Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

KAMILISHENI UJENZI WA MAGEREZA ZA WILAYA-MAJALIWA

$
0
0
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola wakati alipowasili kwenye viwanja vya Gereza la Wilaya ya Ruangwa kufungua Gereza hilo, Juni 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola wakati alipowasili kwenye viwanja vya Gereza la Wilaya ya Ruangwa kuzindua Gereza hilo, Juni 3, 2019. Kulia ni Mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamishina Jenerali wa Magereza,   Phaustine Kasike wakati alipowasili kwenye viwanja vya Gereza la wilaya ya Ruangwa kufungua Gereza hilo, Juni 3, 2019.  Katikati ni mkewe Mary.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Askari Magereza wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kabla ya kufungua Gereza la Wilaya ya Ruangwa, June 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wa tatu kulia) wakifungua Gereza la wilaya ya Ruangwa Juni 3, 20, 19. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa , wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na kushoto ni Kamishina Jenerali wa  Magereza, Phaustine Kisike. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkewe Mary ((wa pili kulia)  wakitazama gari alilolitoa Waziri Mkuu kwa Gereza la Wilaya ya Ruangwa wakati alipofungua Gereza hilo, Juni 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Gereza la Wilaya ya Ruangwa Juni 3, 2019.  Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Maofisa wa Jeshi la Magereza baada ya kufungua Gereza la Wilaya ya Ruangwa, Juni 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa Jeshi la Magereza nchini ukamilishe mkakati wa ujenzi wa magereza za wilaya kwa wilaya zisizokuwa na magereza.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Juni 3, 2019) wakati akifungua Gereza la wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Uzinduzi huo umefanyika kwenye viwanja vya gereza hilo. 

Waziri Mkuu amesema uwepo wa magereza katika wilaya zote nchini utasaidia kumaliza tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu kwenye magereza ya jirani.

“Kutokuwepo kwa magereza ya wilaya kunasababisha msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza ya jirani, pamoja na kuchelewesha upatikanaji wa haki.”

Waziri Mkuu amesema kwamba ufunguzi wa gereza la Ruangwa utatatua tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu katika Gereza la wilaya ya Nachingwea 

Awali wakazi wa wilaya hiyo waliokabiliwa na tuhuma mbalimbali au waliohukumiwa vifungo walikuwa wakipelekwa katika Gereza la wilaya ya Nachingwea.

Amesema kitendo cha kupelekwa Nachingwea kilikuwa kikiwanyima wafungwa na mahabusu fursa ya kuonana na ndugu au mawakili wao kutokana na umbali uliokuwepo.

“Mbali na ndugu na jamaa kushindwa kwenda kuwaona ndugu zao pia Jeshi la Polisi lilikuwa likilaumiwa kuwa linawachelewesha mahubusu kuja kusikiliza mashauri yao.”

Waziri Mkuu amesema uwepo wa gereza hilo katika wilaya ya Ruangwa umeipunguzia Serikali gharama za kuwasafirisha mahabusu na wafungwa kwenda Nachingwea. 
Awali, Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Gereza la Wilaya ya Ruangwa ni nyenzo muhimu katika kuimarisha ulinzi na usalama wa wilaya hiyo.

Amesema gereza hilo ni chachu ya kuimarika kwa uchumi wa wilaya hiyo kwa kupitia sekta ya kilimo kwani kutakuwa na kambi za kilimo, hivyo wananchi nao watajifunza.  

 “Wananchi msilione gereza hili kama adui kwenu, halijaja kuwafunga bali lipo kwa ajili ya kuimarisha amani, ulinzi na usalama wa wilaya yetu pamoja na kutoa elimu mbalimbali.”

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike amesema ujenzi huo umefanywa na kikosi cha ujenzi cha Magereza kwa kutumia nguvukazi ya wafungwa.

Amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa gereza hilo imekamilika na imegharimu sh. bilioni 1.5 hivyo umekamilisha uwepo wa magereza katika wilaya zote za mkoa wa Lindi. Kamishna huyo amesema ujenzi huo ungefanywa na mkandarasi wa nje ungegharimu sh. bilioni 2.226, hivyo kwa kutumia kikosi cha Magereza wameokoa sh. milioni 635.675.

Amesema kwa sasa gereza hilo lina uwezo wa kuwahifadhi wahalifu 250 hadi 280 na likikamilika itakuwa na uwezo wa kuwahifadhi wahalifu 500.
Kamishna Kasike amesema gereza hilo lina ardhi yenye ukubwa wa ekari 80, ambapo ekari saba zitatumika kwa ajili ya majengo ya gereza, maegezo ya magari na karakana.

