Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

NMB YATOA NAFASI KWA WATU WATANO WENYE ULEMAVU KUJIFUNZA MAMBO MBALIMBALI

0
0
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV 

Benki ya NMB imetoa nafasi tano kwa watu wanaoishi na ulemavu kujifunza masuala tofauti ndani ya benki hiyo katika Idara zake mbalimbali kwa kipindi cha awali cha miezi mitatu. 

Benki hiyo imetoa nafasi hizo wakati wa uzinduzi wa mpango maalum ujulikanao kama 'All Inclusive' kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na Taasisi ya CEFA inayojihusisha na watu wenye Ulemavu pamoja na Hospitali ya CCBRT ya Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Rasilimaliwatu kutoka Benki hiyo, Emmanuel Akonaay amesema wametoa nafasi hizo kwa kuangalia ujuzi,mafunzo na elimu zao ambapo watapata nafasi ya kupata mafunzo kwa vitendo katika idara tofauti za benki hiyo.

Akonaay amesema NMB inaamini uwezo wa mtu uko kwenye kipaji na sio muonekano wake wa nje, amesema wametoa nafasi hizo kwa kwa watu wa jamii hiyo kuonyesha vipaji na baadae kutoa ajira kwao pale kutakapokuwa na uhitaji.

Kwa Upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Taaluma ndani ya Rasilimali watu kutoka Benki ya NMB, Joanitha Rwegasira amesema wamepokea Watu 25 watakaopata mafunzo hayo katika masuala ya Kifedha na masuala mbalimbali yakibenki. 

Naye Mmoja wa Watu wanaopata mafunzo hayo, Mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Faudhia Kitenge amesema amepata nafasi yakujifunza masuala mbalimbali ya utendaji wa kibenki.

Faudhia ametoa wito kwa Taasisi nyingine kutoa nafasi kama hizo kwa Watu wenye Ulemavu ili kutoa nafasi kwa kundi hilo kuonyesha vipaji na uwezo kwa jamii.

Mwakilishi kutoka Taasisi ya CEFA, Mratibu Mkuu wa Uwezeshaji Kiuchumi, Gerald Mpangala ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali kutoa mafunzo kama hayo kwa kuwapa Watu hao wenye Ulemavu mafunzo mbalimbali ikiwemo ya Kiuchumi, amewataka Wanafunzi watano waliopata nafasi hiyo kwenye Benki ya NMB kutumia ipasavyo nafasi hiyo kufunza.
Mkuu wa Kitengo Cha Taaluma ndani ya Rasilimali Watu, Joanitha Rwegasira Mrengo akieleza jambo kwenye ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu waliyoifanya  jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu Mwandamizi wa Vipaji, Mafunzo na uendelezaji wa benki ya NMB, Edith Mwiyombela, kizungumza wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu waliyoifanya Makao makuu ya benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu, Emmanuel Akonaay akifafanua jambo wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu  iliyofanyika mwishoni mwa wiki Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mtaalamu Mwanadamizi Uajiri wa Benki ya NMB, Eleanor Maseke akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu waliyoifanya katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja.

NAIBU WAZIRI JULIANA SHONZA AWAASA VIJANA VISIWANI ZANZIBAR KUTHAMINI VIPAJI VYAO

0
0

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akisalimiana na wachezaji wa timu ya Miembeni kabla ya kuanza kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Masauni/Jazeera uliofanyika katika Viwanja vya Tumbaku, Visiwani Zanzibar. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kundemba, kabla ya kuanza kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Masauni/Jazeera uliofanyika katika Viwanja vya Tumbaku, Visiwani 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza kabla ya kuanza mchezo wa Nusu Fainali wa Mashindano ya Masauni/Jazeera uliofanyika katika Viwanja vya Tumbaku, Visiwani Zanzibar. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akizungumza kabla ya kuanza mchezo wa Nusu Fainali wa Mashindano ya Masauni/Jazeera uliofanyika katika Viwanja vya Tumbaku, Visiwani Zanzibar. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Mpigapicha Wetu

Uchaguzi Mkuu Maalum MPC 'wengi watemwa, wachache warejea'

0
0
Mwenyekiti mpya wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza, Edwin Soko (katikati) akitoa salamu zake za shukrani baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika jana Juni 01, 2019 katika ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza kumchangua kushika nafasi hiyo hadi hapo mwakani 2020 uchaguzi mkuu utakapofanyika.

GB Pazzo, BMG
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) uliofanyika jana jumamosi Juni 01, 2019, wamewaondoa viongozi waliokuwa madarakani na kuwachagua viongozi wapya watakaokaa madarakani hadi mwakani 2020 utakapofanyika Uchaguzi/ Mkutano Mkuu.

Hatua hiyo ilijiri huku tayari tayari baadhi ya nafasi kama vile Mwenyekiti na Katibu Mkuu zikiwa wazi baada ya kujiuzulu mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu 2019 kufuatia mashinikizo kutoka kwa wanachama waliokuwa wakiwalalamikia kutotimiza vyema majukumu yao.

Katika uchaguzi huo, Edwin Soko alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti Albert Gsengo, Katibu Mkuu Magreth Kusekwa (akipanda kutoka Katibu Mkuu Msaidizi), Katibu Mkuu Msaidizi Projestus Binamungu, Mweka Hazina Paulina David (akitetea nafasi yake). Aidha mkutano huo pia uliwachagua wajumbe watano wa Kamati Tendaji MPC ambao ni George Binagi, Gloria Kiwia, Nashon Kennedy, Sitta Tuma pamoja na Philmon Malili (akitetea nafasi yake).

Itakumbukwa katika uchaguzi wa mwaka 2015, viongozi wa MPC waliochaguliwa walikuwa ni Mwenyekiti Osoro Nyawana (alijiuzulu), Makamu Mwenyekiti Neema Emmanuel, Katibu Mkuu Calvin Jilala (alijiuzulu), Katibu Mkuu Msaidi Magreth Kusekwa, Mweka Hazina Paulina David huku wajumbe wa Kamati Tendaji wakiwa ni Philmon Malili, Martha Lume, Antony Gervas, Shagatta Suleiman (amehamia mkoani Simiyu kikazi) na Neema Mwita (ametangulia mbele za haki).

Viongozi hao walipaswa kukaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu lakini baadae UTPC ambayo ni taasisi inayolea klabu za waandishi wa habari Tanzania ilibadili Katiba na hivyo kufanya kupindi cha uongozi kwa klabu zote nchini kuwa miaka mitano badala ya mitatu.
Tazama picha na kisha video kujua zaidi yaliyojiri kwenye Mkutano Mkuu Maalum MPC

Makamu Mwenyekiti wa MPC, Albert George Sengo akisisitiza umoja na mshikamano baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Katibu Mkuu MPC, Magreth Kusekwa akitoa shukrani zake baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo ambapo aliahidi ushirikiano ili kuhakikisha MPC inasonga mbele kimaendeleo.
Katibu Mkuu Msaidizi MPC, Projestus Binamungu akitoa salamu za shukrani ambapo alisisitiza uvumilivu miongozi mwa viongozi na wanachama kwa maslahi mapana ya chama.
Mweka Hazina MPC, Paulina David akiwashukru wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwa kumuamini na kumchagua kuitumikia tena nafasi hiyo.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati Tendaji MPC yenye wajumbe wa watano akitoa salamu za shukrani baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Nashin Kennedy akitoa salamu zake za shukrani.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Philmon Malili akiwashukru wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwa kumuamini na kumchagua tena kushika nafasi hiyo kwa mara nyingine.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Sitta Tuma akitoa salamu zake za shukrani baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Gloria Kiwia akiwashukru wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwa kumchagua kushika nafasi hiyo.
Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo kwa kushirikiana na Hilda Kileo (hayuko pichani), akitoa ujumbe wako kwa wanachama na viongozi wapya MPC.
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan (katikati) pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum MPC wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia mijadala kwa umakini.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo akiwemo aliyewahi kuwa Mwenyekiti MPC, Deus Bugaywa (katikati) wakifuatilia mawasilisho mbalimbali kwenye mkutano huo.
Viongozi wapia waliochagua kuiongoza MPC hadi hapo mwakani uchaguzi mkuu uakapofanyika kwa mujibu wa Katiba.
Wanachama wa MPC na viongozi wa UTPC wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wapya MPC.
Wanachama wa MPC na viongozi wa UTPC wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wapya MPC.
Baadhi ya viongozi wapya MPC wakipongezana baada ya uchaguzi.
Maakuli pia yalikuwepo.
Tazama Video hapa chini

MIKOA YA DAR NA TANGA YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WANACHI KUANGAMIZA MAZALIA YA MBU

0
0

Ziara yaWaziri wa afya Ummy Mwalimu,Naibu Waziri wake pamoja na viongozi mbalimbali mkoa wa DSM wakikagua eneo la jangwani katika mkakati wa kupulizia dawa za kuua mazalia ya mbu ili kukabiliana na homa ya dengue kwa mkoa huo 
…………………
Na.WAMJW,Dar es Salaam

Mikoa ya Dar es Salaam na Tanga imetakiwa kushirikiana na wananchi kuangamiza mazalia yote ya mbu kwa kunyunyizia dawa za kuua mbu wapevu kwa kutumia mashine kubwa.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipotembelea eneo la jangwani jijini hapa.

