Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli, Wafanyabiashara Wajadili Fursa na Changamoto za Biashara Nchini

$
0
0
Adelina JohnBosco, MAELEZO Dodoma
Rais John Pombe Magufuli amekutana na wawakilishi wa wafanyabiashara nchini leo Ikulu Jijini Dar es salaam ili kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na jinsi ya kuzitatua kwa ajili ya kukuza uchumi kupitia sekta binafsi nchini.
Licha ya jitihada zinazoendelea kuleta uboreshaji katika sekta ya biashara, Rais ametaja uwepo wa changamoto mbalimbali kwa pande wa Serikali na wafanyabiashara wenyewe ambazo zimekuwa ni kikwazo katika kufanya biashara nchini.
Rais Magufuli amebainisha vikwazo vinavyosababishwa na wafanyabiashara kuwa ni pamoja na ukwepaji kodi unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara na vitendo vya rushwa kuwa ni miongoni mwa changamoto zinazozuia uboreshaji wa sekta ya biashara nchini.
Amesema kuna kampuni 17,446 zinakwepa kodi kwa njia ya mauzo hewa ya biashara za ndani na nje, manunuzi hewa kutoka makampuni hewa na kuagiza kampuni hizo kuchunguzwa zaidi na zikithibitika kukwepa kodi zitalazimika kulipa kodi hiyo katika kipindi cha siku 30 kuanzia sasa.
''Baadhi yenu sio waaminifu mnakwepa kodi, mnatoa rushwa na wengine mmekuwa mkifanya kazi za udalali hasa kwenye biashara ya sukari, mafuta ya kula na korosho'' ameeleza Rais Magufuli
Changamoto nyingine kutoka kwa wafanyabiashara ni kuhujumu uchumi kwa kutokuwa wawazi katika mahesabu yao kwa kuwasilisha vielelezo tofauti vya taarifa ya fedha zinazopelekwa benki na TRA.
Aidha, amewaonya wafanyabiashara wanaobadilisha matumizi ya viwanda yaliyokusudiwa awali wakati yakisajiliwa na kuanzisha biashara nyingine pasipo kufuata utaratibu.
Upande wa Serikali, Rais Magufuli amebainisha changamoto mbalimbali ambazo ni kikwazo kwa biashara nchini kuwa ni pamoja na wingi wa taasisi za udhibiti kama vile TRA, OSHA, TBS, TFDA, Ofisi ya Mkemia Mkuuu, Tume ya Ushindani, EWURA, na SUMATRA ambazo husababisha mwingiliano kimajukumu na kutoza tozo mbalimbali zinazofanana hivyo kudhoofisha ukuaji wa biashara nchini.
Ametaja vitendo vya rushwa kwa baadhi ya watumishi wachache  wa Serikali wasio waadilifu kuwa ni miongoni mwa changamoto inayorudisha nyuma jitihada za wafanyabiashara hasa maeneo ya vizuizi barabarani, bandarini, na TRA.
Katika kuhakikisha changamoto hizi zinatatuliwa, Rais amebainisha mikakati ya Serikali iliyoweka ikiwa ni pamoja na kuandaa kitabu cha mwomgozo na kwamba mapendekezo mbalimbali yameanza kutekelezwa kwa lengo la kuboresha mazingira ya biasha nchini.
''Sasa Brela inatumia utaratibu mpya wa kusajili biashara kwa njia ya mtandao, kufuta baadhi ya ada na tozo zilizokuwa zikitozwa na taasisi za OSHA na Zima moto kabla ya kuanzisha biashara,'' amesisitiza Rais Magufuli.
Aidha amezitaka mamlaka husika katika Serikali kuweka mikakati thabiti ya kuwaendeleza wafanyabiashara wadogo na wakati kama ilivyofanyika kwa wafanyabiashara wakubwa.
''Wafanyabiashara wadogo na wakati ndiyo kitovu cha kukuza uchumi katika nchi, hivyo nashauri waendelezwe kama ambavyo tumeshaanza kwa kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo nchini'', alisisitiza Rsi Magufuli.
Kwa upande mwingine, Rais amezionya taasisi za kifedha kutokana na kuwa na mitaji midogo huku zikiweka masharti magumu na kutoza riba kubwa ikiwemo kuendesha shughuli zake zaidi mijini kuliko vijijini.
''Serikali kupitia Benki Kuu imekuwa ikikopa fedha nyingi kwenye taasisi za kimataifa ikiwemo benki ya dunia kwa ajili ya kutoa dhamana na kuwakopesha wajasiriamali wa hapa nchini, lakini sina hakika kama fedha hizo zinawafikia walengwa,'' amehoji Rais Magufuli.
Rais amewaonya mawakala wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) nje ya nchi wanaowasababishia hasara wafanyabiashara kwa kuidhinisha bidhaa ambazo zinagundulika kuwa hazina viwango zinapokaguliwa baada ya kuingizwa nchini.
Aidha ameziagiza mamlaka husika kuangalia uwezekeno wa kuunganisha baadhi ya mifuko inayosimamia sekta ya biashara ili kuiimarisha na kupunguza gharama za uendeshaji huku akizitaka mamlaka zinazosimamia sekta ya biashara ikiwemo wizara, idara, wakala wa Serikali kuhakikisha changamoto hizo zinafanyiwa kazi mara moja ifikapo mwezi Julai mwaka huu, kwa kuzingatia mapendekezo yote yaliyomo katika kitabu cha mwongozo (Blue Print).
Hata hivyo, rais ametoa pongezi kwa wafanyabiashara halali wanaofuata taratibu elekezi ikiwemo kulipa kodi kwa wakati.
Mkutano huu ni mwendelezo wa mikutano inayofanywa na Rais kwa kuyahusisha makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini, wachimbaji wa madini, wazee na watendaji Serikalini lengo likiwa ni kujadiliana na kuweka mikakati itakayosaidia kukua kwa uchumi kwa maslahi ya Taifa.

