Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

BREAKING NEWS: MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, ELIMU YA KATI NA VYUO VYA UFUNDI 2019 HAYA HAPA


BENKI YA CRDB YAFUTURISHA WATEJA WAKE WA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamis Kigwangalla (kushoto) akizungumza jambo huku Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na Mkewe Bi Sangita Nsekela katika hafla fupi ya Iftar iliyoandalia na Benki hiyo kwa wateja wake na Watoto Yatima, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi ya Iftar iliyoandalia na Benki ya CRDB kwa wateja wake na Watoto Yatima, akipongezwa baada ya kuhutubia na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamis Kigwangalla, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kulia) na Kamanda wa Polisi Mstaafu Kanda ya Dar es salaam Suleiman Kova.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto), Kaimu Mufti, Sheikh Hamid Masoud Jongo (kulia) wakimsikiliza Mbunge wa Sumbawanga Mjini,Aeshi Hilaly baada ya hafla fupi ya Iftar iliyoandalia na Benki hiyo kwa wateja wake na Watoto Yatima, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akitoa hotuba yake katika hafla fupi ya Iftar iliyoandalia na Benki hiyo kwa wateja wake na Watoto Yatima, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay akizungumza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza.

































BARAZA LA KILIMO LAWAKUTANISHA WADAU WA KILIMO KUIJADILI ASDP II.

$
0
0


Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya baraza la kilimo Tanzania Bw Enock Ndondole akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa sekta binafsi katika kilimo, kwa niaba ya mwenyekiti wa Bodi, Mkutano huo umefanyika mkoani morogoro na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo.
Mkurugenzi wa Sera Baraza la Kilimo Tanzania Bw. Timothy Mmbaga akifafanua jambo wakati wa mkutano huo uliokuwa ukijadili mchango wao sekta binafsi katika utekelezaji wa mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo nchini ASDP II.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wa siku moja ulioandaliwa na Baraza la kilimo Tanzania na kufanyika Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi wa sera na Mipango Wizara ya Kilimo Bw. Osward Ruboha,(wa kwanza) Makamo mwenyekiti Baraza la Kilimo Mh Jitu Son na Mjumbe wa Bodi wa Baraza la Kilimo wakifuatilia kwa makini mjadala uliokuwa ukiendelea katika Mkutano huo wa Sekta binafsi katika Kilimo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango Wizara ya Kilimo Bw. Osward Ruboha kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo.(Mwenye suti nyeusi kwa walioketi) akiwa katika Picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa Sekta binafsi katika Kilimo.


Baraza la kilimo Tanzania limewakutanisha wadau wa sekta binafsi katika kilimo ili kujadili mchango wao katika utekelezaji wa mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo nchini ASDP II.

Mkutano huo wa siku moja umefanyika Mkoani Morogoro na kuhudhuliwa na wadau zaidi ya 60 wakiwemo maafisa wa Serikali, Taasisi za Kilimo na wadau wa Kilimo ambapo ulifunguliwa na Mkurugenzi Msaidizi wa sera na Mipango Wizara ya Kilimo Bw. Osward Ruboha kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo.

Kampuni ya GreenWastePro yahamasisha wananchi kutumia mifuko mbadala

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro wakionyesha aina mifuko (vibebeo) ambayo haipaswi kutumika kuanzia leo Juni 01, 2019 baada ya kuanza kwa katazo la Serikali la uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko hiyo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kampuni ya huduma ya usafi ya "GreenWastePro Ldt" imewahimiza wananchi na wafanyabiashara wote nchini kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ni adui wa mazingira na badala yake kujikita kwenye matumizi na biashara ya mifuko mbadala isiyohatarisha mazingira.

Meneja wa kampuni hiyo Kanda ya Ziwa, Salim Madafa ametoa rai hiyo leo jijini Mwanza baada ya zoezi la kuhamasisha katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki na uzinduzi rasmi wa matumizi ya mifuko mbadala. Kampuni ya GreenWestPro ni miongoni mwa wadau wa mazingira walioshiriki kwenye zoezi hilo.

"Mifuko ya plastiki imekuwa na athari kubwa katika uchafuzi wa mazingira, mitaro kujaa maji kutokana na mifuko hiyo kuziba hatua ambayo hukwamisha kazi yetu ya uzoaji taka hivyo nitumie fursa hii kuwahimiza wananchi kutumia mifuko mbadala na kuachana na mifuko ya plastiki" amesisitiza Madafa.

Baadhi ya wafanyabiashara wadogo waliokuwa wakisalimisha mifuko ya plastiki katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza, wameomba Serikali kusaidia uzalishaji wa mifuko mbadala kwa wingi na kusambazwa katika maeneo yote huku ikiuzwa kwa bei nafuu hadi shilingi hamsini (Tsh. 50) kama ilivyokuwa mifuko ya plastiki, tofauti na hivi sasa ambapo inauzwa kuanzia shilingi mia mia tatu (Tsh.300).
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro wakionyesha aina ya mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku kutumika ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala na kuachana na matumizi ya plastiki ambayo ni hatari kwa mazingira.
Meneja wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro Kanda ya Ziwa, Salim Madafa (kushoto) akikusanya mifuko ya plastiki iliyozuiliwa matumizi yake kutoka kwa baadhi ya akina mama wajasiriamali katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza.
Meneja wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro Kanda ya Ziwa, Salim Madafa (kushoto) amesema mifuko ya plastiki ilikuwa ikisababisha uchafunzi wa mazingira hivyo wananchi wahamasike kutumia mifuko mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira.
Mmoja wa wafanyabiashara wadogo katika eneo la "Market Street" jijini Mwanza akiendelea na uuzaji wa mifuko mbadala.
Gari la kisasa la kampuni ya usafi ya GreenWastePro linalotoa huduma ya ukusanyaji uchafu katika Mitaa mbalimbali jijini Mwanza.
Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wadogo waliojitokeza kupata elimu kuhusu matumizi ya mifuko mbadala kwenye zoezi la kuhamasisha katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililofanyika jijini Mwanza.
Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wadogo jijini Mwanza wakifuatilia maelezo mbalimbali kuhusu katazo la kuzalisha, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki na badala yake wajikite kwenye matumizi ya mifuko mbadala.
Wananchi na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro wakiwa kwenye zoezi hilo.
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo pamoja na viongozi wa dini jijini Mwanza wakifuatilia wakifuatilia maelezo mbalimbali kuhusu katazo la kuzalisha, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWestPro Kanda ya Ziwa wakiwapungia mikono wananchi baada ya kutambulishwa kwenye zoezi la kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala ambapo kampuni hiyo ni miongoni mwa wadau muhimu wa usafi na utunzaji wa mazingira.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko Kuu jijini Mwanza (kushoto), akimuonyesha Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) aina ya mifuko mbadala ambayo tayari ameanza kuiuza sokoni hapo.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko Kuu jijini Mwanza (kushoto) akieleza kuhusu upatikanaji wa mifuko mbadala na hivyo kuwatoa hofu wananchi kuhusu upatikanaji wa mifuko hiyo jijini Mwanza.
Meneja wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro Kanda ya Ziwa, Salim Madafa (wa pili kulia) akiteta jambo na wadau wa mazingira jijini Mwanza wakati wa zoezi la kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala na kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki.
Ujumbe muhimu unaohamasisha matumizi ya mifuko mbadaya ambayo ni rafiki kwa mazingira kutoka kampuni ya GreenWestPro inayohusika na usafi na utunzaji wa mazingira kwa sasa ikifanya shughuli zake katika mikoa ya Mwanza, Dodoma na Dar es salaam.
Tazama Video hapa chini

WAZIRI MPINA :SIRIDHISHWI NA BEI YA MAZIWA ,AITAKA BODI YA MAZIWA KUPANGA BEI UPYA

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza katika kilele cha wiki ya maziwa duniani ambapo kitaifa imefanyika mkoani Arusha.

