Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

ngoma azipendazo ankal

0
0
Don Williams anakupa Some Broken Hearts Never Mend

miondoko ya kumeremeta kwenye mnuso

MPANGO WA KUCHANGIA ELIMU MAALUM K'NDONI WAZINDULIWA JIJINI DAR

0
0
Meya wa  wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akionyesha simu za mkononi zitakazo tumika kuchangisha fedha kwa ajili ya   Mpango maalumu wa kuchangia wanafunzi wenye ulemavu katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam baada ya kuuzindua rasmi. Mitandao ya simu itakayotumika  ni M-Pesa namba 0768727314 na Tigo Pesa namba 0712200022.


 Wanafunzi wenye Ulemavu wa kusikia(viziwi)pamoja na walimu wao wakiimba wimbo wa Taifa kwa kutumia lugha ya alama wakati wa uzinduzi Mpango  maalumu wa kuchangia wanafunzi wenye ulemavu katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam. Mitandao ya simu itakayotumika  ni M-Pesa namba 0768727314 na Tigo Pesa namba

 Meya wa  wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akizungumza kwenye uzinduzi  Mpango maalumu wa kuchangia wanafunzi wenye ulemavu katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Elimu Manispaa ya hiyo, Hussein Ramadhani na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo aliye mwakilisha Mkurugenzi…. Mitandao ya simu itakayotumika  ni M-Pesa namba 0768727314 na Tigo Pesa namba

 Mwenyekiti wa Vitengo vya Elimu Maalum katika Manispaa ya Kinondoni,Lessly Nyambo akizungumza kwenye uzinduzi  Mpango Maalumu wa kuchangia wanafunzi wenye ulemavu katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam.

mshabiki wa manchaster united ajiua baada ya timu yake kufungwa 1-0 na newcastle jumamosi

0
0

An absolutely mind-blowingly, insane story has broken out from Kenya as a Manchester United fan committed suicide on Saturday after watching the Red Devils lose 1-0 at home to Newcastle. 
Local police have reported that John Jimmy Macharia, aged 23, jumped to his death from the 7th floor of a building after seeing David Moyes’s team lose at home to the Magpies. 
 According to Nairobi County police chief Benson Kibue, Mr. Macharia told his friends he could not stand and watch the team get beaten twice in a row before he jumped to his death. 
 Police chief Benson Kibue told the media: All witness accounts suggest he committed suicide because the team lost but officers are still talking to those who were with him as part of the investigations into the incident.
 It is not the first time we are losing a young man because of the football in England, which is far away from us. They need to know that is just a game.
 A news report into the suicide of a Kenyan Manchester United fan can be seen below.

Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga atoa mkono wa pole kwa Balozi wa Afrika Kusini nchini Comoro

0
0
Balozi wa Tanzania katika Visiwa vya Comoro Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga na Mkewe Bi. Irene J. Mabiba wakisaini kitabu cha maombolezi   katika Ubalozi wa Afrika Kusini mjini Moroni leo walipokwenda kutoa pole kwa msiba huo

Sherehe za Uhuru kwa Pamoja Tanzania na Kenya Jumamosi jijini Northampton Uingereza

TAMASHA KUBWA LA UJASIRIAMALI KUFANYIKA CCM KIRUMBA, MWANZA DESEMBA 13-15, 2013

Wadau wa Beijing wawatakia Watanzania wote Heri ya Uhuru day

0
0
 Balozi wa Tanzania nchini China Mhe Abdulrahman Shimbo akizungumza na wanafunzi pamoja na wanajumuiya ya Watanzania walio Beijing na Tianjin walipojumuika katika ubalozi wa Tanzania jijini Beijing kwa sherehe hizo
 Jumuiya ya Wanafunzi wa Beijing na Tianjin wakizungumza  na Balozi Abdulrahman Shimbo katika ubalozi wa Tanzania jijini Beijing walipokutanika  Kusheherekea sikukuu ya Uhuru maarufu kama 9 Desemba.

Wasaka Nondozzz huko Beijing, China, Kutoka kushoto ni  wadau Liberata Rushaigo, Fatuma Matulanga, Suleima Serera, Moses Mwangende na Khamis Said. 