Waziri Ummy amefanya maamuzi haya baada ya mikoa hiyo kuathiriwa na ugonjwa wa homa ya Dengue”nimeelezwa mkoa wa Dar es Salaam unahitaji kununua lita 1000 za dawa aina ya Acteric 500 na Icteric 300 kwa ajili ya kunyunyizia mbu wapevu katika mitaa,ninawataka wakurugenzi wa Manispaa kuhakikisha dawahizi zinanunuliwa mara moja na.kufanya upuliziaji katika maeneo yenye mbu”Alisisitiza Wazirj Ummy.

Aidha, amewataka wamiliki na waendeshaji wa migahawa,bar,mahotel,saluni,gareji,mashule,maofisini na sehemu zote zinazozunguka maeneo yao wanakagua mazalia ya mbu,kufukia madimbwi ya maji na kufanya usafi kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu.

Hata hivyo alivitaka vituo vya kutoa huduma za afya vikiwemo vya watu binafsi kuzingatia taratibu na miongozo iliyopo ya kutoa taarifa kwa uongozi wa afya wa halmashauri kila siku wanapopima na.kugundua kuwa ntu ana ugonjwa wa dengue bila kuacha.

Wakati huohuo Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile amewataka watoa huduma za afya ambao sio waaminifu kutotoa majibu yasiyo sahii ya dengue na kutoa dawa zisizostahili kwa ugonjwa huu

“Tutaanza kuchukua hatuakali kwa watu wanaojirekodi na kusambaza klipu zinazosema watu wanywe maji ya mipapai au kupaka mafuta ya nazi ,tunasema ugonjwa huu hauna tiba hivyo mtu yeyote anayeona ana dalili hizo ni kufika kituo cha afya “Alisema Dkt.Ndugulile

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakari Kunenge amesema kama mkoa watatekelza maagizo yote na kuteketeza ugonjwa huo hivyo kuhakikisha wanaanza kupuliza dawa kwenye maeneo ya mazalia na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana kufanya usafi wa mazingira na kuondoa mazalia ya mbu kwa ustawi wa afya

P-SQUARE WANAMUZIKI MATAJIRI ZAIDI NIGERIA.

0
0
Na: Moshy Kiyungi,Dar es Salaam

Wapenzi wa muziki wa kizazi kipya duniani hususan Afrika, kundi la P-Square limeshika nafasi ya simulizi kufuatia kazi zao kukubalika.

Vijana hao wawili wa toka nchini Nigeria, Peter Okoye na Paul Okoye wanaounda kundi maarufu linalojulikana kama P-Square.

Vijana hao wanaelezwa kuwa licha ya kufanya muziki, ni wafanyabiashara wakubwa wa mafuta.Historia ya mapacha Peter na Paul inaeleza kuwa walizaliwa Novemba 18, 1981 jijini Lagos, Nigeria.

Walianza masomo katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Murumba ambayo ilikuwa ni shule ndogo ya Kikatolic huko Jas, nchini Nigeria.Mapacha hao walijiunga na shule ya muziki pamoja na maigizo ambapo walikuwa wakiimba na kucheza kwa kuwaiga akina Machael Jackson, MC Hammer na Bobby Brown.

Mwaka 1997 walianzisha kundi lililojulikana kwa jina la Smooth Criminal ambapo walikuwa wanacheza ‘Break dansi’.Kundi hilo lilianza kama kigenge cha mtaani kilichojulikana kwa majina ya MMMPP (M Clef a.k.a. Itemoh, Michael, Melvin, Peter and Paul).

Mnamo mwaka 1999 vijana hao Peter na Paul, wakaingia rasmi katika masomo ya muziki kuongeza ujuzi wao na kujifunza kupiga Gitaa pamoja na ngoma.Kazi zao za muziki zilianza kuingizwa katika filamu kama Tobi, Mama Sunday, Moment of Bitterness pamoja na Evas River.

Mwaka huo huo wakajiunga na Chuo Kikuu cha Abuja kusomea masuala ya Business Administration.Kwa bahati mbaya kujiunga na chuo hicho kulipelekea kundi lao la Smooth Criminal, kusambalatika kwa sababu M Clef, Michael na Melvin walisoma vyuo tofauti na wao.

Lakini vijana hao Peter na Paul hawakukata tamaa, wakaamua kuunda kundi lao jingine la watu wawili lililojulikana kama "Double P" ambalo nalo baadae jina la kundi hilo lilibadilika mara mbili ambapo liliitwa "P&P" na "Da Pees" na kundi ilo lilipotulia zaidi ndipo likajiita P-Square ambalo liliongozwa na Promota Bayo Odusami aka Howie T.

Mwaka 2001 P-SQUARE walijishindia katika mashindano yaliyojulikana kama "Grab Da Mic" kitendo ambacho kiliwavutia watu wengi mpaka Benson & Hedgesiliyoamua kuwadhamini katika album yao ya Last Nite ambayo iliachiwa na lebo ya Timbuk2 music.

Pia mwaka 2003 walishinda tena katika mashindano ya Amen, kama kundi bora la muziki wa R&B. Mwaka 2005 wakaachia album yao ya pili ya Get Squared chini ya lebo yao Square Records.

Album hiyo ilisambazwa kimataifa na TJoe Enterprises, ingawa walikuwa bado wanaongozwa na Howie T na video ya album yao ya pili ikachukua nafasi ya kwanza katika MTV Base kwa wiki kadhaa. Kundi lao likaweza kuwashirikisha wasanii wengine wa kimataifa kama Ginuwine, Sean Paul, Akon and Busola Keshiro.

Mwaka 2007 wakaachia album yao Game Over ambayo iliwaingizia pesa nyingi baada ya kuuza nakala milioni 8 Kimataifa. Mwaka 2009 wakaachia album yao ya nne Danger ambapo katika album hiyo waliweza kuwashirikisha akina 2Face Idibia, J Martins pamoja na Frenzy

Mwezi April 04, 2010 wakaitwa wasanii wa mwaka katika KORA All Africa Music Shughuli za utoaji tuzo hizo zilifanyika katika mji wa Ouagadougou, nchiniBurkina-Faso. Ambako walijishindia Dollars milioni 1.

P-Square waliweza kurekodi video pamoja na mwanamuziki machachari toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Awillo Longomba.


Mapacha hao wa kufanana, Peter na Paul Okoye, wametangazwa kushika nafasi ya Pili kwa utajiri nchini mwao.

P-Square walifanikiwa kuuza kila album waliyotoa kwa mauzo ya juu yakichagizwa na maonesho mbalimbali wanayofanya na kupelekea wakajitangaza zaidi Duniani.Aidha waliwashirikiana Wasanii wakubwa kama vile Akon, ikapelekea wasanii hao kutangazwa Wasanii bora wa mwaka 2010 kupitia Tuzo za Kora.

Vijana hao wanautajiri unaosemekana ni zaidi ya $3 million huku wakimiliki eneo lenye thamani kubwa nchini Nigeria la Square ville.Wanamiliki mali zenye thamani kubwa yakiwemo magari, ndege aina ya Airbus, waliyoinunua kwa ajili ya kusafiria kutoka katika moja ya Kampuni za Arabuni.

Peter na Paul Okoye, wanamiliki mali mbalimbali katika miji ya Jos na Port Harcout, likiwemo jumba la kifahari lenye thamani ya Naira milioni 400 lililopo katika mji wa Lagos.

Peter na Paul wametajwa kuwa ndio wanamuziki tajiri kuliko wote nchini Nigeria kwa sasa, wakiwa wamerekodi na kuuza albamu kadhaa sehemu mbalimbali duniani.

