Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live

WAZIRI KALEMANI ABAINISHA MALENGO MRADI WA BOMBA LA MAFUTA .

$
0
0

Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV - Bukoba .

Mkutano wa Wadau wa Bomba la Mafuta litakaloanzia Nchini Uganda mpaka Jijini Tanga hapa Nchini Umefunguliwa rasmi na Waziri wa Nishati Medard Kalemani (MB) ambapo masuala mbalimbali yamejadiliwa, yakiwemo yale yanohusu Fursa katika maeneo ya mradi pamoja na namna ya kulinda mradi.

Kikao hicho kilichofanyika mapema June Mosi, 2019 katika Ukumbi wa E.L.C.T Mjini Bukoba kikihudhuriwa na Viongozi kutoka Wizarani, na Mkoani, lengo hasa likiwa ni kujadili namna ya Uharakishaji wa Ujenzi wa Bomba la mafuta litakalokuwa na urefu 

Likipitia Mikoa minane ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Singida, Dodoma Manyara, Arusha na Tanga huku mlango Mkuu ukiwa ni Mkoa wa Kagera.

Akizungumza kabla ya kufungua Mkutano huo, Waziri wa Nishati Mhe. Medard Kalemani amesema kupitia Bomba hili la Mafuta Wanakagera wana nafasi kubwa kuchangamkia fursa katika maeneo yao ambapo Bomba hilo litapitia zikiwemo fursa za kazi za Vibarua, kuuza Chakula, huduma ya Malazi n.k huku masuala mengine yakitaalamu yatachukuliwa na Watanzania wote kulingana na uhitaji, huku jumla ya Ajira zaidi ya Elfu kumi zikitarajiwa kutolewa.

Aidha wakati akijibu Hoja mbalimbali ikiwemo hoja ya Vijiji ambavyo bado havijafikiwa na Umeme Waziri Kalemani amesema Ni lazima Vijiji hivyo vifikiwe Umeme kwanza mapema na haraka iwezekanavyo kabla ya Ujenzi wa Bomba la Mafuta, na pale itakapobidi REA wasaidiwe na TANESCO ili mradi usikwame lengo likiwa ni kukamilisha Ujenzi wa Bomba kwa wakati na ikibidi kabla ya Wakati. 

Ujenzi wa Bomba hili la Mafuta utakaoanza Mwezi Septemba Mwaka huu Linaloanzia Nchini Uganda Urefu wa kilometa 298 na Urefu Kilometa 1147zitakuwa Nchini Tanzania, kwa Mkoa wa Kagera likipita Wilaya za Missenyi, Bukoba Vijijini na Muleba lenye Urefu wa Km. 1445 Kati ya Pumping Station moja itakuwa Kagera, Kati ya Kambi 12, mbili zitakuwa Kagera. Mkutano huo ni mwanzo wa Mkutano mingine mikubwa na midogo ambayo itajadili namna ya Utekelezaji wa Mradi huo.
Pichani ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akitoa salaam zake wakati wa ufunguzi wa Mkutano kujadili utekelezwaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta Mkoani katika Ukumbi wa E.L.C.T Kagera

 Pichani ni Mshiriki wa Mkutano Ndg. Runyogote M/kiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa akitoa ushauri wake juu ya ufanisi wa Mradi wa Bomba la Mafuta. 
 Pichani ni Viongozi pamoja na washiriki wa Mkutano wakiendelea kumsikiliza muwezeshaji (hayupo pichani) wakati akiendelea kuwasilisha mada yake juu ya mradi wa Bomba la Mafuta
 Pichani ni Profesa Anna Tibaijuka (MB) jimbo la Muleba Kusini ambapo pia Bomba litapitia akitoa mchango wake wakati wa mjadala wa Bomba la mafuta.
 Pichani ni Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu wakati akizungumza na wadau waliohudhuria Mkutano wa Kujadili Uharakishwaji wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Mjini Bukoba.

TBS WASHIRIKI MAONESHO WIKI YA MAZIWA,YATOA ELIMU KWA WAJASIRIAMALI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

SHIRIKA la Viwango Tanzania(TBS)limeshiriki katika Maonesho ya wiki ya maziwa yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Abeid Karume lengo ikiwa ni kuelimisha wajasiriamali na wadau katika sekta ya maziwa kuhusu namna ya kuthibitisha ubora wa bidhaa ya maziwa na bidhaa nyinginezo zinazotokana na maziwa.

Maofisa wa TBS wametumia nafasi hiyo kutoa mwito kea wajasiriamali kuthibitisha bidhaa hizo kwani ni bure na kutoa mwito pia kwa wananchi kununua bidhaa zilizothibitishwa na TBS.

"TBS)tumeshiriki katika Maonesho ya wiki ya maziwa ambayo yanayofanyika Viwanja vya Sheikh Abeid Karume,lengo letu kubwa hapa ni kuelimisha wajasiriamali na wadau katika sekta ya maziwa katika kuthibitisha ubora wa bidhaa ya maziwa na bidhaa nyinginezo zinazotokana na maziwa,'amesema mmoja wa maofisa wa TBS wakati wa maonesho hayo.
Ofisa Udhibiti Ubora kutoka TBS Stanford Matee akitoa elimu kwa baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Arusha juu ya masuala ya udhibiti ubora pindi walipotembelea banda letu katika maonesho ya wiki ya maziwa yanayofanyika jijini Arusha

Makamba aiagiza NEMC kufanya kazi bila mapumuziko

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba,amewataka watumishi wa Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira(NEMC) kuhakikisha wanafanya kazi ya msako ya mifuko ya plastiki mpaka siku za mapumziko ili kuondokana na mifuko hiyo.

Waziri Makamba ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati uzinduzi wa sheria ya katazo ya sheria ya mifuko ya plastiki iliyofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam amesema hakuna kulala kwani kazi ya utekelezaji wa sheria ya katazo ya mifuko ya plastiki ndio imeanza Juni Moja.

Katika utekelezaji wa sheria ya katazo ya mifuko ya plastiki Waziri Makamba alifanya ziara ya ukaguzi kwenye soko la kariakoo kuangalia utekelezaji wa agizo la kuanzia leo tarehe moja mwezi wa sita la kutotumia mifuko ya plasticki kwa lengo la kulinda mazingira na afya za wananchi kutokana na kuwepo kwa mahitaji ya makubwa mifuko ya plastiki.