RAIS DKT.MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WAKUBWA KUTOKA KATIKA WILAYA ZOTE NCHINI PAMOJA NA WAJUMBE WA BARAZA LA BIASHARA LA TAIFA TNBC IKULU

$
0
0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika Kitabu chenye majina na orodha ya Makampuni 17447 ambayo yalisajiliwa BRELA lakini yamekuwa yakifanya udanganyifu na ukwepaji wa kodi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika Flash Disk ambazo zina majina  na orodha ya Makampuni 17447 ambayo yamekuwa yakifanya udanganyifu ikiwemo ukwepaji wa kodi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakati wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC pamoja na Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini wakiwa katika Kikao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya  mbalimbali nchini wakichangia hoja mbalimbali katika Kikao chao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Alipa milioni 5 kukwepa kifungo cha mwaka mmoja jela

$
0
0
 
Na Karama Kenyunko 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuhukumu John Chuwa  mkazi wa Barakuda jijini Dar es Salaam, kulipa faini ya sh. milioni 5 au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada kupatikana na hatia kwa kosa la kuchapisha maudhui katika mtandao wa Youtube bila kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Hukumu hiyo imesomwa leo Juni 7, 2019 katika na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde baada ya mshtakiwa kukiri makosa yake hayo.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kasonde amesema, kwa kuwa mshtakiwa amekiri makosa yake yeye mwenyewe na kwamba hajaisumbua mahakama anatiwa hatiani kwa kosa hilo. Ambapo kabla ya kutoa adhabu, alimtaka mshtakiwa kujitetea, nae akaiomba mahakama isimpe adhabu kali kwani mama yake mzazi na wadogo zake wawili wanamtegemea hivyo akipewa adhabu ya kwenda jela watapata tabu.

Mapema, wakili wa Serikali Elizabeth Mkunde, alimsomea mshtakiwa  maelezo ya awali na kudai mwaka 2018 mshtakiwa alifungua mtandao wa YouTube kwa kutumia barua pepe ya jalifilmstz@gmail.com ambamo alikuwa akitoa matangazo ya filamu za kitanzania kupitia simu yake ya mkononi aina ya Huawei Y9 huku akijua hana kibali kutoka TCRA.

Amedai, mshtakiwa alipokamatwa alikutwa na simu mbili za mkononi Huawei na Nokia.

Baada ya kusomwa kwa maelezo hayo, wakili huyo wa Serikali, Mkunde alidai,  kwa sababu mshtakiwa amekiri makosa yake yeye mwenyewe basi anaiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hizo.

Katika kesi hiyo ilidaiwa kuwa katika terehe tofauti kati ya 2018 na Aprili 2019 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa  alichapisha maudhui kupitia mtandao wa Youtube uitwao John Film Entertainment bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Mshitakiwa huyo aliposomewa shtaka lake Juno 4, 2019  alikiri kutenda kosa hilo na alichiwa kwa dhamana hadi leo alipohukumiwa adhabu hiyo ambapo amefanikiwa kulipa faini hiyo na kuachiwa huru.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 07.06.2019

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO

UKEREWE: Upanuzi Kituo cha afya Bwisya kisiwani Ukara wafikia asilimia 95

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella leo Ijumaa Juni 07, 2019 amekagua maendeleo ya upanuzi na ujenzi wa Kituo cha Afya Bwisya kilichopo wilayani Ukerewe na kulidhishwa na ujenzi wake ambao umefikia asilimia 95 kwa mujibu wa mkandarasi.

Upanuzi wa Kituo hicho kwa hadhi ya Hospitali ni sehemu ya agizo la Rais Dkt. John Pombe Maguli alilolitoa baada ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea Septemba 20, 2018 ambapo alielekeza sehemu ya fedha za rambirambi ya ajali hiyo (Milioni 800) zitumike kufanya shughuli hiyo.

Mongella amesema ukarabati huo ulipaswa kukamilika mwezi Machi mwaka huu lakini umechelewa kutokana na changamoto ya miundombinu ya usafiri kwani baadhi ya vifaa ujenzi vinatoka jijini Mwanza na kusafirisha kwa njia ya maji hivyo matarajioni ni mkandarasi kampuni ya Suma JKT kukamilisha kazi hiyo mwishoni mwa mwezi huu.

Pia amekagua maendeleo ya Shule ya Sekondari Nyamanga iliyopo kisiwani Ukara aliyoiwekea jiwe la msingi la ujenzi Mei 02, 2019 na kuelekeza maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa kukamilika kwa wakati ili kutoa fursa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza walioanza masomo shuleni hapo kuelendelea vyema na masomo yao.

Aidha Mongella amekagua matayarisho ya ujenzi wa uzio, mnara na makaburi ya baadhi ya abiria wa Kivuko cha MV. Nyerere waliozikwa katika malalo ya pamoja eneo la Bwisya kisiwani Ukara na kuelekeza Suma JKT kukamilisha pia shughuli hiyo kwa wakati.

Itakumbukwa kwamba Novemba 17, 2018 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo alizindua rasmi ujenzi wa miundombinu katika Kituo hicho unaofanywa na kampuni ya SUMA JKT chini ya usimamizi wa Kamati Maalum iliyoundwa na Mongella.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiangalia ramani ya upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya kilichopo katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.

Kukamilika kwa upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya, kutaondoa adha kwa wananchi zaidi ya elfu thelathini waliokuwa wakivuka maji kwenda Mjini Ukerewe ama Jijini Mwanza kufuata huduma za afya.

