Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Benki ya Posta Tunduru Yatoa msaada wa vifaa saidizi kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi

$
0
0
Na Theresia Malya, Afisa Habari Tunduru
Benki ya posta Tanzania Tawi la Tunduru imekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 2,949,000.00 kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi vyenye wa ngozi waliopo katika shule za msingi na sekondari wilayani Tunduru.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru  Ndg Gasper Balyomi Meneja wa Benki ya Posta tawi la Tunduru Bi. Emajackline Mtemba alisema vifaa hivyo ni mafuta kinga, kofia za kujikinga na mionzi ya  jua (pama), Miwani, Sabuni za kuoga, na Viookuza (Magnifier).

Bi Mtemba aliwaasa watoto hao kutumia vifaa hivyo kusoma vizuri na view chachu ya kuongeza bidii katika masomo yao,kuweni na  nidhamu kwa  kutii wazazi na walimu “lakini vifaa hivi viwe chachu kwenu ya kusoma na kufanya vizuri Zaidi kwenye masomo yenu kwani nyie ndio viongozi wa baadaye na ni matarajio ya benki ya posta ya Tanzania kuwa watoto hawa wenye ulemavu wa ngozi wana nafasi kwenye jamii kama walivyo watoto wengine na ndio viongozi wa baadaye”

Nitoe wito kwa wazazi wote kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu wa ngozi kwani wao wana haki ya kupata elimu kwani ni haki ya msingi kwa kila mtoto na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inawatambua na kuwajali, pia niwakumbushe wazazi kuwawekea watoto Amana kwa ajili ya kusomea ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa Ada.

Akitoa taarifa fupi ya Halmashauri ya Tunduru  mgeni rasmi ambaye pia Mkurugenzi Mtendaji  Ndg. Gasper Zahaoro Balyomi alianza kwa kuishukuru benki ya posta Tanzania  tawi la Tunduru kutoa vifaa saidizi kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wilayani Tunduru ambapo alipokea kofia 72, mafuta kinga chupa 72, sabuni 72, miwani na viookuza kwa ajili ya kugawa kwa wanafunzi hao.

Gasper Balyomi aliendelea kusema Halmashauri ya Tunduru ina shule 149 za serikali kati ya hizo  ndio zilizo na vitengo vya elimu maalum, ambazo ni  Tunduru Mchanganyiko na Namiungo shule ya Msingi.

“Tunduru ina shule za msingi 149 za serikali na shule mbili za Namiungo na Tunduru Mchanganyiko ndio wanapokea watoto wenye mahitaji maalum, lakini ina idadi ya wanafunzi wenye ulemavu  432 ikiwa wasichana ni 167 na wavulana 265, na upande wa shule za sekondari ina wanafunzi 27, wasichana 12 na wavulana 15, lakini watoto wenye ulemavu wa ngozi ni 36 ikiwa wasichana ni 19 na wavulana 17”alisema Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru.

Aidha alisema changamoto kubwa wanayokumbana nayo watoto hawa wenye ulemavu wa ngozi ni pamoja na kukosekana kwa mafuta kinga, miwani, kofia za kujikinga na mionzi ya jua (Pama), lakini pia kukosekana kwa huduma za matitabu ya ngozi katika hospitali za wilaya na badala yake zinapatikana katika hospitali zenye vitengo maalumu kama hospitali KCMC iliyopo Moshi, Bugando mwanza na Muhimbili ambapo wazazi wanashindwa kumudu gharama za kuwasafirisha watoto hawa.

Aliendelea kutanabaisha kwa  kusema  Halmashauri ina walemavu wa aina mbalimbali hivyo ni vyema jamii na wadau wa maendeleo kujitokeza katika kuwawesha ili waweze kusoma na kufikia malengo yao kwani miongoni mwa hawa watoto wapo wenye vipaji ambavyo vinahitaji kuendelezwa.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa Halmashauri ina mpango mkakati wa  kuanzisha ya shule ya watoto wenye mahitaji maalum kwa ajili ya wanafunzi wa sekondari ambao wakifaulu wanashindwa kuendelea na masomo.

Sambamba na kuanzishwa  kwa shule hiyo  lakini kwa sasa tuna mikakati ya kuiombea shule ya sekondari Nandembo iliyopo wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma kuanzisha  kitengo cha Elimu maalum ili kupunguza changamoto ya wanafunzi wanaofaulu kuendelea na masomo ya juu kutumia nafasi zao kwani wengi wanashindwa kwenda shule wanazopangiwa nje ya wilaya kutokana na wazazi kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Halmshauri ya Tunduru Kaimu afisa elimu Bi Loya Mwajabu kwa Benki ya Posta Tawi la Tunduru alisema  serikali kupitia  sera ya elimu ya mwaka 2004 haijabagua watoto kwani watoto wote ni sawa na wanatakiwa kupata elimu kwani ni haki ya msingi.

Alisema Kupata elimu kwa watoto kutamsaidia mtoto kujitambua na kupata urithi ulio sahihi, mama ni mlezi mkubwa na nikuhakikishie kuwa hawa watoto watatumia vifaa hivi vile iliyoelekezwa, wito wetu kwa jamii ni kuwa  hawa wamezaliwa hivi walivyo na wana haki ya kupata elimu kwani ndio ukombozi wao.

Aidha niwaombe wazazi,  jamii na wadau wa elimu na maendeleo ndani nan je ya wilaya ya Tunduru kuguswa na watoto hawa, kuunga mkono juhudi za serikali katika  kuwasaidia vifaa saidizi watoto kwani watoto 432 wenye ulemavu ni wengi sana na sio hawa wenye ulemavu wa ngozi tuu,pia wapo wenye mtindio wa ubongo, bubu viziwi, viwete na wote hawa wanahitaji kusaidiwa kufikia ndoto zao.

 Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri  ya Tunduru Ndg Gasper Balyomi akimvisha kofia ya kujikinga na mionzi ya jua (pama) wakati alipokua akipokea vifaa kutoka kwa meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduru Bi.Emajackline Mtemba  vyenye thamani Tsh 2949,000.00 katika halfa iliyofanyika ukumbi wa Klasta..
  Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri  ya Tunduru Ndg Gasper Balyomi akiongea katika hafla ya kupokea vifaa kutoka kwa meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduru Bi.Emajackline Mtemba  vyenye thamani Tsh 2949,000.00 katika halfa iliyofanyika ukumbi wa Klasta..

 Meneja wa benki ya posta Tanzania tawi la Tunduru Bi Emajackline Mtemba akiongea na wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi, wazazi na walimu wakati alipokuwa akikabidhi vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wilayani Tunduru iliyofanyika katika ukumbi wa Klasta Mlingoti.
 Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Gasper Zahoro Balyomi akikabidhi vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wilayani Tunduru vilivyotolewa na benki ya Posta tawi la Tunduru
 Meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduru Bi.Emajackline Mtemba akikabidhi vifaa saidizi kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi  vyenye thamani ya Tsh.2,949,000.00 kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru Ndg Gasper Zahoro Balymi kwenye halfa iliyofanyika ukumbi wa Klasta Tunduru.