HYUNDAI East Africa Sales Manager Alen Nkya gets pat on the back for supporting local road contractors

0
0
HYUNDAI East Africa Sales Manager, Alen Nkya (left) congratulated by Chairman of Tanzania Roads Association (TARA) Eng. Abdul Awadh by supporting local road contractors by offering quality and affordable Road Construction Equipment during Annual Roads Convention over the weekend at the Karimjee Grounds in Dar es Salaam.

balozi seif ali iddi atoa pole kwa msiba wa mzee mandela, aelekea Afrika kusini msibani

0
0
Na Othman Khamis Ame
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka Nchini leo jioni kuelekea Johannesburg Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuhudhuria sala Maalum ya pamoja ya kuuaga mwili wa Kiongozi mashuhuri Duniani Rais Mstaafu wa nchi hiyo Mzee Nelson Mandela. 
Sala hiyo maalum inayotarajiwa kufanyika kesho kwenye uwanja maarufu wa FNB nchini Afrika Kusini inatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi kutoka zaidi ya nchi sabini Ulimwenguni. 
Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam Balozi Seif aliagwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Nd. Abdullrahman Kinana pamoja na baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na Serikali zote mbili za SMT na SMZ. 
Balozi Seif aliyefuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein ni miongoni mwa Ujumbe wa Tanzania utaoshiriki tukio hilo ukiongozwa na Rais wa Jamuhuri yaMuungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar anatarajiwa kurejea Zanzibar kesho kutwa jioni ya Tarehe 11 mwezi Novemba mwaka 2013. Marehemu Mzee Nelson Madela anayetarajiwa kuzikwa Jumapili ijayo alikuwa Kiongozi shupavu wa Afrika Kusini aliyesimama imara kuongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi uliokuwa ukiendeshwa na Makaburu waliyokuwa wakiitawala nchi hiyo. 
Harakati hizo za Mzee Mandela zilipata nguvu kutokana na msaada wa baadhi ya viongozi kadhaa Barani Afrika, ikiwemo Tanzania, ambazo hatimaye Makaburu hao wakaamua kumfungulia mashtaka na kufungwa jela kwa takriban miaka 27 katika Kisiwa cha Robben ambacho sasa kimekuwa sehemu kubwa ya Utalii Nchini Afrika Kusini. 
Kiongozi huyu ambae ni wa aina yake hapa Duniani alisimama imara kudai haki za watu weusi waliokuwa wakinyanyaswa na kukandamizwa kwa sababu tu ya rangi yao. 
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akitia saini kitabu cha maombolezo ya Kifo cha Mpigania Uhuru wa Afrika kusini Rais wa Kwanza wa Taifa hilo Mzee Nelson Mandela hapo katika Ubalozi wa Nchini Mtaa wa Masaki Jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpa pole Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini Tanzania Mhe. Thanduyise Chiliza kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Katibu Mkuu wa CCM Nd. Abdullrahman Kinana akimshindikiza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julus Nyerere Jijini Dar es salaam akielekea Nchini Afrika Kusini kuhudhuria sala maalumu ya  kuaga mwili wa Kiongozi mashuhuri Duniani Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhani Madabida
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na Katibu Mkuu wa CCM Nd. Abdullrahmana Kinana tayari kupanda ndege kuelekea Nchini Afrika Kusini.Nyuma yake Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi. Picha na Hassan Issa wa OMPR,  ZNZ.

Article 16

OFA KABAMBE YA XMAS NA MWAKA MPYA, KWENDA KUTALII MANYARA NA NGORONGORO, NA KUPUMZIKA KATIKA HOTELI YA KITALII GANAKO LUXURY LODGE

0
0




Tel: +255 22 2125141/2
Mobile: +255 753/655 007284, +255 784 290710, +255 754 288483
Fax: +255 22 2125145
Email: info@ganakoluxurylodge.com
Website: www.ganakoluxurylodge.com

MKURUGENZI MKUU WA PSPF NA MSAFARA WAKE WAUZA SERA ZA MFUKO HUO DMV

0
0
Mkurugenzi mkuu wa PSPF Bwn. Adam Mayingu akiuza sera za PSPF alipokutana na wanaDMV Jumapili Dec 8, 2013. Pamoja na kuanguka kwa theluji DMV Watanzania walijitahidi kutokea kwenye mkutano huo na baada ya mkurugenzi mkuu kumaliza kumwaga sera kulikua na kipindi cha maswali na majibu. Skiliza sera za PSPF hapa chini kama zilivyoelezwa na Mkurugenzi Mkuu huyo.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Iddi Sandaly akitambulisha viongozi wenzake kwa PSPF na kuutambulisha msafara mzima wa PSPF kwa wanaDMV.
Meneja wa mawasiliano, masoko na uenezi wa PSPF Bi. Costantina Martin akifafanua moja ya swali lililoulizwa na mmoja ya Watanzania wa DMV waliofika kwenye mkutano huo.
Meza kuu kutoka kushoto ni Grace Mgaza ambaye ni mjumbe wa bodi ya udhamini  wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Meneja mawasiliano, masoko na uenezi wa PSPF Bi. Costantina Martin, Rais wa Jumuiya DMV, Iddi Sandaly, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bwn. Adam Mayingu, Kaimu deski la Diaspora Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Bi.Rosemery Jairo na Mama Kimolo.
Mwakilishi wa PSPF mlimbwende wa kimataifa Flaviana Matata (kushoto) akifuatilia mkutano huo wengine katika picha ni Magie na DMK.
Juu na chini ni Watanzania wa DMV waliohudhuria mkutano huo.

