Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. SHEIN AJUMUIKA NA WANANCHI WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI KATIKA FUTARI ILIOFANYIKA IKULU ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyewkiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Dkt. Amani Karume, wakipata futari ya tende katika viwanja vya Ikulu Zanzibar na kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, futari hiyo imefanyika jana 2-6-2019,katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika katika Futari Maalum iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Zabnzibar kulia Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dkt. Amani Karume na kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarv Mhe, Seif Ali Iddi, wakijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Maghari katika futari hiyo iliofanyika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika futari Maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika viwanja vya Ikulu Zanzibar kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi. (Picha na Ikulu)


 WANANCHI wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakijumuika katika Futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katikac viwanja vya Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 MABALOZI Wadogo wanaowakilisha Nchi Zanzibar wanaofanyia zao Zanzibar wakishiriki katika hafla ya futari Maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akizungumza na kutowa shukrani kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliofanyika Ikulu Zanzibar (Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na kuagana Rais wa Mstaaf wa Zanzibar Mhe Dkt. Amani Karume, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk., Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Mama Fatma Karume, baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, na kulia Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na kuagana na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Mwananchi aliyehudhuria hafla ya futari iliofanyika viwanja vya Ikulu Zanzibar jana.(Picha na Ikulu)

NAIBU WAZIRI KANYASU AWAONYA WANANCHI WANAOTOA VITISHO KWA ASKARI WANYAMAPORI WA VIJIJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amewataka Wananchi waache tabia ya kuwatishia maisha Askari wanyamapori wa vijiji (VGS) wakati wanapowakataza wananchi hao kuendesha shughuli za kibinadamu katika maeneo ya mtawanyiko na mapito ya wanyamapori (shoroba)

Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu amemtaka Mkuu wa wilaya ya Namtumbo, Mhe. Sophia Mfaume afanye uchunguzi kwa kutumia vyombo vyake vya usalama ili kuwabaini Wananchi hao wanaowatishia Askari wanapotekeleza majukumu yao na watakaobainika hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Mhe. Kanyasu, ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya Askari 20 wa Wanyamapori wa Vijiji wa kutoka mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Singida waliohitimu mafunzo hayo katika Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii cha Likuyu Sekamaganga kilichopo katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma

“leo mmehitimu na tumewaapisha, mmekuwa askari kweli lakini tambueni kuwa kazi za kiuchumi zinapelekea uharibifu mkubwa sana wa mapito ya wanyama, nendeni mkawaelimishe wananchi wasiendelee kuharibu kwa ustawi wa hifadhi zetu"

Amefafanua kuwa maeneo ya mtawanyiko na shoroba lazima zilindwe ili kuruhusu wanyamapori waendelee kuzaliana na pia kwenda kupata virutubisho maalum ambayo havipo mbugani.

'' Tunazihitaji hizi shoroba, tulikuwa tumejisahau shoroba nyingi zimekuwa mashamba na makazi na wanyama wamekuwa hawana sehemu ya kupita'' amesema Kanyasu Amesema shoroba na maeneo ya mtawanyiko zisipokuwepo utalii na Hifadhi vitatoweka.

" Lazima tufike mahali tuamue eneo hili ni kwa ajili ya kilimo na eneo hili kwa ajili ya makazi, haiwezekani maeneo yote tukaanzisha kilimo na makazi ilhali wanyamapori hawana mipaka" Alisisitiza Kanyasu .

Amesema uwepo wa shoroba na maeneo ya mtawanyiko husaidia kupata kizazi imara cha wanyamapori kwani wakifungiwa sehemu moja huzaliana ndugu na kukosa ubora,ikiwamo kuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka askari hao kufanya kazi kwa uaminifu kwa kujiepusha kuungana na mtandao wa majangili.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Namtumbo, Mhe. Sophia Mfaume amewahakikishia askari hao kuwa wafanye kazi kwa kufuta sheria na wale watakaowakwamisha katika kutekeleza majukumu yao hatasita kuwachukulia sheria.

Aidha, Amewataka Wananchi wafuate sheria kwa kuheshimu maeneo ya mtawanyiko na shoroba ili Hifadhi ziendelee kuwepo

Kwa upande wake, Mhitimu wa mafunzo hayo Musa Alfred Wakati akisoma risala, Amemueleza Naibu Waziri kuwa mafunzo waliyopewa yatakuwa chachu katika shughuli za uhifadhi nchini.

Naye Mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Ruvuma, Jaqueline Msongozi amewataka askari hao wa vijiji watekeleze majukumu yao bila kutishwa na mtu yeyote kwa vile maliasili hizo ni za watanzania wote na wao wanazilinda kwa niaba ya Watanzania.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu, akizungumza na wahitimu wakati  akifunga mafunzo ya Askari 20 wa Wanyamapori wa Vijiji wa kutoka mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Singida waliohitimu mafunzo hayo katika Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii cha Likuyu Sekamaganga kilichopo katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungmza na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii cha Likuyu Sekamaganga, Jane Nyau huku akiangalia mnara mpya uliowekwa na TTCL kwa ajili ya huduma za mtandao katika chuo hicho mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufunga mafunzo ya askari 20 wa wanyamapori wa vijiji katika wilya ya Namtumbo mkoani Ruvuma. Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Namtumbo, Sophia Mfaume pamoja na viongozi wengine.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akikagua paredi kwa Askari 20 wa  Wanyamapori wa Vijiji wa kutoka mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Singida wakati akifunga mafunzo kwa wahitimu wa mafunzo hayo katika Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii cha Likuyu Sekamaganga kilichopo katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Ruvuma

