Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Waziri Biteko akutana na Kampuni ya uwekezaji ya Ngwena

$
0
0
Na Issa Mtuwa – Dodoma
Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Mwekezaji wa Kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena” na kufanya nao mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali, kubwa likiwa ni kutoa Ufafanuzi kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Madini inavyotoa fursa na mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya madini hapa nchini.
 Hatua hiyo inafuatia ombi la kampuni hiyo kuomba kukutana na waziri Biteko ili kupata ufafanuzi wa moja kwa moja kutoka kwake kuhusu mabadiliko hayo ya sheria.

Ombi la kutaka kuonana na waziri ni kutokana na kampuni ya Ngwena kupata taarifa za upotoshaji na zisizo sahihi kuhusu mabadiliko ya sheria ya madini yaliyofanywa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu taratibu mbalimbali za uwekezaji na shuguli nyingine zinazo husu sekta ya madini.

Upotoshaji unaofanywa kwa maksudi na baadhi ya watu ndani nan je ya nchi kwa lengo la kutaka kuifanya Tanzania kama sio mahali sahihi pa kuwekeza. 
Biteko ameuambia ujumbe wa kampuni ya Ngwena kuwa, mabadiliko ya sheria yamefanyika kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili mwekezaji na taifa kwa upande mwingine. 

Amefafanua kuwa, tangu mabadiliko hayo yapitishwe hakuna malalamiko ya kupingwa kwa marekebisho hayo kwakuwa yalizingatia maslahi mapana ya kila upande na kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanakuwa rafiki na ndio sababu mpaka sasa tangu marekebisho hayo yafanyike hakuna kampuni au muwekezaji alie acha wala kuonyesha nia ya kufunga shuguli zake kwa sababu ya marekebisho ya sheria.

Ameongeza kuwa, Tanzania inawahitaji sana wawekezaji na mara zote kila panapokuwa na jambo haliendi sawa mara moja hukaa na kujadili na mwekezaji na kutatua changamoto.
 Ameitaka kampuni ya Ngwena kwenda kuwa mabalozi ili kuwaeleza  wengine kuhusu ukweli ulivyo kuhusu marekebisho ya sheria yaliyofanywa na kuachana na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu ambao hawana dhamana ya kuyazungumzia masuala hayo. 

Amewakaribisha watu na wawekezaji wote wanaotaka kupata ufafanuzi wa jambo lolote kutembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
Aidha, kwa upande wa kampuni ya  Ngwena ukiongozwa na Meneja Mkuu H.E Kavishe amemshukuru Waziri kwa ufafanuzi mzuri alioutoa na kwamba walichokuwa wanakisikia na alichokisema waziri ni vitu tofauti na kuongeza kuwa, kuonana kwao kumewafungua masikio na kupata ukweli kutoka kwenye mtu sahihi na mwenye dhamana ya sekta ya madini.

Ameongeza kuwa, ni kweli upotoshaji waliokuwa wanaupata ungeweza hata kuwarudisha nyuma, hivyo watakwenda kufikisha ujumbe kwa wenzao.
Kikao hicho pia, kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Edwin Igenge, na Mkurugenzi wa Sera na Mipango  Wizara ya Madini, Augustine Ollal, Kamishna masaidizi anaeshuugulikia Migodi na Biashara Ali Ali na  Kamishna masaidizi anaeshugulikia Lesseni Maduh.
 Waziri wa Madini Doto Biteko wa Kulia katikati akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na ujumbe wa Kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena” waliomtembelea waziri kupata ufafanuzi kuhusu marekebisho ya sheria ya madini. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila.

 Waziri wa Madini Doto Biteko wa Kulia na Katibu Mkuu wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila kushoto  katikati wakiwasikiliza wageni wao wakati wa kikao cha pamoja na ujumbe wa Kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena” waliomtembelea waziri ofisini kwake kupata ufafanuzi kuhusu marekebisho ya sheria ya madini. 
Waziri wa Madini Doto Biteko hayupo pichani akimsikiliza kwa makini mmoja wa wajumbe wa Kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena” waliomtembelea ofisini kwake kuja kupata ufafanuzi kuhusu marekebisho ya sheria ya madini. 

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO KUHUSU HALI YA USALAMA NCHINI

$
0
0
JESHI  la Polisi Tanzania linapenda kuwashukuru wananchi wote kwa jinsi wanavyoendelea kutoa ushirikiano  kwa kutoa taarifa na ufadhili unaowezesha kubaini, kuzuia na kupambana na uhalifu nchini kwani uhalifu unaendelea kupungua na kuifanya nchi yetu  kuendelea kuwa shwari na salama. 

Yapo  matukio mchache ambayo tunaomba ushirikiano zaidi kutoka kwa wananchi wote katika kupeana elimu ya kuyaepuka kuyatenda matukio kama vile mauaji yanayotokana  na vitendo vya wananchi kujikulia sheria mikononi, wivu wa mapenzi na  ulevi.   Pia matukio ya ubakaji na ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva.  

Jeshi la Polisi Tanzania lina amini kama kila mtu  kwa nafasi yake akishiriki katika kutoa elimu, kuonya na kuwafichua wanaotenda uhalifu huo, kuanzia ngazi ya familia matukio ya aina hiyo yatapungua kwa kiasi kikubwa.

Mtakumbuka pia tarehe 01/06/2019 serikali ilitoa maelekezo kuwa,  ndiyo mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini na utekelezaji ukaanza kwa ufanisi mkubwa.  Jeshi la Polisi linatoa wito agizo hilo liendelee kuzingatiwa na wenye mifuko ya aina hiyo waisalimishe kama ilivyoelekezwa na kama kuna mwenye taarifa za mtu mwenye kumiliki mifuko hiyo atoe taarifa Polisi au mamlaka zingine ili hatua stahiki kwa mujibu wa sheria na kanuni ziweze kuchukuliwa.