Sehemu ya majengo yaliyojengwa kwenye Kituo cha Afya Bwisya wilayani Ukara. 
Tenki la kuhifadhia maji katika Kituio cha Afya Bwisya.
Majengo yaliyojengwa kwenye Kituo cha Afya Bwisya ni pamoja na nyumba ya mtumishi, maabara, wodi ya wazazi, jengo la upasuaji na jengo la kuhifahia maiti.
Upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya umefikia asilimia 95 ambapo asilimia tano zilizosalia zinatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 17, 2019.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikagua maendeleo ya upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya kilichopo Ukara wilayani Ukerewe.
Sehemu ya madarasa katika Shule ya Sekondari Nyamaga kisiwani Ukara.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hii Mei 02, 2019 na kufufua ujenzi wake ambao ulikuwa unasua sua tangu mwaka 2014.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella pamoja akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali amekagua matayarisho ya ujenzi wa mnara, uzio na makaburi ya baadhi ya abiria waliofariki kwenye ajali ya MV. Nyerere na kuzikwa katika eneo la Bwisya kisiwani Ukara.
Baadhi ya viongozi wa CCM wilayani Ukerewe wakiwaombea ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza majisha kwenye ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kilichokuwa kikitoka Kisiwa cha Bugolora kwenda Kisiwa cha Bwisya.
TAZAMA>>> RC Mongella akagua ujenzi wa Hospitali ya Bwisya wilayani Ukerewe

MBUNGE AZZA HILAL ATOA MSAADA WA KOMPYUTA SHULE YA SEKONDARI SOLWA

$
0
0
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa msaada wa Kompyuta nne zenye thamani ya shilingi milioni 8 katika shule ya Sekondari Solwa iliyopo katika jimbo la Solwa mkoani Shinyanga ili waitumie katika masomo yao kuendana na ulimwengu wa teknolojia.
Kompyuta hizo ni sehemu ya Kompyuta 15 zenye thamani ya shilingi milioni 30 zilizopatikana kutokana na juhudi za Mbunge Azza Hilal Hamad kwa kushirikiana na wadau ambao ni Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) shule mbalimbali mkoani Shinyanga.
Akikabidhi Kompyuta hizo kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe, Jasinta Mboneko leo Juni 7,2019 katika shule ya sekondari Solwa,Mhe. Azza amesema kupitia kompyuta hizo wanafunzi watajifunza teknolojia ya kisasa.
“Nimeleta kompyuta hizi 4  aina ya Dell kwenye shule hii ya Solwa yenye jumla ya wanafunzi 708 kwa sababu nataka na nyinyi muijue kompyuta. Nimeona ni vizuri angalau tukaangalia shule zilizopo pembezoni walau wanafunzi wakapata uelewa wa kompyuta angalau kwa uchache wa hizi nilizopata”,alisema Azza.
“Kilichonisukuma ni kuona shule zetu nyingi za vijijini mwanafunzi hadi anamaliza kidato cha nne hata sura ya Computer haijui, kwa hiyo inakuwa changamoto kubwa pale anatoka shuleni na kuendelea na masomo ya kidato cha tano au chuo Computer inaonekana ni kitu kigeni kabisa kwake”,aliongeza.
Mhe. Azza aliushukuru Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana naye kuhakikisha angalau shule za sekondari mkoani Shinyanga zinapata kompyuta ili watoto waweze kujifunza teknolojia ya kisasa.
“Nawashukuru sana UCSAF kwa kunipatia kompyuta, nitaendelea kuwasumbua naomba msinichoke kwani shule nyingi Shinyanga hazina kompyuta. Niwaombe pia wadau wengine waweze kutusaidia katika mkoa wa Shinyanga ili kuondoa changamoto ya Kompyuta katika shule zetu”,alisema Azza.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko alishukuru mbunge huyo kwa kufanikisha kupatikana kwa kompyuta hizo na kuwataka wanafunzi kutunza na kuzitumia vizuri katika kujifunzia masomo yao.
“Sasa hivi dunia imebadilika imekuwa ya Kidigitali zaidi,tumieni kompyuta hizi kujifunza mambo mazuri,mbali na kujifunzia masomo mnaweza kuzitumia pia kupata taarifa mbalimbali za nchi hii. Nanyi walimu hakikisheni mnawasimamia vizuri wanafunzi hawa”,alisema Mboneko.
Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba alisema shule ya sekondari Solwa imekuwa ya kwanza kwenye halmashauri hiyo kupata kompyuta kupitia mbunge Azza na kubainisha kuwa zitasaidia kuwaandaa wanafunzi katika maisha yao.ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (wa pili kulia) na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko (wa tatu kushoto) wakipokelewa na viongozi mbalimbali wa kata ya Solwa wakati wakiwasili katika shule ya sekondari Solwa kwa ajili ya zoezi la makabidhiano ya Kompyuta leo Juni 7,2019.wa pili kushoto ni diwani wa kata ya Solwa Mhe. Awadhi Aboud.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi kompyuta nne kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa leo.Kushoto  Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza katika shule ya sekondari Solwa wakati akipokea kompyuta zilizopatikana kwa juhudi za mbunge Azza Hilal.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi moja ya kompyuta hizo aina ya Dell kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) wakati wa makabidhiano ya kompyuta hizo kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) na  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) wakifurahia wakati wa kukabidhiana Baobonya ya kompyuta.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa wakiwa wamebeba moja ya kompyuta zilizotolewa na Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa wakiwa wamekaa wakati wa makabidhiano ya kompyuta.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad akiwasisitiza wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa kuzingatia masomo yao na kuacha tamaa ya mapenzi ili waweze kutimiza ndoto zao.
Kaimu Afisa Elimu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Jesse George akimshukuru Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad kwa kuwapatia kompyuta ambazo zitawasaidia wanafunzi katika masomo na maisha yao.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba akizungumza wakati wa makabidhiano ya kompyuta huku akiwataka wanafunzi wa kike kutoa taarifa kwa walimu na viongozi mbalimbali pale wanaume wenye tamaa za mapenzi wanapowasumbua.
Mkuu wa shule ya sekondari Solwa akimshukuru Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad kwa kuwapatia msaada wa kompyuta.
Diwani wa kata ya Solwa Mhe. Awadhi Aboud akimshukuru Mbunge Azza Hilal kwa msaada wa kompyuta kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa huku akielezea misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa na Mbunge huyo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi katika sekta ya elimu na afya.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiwasisitiza wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa kuepuka mimba na ndoa za utotoni.
Kushoto  Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba akifuatiwa na Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko wakifurahia jambo wakati wa makabidhiano ya kompyuta kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad  akiagana na wanafunzi wa shule ya Sekondari Solwa baada ya kuwakabidhi kompyuta nne aina ya Dell ili wazitumie kujifunzia masomo yao.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

HOMA YA DENGUE YAPIGA HODI PWANI,WATU 42 TAYARI WAUGUA-NDIKILO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

UGONJWA wa homa ya dengue ,umeingia mkoani Pwani ambapo hadi sasa wagonjwa 42 wameripotiwa kuugua hivyo kusababisha mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa iliyokumbwa na ugonjwa huo.

