Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109573 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA ASHIRIKI SWALA YA EID EL FITR MSIKITI WA ANWAR MSASANI JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya kushiriki katika Swala ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 5, 2019. Kulia ni Mwenyuekiti wa Msikiti huo, Sheikh Alhaji, Suleiman Mohammed. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Msikiti wa Anwari uliopo Msasani jijini Dar es salaam, Sheikh Alhaji Suleiman Mohammed wakati alipowasili msikitini hapo kuswali Swala ya Eid El Fitr, Juni 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika Swala ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwari, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Swala ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Bw. Mohammed Iqbal Noray baada ya kushiriki Swala ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watoto baada ya kushiriki Ibada ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam Juni 5, 2019., (Picha na ofis ya Waziri Mkuu)

CBA Bank Tanzania CLIENT IFTAR

0
0




On 30th May, 2019, CBA Bank Tanzania Limited hosted its annual iftar event for their muslim clients, with the guest of honor being H.E Khamis Kigwangala, the Misister for Natural Resources and Tourism.
Thanking the clients for being part of an amazing journey down the years CBA BANK TANZANIA CEO Mr Gift Shoko noted that it is with the commitment of not only the staff but also a strong loyal base of their existing customers that  CBA BANK has had a great year so far and which is posted on a great adoption of technology and customer service.
“We are a bank of the people and  with out you our beloved clients we wouldn’t have been here, I and my team are working tirelessly day and night to make sure that not one client feels out of place. We are among many banks in Tanzania but want to assure our clients that we are a comparison to none because our core focus has not been what other banks are doing but rather more what our clients wants from us. Customer centric approach has and will always be our core in all of the discussion we make, take and plan as for us your our clients are the most important reason why we are here. Demonstrating this we have extended our support not only to our clients but to the society in general by taking part on so many community activities like sponsoring kids from difficult environments to achieve their dreams “ Said Mr Shoko
The guest of honor however was not only impressed but also had a lot of appreciation for the amazing efforts that have been vividly portrayed by this bank. He acknowledge the great deed of effort that is put in place by the bank on providing good banking services but also their engagement to the community.
“ We as a country have so many underprivileged sets of people in the society and depending only on the government to solve all these issues we shall invest a lot of time but with organizations such as CBA bank taking initiatives to give back and support the society as a representative of the government we appreciate and acknowledge this tremendous support and with the government we shall always be available to support on any way we can so as this bank will not only run smoothly under the regulations but also have more reasons to support the unwell communities” said H.E Kingwangalla

C

Maandalizi ya mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yaanza

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akisalimiana na Katibu Mtendaji wa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, Dkt Stagomena Tax kabla ya kuanza kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania August,2019. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam, June 05,2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (katikati) akishauriana jambo na Katibu Mtendaji wa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC Dkt. Stagomena Tax (kulia) wakati wa kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania August,2019,kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam, June 05,2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (katikati) akimsikiliza Katibu Mtendaji wa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC Dkt. Stagomena Tax (kulia) wakati wa kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania August,2019,kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam, June 05,2019
Maafisa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC walioambatana na Dkt. Stagomena Tax wakisikiliza kwa makini mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo nao wakifuatilia kwa makini, katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Grace Martine, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Stephen Mbundi na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Agness Kayola. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb) (katikati) akiongoza  kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania August,2019.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam, June 05,2019


. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mgeni rasmi Baraza la Eid jijini Tanga, awataka waislamu kuendeleza uadilifu

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka waislamu kote nchini waendeleze utulivu, amani na uadilifu waliouonesha katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani kwa kufanya hivyo, watasaidia kukuza umoja wa kitaifa, uchumi na kuboresha huduma za jamii.

Amesema ni vema wakatambua kwamba uadilifu waliouonesha ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni silaha muhimu hususan katika kuimarisha maendeleo na kudumisha haki, umoja, usawa, upendo na utulivu.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Juni 5, 2019)kwenye Baraza la Eid El Fitri, lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Tanga Beach Resort jijini Tanga.“Nawashi sana kuyaenzi mema yote mliyoyafanya kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan’’.

Kadhalika, Waziri Mkuu amezipongeza taasisi za Kiislamu na imani nyingine ambazo zimejenga shule ili kuchangia maendeleo ya elimu kitaifa lakini amesisitiza kuwa bado kuna haja ya kuongeza shule nyingine na vyuo zaidi pamoja na kuziboresha zile zilizopo ili kusaidia jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za jamii nchini

Amesema licha ya juhudi inazozichukua, Serikali peke yake haina uwezo wa kueneza huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji katika kila pembe ya nchi hivyo, inapotokea taasisi za Kiislamu au madhehebu mengine yakaweka mikakati ya kueneza huduma hizo, basi bila shaka Serikali ipo tayari kuunga mkono juhudi hizo na kuchangia ufanisi wake. 

Wakati huo huo, ameitaka BAKWATA ichukue hatua za makusudi katika kuhakikisha huduma nyingi za maendeleo na za kijamii zinaifikia kwenye mikoa mingi zaidi ya pembezoni. “Huu ni wakati muafaka sasa wa kutafakari ni namna gani Watanzania wa maeneo mengine nao watanufaika na uwepo wa huduma mbalimbali kama vile elimu, afya na nyinginezo.“

Kwa upande wake,Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally ametumia fursa hiyo kuwataka waislam wote nchini wabadilike na waache mazoea ili waweze kusonga mbele kielimu na kiuchumi.

Sheikh Zubeir amesema ni vema kwa waislamu wakajiimarisha kiuchumi kwa sababu kutawaondolea changamoto za kuendesha shughuli zao mbalimbali na hivyo watakuwa wamejiletea maendeleo na kuboresha maisha yao.

Mbali na wito huo pia amewataka waislamu wote wahakikishe wanatii mamlaka yaliyo juu yao , viongozi waliopo madarakani wawe wa kiserikali na wa kidini kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa [TAKUKURU], Diwani Athuman amesema ili nchi iweze kuendelea kuwa na amani,  utulivu na usalama watanzania wote hawana budi kuungana pamoja katika kupiga vita vitendo vya rushwa.

"Rushwa ni dhambi kubwa na hukumu yake mbele ya Mwenyezi Mungu ni moto kwa sababu rushwa ni kipingamizi kikubwa cha maendeleo, hivyo tuungane pamoja kupinga rushwa ndani ya nchi yetu kama Rais Dkt. John Magufuli anavyotuongoza."
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Sheikh Abubakar Zuberi Bin Ally, Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga kushiriki katika Baraza la Eid kwenye ukumbi wa Tanga Beach Reort jijini Tanga, Juni 5, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Baraza la Eid kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort jijini Tanga, Juni 5, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Baraza la Eid kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort jijini Tanga, Juni 5, 2019.
 Baadhi ya  Viongozi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Baraza la Eid kwenye ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort  jijini Tanga, Juni 5, 2019
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Baraza la Eid kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort jijini Tanga, Juni 5, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Baraza la Eid kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort jijini Tanga, Juni 5, 2019.