Waziri wa Mifugo Mhe.Luhaga Mpina akiwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe.Gabriel Daqqaro katika kilele cha siku ya maziwa duniani iliyoadhimishwa kitaifa mkoani Arusha.
 Wanafunzi wakiwa katika Fokeni ya kugawiwa maziwa leo katikabuwanja wa Shekhe Amri Abeid ambapo ni kilele cha siku ya maziwa duniani iliyoadhimishwa kitaifa mkoani Arusha.
 Wanafunzi wakinywa zao maziwa kama wanavyoonekana katika picha
Mara baada ya kugawiwa maziwa leo katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid ambapo ni kilele cha siku ya maziwa duniani iliyoadhimishwa kitaifa mkoani Arusha.


Na.Vero Ignatus Arusha.



Waziri wa Mifugo na Uvuvi amefunga Maadhimisho ya 22 ya kilele cha wiki ya maziwa duniani ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Arusha  yenye kauli mbiu isemayo maziwa yaliyosindikwa kwa afya na buchumi wa viwanda"




Katika sherehe hizo zaidi ya lita za maziwa 5810 zimekusanywa na wadau wa maziwa na kugawa kwa wanafunzi wa shule za msingi,wasiojiweza na katika mahosipitali katika mkoa wa Arusha bure.


Mhe.Mpina amesema  unywaji wa maziwa ni swala muhimu na nyeti katika maisha ya kila siku ya mwanadamu,ambapo amesema Taifa la Tanzania lina zaidi ya mifugo asilimia 60% na ni nchi ya pili Afrika kwa kuwa na mifugo mingi  lakini uzalishaji wake wa maziwa ni duni

"Ukilinganisha uzalishaji wetu hapa nchini haulingani na baadhi ya majirani zetu kwani sisi lita bil 2.2 ambapo sisi tunayomaeneo mazuri ya malisho tofauti na wenzetu,Kenya lita bil.5.6,uganda lita 2.7

Amesema serikali mwaka jana 2018  waliweza kukamata jumla ya lita tani 26.5 za maziwa na nyama ambazo zilijaribu kuingia nchini bila kufuata sheria na utaratibu, amesema Serikali imeendelea kuimarisha mipaka yote na kudhibiti kwani awali wasindikaji wa ndani walikuwa wanakosa soko.

Amesema kuwa serikali inaendelea kuhakikisha uzalishaji na usindikaji wa maziwa unaongezeka ni  pamoja na mipaka yote,nchi zote zinzoingiza maziwa yote yaliyokuwa yanaingia bila kukaguliwa,bila kuchekiwa ubora wake,bila kulipiwa kodi na leseni yote mengine yameisha muda wake yanakamatwa 

AIDHA Mhe.Mpina ametoa maelekezo kwa bodi ya maziwa kwamba ifikapo julai 30 mwaka huu ihakikishe kuwa mwananchi yeyote yule atakayehitaji mtamba asikose na kama itakuwahaipo hapa nchini basi ni vyema ikaagizwa nje ya nchi.



Amewataka bodi hiyo kuhakikisha wanakaa na kujadili bei halali ya maziwa ikishindikana serikali itatoa bei elelevu kwani maziwa yapo wazalishaji wanatafuta soko kwaajili ya kuyauza maziwa yao.



Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro aliyemuwakilisha mkuu wa mkoa anesema kwa asilimia kubwa wakazi wa Arusha ni wafugaji amesema changamoto kubwa iliyopo ni ng'ombe wa asili waliopo wanatoa lita chache sana kulingana na idadi ya ng'ombe waliopo kwa sasa.


Amesema kuhusu swala la viwanda mkoa wa Arusha tayari una jumla ya viwanda 18 na vinaendelea kufanya kazi.
Nae msajili wa Bodi ya maziwa nbi Sophia Mbete amesema kuwa lenho kuu la maonyesho hayo ya maziwa na bidhaanzitokanazo na maziwa ni kubadikishana uzoefu na kujifunza mbinu zanuzalishaji maziwa na usindikaji kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Amesema kuwa wameweza kupata washiriki 22 kutoka Iringa,Songwe,14 kati yao wanatoka mkoa wa Mbeya waliojitokeza kwaajili ya kuja kujifunza isindikaji wa maziwa,siagi,jibini na Mtindi.

Maadhimisho ya 22 ya wiki ya maziwa duniani ambayo yametanyika kitaifa mkoa wa Arusha yalizinduliwa rasmi na Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega na leo yamehitimishwa na Waziri wa Mifugo na Viwanda Luhaga Mpina ambapo wadau 46 wameahiriki pamoja na taasisi 4 za kifedha.

RC Mongella azindua rasmi matumizi ya mifuko mbadala,asema bei itashuka tu

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akigawa mifuko mbadala kwa baadhi ya wananchi jijini Mwanza ili kuhamasisha matumizi ya mifuko hiyo.

Mongella ametumia fursa hiyo kuwatoa hofu wananchi wanaodhani inauzwa kwa gharama kubwa akisema nayo itashuka bei kama ilivyokuwa mifuko ya "Rambo" ambayo wakati inaanza kutumika ilikuwa ikiuzwa kwa gharama kubwa na baadae ikashuka.

Zoezi hilo limefanyika katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza na kwenda sambamba na uzinduzi rasmi wa matumizi ya mifuko mbadala ambapo wananchi na wafanyabiashara wamehimizwa kuendelea kusalimisha mifuko ya plastiki katika ofisi mbalimbali ikiwemo Serikali za Mitaa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye zoezi la kuhamasisha katazo la Serikali kuhusu uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko (vibebeo) ya plastiki kuanzia leo Juni 01, 2019.

Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi amewahimiza wananchi wa Wilaya hiyo kuwa watiifu kutekeleza katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki na kutumia mifuko mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira.
Naibu Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha amesema utekelezaji wa zoezi hilo utazingatia sheria hivyo wananchi waondoe hofu kwani zoezi hilo halitamuonea mtu yeyote na kwa wale ambao bado wana mifuko ya plastiki waendelee kuipeleka katika ngazi husika kama ilivyoelekezwa.
Afisa Mkaguzi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Abel Sembeka akizungumza wakati wa zoezi hilo ambapo amesema matumizi ya mifuko ya plastiki iliyozuiliwa ni ile inayohusisha vibebeo kama vile "Rambo" na kwamba mifuko ya plastiki ya vifungashio kama karanga, binzari na miwa bado haijazuiliwa.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana, akitoa salamu zake kwenye zoezi hilo ambapo amesema Serikali itasimamia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kuzingatia sheria hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya Serikali yao sikivu.
Viongozi mbalimbali mkoani Mwanza wakifuatilia zoezi la kuhamasisha katazo la Serikali kuhusu uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko (vibebeo) ya plastiki.
Wananchi na wadau mbalimbali wa mazingira wakifuatilia zoezi hilo.
Wadau wakiwa kwenye zoezi hilo.
Viongozi wa dini, wafanyabiashara wadogo na wananchi wakifuatilia zoezi hilo.
Wananchi na viongozi mbalimbali wa dini wakinyoosha mikono kuunga mkono katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akionyesha mifuko mbadaya ambayo ni rafiki kwa mazingira inayopaswa kutumika.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akigawa mifuko mbadala kwa baadhi ya viongozi jijini Mwanza ili kuhamasisha matumizi ya mifuko hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akimsikiliza mmoja wa akina mama wanaouza mifuko mbadala jijini Mwanza ambapo Mongella amesema baada ya muda mfupi ujao, mifuko hiyo itaanza kuuzwa kwa gharama nafuu baada ya wafanyabiashara wakubwa kumaliza taratibu za kuitoa bandarini.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akigawa mifuko mbadala kwa baadhi ya wananchi jijini Mwanza ili kuhamasisha matumizi ya mifuko hiyo.
Meneja wa kiwanda cha Falcon kilichopo jijini Mwanza akionyesha baadhi ya bidhaa ikiwemo mbao zinazotengenezwa kwa kutumia mifuko ya plastiki ambapo amewahamasisha wananchi kukusanya mifuko hiyo na kwenda kuiuza kiwandani hapo badala ya kuitapanya ovyo na kuharibu mazingira.
Baadhi ya wajasiriamali wakisalimisha mifuko ya plastiki kwenye zoezi hilo ambapo kampuni ya kufanya usafi ya GreenWestPro ilitumia zoezi hilo kuhamasisha wananchi na wafanyabiashara kusalimisha mifuko ya plastiki.
Zoezi la kusalimisha mifuko ya plastiki likiendelea jijini Mwanza.
Wananchi wameshauriwa kusalimisha mifuko ya plastiki katika ngazi husika ikiwemo ofisi za Serikali za Mitaa badala ya kuitapanya ovyo na hivyo kuhatarisha mazingira.
Kampuni ya GreenWestPro ni mdau mkubwa wa mazingira ambapo inafanya shughuli zake za usafi na utunzaji wa mazingira katika majiji matatu nchini ambayo ni Dar es salaam, Mwanza na Dodoma.
Kampuni ya GreenWastePro imetumia fursa hiyo kuhamasisha wananchi kuachana na matumizi ya mifuko (vibebeo) ya plastiki na kujikita kwenye matumizi ya mifuko mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira.
Tazama BMG Online TV hapa chini
 Wananchi na wafanyabiashara watakiwa kusalimisha mifuko ya Plastiki
Ukikutwa na mifuko ya plastiki, adhabu yake ni hii hapa

MAJALIWA AIKABIDHI AZAM KOMBE LA UBINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kikombe cha Ubingwa wa Shirikisho la Azam (ASFC), nahodha wa Azam, Aggrey Moris baada ya Azam kuifunga Lipuli 1-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa kwenye uwnja wa Ilulu mjini Lindi Juni 1, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri )
Mshambuliaji wa Azam, Donald Ngoma akichanja mbuga kuelekea lango la Lipuli huku akizongwa na mlinzi wa Lipuli Haruna Shamte katika mechi ya fainali ya mashindano ya Shirkisho la Azam kwenye uwaja wa Ilulu mjini Lindi Juni 1, 2019. Azam ilioshinda 1-0. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkiuu)
Mshambuliaji wa Azam, Obey Chirwa akimtoka Mlinzi wa Lipuli N. Lufunga katika mechi ya fainali ya ubingwa wa mashindano ya Shirikisho la Azam iliyochezwa kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi Juni 1, 2019. Azam ilishinda 1-0. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

AZAM FC YAUNGANA NA SIMBA KIMATAIFA

$
0
0
*Ni baada kuifunga Lipuli fainali za ASFC

TIMU ya Azam FC imefuzu michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika msimu ujao baada ya kuifunga Lipuli FC bao 1-0 kwenye fainali za Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Mbali na kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika, timu ya Azam imeondoka na kitita cha sh. milioni 50, medani pamoja na kombe.

Fainali hizo zimefanyika leo (Jumamosi, Juni 1, 2019 katika uwanja wa Ilulu, Manispaa ya Lindi ambapo ushindi huo unaifanya Azam FC kuungana na Simba kuliwakirisha Taifa kwenye michezo ya Kimataifa itakayoanza Novemba mwaka huu.

Mshambuliaji wa Azam Obrey Chirwa ndio aliyeiwezesha timu yake ya Azam kuibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya kufunga bao la ushindi katika kipindi cha pili.


Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, timu ya Lipuli FC iliyong’ara kwa kutawala mchezo kwenye kipindi cha kwanza, ilishindwa kutumia nafasi nyingi ilizozipata kuifunga Azam.

Mbali na timu ya Lipuli kuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo, pia timu hiyo imetoa mchezaji bora wa mechi ya fainali, Paul Ngalema pamoja na mfungaji bora wa mashindano hayo Seif Rashid.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JUNI 1, 2019.

Mshambuliaji wa Azam, Donald Ngoma akichanja mbuga kuelekea lango la Lipuli huku akizongwa na mlinzi wa Lipuli Haruna Shamte katika mechi ya fainali ya mashindano ya Shirkisho la Azam kwenye uwaja wa Ilulu mjini Lindi Juni 1, 2019. Azam ilioshinda 1-0. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkiuu)


MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA WAAHIDI KUSIMAMIA HAKI YA WANACHAMA WAKE

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umewataka watoa huduma katika vituo vya afya na hospitali nchi nzima walio katika orodha ya mfuko huo kutowanyanyapaa wanachama wake.

Kauli hiyo imetolewa leo wakati wa kikao kazi kati ya watumishi wa mfuko huo na Wahariri wa vyombo vya habari nchini kilichofanyika ukumbi wa Idd Nyundo uliopo katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mbele ya Wahariri pamoja na kujadili masuala mbalimbali, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard Konga amesema anachofahamu vituo vyote vinavyotoa huduma za afya kwa wateja wa mfuko huo wanaelewa taratibu zilizokuwepo na amesisitiza kila mwanachama anayo haki kupata huduma kulingana na aina ya kadi aliyonayo.

Ameongeza kuwa alishawahi kupokea malalamiko katika baadhi ya hospitali, lakini baada ya kufuatilia kwa sasa kila kitu kipo sawa huku akieleza unajua mfuko wao una wateja wengi, kama wataamua kuacha kufanya kazi hospitali yoyote basi itapoteza watu kwa kiasi kikubwa.

Amesema ndio maana wameweka wazi kwa yeyote anayeonesha kunyanyapaliwa au kutendewa kinyume na taratibu za huduma za kiafya atoe taarifa kwetu tutalishughulikia ndani ya muda mfupi.