Amesema katika utekelezaji wa agizo hilo ni wakati wa bodi ya NEMC kuhakikisha wafanya kazi ambao wapo kwenye kikosi kazi cha kukagua watumiaji wa mifuko hiyo iliyokatazwa kufanya kazi kwa kasi zaidi ikiwemo kufanya kazi mpaka siku za mapumziko.

"Katika kipindi hiki cha utekelezaji wa sheria hii mpya ni wakati wa bodi ya Nemc kuwataka wafanya kazi waliopewa kufanya kazi ya ukaguzi wa mifuko kufanya kazi mpaka siku ya mapumziko kuhakikisha mifuko hii inapotea."amesema Makamba.

Makamba amesema nchi haijakurupuka Kaukataza matumizi ya mifuko ya plastiki baada ya kubaini mifuko hiyo ibaharibu mazingira ambapo akitoa mfano endapo Tanzania ikiendelea na matumizi ya mifuko hiyo katika kipindi cha miaka 20 ijayo Baharini kutakuwa na mifuko mingi kuzidi samaki jambo analodai ni hatari kwa mazingira.

Hata hivyo, Waziri Makamba amesema shehena ya mifuko ya plastiki iliyopatikana kutoka kwa watumiaji itapelekwa kutengenezea Bomba na madawati hivyo akiwasihi wananchi kusalimisha ya plastiski kwenye mamlaka husika .

Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya ya NEMC,Profesa Esnati Osinde amesema watataendelea kutoa elimu hadi kwa viongozi wa dini kuhakikisha wananchi wanapata elimu juu ya madhara ya matumizi ya mifuko ya plastiki.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  January Makamba akizungumza na watendaji  wa  Baraza la Taifa la Uhifadhi wa  Mazingira (NEMC) katika utekelezaji wa Sheria ya uzuiaji wa mifuko ya plastiki katika soko la Kariakoo
 Mifuko mbadala ambayo wanatakiwa kutumia wananchi katika Kubebea bidhaa mbalimbali.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira Dkt. Samwel Gwamaka akitoa mikakati ya Baraza katika utekelezaji wa sheria ya katazo ya mifuko ya plastiki.
 Wajasiriamali wakionesha vibebesheo mbalimbali katika uzinduzi wa sheria ya katazo ya mifuko ya plastiki  iliyofanyika mbagala jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  January Makamba akizungumza wakati uzinduzi wa sheria katazo ya mifuko ya plastiki iliyofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.
 Vibebesheo mbalimbali ambavyo vinatakiwa kutumika ubebaji wa bidhaa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na January Makamba akiangalia mfuko mbadala baada  ya kuanza sheria ya katazo la mifuko  plastiki  katika operesheni iliyofanyika Kariakoo jijini Dar es Salaam.

MBUNGE MAVUNDE ATATUA CHANGAMOTO YA KIVUKO KATA YA MIYUJI JIJINI DODOMA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo ametembelea eneo la Mathias Kata ya Miyuji Jijini Dodoma kujionea adha na changamoto ya kivuko wanayopata wananchi wa eneo hilo kutokana na uwepo wa korongo kubwa ambalo hupitisha maji mengi kipindi cha mvua na hivyo kukatisha mawasiliano kati ya eneo hilo na maeneo mengine.

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa eneo hilo,Diwani wa Kata ya Miyuji Mh David Mgongo ameeleza changamoto hiyo kubwa kiasi cha kupelekea wanafunzi kushindwa kwenda Shule kipindi cha Mvua na wananchi kukosa huduma muhimu kutokana na adha hiyo.

Mbunge Mavunde amewahakikishia wananchi hao kujengwa kwa kivuko hicho ndani ya muda mfupi kama ambavyo aliahidi wakati wa Kampeni na kwamba mkandarasi amepatikana na fedha kiasi cha Tsh 199,000,000 zitatumika kwa ajili ya ujenzi huo chini ya TARURA na shughuli rasmi za Ujenzi zitaanza wiki ya Tarehe 3.06.2019 ,pia Mbunge Mavunde ameahidi kujenga kivuko kidogo cha watembea kwa miguu ambacho kitajegwa mita 70 kutoka kivuko kikubwa kinapojengwa.

Wananchi wa eneo hilo wamemshukuru sana Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele kushughulikia matatizo yao na kuahidi kujitolea nguvukazi wakati wa zoezi lote la ujenzi ili na wao kuunga mkono juhudi za Mbunge huyo.
 Sehemu ya kivuko chenye changamoto kwa wakazi wa kijiji cha Mathias.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu wa Bunge,Kazi,Ajira na Watu wenye Ulamavu Anthony Mavunde akitoa maelekezo kuhisiana na suluhisho ya kivuko katika eneo la Mathias wakati alipofanya ziara hapo.
 Naibu Waziri Anthony Mavunde akipita katika kivuko hicho
 Naibu Waziri nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu wa Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Anthony Mavunde akiangalia Kivuko katika eneo la Mathias Kata ya Miyuji kilicho haribika kutokana na mvua za hivi karibuni.
Naibu Waziri Anthony Mavunde akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mathias kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili Wananchi wa kijiji hicho.

WANAFUNZI 100 SHULE ZA SEKONDARI DAR WACHAGULIWA KUUWAKILISHA MKOA MASHINDANO YA UMISETA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WANAFUNZI 100 kutoka Shule za Serikali na binafsi wamechaguliwa kujiunga kwenye timu ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano ya UMISETA ambayo yanatarajiwa kufanyika mkoani Mtwara.

Waliochaguliwa kujiunga na timu ya Mkoa wa Dar es Salaam ni baada ya kufanyika kwa mashindano ya UMISETA kwa ngazi ya Wilaya ambapo zote zilishiriki na kupitia mashindano wamepatikana wanafunzi hao ambao wapo wa michezo mbalimbali.

Akizungumza baada ya kutajwa majina ya wanafunzi hao kati ya wanafunzi 500 walioshiriki ngazi ya Wilaya ,Katibu Tawala Msaidizi(Utawala na Utumishi)Mkoa wa Dar es Salaam Lawrence Malangwa

amewataka wanafunzi wote kuwa na nidhamu kwa kipindi chote watakachokuwa kwenye mashindano hayo huku akionya ni marufuku kutumia mamluki kwani vijana hao wanasifa zote zinazostahili.

