Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI


SERIKALI ZANZIBAR YAWABAINI WAVAMIZI WA SHAMBA LA MAREHEMU BINTI KANGETA

$
0
0
Timu ya Viongozi Watendaji Wakuu wa Wilaya ya Kati ikiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar inakamilisha uchunguzi wa kuwabaini Watu waliohusika na uvamizi wa Shamba la Marehemu Binti Kangeta ambae amefariki Dunia akiwa hana mrithi.

Wakati Shamba hilo liliopo Shehia ya Ghana Wilaya ya Kati kwa sasa linatumiwa na Wananchi wa maeneo hayo kwa shughuli za Kilimo wakijitokeza Watu waliovamia Shamba hilo kinyume na Sheria na Taratibu za Serikali wakiwaonya Wananchi hao kuondoka katika maeneo hayo wakidai wameshamilikishwa Shamba hilo kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Mkuu wa Wilaya ya Kati Bibi Hamida Mussa Khamis aliwaeleza Wananchi wa Maeneo hayo kwamba sheria za Ardhi zilizopo Nchini ziko wazi zikielezea kwamba mmiliki wa shamba lolote akiwa hana mrithi anapofariki Dunia umiliki wake hurejea Serikalini.

Bibi Hamida aliweka wazi kwamba kwa sasa Shamba hilo licha ya kwamba Wananchi hao wanaendelea na shughuli zao za Kilimo lakini umiliki wake uko chini ya Serikali Kuu.

Alionya kwamba Serikali haitasita kumchukulia hatua za Kisheria Mtu au Kikundi chochote chenye nia ya kutaka kujimilikisha Shamba hilo kinyume na Taratibu jambo ambalo likiachiliwa kuendelea linaweza kuleta mgogoro unaoweza kuepukwa mapema.

Bibi Hamida alifahamisha kwamba Mtu yoyote anayetaka kutumia shamba hilo hawezi kujimilikisha mwenye binafsi bali anawajibika kufuata Taratibu kwa kuandika maombi na kupelekea Serikalini yatakayofikia hatua ya kupata ithibati kamili juu ya matumizi ya Shamba hilo.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed alionya kwamba Wizara haitosika kumsimamisha Kazi na hatimae kumfukuza Kazi mara moja Mfanyakazi ye yote atakayebainika kujihusika na migogoro ya Ardhi.

Nd. Shaaban Seif aliwathibitishia Wananchi hao kwamba hakuna Kiongozi ye yote wa Ofisi hiyo inayosimamia shughuli za Serikali anayeweza kutoa kibali au ruhusa ya Matumizi ya Shamba au Ardhi wakati Wizara inayosimamia jukumu hilo ipo kwa mujibu wa Sheria na Taratibu za Nchi.

Katibu Mkuu Shaaban alimtahadharisha Sheha wa Shehia ya Ghana kuwa makini na baadhi ya Matapeli wenye tabia ya kuwatisha Wananchi Mitaani kwa visingizio vya kuwa wako karibu na Wakubwa wenye madaraka ya juu Serikalini.

Kwa upande Wao Wanachi wanaolima katika Shamba hilo wameelezea faraja yao kutokana na ujio wa Timu hiyo ya Viongozi Watendaji Wakuu wa Wilaya ya Kati ikiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kufuatilia tatizo hilo.

Walisema faraja yao imekuja kufuatia dalili ya kuzimwa kwa vitisho la Watu waliojifanya kupewa umiliki wa Shamba hilo ambao tayari walikuwa wameshaanza harakati za kuweka mipaka huku wakiwaonya Wananchi hao kuacha kulima mara moja ndani ya shamba hilo
 Timu ya Viongozi Watendaji Wakuu wa Wilaya ya Kati ikiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiangalia Shamba la Marehemu Binti Kangeta ambae amefariki Dunia akiwa hana mrithi liliopo Kijiji cha Ghana Wilaya ya Kati.
 Baadhi ya Wakulima wa Kijiji cha Ghana wanaolima katika Shamba la Marehemu Binti Kangeta lililovamiwa na Watu wasiojuilikana na kuamuru Wakulima hao waache kulima mara moja.
 Mkuu wa Wilaya ya Kati Bibi Hamida Mussa Khamis akiwaeleza Wananchi wa Ghana sheria za Ardhi zilizopo Nchini ziko wazi zikielezea mmiliki wa shamba lolote akiwa hana mrithi anapofariki Dunia umiliki wake hurejea Serikalini.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed akitoa onyo kwa kumsimamisha Kazi na hatimae kumfukuza Kazi mara moja Mfanyakazi ye yote atakayebainika kujihusika na migogoro ya Ardhi.
 Bibi Tatu Mohamed Seif akishukuru kwa niaba ya Wakulima wenzake ujio wa Timu ya Viongozi hao iliyoleta faraja kwao kujenga matumaini ya kuendelea kulima katika shamba la Marehemu Bibi Kangeta huko Ghana.

Baadhi ya maeneo ya Shamba la Marehemu Bibi Kangeta liliopo Kijiji cha Ghana Wilaya ya Kati lililovamiwa na Watu Matapeli wanaotaka Wakulima wa eneo hilo waondoke. Picha na – OMPR – ZNZ.


ASKARI POLISI AELEZA NAMNA ALIVYOPIGWA JIWE WAKATI AKIZUIA MAANDAMANO YA WAFUASI WA CHADEMA

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

ASKARI Polisi namba H 7856  PC Fikiri Mgeta (28), ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alilazwa siku tatu katika Hospitali ya Polisi Kilwa road, baada ya kupigwa jiwe kichwani wakati akizuia wa maandamano ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mgeta anayefanya kazi Kituo cha Polisi Oysterbay anakuwa shahidi wa nne katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi hao akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Jacqueline Nyantori, shahidi huyo akiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amedai kuwa alipigwa na jiwe kichwani pamoja na mkononi ambayo yalimuumiza na kusababisha kutoka damu nyingi.

Mgeta amedai kuwa tukio hilo lilitokea Februari 16, mwaka jana wakati walipokwenda kutuliza waandamanaji waliokuwa wamebeba mawe, chupa na fimbo eneo la Mkwajuni wilaya ya Kinondoni.

Shahidi huyo amedai kuwa chanzo cha kupigwa na mawe ni baada ya waandamanaji hao wakiongozwa na Mbowe kutotii ilani iliyotolewa na Ofisa Operesheni wa Polisi  sambamba na mabomu ya machozi yaliyopigwa.

"Afande Ngiichi aliagiza mabomu yatumike kutuliza waandamanaji lakini muitikio ulikuwa hasi kwani waliendelea kusonga mbele kuwafuata askari huku wakiimba na kurusha mawe," amedai Mgeta.

Shahidi huyo alidai mawe yalirushwa zaidi upande wa askari na ndipo mmoja wa askari Koplo Rahimu alipigwa na jiwe  na kuanguka chini huku akidai kuwa baada ya kuanguka alilalamika  ameumizwa upande wa shingo na kupoteza fahamu.

"Afande alitoa amri tumsaidie mwenzetu hivyo nikiwa katika kumsaidia nilipigwa na jiwe  mkono wa kulia na nilipoteza saa, nikiwa katika hamaki nilipigwa tena na jiwe kichwani ambalo liliniumiza hadi nilisikia kizunguzungu," alieleza.

Pia amedai kuwa hakuweza kuendelea na kazi yake kwani alichukuliwa na askari mwenzake na kumpeleka kwenye gari  na kupelekwa hospitali ya Polisi Kilwa Road kwa ajili ya matibabu zaidi.

Mgeta amedai kuwa alifika hospitalini hapo majira ya saa 1 kwenda saa 2 usiku akiwa na fomu namba tatu ya polisi (PF 3), na kuanza kupatiwa huduma ya kwanza.

Mgeta ameieleza mahakama kuwa alilazwa hospitalini hapo kwa siku tatu kuanzia Februari 16 hadi 18, mwaka jana ndipo saa 10 jioni ya siku hiyo daktari alimruhusu kwenda mapumziko ya wiki mbili nyumbani.

Hata hivyo, shahidi ameiomba mahakama kupokea PF3 hiyo ili itumike kama kielelezo na upande wa utetezi haukuwa na pingamizi.

Akielezea tukio hilo, Mgeta amedai kuwa aliajiriwa na Jeshi la Polisi mwaka 2015 baada ya kupata mafunzo kutoka Chuo cha Polisi Moshi.