Pia Konga amesema lipo tatizo la wizi au ubadhirifu katika baadhi ya watoa huduma. "Mifuko mingi ya bima ya afya duniani inalalamikia wizi unaofanywa kati ya wanachama kudanganya watoa huduma kuwema bili kubwa ya matibabu kinyume na bili halisi au watumishi wasio waaminifu wa NHIF kuuibia mfuko,".

"Zipo kesi nyingi tunazifuatilia kwenye baadhi ya hospitali. Lakini kwa sasa tunafanya utafiti. Tukishajipanga tutalimaliza hili tatizo.Lakini pia lipo tatizo la wanachama kuendelea kuwa na wategemezi waliopitisha umri wa miaka 18. Tunaamini huyo anatakiwa kuwa katika utaratibu mwingine wa uchangiaji. Ndiyo maana tyliamua kupeleka huduma za bima ya afya kwa wanafunzi ambapo wanalipia Sh 50,400 kwa mwaka," amesisitiza Konga.

Awali akiwasilisha mada kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, Mkurugenzi wa Wanachama wa NHIF, Mbaruku Magawa amesema wamekuwa wakikipa fedha nyingi katika vituo vyote vilivyo kwenye utaratibu wao ili kuhakikisha wanachama wanapata huduma stahiki.

"Mfano kwa mwaka 2018/19 tumelipa jumla ya Sh Bilioni 339.06 kwa vituo vya afya 7,400 nchini. Hapo zikiwemo hospitaki za mikoa, wilaya, Zahanati na Hospitali ya Taifa," amesema Magawa.

Amebainisha kwamba mfuko huo ulioanzishwa mwaka 2001 kwa Sheria Sura namba 395 umetimiza miaka 18. Ambapo hadi sasa kuna wanachama 16,969,943 sawa na asilimia 32 ya watanzania wote.

Wanajipanga kuhakikisha watanzania wengi zaidi wanajiunga na mfuko huo ili kupata huduma za afya kwa wakati na gharama nafuu. Hasa ikizingatiwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanaongezeka siku hadi siku.

Akitolea mfano, takwimu za mfuko zinaonyesha mwaka 2014/15 idadi ya wagonjwa waliotibiwa magonjwq yasiyo ya kuambukizwa walikua 286,806.

Na kwamba ndani ya miaka minne idadi imeongezeka maradufu ambapi takwimu za mwaka 2017/18 zinaonyesha kuna wagonjwa 1,574,803 waliotibiwa kupitia NHIF wakisumbuliwa na maradhi yasiyo ya kuambukiza.

Wakati huo huo NHIF imeahidi kuwa karibu na wanachama wake kwa kutoa taarifa za mara kwa mara kupitia vyombo vya habari ikiwemo elimu juu ya umuhimu wa kuwa na bima ya afya lakini pia kuzisaidia baadhi ya hospitali zisizo na uwezo wa kuwa na vifaa tiba kwa kuwapa mikopo ili wanachama wao wapate huduma popote ndani ya nchi.

Akitoa shukrani kwa watumishi wa mfuko huo kwa niaba ya wahariri wa vyombo vya habari nchini,Celina Wilson kutoka Gazeti la Uhuru amesema wahariri kupitia kikao hivyo ameongeza uelewa na ufahamu kuhusu mfuko wa Taifa wa Bima ya afya huku akieleza wahariri watahakikisha wanakuwa makini katika kuandika habari za mfuko huo.

"Tunawahakikishia Wahariri tutatumia kalamu zetu na vyombo vyetu vizuri katika kuandika habari zinazohusu afya.Kuna mengi ambayo tumeyafahamu kupitia kikao hiki,kikubwa tuendeleee kushirikiana na wahariri tupo tayari,"amesema Wilson.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Bernard Konga akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini leo jijini Dar es Salaam
Mmoja ya wahariri akizungumza wakati wa kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari nchini na maofisa wa NHIF .Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es Salaam
Mhariri kutoka Gazeti la Uhuru Celina Wilson akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya(NHIF) baada ya kufanyika kikao leo jijini Dar es Salaam.
Maofisa wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya wakawa katika picha ya pamoja na Wahariri wa vyombo vya habari nchini

WAZIRI SIMA AONGOZA OPERESHENI YA MIFUKO PLASTIKI SINGIDA

$
0
0
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Mussa Sima akigawa mifuko mbadala kwa wananchi iliyotolewa na Kanisa la Full Gospel la mjini Singida kuashiria upigaji marufuku mifuko mbadala.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Mussa Sima akizungumza na wananchi katika soko kuu la mjini Singida wakati wa opresheni ya kukagua utelekezaji wa katazo la mifuko ya plastiki
Kikosi kazi cha ukaguzi wa mifuko ya plastiki kikikagawa utelekezaji wa katazo la mifuko hiyo soko kuu mjini Singida leo.
Wajumbe wa kikosi kazi cha katazo la mifuko ya plastiki Said Athuman (kulia) na Mhandisi Boniphace Guni wakiwa katika duka la mmoja wa wafanyabiashara aliyeachana na mifuko ya plastiki na kuanza kuuza mifuko mbadala
***********************************************

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Mussa Sima amewataka wafanyabiashara wa mifuko mbadala kutotumia fursa hiyo kuwakandamiza wananchi kwa kuiuza kwa bei ya kubwa.

Mhe. Sima ametoa kauli hiyo leo mjini Singida wakati aliposhiriki operesheni ya kukagua utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki ambalo limenza Juni mosi mwaka huu.

Katika opresheni hiyo iliyoambatana na ugawaji wa mifuko mbadala iliyotolewa na Kanisa la Full Gospel kwa wananchi mjini hapa alisema ni busara kwa wafanyabiashara hao kuweka bei inayowawezesha wananchi kuweza kuinunua."Ndugu wafanyabiashara tusiwakomoe Watanzania wasije kuona sasa mifuko hii ni ghali na kuona ni bora turudi katika mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku," alisema.

Naibu Waziri Sima ambaye alikuwa mgeni rasmi katika operesheni hiyo
akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi alisema
wataalamu kutoka serikalini watatembelea viwandani kuona kama bei rafiki kwa mwananchi inatumika.

Aidha aliwataka wananchi hususan vikundi vya wanawake kutumia fursa hiyo kusuka vikapu kwa ajili ya kubebea bidhaa na hivyo kujipatia kipato ambapo alisema kwa kufanya hivyo tutajenga utamaduni kama wa zamani na kuachana na mifuko ya plastiki. Operesheni ya kukagua utekelesaji wa katazo la mifuko ya plastiki linaloratibiwa na Ofisi ya Makamu ilibaini wananchi wengi kupata uelewa wa madhara ya
mifuko ya plastiki.

Wananchi mbalimbali wameitikia wito wa kuanza kutumia mifuko mbadala katika masoko na maduka ambapo wamesema wanaipongeza Serikali kwa kuliona hilo na kupiga marufuku mifuko hiyo. Zoezi hilo limeenda sambamba na utoaji wa elimu kuhusu madhara ya mifuko ya plastiki na fursa za uwekezaji wa mifuko mbadala kama ambavyo ilitolewa na wakaguzi kutoka Baraza la Taifa Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Pia mkoa huo ulifanya maandamano ya kuunga mkono katazao hilo na kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala ambapo yalihudhuriawa viongozi mbalimbali kutoka mkoa huo.

