Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

VIONGOZI NA WATUMISHI WA UMMA WAKUMBUSHWE KUTIMIZA WAJIBU WAO

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Umma mkoani humo, wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi. 
Baadhi ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani humo, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi. 
Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele, akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi. 
Afisa Maadili kutoka Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Onesmo Msalangi akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi. 
Baadhi ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi. 

********************************************** 


Na Stella Kalinga, Simiyu 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema ni vema Sekreatarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma iendelee kuwakumbusha viongozi na watumishi wa umma nchini kutimiza wajibu wao ili kuweza kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali. 

Mtaka ameyasema hayo Juni 03, 2019 Mjini Bariadi, wakati akifungua mafunzo kwa Viongozi wa Umma mkoani Simiyu, ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora. 

Amesema ikiwa kila mmoja katika Utumishi wa Umma atatimiza wajibu wake jamii na nchi kwa ujumla wake itaweza kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali katika nyanja mbalimbali kwa wakati. 

“Ni vizuri Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiendelea kuwakumbusha watu wote wanaofanya kazi zinazoihusu jamii kutimiza wajibu wao, kila mmoja akitimiza wajibu wake yapo mambo mengi sana sisi kama jamii, nchi, mkoa na kwa namna ambavyo uongozi na mgawanyiko wa .nchi yetu ulivyo tutafikia malengo yetu kwa wakati” alisema Mtaka. 

Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa Umma ambao ni watoa maamuzi katika maeneo yao ya kazi kuwa makini katika kutoa maamuzi na wahakikishe wanafanya maamuzi kwa wakati. 

Kwa upande wake Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele amesema viongozi wa Umma wanapaswa kutoa maamuzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa ili kutoiletea hasara Serikali. 

Ameongeza kuwa Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma itaendelea kutoa elimu kwa viongozi wa umma juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi ya uadilifu katika uongozi na endapo ikitokea kiongozi yeyote atakengengeuka na kutofuata maadili sheria itachukua mkondo wake. 

Kwa upande wake Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio ameshukuru Sekretarieti ya Maadili kwa kutoa mafunzo ya maadili kwa viongozi wa Umma na akatoa wito kwa viongozi hao kuwa waadilifu, kutekeleza majukumu yao na kutojilimbikizia mali kinyume na taratibu na maadili ya viongozi wa Umma. 

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa ametoa wito kwa Sekretarieti ya Maadili kwa viongozi wa Umma kutoa elimu ya maadili kila viongozi wapya wanapoteuliwa au kuchaguliwa, hususani madiwani wanapochaguliwa na kuunda Mabaraza mapya ya madiwani ili wajue misingiya uadilifu inayopaswa kuwaongoza katika kazi zao

Salamu za Idd kutoka kwa IGP SIRRO

TPA YAWAKARIBISHA WADAU KUTUMIA CHEREZO YA MAJINI ILIYOPO ZIWA VICTORIA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Kwa upande wa Maziwa makuu katika eneo la Ziwa Victoria imewakaribisha wadau na wafanyabishara wa majini katika ziwa hilo kutumia Cherezo ya ndani ya maji iliyopo katika bandari ya Mwanza hili kuweza kukarabati meliz zao kwa ufanisi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza Bw. Geoffrey Lwesya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza ambao wapo katika ziara ya kutembelea na kutangaza miradi ya maendeleo ya bandari zilizo katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa

" Nawaomba wafanyabiashara wenye meli zao katika ziwa Victoria waje wafanye matengenezo kwa kutumia hii cherezo kwa ajili ya usalama wa vyombo vyao ,kumekuwa na maneno maneno juu ya gharama za kutumia hii cherezo ni kubwa lakini ukweli ninao waambia kuwa gharama zetu ni nafuu sana ambazo kila mtu anayemiliki meli katika ziwa hili anaweza kuzimudu"
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza,Geoffrey Lwesya akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza ambao wapo katika ziara ya kutembelea na kutangaza miradi ya maendeleo ya bandari zilizo katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza,Geoffrey Lwesya akiwaonyesha sehemu ya Cherezo mpya inayojengwa na Serikali ya awamu ya tano ambayo ipo katika Bandari ya Mwanza 
 Sehemu ya Cherezo Mpya inayojengwa katika Bandari ya Mwanza ambapo ni moja ya maboresho ya bandari hiyo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. John Pombe Magufuli
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza, Geoffrey Lwesya akiongozana na waandishi wa habari leo jijini Mwanza ambao wapo katik ziara ya kutembelea na kutangaza miradi ya maendeleo ya bandari zilizo katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa
 Sehemu ya Makuli wanaopakua Mizigo katika Bandari ya Mwanza wakipakua mzigo wa Mbao unaoshushwa kwenye meli tayari kwa ajili ya kusafirishwa.
Cherezo ya Ndani ya Maji iliyopo katika Ziwa Victoria inayomilikiwa na Mamlaka ya Bnadari Tanzania yenye urefu wa Km 110 kama inayoonekana kwa juu ikiwa aijazama kwenye maji.

WAZIRI MKUU KABIDHIWA KISIMA CHA MAJI

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua maji baada ya kukabidhiwa kisima cha maji cha kijiji cha Nandagala ‘B’ kilichojengwa kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uturuki nchini Juni 3, 2019. Kulia ni Muambata wa Ubalozi wa Uturuki anayeshughulikia masuala ya jamii nchini, Muhammed Cicek na kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Turkish Maarif Foundation, Oguz Hamza Yilmaz. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MWALIMU SHULE YA MSINGI AKUTWA NA AK 47

$
0
0


Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana, akiwaonyesha waandishi wa habari silaha aina ya AK 47 ambayo ilikutwa kwa mtuhumiwa aitwaye Solomon Letato kipuker ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Naan iliyopo Loliondo wilayani Ngorongoro. 


Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha 

Mtu mmoja aitwaye Solomon Letato Kipuker (30) ambaye ni Mwalimu wa shule ya Msingi Naan iliyopo kata ya Enguserosambu tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro amekatwa akiwa na silaha aina ya AK 47 ikiwa na risasi Tano ndani ya Magazine. 

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shanna, amesema kwamba tukio hilo limetokea Juni 2 mwaka huu baada ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa kushirikiana na Kikosi Kazi cha kupambana na uhalifu hasa ujangili kupata taarifa za Kiintelijensia na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo. 