Wameingizwa kwenye klabu ya Mabilionea wa Nigeria.

MAJALIWA AKAGUA UJENZI SHULE YA SEKONDARI LUCAS MALIA,AKUTANA NA WENZAKE ALIOSOMA NAO SHULE YA MSINGI

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Mnacho wilayani Ruangwa, Juni 2, 2019. Kushoto ni Mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu David Mwakalobo. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Paroko wa Parokia ya Mnacho wilayani Ruangwa, Padri Gerold Nyagau wakimsikiliza Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa wakati alipozungumza baada ya Ibada ya Jumapili kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mnacho, Juni 2, 2019. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Paroko wa Parokia ya Mnacho, Padri Gerold Nyagau (wa pili kushoto) wakati alipokagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Mnacho wilayani Ruangwa, Juni 2, 2019. Kushoto ni Mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu David Mwakalobo. ……… 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Bibi Agnes Venance (kulia) na BW. Paskazi Mashimo (katikati) ambao alisoma nao katika Shule ya Msingi ya Mnacho wilayani Rungwa kwenye miaka ya 70 . Alisalimiana na wanafunzi wenzake hao baada ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Mnacho wilayani Ruangwa, Juni 2, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimina na Watawa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mnacho baada ya Waziri Mkuu, kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia wilayani Ruangwa, Juni 2, 2019. 


WAZIRI MKUU AUSHUKURU UONGOZI WA KANISA 
*Ni baada ya kutoa sehemu ya eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa shule 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameushukuru uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Lindi kwa kutoa sehemu ya eneo lake na baadhi ya majengo kwa ajili ya ujenzi wa shule. 

Jimbo Katoliki la Lindi limetoa eneo hilo lilipo katika Parokia ya Mnacho wilayani Ruangwa ambalo awali ilikuwa shule ya msingi ya Mnacho sasa imebadilishwa na kuwa sekondari. 

Waziri Mkuu ametoa shukurani hizo leo (Jumapili, Juni 2, 2019) alipokwenda kwenye kanisa Katoliki la Theresia wa Mtoto Yesu, Parokia ya Mnacho kuwasalimia waumini. 

Amesema lengo la kuibadilisha shule hiyo kuwa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia ni kuwawezesha watoto wa kike wa Wilaya hiyo kusoma katika mazingira mazuri. 

Waziri Mkuu ambaye ameambatana na Mkewe Mary amesema shule hiyo ya bweni itawapunguzia vishawishi watoto wa kike, hivyo kuwawezesha kutimiza malengo yao. 

Awali, uongozi wa Parokia hiyo uliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuboresha huduma za jamii zikiwemo za afya, elimu pamoja na miundombinu katika wilaya hiyo. 

Naye, Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa amewaomba viongozi wa dini washikamane na wahakikishe wanatatua changamoto ya mmomonyoko wa maadili. 

Amesema changamoto ya mmomonyoko wa maadiji katika jamii hususani kwa vijana ni kubwa, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha kwamba wanawarejesha kwenye maadili bora. 

Kadhalika, Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia na amesema kwamba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake. 

Shughuli zinazoendelea katika shule hiyo ni pamoja na ujenzi wa mabweni, vyumba vya madarasa, maabara na nyumba nne za walimu ambazo tayari ujenzi wake umekamilika.

DKT. MWANJELWA: WATUMISHI HOUSING JITANGAZENI, PUNGUZENI WAKANDARASI

0
0
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa ameitaka Taasisi ya Watumishi Housing Company (WHC) kujitangaza kwa Watumishi wa Umma, Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Wananchi ili kupata wateja kwenye Mradi wa Nyumba uliopo Gezaulole, Kigamboni na Bunju B jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada yakutembelea miradi ya ujenzi wa Nyumba hizo zinazosimamiwa na Watumishi Housing, Dkt. Mwanjelwa amesema WHC inapaswa kujitangaza kwa wateja ambao ni Watumishi wa Umma na Watanzania ili kujua kuhusu Nyumba hizo bei zake, pamoja na mandhari ya nyumba hizo. 

"Kila kizuri mnachokifanya Watanzania watajuaje?, Taasisi hii ipo Kisheria, Kikatiba, lazima mseme msikike kwa Watanzania, Watumishi wa Umma wajue mandhari,  waweza kujipanga kuweza kumudu gharama za Nyumba hizo," amesema Dkt. Mwanjelwa

"Sehemu kama Dodoma, Gezaulole Kigamboni kuna miradi mikubwa ya Nyumba, jitahidini kutangaza miradi hiyo", ameongeza Dkt. Mwanjelwa 

 Kuhusu suala la Wakandarasi, Dkt. Mwanjelwa amehoji uwepo wa Wakandarasi wanne katika mradi huo, ambapo amesema hakuna haja yakuwa na wingi huo ili kupunguza gharama, ameomba Kampuni ya Watumishi Housing kusimamia zaidi mradi huo. 

Pia Dkt. Mwanjelwa amewata WHC kufanya vizuri zaidi kuboresha mapungufu yote kwenye miradi hiyo, ili kupata matokeo mazuri kwa kutumia ubunifu waliokuwa nao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC) , Dkt. Fredy Msemwa ameahidi kuyafanyia kazi maagizo na maelekezo ya Naibu Waziri nakurejesha mrejesho uliokuwa wazi, amesema watakaa chini kurejea upya mkakati wa Elimu kwa Umma na Masoko katika kujitangaza ili kukidhi matarajio ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

"Sisi kama Taasisi tutakaa chini kurejea vizuri mkakati wetu mpya wa Elimu ya Umma na Masoko ili kukidhi matarajio yako wewe Naibu Waziri na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora tukiweza kufanya hivyo tutakuwa tumefikia matarajio ya Serikali, cha muhimu zaidi ni Watumishi wa Umma na Walengwa wengine kuweza kujua uwepo wa mradi wa Nyumba hizo, "amesema Dkt. Fredy

Amesema WHC tayari imefika kwenye Mikoa 16 hapa nchini sehemu ngumu kwenye ujenzi wa Shule za Kata zenye mazingira magumu, amesema wamewafikia Watumishi wa Umma kwa bei nafuu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa (kulia) akizungumza jambo na   Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa wakati wa ziara ya kutembelea mradi ya ujenzi wa nyumba wa Gezaulole, Kigamboni jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Emmanuel Mssaka wa Michuzi Tv)
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa  (katikati) akiwa ameambatana na watendani mbalimbali  wakitembelea Miradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea miradi ya nyumba zilizopo Gezaulole, Kigamboni na Bunju B jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya  kutembelea miradi ya nyumba zilizopo Gezaulole, Kigamboni na Bunju B jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa majengo ya Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa majengo ya Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. 


Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa barabra katika  Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Emmanuel Mssaka wa Michuzi Tv)

ACHENI WALIOTEULIWA WATEKELEZE ILANI

0
0
MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Thuwayba Edington Kisasi akifungua mafunzo ya kuhamasisha daftari la wapiga kura na suala la mikopo kwa wanawake viongozi wa UWT mkoa mkoa wa Kaskazini Unguja. Kulia ni Mbunge wa viti maalumu wa mkoa huo, Angelina Adam Malembeka kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Mkoani humo Maryam Muharami Shomari.
MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Kaskazini Unguja, Angelina Adam Malembeka (kulia) akihamasisha jambo kwenye mkutano mafunzo ya kuhamasisha daftari la wapiga kura na suala la mikopo kwa wanawake viongozi wa UWT mkoa mkoa wa Kaskazini Unguja.
MGENI rasmi katika mkutano huo, Thuwayba Edington Kisasi (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na viongozi wa UWT mkoa wa Kaskazini Unguja, watatu kushoto ni Mbunge wa viti maalun nkoani humo Angelina Adam Malembeka
MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Kaskazini Unguja, Angelina Adam Malembeka (kushoto) akihamasisha wanawake viongozi wa UWT wa mkoa wa Kaskazini Unguja juu ya daftari la wapiga kura na sala la mikopo kwa wanawake wa UWT kwenye kumbi wa mikutano wa CCM mkoa.
(PICHA NA MARTIN KABEMBA).
………………
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR
VIONGOZI na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kaskazini Unguja wametakiwa kuwasaidia viongozi waliochaguliwa kuteleleza ilani na ahadi walizozitoa wakati wa uchaguzi uliopita badala ya kukumbatia wagombea wa uchaguzi ujao.