 Baadhi ya Askari wa wanyamapori wa Jamii wakiwa wanamsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati akizungumza nao katika mahafali ya kufuzu mafunzo yao katika Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili cha Likuyu Sekamaganga,
Mkuu wa chuo Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili cha Likuyu Sekamaganga akizungumza wakati wa mahafali ya kufuzu kwa Askari wanyamapori wa Jamii mkoani Ruvuma. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-WMU)

Vodacom Tanzania yafuturisha wateja wake jijini Dar

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla akisalimiana na Sheikh Othman Zuberi katika hafla ya futari iliyoandaliwa na kitengo cha Biashara cha kampuni ya Vodacom Tanzania kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja wateja wake  jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi na Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Arjun Dhilon 
 Waziri wa maliasili na utalii, Hamis Kigwangalla (Katikati)akizungumza kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Idara ya biashara ya kampuni ya Vodacom Tanzania katika kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja wateja wake jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa maliasili na utalii, Hamis Kigwangalla (Katikati) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom, Hisham Hendi (Kushoto) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Idara ya biashara ya kampuni hiyo katika kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja wateja wake jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. 
Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Idara ya biashara ya kampuni ya Vodacom Tanzania katika kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja wateja wake jijini Dar es Salaam.
 Picha ya pamoja

UJUMBE MARIDHAWA KUTOKA DAWASA: USAFI WA MAZINGIRA NI UTU

Polisi Iringa wakamata watuhumiwa wa ujangili wa meno ya tembo

$
0
0
Na Francis Godwin, Iringa 

Jeshi la polisi linawashikilia watuhumiwa wanne kwa makosa mbali mbali likiwemo la kukutwa na meno ya tembo,  kamanda Bwire alisema kuwa katika tukio la kwanza lililotokea tarehe 1 juni katika vijiji vya Mbawi ,Masisiwe , Chita na Ihimbo jeshi la polisi kwa kushirikiana na kikosi kazi cha taifa cha kupambana na ujangili ,kikosi cha kuzuia ujangili na TFS - Tanza nia Forest Service walifanya msako wa pamoja na kuwakamata watuhumiwa wawili pamoja na silaha aina ya SMG iliyoporwa na watuhumiwa hao wa ujangili .

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire amewaeleza leo waandishi wa habari ofisini kwake kuwa watuhumiwa hao wa ujangili ndio ambao wamehusika la mauaji ya askari wa hifadhi hya Udzungwa wilaya ya Kilolo Mwita Raphael (28) aliyeuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali /silaha kifuani na kumpora silaha aina ya SMG namba 260332 TZWD'KDU/IR/ 1990 mali ya KIDU ambayo imepatikana na watuhumiwa hao wawili .

Mbali ya tukio hilo alisema kuwa watu wengine wawili wakazi wa kijiji cha Wenda kata ya Tanangozi wilaya ya Iringa walikamatwa na jeshi la polisi kwa kushrikiana na afisa wanyamapori walimkamata Geofrey Kiswaga (35) mkulima akiwa na Nelson Kiduru (31) wakiwa na meno ya Tembo mamatu yenye uzito wa 8Kg ambayo thamani yake bado kufahamika waliyokuwa wameyahifadhi kwenye mfuko wa salfeti kwenye pikipiki namba Mc 116 BMZ aina ya Fekoni iliyokuwa ikiendeshwa na Kiduru wakitokea kijiji cha Nyamihumu Kidamali .

Kuwa watu hao walikuwa wakielekea kijiji cha wenda kufanya biashara ya meno hayo kwa wanunuzi ambao bado wanatafutwa na jeshi la polisi .

Wakati huo huo jeshi la polisi mkoa wa Iringa limewataka wakazi wa mkoa wa Iringa kuondoa hofu wakati wa sikukuu ya Idd kwani jeshi la polisi limejipanga kuhakiisha ulinzi na usalama unawekwa katika maeneo yote ya starehe na ibada kwa waumini wa dini ya Kiislam.

Kamanda Bwire alitoa onyo kwa madereva wa pikipiki na vyombo vya moto kuendesha kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuepuka kuendesha vyombo hivyo wakiwa wamelewa pombe huku akiwataka wananchi mkoani hapa kutoondoka wote majumbani kwao kwenda katika starehe kwani kufanya hivyo ni kukaribisha wezi nyumbani .

Aidha jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia Jupista Mhinza (30) mkazi wa kijiji cha Kilolo mkoani hapa kwa tuhuma za kumchoma na kijinga sehemu za siri mtoto wake wa miaka 6 baada ya kuchelewa kurudi nyumbani .
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Bwire aliwaeleza waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku katika kijiji cha Kilolo kata ya Kasanga tarafa ya Kasanga wilaya ya Mufindi ,ambapo mwanamke huyo alichukua uamuzi huo baada ya mtoto huyo ambae ni mwanafunzi wa shule ya msingi Kilolo kuchelewa kurudi nyumbani .