Wilaya zilizokumbwa na ugonjwa huo ni pamoja na Mkuranga wagonjwa 35,Rufiji wanne na Kibaha Mji watatu.

Akizungumza,wakati wa  kikao maalum cha kamati ya ulinzi na usalama,kilichoshirikisha kamati ya amani na wadau mbalimbali kujadili juu ya hali hiyo mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,alieleza mgonjwa wa kwanza aligundulika mei 8 mwaka huu.

"Hakuna kifo kilichoripotiwa ,wagonjwa waliougua ni 42,tukizungumzia dengue tusisahau na kuweka mikakati kudhibiti na kipindupindu "

Ndikilo alizitaka kamati za afya wilaya kuupa kipaombele ugonjwa huu na kufanya vikao kujadili suala hili ilihali wananchi wapate taarifa sahihi ya ugonjwa huo ,dalili zake na namna ya kutibiwa.

Aliwaelekeza viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kuwapa elimu waumini wao kuhusu ugonjwa wa homa ya dengue.

Nae Mganga mkuu wa mkoa wa Pwani Gunini Kamba alifafanua ugonjwa huu uliingia mwaka 2014 na kuugua wagonjwa 400 ila kipindi hiki kimezidi kufikia wagonjwa 3,609.

Aliwaasa wananchi ,wakiwa na dalili za homa wakimbilie vituo vya afya kujua hali zao na waachane na imani potofu kukimbilia kwa waganga.

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama,aliwataka wananchi washirikiane na serikali kudhibiti gonjwa hilo ikiwemo kutunza mazingira na kupulizia dawa maeneo ya kutuama maji.

Ugonjwa wa dengue ni ugonjwa unaoenezwa kwa kuumwa na mbu aina ya Aedes mwenye virusi vya ugonjwa huo na dalili zake kuu ni homa kali ya ghafla,kuumwa kichwa sehemu za machoni na maumivu makali ya misuli na viungo vya mwili ,kutapika na uchovu.

KIKAO CHA RAIS DKT.MAGUFULI NA WAFANYABIASHARA WAKUBWA KUTOKA WILAYA ZOTE NCHINI NA WAJUMBE WA BARAZA LA BIASHARA LA TAIFA IKULU KATIKA PICHA

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wakisimama wimbo wa Taifa ulipopigwa mwanzo wa mkutano wake na  Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa Kikao chao na Rais  katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 

.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   akizungumza na Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika kitabu chenye majina na orodha ya Makampuni 17447 ambayo yalisajiliwa BRELA lakini yamekuwa yakifanya udanganyifu na ukwepaji wa kodi wakati  akizungumza na Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha ameshika kitabu chenye majina na orodha ya Makampuni 17447 ambayo yalisajiliwa BRELA lakini yamekuwa yakifanya udanganyifu na ukwepaji wa kodi wakati  akizungumza na Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha flash disk yenye majina na orodha ya Makampuni 17447 ambayo yalisajiliwa BRELA lakini yamekuwa yakifanya udanganyifu na ukwepaji wa kodi wakati  akizungumza na Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 

 Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC wakiwa katika Kikao chao na Rais  katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 

 Mawaziri na Makatibu Wakuu waliohudhuria wakimsikiliza Rais katika kikao hicho katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Mawaziri waliohudhuria wakimsikiliza Rais katika kikao hicho katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC wakiwa katika Kikao chao na Rais  katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 

 Mwenyekiti wa umoja wa mabenki Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa benji ya CRDB Abdulmajid Nsekela akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wafanyabiashara kwenye kikao hicho
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC wakati wa chakula cha mcha alichowaandalia wakati wa mapumziko ya Kikao alichofanya nao  katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika  akibadilishana mawazo na  Kamishna wa Polisi Diwani Athumani Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana
 Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongea wakati wa mkutano huo wa Rais na  Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akiongea wakati wa mkutano huo wa Rais na  Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu orodha ya Makampuni 17447 ambayo yalisajiliwa BRELA lakini yamekuwa yakifanya udanganyifu na ukwepaji wa kodi.

 Viongozi wa Sekta ya Kibenki wakipeana mikono na Rais baada ua kikao chao katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam

 Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika Wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa TNBC wakipeana mikono na Rais baada ua kikao chao katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 

 Mawaziri waliohudhuria wakipeana mikono na Rais baada ua kikao hicho katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Mawaziri waliohudhuria wakipeana mikono na Rais baada ua kikao hicho katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA IKULU

Newz Alert: Rais Dkt Magufuli atengua uteuzi wa Waziri wa Viwanda na Biashara na Kamishna Mkuu wa TRA

MBUNGE AZZA HILAL ATOA MSAADA WA KOMPYUTA SHULE YA SEKONDARI SOLWA

$
0
0

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa msaada wa Kompyuta nne zenye thamani ya shilingi milioni 8 katika shule ya Sekondari Solwa iliyopo katika jimbo la Solwa mkoani Shinyanga ili waitumie katika masomo yao kuendana na ulimwengu wa teknolojia.