Amesema anaamini walimu waliochaguliwa kwenda na wanafunzi hao watakuwa makini kuhakikisha wenye sifa wanapata nafasi ya kushiriki mashindano hayo na wanauhakika Mkoa wa Dar es Salaam wataibuka washindi wa jumla

Pia ameagiza wanafunzi waliochaguliwa kwa ngazi ya Mkoa kwenda kwenye mashindano hayo kabla ya kuondoka wapimwe afya zao ili kuwa na uhakika wa uimara wa afya kabla hawajaondoka.

Malamgwa ameongeza wanafunzi hao wanatakiwa kutambua wakati wanajiandaa kwenda Mtwara watambue wamepewa dhamana ya kuwawakilisha wanafunzi wote wa sekondari kwa Mkoa wa Dar es Salaam na hivyo wanapaswa kujituma na kuonesha bidii wakiwa mchezoni

Kwa upande wake Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Hamis Lissu amesema kuwa wamejiandaa vizuri na watarudi na ushindi mnono wa kitaifa na kwamba wao wanakwenda kutetea ubingwa wao kwani miaka yote wamekuwa wataibuka washindi katika mashindano hayo.

Lissu amefafanua wanafunzi hao wanatoka katika shule za serikali na binafsi na waliochaguliwa wamepatikana baada ya kufanyika kwa mashindano kwa wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam.

Amefafanua wakati wa wote wa mashindano kwa ngazi ya Wilaya hakuna mwanafunzi yoyote ambaye ameumia na hilo ni jambo la kujipongeza.
Walimu na mwanafunzi kutoka Wilaya ya Ilala wakikabidhiwa Kombe baada ya kuibuka washindi wa jumla katika mashindano ya UMISETA ngazi ya Wilaya

Mmoja wa wanafunzi wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam akipokea kikombe kutoka kwa mgeni rasmi kabla ya kutangazwa kwa.majina ya wanafunzi waliochaguliwa kwa ngazi ya Mkoa kwa ajili ya mashindano hayo
 Wanafunzi wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakishangilia baada ya kuibuka washindi wa jumla  kwenye mashindano ya UMISETA kwa ngazi ya Wilaya
 Baadhi ya wanafunzi ambao wamechaguliwa kuuwakilisha Mkoa wa Dar es Salaam kwenye mashindano ya UMISETA wakipatiwa utararibu na maelezo kuhusu mashindano hayo
Walimu kutoka shule za sekondari Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kichaguliwa kuungana na  wanafunzi 100 kutoka Mkoa huo wanaokwenda kushiriki mashindano ya UMISETA yanayotarajia kufanyika mkoani Mtwara 
Wanafunzi  wa shule za sekondari Wilaya ya Ilala Dar es Salaam wameibuka washindi wa pili kwa ngazi ya Wilaya katika mashindano ya UMISETA

BENKI YA EXIM YAFUTURISHA WATEJA WAKE WA TANGA NA MTWARA

$
0
0
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Andrew Lyimo akizungumza na wageni waalikwa pamoja na wateja wa benki hiyo jijini Tanga wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evodi Mmanda akizungumza na wageni walikwa pamoja na wateja wa benki y Exim Mkoani Mtwara waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mwishoni mwa wiki.

Sheikh mkuu wa Mkoa wa Tanga, Sheikh Ally Luwuchu akizungumza na wageni walikwa pamoja na wateja wa benki ya Exim jijini Tanga waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wateja wa benki ya Exim wakipata chakula walipohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo jijini Tanga mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim wakifuturu pamoja na wageni waalikwa pamoja na wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo jijini Tanga mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Benki ya Exim tawi la Mtwara Bw Ramadhani Magera (katikati) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki
Meneja wa Benki ya Exim tawi la Mtwara Bw Ramadhani Magera (kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Sheikh Nurdin Mwangochi akizungumza na wageni walikwa pamoja na wateja wa benki ya Exim Mkoani Mtwara waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mwishoni mwa wiki

SERIKALI INAJENGA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU ILI KUWAWEZESHA WATUMISHI WA UMMA KUPATA MAKAZI BORA

$
0
0

Mwonekano wa baadhi ya majengo ambayo ni nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Company kwa ajili ya makazi kwa Watumishi wa Umma na Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii kwa lengo la kuwauzia na kupangisha. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikagua baadhi ya nyumba za makazi zilizojengwa Bunju B mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya kuuza na kuwapangisha Watumishi wa Umma na Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akihimiza uwajibikaji kwa watendaji wa Watumishi Housing Company (hawapo pichani) kabla ya kutembelea miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Watumishi wa Umma zilizopo Gezaulole Kigamboni na Bunju B mkoani Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa akiwasilisha kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) taarifa ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Watumishi wa Umma zilizopo Gezaulole Kigamboni.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa mara baada ya kutembelea miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Watumishi wa Umma na Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii zilizopo Gezaulole Kigamboni na Bunju B mkoani Dar es Salaam. 

………………… 

Serikali imeendelea kuwajali Watumishi wa Umma nchini kwa kuwajengea nyumba bora za gharama nafuu kupitia miradi ya ujenzi wa nyumba inayotekelezwa na Watumishi Housing Company katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwawezesha watumishi kumiliki nyumba bora za kuishi. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipotembelea miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi Gezaulole Kigamboni na Bunju B mkoani Dar es Salaam. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, amejionea nyumba zilizojengwa kisasa, gharama nafuu na zenye viwango vinavyostahili kwa makazi ya watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii ambao ndio walengwa wakuu wa miradi hiyo. 

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewaagiza watendaji wa Watumishi Housing Company kuhakikisha wanakuwa na mkakati madhubuti wa kutoa taarifa kwa watumishi wa umma juu ya uwepo wa nyumba zilizojengwa na kampuni hiyo, sehemu zilipo na bei elekezi kwa wanaohitaji kununua, ikiwa ni pamoja na bei ya kupangisha. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amekamilisha ziara yake ya kikazi mkoani Dar es Salaam ya kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Watumishi wa Umma na wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji wa Watumishi Housing Company.

WAOGELEAJI TANZANIA HATI HATI KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA

$
0
0

Dar es Salaam. Waogeleaji wa timu ya Taifa ya Tanzania waliochaguliwa kuunda timu ya Taifa kwa ajili ya mashindano ya dunia wapo katika hatihati ya kushiriki kutokana na ukata wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA). 