" mtoto huyo alikuwa akicheza na watoto wenzake hivyo kuchelewa kurudi nyumbani kitendo kilicho mkwaza mama mazazi na kuamua kuanza kumshambulia kwa kipigo na kisha kuamua kumchoma na kijinga cha moto katika sehemu zake za siri na kumjeruhi vibaya " alisema kama Bwire 

Mtoto huyo amelazwa katika kituo cha afya Kasanga akiendelea na matibabu na mwanamke huyo anashikiliwa na jeshi la polisi na atafikishwa mahakamani kwa tuhuma hiyo ya kumjeruhi mtoto huyo .
kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire akionesha kwa waandishi wa habari jana silaha aina ya SMG namba 260332 TZWD'KDU/IR/ 1990 mali ya KIDU inayodaiwa kuporwa kwa askari wa hifadhi ya Udzungwa Mwita Raphael (28) aliyeuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kabla ya kuporwa siaha hiyo na watu wanaodhaniwa na majangili

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAOMBA KUIDHINISHIWA BAJETI YA SHILINGI TRILIONI 11.94 MWA 2019/2020

$
0
0
 
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
 aadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga (kushoto). Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (katikati) na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga, wakifuatilia mawasilisho ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango yaliyowasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
 Baadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, baada ya kuwasilishwa kwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ambapo imeliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha shilingi trilioni 11.94 kwa ajili yamatumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)  na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, wakifuatilia kwa makini michango ya Wabunge wakijadili  Hotuba ya Bajeti ya Wizara ambapo Wizara imeliomba Bunge kuidhinishiwa kiasi cha shilingi trilioni 11.94 kwa ajili yamatumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)  na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, wakifuatilia kwa makini michango ya Wabunge wakijadili  Hotuba ya Bajeti ya Wizara ambapo Wizara imeliomba Bunge kuidhinishiwa kiasi cha shilingi trilioni 11.94 kwa ajili yamatumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango

HOTUBA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO MWAKA 2019/20

$
0
0
  Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.

WAHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 20 AU JELA MWAKA MMOJA NA NUSU KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA KAZI BILA KIBALI

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MKURUGENZI wa kampuni ya Biabana,  Anna Kristina Edler, (54) na mumewake, Anders Svensson 58   wamehukumiwa kulipa faini ya sh. Milioni 20 au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu gerezani baada ya kukiri tuhuma za kuajiri raia wa nje ya nchi na kujihusisha na kazi bila ya kuwa na kibali nchini

Hukumu hiyo imesomwa, leo Juni 3, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo washtakiwa hao raia wa Swideni wanakabiliwa na mashtaka mawili, likiwemo La kufanya kazi nchini bila ya kuwa na  kibali.

Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka  yao, washtakiwa wamekili na wamehukumiwa kulipa faini ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu gerezani.

 Mapema akisoma mashtaka yao, wakili wa serikali, Daisy Makakala amedai kati ya Agosti 18 mwaka Jana na Aprili 3, 2019 huko Mikocheni, mshtakiwa Elder,  akiwa kama mkurugenzi wa kampuni ya Biabana Ltd alimuajiri Anders na kufanya kazi  katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka idara yavUhamiaji.
Katika shtaka la pili imedaiwa, aiku na mahali hapo mshtakiwa Enders alijihusisha na kazi kama muajiriwa wa kampuni ya Biabana LTD bila ya kuwa na kibali kinachotolewa na idaravya Uhamiaji.

Mpaka tunaondoka Mahakamani hapo, wazungu hao walikuwa hawajafanikiwa kulipa fine na wameenda gerezani

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA ASKOFU DKT. JOSEPHAT GWAJIMA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Naibu Waziri Ofisi wa Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira Anthony Mavunde wakwanza kutoka kushoto. PICHA NA IKULU

TAARIFA YA KUSITISHWA KWA MATUMIZI YA PASIPOTI ZA ZAMANI ZINAZOSOMEKA KWA MASHINE (MRP) IFIKAPO TAREHE 31 JANUARI 2020

$
0
0
Kufuatia kuzinduliwa na kuanza kutumika  kwa Pasipoti Mpya za Kielektoniki  (e Passport), Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji inapenda kuufahamisha umma kuwa, tayari imekamilisha  ujenzi wa miundo mbinu ya utoaji wa huduma ya pasipoti hizo katika Mikoa ishirini na tisa (29), Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu, Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar na Ofisi za balozi za Tanzania  Ishirini  na tatu (23) zilizopo nje ya Nchi;

ambazo ni Uingereza (London), Ufaransa (Paris), Marekani (Washington DC na  New York), Canada (Ottawa), Israel (Telaviv), Saudi Arabia (Jeddah na Riyadh), Comoro (Moron), Kenya (Nairobi na  Mombasa), Ujerumani (Berlin), Algeria (Algiers), Italia (Rome), Nigeria (Abuja), Misri (Cairo), Uholanzi (The Hague), Ubelgiji (Brussels), Zambia (Lusaka), India (New Delhi), Malawi (Lilongwe), China (Beijing), Malaysia (Kuala Lumpur). 

Nchi ambazo zitafunguwa Mfumo huo hivi karibuni ni Afrika Kusini, Msumbiji na Zimbabwe. Aidha, kwa Balozi zilizosalia, kazi ya ufungaji mitambo ya huduma hiyo inaendelea na itakamilika hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu.

Kwa Msingi huo, Idara ya Uhamiaji inawakumbusha  Watanzania wote Ndani na Nje ya Nchi kuwa matumizi ya Pasipoti za zamani yatasitishwa ifikapo tarehe 31 Januari, 2020.