“Mtuhumiwa huyo ni miongoni mwa wafanyabiasahara haramu wa nyara za Serikali ikiwemo meno ya Tembo ambapo mara baada ya kumhoji alikiri kumiliki silaha hiyo kwa kushirikiana na wenzake ambao bado Jeshi la Polisi tunawatafuta”. Alifafanua Kamanda Shana. 

Aidha Kamanda Shana alisema kwamba, mtuhumiwa huyo alikiri pia kujihusisha na ukodishaji wa silaha hiyo katika matukio mbalimbali ya kiuhalifu hasa utekaji ambayo yalishawahi kutokea wilayani humo kipindi cha nyuma. 

Hata hivyo Kamanda Shana alimpongeza Kamishna wa Uhifadhi (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi kwa kuzidi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kupambana na matukio mbalimbali ya uhalifu ndani ya mkoa huu wa Arusha. 

Katika Operesheni zinazoendelea kila siku ndani ya wilaya zote sita za mkoa huu, Mei 30 mwaka huu, Jeshi hilo lilifanikiwa kuwakamata watu watatu (Majina yamehifadhiwa) wakiwa na jumla ya vipande vinne vya Meno ya Tembo katika Kata ya Maji ya Chai tarafa ya King’ori wilayani Arumeru na wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani hivi karibuni.

PUBLIC NOTICE on IATA payment cycles for Air tickets issued in Tanzania.

$
0
0
We wish to remind consumers of Air ticketing services and the general public of the International Air Transport Association [IATA] payment cycles for Air tickets issued in Tanzania.
The credit period enjoyed by IATA accredited air ticketing Agents in Tanzania is 15 days – and may be reduced further to 7 days. Agents failing to meet payment deadlines will be declared defaulters and denied facilities to issue tickets. Consequently, in order to protect the industry from a crisis arising from potential massive defaults, existing credit terms for air tickets will change drastically and can be also in favour of cash / credit card / prepayments as well.
This is therefore to advise all consumers of air travel services especially corporate entities and Government departments to take note of these terms and conditions. Please ensure that necessary adjustments in payment plans to conform to the new requirements of the relevant agent.
Kindly contact your travel agent immediately to discuss payment plans available in the market to avoid disruptions of your travel plans.
TASOTA SECRETARIAT
Tanzania Society of Travel Agents – TASOTA – is the national association representing the interests of Travel Agents in Tanzania. It serves as the single voice of Travel Agents in the industry with a mandate to promote the highest code of ethical and professional standards members in their dealings with consumers and each other.
For more clarification, please contact the Executive Secretary
on +255-685-577229 or e-mail: info@tasota.org

WACHEZAJI 38 WA TIMU YA TAIFA STARS WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MOYO

$
0
0

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Siza Ngomero akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiogram) mchezaji wa timu ya Taifa Stars Feisal Salum wakati wa uchunguzi wa kina wa magonjwa ya moyo kwa wachezaji wa timu hiyo leo Jijini Dar es Salaam. 
Fundi Sanifu wa Moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abuu Dalidali akimpima kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (Electricalcardiography –ECG) mchezaji wa timu ya Taifa Stars Yahaya Zaid wakati wa kuwafanyia uchunguzi wa kina wa magonjwa ya moyo wachezaji wa timu hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Wachezaji hao wamefanyiwa uchunguzi wa kina wa magonjwa ya moyo kabla ya kwenda nchini Misri kushiriki mashindano ya AFCON yatakayoanza tarehe 21/06/2019.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Daktari wa timu ya Taifa Stars Emily Urasa wakati wa kuwafanyia uchunguzi wa kina wa magonjwa ya moyo wachezaji wa timu hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Wachezaji hao walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph) na mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography –ECG). 
Picha na: Genofeva Matemu – JKCI 
…………………. 
Wachezaji 38 wa timu ya Taifa Stars wamefanyiwa uchuguzi wa kina wa magonjwa ya moyo kama Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) linavyoelekeza kabla ya kuanza kwa mashindano ya kombe la Mataifa ya Africa (AFCON) ni lazima wachezaji wanaoshiriki mashindano hayo wapimwe afya zao. 

Vipimo walivyofanyiwa wachezaji hao ni vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph) na mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography –ECG). Upimaji huu umefanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). 

Taasisi yetu ni Hospitali iliyothibitishwa na CAF kuwa inakidhi vigezo vyote vya upimaji wa magonjwa ya moyo. Uthibitisho huu ulitolewa kabla ya kuanza kwa mashindano ya AFCON kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 yaliyofanyika mapema mwaka huu hapa nchini .JKCI ilikaguliwa na kuthibitishwa na wakaguzi kutoka CAF. 

Matokeo ya vipimo hivyo yatasaidia kufahamu afya za wachezaji na utimamu wao wa kimwili kabla ya kwenda kushiriki katika mashindano ya AFCON yanayotarajia kuanza tarehe 21/06/2019 huko nchini Misri. 

Tunatoa wito kwa vilabu vya mpira hapa nchini kuwaleta wachezaji wao kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo hii itawasaidia wachezaji hao kufahamu kama wanamatatizo au la na kuepukana na vifo vya ghafla vinavyoweza kuwapata wakiwa uwanjani. Kwa upande wa wananchi kabla ya kujiunga na vilabu vya mazoezi ni muhimu wakapima afya zao yakiwemo magonjwa ya moyo..

POLISI PWANI YAWASAKA WATU WANNE WANAODAIWA KUPORA PIKIPIKI

$
0
0


Mwamvua Mwinyi,Kibaha 

JESHI la polisi mkoani Pwani,linawasaka watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao wanadaiwa kupora pikipiki eneo la Kidimu kata ya Pangani Kibaha Mjini . 

Aidha jeshi hilo limewatahadhalisha madereva bodaboda kuacha kuamini abiria wanaokodisha pikipiki zao kwenda nje ya mji kwani sio wote ni abiria wema. 

Akielezea juu ya tukio hilo,kamanda wa polisi mkoani Pwani Wankyo Nyigesa alisema kuwa ,watu hao wakiwa Kidimu kata ya Pangani,barabara ya Kibaha kupitia Mapinga kuelekea Bagamoyo walipora pikipiki ambayo mmoja wao aliikodi kutokea Mwanalugali Kibaha. 

Wakiwa Kidimu walitumia gari Toyota IST rangi ya silver yenye namba za usajili T.355 DMA ambapo mmoja wao alikimbilia Mwanalugali na kukodisha pikipiki yenye namba MC 401 CDW aina ya hajoue ya bwana Amani Ambele. 

Wankyo, anasema baada ya hapo jambazi huyo aliomba apelekwe Kidimu kwa sh.3,000 ambako Kidimu kulikuwa tayari na wenzie watatu wakiwa na gari yenyr namba T 355 DMA . 