Tanzania imepata nafasi ya kushiriki katika mashindano mawili, mashindano ya dunia ya waogeleaji wakubwa yaliyopangwa kufanyika Gwangju, Korea Kusini kuanzia Julai 12 mpaka 28 na mashindano ya vijana yaliyopangwa kufanyika Budapest, Hungary kuanzia Agosti 20 mpaka 25. 
TSA imewachaguwa waogeleaji wanne, Hilal Hilal, Collins Saliboko (wanaume) na wanawake ni Sylvia Caloiaro na Shivani Bhatt. 

Waogeleaji hao wataambatana na kocha wao, Alexander Mwaipasi na viongozi wawili, Mwenyekiti, Imani Alimanya na makamu wake, Asmah Hilal. 

Chama hicho kinahitaji Sh38,772,000 kwa ajili ya mashindano hayo huku shirikisho la dunia la mchezo huo, Fina litagharimia ticketi za safari tu kwa waogeleaji watatu na viongozi wawili kwa masharti ambayo yanaitaka TSA kutumia gharama zake na baadaye kurudishiwa mara baada ya mashindano. 

Fina pia imeitaka TSA kutafuta Sh80,760,000 kwa ajili ya kuwasafirisha waogeleaji saba kwa ajili ya mashindano ya dunia ya vijana. Waogeleaji hao ni Dennis Mhini, Delvin Barick, Christopher Fitzpatrick, Christian Shirima na Isam Sepetuambao watashindana kwa upande wa wavulaa na wasichana, Kayla Temba na Laila Rashid. 

Kama ilivyo kwa waogeleaji wakubwa, Fina italipia waogeleaji watatu na kiongozi mmoja tu kwa masharti kuwa shirikisho la dunia litarejesha fedha hizo mara baada ta TSA kuwasilisha madai mara baada ya mashindano. 
Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro alisema kuwa masharti hayo yanawafanya wao (TSA) kutafuta Sh milioni 120, jambo ambalo linawaweka katika wakati mgumu. 

“Tunawaomba wadau watusaidie kupata fedha hizo. Shirikisho letu halina fedha na kwa sasa tupo katika hatihati ya kushiriki kutokana na hali hiyo,” alisema Inviolata. Alisema kuwa hata waogeleaji ambao wapo chini ya Fina, hawataweza kwenda kushindana kama hatutaweza kutafuta fedha ambazo baadaye Fina watarejesha. 

“Tupo katika wakati mgumu sana, tunaomba wadau na serikali itusaidie, waogeleaji wetu wapo katika mazoezi makali na wana nia ya kufanya vizuri katika mashindano hayo,” alisema.

OHOOOOO

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 2,2019

Mwili wa Etienne Tshisekedi wapata maziko ya kitaifa DR Congo

$
0
0
 Kwa wafuasi wake sherehe hiyo ya misa ya wafu ni ushindi dhidi ya serikali iliokuwepo
 
Jeneza la marehemu Etienne Tshisekedi likibebwa

 Rais wa Rwanda Paul kagame akitoa heshima zake za mwisho

 Wale waliopata wito rasmi waliruhusiwa kuingia

 Kulikuwa na biashara ya mau nje ya uwanja huo
Wafuasi wa mkongwe huyo wa upinzani walihudhuria mazishi yake


Miaka miwili baada ya kifo chake nchini Ubelgiji, mazishi ya kitaifa yamefanyika kwa kiongozi wa zamani wa upinzani nchini DR Congo Etienne Tshisekedi.

Mwili wake ulisafirishwa nyumbani siku ya Alhamisi kufuatia mgogoro kati ya familia yake na serikali ya iliopita .

Mgogoro huo ulikwisha baada ya mwanawe kuwa rais mwaka uliopita.

Makumi ya maelfu ya watu walihudhuria Ibada ya wafu katika uwanja wa mashahidi mjini Kinshasa wakiongozwa na Askofu Fridolin Ambongo.

Kanisa katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini humo liliwataka wafuasi wake kuhudhuri kwa wingi katika mazishi hayo.

Siku ya Ijumaa , rais wa Rwanda na Angola walikua miongoni mwa idadi kubwa ya watu waliojitokeza ili kutoa heshima yao ya mwisho kwa marehemu kufuatia miaka kadhaa ya uhasama kati ya taifa lake na DR Congo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA BBC Swahili.

Wanaotuma maombi ya kutaka Visa ya kwenda Marekani sasa kutoa majina yao ya mitandaoni

$
0
0
Wote wanaotuma maombi ya kupata Visa kueleka nchini Marekani sasa watahitajika kutoa majina yao ya mitandao ya kijamii, anwani zao na nambari za simu katika sheria mpya zilizowekwa.

Kulingana na sheria mpya za idara ya maswala ya kigeni, wanaotuma maombi ya Visa watahitajika kutoa majina yao ya mitandaoni mbali na anwani za miaka mitano pamoja na nambari za simu.

Wakati sheria hiyo ilipopendekezwa mwaka jana, mamlaka ilikadiria kwamba itaathiri takriban watu milioni 14.7 kila mwaka.Hatahivyo baadhi ya wanadiplomasia na maafisa wanaotuma maombi ya kibali hicho huenda wakasamehewa.

Hatahivyo watu wanaoelekea Marekani kufanya kazi ama kusoma watalazimika kutoa habari zao .

''Tunajaribu kutafuta mikakati ya kuimarisha ukaguzi wetu ili kuwalinda raia wa Marekani , huku tukiunga mkono wale wanaosafiri kihalali'' , ilisema Idara hiyo.

Awali , ni watumaji maombi waliohitaji ukaguzi wa zaidi -kama vile watu waliosafiri katika maeneo yanayodhibitiwa na magaidi -ambao wangelzimika kutoa data hiyo.

Lakini asasa wanaotuma maombi watalazimika kutoa majina ya akaunti zao katika mitandao ya kijamii, mbali na kutoa maelezo ya akaunti zao katika mtandao yoyote.

''Mtu yeyote atakayedanganya kuhusu matumizi yao ya mitandao ya kijamii huenda akakabiliwa na adhabu kali ya uhamiaji'', kulingana na afisa aliyezungumza na The Hill.

Utawala wa rais Donbald Trump ulipendekeza sheria hizo mnamo mwezi Machi 2018.