Amedai siku ya tukio alipangiwa kufanya doria eneo la Mwananyamala na majira ya jioni walipewa taarifa na kiongozi wao kuwa kuna mkusanyiko wa watu unaoashiria uvunjifu wa amani.

"Tuliitikia wito na tukaelekea tulipoelekezwa eneo la Mkwajuni ambako tulikuta viongozi na wafuasi wa Chadema wakiwa zaidi ya 500 wamefunga barabara huku wakiwa na uhamasishaji kwa njia ya nyimbo hali iliyoashiria kuvunja amani," alidai Mgeta.

Shahidi huyo amedai kuwa wakiwa wanatumia gari la Polisi walipita kwa shida katikati ya maandamano hayo na walikuta ilani inatamkwa huku ikitaja jina la Rais John Magufuli.

Mgeta  amedai  kuwa mkusanyiko huo ukiongozwa na viongozi wa Chadema ambao alidai wengine anawafahamu kwa majina na sura huku wengine akiwafahamu kwa sura pekee,  haukutii amri iliyokuwa inatolewa.

shahidi huyo amedai kuwa aliwatambua baadhi ya viongozi hao kupitia kwenye shughuli mbalimbali za kisiasa ikiwemo kampeni na Bungeni.

Mgeta  amedai kuwa viongozi hao waliendelea kuhamasisha kwa ishara ya mikono kwa kuwahimiza wafuasi wasonge mbele kuwafuata askari na walikuwa wakirusha mawe.

Mbali ya Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa, Dk Vincent Mashinji ,  Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,  Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji,  Mbunge wa Kawe,  Halima Mdee,  Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda,  Ester Bulaya.

ELIMU YA UFUNDI NI NYENZO KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA-NAIBU WAZIRI OLE NASHA

$
0
0

Mwenyekiti wa baraza la elimu ya Ufundi NACTE John Kondoro, kulia akimuelekeza jambo Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha katikati, wakati akiwasili kabla ya kufungwa kwa maonyesho hayo leo, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Averina Semakafu.
Mhadhiri wa chuo cha College of Agriculture and Natural Resources, Deodatus Tibenda akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha, juu ya shughuri zinazofanywa na chuo hicho kabla ya kufungwa kwa maadhimisho hayo leo Jijini Dodoma.
Baadhi ya wawakilishi wa Taasisi mbalimbali wakiwa katika hafla ya kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Elimu ya Ufundi NACTE Adolph Rutayuga akizungumza wakati wa hafla ya kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi NACTE, John Kandoro, akizungumza wakati wa hafla ya kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi a Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha, akizungumza wakati wa hafla ya kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, akiwapungia mikono wadau wa maonyesho ya Elimu ya Ufundi, wakati wa hafla ya kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wadau na wamiliki wa taasisi zilizoshiriki katika maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma.

..................

Na.Mwaandishi wetu,Dodoma

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha, amesema elimu ya ufundi ni muhimu katika maendeleo, kwa sababu inakuza taaluma hasa kipindi hiki cha kutengeneza uchumi wa Viwanda.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akifunga maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yaliyofanyika uwanja wa Jamhuri Dodoma yenye lengo la kukutanisha taasisi zote zilizochini ya NACTE.

Amesema kama Elimu ya Ufundi itasimamiwa kikamilifu italeta tija hasa kipindi hiki tunajenga uchumi wa viwanda, kwa sababu elimu ya ufundi inasaidia kukuza wataalamu ambao watasaidia katika viwanda.

Aidha amefurahishwa katika maonyesho hayo kuona vijana ambao ni mazao ya vyuo vya ufundi wakiwa na bidhaa mbalimbali ambazo wamezitengeneza wenyewe na kujiajiri kupitia elimu ya ufundi.

“Ndugu zangu nimepita kwenye mabanda humo nimeona vijana ambao wametoka katika vyuo hivi na wamejiajiri na wanafanya kazi nzuri sana, hii elimu ya ufundi ni muhimu sana inazalisha wataalumu ambao watatusaidia katika viwanda na Nyanja mbalimbali tunapojenga uchumi wa viwanda” amesema Ole Nasha.

Aidha amesema serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wadau wa sekta binafsi ambao wanamalengo ya kuleta mabadiliko kwa nchi hasa kipindi hiki cha ujenzi wa viwanda serikili itakuwa bega kwa bega kuwaunga mkono kuhakikisha sekta hizo zinasongambele.

Amesema serikali inathamini sana uwekezaji wa sekta binafsi kwa sababu zinamchango mkubwa sana na hasa katika kuinua elimu katika Nyanja mbalimbali hapa nchini.

“Ukiangalia hapa nchini kuna vyuo vya ufundi mia t
ano arobaini(540) na vyuo binafsi ni mia tatu kumi na tisa(319) vyote hivi ni vyuo vya watu binafsi vya serikali ni kama mia mbili tu na kidogo, unaona sasa sekta binafsi ilivyo na mchango mkubwa” amesema Ole Nasha.

Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa baraza la Elimu ya Ufundi nchini NACTE Adolph Rutayuga, amesema maonyesho hayo yalikuwa na mafanikio makubwa, na wamedhamilia kuyafanya kuwa endelevu na baraza litaendelea kuyaboresha ili kuwa bora zaidi.

Amesema lengo la maadhimisho hayo ni kukuza taasisi hizo na kubadilishana uzoefu miongoni mwa taasisi hizo, na ni fulsa kwa wanafunzi wa taasisi hizo kujiajiri na kubainisha kuwa miongoni mwa waliokuwa wakitoa maelezo katika mabanda hayo ni wanafunzi wa taasisi hizo.

“Mheshimiwa maadhimisho hayo yamekuwa ya mafanikio sana na ili kuboresha zaidi kutekubaliana yawe ya kila mwaka angalau mara moja kuzikutanisha taasisi hizi kukutana kwa pamoja,na tumedhamilia katika maadhimisho yajayo kuongeza taasisi nyingi zaidi katika maonyesho haya” amesema Rutayuga.

Maadhimisho haya yalianza tarehe 27 mwezi huu nayamefungwa rasmi leo ambapo yamedumu kwa siku tano yaliyokuwa na lengo la kukutanisha taasisi zote zilizopo chini ya NACTE ili kuzitangaza taasisi hizo na maonyesho yalibebwa na kauli mbiu isemayo, “Elimu ya Ufundi na Mafunzo kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda Tanzania”.

Job Announcement at the African Commission for Nuclear Energy

$
0
0
Dodoma, 31 Mei 2019


Job Announcement at the African Commission for Nuclear Energy
The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the African Commission for Nuclear Energy (AFCONE) inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Desk Officer available at the AFCONE.


For more details and application instructions, candidates are advised to visit:https://www.pnet.co.za/cmp/en/African-Commission-on-Nuclear-Energy-AFCONE-27508/work.html.


Application deadline is 16th June 2019.


Issued by;

Government Communication Unit,

Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation


Waziri Biteko ashuhudia makabidhiano ya dhahabu iliyokamatwa Mwanza

$
0
0
Na GB Pazzo, BMG

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameshuhudia makabidhiano ya mali ikiwemo dhahabu iliyokamatwa katika Wilaya Sengerema mkoani Mwanza, ikisafirishwa kinyume na sheria baada ya kutaifishwa na mahakama kuwa mali ya Serikali.


Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 31, 2019 jijini Mwanza baina ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango aliyewakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Khatibu Kazungu.


Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Biteko amewasihi wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuachana na utoroshaji wa madini kwani biashara hiyo kwa sasa ni zilipendwa hivyo wafanye shughuli zao kwa kuzingatia sheria.


Naye DPP Biswalo Mganga amesema mali zilizotaifishwa ni dhahamu kilo 319 yenye thamani ya shilingi bilioni 27.018, fedha taslimu shilingi 305, mzani wa kupimia ubora wa madini, mizani ya kupimia madini pamoja na magari mawili ambapo vyote kwa pamoja vilikamatwa mwezi januari mwaka huu wilayani Sengerema. Aidha ameongeza kwamba dhahabu kilo tano iliyokamatwa mkoani Geita nayo imekabidhiwa serikalini baada ya kutaifishwa pia.


