba vipya 4 vya kliniki ambavyo vitawawezesha Madaktari kuwaona watoto 60 kwa siku.

Prof. Janabi amebainisha kuwa kabla ya kupatiwa jengo hilo, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ililazimika kuwachanganya watoto na watu wazima katika sehemu moja iliyojumuisha chumba cha ICU, wodi na pia kliniki ambayo iliwawezesha Madaktari kuona wagonjwa kati ya 25 na 30 tu kwa siku.


"Kwa furaha kubwa kabisa, mwezi uliopita jengo letu limekwisha kama unavyoliona lina vitanda 40 kwa ajili ya watoto tu, lina vitanda 8 kwa ajili ya wagonjwa mahututi (ICU) kwa watoto tu na muda wowote kuanzia sasa tutalifungua.

"Sasa nini faida kubwa ambayo tutaipata sisi kama Madaktari, sasa hivi watoto wagonjwa wakitoka chumba cha upasuaji (Theatre) watakwenda moja kwa moja kwenye ICU ya watoto, hii ni tofauti na hali ilivyokuwa kwenye hili jengo kubwa tulilokuwepo ambapo Daktari alikuwa anaingia wodini anamuona mgonjwa wa kwanza mtu mzima ana kilo 90, kitanda kinachofuatia kuna mtoto ana kilo 5 ambaye pia tumemfanyia upasuaji, kwa hiyo uwezekano wa kufanya makosa ulikuwa mkubwa sana iwe kwenye kutoa dawa au huduma nyingine. Ndio maana tunamshukuru sana Mhe. Rais Magufuli kwa kutusaidia na ufanisi wetu wa kazi utakuwa mkubwa zaidi" amesema Prof. Janabi.

Aidha, Prof. Janabi amewashukuru wadau binafsi waliochangia ukarabati wa jengo hilo wakiwemo Jumuiya ya Kihindi ya BAPS na Benki ya CRDB waliofanikisha kukamilika kwa jengo hilo.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa taasisi hiyo Dkt. Naiz Majani amesema tatizo la magonjwa ya moyo hapa nchini ni kubwa ambapo katika kila watoto 100 wanaozaliwa 1 ana tatizo la moyo hivyo kujengwa kwa jengo hilo kuna umuhimu mkubwa kwa Watanzania ambao awali walikosa huduma ama kulazimika kwenda nje ya nchi.

Kilimo chanzo upotevu wa misitu: Utafiti

$
0
0
NA SULEIMAN MSUYA

UTAFITI uliofanywa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), chini ya ufadhili wa Mfuko wa Critical Ecosystem Partnership (CEPF) umebaini kuwa asilimia 89 ya upotevu wa misitu nchini unachangiwa na shughuli za kilimo.

Matokeo ya utafiti huo yametolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa TFCG, Emmanuel Lyimo wakati akiwasilisha mada kuhusu sababu zinachangia upotevu wa misitu nchini kwa maofisa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Serikali Kuu waliokutana mkoani Morogoro.

Lyimo alisema katika utafiti huo walishirikisha maeneo 120 katika wilaya 62 na mikoa 22 ambapo kila mahali kilimo kilionekana ni sehemu ya sababu kubwa ya upotevu wa misitu.

"Tumetumia miezi sita kuzunguka katika wilaya 62 mikoa 22 na maeneo 120 kuangalia kinachopelekea upotevu wa misitu na tumebaini asilimia 89 hali hiyo inasababishwa na shughuli za kilimo cha kuhamahama," alisema.

Alisema utafiti huo umeonesha uvunaji mkaa, uchomaji moto na ufugaji unachangia upotevu wa misitu kwa asilimia 7, uchomaji moto na ufugaji asilimia 3 na uanzishaji wa mashamba maypa ya miti asilimia 1.

Lyimo alisema utafiti ulibaini zao ambalo linalimwa zaidi katika maeneo ambayo misitu imevunwa ni mahindi, ufuta, kunde, mtama, mpunga, maharage, muhogo, alizeti na korosho.