DSTV YAMTAMBULISHA SALAMA JABIR, KUTANGAZA KISWAHILI AFCON 2019

0
0
MultiChoice Tanzania imetambulisha kampeni yao mpya ya Tupogo, ambayo ni maalumu kwa ajili ya mashindano ya Mataifa ya Afrika 2019 ‘AFCON’ nchini Misri kupitia + 255 Global Radio iliyopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Juni 21 ambapo Tanzania ipo kundi C ikiwa na timu nyingine ambazo ni Kenya, Senegal na Algeria. 

Ofisa Masoko wa Multchoice Tanzania, Shumbana Walwa kupitia +255 Global Radio alisema wateja wanaotumia king’amuzi cha DSTV watawapa nafasi ya kuangalia mechi hizo kwa lugha ya Kiswahili, huku kivutio akiwa mtangazaji mpya wa michezo Salama Jabir ambaye atatangaza mpira kwa mara ya kwanza kwa Lugha ya Kiswahili. 

Watangazaji wengine watakaotangaza michuano hiyo kupitia Super Sport ni pamoja na Ibrahim Masoud ‘Maestro’ , Maulid kitenge na Edo Kumwembe, amewaomba watanzania ambao hawatumii DSTV kujipatia king’amuzi ambacho kimeshaunganishwa na kifurushi cha Compact kwa 99,000/- ambacho kifurushi hicho kitakuonyesha mechi zote za michuano hiyo ya AFCON. 
Kwa wakazi wa Dar, piga namba hii 0659070707 utaletewa ulipo pamoja na huduma ya ufundi pia amesema kwa watazamaji wa kawaida wataweza kutazama mechi hizo 52 kupitia kifurushi cha DSTV bomba kwa lugha ya Kiswahili. Pia mchambuzi mkongwe nchini, Masoud Maestro alisema kuwa wamejipanga vilivyo kuja kuwapa watanzania burudani ya uchambuzi mzuri pamoja na kufurahia Lugha adhimu ya Kiswahili.

UNIGLOBE SKYLINK TRAVEL & TOURS, FIRST CAR RENTAL SHINE GLOBALLY

UTEUZI WA WAGOMBEA UDIWANI KATIKA KATA 32 ZA TZ BARA

0
0
Tarehe 31 Mei, 2019, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza kuwa ni siku ya uteuzi wa wagombea katika Uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata Thelathini  na mbili (32) za Tanzania Bara. Uteuzi huo ulifanyika kama ilivyopangwa.

Katika Kata hizo Thelathini na mbili (32), jumla ya wagombea 98 kutoka katika Vyama kumi na nne (14) vya Siasa walichukua Fomu za Uteuzi.  Vyama hivyo ni pamoja na AAFP, UMD, ADA – TADEA, CCK, CCM, CHADEMA, CUF, DEMOKRASIA MAKINI, NCCR - Mageuzi, NRA, SAU, TLP, UDP na UPDP.
Hadi muda wa mwisho wa uteuzi tarehe 31 Mei, 2019 saa 10: 00 jioni kati ya wanachama 98 waliochukua fomu za uteuzi, 41 walirejesha fomu hizo, kati ya hao 27 walikidhi vigezo na kuteuliwa kuwa wagombea. Wanachama wengine watano (5) hawakuteuliwa kuwa wagombea kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kurejesha fomu za uteuzi nje ya muda, kukosa uthibitisho wa malipo ya dhamana na wagombea kuwa na idadi pungufu ya wadhamini.  
Jumla ya wagombea Watano (5) wa nafasi ya Udiwani waliwekewa pingamizi kwa Msimamizi wa Uchaguzi na hivyo kupelekea wagombea wawili (2) kuenguliwa kutoka katika orodha ya wagombea wa nafasi ya Udiwani.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea Rufaa moja (1) kutoka kwa Mgombea Udiwani wa Kata ya Ipole iliyopo Halmashauri ya Wilaya Sikonge kupitia Chama cha Wananchi CUF, na malalamiko kutoka kwa wagombea wa CHADEMA na CUF katika Kata ya Murangi  iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Malalamiko yao ni dhidi ya maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi ya kuwaondoa kwenye orodha ya wagombea udiwani.
Tume katika kikao chake kilichofanyika leo tarehe 4 Juni, 2019 kimetoa maamuzi kama ifuatavyo:-
Kwanza, Tume imekubali rufaa moja ya mgombea Udiwani wa CUF katika Kata ya Ipole Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge na hivyo kumrejesha kuendelea kuwa kugombea katika nafasi hiyo.
Pili, Tume imekubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi katika Kata ya Murangi  iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya kuwaondoa Wagombea wa CUF na CHADEMA katika orodha ya wagombea na hivyo Wagombea kuendelea kuenguliwa kugombea Udiwani.
Katika Uteuzi huu wa Udiwani katika Kata thelathini na mbili (32, jumla ya Wagombea udiwani katika Kata 29 wamepita bila kupingwa, na mgombea wa CUF kutoka Kata ya Kyaitoke Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na mgombea wa ACT –Wazalendo kutoka Kata ya Boma iliyopo katika Halmashauri ya Mji  Mafinga wamejitoa kwenye kinyang’anyiro hicho, hivyo Kata moja (1) ndio itakayofanya uchaguzi hapo tarehe 15 Juni, 2019, kata hiyo ni Ipole Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Kampeni za uchaguzi zimeshaanza kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi na zitaendelea hadi tarehe 14 Juni, 2019 ikiwa ni siku moja kabla ya siku ya Uchaguzi.
Taarifa zaidi kuhusu walioteuliwa inapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya www.nec.go.tz na Ofisi za Tume Makao Makuu.
Imetolewa leo tarehe 4 Juni, 2019.

Dr. Athumani Kihamia

MKURUGENZI WA UCHAGUZI

TPA YAKAMILISHA UJENZI GATI YA MWALONI MUSOMA YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 605

0
0
 
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii, Musoma

Mradi wa ujenzi wa Gati mpya ya Mwalo wa Musoma unaojengwa na Mamlaka ya bandari ,umefikia  katika hatua za mwisho na wakazi wa eneo hilo wameanza kuutumia kwa ajili ya shughuli za kibiashara.

Akizungumza  na Waandishi was Habari mapema leo Mkoani Mara katika ziara ya kutembelea na kutangaza miradi ya Maendeleo iliyopo katika bandari za Ziwa Victoria, Mhandisi wa TPA,Abraham Msina amesema ujenzi huo umegharimu kiasi Cha shilingi Milioni605 .

"Mradi huu ambao ulianza tangu Novemba 2018 na kukamilika Mwaka huu May chini ya kampuni ya Kitanzania ambayo inaitwa Pentel  utaweza kuongeza mapato kwa mamlaka ya bandari na kurahisisha usafiri kwa wakzi wa eneo la Musoma"

Mhandisi Msina amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa Sana kwa Jamii kwani  lengo ni kusaidia upakiaji wa abiria na boti ndogo za mizigo na uvuvi.