 

Katika picha ni viongozi wa Benki ya Posta Tawi la Tunduru, viongozi wa Idara ya Elimu Msingi  na watoto wenye Ulemavu wa ngozi baada ya kukabidhiwa vifaa saidi kwa ajili ya kujikinga na madhara yatokanayo na jua na magonjwa ya ngozi.



NAFASI ZA KAZI

TECNO YAZINDUA BODA LA SPARK 3

$
0
0
Kampuni ya simu ya TECNO mobile inawakaribisha wateja wake kununua simu mpya iliyozinduliwa hivi karibuni aina ya TECNO SPARK 3 na kujishindia zawadi kemkem ikiwemo pikipiki mpya.

Promotion hiyo iliyopewa jina la boda la spark 3 inaanza kwa mkoa wa dar es salaam kisha kuenea mikoa mingine hapo baadae, mteja atakaenunua TECNO spark 3 kwenye maduka maalumu ya TECNO yenye promotion hiyo atapewa nafasi ya kuondoka na zawadi za papo kwa papo kama power bank yenye mAh 5000 na pamoja data cable,

TECNO Spark 3 ni simu ya kijanja yenye uwezo mkubwa wa kupiga picha pamoja na kufanya vitu mbali mbali mitandaoni imezinduliwa takribani mwezi mmoja ikiwa ndio simu inayofanya vizuri zaidi kwa upande wa simu janja za kipato cha kati.

TECNO SPARK 3 ina ubora wa kamera yenye megapixel 13, huku mtumiaji anapata nafasi ya kuifadhi vitu vyake kwenye GB 16 za memory ya ndani na muonekano wake ni wakijanja na ndio maana inafanya vizuri sokoni,
Mshindi wa pikipiki atapatikana mwisho wa mwezi wa sita kwa njia ya bahati nasibu itakayo chezeshwa live kupitia mitandao ya kijamii ya TECNO mobile hasa Instagram

WAZIRI MKUU AZIAGIZA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO YA MICHEZO

$
0
0




WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza halmashauri zote za majiji na miji zihakikishe kuwa kuanzia sasa zinatenga maeneo ya michezo na burudani kila zinapopima viwanja.

“Naagiza kuanzia sasa, maeneo yote yanayopimwa na halmashauri na miji yote nchini, lazima yazingatie uwepo wa maeneo ya michezo na burudani,” amesisitiza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Juni 10, 2019) wakati akifungua mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za msingi na sekondari Tanzania, katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara. Zaidi ya wanafunzi 5,400 wanashiriki mashindano hayo.

Pia, amezitaka Halmashauri ziweke mpango madhubuti wa kuyaendeleza maeneo ya michezo na burudani sambamba na miundombinu inayozingatia mahitaji ya wote bila kubagua.

Amesema katika baadhi ya maeneo kumekuwepo na uhaba wa viwanja vya michezo kwa sababu ya mipango miji isiyozingatia mipango endelevu ya sekta mbalimbali.

Hivyo, Waziri Mkuu ameagiza yafanyike marekebisho na hatua za haraka ili kutoa fursa ya ukuaji wa michezo na kusaidia wananchi kushiriki michezo, mazoezi na kupata burudani.

Amesema ifikapo Septemba 30, 2019, kila halmashauri iwe imefanya mapitio ya maeneo yote yaliyokuwa yamepimwa kwa matumizi ya huduma maalum ikiwemo michezo, burudani, shule na ibada na kutoa taarifa kama yanatumika kwa ajili hiyo au vinginevyo.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia irudishe na iimarishe mchepuo wa Elimu kwa Michezo Chuo cha Ualimu Butimba ili kupata wataalam zaidi. 

“Halmashauri ziendelee kuwaruhusu walimu mbalimbali nchini kuhudhuria mafunzo ya michezo katika chuo cha Mendeleo ya Michezo Malya ili kupunguza uhaba wa watalaam wa michezo katika shule mbalimbali na nchini kwa ujumla.”

Waziri Mkuu amesema michezo ni muhimu kwa wanafunzi kwa kuwa itawaepusha vijana na makundi yasiyofaa yakiwemo matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine visivyoendana na maadili ya Kitanzania.

Amesema michezo itawawezesha vijana kuwa na afya bora na kufanya vema katika masomo yao kwa kuwa ili waweze kusoma vema ni sharti afya zao ziwe njema. Pia sanaa itasaidia katika kuutambulisha utamaduni wetu ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. 

“Kwa hiyo, ni vema tukatambua kuwa michezo na sanaa ni sehemu ya elimu bora. Hivyo, ni muhimu kutekeleza dhana ya elimu ya michezo ili tuweze kufikia maendeleo tarajiwa.”

 Kadhalika, Waziri Mkuu amesema sambamba na michezo iliyozoeleka, pia wanaweza kuibua michezo yao ya asili ambayo itautambulisha utamaduni wetu. “Nitoe wito kwa shule zetu, ziendeleze ubunifu wa kuibua vipaji vya sanaa na michezo ya asili katika maeneo yetu kwa lengo la kuenzi utamaduni wetu.”

Akizungumzia kuhusu mashindano ya mwaka huu ambayo yameshirikisha wanafunzi wengi zaidi wenye mahitaji maalumu, Waziri Mkuu amesema waendelee kuwahusisha wanafunzi wote katika michezo, sanaa na burudani bila kujali aina ya ulemavu walionao. 

Amesema jambo hilo ni muhimu kwa kuwa vipaji vipo kwa wote na fursa ndizo zitakazowawezesha kuonesha vipaji hivyo na kuvikuza.

Waziri Mkuu amewasisitiza wadau wote wa shule za msingi, sekondari, vyuo, sehemu za kazi na wizara, waweke mipango ya kudumu ya kuwashirikisha watu wenye mahitaji maalumu katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi bila ubaguzi wowote. 

“Hakikisheni baadhi ya vikwazo katika kushirikisha watu wenye mahitaji maalumu kwenye michezo vinaondolewa. Vikwazo hivyo ni pamoja na kutokuwepo kwa mipango endelevu katika maeneo mbalimbali na uwepo wa mitazamo hasi ya baadhi ya walimu, wazazi na viongozi katika maeneo yao dhidi ya uwezo wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.”

Aidha, Waziri Mkuu ametuamia fursa hiyo kuupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kuwa mmoja kati ya Mikoa ya mfano katika kutekeleza agizo lake la mwaka jana alilolitoa kupitia michezo hiyo la kuanzishwa kwa shule maalumu za michezo.