Aidha,  kama mnavyofahamu tunaelekea kipindi cha sikukuu ya Eid El Fitri ambayo husheherekewa  duniani kote baada ya mfungo wa  Mwezi  Mtukufu wa Ramadhani.  Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watanzania wote kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama ili waweze kusheherekea kwa amani na utulivu sikukuu hiyo kubwa na muhimu.

Kila  mmoja ajiepushe na vitendo ambavyo vinaweza kuhatarisha  usalama wa maisha na mali zao kama vile kuacha nyumba bila waangalizi, ulevi wa kupindukia, kuruhusu vijana na watoto walio chini ya uangalizi wa wazazi kwenda katika nyumba za starehe au maeneo yanayoweza kuhatarisha usalama na utu wao. Kujiepusha kuendesha vyombo vya moto bila kufuata sheria za usalama  barabarani kama vile kuendesha chombo cha moto ukiwa umelewa , mwendo kasi, pamoja na kujaza abiria kupita kiasi.

Pamoja na kwamba,  Jeshi la Polisi katika Mikoa yote  limejipanga kikamilifu kuimarisha  ulinzi  katika maeneo yote ya ibada na  maeneo mengine ambayo yatakayokuwa na mikusanyiko  mikubwa  ya watu tunaelekeza kila mmoja  usalama uanzie kwake  na kwa wale wanaomiliki maeneo ya starehe wazingatie maelekezo ya kiusalama waliopewa na 
Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi  na watakayoendelea kuwapa.  Pia tunatoa onyo kwa wale wanaodhani wanaweza kutumia sherehe hizi kufanya uhalifu watambue kuwa watashughulikiwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za nchi.

Tunawaomba  wananchi wote pale watakapoona viashiria au kumtilia mtu mashaka kuwa huenda akawa  mhalifu watoe  taarifa kupitia  namba  za simu za bure  0787 668 306 au 111 au 112.
                    
Tunawatakia  Watanzania wote Sikukuu njema yenye amani na utulivu  ya Eid El  Fitri.

Imetolewa na: 
DAVID A. MISIME - SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.

Tigo kuwapeleka wateja wake Misri kushuhudia michuano ya Afrika

$
0
0

Wateja wa Tigo wanayo nafasi ya kujishindia safari ya kwenda Misri kushuhudia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika pamoja na fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 50 kupitia promosheni mpya inayojulikana kama SOKA LA AFRIKA.

Kupitia promosheni hiyo, wateja 10 wa Tigo wataweza kujishindia tiketi za kwenda kushuhudia mashindano haya makubwa barani Afrika, ambapo timu ya taifa, Taifa Stars nayo itakuwa inashiriki kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36.

Ili wateja waweze kushiriki katika promosheni hii ya SOKA LA AFRIKA na kujipatia nafasi ya kuwa mamilionea pamoja na kushinda tiketi, watatakiwa kutuma neno SOKA kwenda 15670 au kutembelea tovuti ya www.tigosports.co.tz ili kuweza kujibu maswali yanayoihusu mashindano hayo yanayofanyika nchini Misri.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa SOKA LA AFRIKA, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa kampuni hiyo, David Umoh, alisema SOKA LA AFRIKA ipo mahususi kwa ajili ya kuwazawadia wateja waaminifu wa Tigo ambao siku zote wamekuwa mstari wa mbele kutumia bidhaa na huduma za kampuni hiyo katika kutumia huduma na bidhaa zetu.

“Tunaamini kwa kutumia mashindano haya, tunaweza kupata fursa nzuri kutoa habari, elimu na burudani kwa kutumia jukwaa la mawasiliano na michezo,” alisema Umoh.

Fainali za Mataifa ya Afrika, ni mashindano makubwa kuliko yote barani Afrika ambayo yanawaleta pamoja wachezaji wa Kiafrika wanaoshiriki ligi kubwa na zenye ushindani ndani na nje ya bara hili.

“Tunaamini itakuwa ni jambo zuri kwa wateja wetu kupata nafasi ya kwenda kushuhudia mashindano haya makubwa ikiwa ni pamoja na kushangilia timu yetu ya Taifa Stars itakayotuwakilisha. Tunawatakia kila kheri,” aliongeza Umoh.

Akizungumzia zawadi za fedha zitakazotolewa, Umoh alisema, “Zaidi ya wateja mia moja watashinda fedha kila siku, kila wiki na kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu.Umoh aliwahimiza wateja wa Tigo kushiriki katika promosheni hiyo na kusema kuwa kadiri mteja anapojibu maswali, ndivyo anavyozidi kujiongezea pointi na nafasi kubwa zaidi ya kushinda tiketi kwenda Misri au mamilioni ya pesa. 
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma wa Tigo David Umoh (kushoto) na Ikunda Ngowi ambaye ni mtaalamu wa huduma za ziada wakionyesha mipira wakati wa uzinguzi wa promosheni ya SOKA LA AFRIKA itakayawezesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia mamilioni pamoja tiketi ya kwenda kushuhudia mashindano ya Mataifa ya Afrika nchini Misri.


Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma wa Tigo David Umoh (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya SOKA LA AFRIKA itakayawezesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia mamilioni pamoja tiketi ya kwenda kushuhudia mashindano ya Mataifa ya Afrika nchini Misri. Kulia ni Ikunda Ngowi ambaye ni Mtaalamu wa Huduma za ziada .