Aidha, idara inawasisitiza wale wote wenye Pasipoti za zamani (MRP) na wanaokusudia kusafiri nje ya Nchi hivi karibuni, kuhakikisha wanabadilisha Pasipoti zao mapema kabla ya mwezi Julai mwaka huu ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza wa kurejeshwa katika Viwanja vya Ndege na Vituo vya Mipakani wakati wa kutoka Nchini. Ni hitajio la Kisheria kwa Pasipoti kuwa na angalau uhai wa kuanzia miezi sita ili mwenye pasipoti hiyo aweze kuomba Visa ya Nchi anayokwenda na kuruhusiwa kuondoka Nchini kupitia Vituo vya kuingia na kutoka nchini.
Imetolewa na 

Ally M. Mtanda (SI)
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji 
Makao Makuu, Dar es Salaam

AZANIA BANK HOST AN IFTAR EVENT IN ARUSHA

$
0
0
Azania Bank's Managing Director Mr. Charles Itembe talking to customers during Iftar event which was organised by Azania Bank for its customers in Arusha over the weekend.
Arusha Region's Assistant Sheikh, Rajab Kiungiza shaking hands with one of the Azania Bank's customers during Iftar event which was organised by Azania Bank for its customers in Arusha over the weekend. Looking on is the Azania Bank's Managing Director Mr.Charles Itembe.
Some of Azania Bank customers during the Iftar event which was organised by Azania Bank for its customers in Arusha. The event took place over the weekend.

Mkemia Mkuu Wa Serikali Asisitiza Kuzingatia Ueledi

$
0
0


Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama) akiongea na Wakaguzi wa Kemikali (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia ulioandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kufanyika leo katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Kurasini, Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara za Huduma za Ubora wa Bidhaa, Sabanitho Mtega, Maendeleo ya Biashara, George Kasinga, Usimamizi wa Kemikali, Daniel Ndiyo na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Elias Mulima.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Kemikali, Daniel Ndiyo
(aliyesimama), akizungumza na Wakaguzi wa Kemikali (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa tatu kulia) kufungua Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali leo.
Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia wakimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo.
Mkaguzi wa kemikali na Maabara za Kemia kutoka Maabara ya Kanda ya Kaskazini, Jovitus Mukela (aliyesimama), akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakaguzi mara baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufungua Mkutano huo.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyekaa katikati), akiwa pamoja na Wakurugenzi na Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali mara baada ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi hao uliofanyika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Kurasini, Dar es Salaam.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amewasisitiza wakaguzi wa kemikali na maabara za kemia kuzingatia ueledi, uadilifu na uaminifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.Mkemia Mkuu wa Serikali amezungumza hayo leo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia kutoka Mamalaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali uliofanyika Baraza la Maaskofu, Kurasini, Dar es Salaam.

Serikali imetupa majukumu ya kusimamia Sheria ya Mamlaka ya Maaabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani na Sheria ya Vinasaba vya Binadamu hivyo tunapaswa kuzingatia ueledi, uadilifu, uaminifu na upendo ili kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa ufanisi.

“Tutambue Serikali yetu imejielekeza katika kujenga uchumi wa viwanda na inajitahidi kuwekeza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara ikiwemo wanaojihusisha na kemikali, hivyo tunapotekeleza majukumu yetu tunapaswa kuelewa uelekeo huo wa Serikali na kufanya maamuzi kwa wakati na haraka ili kutokwamisha wadau wetu huku tukizingatia Sheria” alisema Mafumiko.

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali alisema Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti inawapongeza wakaguzi hao kutokana na kazi kubwa wanayofanya na inawahamasisha kuboresha zaidi huduma kwa wadau kwa kufuata Sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza kama watumishi wa umma.

“Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti inatambua mchango mkubwa wa wakaguzi katika kusimamia Sheria na kuingiza maduhuli ambayo taasisi inatumia katika kuboresha huduma na kujiendesha. Tunatambua changamoto zipo na tunaendelea

kuzifanyia kazi kama kuongeza watumishi na vitendea kazi. Tuna maeneo ya msingi ya kuyawekea kipaumbele hasa kwenye uwekezaji wa mitambo ya kisasa ya maabara na teknolojia ili kuwawezesha wakaguzi kutoa huduma bora na za haraka kwa wadau. Tufanye kazi kama familia ili kuweza kutekeleza majukumu yetu kwa mafanikio.” Alimaliza.

Akitoa neno la shukrani, Mkaguzi wa Kemikali, Bw. Jovitus Mukela alimshukuru Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko kwa nasaha nzuri za ufunguzi wa Mkutano huo.

Kwa niaba ya wakaguzi wenzangu tunakushukuru sana kwa nasaha na maneno mazuri uliyotuambia maana pia yanatukumbusha majukumu yetu na napenda kuwaomba wakaguzi wenzangu kuzingatia yale yote yaliyozungumzwa na kushirikiana kutoa huduma nzuri, kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeitendea haki Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, sisi wenyewe na nchi kwa ujumla.” alisema Mukela.

KESI YA ALIYEKUWA MHASIBU TAKUKURU YAKWAMA TENA, KISA MASHAHIDI WASHINDWA KUFIKA MAHAMANI

$
0
0

Na Karama Kenyunjo, Globu ya jamii

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi kuwa, wameshindwa kuwaita mashahidi kuja kutoa ushahidi wao leo, sababu mpaka sasa mashahidi watano waliotoa ushahidi bado hawajalipwa stahiki zao.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa ameeleza hayo leo Juni 3,mwaka 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wakati kesi hiyo illipoitwa leo kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.