Mkoa wa Simiyu umejenga Shule ya Sekondari itakayokuwa kituo cha kukuza vipaji vya wanafunzi katika michezo. “Naagiza mwakani wanafunzi wote walioonesha vipaji katika michezo watakaofaulu Mtihani wa Elimu ya Msingi wapangwe katika shule hiyo ili wakakuze vipaji vyao.” 

Amesema bila ya kuwa na mipango ya kulea na kukuza vipaji kutoka ngazi za chini Taifa haliwezi kupata mafanikio katika michezo nchini. Kwani katika kipindi ambapo michezo hiyo ilisitishwa kiwango cha michezo ya aina mbalimbali kilikuwa chini sana.

“Tangu tumerejesha shughuli za michezo katika shule zetu tumekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kupata wachezaji wanaofuzu kucheza soka la kulipwa kwenye viwango vya kimataifa kama Mbwana Samatta (Genk –Belgium), Simon Msuva (Difaa El Jadid – Morocco), “

Wengine ni Shiza Kichuya (Enppi –Misri), Thomas Ulimwengu (JS Saoura – Algeria), Hamid Mao (Petrojet – Misri), Adi Yusuph (Blackpool –England), Hassan Kessy (Nkana – Zambia), Yahya Zaydi (Ismaily –Misri), Shabani Chilunda, (Tenerife – Hispania) Rashid Mandawa (BDF- Botswana), Farid Mussa ( Tenerife– Hispania).

Waziri Mkuu amesema pamoja na mafanikio yaliyopatikana, jitihada zaidi zinahitajika ili kuwa na maendeleo ya kutosha katika shughuli za michezo nchini.

Hivyo, Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI wakamilishe tathmini ya shule 56 za Serikali zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza vipaji vya michezo.

Ufunguzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Maafisa Elimu kutoka mikoa yote nchini, walimu wa michezo pamoja na Maofisa wengine wa Serika
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jafo wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mtwara kufungua michezo ya UMISETA kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Juni 10, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wanamichezo wakati alipowasili kwenye uwanja wa Nangwada Sijaona mjini Mtwara kufungua Mashindano ya UMISETA, Juni 10, 2019. Wengine Pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelsius Byakanwa, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako, na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza.
 Wanamichezo kutoka Mkoa wa Simuyu wakiingia kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona kushiriki katika Ufunguzi wa Michezo ya UMISETA uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya soka  mkoa wa Tanga wakati alipofungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara Juni 10, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya soka ya mkoa wa Mtwara wakati alipofungua mshindano ya UMISETA  kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Tanga Juni 10, 2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

ASKARI, MFANYAKAZI WA TRA WALIOTAJWA IKULU KWA RUSHWA WAFIKISHWA KORTINI

$
0
0


ASKARI Polisi wawili na mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), waliotajwa na mfanyabiashara Ikulu kwamba wamemdai rushwa na kuzuia mzigo wake tangu mwaka 2016 wamepandishwa kizimbani.

Mfanyabiashara huyo aliwataja katika mkutano wa Rais Dk. John Magufuli na wafanyabiashara uliofanyika Juni 7, mwaka huu ikulu jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Juni 10, kwa tuhuma za kushawishi kupewa rushwa ya Sh milioni mbili na mfanyabiashara Ramadhan Ntuzwe.

Washtakiwa ambao ni askari na namba zao ni H 4086 PC Simon Sungu, H 4810 PC Ramadhan Uwezi wa Kituo cha Polisi Osterbay na Mfanyakazi wa TRA, Charity Ngalawa.

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Sophia Gula aliwasomea washtakiwa shtaka linalowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Amedai washtakiwa wanashtakiwa kwa kushawishi rushwa, wanadaiwa Oktoba 29, 2016 maeneo ya Kimara mwisho, wakiwa wafanyakazi wa TRA na Polisi walidai rushwa ya Sh milioni mbili kutoka kwa Ntuzwe.

Washtakiwa wanadaiwa walidai rushwa hiyo kama kishawishi cha kuruhusu mzigo wake ambao unadaiwa ulikadiriwa kodi ndogo jambo ambalo lilikuwa chini ya wakubwa wao.

Washtakiwa walikana kutenda makosa hayo, Jamhuri walidai upelelezi haujakamilika na hapakuwa na pingamizi kwa washtakiwa kupata dhamana.

Mahakama ilikubali kuwapa dhamana kwa masharti ya kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni tano, washtakiwa walitimiza masharti wako nje kwa dhamana. GPL

BANDARI YA KAGUNGA MKOANI KIGOMA YAKAMILIKA

$
0
0
Bandari ya Kagunga Mkoani Kigoma inavyoonekana kwa juu mara baada ya kufanyiwa ukarabati ambapo itaweza kuhudumia Nchi  tatu  ,Burundi,Congo na Zambia

Maamuzi ya JPM ni Muhimu Kuelekea TZ ya Viwanda 2025 - Wasomi CBE Dodoma

BUNGALOW LINAUZWA KIJITONYAMA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Bungalow lililo kwenye high density plot 447 block 45C Kijitonyama jijini Dar es salaam. Bei ya juu ni TZS300m ya chini 250m. Lipo barabara ya Bahari Motor Bazaar karibu ya ofisi ya Hashim Rungwe! 
Kwa mawasiliano piga:  
0713415038/0757224489/0786948692





Mtangazaji Clouds FM Meena Ally aweka wazi mipango yake

Register Now for next week's event. 2019 IT Annual Conference.

MIRADI YA SHILINGI BILIONI 22.9 YAZINDULIWA ARUMERU

$
0
0

Na.Vero Ignatus,Arumeru.

Mwenge wa uhuru umezindua miradi yenye thamani ya shilingi Bilioni 22.9 na miradi I6 katika sekta ya kiliko,afya,maji ,kilimo,ufugaji kwenye halmashauri zote mbili za Arusha DC na Meru.

Licha ya mwenge huo kuzindua miradi hiyo bado kumekuwa na changamoto katika baadhi ya miradi ambayo imetembelewa ambapo Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ameahidi kusimamia kuhajikisha changamoto hizo zinanalizika kabisa.

Muro ameyaeleza hayo mapema jana wakati akikabidhi mwenge huo wa uhuru kwa mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro eneo la Moivaro jijini Arusha.

Hata hivyo ameeleza kuwa kati ya miradi 16 mradi iliyozinduliwa na mwenge huo, mradi mmoja wa Maji ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2017 umekuwa na changamoto kutokana na wahusika kutofanya kazi kama inavyotakiwa katika mradi huo.

"Mwenge wa mwaka huu ni wa kweli kweli hauna mchezo na ukikuta kuna changamoto yeyote unaelimisha na kuelezwa namna ya kuitatua na pale walipofanya vizuri mwenge unawapongeza" Alisema Muro.