MFUMO WA “AJIRA PORTAL” KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA UPENDELEO WA AJIRA SERIKALINI

$
0
0



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akifungua mafunzo ya mfumo mpya wa “Ajira Portal” kwa Maafisa Rasilimaliwatu serikalini yaliyofanyika jijini Dodoma. 
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya wa “Ajira Portal” wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dodoma. 
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akifafanua changamoto za mifumo ya awali ya uombaji kazi, kabla ya ufunguzi wa mafunzo ya mfumo mpya wa “Ajira Portal” kwa Maafisa Rasilimaliwatu jijini Dodoma. 
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ACP Ibrahim Mahumi akizungumza kabla ya ufunguzi wa mafunzo ya mfumo mpya wa “Ajira Portal” kwa Maafisa Rasilimaliwatu jijini Dodoma. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wa serikali baada ya kufungua mafunzo ya mfumo mpya wa “Ajira Portal” kwa Maafisa Rasilimaliwatu jijini Dodoma. Wengine ni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ACP Ibrahim Mahumi (kushoto). 

*********************************************** 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) amewataka waajiri
nchini kuhakikisha wanautumia vizuri mfumo wa “Ajira Portal” ili kukabiliana na changamoto ya upendeleo wa ajira serikalini. 

Mhe. Mkuchika ameyasema hayo, alipokuwa akizindua mafunzo kuhusu
mfumo mpya wa “Ajira Portal” kwa Maafisa Rasilimaliwatu serikalini jijini
Dodoma. 

Mhe, Mkuchika amesema mfumo mpya wa “Ajira Portal” utaongeza ufanisi
katika suala la ajira kwani umeundwa ili kurahisisha mchakato wa ajira kati
ya Sekretarieti ya Ajira, waombaji wa kazi na waajiri serikalini. 

“Matumizi sahihi ya mfumo huu yataongeza ufanisi, yatapunguza siku za
kuendesha michakato ya ajira na yatamwezesha mwajiri kutuma kibali
chake kupitia mtandao na kuweza kufuatilia maendeleo ya kibali cha ajira
kupitia mtandao” Mhe. Mkuchika amefafanua. 

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, mfumo huu pia utafikisha majina ya
waombaji wa ajira waliofaulu usaili kwa waajiri wote nchini siku hiyohiyo
yanapotumwa na Sekretarieti ya Ajira. 

Amesema kuwapo kwa mfumo wa “Ajira Portal” kutaifanya serikali
iondokane na kasumba ya kuajiri watu wanaodanganya sifa zao halisi kwa
kuwa mfumo huo umewezeshwa kuongea na mifumo mingine mikubwa ya
utambuzi nchini ikiwemo NIDA, NACTE na NECTA. 

“Sitafurahishwa na sitapenda kupata taarifa kwamba bado kuna waajiri
katika sekta ya umma hawatumii mfumo huu unaodhibiti vitendo vya
upendeleo na unaookoa muda wa mchakato wa ajira serikalini” Mhe.
Mkuchika amesema. 

Akizungumza kwa Niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ACP Ibrahim Mahumi amesema kwa
mujibu wa tafiti aliyoifanya, Tanzania ni nchi pekee kwenye ukanda wa
Afrika Mashariki na Kati inayoongoza kwa kuwa na mfumo wa “Ajira
Portal”.

Awali, akitoa maelezo ya mfumo, Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi amesema Sekretarieti ya Ajira
imeamua kubuni mfumo mpya wa “Ajira Portal” ili kukabiliana na
changamoto zilizojitokeza katika mfumo wa awali zilizokuwa
zinachelewesha mchakato wa ajira serikalini. 

Bw. Xavier amesema, Sekretarieti ya Ajira ilikuwa ikitumia magazeti, mbao
za matangazo, televisheni, redio na tovuti kutangaza nafasi za ajira
serikalini ambapo mifumo hiyo iliisababishia serikali hasara kwa kuwa
gharama nyingi zilitumika kutangaza ajira hizo. 

Mafunzo ya “Ajira Portal’ kwa Maafisa Rasilimaliwatu serikalini
yamefanyika kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi wao na kuwawezesha
kuwa na taarifa sahihi za waajiriwa zinazowafikia kwa wakati.

DK.MABODI AFUNGUA MAFUNZO YA UWT MKOA WA MJINI.

$
0
0
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akifungua Mafunzo ya Siku Moja ya UWT Mjini Unguja, kuanzia ngazi za Wadi hadi Mkoa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Sheikh Idrissa Abdul Wakili uliopo Kikwajuni 
BAADHI ya Viongozi na Watendaji wa UWT Ngazi za Wadi hadi Mkoa wa Mjini Unguja. 

***************************************** 

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR. 

WANAWAKE wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Tanzania Mkoa wa Mjini Unguja wametakiwa kujipanga vizuri kwa kuhakikisha CCM inapata Ushindi mkubwa wa Kihistoria katika Uchaguzi Mkuu wa Dola mwaka 2020. 

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi wakati akifungua Mafunzo Elekezi ya Kuwajengea Uwezo Viongozi mbali mbali wa UWT kuanzia ngazi za Wadi hadi Mkoa wa Mjini yaliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakili Kikwajuni Unguja. 

Dk.Mabodi amesema Wanawake wa CCM wanatakiwa kuwa Mstari wa mbele katika kuandaa Mazingira rafiki ya upatikanaji wa Ushindi wa Chama Cha Mapinduzi katika UchaguzI Mkuu ujao, kwa kuongeza Wanachama wapya na kuhakikisha wanaipigia kura nyingi CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujaop. 

Amesema Wanawake wana historia kubwa na nzuri ya kufanikisha harakati za ushindi wa Chama na mikakati mbali mbali ya Ukombozi wa Nchi za Afrika. 

Alieleza kwamba UWT pamoja na Jumuiza zingine za CCM zinatakiwa kushirikiana pamoja katika kuandaa mazingira ya Ushindi katika Uchaguzi ujao ili kutimiza kwa vitendo kauli mbiu ya Umoja ni Ushindi ndani na nje ya CCM. 

Akizungumzia Mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu huyo Dk.Mabodi,amesema Mafunzo ni jambo muhimu sana katika shughuli za Kisiasa kwani Viongozi na Watendaji wanajengewa uwezo wa masuala mbali mbali ili watekeleze majukumu yao kwa uhakika. 

“Mafunzo haya yasiishie katika Ngazi ya Wadi tu bali yashuke mpaka ngazi za Matawi hadi Mashina kwa lengo la kuhakikisha Jeshi letu linakuwa na uwezo mkubwa wa kufanikisha Ushindi wa CCM Mwaka 2020.”alisema Dk.Mabodi. 

Katika maelezo yake Dk.Mabodi aliwasihi Wanawake hao kutojihusisha na masuala ya makundi ya kubeba Wagombe wa nafasi za Urais,Ubunge,Uwakilishi na Udiwani kabla ya Chama kutoa maelekezo ya kuana kampeni, na atakayebainika kufanya hivyo CCM itamchukulia hatua za Kimaadili. 