“Walipofika hapo abiria ambae ni anaedaiwa kuwa ni jambazi alimfunga kitambaa cheusi usoni na kumuingiza katika gari na kisha kuondoka na pikipiki” 

“Bahati nzuri madereva boda wengine wa mjini Kibaha walipata taarifa na kuanza kulifukuzia gari hilo na walipolipata walilichoma moto na liliteketea huku majambazi hayo yakifanikiwa kukimbia”alifafanua Wankyo. 

Wankyo alielezea kuwa, baada ya madereva bodaboda hao kuteketeza gari hilo kwa moto walitoa plate namba ,kadi ya gari na bima na kuwasilisha polisi. 

Wakati huo huo kamanda huyo alisema jeshi hilo limejipanga kufanya misako ili kulinda raia na mali zao wakati wa sikukuu ya iddi el fitri. 

Hata hivyo Wankyo,aliwaasa madereva kuacha kukiuka sheria za usalama barabarani wakati wa sikukuuu na kuacha kutumia vileo wakiwa wanaendesha.

MFANYABIASHARA APORWA MIL 55 BAADA YA KUDAIWA KUNYWESHWA SUMU .

$
0
0
Watu wawili wa familia moja, wanashikiliwa na Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara wa ufuta Oswald Malambo na kupora kiasi cha shilingi milioni 55.

Watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa Kata ya Ifumbo Wilayani Chunya, inasemekana waliweka kitu kinachodhaniwa ni sumu kwenye kinywaji alichotumia mfanyabiashara huo, wakati wakiwa kwenye hotel baada ya kufanikiwa kuuza ufuta.

Kamada wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ulrich Matei, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi.

Kamanda, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Raphael Walolile na Goliat Walolile.Amesema tukio hilo lilitokea Juni 2 mwaka huu na kwamba marehemu ndiye aliyetoa taarifa za kwamba alinyweshwa sumu na watuhumiwa lakini bado haijathibitishwa.

“Kwa sasa bado tunasubiri taarifa za daktari na kama itabainika ni sumu sheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwa na kufunguliwa shitaka la mauaji,”

Aidha, akizungumzia hilo, Msemaji wa familia hiyo, Mhandisi Selemani Malambo, alisema ndugu yao alienda kuuza ufuta eneo la Mbalizi Halmashauri ya Mbeya, akiwa mzima lakini baada ya kuuza ufuta wakati akijiandaa kurudi aliombwa na watuhumiwa wakafanye mazungumzo.

Mhandisi Malambo amesema watuhumiwa walimtaka ndugu yao huyo wakazungumze naye kwenye moja ya bar zilizopo katika eneo la Kabwe Jijini Mbeya na alipofika katika eneo hilo, watuhumiwa hao, walimtaka awaache wadogo zake nje jambo lililofanyika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Urlch Matei

NIDHAMU YAMBEBA MONALISA ASAINI MKATABA NA COWBELL

$
0
0

Na.Khadija seif,Globu ya jamii

KAMPUNI ya Hawaii kupitia bidhaa ya maziwa ya cowbell wamsainisha mkataba msanii wa bongo movie monalisa.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo meneja masoko amesema wanategemea ubalozi huo utakua wa ufanisi zaidi na kukuza kipato katika kampuni hiyo.

"Wapo wasanii wengi lakini tumeweza kumpa ubalozi huo monalisa kutokana na sababu nyingi ikiwemo jamii inamchukuliaje pamoja na swala la heshima na nidhamu,"

Mpanda ameweka wazi kuwa hofu kubwa kwa makampuni kujitokeza kutoa ubalozi kwa wasanii wengine ni kutokana na kuhusishwa kwenye skendo chafu na kupelekea wateja kutokua na imani na bidhaa husika.

Kwa upande wake Yvonne cherry a.k.a Monalisa amewapongeza kampuni hiyo kwa kuona juhudi zake na kumteua kua balozi wa muda wa kipindi cha mwaka mmoja.

"Nategemea kuwa na matunda mazuri kwenye kazi zangu na ufanisi mkubwa kwenye kampuni ili kuwafikia wateja wote,"

Hata hivyo amewataka wasanii wengine kujenga misingi mizuri ya nidhamu ili kupewa mikataba mbalimbali kunufaika wao wenyewe na kuongeza pato la taifa.


FORUMCC YAHAMASISHA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA KWA KUJIKITA KATIKA KUTENGENEZA NISHATI MBADALA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la FORUMCC Rebecca Muna amesema kuna kila sababu ya kuhakikisha wananchi wote wakiwamo vijana wanapata elimu kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Pia amesema iko haja kwa vijana pamoja na mambo mwngine kutumia fursa ambazo zinazojitokeza kutokana na athari za mabadiliko ya kimazingira na tabianchi kuwa fursa ikiwa pamoja na kujikita katika nishati mbadala .

Muna ameyasema hayo leo kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam ambapo FORUMCC kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini wameadhimisha Wiki ya Mazingira kwa kuandaa maonesho ya nishati mbadala pamoja na mchezo wa mpira wa miguu ambapo timu ya kutoka Abby Enviroment & Agriculture Company Service wameibuka washindi wa Kombe la Mazingira,hivyo wametangazwa kuwa mabalozi wa mazingira.

Akifafanua zaidi Muna amesema FORUMCC kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya(EU) wana mradi uliojikita katika mabadiliko ya tabianchi na mazingira,hivyo kupitia ufadhili huo wamekuwa mstari wa mbele kuwashirikisha Watanzania kukabiliana na mabadiliko yatabianchi.

"Leo hii ikiwa tunaadhimisha wiki ya mazingira FORUMCC tumeona tunakilasababu kuwakutanisha vijana ambao ni wadau wa mazingira kwa kuwaandalia michezo wanayoipenda na wakati huo huo kuitumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa vijana.

" Kupitia siku hii ya leo ya kuadhimisha wiki ya mazingira tunawapa ujumbe kwamba watumie fursa iliyopo kwa kuanzisha nishati mbadala.Tunafahamu Serikali imezuia mifuko ya plastiki ,hivyo vijana wanayo nafasi kutengeneza mfuko mbadala na hatimaye wakajiongezea kipato,"amesema.

Ameongeza kuwa kuna fursa ambazo zinakuja na mabadiliko ya tabia nchini huku akitoa mfano kuwa wananchi wanatakiwa kutumia mkaa mbadala ya kuendelea kukata miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa.

"Kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuna majukumu tunayoendelea nayo kupitia miradi mbalimbali.Hivyo mbali ya kujikita kwa vijana tumeanzisha vikundi vya wanawake na wanaume kwa ajili ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira nchini.

"Tunavyo vikundi 20 na kila kikundi kina watu kati ya watu 30 mpaka watu 50, na hao wanajihusisha na usafi wa mazingira kwa kukusanya taka na kisha taka hizo kutumika kuzalisha nishati mbadala na bidhaa nyingine zitokanazo na taka," amesema Muna.

Amefafanua katika kuhakikisha vikundi hivyo vinawajibika ipasavyo ,FORUMCC imekuwa ikitoa mafunzo kwa wanavikundi hao, kuwapatia vifaa na soko la kuuzia bidhaa ambazo zinatokana na taka wanazokusanya na hiyo ni kwa Ilala.

"Licha ya kuwa  Ilala kwa hapa Dar es Salaam,pia tupo mkoani Singida ambako kule tupo kwenye kata tatu za Kijota,Mrama na Mtinko ambako wananchi wa maeneo hayo tunawasaidia katika kulima kilimo ambacho kinahimili athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mbali na kufanya kazi na vikundi,FORUMCC imekuwa ikihakikisha suala la uwajibikaji kuanzia kwa wananchi, serikali,sekta za umma na binafsi ambapo kila mmoja anatakiwa kuwajibika kukabiliana na mabadiliko yabtabianchi kwa kuwa na teknolojia rafiki katika kutunza mazingira.

"  Tumekuwa tukikuza uwajibikaji kwa watoa maamuzi na wapanga mipango na watunga sera.Tunatamani kuona kwenye mipango yao kunakuwa na mikakati thabiti ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na mazingira kwa ujumla.

"Na kwa ngazi ya Taifa FORUMCC tunahakikisha tunafuatilia kwa karibu  bajeti zote zinazohusu mazingira kama zinakuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.Hata hivyo uwepo wa sera na sheria tunaamini utasaidia kuongeza uwajibikaji," amesema Muna na kuongeza "Kwa ujumla tunayo miradi mingi ambayo tunaifanya ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
 Washindi wa pili wa michuano ya Kombe la mazingira kutoka timu ya Kajenjere wakiwa na kombe lao wakionesha furaha yao mbele ya viongozi wa Manispaa ya Ilala na FORUMCC
Msemaji wa Manispaa ya Ilala Tabu Shaibu ( kulia)akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Rebecca Muna wakifurahia jambo baada ya timu ya Abby FC kutangazwa kuwa mabalozi wa mazingira baada ya mashinda Kombe la mazingira

WANANCHI CHIBOLI KUFURAHIA SIKUKUU YA EID EL-FITR NA UMEME

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (kushoto kwa Naibu Waziri), Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga (kulia kwa Naibu Waziri) wakishangilia mara baada ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino. 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akikata utepe kuashiria umeme kufika kwenye Kisima cha Maji katika Kijiji cha Chiboli, wilayani Chamwino. Wa tatu kulia ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na wa Pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga. 
Zahanati katika Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino ambayo imepata umeme kupitia mradi wa BTIP (kV 400) uliosambaza umeme katika Vijiji 121 vinavyopitiwa na mradi huo kutoka Iringa hadi Shinyanga. 
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino. 
…………………………. 

Wananchi katika Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino, Jimbo la Mtera, watasherehekea sikukuu ya Eid El-fitr wakiwa na umeme kwa mara ya kwanza, baada ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu kuwasha umeme katika Kijiji hicho. 
Akiwa ameambatana Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga, Naibu Waziri wa Nishati, amewasha umeme katika Zahanati ya Kijiji hicho pamoja na Kisima cha Maji ambapo Kijiji hicho kimepata umeme kupitia mradi wa BTIP (kV 400) ambao umesambaza umeme katika Vijiji 121 vinavyopitiwa na mradi kutoka Iringa hadi Shinyanga. 
Akizungumza na Wananchi, Mgalu alisema kuwa, kuwashwa kwa umeme katika Kijiji hicho ni muendelezo wa utekelezaji wa adhma ya Serikali ya Awamu ya Tano kufikisha umeme katika Vijiji vyote nchini. 
Amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani mwaka 2015 kulikuwa vijiji takribani 2,018 vyenye umeme ambapo kuanzia Januari 2016, vijiji vipya vilivyoongezeka ni takribani 5000 hivyo hadi sasa vijiji 7,290 vina umeme kati ya Vijiji 12,268. 
Kuhusu usambazaji umeme katika maeneo ambayo hayajapata umeme ingawa yamepitiwa na miundombinu alisema kuwa, kuna mradi wa ujazilizi, mzunguko wa Pili unaolenga kuongeza wigo wa kuunganisha umeme katika vitongoji mbalimbali na Dodoma ni kati ya Mikoa itakayoguswa na mradi huo. 
Naibu Waziri, pia alisisitiza wananchi kutumia vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) ambavyo vitawawezesha kuondokana na gharama za wiring na kuwezesha kuunga wateja wengi katika mradi huo wa BTIP. 
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde alishukuru Serikali kwa kupeleka umeme katika Kijiji hicho, hata hivyo aliomba umeme huo ufike katika maeneo muhimu kama vile shamba la umwagiliaji, nyumba za ibada, na vitongoji vya Kijiji hicho. 
Aidha, aliipongeza Serikali kwa kufanya kazi bila ubaguzi kwani idadi ya watu katika Kijiji hicho si kubwa ukiliganisha na vijiji vingine lakini Serikali haikungalia idadi ya watu hao ili kufikisha umeme katika Kijiji hicho wala hadhi ya nyumba. 
Wilaya ya Chamwino, ina vijiji 107 na vijiji 54 tayari vimesambaziwa umeme huku kazi ya usambazaji ikiendelea kupitia miradi mbalimbali kama REA Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza na BTIP.

TANROADS MANYARA WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

$
0
0
Mkuu wa mipango wa Tanroads Mkoani Manyara, mhandisi Dutu Masele (kulia) na mhasibu Julieth Kyaruzi wakishiriki kupanda mti kati ya miti 100 iliyopandwa na watumishi wa Tanroads Manyara. 
Watumishi wa Tanroads Mkoani Manyara, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupanda miti 100 pembeni ya barabara kuu ya Babati-Singida katika wiki ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani. 
Meneja wa Tanroads Mkoani Manyara mhandisi Bashiri Rwesingisa katikati (mwenye kofia) na watumishi wengine wa Tanroads wakishiriki kusafisha mazingira ya mjini Babati kwenye wiki ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani. 