Alisema iwapo hali hiyo itaendelea bila kuwepo mipango ya kuendeleza sekta ya misitu ni wazi rasilimali hiyo itapotea na kukosekana kwa mbao kwenye vijiji pia kukosekana kwa vyanzo vya maji, uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

"Pia uwezo wa kudhibiti uharibifu utakosekana hasa vijijini hivyo maofisa wanaohusika na usimamizi wa rasilimali misitu wanatakiwa kuongeza juhudi kukabiliana na hali hiyo," alisema.

Lyimo alisema ili maofisa hao kutoka Serikali za mitaa na serikali kuu kuweza  kukabiliana na hali hiyo wanapaswa kuanzisha Usimamizi wa Misitu ya Jamii (CBFM), jamii kunufaika moja kwa moja na rasilimali misitu na kuwepo kwa usawa katika maamuzi kuhusu matumizi ya ardhi kwa kushirisha wadau mbalimbali hasa kilimo, ardhi na misitu.

Kwa upande wake Ofisa Misitu Mkuu Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii, Seleboni John alisema Serikali imejipanga kikamilifu kusimamia sera ya misitu na sheria ili misitu iwe endelevu.

"Taarifa zinaonesha uharibifu wa misitu umeongezeka kutokana na kilimo, uchomaji mkaa na uvunaji wa mbao kinachohitajika ni wadau kushirikiana kudhibiti kama wanavyofanya TFCG, Mjumita na TaTEDO," alisema.

Mwakilishi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Kanda ya Mashariki, Benadetta Kadala alisema wakala huo umejipanga kulinda misitu kwa kufuata sheria kanuni.Aidha, Kadala alisema TFS itahakikisha misitu ya vijiji inakuwa salama na endelevu kwa kusimamia uvunaji wa sheria.

Ofisa Misitu wa Mkoa wa Morogoro Joseph Chuwa alisema utafiti huo umeonesha hali halisi ya uharibifu hivyo wao kama maofisa misitu, maliasili, kilimo, ardhi na sheria hawana budi kujipanga upya kukabiliana na hali hiyo.

Chuwa alisema iwapo wao wataongeza jitihada ya usimamizi katika kulinda misitu ni dhahiri wafanya maamuzi wataungana nao kwenye kampeni hiyo.
Ofisa Misitu Mkuu wa Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii, Seleboni John akielezea mikakati ya Wizara hiyo katika kuendeleza misitu kwa maofisa serikali kutoka wilaya mbalimbali katika warsha iliyoandaliwa na Shirika la Uhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi Misitu Tanzania (Mjumita) na Shirika la Kuendeleza Nishati ya Asili Tanzania (TaTEDO). Picha na Suleiman Msuya.

RELI NA MATUKIO: RELI YA TANGA - ARUSHA UFUFUAJI NI 80%, STESHENI YA SGR DAR MAMBO MSWANO

MAONESHO YA BIASHARA NA UTALII YAFIKIA TAMATI JIJINI TANGA

$
0
0
  Naibu waziri wa mawasiliano na utalii Costantine Kanyasu akimsikiliza mmoja wa wakinamama wajasiriamali akitoa maelezo ya biashara yake  katika Maonesho ya Biashara na Utalii  yaliyofungwa April 8 2019 katika viwanja wa Mwahako jijini Tanga
 Naibu waziri wa mawasiliano na utalii Costantine Kanyasu akisaini kitabu cha wageni katika banda la wanawake wajasiriamali katika Maonesho ya Biashara na Utalii katika viwanja wa Mwahako jijini Tanga.
  Naibu waziri wa mawasiliano na utalii Costantine Kanyasu katika picha ya pamoja na watumishi katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika viwanja wa Mwahako jijini Tanga.
 Meneja wa TRA mkoa wa Tanga,Specioza Owure akitoa maelezo kwenye banda la mamlaka hiyo kwa naibu waziri wa maliasili na utalii Costantine Kanyasu wakati alipokuwa akitembelea, kabla ya kufunga maonesho hayo katika viwanja wa Mwahako jijini Tanga.
 Afisa uhusiano wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingiraTanga UWASA Dora Killo akitoa maelezo  kwa naibu waziri wa maliasili na utalii Costantine Kinyasu  katika kilele cha maonesho hayo katika viwanja wa Mwahako jijini Tanga.a.