Ametaja kuwa hapo awali Wakazi wa la Musoma walikuwa wakipaki vyombo vyao kando tu lakini kwa sasa Kila mtu anaweza kupaki chombo kwa usalama
 Mhandisi wa Mamlaka ya Bandari katika Ziwa Victoria , Abraham Msina akizungumza na Waandishi wa habari juu ya mradi mkubwa wa ujenzi wa gati ya Mwalo wa Musoma mkoani mara
 Moja ya boti zinazopaki katika Gati Mpya ya Mwalo wa Musoma katika mkoa wa Mara ikipakia mizigo katika bandari hiyo iliyojengwa kwa gaharama ya Milioni 605
 Mmoja wa Wakazi wa Musoma David Katikilo akieleza faida zilizopatikana mara baada ya kukamilika kwa mradi huo wa Bandar
 Mhandisi Mjenzi akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa TPA Hatua zilizobakki katika kukamilisha mradi huo wa ujenzi wa bandari mpya ya Mwaloni
Gati ya Mwaloni  Musoma Mkoani Mara inavyoonekana kwa juu mara baada ya kukamilika

WATANZANIA WAISHIO DENMARK,ICS WASHEREHEKEA SIKUKUU YA EID -EL-FITR NA WATOTO WENYE UALBINO

0
0
Shirika lisilo la kiserikali la Investing in Childrean and Societies (ICS Africa) kwa kushirikiana na Watanzania Waishio Denmark,shirika la CIS na familia ya Robert Mugeta iliyopo Marekani wamesherekea Sikukuu ya Eid El-Fitr pamoja na Watoto wenye mahitaji maalumu (wenye ualbino,viziwi na wasioona) waliopo katika bweni la Shule ya Msingi Buhangija 'Kituo cha Buhangija' Mjini Shinyanga.

Wadau hao wa watoto wameungana na watoto hao leo Juni 5,2019 kusherehekea Sikukuu ya Eid kwa kucheza,kunywa,kula pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali ikiwemo sabuni,pipi na biskuti. Akizungumza wakati wa sherehe hizo, Meneja wa Shirika la ICS nchini Tanzania linalohusika na masuala mbalimbali ikiwemo malezi na makuzi bora ya watoto,ulinzi na usalama kwa watoto, Kudely Sokoine Joram amesema wanapenda watoto hivyo furaha yao ni kuona watoto hao wanafurahi kama watoto wengine katika jamii.

 “Tumefanikisha jambo hili kwa kushirikiana na Watanzania wenzetu waishio Denmark,shirika la CIS la Denmark na familia ya Robert Mugeta iliyopo Marekani .Tumekuja hapa kusherehekea na watoto sikukuu ya Eid El Fitr lengo ni kuwafanya watoto hawa wajisikie 
wanathaminiwa,wanapendwa na tunawajali waone kuwa wao ni sehemu ya jamii”,ameeleza Sokoine. 

“Watoto hawa wengi wakiwa ni wenye ualbino wanaishi pamoja hapa Buhangija,tumeona ni vyema kusherehekea nao pamoja tofauti na watoto waliopo majumbani ili kuwapa furaha.Tunaushuru serikali na uongozi wa shule kwa kuturuhusu kujumuika nao. Kwa kweli watoto wamefurahia sana”,amesema Sokoine. 

Sokoine ameongeza kuwa wataendelea kushirikiana na wadau wote wakiwemo Watanzania Hawa waliopo Denmark,Marekani pamoja serikali kuhakikisha wanapata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili shule ya Buhangija ‘Kituo cha Buhangija ikiwemo kuhakikisha watoto hao wanakua salama na kupata Haki zao za msingi ikiwemo mazingira salama. 

“Sisi ICS Africa kwa kushirikiana na marafiki zetu pamoja na wadau wengine tutaendelea kushirikiana na serikali kutatua changamoto zilizopo hapa,Tukio la leo ni hatua za mwanzo za kutengeneza mahusiano lakini Mwenyezi Mungu akitujalia tuna kazi kubwa ya kufanya hapa shuleni siku zijazo”,amesema. 

Aidha amewataka watoto hao kuwa watiifu,kufuata maelekezo wanayopewa na walimu na kusoma kwa bidii,kushirikiana na kuwapenda wenzao ili waweze kutimiza ndoto zao. Kwa upande wao,watoto hao wameeleza kufurahia ujio wa wadau hao huku wakizitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni ukosefu wa fensi na taa kwenye mabweni mapya yaliyojengwa hivyo kuomba wadau kujitokeza kuwasaidia.
Meneja wa Shirika la ICS Africa Tanzania Kudely Sokoine Joram akizungumza na watoto wenye ualbino,wasioona na viziwi katika bweni la Shule ya Msingi Buhangija wakati wa kusherehekea Sikukuu ya Eid - El-Fitr leo Juni 5,2019. Sherehe hiyo imeandaliwa na shirika la ICS kwa Kushirikiana na Watanzania waishio Denmark na Marekani - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Meneja wa Shirika la ICS Africa Tanzania Kudely Sokoine Joram akizungumza na watoto wanaoishi katika bweni la Buhangija.
Meneja wa Shirika la ICS Africa Tanzania Kudely Sokoine Joram na watoto wakizungumza live kwa njia ya simu 'Video Call' na Watanzania waishio Denmark ambao hawajafanikiwa kufika Buhangija kusherehekea Sikukuu ya Eid El-Fitr pamoja na watoto.
Kulia ni Meneja wa Shirika la ICS Africa Tanzania Kudely Sokoine Joram akikabidhi zawadi ya sabuni za kufulia maboksi nane kwa ajili ya watoto hao.
Watoto wakishindana kucheza muziki.
Meneja wa Shirika la ICS nchini Tanzania Kudely Sokoine Joram akicheza wimbo wa Diamond Platnmuz 'Tetema' na Watoto.
Meneja wa Shirika la ICS Tanzania Kudely Sokoine Joram akitoa zawadi ya pipi kwa watoto waliocheza muziki.
Afisa Huduma kwa jamii kutoka Idara ya huduma za uangalizi,Wizara ya Mambo ya Ndani, Monica Dawa akigawa juisi kwa watoto.
Zoezi la kugawa zawadi likiendelea.
Watoto wakilishukuru shirika la ICS na Watanzania waishio Denmark,shirika la CIS na familia ya Robert Mugeta iliyopo USA kwa kusherehekea nao pamoja sikukuu ya Eid El- Fitr na kueleza changamoto ya ukosefu wa fensi na taa kwenye mabweni mapya. 
MC wakati wa sherehe hizo,Mwalimu Jackson Leonard akitoa neno la shukrani kwa shirika la ICS na Watanzania waishio Denmark,shirika la CIS na familia ya Robert Mugeta iliyopo USA.
Mwalimu mlezi wa watoto hao,Flora Gelard akizungumza na kueleza changamoto walizonazo kuwa ni kukosa ajira hivyo wanafanya kazi kwa kujitolea zaidi.
Ugawaji chakula kwa watoto ukiendelea. Nyama ya kuku,nyama ya ng'ombe,pilau,chips,matunda,maji,soda kama kawaida.
Afisa Huduma kwa jamii kutoka Idara ya huduma za uangalizi,Wizara ya Mambo ya Ndani, Monica Dawa akiwafungulia soda watoto huku wakiendelea kula chakula.
Huku Meneja wa Shirika la ICS Africa Tanzania Kudely Sokoine Joram akigawa soda upande mwingine Afisa Huduma kwa jamii kutoka Idara ya huduma za uangalizi,Wizara ya Mambo ya Ndani, Monica Dawa akifungua soda.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija.
Picha ya pamoja baada ya sherehe : Kikosi kilichofanikisha maandalizi ya sherehe za sikukuu ya Eid El Fitr kwa watoto wenye ualbino,wasioona na Wasiosikia katika bweni la Buhangija mjini Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Mkuranga yapewa elimu ya ufugaji bora