“Ekari 56 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 100 za makazi, ekari sita ujenzi wa majengo ya huduma kama zahanati na ekari nane zitatumika katika kilimo cha bustani.”

Baadhi ya wananchi waliohudhuria ufunguzi huo wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuboresha huduma za jamii.

Mmoja wa wananchi hao Zena Selemani amesema kabla ya ujenzi wa gereza hilo walikuwa wanashindwa kuwatembelea ndugu zao walofungwa katika gereza la Nachingwea.

RAIA WA SWIDEN WANUSURIKA KUFUNGWA JELA BAADA YA KULIPA FAINI YA MIL 20/- KILA MMOJA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

MKURUGENZI wa Kampuni ya Biabana Anna Kristina Edler, (54) na mumewe Anders Svensson 58 wamefanikiwa kulipa faini ya Sh.milioni 20 kwa kila mmoja na hivyo kukwepa kifungo cha kwenda jela mwaka mmoja na nusu.

Edler na Svensson walikuwa wamehukumiwa na kulipa faini hiyo au kutumikia kifungo hicho baada ya kukiri tuhuma za kuajiri raia wa nje ya nchi na kujihusisha na kazi bila ya kuwa na kibali nchini

Wakati hukumu ikisomwa mahakamani hapo leo Juni 3,mwaka 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo washtakiwa hao raia wa Swiden wanakabiliwa na mashtaka mawili, likiwemo la kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali.

Baada ya kusomewa mashtaka yao, washtakiwa wamekiri na wamehukumiwa kulipa faini au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu gerezani.

Mapema akisoma mashtaka yao, Wakili wa Serikali Daisy Makakala amedai kati ya Agosti 18 mwaka Jana na Aprili 3, 2019 huko Mikocheni jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Elder akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Biabana Ltd alimuajiri Anders na kufanya kazi katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka idara yavUhamiaji.

Katika shtaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo mshtakiwa Enders alijihusisha na kazi kama muajiriwa wa kampuni ya Biabana LTD bila ya kuwa na kibali kinachotolewa na idaravya Uhamiaji.

Hata hivyo wamefanikiwa kukwepa kifungo cha kwenda ndani jela mwaka mmoja na nusu jela baada ya kulipa faini ya Sh.milioni 20 kwa kila mmoja.

WADAU WAKUTANA KUJADILI MAPENDEKEZO YA SHERIA NDOGO KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amefungua mkutano wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto kwa ajili ya kujadili Mapendekezo ya sheria ndogo za vijiji/halmashauri za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga.

Mkutano huo uliolenga kujadili kwa pamoja mikakati inayolenga kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto ili kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga,umefanyika leo Jumatatu Juni 3,2019 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Telack alisema ili kuondoa vifo hivyo ni vyema akina mama wajawazito wanahudhuria kliniki akibainisha kuwa pia ni jukumu la baba kumhamasisha mkewe kuhudhuria kliniki na kujifungulia kwenye vituo vya afya.

“Takwimu za mwaka 2018 zinaonesha kuwa vifo vitokanavyo na uzazi mkoani Shinyanga vilipungua hadi 56 kutoka vifo 73 mwaka 2017,vifo vya watoto wachanga vilipungua kutoka 915 mwaka 2017 hadi 913 mwaka 2018”,alieleza.

“Ingawa takwimu za vifo zinaonesha kupungua.Nia ya serikali ni kuhakikisha mama mjamzito anajifungua salama na mtoto wake anakua,Sote tutambue kuwa hakuna mama anayestahili kufa wakati wa uzazi wala mtoto mchanga,hivyo ni lazima wadau wote tusongeze jitihada,mikakati na rasilimali ili kuhakikisha tunakuwa na vifo 0”,aliongeza Telack.

Mkuu huyo wa mkoa alisema,Rasimu ya mapendekezo ya uundwaji wa sheria ndogo za kuboresha afya ya uzazi na mtoto imejumuisha mawazo kutoka kwa watendaji wa sekta ya afya ngazi za halmashauri na kusititiza kuwa sheria ndogo zitakazoundwa zisikinzane na Sheria mama,sera na miongozo katika sekta ya afya.

“Ninafurahi kuona kwamba moja ya mkakati katika makubaliano yetu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ unatekelezwa.Nawaelekeza wanasheria wa halmashauri na Mwanasheria wa mkoa ambao pia ni washiriki wa mkutano huu kutumia weledi wao kushauri na kuhakikisha kwamba kazi hii inakamilika kwa wakati”,aliongeza.