Baada ya kupokea mali hizo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Khatibu Kazungu ametoa shukrani kwa mamlaka zote zilizofanikisha kukamatwa, kutoa ushahidi na kutaifishwa na kwamba zitatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Madini, Khatibu Kazungu (wa kwanza kulia) wakishuhudia vipimo vya madini yaliyokamatwa wilayani Sengerema kabla ya kufanya makabidhiano.
Makabidhiano ya mali hizo yamefanyika leo jijini Mwanza na kushuhudiwa pia na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Madini yaliyokamatwa yakipimwa kabla ya makabidhiano kufanyika, hatua hii inajiri maada ya mahakama kutaifisha madini hayo.
Watuhumiwa 12 wakiwemo wenye mali wanne na askari polisi wanane walikamatwa wakihusishwa kuhusika na utoroshaji wa madini hayo wilayani Sengerema ambapo wenye mali walipatikana na hatia na kuhukumiwa huku askari polisi wakikana mashtaka dhidi yao ambapo bado kesi yao inaendelea mahakamani.
Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Madini, Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella wakishuhudiano vipimo vya madini hayo kabla ya kufanyika makabidhiano.
Viongozi mbalimbali wakishuhudia makabidhiano ya madini hayo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

Tigo yazindua ofa ya ‘Saizi Yako’ inayokidhi mahitaji ya kila mteja

$
0
0

    Afisa Biashara Mkuu wa kampuni ya Tigo Tarik Boudiaf(kati kati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa mpya inayojulikana kama ‘Saizi Yako‘ uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo, Idara ya Huduma za Masoko William Mpinga na kulia ni Balozi wa kampeni hiyo Lucas Muhavile maarufu kama Joti.

    Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko wa kampuni ya Tigo William Mpinga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa mpya inayojulikana kama ‘Saizi Yako‘ uliofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Afisa Biashara Mkuu Tigo Tarik Boudiaf akifuatiwa na Balozi wa kampeni hiyo Lucas Muhavile maarufu kama Joti

  Balozi wa Kampeni mpya ya Tigo inayojulikana kama ‘Saizi Yako’ Lucas Muhavile maarufu kama ‘Joti’ akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Afisa Biashara Mkuu Tigo Tarik Boudiaf na William Mpinga ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko wa kampuni hiyo.

Afisa Biashara Mkuu wa kampuni ya Tigo Tarik Boudiaf(kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mchekeshaji Lucas Muhavile maarufu kama Joti (kati kati) Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko wa kampuni ya Tigo William Mpinga muda mfupi baada ya uzinduzi wa ofa mpya inayojulikana kama ‘Saizi Yako‘ uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Wateja wa Tigo sasa wana kila sababu ya kufurahi baada ya uzinduzi wa ofa mpya ya ‘Saizi Yako’ inayolenga kuwapatia huduma za intaneti, muda wa maongezi na SMS kutokana na mahitaji mahususi ya kila mteja kwa gharama nafuu.

Ofa hii ya ‘Saizi Yako’ ni ya kipekee sana kwa sababu inawapatia wateja ambazo ni mahususi kwa kila mteja hivyo kuwaridhisha wateja wa sasa na wa baadaye wakiangalia gharama wanayoitumia kulinganisha na huduma wanayoipata. Ofa hii pia inapatikana kupitia menyu iliyorahisishwa ili wateja waweze kuipata na kuinunua kwa urahisi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa ofa hii kutoka makao makuu ya Tigo, Dar es Salaam, Afisa Biashara Mkuu wa Tigo, Tarik Boudiaf, alisema kwamba lengo la kampuni hiyo ni kutoa ofa bora, zenye mahitaji yote ya mteja sehemu moja, kwa gharama nafuu, na zitakazo kidhi mapendekezo na mahitaji ya wateja wao.

“Tumezingatia tabia, mahitaji na mienendo ya wateja wetu kwa miaka mingi sasa. Na kinachotufanya tuwe wabunifu ni kwamba tunatambua kwamba kila mteja wetu ni wa kipekee. Hivyo, tumeamua kubuni ofa hii ya ‘Saizi Yako’ ambayo ina mahitaji yote ya mteja sehemu moja na inayozingatia mahitaji yao mahususi. Sasa tunatoa fursa kwa wateja wetu kuweza kupata ofa za kipekee kwa kuzingatia matumizi yao ya kila siku na kwa gharama nafuu,” alisema Boudiaf.

Boudiaf pia alieleza kwamba, kama mteja anatumia muda wa maongezi zaidi kuliko intaneti na SMS, basi atapata kifurushi bora cha muda wa maongezi. Na mteja akitumia zaidi intanet kuliko muda wa maongezi na SMS, mteja huyo atazawadiwa kifurushi bora cha intanet. Utaratibu huo huo utafuatwa pia kwa ajili ya SMS.

“Tunaamini kwamba ‘Saizi Yako’ itaendana na mahitaji, bajeti na maisha ya wateja wetu. Kuwapatia ofa ambayo wataweza kupata kila wanachohitaji sehemu moja, kwa ajili yao, pia inamaanisha kwamba, sisi kama Tigo, tunatambua na kufanyia kazi mahitaji ya wateja wetu yanayobadilika kila siku. Uelewa wetu wa wateja pia unajenga mahusiano yetu nao na kuwafanya watuthamini zaidi,” aliongeza Boudiaf.

Kufurahia ofa maalumu ya ‘Saizi Yako’, wateja wanaweza wakapiga *147*00# au *148*00# kwa urahisi na kuchagua ‘Saizi Yako’. Ofa hii pia itapatakina katika Tigo Pesa APP hivi karibuni. 

JAFO AFURAHISHWA UJENZI MIRADI YA KIMKAKATI HALMASHAURI YA MJI NJOMBE, WAKANDARASI WALIA NA MSAMAHA WA VAT.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Salum Hamdun,Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Wataalamu Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Mji Njombe wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko la kisasa katika Halmashauri Ya Mji Njombe
Mhandisi anayesimamia ujenzi wa soko la kisasa Njombe Justin Mboka akiwa ameambatana na Waziri Jafo wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa soko la kisasa katika Halmashauri ya Mji Njombe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akitoa maelekezo wakati alipokagua shughuli za uendeshaji stendi mpya Njombe.
Ujenzi wa soko la Kisasa ukiendela katika Mtaa wa Kwivaha Halmashauri ya Mji Njombe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akiwa anazungumza na wasafiri na wadau wa usafirishaji waliokuwepo katika stendi kuu mpya Njombe
Mratibu wa Mradi wa ujenzi wa stendi Mhandisi Damasco Tembo wa (kwanza kushoto) akitoa maelezo ya shughuli zilizosalia za ujenzi wa stendi mpya ya mabasi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo wakati alipokagua stendi hiyo.Kulia kwa Jafo ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri akifuatiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri Illuminatha Mwenda
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza na Mama Lishe(hawapo pichani ) wanaofanya biashara zao katika eneo la stendi mpya ya Njombe
Mhandisi anayesimamia ujenzi wa soko la kisasa Njombe Justin Mboka akimuonesha Waziri Jafo matenki yaliyochimbwa ardhini kwa ajili ya kuifadhi maji yatakayovunwa katika eneo la soko.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya stendi na ujenzi wa soko.Nyuma ya Mkurugenzi ni Mwenyekiti wa Halmashauri Edwin Mwanzinga



******************************************

Hyasinta Kissima- Afisa Habari H/Mji Njombe.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo ameonyesha kufurahishwa na ujenzi wa soko la kisasa katika Halmashauri ya Mji Njombe ujenzi ambao unatarajiwa kukamilika ifikapo octoba 2019 na kugharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.9.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kuona shughuli za ujenzi zinazoendelea katika soko hilo Jafo amesema kuwa licha ya kuwepo na ujenzi wa miradi ya masoko katika Mikoa ya Mtwara, Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam ujenzi wa soko la Njombe ni wa kipekee na wenye viwango vya hali ya juu na kufurahishwa na namna Halmashauri ilivyoweza kuwashirikisha wafanyabiashara katika kila hatua za ujenzi na kutoa ushauri wao na kwa jinsi Halmashauri ilivyoweza kubuni na kutenga eneo kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua ambayo yatakuwa yakihudumia eneo lote la soko jambo ambalo limekuwa halitekelezwi kwenye miradi mingi.

“Mimi huwa nakuja kukagua kazi sio kutembelea. Binafsi nimeridhishwa na kufurahishwa sana na ujenzi unaoendelea wa soko. Hiki ni kitega uchumi kikubwa sana kwa Halmashauri na kitabadili mandhari ya Mji wa Njombe. Katika Kanda ya Nyanda za juu kusini soko hili litakuwa la kipekee niwapongeze mmefanya kazi nzuri na hamjanitia hasira. Mkandarasi unafanya kazi nzuri sana na ninaomba uhakikishe kuwa unamaliza kazi kwa wakati.”Alisema Jafo.