Amedai kuwa kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini wameshindwa kuwaita mashahidi wengine kwa sababu shahidi wa 9,10,11,12 na 13 ambao tayari walishatoa ushahidi wao bado hawajalipwa stahiki zao, hivyo ameiomba mahakama itoe amri kwa uongozi wa Mahakama ili mashahidi hao waweze kulipwa stahiki zao

Baada ya kutolewa taarifa hiyo, Hakimu Simba amesema watalitatua tatizo hilo sababu kesi hiyo ni ya muda mrefu na walikubaliana waletwe mashahidi wa kutosha ili kesi imalizike haraka. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 17 mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa na itaendelea kusikilizwa Juni 18, 20 na 24.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera. Gugai na mwenzake watatu wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

TAASISI ZA FEDHA ZATAKIWA KUCHANGAMKIA VIWANDA VYA USINDIKAJI MAZIWA

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akizungumza jambo na Meneja Mwandamizi wa idara ya Kilimo biashara NMB Oscar Rwechungura pamoja na wafanyakazi wa NMB kwenye banda la benki hiyo wakati wa Wiki ya Maziwa kitaifa iliyofanyika jijini Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia) akizungumza jambo na Afisa Utafiti wa benki ya NMB, Mboka Mwanitu na Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro (kushoto) wakati wa Wiki ya Maziwa kitaifa iliyofanyika jijini Arusha.
Afisa Utafiti wa benki ya NMB makao makuu, Mboka Mwanitu akiwasilisha mada juu fursa za mikopo inayotolewa na benki hiyo kwenye sekta ya Maziwa wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Maziwa kitaifa iliyofanyika jijini Arusha.
 

Mwandishi Wetu, Arusha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo,Profesa Elisante Ole Gabriel amezitaka taasisi za fedha nchini kuchangamkia fursa ya soko la usindikaji wa maziwa ambalo linahitaji uwekezaji wa kimkakati kutokana na sehemu ndogo ya maziwa yanayotoka kwa wafugaji ndiyo yanayosindikwa.

Profesa Ole Gabriel ametoa rai hiyo katika kongamano la 10 la Wiki ya Maziwa kitaifa nchini kuwa kiwango cha maziwa kwa mwaka ni takribani lita 2.7 bilioni wakati kiwango cha maziwa kinachosindikwa ni lita 56 milioni pekee hatua inayomnyima mapato mazuri mfugaji.

“Nitoe wito kwa taasisi za fedha kuchukua fursa hii muhimu kwa kuwekeza kwa nguvu kwenye mnyonyoro wa thamani ili kuyapa thamani maziwa yetu,ipo fursa kubwa ambayo itawasaidia wafugaji na taasisi zenu kupata faidi,”alisema Ole Gabriel

Kongamano hilo limewaleta wadau kutoka mikoa mbalimbali na nje ya nchi linajadili namna ya kuongeza uzalishaji bora wa maziwa na namna ya kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa mbegu bora za uhamilishaji,malisho ya mifugo,masoko ya maziwa na uhaba wa viwanda vya usindikaji wa maziwa.

Mweneyekiti wa Bodi ya Maziwa nchini,Lucas Malunde alisema viwanda zaidi vinahitajika kwaajili ya kuongeza kiwango cha maziwa yaliyosindikwa ambayo yanamhakikishia faida mfugaji na mtumiaji wa maziwa.
Alisema kiwango cha matumizi ya maziwa kwa mtu mmoja hapa nchini kipo chini kiasi cha lita 49 kwa mwaka wakati lengo ni kumwezesha kila mtu kutumia lita 200 kwa mwaka.

Afisa Utafiti wa benki ya NMB, Mboka Mwanitu alisema benki hiyo imetenga kiasi cha Sh 500 bilioni “for AVC” na tasnia ya maziwa kwa ujumla na hadi sasa wapo wajasiriamali walionufaika kwa kuchukua mkopo wa Sh 30 bilioni na hii imetokana na kuongezeka kwa mahitaji ya maziwa nchini.

Alisema mikopo yao imejielekeza kwenye kupata mbegu bora za ng’ombe,kuwa na vituo bora vya kukusanyia maziwa ,vifaa vya kisasa vya usindikaji wa maziwa,malisho na huduma za chanjo na matibabu .

GGM, TACAIDS kuzindua Kilimanjaro Challenge kwa lengo La kukusanya fedha za kutokomeza Ukimwi

$
0
0

Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) inatarajia kuzindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2019), na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka 2019 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini.

Kilimanjaro Challenge ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania na Dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila kuathiriwa na VVU/UKIMWI katika miaka ijayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko alisema takwimu zilizotolewa na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), zimeonesha kupungua kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 5.1 % mwaka 2011/ 2012 hadi asilimia 4.7% mwaka 2016/17.

Alisema mwaka wa 2016, inakadiriwa kuwa watu milioni 1.5 nchini wanaoishi na VVU na UKIMWI hadi sasa watu 225 wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa siku. Ugonjwa huu umewaathiri zaidi vijana na watoto yatima zaidi. Tunahitaji kubadilisha hali hii.

Aidha, aliongeza kuwa lengo la kukusanya fedha ni kuweza kusaidia serikali ya Tanzania katika jitihada zake kufikia sifuri tatu. Sifuri katika maambukizi mapya, sifuri ya unyanyapaa, sifuri katika vifo vitokanavyo na UKIMWI.

“TACAIDS kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na wadau wengine kwa kupitia mpango huu wa Kili Challenge tunapenda kutoa mchango na ushirikiano wetu kwa Taifa ili kutunisha mfuko utakaowezesha kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huu. Tuna matumaini ya kujenga timu imara yenye hamasa ya kupambana na janga hili.

“Tunatoa wito kwa makampuni na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, wajitokeze ili tusaidiaane kutunisha mfuko wa Kili Challenge na mwishowe kufikia malengo yetu ya kuhakikisha tunakuwa na kizazi kisicho na maambukizi ya VVU/ UKIMWI,” alisema Dkt. Leonard Maboko.