Kompyuta hizo ni sehemu ya Kompyuta 15 zenye thamani ya shilingi milioni 30 zilizopatikana kutokana na juhudi za Mbunge Azza Hilal Hamad kwa kushirikiana na wadau ambao ni Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) shule mbalimbali mkoani Shinyanga.Akikabidhi Kompyuta hizo kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe, Jasinta Mboneko leo Juni 7,2019 katika shule ya sekondari Solwa,Mhe. Azza amesema kupitia kompyuta hizo wanafunzi watajifunza teknolojia ya kisasa.

“Nimeleta kompyuta hizi 4 aina ya Dell kwenye shule hii ya Solwa yenye jumla ya wanafunzi 708 kwa sababu nataka na nyinyi muijue kompyuta. Nimeona ni vizuri angalau tukaangalia shule zilizopo pembezoni walau wanafunzi wakapata uelewa wa kompyuta angalau kwa uchache wa hizi nilizopata”,alisema Azza.

“Kilichonisukuma ni kuona shule zetu nyingi za vijijini mwanafunzi hadi anamaliza kidato cha nne hata sura ya Computer haijui, kwa hiyo inakuwa changamoto kubwa pale anatoka shuleni na kuendelea na masomo ya kidato cha tano au chuo Computer inaonekana ni kitu kigeni kabisa kwake”,aliongeza.

Mhe. Azza aliushukuru Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana naye kuhakikisha angalau shule za sekondari mkoani Shinyanga zinapata kompyuta ili watoto waweze kujifunza teknolojia ya kisasa.

“Nawashukuru sana UCSAF kwa kunipatia kompyuta, nitaendelea kuwasumbua naomba msinichoke kwani shule nyingi Shinyanga hazina kompyuta. Niwaombe pia wadau wengine waweze kutusaidia katika mkoa wa Shinyanga ili kuondoa changamoto ya Kompyuta katika shule zetu”,alisema Azza.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko alishukuru mbunge huyo kwa kufanikisha kupatikana kwa kompyuta hizo na kuwataka wanafunzi kutunza na kuzitumia vizuri katika kujifunzia masomo yao.

“Sasa hivi dunia imebadilika imekuwa ya Kidigitali zaidi,tumieni kompyuta hizi kujifunza mambo mazuri,mbali na kujifunzia masomo mnaweza kuzitumia pia kupata taarifa mbalimbali za nchi hii. Nanyi walimu hakikisheni mnawasimamia vizuri wanafunzi hawa”,alisema Mboneko.

Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba alisema shule ya sekondari Solwa imekuwa ya kwanza kwenye halmashauri hiyo kupata kompyuta kupitia mbunge Azza na kubainisha kuwa zitasaidia kuwaandaa wanafunzi katika maisha yao. ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (wa pili kulia) na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko (wa tatu kushoto) wakipokelewa na viongozi mbalimbali wa kata ya Solwa wakati wakiwasili katika shule ya sekondari Solwa kwa ajili ya zoezi la makabidhiano ya Kompyuta leo Juni 7,2019.wa pili kushoto ni diwani wa kata ya Solwa Mhe. Awadhi Aboud.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi kompyuta nne kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa leo.Kushoto Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza katika shule ya sekondari Solwa wakati akipokea kompyuta zilizopatikana kwa juhudi za mbunge Azza Hilal.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi moja ya kompyuta hizo aina ya Dell kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) wakati wa makabidhiano ya kompyuta hizo kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) wakifurahia wakati wa kukabidhiana Baobonya ya kompyuta.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa wakiwa wamebeba moja ya kompyuta zilizotolewa na Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa wakiwa wamekaa wakati wa makabidhiano ya kompyuta.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad akiwasisitiza wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa kuzingatia masomo yao na kuacha tamaa ya mapenzi ili waweze kutimiza ndoto zao.
Kaimu Afisa Elimu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Jesse George akimshukuru Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad kwa kuwapatia kompyuta ambazo zitawasaidia wanafunzi katika masomo na maisha yao.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba akizungumza wakati wa makabidhiano ya kompyuta huku akiwataka wanafunzi wa kike kutoa taarifa kwa walimu na viongozi mbalimbali pale wanaume wenye tamaa za mapenzi wanapowasumbua.
Mkuu wa shule ya sekondari Solwa akimshukuru Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad kwa kuwapatia msaada wa kompyuta.
Diwani wa kata ya Solwa Mhe. Awadhi Aboud akimshukuru Mbunge Azza Hilal kwa msaada wa kompyuta kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa huku akielezea misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa na Mbunge huyo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi katika sekta ya elimu na afya.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiwasisitiza wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa kuepuka mimba na ndoa za utotoni.
Kushoto Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba akifuatiwa na Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko wakifurahia jambo wakati wa makabidhiano ya kompyuta kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad akiagana na wanafunzi wa shule ya Sekondari Solwa baada ya kuwakabidhi kompyuta nne aina ya Dell ili wazitumie kujifunzia masomo yao.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Jarida Toleo Maalum la Wizara ya Madin

HATIMAE WAISLAM WAKABIDHIWA KIWANJA CHAO CHA OMUGAKORONGO - KARAGWE .

$
0
0
 Anaadika Abdullatif Yunus wa Michuzi Tv - Karagwe .

Mgogoro uliofukuta takribani Miaka 30 ukihusisha Waislam wa Wilayani Karagwe Mkoani Kagera, dhidi ya wavamizi 14 waliovamia Eneo la Ardhi ya Waislam hao lililopo Omugakorongo, Kayanga Karagwe umemalizika baada ya Serikali kulikabidhi rasmi eneo hilo kwa Waislam.

Akikabidhi Eneo hilo mnamo June 7, 2019 kwa niaba ya Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka, kwanza amewashukuru wale wote waliowahi kuvamia Eneo hilo na kisha wakajiondoa kwa hiari, pili na kuwataka wale ambao wamebaki kuondoka Mara moja ili Wenye haki ya kumiliki Eneo hilo wafanye mambo yao.