Awali akipokea taarifa ya maendeleo ya shughuli za uendeshaji wa stendi na umaliziaji wa ujenzi kutoka kwa Mratibu wa Mradi Mhandisi Damasco Tembo, Mhandisi huyo alisema kuwa kwa sasa ujenzi wa stendi hiyo umekamilika kwa asilimia 96 na unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Juni 2019 na kubainisha changamoto kubwa ya kutopatiwa kwa msamaha wa ongezeko la thamani VAT kwa Wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa soko na stendi jambo linakwamisha kukamilika kwa wakati kwa miradi hiyo.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa hiyo Jafo ameahidi kushughulikia changamoto ya msamaha wa ongezeko la thamani VAT changamoto iliyoibuliwa na wakandarasi wote wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa soko na stendi na ameitaka Halmashauri kupata suluhu ya jambo lililokwamisha uwepo wa ujenzi wa kituo cha mafuta ndani ya stendi kama ilivyokuwa kwenye mchoro wa awali.

“Lengo la miradi hii ni kwa ajili ya kukuza Miji na kuzijengea Halmashauri uwezo wa kujitegemea. Kama ramani ya stendi hii ilikua na eneo la kituo cha mafuta, na eneo limetengwa rasmi kwa ajili ya shughuli hiyo sioni sababu ya kusitisha ujenzi wa kituo hicho. Kama ni sababu za kiusalama zilizowafanya kusitisha ujenzi wa kituo hicho cha mafuta sina shaka nalo lakini kama mmesitisha kutokana na ushauri kwamba maeneo ya jirani na stendi kuna kituo cha mafuta basi Miji mingine isingekuwa na vituo vya mafuta maana kila sehemu vipo mimi nadhani hiyo ya kuwepo kwa vituo vya jirani sio hoja.’’Jafo alifafanua,

Jafo aliendelea kusema “Swala la msamaha wa VAT ni changamoto inayoikabili miradi mingi inayosimamiwa na TAMISEMI. Hapa Njombe naona tena changamoto hii inajirudia licha ya Mheshimiwa Rais kutoa maelekezo kuhusiana na suala hili. Naomba nichukue changamoto hii na nitaiwasilisha kwa Waziri wa Fedha kwa utekelezaji. Mimi nataka Halmashauri hizi zifuzu na kufikia uchumi wa kujitegemea.”Alisema

Naye Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri amemuahidi Mheshimiwa Jafo kuendelea kusimamia kwa ushirikiano shughuli zilizosalia za ujenzi na kumwambia kuwa pale patakapohitaji msaada hawatasita kuwasiliana kwa ajili ya kuhakikisha kuwa changamoto zinatatuliwa ili Wananchi wa Njombe waweze kunufaika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda amemshukuru Mheshimiwa Jafo kwa kutembelea mradi wa soko na kukagua shughuli za uendeshaji wa stendi na kuahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Waziri huyo katika ziara yake.

“Sisi tutaendelea kusimamia kazi hizi kwa nguvu zote. Tutakuwa na vikao kila wiki kuangalia hatua ya namna gani tunamaliza shughuli za soko. Kuhusu wazo la kuendelea na ujenzi wa kituo cha mabasi ndani ya stendi tutaangalia sheria, kanuni, taratibu na hali za kiusalama kama vyote vinaruhusu tuone namna ya kurejesha ule mradi katika stendi yetu mpya.”Alisema Mwenda.

Mradi wa ujenzi wa stendi unatarajiwa kuingizia Halmashauri mapato ya zaidi ya milioni mia mbili hamsini kwa mwaka huku mradi wa soko ukitarajiwa kuingiza zaidi ya milioni mia tatu kwa mwaka pindi itakapokamilika.

Waziri Hasunga aanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kuiuzia Zimbabwe mazao ya kilimo

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha dharura na Wakurugenzi wa Taasisi na Idara mbalimbali za Wizara ya Kilimo kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo katika mji wa serikali Ihumwa Jijini dodoma leo tarehe 31 Mei 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha dharura na Wakurugenzi wa Taasisi na Idara mbalimbali za Wizara ya Kilimo kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo katika mji wa serikali Ihumwa Jijini dodoma leo tarehe 31 Mei 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha dharura na Wakurugenzi wa Taasisi na Idara mbalimbali za Wizara ya Kilimo kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo katika mji wa serikali Ihumwa Jijini dodoma leo tarehe 31 Mei 2019. Wengine pichani ni Naibu Waziri Mhe Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe pamoja na na Prof Siza Tumbo, Naibu katibu Mkuu.


Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 31 Mei 2019 ameitisha kikao cha dharura na Wakurugenzi wa Taasisi na Idara mbalimbali za Wizara ya Kilimo lengo ni kuanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuiuzia nchi ya Zimbabwe mahindi na mazao mengine kiasi cha Tani Laki Nane (800,000).

Itakumbukwa mapema wiki hii, Rais John Pombe Magufuli alipoitembelea Zimbabwe kwa mwaliko wa Mwenyeji wake Rais Emmerson Mnangagwa. Rais Mnangagwa alimweleza Rais Magufuli kuwa Zimbabwe inakabiliwa na upungufu wa chakula na kuiomba Tanzania iiuzie sehemu ya chakula chake cha ziada ombi ambalo Rais Magufuli alilikubali.

Waziri Hasunga amesema ujumbe kutoka Serikali ya Zimbabwe utawasili nchini kuanzia Siku ya Jumanne ya Tarehe 3 Juni na unatajiwa kuwa nchini mpaka tarehe 7 ya Mwezi Juni, 2019.

Waziri Hasunga ameongeza kuwa ujumbe huo kutoka Zimbabwe unakuja kwa ajili ya kuangalia na kujiridhisha kuhusu mambo ya msingi kama ubora wa chakula na mambo mengine ya awali.

Waziri wa Kilimo amesema kimsingi Serikali zote mbili zimekubaliana kuwasaidia Wananchi kwa njia ya biashara na kuongeza kuwa huu ni mwanzo kwa kufanya biashara endelevu baina ya nchi hizi mbili na kuongeza kwa biashara hiyo, itakuwa endelevu mwaka hadi mwaka.

Mhe. Hasunga amesema Zimbabwe imefikiria pia kuanza kununua mazao mengine kama korosho kwa kuwa imeona fursa ya kupata mazao yenye ubora na kwa bei nzuri ipo Tanzania kwamba baadae mazao mengine ya mbegu za mafuta, jamii ya mikunde, mboga na matunda yataanza kununuliwa na Taifa hilo la Kusini mwa Afrika.

SACH YAFUTURISHA WATOTO WALIOWAHI KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO ISRAEL

$
0
0
Baadhi ya wazazi na watoto waliokuwa na magonjwa ya moyo na kutibiwa nchini Israel wakila futari iliyoandaliwa na shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (SACH) kwaajili ya watoto hao hivi karibuni katika Hotel ya Protea Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wadau walioudhuria futari iliyoandaliwa na shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (SACH) la nchini Israel kwaajili ya watoto waliofanyiwa upasuaji wa moyo na madaktari wa SACH hivi karibuni katika Hotel ya Protea Jijini Dar es Salaam.
Madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (SACH) la nchini Israel na Canada wakila futari iliyoandaliwa na SACH kwaajili ya watoto waliowahi kufanyiwa upasujai wa moyo na madaktari wa SACH hivi karibuni katika Hotel ya Protea Jijini Dar es Salaam
Madaktari kutoka shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (SACH) la nchini Israel katika picha ya pamoja na mzazi na mtoto waliyewahi kumfanyia upasuaji wa moyo miaka miwili iliyopita nchini Israel wakati wa futari iliyoandaliwa na SACH kwa ajili ya watoto waliowahi kufanyiwa upasuaji wa moyo na madaktari hao hivi karibuni katika Hotel ya Protea Jijini Dar es Salaam
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel na Canada katika picha ya pamoja na wazazi na watoto waliowahi kufanyiwa upasuaji wa moyo na madaktari hao wakati wa futari kwa ajili ya watoto hao iliyofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam.