Akipokea mwenge huo ,mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro, amesema mwenge huo utakagua,kuzindua,kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 8 yenye thamani ya shilingi bilioni 521 ambayo inahusisha,afya elimu, maji ,mazingira na ujasriamali .

auli mbiu ya mwaka huu ni Maji ni haki ya kila mtu tutunze vyanzo vyake ,tukumbuke kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.Mwenge huo kesho utakabishiwa wilayani Monduli na siku inayofuata utakabidhiwa wiolayani Karatu ambapo utahitimisha mbio zake mkoani Arusha na kukabidhiwa mkoani Manyara.

WAZIRI WA NISHATI AFANYA ZIARASHINYANGA, AWASHA UMEME VIJIJINI

$
0
0


Waziri wa Nishati nchini Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara mkoani Shinyanga kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini (REA),kufuatilia uimara wa umeme pamoja na kuhamasisha wananchi kulipia shilingi 27,000/= ili waunganishiwe umeme kwenye nyumba zao.

Ziara hiyo imefanyika leo Jumatatu Juni 10,2019 katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambapo Waziri Kalemani amezungumza na wananchi wa Mwakitolyo,Lyabukande,Mahembe na kuwasha umeme katika vijiji vya Mishepo,Itwangi na Ibingo ambavyo awali vilirukwa katika mradi wa REA.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Dkt. Kalemani alisema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 36 kwa ajili ya kufikisha umeme vijijini huku akikisitiza kuwa ifikapo Desemba 2019 vijiji vyote viwe vimepata huduma ya umeme.

“Tunataka ifikapo mwezi Desemba kila kijiji kiwe kimepata umeme,mwananchi utatakiwa kulipia shilingi 27,000/= tu,ukishalipa hiyo wewe dai umeme huhitaji kuuliza nguzo ziko wapi,nguzo siyo jukumu lako…wewe subiri kuunganishiwa tu umeme ndani ya siku saba. Tunataka wananchi wapate umeme bila kujali wanaishi kwenye nyumba za namna gani”,alisema Dkt. Kalemani.

“Tunahitaji kuona taasisi zote zikiwemo shule,zahanati,makanisa,misikiti inapata umeme hata kama zipo mbali kiasi gani na ili kupunguza gharama za kuunganisha mfumo wa umeme ndani ya nyumba ‘Wiring’ tunashauri wananchi mtumie kifaa cha “UMETA”,alisema Dkt. Kalemani.

Hata hivyo Waziri huyo alieleza kutoridhishwa na kasi ndogo ya Wakandarasi wa mradi wa Umeme Vijijini mkoani Shinyanga Kampuni ya Angelique International Limited’ ambapo aliagiza jeshi la polisi kumuweka chini ya ulinzi Meneja wa kampuni hiyo,bwana Dilip Singh na wenzake,Dilip Patra na Ramashakur.

“Mhe. Mkuu wa wilaya naomba uchukue hati ya kusafiria ya Mkandarasi huyu,badala ya kukaa kwenye Site yeye anaishi India,amekuja leo baada ya kusikia nakuja. Nataka awepo Shinyanga mpaka pale atakapomaliza kufanya kazi tuliyompa,tunataka wananchi wapate umeme,nanyi TANESCO hakikisheni mnaweka vituo kwenye vijiji hatutaki wananchi wawafuate mjini”,aliongeza Dkt.Kalemani.

Awali Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe.Azza Hilal na Mbunge wa Jimbo la Solwa,Ahmed Salum walimweleza waziri huyo kuwa mradi wa umeme vijijini umekuwa ukisuasua mkoani Shinyanga kutokana na kasi hafifu ya wakandarasi.

“Mbali na Wakandarasi kuwa wazito katika utekelezaji wa mradi wa REA,changamoto nyingine ni baadhi ya vijiji kurukwa hivyo kwenye baadhi ya vijiji wananchi wamekuwa watazamaji tu wa nyaya na nguzo za umeme,nakuomba Mhe. Waziri uwahurumie wananchi hawa nao wapate umeme”,alisema Mhe. Azza huku amepiga magoti mbele ya Waziri Kalemani.
Waziri wa Nishati nchini Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia) akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko wakati akiwasili katika kijiji cha Mahembe kilichopo katika kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akiwa katika ziara yake mkoani Shinyanga kukagua utekelezaji wa mradi wa Umeme Vijijini (REA awamu ya tatu). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waziri wa Nishati nchini Dkt. Medard Kalemani akiwahamasisha wakazi wa Mahembe kulipia shilingi 27,000/= ili waunganishiwe huduma ya umeme kwenye nyumba zao.

Hapa ni katika kijiji cha Lutolyo zoezi la kuweka nguzo za umeme likiendelea : Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa maelekezo kwa Wakandarasi wa mradi wa Umeme Vijijini kuhakikisha wanatumia wananchi wa kwenye vijiji kama vibarua badala ya kuleta watu wengine nje ya vijiji.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza katika shule ya Sekondari Mishepo kabla ya kuwasha umeme kwenye shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Ng'wang'hosha kata ya Nyamalogo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Dkt.Kalemani aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa maagizo kwa wakandarasi wa Mradi wa Umeme Vijijini (kulia) kuhakikisha wanasambaza kwenye nyumba zote katika shule ya sekondari Mishepo na kuwapatia umeme wananchi wa vitongoji vyote vya kijiji cha cha Ng'wang'hosha kata ya Nyamalogo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akikata utepe ikiwa ni ishara ya Uwashaji umeme katika shule ya sekondari Mishepo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme katika shule ya sekondari Mishepo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akikata utepe wakati akiwasha umeme katika nyumba ya bwana Hamis Mgalula mkazi wa kijiji cha Ibingo kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (wa pili kushoto).
Wananchi wakishuhudia umeme ukiwashwa katika familia ya ya bwana Hamis Mgalula
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitabasamu baada ya kuwasha umeme katika nyumba ya bwana Hamis Mgalula mkazi wa kijiji cha Ibingo kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (angalia taa hapo juu...mambo safi kabisa kwenye nyumba ya tembe).
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akimkaribisha Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ukiwasili katika Kijiji cha Mwakitolyo namba 5 katika kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kumweleza kuwa miongoni mwa changamoto katika kata hiyo ni umeme.
Mbunge wa Jimbo la Solwa,Mhe. Ahmed Salum akitoa salamu kwa wananchi wa Mwakitolyo
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akimpongeza Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal na Mbunge wa Jimbo la Solwa, mhe. Ahmed Salum kwa jitihada mbalimbali wanazofanya katika kuwasaidia wananchi ikiwemo kuwapigania kupata huduma ya umeme. 
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwaagiza wataalamu wakiwemo wakandarasi na viongozi wa TANESCO kuhakikisha wanasimika nguzo za umeme haraka iwezekavyo Mwakitolyo ili wananchi waanze kupata huduma ya umeme. Mwakitolyo namba 5 ni miongoni mwa vijiji ambavyo vilikuwa vimerukwa kwenye mradi wa REA.
Wakazi wa Mwakitolyo wakimsikiliza Dkt. Kalemani.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwahamasisha wananchi kutumia kifaa 'UMETA' ili kupunguza gharama za kuunganisha mfumo wa umeme majumbani.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwahamasisha wakazi wa Kijiji cha Lyabukande kata ya Lyabukande kulipia shilingi 27,000/= ili wapate huduma ya umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akipiga makofi baada ya kukata utepe ishara ya kuwasha umeme katika shule ya msingi Luhumbo iliyojengwa mwaka 1945.
Viongozi mbalimbali wakifurahia baada ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kuwasha umeme katika shule ya msingi Luhumbo iliyopo katika kijiji cha Itwangi.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal akipiga magoti kumuomba Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani vijiji ambavyo havina huduma ya umeme ikiwemo Danduhu,Chembeli,Bukumbi,Mwanono n.k vipatiwe huduma ya umeme kama ilivyofanyika kwenye kijiji cha Itwangi ambacho kilikuwa kimerukwa kwenye mradi wa REA.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Itwangi.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiagiza wakandarasi wa mradi umeme vijijini kutoka Kampuni ya Angelique International Limited’ kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kushindwa kutekeleza kwa wakati kazi ya kuwapelekea umeme wananchi. Wa tatu kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo,bwana Dilip Singh na wenzake wawili raia wa India ,Dilip Patra na Ramashakur (kulia).
Meneja wa Kampuni ya Angelique International Limited’ ,bwana Dilip Singh na wenzake wawiliDilip Patra na Ramashakur wakipanda kwenye gari la polisi.
Baada ya kumaliza ziara : Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa maelekezo kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na Meneja wa TANESCO mkoa wa Shinyanga,Mhandisi Fedgrace Shuma (kulia).Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1Blog

