Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

TANGAZO LA KIFO CHA JANE SAMATTA

$
0
0
Mheshimiwa Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta anasikitika kutangaza kifo cha mtoto wake mpendwa Jane Samatta kilichotokea tarehe 09/12/2013 katika Hospital ya TMJ. 
Mazishi yatafanyika Alhamisi tarehe 12/12/2013 saa 10 Alasiri katika Makaburi ya Kinondoni.

 Ikitanguliwa na Misa itayofanyika katika kanisa la Anglican St. Albano.

Bwana alitoa Bwana ametwaa. 
Jina la Bwana lihimidiwe.


Amina.


Article 5

Wahamiaji haramu 56 wakamatwa mkoani Kilimanjaro

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

WAHAMIAJI haramu 56, Raia wa nchini Ethiopia, wamekamatwa katika Kijiji cha Jiungeni, Kata ya Ruvu, wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Ofisini Kwake, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alisema Wahabeshi hao walikamatwa majira ya saa sita usiku, usiku wa kuamkia Juzi, wakiwa katika Lori aina ya Fuso, yenye namba za usajili, T188 AYU, mali ya kampuni ya E.Lyimo ya Mjini Moshi.

Kamanda Boaz alisema baada ya kupata taarifa ya uwepo wa watu wanaotiliwa mashaka kijijini hapo, polisi walianza kufuatilia na kuwahi Gari hilo likiwa na Wahamiaji hao ambao hata hivyo bado haijafahamika walikuwa wakielekea wapi.

“Polisi waliwahi baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi na kukamata wahabeshi 56, walikuwa wanasafirishwa kwenye Lori aina ya Fuso, namba za usajili T188 AYU mali ya E.Lyimo ya mjini Moshi, bado hatujafahamu walikuwa wanaelekea wapi lakini uchunguzi unaendelea,” alisema Boaz.

Kamanda Boaz alisema mbali na Wahabeshi hao 56, Polisi walifanikiwa kuwakamata Watanzania Watatu akiwemo Dereva wa Lori hilo, aliyetambulika kwa jina la Daniel Mfinanga pamoja na wenzake wawili ambao majina yao yanahifadhiwa kutokana na sababu za kiupelelezi.

Aidha Kamanda Boaz aliongeza kuwa Utingo wa Lori hilo, aliyemtaja kwa jina la Ismael Juma, alifanikiwa kutoroka na kwamba jeshi hilo kwa sasa linaendelea na msako ili kumtia mbaroni.
Kundi la wahamiaji haramu zaidi ya 40 wanaodhaniwa kuwa ni wa kutoka Ethiopia na Somalia wakishuka kwenye Lori aina ya fuso katika kituo kikuu cha muda baada ya kukamatwa wilayani Same wakijiandaa kusafirishwa kwenda nchi ya Afrika kusini.
Wahamiaji haramu wakiwa katika ofisi za kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro muda mfupi baada ya kufikishwa wakitokea wilayani Same ambako walikutwa wakijiandaa kutaka kusafirishwa kwenda Afrika kusini.
Gari aina ya Fuso lililokutwa likiwa limebeba wahamiaji haramu tayari kuwasafirisha kwenda Afrika kusini.

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANZANIA BARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam, jana usiku wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru, alipomwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika kuhitimisha sherehe hizo. Kushoto kwake ni Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein na mkewe Bi Mwanamwema Shein.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam, jana usiku wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru, alipomwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika kuhitimisha sherehe hizo. Kushoto kwake ni Rais wa Zanzibar, Dkt. 
Mohamed Ali Shein na mkewe Bi Mwanamwema Shein.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Shein, wakifurahia burudani ya ngoma za asili iliyokuwa ikiendelea jukwaani wakati wa hitimisho la sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal na (kulia) ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Bi Mwanamwema Shein.
 Wasanii wa ngoma ya asili ya Kabila la Wahaya 'Kakau Band', wakitoa burudani jukwaani wakati wa sherehe hizo zilizohitimishwa kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha ngoma za asili kutoka mkoa wa Katavi, kikitoa burudani jukwaani wakati wa sherehe hizo zilizohitimishwa kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Confirmation of foreign Heads of State and Government attending activities relating to Former President Mandela's passing

Article 1

LIVE: IBADA KUU (MEMORIAL SERVICES) YA MZEE NELSON R. MANDELA HIVI SASA UWANJA WA FNB STADIUM JOHANNESBURG

TAMASHA LA UJASIRIAMALI KURINDIMA MWANZA IJUMAA HADI JUMAPILI

$
0
0
MENEJA Mkuu wa kampuni ya Global Publishers Ltd, ambaye pia ni mratibu mkuu wa Tamasha la Ujasiriamali linalotarajiwa kufanyika Ijumaa hii hadi Jumapili jijini Mwanza, Abdallah Mrisho, leo ameongea na baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini na kuwaleleza kuhusu tamasha litakalofanyika siku ya Ijumaa katika Viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo mikakati yote imekamilika.