Mtaalamu wa Huduma za Ziada wa Kampuni ya Tigo Ikunda Ngowi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya SOKA LA AFRIKA itakayawezesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia mamilioni pamoja tiketi ya kwenda kushuhudia mashindano ya Mataifa ya Afrika nchini Misri. Kushoto ni Ikunda Ngowi ambaye ni Mtaalamu wa Huduma za ziada.

SUA yawafuturisha wanajumuiya wa Kiislaam.

$
0
0
Uongozi wa Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA umewafuturisha wanajumuia wa kiislamu wa SUA chuoni hapo.

Lengo la futari  hiyo  ni kuwakutanisha pamoja Wafanyakazi na wanafunzi chuoni hapo ili kubadilishana mawazo,kufahamiana  na kujenga mahusiano bora miongoni mwao.

Hafla hiyo ilijumuisha viongozi mbalimbali wa BAKWATA Mkoa ambao walipata nafasi ya kuzungumza na kuelezea maana nzima ya Funga na umuhimu wa elimu kwa Waislamu.
 Mwenyekiti wa Jumuiya wa Waislamu SUA Anaitwa Profesa Wahab  Kimaro akitoa neno katika wanajumuiya namna alivyoagiza Mtume Mohammad kuhusiana na Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 Imam wa Msikiti wa SUA, Said Msuya akitoa mawaidha wakati wa Futari iliyoandaliwa na Chuo  Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine kwa ajili ya wanajumuiya wa wakiislaam wa Chuo hicho.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Profesa  Raphael Chibunda(Mwenye Kanzu Nyeupe katikati Mbele) Akifurahia jambo na Viongozi wa BAKWATA mkoa wakati viongozi mbalimbali wakitoa salamu.

POLISI ARUSHA WAMSHIKILIA MWALIMU WA SHULE YA MSINGI KWA KUMKUTA NA SILAHA YA KIVITA

$
0
0
Lucas Muyovela na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

MWALIMU wa Shule ya Msingi Naan iliopo katika Kata ya Engserosambu tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha Solomon Letato Kipuker(30)anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na silaha ya kivita aina ya AK47 ikiwa na risasi tano zikiwa kwenye magazine.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 4,mwaka 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Johnathan Shanna amesema kuwa tukio hilo limefanikiwa baada ya jeshi hilo kwa kushirikiana na kikosi kazi kabambe na jasiri dhidi ya ujangili na uhalifu wa silaha za moto Kanda ya Ziwa chini ya uwezeshwaji wa tanapa na kufafanua kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa mapema Juni 2 mwaka huu katika Kata Engserosamb.

Amesema mtuhumiwa huyo pia ni miongoni mwa wafanyabiashara haramu wa uingizaji wa silaha za moto ndani ya nchi pia mtuhumiwa huyo anahusishwa na ufanyaji biashara ya nyara za Serikali hasa hasa meno ya tembo pamoja na pembe za faru pia anatuhumiwa kujihusisha na shughuli za ujangili kwa ujumla.

"Mara baada ya kumuhoji alikiri kumiliki silaha hiyo ya kivita kwakushirikiana na watuhumiwa wengine ambao bado wanatafutwa aidha baada ya kumuhoji alisema silaha hizo pia amekuwa akizikodisha katika mapigano ya kikabila baina ya jamii za wasonjo, watemi pamoja na wamasai pia wamekuwa wakitumia katika matukio ya ujambazi na utekaji wa Wawatalii na wananchi na mali zao,"amesema Shanna.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha Aina AK47ikiwa na risasi moja iliyokuwa imetekelezwa kwenye ofisi ya Kijiji cha Mbukeni Kata, Liliondo baada ya jeshi hilo kupata taarifa zakiitelenjensia kubaini uwepo wa bunduki.

Kamanda huyo amesema katika tukio lingine jeshi la polisi linawashikilia majangili sugu wakiwa na nyara za Serikali tangu Juni 30 mwaka huu katika kitongoji cha Maji ya Chai wilayani Arumeru.

Amesema jumla ya watuhumiwa watatu ambao majina yamehifadhiwa wameojiwa na wamekiri kujihusisha na biashara ya ujangili wakiwa na vipande vinne vya meno ya tembo walivyokuwa wamehifahi kwenye mifuko ya sandarusi.
Kamanda amesema watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani pindi upelelezi utakapo kamilika.Ametoa mwito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi zitakazo wezesha kuimarisha usalama wa raia na mali Zao.

Wajumbe wa Baraza Muhimbili wahimizwa kuboresha utendaji kazi

$
0
0
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wametakiwa kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo ili kufikia malengo ya utoaji wa huduma bora za ubingwa wa juu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MNH, Prof. Charles Majinge wakati akizindua Baraza jipya la Wafanyakazi.

Baraza limeshauriwa pia kusimamia majengo, matumizi ya fedha, vitendea kazi pamoja na utendaji wa wafanyakazi ili kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma bora za afya.

“Heshima ya Muhimbili katika kutoa huduma bora za afya imerudi. Ni lazima tuifanye Muhimbili iwe Hospitali ya Taifa kwa maana tuendelee kutoa huduma bora za kibingwa, tuwe kimbilio la wagonjwa,” amesema Prof. Majinge.

Prof. Majinge amelitaka baraza kutunza Muhimbili yakiwamo majengo na vitendea kazi kwa ajili ya vizazi vijavyo na kwamba wafanyakazi wanatakiwa kuthamini sehemu ya kazi kwa kuwa ni mahali ambako wanatumia muda mwingi kazini kuliko majumbani.