0
0
Ili kupunguza umaskini kwa mwananchi mmoja mmoja na kuwainua kiuchumi halmashauri ya mkuranga kwa kushirikiana na wizara ya mifugo na uvuvi imeendesha mafunzo ya siku moja ya ufugaji kwa wafugaji wa wilaya hiyo yatakayo wawezesha kujitegemea kiuchumi,na kufanya nchi iweze kufikia uchumi wa kati wa viwanda.


Akifungua mafunzo hayo leo katika ukumbi wa Flex Hotel Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Hamisi Ulega(Mb) aliwataka washiriki wawe watulivu na wasikivu na kuwa mabalozi wa nzuri kule waendapo.

Aidha Ulega aliwataka wananchi wa Wilaya ya Mkuranga kuyatumia mafunzo hayo ya ufugaji wa kisasa vizuri ili yalete tija na hatimaye wajikwamue kiuchumi sambamba na kupaisha mapato ya Halmashauri ya Wilaya na nchi kwa ujumla.

Ulega pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina kwa kuichagua wilaya hiyo ambayo yeye ni Mbunge kutoa elimu ya ufugaji bora. “Nawaomba mtumie fursa hii vizuri kujikwa mua kiuchumi na yasiishie hapa mkawape elimu na wengine.” Alisema ulega

“Naomba niwaambie mafunzo haya hatujaanza kutoa hapa tumeshatoa katika Wilaya mbili ikiwemo Simanjiro mkoani Manyara na Kaliuwa Mkoani Tabora lengo ni kutoa elimu na kuwajengea uwezo wananchi juu ya ufugaji bora wa kisasa.”alisema

Hata hivyo ulega aliwataka wananchi kujikita kwenye ufugaji kama mbadala wa kilimo cha korosho , huku akishukuru wizara kwa kuichagua wilaya hiyo kuwa kituo cha uksanyaji maziwa kwa kanda sambamba na kiwanda cha chakula cha mifugo ambacho malighafi yake ni mihogo.

Alisema kituo hicho cha ukusanyaji wa maziwa kitakuwa na uwezo wa ukusanyaji wa maziwa kuanzia lita elfu tano mpaka elfu kumi kwa siku hivyo ametoa wito kwa wananchi kufuga kwani soko lipo

Hata hivyo Ulega amewatoa hofu wananchi kuhusu mtaji na kusema kuwa wilaya imejipanga vizuri wanachotakiwa ni kuunda vikundi ili waweze kupatiwa mikopo kwani kuna fursa nyingine ya ujio wa Benki ya kilimo ambayo itakopesha vikundi vya wafugaji na wavuvi kwa masharti nafuu

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mhandisi Mshamu Munde alishukuru ujio wa wataalamu toka wizarani hiyo akiweka bayana viwango vya ardhi ya kutosha vilivyopo katika halmashauri hiyo kwa ajili ya viwanda mbalimbali vinavyotoa fursa kwa wakulima na ufugaji.

Akizungumza wakati wakufunga mafunzio hayo Mkuu wa wilaya ya Mkuranga,Filbeto Sanga alisema anaishukuru wizara kwa kuleta mafunzo hayo kwani inawezekana ikawa muorobaini wa wafugaji kahamhama na kupunguza migogoro ya wakulima na wafuaji katika wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega(Mb)akizungumza na waanchi wa wila ya Mkuranga leo wakati wa kufungua mafunzo ya ufugaji bora yaliyo fanyika katika ukumbi wa Flex Wilayani Mkuranga mkoani Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkufanga, Mhandisi Mshamu Munde akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo ambapo alishukuru ujio wa wataalamu toka Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwa kutowa mafunzo ya ufugaji bora.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega(Mb) akisaliamina na wananchi,viongozi na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani mara baada ya kuwasali katika ukumbi wa Flex kwa ajili ya kufungua mafunzo ya ufugaji bora.
Mratibu wa Dawati la sekta Binafsi kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi,Stephen Michael akifafanua jambo katika mafunzo ya ufugaji bora aliyo fanyika katika ukumbi wa Flex Hotel Wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Baadhi ya wananchi na viongozi na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani wakimsikilza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah 

Ulega(Mb) hayupo pichani alipo kuwa akufungua mafunzo ya ufugaji bora yaliyo fanyika katika ukumbi wa Flex leo Wilayani Mkuranga mkoani Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

RC NJOMBE AKABIDHI TUZO UHIFADHI WA MAZINGIRA MIKOA YA IRINGA , NJOMBE NA MBEYA AAGIZA WATENDAJI WAZEMBE KUWAJIBISHWA

0
0

Na Francis Godwin, Njombe 

MKUU wa mkoa wa Njombe Chistopher Ole Sendeka ameagiza wakuu wa kuwachukulia hatua kali watendaji wa kata ambazo zimeshindwa kurejesha fomu zilizotolewa kwa watendaji wa kata zote za mikoa ya Iringa , Njombe na Mbeya kwa ajili ya ushiriki wa tuzo ya hifadhi za Taifa (TANAPA) hifadhi ya Ruaha tuzo ya kuhifadhi mazingira mwaka 2019.

Akizungumza jana katika kijiji cha Magoye wilayani Makete mkoani Njombe wakati wa kilele cha shindano la tuzo za Tanapa ya kuhifadhi mazingira kwa mwaka 2019 , mkuu huyo wa mkoa alisema lengo la kuanzisha tuzo hizo ni utekelezaji wa agizo la serikali ya awamu ya tano chini ya rais Dkt John Magufuli hivyo kitendo cha baadhi ya watendaji kukwamisha zoezi hilo ni kosa na lazima hatua kali zichukuliwe dhidi yao .

Alisema kuwa pamoja na taarifa za waandaaji wa tuzo hizo kuonyesha idadi ya washiriki wa shindano la tuzo hizo imezidii kuongezeka ila kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi kushindwa kufikishiwa fomu za shindano hilo kutoka kwa watendaji wa kata ambao walikabidhiwa fomu ili kuzigawa kwa wananchi wote jambo ambalo ni ukiukaji wa agizo la serikali la utunzaji wa mazingira nchini .

