Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live

MUME AMFYEKA MKEWE MIGUU NA MIKONO

$
0
0
Tazama video ya kipindi maalum cha 'Wanawake Live' inayokuonesha stori ya yule mwanamke aliyefekwa miguu na mikono na mumewe. 
 PART 1:  
 PART 2:

Taarifa ya Ndugu Albert Msando Mwanasheria wa Mh. Zitto Kabwe aliyoitoa leo kwa vyombo vya habari

Remarks by President Obama at Memorial Service for Former South African President Nelson Mandela

MALKIA MAXIMA WA UHOLANZI AWASILI NCHINI

$
0
0
 
Malkia  Maxima wa Uholanzi akiwa amefuatana na Mwenyeji wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. Mwingine pembeni ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Raymond Mushi.

Malkia Maxima kwa pamoja na Mhe. Mama Salma wakifurahia burudani kutoka kwa mojawapo ya vikundi vilivyokuwepo uwanjani wakati wa mapokezi.
 
Wakuu wa Wilaya za Kinondoni na Temeke, Mhe. Jordan Rugimbana (wa nne kutoka kushoto) na Mhe. Sophia Mjema (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa uwanjani hapo wakati wa mapokezi ya Malkia Maxima. Wengine ni Balozi Dora Msechu (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Victoria Mwakasege (wa pili kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika na Bw. Songelaeli Shila, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa  katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Mama Salma akimtambulisha kwa Malkia Maxima  Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Ne na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu. Pembeni kwa Balozi Msechu ni Bibi Victoria Mwakasege, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ulaya na Amerika.

Malkia Maxima kwa pamoja na Mama Salma wakifurahia  wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshoghulikia masuala ya Chakula (WFP), Bi. Ertharin Cousin akiwaeleza jambo mara baada ya Malkia Maxima kuwasili nchini.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini, Dkt. Alberic Kacou (kushoto) akiwaeleza jambo Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Wilson Masilingi (katikati)  na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jaap Frederics wakati wa mapokezi ya Malkia Maxima wa Uholanzi.

Rais Kikwete katika shughuli ya kumbukumbu ya mzee nelson mandela nchini afrika kusini

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya Mzee Nelson Mandela Uwanja wa FNB jijini Johannesburg Jumanne Novemba 10, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwatambulisha  viongozi mbalimbali wa Afrika kwa Rais Barack Obama wa Marekani  wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya Mzee Nelson Mandela Uwanja wa FNB jijini Johannesburg Jumanne Novemba 10, 2013. PICHA NA IKULU

TASWIRA ZA KUKUMBUWA WAKATI RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WALIPOMTEMBELEA MADIBA ENZI ZA UHAI WAKE

When World Leaders Get All Touchy-Feely

magazeti sauzi


SUMMER 2014 WASHINGTON FELLOWSHIP FOR YOUNG AFRICAN LEADERS APPLICATION INSTRUCTIONS

Msanii saidi wa Ngamba a.k.a mzee small bado yu hai, amlaani aliyemzushia mauti

$
0
0
Courtesy of Bongo5
Mzee Small akiwa na familia yake

Mandela Long Walk to Freedom Official Trailer

FUATILIA HAPA SHUGHULI NZIMA YA KUAGWA KWA MWILI WA HAYATI MZEE NELSON MANDELA JIJINI PRETORIA LIVE!

TANGAZO LA MUALIKO.

$
0
0
ASASI YA CULTURAL HARMONY AND REFORM FORUM (CHRF) INAYOSHUGHULIKA NA KUKUZA AMANI, UMOJA, UPENDO NA MAADILI MEMA MIONGONI MWA JAMII, INAKUALIKA KATIKA UZINDUZI WAKE SIKU YA JUMATATU TAREHE 16/12/2013 SAA 3.00 ASUBUHI.KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE- AMBAPO MGENI RASMI NI RAISI WA AWAMU YA PILI MHE.ALI HASSAN MWINYI . WOTE MNAKARIBISHWA.