Katika kikao, Prof. Majinge amewataka wajumbe kutatua changamoto zinazojitokeza sehemu ya kazi ikiwamo migogoro ili kuimarisha utendaji kazi.

Awali, wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi kuzindua Baraza hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru amewataka wajumbe wa Baraza kuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa kuhimizana kufanya kazi kwa bidii na maarifa.

Amesema ni muhimu kuhakikisha kila mjumbe wa Baraza hili anatumia nafasi aliyopewa kama kiongozi ili uwakilishi wake uweze kuleta tija mahali pa kazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Muhimbili leo kwenye kikao cha 21 kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa hospitali wakimsikiliza mwenyekiti wa bodi, Prof. Majinge leo.
Mkurugenzi wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akisisitiza jambo kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi leo.
Wajumbe wakifuatilia mkutano leo.
Afisa Mchunguzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bi. Christine Temba akitoa mada kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Muhimbili.
Wajumbe wakifuatilia mada kuhusu rushwa ambayo imetolewa leo kwenye mkutano.
Baadhi ya wajumbe wakihesabu kura baada ya kupiga kura kumchagua katibu na katibu msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi la Muhimbili.
Wajumbe wakifuatilia shughuli ya kuhesabu kura leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi leo.

SPIKA NDUGAI AWAPONGEZA WANAFUNZI ST.ANNE MARIE, BRILLIANT

$
0
0
Wanafunzi zaidi ya 120 wa shule ya sekondari ya St Anne Marie Academy na Brilliant waliofaulu kwa daraja la kwanza na la pili kwenye mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2018 wakiwa kwenye ukumbi wa zamani wa Bunge wa Msekwa wakipewa elimu kuhusu Bunge linavyoendeshwa. Shule hiyo imekuwa na utaratibu wa kuwapa motisha wanafunzi hao wanapofanya vizuri kwenye mitihani yao.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WANAFUNZI zaidi ya 120 wa Shule ya St.Anne Marie Academy na Brilliant ambao wamefanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, wametinga Bungeni, huku Spika wa Bunge Job Ndugai akiwapongeza kwa kufaulu kwenye masomo yao.

Akitangaza wageni waliotembelea Bunge Mjini Dodoma Spika Ndugai amesema wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili kwenye matokeo hayo.

Amempongeza Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijiji(CCM), Jasson Rweikiza ambaye ndiye mmiliki wa shule hizo, kwa malezi mazuri kwa watoto hao ambao wameweza kufaulu kwa kiwango kikubwa na kuwataka wengine kuiga mfano huo.

Akizungumzia ziara hiyo ya kimasomo ya wanafunzi hao, Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyetabura amesema kuwa wanafunzi hao wamepewa ziara hiyo kama motisha kutokana na kufanya vizuri sana kwenye mitihani yao.

Ameongeza wanafunzi waliopata fursa hiyo ni wanafunzi 29 wa St.Anne Marie waliopata daraja la kwanza na 59 waliopata daraja la pili na sita wa shule ya Briliant  waliopata daraja la kwanza na 20 waliopata daraja la pili.

Ndyetabura amesema imekuwa kawaida kwa shule hiyo kuwapa motisha wanafunzi wa shule hizo na ndiyo sababu shule imekuwa ikipata matokeo mazuri kwenye mitihani mbalimbali ya kitaifa.

Amesisitiza kuwa wanatarajia kuanza kuwapeleka nchini Dubai, Uingereza hadi Marekani wanafunzi watakaokuwa wanafanya vizuri kwenye mitihani yao ili iwe chachu kwa wengine kufanya vyema kwenye mitihani ya ndani na ile ya kitaifa.

"Shule imejiwekea utaratibu wa kuwapa motisha wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi na huwa tunakawaida ya kuwapeleka mbuga za wanyama kama Serengeti, Mikumi, Ngorongoro hivyo tutaanza kuwapeleka Ulaya," amesema.
Mkurugenzi wa shule za Sekondari St. Anne Marie Academy na Brilliant ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Jasson Rweikiza kushoto Jasson Rweikiza akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo waliokwenda kutembelea bungeni Dodoma baada ya kupata daraja la kwanza na la pili kwenye matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018. Kulia ni Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndasa.

HESLB yatangaza sifa, uratatibu wa kuomba mikopo kwa 2019-2020

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 unaotaja sifa, vigezo na utaratibu wa kuwasilisha maombi ya mikopo ya elimu ya juu na kuwasihi waombaji mikopo watarajiwa kuusoma kwa makini na kuuzingatia.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amewaambia wanahabari leo (Jumanne, Juni 4, 2019) jijini Dar es salaam kuwa lengo la kutoa mwongozo huo ni kuwawezesha waombaji mikopo kuandaa nyaraka muhimu zinazotakiwa.

Kwa mujibu wa Badru, HESLB imetoa mwongozo huo kabla ya kufungua mfumo wa maombi ya mkopo ili kuwawezesha waombaji mikopo watarajiwa kuandaa nyaraka muhimu. Mfumo wa maombi kwa njia ya mtandao utafunguliwa Juni 15, 2019 na utafungwa Agosti 15, 2019.

Uzoefu na sababu za kutoa mwongozo
“Uzoefu wetu unaonesha kuwa waombaji wengi hukimbilia kwenye mtandao na kujaza fomu za maombi wakati mwingine bila kusoma mwongozo. Mwaka huu tumetoa mwongozo huu kwanza ili wausome kwa wiki takribani mbili kabla ya kuruhusiwa kuanza kujaza fomu kwa njia ya mtandao,” amesema Badru na kuongeza kuwa katika mwaka 2018/2019, waombaji zaidi ya 9,000 kati ya 57,539 waliokuwa na sifa za msingi walikosea kujaza fomu za maombi.