****************************************** 

MENEJA wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) Mkoani Manyara mhandisi Bashiri Rwesingisa ameongoza wafanyakazi wa mkoa huo kwa kupanda miti 100 na kusafisha mazingira ya Mjini Babati katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani. 

Mhandisi Rwesingisa ameongoza maadhimisho hayo ya siku ya mazingira dunia walioadhimisha kwa siku tano, kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii. Akizungumza mjini Babati, mhandisi Rwesingisa alisema katika maadhimisho hayo kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Tanroads Manyara, wamefanya shughuli mbalimbali za kijamii. 

Alisema wamefanya maandamano ya kufanya usafi, utoaji elimu kwa umma na kuotesha miti katika barabara kuu na za mkoa huo zinazomilikiwa na Tanroads mkoani humo. 

Alisema wamesafisha alama za barabarani na kuondoa zilizoharibiwa na kurudisha alama za barabarani zilizoibiwa au kuharibiwa. 

“Pia wafanyakazi wa Tanroads mkoani Manyara kwenye wiki ya maadhimisho hayo wamepanda miti 100 na mingine 100 inatarajiwa kupandwa pembeni ya barabara kwa lengo la utunzaji mazingira,” alisema mhandisi Rwesingisa. 

Alisema pamoja na kuotesha miti na kufanya usafi wa mazingira katika hifadhi ya barabara pia wamezibua mitaro na kufyeka nyasi kandokando mwa barabara. “Tumefanikisha pia kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari na vipeperushi kuhusu hifadhi ya barabara na utunzaji wa mazingira ya barabara kuu na ya mikoa,” alisema mhandisi Rwesingisa. 

Mmoja kati ya wafanyakazi wa Tanroads mkoani Manyara, Julieth Kyaruzi alisema amefurahia kushiriki kwenye maadhimisho hayo akiwa na watumishi wenzake. 

“Kwa hizi siku nne tumefanya kazi mbalimbali za mikono yetu kwa pamoja katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani kwa hapa hapa mkoani kwetu Manyara,” alisema Kyaruzi.

TAARIFA YA UTEUZI NA KUPANDISHWA VYEO KWA MAAFISA WAANDAMIZI WA UHAMIAJI

Dkt. Gwajima Awakumbuka Yatima, Awapa mkono wa Eid

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy
Gwajima akiwa katika picha ya Pamoja na watoto wa kituo cha matumaini
kilichopo Miuji Jijini Dodoma. 
Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy
Gwajima akifurahia kumbeba mtoto Queen wakati alipotembelea kituo cha
kwatoto cha matumaini kilichopo Miuji Jijini Dodoma. 
Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy
Gwajima akizungumza na mtoto wakati akikagua kituo wakati wa ziara yake
katika kituo cha matumaini kilichopo Miuji Jijini Dodoma. 
Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy
Gwajima akifurahi katika picha ya Pamoja na mtoto Maria wa kituo cha
matumaini kilichopo Miuji Jijini Dodoma. 
Afisa Ustawi wa Jamii toka OR-TAMISEMI anayeshughulikia watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi Nkinda Ziada Shekalaghe akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Dr.Dorothy Gwajima. 
Baadhi ya watoto katika picha ya pamoja wakimskiliza Dr.Dorothy Gwajima
wakati wa ziara yake katika kituo cha matumaini kilichopo Miuji Jijini
Dodoma. 

********************************** 

Atley Kuni, OR- TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Doroth Gwajima amewataka wazazi na walezi kuwa makini na kuimarisha ulinzi na usalama wa mtoto wakati wa msimu sikukuu ya Eid. 

Dr.Gwajima ameyasema hayo alipotembelea kituo cha kulelea watoto cha
Nyumba ya matumaini kilichopo Kata ya Miuji Jijini Dodoma na kutoa misaada ya vitu mbali mbali kwa ajili ya sikukuu. 

“Ni wajibu wa kila mzazi kutekeleza jukumu lake la msingi la kuhakikisha mtoto yuko salama na anasherekea sikukuku katika mazingira rafiki na yenye kumjenga kimwili na kiakili zaidi bila kupata dhahama ya aina yeyote” Alisema Gwajima.

Aidha Dr. Gwajima amekipongeza kituo hicho kwa jukumu kubwa walilo nalo lakuhakikisha watoto waliopo hapo wanapata malezi bora huku akiwaasa watoto kuzidisha upendo na mshikamano miongozi mwao. 

“Tunatekeleza hili kwakuwa ni wajibu wetu kuwalea watoto kwani hata sisi leo tumekuwa watu wazima kwa sababu ya juhudi za wakubwa zetu, nanyi watoto mtakuwa wakubwa kama sisi na mtakuja kuwa viongozi wa taifa hili katika nyanja mbali mbali, hivyo pendaneni na kuishi kwa amani na msome kwa bidii” alisema Gwajima. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya ustawi wa Jamii, OR-TAMISEMI, Rashed Maftah, alisema zoezi hilo ni moja ya majukumu yao ya msingi na wajibu wao katika kuzihudumia Mamlaka zote 184 nchini katika kuhakikisha watoto waliokatika mazingira magumu wanapata vituo vya kuwalea katika misingi bora na usalama wao unaimarika. 

“Dini iliyosafi ni yenye kuwajali Yatima na wenye uhitaji kwa kuunganika na kushiriki nao katika mahitaji yao ya Msingi, aidha Sheria ya mtoto namba 21 ya  mwaka 2009 kanuni ya 12 inahimiza suala la kulelea watoto” Alisema Maftah. 

Akizungumza kwa niaba ya Walezi wa kituo hicho, mmoja ya walezi, Sister Urea, alisema kituo hicho kina jumla ya watoto 63 na kimekuwa kikifanya kazi zake toka mwaka 1995 kwa kuhudumia watoto wanaopatikana katika mazingira magumu na ukatili wa kijinsia kutoka mikoa ya Dodoma na Singida. 

Akishukuru kwa niaba ya wenzake mtoto Mariah Zahoro, alimshukuu Naibu
Katibu Mkuu na ujumbe wake huku akiomba zoezi hili lisiwe la mwisho bali liwe endelevu kwani wanapopata wageni wanao watembelea wanafarijika sana. 

“Tunawashukuru sana kuja kutuona na kutupatia misaada, lakini msiishie kuja kuleta misaada tu, hata kama hamna kitu msisite kuja kutusalimia na kuongea na sisi, tunaomba Mungu awazidishie pale mlipotoa na siku nyingine tena mtukumbuke” alisema Mariah. 