Akifungua mafunzo ya siku moja yaliyoshirikisha viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa CCM mkoani humo, Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Thuwayba Eddington Kisasi alieleza kuwa kufanya hivyo kunapelekea viongozi waliopo madarakani kushindwa kusimamia ahadi zao.

Alisema wapo baadhi ya viongozi wa chama lkatika ngazi mbali mbali wameanza kuwakumbatia wanachama ‘wanaojipitishapitisha’ kwa lengo la kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao watambue kuwa kufanya hivyo wakati huu ni kukiuka kanuni za uchaguzi za chama hicho.

Mafunzo hayo yaliyolenga kuhamasisha ujasiriamali na mikopo kwa wanawake na uimarishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura yaliandaliwa kwa pamoja kati ya mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Angelina Adam Malembeka na UWT Mkoa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi iliyoagiza kuinuliwa kwa hali za kiuchumi za wanawake katika ngazi zote.

Alisema kanuni za uchaguzi za CCM zinakataza mtu kufanya kampeni kabla ya wakati hivyo viongozi wanaoandaa wagombea na kupanga nao mikakati wanapaswa kujua kuwa wanachochea vurugu ambazo zinakwaza kasi ya utekelezaji wa ilani na kuchelewesha upatikanaji wa maendeleo ya jamii.

“Chama kiliweka muongozo na ndio maana Mwenyekiti wetu (Dk. John Magufuli) alikataza Mambo ya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ili tupate kuteleleza ahadi tulizoweka kwa wananchi wetu na nyinyi no mashahidi kwamba kabla ya 2020 tumeshatekeleza ilani kwa zaidi ya asilimia 90 Tanzania bara na Zanzibar”, alieleza Kisasi.

Aidha aliwataka viongozi hao kuwa mabalozi wazuri na kuisambaza elimu waliyopatiwa kwa wanachama wenzao kwani yana umuhimu mkubwa katika maendeleo ya jamii na siasa za Tanzania.

“Tuliahidi kuinua uchumi wa wanawake katika ilani ya uchaguzi kupitia njia mbali mbali zikiwemo za ujasiriamali na uanzishwaji wa viwanda hivyo mafunzo haya yana mchango mkubwa katika kuendeleza vikundi vya kiuchumi tulivyonavyo katika shehia, wadi, wilaya na mikoa yetu”, alisema Makamu huyo wa Mwenyekiti.

Aidha aliwataka wajasiriamali nchini kutumia fursa ya marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki iliyoanza Juni mosi mwaka huu Tanzania bara, kutengeneza mifuko mbadala ya kubebea bidhaa na kuipeleka huko ili kujiendeleza kiuchumi.

Akizungumzia uimarishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, Kisasi aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuhamasisha jamii kwenda kuhakikisha taarifa zao na kuwasaidia vijana wenye sifa waweze kujiandikisha.

“Utekelezaji wa ibara ya 5 ya katiba ya chama chetu wa kushinda uchaguzi haupo wakati wa uchaguzi pekee bali huanza mapema na huu ndio wakati wake ili kuzichungachunga kura za ushindi wetu ifikapo 2020”, alieleza Makamu Mwenyekiti huyo.

Akiwasilisha mada juu ya ujasiriamali na mikopo Mkurugenzi wa taasisi inayojihusisha na elimu ya ujasiriamali na utoaji wa mikopo ya jijini Dar es salam Nickson Martin alisema ili kuwa na uzalishaji wenye tija ipo haja ya wajasiriamali kuzingatia elimu na uwekaji kumbukumbu za biashara zao kujua maendeleo ya shughuli zao.

“Ni lazima mkubali kubadilika na kuweka mikakati kuzifikisha ndoto zenu na za serikali yetu ya kuimarisha uchumi wa watu wake kupitia uchumi wa viwanda”, alisema Nickson.

Nae Katibu Msaidizi wa CCM mkoani humo Shafi Hamad Ali akiwasilisha mada ya umuhimu wa daftari la kudumu alisema viongozi wa ngazi zote za chama hicho wanapaswa kujidhatiti na kuhakikisha wanatekeleza maagizo na maelekezo ya chama kama inavyoelekezwa na katiba ya CCM na ya jumuiya zake.

“Msingi wa ushindi katika uchaguzi wa chama chetu ni umoja na mshikamano na ndio maana sote tunawajibika kuhakikisha chama kinashinda katika chaguzi za kutafuta dola na daftari ndio chanzo cha ushindi siku zote”, alisema Shafi.

Akitoa shukran za washiriki wa mafunzo hayo Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Angelina Adam Malembeka alieleza kuwa ataendelea kuwatafutia wanawake wa mkoa huo fursa za kujikomboa kiuchumi ili waweze kujitegemea na kusaidia maendeleo ya familia zao.

Alisema iwapo wanawake hao watatumia kikamilifu fursa za mikopo inayotolewa na taasisi za serikali na za binafsi wanaweza kupiga hatua kubwa za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda.

Alisema mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo aliyowahi kuwapatia wananchi wa mkoa huo kwsa kushirikiana na wadau mbali mbali ambapo hapo awali makundi mbali mbali ya wanawake yalipatiwa mafunzo ya utengenezaji chaki na mishumaa ili kujiongezea kipato.

“Baada ya kupata mafunzo yale nimeona nije na haya ya kuwaonesha fursa za kuendeleza miradi yetu ili siku moja tuwe na viwanda vidogo vidogo na vya Kati, hapo tutakuwa tumejikomboa kiuchumi kweli kweli”, alisema Malembeka.

Alizungumzia mafunzo hayo mmoja ya washiriki wa mafunzo hayo ambae ni Katibu wa UWT jimbo la Kijini Maryam Rashid Mussa alisema yamewasidia kuziona na kutambua fursa za misaada na kwamba watayatumia kuimarisha mitaji yao na chama kwa ujumla.

Mafunzo hayo yalishirikisha jumla ya viongozi wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa huo 120 yalifungwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa anaetokea jumuiya ya wazazi Tanzania Suleiman Juma Kimea ambae aliwasisitiza washiriki mafunzo hayo kusimamamia misingi na maadili ya chama hicho ili kuepuka mizozo isiyo ya lazima.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 3,2019

WATAALAM WA BIOTEKINOLOJIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA COSTECH,SERIKALI

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi (COSTECH) Dk.Amos Nungu akizungumza na wanasayansi pichani hawapo kuhusu wanasayansi hao kushirikiana na tume hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Maurilio Kipanyula.
Wanasayansi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi Teknolojia COSTECH Dk Amos Nungu,wa pili kushoto na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Teknolojia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Maurilio Kipanyula.
Mratibu wa Biotekinolojia na Usalama wa Chakula COSTECH, Dk.Beatrice Lyimo akielezea majukumu ya Idara yake kwa wanasayansi watafiti
……………………
NA SULEIMAN MSUYA
WANASAYANSI wa masuala ya Biotekinolojia nchini wametakiwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ili kuendelezea teknolojia hiyo ambayo ni mpya nchini.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk.Amos Nungu wakati mwandishi wa habari Mkoani Morogoro.Alisema COSTECH ipo tayari kushirikiana na wanasayansi hao wa masuala ya Biotekinolojia nchini kuhakikisha tafiti zao zinakuwa na matokeo chanya kwa jamii.

Dk.Nungu alisema pia COSTECH imekuwa ikiendeleza wabunifu mbalimbali ambao wanabuni vitu vyenye matokeo chanya kwa jamii.“Tumekuwa tukiwezesha taasisi, watafiti na wabunifu mbalimbali hivyo sisi tupo wazi kwa nyie wanasayansi kuja na maandiko yenu na tutayafanyia kazi kulingana na fedha zilizopo, msisubiri mpaka tutangaze,” alisema.

Mkurugenzi huyo wa COSTECH alisema iwapo kada hiyo ya wanasayansi hasa wa masuala ya Biotekinolojia watapata nafasi ya kuonesha tafiti zao ni wazi dhana ya nchi kufikia uchumi wa kati itafanikiwa.

Alisema tume itahakisha tafiti hizo zinafika Serikalini kirahisi na kufanyiwa kazi kwa maslahi ya nchi na wananchi.

Aidha, Dk.Nungu amewashauri wanasayansi kutumia lugha ambayo inaeleweka kwa waandishi wa habari ili kurahisisha kutoa taarifa sahihi kuhusu tafiti zao Biotekinolojia.Alisema wapo wanasayansi ambao wanatumia lugha za kisayansi hali ambayo inakwamisha mwandishi na jamii kushindwa kuelewana.