Aidha Mhe. Mheluka akikabidhi Eneo hilo baada ya kulikagua na kujiridhisha, amewataka Waislam kushughulikia upimaji wa eneo lao, akiaahidi kutoa usaidizi wa jambo hilo, na pia kuwataka kuliendeleza kwa shughuli mbalimbali huku akisisitiza kuwa Serikali haipo Tayari kuona eneo kubwa kama hilo likiwa limebaki wazi bila kuliendeleza.

Itakumbukwa kuwa Eneo hilo lenye ukubwa wa Hekali 13, hapo awali Waislam walilipata kutoka Serikali ya kijiji (Abakungu), na kukabidhiwa kwa Taasisi iliyokuwa inasimamia masuala ya kiislam ya East Africa Muslim Welfare Society (EMWAS) Mwaka 1990, ambapo mnamo 1968 Taasisi hiyo ilivunjwa na Kuundwa (BAKWATA) hivyo Mali zote kikiwemo kiwanja hicho zilizokuwa wakakabidhiwa Bakwata.

Pamoja na ucheleweshwaji wa haki hiyo, tayari BAKWATA wameshinda shitaka lao katika mahakama ya Ardhi ya Kata, Wilaya, licha ya mvamizi mmoja kukata rufaa bado pia ameshindwa katika shitaka hilo.
 Pichani Mkuu wa Wilaya Karagwe, Mhe. Mheluka (Mwenye Suti) akiwa na waumini na Sheikh wa (W) Karagwe, wakitembelea na kukagua kiwanja cha Omugakorongo Karagwe ambacho kimekuwa na mgogoro kwa kipindi kirefu.

 Pichani ni eneo ambalo miaka ya 1968 palijengwa msikiti mahala hapa, na kubomolewa na wavamizi, licha mabaki ya vipande vya tofali kusalia sehemu hii.
 Sehemu ya Waumini wa Kiislam Karagwe wakiendelea kuwasikiliza Viongozi kabla ya kukabidhiwa Eneo lao. 
Pichani ni Sheikh wa (W) Karagwe, Nassib Abdul, akitoa Maelezo machache kwa Mkuu wa Wilaya Karagwe Godfrey Mheluka, katika ni Sheikh wa (W) Kyerwa.

TUNDURU WAENDESHA KAMPENI YA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA NGOZI NA UKOMA KWA VIJIJI VYA MPAKANI VINAVYOPAKANA NA MSUMBIJI

$
0
0
 Mmoja ya vingozi wa kijiji cha Mbati akihamasisha wananchi wa kijiji hicho kupima magonjwa ya ngozi na Ukoma kabla ya kuanza uchunguzi wa ugonjwa huo jana ulioongozwa na Mratibu wa kifua kikuu na Ukoma Hospitali ya wilaya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole.
 Baadhi ya wananachi wa kijiji cha Mbati kata ya Mbati wilaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma wakisubiri kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya ngozi na Ukoma wakati wa zoezi la uchunguzi wa magonjwa hayo kwa wananchi wa vijiji vilivyopo mpakani na Nchi jirani ya Msumbiji  kampeni inayoongozwa na Mratibu wa kifua kikuu na Ukoma Hospitali ya wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole.

 Mratibu wa kifua Kikuu Ukoma wa Hospitali ya wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongoleakiongea  wananchi wanaoishi vijiji vilivyopo mpakani mwa Tanzania na Msumbuji hasa baada ya kubainika kuwa wananchi wa maeneo  hayo wameathirika kwa kiwango kikubwa na ukoma.
Mratibu wa kifua Kikuu Ukoma wa Hospitali ya wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole akimchunguza magonjwa ya ngozi  mkazi wa kijiji  cha Mbati wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mohamed Musa wakati wa zoezi la uchunguzi wa magonjwa ya  ngozi na Ukoma kwa wananchi wanaoishi vijiji vilivyopo mpakani mwa Tanzania na Msumbuji hasa baada ya kubainika kuwa wananchi wa maeneo  hayo wameathirika kwa kiwango kikubwa na ukoma.

TCRA YAENDELEA KUJIKITA KUTOA ELIMU ZAIDI YA USAJILI WA LAINI KUTUMIA ALAMA ZA VIDOLE

$
0
0
Wakazi wa Dodoma na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Mkuu wa TCRA Kanda ya Kati  Mhandisi Antonio  Manyanda amesema ni fursa kwa wananchi wa Dodoma kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano. 

Manyanda amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole. 

"TCRA iko karibu na wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema Manyanda.
 Wananchi wakikamilisha usajili wa Laini za Simu kwa Kutumia alama za vidole. Katika Mnada jijini Dodoma.

 Wananchi wakiwa katika Mnada na kupata huduma za mawasiliano katika Mnada huo jijini Dodoma.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Bidhaa za Mawasiliano  Thadayo Ringo akitoa  maelekezo kwa Wananchi wa Dodoma  katika  kampeni ya Mnada kwa Mnada inayoendeshwa na TCRA
 Mwananchi wa Dodoma  akiweka alama za vidole kwa ajili ya laini za simu.
Timu ya TCRA  ikiwa katika picha ya pamoja  katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada  jijini Dodoma.

SHERIA MPYA,HUWEZI TENA KUKOPEA KIWANJA,SHAMBA AMBALO HALIJAENDELEZWA HATA KAMA UNA HATIMILIKI.