WAZIRI KIGWANGALLA AINGILIA KATI NA KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI HIFADHI NGORONGORO NA WANANCHI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa Kata ya Alaitole ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alipofika kutatua mgogoro wa wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro. Hata hivyo Waziri Kigwangalla ameumaliza mgogoro huo kwa kuagiza wakazi hao wapewe kibali cha ujenzi na mamlaka hiyo katika eneo lililopendekezwa. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akisikiliza maoni na hoja za wananchi wa Kata ya Alaitole alipofika kutatua mgogoro wa wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika eneo lao la Esere, wilayani Ngorongoro jijini Arusha. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe.William Ole Nasha akizungumza na wakazi wa Kata ya Alaitole iliyo ndani ya Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambayo ilizuiwa kujenga shule ya bweni ya wasichana na mamlaka hiyo zuio ambalo limeondolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii aliyefika katika kata hiyo kutatua mgogoro huo. 
Mkutano wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na wananchi wa Kata ya Alaitole katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Mhe. Kigwangalla alifika kutatua mgogoro uliohusisha wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa Kata ya Alaitole ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kupitishwa na katika eneo lilipoonekana fuvu linalosadikiwa kuwa ni la binadamu wa kale ambalo bado taarifa zake zinaendelea kufanyiwa utafiti katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe.William Ole Nasha na askari wa uhifadhi wakiangalia eneo itakapojengwa shule ya wasichana ya bweni ya kata ya Alaitole. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, viongozi na wananchi wa Kata Alaitole wakitazama eneo lilipoonekana fuvu linalosadikiwa kuwa ni la binadamu wa kale lililogunduliwa na wakazi hao katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro. Taarifa kuhusu fuvu hilo zinaendelea kufanyiwa utafiti na watalaam. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana kwa furaha na wananchi wa Kata ya Alaitole ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alipofika kutatua mgogoro wa wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro. PICHA/ Wizara ya Maliasili na Utalii. 
…………………… 
WMU – Ngorongoro, ARUSHA. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro uwaruhusu wananchi wa Kata ya Alaitole wajenge shule ya wasichana ya bweni katika eneo la Esere lililo ndani ya Mamlaka hiyo ili waweze kupata elimu kufuatia wananchi hao kuzuiwa kwa muda mrefu kutekeleza mradi huo. 
Aidha, ameutaka uongozi wa Mamlaka hiyo utoe kibali cha kuwawezesha wananchi kata hiyo kuanza ujenzi haraka iwezekanavyo ili fedha zilizotolewa na Serikali shilingi milioni 298 zianze kutumika. 
Dkt. Kigwangalla ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Kata Alaitole wilayani Ngorongoro kwenye mkutano wa hadhara uliowashirikisha viongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, viongozi serikali wa kata hiyo, viongozi wa mila wa kabila la Masai na madiwani na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe. William Ole Nasha. 
Amesema Serikali inaunga mkono juhudi zote za wananchi za kujiletea maendeleo akifafanua kwamba hatua ya wananchi hao kuamua kujenga shule ya Sekondari ya Bweni ni jambo la linalopaswa kupongezwa na kila mpenda maendeleo. 
“Mnacho kitaka kiko wazi, mnataka maendeleo ya watoto wenu, katika hili mmesema kila baba anatoa elfu hamsini na wanawake wanatoa elfu ishirini, hili ni jambo kubwa achilia mbali nguvu kazi mnayojitolea na tayari serikali imeshaleta milioni 298, haiingii akilini eneo linalochangia kuleta na kuingiza mapato mengi Serikalini kiasi cha bilioni 126 likose shule” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla. 
Dkt. Kigwangalla ameeleza kuwa ujenzi shule hiyo utawaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wananchi hao kwenye mipango yao ya utekelezaji miradi ya maendeleo. 
Amesema jamii hiyo pamoja na mazingira wanayoishi kuwa ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro wanahitaji elimu. Aidha, amesema pia ni muhimu katika sekta ya utalii kupitia utamaduni wao akiongeza kuwa kazi ya Wizara ni kuona mafanikio ya sekta ya utalii yanakuwa kwa kuongeza mapato na sio migogoro. 
Dkt. Kigwangalla amesema Hifadhi ya Ngorongoro ni hifadhi mseto inayoruhusu binadamu na wanyama kuwepo katika eneo moja na kwamba hiyo ipo kwa mujibu wa sheria akiitaka Mamlaka hiyo kuyatazama vizuri majukumu yake ya kuendeleza Utalii, Kulinda rasilimali zililizopo kwa maana ya kuhifadhi na kuhudumia jamii iliyo ndani ya hifadhi hiyo. 
Katika hatua nyingine ameutaka uongozi wa Mamlaka hiyo uendelee kufanya mazungumzo na wananchi hao badala ya kujielekeza katika matumizi ya nguvu ili kupata uelewa wa pamoja akitolea mfano wa eneo la Loliondo ambalo hivi sasa lina utulivu. 
“ Viongozi wa Mamlaka mnalo jukumu la kuwasikiliza wananchi na kuamua kwa pamoja, eneo la Ngorongoro ni Urithi wa dunia na litaendelea kuwa hivyo kwa kuheshimu na maslahi ya Taifa na maslahi ya walio walio wengi” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla. 
Kuhusu mahusiano baina ya wananchi na wahifdhi Dkt. Kigwangalla amesema kuwa kupitia mkutano wake na wananchi amebaini kuwepo kwa tatizo la mawasiliano na mahusiano baina ya wananchi wa eneo hilo na watumishi wa Serikali walio chini ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro akibainisha kwamba tayari serikali imeliona jambo hilo na inaendelea kulifanyia kazi. 
Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe. William Ole Nasha akizungumza wakati wa mkutano huo amempongeza na kumshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha ulinzi wa rasilimali za Taifa katika maeneo mbalimbali nchini. 
Amemwomba aeendelee kutembelea maeneo mengine ya jimbo hilo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi wa kata za wilaya hiyo kwa lengo la kudumisha mahusiano mema. 
Mhe. Ole Nasha ameeleza kuwa hatua ya Wizara kutafutia ufumbuzi mgogoro huo wa ujenzi wa shule ya wasichana ya bweni, vile vile uamuzi wa serikali kutoa eneo na fedha kiasi cha shilingi milioni 298 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo katika eneo lililokubaliwa ni ishara tosha kwamba Serikali inawalinda na kuwajali wananchi wake. 
Amesema wananchi wa jimbo la Ngorongoro pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wako ni wasikivu na wako tayari muda wote kushirikiana na Serikali ikiwemo ulinzi wa rasilimali zilizopo na kuendeleza uhifadhi katika hifadhi ya Ngorongoro. 
Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Alaitole wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemshukuru Dkt. Kigwangalla kwa kuamua kuwafuata na kuzungumza nao katika makazi yao wakimpongeza kwa juhudi zake za kutatua changamoto mbalimbali kwa maslahi ya wananchi na uhifadhi. 
Aidha, wamemwomba kuendelea kuisimamia sekta ya uhifadhi nchi wakitoa wito wa kudumisha mahusiano mema baina ya wananchi na wahifadhi.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 11,2019