 NAibu Waziri wa Maliasili  na Utalii akitembelea banda la mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Tanga 
 Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga UWASA akipokea cheti cha ushindi wa kwanza kwenye taasisis za umma zilizoshiriki katika kilelle cha maonesho ya kibiashara ya kimataifa jijini Tanga
Afisa Maeneleo ya jamii jijini Tanga,Moses Kiksibo akipokea cheti kwenye maonyesho hayo katika viwanja wa Mwahako jijini Tanga.
Picha zote na Mbonea Herman

NHIF TANGA WATUMIA MAONYESHO YA BIASHARA NA UTALII YATOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU CHF ILIYOBORESHWA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii .Constantine Kanyasu kushoto akimsikiliza kwa umakini Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu wakati alipotembelea alipokwenda kufunga  maonyesho ya saba ya biashara ya kimataifa yaliyokuwa yakiendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii .Constantine Kanyasu kushoto akimsikiliza kwa umakini Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu wakati alipotembelea alipokwenda kufunga  maonyesho ya saba ya biashara ya kimataifa yaliyokuwa yakiendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii .Constantine Kanyasu kulia akipima uzito kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima Afya mkoani Tanga (NHIF) mara baada ya kulitembelea
 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu juu ya CHF iliyoboreshwa mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam ambaye alitembelea banda lao Devutia Kulembeka
 Mhudumu wa Afya kulia akiendelea na shughuli kwenye banda hilo
 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakipima afya zao
  Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakipima afya zao


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga umetumia maonyesho ya saba ya biashara ya kimataifa kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na CHF iliyoboreshwa ili waweze kujiunga nayo na kuweza kunufaika.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko huo mkoani hapa Ally Mwakababu wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.

Alisema wameona washiriki kwenye maonyesho hayo ili pia kutoa elimu ya bima ya afya kwa watumishi, wananchi binafasi, wanafunzi na watoto ikiwa ni mkakati wao wa kufikia watu wengi zaidi

“Tunashukuru kwenye maonyesho haya tumepata fursa ya kutoa elimu ya CHF iliyoboreshwa na nia kubwa ni kwamba kila mwananchi awe na kinga ya matibabu wakati wote”Alisema

Meneja huyo alisema licha ya kutoa elimu hiyo lakini pia wanafanya zoezi la kupima afya za wananchi wanaotembelea banda lao ikiwemo kupima uzito lakini pia wanapima sukari na baadae kutoa ushauri wa wananchi wanaopita kwenye banda lao.

Alieleza ushauri huo ni kwamba baada ya kupimwa wanatakiwa kufanye nini hivyo wanaamini wananchi wakitumia banda hilo watapata huduma ya vipimo bure na kupata ushauri mzuri.