Ili kutatua tatizo hilo mwaka 2019/2020, Badru amesema HESLB imetembelea shule za sekondari 81 katika mikoa 17 ya Tanzania Bara na Zanzibar na kukutana na wanafunzi 27,489 ambao walielimishwa kuhusu sifa na utaratibu wa kuomba mkopo kwa usahihi.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema mwongozo huo unapatikana katika lugha za kiingereza na kiswahili katika tovuti ya HESLB ambayo ni www.heslb.go.tz

“Pamoja na mwongozo huo, pia tumeandaa kijitabu chenye maswali na majibu yanayoelekeza namna ya kuomba mkopo kwa lugha ya kiswahili … nacho pia kinapatikana kwenye tovuti yetu na tunawashauri wakisome,” amesema Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Nyaraka muhimu za kuandaa
Waombaji wote wanatakiwa na vyeti vya kuzaliwa ambavyo vimethibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA). Aidha, kwa waombaji mikopo ambao wazazi wao wamefariki dunia, watatakiwa kuwa na nakala za vyeti vya vifo ambavyo vimethibitishwa na RITA au ZCSRA.

“Vilevile tunafahamu kuwa kuna wanafunzi waliofadhiliwa na taasisi mbalimbali katika masomo yao ya sekondari au stashahada, hawa wanatakiwa kuwa na barua kutoka katika taasisi hizo,” amesema Badru katika mkutano huo uliohudhuriwa na Mkurugenzi wa Upangaji Mikopo wa HESLB Dkt. Veronika Nyahende.

Kwa wanafunzi wenye ulemavu au wenye wazazi wenye ulemavu, Badru amesema wanapaswa kuwa na barua zinazothibitisha ulemavu wao kutoka kwa waganga wakuu wa wilaya au mikoa.

Maeneo muhimu yaliyoboreshwa kwa 2019/2020
Katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji huyo aligusia maeneo muhimu yaliyoboreshwa katika utoaji mikopo kwa lengo la kuwafikia wanafunzi wahitaji wengi zaidi.

“Baada ya kupokea maoni ya wadau, tumeongeza umri wa waombaji mikopo kutoka miaka 33 hadi 35 na pia mwaka huu tutapokea maombi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita au stashahada ndani ya miaka mitano iliyopita … kabla ilikuwa miaka mitatu tu,” amesema Badru.

Malengo na bajeti
Katika mwaka wa masomo 2019/2020, Serikali kupitia HESLB imepanga kutoa mikopo na ruzuku ya elimu ya juu yenye thamani ya TZS 450 bilioni kwa jumla ya wanafunzi 128,285. Kati ya hao, wanafunzi 45,000 watakuwa wa mwaka wa kwanza. Mwaka huu 2018/2019, unaoelekea mwisho; jumla ya TZS 427.5 bilioni zilitolewa kwa jumla ya wanafunzi 123,000.

Dawati la huduma kwa wateja
Pamoja na mwongozo uliotolewa, dawati la huduma kwa wateja litakuwa wazi ili kutoa ufafanuzi pale utakapohitajika. Wateja wetu pia wanaweza kupiga simu au kutuandikia barua pepe anuani na namba: Simu: 0736 665533 au 0738 66 55 33 au 022 5507910; Barua pepe: adcp@heslb.go.tz au info@heslb.go.tz

Taarifa hii pia inapatikana kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru akiongea kuhusu sifa na urataibu wa utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Utoaji Mikopo wa HESLB Dkt. Veronica Nyahende.

SUA yawafuturisha wanajumuiya wa Kiislaam

$
0
0
Uongozi wa Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA umewafuturisha wanajumuia wa kiislamu wa SUA chuoni hapo.

Lengo la futari  hiyo  ni kuwakutanisha pamoja Wafanyakazi na wanafunzi chuoni hapo ili kubadilishana mawazo,kufahamiana  na kujenga mahusiano bora miongoni mwao.

Hafla hiyo ilijumuisha viongozi mbalimbali wa BAKWATA Mkoa ambao walipata nafasi ya kuzungumza na kuelezea maana nzima ya Funga na umuhimu wa elimu kwa Waislamu.
 Mwenyekiti wa Jumuiya wa Waislamu SUA Anaitwa Profesa Wahab  Kimaro akitoa neno katika wanajumuiya namna alivyoagiza Mtume Mohammad kuhusiana na Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 Imam wa Msikiti wa SUA, Said Msuya akitoa mawaidha wakati wa Futari iliyoandaliwa na Chuo  Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine kwa ajili ya wanajumuiya wa wakiislaam wa Chuo hicho.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Profesa  Raphael Chibunda(Mwenye Kanzu Nyeupe katikati Mbele) Akifurahia jambo na Viongozi wa BAKWATA mkoa wakati viongozi mbalimbali wakitoa salamu.

WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUJIBU MASHTAKA YA KUCHAPISHA MAUDHUI YA MTANDAO WA "YOUTUBE" BILA KIBALI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

WATU wanne wakazi wa sehemu tofauti jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shitaka la kuchapisha maudhui ya Youtube bila ya kuwa ba kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Washitakiwa hao ambao wamefikishwa mbele ya mahakimu wanne tofauti mahakamani hapo ni Charles Kombe (24) mkazi wa Mikocheni, John Chuwa (28), mkazi wa Barakuda ,Amos Warema (27) na Raymond Mkoroka (30).