Wakati huo, Muungano wa wanaraharakati nchini Marekani American Civil Liberty ulisema kuwa hakuna ushahidi kwamba ukaguzi huo wa mitandao ya kijamii unafanyika kwa njia ya haki na kusema kuwa hatua hiyo itawafanya watu kujizuia mitandaoni.

Trump aliahidi kuweka sheria kali za uhamiaji wakati wa kampeni ya uchaguzi wa 2016. Alitaka wahamiaji kufanyiwa ukaguzi wa kiwango cha juu wakati wa utawala wake.

KUSOMA ZAIDI BOFYA BBCSwahiili.com

TAARIFA YA KUPOTEA KWA KIJANA SALUM RAMADHAN SALUM ABICHI (18)

$
0
0
Habari za Leo,

Pole na majukumu ya siku nzima. 

Napenda kukujulisha kuwa ndugu Salum Ramadhan Salumu (18) ,BADO hajapatikana wala hatujapata taarifa zake.

Tafadhali naomba msaada wako wa kila njia (Instagram,Facebook,Twitter,Radio,TV,Blog,Makundi ya WhatsApp,Website Nakadhalika) kusambaza taarifa ya Kupotea kwa kijana Salum Ramadhan Salum (18) ambaye hakurejea nyumbani tangu tarehe 12th May 2019. Mara ya mwisho ameonekana stendi ya Ukonga madafu akipanda gari ya kutoka Gongo la Mboto likielekea buguruni ikiwa ni safari yake ya kurejea nyumbani majira ya saa 2 usiku. 

Alikuwa amevaa shati jeupe na Suruali ya kijivu na saa rangi ya dhahabu na sendoz za wazi. Tafadhali toa taarifa kituo cha polisi kilicho karibu na wewe au naomba unijulishe kwa kupiga ama kuandika sms kwenda nda namba 0713/0766-202748. 

 Ni kijana mpole na mwenyeji wa Kiwalani BomBom kwa DSM na Mwanza ndio alipozaliwa. 

Naaomba Ushirikiano wenu kwenye changamoto hii.

Asante

JESHI LA POLISI PWANI LATOA VYAKULA KUELEKEA IDD EL FITRI KWA WATOTO YATIMA SANZE,KISARAWE-WANKYO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KISARAWE

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Pwani Kamishina Msaidizi (ACP) ,Wankyo Nyigesa, ametoa vyakula mbalimbali ikiwemo mchele kilo 100,sukari kilo 50 ,juice,mafuta ya kula na fedha katika kituo cha kulelea watoto yatima huko Sanze ,kata ya Kazimzumbwi,Kisarawe ikiwa ni kuelekea sikukuu ya Eid el fitri. 

Akiwa kituoni hapo pia aliungana na watoto wenye mahitaji maalum katika kwenye iftari ya pamoja na jeshi hilo .

Akizungumza na waandishi wa habari,Wankyo aliwaambia kwamba ,ni utamaduni wa kawaida kwa jeshi la polisi mkoa kujumuika na watoto yatima,wadau na makundi maalum katika jamii kwenye kipindi hiki cha mfungo.

Alieleza, tayari Jeshi la Polisi mkoani hapo limeftarisha katika wilaya ya Kibaha ,wadau mbalimbali na katika kuendeleza utamaduni waliojiwekea likaona ipo haja ya kuftari na watoto wenye uhitaji.

"Katika kuhakikisha watoto hao wanasherekea sikukuu ya Eid el fitri kwa furaha, Jeshi hili Mkoa wa Pwani limetoa vitu mbalimbali kama mchele, mbuzi, mafuta ya kula, sabuni, sukari, chumvi, juice na fedha"alifafanua Wankyo.

Nae msimamizi wa kituo hicho, Florida Frank, alielezea,Jeshi hilo limeonyesha mfano kwa taasisi zingine ndani ya serikali kwa kitendo cha kuwakimbilia na kuftari pamoja na kutoa mkono wa Eid kwa watoto hao jambo ambalo litawafanya kusherekea Eid kwa furaha.

"Kituo hiki ,kina watoto 26 kati yao wa kiume ni 15 na wa kike 11 wakiwa na walezi sita , na kilianzishwa toka mwaka 2007"alieleza Florida.

Alisema wapo watoto wenye umri kati ya miak 04 hadi 22 wanaosoma shule za chekechea 04, msingi 10, sekondari 08, cheti 01, na wasiosoma 03 bado wanaandaliwa utaratibu wa elimu na kituo kinajiendesha kwa kufanya ujasiliamali wa kutengeneza batiki na taulo za wanawake.


POLISI PWANI YAKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 89.3 KUTOKANA NA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI

$
0
0


NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

JESHI la polisi mkoani Pwani ,kupitia kikosi cha usalama barabarani limefanikiwa kukusanya zaidi ya sh.milioni 89.3 kutokana na makosa ya usalama barabarani na madai ya serikali yapatayo 2,266 .

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,alisema jeshi hilo kupitia kikosi hicho lilifanya operesheni maalum yenye lengo la kudhibiti matumizi mabaya ya barabara.

Wankyo alieleza, katika operesheni hiyo walikamata makosa ya mwendokasi,kupita magari mengine sehemu isiyoruhusiwa na kupakia mizigo kupita kiasi.

Makosa mengine ni pamoja na madereva walevi na ukaguzi wa magari yanayobeba wanafunzi na pikipiki ambapo jumla ya makosa 1,680 yaliandikiwa faini na kukusanywa milioni 50.4.

"Madai ya serikali ni 586 ambapo makusanyo ni sh.milioni 38.938.5 jumla makosa na madai 2,266 na makusanyo milioni 89.338.5"alifafanua Wankyo.

Hata hivyo ,Kamanda huyo alisema ,katika operesheni hiyo makosa ya magari na pikipiki yalikamatwa na watuhumiwa walionywa na wengine kutozwa faini ya papo kwa papo na magari yaliyokuwa na madai ya serikali kulipia madai.

Wankyo alichukua fursa hiyo, kutoa rai kwamba,askari wa usalama barabarani wataendelea kutandazwa na wapo kazini muda wote ili kuhakikisha hakuna chombo cha moto kitakachofanikiwa kupita ndani ya mkoa huo bila kukaguliwa.