Alisema CCM imekuwa Mstari wa mbele katika kuhamasisha Jamii kuenzi Amani na Utulivu Nchini ili kutoa nafasi pana kwa Serikali kutekelea kwa Ufasini shughuli mbali mbali za Maendeleo. 

Alisema kwa kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Awamu ya Pili ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Nchi imepiga hatua kubwa za Kimaendeleo kutokana na kuimarika kwa Amani. 

Naye Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo alisema Umoja huo unaendelea kutoa mafunzo mbali mbali ya kuwajengea uwezo Viongozi na Watendaji wake ili waingie katika harakati za Uchaguzi Mkuu ujao wakiwa na uwezo mzuri wa Kiutendaji na Kiuongozi. 

Akitoa shukrani kupitia Magfunzo hayo Mbunge wa Viti Maalum kupitia Mkoa wa Mjini Unguja Mhe.Asha Abdallah “Mshuwa”, alisema watayafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Mgeni rasmi kwa lengo la kuimarisha UWT na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla. 

Amefafanua kwamba Wanawake wa Mkoa huo wapo tayari kupambana Vita ya Kisiasa na kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika ngazi mbali mbali katika Uchaguzi Mkuu Ujao. 

Mafunzo hayo ya kuwajengea Uwezo wa masuala mbali mbali ya Kiuongozi Wanawake wa UWT, yameandaliwa na Wabunge na Wawakilishi wa Viti Maalum wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja.

Katazo la Matumizi ya mifuko ya Plastiki lafanikiwa kwa 99% Jijini Dodoma

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AONGOZA OPARESHENI YA UKAGUZI WA MIFUKO YA PLASTIKI JIJINI DODOMA

$
0
0

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Joseph Malongo akinunua kikapu ikiwa ni kuhamasisha viongozi kutumia mifuko mbadala na kuachana na mifuko ya plastiki jijini Dodoma 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Joseph Malongo akiongea wakati wa uzinduzi wa operesheni ya zuio la mifuko la mifuko ya plastiki ilyofanyika jijini Dodoma ikiwa ni agizo la Serikali kuwa ifikapo tarehe 1 juni hakuna tena kutumia mifuko ya plastiki 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Joseph Malongo akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi cha kuzuia mifuko ya plastiki jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa operesheni ya kukagua mifuko ya plastiki jijini humo. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Joseph Malongo akiwa pamoja na Katibu Tawala mkoa wa Dodoma wakati wa ukaguzi wa mifuko ya plastiki kwenye maduka na masoko jijini Dodoma. 
Sehemu ya Wakazi wa jiji la Dodoma waliohudhuria katika uzinduzi wa operesheni ya ukaguzi wa mifukoya plastiki jijini Dodoma. 
………………….. 
Wito umetolewa kwa Wakazi wa Dodoma na Wilaya zake kuacha kabisa kautumia mifuko ya plastiki na kuanza mara moja matumizi ya mifuko mbadala ikiwa ni kutii agizo la Serikali la kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki. 


Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Joseph Malongo wakati wa uzinduzi wa operesheni ya kukagua mifuko ya plastiki katika jiji la Dodoma ambapo ni kutii agizo la Serikali la ukomo wa matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia juni 1. 

Akiongea katika oparesheni hiyo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais ndiyo Wasimamizi wakubwa wa mazingira Nchini, hivyo amefurahi kuona elimu juu ya katazo la mifuko ya plastiki kwa jiji la Dodoma imefika kwa Wananchi kwa sababu ambao wamekutwa na mifuko ya plastiki ni wachache sana kulinganisha na Wananchi wanaotumia mifuko mbadala kwa siku ya leo. ‘Elimu imefika kwani kila Mwananchi namuona kabeba mfuko mbadala, vikapu n.k” alisema Injinia Malongo 

Naye Mkuu wa Wilaya wa jiji la Dodoma Mh. Protabas Katambi amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na anawaagiza Wananchi na Wafanyabiashra wa jiji laDodoma kutii agizo la Serikali na kuachana kabisaa na matumizi ya mifuko ya plastiki. ‘Mwananchi atakayekutwa na mfuko wa plastiki hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yake, hili suala syo mchezo mchezo nia agizo la Serikali” alisema Katambi 

Operesheni hiyo ya kukagua mifuko ya plastiki imekuja baada ya Waziri Mkuu wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kutoa agizo bungeni kuwa ifikapo juni 1 hakuna Mwananachi atakayeruhusiwa kutumia mifuko ya plastiki Nchini Tanzania.

Usajili John Stephen Akhwari nternational marathaon yaanza

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha


ZOEZI la usajili kuelekea mashindano ya mbio za riadha ya John Stephen Akhwari International Marathoni limeanza huku mbio hizo zikitarajiwa kufanyika Juni 9 mwaka huu.

Mbio hizo za wazi za kilomita 21,kilomita 5 na km 2 ambazo zitafanyika katika uwanja wa Kumbu kumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa zinatarajiwa kushirikisha zaidi ya wanariadha 1500 kutoka ndani na nje ya nchi .

Mkurugenzi wa mbio hizo Sylvester Orao ameliambia Championi ijumaa kuwa zoezi la usajili limeanza katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa na kuwaomba wanariadha wote wanaotarajia kushiriki wafike kujiandikisha tayari kabisa kwa mbio hizo na kuongeza kuwa garama uandikishaji ni shilingi elfu kumi na tano.

“ Ndio mara ya kwanza mbio zetu kufanyika naamini zitapata uzoefu mkubwa lakini pia wapo wadhamini ambao wametuunga mkono mpaka sasa kuhakikisha mbio hizi zinafanyika kwa ubora uliokusudiwa,”alisema Orao.

Alisema tayari washiriki kutoka nje ya nchi wameanza kujiandikisha kwa njia ya mtandao ikiwa ni kutoka katika nchi za Kenya Cameroon,Nigeria,Uholanzi ,Marekani na Uingereza huku washiriki kutoka ndani ya nchi mikoa ya Morogoro,Mtwara,Dar es salaam,Tanga,Kilimanjaro na Manyara pia wamethibitisha kushiriki.

Zawadi kwa washindi wa kilomita 21 kwa wanawake na wanaume ,mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi laki nane,mshindi wa pili atapata laki sita na mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi laki nne huku mshindi wa nne hadi wa kumi zawadi za fedha pia zitatolewa.

Mbali na zawadi kwa washindi wa km 21 pia washindi wa km 5 kuanzia namba moja hadi sita atapata fedha taslimu,huku medali za dhahabu zikitolewa kwa wale watakaokimbia km 21,shaba kwa km 5 pia vyeti vya uthibisho wa ushiriki utatolewa.