$
0
0
Na Bashir Yakub
Wiki iliyopita niliandika kuwa ujenzi wa fensi pekee kwenye kiwanja sio maendelezo halisi kwa mujibu wa kanuni mpya za sheria ya ardhi tofauti na tulivyozoea. Leo tena tunatizama Sehemu ya (iii) kanuni ya 7 ya kanuni mpya kanuni za Sheria ya Ardhi kupitia tangazo la serikali  namba 345 la tarehe 26/ 4 / 2019.
Kanuni ya 7(1) inasema kuwa mwenye kiwanja/shamba ambalo halijaendelezwa au lenye maendelezo hafifu,endapo ataomba mkopo na kuweka rehani ardhi hiyo, atatakiwa ndani ya miezi sita tokea siku alipoweka rehani, apeleke taarifa kwa kamishna wa ardhi kuonesha ni  namna gani pesa yote au sehemu ya pesa alizokopa zimetumika katika kuendeleza ardhi husika.
Kutokana na kanuni hii maana yake ni kuwa ardhi unayokopea inatakiwa kuwa imeendelezwa au kama haijaendelezwa basi kiasi cha pesa unachopata kupitia mkopo lazima kitumike kuendeleza ardhi hiyo uliyotumia kukopea bila kujali umekopa hela ili kuzifanyia nini. Na hii ni kwa ardhi zenye hatimiliki. Mwenye ardhi atatakiwa ndani ya miezi sita  tokea kuweka ardhi yake rehani apeleke taarifa maalum kwa kamishna wa ardhi kuonesha ni namna gani hela yote au sehemu ya hela aliyoipata ilivyotumika kuendeleza ardhi aliyoweka rehani.
MFANO, una kiwanja chenye hatimiliki, lakini hakijaendelezwa(un-developed) au kimeendelezwa lakini maendelezo hafifu(under-development) kama kujenga fensi tu, au kijumba kibovu cha mlinzi nk.Sasa unaomba mkopo benki wa Tsh milioni 50 na rehani yako ni kiwanja hicho. Benki wao watatizama na kuona kuwa kiwanja unachoweka rehani hakijaendelezwa au kina maendelezo hafifu.

                                       KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com

eGA yakabidhi mfumo Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali

$
0
0
 Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Clement  Mashamba akizungumza wakati wa kupokea mfumo wa Kieletroniki kutoka Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) jijini  Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Usimamizi wa Huduma za Tehama wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Injinia Benedict Ndomba akitoa maelezo ya mfumo kwa Wakili Mkuu wa Serikali  wakati wa makabidhiano yaliiyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Ubora na Udhibiti wa Mashauri wa  Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali  Evarist Mashiba akitoa maelezo watavyosimamia mfumo katika utoaji  huduma kwa wadau,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi  wa Usimamizi wa Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama)  wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Injinia Benedict Ndomba akizungumza wakati wa Kukabidhi mfumi kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) umeikabidhi Mfumo wa Kieletroniki Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mfumo katika kutika kurahisisha utoaji wa taarifa kwa wadau wa utoaji haki na Maamuzi katika mashauri mbalimbali.

Akizungumza na waandishi  habari wakati wa makabidhiano hayo   Mkurugenzi wa Usimamizi wa  Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Injinia Benedict Ndomba amesema wametengeneza mfumo huo ili kukidhi mahitaji ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali katika kurahisisha utoaji wa huduma wa Taasisi za Serikali.

Amesema katika awamu ya kwanza imetengenezwa moduli itakayosaidia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali katika kutekeleza majukumu mbalimbali yanayohusiana na majalada ya mashauri na wanauwezo wa kuongeza kutokana na mahitaji ya Ofisi hiyo.

Wakili Mkuu wa Serikali  Dkt.Clement Mashamba amesema mfumo huo umetengenezwa kwa wakati na kuzingatia mahitaji yaliyoainishwa na ofisi yake kwa sasa na kuwa karibu na eGA ili kuendesha kazi kwa ufanisi.

"Mfumo huu kwetu utasaidia kuboresha usimamizi wa mashauri ikiwa ni pamoja na udhibiti ubora wa huduma zinazotolewa na ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali pamoja na kuongeza kasi ya utendaji wa ofisi kwa wadau " amesema Dkt. Mashamba

Mkurugenzi wa usimamizi wa mashauri na udhibiti ubora Evarist Mashiba ameeleza kuwa mfumo huo utasaidia shughuli za upokeaji na usimamizi wa mashauri kutoka mahakamani. 

"Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilikuwa haina mfumo wa kieletroniki kukabidhiwa kwa mfumo huu utawezesha kuharakisha shughuli zote za usimamizi wa mashauri na maamuzi kwa wadau wetu.ameeleza Mashiba.

NIDHAMU YAWAONDOA MKUDE, AJIBU KIKOSI CHA TAIFA STARS YA AFCON 2019

$
0
0
Kocha Mkuu wa TaifaStars Emmanuel Amunike ametaja kikosi chake cha  wachezaji 32 wanaoondoka nchini leo kuelekea Misri kwaajili ya kambi ya wiki mbili kabla ya kutaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kitakachoshiriki AFCON2019 kuanzia Juni 21 mwaka huu.

Katika kikosi hicho Kocha Amunike amewaacha wachezaji saba kutoka kwenye orodha ya wachezaji 39 wa kikosi cha awali kilichotangazwa mapema mwezi Mei akitumia kigezo za nidhamu na kujituma kwao mazoezini.

Wachezaji walioachwa ni Ibrahim Ajibu (Yanga), Jonas Mkude (Simba SC), Ally Ally (KMC), Kennedy Juma (Singida United), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Kassim Khamis (Kagera Sugar) na Shomari Kapombe (Simba SC). Wachezaji 32 wanaoondoka leo ni:

Magolikipa
1. Aishi Manula - Simba SC.
2. Metacha Mnata - Mbao FC.
3. Suleiman Salula - Malindi FC.
4. Aron Kalambo - Tz Prisons.
5. Claryo Boniphace - U20.

Mabeki
6. Hassan Kessy - Nkana FC. 
7. Vicent Philipo - Mbao FC.
8. Gadiel Michael - Yanga SC.
9. Abdi Banda - Baroka FC
10. Ally Mtoni - Lipuli FC.
11. Mohamed Hussein - Simba SC.
12. Agrey Moris - Azam FC
13. Kelvin Yondan - Yanga
14. Erasto Nyoni - Simba SC.
15. David Mwantika - Azam FC.

Viungo wa kati
16. Feisal Salum - Yanga SC.
17. Himid Mao - Petrojet. 
18. Mudathir Yahya - Azam FC.
19. Frank Domayo – Azam FC
20. Fred Tangalu - Lipuli FC.