“ Kwa kuwa fomu hizi zimetolewa kwa watendaji wa kata zote za wilaya za Mbarali , Makete , wanging’ombe , Kilolo na Mufindi lengo lilikuwa ni kuona wananchi wa kata zote wanashirikishwa kikamilifu katika shindano hilo ila yapo malalamiko kuwa wananchi baadhi wameshindwa kufikishiwa fomu hizo na baadhi ya watendaji sasa naagiza wakuu wa wilaya kuwatafuta watendaji hao ambao wameshindwa kufikisha fomu hizo kwa wananchi na kuwachukulia hatua ili iwe fundisho kwa wakati mwingine kwa kila mmoja kutekeleza agizo la uhifadhi wa mazingira na mimi katika mkoa wangu watendaji hawa nitataka wachukuliwe hatua “ alisema ole Sendeka.

Alisema kuwa suala la uhifadhi wa mazingira si suala la mchezo wala la utani kwani kila mtanzania ni mhifadhi na jitihada zinazoonyeshwa na serikali chini ya rais Dkt Magufuli ambae yeye na makamu wake wa rais ni wahifadhi namba moja hivyo lazima kila mmoja kuunga mkono jjitihada hizo kwa kushiriki utunzaji wa mazingira .

“ Mheshimiwa rais wetu Dkt Magufuli kama mhifadhi mazingira namba moja kazi hii amemkabidhi makamu wa rais mama Samia Suluhu Hassan ambae kila mmoja amekuwa akishuhudia kazi kubwa ambayo amekuwa akiifanya ikiwa ni pamoja na kutuita wakuu wa mkoa wote wa mikoa ya nyanda za juu kusini pamoja na wakuu wa wilaya ili kuokoa Ikolojia ya mtu Ruaha mkuu hivyo hatuna mchezo na kazi hii “ alisema mkuu huyo wa mkoa.

Alisema kuwa kilimo endelevu ,uvuvi endelevu na uvunaji miti endelevu vyote vinawezekana iwapo kila mmoja atachukua jukumu la kuwa mhifadhi wa mazingira yanayomzunguka katika maeneo yake na suala la ushirikishwa wa wananchi kwenye tuzo hizo za Tanapa ni jukumu la viongozi wote wa vijiji na kata .

Aidha aliwapongeza wakuu wa mikoa ya Iringa , Mbeya na wakuu wote wa wilaya hizo na wakurugenzi ambao kwa pamoja wamefanikisha maeneo yao kushiriki tuzo hizo nakushindwa kwa miaka yote mitatu mfululizo toka kuanzishwe kwa shindano la tuzo hizo za uhifadhi wa mazingira na kutaka uhamasishaji kuendelea zaidi ili idadi ya washiriki idizi kuwa juu .

Meneja wa Miradi ya Ujirani Mwema wa TANAPA , Ahmed Mbugi alisema kuwa mpango wa tuzo hizo ulianza kutekelezwa mwaka 2016 katika wilaya tano za mikoa ya Iringa , Mbeya na Njombe na kuwa na washiriki 56 ,mwaka 2017 idadi ya washiriki iliongezeka na kufikia jumla ya washiriki 171 ,mwaka 2018 washiriki 245 na mwaka huu 2019 idadi imeongezeka zaidi na kufikia washiriki 680.

Alisema washirikiki waliojitokeza ni watumiaji maji ,shule , serikali za vijiji ,watu binafsi pamoja na taasisi binafsi zinazofanya kazi ya uhifadhi wa mazingira, utoaji elimu na upandaji miti ya uhifadhi wa misitu ya asili ,uhifadhi wa ardhi na uhifadhi wa mazingira na wanyamapori .

Hata hivyo alisema pamoja na TANAPA kuwezesha shindano hilo pia wadau mbali mbali wamekuwa wakijitokeza kuwezesha ambao ni halmashauri ya Kilolo, Mufindi, Makete ,Mbarali , wanging’ombe na washirika wengine kama Regrow Tanzania , shirika la mazingira Duniani (WWF) malihai Club of Tanzania Nyanda za juu kusini bonde la maji Rufuji .

Pia vyombo vya habari ambavyo vimeweza kutoa mchango mkubwa katika kuhamasisha jamii kutambua na kushiriki tuzo za uhifadhi wa mazingira .

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa katika kilele cha utoaji tuzo hizo mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema kuwa mkoa wa Iringa umejipanga kuendelea kuhifadhi mazingira na tayari umekuwa ukitekeleza maagizo mbali mbali ya serikali katika utunzaji na uendelezaji wa mazingira .

Aidha alisema suala la elimu ya utunzaji wa misitu imeendelea kutolewa na kutoa elimu ya wananchi kuepuka uchomaji moto misitu pia kuhamasisha wananchi kuendelea kutumia mifuko mbadala badala ya kutumia mifuko ya rambo isiyo rafiki na mazingira .

Mwandamizi mratibu wa tuzo ya TANAPA hifadhi ya Ruaha katika uhifadhi wa mazingira mwaka 2019 Yassin Sharif ambae ni aliwataja washindi wa kwanza kwa kila wilaya ambao walikabidhiwa cheti pamoja na hundi ya shilingi milioni 2 kuwa ni Lenatusi Sublime kutoka kijiji cha Wotalisoli wilaya ya Kilolo , kijiji cha Ugute wilaya ya Mufindi , Jumuiya ya watumiaji maji Mbumtilu wilayani Wanging’ombe , shule ya sekondari Mengele wilaya ya Mbarali na kwa wilaya ya makete ni Shule ya sekondari Mlondwe .

Wakati washindi wa pili ambao walipata hundi ya shilingi milioni 1.5 na cheti kutoka wilaya ya Kilolo ni kijiji cha Ikula , wilaya ya Mufindi Kikundi cha Igomaa, wilaya ya wanging’ombe Atukuzwe Erasto , wilaya ya Mbarali Ambokile Twikasyege na wilaya ya Makete ni Jacob Sanga .

Washindi wa tatu katika kila wilaya ambao walizawadiwa cheti na hundi ya shilingi milioni 1 kila mmoja kwa wilaya ya Kilolo ni kamati ya maliasili na mazingira kijiji cha Msosa , wilaya ya Mufindi shule ya msingi langamoto , wilaya ya wanging’ombe Kijiji cha Makoga , wilaya ya Mbarali Jumuiya ya watumia maji mto Mbarali na wilaya ya akete ni kijiji cha Ikuwo .


Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiindi wa tuzo za uhifadhi mazingira na waratibu na viongozi mbali mbali


Mwakilishi wa  kituo cha Radio  Ebony  FM  Maregesi Gilsoni akikabidhiwa  cheti  na mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher  Ole Sendeka

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MWANAMWEMA SHEIN ATOWA MKONO WA EID FITRY KWA WAZEE WA SEBLENINA WELEZO NA WATOTO WA SOS NA MAZIZINI ZANZIBAR

0
0


MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasalimia na kutowa Mkono wa Eid Fitry Wazee wa Kijiji cha Welezo Unguja Wilaya ya Magharibi A Unguja, alipofika kuwatembelea leo 5-6-2019.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsalimia na kumpa Mkono wa Eid Fitry Mzee wa Kijiji cha Wazee Welezo Zanzibar Mzee. Kasuka Mwanakere, alipofika kuwatembelea leo na kutawa Mkono wa Eid Fitry, baada ya kumalizika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsalimia mmoja wa Wazee wanaoishi katika nyumba za Wazee Welezo Zanzibar Mzee. Ramadhani Mussa ,a kumpa mkono wa Eid Fitry.leo alipofika kuwatembelea.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza Kiongozi wa nyumba za Wazee Welezo Zanzibar Sister Gemma Rodrigues, alipofika katika makaazi yao kuwatembelea na kutowa mkono wa Eid Fitry.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico akizungumza wakati wa hafla ya kutowa mkono wa Eid Fity kwa Watoto hao alipofika katika makaazi yao kuwatembelea leo.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mwanamwema Shein, akitowa Mkono wa Eid Fitry kwa Watoto Wanaoishi Nyumba ya Watoto wa Serikali ya Mazizini Zanzibar alipofika kuwatembelea.(Picha na Ikulu)

Tanzania Nchi ya 34 Africa Kupiga Marufuku Mifuko ya Plastiki

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 6,2019

MRATIBU MISS ILALA AKEMEA WAREMBO WANAONESHA MAUNGO YAO JUKWAANI MAKUSUDI

0
0
     *Hatutasita kukemea washiriki watakaosababisha maungo yao kuonekana kimakusudi.

Na.Khadija seif,Globu ya jamii
 
MCHAKATO wa kumsaka mlimbwende wa wilaya ya ilala umefunguliwa rasmi jijini Dar es salaam.

Akizungumza na michuzi tv mratibu wa mashindano hayo Lucas  Rutainurwa amesema mashindano hayo yamefunguliwa rasmi hivyo warembo wajitokeze kuchukua fomu kwa ajili ya kitambulika kama washiriki katika kinyang'anyiro hicho.

"Fomu zinapatikana na kwa mwaka jana tumefanya mapinduzi mengi mazuri kwani tuliweza kutoa kumi bora ambao walishiriki katika kinyang'anyiro cha nchi (miss Tanzania),"

Hata hivyo ameeleza kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mwanzo mwa mwezi julai mwaka huu na mshindi wa kwanza atajipatia kitita cha fedha 1000,000 na wapili 5000,00 huku mshindi wa pili

"Vigezo kwa mshindi vipo wazi cha kwanza aweze kupita jukwaani na vazi la ubunifu ambalo halitaweza kuonyesh maungo yake ya ndani, ulimbwende sio kuonyesha maungo ni kupotosha jamii hatutasita kulikemea jambo hilo.

Aidha,ametaja nidhamu ya hali ya juu, ufahamu wa kujieleza ,kuwa na  mtanzania vikiwa ni vigezo ambavyo vitaweza kumpa nafasi mlimbwende kushiriki kikamilifu shindano hilo.

Pia ametoa rai kwa makampuni kujitokeza kudhamini mashindano hayo kwani ni moja ya kuwapa fursa wasichana wakitanzania kujitangaza kimataifa na kuonekana vioo katika jamii na mfano wa kuigwa kupitia kazi za wanamitindo.

Kwa upande wake mshindi wa pili wa mashindano hayo Sheila Rajab amesema kupitia mashindano hayo amejifunza vitu vingi,kuishi na washiriki wengine,kujua tabia zao,kukutana na wabunifu wakubwa mbalimbali.

"Kitu ambacho watu wengi hawafahamu ni kuwa huwezi kufika mlimbwende wa dunia bila kupitia hatua za chini ikiwemo mlimbwende wa wilaya hadi mkoa ",

Aidha amewaomba wasichana wenye vigezo wajitokeze kwa wingi ili kushiriki.


WATANZANIA WASHAURIWA KUTENDA MEMA NA KUSAIDIA MAKUNDI MAALUM YA KIJAMII

0
0
Diwani wa Kata ya Buza James Mkude Mwenye sharti jeusi na Mwenyekiti wa Jogging wilaya ya Temeke Mussa Mtulia wakiwa katika picha zenye matukio tofauti baada ya kushiriki katika chakula cha pamoja na kutoa zawadi mbalimbali kwenye kituo cha UMRA cha kulea watoto yatima kilichopo Yombo Buza Mtaa wa mashine ya maji Kata ya Buza leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Jogging Wilaya ya Temeke Mussa Mtulia na Diwani wa Kata ya Buza James Mkude wakitoa nasaha zao Mara baada ya kushiriki katika chakula cha pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha yatima cha UMRA,ambacho kipo Mtaa wa Mashine ya maji Kata ya Buza.


WATANZANIA wameshauriwa wakati wote kutenda mema na zaidi kusaidia makundi Maalum pamoja na watoto yatima kwani kufanya hivyo Ndio sehemu ambayo inaweza kusaidia kukutanishwa na Mungu. 

Ushauri huo umetolewa Dar Es Salaam leo na Diwani wa Kata ya Buza Manispaa ya Temeke James Mkude Baada ya kushiriki katika kula chakula cha pamoja kwenye kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika Mazingira magumu cha UMRA kilichopo Mtaa wa Yombo mashine ya maji ikiwa sehemu ya kusherekea sikuku ya Idd. 

Diwani wa (CCM)ambaye alikua na Mwenyekiti wa Chama cha Jogging Wilaya ya Temeke ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasimi Mussa Mtulia ,James Mkude alisema katika wakati kama huu ndio muda muafaka wa kufanya jambo kwa ajili ya makundi Maalum ikiwa pamoja na yatima na alichokifanya kiongozi huyo wa Jogging ni cha kupongezwa. 

“Haya yaliyoliyofanywa na Mwenyekiti Mtulia kwa ajili ya watoto wetu hawa ni mfano wa kuigwa kwani ameacha kukaa na familia Siku kama hii ya sikuku lakini ameamua kuja Kula chakula pamoja na yatima pamoja na kutoa sadaka yake hapa ” amesema Diwani mkude 

Pia aliwataka viongozi wa Kata hiyo Chama na Serikali .kujenga tabia ya kutembelea kwenye Vituo vya watoto yatima ili kujua Mazingira na namna wanavyokabiliana na changamoto mbalimbali. 

Katika kuhakikisha watoto hao wanapata huduma bora alifanya harambee ya kuchangisha Fedha ambapo zilipatikana jumla ya shilingi laki 110,000 ambazo zitumika kununua gas pamoja na mahitaji mengine. 