Alibainisha kuwa,watumiaji wa barabara za mkoa huo wasichukulie kigezo cha kumalizika kwa operesheni hiyo kukiuka sheria za usalama barabarani kwani atakaefanya uzembe wa makusudi atachukuliwa hatua za kisheria na kupigwa faini lengo likiwa kupunguza ajali mkoani humo.

SERIKALI YAJIPANGA KUONDOKANA NA CHANGAMOTO YA MALISHO YA MIFUGO NCHINI

$
0
0

Na. Edward Kondela

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema wizara hiyo ina mpango wa kuondokana na changamoto ya malisho ya mifugo ambayo imekuwa ikisababisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Prof. Gabriel amesema hayo katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, kwenye hafla fupi ya kupokea matrekta saba kwa ajili ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) pamoja na Shamba la Malisho Vikuge kupitia mradi wa kuunganisha matrekta wa URSUS-TAMCO unaofadhiliwa na Serikali ya Poland.

Akizungumza katika hafla hiyo katibu mkuu huyo amesema matrekta manne ambayo yamenunuliwa na TALIRI kwa njia ya mkopo wa miaka miwili wenye thamani ya takriban Tshs. Mil 220 na matrekta matatu ambayo yamenunuliwa kwa fedha taslimu Tshs. Mil 192.1 na Ofisi ya Msajili Hazina kwa ajili ya Shamba la Malisho Vikuge, yatatumika kwa ajili ya kilimo kwenye mashamba ya malisho ya mifugo na kuongeza wingi wa upatikanaji wa malisho na yenye ubora kwa mifugo pamoja na kuondoa migogoro ya wafugaji kuingiza mifugo yao katika mashamba ya wakulima pamoja na ufugaji wa kuhamahama kwa ajili ya kutafuta malisho.

“Wizarani tunataka kuondokana na tatizo la malisho katika nchi hii ambalo limeainishwa kwenye ibara ya 25 katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, changamoto ya malisho ni kubwa kwa wafugaji tunaamini tutakapoondokana na changamoto ya malisho, changamoto ya maji tutapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro iliyopo, tutapunguza tatizo la ubora wa mifugo yetu, ndiyo maana tumeamua kuanzia Shamba la Malisho Vikuge.” Alisema Prof. Gabriel

Katibu mkuu huyo pia ameitaka TALIRI kuhakikisha matrekta hayo yanatumika ipasavyo kwa ajili ya kuzalisha kwa kutumia mtaji huo na kulipa deni kwa wakati ili taasisi nyingine za serikali zilizo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ziweze kunufaika na mkopo huo ikiwemo Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) ambayo imekuwa na mashamba makubwa ya uzalishaji wa mifugo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Prof. Damian Gabagambi, shirika ambalo linasimamia mradi wa kuunganisha matrekta wa URSUS-TAMCO amesema faida ambayo wanataka kuiona kupitia mradi huo hapa nchini ni kubadilika kutoka kilimo cha mkono hadi kilimo cha kutumia matrekta.

“Serikali ilipoanzisha mpango huu haikuanzisha ili kupata faida kama wafanyabiashara wengine, faida ambayo serikali inatarajia kupitia mpango huu ni kilimo kilichobadilika, kilimo ambacho kinaondoa jembe la mkono kwa hiyo kupitia mradi huu, serikali imejipanga kupeleka jembe la mkono makumbusho.” Alisema Prof. Gabagambi

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI Dkt. Eligy Shirima na Meneja wa Shamba la Malisho Vikuge Bw. Richard Mdegipala wamesema wanatakiwa kuleta mabadiliko katika sekta ya mifugo hususan kwa kuboresha malisho ya mifugo na kuondokana na tabia ambayo wafugaji wengi wanatumia kwa miaka mingi ya kutafuta malisho ya mifugo yao porini.

Aidha wamesema matrekta hayo yatatumika pia na majirani wa taasisi ya TALIRI pamoja na Shamba la Malisho Vikuge na kwamba matrekta hayo yatawawezesha kuongeza gawio kwenye mfuko mkuu wa serikali.

Hadi sasa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kupitia mradi wa kuunganisha matrekta wa URSUS-TAMCO limeshauza matrekta 413 katika maeneo mbalimbali nchini.

KINARA MATUKIO YA UBAKAJI WANAWAKE 'TELEZA' KIGOMA AKAMATWA

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

VYOMBO vya dola Mkoani Kigoma vimefanikiwa kumkamata kijana Hussein Hamis maarufu(Orosho)anayetuhumiwa kuwa kinara wa ubakaji na kujeruhi wanawake kinguvu kingono nyakati za usiku.

Kijana huyo aliyekamatwa pamoja na watuhumiwa wengine tisa wakitambuliwa kama"teleza"ambapo huwaingia kingono akina wanawake kinguvu,kuwaibia na kuwajeruhi wakiwa wanejipaka oil chafu au mafuta ya mawese ili wanaposhika wawe wanateleza.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Kigoma mjini Samson Hanga amesema kuwa baada ya kuwepo taarifa hiyo ya vijana wanaoingilia akina mama kingono kwa nguvu vyombo vya dola viliendesha zoezi la msako mkali kwa kushirikiana na wananchi ili kuweza kuwakamata wahalifu.

"Tulitengeneza namna namna bora ya kuwakamata wahusika ambapo tulifanya zoezi la upigaji kura ya siri tukapata majina na majina mengine tulipata kupitia vyombo vya dola mpaka sasa tumesha kamata vijana 9 wapo mahabusu na upelelezi unaendelea"alisema

Hanga alisema kuwa katika majina yaliyotajwa na kupigiwa kura mtuhumiwa mmoja alitajwa sana na akina mama waliofanyiwa vitendo vya ukatili ambaye ni Hussein Hamis(Orosho).

"Unajua serikali ina mkono mrefu na macho makubwa yule kijana alipopataarifa kuwa tunamtafuta alikimbilia kwa mama yake kijiji cha Kagongo baadae akakimbia tena kijiji cha Kagunga juzi jioni tukafanikiwa kumkamata Wilayani Kasulu na kuletwa hapa kituo cha polisi kwaajili ya hatua zaidi"alisema

Alisema pia wamefanya gwaride la utambuzi kwa wahanga kuwatambua hao vijana 10 waliokamatwa.Alisema msako bado unaendelea yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja kabla vyombo vya dola havijambaini na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaobainika.