Introducing CHEZA audio by Phillz

MENEJA KIONGOZI UHUSIANO WA PSSSF EUNICE CHIUME ATEMBEELA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MENEJA Kiongozi Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi.Eunice Chiume, amefanya ziara ya kutembelea vyombo vya habari vinne jijini Dar es Salaam leo Juni 10, 2019 kwa lengo la kueleza shughuli za Mfuko huo ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano mema ya ushirikiano baina ya Mfuno na tasnia ya habari.
Katika ziara hiyo iliyoanzia kwenye ofisi za The Guardian Limited Mikocheni jijini Dar es Salaam, Bi. Eunice alifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi ambapo walipokelewa na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Bi. Beatrice Bandawe na kisha baadaye kufanya mazungumzo yaliyowahusisha, pia Mhariri Mtendaji wa The Guardian, Bw. Wallace Mauggo na wahariri wengine.
Baada ya kutembelea The Guardian, ziara ya Bi. Eunice ilimfikisha pia kwenye ofisi za Global Group zinazomiliki vyombo vya habari vya kielekrtorniki na magazeti, na kisha kumaliza ziara yake kwenye ofisi za EML na EFM Radio.
Akizungumza kwa nyakazi tofauti kwenye ofisi za vyombo hivyo, Meneja huyo alisema, nia ya ziara hiyo ni kueleza shughuli za Mfuko huo ambao ni matokeo ya kuunganishwa mifuko mine ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.
“Lakini niseme tu kwamba vyombo vya habari ni wadau wakubwa katika kuhakikisha Umma wa watanzania unapata habari na taarifa mbalimbali zinazohusu Mfuko huu mpya wa PSSSF kwa hivyo tumeona ni muhimu kuwatembelea ili kubadilishana mawazo na kujenga mahusiano mema ya kiutendaji.” Alsiema Meneja huyo Kiongozi.
Alisema, PSSSF ilianza rasmi kutekeleza majukumu yake tarehe 1 Agosti, 2018, hivyo bado ni Mfuko mpya ambapo wanachama na wastaafu wa Mfuko huu wanalazimika kujua sheria mpya zinazoendesha Mfuko na watu pekee wanaoweza kufikisha elimu hiyo kwa haraka ni vyombo vya habari.
“Kwa sasa nitoe wito tu kwa wastaafu wote kwenda kwenye ofisi zetu zilizoenea nchi nzima bara na visiwani ili kuhakiki taarifa zao kwani zoezi hilo ni muhimu na linaendelea.” Alisema.
 Meneja Kiongozi Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Ummae (PSSSF), Bi.Eunice Chiume, (watatu kushoto), Afisa Uhsiano mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, (wakwanza kushoto), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Bi. Beatrice Bandawe (wane kushoto), Mwandishi Mkuu wa gazeti hilo, Bi. Salome Kitomari (watano kushoto), Mhariri msanifu, Deodatus Muchunguzi (wakwanza kulia) na mkuu wa kitengo cha digitali cha gazeti hilo, muda mfupi baada ya Meneja huyo kutembelea chumba cha habari cha The Guardian katuka ziara ya kutambulisha Mfuko huo mpya kwa vyombo vya habari nchini. Ziara hiyo imefanyika leo Juni 10, 2019.akizungumza na uongozi wa gazeti la Nipashe, chini ya Mhariri 
  Meneja Kiongozi Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Ummae (PSSSF), Bi.Eunice Chiume, (kushoto), akizungumza na uongozi wa gazeti la Nipashe, chini ya Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo, Bi.Beatrice Bandawe, (watatu kushoto) alipotembelea chumba cha habari cha gazeti hilo jijini Dar es Salaam leo Juni 10, 2019. Bi.Chiume ameanza ziara ya kutembelea vyombo vya habari ili kueleza shughuli za Mfuko huo mpya ikiwa ni pamoja na kukuza ushirikiano
 Meneja Kiongozi uhusiano Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Ummae(PSSSF), Bi.Eunice Chiume, (wapili kushoto, akiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko hio, Bw.Abdul Njaidi, (kushoto), akizungumza na uongozi wa gazeti la Nipashe, chini ya Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo, Bi.Beatrice Bandawe, (watatu kushoto) alipotembelea chumba cha habari cha gazeti hilo jijini Dar es Salaam leo Juni 10, 2019. Bi.Chiume ameanza ziara ya kutembelea vyombo vya habari ili kueleza shughuli za Mfuko huo mpya ikiwa ni pamoja na kukuza ushirikiano.
 Bi. Eunice Chiume akizungumza katika kutano huo wa pamoja na uongozi wa gazeti la Nipashe na The Guardian.
 Mhariri Mtendajiw a gazeti la The Guardian, Bw. Wallace Mauggo, (kushoto), akizunguzma na Meneja Kiongozi uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Ummae(PSSSF), Bi.Eunice Chiume kwenye chumba cha habari cha The Guardian jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019.
 Bi. Eunice akisindikizwa na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Bi. Beatrice Bandawe mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea chumba cha habari cha The Guardian. Wengine ni Afusa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kulia) na Mwandishi Mkuu wa Nipashe, Bi. Salome Kitomari.
 Meneja wa kampuni ya Global Group, Bw. Abdallah Mrisho (kulia), akimpa maelezo Meneja Kiongozi Uhusiano Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi.Eunice Chiume, (wapili kushoto, akiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko hio, Bw. Abdul Njaidi, (watatu kushoto) wakati alipotembelea chumba cha habari cha Global Publishers, Sinza jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019. Wakwanza kushoto ni Mhariri Mytendaji wa magazeti yanayomilikiwa na kampuni hiyo, Bw. Saleh Ally.
 Bi. Eunice Chiume, (watatu kushoto) akiwa na Bw. Abdul Njaidi (kulia), wakiongozwa na wenyeji wao, Meneja wa Global Publishers, Bw. Abdallah Mrisho (wakwanza kushoto) na Bw. Salehe Ally wakati alipote,mbelea ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Juni 10, 2019.
 Mwenyekiti na Afisa Mtednaji Mkuu wa Global Group, Bw. Eric Shigongo (kushoto), akimsikizia Meneja Kiongozi Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi.Eunice Chiume wakati alipotembelea vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019.
 Bi. Eunice Chiumew akiwa kwenye studio za Global Radio
 Mkurugenzi Mtendaji wa EML na EFM Radio Bw.Francis Anthony Ciza akisalimiana na Meneja Kiongozi Uhusiano PSSSF Bi. Eunice Chiume wakati alipotembela ofisi za vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019
Bi. Eunice Chiume akipokelewa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa  EFM Radio, Bw.Dennis Busulwa (Ssebo) wakati alipotembelea ofisi za Radio hiyo jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019.