Wote kwa pamoja wanadaiwa kuchapisha mtandaoni maudhui hayo katikà tarehe tofauti kati ya mwaka 2018 na Mei mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Wakili wa serikali Elizabert Mkunde  amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Mbando  kuwa, kati ya Agosti 1 ,2017 na Mei 21, 2019 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.
Mshtakiwa Kombe alichapisha maudhui hayo kupitia mtàndao wake wa Youtube  uitwao Charles Kombe bila kibali.

Hata hivyo, mshtakiwa Kombe amekana kutenda shitaka hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kuwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya Sh.milioni 5 kila mmoja.


Mshitakiwa chuwa, amesomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde ambapo Imedaiwa, kati ya mwaka 2018 na Aprili 2019 jijini Dar es Salaam mshtakiwa alichapisha maudhui kupitia mtandao wa Youtube uitwao John film entertainment bila ya kuwa na kibali kutoka TCRA.


Mshtakiwa Chuwa amekiri kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kujidhamini mwenyewe kwa bondi ya sh milioni tano

Kesi imeahirishwa hadi Juni 7 mwaka huu mshitakiwa atakaposomwewa Maelezo ya awali.


Katika kesi nyingine mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega imedaiwa na wakili wa serikali Candid Nasua kuwa  kati ya Novemba 2018 hadi Mei 17 mwaka huu katika maeneo tofauti katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam mshitakiwa Warema

alisambaza maudhui hayo kupitia mtandao wa Youtube uitwao Pro Media Tanzania bila kuwa na kibali kutoka TCRA.


Mshitakiwa amekana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama ilimtaka  kujidhamini mwenyewe na kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya sh. milioni 3.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 4 mwaka huu na upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. 

Kwa upande wake mshtakiwa  Mkoloka alisomewa shitaka lake  na wakili wa serikali Elia Athanas mbele ya Hakimu Mkazi Rwezile.

Mshitakiwa amekana shtaka hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kuwa na mdhamini mmoja na kujidhamini mwenyewe kwa kusaini bondi ya Sh. Milioni 5.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 4 mwaka huu itakapotajwa.

SPIKA JOB NDUGAI AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI TAASISI YA KINGDOM LEADERSHIP NETWORK TANZANIA JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (Kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi kutoka Taasisi ya Kidini ya Kingdom leadership Network Tanzania (KLNT), Mhe. Ibrahim Kaduma alipomtembelea leo nyumbani kwake Kisasa Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (Kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi kutoka Taasisi ya Kidini ya Kingdom leadership Network Tanzania (KLNT), Mhe. Ibrahim Kaduma alipomtembelea leo nyumbani kwake Kisasa Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (Kushoto) akimsikiliza na Mwenyekiti wa Bodi kutoka Taasisi ya Kidini ya Kingdom leadership Network Tanzania (KLNT), Mhe. Ibrahim Kaduma alipomtembelea leo nyumbani kwake Kisasa Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na viongozi wakuu kutoka Taasisi ya Kidini ya Kingdom leadership Network Tanzania (KLNT), walioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo Mhe. Ibrahim Kaduma, walipomtembelea leo nyumbani kwake Kisasa Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa tatu kulia) akiwa katika sala ya pamoja na viongozi wakuu kutoka Taasisi ya Kidini ya Kingdom leadership Network Tanzania (KLNT), walipomtembelea leo nyumbani kwake Kisasa Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Job Ndugai (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu kutoka Taasisi ya Kidini ya Kingdom leadership Network Tanzania (KLNT), walioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo Mhe. Ibrahim Kaduma (wa tatu kulia), walipomtembelea leo nyumbani kwake Kisasa Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

KARAGWE WAMUELEWA MRISHO MPOTO UJENZI WA VYOO BORA

$
0
0
 Msanii wa Muziki wa Kughani Mrisho Mpoto akizungumza na Wazee wa Karagwe Mkoani Kagera wakati wa kampeni yake ya kuhamasisha ujenzi was vyoo Bora inayojulikana usichukulie poa nyumba no choo
 Msanii wa Muziki wa Asili Mrisho Mpoto akiwa ameketi na Wanafunzi wa Karagwe waliofika kugatilia kampeni za Nyumba ni choo.
Mmoja ya Wakazi wa Karagwe Mkoani Kagera akimpigia magoti Msanii Mrisho Mpoto Kama ishara ya Heshima kwake kwa kazi anazofanya.

MAKAMBA ARIDHISHWA NA KASI YA UZALISHAJI WA MIFUKO MBADALA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiangalia moja ya mifuko mbadala inayozalishwa katika Kiwanda cha African Paper Bag Ltd kilichopo Chang’ombe Dar es Salaam. Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha mifuko ya Non-Woven zaidi ya laki moja na mifuko ya karatasi ipatayo laki tano kwa siku.
 Hasnai Mawji, Mkurugenzi Msaidizi kutoka African Paper Bag Ltd (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba mara baada ya kutembelea kiwanda hicho kuona uzalishaji wa mifuko rafiki kwa mazingira. Kiwanda hicho kinazalisha mifuko ya karatasi na Non-Woven.
Waziri Makamba akikagua Kiwanda cha Green Earth Paper Product kinachozalisha mifuko mbadala eneo la Mbezi Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bw. Robert Mosha amesema kwa sasa mahitaji yameongezeka na kuainisha kuwa tawi lingine la Kiwanda hicho linapatika Moshi – Kilimanjaro na yote yameongeza uzalishaji .

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba amefanya ziara ya kikazi ya kukagua viwanda vinavyozalisha mifuko mbadala ikiwa ni siku ya nne tangu kuanza kwa utekelezaji wa Sheria ya Marufuku ya Mifuko ya Plastiki nchini.