Makamu wa rais miradi endelevu wa kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo alisema shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika tarehe 4 Juni mwaka huu na kuzinduliwa na Waziri wa Uwekezaji Angellah Kariuki ambapo atafanya zoezi la ugawaji wa fedha zilizokusanywa mwaka jana 2018 zilizopatikana baada ya wadau mbalimbali kupanda na kuendesha baiskeli na kuzunguzuka Mlima Kilimanjaro.

Alisema kuna tatizo linaloikabili jamii sasa ambapo baadhi yao wanawatenga na kukataa kuishi na watu wenye maambukizi ya VVU/ UKIMWI, kutokana na tatizo hilo Mgodi wa Dhahabu wa Geita, umeamua kuwekeza katika mradi huu kwa kuuwezesha kuwa mradi wa kitaifa na si wa GGM

“Huu ni mwaka wa 18 sasa tangu Kili Challenge ianze. Pia zaidi ya watu 800 kutoka pande mbalimbali za dunia wameshiriki. Taasisi zaidi ya 40 zimefaidika kutokana na utunishaji wa mfuko huu kwa sababu taasisi ambazo hazina fedha za kuendesha kampeni na shughuli mbalimbali za mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI zimekuwa zikifaidika na mfuko huu. Pamoja na mambo mengine, watoto waliopoteza wazazi wao sasa wanaweza kutabasamu tena kutokana na uangalizi pamoja na upendo wanaoupata kutokana na mfuko huu.

“Tunapenda pia kutambua ushirikiano wa kampuni na taasisi mbalimbali kama vile ACACIA, AKO, Mantrac, NSSF, PUMA, TOYOTA, Prime Fuels, Coastal Aviation, Airtel, Capital Drilling, PPF, Serena Hotel, Geita Power Limited, SGS na wadau wengine tunaoshirikiana nao. Tunawashuruku kutokana na ushirikiano wenu katika mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI hivyo, tunaweza kufurahia mafanikio haya kwa kuwa na mradi endelevu,” aliongeza Simon Shayo.

Balozi wa Kili Challenge ambaye pia ni mwanamuziki maarufu nchini Tanzania, Mrisho Mpoto alisema jamii inapaswa kuacha kuwa tegemezi kwa sababu ina uwezo wa kujisimamia kwa kutumia vyombo vya habari, na watu wenye ushawishi mkubwa na kwa pamoja; UKIMWI unaepukiki.

Makamu wa rais miradi endelevu wa kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu uzinduzi wa zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2019), na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka 2019 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini. Uzinduzi huo unafanyika Juni 4 mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko.

Wafanyabiashara Nzega Wamlalamikia Meneja Wa TRA Tabora

$
0
0
Editha Edward-Tabora 

Wafanya biashara wilayani Nzega mjini Mkoani Tabora wamelalamikia mwingiliano wa kimamlaka wa ukusanyajj wa ushuru wa  huduma  kati ya Halmashauri ya wilaya ya Nzega na mamlaka ya mapato  Tanzania (TRA) ambayo yamekuwa yakiwaathiri  kibiashara wilayani humo 

Yamesemwa hayo katika kikao kilichoitishwa na meneja wa mamlaka ya mapato  Tanzania (TRA)  mkoa wa Tabora Thomas  Masese  ambacho alikiitisha kwa ajili ya kupokea ushauri na kero kutoka kwa Wafanyabiashara wa wilayani humo wakaitumia fursa hiyo kulalamikia mwingiliano wa ukusanyaji wa ushuru baina ya Halmashauri ya mji na TRA

Baadhi ya Wafanyabiashara hao akiwemo self Haruna wametaka kujua ni nani mwenye dhamana ya kukusanya ushuru kati ya   TRA  na Halmashauri ya mji na kwa viwango gani vya malipo na kwa biashara zipi ambazo wanapaswa kulipia ili kuondoa mkanganyiko huo

Katika kikao hicho Wafanyabiashara hao wameiomba TRA kuongeza timu ya Maafisa ili kuharakisha kutembelea biashara na kutoa ukadiliaji wa ulipaji wa kodi pamoja na kuhimiza kampuni iliyopewa jukumu la kusambaza Mashine za EFD toka mwaka juzi kupeleka Mashine hizo

Akijibu malalamiko hayo meneja wa mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Tabora Thomas Masese amebainisha  utofauti wa ukusanyaji wa ushuru kati ya taasisi yake na Halmashauri kwa kuchukua asilimia kutoka kwa Wafanyabiashara na kuwa ahidi Wafanyabiashara hao kukutana na Mkurugenzi ili kuweza kuondoa usumbufu huo.
Pichani ni Meneja wa TRA Tabora  Thomas Masese akizungumza na Wafanyabiashara katika kikao kilichofanyika mjini Nzega.

UZINDUZI WA MASHINDANO YA UMITASHUMTA YAFANYIKA JIJINI ARUSHA CHINI YA UDHAMINI WA TTCL

$
0
0


Kutoka katikati ni Afisa Utamaduni Jiji la Arusha Benson Maneno,aliyepo kulia kwake ni Meneja wa TTCL mkoa wa Arusha na Manyara,Brown Japhet
Meneja wa TTCL mkoa wa Arusha na Manyara,Brown Japhet akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Arusha katika katika uzinduzi rasmi wa michezo ya UMITASHUMTA.
Meneja wa TTCL mkoa wa Arusha na Manyara,Brown Japhet akimkabidhi mpira Afisa Utamaduni Jiji la Arusha Benson Maneno kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mashindano hayo.
Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Ngarenaro Nuru Jofrey Mungure mchezaji wa mpira wa miguu ameihakikishia shule yake kuwa watafanya vizuri hadi kufikia ngazi ya Taifa.
Mwanafunzi Salha,Mashaka Rajabu kutoka shule ya msingi Ngarenaro amewaomba wazazi wavumbue vipaji vya watoto wao wasivifike kwani michezo ni Afya na Ajira.
Mwanafunzi kutoka shule mojawapo katika Jiji la Arusha anayecheza mpira wa mikono Handball



Na.Vero Ignatus,Arusha.