RAIS KIKWETE AWASILI AFRIKA KUSINI KUHUDHURIA MAZIKO YA MZEE NELSON MADELA

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Afrika Kusini usiku wa kuamkia leo  Desemba 10, 2013 tayari kuhudhuria maziko ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serilai, Ibada Kuu ya kumwombea Marehemu itafanyika leo Desemba 10, 2013 katika Uwanja wa FNB Johannesburg, ambapo viongozi na watu mashuhuri mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wataungana na wananchi wa Afrika Kusini katika shughuli hiyo ya kihistoria. 
Kesho Novemba 11 hadi Novemba 13, 2013 mwili wa marehemu utakuwepo katika jengo la Union Building ambapo viongozi na watu mashuhuri watatoa heshima zao za mwisho. Jengo hilo ni kama Ikulu ya nchi hiyo.
Maziko yatafanyika Desemba 15, 2013 katika kijiji cha Qunu, Mthatha, Easter Cape
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria alikowasili usiku wa kuamkia leo tayari kuhudhuria mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
Rais Kikwete akisalimiana na Mwambata wa Kijeshi katika Ubalozi wa Tanzania Afrika kusini katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake mwenye ushungi kichwani ni Mama Salma Kikwete
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahman Kinana. PICHA NA IKULU

ngoma azipendazo ankal

0
0
Ngoma ya 'Muziki Gani' wa Nay Wa Witego Ft Diamond Platnumz ni noma!

miondoko ya kumeremeta kwenye mnuso

AUDIO YA MAZUNGUMUZO YA MHE. JANUARY MAKAMBA NA WANADMV

0
0
Mhe. January Makamba akiongea na wanaDMV siku ya Jumapili kwenye ukumbi wa Mirage uliopo Langley Park, Maryland Sikiliza maongezi hayo hapo chini yalivyokua  maswali na majibu

Mdau Saidi Yakubu alipolamba Nondoz ya Uwakili na kuzawadiwa tuzo maalum ya kuwa mfano bora kwa Diaspora

0
0
Meya wa London,Haruna Mbeyu akimpongeza Wakili Saidi Yakubu mara baada ya sherehe za kuwaapisha.Wengine pichani ni wana diaspora waliojitokeza kumpongeza kwa kuapishwa kuwa wakili.
Mdau wa Watanzania waishio nchini Uingereza,Bi Mariam Mungula akielezea tuzo ya "Award of Recognition" waliyompa Wakili Saidi Yakubu ambae amekuwa ni miongoni mwa wadau wanaosukuma gurudumu la maendeleo ya Diaspora.Tuzo hiyo inayosomeka "Award of Recognition,Presented to Mr Saidi Othman Yakubu,Advocate and Private Secretary to the Deputy Speaker,Parliament of Tanzania for his Outstanding Contribution and Being a Role Model to Tanzanians in Diaspora" imetolewa na taasisi ya East Africa Education Foundation - UK kwa Wakili Yakubu kwa mchango wake kwa wana diaspora.
Wakili Saidi Yakubu baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo katika picha ya pamoja na wana diaspora waliomkabidhi.Wa pili kulia ni mai waifu wake,Bi Dida.
Picha ya pamoja na mawakili wapya walioapishwa siku hiyo na Jaji Mkuu,Jaji Kiongozi na viongozi wengine wa tasnia ya sheria nchini.
Mdau Yakubu akiwa na familia yake baada ya kulamba nondoz ya uwakili siku hiyo. Picha kwa Hisani ya East Africa Education Trust- UK.

SAYANSI ILENGE KUWAONDOLEA MATATIZO WATU MASKINI-BALOZI MANONGI

0
0
Mhe. Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati wa mkutano wa pembezoni uliokuwa umeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Elimu, Sayansi na Utamaduni ( UNESCO) na Baraza la Kimataifa la Sayani ICSU), Balozi Manongi alikuwa kati ya wanajopo wanne walioongoza majadiliano hayo.Wengine kutoka kushoto ni Bi. Vibeke Jense ambaye ni Mkurugenzi wa UNESCO Ofisi ya New York, katikati ni mwedesha majadiliano na kulia kwa Balozi Manongi ni Bw. Gisbert Glaser Mshauri Mwandamizi kutoka Baraza la Kimataifa la Sayansi ( ICSU).
Bw. Hassan Mshinda, ambaye ni Kamishna kutoka Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia akichangia katika majadiliano hayo.
sehemu ya washiriki wa mkutano huo.
Washiriki wengine wakifuatili kwa makini majadilianyo hayo kuhusu nafasi ya sayansi na teknolojia katika utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu, majadiliano hayo yaliandaliwa kwa ushirikiano wa UNESCO na ICSU.
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akibadilishana mawazo na Bw. Gisbert Gladser ambaye katika majadiliano hayo, alitaka kufahamu Tanzania inatumiaje uzoefu wake na mafanikio yaliyoainishwa katika majadiliano hayo kuzisaidia nchi nyingine za Afrika akilenga katika uhusiano na ushirikiano baina ya nchi za Kusini ( South- South Cooperation ).