Mrisho alisema tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Benki ya NMB na Street University, limeandaliwa kuwawezesha vijana na wakazi wa Jiji la Mwanza kutambua mbinu mbalimbali za kujikwamua kimaisha. Watoa mada watakuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric James Shigongo, James Mwang’amba, Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) na Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

Kwa upande wa burudani kutakuwa na wasanii Fid Q, H. Baba, Young Killer, Jitta Man na Sugu. Pia kutakuwa na wasanii wa muziki wa Injili ambao ni Martha Mwaipaja atakayeimba sambamba na Masanja Makandamizaji na Edson Mwasabwite.
Mratibu wa Tamasha la Ujasiriamali, Abdallah Mrisho (wa pili kulia) akiongea jambo na waandishi wa habari leo ndani ya ukumbi wa The Atriums Hotel iliyoko Sinza, Afrika Sana jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha (wa pili kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni mratibu wa tamasha hilo, Abdallah Mrisho na kushoto ni H. Baba.


FM Academia kuzindua albam mpya Dec 21, Mashujaa kupamba

$
0
0
BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica 'Wazee wa Kibega' inatarajia kupamba uzinduzi wa albamu ya 'Chuki ya Nini' ya bendi ya FM Academia utakaofanyika Desemba 21 mwaka huu jijini Dar es Salaam. 

Hayo yalisemwa jana Rais wa bendi hiyo, Nyoshi El-Saadat alipokuwa akizungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi huo aliodai kuwa utakuwa wa kishindo. 

"Hii ni albamu yetu ya kumi ambayo imeandaliwa kwa ubora wa kimataifa na sasa iko tayari kuzinduliwa Desemba 21 tukisindikizwa na bendi ya Mashujaa Musica," alisema Nyoshi. Nyoshi alitaja nyimbo za albamu hiyo kuwa ni 'Fataki', 'Otilia', 'Ndoa ya Kisasa', 'Neema', 'Dai Chako Ulaumiwe', 'Maisha', 'Madudu', 'Miraessa' na 'Intro' ambazo zote zimeshaingizwa kwenye video. 

Aliongeza kusema kuwa katika uzinduzi huo watawakumbuka pia kwa kuwaombea watu wawili maarufu waliofariki dunia ambao ni Rais wa zamani wa Afrika Kusini mzee Nelson Mandela na mwanamuziki mkongwe wa Kongo, Tabu Ley. Bendi ya FM Academia ilizindua albamu ya kwanza ya 'Hadija' mwaka 1998 kisha ikafuatia ya pili iitwayo 'Atomic' iliyozinduliwa mwaka 1999 na baadaye mwaka uliofuata wa 2000 bendi hiyo ilizindua albamu ya tatu iliyopewa jina la 'Prison'.

 'Wazee wa Ngwasuma' hawakuishia hapo, mwaka 2001 walizindua albamu ya nne iitwayo Freedom na kufuatiwa na ya tano ya 'Mpambe Nuksi' iliyozinduliwa mwaka 2001 na kisha ikafuata ya sita iitwayo 'Dotnata' mwaka 2003 kabla ya 'Dunia Kigeugeu' iliyozinduliwa mwaka 2006. 

Baada ya hapo bendi hiyo ilikaa kidogo hadi mwaka 2010 ilipozindua albamu mbili kwa mpigo ambazo ni 'Vuta Nikuvute' na 'Heshima kwa Wanawake' na sasa mwaka huu wa 2013 unaumalizia kwa kuzindua albamu ya 'Chuki ya Nini'.

GERMANY CONTRIBUTES 24 MILLION EUROS TO EAC TO SUPPORT MEDIA RELATIONS AND WATER SECTOR DEVELOPMENT

$
0
0
The Federal Republic of Germany today announced a new commitment to the East African Community (EAC) in order to support higher education and training for future journalists and media professionals.

Germany makes available a financial contribution of 14 million Euros in support of the Graduate School of Media and Communications (GSMC) of the Aga Khan University, a recently established Centre of Excellence for media education in East Africa.