Dk.Nungu alisema pia wanasayansi wanapaswa kuandaa taarifa za tafiti zao kwa ufupi ili watoa maamuzi waweze kuelewa na kuchukua uamuzi.“Niwaomba ndugu zangu wanasayansi mnapoandaa taarifa za tafiti zenu zingatieni lugha ambayo ni rahisi kueleweka kwani itasaidia jamii kupata ujumbe sahihi,” alisema Dk.Nungu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (STI), Profesa Maurilio Kipanyala alisema Serikali kupitia idara hiyo imedhamiria kuendeleza teknolojia nchini ikiwemo Biotekinolojia.

Alisema serikali imekuwa ikishirikiana na taasisi kama COSTECH, Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikukuu cha Mbeya (MUST), Chuo Kikuu cha Nelson Mandeka na Tume ya Mionzi Tanzania.

“Sisi dhana hii tunaitekeleza katika dhana ya STI lakini pia Biotekinolojia ipo ndani kinachohitajika ni kuondoa wigo uliopo kati ya pande husika,” alisema.Alisema Serikali imekuwa ikitoa fedha za utafiti kwa COSTECH ambapo kwa mwaka wa fedha 2018/19 ilitengewa Sh.Bilioni 8.6 na mwaka unaokuja 2019/20 wametengewa Sh.Bilioni 6.7.

Alisisitiza uandaaji wa taarifa kwa ufupi ili kujenga hoja kwa watoa maauzi waeeze kuongeza bajeti ili tafiti zifanyike.Prof.Kipanyula alisema uwekezaji wa fedha katika tafiti unahitaji kupata matokeo ambayo yatamaliza changamoto za jamii.

Mkurugenzi huyo alisema idara itahitaji kupata taarifa kuhusu masuala ya Biotekinolojia ili kuangalia kuwa inaendana na sera ya serikali katika eneo hilo.“Ushirikiano ndio njia sahihi ya kufanya kazi hasa hizi za utafiti ni imani yangu nyie kama wanasayansi mtazingatia hilo na Biotekinolojia itasambaa kila mahali,” aliongeza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanasayansi watafiti kutoka vyuo mbalimbali nchini walisema iwapo tafiti zao zikitekelezwa ni dhahiri Tanzania ya uchumi wa kati itafikiwa.

Baadhi ya wanasayansi hao ni Dk.Miccah Seith wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dk.Charles Lyimo wa SUA, Dk.Siana Nkya wa Chuo Kikukuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) na Dk.Daniel Maeda wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Wanasayansi hao wamesema maendeleo amabayo yanaonekana duniani kwa sasa asilimia kubwa yamejikita kwenye Biotekinolojia hivyo Tanzania inapaswa kuwekeza eneo hilo.

EXTRA MUSICA ILIVYOTIKISA KONGO BRAZAVILLE.

0
0
Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.

Muziki wa dansi umeshika nafasi kubwa katika burudani katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Kongo Brazzaville.

Watu wa nchi hizo wanaongea lugha moja ya Lingala pia wamepakana, ambapo sehemu ya mipaka yao imetenganishwa na mto Kongo.

Makala hii inaizungumzia bendi ya Extra Musica, iliyoko Kongo Brazzaville. Ilianzishwa mwaka 1993 jijini Brazzaville ikiwa na waasisiwa wake akina Ibabi Okambi Rogatien ‘Roga Roga’, ambaye ni mahiri kwa kulicharaza gitaa la solo. Aidha Roga Roga ndiye kiongozi wa kundi hilo hadi sasa. 

Mwigine ni Espe Bass, ambaye ni muungurumishaji wa gitaa la besi.
Mwaka 1995, wanamuziki wa bendi hiyo waliachia albamu yao ya kwanza ya Nouveaux Missiles, iliyowatambulisha vyema kwenye ulimwengu wa muziki.

Albamu hiyo ilipambwa na nyimbo nyingi kali hususani ule Fred Nelson. Wanamuziki walioshiriki kwenye albamu hiyo mbali na Roga Roga na Espe Bass, ni pamoja na Guy Guy Fall, Quentin Moyascko, Oxygen Mbon Slyvain, Dou Dou Copa ‘Elenga Laka Bienvenu’, Dominique, Christian na Herman Nagasaki ambao wote ni waimbaji pamoja na kunengua.

Wanamuziki wengine walikuwa akina Killa Mbongo aliyekuwa ‘rapa’, Durell Loemba, ambaye ni mcharazaji wa gitaa la rhythm, kwa upande wa uchanganyaji drums, yupo Ngolali G’Ramatoulaye na Christian Kingstall alikuwa anabofya kinanda.

Wanamziki wa bendi hii ya Extra Musica walijizolea sifa lukuki, wakapendwa na wapenzi wengi kwa jinsi walivyo wajuzi katika kulishabulia jukwaa wakinengua katika maonesho yao yote.Bendi hiyo wanenguaji wake niyo hao wanamuziki wenyewe, tofauti na bendi nyingine ambazo hutumia kuchanganya wanenguaji wa kiume na wa kike.

Ndiyo sababu wao walipenda kujiita wao ni ‘La Difference’ (wa tofauti).
Kwenye albamu hiyo ya kwanza, kulikuwa na wanamuziki wengine ambao hawakupata nafasi ya kurekodi wakiwemo akina Pinochet Thierry, Regis Touba, Cyrille Molanga na Arnaud Luguna.

Albamu hiyo ya Nouvoeaux Missiles, ilisababisha wanamuziki wengine nje ya bendi yao kuvutiwa nayo mmojawapo alikuwa ni Samba Brice ‘Abillissi’, aliyeamua kujiunga nao.Albamu ya pili ya Confirmation ya mwaka 1996, ilipelekea kundi hilo kuzidi kutikisa vilizvyo hadi wakapata mialiko mingi barani Afrika na Ulaya.

Yaelezwa kuwa albamu hiyo ya Confirmation iliuza nakala nyingi mno kuzidi ile ya mwanzo.Lakini mafanikio hayo yalisababisha kuzuka kwa mgogoro mkubwa wa kimasilahi. Hali iliyofanya baadhi ya wanamuziki wake wakiwamo akina Christian na Guy Guy Fall, kujiondoa kundini japokuwa kuondoka kwa wanamuziki hao, Extra Musica iliendelea kuwa imara.

Ilipotoka albamu ya tatu ya Ouragan mwaka 1997, wanamuziki Herman Nagassaki na Samba Brice ‘Abilliss’, waliziba vilivyo mapengo ya Guy Guy Fall na Christian .Mgogoro wa chini kwa chini ulikuwa ukifukuta miongoni mwa wanamuziki wa bendi hiyo na uongozi.

Baadhi ya wanamuziki walishindwa kuvumilia wakaihama bendi hiyo.
Wanamziki hao walikuwa ni Arnaud Laguna, Quentin Mayascko, Durell Loemba, Cyrille Malonga, Regis Touba na Pinochet Thierry.Wakaenda kuunda kundi lao jingine walilolipa majina ya Z.I. International, chini ya uongozi wa Cyrille Malonga, Regis Touba, Pinochet Thierry na Durrell Loemba.

Baada ya bendi ya Extra Musica kukimbiwa na wanamuziki hao, walikaa chini na kuamua kuwatafuta wanamuziki wengine vijana wenye vipaji vikubwa.Walifanikiwa kuwapata vijana hao akina Gildas Pozzi, na Emery Mboma. Wakati huohuo Sonor alichukua nafasi ya ucharazaji wa gitaa la rhythm, lilokuwa likishikwa na Durell Loemba.

Mara baada ya kuwaingiza vijana hao kundini, mwaka 1998 waliachia albam yao ya nne ya Extra Major.

Albamu hiyo ilivunja rekodi ya mauzo ya albamu zote za awali na kuwaletea tuzo nyingi barani Afrika, ikiwemo ya Kora kwa kuteuliwa kuwa bendi bora ya muziki kwa bara la Afrika.Mwaka uliofuatia waliachia albamu nyingine tano zilizokuwa kali mno.

Kati ya albamu hizo ile ya Shalai ilisababisha kuwapata wanamuziki wengine wakali akina Papy Batin Maboulango na Boudouin Massipi.Rapa wao wa kutumainiwa Killa Mbango, alijitoa kundini akaachana na muziki. Lakini baadaye alirejea tena kundini.