BENKI YA CRDB YATWAA TUZO YA MWAJIRI BORA 2013

0
0
Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akizungumza katika hafla ya utoaji Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka, ambapo benki hiyo ilikuwa moja ya wadhamini katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akimkabidhi cheti Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka kutokana na mchango wa benki hiyo katika kufanikisha sherehe za utoaji wa Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka (EYA 2013), ambapo benki hiyo ilikuwa moja ya wadhamini katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka (kushoto) akimkabidhi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka Tuzo ya Fedha ya ushindi wa pili ya Mwajiri Bora wa Mwaka (EYA 2013), zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa benki hiyo, Timoth Fasha. Sherehe hizo zilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Benki ya CRDB, ilikuwa pia Mdhamini wa Fedha (Gold Sponsor) wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa waajiri bora, ambapo ilikabidhiwa cheti cha udhamini.
Wadhamini wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal
Mkurugenzi wa tawi la Vijana, Pelesi Fungo.
Kaimu Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela akipeana mkono na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akipeana mkono na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi wa Rasirimali Watu wa Benki ya CRDB, Timoth Fasha.
Mkurugenzi wa tawi la Lumumba, John Almasi (kulia), Mkurugenzi wa tawi la Kijitonyama, Lucas Busigaz, Mkurugenzi wa tawi la Vijana, Peres Fungo, na Mwanasheria wa Benki ya CRDB wa pili kushoto na Ofisa Uhusiano wa Benki ya CRDB, Tumain Kamuhanda. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa benki hiyo, Timoth Fasha.

DAR ES SALAAM, Tanzania

BENKI ya CRDB imefanikiwa kutwaa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2013  (EYA), iliyotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika jijini Dar es Salaam, hivyo kuendelea kuwa kinara miongoni mwa waajiri wa taasisi za fedha.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Huduma Shirikishi, Esther Kitoka, alisema CRDB inajivunia kiwango chake katika kuwajali na kuwathamini wafanyakazi, hivyo kuwawezesha kutwaa tuzo hiyo mara pili mfululizo.

Aliongeza kuwa, ili kuhakikisha wanafanikiwa kutwaa Tuzo ya Mwajiri Bora (EYA), ambayo mwaka huu imechukuliwa na Kampuni ya Simu ya Vodacom, wamejipanga kuboresha maafunzo miongoni mwa waajiriwa wao ili kuwaongezea ufanisi kazini.

“Mwakani tutakuwa na mafunzo ya wafanyakazi wetu katika Chuo Kikuu cha Milpark cha Afrika Kusini, ili kuboresha ufanisi miongoni mwa wafanyakazi na kurutubisha CV zao, vyote vikiwa ni kwa ustawi wa Benki CRDB na wateja wetu kwa ujumla,” alisema Kitoka.

Kitoka akasisitiza kuwa, kupitia mikakati hiyo, wanaamini mwakani Benki ya CRDB wataibuka washindi wa jumla (overall), hasa baada ya kutanua huduma zake hadi nje ya nchi kupitia matawi yake nchini Burundi na huduma za China UnionPay na China Desk.

Kwa upande wake Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka aliwapongeza washindi wote waliotwaa tuzo katika hafla hiyo, huku akiwataka kuboresha mazingira ya kazi miongoni mwa waajiriwa, kama ishara ya kuthamini mchango wao kwa kampuni na taifa.

Kabaka aliongeza kuwa, mhimili mkuu wa ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote duniani ni utendaji uliotukuka miongoni mwa waajiriwa wa sekta rasmi na isiyo rasmi, ambao wasipoboreshewa mazingira, hawatokuwa wazalishaji wazuri kwa ustawi wa taifa.

Awali akifungua hafla hiyo, mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal, aliwataka waajiri wote nchini kutumia hafla ya tuzo za Mwajiri Bora kama nia ya kujibu maswali lukuki kuhusu uzalishaji wa bidhaa na utawala bora mahali pa kazi.

Jumla ya tuzo 21 zilitolewa kwa kampuni mbalimbali zilizoshiriki katika mchakato huo uliokuwa chini ya udhamini mkuu wa Ultimate Security (Platinum Sponsor) na benki ya CRDB (Gold Sponsor) na kuratibiwa na ATE.
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images