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Jogging wilaya ya Temeke Mussa Mtulia,alisema kuwa pamoja na kushiriki katika vikundi vya kimichezo lakini pia wanashiriki katika kusaidia yatima na hata watoto wanaoishi kwenye Mazingira Magumu. 

Amesema awali wazazi na Jamii walichukulia kama Jogging ni sehemu ya mambo yasiyofaa katika Jamii lakini ukweli michezo ni ajira,Afya,na tangu wameazisha mifumo hiyo matunda yanaonekana. 

“Katika haya ambayo tunayafanya hata Serikali imekuwa ikiunga mkono haya tunayoyafanya na wanametambua rasim na ndio maana hata wanapomaliza kufanya matembezi mwisho wasiku wanashiriki katika shughuli za kijamii..” Amesema Mtulia 

Pia alisema Mbali na.michezo lakini wamekuwa wakishiriki upandaji miti ,kufanya shughuli za usafi hivyo vijana na wazazi wasifikiri kwamba yanafanyika mambo ya hovyo nakwamba wanashiriki katika Jamii kama walivyofanya jana katika kituo hicho cha watoto yatima cha UMRA . 

Naye Mlezi wa watoto hao na mmliki wa kituo hicho Rahma Juma alishukuru viongozi hao huku akibainisha baadhi ya changamoto ambazo anakabiliana nazo ikiwa pamoja na ukosefu wa sare za shule kwa watoto,pamoja na mambo mengine,nakutumia fursa hiyo kuomba misaada zaidi.

Usajili John Stephen Akhwari nternational marathaon waanza

0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

ZOEZI la usajili kuelekea mashindano ya mbio za riadha ya John Stephen Akhwari International Marathoni limeanza ,huku mbio hizo zikitarajiwa kufanyika Juni 9 mwaka huu.

Mbio hizo za wazi za kilomita 21,kilomita 5 na km 2 ambazo zitafanyika katika uwanja wa Kumbu kumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa zinatarajiwa kushirikisha zaidi ya wanariadha 1500 kutoka ndani na nje ya nchi .

Mkurugenzi wa mbio hizo Sylvester Orao ameliambia Championi ijumaa kuwa zoezi la usajili limeanza katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa na kuwaomba wanariadha wote wanaotarajia kushiriki wafike kujiandikisha tayari kabisa kwa mbio hizo na kuongeza kuwa garama uandikishaji ni shilingi elfu kumi na tano.

“ Ndio mara ya kwanza mbio zetu kufanyika naamini zitapata uzoefu mkubwa lakini pia wapo wadhamini ambao wametuunga mkono mpaka sasa kuhakikisha mbio hizi zinafanyika kwa ubora uliokusudiwa,”alisema Orao.

Alisema tayari washiriki kutoka nje ya nchi wameanza kujiandikisha kwa njia ya mtandao ikiwa ni kutoka katika nchi za Kenya Cameroon,Nigeria,Uholanzi ,Marekani na Uingereza huku washiriki kutoka ndani ya nchi mikoa ya Morogoro,Mtwara,Dar es salaam,Tanga,Kilimanjaro na Manyara pia wamethibitisha kushiriki.

Zawadi kwa washindi wa kilomita 21 kwa wanawake na wanaume ,mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi laki nane,mshindi wa pili atapata laki sita na mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi laki nne huku mshindi wa nne hadi wa kumi zawadi za fedha pia zitatolewa.

Mbali na zawadi kwa washindi wa km 21 pia washindi wa km 5 kuanzia namba moja hadi sita atapata fedha taslimu,huku medali za dhahabu zikitolewa kwa wale watakaokimbia km 21,shaba kwa km 5 pia vyeti vya uthibisho wa ushiriki utatolewa.

Akizungumzia suala la vibali kwa wanariadha watokao nje ya nchi liko pale pale kwani hata shirikisho la Riadha nchini(RT) linahimiza wote wanaotoka nje ya nchi waje na vibali kutoka katika vyama vyao ili waweze kushiriki.

Alisema lengo la mashindano ni kumunzi mwanariadha wa zamani alieiletea Tanzania heshima mwaka 1968 katika mashindano ya Olimpiki ya Mexico mzee John Stephen Akhwari ambae licha ya kuumia mguu katika mashindano hayo lakini alipambana na kumaliza mbio na kufanikiwa kuweka historia katika mashindano ya Olimpiki
Mkurugenzi wa mbio za John Stephen Akhwari International Marathoni Sylvester Orao akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani).

WANAFUNZI WAJERUMANI WAFUNDISHA KWA KUJITOLEA TARANGIRE

0
0
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Fachakademien cha nchini Ujerumani wakiwa kwenye shule ya Tarangire Pre and Primary English Medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, ambapo wanafundisha kwa kujitolea.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya awali na msingi Tarangire ya mjini Babati Mkoani Manyara wakiwa kwenye mazingira ya shule hiyo.


KATIKA kushiriki mafunzo kwa vitendo wanafunzi wa chuo kikuu cha Fachakademien wa nchini Ujerumani wamejitolea kuwafundisha wanafunzi wa shule ya Tarangire Pre & Primary English Medium ya Mjini Babati Mkoani Manyara, kwenye kufanikisha ushirikiano na mahusiano mema. 

Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Tarangire, Eva Mrutu akizungumza jana alisema wamefarijika kupata ugeni huo kutoka nchini Ujerumani ambao kwa namna moja au nyingine wamewaongezea ujuzi wanafunzi wao. 

Mrutu alisema wageni hao kutoka Ujerumani wamewafundisha wanafunzi wao mambo mapya ambayo walikuwa hawajafundishwa. 

“Wanafunzi wetu wamefurahi kupata mambo mapya ikiwemo michezo na nyimbo mbalimbali ambazo hawakuwahi kuziimba ila zimewaongezea morali ya kusoma zaidi” alisema Mrutu. 

Mmoja kati ya wanafunzi hao wa chuo kikuu cha Fachakademien Rebecca Steve alisema hii ni mara yake ya kwanza kufika Tanzania na amefurahishwa na ukarimu ulioonyeshwa kwao. 

“Tutarudi, tena hapa nchini Tanzania kwani watu wake ni wakarimu, wema na wenye upendo kwa wageni kwa hakika tunefurahi mno kufika hapa shule ya Tarangire,” alisema Rebecca. 

Mwanafunzi wa darasa la nne kwenye shule hiyo ya Tarangire, Jackline Peter alisema walimu hao kutoka nchini Ujerumani walimfundisha kuchora na kuchanganya rangi. 

Mwanafunzi wa darasa la tatu Philipo Tabari alisema alifurahia nyimbo mpya walizofundishwa ikiwemo wimbo wa tembo ni mnyama mzuri. 

Mwalimu wa kitengo cha masoko, Judith Misana alisema shule yao ipo kwenye miteremko ya mlima Kwaraa mjini Babati barabara kuubya Mamire karibu na chuo cha Veta Manyara. 