The education and training programmes of the GSMC will have a strong regional focus and will foster a diverse array of media leaders, enterprises and institutions that will be distinguished by high standards of competence, ethics, professionalism and social responsibility. The GSMC will closely cooperate with the Deutsche Welle Akademie (DWA), which is the media development division of Germany’s well known international broadcaster Deutsche Welle (DW).

Furthermore, the Federal Republic of Germany announced a new commitment to the East African Community in the water and sanitation sector. The EAC and Germany believe that coordinated trans boundary investment approaches are needed to cope with the growing demand for safe water, to fight increasing pollution of water systems and to deal with climate-related challenges.

In this regard, Germany committed a first tranche of 10 million Euros to the ‘Trans boundary Water Supply and Sanitation Programme’ in order to contribute to improved water and sanitation infrastructure in selected EAC border towns. The programme will be implemented with the Lake Victoria Basin Organisation (LVBC) of the EAC as Project Executing Agency.

The commitments were announced by a high-ranking German delegation, led by Ralf-Matthias Mohs, Head of Division East Africa, Federal Ministry for Development Cooperation, including Hans Koeppel, Chargé d´Affaires at the German Embassy Dar es salaam, Lena Thiede, Head of Cooperation EAC at the German Embassy Dar es salaam, as well as Burkhard Hinz, Regional Manager West and East Africa, KfW Development Bank.

Speaking at the ceremony Secretary General of East African Community Amb. Dr. Richard Sezibera said today’s  signing  demonstrates the strong partnership between the EAC and the Federal Republic of Germany. He applauded Germany for its commitment and consistent support  towards EAC Project and Programes. 

Amb Sezibera affirmed EAC’s readiness to continue close cooperation with the Federal Republic of Germany.

Hans Koeppel, Chargé d´Affaires at the German Embassy in Tanzania, said: “The new commitments underline that Germany continues to be a strong partner for the EAC, contributing to an integration process that puts the people in the centre”.

Since as early as 1998, Germany’s development cooperation, on behalf of the German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ), contributes to the capacity development of the Secretariat of the EAC and the regional integration in East Africa through a variety of programmes and projects. Germany’s funding for Technical and Financial Cooperation with the EAC amounts to a total of 125.9 million Euros. Germany also provides substantial support for the water and governance sectors in selected EAC member states.

NHIF kuendelea kuelimisha Umma namna ya kujikinga na Maradhi

$
0
0
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tanga Bi. Monica Kalani akitoa nasaha kwa washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa vipindi vya elimu kwa umma yaliyoendeshwa na TBC kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akitoa maelezo ya awali wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Huduma za Radio katika Shirika la Utangazaji Tanzania Suzan Mungy akielezea namna mafunzo yalivyoendeshwa kwa washiriki hao.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya ufungaji wa mafunzo hayo.
Mmoja wa washiriki kutoka kitengo cha Damu Salama Bw. Rajab Mwenda kipokea cheti cha kushiriki mafunzo ya uaandaji wa vipindi vya elimu kwa umma.

IN LOVING MEMORY

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

warsha ya asasi za kiraia na wanahabari kuhusu mazingira yafunguliwa leo mkoani Tanga

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Tanga Bi. Halima Dendego, akifungua warsha ya asasi za kiraia na wanahabari kuhusu mazingira inayoendelea mkoani Tanga kati ya tarehe11-12 Desemba 2013.Warsha hiyo imeandaliwa na WWF-Tanzania.
Meneja Uhifadhi wa mazingira wa WWF-Tanzania,Gerald Kamwenda akitoa mada katika warsha ya asasi za kiraia na wanahabari inayoendelea mkoani Tanga
Wadau wakisikilza mada katika warsha ya asasi za kiraia na wanahabari kuhusu mazingira inayoendelea mjini Tanga.
Washiriki wa warsha ya asasi za kiraia na wanahabari kuhusu mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Tanga Bi. Halima Dendego.

JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA LAKAMATA BANGI KETE 650, GRAMU 600 ZA MBEGU, GRAMU 350 ZA BANGI NA GOBOLE MOJA