Akiwasilisha rasimu ya sheria ndogo za vijiji/halmashauri za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt.Rashid Mfaume alivitaja visababishi vinavyochangia vifo vya mama na mtoto kuwa ni kutokuhuduria kliniki kwa wakati na mfumo dume unaosababisha mwanamke kutokuwa na maamuzi.

Alisema sababu zingine kuwa ni kutokufuata ushauri unaotolewa na wataalamu,mila na desturi potofu pamoja na jamii kukosa elimu ya kutosha kuhusu dalili za hatari za mjamzito,mzazi ana watoto wachanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akifungua mkutano wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto ili kujadili Mapendekezo ya sheria ndogo za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza katika mkutano wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko,kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt.Rashid Mfaume akiwasilisha Mapendekezo/rasimu ya sheria ndogo za vijiji/halmashauri za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto ili kujadili Mapendekezo ya sheria ndogo za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa Huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoa wa Shinyanga,Joyce Kondoro akitoa taarifa ya huduma za afya ya mama na mtoto mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akiongoza majadiliano wakati wa mkutano wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto ili kujadili Mapendekezo ya sheria ndogo za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga.
Wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Wenyeviti wa halmashauri za wilaya wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Boniface Butondo akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Simon Berege akichangia hoja ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

HALI ILIVYO KINONDONI KUELEKEA SIKUKUU YA EID EL FITR

$
0
0
Wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye mnada unaofanyika kwenye viwanja vya biafra wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam waki nunua mahitaji mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya sikuku ya Eid El Fitr hali hii imekuwa ni kawaida kutokea katika maeneo mbalimbali ya jiji hasa inapofika wakati wa kukaribia sikukuu. (picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
Wakinamama wakiewa katika zoezi la kusagula sagula viwalo mbalimbali vya kutokea sikukuu.
Wananchi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa katika harakati za kutafuta mahitaji kuelekea sikukuu ya kuhitimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani katika mnada unaofanyika katika viwanja vya Biafra, wilaya ya Kinondini Dar es salaam.

MTUHUMIWA ATINGA MAHAKAMANI AKIWA AMEVAA NGUO ALIZOMWIBIA HAKIMU

$
0
0
*Hakimu apata mshtuko ahairisha kesi, amswekwa mtuhumiwa rumande, kesi kusikilizwa Juni 11 na hakimu mwingine

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
HAKIMU katika Mahakama ya Wilaya ya Otuke huko Uganda Kaskazini Alhamisi iliyopita aliachwa na mshangao baada ya mtuhumiwa kuingia mahakamani hapo akiwa amevaa nguo zake zilizoibiwa ambapo 
Kufuatia tukio hilo Hakimu alilazimika kuahirisha usikilizwaji wa kesi zote za siku ile kwa wiki moja kwa ajili ya kuimarika  kutokana na mshtuko alioupata.

Imeelezwa kuwa mshukiwa huyo aliyeingia mhakamani hapo aliachiwa huru na jaji Benjamin Seruru tarehe  24 Mei baada ya kukutwa na hatia  za kuiba mabegi, mtuhumiwa huyo Jimmy Oteng (34) mkazi wa Okelo katika kijiji cha Amone alikutwa na hatia za kuiba begi moja la ufuta kutoka nyumba moja  huko Okelo mwaka 2018 na akahukumiwa kifungo cha miezi 6 gerezani.

Hata hivyo Mei 24 hakimu Seruru aliamua kumwachia huru baada ya kushindwa kupatikana kwa baadhi ya ushahidi dhidi yake.

Siku moja baada ya kuachiwa kutoka jela Oteng alifanya tukio la wizi nyumbani kwa hakimu huyo kwa kuiba suti jozi nne na nguo nyingine pamoja na madumu mawili ya lita 20 aliyodhani ni ya mafuta ya kupikia na alikamatwa siku ya jumatano wiki iliyopita.

 Kamanda wa polisi wa Otuke alilieleza gazeti la Daily Monitor kuwa mtuhumiwa huyo amewahi kuiba katika nyumba mbili za watumishi wa mahakama ambao walieleza kuwa Oteng amewahi kuiba mafuta ya kupikia pamoja na vifaa vingine vya nyumbani na baadaye kwenda nyumbani kwa hakimu kufanya wizi huo.

Imeripotiwa kuwa Oteng amekuwa akifanya matukio hayo wakati  mvua ikinyesha au wahusika wakiwa wameenda katika shughuli zao.

Imeelezwa kuwa baada ya kuiba katika nyumba ya hakimu alikutwa na wawindaji wawili amejificha katika kichaka huko Odugu katika kata ya Otuke ambao waliwaita polisi na akakamwatwa akiwa na vitu mbalimbali vilivyoibiwa katika nyumba ya hakimu zikiwemo suti jozi nne.