“Wazazi na walezi tinawakaribisha wote waleteni watoto wapate elimu nzuri hapa kwetu Tarangire kupitia kauli mbiu ya shule yetu ya juhudi katika kutafuta elimu na Mungu,” alisema Misana. 

Alisema shule hiyo ina wana walimu wazuri wenye kufundisha masomo bora, mabasi ya kusafirisha wanafunzi kila siku, vyakula vizuri wanavyolima wenyewe na sehemu nzuri za kulala.

WANAFUNZI WA JESHI LA UWOKOVU WAFURAHIA ‘OUTING’ YA TVP BAGAMOYO

0
0

Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Jeshi la Uwokovu wamefurahia safari yao ya kwenda kutembelea sehemu za mji wa kihistoria wa Kaole uliopo mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani, ikiwa sehemu yao ya kujifunza kwa vitendo walichokisoma darasani kwa kipindi cha miaka 7 kabla ya kumaliza elimu yao ya shule ya msingi miezi michache ijayo.

Wakiambatana na wafanyakazi wa True Vision Production (TVP) waliofadhili safari hiyo ya sehemu ya kujifunza kwa vitendo (study tour), wanafunzi hao wamesema wamepata faraja sana kupata ufadhili wa safari hiyo.

Kilichowafurahisha  zaidi ni wafanyakazi wa TVP kujumuika nao, kuwahudumia wale wenye ulemavu wa viungo na kula nao pamoja chakula cha mchana.
Wakiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzao, Noah Michael (15) amesema wamejifunza biashara ya utumwa ilivyoanza Pwani ya Afrika ya Mashariki, kikubwa zaidi akiwaomba TVP kuendelea kujitolea kwa wanafunzi wenye uhitaji.

“Tumejifunza mambo mengi, tumefurahia pia chakula kitamu, kikubwa zaidi TVP tumekuwa nao katika matembezi yetu, wametuletea chakula mezani na kuwa sehemu ya walezi wetu,” amesema Michael.
Naye Joyce Mahona (14) , mwenye ndoto ya kuwa daktari, amesema amejifunza jinsi watumwa walivyokuwa wanauzwa, ameona msikiti wa kwanza kabisa kujengwa katika karne ya 13, kisima cha kale na kuona makaburi wa watu wa kale.

Alanus Lugome amesema mbali ya kuona vitu vingi vya kale, kikubwa zaidi kilichomshangaza ni kuuona mti wa ubuyu wenye miaka zaidi ya 500.
Katika kudhihirisha ule usemi usemao ‘Disability is not Inability (ulemavu sio sababu ya kushindwa au kutojua kitu), wanafunzi hao walimshangaza mtembeza watu maeneo ya kale (Tour Guider), Leo Tagalile kwa maswali mazuri waliyouliza wanafunzi juu ya mji huo wa kihistoria.

Miongoni mwa maswali waliyoyauliza ni pamoja na kutaka kujua akina nani waliokuwa wenyeji wa eneo hilo kabla ya ujio wa wakoloni, kwa nini paliitwa Kaole na je mbuyu huo bado unatoa matunda licha ya kuwa na umri wa miaka 500?.

Pia wanafunzi hao, mbali na kuiona bandari ya kwanza katika Pwani ya Afrika ya Mashariki, pia walitembelea jengo la The Caravan Serai, lililojengwa mwaka 1870 kwa ajili ya kupokea watumwa waliotoka sehemu mbalimbali kama vile Kilwa Masoko kabla ya kuuzwa.
“Mmefanya kitengo kikubwa sana kwa sababu wanafunzi wenye ulemavu wa viungo, huwa hawaamini kama jamii nyingine inawakubali na kuwathamini,”
“Siku zote wanajisikia faraja sana watu wengine wanapojumuika nao sababu wengine hata jamii zao zinawatenga,”

“Wao wamezoea kuwa karibu na jamaa zao na walimu wao tu, wakitokea watu wengine tofauti kama TVP na kuwa nao siku nzima, wao wanafarijika sana,” amesema Anne Kibanga Mwamgunda, mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, inayojumuisha “TT
“Mbali ya kuwasaidia katika mitihani, pia itawapa kumbukumbu muhimu katika maisha yao,” amesema mwalimu Emmanuel Ibrahim.

Amesema mara ya mwisho wanafunzi wake kutembelea Kaole ni miaka miwili iliyopita kwa ufadhili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni za IPP, marehemu Reginald Mengi.
Mmoja wa wafanyakazi wa TVP, David Sevuri amesema wamejisikia faraja kuwasaidia wanafunzi hao kwenda katika mji huo wa Pwani ya Bagamoyo kama sehemu ya kujifunza kwa macho, baada ya nadharia ya darasani.

“Tuliwahi kuwatumia wanafunzi watatu kutoka shuleni kwenu kutengeneza tangazo la televisheni la Haki Elimu, hivyo tukaona sababu nyingine ya kuwa karibu na nyinyi,”amesema Sevuri.
TVP, inayojihusisha na utengenezaji wa Makala maalumu za video (documentary) na matangazo ya radio, ilitoa pia magunia ya unga, mchele na mafuta kama sehemu ya msaada wa chakula kwa watoto hao.
 Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya True Vision Production wakiwasaidi watoto wenye ulemavu wakati wa ziara yao
 David Sevuri akiwakabidhi wanafunzi wa shule ya msingi Jeshi la Uwokovu sehemu ya vyakula wakati wa ziara yao ya Kaole
 Mbali na kuona sehemu za kale, vyakula pia vilikuwa sehemu ya ziara hiyo
 Mmoja wa wanafunzi akichukua kumbukumbuku muhimu kama anavyoonekana
Ulikuwa ni wajibu wa TVP crew kuwahudumia kama Isaac Lukando anavyoonekana pichani

RC MTWARA AZINDUA SOKO LA MADINI

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa wa pili kushoto leo akikata utepe katika uzinduzi wa soko la madini mkoa wa mtwara, kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya mtwara Evod Mmnda kushoto ni katibu tawala wa mkoani humo Dkt. Jilly Maleko.(PICHA NA FATNA MWINYIMKUU)

  Mtaalmau wa madini mkoa wa mtwara Aidan Mhando kulia leo akitoa amaelezo kwa mkuu wa mkoa huo Gelasius Byakanwa alioko kati kati kuhusu madini yanayopatikana mkoani humo wakati wa uzinduzi wa soko la madini mkoani humo kushoto ni mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda anayefata ni katibu tawala wa mkoani humo Dkt. Jilly Maleko.
 Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa kati kati leo akiwa ameshika moja ya madini yanayozalishwa mkoani humo na kutaka elimu zaidi kuhusu madini hayo kutoka kwa mtaalamu wa madini mkoani humo Aidan Mhando kulia wakati wa uzinduzi wa soko la madini mkoani humo kushoto ni mkuu wa wilaya ya mtwara Evod Mmada.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa kati kati leo akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya ulinzi mkoani humo wakati wa uzinduzi wa soko la madini mkoa wa mtwara.
Viewing all 109573 articles
Browse latest View live




Latest Images