Picha na: JKCI

MWAKIBINGA AENDA KINYUME NA KIDERA WA CHADEMA AMPIGA TAMKO ZITO

$
0
0


Ndugu Wanahabari, mimi ni Philipo Mwakibinga mwanachama wa kawaida wa CCM niliyetokea upinzani. Kama mnakumbukumbu mwaka wa jana mimi ni mmoja wa watu ambao kwa dhamira zao bila shurti tuliachana na siasa za upinzani za majitaka na ghiriba kisha kujiunga na CCM ili kupata fulsa ya kujenga taifa kwa bila ubabaishaji wowote. 

Na ikumbukwe kuwa sote tuliotoka huko hakuna hata mmoja aliyesifia upinzani bali tuliuponda na kuanika hadharani maovu ya upinzani na hasa mifumo mibovu na ombwe la uongozi ambapo hadi sasa vyama vya upinzani havijabadirika bado ni vibovu vinazidi kudorora kila kukicha.

Ndugu wanahabari, nimejitokeza kuongea nanyi baada ya kusikia taarifa iliyoandaliwa na CHADEMA kisha kutolewa na mtu anayejulikana kwa jina la KIDERA. Kidera ametoa kauli huku akiwa chini ya ulinzi wa viongozi wa CHADEMA na akiwa kama mateka wa kisiasa.

Hivyo kwa yale yote aliyoyasema nimeona nivyema na nibora sana mimi kama Mwanachama wa kawaida kabisa ndani ya CCM tena nikiwa nimetoka huko upinzani nisikae kimya na kuacha uongo, na uzushi ukatamalaki. Nasema wazi kuwa kinachofanywa sasa ni mkakati wa hovyo wenye nia ovu unaofanywa na CHADEMA na mawakala wao katika kukengeusha Demokrasia tulivu inayosifiwa Ulimwenguni kote iliyopo ndani ya Taifa letu.

Ndugu Wanahabari nivyema nikafafanua mambo yafuatayo:

Suala la Kwanza: KUNATOFAUTI KUBWA KATI YA CCM NA UPINZANI.

CCM ni chama kinachoongozwa na, Kanuni, taratibu na miongozo. Hii haipo katika chama chochote cha Upinzani. Huko kwa wenzetu ambako siye tumekulia Kanuni, taratibu na miongozo vipo kwenye nguvu za mtu mmoja tu. Mfano CHADEMA kila jambo lipo katika hatima ya mikono ya Kiongozi mmoja. Hivyo mtu anapotoka CCM nakurudi huko jua kashindwa kuishi kwa kanuni, taratibu na miongozo bali anapenda kuishi kihovyo hovyo. 

Hii ni hatari sana na kwenye chama cha upinzani ukifanya mambo ya hovyo ndiyo unakua maarufu kwani unakua umewakosha wahovyo wenzio. Utaitwa Kamanda, Mzalendo na majina mengi ya namna hiyo. Uhovyo wa namna hiyo CCM haupo kabisa na, ukizoea ujinga huo huwezi kuishi CCM utaondoka kama KIDELA maana utaona kama unatengwa maana kila mmoja yupo busy kutatua changamoto za jamii.

Suala la Pili: UTARATIBU NA MFUMO WA UONGOZI NDANI YA CCM UNAELEWEKA: Ndani ya CCM upatikanaji wa uongozi kwa nafasi za kugombea ni kila baada ya miaka mitano. Hivyo kama uchaguzi umefanyika na hukupata nafasi inabidi uungemkono waliochaguliwa kwaajili ya kufanya kazi ya Chama na Taifa kwa ujamla hii ndiyo demokrasia yenye misingi ya haki na usawa. 

Isipokua nafasi za kuteuliwa hizi hupatikana kulingana na matakwa ya kanuni, taratibu na mahitaji ya mamlaka za uteuzi kwa mujibu wa miongozo. Hivyo waliokosa nafasi kama bado wanahitaji kupata nafasi za kugombea lazima usubiri baada ya kipindi hicho tajwa hapo juu. HIVYO CCM NDICHO CHAMA CHENYE KATIBA BORA ZAIDI YENYE KUZINGATIA DEMOKRASIA PANA. Sasa KIDERA anatoka CHADEMA anataka uchaguzi ufanyike ili kupata madaraka kwasababu tu kahamia. 

Hakuna demokrasia ya namna hiyo huku CCM hayo yapo CHADEMA ndiyo maana kuna nafasi hazieleweki zinapatikanaje kwani ni chama kisicho na misingi inayoeleweka ni kikundi tu bora hata SACCOS zina utaratibu fulani kwa wakopaji wake lakini hawa wenzetu wako hivyo mnavyowaoana. KIDERA alipaswa kufanya tafiti kwanza juu ya CCM kabla hajahamia na kushindwa kufanya hivyo ni wazi kajianika kuwa mtu asiye makini na hii ni dalili mbovu kwa wanasiasa wa aina ya KIDERA maana hawana mapenzi ya kweli na Demokrasia bali wanakua wanaajenda binafsi tofauti na malengo madhubuti ya chama cha siasa.

Suala la Tatu: UAMINIFU WA KIDERA UNATIA MASHAKA HATA KWA HISTORIA YAKE:

Kidera ni kijana mwenye tamaa. Hata Chadema wanamjua vizuri amekua mtu mwenye kuendekeza tamaa ya madaraka kwa muda sasa. Hili linatokana na yeye kufanya siasa huku akiwa hana kazi nyingine yoyote ya kufanya. Hivyo anachofanya ni kulazimisha siasa iwe sehemu ya kupata mkate wake wa kila siku. Nakumbuka tulipokua ukonga kwenye uchaguzi mdogo alipohamia CCM aliwahi kuja na bajeti ya kiasi cha shilingi milioni 10 aliyoiandaa chumbani kwake ili apewe pesa akidai anavijana watasaidia kuleta siri za CHADEMA. 

Kila mmoja alimshangaa alipoambiwa hakuna CCM ya hivyo na kuona amepuuzwa ndiyo akaanza kupika majungu na kwenda kuramba nyayo hao waliomfuga ili arudi kama alivyofanya. Undumila kuwili alionao ni hatari sana katika hatma yake ya kisiasa. Kidera huyu ndiye yule Aliyegombea kura za maoni ndani ya Chadema aliposhindwa akaanza kuwachafua viongozi wake ndiye aliyeleta migogoro ya UKAWA huko Segerea kama mnakumbuka. 

Nao CHADEMA kwasababu ya kuleana kizembe wakampa uenyekiti wa jimbo akatulia kidogo. Ulipofika uchaguzi wa Serikali za Mitaa akagombea Uenyekiti wa Mtaa na alipopata tu alitumia nafasi hiyo kujipatia pesa zile ndogo ndogo baada ya kurubuni watu huko wakisuruhisha migogoro. 

Hayuko safi hata kidogo. Rekodi yake tu inamfanya akose uhalali wa kuzungumza hata mbele ya wenye akili za kupambanua mambo. Sasa alipohamia CCM kwa kuamini yeye ni mtu muhimu kwahiyo atapata cheo kikubwa zaidi ndiyo njaa imemshika sasa kakoma kwa tamaa yake ya Fisi.

 Anasema kuna viongozi walimuahidi madaraka kama siyo upungufu wa ufikiri kichwani unawezaje kuahidiwa madaraka yasiyo kuwepo na wewe ukaamini? Hakuna jambo hilo ni mwamvuli tu mbovu wanatumia na wenzake hao ilikujificha wakitaka kuhalalisha uongo wao. Huyu ni mpiga dili tu wa kisiasa ambaye kashindwa kuvumilia CCM maana huku unapaswa kuwa na kazi inayokupa kipato na ndipo ushiriki siasa.

Suala la Nne: CCM ni chama bora zaidi barani Afrika. Ndicho chama cha ukombozi kinachotoa dira ya maendeleo. Mtakumbuka Prof. Lumumba wa Kenya alitaja vyama viwili tu vinavyostahili kubaki barani Afrika katika vyama hivi CCM moja wapo. Sasa asije mtu yeyote akachukulia poa na kufikiri ni chama cha mchezo huyu atajikuta yuko peke yake. Sehemu pekee ya kufanya siasa za mchezo, masiara na kupoteza muda ni huko upinzani walikozoea ambako nirahisi kupeana umaarufu wa ajabu kwa sababu ya mambo ya hovyo. CCM imepewa mamlaka na Wananchi kwasababu inamipango endelevu. 