NBC YAMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA WEKA UPEWE

$
0
0
 Mkuu wa Huduma za Rejereja za Kibenki wa Benki ya NBC Tanzania, Mussa Jallo (wa pili kushoto) akizungumza katika  hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Weka Upewe’ ya benki hiyo ambayo washindi wanne walikabidhiwa pikipiki mpya aina ya Honda. Hafla hiyo ilifanyika pamoja na uchezeshwaji wa droo ya pili katika Tawi la NBC Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe, Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mabonye na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Chiku Saleh. 
 Mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya NBC Weka Upewe, Festo Mukerebe (kulia) akionyesha ufunguo wa pikipiki aina ya Honda, mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Kanda wa NBC, Rachel Mwalukasa (kushoto) katika hafla hiyo iliyofanyika katika Tawi la Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Huduma za Rejereja za Kibenki wa Benki ya NBC Tanzania, Mussa Jallo (kulia) akikabidhi zawadi ya pikipiki mpya aina ya Honda kwa Dk. Isaya Mpelumbe aliyopokea kwa niaba ya mtoto wake, Edna Ndumbaro aliyeshinda katika droo ya kwanza ya promosheni hiyo.
 Meneja wa NBC Tawi la Ubungo, David Nsimba (kushoto) akikabidhi funguo ya pikipiki mpya aina ya Honda kwa Hassan Khamis aliyepokea kwa niaba ya Prof. Peter Maina wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye naye aliibuka kidedea katika droo ya kwanza ya promosheni ya NBC Weka Upewe.
Mmoja wa washindi wa promosheni ya Weka Upewe ya benki ya NBC, Festo Mukerebe akitoa shukrani zake kwa benki ya NBC mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya pikipiki mpya aina ya Honda. Kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na kushoto kwa Alina ni mke wa Festo, Alphoncena Mukerebe.

MKUTANO WA TISA WA MAWAZIRI WA NCHI WANACHAMA WA SHIRIKA LA BIASHARA LA DUNIA (WTO) WAFANYIKA MJINI BALI, INDONESIA

$
0
0
Ujumbe kutoka Tanzania ulioshiriki kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO) uliofanyika mjini Bali, Indonesia kuanzia tarehe 3 – 6 Desemba, 2013 ukiongozwa na Mhe. Dkt Abdallah O. Kigoda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara.
 Mheshimiwa Dkt. Abdallah O. Kigoda (Mb.), Waziri wa Viwanda na Biashara akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Biashara wa Misri Mhe Mounir ABDEL NOUR na ujumbe wake walipokutana katika Mkutano wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO) uliofanyika mjini Bali, Indonesia hivi karibuni.
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah O. Kigoda (Mb) akijadiliana jambo na Ndg. Lucas Saronga, Mkurugenzi wa Idara ya Utangamano wa Biashara Wizara ya Viwanda na Biashara kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Shirika la Biashara la Dunia uliofanyika mjini Bali, Indonesia kuanzia tarehe 3 – 6 Desemba, 2013
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah O. Kigoda (Mb) akijadiliana jambo na Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Finland  Mhe Alexander STUBB kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Shirika la Biashara la Dunia uliofanyika mjini Bali, Indonesia kuanzia tarehe 3 – 6 Desemba, 2013. Mwingine ni Ndg. Lucas Saronga, Mkurugenzi wa Idara ya Utangamano wa Biashara Wizara ya Viwanda na Biashara Tanzania.


Diagnostic Review for Increasing Consumer Awareness and Protection and Financial Services in Tanzania

$
0
0
The World Bank today presented at a Bank of Tanzania Dissemination Workshop the findings of the Diagnostic Review for Increasing Consumer Awareness and Protection and Financial Services in Tanzania conducted in January 2013. The study is in line with the revised standard framework of Consumer Protection Financial Literacy (CPFL) published in 2012, based on in-depth country-level reviews of good practices of consumer protection and financial literacy.

The CPFL review considered consumer protection issues in the banking, microfinance and pensions sectors with a particular focus on issues related to institutional structures, the legal and regulatory framework, transparency and disclosure, business practices and dispute resolution. A review was also undertaken of initiatives related to financial literacy.