Viungo wa pembeni
21. Yahya Zayd - Ismailia.
22. Miraji Athuman – Lipuli FC.
23. Farid Musa – Tenerife.
24. Shiza Kichuya – ENPPI.
25. Saimon Msuva – Difaa El Jadidi.

Washambuliaji
26. Shaban Chilunda - Tenerife.
27. Rashid Mandawa – BDF.
28. Mbwana Samatta – KRC Genk.
29. Thomas Ulimwengu – JS Saoura.
30. John Bocco – Simba SC. 
31. Kelvin John – U17.
32. Adi Yusuph – Blackpool.

TAARIFA KWA WAKAZI WA MLANDIZI,KIBAHA NA DAR ES SALAAM WANAOPATA MAJI KUPITIA MTAMBO WA RUVU JUU.

DIWANI MSOPHE ATOA MSAADA WA VYAKULA,SABUNI NA MADAFTARI KWA MAKUNDI YENYE UHITAJI KIPUNGUNI

$
0
0

Na Saidi Mwishehe,Globu ya jamii

DIWANI wa Kata ya Kipunguni iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam Mohammed Msophe ameamua kutoa msaada wa vyakula na sabuni kwa wajane, walemavu ma watoto yatima.

Mbali na kutoa msaada wa vyakula na ,sabuni pia ametoa msaada wa madaftari na kalamu kwa wanafunzi waliopo ndani ya Kata hiyo wanaosoma shule za msingi na sekondari ikiwa ni mkakati wa kuhamasisha elimu na kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya tano chini ya uongozi mhari wa Rais Dk.John Magufuli ambayo imeamua elimu ya msingi na sekondari iwe bure.

Akizungumza leo wakati wa ugawaji msaada huo kwa makundi hayo Diwani Msofe amesema msaada huo umetoka kwa marafiki zake waliotaka kusaidiwa kwa makundi hayo,hivyo yeye amewezesha msaada huo kufika kwa walengwa walioko kwenye kata yake.

"Marafiki zangu ndio walioamua kutoa msaada huu,nami jukumu langu ni kuhakikisha makundi ambayo yanatakiwa kupatiwa msaada huu.Asilimia 95 ya waliopata msaada ni watu wenye walemavu,watoto yatima,wajane na wale wanatoka kwenye familia za wasiojiweza kutokana na sababu mbalimbali.

"Pia tumetoa msaada kwa kugawa madaftari,panseli na kalamu kwa wanafunzi,lengo ni kuhamasisha elimu ndani ya Kata yetu na wakati huo huo kuunga mkono juhudi za Rais wetu mpendwa katika ya sekta ya elimu,kwani tunatambua Serikali ilitangaza elimu bure kwa shule za msingi na sekondari,"amesema Msophe.

Amefafanua matarajio yao ni kusaidia wananchi 3000 waliopo katika Kata hiyo huku akielezea kupitia marafiki zake wamekuwa wakisaidia jamii kwa kutoa msaada ya kijamii na kuahidi kuendelea kufanya hivyo kadri watakavyopata.

Wakati huo huo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa ndani ya Kata hiyo pamoja na mafanikio ,kilio cha wananchi ni sekondari ya Kata kwani wanafunzi wanalazimika kwenda mbali mrefu,hivyo ombi lao ni kujengewa sekondari na tayari eneo limepatikana na kinachohitajika ni fidia.

Pia amesema changamoto nyingine ni kulosekana kwa kituo cha afya cha kata huku akieleza tayari msingi ulishaanza kujengwa ,hivyo Serikali inaweza kuendelea kwa kuanzia hapo."Changamoto kubwa ni kulosekana kwa kituo cha afya cha Kata,tayari tulishaanza kutafuta ufumbuzi kwa kuanza ujenzi wa msingi.Tunaomba Serikali itusaidie."

Diwani Msophe pia amesema kuna changamoto ya barabara ambapo amesema anafahamu mikakati ya Serikali katika kuboresha miundombinu ya barabara,hivyo ombi la wananchi ni kuona barabara yao inakuwepo kwenye mpango wa kuboreshwa.

Kwa upende wa wananchi wa Kata hiyo ikiwemo Mariamu Mwinyimvua na Athanas Michael wamesema wanampongeza Diwani wao kwa kujali na kuthamini makundi yenye uhitaji ambapo kupitia marafiki zake amewezesha kupatikana kwa msaada huo.

Wamesema kikubwa ambacho wanakitamaza wao sio udogo au ukubwa wa msaada ambao wameupata bali wanauona upendo,huruma na unyenyekevu wa Msophe kwa wananchi anawatumikia vila kujali hali zao.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kipunguni wakiwa kwenye foleni ya kwenda kuchukua msaada wa vyakula na sabuni kutoka kwa Diwani wa kata hiyo
 Diwani wa Kata ya Kipunguni Mohammed Msophe akiwaa ameshikana mkono na mmoja ya wakati wa kata hiyo baada ya kumkabidhi msaada wa McHale,maharege na sabuni.Diwani huyo leo America msaada wa vyakula ,madaftari na sabuni kwa wananchi wenye uhitaji maalum wakiwamo walemavu,wajane,yatima na wasiojiweza.
 Mmoja wa wananchi wa Kata ya Kipunguni jijini Dar es Slaam akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa Diwani wa kata hiyo Mohammed Msophe
 Diwani wa Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam akikabidhi msaada wa madaftari na kalamu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walioko ndani hiyo
 Diwani wa Kipunguni Mohammed Msophe akikabidhi msaada wa vyakula na sabuni kwa moja ya wakati wa kazi wa kata hiyo wakati wa utoaji msaada wa vyakula,sabuni na madaftari
Sehemu ya wananchi wa Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam wakiwa nje ya Ofisi za Serikali ya Mtaa wakisubiri kuingia ndani kwenda kuchukua msaada wa vyakula kutoka kwa Diwani wao Mohammed Msophe
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Latest Images