Extra Musica ilichukuam kipindi kirefu kutoa albamu ya sita ya Trop C’Est Trop ya mwaka 2001.Rapa mwingine alijulikana kwa jina la Arafat, nae alijiunga na bendi hiyo, akichukua nafasi iliyoachwa wazi kwa mara nyingine tena na Killa Mbongo.

Baada ya kutoka na albamu hiyo, waliamua kubadilisha kidogo majina ya bendi yao ikaitwa Extra Misica Zagul.Mara baada ya kutoa albamu ya saba ya Obligatoire mwaka 2004, mwimbaji wao Dou Dou Copa naye akajiondoa kundini akafuatiwa na Oxygene mwaka 2005.

Kuodoka kwa wanamuziki hao hakukuithiri Extra Musica Zagul, kwani waliachia albamu ya nane ya La Main Noire mwaka 2006 na nyingine ya tisa ya Sorcellirie ‘Kindoki’ ya mwaka 2011.Pamoja na kukimbiwa na vijana wake wengi, kiongozi wao Roga Roga, bado anaendelea kuamsha muziki mkali akiwa na vijana wengine wenye vipaji vikali.

Hili ndilo kundi la Extra Muzica Zagul kutoka Kongo Brazzaville, japo sasa kuna makundi mengine kadhaa yameundwa yakitokea ndani ya bendi hiyo.
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba: 0713331200, 0784331200, 0736331200 na 0767331200.

MCHEZO WA PLAY OFF KAGERA SUGAR NA PAMBA WAAHIRISHWA.

0
0
Abdullatif. Yunus Michuzi Tv.

Mchezo wa Play off uliokuwa uchezwe dhidi ya Kagera Sugar na Pamba umeahirishwa mpaka kesho kwa kile kilichodaiwa kuwa Timu ya Pamba Fc ya Jijini Mwanza kugomea Mechi hiyo kurushwa hewani Mubashara na Azam TV ambao wamefika hapo uwanjani mapema kwa ajili ya kurusha mchezo huo.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi inasema imelazimika mchezo huo kuahirisha mpaka kesho ambapo sasa utarushwa, ingawa Mpaka sasa Timu ya Pamba haijatoa sababu za kugomea matangazo hayo, ilihali Azam wana lengo la kuweka mambo bayana.

SERIKALI KUBORESHA SERA YA MBEGU ILI KUWASAIDIA WAKULIMA NCHINI..

0
0
Hussein Stambuli, Morogoro

SERIKALI inampango wa kuboresha sera ya mbegu ili kuimarisha suala la upatikanaji wa mbegu zitakazowasadia wakulima na kuleta tija katika kilimo nchini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Profesa Raphael Chibunda kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mathew Mtigumwe wakati akifunga mdahalo wa mbegu wa siku mbili uliohusisha wataalamu wa mbegu, wazalishaji, wasimamizi, wauzaji na wakulima ulioandaliwa na Wizara ya Fedha Tanzania kupitia mradi wa mabadiliko ya tabia nchi uliofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya.

“kwa sasa Serikali inafanya mapitio ya sera za kilimo ambapo tumeibua mjadala wa masuala ya kuboresha sera ya mbegu na Wizara itayachukua na kuboresha sera ambazo zitatekelezwa ili kuimarisa upatikanaji wa mbegu bora ambazo wakulima watakuwa na uwezo wa kuzinunua ili kuboresha kilimo nchini” alisema Prof. Chibunda

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Udhibiti wa ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) Patrick Ngwediagi kwa niaba ya wataalamu wa mbegu walioshiriki mdahalo huo na kutoa mapendekezo yao, aliiomba Serikali na wadau wa mbalimbali kuchukua hatua stahiki zitakazowezesha kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi hasa kwenye upatikanaji wa mbegu zinazokabiliana na hali hiyo. 

Pia alisema, wameazimia kuwe na juhudi kubwa za kuboresha upatikanaji wa mbegu ikiwa bora kwa kupitia sheria zilizopo ambapo inapaswa udhibiti wa ubora wa mbegu uimarishwe ili wakulima wanufaike na wanachokipanda.
 wataalamu wa mbegu walioshiriki mdahalo wakifuatilia kinachoendelea katika mkutano huo mkoani morogoro
wataalamu wa mbegu walioshiriki mdahalo wakifuatilia kinachoendelea katika mkutano huo

Wageni ndani ya jiji la Dar wakikaribishana

Taarifa rasmi ya Tukio la Mama Mjamzito kujijeruhi Kirando - Rukwa

0
0

Mganga Mkuunwa Mkoawa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu akimjulia hali mama mjamzito anayesadikiwa kujijeruhi tumboni na kutoa mtoto Bi Joyce Mweupe akiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa mara baada ya kupokewa na kupatiwa matibabu. 
Bi Joyce Mweupe akisaidiwa kunyanyuka na Mganaga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface kasululu akisaidiana na muuguzi wa hospitali hiyo ya Rufaa Veronica Wambura. 
Bi Joyce Mweupe akiwa na Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Veronica Wambua pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. John Lawi (kushoto)
Mama mjamzito anayesadikiwa kujijeruhi tumboni na kutoa mtoto Bi Joyce Mweupe akiwa kitandani baada ya kupokewa na wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na kupatiwa matibabu
.…….. 
Kuanzia tarehe 30 Mei, 2019 kuna taarifa zilizosambaa na kutolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu mama mjamzito anayesemekana kujijeruhi maeneo ya tumboni na kupelekea kutoa mtoto tumboni,tukio lililotokea katika kata ya Kirando Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa. Baada ya kupokea taarifa hizo timu ya ufuatiliaji iliyoundwa na wataalam wanAfya kutoka ngazi ya Mkoa na Wilaya husika ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa ilifanya ufuatiliaji wa tukio hilo kwa lengo la kupata uhalisia wake na kubaini mambo yafuatayo: 

1. Mhusika katika tukio hili ni Bi Joyce Mweupe Kalinda mwenye umri 
wa miaka 32 anayeishi katika Kitongoji cha Kalya, Kijiji cha Kamwanda, Kata ya Kirando, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa, umbali wa takribani kilometa moja kutoka Kituo cha  Afya Kirando.

 2. Bi Joyce alipokelewa katika kituo cha Afya Kirando kilichopo katika 
kata ya kirando Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi majira ya saa 09:30 alfajiri ya tarehe 30 Mei 2019 akiwa amesindikizwa na ndugu zake wawili (Wifi na Shangazi yake) kwa lengo la kujifungua ambapo alipokelewa na kufanyiwa uchunguzi wa awali. 

Page 1 of 3 

Katika uchunguzi huo ilibainika kuwa mama huyo alikuwa na 
ujauzito unaokadiriwa kuwa na miezi tisa, akiwa na dalili za 
uchungu katika hali ya kawaida kiafya. 

4. Baada ya uchunguzi wa awali kukamilika alipelekwa katika wodi ya wazazi wanaosubiri kujifungua kwa ajili ya kupumzika huku watoa  huduma wakiendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wengine. 

5. Katika ujauzito huu alikuwa akihudhuria kliniki ya Afya ya Mama 
na Mtoto katika Kituo cha Afya Kirando ambapo alifanikiwa kufanya mahudhurio matatu na hudhurio la mwisho likiwa ni tarehe 08 Mei, 
2019 

6. Mnamo saa 10:30 alfajiri wakati watoa huduma wakifuatilia kujua 
maendeleo yake ndipo walipobaini kuwa Bi Joyce hakuwepo ndani ya wodi na hivyo kuanza kumtafuta katika maeneo mbalimbali ya kituo cha afya na kutoa taarifa kwa mlinzi na uongozi wa kituo cha 
afya. 

7. Wakati juhudi za kumtafuta zikiendelea, majira ya saa 12:30 asubuhi 
Bi Joyce aliletwa kituoni akiwa amebebwa kwenye godoro na watu watatu (Mojawapo akiwa ni mwenyekiti wa Kijiji cha Kamwanda) 
huku akivuja damu nyingi.

8. Watoa huduma walimpokea mgonjwa na kumuona akiwa 
ametapakaa damu, mtoto akiwa nje ya tumbo. Baada ya kumchunguza Bi Joyce alibainika kuwa na jeraha lilililosababishwa na kitu chenye ncha kali tumboni huku sehemu ya utumbo, mfuko wa uzazi, kondo la nyuma na mtoto vikiwa nje na yeye mwenyewe akiwa hajitambui. Baada ya hapo timu ya Kituo cha Afya ikongozwa na Mganga Mfawidhi Dkt. Gideon Msaki iliendelea na huduma za upasuaji wa dharura kwa ajili ya kuokoa Maisha ya Bi Joyce. 