Hivyo KIDERA anaposema haoni mazingira ya kufanya siasa akiwa ndani ya CCM niwazi hajui maana ya Siasa. Atambue kuwa CCM inaamini kuwa SIASA NI MAENDELEO na siyo makelele yasiyo na masingi. Kajidhalilisha kwani kakimbia siasa ya maendeleo na kwenda kwenye siasa ya makelele, kupinga kila kitu na kulalama pasipo kuwa majibu na suluhu za matatizo ya jamii.

Suala la Tano: kutokana na mfumo bora wa CCM ndiyo maana chama hiki kimetoa RAIS BORA ZAIDI BARANI AFRIKA. Ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM. Ninyi ni mashahidi mmeona namna anavyopokelewa na kuhitajika kwenye mataifa ya wenzetu. Tumeona Alipokwenda S.Afrika, Namibia na Zimbabwe. Mapokezi aliyoyapata na namna anavyoheshimika sana. Hii ni alama kubwa na tunu kwa Taifa letu.

SUALA LA SITA: NAWAONYA Viongozi wa CHADEMA hasa Bonphace Jackob kuacha kuacha upotoshaji wa makusudi wakati wanajua kabisa KIDERA si mwenzao siku nyingi. Bonphace anajua kabisa namna KIDERA alivyotoka na kurudi ndani ya CHADEMA vikao vyote mlivyokuwa mnakaa na namna alivyokuwa anawasiliana na ninyi tunajua. Sasa kuhadaa UMMA kwamba CCM hakuna mazingira ya safi ya kufanya Sisa wakati KIDERA huyo ndiye aliyeeleza watu wa UKONGA kwenye kampeni mambo yote maovu ya CHADEMA na VIONGOZI wake akiwemo huyo BONPHACE.

HIVYO: Natoa Rai kwamba wale wote walio hamia CCM kwa kufuata mkumbo, kusaka madaraka na kufikiri atapata nafuu ya kubebwa ni Bora watoke warudi huko walikozoea upuuzi wa namna hiyo. CCM ni kazi, Uzalendo uliotukuka, na sehemu ya kuwa mtumishi wa umma. CCM ni uadilifu malengo ya kitaifa na kuwa majibu sahihi ya maswali ya jamii. Tuwapuuze wale wote wasio na hekima kwani wamebembendwa kisiasa huko walikotoka wanataka kuendekeza udumavu wa kisiasa. Wale tuliohamia kwasababu ya kulipenda taifa na kuamini kazi inayofanywa na CCM na viongozi wake kupitia mwenyekiti ambaye ndiye Rais wa Nchi basi tuendelee kuchapa kazi na kuwa majibu sahihi ya matatizo ya Watu.

WAZIRI AZITAKA KAMPUNI ZUNAZOUNDA MAGARI YA UTALII KUFANYA KAZI KWA USHINDANI,AWATAKA KUEPUKA MIGOGORO ISIYO YA LAZIMA

$
0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.George Kakunda,Satbir Hanspal Mkurugenzi wa kiwanda cha Hanspaul Mrisho Gambo Mkuu wa Mkoa wa Arusha 
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.George Kakunda,Satbir Hanspal Mkurugenzi wa kiwanda cha Hanspaul Mrisho Gambo Mkuu wa Mkoa wa Arusha 


Na.Vero Ignatus,Arusha

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.George Kakunda ametembela kiwanda cha kuunda bodi za magari ya utalii cha Hunspaul kilichopo njiro mkoani Arusha na kutoa maelekezo kwa Taasisi ya Brela na Tume ya Ushindani wa Kibiashara FCC kuangalia namna kampuni hizo na RSA ya Moshi zinazotengeneza magari ya utalii ili ziweze kufanya biashara zao kwa ushindani na kuepusha migogoro isiyo ya lazima.

Mhe Waziri ameyasema hayo leo ikia ni siku moja baada ya kutembelea kiwanda cha RSA na kupokea malalamiko toka kwa wamiliki wa kiwanda hicho juu ya kuigwa kwa nembo yao ya kibiashara na moja ya kiwanda kilichopo mkoani Arusha.

"Ninaagiza BRELA na FCC waje hapa sio kwa lengo la kufunga kiwanda hiki ila ni kwaajili ya kuhakikisha kwamba utaratibu unawekwa vizuri ili uzalishaji wa Moshi uendelee na Uzalishaji wa Arusha uendelee na hiyo ndiyo kauli yangu ya mwisho kwani kiwanda hiki kimefanya uwekezaji mkubwa nawa kisasa na meshuhudia ubunifu mkubwa ikiwemo utenegenezaji wa magari yanayotumia umeme" alisema Mhe. Waziri.

Satbir Hanspal Mkurugenzi wa kiwanda cha Hanspaul amemshukuru waziri wa viwanda na biashara kwa kutembelea kiwanda chao na kujionea uzalishaji unaoendelea,ambapo amesema wao kama wawekezaji wazawa wanajivunia serikali inayojali changamoto za wawekezaji kwani bado wana fursa kubwa ya uwekezaji nyumbani.

“ Wawekezaji wazawa unajivunia sana kuwa na serikali inayojali changamoto za wawekezaji, Tanzania bado kuna fursa kubwa sana ya uwekezaji na sisi tumeamuakuwekeza nyumbani ndio maana pamoja na kiwanda hiki cha kutengeneza magari ya watalii tumefungua na kiwandakingine cha kutengeneza mifuko ya karatasi ili kutoa suluhisho baada ya serikali kupiga marufuku mifuko yaplastiki” alisema Satbir.

Mrisho Gambo Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo amesema wao kama Serikali ya Mkoa wamejipanga kutoa ushirikiano kwawawekezaji wote walioko mkoani Arusha,amesema japo kuwa wanakumbana na changamoto za kibiashara lengo kuu ni kulinda chata zetu ndani kibiashara.

“Sisi kama Mkoa tunajivunia sana uwekezaji huu na kuwepokwa kiwanda hiki Mkoani Arusha kwani ni sifa kwa mkoawetu na nchi kwa ujumla, hivyo nipende kuwatia moyowawekezaji hawa wakati wowote wanapokumbana nachangamoto za kibiashara lengo letu ni kulinda brand zetu zandani” alisema Gambo.

Katika ziara hiyo Mhe Waziri Kakundo aliweza kutembelea kiwanda cha Hanspaul Industries Liimites kinachotengeneza mifuko ya karatasi kujionea uwekezaji mkubwa  ambapo amewapongeza wawekezaji hao kwa kuweza kutafuta suluhisho baada yakatazo la mifuko ya plastiki kuanzia tarehe 01 June 2019

VIONGOZI TUACHE KUWAGAWA WANACHAMA - MNEC KAGERA

$
0
0
Anaadika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV - Bukoba.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg. Willbroad Mutabuzi amewataka Viongozi waliopewa dhamana ndani ya CCM kutowagawa wanachama, na kuwakumbusha kuwa Vyeo ni dhamana, na kuacha migogoro isiyokuwa na tija ndani ya Chama.

Akizungumza na Viongozi wa CCM Mara baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Bukoba Mjini,  mapema Mei 30, 2019 Ndg. Mutabuzi amesema katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu mwakani, Viongozi waliopo madarakani katika ngazi mbalimbali ndani ya CCM, Hawana budi kuheshimiana na kuvumiliana kwa kila hali pasipo kugawanyika na kuwagawa wanachama.

Ndg. Mutabuzi amewakumbusha Viongozi hao kuwa nafasi walizonazo ni za muda tu kwani yeyote anaweza kupewa au kuwekwa katika nafasi hiyo, hivyo si busara kugawa wanachama katika makundi kwani Chama ni cha Wanachama na sio Mali ya Mtu Binafsi, na kuwataka wale wote wanaotumia Vitisho kwa wanaowaongoza kuacha Mara moja.

Aidha kwa upande mwingine MNEC huyo Ndg. Mutabuzi ameishukuru Serikali ya Wilaya Chini ya Mkuu wa Wilaya Deodatus Kinawiro, jinsi inavyotoa ushirikiano, na kuomba ushirikiano huo baina ya Taasisi hiyo na Ofisi uendelee na isiwe ni ushirikiano wa mtu na Mtu.