Halmashauri ya Jiji la Arusha imeingia ubia na Shirika la simu la TTCL ,Mkoani Arusha,katika maswala ya mashindano ya michezo kwa vijana katika shule za Msingi UMITASHUMTA

Benson Maneno ni Afisa utamaduni katika Jiii la Arusha amesema Michezo hiyo imedhaminiwa na TTCL katika msimu wote wa mashindano ambapo yataanza kesho june 4 na kushirikisha vijana 500 lakini katoka mchujo watachukua vijana 100 peke yake ambao watawaingiza katika timu ya mkoa wa Arusha

Maneno amesema Halmashauri ya Jiji la Arusha imejipanga kikamilifu kwa mashindano hayo kuhakikisha inafanya vizuri ambapo tamebeba kauli mbiu isemayo "Michezo na TTCL Rudi nyumbani kumenoga"

Kwa upande wake Meneja wa TTCL mkoa wa Arusha na Manyara,Brown Japhet amesema kampuni hiyo imeguswa kusaidia sekta ya michezo katika.Jiji la Arusha kwa kuwa michezo ni sehemu ya ajira na wanamichezo wengi duniani wanamafanikio makubwa kutokana na michezo.

Amesema kupitia michezo hiyo kampuni ya TTCL itajitangaza Kitaifa na kimataifa na amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kuitangaza kampuni hiyo ya kitanzania inayoungwa mkono na serikali.

Katika hafla hiyo likiendana na ugawaji wa line za simu za TTCL kwa washiriki ambapo wamepata fursa kujipatia kama sehemu ya wadau muhimu katika kulitangaza kampuni hilo .

MKUTANO WA NISHATI KWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAANZA ARUSHA

$
0
0
Na Veronica Simba – Arusha
Mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki, umeanza leo Juni 3, 2019 jijini Arusha.

Akifungua Mkutano huo katika siku ya kwanza ambao unahusisha ngazi ya wataalamu wa sekta husika; Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na Utawala, Christopher Bazivamo, amewataka kujadili kwa uwazi changamoto zinazokabili nchi wanachama hususan upatikanaji wa umeme wa uhakika ili kuainisha mikakati ya kuzitatua.

“Jamii zetu bado hazijawa na umeme wa uhakika ukilinganisha na sehemu nyingine za Dunia. Hii ni changamoto ambayo tunahitaji kuitafutia ufumbuzi. Tujadili kwa uwazi ili tuone wapi tunakwama na namna gani tutatue,” amesisitiza.

Akifafanua zaidi, Bazivamo amesema changamoto za nishati kwa nchi za Afrika Mashariki zinahusisha mambo mbalimbali ikiwemo nishati ya kupikia ambayo ameeleza kuwa asilimia kubwa ya wanajamii wa ukanda husika wangali wanatumia kuni na mkaa; hali inayochangia uharibifu wa mazingira.

Amesema haitoshi kuwaonesha wananchi kuwa nishati ipo isipokuwa kuchukua hatua za kuifanya ipatikane kwao na kwa bei wanayoweza kuimudu.

Aidha, Bazivamo amewashauri wataalamu husika, kuhakikisha wakati wanahamasisha uwekezaji katika uzalishaji wa umeme, wahamasishe pia uwekezaji katika usambazaji wa nishati hiyo ili kuwezesha hali ya upatikanaji wake kwa jamii.  

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo wa 14 unatarajia kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa miradi na programu katika sekta ya nishati pamoja na maagizo yaliyotolewa katika Mkutano wa 13 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati.

Aidha, Mkutano utapokea Rasimu ya Makubaliano ya Awali (MoU) iliyoandaliwa na Sektetarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Mradi wa Umeme wa Nsongezi katika Mto Kagera unaotarajiwa kutekelezwa kwa ushirika wa nchi za Tanzania, Uganda na Rwanda ili ipitiwe na nchi husika.

Mkutano ngazi ya Mawaziri utafanyika Juni 7 mwaka huu, ambayo ndiyo siku ya mwisho ya mkutano husika.

Tanzania inawakilishwa na wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na taasisi mbalimbali zinazohusiana na nishati kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na Utawala, Christopher Bazivamo, akifungua Mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ngazi ya wataalamu, Juni 3, 2019 jijini Arusha.


Wajumbe wa Mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ngazi ya wataalamu, wakishiriki ufunguzi wa Mkutano huo Juni 3, 2019 jijini Arusha.

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA BALOZI WA UTURUKY NCHINI TANZANIA NA UJUMBE WAKE IKULU ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Mhe. Ali Davutaglu, alipofika Ikulu Zanzibar na Ujumbe wa Kampuni ya Okan kutoka Nchini Uturuki.(Picha na Ikulu)


 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania kushoto Mhe. Ali Davutaglu,Mwenyekiti wa Kampuni ya Okan, Bwa. Bekir Okan na Ugur Erkray, wakiwa katika mazungumzo hayo yaliofanyika Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Okan ya Uturuki Bwa. Bekir Okan na Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Mhe. Ali Davuttaglu, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Balozi Seif ashiriki futari na wananachi wa Mbweni

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Afria Bwana Wasia Mushi kushoto yake kuelekea kwenye futari ya pamoja iliyoandalia na Benki hiyo katika Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni.
 Balozi Seif akisalimiana na Naibu Waziri Kiongozi Mstaafu wa SMZ MH. Omar Ramadhan Mapuri ambae ni Mteja wa Benki ya Afrika kabla ya kuanza kwa Futari ya pamoja.
 Balozi Seif akijumika na Watu mbali mbali katika Futari ya pamoja pamoja iliyoandalia na Benki hiyo katika Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akijumuika na Watu mbali mbali katika Futari ya pamoja pamoja iliyoandalia na Benki hiyo katika Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni.