Akizungumzia suala la vibali kwa wanariadha watokao nje ya nchi liko pale pale kwani hata shirikisho la Riadha nchini(RT) linahimiza wote wanaotoka nje ya nchi waje na vibali kutoka katika vyama vyao ili waweze kushiriki.
Alisema lengo la mashindano ni kumunzi mwanariadha wa zamani alieiletea Tanzania heshima mwaka 1968 katika mashindano ya Olimpiki ya Mexico mzee John Stephen Akhwari ambae licha ya kuumia mguu katika mashindano hayo lakini alipambana na kumaliza mbio na kufanikiwa kuweka historia katika mashindano ya Olimpiki

picha maktaba mwanariadha wa kimataifa John Stephen Akhwari akiwa ameshika baadhi za medali alizoshinda kipindi alipokuwa akikimbia akishiriki mbio mbalimbali

WAZIRI MKUU AWATANGAZIA NEEMA WAKULIMA WA KOROSHO

$
0
0

*Asisitiza kwamba madai yote kumalizwa ndani ya mwaka huu wa fedha 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa kuwa Serikali italipa fedha hizo ambazo ni zaidi ya bilioni 20 mwaka huu. 

Amesema wakulima ambao bado hawajalipwa au kumaliziwa malipo yao baada ya Serikali kumaliza uhakiki majina yao yatapelekwa TADB kwa ajili ya malipo. 

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Juni 1, 2019) katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Lindi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa. 

“Wakulima wote wanaodai malipo yao ya korosho watalipwa katika mwaka huu wa fedha kwa kuwa ni haki yao na kwamba Serikali haitodhulumu haki ya mkulima yeyote.” 

Kadhalika, Waziri Mkuu amesisitiza suala la uboreshwaji wa miundombinu mbalimbali ya kutolea huduma zikiwemo barabara ili ziweze kupitika kwa urahisi wakati wote. 

Amesema uboreshwaji wa mbiundombinu pamoja na huduma nyingine za jamii ni jukumu la watendaji, hivyo wahakikishe wananchi wote wanahudumiwa bila ya kubaguliwa. 

“Kila aliyepewa jukumu ahakikishe analitekeleza ipasavyo. Watendaji hakikisheni mnawatumikia Watanzania wote vizuri, kusiwe na ubaguzi wa kisiasa, kidini na kikabila.” 

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amesema zoezi la malipo ya fedha za korosho zilizohakikiwa linaendele. 

Amesema hadi Mei 31 mwaka huu kilo 51,990,999.97 zenye thamani ya sh. bilioni 171,570,299,912 ambazo ni sawa na asilimia 87.6 zimeshalipwa kwa wakulima husika. 

Mkuu huyo wa mkoa amesema kiasi cha bilioni 23,404,086,508 bado hazijalipwa kwa wakulima wa korosho wa mkoa wa Lindi. Korosho hizo zilihakikiwa kituo cha Mtwara. 

Kikao hicho kimehudhuriwa na wabunge wa mkoa wa Lindi, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa pamoja na Wakuu wa Idara.

UBALOZI MDOGO WA CHINA WATOA MSAADA KWA WATOTO

$
0
0
Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Mama Liu Jie akikabidhi kopo la Maziwa ikiwa ni moja ya msaada aliotoa kwa watoto yatima wanalelewa katika nyumba ya Serekali iliyopo Mazizini Mjini Zanzibar. Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico na Mke wa Balozi Mdogo wa China Mama Liu Jie katika picha ya pamoja na watoto yatima.Picha na Makame Mshenga. 
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico (kushoto) akiwa na Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Mama Liu Jie wakitembelea nyumba ya kulelea watoto yatima Mazizini alipofika kutoa misaada ya vitu mbalimbali. Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Mama Liu Jie akizungumza na watoto yatima wanaolelewa kwenye nyumba ya serekali iliopo Mazizini alipofika kutoa msaada wa vitu mbalimbali, ikiwa ni miongoni mwa shamrashara za kuelekea siku ya watoto wa Afrika zitakazoazimishwa juni 16. 
……………………. 
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 01.05.2015 
Ubalozi mdogo wa China ulipo Zanzibar umekabidhi msaada wa Chakula na Vifaa mbalimbali kwa Watoto wanaoishi nyumba ya kulelea Watoto Mazizini ikiwa ni mwendelezo wa kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia wa muda mrefu katika ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa China. 
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Mabegi ya Shule, Kalamu, Madafatari, Mipira ya kuchezea, Maziwa, Sabuni na Manukato ili visaidie kuwafariji Watoto hao kuelekea siku kuu ya Idd na maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika. 

Akikabidhi Msaada huo kwa niaba ya Ubalozi wa China Mke wa Balozi wa China Mama Liu Jie amesema nchi rafiki wa China zimeongezeka duniani lakini kamwe China haiwezi kuisahau Tanzania ambayo imekuwa rafiki wa muda mrefu. 

Amesema China itaendeleza uaminifu wake wa kisiasa na Tanzania na kushirikiana katika nyanja za kiuchumi na biashara. 
Mama Lui ameongeza kuwa China itazidisha nguvu ya misaada kwa Tanzania kwa lengo la kuwasaidia wananchi wake kuishi kwa furaha na amani. 

“Miaka ya 1970 ambapo uchumi wa China ulikuwa mdogo tuliweza kusaidia kujenga Reli ya TAZARA, hivyo tutaendelea kusaidia mambo mengine muhimu katika kipindi hiki ambapo uchumi wa China umekuwa na kuwa Taifa la Pili duniani kiuchumi.” Alisema Mama Lui. 

Kwa upande wake Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Moudline Cyrus Castiko ameishukuru China kwa kuendelea kuisadia Tanzania katika Nyanja mbali mali za kimaendeleo. 

Amesema Watoto ni nguvu kubwa ya kujenga Makabila na Taifa hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuwasaidia ili kutimiza malengo yao. 
Amempongeza Mke wa Balozi huyo wa China kwa misaada mbali mbali anayoitoa kwa Watoto ambapo mwaka 2017 akiwa na Mke wa Rais Shein waliletea Vyakula, Vifaa vya kusomea na kupima afya za Watoto kituoni hapo. 

Waziri Castiko ametoa wito kwa jamii kutoa misaada ya mahitaji kwa Watoto wanolelewa katika kituo hicho cha Mazizi ili kuwafariji. 
“Kila mtu anahitaji kuguswa na watoto hawa ambao hawana Wazazi na wito wangu anayetaka kuwasaidia aje kituoni ili awasaidie, kwa wale wasio na uwezo hata kuwapa Mayatima hawa maneno ya faraja ni msaada mkubwa kwao” aliongeza Mama Castiko. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa amesema kituo hicho cha kulelea Watoto kwa sasa kina jumla ya Watoto 30 ambapo kati yao 16 ni Wasichana na 14 ni Wavulana. Amesema Watoto hao wanahitaji kupendwa na kutiwa moyo ili watakapokuwa watu wazima nao waweze kuwa na upendo wa kuihudumia wenzao na nchi kwa ujumla. 

Urafiki wa Jamhuri ya Watu wa China na Tanzania una historia ndefu inayoimarishwa kila leo ambapo huu ni mwaka wa 55 tangu nchi hizo zianzishe uhusiano wa kidiplomasia.