DKT. MAGUFULI ATOA YA MOYONI...ATUMA UJUMBE MZITO KWA ALIOWAPA NAFASI

$
0
0

*Asema huu si wakati wa kubembelezana na kuambiana maneno matamu
*Awapa maagizo mazito Waziri Viwanda na Biashara , Kamishna TRA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amesema ataendelea kutengua tu iwapo aliowapa nafasi watashindwa kufanya kazi ambayo anaitarajia na kwamba huu si wakati wa kubembelezana na kuambiana maneno mazuri.

Amesema Watanzania wanahitaji kuona matokeo mazuri kutoka serikalini na yeye atahakikisha anatimiza kiu hiyo, hivyo ambaye atashindwa hatamuacha abaki huko. pia ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa hata ambao amewaapisha leo wakishindwa kutimiza majukumu yao atawaondoa tu.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla za kuwaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa, Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Charles Kichere na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

"Ujue Watanzania wanataka kuona matokeo. Kuambiana maneno mazuri hakusadii.Sisi tunataka matokeo. Mimi jukumu langu ni kuteua ili kiu ya Watanzania ifanikiwe.

"Nimpongeze Kakunda(aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara) amekuja hapa na huko ndiko kukomaa kisiasa. Hizi kazi ni za muda, maisha yenyewe ni ya muda. Joseph Kakunda amejitoa, amesimama hapa na hiyo ndio sawa.

"Mimi nataka matokeo na Watanzania wanataka kuona utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo tumeahidi inatekelezwa. Changamoto za wafanyabishara ni nyingi, kulikuwa na ubaya gani, Waziri wa Viwanda na Biashara, Naibu Waziri na Katibu Mkuu kukutana na wafanyabiashara na kuzungumza nao. Kuna ubaya gani? Nani aliwazuia?Amehoji Rais Magufuli.

Ameongeza kitendo cha Waziri wa Viwanda na Biashara kutokutana na wafanyabiashara na kutatua matatizo yao ndio maana wanasema hawamjui. "Hata ningemsimamisha Stella Manyanya huenda wangesema hawamjui".

Rais Magufuli ameongeza kuwa, kuna korosho zimekaa tu kwenye maghala , tena wakati zinavunwa hakukua na nchi nyingine iliyokuwa na korosho lakini Wizara ya Viwanda na Biashara ikasubiri hadi nchi nyingine nazo zimevuna korosho na kuingiza sokoni.

"Waziri Bashungwa najua baada ya kukuteau wapo ambao wamekupongeza lakini mimi nakupa pole, maana nikiona mambo hayaendi natakutengua tu. Waziri Kabudi na Mpango wanashindwa kusema ukweli lakini pumbavu nimeshawaambia mara nyingi, inakuja tu licha ya kunizidi umri.

"Tuko kwenye vita haiwezekani tuko kwenye vita halafu tunabembelazana, lazima tuseme ukweli.Katika korosho Wizara ya Kilimo imefanya kazi yake kwa kukusanya korosho tani 223, 000 ambazo zipo kwenye maghala.

"Wametimiza wajibu wao lakini Viwanda na Biashara wamebangua tani 2000, hizi zingine abangue nani? Wizara ya Viwanda na Biashara ndio inayofanya biashara lakini wameshindwa na ilikuwa nitengue kuanzia juu hadi chini.

"Waziri Bashungwa ukienda pale Viwanda na Biashara nenda kafanye kazi.Usimchekee mtu , ni afadhali wakuchikie lakini niliyekuteau ni kusifu.Yale ambayo yapo pale nenda katatue,"amesema Rais Magufuli.

"Viwanda ambavyo vimeshindwa kufanya kazi sio tu kuviorodhesha bali kavichukue.Kwa mfano kiwanda cha nguo pale Mbeya kinakwenda kubadilishwa kuwa cha Pipi, haiwezekani hii nchi iwe ya kula mapipi."

Kwa upande wa TRA, Rais Magufuli amesema kuwa Dk.Philipo Mpango akiwa Kaimu Kamishna pale TRA alifanikiwa kukusanya kodi kutoka Sh.bilioni 850 hadi Sh.trilioni 1.3 na ndipo alipoamua kumteua kuwa Waziri wa Fedha .

"Wengine wote mkienda pale mnabaki kuwa tu hapo hapo mtadhani mmekariri.Aliyekuwa Kamishna wa TRA nimemtumia sms zaidi ya 30 za malalamiko lakini ukifuatilia hakuna matokeo.Dhambi ambayo ninayo siwezi kusahau jambo lazima nifuatilie.