 Washiriki wa Futari ya pamoja kutoka maeneo mbali mbali waliojumuishwa na Uongozi wa Benki ya Afrika iliyofanyika katika Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni.
 Meneja wa Benki ya Afrika Tawi la Zanzibar Bwana Juma Burhan akitoa maelezo ya ufanisi wa majukumu ya Taasisi hiyo ya Fedha.
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Afrika { BOA} Bwana Wasia Mushi akiipongeza SMZ na Wananchi wa Zanzibar kwa kuipokea vyema Benki hiyo tokea ilipoanza kutoka huduma Visiwani Miaka Mitatu iliyopita.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Afrika { BOA} Bwana Wasia Mushi wakiteta wakati wa Futari ya pamoja hapo Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa nasaha ya watedaji wa Taasisi za huduma za Fedha kuzingatia uadilifu katika majukumu yao ya kila siku. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema umainifu mkubwa unaowajibika kutekelezwa na Watendaji wa Taasisi zote zinazosimamia masuala ya Fedha mahali popote pale ndio jambo la msingi linaloshajiisha Jamii kujenga imani ya kuwekeza mitaji yao kwenye Taasisi hizo.

Alisema udokoaji wa mitaji ya wateja ambayo wakati mwengine hufanywa na watendaji wasio waaminifu hupelekea baadhi ya Taasisi hizo kulazimika kufungwa na Mamlaka za Serikali zinazosimamia taasisi hizo baada ya kufilisika.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa tahadhari hiyo mara baada ya Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Uongozi wa Benki ya Afrika {BOA} iliyowashirikisha Wateja, Viongozi na Wananchi tofauti na kufanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinatul Bahr iliyopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Alisema uaminifu ni silaha kubwa na ya msingi inayoleta msukumo wa kujenga Imani thabiti baina ya Wateja na Taasisi zinayosimamia na kutunza Mitaji yao jambo linalopaswa kuzingatiwa kwa uadilifu uliotukuka.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi na Watendaji wa Benki ya Afrika {BOA} kwa kufanyakazi kwa uadilifu uliopelekea Tawi la Benki hiyo liliopo Zanzibar kuongoza katika utoaji wa huduma za Kibenki ikilinganishwa na Matawi mengine ya Benki hiyo yaliyopo Tanzania.

Alisema uadilifu huo umemtia moyo na kushawishika kuwa tayari kufungua Akaunti ndani ya Benki hiyo na kuwashawishi Wananchi pamoja na Watumishi wa Taasisi za umma kuitumia fursa hiyo adhimu kwa maslahi yao ya sasa na hapo baadae.

Balozi Seif aliuhakikishia Uongozi wa Benki ya Afrika kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa tayari muda wowote kutoa msaada katika kuona malengo ya Benki hiyo yanafanikiwa kama yalivyopangwa.

Akizungumzia ucha mungu uliokuwa ukitekelezwa na kuzingatiwa na Waumini wa Dini ya Kiislamu ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Balozi Seif alisisitiza umuhimu wa kuendelezwa yale yote mazuri katika Miezi ijayo ambayo yalifanywa katika kipindi hicho.

Alisema haitapendeza hata kidogo na ni dhambi kwa Waumini hao kuwa na tabia yaWanyama wanaofungiwa kwenye zizi wanapoachiliwa ikawa balaa inayoenea mitaani na kuleta mtafaruku katika Jamii.

Mapema Meneja wa Benki ya Afrika Tawi la Zanzibar Bwana Juma Burhan alisema Taasisi hiyo ya Fedha imefanya mambo makubwa tokea kuanzishwa kwake Zanzibar Miaka Mitatu iliyopita kutokana na kuungwa mkono na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wananchi mbali mbali.

Bwana Juma alisema kipindi hicho cha miaka Mitatu kimeiwezesha Benki hiyo kusaini Mkataba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kutoa mikopo kwa Watumishi wa Wizara 10 za SMZ.

Alisema mikopo hiyo iliyohusisha miradi tofauti ya kuwaongezea uwezo wa kipato cha kukimu Maisha Watumish hao pia ilizihusisha Taasisi Saba Binafsi zinazotoa huduma Visiwani Zanzibar.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Afrika { BOA} Bwana Wasia Mushi alieleza kwamba Zanzibar imejionyesha katika ramani ya Dunia kukua kwa haraka Uchumi wake jambo ambalo Taasisi za Kifedha zina kila sababu ya kuwekeza miradi yao katika kutoa huduma za haraka kwa wateja.

Bwana Mushi alisema ufanisi wa huduma za Fedha kama ulivyopatikana kwa Tawi la Benki yao hapa Zanzibar kuongoza kwa huduma zake ikilinganishwa na Matawi 16 yaliyopo Nchini Tanzania ni jambo la msingi katika Maendeleo ya Taifa na Wananchi wake.

Alisema Benki hiyo ya Kimataifa iliyopata mafanikio makubwa tokea kuasisiwa kwake Nchini Morocco hivi sasa imeshakuwa na Matawi 18 pekee ndani ya Bara la Afrika, Marekani, China wakati Nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki zikisheheni Matawi ya Benki hiyo.


Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images