Kamanda wa polisi alieleza kuwa Oteng alifikishwa mahakamani siku ya alhamisi ambapo hakimu Seruru alihairisha kusikiliza kesi hiyo na kuamuru mtuhumiwa kubaki rumande hadi Juni 11 ambapo kesi hiyo itasikilizwa tena.

RC MAKONDA ATIMIZA AHADI YA KUWASHIKA MKONO WACHEZAJI WA SIMBA, AWAKABIDHI KITITA CHA MILIONI 24.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amewakabidhi wachezaji wa Simba kitita cha shilingi milioni 24 kama sehemu ya zawadi na hamasa kufuatia Timu hiyo kuchukuwa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara na kuingia katika robo fainali ya Klabu bingwa Afrika.

RC Makonda amewataka wachezaji hao kutumia fedha hizo kuanzisha miradi ya maendeleo itakayowasaidia kujipatia  kipato pindi watakapostaafu mpira huku akiwataka kutumia umaarufu na Brand zao kujiingizia kutengeneza kipato.

Aidha RC Makonda amesema katika mgawanyo wa fedha hizo Golikipa wa Simba Aish Manula amepokea kiasi cha Shilingi Milioni10, Wachezaji tisa Milioni 1 kila mmoja, Mchezaji bora wa kike wa Simba Queen Milioni 2 na Msemaji wa Simba Haji Manara ambae amepatiwa Milioni 3 kama sehemu ya kutambua mchango wake kwenye uhamasishaji wa mashabiki kujaa uwanjani.

Pamoja na hayo RC Makonda amewaasa wachezaji kuongeza morali ya uchezaji ili waendelee kunyakua ubingwa na kushika nafasi za juu katika ligi za kimataifa.

Hata hivyo RC Makonda amewataka wachezaji kuchukulia michezo kama pesa,uchumi, Amani na biashara inayoweza kuwafanya hao binafsi wanufaike kiuchumi na kulipatia taifa mapato ya kutosha kupitia mapato yanayoenda kwenye manispaa.

GWAJIMA ATINGA IKULU...ASEMA ILI ULE CHIPS MAYAI NI LAZIMA BAADHI YA MAYAI YAVUNJWE

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dk.Josephat Gwajima ametinga Ikulu ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza wazi kwamba ili ule Chips Mayai ni lazima baadhi ya mayai yavunjike.

Ameeleza namna ambavyo anafurahishwa na jitihada za Rais Dk.John Magufuli za kuleta maendeleo huku akitumia nafasi hiyo kumshukuru kwa jitihada zake za ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika Bonde la Mto Rufuji maarufu kwa jina la Stiegler.

Akizungumza leo Juni 3,2019 akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam, Askofu Dk.Gwajima amesema ni jambo nzuri kutoa shukrani kwa Rais Dk.John Magufuli kwa jitihada zake za kuleta maendeleo na hasa katika kuimarisha sekta ya nishati ya umeme.

"Kwanza ni jambo nzuri kuelewa ili ule Chips Mayai lazima uvunje baadhi mayai. Kuna mayai lazima yavunje.Namshukuru Rais kwa juhudi zake katika mradi wa umeme wa Stiegler, mahala ambapo tutazalisha umeme mwingi tofauti na hapo zamani .

"Kumbuka wakati wa Mwalim Nyerere,wakati wa Mwinyi, wakati wa Mkapa na wakati wa Jakaya Kikwete tulikuwa tunazalisha umeme kiasi lakini kupitia .... tutazalisha umeme mwingi kuliko Tanzania ilipoanzia,"amesema Askofu Gwajima.

Ameongeza kama ambavyo inafahamika watu wengi wa nchi za Magharibi wanasema eneo hilo ni kwa ajili ya mazingira pamoja na mambo mengine lakini ukweli hizo ni siasa za kimataifa.

"Kwa mfano ukiangalia miaka iliyopita kulikuwa na mkataba kule Japani uliokuwa unafahamika Mkataba wa Kioto na Marekani walikataa kusaini ule mkataba.Hivyo hata sisi tunatakiwa kulinda Interest zetu,"amesema Askofu Gwajima.

Kuhusu ujumbe wake kwa Watanzania,Askofu Gwajima amesema huu ni wakati wa kukimbia na si kutembea hivyo lazima twende na kasi ya dunia."Dunia inakimbia hivyo lazima nasi Watanzania tukimbie ili twende pamoja na dunia."

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima Ikulu jijini Dar es Salaam. 