WAZIRI WA NISHATI AFANYA ZIARASHINYANGA, AWASHA UMEME VIJIJINI

$
0
0
Waziri wa Nishati nchini Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara mkoani Shinyanga kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini (REA),kufuatilia uimara wa umeme pamoja na kuhamasisha wananchi kulipia shilingi 27,000/= ili waunganishiwe umeme kwenye nyumba zao.
Ziara hiyo imefanyika leo Jumatatu Juni 10,2019 katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambapo Waziri Kalemani amezungumza na wananchi wa Mwakitolyo,Lyabukande,Mahembe na kuwasha umeme katika vijiji vya Mishepo,Itwangi na Ibingo ambavyo awali vilirukwa katika mradi wa REA.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Dkt. Kalemani alisema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 36 kwa ajili ya kufikisha umeme vijijini huku akikisitiza kuwa ifikapo Desemba 2019 vijiji vyote viwe vimepata huduma ya umeme.
“Tunataka ifikapo mwezi Desemba kila kijiji kiwe kimepata umeme,mwananchi utatakiwa kulipia shilingi 27,000/= tu,ukishalipa hiyo wewe dai umeme huhitaji kuuliza nguzo ziko wapi,nguzo siyo jukumu lako…wewe subiri kuunganishiwa tu umeme ndani ya siku saba. Tunataka wananchi wapate umeme bila kujali wanaishi kwenye nyumba za namna gani”,alisema Dkt. Kalemani.
“Tunahitaji kuona taasisi zote zikiwemo shule,zahanati,makanisa,misikiti inapata umeme hata kama zipo mbali kiasi gani na ili kupunguza gharama za kuunganisha mfumo wa umeme ndani ya nyumba ‘Wiring’ tunashauri wananchi  mtumie kifaa cha “UMETA”,alisema Dkt. Kalemani.
Hata hivyo Waziri huyo alieleza kutoridhishwa na kasi ndogo ya Wakandarasi wa mradi wa Umeme Vijijini mkoani Shinyanga Kampuni ya Angelique International Limited’ ambapo aliagiza jeshi la polisi kumuweka chini ya ulinzi Meneja wa kampuni hiyo,bwana Dilip Singh na wenzake,Dilip Patra na Ramashakur.
“Mhe. Mkuu wa wilaya naomba uchukue hati ya kusafiria ya Mkandarasi huyu,badala ya kukaa kwenye Site yeye anaishi India,amekuja leo baada ya kusikia nakuja. Nataka awepo Shinyanga mpaka pale atakapomaliza kufanya kazi tuliyompa,tunataka wananchi wapate umeme,nanyi TANESCO hakikisheni mnaweka vituo kwenye vijiji hatutaki wananchi wawafuate mjini”,aliongeza Dkt.Kalemani.
Awali Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe.Azza Hilal na Mbunge wa Jimbo la Solwa,Ahmed Salum walimweleza waziri huyo kuwa mradi wa umeme vijijini umekuwa ukisuasua mkoani Shinyanga kutokana na kasi hafifu ya wakandarasi.
“Mbali na Wakandarasi kuwa wazito katika utekelezaji wa mradi wa REA,changamoto nyingine ni baadhi ya vijiji kurukwa hivyo kwenye baadhi ya vijiji wananchi wamekuwa watazamaji tu wa nyaya na nguzo za umeme,nakuomba Mhe. Waziri uwahurumie wananchi hawa nao wapate umeme”,alisema Mhe. Azza huku amepiga magoti mbele ya Waziri Kalemani.
NIMEKUWEKEA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA ZIARA YA WAZIRI KALEMANI...Tazama hapa chini
Waziri wa Nishati nchini Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia) akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko wakati akiwasili katika kijiji cha Mahembe kilichopo katika kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akiwa katika ziara yake mkoani Shinyanga kukagua utekelezaji wa mradi wa Umeme Vijijini (REA awamu ya tatu). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waziri wa Nishati nchini Dkt. Medard Kalemani akiwahamasisha wakazi wa Mahembe kulipia shilingi 27,000/= ili waunganishiwe huduma ya umeme kwenye nyumba zao.
Hapa ni katika kijiji cha Lutolyo zoezi la kuweka nguzo za umeme likiendelea : Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa maelekezo kwa Wakandarasi wa mradi wa Umeme Vijijini kuhakikisha wanatumia wananchi wa kwenye vijiji kama vibarua badala ya kuleta watu wengine nje ya vijiji.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza katika shule ya Sekondari Mishepo kabla ya kuwasha umeme kwenye shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Ng'wang'hosha kata ya Nyamalogo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Dkt.Kalemani aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa maagizo kwa wakandarasi wa Mradi wa Umeme Vijijini (kulia) kuhakikisha wanasambaza kwenye nyumba zote katika shule ya sekondari Mishepo na kuwapatia umeme wananchi wa vitongoji vyote vya kijiji cha cha Ng'wang'hosha kata ya Nyamalogo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.  