Akiwa katika Kiwanda Cha African Paper Bag Ltd kilichopo katika eneo la Chango’mbe jijini Dar es Salaam Waziri Makamba amesema ameridhishwa na kasi ya kiwanda hicho ambacho kinazalisha mifuko ya karatasi laki tano kwa siku na mifuko ya ‘Non-Woven’ ipatayo laki moja kwa siku.
“Wajibu wa Serikali si kupiga marufuku na kuondoka, tunahakikisha tunaziba pengo la mifuko ya plastiki kwa kuweka mazingira wezeshi kwa uzalishaji wa mifuko mbadala yenye ubora na bei nzuri kwa watu. Lazima tuwasaidie wajasiriamali, wafanyabiashara na wenye viwanda kuzalisha mifuko ili kuziba pengo la mahitaji kwa kuwa na mifuko mbadala yenye ubora na viwango vinavyokidhi mahitaji” Makamba alisisitiza.

Amesema kuondoka kwa mifuko ya plastiki kumeibua fursa mpya za uchumi shirikishi, ajira mpya, mapato mapya na kusisitiza kuwa Shirika la Viwango Nchini (TBS) linaandaa viwango vipya vya ubora wa mifuko hiyo mbadala vitakavyobainisha malighafi na unene wa mifuko mbadala itakayozalishwa ili kuwalinda watumiaji ikiwa ni pamoja na taarifa zitakazoainisha mfuko husika una uwezo wa kubeba kilo ngapi.

Mkurugenzi Msaidizi kutoka Kampuni ya African Paper Bag Ltd Bw. Hasnai Mawji amesema kuwa kwa sasa mahitaji ya mifuko kiwandani kwake ni makubwa sana na wameongeza uzalishaji kwa kuagiza mashine mpya mbili sambamba na kuongeza idadi ya watumishi kukidhi mahitaji kwa sasa.
“Kiwanda chetu kinazalisha mifuko tani 100 kwa mwezi na tumeagiza mashine nyingine ili kuongeza uzalishaji wa kufikia tani 200 kwa mwezi na sasa tunafanya kazi masaa 24, shifti zimeongezeka kutoka shifti 1 ya awali na sasa tuna shifti 3, tumeongeza ajira kutoka watu 30 awali na sasa tuna watumishi 60 na lengo ni kufika watumishi 100” Alilisitiza Bw. Mawji.

Katika hatua nyingine Waziri Makamba pia amepata fursa ya kutembelea Kiwanda cha Green Earth Paper Product Ltd kilichopo katika eneo la Mbezi Makonde chenye uwezo wa kuzalisha mifuko 22,000 kwa siku na kusisitiza kuwa katazo la mifuko ya Plastiki si kwa faida ya mazingira pekee bali pia ni muhimu katika kuinua uchumi na ustawi wa watanzania.

Aidha Mkurugenzi wa Kiwanda cha Green Earth Paper Product Bw. Robert Mosha amesema kuwa katika kipindi cha miezi mitatu kabla ya zuio kiwanda hicho kilipokea oda ya kiasi cha Shilingi Milioni 124 na katika kipindi cha mwezi mmoja baada ya zuio la mifuko ya plastiki kiwanda hicho kimepokea mahitaji yenye thamani ya Shilingi 124 ikiwa ni kiwango cha juu ukilinganisha na mahitaji ya awali kwa kipindi kifupi.

Kuanzia tarehe 1 Juni Serikali imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya Plastiki nchini ikiwa ni pamoja na Utengenezaji, Uingizaji, Usambazaji, Usafirishaji na Matumizi ya Mifuko hiyo bila kujali unene wake.

BARAGUMU : MJADALA MAKINI KUHUSU UMUHIMU WA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI

INTRODUCING WAJOMBA'S NEW SONG "MURUA"


BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 04.06.2019

RC MAKONDA ABAINI MAMBO 5 OPERESHENI UKAGUZI VITAMBULISHO VYA WAMACHINGA SOKO KARIAKOO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa ameongoza Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam na Katibu Tawala wa mkoa huo leo wamefanya operesheni ya ukaguzi na matumizi ya vitambulisho vya wamachinga kwenye soko la Kariakoo na kubaini uwepo wa ukiukwaji mkubwa wa matumizi ya vitambulisho hivyo. 

Katika ziara hiyo RC Makonda amebaini mambo matano ikiwemo Wafanyabiashara kufoji vitambulisho, wafanyabiashara kuazimishana vitambulisho, wafanyabiashara kukodi vitambulisho kwa shilingi 1,000, utofauti wa jina linalotumika kwenye kitambulisho kutofautiana na jina analotumia kwenye vitambulisho vingine pamoja na uwepo wa idadi kubwa ya wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho. 

Kutokana na hayo RC Makonda amewaagiza wakuu wa Wilaya kuanza msako Mara moja wa kuwakamata wafanyabiashara waliofoji vitambulisho na wasiokuwa na vitambulisho iliwaweze kuchukuliwa hatua za kisheria. 
Hata hivyo RC Makonda amesema ataandika barua ya Kumuomba Rais Dkt.John Magufuli amuongezee vitambulisho vingine 25,000 na kufanya mkoa huo kuwa na idadi ya vitambulisho 200,000

Rais Dkt. Magufuli azungumza na Makatibu Tawala Wilaya zote pamoja na Makatibu Tarafa Ikulu jijini Dar es Salaam

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makatibu Tawala wa Wilaya zote pamoja na Makatibu Tarafa wa Tarafa zote katika Kikao kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Makatibu Tawala wa Wilaya zote pamoja na Makatibu Tarafa wakiwa Ikulu jijini Dar es Salaam 
 


 

Wajumbe wa Baraza Muhimbili wahimizwa kuboresha utendaji kazi

$
0
0

Mkurugenzi wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akisisitiza jambo kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi leo 
Wajumbe wakifuatilia mkutano leo. 
Afisa Mchunguzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bi. Christine Temba akitoa mada kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Muhimbili
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa hospitali wakimsikiliza mwenyekiti wa bodi, Prof. Majinge leo. 
Baadhi ya wajumbe wakihesabu kura baada ya kupiga kura kumchagua katibu na katibu msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi la Muhimbili. 
Wajumbe wakifuatilia shughuli ya kuhesabu kura leo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi leo. 