MAGOLI YOTE NA PENATI: TEAM SAMATTA 6-3 TEAM KIBA (SAMAKIBA FOUNDATION - 2/6/2019)

RAIS DKT. MAGUFULI AFIKA KATIKA SOKO LA FERRY WAKATI ALIPOKUWA KATIKA MATEMBEZI YA JIONI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara wa Samaki katika Soko la Samaki la Ferry kuhusu umuhimu wa kutumia mifuko mbadala na kuachana na kutumia mifuko ya plastiki wakati alipopita katika matembezi ya jioni.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Samaki mbalimbali katika Soko la Ferry mara baada ya kufika eneo hilo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amebeba samaki wake kwa kutumia Kikapu mara baada ya kuwanunua katika Soko la Samaki la Ferry jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Samaki kabla ya kumnunua kutoka kwa mfanyabiashara wa Samaki Abraham Kaberege wakati alipkuwa katika matembezi ya jioni katika maeneo ya Soko hilo la Ferry jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua samaki huyo mara baada ya kumkagua. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wauza kahawa katika eneo la Soko la Ferry ambapo aliagiza kuboreshwa kwa sehemu ya biashara hiyo kuanzia siku ya kesho. PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI ATINGA SOKO LA SAMAKI FERRY AKIWA KATIKA MATEMBEZI YA JIONI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara wa Samaki katika Soko la Samaki la Ferry jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kutumia mifuko mbadala na kuachana na kutumia mifuko ya plastiki wakati alipopita katika matembezi ya jioni.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipatana bei ya Samaki aina ya Lobster na mmoja wa wachuuzi katika Soko la Ferry mara baada ya kufika eneo hilo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipatana bei ya Samaki na wachuuzi katika Soko la Ferry mara baada ya kufika eneo hilo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka baada ya kununua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Samaki kabla ya kumnunua kutoka kwa mfanyabiashara wa Samaki Abraham Kaberege wakati alipkuwa katika matembezi ya jioni katika maeneo ya Soko hilo la Ferry jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wauza kahawa katika eneo la Soko la Ferry ambapo aliagiza kuboreshwa kwa sehemu ya biashara hiyo kuanzia siku ya kesho. PICHA NA IKULU

Zoom Tanzania Embarks on a C2C Revolution

$
0
0
Since its beginning, Zoom Tanzania has been at the forefront of innovation. Whether by introducing a digital yellow pages in the late 2000’s, or providing a platform to support online trading, Zoom Tanzania has continuously improved the way it connects buyers and sellers through its digital platform. 
Staying true to its vision, Zoom Tanzania is further improving the way it does business, so that every Tanzanian can sell anything and everything. This will bolster the C2C growth in the country by creating a safe space for private individuals to sell many of the items they don’t have a use for. 

What does this mean? 
All sellers, both business and private, can list whatever they want to sell, without incurring any costs. If you’ve never sold something online before, now is the perfect time to start! And the benefits of selling unwanted goods are many. 
Make extra cash, free up space and even protect the environment by no longer resorting to dumping old items. Zoom Tanzania wants to empower sellers to become digitally savvy, fully able to manage their own listings and post whenever they want to. Sellers, and buyers, will be supported on every step of their journey, through online and offline education materials and How-to Guides covering topics from creating an account, to posting a great listing, to trading safely online, and more. 

Feedback and questions are always welcome and you can reach out to our committed team via the website (https://www.zoomtanzania.com/contact) or find us on Facebook, Instagram or Twitter. 

Zoom Tanzania is here to stay, dedicated to providing quality, varied content and being a safe platform to trade, and the same rigorous standards of moderation will be applied. Zoom is the place to find what you need, anywhere in the country. 

Zoom Tanzania, backed by Ringier One Africa Media (ROAM), is Tanzania’s number 1 online marketplace, trusted by thousands of buyers and sellers daily. ROAM is committed to transforming lives by connecting people through the power of online communities, both in Tanzania and across the African continent.

Zoom Tanzania Kuleta Mapinduzi ya Matangazo ya Mtandaoni

$
0
0

Tangu kuanzishwa kwake, Zoom Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika uvumbuzi wa jinsi ya kukutanisha watu na fursa mbalimbali. Kuanzia ujio wa kurasa za njano za digitali mwishoni mwa miaka ya 2000, mpaka kuanza kwa mtandao unaosaidia mauzo na manunuzi ya mtandaoni, Zoom Tanzania imejikita katika kuboresha jinsi inavyokutanisha wauzaji na wanunuzi kupitia mtandao wake.