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani  akikata utepe ikiwa ni ishara ya Uwashaji umeme katika shule ya sekondari Mishepo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme katika shule ya sekondari Mishepo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akikata utepe wakati akiwasha umeme katika nyumba ya bwana Hamis Mgalula mkazi wa kijiji cha Ibingo kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (wa pili kushoto).
Wananchi wakishuhudia umeme ukiwashwa katika familia ya ya bwana Hamis Mgalula
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitabasamu baada ya kuwasha umeme katika nyumba ya bwana Hamis Mgalula mkazi wa kijiji cha Ibingo kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (angalia taa hapo juu...mambo safi kabisa kwenye nyumba ya tembe).
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akimkaribisha Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ukiwasili katika Kijiji cha Mwakitolyo namba 5 katika kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kumweleza kuwa miongoni mwa changamoto katika kata hiyo ni umeme.
Mbunge wa Jimbo la Solwa,Mhe. Ahmed Salum akitoa salamu kwa wananchi wa Mwakitolyo
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akimpongeza Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal na Mbunge wa Jimbo la Solwa, mhe. Ahmed Salum kwa jitihada mbalimbali wanazofanya katika kuwasaidia wananchi ikiwemo kuwapigania kupata huduma ya umeme. 
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwaagiza wataalamu wakiwemo wakandarasi na viongozi wa TANESCO kuhakikisha wanasimika nguzo za umeme haraka iwezekavyo Mwakitolyo ili wananchi waanze kupata huduma ya umeme. Mwakitolyo namba 5 ni miongoni mwa vijiji ambavyo vilikuwa vimerukwa kwenye mradi wa REA.
Wakazi wa Mwakitolyo wakimsikiliza Dkt. Kalemani.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani  akiwahamasisha wananchi kutumia kifaa 'UMETA' ili kupunguza gharama za kuunganisha mfumo wa umeme majumbani.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwahamasisha wakazi wa Kijiji cha Lyabukande kata ya Lyabukande kulipia shilingi 27,000/= ili wapate huduma ya umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akipiga makofi baada ya kukata utepe ishara ya kuwasha umeme katika shule ya msingi Luhumbo iliyojengwa mwaka 1945.
Viongozi mbalimbali wakifurahia baada ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kuwasha umeme katika shule ya msingi Luhumbo iliyopo katika kijiji cha Itwangi.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal akipiga magoti kumuomba Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani vijiji ambavyo havina huduma ya umeme ikiwemo Danduhu,Chembeli,Bukumbi,Mwanono n.k vipatiwe huduma ya umeme kama ilivyofanyika kwenye kijiji cha Itwangi ambacho kilikuwa kimerukwa kwenye mradi wa REA.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Itwangi.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiagiza wakandarasi wa mradi umeme vijijini kutoka Kampuni ya Angelique International Limited’ kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kushindwa kutekeleza kwa wakati kazi ya kuwapelekea umeme wananchi. Wa tatu kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo,bwana Dilip Singh na wenzake wawili raia wa India ,Dilip Patra na Ramashakur (kulia).
Meneja wa Kampuni ya Angelique International Limited’  ,bwana Dilip Singh na wenzake wawiliDilip Patra na Ramashakur wakipanda kwenye gari la polisi.
Baada ya kumaliza ziara : Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa maelekezo kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na Meneja wa TANESCO mkoa wa Shinyanga,Mhandisi  Fedgrace Shuma (kulia).
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1Blog