"Haiwezekani Kamishna kukadiri kodi, anakadiria vibata halafu Kamishna wa TRA upo kimya tu unamuangalia. Haiwezekani kodi ya ndani inashuka halafu unakaa kimya.

"Kuna wafanyabiashara wanapakia mizigo wakidai inakwenda nje lakini wakifika mpakani wanagonga mhuri na kurudi nchini na TRA iko kila mahali, Kamishna yupo.TRA mnashikilia vifaa vya kuchimba dhahabu, vifaa vimekaa zaidi ya mwaka mzima.

"Alikuwa anadaiwa sijui Sh.milioni moja wakamuongezea nyingine,Wanashindwa kufahamu kuwa muwekezaji anaweza kuongeza ajira, Siku ile ya wafanyabiashara nakuuliza na wewe(Kichere) halafu na wewe unaangalia mwingine,"amesema Rais Magufuli.

Amesema ameamua kumteua kuwa Katibu Tawala na huko nako akishindwa nako anamuondoa na huo ndio ukweli.

"Niliyekuteau kwenda TRA nenda kafanye kazi, najua watasema wamepita wengi na wewe utapita na kuna watu wako TRA wanajifanya hawagusiki, nenda kawaguse., nchi hii bila kodi haiende,"amesema Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa wanajeshi wanahitaji mshahara na asipowalipa atawakuta pale Ikulu, atawajibu nini. "Kwa hiyo usicheke na mtu, kuna uwezekano usiende mbinguni lakini Watanzania milioni 50 tutakusuma tu uende mbinguni, nenda kakusanye kodi kwa ajili ya Watanzania, bila kodi hakuna nchi.

"Kuna wafanyabishara wazuri sana na ukienda watakupa ushirikiano, kuna wafanyabiashara walikuwa wanafoji na mazingira yalikuwa yanaruhusu kufanya hivyo, kaa nao waulize wanaweza kulipa ngapi. "Kuna watumishi wanafanya mambo ya hivyo na kusema wametumwa kutoka juu, usikubali kuendelea nao wakifanya mambo ya hovyo timua tu, hakuna ubaya kama unao watumishi 1000 halafu 200 ukawatimua kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao,"amesema Rais Magufuli.

Amemwambia Kamishna mpya wa TRA kuwa anajua siku atapoingia kazini watampelekea maua na hata ambao hawastahili kumuita bosi, watamuita bosi.

"Kwanza jana kuna ujumbe nimekutumia wa malalamiko nadhani umeupata au bado? kuna mipaka ambayo inafanya vizuri, Tunduma na Sirali hawafanyi vizuri , wale makamishna wa vituo hivyo fukuza.

"Tena mnaowahamisha wengi mnawapeleka kodi , hawa ambao mtakuwa mnawaondoa peleka kwenye Wizara nyingine huko,wapeni hata umesenja wabebe mafaili na hata ofisi yangu ikiwezekana waleteni tu niwabebeshe mafaili,"amesema.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kihutubua baada ya baada ya kuwaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bw. Charles Kichere na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Edwin Mhede na kushuhudia kupokewa shilingi bilioni 3 kama Fidia ya kila mwezi ya kampuni ya Airtel na dola milioni moja mchango binafsi wa Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumatatu Juni 10, 2019

SPIKA WA BUNGE LA RWANDA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA UMOJA WA WABUNGE WANAWAKE TANZANIA JIJINI DODOMA

$
0
0
 Mwenyekiti umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Margaret Sitta (katikati) akizungumza na ugeni kutoka Bunge la Rwanda pamoja na wajumbe wa umoja huo(wote hawapo kwenye picha)  katika kikao kilichofanyika leo nyumbani kwa Spika Ndugai uzunguni Jijini Dodoma. Kushoto ni Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson

 Mwenyekiti umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Margaret Sitta akizungumza na ugeni kutoka Bunge la Rwanda pamoja na wajumbe wa umoja huo katika kikao kilichofanyika leo nyumbani kwa Spika Ndugai uzunguni Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille na kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
Makamu Mwenyekiti umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Suzan Lyimo, Katibu wa Umoja huo, Mhe. Lolensia Bukwimba wakifuatilia mazungumzo baina yao na ugeni kutoka Bunge la Rwanda uliofanyika leo nyumbani kwa Spika Ndugai uzunguni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MRADI WA MTO RUVU KUTIBU TATIZO LA MAJI SIMANJIRO

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, amesema changamoto ya upungufu wa maji kwa jamii ya wafugaji wa Kata tatu za Orkesumet, Edonyongijape na Langai itapatiwa ufumbuzi Mei mwakani baada ya mradi mkubwa wa maji wa mto Ruvu kukamilika.

Millya aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lormorjoi kwenye ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza kero, changamoto, malalamiko na kuongea na wananchi. 

Alisema mradi huo mkubwa wa maji kutoka mto Ruvu wilayani Same utagharimu kiasi cha sh41.5 bilioni pindi utakapokamilika mwakani.  Alisema tangu dunia iumbwe na Mungu, jamii ya wafugaji haijawahi kupata mradi mkubwa wa maji kama huo utakaokuwa mkombozi kwao.  Alisema anamshukuru Rais John Magufuli kwa kufanikisha mradi huo mkubwa kwani utakuwa msaada wenye kuhitajika mno kwenye jamii hiyo ya wafugaji. 

"Hivi sasa mkandarasi yupo kwenye eneo la mradi akiendelea kufanya kazi yake ili kufanikisha shughuli hiyo ambayo itakamilika mwaka ujao," alisema Ole Millya.  Hata hivyo, kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Celestine Silayo alisema mradi huo utawanufaisha pia wakazi wa pembezoni mwa kata ya Orkesumet kwani walishabainisha kwenye andiko lao. 

Silayo alisema baadhi ya vitongoji vya kata za Langai na Edonyongijape ambavyo havijawekwa kwenye mradi huo vitaingizwa ili navyo viweze kunufaika na mpango huo.  Mkazi wa kijiji cha Lormorjoi, Julius Saitoti alitoa ombi kwa mbunge huyo kuhakikisha mradi huo mkubwa wa maji unapita pia kwenye kijiji chao kwa faida ya jamii na mifugo yao. 

Saitoti alisema jamii ya eneo hilo ina uhitaji mkubwa wa mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa utawanufaisha na wao hivyo wasisahaulike pindi ukikamilika. Mradi huo mkubwa wa maji wa mto Ruvu ukikamilika unatarajia kuwanufaisha zaidi ya watu 50,000 wa kata za Orkesumet, Langai na Edonyongijape, pamoja na mifugo yao. 
  Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara James Ole Millya (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Jackson Sipitieck (aliyevaa shati la kijani) wakati wakikagua majengo ya hospitali ya wilaya hiyo iliyotengewa kiasi cha shilingi bilioni 1.5
Baadhi ya wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakitoa maelezo ya miradi mbalimbali iliyofanyika kwenye kata ya Komolo kwa mbunge wa jimbo hilo James Ole Millya.
Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya akizungumza kwenye mkutano wake na wananchi wa eneo hilo.