Ili kubakia katika Maono yake, Zoom Tanzania inaendelea kuboresha jinsi inavyofanya biashara, ili kila Mtanzania aweze kuuza kitu chochote. Hii itakuza biashara ya kifungu cha mnunuzi kwenda kwa mnunuzi (C2C) nchini kwa kutengeneza nafasi rafiki na salama kwa mtu wa kawaida asiyekuwa mfanyabiashara kuuza vitu asivyovihitaji mtandaoni.

Hii ina maana Gani?

Wauzaji wote, wafanyabiashara na wasio wafanyabiashara, wanaweza kuuza kitu chochote kwenye mtandao wa Zoom Tanzania bila ya malipo yoyote. Kama haujawahi kuuza kitu mtandaoni, huu ni muda mzuri kuanza.

Kuna manufaa mengi kwa Watanzania yatokanayo na kuuza vitu vitu wasivyovihitaji. Wanaweza kupata kipato cha ziada, wanaweza kuweka huru nafasi iliyokuwa imechukuliwa na vitu wasivyovihitaji na kuitumia kwa tija zaidi, na pia wanaweza kuchochea jitihada za kulinda mazingira kwa kutokutupa vitu wasivyovitumia.

Zoom Tanzania itawapatia elimu wauzaji wake jinsi ya kuutumia mtandao wake ili waweze kusimamia matangazo yao, na kuwa uwezo wa kutangaza vitu wanavyouza pale wanapotaka. Wauzaji na wanunuzi watasaidiwa katika kila hatua ya safari hii, kupitia elimu itakayokuwa ikitolewa mtandaoni na nje ya mtandao. Pia kutakuwa na makala zitakazogusia jinsi ya kufungua akaunti, jinsi ya kuweka tangazo vizuri, jinsi ya kufanya mauzo na manunuzi salama nakadhalika. Mrejesho na maswali yanakaribishwa na wateja wanaweza kuwasiliana na timu yetu kupitia tovuti ya (www.zoomtanzania.com), kwa namba za simu, ama kupitia mitandao yetu ya kijamii.

Zoom Tanzania iko na itaendelea kuwepo, ikijizatiti kuwa mtandao wenye bidhaa tofauti na zenye ubora, na mtandao wenye usalama kutokana na njia madhubuti za uthibitisho wa vitu vinavyouzwa. Zoom Tanzania ni sehemu unayoweza kupata chochote unachotaka, popote nchini.

Zoom Tanzania, ikiwa chini ya Ringier One Africa Media (ROAM), ni mtandao namba moja Tanzania wa mauzo na manunuzi unaoaminiwa na maelfu ya wauzaji na wanunuzi kila siku. ROAM ina malengo ya kubadilisha maisha kwa kuunganisha watu kupitia nguvu za mitandao ya kijamii, kote Tanzania na Afrika kwa ujumla.

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAOMBA KUIDHINISHIWA BAJETI YA SHILINGI TRILIONI 11.94 MWA 2019/2020

$
0
0
 
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
 aadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga (kushoto). Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (katikati) na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga, wakifuatilia mawasilisho ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango yaliyowasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
 Baadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, baada ya kuwasilishwa kwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ambapo imeliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha shilingi trilioni 11.94 kwa ajili yamatumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)  na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, wakifuatilia kwa makini michango ya Wabunge wakijadili  Hotuba ya Bajeti ya Wizara ambapo Wizara imeliomba Bunge kuidhinishiwa kiasi cha shilingi trilioni 11.94 kwa ajili yamatumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango

VOA SWAHILI: Duniani Leo June 3, 2019

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AJUMUIKA NA WANANCHI WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI KATIKA FUTARI VIWANJA VYA IKULU ZANZIBAR

$
0
0

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyewkiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Dkt. Amani Karume, wakipata futari ya tende katika viwanja vya Ikulu Zanzibar na kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, futari hiyo imefanyika jana 2-6-2019,katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika katika Futari Maalum iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Zabnzibar kulia Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dkt. Amani Karume na kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarv Mhe, Seif Ali Iddi, wakijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Maghari katika futari hiyo iliofanyika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika futari Maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika viwanja vya Ikulu Zanzibar kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi. 