ATZ Law Chambers Rebrands to A&K Tanzania, Expands Leadership Team

$
0
0
We wish to notify you that Anjarwalla & Khanna (A&K) Tanzania has taken over the practice of ATZ Law Chambers. The firm’s core leadership team will now include Partner, Geoffrey Dimoso and Director, Shemane Amin who joined in April and February respectively.
Driven by the firm’s vision to complement its robust local practice with the capability to service clients regionally and in recognition of the value that our clients have gained as a result of our cross-border collaboration with A&K Kenya, these developments will enable us to strengthen our regional offering by providing greater access to a broader pool of specialist teams and resources.
Our office address, client engagement terms, and operations in our Dar es Salaam office will remain unchanged, but our offering will now be bolstered by the expansion of the leadership team.
In his new role, Mr. Dimoso will work closely with the rest of the A&K Tanzania leadership team to ensure that the firm continues to provide exceptional service to clients in Tanzania and the wider region. With over 15 years of experience in private practice, Dimoso headed the legal department and served as company secretary of the Commercial Bank of Africa (Tanzania), and previously, Azania Bank. 
Dimoso is a practicing Advocate of the High Court of Tanzania and holds a Master of Laws degree and a Bachelor of Laws degree from the University of Dar es Salaam. He is certified as a director by the Commonwealth Centre for Corporate Governance (Kenya) and the Institute of Directors (Tanzania), and is a member of various professional bodies, including the Tanganyika Law Society and the East African Law Society.
Tasked with managing the firm’s client experience and overseeing operations, Ms. Amin joined A&K Tanzania from Philip Morris where she held a dual management role as the Manager for Corporate Affairs and the Manager for Commercial, Strategy and Planning.  Prior to that, she worked as a Corporate Advisor at Mohammed Enterprises Tanzania Limited, where she oversaw complex corporate transactions.  
Ms. Amin started her legal career in the United States, where she worked for law firm Brown Rudnick LLP. She is a graduate of Boston University School of Law, where she obtained a Juris Doctor degree, after graduating from Duke University with a Bachelor of Arts degree on full scholarship from the Robertson Scholars Program.
We are confident that the rebranding and entry of our new team members and our offering to clients in Tanzania and across Africa will be bolstered. Similarly, we remain grateful to our clients and other key stakeholders whose support has continually facilitated our growth.
As the exclusive ALN firm in Tanzania, A&K Tanzania will continue to leverage the alliance’s “one-stop-shop” approach on cross-border matters to provide integrated solutions to support clients in doing business across the continent.
About the Firm
A&K Tanzania is a leading full service corporate and commercial law firm based in Tanzania’s commercial capital, Dar es Salaam. The firm is uniquely placed to advise clients on the legal and commercial aspects of doing business in Tanzania. Our team of lawyers has significant experience handling sophisticated local and cross-border transactions in corporate M&A, projects and infrastructure, real estate, banking and finance, capital markets, insolvency, mining, energy, telecommunications, competition, and employment.
A&K Tanzania is strengthened by the firm’s pan-African reach through ALN, a leading alliance of top-tier independent firms in fifteen countries across Africa. The firm also works closely with ALN’s Regional Office in the UAE, Anjarwalla Collins & Haidermota.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images