RAIS MSTAAFU MWINYI AKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA MASHINDANO YA KUHIFADHI KURANI KIKWAJUNI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimkabidhi zawadi Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Kurani, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi.Mashindano hayo yamefanyika leo katika Viwanja vya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mjiini, Twalib Ali Twalib akikabidhi msaada wa vitabu vitakavyoenda katika madrasa mbalimbali Visiwani Zanzibar kwa Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Kurani, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, wakati wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani yaliyofanyika leo Visiwani Zanzibar.Wakwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni na anayefuatia ni Mwakilishi wa jimbo hilo, Salehe Nassor Jazzera

Mshindi wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Juzuu Kumi na Tano, Abdallah Hassan, akibeba zawadi ya televisheni aliyokabidhiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi (watatu kushoto), wakati wa fainali za mashindano yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mapinduzi, Visiwani Zanzibar.Wakwanza ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, akimkabidhi zawadi Mshindi wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Juzuu Tano, Asia Abdallah wakati wa fainali za mashindano hayo yaliyofanyika leo, katika Viwanja vya Mapinduzi, Visiwani Zanzibar.Wakwanza ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.
Mshiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani katika Jimbo la Kikwajuni, Thureiya Abdallah akisoma Kurani wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.

HALMASHAURI YA ILALA WAZINDUA WIKI YA MAZINGIRA,YAHIMIZA WANANCHI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau wa mazingira wakiwemo FORUMCC wamezindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Mazingira.

Wakati wa uzinduzi huo viongozi wa Halmashauri hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wamehimiza wananchi wote kuendelea kuuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha mazingira yanakuwa safi wakati wote.

Akizungumza kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mjema amesema kuna kila sababu kila mmoja wetu kuungana na Serikali katika kukomesha matumizi ya mifuko ya Plastiki na kufafanua katika wiki hii ya mazingira kutafanyika kampeni ya nguvu ya kuhamasisha utunzaji mazingira.

"Ilala tumejipanga na tutaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha usafi wa mazingira inaendelea kuwa kipaumbele chetu.Tukatae mifuko ya Plastiki,tukae uchafu,"amesema Mjema.

Kwa upende wake Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Rebecca Muna amesema kupitia Mradi wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya(EU) wataendelea kushirikiana na Ilala na Serikali kwa ujumla kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na changamoto za kimazingira

"Hii ni wiki ya mazingira,hivyo sisi FORUMCC chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya tumekuwa na mradi wa mabadiliko ya tabianchi na mazingira.Tumekuwa tukifanya kazi na Serikali na kwa Dar es Salaam tunashirikiana na Ilala na kwa kweli zinakwenda vizuri.

"FORUMCC tunaridhishwa na namna ambavyo viongozi wa Serikali ya Tanzania ambavyo nimejipanga na wako mstari wa mbele katika suala la mazingira na Tabianchi.Tunafahamu Serikali imepiga marufuku mifuko ya plastiki,nasi ni wajibu wetu kuunga mkono,"amesema.

Awali wakati anamkaribisha Mkuu wa Wilaya kuzungumza na wadau wa mazingira,Kaimu Meya wa Ilala Omar Kumbilamoto ametumia nafasi hiyo kueleza wanatambua mchango wa wadau hao kwani wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha Ilala inakuwa safi.

Hata hivyo amesema kupitia kikao kilichoitishwa na FORUMCC kwa kushirikiana na Ilala kuna mambo kadhaa ambayo yamejitokeza kwa upende wa wakandarasi wa kuzoa taka ,hivyo watakutana nao kujadiliana kwa kina na hatimaye kuondoa changamoto zilizoko.

"Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,mazingira safi katika wilaya yetu ni kutokana na wadau wa mazingira tulionao ambao wanafanya kazi kubwa sana.Hata hivyo kilio chao ni muda uliowekwa kwenye mkataba wa uzoaji taka.Wamewekewa mwaka mmoja mmoja wakati zamani ilikuwa miaka mitatu,tutakaa tuone tunafanyaje,"amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema akiwa amebeba kikapu ikiwa ni ishara kwa wananchi kutumia mfuko mbadala baada ya kuanza kutekelezwa kwa sheria ambayo imezuia matumizi ya mifuko ya plastiki.Mjema alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira inayoanza leo na kumaliza Juni 5,mwaka huu
Kaimu Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Omari Kumbilamoto (aliyesimama)akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema(wa kwanza kulia)akiwa anasikiliza jambo kwa umakini wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira.Wengine walioko waliokuwa naye ni viongozi wa Wilaya ya Ilala
Viongozi wa Wilaya ya Ilala wakiwa pamoja na wadau wa mazingira wakiwa wenye picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Rebecca Muna(wa kwanza kushoto)akiwa na mwanamuziki wa Singeli Msaga Sumu wakipata burudani.
Wadau wa mazingira wakiburudika kwa nyimbo za Singeli wakati Mwanamuziki Msaga Sumu akitumbuiza.
Wasanii wa FORUMCC wakitoa  burudani kwa wadau wa mazingira

ATHARI ZA MAFURIKO KYELA WANANCHI WAITAKA SERIKALI IWATAFUTIE MAENEO.

$
0
0
Wananchi wa Kata sita zilizokumbwa na mafuriko Wilayani Kyela, wameiomba serikali kuwatafutia maeneo mapya ya makazi.

Wamesema, kutokana na Kata hizo kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hasa nyakati za misimu ya mvua, wameona kuna haja ya wao kuondoka na kwenda kuishi kwenye maeneo ya miinuko.

Ombi hilo, wamelitoa leo wakati wakizungumza na mwandishi wa Michuzi Blog, alipotembelea eneo hilo na kushuhudia uharibifu wa mali za watu na mazingira uliosababishwa na mafuriko hayo.Baadhi ya Kata zilizokumbwa na mafuriko hayo ni Kata ya Ikama, Kajunjumale, Katumbasomgwe na Talatala.

Akizungumzia hilo, baadhi ya watu waliokumbwa na kadhia hiyo, Elia Mwakipesile na Kasutu Mwambandile, wamesema hali ilivyo sasa wapo tayari kuyahama maeneo hayo ya mabondeni lakini wanaiomba serikali kuwatafutia maeneo mengine rafiki.

Hata hivyo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, imetembelea eneo hilo na kutoa pole ya shilingi miloni moja na kusisitiza kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuachana na tabia ya kujenga mabondeni.

"Suala la kuhamisha watu waliojenga mabondeni halijawahi kuwa jambo rahisi sana, mtakumbuka majanga yaliyotokea jangwani ilibidi hadi nyumba zivunjwe kwahiyo hata huku lazima elimu itolowe, ” amesema.

Jumla ya watu sita wanasadikiwa kupoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za April 29 na Mei 11 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya (Kulia) Mh Albert Chalamila akimkabidhi Fedha kiasi cha Shilingi Mil 1 ili Mkuu wa Wilaya ya Kyela Cloudia Kitta ili kusaidia katika uboreshaji wa Miundombinu ya barabara ambayo imeathirika na Mafuriko
Eneo la Mashamba ya Mapunga kijjiji Cha Bujonde Kata Kajunjumele ambayo yaliathiriwa kwa kiasi kikubwa na mafuriko yaliyotokana na Mvua zilizotokea April 29 na Mei 11 Mwaka huu.
Mzee Elia Mwakipesile Mkazi wa Kijiji cha Bujonde Wilaya ya Kyela ambaye ni mmoja wa waathirika wa mafuriko yaliyotokea April 29 na Mei 11 Mwaka na Kusababisha Vifo vya watu 6
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images