 WANANCHI wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakijumuika katika Futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katikac viwanja vya Ikulu Zanzibar.
 MABALOZI Wadogo wanaowakilisha Nchi Zanzibar wanaofanyia zao Zanzibar wakishiriki katika hafla ya futari Maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akizungumza na kutowa shukrani kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliofanyika Ikulu Zanzibar
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na kuagana Rais wa Mstaaf wa Zanzibar Mhe Dkt. Amani Karume, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk., Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Mama Fatma Karume, baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, na kulia Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na kuagana na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Mwananchi aliyehudhuria hafla ya futari iliofanyika viwanja vya Ikulu Zanzibar jana.
(Picha zote na Ikulu)

KAMILISHENI UJENZI WA MAGEREZA ZA WILAYA - WAZIRI MKUU MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa Jeshi la Magereza nchini ukamilishe mkakati wa ujenzi wa magereza za wilaya kwa wilaya zisizokuwa na magereza.
Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Juni 3, 2019) wakati akifungua Gereza la wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Uzinduzi huo umefanyika kwenye viwanja vya gereza hilo. 
Waziri Mkuu amesema uwepo wa magereza katika wilaya zote nchini utasaidia kumaliza tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu kwenye magereza ya jirani.
“Kutokuwepo kwa magereza ya wilaya kunasababisha msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza ya jirani, pamoja na kuchelewesha upatikanaji wa haki.”
Waziri Mkuu amesema kwamba ufunguzi wa gereza la Ruangwa utatatua tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu katika Gereza la wilaya ya Nachingwea 

Awali wakazi wa wilaya hiyo waliokabiliwa na tuhuma mbalimbali au waliohukumiwa vifungo walikuwa wakipelekwa katika Gereza la wilaya ya Nachingwea.
Amesema kitendo cha kupelekwa Nachingwea kilikuwa kikiwanyima wafungwa na mahabusu fursa ya kuonana na ndugu au mawakili wao kutokana na umbali uliokuwepo.
“Mbali na ndugu na jamaa kushindwa kwenda kuwaona ndugu zao pia Jeshi la Polisi lilikuwa likilaumiwa kuwa linawachelewesha mahubusu kuja kusikiliza mashauri yao.”
Waziri Mkuu amesema uwepo wa gereza hilo katika wilaya ya Ruangwa umeipunguzia Serikali gharama za kuwasafirisha mahabusu na wafungwa kwenda Nachingwea. 
Awali, Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Gereza la Wilaya ya Ruangwa ni nyenzo muhimu katika kuimarisha ulinzi na usalama wa wilaya hiyo.

Amesema gereza hilo ni chachu ya kuimarika kwa uchumi wa wilaya hiyo kwa kupitia sekta ya kilimo kwani kutakuwa na kambi za kilimo, hivyo wananchi nao watajifunza.  

 “Wananchi msilione gereza hili kama adui kwenu, halijaja kuwafunga bali lipo kwa ajili ya kuimarisha amani, ulinzi na usalama wa wilaya yetu pamoja na kutoa elimu mbalimbali.”

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike amesema ujenzi huo umefanywa na kikosi cha ujenzi cha Magereza kwa kutumia nguvukazi ya wafungwa.
Amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa gereza hilo imekamilika na imegharimu sh. bilioni 1.5 hivyo umekamilisha uwepo wa magereza katika wilaya zote za mkoa wa Lindi. Kamishna huyo amesema ujenzi huo ungefanywa na mkandarasi wa nje ungegharimu sh. bilioni 2.226, hivyo kwa kutumia kikosi cha Magereza wameokoa sh. milioni 635.675.

Amesema kwa sasa gereza hilo lina uwezo wa kuwahifadhi wahalifu 250 hadi 280 na likikamilika itakuwa na uwezo wa kuwahifadhi wahalifu 500.
Kamishna Kasike amesema gereza hilo lina ardhi yenye ukubwa wa ekari 80, ambapo ekari saba zitatumika kwa ajili ya majengo ya gereza, maegezo ya magari na karakana.
“Ekari 56 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 100 za makazi, ekari sita ujenzi wa majengo ya huduma kama zahanati na ekari nane zitatumika katika kilimo cha bustani.”
Baadhi ya wananchi waliohudhuria ufunguzi huo wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuboresha huduma za jamii.
Mmoja wa wananchi hao Zena Selemani amesema kabla ya ujenzi wa gereza hilo walikuwa wanashindwa kuwatembelea ndugu zao walofungwa katika gereza la Nachingwea.
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola wakati alipowasili kwenye viwanja vya Gereza la Wilaya ya Ruangwa kufungua Gereza hilo, Juni 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola wakati alipowasili kwenye viwanja vya Gereza la Wilaya ya Ruangwa kuzindua Gereza hilo, Juni 3, 2019. Kulia ni Mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamishina Jenerali wa Magereza,   Phaustine Kasike wakati alipowasili kwenye viwanja vya Gereza la wilaya ya Ruangwa kufungua Gereza hilo, Juni 3, 2019.  Katikati ni mkewe Mary.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Askari Magereza wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kabla ya kufungua Gereza la Wilaya ya Ruangwa, June 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wa tatu kulia) wakifungua Gereza la wilaya ya Ruangwa Juni 3, 20, 19. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa , wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na kushoto ni Kamishina Jenerali wa  Magereza, Phaustine Kisike. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkewe Mary ((wa pili kulia)  wakitazama gari alilolitoa Waziri Mkuu kwa Gereza la Wilaya ya Ruangwa wakati alipofungua Gereza hilo, Juni 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Gereza la Wilaya ya Ruangwa Juni 3, 2019.  Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Maofisa wa Jeshi la Magereza baada ya kufungua Gereza la Wilaya ya Ruangwa, Juni 3, 2019. 
(Picha na Habari na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAOMBA KUIDHINISHIWA BAJETI YA SHILINGI TRILIONI 11.94 KWA 2019/2020