The World Bank is supporting countries all around the world in their efforts to strengthen consumer protection and financial literacy frameworks. The Good Practices are a compilation of the most frequently used practices that have been successfully carried out in the field. They represent a summary of useful approaches for the improvement of conduct of financial institutions when dealing with retail customers and aim to provide a reference for policymakers in designing their financial consumer awareness and protection.

“We are pleased by the steps and activities that have been undertaken so far in Tanzania aiming a strengthening consumer protection and financial literacy levels of the Tanzanian population” says Andrea Dall’Olio, the World Bank Sector Leader covering Finance and Private Sector Development for Tanzania, Uganda and Burundi. “The Team has been very impressed by the drive, determination and enthusiasm of the key stakeholders working on these issues and we hope to continue this very fruitful partnership with Bank of Tanzania in the implementation of key recommendations. Going forward, the World Bank look forward to working with key stakeholders on important issues associated with the CPFL framework in Tanzania.”

Notwithstanding these positive developments the report highlights further areas of reform in order to address institutional arrangements and the limited requirements concerning disclosure, dispute resolution and fair business practices. The report also notes the need to accelerate implementation of Tanzania’s financial education framework.

In the context of Tanzania the following challenges seem to be particularly relevant when designing and strengthening the existing CPFL framework: (i) the increased usage of delivery channels, in particular financial services delivered via mobile phones, have filled a critical need for consumers in Tanzania but raised important issues of consumer protection; (ii) the large share of the population is living in rural areas and with prevailing low levels of financial literacy which limits the use of formal financial services and increases the risk of consumer rights abuses.

TUMEWADHIBITI M23 NGUVU ZETU SASA ZIKO KWA FDLR- MONUSCO

$
0
0
Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika Eneo la Maziwa Makuu, Mary Robinson akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, baada ya yeye na Bw. Martin Kobler (kulia) ambaye ni Muwakilishi wa Katibu Mkuu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa MONUSCO kuwasilisha taarifa zao mbele ya Baraza Kuu la Usalama, katika mkutano wa ndani wa Baraza hilo uliofanyika siku ya jumatano. katika mkutano huo wakuu hao wawili walielezea kuridhishwa kwao na hali ya kijeshi na kisiasa inavyoendelea katika DRC hususani eneo la Mashariki ya nchi hiyo. pamoja na mchakato wa utekelezaji wa Mpango Mpana wa Umoja wa Mataifa kuhusu siasa, amani, usalama na maendeleo katika DRC na eneo la Maziwa na matarajio kuhusu mazungumzo ya Kampala ( Kampala Talks).

NSSF YANOGESHA SIKU YA FAMILIA BULYANHULU

$
0
0
KAHAMA, Shinyanga

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limetoa kiasi cha shilingi milioni 2, fulana 450 na kalenda 180 kwa uongozi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko Kakola, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kufanikisha sherehe za Siku ya Familia ya Wafanyakazi wa mgodi huo.

Siku ya Familia 'Bulyanhulu Family Day 2013' ya Bulyanhulu Gold Mine ilifanyika mgodini hapo Desemba 8 mwaka huu, ambako pamoja na mambo mengine, NSSF ilitoa elimu ya kina kwa wachimbaji, maofisa na wafanyakazi wengine mgodini, kuhusiana na mafao na huduma zingine za shirika.

Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga, shirika hilo lina wanachama zaidi ya 3000 katika mgodi wa Bulyanhulu, ambao kupitia siku hiyo walijumuika pamoja, ikiwamo kufurahi na kutanua uelewa wao juu ya huduma zinazotolewa na NSSF.

Katika sherehe hizo, licha ya wafanyakazi na viongozi kutambuana na kubadilishana mawazo, NSSF pia ilitoa elimu ya kutosha kuhusu huduma zake, ikiwamo ya mafao mbalimbali yatolewayo na shirika hilo kwa wanachama wake wakati wakiwa kazini na baada ya kustaafu.