Baada ya huduma za upasuaji wa dharura kufanyika timu ya ufuatiliaji iliendelea na ufuatiliaji zaidi wa tukio hili na kubaini ifuatavyo: 

1. Bi Joyce alipotoka kituo cha Afya alirudi nyumbani kwake 
anapoishi yeye,mtoto wake wa kiume aitwaye Linus Sindani 
Page 2 of 3 
anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 12 au 13 na mume 
wake ambaye siku ya tukio hakuwepo nyumbani. 2. Mara baada ya kurudi nyumbani Bi Joyce alimwagiza mwanaye 
(Linusi) kwenda kumuita shangazi yake ambaye anaishi maeneo ya jirani na nyumbani kwao. Waliporudi wakiwa na shangazi ndipo walipomkuta Bi Joyce akiwa ameloa damu na hivyo kutoa taarifa kwa majirani na mwenyekiti wa Kijiji kwa ajili ya msaada 
zaidi. Hitimisho 

1. Timu ya ufuatiliaji imejiridhisha kuwa huduma za dharura za 
upasuaji wa kuokoa Maisha ya Bi Joyce zimefanyika kwa mafanikio makubwa katika kituo cha Afya Kirando na kwamba mama na mtoto ambao kwa sasa wamehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa 
kwa uangalizi zaidi wanaendelea vizuri 2. Tunatoa pongezi kubwa kwa watumishi wa Kituo cha Afya Kirando 
kwa juhudi kubwa walizofanya kuokoa Maisha ya Bi Joyce Kalinda. 3. Tukio hili limeripotiwa katika jeshi la Polisi kwa ajili ya kuendelea na uchunguzi zaidi.

QNET YAFUTURISHA MKOANI DODOMA

0
0


Watoto wa vituo mbalimbali kumi vya kulelea watoto wenye uhitaji mkoani Dodoma, wakipata futari iliyoandaliwa na Kampuni ya QNET jana. Hafla hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya watoto 200 kutoka vituo hivyo na kuongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Mustapha Shaaban, Wawakilishi wa QNET na wawakilishi toka Bakwata.
…………………… 

QNET INASHEREHEKEA ARI YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KWA KULETA FARAJA KWA WENYE UHITAJI NA KUSAIDIA JAMII AFRIKA IKIWEMO TANZANIA

QNET YAUNGANA NA YATIMA JIJINI DODOMA KWA KUANDAA FUTARI KWA ZAIDI YA WATU 200
 
kampuni ya biashara ya mtandao duniani, sambamba na tamaduni zake na jitihada za kusaidia jamii, kusambaza upendo, huruma na ukaribu kwa kutoa msaada na kuleta faraja kwa jamii nyingi zisizo na uwezo barani Afrika. Katika zoezi ambalo lilifanyika katika nchi zote ambako kampuni hii inaendesha shughuli zake barani Afrika, QNET sambamba na wawakilishi wake wa kujitegemea (IRs), mawakala na wafanyakazi imeleta faraja, tumaini na tabasamu kwenye nyuso za wengi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Kampuni ya QNET inaendeshwa na falsafa ya RYTHM – Jiinue Kusaidia Wanadamu (‘Raise Yourself to Help Mankind’) imeandaa kampeni hii ya mwaka kusaidia kuboresha maisha ya familia na watoto wengi wasio na uwezo kwa kuwapatia mahitaji muhimu kama vile chakula, vinywaji na msaada wa kifedha kwa madhumuni ya elimu na kibinadamu. 

Hafla ya Futari Jijini Dodoma imewaleta pamoja zaidi ya watoto yatima 200 kutoka katika wilaya kumi za mkoa huo. Pamoja na hafla hiyo ya Iftar kampuni ya QNET imetoa zawadi za mbuzi, kilo 100 za mchele, kilo 50 za unga, kilo 25 za maharage, kilo 25 za sukari na lita 20 za mafuta ya kula kwa kila vituo kumi vya watoto yatima mkoani humo. 

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Shaaban alitoa wito wa amani na kuihamasisha jamii kuiga mfano uliofanywa na QNET katika kusherehekea mwezi mtukufu wa Ramadhani. Sheikh Shaaban ameipongeza kampuni ya QNET kwa kutayarisha Iftar kwa vituo vya watoto yatima Jijini Dodoma, chaguo ambayo inaunga mkono mkakati wa serikali ya kuhamisha makao yake Jijini humo. Pia alishukuru kampuni ya QNET kwa moyo wa msaada na ushirikiano hasa katika mwezi huu wa Ramadhan. 

Akiongea katika hafla hiyo, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi Mwanahamisi Mukunda alisema ‘Tendo hili la Iftar imesaidia serikali ya mkoa katika utekelezaji wa majukuku yake pamoja na kuwaangalia watoto yatima’.
Hafla ya Iftar Jijini Dodoma iliudhuriwa pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Dodoma, wawakilishi wa baraza la kislamu Tanzania-BAKWATA, viongozi wa dini la kislamu wa mkoa pamoja na wawakilishi wa kampuni ya QNET. 

Katika nchi za Senegali, Cameroon, Kenya, Niger, Mali, Burkina Faso, Togo, Guinea, Ivory Coast na Ghana, QNET imetoa magunia ya mchele, magaloni ya mafuta ya mboga, vinywaji baridi, vifaa vya usafi na fedha taslimu kwa yatima, jamii za waisiliamu, vituo vya kutoa msaada wa kielimu na ofisi ya misaada ya Imamu mkuu. 

Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET Kanda ya Afrika chini ya jangwa la Sahara, wakati akitoa maoni kuhusu CSR ya Ramadhani ya QNET kwa mwaka huu, alisema: 

“QNET imekuwa ikifanya hivi kwa miaka mingi. Kampeni ya kutoa msaada katika kipindi cha mwezi wa Ramadhan ni moja ya njia tunazotumia kuzifikia jamii kusaidia watu. Kadri tunavyoendelea katika biashara yetu, tunaamini katika kusambaza faraja na utoshelevu unaokuja pamoja nao. Kwa kweli ni muhimu sana, inatia moyo na inakamilisha jitihada za QNET. 
 
Inawezesha watu, 
inaonyesha upendo kwa jamii na pia inahamasisha wafanyakazi wetu na Wawakilishi wetu wa Kujitegemea (IRs), kadri wanavyoshiriki wao binafsi katika kuboresha maisha ya wengine. Malengo yetu ya kibiashara pia ni kuhusu kutengeneza fursa kwa watu, kufanya maisha ya watu kuwa bora na kuwawezesha watu kuwasaidia waweze kuishi maisha ya ukamilifu. Tunaita hiyo kuwa ni kuishi kikamilifu” 

Mwaka jana, Kituo cha Uwajibikaji wa Mashirika kwa jamii cha Afrika ya Kusini kiliitunukia QNET kuwa kampuni bora ya mwaka ya kimtandao ya uwajibikaji kwa jamii (E-Commerce CSR Company of the Year) kwa uwajibikaji wake katika kusaidia jamii na kuleta mabadiliko bora.

Tangazo la Utoaji wa Hati Fungani kutoka Benki ya NMB.

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA BARAZA LA TAIFA LA USHAURI KWA WATU WENYE ULEMAVU

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amezindua rasmi Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu huku akilitaka baraza hilo kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano ili kuleta tija na mafanikio makubwa kwa Watu wenye Ulemavu nchini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo alisema kuwa baraza linajukumu kubwa katika kuhakikisha usimamizi wa sekta ya watu wenye ulemavu pamoja na kuishauri Serikali juu ya masuala mbalimbali ya kundi hilo maalumu.

“Mtambue nafasi mliyopewa ni dhamana kubwa katika kuwahudumia watu wenye ulemavu ambao ni takribani asilimia 5 ya watanzania, hivyo ni vyema mkashirikiana na Serikali kubuni mikakati itakayosaidia kutatua changamoto zinazowakabili wenye ulemavu”, alisema Mhagama

Alifafanua kuwa Baraza hilo limeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya Mwaka 2010 na Sheria hiyo imeeleza majukumu ya Baraza ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri.