$
0
0
Na: Sylvester Onesmo 
wa Jeshi la Polisi Dodoma
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JOYCE EMMANUEL maarufu kwa jina la SIIJIA mwenye umri wa miaka 33,  mkaazi wa Kijiji cha Godegode Wilayani Mpwapwa akiwa anajishughulisha na biashara haramu na kukamatwa na kete 650 za bangi, mbegu za bangi gm 600, bangi ambayo haijafungwa gm 350 na pombe ya moshi lita 2 na nusu. 
 Akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwakwe Kaimu Kamanda Mkoa wa Dodoma ACP – SUZAN S. KAGANDA amesema uchunguzi wa awali unaonyesha mtuhumiwa huwa anasafirisha bidhaa hizo kutoka Wilayani Mpwapwa mpaka Mkoa jirani wa Morogoro ambako ndiko anauza biashara hiyo.Amesema  mtuhumiwa atapelekwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. 
 Kamanda KAGANDA amesema Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoani humo limefanya msako tarehe 10/12/2013 katika kijiji cha Isinghu Tarafa ya Mpwapwa Mjini Wilaya ya Mpwapwa katika nyumba ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la ZAMOYONI S/O MANYELEZI mwenye umri wa miaka 26, mgogo, mkulima, mkazi wa Kijiji cha Isinghu na kufanikiwa kukamata bunduki aina ya Gobole lisilokuwa na namba alilokuwa akimiliki kinyume cha sheria.  Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili mara baada ya upelelezi kukamilika. 
 Aidha Kamanda KAGANDA amesema katika msako unaoendeshwa na Jeshi la Polisi huko eneo la Kiboriani Wilayani Mpwapwa amekamatwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la GOSTON MGIRE mwenye miaka 28, mkulima, mmasai akiwa anajishughulisha na kilimo cha bangi. Polisi walifanya upekuzi shambani humo na kukuta shamba la ukubwa wa robo heka likiwa limelimwa bangi na kuliharibu. Mtuhumiwa ambaye ni mmiliki wa shamba hilo anashikiliwa na Jeshi la Polisi na atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika.
 Msako unaendelea kufanyika maeneo mbalimbali hasa wakati huu wa kuelekea mwisho wa mwaka na sikukuu ya X-Mass. 
 Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi na jamii kwa ushirikiano wa kutupatia taarifa zinazofanikisha kukamatwa wahalifu. Tunatoa rai kwa wakazi wa Mjini Dodoma kuwa waangalifu na kuzingatia utii wa sheria bila shuruti, hususani katika kipindi hiki kuelekea sikukuu na mwaka mpya.
Kamanda Kaganda akionesha kwa wanahabari gobole lililokamatwa Mpwapwa
Juu na chini Kamanda Kaganda akionesha shehena ya bangi na mbegu za zao hilo haramu zilizokamatwa

Sehemu ya shehena ya bangi na mbegu za zao hilo haramu

Restless Development ICS to host second career fair at the IFM in Dar Es Salam on December 14, 2013

$
0
0
Restless Development is a development agency which works in 8 different countries, including 6 in Africa. Their head office is based in London, UK. · The ICS programme is a volunteer scheme for 18-25 year olds and is funded through the UK Government’s Department for International Development (DFID), which brings together volunteers from Tanzania and the UK to work together to the tackle the pressing problem of graduate unemployment · The ICS programme was designed to focus on graduate unemployment throughout Dar Es Salam after research conducted at the start of 2013 revealed that young people within Tanzania lack information regarding the core soft skills employers look for in their employees.

Restless Development Tanzania will be hosting a career fair at Institute of Financial Management University in Posta on the 14thDecember from 10am-3pm. The event, which will be open to all university students throughout Dar Es Salam, is run as part of Restless Development’s International Citizen Service scheme (ICS), a programme which focuses on tackling the pressing problem of graduate unemployment throughout the city by delivering peer to peer employability skills sessions in universities. These workshops cover a wide range of topics including the core skills employers look for, advice regarding CV writing, and how to become self-employed. The response to these sessions has been overwhelmingly positive with a consistent rate of attendance, reaching over 500 students across the six universities Restless Development currently works in.
The aim of the careers fair will be to offer upcoming university graduates the chance to discuss first hand with potential future employers what they look for in an employee, along with offering students the chance to learn more about what opportunities might be open to them after they graduate. In addition, the event will be a good opening for employers to network with upcoming graduates and see what they could potentially bring to the company in the future.

The companies who have so far confirmed to attend the event include: Airtel, Quality Group, Learn IT and VSO.

This will be the second career fair organised as part of the Restless Development ICS scheme. The first, which took place in July 2013 at the British Council in Posta, had 12 businesses in attendance and over 250 students.




·       

Toyota Grand Hiace luxury inauzwa

$
0
0
  2000 Toyota Grand Hiace Luxury iko oda kabisa inauzwa bei nzuri tu. Mwenye kuitaka  na hakuna madalali Call:



Yaliyowasilishwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo kwenye kongamano la rasilimali na madini lililofanyika chuo kikuu cha Dar es salaam

Remembering Mandela's "Long Walk to Freedom" at the White House

KIJIWE CHA UGHAIBUNI

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images