Mafao yanayotolewa na NSSF ni Fao la Matibabu, Kuumia Kazini,Uzazi, Mazishi, Urithi, Ulemavu, Uzee pamoja na Mikopo kwa Wanachama kupitia Saccos.
 Meneja Mkuu wa Bulyanhulu Gold Mine, Peter Buger (kushoto)  akimshukuru, Kaimu Meneja wa NSSF Kanda ya Kahama, Lusato Ernest baada ya kupokea msaada wa sh. milioni 2 kwa ajili ya kufanikisha ya sherehe za siku ya familia iliyofanyika Kakola wilayani  Kahama mkoani Shinyinga. 

 Mwakilishi wa NSSF Kakola, Barry Mwaga akitoa maelezo kuhusu athari za kujitoa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii na Umuhimu wa Fao la kuumia Kazini kwa wafanyakazi wa migodini.  

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA TAIFA HUDUMA ZA FEDHA NCHINI

$
0
0
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) , Prof. Benno Ndulu, akisaini mfano wa cheti cha Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye lengo la kusimamia na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Wanaoshuhudia nyuma (katikati) ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kulia kwake ni Malkia Maxima wa Uholanzi (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha Sada Mkuya Salumu. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha, wenye lengo la Kusimamia na kutatua ufumbuzi wa changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Malkia Maxima wa Uholanzi, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye lengo la Kusimamia na kutatua ufumbuzi wa Changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Mohammed Gharib Bilal imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Malkia Maxima wa Uholanzi na Naibu Waziri wa Fedha, Sada Mkuya Salumu, wakiwa wameshikilia Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha baada ya kuzinduliwa leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania.
Baadhi ya wadau wa Sekta za Fedha waliohudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, alipokuwa akihutubia, wakati wa uzinduzi.Picha na OMR

NEWS ALERT: WATU 12 WAPOTEZA MAISHA, 30 WAMEJERUHIWA VIBAYA KWENYE AJALI YA BASI MKOANI TANGA LEO. RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

$
0
0
Basi la Abiria la Kampuni ya Burudani linavyoonekana baada ya kupata ajali mbaya sana leo iliyopelekea kupoteza maisha kwa watu 12 huku wengine zaidi ya 30 wakiwa kwenye hali mbaya.ajali hiyo imetokea leo eneo la Kwaluguru,Kwedizinga  wilayani Handeni,Mkoani Tanga.
WATU 12 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada  ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria la Kampuni ya Burudani linalofanya safari zake kati ya Korogwe mkoani Tanga kwenda Jijini Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.

 Ajali hiyo imetokea mapema leo asubuhi majira ya saa 1.30 katika eneo la Kwaluguru,Kwedizinga  wilayani Handeni,Mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea ajali hiyo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga,Constantine Massawe alisema kuwa ajali hiyo iliyohusisha gari lenye namba za usajili T 610 ATR aina ya Nissan,imetokea leo na kusababisha vifo vya abiria 12 na wengine zaidi ya 30 wako kwenye hospitali ya Wilaya ya Korogwe,wakiendelea kupatiwa matibabu.

Kamanda Massawe aliendelea kusema kuwa  dereva wa basi hilo ajulikanaye kwa jina la Luta Mpenda(35) ni miongoni mwa watu wanaosadikiwa kufa na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Korogwe ya Magunga.

“Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya magunga na hali zao bado siyo nzuri sana lakini na miili ya marehemu pia imehifadhiwa magunga”,alisema Kamanda Massawe.

Hata hivyo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo alipofika kwenye kona ya eneo la Kwalaguru gari lilimshinda na  kupinduka. 
Wakazi wa Wilaya ya Korogwe wakiwa wamefurika kwenye Hospitali ya Magunga walipohifadhiwa marehemu na majeruhi.
Wauguzi wa Hospitali ya Magunga wakiendelea kutoa huduma kwa majeruhi wa ajali hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo akitokea chumba cha maiti cha Hospitali hiyo.
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live




Latest Images