MTENDAJI MKUU TEMESA ATEMBELEA NA KUKAGUA KARAKANA MPYA IFAKARA

$
0
0
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto, Mhandisi Jairos Nkoroka (wa tatu kulia) pamoja na wafanyakazi wakikagua propella za vivuko vilivyohifadhiwa katika karakana ya mji wa Ifakara baada ya daraja la mto Kilombero kukamililika. Vivuko hivyo, MV.Kilombero I na II vitaanza kukarabatiwa na kuunganishwa hivi karibuni tayari kwa hatua ya kupelekwa katika eneo la Kikove Malinyi kwa ajili ya kutoa huduma. 
 Mhandisi Jairos Nkoroka kushoto akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle mashine ya kugandamiza vipuri vya magari (press machine) wakati alipotembelea kukagua utendaji kazi wa karakana hiyo mpya ya TEMESA iliyoanza kutoa huduma mwezi Juni mwaka huu katika Halmashauri ya mji wa Ifakara wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Karakana hiyo sasa itahudumia wilaya zote za karibu ikiwemo wilaya ya Ulanga na Malinyi ambazo awali zilikuwa zikitegemea kupata huduma Morogoro mjini.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua mashine ya kupimia uwiano wa matairi ya magari (wheel balance) iliyopo katika karakana ya TEMESA katika Halmashauri ya mji wa Ifakara wakati alipoitembelea kujionea utendaji kazi wake mara baada ya kuanza kutoa huduma Juni mosi mwaka huu. Karakana hiyo sasa itahudumia wilaya zote za karibu ikiwemo wilaya ya Ulanga na Malinyi ambazo awali zilikuwa zikitegemea kupata huduma za matengenezo ya magari na mitambo kutoka Morogoro mjini.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa pili kushoto) akifurahia jambo na wafanyakazi mara baada ya kumaliza kukagua mipaka ya karakana ya TEMESA Ifakara iliyoanza kutoa huduma Juni mosi mwaka huu katika Halmashauri ya mji wa Ifakara wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Karakana hiyo sasa itahudumia wilaya zote za karibu ikiwemo wilaya ya Ulanga na Malinyi ambazo awali zilikuwa zikitegemea kupata huduma za matengenezo ya magari na mitambo kutoka Morogoro mjini.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua kivuko cha MV. Kilombero I kilichohifadhiwa katika karakana ya mji wa Ifakara baada ya daraja la mto Kilombero kukamililika. Kivuko hicho pamoja na kivuko cha MV. Kilombero II vitaanza kukarabatiwa na kuunganishwa hivi karibuni tayari kwa hatua ya kupelekwa katika eneo la Kikove Malinyi kwa ajili ya kutoa huduma.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto akikagua kivuko cha MV Kilombero II ambacho kimehifadhiwa katika karakana hiyo baada ya huduma za kivuko kufungwa katika mto Kilombero kutokana na kukamilika kwa daraja. Kivuko hicho pamoja na kivuko cha MV. Kilombero I vinatarajiwa kuanza kufanyiwa ukarabati tayari kwa hatua ya kupelekwa katika eneo la Kikove Malinyi kwa ajili ya kutoa huduma katika maeneo hayo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa karakana mpya ya TEMESA iliyopo katika Halmashauri ya mji wa Ifakara wilayani Kilombero mara baada ya kumaliza kukagua karakana hiyo.

MAHAKAMA YAAMURU KUKAMATWA KWA WEMA SEPETU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu kumkamatwa  kwa kuruka dhamana.Wema anashtakiwa mahakamani hapo na kesi ya kusambaza  video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.

Mahakama imeto hati hiyo ya kumkamatwa Wema, leo Juni 11,2019  mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonda, baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto kudai kwamba mshtakiwa hayuko mahakamani na hakuwa na taarifa yoyote.

Hata hivyo utetezi uliotokewa na wakili wa Wema, utetezi, Ruben Simwanza, ambae amedai mshtakiwa alifika Mahakamani lakini ameugua ghafla na hivyo ameshindwa kuingia katika chumba cha Mahakama, haukuweza kumsaidia Wema, na hivyo amri ya yeye kukamatwa ikatolewa.

Akitoa uamuzi huo, jakimu Kasonde amesema Mahakama inatoa hati ya kumkamata mshtakiwa kwa sababu kama alifika alishindwa nini kuingia mahakamani.

Katika kesi hiyo, Wema anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono katika mtandao wa kijamii,  kosa analodaiwa kutenda  kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, ambapo anadaiwq kusambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina maudhuil.

RAIS DKT MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA, ASHUHUDIA AIRTEL WAKITOA SHILINGI BILIONI 3 KAMA FIDIA NA DOLA MILIONI MOJA MCHANGO BINAFSI WA MWENYEKITI WA AIRTEL

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akimuapisha Bw. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara  Kichere Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu

Juni 10, 2019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi vitendea kazi baada ya kumuapisha Bw. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara  Kichere Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Juni 10, 2019  

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Edwin Mhede kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Juni 10, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Charles Kichere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Juni 10, 2019


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na waalikwa akishuhudia Jaji mstaafu, Harold Nsekela ambaye ni Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Utumishi wa Umma akiwalisha kiapo
cha Maadili ya Viongozi wa Umma Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bw. Charles Kichere na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Edwin Mhede Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Juni 10, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akipokea mfano wa hundi ya dola milioni moja za Kimarekani toka kwa Mwenyekiti

wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal ukiwa kama mchango wake binafsi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru, Ihumwa, Dodoma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Juni 10, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akipokea mfano wa hundi wa Shilingi Bilioni 3 zikiwa ni Fidia kwa serikali ya

miezi mitatu kwa hesabu ya shilingi bilioni moja kwa kila mwezi ya Kampuni ya Airtel kwa  Serikali  toka kwa Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Juni 10, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal kwa kutoa dola milioni moja kama mchango wake binafsi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru, Ihumwa, Dodoma pamoja na shilingi bilioni tatu za Fidia ya mwezi miezi mitatu kwa hesabu ya shilingi bilioni moja kila mwezi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Juni 10, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal baada ya kuwaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Lugha

Bashungwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bw. Charles Kichere na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Edwin Mhede na kushuhudia kupokewa kwa Fidia ya kila mwezi ya kampuni ya Airtel na mchango binafsi  wa Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Juni 10, 2019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kihutubua baada ya  baada ya kuwaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bw. Charles Kichere na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Edwin Mhede na kushuhudia kupokewa shilingi bilioni 3 kama  Fidia ya kila mwezi ya kampuni ya Airtel na dola milioni moja mchango binafsi  wa Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Juni 10, 2019





Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images