Kwa Mujibu wa Afisa Ustawi wa Jamii kutoka jijini Dodoma, kituo cha Nyumba ya Matumaini kilichopo Kata ya Mihuji ni moja kati ya vituo vinane vilivyopo ndani ya Halmashauri hiyo ambavyo vimekuwa mstari wa mbele kulinda haki za watoto.

Dk. Ndungulile azindua kampeni ya Kilimanjaro Challenge

$
0
0
Meneja wa Kili Challenge Manace Ndoroma (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile (wa tano kushoto), Mkurugenzi wa Tacaids, Dk. Leonard Maboko (wa nne kushoto), Makamu wa rais miradi endelevu wa kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo (watatu kulia) pamoja na viongozi wengi waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2019), na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka 2019 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini. Katika hafla hiyo GGM walikabidhi Tacaids hundi ya Sh bilioni 1.173.
Mkurugenzi wa Makao ya watoto moyo wa huruma – Geita, Sr. Adalbera Mukure akielezea namna kampeni ya Kili Challenge kupitia GGM ilivyonufaisha kituo hicho na kuwezesha watoto zaidi ya 137 wanaolelewa katika kituo hicho kupata huduma mbalimbali ikiwamo elimu. Kulia kwake ni George Emanuel na kushoto ni Rosemarry Emanuel ambao ni baadhi ya watoto waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Kili Challenge jijini Dar es Salaam. 
1. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akizungumza katika uzinduzi wa katika hafla ya uzinduzi wa zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2019), na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka 2019 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini. Katioka hafla hiyo GGM walikabidhi Tacaids hundi ya Sh bilioni 1.173.
Makamu Rais wa Mgodi wa dhahabu Geita (GGM), Simon Shayo (wa pili kulia) akikabidhi hundi ya Sh milioni 150 kwa Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Dk Faustine Ndungulile na Mkurugenzi Mtenda wa Tacaids, Dk. Leonard Maboko. Mchango huo unalenga kudhibiti maambukizi ya VVU kwa kupitia kampeni ya Kilimanjaro Challenge inayoratibiwa na GGM pamoja na Tacaids.


· GGM, Tacaids wakusanya Sh bilioni 1.5 kudhibiti Ukimwi

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile jana 4, June 2019 amezindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2019), na kuendesha harambee iliyowezesha kupatikana zaidi ya Sh bilioni 1.5 fedha zilizochangwa kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini.

Aidha, amesema Serikali inatarajia kupeleka bungeni Muswada wa Sheria wa kushusha umri wa kuridhia vijana kupata huduma zaUKIMWI kutoka miaka 18 hadi miaka 15 ili kupunguza wimbi la maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI (VVU) hususani kwa vijana.

Hatua hiyo imekuja baada ya Tume ya Taifa ya Kuthibiti UKIMWI nchini (TACAIDS)), kubainisha kuwa kwa siku zaidi ya watu 200 hupata maambukizi mapya ya VVU, huku kati yao vijana 80 wenye umri wa miaka 15 hadi 24 pia huambuki kwa siku.

Kilimanjaro Challenge ni mfuko muhimu unaoratibiwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa kushirikisha taasisi za nje na ndani ya nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI.

Dk. Ndugulile akizungumza katika hafla hiyo alisema tatizo la ugonjwa wa UKIMWI linabadilika kila mara hivyo kuchangia zaidi ya asilimia 40 ya vijana kuathiriwa huku asilimia 80 ya vijana hao wakiwa ni vijana wa kike.

“Serikali tumeanza kuliona hilo na kuchukua hatua, hatua ya kwanza kwanza kushusha umri wa kuridhia kwani ni kweli wanaanza kujamiiana wakiwa umri wadogo, takwimu zinaonesha kuanzia wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 19, asilimia 27 ni wajawazito au wana watoto.

“Kwa hali hii ya maambukizi tumeamua kupeleka muswada bungeni kushusha umri wa ridhaa hadi miaka 15. Ili sasa iweze kuruhusu kijana kuweza kupata huduma, kwa sababu kwa sasa inabidi apate ridhaa ya mzazi au mlezi,” alisema Dk. Ndugulile.

Aidha, alisema wizara hiyo italeta mpango wa kuruhusu watu kujipima wenyewe ili kutoa motisha kwa akina baba kupima VVU” 

“Kama ilivyo kwa wanawake wanavyojipima ujauzito na kina baba watahamasika kujipima na naamini litawapa motisha,” alisema.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Dk. Leonard Maboko alisema muswada huo ukipitishwa na kuwa sheria utasaidia vijana kupata huduma zaUKIMWIkwa haraka bila ridhaa ya mzazi au mlezi kama ilivyo sasa.
Alisema hadi sasa Tanzania inao watu milioni 1.5 wenye VVU ambao ni sawa na asilimia 4.7.

“Lakini maambukizo mapya yamepungua kutoka 80,000 miaka mine iliyopita hadi 72,000. Katika kundi hili watanzania 6000 wanapata maambukizo mpaya kwa mwezi na kwa siku ni 200,” alisema.
Aidha, alisema sababu za vijana kupata maambukizo zaidi ni kutoka kwenye utoto kwenda kwenye ujana. 

“Hawajapata elimu sawasawa hivyo inakuwa rahisi kwake kufanya maamuzi ambayo hana taarifa za kutosha. Lakini pia vijana wa kike kutaka kupata vitu kwa haraka.“Ndio maana tuna miradi ambayo inagusa kaya maskini kwa kuwasaidia kupata elimu ya ujasiriamali katika mikoa mitatu,” alisema.

Kutokana na tatizo hilo Makamu wa rais miradi endelevu wa kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo alisema kwa mwaka huu katika kampeni hiyo ya kuchangia afua za UKIMWI wamelenga kukusanya Sh bilioni mbili.

Hata hivyo, alisema hadi sasa tayari wamekusanya zaidi ya Sh bilioni 1.5 sawa na asilimia 67 ya lengo la kampeni hiyo ya mwaka huu ambayo sasa inatimiza miaka 17 tangu kuanzishwa kwake.

Alisema tangu kuanzishwa kwa Kilimanjaro Challenge, zimekusanywa zaidi ya Sh bilioni 13 ambazo zimenufaisha asasi na taasisi mbalimbali 50 zinazoshughulikia masuala ya UKIMWI.“Lengo kuhakikisha maambukizi mapya yanatokomea na kufikia lile lengo la sifuri tatu,” alisema.