Mbali na shukrani hizo Ndg. Mutabuzi amewasisitiza Madiwani hasa wa CCM kutembea kifua mbele wakinadi Yale yote yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli, ikiwemo miradi ya Barabara, Umeme, Afya, Miundombinu  n.k ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Sambamba na Madiwani hao kurudi kwa wananchi kusikiliza na kuzitafutia Ufumbuzi kero zinazowakabili katika maeneo yao.
 Ndg. Mutabuzi akisaini katika Kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili Ofisi za CCM kabla ya kuongea na Viongozi wa Chama (W).
 Pichani ni MNEC wa Kagera Ndg. Willbroad Mutabuzi akivishwa Skafu na Vijana wa Chipukizi Mara baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM (W) Bukoba Mjini.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 31.05.2019

VOA SWAHILI: Duniani Leo May 31st, 2019


SERIKALI KUSAIDIA UANZISHWAJI WA KITUO CHA KUATAMIA UBUNIFU NA BIASHARA CHA CHUO KIKUU MZUMBE

$
0
0


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akikagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akikagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa hosteli hizo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa hosteli hizo.Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya waziri kukagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi.
Mwanafunzi anayesomea sheria akionyesha bidhaa zake wakati wa kufunga kambi ya ujasiriamali.
Bidhaa mbalimbali za wanafunzi wajasiriamali wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akipewa maelezo kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa chuo Kikuu Mzumbe juu ya kilimo cha kisasa.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akizungumza wakati wa kufunga kambi ya ujasiriamali chuoni hapo.
Mzungumzaji Mkuu wa Kambi ya Ujasiriamali ya Mwaka 2019, Ahmed Lussasi ambae ni mhitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Mwazilishi mwenza wa Kampuni ya MAXOM AFRICA, akizungumzia mafanikio aliyoyapata pamoja na changamoto zake.
Mkuu wa Shule ya Biashara Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Hawa Tundui (kushoto), akifuatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani),
Baadhi ya washiriki. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa kufunga Kambi ya Ujasiriamali 2019.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka akimkaribisha Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, wakati wa ziara yake chuoni hapo mkoani Morogoro.
Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akisalimiana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Prof. Ganka Nyamsogoro.
Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa hosteli za wanafunzi chuoni hapo. Mhandisi wa ujenzi katika hosteli za Chuo Kikuu Mzumbe, Focus Odecho, akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa hosteli hizo.




Morogoro, Tanzania

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako amesema Wizara yake iko tayari kusaidia kutafuta rasilimali kwa ajili ya kuanzisha kituo cha kuatamia Ubunifu na Biashara “Innovation and Business Incubation Centre “ cha Chuo Kikuu Mzumbe, ambacho kitatoa fursa kwa wanafunzi wanaosoma katika Chuo hicho na Vyuo vingine na vijana wengine wenye mawazo ya kiubunifu, ujasiriamali na biashara, kuyaboresha mawazo na shughuli zao za kiubunifu ili ziweze kuwa biashara kamili.

Waziri Ndalichako amesema hayo katika kilele cha kambi ya ujasiriamali ya Chuo Kikuu Mzumbe iliyofanyika katika Kampasi yake Kuu Morogoro ambapo amepongeza hatua hiyo ya kuanzishwa kwa kambi hiyo ambayo ni mara ya tatu inafanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017, huku akisema utaratibu huo ni tafsiri sahihi na kwa vitendo ya agenda ya Kitaifa ya kujenga Uchumi wa Viwanda.

“Nimefurahi sana leo kuona bidhaa na ubunifu wa hali ya juu hapa na kusikia kuwa Kambi hii imeendelea kuvutia watu wengi, wakiwemo wanafunzi, baadhi ya wafanyakazi na watu wengine kutoka jamii zinazotuzunguka, utaratibu huu utakuwa na faida ya muda mrefu kwa Chuo kwani wahitimu wenu watakuwa wameiva kinadharia na kivitendo, na wenye uwezo wa kujiajiri na kutengeneza ajira”.

Ndalichako amevitaka vyuo vingine kuiga mfano huu ambao unatoa fursa ya kukitangaza Chuo ambapo watanzania wataweza kujionea namna ambavyo fani mnazofundisha kama Uongozi wa Biashara, Ujasirimali, Uchumi na Mipango, TEHAMA, na zingine zinavyotayarisha wahitimu ambao wana mawazo ya kibunifu na ujasiriamali na mtazamo wa kibiashara.

Ndalichako amewataka Chuo Kikuu Mzumbe kuhahakisha kupitia kituo hicho atamizi kinawezesha wabunifu wao kushiriki katika mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU), kwa lengo la kuhamasisha ubunifu nchini yanayoratibiwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.

Akizungumza katika kilele hicho Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka amesema kambi hiyo inashirikisha wanafunzi wa Mzumbe na wengine, wahitimu wa Mzumbe ambao ni wajasiriamali. Ameongezea pia kuwa kupitia kambi hiyo wanafunzi wenye mawazo ya kibiashara pia hukutanishwa na wafanyabiashara walibobea na ili kupata uzoefu. Kusiluka ameahidi kusimamia uanzishwaji wa haraka wa kituo atamizi kwani kitasaidia kukuza mawazo ya kibunifu kuwa biashara kubwa nchini zitakazo changia pato la Taifa.

Nae mzungumzaji Mkuu wa kambi ya Mwaka 2019. Ndugu Ahmed Lussasi ambae ni mhitimu wa Chuo kikuu Mzumbe na Mwazilishi mwenza wa kampuni ya MAXOM AFRICA, kampuni inayofanya vizuri katika biashara, amesema anapongeza wazo la kituo atamizi na ameiomba Serikali kulipa kipaumbele , kwani biashara yao ilianza kwa kulelewa katika kituo atamizi na hatimae kukua. Lusassi kama mmoja wa wahitimu amekitaka Chuo kuwa na mfumo mzuri wa kushirikisha wahitimu wake katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya Chuo hicho.

Katika kambi hiyo Ndalichako amezindua bidhaa mbalimbali zilizobuniwa na wanafunzi wabunifu na wajasiriamli katika chuo hicho, ikiwa ni pamoja na kitabu kilichoandikwa na mwanafunzi wa Chuo hicho. Kwa mwaka 2019 wanafunzi 48 wameandikisha mawazo yao ya kibunifu ili yaweze kuboreshwa.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Takwimu za mimba zamshitua Kamanda wa Polisi Mwanza "hatuwezi kukubali"

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, ACP. Jumanne Muliro akifungua kikao kazi cha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali za Mitaa, Ustawi wa Jamii, Dawati la Jinsia, Jeshi la Polisi na wataalamu wa afya mkoani Mwanza.

Kikao hicho kiliandaliwa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto (KIVULINI) la jijini Mwanza ili kuweka mikakati ya kuboresha upatikanaji wa huduma rafiki za afya kwa vijana na wahanga wa ukatili ikiwemo ubakaji na kutokomeza mimba katika umri mdogo.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa “sauti yangu, haki yangu katika kupunguza mimba za umri mdogo Manispaa ya Ilemela” unaosimamiwa na shirika la KIVULINI.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Wanahabari wakinasa matukio kwenye warsha hiyo ya kikazi.
Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akifafanua jambo kwenye kikao hicho.
Mwakilishi kutoka jeshi la polisi mkoani Mwanza akiongoza wajumbe wa kikao kazi hicho kuweka mikakati ya upatikanaji wa huduma rafiki kwa wahanga wa ukatili.
Mmoja wa washiriki wa kikao kazi hicho akichangia mada.
Tazama BMG Online TV hapa chini
Attachments area

SERIKALI KUPELEKA MIRADI MITATU MIKUBWA YA MAJI MKOANI TANGA

$
0
0

NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto akipata futari na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly katikati wakati futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kwa ajili ya wafanyakazi na majirani zao kwa ajili ya kujenga mshikamano na umoja miongoni mwao.
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto akipata futari na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly katikati wakati futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kwa ajili ya wafanyakazi na majirani zao kwa ajili ya kujenga mshikamano na umoja miongoni mwao.
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto akipata futari na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly katikati wakati futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kwa ajili ya wafanyakazi na majirani zao kwa ajili ya kujenga mshikamano na umoja miongoni mwao.
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto akipata futari na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly katikati wakati futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kwa ajili ya wafanyakazi na majirani zao kwa ajili ya kujenga mshikamano na umoja miongoni mwao.
Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gispson George kushoto akiwa na Katibu wa Naibu Waziri wa Maji Lichela katikati na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange wakipata futari hiyo
PRO wa Tanga Uwasa Dorrah Killo akishiriki kugawa futari
Sehemu ya wafanyakazi na majirani wakipata futari hiyo

NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema wizara hiyo inatarajiwa kupeleka miradi zaidi ya mitatu mikubwa mkoani Tanga kwa maana ya ile ya miji 28 Tanzania Bara na mmoja wa Visiwani.