“Ni matumaini yangu mtakuwa washauri wazuri wa masuala ya watu wenye ulemavu kwa kuzingatia usawa kwa wote na si maslahi binafsi,” alisisitiza Mhagama.

Sambamba na hilo alimpongeza Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Dkt. Lukas Kija kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Wajumbe wengine kutokana na uaminifu na uwezo walionao katika kusimamia masuala ya Watu wenye Ulemavu.

Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha Watu wenye Ulemavu wanapata haki zao za msingi na kwa ajili ya ustawi wao katika Nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, afya, uchumi, kuwa na miundombinu rafiki pamoja na nyenzo za kujimudu.

Aidha Waziri Mhagama alitoa rai kwa watendaji wa Baraza hilo kuwa na miongozo yote inayohusu masuala ya Watu wenye Ulemavu itakayo wawezesha kufanikisha utendaji wao wa kazi.

Kwa Upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amesema kuwa Serikali katika mwaka 2019/2020 itaanza mapitio ya Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 ili kuwawezesha watu wenye ulemavu kwenda sambamba na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija alieleza kuwa wapo tayari kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayosimamia haki na ustawi wa Watu wenye Ulemavu.

Aliongeza kuwa Baraza hilo lipo tayari kutoa ushauri na hoja zenye tija kwa Serikali juu ya masuala mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu. 

Pia, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe alieleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa Baraza hilo na kufanya kazi pamoja katika kutatua changamoto zinazowakabili Watu wenye Ulemavu nchini ikiwemo migogoro na migongano kwa wadau.

Uzinduzi wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu umefanyika Juni 2, 2019 jijini Dodoma ambapo Baraza hilo litaongoza kwa kipindi cha miaka mitatu (2019 hadi 2021) likiongozwa na Mwenyekiti Dkt. Lukas Kija. Awali Baraza hilo lilikuwa likiongozwa na Dkt. Edward Bagandanshwa ambalo limemaliza muda wake mwaka 2017.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wajumbe wa Baraza jipya la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa baraza hilo kushirikiana na Serikali wakati akizindua Baraza hilo katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF, Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akielezea jambo kwa wajumbe wa Baraza wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo uliofanyika tarehe 2 Juni, 2019 Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti mpya wa Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wa pili kutoka kulia na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa wa pili kutoka kushoto mara baada ya kuzinduliwa kwa Baraza hilo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akifafanua jambo kwa wajumbe wa Baraza hilo (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF, Juni 2, 2019 Jijini Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
 Sehemu ya wajumbe wa Baraza hilo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akizindua Baraza hilo Jijini Dodoma.
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha huduma kwa Watu wenye Ulemavu Bi. Josephine Lyengi akielezea jinsi kitengo hicho kinavyohudumia Watu wenye Ulemavu.
 Mkalimani wa lugha za alama Bw. Baster Mlawa (kulia) akimfafanulia Mwenyekiti Chama cha Viziwi Tanzania Bw. Nedrosy Mlawa wa pili kutoka kulia (wenye uziwi) kuhusu maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa mkono wa pongezi kwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija wakati wa hafla ya kuzindua Baraza hilo, Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya wajumbe wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza jipya la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza jipya la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu mara baada ya kuzindua Baraza hilo Jijini Dodoma. Wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti mpya wa Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija, wa pili kutoka kushoto ni Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe na kulia ni Katibu Taifa wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bw. Jonas Lubayo.

Oparesheni sakakata la rambo mjini Singida yaenda vizuri

0
0

Mkazi wa mjini Singida akiwa amenunua mahitaji yake na kubeba katika
mfuko mbadala au halisi kama ambavyo inaitwa ikiwa ni katika utekelezaji
wa katazo la mifuko ya plastiki. 
Mwananchi wa mjini Singida akionesha mfuko mbadala ambao anautumia
kubebea bidhaa anazonunua dukani akitii sheria bila shuruti ambayo
imeanza kutekelezwa Juni mosi. 
Mifuko mbadala inayoagizwa kutumika badala ya ile ya plastiki kama
inavyoonekana wakati wa utoaji elimu kuhusu katazo la mifuko ya plastiki
sambamba na oparesheni ya kukagua kama bado ipo kwenye maeneo
mbalimbali mjini Singida. 
Mfanyabiashara wa nyama akionesha mifuko mbadala anayoitumia
kuwafungashia kitoweo hicho wateja kufuatia katazo la mifuko ya plastiki
ambayo ilizoeleka kutumika. 
Mifuko mbadala ikiwa imetundikwa kwa ajili ya kuhudumia wateja katika soko la mjini Singida ambapo kikosi kazi kilichoundwa na Serikali kikipita kukagua iwapo mifuko hiyo ikiendelea kutumika ama la. 

************************************** 

Oparesheni ya kukagua mifuko ya plastiki na utoaji elimu kuhusu katazo la mifuko ya plastiki linaloratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais limekwenda vizuri katika Mkoa wa Singida. 

Hayo yamebainishwa na Mkaguzi wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati, Mhandisi Boniphace Guni wakati wakati wa oparesheni hiyo maeneo mbalimbali ya mkoa huo. 

“Zoezi limekwenda vizuri na tunamshukuru Naibu Waziri (Mhe. Mussa Sima) kwa kuhamaisha na kutoa elimu na tumeona wananchi wamepata uelewa na adhabu yote hii ni kuwafanya waache kutumia mifuko hii iliyokatazwa kisheria”. alisema. 

Guni alisema tathmini inaonesha na kuwa NEMC ambayo ni mojawapo ya wajumbe wa kikosi kazi wameshirikiana na maafisa kutoka Manispaa ya Singida wameshuhudia mifuko hiyo ikisalimishwa baada ya agizo la Serikali. 

Aliongeza kuwa jamii kutokana na elimu iliyotolewa wananchi wameweza kupata uelewa wa madhara ya kutumia mifuko ya plastiki na kuwa ni hatari kwa afya na mazingira. 

Aidha, Mkaguzi huyo alisema wananchi wametambua fursa za kuzalisha mifuko mbadala ambayo imekuwa inahitaji kwa kiwango kikubwa baada ya kupigwa marufuko kwa mifuko ya plastiki. 

&qu t;Mhandisi Guni aliishukuru Serikali kwa kwa kutunga sheria ambazo zinasaidia kulinda afya za wananchi ingawa wapo wasiopendi kuifuata, jukumu letu ni kuendelea kutoa elimu na inapobidi kutoa adhabu inapoonekana kutoheshimiwa”alisisitiza. Kwa upande wake Afisa Mazingira kutoka Manispaa ya Singida, Arafa Halifa alisema wananchi wamekuwa na muitikio mzuri katika kutekeleza katazo hilo. 

Halifa alibainisha kuwa kuna wafanyabiashara wanane ambao
walisalimisha mifuko hiyo hivi karibuni huku mwingine akisalimisha shehena kubwa katika ofisi za manispaa hiyo. 

Alisema zoezi kubwa linaloendelea kwa sasa tangu sheria zianze kutumika Juni mosi ni kuzunguka kaika maduka , masoko na sehemu zingine za biashara na kuona kama katazo linatekelezwa. 

“Bado pia tunaendelea kutoa elimu na kusimamia sheria kama haifuatwi basi tunatekeleza adhabu na hapa kama unavyoona sisi manispaa tumeunda kikosi kazi kikiwa na maafisa mbalimbali wakiwemo wa biashara, mazingira, maendeleo ya jamii na mwanasheria”. alisema. 

Afisa mazingira huyo alisema pamoja na mambo mengine amekuwa akisikia kilio cha wananchi kuomba kasi ya uagizaji mifuko mbadala iwe kubwa kwani kuna mahitaji makubwa.

WAHITIMU MAFUNZO YA UHIFADHI WA MALIASILI KWA JAMII WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELEKULINDA MALIASILI ZA NCHI

0
0
MBUNGE wa Viti Maalum (CCM), Jacqueline Msongozi amewataka wahitimu wa mafunzo ya uhifadhi wa maliasili kwa jami kuwa mstari wa mbele katika kupambana na majangili pamoja na kulinda maliasili za Taifa licha ya changamoto wanazokutana nazo pindi wanapotekeleza majuku yao. Wito huo ameutoa wakati wa kufunga mafunzo ya VGS katika Chuo cha mafunzo ya uhifadhi wa maliasili kwa jamii Likuyusekamaganga kilichopo Wilaya ya NAMTUMBO mkoani RUVUMA .
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images