Alisema tangu kampeni hiyo ianzishwe watu zaidi ya 800 wamepanda Mlima Kilimanjaro, na mwaka huu wanategemea zaidi ya watu 80 wakiwamo waendesha baiskeli.

Aidha, Mkurugenzi wa Makao ya watoto moyo wa huruma – Geita, Sr. Adalbera Mukure alisema tangu kituo hicho kifunguliwe mwaka 2006 kwa kuwezeshwa na GGM, kimeweza kuboresha maisha ya watoto mbalimbali.
Alisema kituo kimesomesha watoto 18 wa chekechea, shule za msingi, 70, sekondari 29, kidato cha tano na sita 8, vyuo vikuu wawili, mmoja chuo cha walimu, wawili wameajiriwa kwenye sekta binafsi na wawili bado hawajapata ajira.

“Tunaomba michango yenu ili kuwezesha ujenzi wa shule ya English medium ili kuwezesha watoto kusoma na hata watoto wa nje ya kituo kusoma na fedha zitakazopatikana kutumika kuendesha kituo,” alisema.

Meneja wa Kili Challenge Manace Ndoroma alisema bodi ilikaa na kuamua kuwa mwaka huu zitatolewa Sh milioni 800 ambazo kati yake Sh milioni 550 zitabakia kusubiri maombi ya asasi mbalimbali zitakazowasilisha maombi yao.

“Sh Milioni 150 zitaenda Tacaids kujenga vituo vyta huduma za ukimwi. Sh Milioni 50 moyo wa huruma kuwezesha kituo kiuchumi Sh milioni 50 zitakwenda kwa mfuko waUKIMWI (ATF) wakati Sh bilioni 1.173 zilizotolewa na GGM zitaenda Kili Trust Fund,” alisema.

CCM YAWATAKA WAHANDISI WA MAJI KUWA WABUNIFU WA MIRADI ENDELEVU

$
0
0
Mwenyekiti CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba akinywa maji ya moja ya kisima cha Kimbiji na Mpera mapema leo mara baada ya kutembelea miradi ya maji inayoendeshwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) pamoja na kukagua maendeleo yake. Wa kwanza kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo (mwenye tai nyekundu). Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo (kwanza kulia) akitoa maelezo machache kwa kamati ya siasa ya mkoa wa Dar es Salaam. 
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akimaliza kupokea kamati ya siasa ya mkoa wa Dar es Salaam wakati wa ziara kukagua mradi ya DAWASA. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akifafanua jambo. 
Mjenzi wa visima akitoa maelezo machache wakati wa ziara ya Kamati ya siasa ya ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam iliyoongozwa na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba kutembelea miradi ya maji inayoendeshwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) pamoja na kukagua maendeleo yake. 
Mwenyekiti CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) mapema leo Juni 4, 2019 wakati Kamati ya siasa ya ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam ilipotembelea maendeleo ya miradi yao mbali mbali.
Kamati ya siasa ya ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa pamoja na wafanyakazi wakisikiliza. Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza machache mbele ya wafanyakazi wa DAWASA. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja nae akieleza machache.
Bi. Peresi Msonya Mwakilishi wa Wafanyakazi akitoa shukrani. 


Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Wahandisi wa Maji nchini watakiwa kuwa wabunifu wa miradi itakayoliwezesha taifa kuvuna na kuhifadhi maji ya mvua ili yatumike kipindi kijacho. Maji ya Mvua yamekuwa yakipotea hivyo wakiweza namna ya kuyaweka ili yatumike baadae itasaidi kuvusha jamii pindi mito inapokauka. 

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba wakati wa ziara ya Kamati ya siasa ya ya CCM Mkoa wa Dar es salaam kutembelea miradi ya maji inayoendeshwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) pamoja na kukagua maendeleo yake.

 Amesema kuwa ifike wakati mamlaka zinazosimamia maji kuendelea kuwa wabunifu katika uhifadhi maji. Pia amewapongeza DAWASA kwa kusimamia na kufanikisha miradi mbalimbali ya maji kwa fedha za ndani na kuacha kutengemea wafadhili kila kukicha. "Jambo jema sana mnalolifanya nawaomba muendelee na moyo wa kujitoa na kusimamia miradi yenu vyema mnayotumia fedha zenu za ndani, tena kwa uaminifu wa hali ya juu," amesema. 

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amewapongeza DAWASA kwa kuendelea kuamini na serikali kwa kusimamia miradi mikubwa ya usimamizi wa maji Dar es Salaam. Profesa Mkumbo amesema Serikali inaimani na nyie ndiyo maana miradi mikubwa mnapewa ili ni jambo jema hivyo naomba usiiangushe na ikamilishe kwa wakati. Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja amewaomba wafanyakazi kuendelea kufanyakazi kwa bidii ili waweze kusimamia malengo yao vyama. Mhandisi Luhemeja amesema DAWASA ipo kamili kuendelea kuwapa maji wakazi wa Dar es Salaam na Pwani ili kufikia lengo la usambazaji wa maji kwa asilimia 95.

WATANZANIA MILIONI TANO KUPATIWA ELIMU KUHUSU UMUHIMU WA KUTUMIA NISHATI MBADALA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MRATIBU wa Mradi wa kutoa elimu kuhusu muhimu wa  kutumia  nishati mbadala Euphrasia Shayo kutoka FORUMCC amesema wanatarajia kutoa elimu hiyo kwa Watanzania milioni tano ndani ya miezi 20 kuanzia Mei mwaka huu.

Shayo amesema hayo wakati wa maadhimisho ya mazingira ambayo kwa Dar es Salaam yamefanyika Viwanja vya Jakaya Kikwete ambapo wadau mbalimbali wa nishati mbadala wameonesha namna ambavyo wanatengeneza bidhaa ambazo lengo lake ni kuhakikisha Watanzania wanakuwa na uelewa wa kutunza mazingira kwa kutumia nishati mbadala.

Akifafanua zaidi Shayo amesema mradi huo unafanyika chini ya ufadhili wa Hivos ambao wako nchini Finland na kwa kutambua muhimu wa kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi wameona haja ya kuufadhili mradi huo wakiamini ni mradi wenye tija kwa jamii.

"Ni mradi ambao FORUMCC tunautekeleza kwa ufadhili wa Hivos ,lengo letu ni kuwafikia Watanzania milioni tano ambao watakuwa na uelewa wa umuhimu wa kutumia nishati mbadala ili kutunza mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,"

Amesisitiza wanatoa elimu ya nishat mbadaa kama njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kuwa na mazingira endelevu na kwamba mradi huo unawalenga wananchi,Serikali, taasisi za umma na binafsi, taasisi za elimu ya juu na vyombo vya habari ambavyo vinamchango mkubwa wa kufikisha taarifa za mabadiliko ya tabianchi na athari zake.