Aweso aliyasema hayo leo wakati halfa ya futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kwa ajili ya wafanyakazi na majirani zao kwa ajili ya kujenga mshikamano na umoja miongoni mwao.

Alisema kwamba miradi hiyo itakwenda kwenye wilaya za Handeni, Muheza na Pangani ambazo zitanufaika nao ili kuweza kuondosha changamoto za huduma hiyo zilizopo kwenye maeneo yao .

“Sisi kama Wizara tumeona kazi nzuri inayofanywa na Tanga Uwasa kwani hivi sasa wanatoka Tanga Jiji wanaenda maeneo mengine ikiwemo Lushoto wanasimamia miradi, Muheza na Handeni hivyo sisi tutaongeza nguvu”Alisema Naibu Waziri huyo

Aidha alisema watahakikisha wanawezeshwa kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ikiwemo kuwasimamia wakandarasi wanayoitekeleza ili miradi hiyo iweze kutekeleza kwa waledi mkubwa na hatimaye kuweza kuondosha changamoto zilizopo kwenye maeneo husika.

Awali akizungumza katika futari hiyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema hafla hiyo ilikuwa ni kuwafuturisha wafanyakazi wao waislamu na majirani kwa ajili ya kujenga umoja miongoni mwao.

Alisema kwa sababu wamekuwa wakikaa pamoja kwa umoja lengo kuwakumbuka waislamu waliofunga kwenye kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa ramadhani kwani suala la kufunga ni muhimu sana kwa ajili ya kufanya ibada.

Hata hivyo aliwatakia kilala heri waislamu katika mfungo kwa sababu unawapa nguvu zaidi ya kuishi maisha mema zaidi na kuweza kushindana na vishawishi.

RC NDIKILO AIELEKEZA WILAYA YA KIBITI KUONGEZA KASI MARA DUFU KUKAMILISHA UJENZI HOSPITAL YA WILAYA

$
0
0
MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amemuelekeza mkurugenzi wa halmashauri ya Kibiti pamoja na mkuu wa wilaya ya hiyo kusimamia ujenzi wa hospital ya kisasa ya wilaya na kuzidisha kasi ya kupeleka vifaa vya ujenzi ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ifikapo juni mwaka huu.

Aidha ameitaka idara ya manunuzi kuongeza ushirikiano katika suala hilo pasipo kusiganasigana ilihali kazi hiyo ikamilike kwa muda lengwa.

Akikagua hatua ya ujenzi ulipofikia wa hospital ya wilaya ya Kibiti, kata ya Mtawanya ,Ndikilo aliwapongeza kwa kasi wanayokwenda nayo na kuwaasa kutumia vizuri muda wa mwezi mmoja uliobaki vizuri .

Hata hivyo ,alimuambia mkurugenzi ahakikishe pia transformer linawashwa haraka ambapo litasaidia kurahisisha baadhi ya kazi zinazotegemea umeme na kufanya kazi usiku na mchana.

"Watendaji wafanye kazi na wewe,washirikiane kwenye njia yako,ofisa ununuzi na mganga mkuu wa wilaya muwe kwenye njia moja"

"Kama kuna mtendaji atakukwamisha kupitia njia yako ya kwenda kumaliza ujenzi huu kwa wakati basi mchafulie faili lake ,simple tuu"alisisitiza Ndikilo.

Awali mkurugenzi wa Kibiti ,Alvera Ndabagoye alisema,kati ya halmashauri 67 nchini zilizopokea bilioni 1.5 kila moja,kwa ajili ya ujenzi wa awali wa hospital za wilaya,":'wao walianza ujenzi mwezi wa tatu na  kwasasa ujenzi upo hatua ya linta.

Nae mkuu wa wilaya ya Kibiti, Gulam kifu ,ana matumaini mwezi mmoja uliobakia watakamilisha ujenzi huo na wamepokea maagizo ya mkuu huyo wa mkoa.



ELIMU YA AJASILIAMALI YASAIDIA VIJANA ZAIDI YA 9000 KUJITAMBUA

$
0
0

Na Woinde Shizza Michuzi TV, Arusha 

Jumla ya vijana 9,339 kutoka vikundi 380 katika mikoa ya Iringa, Njombe, Songwe, na Mbeya wamenufaika na elimu mbalimbali ikiwemo ya ujasiriamali ambayo imewawezesha kujitambua na kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Aidha vijana hao wamenufaika katika elimu  kuhusu akiba na mikopo,  utunzaji wa fedha, ujasiliamali na ujuzi tete, mpango biashara na kilimo biashara ambazo kwa pamoja zimewawezesha wao kujitegemea.

Hayo yalisemwa mkoani Arusha katika sherehe za wiki ya unywaji maziwa duniani ambayo kitaifa inafanyika jijini Arusha na Meneja wa kilimo biashara kutoka shirika la Heifer International linaloongoza jitihada za kutokomeza njaa na umaskini ,huku likizingatia kutunza mazingira, Frimina Kavishe wakati akizungumzia jinsi ambavyo wamewezesha vijana katika nyanja mbalimbali katika kujikwamua kiuchumi.

Frimina alisema kuwa, vijana hao wamefikiwa kupitia mradi wa ushirikishwaji vijana katika sekta ya kilimo na mifugo Afrika mashariki (EAYIP) ambapo wamelenga vijana kuanzia umri wa miaka 15-24 kwani ni kundi lililosahaulika Sana na lina vipaji vikubwa ambavyo vinahitaji kuendelezwa .

"mradi huu umeanzishwa kwa ushirikiano na Taasisi ya mastercard ukilenga kuboresha maisha ya vijana nchini Tanzania na Uganda kwa kutengeneza fursa za ajira na ujasiriamali miongoni mwa vijana 25,000 hadi kuisha kwa mradi huo ifikapo mwaka 2021 na unalenga vijana wanaokosa fursa za kiuchumi na mradi huu ulianza tangu oktoba 2016"alisema Frimina.

Aliongeza kuwa, mradi huu una malengo mkakati minne ikiwa ni pamoja na kuwapatia ujuzi na maarifa vijana ili waweze kujiajiri kupitia mnyororo wa dhamani wa maziwa, kuku, mboga mboga na matunda, mahindi, samaki,viazi mviringo na mimea jamii ya mikunde sambamba na kuwaunganisha na taasisi za kifedha, kuweka mazingira wezeshi ili kuvutia vijana wengi kujiajiri kwenye sekta ya kilimo na mifugo na kudurufu muundo wa vitovu yaani (sehemu za biashara).

Naye Meneja ushirika wa wajasirimali vijana wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe, George Hayuka alisema kuwa, lengo kubwa la mradi huo ni kuongeza kipato kupitia ajira na maendeleo ya kibiashara katika sekta ya kilimo huku ukilenga kuwajengea uwezo vijana katika ujuzi maalumu juu ya kuanzisha biashara ama kupata ajira kupitia shughuli za kilimo.

Hayuka alisema kuwa, mradi huo pia unalenga kuendeleza ama kurudufu muundo wa vitovu katika minyororo mipya ya thamani kama vile kuku, kilimo cha mbogamboga, matunda na mazao ya nafaka na mizizi sambamba na kuongeza ushiriki wa vijana wa kike na wa kiume .

Aliongeza kuwa, baada ya kumalizika kwa mradi huo, shirika hilo wakishirikiana na wafadhili wa taasisi ya mastercard wameanzisha Vitovu 7 kama sehemu ya biashara yaani ushirika wa vijana ambao utakuwa ukiendelea mara baada ya kumalizika kwa mradi huo huku wakiunganishwa na masoko ili wawe na uhakika wa soko la bidhaa zao na kupata huduma mbalimbali.

Naye Mwenyekiti wa Chama kikuu cha wafugaji mkoa wa Songwe, Isaya Mbindi alisema kuwa, shirika hilo limewawezesha wafugaji hao kufuga ngombe wa kisasa sambamba na kupata elimu juu ya uhimilishaji kupitia mradi wa uendelezaji wa sekta ya maziwa Afrika mashariki (EADD).

Mbindi alisema kuwa, kupitia mradi huo wa EADD wa miaka mitano ambao ulianza mwaka 2003 na upo mbioni kumalizika wameweza pia kuanzisha viwanda vidogovidogo ambapo wameweza kujiunga kwenye vyama vya ushirika ambapo wameweza kunufaika zaidi ya wafugaji mia nne kwa mkoa wa Songwe.


Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>