Hadija Khamis Mkazi wa mwanga kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji ni mmoja wahanga wa matukio ya "teleza"ameishukuru serikali kwa kufanikiwa kuwakamata vijana waliokuwa wanafanya vitendo vya kikatili kwa wanawake hasa wa kata za mwanga kusini na kaskazini.

"Unajua hadi sasa yaani siamini kama kweli "teleza amekamatwa tulikuwa tunaishi bila ya amani mimi alipoingia kwangu alinikata na panga mara nne hapa nina maumivu makali hata kazi siwezi kufanya"alisema

"Hawa wapo wengi mimi sababu matukio yanaweza tokea usiku mmoja hata mawili kwa maeneo tofauti serikali iwachukulie hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine na tabia hii iweze kuisha kabisa"alisema

Martha Jerome Mkurugenzi wa asasi ya women promotion Center amesema suala la "teleza"linaumiza mioyo wanaiomba serikali kusaidiana na jamii kutokomeza swala hili.

"Unajua sasa hivi suala la "teleza"limekuwa gumzo Kigoma kwakweli linaumiza moyo,kinatuumiza sisi kama asasi tutahakikisha tunashirikiana na serikali kutokomeza suala hili tutaingia mtaani,naiomba serikali,viongozi wa dini asasi mbalimbali tusaidiane kutokomeza hili jambo"alisema
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Hanga akitoa taarifa kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu kukamatwa kwa vijana 10 wanaotuhumiwa kwa matukio ya kuwaingilia kinguvu wanawake na kuwaibia pamoja na kuwajeruhi maarufu kwa jina la "teleza"

Wananchi Wa Malolo Wafaidika Na Ziara Ya Mbunge Mwakasaka

$
0
0
Na, Editha Edward-Tabora 

Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini Mhe, Emmanuel Mwakasaka amefanya Ziara ya kukutana na Wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa Mrejesho juu ya Uwakilishi wake katika bunge 

Katika Ziara hiyo Mwakasaka ametekeleza ahadi zake kwa wananchi wa kata ya Malolo alizoahidi hapo nyuma Mwakasaka amewawezesha kikundi cha wanawake kilichopo kata ya Malolo kwa kuwapatia kiasi cha fedha cha Sh. 500,000 kwa ajili ya kufanya shughuli za ujasiriamali 

Pia amewawezesha vijana wa kata ya Malolo welding kwa kuwapatia Mashine kwa ajili ya kufanya shughuli za uchomeleaji ili waweze kujipatia kipato, na ametoa vifaa vya michezo kwa timu ya wavulana ya kata ya Malolo kwa kuwapatia mipira Miwili, Filimbi, pamoja na pump ya kujazia mipira 

Kwa hatua nyingine madereva wa Tax wapatao 36 wamejiunga na chama Cha Mapinduzi CCM ili kumuunga mkono Mhe, Mwakasaka kwa Kazi kubwa anayoendelea kuifanya Tabora Mjini 

Aidha Mwakasaka amewataka wananchi hususani kikundi cha wanawake pamoja na vijana kutumia msaada huo katika kujikwamua kiuchumi na kuwataka wafanye Kazi Ili kusaidia jamii ya watu wengine wa familia zao kwa ujumla pia Ziara hiyo imeqmbatana na naibu Waziri Eng.Nditiye Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi mawasiliano.
 Pichani ni mbunge wa Jimbo la Tabora mjini  Mhe, Emmanuel Mwakasaka akiwakabidhi Wanawake Wa kata ya Malolo Fedha.
 Pichani ni vijana wa kata ya Malolo wakiwa wamebeba vifaa vya michezo walivyopatiwa na mbunge Mwakasaka.
 Mbunge Emmanuel  akizungumza na  Wananchi wa Kata ya Malolo Mkoani Tabora.
Mbunge Mwakasaka akisalimiana na baadhi ya  vijana wa kata ya Malolo waliojiunga na Chama Cha CCM.

SOS CHILDREN'S VILLAGES NA PATEL BROTHERHOOD WAKABIDHI VYUMBA VYA MADARASA CHANIKA

$
0
0
*Wahaidi kuendelea kushiriki katika sekta hiyo na kuwaomba wadau wengi zaidi kujitokeza katika kuboresha zaidi mazingira ya ujifunzaji kwa wanafunzi ili waweze kufikia malengo yao 

SHIRIKA la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood  wamekabidhi vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Chanika ikiwa ni mwendelezo wa kuinua sekta ya elimu hasa katika masuala miundombinu na vitendea kazi. 

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano Meneja mradi kutoka Shirika la  SOS Children Villages  Elamu Mkayange amesema kuwa katika miradi inatekelezwa na Shirika ilo ni kusaidia katika sekta ya elimu, na katika mradi huo wamefanya ukarabati wa madarasa 11 ambayo yamegharimu shilingi milioni 80, pamoja na vitabu 150 na shule 10 kutoka Chanika zipo katika mpango wa kupewa vitabu.

Amesema kuwa hadi sasa wamejenga maktaba 2 na vyoo katika shule zilizopo kata za Chanika na Zingiziwa huku akieleza kuwa wamelenga zaidi ya watoto 2000 ambao watafurahia maisha katika sekta ya elimu, amesema kuwa zaidi ya Bilioni 1.8 zimetengwa ili kuendeleza sekta ya elimu katika kata za Chanika na Zingiziwa na ameiomba Serikali na wadau mbalimbali kujitokeza na kusaisia sekta hiyo muhimu.

Kwa upande wake msemaji wa taasisi ya Patel Brotherhood Anil Patel amesema kuwa lengo la kutoa kusaidia sekta hiyo ni kuinua sekta ya elimu kwa kuweka mazingira rafiki wa wanafunzi ili waweze kutimiza ndoto zao.

Amesema kuwa wataendelea kuchangia vitendea kazi hasa vitabu na miundombinu ili watoto waweze kutimiza ndoto zao.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chanika Ladislaus  Mutanda amesema kuwa wamekuwa n changamoto ya madarasa katika kata ya Chanika na hiyo ni kutokana na uhamiaji wa makazi mapya katika maeneo hayo, hivyo madarasa bado hayatoshelezi.

Mutanda ameiomba wizara ya Elimu kuangalia suala hilo la upungufu wa madarasa ili waweze kuchukua wanafunzi wengi katika kata hiyo iliyo na shule za Umma 5 pekee.