"Kama ambavyo nimeeleza hapo awali,elimu ambayo tunaitoa ni kwa kutumia njia mbalimbali kama kuendesha mauzo kwa kutumia semina,mijadala,kufanya tafiti pamoja na kufuatilia bajeti ya Wizara ya nishati na wizara zinazohusika na mazingira iwapo wanatalenga fedha kwa ajili ya kuhamasisha jamii kutumia nishati mbadala kama njia ya kutunza mazingira.Faida kubwa kwa Hivos ni kuna dunia inakuwa mahali salama kimazingira,"amesema.

Amefafanua kuwa kabla ya kuanza kwa Bunge wadau wanakutana kwa ajili ya kuangalia bajeti kama imezingatia masuala ya mazingira na kisha kama kuna haja ya kutoa mapendekezo basi wanafanya hivyo kwa kuhakikisha  wanafuata utaratibu unaohitajika kwani FORUMCC wanashirikiana kwa karibu na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali.

Baadhi ya wadau wa mazingira ambao wameshiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya mazingira ambayo FORUMCC wameshirikiana na Manispaa ya Ilala kuifanikisha, wamesema ni vema jamii ikajikita kutumia nishati mbadala kama njia sahihi ya kutunza mazingira.

Ofisa mauzo wa Kampuni ya Mobisol ambao wanauza Sola Wilson Mosses amesema kuna kila sababu ya wananchi kutumia nishati mbadala kama sehemu ya kutunza mazingira huku akifafanua kwa kutumia umeme wa Sola inasaidia kupunguza hewa ukaa ambayo itasababisha kuchafua mazingira."Umeme wa Sola ni marafiki wa mazingira tofauti na kutumia mafuta kusabisha umeme kwani mafuta yanachafua mazingira,".

Amesema kwa sasa kunamuamko kwa watanzania kwani wengi wao wameona kutumia nishati mbadala kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kila na maonesho ya wiki ya mazingira yaliyoandaliwa na FORUMCC yameongeza chachu ya kutumia nishati mbadala nchini Tanzania.
 Baadhi ya akina mama wakiwa wameshika karatasi zenye ujumbe wa kuhamasisha jamii kutumia nishati mbadala ili kinda mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.Kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya Mobisol  Wilson Mosses.
Msemaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Tabu Shaibu(wa pili kushoto) akiwa na  Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Rebecca Muna wakipata maelezo kuhusu namna ambavyo nishati mbadala inavyosaidia kutunza mazingira

 Mratibu wa Mradi wa kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutumia nishati mbadala unaofadhiliwa na Hivos Euphrasia Shayo (kushoto)kutoka FORUMCC akiwa ameshika karatasi yenya ujumbe unaozungumzia nishati mbadala wakati wa maadhimisho ya wiki ya mazingira .Kulia ni Meneja mauzo wa Kampuni ya Mobisol Wilson Mosses ambao wanauza Sola kama nishati mbadala
 Mratibu wa Mradi wa kutoa elimu kuhusu nishati mbadala Euphrasia Shayo kutoka FORUMCC akisaini kitabu baada ya kufika kwenye banda la kampuni ya Mobisol  wanaojihusisha na uuzaji wa Sola kama nishati mbadala .Aliyesimama ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo  Wilson Mosses
 Mariam Tindwa akifafanua jambo kwenye maonesho ya wiki ya mazingira namna ambavyo wanatumia taka kutengeneza nishati mbadala ikiwemo mkaa unaotoka na taka

Prof. Kabudi azungumza na Idara ya Itifaki ya Wizara yake.

$
0
0
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akizungumza na Watumishi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) alipokutana nao kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye nafasi hiyo tarehe 3 Machi 2019. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Prof. Kabudi aliwataka Watumishi wa Wizara kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu miongozo na maelekezo mbalimbali pamoja na kuwa wazalendo na kufanya kazi zao kwa kushirikiana na kwa weledi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Balozi Grace Martin na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Katika Wizara ya Mambo ya Nje. Aidha, mazungumzo hayo ni mwendelezo wa Vikao vya Prof. Palamagamba John Kabudi na Watumishi wa Wizara yake, ambapo yamefanyika katika Ofisi ndogo jijini Dar es Salaam tarehe 04 Juni, 2019 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akutana kwa mara ya kwanza na kiting cha Itifaki cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 
Mkuu wa Kitengo cha Itifaki cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Grace Martini akitoa maelezo ya majukumu ya kitengo hicho kwa Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi alipokutana na Kitengo hicho kwa mara ya kwanza katika ofisi ndogo za Wizara hiyo jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Idara ya Itifaki wakimsikiliza Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi ambaye hayupo pichani alipozungumza nao 
Sehemu nyingine ya Watumishi wakifurahia jambo wakati wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani) 
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye mkutano wao na Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (hayupo pichani). 
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Idara ya Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

TUTUMIE SIKU YA EID KWA KUTENDA MEMA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka waislamu wote nchini watumie siku kuu ya Eid el Fitr kwa kutenda matendo mema pamoja na kuwakumbuka yatima na wajane.

“Leo ni siku kubwa na muhimu waislamu wanahitimisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, hivyo tuendeleze matendo mema.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 5, 2019) wakati aliposhiriki swala ya Eid El Fitr katika msikiti wa Anwar uliopo Msasani jinini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema wakati huu ni mzuri kwa kuimarisha mshikamano miongoni mwenu na madhehebu mengine, hivyo hakikisheni mnayaendeleza mambo mema yote.

“Tumeona utulivu uliojitokeza katika mwezi mtukufu, na jambo hili limesisitizwa na viongozi wa dini. Tuendelee kuwa wamoja, tuimarishe mshikamano na tuvumiliane.”

Pia, Waziri Mkuu amewakumbusha wazazi na walezi kuwaongoza watoto kwa kuwapa mafundisho ya dini yatakayowawezesha kumjua Mwenyezi Mungu na kuwa raia wema.

Awali, Imamu wa msikiti huo, Sheikh Mhina alisema waislamu wanatakiwa kuitumia siku ya leo kwa kuhamasisha Amani pamoja na kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo.

Pia amewasisitiza wayaendeleze mema yote waliyoyafanya katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu na kuwajali wazazi wao.
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images