*********************************** 

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wametakiwa kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo ili kufikia malengo ya utoaji wa huduma bora za ubingwa wa juu. 

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MNH, Prof. Charles Majinge wakati akizindua Baraza jipya la Wafanyakazi. 

Baraza limeshauriwa pia kusimamia majengo, matumizi ya fedha, vitendea kazi pamoja na utendaji wa wafanyakazi ili kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma bora za afya. 

“Heshima ya Muhimbili katika kutoa huduma bora za afya imerudi. Ni lazima tuifanye Muhimbili iwe Hospitali ya Taifa kwa maana tuendelee kutoa huduma bora za kibingwa, tuwe kimbilio la wagonjwa,” amesema Prof. Majinge. 

Prof. Majinge amelitaka baraza kutunza Muhimbili yakiwamo majengo na vitendea kazi kwa ajili ya vizazi vijavyo na kwamba wafanyakazi wanatakiwa kuthamini sehemu ya kazi kwa kuwa ni mahali ambako wanatumia muda mwingi kazini kuliko majumbani. 

Katika kikao, Prof. Majinge amewataka wajumbe kutatua changamoto zinazojitokeza sehemu ya kazi ikiwamo migogoro ili kuimarisha utendaji kazi. 

Awali, wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi kuzindua Baraza hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru amewataka wajumbe wa Baraza kuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa kuhimizana kufanya kazi kwa bidii na maarifa. 

Amesema ni muhimu kuhakikisha kila mjumbe wa Baraza hili anatumia nafasi aliyopewa kama kiongozi ili uwakilishi wake uweze kuleta tija mahali pa kazi

SIMANJIRO YATOA MKOPO WA SH230.8 MILIONI KWA VIKUNDI 71

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula (kushoto) akipeana mkono na viongozi wa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu baada ya kupokea mkopo uliotolewa na Halmashauri ya Wilaya hiyo
Baadhi ya vikundi vya wajasiriamali, wanawake, vijana na walemavu waliopatiwa mkopo wa sh230.8 milioni na Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula (kushoto) akipokea mfano wa hundi kutoka benki ya NMB.

******************************************
HALMASHAURI ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, imevipatia vikundi 71 vya wanawake, vijana na walemavu, sh230.8 milioni ya mikopo kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ili kuwanyanyua kiuchumi. 

Ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Asia Ngalisoni akizungumza jana alisema vikundi hivyo ni vya kata 14 vilivyonufaika na mkopo huo. 

Ngalisoni alisema mkopo huo umenufaisha vikundi 71, ambapo 59 ni vya wanawake 1,531, vikundi tisa vya vijana 238 na vikundi vitatu vya walemavu 57. 

Alisema hadi mwezi Mei mwaka huu halmashauri hiyo imekusanya sh1.7 bilioni ikiwemo mapato ya ndani na marejesho ya fedha za vikundi vilivyokopeshwa awali. 

“Mfuko huu unawanufaisha wananchi waliojiunga katika vikundi vyenye shughuli za ujasiriamali au vinavyokusudia kuanzisha shughuli za ujasiriamali mdogo au wa kati,” alisema Ngalisoni. 

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula alisema fedha hizo zinazotolewa hazina riba hivyo vikundi hivyo vinapaswa kuchukua mikopo hiyo na kurejesha kiasi kile kile walichokopa. 

“Nitoe wito kwa vikundi vyote vilivyokopeshwa na halmashauri virejeshe fedha hizo kwa wakati ili wengine nao waweze kukopa na kujikwamua kiuchumi,” alisema Chaula. 

“Mfuko huu unawanufaisha wananchi waliojiunga katika vikundi vyenye shughuli za ujasiriamali au kinakusudia kuanzisha shughuli za ujasiriamali mdogo au wa kati,” alisema Chaula. 

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Jackson Sipitieck alimpongeza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri yake Yefred Myenzi kwa kusimamia ipasavyo mapato hadi kufanikisha utolewaji wa mikopo hiyo. 

“Wakati halmashauri nyingine zikisuasua kufanikisha mikopo sisi Simanjiro tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani tunatoa mikopo hadi fedha nyingine zimebaki,” alisema Sipitieck. 

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi alitoa wito kwa vijana wa eneo hilo kuchangamkia fursa hiyo kwani mwitikio wao bado ni mdogo. 

“Zile fedha zenu vijana za asilimia nne mnazopaswa kupewa hamjazichukua hivyo vijana wa Simanjiro mnapaswa kubadilika ili mnufaike kupitia mikopo hii tunayoitoa,” alisema Myenzi. 

Katibu wa walemavu mji mdogo wa Mirerani, William Orata alisema kupitia mkopo waliopata wamefanikisha uanzishwaji wa mashine ya kusaga nafaka. 

Mmoja kati ya wanawake walionufaika na mkopo huo, Susan Alanyamuna alisema wameweza kutengeneza sabuni aina ya Sidai.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images