$
0
0

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
 aadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga (kushoto). Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (katikati) na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga, wakifuatilia mawasilisho ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango yaliyowasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
 Baadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, baada ya kuwasilishwa kwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ambapo imeliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha shilingi trilioni 11.94 kwa ajili yamatumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)  na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, wakifuatilia kwa makini michango ya Wabunge wakijadili  Hotuba ya Bajeti ya Wizara ambapo Wizara imeliomba Bunge kuidhinishiwa kiasi cha shilingi trilioni 11.94 kwa ajili yamatumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)  na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, wakifuatilia kwa makini michango ya Wabunge wakijadili  Hotuba ya Bajeti ya Wizara ambapo Wizara imeliomba Bunge kuidhinishiwa kiasi cha shilingi trilioni 11.94 kwa ajili yamatumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango

BAKITA yaendelea na kutambua vituo vya Kswahili ndani na nje ya nchi.

$
0
0
 Askofu Dkt. Godfrey Malassy (kati) akikabidhiwa cheti cha utambuzi wa kituo chake binafsi cha Lugha ya Kiswahili na Utamaduni kilichoko huko Pretoria, Afrika Kusini. Anae kabidhi cheti ni Dkt. Sewangi Katibu Mtendaji BAKITA ofisi za Baraza hilo Kijitonyama Dar es salaam Jumatatu Juni 3, 2019. Kulia kwa Askofu ni ndugu Anorld Msofe, mchunguzi lugha na mratibu wa mafunzo ya Kiswahili kwa wageni BAKITA
  Askofu Dkt. Godfrey Malassy (kati) baada ya kukabidhiwa cheti cha utambuzi wa kituo chake binafsi cha Lugha ya Kiswahili na Utamaduni kilichoko huko Pretoria, Afrika Kusini. Kulia ni Dkt. Sewangi Katibu Mtendaji BAKITA wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Baraza hilo Kijitonyama Dar es salaam Jumatatu Juni 3, 2019. Kushoto ni  ndugu Anorld Msofe, mchunguzi lugha na mratibu wa mafunzo ya Kiswahili kwa wageni BAKITA
Askofu Dkt. Godfrey Malassy (kati) baada ya kukabidhiwa cheti cha utambuzi wa kituo chake binafsi cha Lugha ya Kiswahili na Utamaduni kilichoko huko Pretoria, Afrika Kusini. Kulia ni Dkt. Sewangi Katibu Mtendaji BAKITA wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Baraza hilo Kijitonyama Dar es salaam Jumatatu Juni 3, 2019. Kushoto ni  ndugu Anorld Msofe, mchunguzi lugha na mratibu wa mafunzo ya Kiswahili kwa wageni BAKITA.

Rwanda,Burundi na Zimbawe Zinahitaji Tani Zaidi ya Milioni Moja Za Mahindi - Hasunga

IGP SIMON SIRRO AWAONYA ASKARI WA UPELELEZI WANAOJIINGIZA KWENYE RUSHWA

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la  Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewaonya askari wa kitengo cha Upelelezi ndani ya Jeshi hilo kuhakikisha hawajiingizi kwenye vitendo vya rushwa sambana na kufanyakazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya Jeshi.
IGP Sirro ameyasema hayo wakati akizungumza na askari wanaopatiwa Mafunzo ya Upelelezi yanayofanyika katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Kurasini Dar es salaam, ambapo amewataka kuhakikisha wanapunguza mlundikano wa majalada mbalimbali ya kesi, sambamba na kupata ushahidi wa kutosha utakaowatia hatiani watuhumiwa wa makosa mbalimbali mara wanapofikishwa mbele ya mahakama.

Naye Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCP Charles Kenyera, amesema kuwa, ni vyema askari wa upelelezi kujikita katika kufanyakazi kwa uaminifu ili kutenda haki kwa wananchi na kwamba Jeshi la Polisi halitosita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu kwa askari wasiofuata taratibu na sheria za nchi.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Latest Images