Pia amezishukuru sana Sos Children's Villages na na Taasisi ya Patel Brotherhood kwa kuendelea kushirikiana nao katika kuendeleza sekta za elimu na kuiomba serikali na wadau mbalimbali kuzidi kushirikiana ili kuipeleka sekta ya elimu mbali zaidi.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas akizungumza na wakati wa kukabidhiwa vyumba vya madarasa 11 katika shule ya msingi Chanika kutoka kwa Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood waliokarabati madarasa hayo.
Meneja mradi kutoka Shirika la  SOS Children Villages  Elamu Mkayange akizungumza kuhusu mradi wa kukarababti madarasa 11 ya shule ya Msingi Chanika pamoja na kutoa msaada wa Vitabu kwenye Shule zilizopo kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam.
 Msemaji wa Taasisi ya Patel Brotherhood Anil Patel akizungumza kuhusu Taasisi yao inavyosaidia jamii lengo la kuinua sekta ya elimu na kuweka mazingira rafiki wa wanafunzi ili waweze kutimiza ndoto zao wakati wa kukabidhi madarasa 11 yaliyokarabatiwa.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chanika Ladislaus  Mutanda akizoma risala kwa mageni rasmi aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala wakati wa wakati wa kukabidhiwa vyumba vya madarasa 11 katika shule ya msingi Chanika kutoka kwa Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood waliokarabati madarasa hayo.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas(wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madarasa 11 ya shule ya Msingi Chanika yaliyokarabatiwa na Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood.

Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas  akimshukuru Msemaji wa Taasisi ya Patel Brotherhood Anil Patel mara baada ya kuzindua madarasa 11 ya shule ya Msingi Chanika yaliyokarabatiwa na Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kugawa vitabu kwa shule 10 zilizopo katika kata ya Chanika jijini Dar es Salaam vilidhaminiwa na Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas akimkabidi mwanafunzi wa shule ya Msingi Chanika baadhi ya vitabu vya shule hiyo wakati wa zoezi la kugawa vitabu kwa shule takribani 10 zilizopo kwenye kata ya Chanika jijini Dar es Salaam.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas(katikati)  akimshukuru Meneja mradi kutoka Shirika la  SOS Children Villages  Elamu Mkayange(wa kwanza kushoro) kwa kuweza kutoa msaada wa vitabu pamoja ukarabati wa Madarasa 11 kwenye shule ya msingi Chanika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Chanika wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa vyumba vya madarasa 11 katika shule ya msingi Chanika vilivyokarabatiwa na Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood.


Baadhi  ya vitabu vilivyotolewa na  Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood kwa ajili ya Shule 10 zilizopo kata ya Chanika jijini Dar es Salaam.
 
 Baadhi ya madarasa ya Shule ya Msingi Chanika yaliyofanyiwa ukarabati na Shirika la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Patel Brotherhood.

MKEMIA MKUU WA SERIKALI AWASITIZA WAKAGUZI KUZINGATIA UELEDI

$
0
0
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewasisitiza wakaguzi wa kemikali na maabara za kemia kuzingatia ueledi, uadilifu na uaminifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Mkemia Mkuu wa Serikali amezungumza hayo leo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia kutoka Mamalaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali unaofanyika Baraza la Maaskofu, Kurasini, Dar es Salaam. 

“Serikali imetupa majukumu ya kusimamia Sheria ya Mamlaka ya Maaabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani na Sheria ya Vinasaba vya Binadamu, hivyo tunapaswa kuzingatia ueledi, uadilifu, uaminfu na upendo ili kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa ufanisi.

Tutambue Serikali yetu imejielekeza katika kujenga uchumi wa viwanda na inajitahidi kuwekeza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara ikiwemo wanaojihusisha na kemikali, hivyo  tunapotekeleza majukumu yetu tunapaswa kuelewa uelekeo huo wa Serikali na kufanya maamuzi kwa wakati na haraka ili kutokwamisha wadau wetu huku  tukizingatia Sheria.”

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali alisema Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti inawapongeza wakaguzi hao kutokana na kazi kubwa wanayofanya na inawahamasisha kuboresha zaidi huduma kwa wadau kwa kufuata Sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza kama watumishi wa umma.

“Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti inatambua mchango mkubwa wa wakaguzi katika kusimamia Sheria na kuingiza maduhuli ambayo taasisi inatumia katika kuboresha huduma na kujiendesha. Tunatambua changamoto zipo na tunaendelea kuzifanyia kazi kama kuongeza watumishi na vitendea kazi. Tuna maeneo ya msingi ya kuyawekea kipaumbele hasa kwenye uwekezaji wa mitambo ya kisasa ya maabara na teknolojia ili kuwawezesha wakaguzi kutoa huduma bora na za haraka kwa wadau. Tufanye kazi kama familia ili kuweza kutekeleza majukumu yetu kwa mafanikio.” Alimaliza.

Akitoa neno la shukrani, Mkaguzi wa Kemikali, Bw. Jovitus Mukela, alimshukuru Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko kwa nasaha nzuri za ufunguzi wa Mkutano huo.

Kwa niaba ya wakaguzi wenzangu tunakushukuru sana kwa nasaha na maneno mazuri uliyotuambia maana pia yanatukumbusha majukumu yetu na napenda kuwaomba wakaguzi wenzangu kuzingatia yale yote yaliyozungumzwa na kushirikiana kutoa huduma nzuri, kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeitendea haki Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, sisi wenyewe na nchi kwa ujumla.” alimaliza 
 Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akiongea na Wakaguzi wa kemikali (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia ulioandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kufanyika leo katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Kurasini, Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara za Huduma za Ubora wa Bidhaa, Sabanitho Mtega, Maendeleo ya Biashara, George Kasinga, Usimamizi wa Kemikali, Daniel Ndiyo na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Elias Mulima.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Kemikali, Daniel Ndiyo (aliyesimama), akizungumza na Wakaguzi wa Kemikali (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa tatu kulia) kufungua Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali leo.
 Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia wakimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo.
 Mkaguzi wa kemikali na Maabara za Kemia kutoka Maabara ya Kanda ya Kaskazini, Jovitus Mukela (aliyesimama), akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakaguzi mara baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufungua Mkutano huo.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyekaa katikati), akiwa pamoja na Wakurugenzi na Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali mara baada ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi hao uliofanyika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Kurasini, Dar es Salaam. 
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live




Latest Images